Kama ulimwengu ujao utakuwa na watakatifu tu, sasa hao watakaotawaliwa watatoka wapi?

Kama ulimwengu ujao utakuwa na watakatifu tu, sasa hao watakaotawaliwa watatoka wapi?

JIBU: Kuna mambo mawili ya kufahamu jambo la kwanza ni kuwa mara baada ya huu ulimwengu wa sasa kuisha, kutakuwa na utawala mwingine mpya ujulikanao kama utawala wa amani wa Yesu Kristo wa miaka 1000 (Ukisoma Ufunuo 20:6 utaona jambo hilo). Na mara baada ya huo utawala wa miaka 1000 kuisha kutakuwa na umilele ambapo wakati huo ndio ile mbingu mpya na nchi mpya vitafunuliwa..Na maskani ya Mungu itakuwa ni pamoja na wanadamu. Ambapo Mungu atafanya makao yake na wanadamu milele na milele isiyokuwa na mwisho (Ufunuo 21:3)

Sasa katika ule utawala wa miaka 1000, ambapo Kristo atarudi na watakatifu wake aliowanyakua zamani, (Yuda 1:14) utakuwa ni utawala wa amani lakini bado biblia inarekodi waovu watakuwepo pia (Isaya 65:20)…Lakini katika mbingu mpya na nchi mpya ambayo itaanza mara baada tu ya utawala huu wa miaka elfu moja kuisha, waovu hawatakuwepo kabisa.

Sasa hawa waovu watakaokuwepo ndani ya utawala huo (waliozaliwa humo) ndio watakaotawaliwa na watakatifu wakati ule utakapofika.. Na ndio maana Bwana Yesu anatuhimiza sasa na kutuambia..

Ufunuo 2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.

28 Nami nitampa ile nyota ya asubuhi.

29 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.

Vilevile katika huo utawala wa miaka elfu moja, na pia baada ya utawala huo kupita kutakuwa na shughuli maalumu (au tuseme sekta maalumu) ambazo Mungu ameziandaa zifanywe na zisimamiwe na watakatifu wake tu. Lakini sasa hizo hazifanywi na kila mtakatifu tu, hapana, bali zitafanywa kulingana na auminifu wa mtakatifu husika alipokuwa hapa duniani..Tunasoma hilo katika.

Mathayo 24:45 “Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake?

46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo.

47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote.

48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;

49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi;

50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,

51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Unaona? Sasa hapa ndipo yatakapotokea matabaka hata katikati ya watakatifu. Wale ambao walikuwa waaminifu katika kazi ya Mungu na katika utakatifu wakiwa hapa duniani watapewa vyeo vya juu zaidi katika enzi ya Mungu, na wale waliokuwa waaminifu kidogo watapewa kidogo..kama Bwana Yesu alivyosema katika kitabu cha Luka…

Luka 19:16 “Akaja wa kwanza, akasema, Bwana, fungu lako limeleta faida ya mafungu kumi zaidi.

17 Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.

18 Akaja wa pili, akasema, Bwana, fungu lako limeleta mafungu matano faida.

19 Akamwambia huyu naye, Wewe uwe juu ya miji mitano.

20 Akaja mwingine akasema, Bwana, hili ndilo fungu lako, ambalo nililiweka akiba katika leso.

21 Kwa maana nilikuogopa kwa kuwa u mtu mgumu; waondoa usichoweka, wavuna usichopanda.

22 Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, niondoaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;

23 basi, mbona hukuiweka fedha yangu kwa watoao riba, ili nijapo niipate pamoja na faida yake?

24 Akawaambia waliosimama karibu, Mnyang’anyeni hilo fungu, mkampe yule mwenye mafungu kumi”

Hivyo kwa kuhitimisha ni kwamba, vyeo vitakuwepo na kutawala pia kutakuwepo..Isipokuwa kutawala kutaishia katika ule utawala wa miaka 1000, lakini vyeo na ngazi zitaendelea mpaka umilele kwenye mbingu mpya na nchi mpya.. kwasababu huko hakutakuwa na waovu tena, Isipokuwa sote tutamilika na yeye. Lakini sote hatutakuwa ngazi moja…

2Timotheo 2:12 “Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi”;

Hivyo tufanye bidii ili tuwepo na Bwana katika utawala wake na mpaka mwisho hadi tutakapoifikia ile nchi mpya na mbingu mpya..

2Petro 3:13 “Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake”.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe au piga namba hii +255693036618/ +255789001312

  Au Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada nyinginezo

KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000

UTAWALA WA MIAKA 1000.

MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 2)

Kati ya Unyakuo,dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 kipi kinaanza

USITOKE NJE YA HIFADHI YA MUNGU.

Easter ni nini?..Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?

Milima ya Ararati ipo wapi kwasasa? (Mwanzo 8:4)

Rudi Nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments