Jina kuu la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Karibu tujifunze Biblia, (Neno la Mungu wetu), ambalo ndio taa iongozayo miguu yetu katika safari yetu ya kwenda mbinguni kwa Baba.
Neno la Mungu ni ufunuo mkamilifu zaidi ya Ndoto tuotazo au maono tuonayo..
Leo tutajifunza kwa mtu mmoja katika maandiko, aliyepokea Ndoto kutoka kwa Mungu, na jinsi alivyoipambanua na kisha tutajifunza kitu. (Na mtu huyo si mwingine Zaidi ya mke wa Pilato)
Kabla ya Bwana Yesu kusulubiwa aliota ndoto!. Na ndoto yenyewe ilikuwa inamwonesha kuwa Bwana Yesu kuwa hakustahili kupitia yale mateso. Ndoto ile ilikuwa ni ya kiMungu ikimwonesha kuwa Bwana Yesu alikuwa ni mtu wa haki, na hakustahili kwa vyovyote kusulubiwa. Na pengine labda mke wa Pilato aliota Zaidi ya mara katika ule usiku, ikiwa na ujumbe ule ule, kuwa Bwana Yesu hapaswi kusulubiwa. (Kwasababu maandiko yanasema Mke wa Pilato aliteswa sana katika ndoto).
Mathayo 27:19 “Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, USIWE NA NENO NA YULE MWENYE HAKI; KWA SABABU NIMETESWA MENGI LEO KATIKA NDOTO KWA AJILI YAKE”.
Sasa ndoto hiyo ilitoka kwa Mungu, kwasababu kamwe shetani hawezi kumshuhudia Bwana Yesu kuwa ni mwenye Haki!..wala hawezi kujifitini mwenyewe, kwamaana huku nje kanyanyua jeshi la kutaka kumsulubisha Bwana na wakati huo huo hawezi kumpa ndoto mke wa Pilato kwamba asimsulubishe!.. ni jambo ambalo haliwezekani!. Kwahiyo ni wazi kuwa Ndoto aliyopokea Mke wa Pilato ni kutoka kwa Mungu asilimia mia.
Lakini wakati huo huo maandiko yanasema kuwa KRISTO ni lazima asulubiwe!! Afe, azikwe na siku ya tatu afufuke!.
Sasa swali ni je! Mungu anajichanganya?, huku aseme kuwa Kristo ni lazima asulubiwe na kufa na kufufuka halafu sehemu nyingine amwoneshe mke wa Pilato kuwa Kristo ni mwenye haki hapaswi kusulubiwa?.
Jibu ni la! Mungu kamwe hajichanganyi!..isipokuwa sisi pambanuzi zetu ndizo zinazojichanganya!..
Maandiko yanasema..
Yeremia 23:28 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana. 29 Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?”
Yeremia 23:28 “Nabii aliye na ndoto, na aseme ndoto yake; na yeye aliye na neno langu, na aseme neno langu kwa uaminifu. Makapi ni kitu gani kuliko ngano? Asema Bwana.
29 Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?”
Umeona hapo Ndoto ni MAKAPI na Neno la Mungu ni NGANO.
Ndoto na Maono vina ukweli, lakini si ukweli uliokamilika.. Ndio maana unaona hapo! Mke wa Pilato kaishia kuoneshwa tu kuwa YESU NI MWENYE HAKI HASTAHILI KUSULUBISHWA BASI!!..jambo ambalo ni kweli kabisa!… lakini kiuhalisia sio ukweli uliokamilika, ni ukweli ulio Nusu!!.. Ukweli uliokamilika ni ule unaosema “YESU NI MWENYE HAKI HASTAHILI KUSULUBIWA LAKINI KWAAJILI YA MAKOSA YETU, AMEKUBALI KUFA ILI SISI TUOKOLEWE”..Na ukweli huo huwezi kuupata kwa ndoto wala kwa maono, wala kwa ufunuo binafsi, bali unapatikana tu kwenye Neno la Mungu(biblia)… Ambalo mke wa Pilato alilikosa.. Hivyo ndoto yake ikaishia hapo “Yesu ni Mwenye haki” ikawa ni Mapaki!, ijapokuwa imetoka kwa Mungu!.. Lakini Neno la Mungu likabaki thabiti kuwa Kristo ni mwenye haki lakini lazima afe!.
Luka 9:22 “akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka”.
Je na wewe umewahi kuota ndoto za namna hiyo au zinazokaribia kufanana na hizo, kiasi kwamba ukaamini ni Bwana kazungumza na wewe ? nataka nikuambie USIRIDHIKE TU!..Kwasababu ulichokiona pengine ni ufunuo Nusu!, na si mkamilifu..
Pengine Mungu kakuonesha kwenye ndoto umenyakuliwa? Na ukaamini kuwa ni kweli utaenda mbinguni..lakini ukijitazama bado unavaa vimini, unatukana, unazungumza uongo, unaiba, unazini?.. Fahamu kuwa ndoto uliyoota pengine ni ya Mungu lakini bado ni MAKAPI!, Tafuta kuijua ngano halisi.. Ngano halisi inatufundisha endapo tukiishi maisha matakatifu ndio tutanyakuliwa, hiyo ndio ngano!.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu”.
Hiyo ndiyo Ngano!, ambayo Mungu anaiangalia.. haijalishi umemwona malaika katika ndoto akikwambia kuwa Mungu anapendezwa na wewe!.. Kama wewe ni mwasherati, ulichokisikia kutoka kwa huyo Malaika ni makapi!.. Neno la Mungu litabaki thabiti! Kuwa utaurithi tu uzima wa milele endapo utaacha uasherati wako, hivyo ili maono uliyoyaona yakamilike ni lazima Neno la Mungu liongezeke juu yake kwamba Uache na usherati…. Siku ile hatutahukumiwa kulingana na maono tuliyoyosikia au ndoto tulizoziota au sauti tulizozisikia au mafunuo tuliyoyapata au mahubiri tuliyoyahubiri..bali tutahukumiwa kwa NENO LA MUNGU (mambo yaliyoandikwa ndani ya kitabu cha uzima, ambacho ni BIBLIA).
Je unalithamini NENO?.. Au unaishi kwa ndoto?.. Ndoto zako ni nzuri, na pengine ni kweli zimetoka kwa MUNGU kama za yule mke wa Pilato, lakini je! Neno la Mungu lina nafasi gani katika Maisha yako?. Jazima maono yako nyama kwa Neno la MUNGU, Jazia ndoto zako nyama kwa Neno la Mungu. Mke wa Pilato alikosa Neno tu!, ingawa alikuwa anakipawa cha ndoto, lakini ndoto zake zikawa makapi yapeperushwayo na upepo, na sisi tusilikose Neno, ili maono yetu, ndoto zetu, funuo zetu ziwe thabiti na kamilifu.
Tenga muda mwingi sana (sio kidogo )kusoma biblia, jua nyakati na majira yaliyoandikwa kwenye biblia, tambua uweza wa Neno la Mungu, nguvu ya Neno la Mungu, jifunze kwa undani Maisha ya Bwana Yesu, soma vitabu vyote vya kwenye biblia usiache hata kimoja, tafuta sehemu mbali mbali wanazofundisha Neno la Mungu lisiloghoshiwa, jifunze hapo, linganisha mambo na mistari mbali mbali katika biblia. Na Roho Mtakatifu uliyempokea ambaye anakufunulia mambo katika ndoto atakufunulia pia na maandiko na utakuwa mwenye nguvu nyingi kiroho.
Bwana atubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Mada Nyinginezo:
Je! “Mke wa ujana wako” ni yupi kibiblia?
FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.
CHUKIZO LA UHARIBIFU
Akawaambia Enendeni ulimwenguni mwote,MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE.(Marko16:15.) Yesu Anamaanisha nini kusema MKAIHUBIRI INJILI KWA KILA KIUMBE?
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Rudi nyumbani
Kibiblia Kitanga ni sehemu ya mwisho wa mkono wa Mtu, au mnyama..kwa jina lingine ni kiganja.
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi.
Danieli 5:24-25 [24]Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa. [25]Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.
Huu ni ule wakati mfalme Belshaza wa Babeli alipokuwa ameketi nankufanyia anasa vyombo vitakatifu vya Mungu pamoja na makahaba wake..ndipo hapo hapo kiganja cha mkono kikatokea na kuanza kuandika ukutani maneno hayo, mene mene tekeli na peresi.
Utalisoma Neno hilo pia katika vifungu hivi.
Mambo ya Walawi 14:26-27 [26]kisha kuhani atamimina sehemu ya hayo mafuta katika kitanga cha mkono wake mwenyewe wa kushoto; [27]kisha kuhani atanyunyiza baadhi ya hayo mafuta yaliyo katika mkono wake wa kushoto, kwa kidole chake cha mkono wa kuume mara saba mbele za BWANA;
Mambo ya Walawi 11:27 [27]Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.
Isaya 49:16 [16]Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.
Soma pia; ( 2Wafalme 9:35, Danieli 10:10,
Lakini Je nini tunaweza kujifunza kila tutazamapo kitanga/ vitanga vyetu.?
Ukiwa mwovu..kumbuka kuwa siku moja kitanga cha Mungu kitakuandikia hukumu kama kilivyomwandikia Belshaza mfalme wa Babeli..kama wewe ni mfanyaji wa anasa, ni mzinzi, ni mlevi, ni mchawi, unaabudu sanamu..Bwana atakuadhibu kwa hukumu mbaya sana. Ya mene, mene, tekeli na Peresi.
Ukifikia hii hatua basi habari yako inakuwa imeishia hapo hapo.
Lakini ikiwa wewe unampenda Mungu na kumcha yeye, na kuyafanya maagizo yake..Vilevile ameahidi atakuandika katika vitanga vyake…ikiwa na maana mtu akiandika jambo katika kiganja chake lengo lake ni ili asikusahau, si ndio?..Ndivyo ilivyo kwa Mungu, kwa watu wake wampendao..amewaandika katika viganja vyake kamwe hawezi kuwasahau.
Isaya 49:14-16 [14]Bali Sayuni alisema, YEHOVA ameniacha, Bwana amenisahau. [15]Je! Mwanamke aweza kumsahau mtoto wake anyonyaye, hata asimhurumie mwana wa tumbo lake? Naam, hawa waweza kusahau, lakini mimi sitakusahau wewe. [16]Tazama, nimekuchora katika vitanga vya mikono yangu; kuta zako ziko mbele zangu daima.
Bwana akubariki.
Makanwa ni nini katika biblia? (Danieli 6:22)
Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”
Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?
Mwana anayependwa na wazazi wake ni lazima apitie vipindi vya kurudiwa! (maana yake vya kuonywa, au wakati mwingine kuadhibiwa pale anapokosa). Na kama sisi wanawadamu tunawarudi watoto wetu pale wanapofanya makosa, kadhalika Mungu naye anawarudi watoto wake pale wanapokosa.
Kumbuka sio watu wote wanaorudiwa na Mungu duniani, wengi wanapigwa tu na Mungu.. na wachache sana wanarudiwa.. Wanaorudiwa ni wana wa Mungu na wanaopigwa ni wana wa ulimwengu huu, waliomkataa Mungu.
Kurudiwa ni kitendo cha kurekebishwa kwa adhabu.. Maana yake unaadhibiwa ili ujirekebishe. Bwana Mungu anapomrudia mwana wake, anakuwa anamwonesha kosa lake, huku anamwadhibu, hivyo anayeadhibiwa anajua adhabu hiyo ni kutokana na kosa fulani.
Lakini anayepigwa na Mungu, mara nyingi anakuwa hajui chochote.. kwasababu uhusiano wake na Mungu upo mbali sana.. kama hata kuipambanua sauti ya Mungu hawezi, au haamini hata kuna Mungu atawezaje kujua kuwa anayemwadhibu ni Mungu?. Hivyo ataona mabaya tu yanamjia! Na hatajua chanzo, ndio hivyo atababaika kwenda kutafuta suluhisho huku na huko, hadi hata kwa waganga, kutafuta chanzo cha tatizo lake.
Na wewe kama mwana wa Mungu (yaani uliyemwamini Bwana na kutubu na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu), utapitia hivyo vipindi vya kurudiwa na Bwana.
Unapogundua umefanya jambo fulani ambalo sio zuri, na unaona mkono wa Bwana upo juu yako kutokana na hicho ulichokifanya. Basi huo ni wakati kufanya yafuatayo.
1 . JIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA.
Ukigundua hiyo shida au hasara iliyokupata ni kutokana na Uongo uliousema muda mchache nyuma, fahamu kuwa umerudiwa na Bwana, hivyo ni wakati wa kulitambua hilo kosa na kujifunza, ili siku nyingine usilirudie tena.
Ukiona ajali hiyo uliyoipata ni kutokana na Hasira uliyomwonea ndugu yako muda mchache nyuma, hapo umerudiwa, hivyo jifunze kutokana na makosa.
Ukiona furaha au amani imeondoka ndani yako, na hiyo ni baada ya kumkosa ndugu yangu muda mfupi tu nyuma, fahamu kuwa ni Bwana amekurudi
Ukiona magonjwa fulani, au tabu fulani zimekuandama baada tu ya kuacha Maombi uliyokuwa umezoea kuyaomba jua ni Bwana anakurudi. Hivyo rudia upesi ratiba yako ya kuomba.
Ukiona siku hiyo umekosa chakula, au riziki, baada tu ya wewe kumfungia riziki mwingine jua ni Bwana amekurudi, hivyo jirekebishe haraka sana.
Na mambo mengine yote ni hivyo hivyo… Ukiona kuna vishida au vitabu unavipitia baada ya kuokoka, ni mkono wa Bwana huo juu yako, ni kiboko cha Bwana!.. Na lengo la kurudiwa huko si kukudhoofisha wewe bali kukuimarisha.. ili uwe mkamilifu zaidi..
Ufunuo 3:19 “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu”.
Mfano wa kudharau kurudiwa na Bwana ni pale unapoadhibiwa na unajua kabisa kwamba tatizo hili ni kutokana na kosa lile ulilolifanya, labda kutokana na uwongo uliousema, au kutokana na kiburi ulichokionesha, au kutokana na mawazo mabaya uliyoyawaza n.k, Na baada ya kujua hayo hujifunzi kutokana na makosa hayo, ili wakati mwingine usirudie tena..lakini badala yake unapuuzia!!, unachukulia kiwepesi..hapo umeyadharau marudia ya Bwana kama maandiko yanavyosema..
Waebrania 12:5 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye; 6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye”.
Waebrania 12:5 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye”.
Jambo la tatu: Usizimie moyo, Usife moyo wala usikate tamaa, unapoona unapitia hizo adhabu ndogo ndogo…usikate tamaa kabisa.. Jirekebishe tu na kisha songa mbele, kwasababu ni adhabu ya funzo tu na si ya kukukomoa wewe..
Tusome tena mstari huo..
Waebrania 12:5 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, WALA USIZIMIE MOYO UKIKEMEWA NAYE”
Adhabu siku zote si kitu kizuri!, lakini hatuna budi kuzistahimili maadamu ni kweli tumekosa, Vile vile hatuna budi kuendelea kumpenda Mungu hata kama anatuadhibu!!, Mwana mwenye hekima hawezi kumchukia baba yake au mama yake anapomwadhibu kwa kosa ambalo kweli kalifanya..Kadhalika na sisi hatuna budi kuendelea kumpenda Bwana, na kumtumikia, kwasababu hayo yote yametupata kwa faida yetu sisi na si yake..
Waebrania 12:6 “Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. 7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. 11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. 12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, 13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe”.
Waebrania 12:6 “Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali.
9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani.
12 Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,
13 mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe”.
Je wewe ni mwana halali wa Mungu?.. kumbuka tunafanyika wana kwa kumwamini Bwana Yesu tu peke yake..
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake”.
Kama hujampokea Bwana Yesu, bado wewe ni mwana haramu, asiyeweza kurudiwa.. Na hakuna faida yoyote ya kuwa Mwana haramu, kwasababu huna urithi..hivyo mpokee leo Bwana Yesu na ukabatizwe uweze kuwa mwana wa Mungu.
Maran atha!
MJUE SANA YESU KRISTO.
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?
ADHABU KALI KUTOKA KWA MUNGU, ITAMPATA MTU WA NAMNA GANI?
SWALI: Biblia inaposema mwanamke ataokolewa kwa uzazi wake, inamaanisha nini?
1Timotheo 2:14 “Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. 15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi”.
1Timotheo 2:14 “Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
15 Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi”.
JIBU: Tofauti na inavyotafsiriwa na watu wengi, kwamba andiko hilo linamaanisha kuwa mwanamke yeyote ambaye atakuwa na watoto wa kulea, basi mwisho wa siku ataokolewa kwa kutimiza tu kusudi hilo. Mtazamo ambao sio sahihi na unakinzana na maandiko, Kwasababu kama kila mwanamke angekuwa anaokolewa kwa namna hiyo, hata wanawake wachawi nao wangeokolewa kwasababu na wao pia wanao watoto wa kulea.
Lakini biblia ilimaanisha nini kuandika hivyo?
Mtume Paulo aliandika maneno hayo, kuonyesha jinsi gani huduma ya mwanamke ambaye ana watoto jinsi ilivyo na nguvu hata kusababishia wokovu kwake mwenyewe IKIWA atawalea watoto wake katika misingi ya imani, upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi kama ilivyoainishwa hapo..Na sio kwa kuzaa tu basi.
Kwasababu atakuwa ameifanya huduma ya kuokoa kizazi kingine.. Tengeneza picha kama wanawake wote ulimwenguni wangekuwa wanatimiza wajibu wao huu wa kuwalea watoto wao katika misingi ya imani, leo hii, kusingekuwa na haja ya kuhubiri injili kwasababu watoto wote wangekuwa tayari wanamjua Mungu. Lakini injili imekuwa ngumu kwa kizazi cha sasa kwasababu jambo la kwanza mzazi analolithamini kwa mtoto wake ni elimu tu, Mungu ni ziada, mtoto akifaulu darasani ndio furaha yake kubwa, wakati hajui hata mstari mmoja wa biblia. Hajui hata pambio moja la kumsifu Mungu. Mzazi haoni aibu hata mtoto wake anakuwa hadi mtu mzima hajui biblia ina vitabu vingapi.
Kwahiyo hapo mtume Paulo alikuwa anaonyesha nguvu iliyopo katika mwanamke kulea watoto wake vema, ambayo mwisho wa siku itampelekea hata na wokovu wake mwenyewe. Kwamfano Mungu akiona mtoto Yule ambaye alilelewa katika misingi kama Samweli, amekuwa sababu ya wokovu kwa Israeli, unategemea vipi Mungu amwache mama aliyemlea?. Ni sawa tu na yule anayewavuta watu kwa Kristo, ambao biblia inasema kitendo hicho kina nguvu ya kuokoa roho ya mhubiri na kufunika wingi wa dhambi zake.
Yakobo 5:20 “jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi”.
Kwahiyo ikiwa wewe ni mwanamke na Mungu kakujalia watoto ujue jukumu lako la kwanza, la injili ni kwa watoto wako, hakikisha hao wanakuwa katika misingi ya kumcha Mungu, wafundishe, na pale wanapokosea Mungu kakupa ruhusu ya kuwaadhibu, lengo ni kuwaweka katika mstari wa kumcha Bwana, na sio kuwatesa. Ukifanya hivyo matokeo yake utakuja kuyaona baada ya haya maisha hapa duniani.
Tito 2:4 “ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; 5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe”.
Tito 2:4 “ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao;
5 na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe”.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.
Raheli aliwalilia vipi watoto wake?
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.
Tusome,
Kutoka 3:5 “Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Viatu Musa alivyoambiwa avivue ni vya mwilini kabisa!, na si vya rohoni. Na tunasoma si tu Musa peke yake bali hata Yoshua kuna mahali alifika akaambiwa avue viatu vyake (Yoshua 5:15).
Katika agano la kale Usafi mbele za Mungu ulithibitishwa kwa vitu vya nje!…kama kuoga, kunawa, kutawadha, kufua n.k! Kwamfano watu walikuwa hawali chakula kabla hawajanawa mpaka kwenye viwiko..Mtu yeyote aliyekula bila kunawa alionekana ni mchafu (najisi), mbele za Mungu na wanadamu.
Marko 7:2 “wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa. 3 Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao 4 tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.”.
Marko 7:2 “wakaona wengine katika wanafunzi wake wakila vyakula kwa mikono najisi, yaani, isiyonawiwa.
3 Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao
4 tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.”.
Ndivyo Mungu alivyotembea na watu wa agano la kale. (Usafi ulithibitika kwa vitu vya nje). Ndio maana tunaona hata hapo Musa alipokutana na Mungu alimwambia avue viatu vyake, kadhalika wakati Fulani Mungu alipotaka kukutana na wana wa Israeli na kusema nao katika mlima huo huo, aliwaambia wafue nguo zao wawe safi (Kutoka 19:10).
Sasa kwanini Musa aambiwe avue viatu na si kitu kingine?.. Viatu ni vazi linalokanyaga uchafu wa kila aina njiani, kiatu hicho hicho hapa kinakanyaga taka, mbele kidogo kinakanyaga mavumbi..mbele tena kidogo kinakanyaga kinyesi cha mtu au mnyama.. hivyo si kitu kisafi!. Ndio maana Musa akaambiwa avue viatu vyake.
Lakini je! Hiyo ni sheria hata sasa?, kwamba tukitaka kwenda kwenye nyumba za ibada kukutana na Mungu ni lazima tuvue viatu vyetu, au tuoge au tutawadhe ili tusiwe najisi mbele za Mungu?
Jibu ni la!, Usafi wa nje, hautosogezi karibu na Mungu. Kutokuoga na kuingia kwenye nyumba ya ibada hakutufanyi tukataliwe na Mungu, vile vile kuingia katika nyumba ya Mungu na viatu mguuni hakutufanyi tuwe najisi.
Bwana Yesu alisema…
Mathayo 15:16 “Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili? 17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? 18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19 Kwa maana MOYONI HUTOKA MAWAZO MABAYA, UUAJI, UZINZI, UASHERATI; WIVI, USHUHUDA WA UONGO, NA MATUKANO; 20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; LAKINI KULA KABLA HAJANAWA MIKONO HAKUMTII MTU UNAJISI”.
Mathayo 15:16 “Yesu akasema, Hata sasa ninyi nanyi mngali hamna akili?
17 Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.
19 Kwa maana MOYONI HUTOKA MAWAZO MABAYA, UUAJI, UZINZI, UASHERATI; WIVI, USHUHUDA WA UONGO, NA MATUKANO;
20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; LAKINI KULA KABLA HAJANAWA MIKONO HAKUMTII MTU UNAJISI”.
Lakini hiyo haitupi amri ya kuwa wachafu wakati wote!, kwamba tuifanye nyumba ya Mungu jalala!..au tusiwe watu wa kuoga, au tusiwe watu wa kunawa mikono kabla ya kula!. Tuna wajibu wa kuwa wasafi kwa kadri tuwezavyo!..na kuifanya nyumba ya Mungu kuwa safi wakati wote, kama viatu vina matope ni vizuri kuvisafisha nje kabla ya kuingia navyo ndani kwenye nyumba ya ibada (Hiyo inahitaji tu akili za kawaida, kupambanua!).. lakini sio kulifanya jambo hilo ndio msingi wa kumkaribia Mungu. La! Hatumkaribii Mungu kwa hayo mambo.
Hivyo tunapaswa tuvue viatu vya roho zetu, na si vya mwilini, viatu vyetu vya rohoni ndivyo vinavyobeba uchafu wa kila aina wa haya maisha!, ambao ndio huo Bwana alioutaja.. Uongo, mawazo mabaya, uasherati, uzinzi, wizi na mengine yote yanayofanana na hayo,
Je! Umempokea Yesu?, umeoshwa dhambi zako kwa damu?, viatu vya moyo wako umevivua?
Bwana Yesu yu karibu!
Gidamu ni nini? Kwanini Yohana alisema hastahili kuzilegeza gidamu za Yesu?
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Bwana wetu Yesu Kristo atukuzwa. Ni siku nyingine tena tumepewa neema ya kuiona, hivyo nakukaribisha tujifunze Neno la Mungu, maadamu siku yenyewe inakaribia.
Kama vile “Utakatifu na utakaso” vinavyokwenda Pamoja, vivyo hivyo, “Dhambi na Unajisi” ni vitu vinavyokwenda bega kwa bega.
Tofauti na Dhambi na unajisi ni ipi?
Dhambi ni kitendo mtu anachofanya kinyume na Mungu, na huwa inaambatana na kuvunja sheria, au maagizo yake. Kama vile kuzini, kuua, kuabudu sanamu n.k.
Lakini unajisi ni kitendo mtu anachokifanya kinyume na yeye mwenyewe, ambacho mwisho wa siku kinampelekea, Mungu kujitenga naye au kumuacha kwa muda Fulani.
Mtu mwenye dhambi unajisi hauna nguvu kwake bali dhambi tu, ..Lakini mtu aliyeokoka vyote vina madhara kwake, yaani dhambi na unajisi.
Ni sawa na doa jeusi lililopo katika shati, jeupe, doa hilo lingekuwa katika shati jeusi, shati hilo lingeendelea kuvalika kwasababu doa halionekani, lakini likiwa katika shati jeupe hata kama litakuwa safi vipi, doa lile tayari limeshaharibu kila kitu. Sasa huo ndio unajisi. Ambao mtu mchafu, hauna madhara yoyote kwake, lakini kwa msafi ni pigo kubwa.
Sasa kabla kufahamu Zaidi, embu tuangalie kwa agano la kale baadhi ya unajisi ulikuwa katika mambo gani.
Zamani, ilikuwa ukila au ukishika mzoga wa wadudu, au Wanyama ambao ni najisi, adhabu yake ilikuwa na wewe unakuwa najisi, kwa muda wa siku nzima..
Walawi 11:23 “Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu. 24 Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Walawi 11:23 “Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu.
24 Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Soma pia Walawi 11:29-32
Halikadhalika, kulikuwa na unajisi, wa kujifungua, ikiwa mwanamke atajifungua tu, kile kitendo cha kutokwa damu, tayari ni unajisi ambao unakugharimu siku saba, Pamoja na hayo, unajisi huo ulimgharimu siku nyingine tena 33, au 66 ikiwa ni mtoto wa kiume.. Kufanya jumla ya siku 40 kwa wa kiume, na siku 80 kwa wakike.
Unajisi huu ulikuwa pia katika kugusa maiti, au kutokwa na uchafu mwilini Soma(Walawi 15:16-20). Ulikuwa unakuwa najisi kwa muda wa siku 7, baada ya kujitakasa.
Sasa nachotaka uone ni kuwa, makosa kama haya aliyafanya mtu juu yake mwenyewe, ambayo hata huwezi kuyaona katika zile amri 10, lakini Mungu aliyatazama sana.
Katika agano la kale, wapo ambao walikuwa wanajitahidi kutotenda dhambi, yaani hawazini, hawaabudu sanamu, hawaibi, wanazitunza sabato n.k.
Lakini walikuwa wanakoseshwa na vitu vidogo tu kama hivyo vya unajisi, Na hivyo vikawa vinatia doa ukamilifu wao. Na matokeo yake, wakawa hawaruhusiwi kuingia hemani kwa Mungu, au katika mkusanyiko wowote wa watakatifu kwa kipindi Fulani, kulingana na aina ya unajisi wenyewe.. kama ni siku moja, au wiki, au miezi..
JE! Katika agano jipya unajisi upoje?
Unajisi wa sasa sio kama ule wa zamani, wa kushika, au kuionja, au kutokwa na vitu mwilini hapana.. Unajisi wa sasa wa mtu upo moyoni, Bwana Yesu alisema hivi;
Mathayo 15:17 “Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni? 18 Bali vitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi. 19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano; 20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi”.
Mathayo 15:17 “Hamjafahamu bado ya kuwa kila kiingiacho kinywani hupita tumboni, kikatupwa chooni?
19 Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
20 hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi”.
Kama tunavyosoma, hapo, yale mambo ambayo yanakutoka moyoni, kama vile tamaa, uzinzi, uasherati, n.k. Sasa kumbuka hasemi kufanya uzinzi, au uasherati, bali kukutoka..yaani mawazo ya uzinzi au ya uasherati, hayo ndiyo yanayokutia wewe unajisi, kama mtakatifu.
Unaweza kweli ukawa huzini na wanawake, lakini kuruhusu tu tamaa ndani yako, tayari umeshajitia unajisi, unaonekana kama vile tayari umezini sawasawa na maneno ya Bwana Yesu (Mathayo 5:28).
Na matokeo yake, inaweza kukuchukua kipindi Fulani kirefu, usiuone uwepo wa Mungu maishani mwako, kwasababu ya unajisi tu kama huo.
Pengine, unawasengenya wengine, unatukana, una chuki na wengine, kiburi, kijicho n.k.(Soma Marko 7:17-23) mambo kama hayo yanaweza kukufanya uikose furaha ya wokovu kwa kipindi kirefu sana, hata baada ya kutubu kwako.
Hivyo unajisi ni wakujiepusha nao sana wewe kama mtakatifu wa Mungu, unaweza ukawa hauuji lakini kitendo tu cha kumchukia ndugu yako, tayari ni sawa na muuji. Umeshajitia unajisi.
Ili uendelee kubaki katika uwepo wa Mungu wakati wowote, uulinde sana moyo wako.
Bwana atusaidie sana.
Lumbwi ni nini katika biblia?
JIEPUSHE NA UNAJISI.
UTAKASO NI SEHEMU YA MAISHA YA MKRISTO YA KILA SIKU.
SHINA LA UCHUNGU, LISICHIPUKE NDANI YETU.
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Nakusalimu katika jina kuu sana la Bwana wetu Yesu Kristo, Karibu tuyatafakari maneno ya uzima, ambayo pekee ndio yanayoweza kutufanya sisi tuwe huru kweli kweli hapa duniani( Yohana 8:32).
Leo tutajifunza, kanuni mojawapo ya kibiblia ambayo itatusaidia sisi kuweza kupokea jumbe, au mafunuo, au maarifa sahihi kutoka kwa Mungu, Imenisaidia mimi, naamini pia itakusaidia na wewe.
Kanuni ya sisi kuzungumza na Mungu, ni tofauti na ya kwake kuzungumza na sisi. Sisi tukitaka kuwasiliana naye tunachofanya ni moja kwa moja kwenda katika uwepo wake, na kupiga magoti na kupelekea haja zetu kwake, Na tukishamaliza tutanyanyuka na kuondoka na kwenda katika shughuli zetu.
Lakini Mungu, hana utaratibu huo wa kuzungumza na wewe papo kwa papo, kwa wewe ufanyavyo. Na hiyo imewafanya watu wengi wakate tamaa, pale wanapoona hakuna mwitikio wowote, kutoka upande wa pili wa Mungu.
Lakini leo tutajifunza kanuni ambayo muhimu sana kuizingatia ikiwa wewe unataka kumsikia Mungu, au kupokea mafunuo sahihi kutoka kwake.
NA KANUNI YENYEWE NI “UTULIVU”
Sauti ya Mungu ya kweli ipo katika utulivu, na si mahali pengine, Eliya alikuwa ni nabii ambaye Bwana anazungumza naye na kumpa taarifa nyingi, lakini hakuwahi kuisikia sauti ya Mungu vizuri, hadi siku ile alipokuwa katika utulivu, na ndio maana utaona akaufunika uso wake, alipomsikia (kuonyesha kuwa amemwona Mungu, hivyo hastahili hata kuzungumza naye). Lakini mara nyingine zote huko nyuma hakuwahi kuufunika uso wake. Utajiuliza ni kwanini? Ni kwasababu Mungu hakuwa karibu naye kama alivyomwona siku hiyo, alipokaa katika utulivu (1Wafalme 19:9-13).
Elisha alipotaka kupokea taarifa sahihi, na maagizo kutoka kwa Bwana juu ya nini yafanye yale mataifa matatu yaliyotaka kuangamizwa na taifa la Moabu,..hakukurupuka tu na kuzungumza na Bwana, bali alitaka kwanza kukaa katika utulivu, akamwita mpiga kinanda,aimbe naye nyimbo za kumsifu Mungu, ndipo taarifa sahihi zikamshukia baadaye.
2Wafalme 3:14 “Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe. 15 Ila sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga, mkono wa Bwana ukamjia juu yake. 16 Akasema, Bwana asema hivi, Fanyeni bonde hili lijae mahandaki. 17 Kwa kuwa Bwana asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji; nanyi mtakunywa, ninyi, na ng’ombe zenu, na wanyama wenu. 18 Na jambo hili ni jepesi machoni pa Bwana; pia atawatia Wamoabi mikononi mwenu”.
2Wafalme 3:14 “Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe.
15 Ila sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga, mkono wa Bwana ukamjia juu yake.
16 Akasema, Bwana asema hivi, Fanyeni bonde hili lijae mahandaki. 17 Kwa kuwa Bwana asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji; nanyi mtakunywa, ninyi, na ng’ombe zenu, na wanyama wenu.
18 Na jambo hili ni jepesi machoni pa Bwana; pia atawatia Wamoabi mikononi mwenu”.
Vilevile Mungu alipotaka kuzungumza na Musa, ili kumpa zile mbao mbili za amri na sheria yake, alimwita mlimani, , lakini utaona Musa hakwenda moja kwa moja tu,hadi kileleni bali ilimbidi asubirie chini kwa muda wa siku sita (6). Ndipo siku ya saba akasikia sauti ya Mungu ikimwita apande mlimani.
Kutoka 24:15 “Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima. 16 Na huo utukufu wa Bwana ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu. 17 Na kuonekana kwake ule utukufu wa Bwana kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli. 18 Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arobaini, mchana na usiku”.
Kutoka 24:15 “Musa akapanda mlimani, lile wingu likaufunikiza mlima.
16 Na huo utukufu wa Bwana ukakaa juu ya mlima wa Sinai; lile wingu likaufunikiza siku sita; na siku ya saba akamwita Musa toka kati ya lile wingu.
17 Na kuonekana kwake ule utukufu wa Bwana kulikuwa kama moto uteketezao, juu ya mlima machoni pa wana wa Israeli.
18 Musa akaingia ndani ya lile wingu, akapanda mlimani; Musa akawa humo katika ule mlima siku arobaini, mchana na usiku”.
Kwa mifano hiyo michache ni kutuonyesha na sisi kuwa, tukitaka tumsikie Bwana, hatuna budi kuwa katika utulivu rohoni, kwamfano unapokwenda kuomba, usiishie kuzungumza tu maneno yako halafu basi unaondoka, mpe Bwana nafasi, kaa chini imba, baadaye tafakari uweza wa Mungu, soma biblia, tafakari tena, kisha rudia tena kuomba.. kwa jinsi unavyokaa sana katika uwepo wa Mungu, ndivyo unavyompa nafasi Mungu ya kushuka na kukuhudumia.
Ghafla tu utaona wingu linakushukia roho, na hapo hapo unapokea ufunuo au maarifa, au taarifa Fulani ambazo hukuwahi kuziwaza au kuzifikiri, hapo ujue tayari ni Mungu huyo, au utapokea amani Fulani, au ufumbuzi Fulani, au agizo Fulani, hapo ujue Mungu anazungumza na wewe. Lakini inahitaji utulivu wa kitambo kidogo, wakati mwingine hata masaa kadhaa. Ni kweli yapo majira utaomba tu na kuondoka, lakini yapo majira ni lazima ujiwekee muda kwa Mungu, apate nafasi ya kusema na wewe.
Vilevile, yafanya Maisha yako, yawe katika utulivu, ukiwa ni mtu wa kukesha tu mitandaoni, kuchat chat kwenye magroup, au muda wote kutazama tazama, tv au tamthilia, au muvi, miziki au michezo michezo, au kuzurura zurura, leo party hii, kesho ile.. Fahamu kuwa mambo kama hayo ni adui mkubwa sana wa Mungu kuzungumza na wewe, haijalishi utakuwa ni mwombaji kiasi gani, hutakuwa unaona mwitikio wowote kutoka kwa Mungu. Hiyo ni kwasababu haupo katika utulivu.
Kuwa mtulivu maishani, tumia muda wako, kusikiliza nyimbo za sifa kama Elisha alivyokuwa anafanya, tumia weekend zako kwenda mikesha kuomba, soma sana biblia, punguza marafiki ambao ni maadui wa Imani yako, zungumza sana Habari za Kristo, katika mazungumzo hayo utaona ufunuo unaingia ndani yake, kwasababu Kristo kashaungana nawe katika kinywa chako kama ilivyokuwa kwa wale watu wawili wa Emau (Luka 24:13)
Ukizingatia hivyo. Utamsikia, kama sio kupokea mafunuo mengi kutoka kwake, daima jiweke katika utulivu.
Sote tunatamani Mungu azungumze nasi, lakini tumekuwa na wasiwasi, tukadhani kuwa Mungu yupo mbali sana, na anasema tu na watumishi wakubwa, au manabii, hawezi kusema na wewe. Ukweli ni kwamba, Karama ya mtu, sio kigezo cha Mungu kuzungumza naye, haijalishi atasikia sauti, au maono, au ndoto nyingi kiasi gani. Mungu anaweza kuzungumza na kila mtu, kulingana na njia yake mwenyewe aliyotaka azungumze naye.
Japokuwa Eliya alikuwa karibu sana na Mungu, na kupokea maono mengi, na taarifa nyingi kutoka kwa Yehova, lakini hakuwahi kumsikia Mungu mwenyewe, na ndio maana hakuwahi kuufunika uso wake, maana yake hakusitiri uovu wake, alipokuwa anaongea na Mungu hadi siku ile alipokaa katika utulivu na ndio akamsikia Bwana kwa mara nyingine.,
1Wafalme 19:9 “Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya? 10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe. 11 Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi; 12 na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu. 13 Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya?”
1Wafalme 19:9 “Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya?
10 Akasema, Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanitafuta roho yangu, waiondoe.
11 Akasema, Toka, usimame mlimani mbele za Bwana. Na tazama, Bwana akapita; upepo mwingi wa nguvu ukaipasua milima, ukaivunja-vunja miamba mbele za Bwana; lakini Bwana hakuwamo katika upepo ule; na baada ya upepo, tetemeko la nchi; lakini Bwana hakuwamo katika lile tetemeko la nchi;
12 na baada ya tetemeko la nchi kukawa na moto; lakini Bwana hakuwamo katika moto ule; na baada ya moto sauti ndogo, ya utulivu.
13 Ikawa, Eliya alipoisikia, alijifunika uso wake katika mavazi yake, akatoka, akasimama mlangoni mwa pango. Na tazama, sauti ikamjia, kusema, Unafanya nini hapa, Eliya?”
SAUTI YA MUNGU IPO KATIKA UTULIVU.
Jambo ambalo, wakristo wa sasa tunalikwepa sana,
NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?
USIISHI KWA NDOTO!
TEGEMEA MUNGU KUZUNGUMZA NAWE KATIKA MAMBO MADOGO
KUNA MAJIRA MUNGU ATAIVURUGA MIPANGO YETU.
1Petro 1:13 “Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo. 14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu”.
1Petro 1:13 “Kwa hiyo vifungeni viuno vya nia zenu, na kuwa na kiasi; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.
14 Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu”.
Popote panapozungumziwa “kujifunga viuno” katika biblia panamaanisha “kuwa na utayari”. Kama ni msomaji mzuri wa biblia utakumbuka kipindi wana wa Israeli wanatolewa Misri na Mungu, ile siku ya kwanza, wakiwa wanamla Yule pasaka, Bwana Mungu aliwaambia wamle huku wamevaa viatu vyao miguuni, na kujifunga mikanda viunoni (maana yake wawe katika mazingira ya kuondoka)..sio wawe katika mazingira ya kulala baada ya kula, bali mazingira ya kuondoka baada ya kula.
Kutoka 12:10 ‘Wala msisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. 11 Tena mtamla hivi; MTAKUWA MMEFUNGWA VIUNO VYENU, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana”.
Kutoka 12:10 ‘Wala msisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto.
11 Tena mtamla hivi; MTAKUWA MMEFUNGWA VIUNO VYENU, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya Bwana”.
Kwahiyo “kujifunga viuno” kunamaanisha “kujiweka tayari”. Hivyo tunaposema “tujifunge viuno vya akili zetu” tutakuwa tunamaanisha “tuwe tayari kiakili”.. Vile vile tunaposema “tujifunge viuno vya roho zetu, wakati wa kumngojea Bwana”..tutakuwa tumemaanisha “tujiweke tayari katika roho zetu katika kumngoja Bwana” kama Bwana alivyosema katika Luka 12:35..
Luka 12:35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; 36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara. 37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia”.
Luka 12:35 “Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka;
36 nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
37 Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia”.
Vile vile tunaposema “tujifunge viuno vya Nia zetu” maana yake ni “tuwe/tujiweke tayari Nia zetu” Kwa jambo fulani linalofuata.
Kwahiyo huo mstari wa 1Petro 1:13 badala ya kusema “vifungeni viuno vya Nia zenu”…tunaweza kuuweka hivi “Kwa hiyo kuwenu tayari katika Nia zenu; mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo”.
Je! Na sisi viuno vyetu vimefungwa?…tupo tayari katika Nia zetu?, Tupo tayari kwenda mbinguni?..Tupo tayari kuihubiri injili?, tupo tayari kumtumikia Mungu kwa mioyo yetu yote na nguvu zetu zote?
2Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; 2 lihubiri neno, UWE TAYARI, WAKATI UKUFAAO NA WAKATI USIOKUFAA, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”.
2Timotheo 4:1 “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
2 lihubiri neno, UWE TAYARI, WAKATI UKUFAAO NA WAKATI USIOKUFAA, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”.
Hizi ni siku za Mwisho na Kristo anarudi siku yoyote, na atakaporudi alisema atarudi na ujira wake..
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”.
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
KIKWAZO CHA EUODIA NA SINTIKE.
Je ni sahihi kuweka walinzi kulinda mali zetu?
Ni kwa namna gani, upendo husitiri wingi wa dhambi? (1Petro 4:8).
CHAMBO ILIYO BORA.
Unaweza kujiuliza je! Sisi tumeitiwa kutumbuiza?.. Jibu ni Ndio! sisi tumeitiwa kutumbuiza lakini si kwenye majukwaa ya dansi au anasa. Bali mbele za Malaika na wanadamu kupitia Maisha yetu ya usafi na utakatifu!.
1Wakorintho 4:9 “Maana nadhani ya kuwa Mungu ametutoa sisi mitume mwisho, kama watu waliohukumiwa wauawe; kwa sababu TUMEKUWA TAMASHA KWA DUNIA; kwa malaika na wanadamu”.
Maana yake Maisha yetu ni kama tamthilia inayotazamwa!, ambayo baada ya kuisha itatolewa hukumu kama ni nzuri au mbaya!.
Kutumbuiza ni kitendo cha kuonesha ujuzi wako na kipaji chako mbele ya watu wanaokuzunguka kwa lengo la kupata fedha!,
Wanaoimba na kucheza dansi kwenye majukwaa wanatumbuiza!, wanaoruka sarakasi kwenye majukwaa huku wanaimba wanakuwa wanatumbuiza, wanaocheza na nyoka mbele za umati wanakuwa wanatumbuiza! N.k
Leo napenda tuangalie kibiblia hii namna ya kutumbuiza kwa kutumia nyoka.
Kipindi cha Nyuma kidogo!, na hata sasa katika nchi baadhi, kuna mchezo wa kutafuta nyoka wenye sumu kali (kama Kobra), na kisha kujifunza kuwapumbaza kwa nyimbo na sauti za filimbi, na kwenda nao kufanya maonyesho kwenye matamasha kwa lengo la kupata fedha!, Watu walipowaona watu hao wanauwezo wa kusimama mbele ya Nyoka wenye sumu bila kudhuriwa, waliburudika na kuwapa fedha nyingi kuliko hata wale waliokuwa wanaruka sarakasi au kuimba tu peke yake!, kwasababu ni jambo ambalo lilikuwa si la kawaida!.
Lakini pamoja na hayo ulikuwa ni mchezo wa hatari sana, kwani endapo ikitokea ajali yule Nyoka akamwuma yule Mtumbuizaji, basi mchezo ndio umeishia pale pale na hakuna fedha yoyote atakayopata huyo mtumbuizaji!, Hivyo ilihitaji umakini mkubwa..
Sulemani kwa hekima alisema..
Mhubiri 10:11 “NYOKA AKIUMA ASIJATUMBUIZWA, BASI HAKUNA FAIDA YA MTUMBUIZI”.
Hii ni hekima ya kidunia tu ambayo Sulemani aliitoa kwa kutazama Maisha ya watumbuizaji!. Lakini hakuisema tu hiyo hekima kutufurahisha!, la!, bali hekima hiyo ina funzo kubwa sana kwetu wakristo ndio maana ipo kwenye biblia!, ingekuwa haina funzo lolote isingewekwa kwenye biblia.
Na sisi wakristo ni watumbuizaji!, Na Nyoka ni adui yetu shetani!..ambaye anasimama kutupinga siku zote!, akitafuta kutudhuru siku zote katika Maisha yetu ya hapa duniani, Na mbingu inatutazama tutaumalizaje mchezo wetu!, jinsi gani tutampumbaza shetani mpaka mwisho, ili tupokee Tuzo bora!.
Endapo tukisimama mpaka mwisho wa muda wetu bila kuangushwa na shetani aliyeko mbele yetu basi tutapokea tuzo kubwa sana mbinguni, lakini tukiumwa na shetani kama maandiko yasemavyo hapo juu.. “Nyoka akiuma asijatumbuizwa, Basi hakuna faida ya mtumbuizi”.
Hatuna faida yeyote tutakayoipata endapo tukiruhusu shetani atuangushe.
Sasa tunampumbazaje shetani?
Zamani hawa watu waliokuwa wanawapumbaza nyoka!, walitumia sauti za filimbi, walikuwa wanazipuliza filimbi zile kwa ustadi, na walikuwa hawapotezi umakini katika hilo, walijua kwa kupoteza umakini kidogo tu!, wale nyoka akili zao zinawarudia na kuwadhuru!..Sasa zile filimbi hazikuwa zinawaburudisha wale nyoka hata washindwe kuwauma..la!, bali zilikuwa zinawachanganya!..zinawafanya wale nyoka, wakose sababu ya kuwauma!..kwani nyoka ili amuume mtu, ni lazima apate shabaha ya utulivu katika akili yake, sasa zile sauti za filimbi zilikuwa zinawakosesha shabaha, hivyo wanakuwa wanababaika na kusubiri wakati zitakapotulia..
Sasa wakati zile sauti zinawapumbaza wale nyoka, wakati huo huo zinawafurahisha watazamaji..
Na sisi wakristo ili shetani ashindwe juu ya Maisha yetu!, hatuna budi muda wote tupulize filimbi zetu za kiroho, huku tukimkabili adui yetu shetani. Na wakati filimbi hizo zinampumbaza shetani na majeshi yake, wakati huo huo zitakuwa zinaifurahisha mbingu.
Sasa Filimbi hizo za kiroho ni zipi?
Zifuatazo ni filimbi za kiroho.
1/Utakatifu
3/Maombi
4/Kusoma Neno
2/Ushuhudiaji
Tukizipuliza filimbi hizi Nne!, basi shetani atakuwa hana nguvu zozote kwetu, atakuwa kama ZUZU!, mpaka tunamaliza safari yetu hapa duniani!.
Na faida kubwa ya kumfanya shetani zuzu hapa duniani ni Thawabu kubwa kule mbinguni, na heshima kubwa!..kwasababu yeye aliyekuwa anajiona ni kitu!, amekuwa takataka mbele yetu!.
Bwana atusaidie tusiyapunguze mambo hayo..Maana tukipunguza utakatifu, Maombi, Kusoma Neno, na Ushuhudiaji basi tunamrejeshea shetani shabaha yake!, na akituangusha basi anguko letu linakuwa kubwa na hatutakuwa na thawabu yoyote baada ya Maisha haya.
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
Wale Nyoka wa Moto jangwani, walikuwa ni wa namna gani?
TUMEPEWA AMRI YA KUKANYAGA NGE NA NYOKA.
KUOTA NYOKA.
SWALI: Biblia inamaana gani kusema Yesu atawachunga kwa fimbo ya chuma..kwanini iwe ya chuma?
Ufunuo wa Yohana 19:15 [15]Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
JIBU: Fimbo ya mchungaji sikuzote ni fimbo ya mti…ambayo ukichapwa haiwezi kukuletea madhara makubwa sana, zaidi ya maumivu tu mwilini..
Lakini tengeneza picha unapigwa kwa chuma iliyoundwa kwa mfumo wa fimbo..kama vile nondo ngumu..unategemea ni nini kitatokea hapo katika mwili? Sio kusikia tu maumivu lakini pia kuharibika kwa baadhi ya viungo kama vile misuli na mifupa kuvinjika kutatokea. Na kama ukipigwa sehemu mbaya kama vile kichwani..moja kwa moja ni mauti. Kwasababu anayekupiga hana lengo la kukuadhibu bali kukuharibu.
Ndivyo inavyomuonyesha Bwana Yesu, atakapokuja kuwa katika ule utawala wa miaka 1000 hapa duniani.
Kama vile tunavyosoma katika maandiko kuwa yeye ni mchungaji mwema (Yohana 10:14-16)..Ikiwa anamaanisha kuwa Leo hii anatuchunga kondoo wake kwa fimbo ya mti, na ndio maana anapotuadhibu hatuangamii kabisa kwasababu sisi ni kondoo anayetupenda na kututakia mema, anafanya hivyo kwa lengo la kitufanya tu tusitoke katika njia adui akatuangamiza.
Lakini atakapokuja na kutawala kama mfalme wa wafalme biblia inatuambia Amani itatawala duniani kote…kiasi kwamba waovu watakuwepo lakini kwa ule utiisho wake tu, hakuna dhambi yoyote itakayochukua nafasi, kwani adhabu zitakuwa kali kwa watu watakaojaribu kuipindisha amani.
Kwasababu wakati huo atakuwa hachungi kondoo tena kwasababu watakuwa wameshaokolewa, bali atashughulika na mbwa mwitu, hao ndio watapigwa kwa fimbo hiyo kali.
Isaya 65:20 [20]Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa.
Hiyo ndio fimbo ya chuma..uovu wala waovu hawatavumilika kwa namna yoyote ile..Vilevile kushindwa kutekeleza maagizo ya ufalme wa Bwana Yesu utakumbana tu na fimbo hiyo ya chuma. Soma (Zekaria 14:17-20).
Kumbuka Jambo hilo atalitekeleza Kristo pamoja na watakatifu wake, wale ambao waliushinda huu ulimwengu wakaenda naye katika unyakuo.
Ufunuo wa Yohana 2:26-27 [26]Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa, [27]naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu.
Hivyo ni vizuri ukafahamu kuwa Kristo anazo fimbo mbili…Ni heri sasa ukubali kuchungwa naye kwa fimbo ya miti…wakati utafika kabla hata ya utawala wenyewe kuanza…fimbo hiyo ya chuma ataipitisha kwa ulimwengu mzima, kwa yale mapigo atakayoyashusha humu ulimwengu ili kuwaangamiza wote..
Si jambo la kulitamani hata kidogo. Ni heri umpe Kristo maisha yako leo hii ayaokoe, akupe uzima wa milele. Hizi ni nyakati za mwisho. Unyakuo upo mlangoni.
Ikiwa utapenda kupata somo lote la utawala wa miaka 1000 wa Yesu Kristo utakavyokuwa..nitumie ujumbe inbox kwa namba hii +255693036618..nikupe somo lake.
UTAWALA WA MIAKA 1000.
Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasichukue chochote isipokuwa fimbo tu?
Ni kwa namna gani Yesu ni Simba wa Yuda?
Nini maana ya Dirii, Chepeo na Utayari?
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?