Je! Siku ilihesabiwaje kabla ya jua na mwezi kuumbwa?

Je! Siku ilihesabiwaje kabla ya jua na mwezi kuumbwa?

Swali: Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma jua na mwezi viliumbwa katika siku ya 4 , sasa napenda kujua kabla ya hapo siku zilihesabiwaje, maana jua ndilo linalotenga mchana na usiku…na maandiko yanatuonyesha kuwa lilikuja kuumbwa siku ya 4?

Jibu: Ni kweli jua na mwezi viliumbwa siku ya 4, tena baada ya miti na miche ya kondeni kuumbwa (Mwanzo 1:14).

Lakini ukisoma kuanzia mstari wa pili katika kitabu hiko cha Mwanzo, utaona Mungu tayari alikuwa ameshaumba mchana na usiku na ameshatenga giza na nuru.

Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.

2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; MUNGU AKATENGA NURU NA GIZA.

5 MUNGU AKAIITA NURU MCHANA, NA GIZA AKALIITA USIKU. IKAWA JIONI IKAWA ASUBUHI, SIKU MOJA”.

Umeona?..kumbe tayari Mungu alikuwa ameshaumba mchana na usiku kabla hata ya kuumba jua. Maana yake hata kama asingeumba jua bado majira na mchana na usiku yangekuwepo kwasababu yeye mwenyewe ndio Nuru ya ulimwengu (mwilini na rohoni).

Yohana 8:12 “Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima”.

Ndio maana katika ile mbingu mpya na nchi mpya hakutakuwepo  na jua na bado Nuru itakuwepo.

Ufunuo 21:23 “Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo”.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa Mungu aliumba mchana na usiku, kabla ya kuliumba jua..na hiyo ni kuonyesha utukufu wake yeye, na pia kuonyesha kuwa yeye ndiye Nuru halisi Na ndio chanzo cha Nuru yote.

Je umempokea Bwana Yesu aliye Nuru ya kweli? Kama bado fahamu kuwa bado upo gizani ijapokuwa jua linakumulika…kwahiyo ni vyema ukafanya maamuzi thabiti leo ya kumpokea na kuokoka.

Yohana 12:46 “Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani”

Soma pia Yohana 9:5 na Yohana 11:9.

Bwana Yesu akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi?

HAMA KUTOKA GIZANI

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?

Je mke wa Musa alikuwa ni Mweusi?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Thenashara Devd
Thenashara Devd
11 months ago

nam nam mtumish nashkuru kwa jibu zuri limeniweka ktk kuzd kukua nakulifaham nen0 kiundan zaid nazaid mbarkiw sana huduma ya wingu la mashaidi