Matendo 9:36 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
Matendo 9:36 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa.
37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani.
Bwana Yesu asifiwe..
Ulishawahi kujiuliza kulikuwa na umuhimu gani, biblia kueleza tafsiri ya jina la mwanafunzi huyu aliyeitwa Tabitha?. Ukishaona mahali Fulani tafsiri ya jina la mtu inatolewa basi ujue kuna jambo Mungu anataka tujifunze, kwa huyo.
Mfano wa mtu mwingine kama Tabitha alikuwa ni Petro, Ukisoma Yohana 1:42, Bwana Yesu anafunua tafsiri ya jina lake.
Yohana 1:42 “Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).”
Unaona, kulikuwa na sababu ya Bwana kueleza tafsiri ya lile jina kwamba ni Jiwe/mwamba , ikiwa na maana kuwa zipo tabia, ambazo alikuwa nazo, au atakuja kuzionyesha zinazomwakilisha JIWE KUU mwenyewe ambaye ni Yesu Kristo..
Jambo hilo utalithibitisha mbeleni kidogo, katika Ufunuo alioupata kutoka kwa Mungu, kuhusiana na Bwana wetu Yesu Kristo, tusome;
Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.
Mathayo 16:15 “Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni”.
Umeona akiwa anamaanisha kuwa juu ya mwamba(yaani Ufunuo alioupata kuhusiana na Yesu ni nani), ndio Bwana Yesu atalijengea kanisa lake hapo. Kwahiyo utaona kutolewa tafsiri ya jina lake tangu kule mwanzoni ni kwasababu ya matendo au funuo alizokuwa anazipata kuhusiana na Yesu Kristo, kama msingi wa Kanisa.
Sasa tukirudi kwa Tabitha naye, tafsiri ya jina lake linatolewa, kwamba ni PAA.
Paa, ni aina ya swala. Mwanzoni nilitafakari sana kwanini aitwe swala, asiitwe labda simba, au au kifaru, au dubu, majina yenye sifa, lakini badala yake anaitwa swala.
Je swala anatabia gani nzuri?
Swala ni mnyama ambaye ni mwepesi sana, miguu yake ipo haraka mno, na ni mwepesi wa kurudia juu, kiasi kwamba akikimbia, katika nyasi ndefu au uwanda tambarare, hata simba hawezi kumkamata, mnyama pekee pirini ambaye anaweza kumkimbiza swala (Paa). Ni duma tu peke yake, tena kumpata kwake ni kwa shida sana.
Hivyo hiyo inamfanya, awe salama muda mwingi, akiwa porini.
Katika biblia mashujaa wa Bwana vitani walifananishwa na Paa, Kwamfano mmoja wa mashujaa wakuu wa Daudi aliyeitwa Asaheli alisifika kuwa mwepesi wa miguu kama swala hawa..
2Samweli 2:18 “Na wana watatu wa Seruya walikuwako huko, Yoabu, na Abishai, na Asaheli; na Asaheli alikuwa mwepesi wa miguu kama kulungu”.
“Kulungu, Paa, na Ayala” ni jamii hiyo hiyo moja ya Swala.
Soma pia,
1Nyakati 12:8 “Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;
Soma tena;
2Samweli 22:34 “Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. 35 Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba”.
2Samweli 22:34 “Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
35 Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba”.
Wimbo 8:14 “Ukimbie, mpendwa wangu, Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya manukato”.
Sasa mpaka hapo utapata picha ni kwanini Tabitha, aliitwa Paa, ni kwasababu miguu yake ilikuwa ni mepesi katika kutenda matendo mema. Mpaka akasifika katika mji mzima wa Lida, jinsi gani alikuwa tayari kwenda kuwashonea mitume nguo, na kanzu, Pamoja na watakatifu wengine,bila kuombwa wala kuulizwa, Jinsi gani alivyokuwa mwepesi wa kumtolea Mungu. Bila kusukumwa sukumwa, au kukumbushwa kumbushwa, yeye mwenyewe kama swala, alikimbia kutekeleza majukumu yake ya kiutumishi, Zaidi ya watu wote waliokuwa katika ule mji wa Lida.
Hatimaye akafa, lakini watu walimwona kama hastahili kuondoka mapema, watu waliliona pengo lake lilivyo kubwa, hadi wakati ule Petro, alipokwenda katika mji huo, kulikuwa na maiti nyingi lakini hakuitwa kwa mojawapo ya maiti hizo bali ya Dorkasi tu;
Matendo 9:36 “Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. 37 Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. 38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu. 39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. 40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi”.
38 Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.
39 Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao.
40 Petro akawatoa nje wote, akapiga magoti, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi”.
Hii ni kutufundisha kuwa, ili Mungu awe naye mwepesi kama Swala kutuhudumia, basi na sisi tuonyeshe wepesi wetu kwake. Je sisi nasi ni wepesi wa kutenda matendo mema kama Tabitha? Je tu wepesi kutoa mali zetu na vitu vyetu kwa ajili ya utumishi wa Bwana? Au tu wabinafsi, au mpaka tukumbushwe, au mpaka tulazimishwe, au mpaka tuvutwe vutwe?
Wakati mwingine kwanini, majibu ya maombi yetu yanachelewa?, Ni kwasababu sisi wenyewe sio wepesi kwa Bwana, tunamfanya yeye naye awe mzito.
Tuifanya miguu yetu mepesi, ili wakati wa haja zetu Bwana naye awe mwepesi kutusaidia, kama alivyofanya kwa Dorkasi.
Habakuki 3:19 “YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka”.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
hMada Nyinginezo:
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.
Ayala, Paa na Kulungu ni wanyama gani?
Kwanini wakristo walipomuona Petro akigonga walisema “Ni malaika wake”?
MUNGU WANGU,MBONA UMENIACHA?.
USIPUNGUZE KUTUMBUIZA!
Rudi nyumbani
Ahimidiwe Bwana wetu Yesu Kristo, utukufu na heshima vina yeye milele na milele.Amen
Wakati fulani mfalme wa Israeli aliyeitwa Yehoashi alimfuata Elisha ili kumjulia hali kabla hajafa.
Kama tunavyosoma habari ile Elisha alimwambia achukue mshale kisha aurushe upande wa mashariki kupitia dirishani. Na alipofanya vile Elisha alimwambia huo ni mshale wa ushindi dhidi ya maadui zake washami..
Hivyo mfalme alipoona vile jinsi alivyopewa maagizo mepesi na yenye uhalisia wa ushindi kwa tendo la kutupa mishale, hakuwa na shaka yoyote kusikia pengine Elisha atampa maagizo mengine kama hayo, ya kurusha mishale mingine mingi Zaidi ili kuwapiga maadui zake walio karibu naye.
Lakini mambo yalikuwa ni kinyume na mtazamo wake kwani Elisha alimwagiza apige mishale yake ardhini badala ya kuirusha juu, kama alivyofanya hapo kwanza, tendo hilo likaweka ukakasi kwake “kutupa mishale ardhini”!? pengine alidhani ni mishale inayomrudia yeye.
Tusome..
2 Wafalme 13:14-19
[14]Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake! [15]Elisha akamwambia, Twaa uta na mishale; naye akatwaa uta na mishale. [16]Akamwambia mfalme wa Israeli, Weka mkono wako katika uta; naye akaweka mkono wake juu yake. Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme. [17]Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza. [18]Akasema, Itwae mishale; akaitwaa. Akamwambia mfalme wa Israeli, Piga chini; akaipiga nchi mara tatu, akaacha. [19]Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.
[14]Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!
[15]Elisha akamwambia, Twaa uta na mishale; naye akatwaa uta na mishale.
[16]Akamwambia mfalme wa Israeli, Weka mkono wako katika uta; naye akaweka mkono wake juu yake. Elisha akaweka mikono yake juu ya mikono ya mfalme.
[17]Akasema, Lifungue dirisha linaloelekea mashariki; akalifungua. Basi Elisha akasema, Piga; akapiga. Akasema, Mshale wa BWANA wa kushinda, naam, mshale wa kushinda Shamu, kwa maana utawapiga Washami katika Afeki hata utakapowaangamiza.
[18]Akasema, Itwae mishale; akaitwaa. Akamwambia mfalme wa Israeli, Piga chini; akaipiga nchi mara tatu, akaacha.
[19]Yule mtu wa Mungu akamkasirikia, akasema, Ingalikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.
Umeona, hakujua kuwa ile ya kupiga chini ndio mishale ya ushindi, kinyume chake akawa na hofu matokeo yake akapiga michache tu (yaani mitatu)..
Ni jambo la kawaida hata leo, Mungu anawaagiza watakatifu wake warushe mishale mingi mahali ambapo ni kinyume na matarajio yao..lakini mashaka yanawaingia, wanaona kama wanafanyakazi bure, na kupoteza nguvu.
Ndugu yangu vita vya kiroho ukivitazama kwa jicho la mwilini ni rahisi sana kukata tamaa, kwasababu unaweza ukajiona kama unapoteza tu nguvu zako na muda..kama vile kupiga mishale chini..
Unapokuwa katika maombi, usitazamie kuona badiliko lolote la nje labda mbingu imekuwa ya blue, au usikie mapanga yakipigwa na malaika katika anga la kwanza hapana..zaidi sana utaona ni kama siku nyingine tu ya kawaida, umeomba bure, umeuchosha mwili bure. Lakini katika roho umeangusha ngome nyingi sana za ibilisi, tena na kwa jinsi unavyozidi kudumu zaidi na zaidi katika kuomba ndivyo unavyomfukuza shetani mbali nawe kabisa kabisa .
Hivyo hupaswi kukata tamaa au kuacha kuomba kwasababu hiyo mishale ya ardhini ndio yenye mapigo ya Mungu kuliko ile ya juu.
Unaposhea Neno la Mungu na wengine mtandaoni unaweza usione Matokeo yoyote ya kile unachokifanya, lakini wewe endelea Shea sana kwasababu hiyo ndio mishale ya ushindi unayoidharau wewe.
Unapohubiri mitaani au masokoni, unaweza ukaona kama unawapigia tu watu makelele, au watu hawakusikilizi, lakini hiyo ndio mishale ya ushindi katika vita vyako.
Njia za Mungu sio njia zetu. Wewe utarusha juu, yeye atataka urushe chini..huwezi kumpangia kanuni ya vita.
Hivyo tufanyapo jambo lolote la ki-Mungu tusipime-pime sana au kuchunguza-chunguza sana kwa jicho la nje, kwasababu ukifanya hivyo itakuwa ni rahisi kukata tamaa…bali tufanye kile alichotuagiza kwa bidii kana kwamba tunapoteza nguvu zetu bure, na matokeo yake tutakuja kuyaona baadaye katika ulimwengu wa roho.
Ongeza michale yako ya chini.
Bwana akubariki.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?
Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?
Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?
Kutia mkono chini ya paja kama ishara ya kiapo, kulimaanisha nini?
WhatsApp
Jibu: Tusome,
Walawi 3:3 “Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo, 4 na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na HICHO KITAMBI KILICHO KATIKA INI, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa”.
Walawi 3:3 “Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,
4 na figo zake mbili, na mafuta yaliyoshikamana nazo, yaliyo karibu na kiuno, na HICHO KITAMBI KILICHO KATIKA INI, pamoja na hizo figo; hayo yote atayaondoa”.
Kulingana na lugha yetu, tumezoea kutafsiri neno “kitambi” kama “tumbo lililotoka nje”..yaani unapotaja kitambi tu!, basi picha ya kwanza kujitengeneza akilini ni “mtu mwenye tumbo kubwa” lakini kiuhalisia neno kitambi tafsiri yake sio tumbo.. bali ni “kitu chochote ambacho kimevimba au kimejaa na kutengeneza mduara”. Pulizo lililojaa upepo au lililojaa maji limetengeneza kitambi! Kwa ule ujazo na ule mduara.
Kadhalika “Ini” linacho “kitambi” na kitambi chenyewe ndio ule mduara wake.. Na ini linatabia ya kuongezeka ukubwa na kupungua kama vile tumbo lilivyo, mtu leo utamwona yupo kawaida kesho atakuwa na kitambi, kadhalika wachunguzi wanasema Ini nayo linakua, hata likipunguzwa baada ya kipindi Fulani linaota tena na kuwa kubwa, (kitambi chake kinaongezeka..)
Bwana alimwagiza Haruni na wanawe kulitwaa Ini, Pamoja na kitambi chake hicho, Pamoja na figo na mafuta yaliyo yaliyoshikamana na viungo hivyo, na kuviteketeza juu ya madhahabu kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana.(Maagizo hayo Bwana aliwapa wakati watu watakapotaka kuleta sadaka za amani mbele za Bwana)
Na kwanini Bwana alivihitaji viungo hivyo vya ndani vichache tu! na si viungo vyote kama miguu, nyama n.k? bali alihitaji tu FIGO na INI?
Ni kwasababu viungo hivyo viwili yaani FIGO, Pamoja na INI vinahusika katika kuchuja sumu inayoingia Mwilini. Mtu au Mnyama akiondolewa FIGO au INI anamuda mfupi sana wa kuishi, kwani atakufa kwa sumu itakayoingia mwilini mwake kwa njia ya chakula au maji!..kwani vyakula tunavyokula vinayo sumu nyingi lakini ini, inavunja vunja ile sumu ya kukibakisha kile chakula salama.
Ikifunua kuwa na sisi tunapomtolea Mungu sadaka za amani kama hizo, basi sehemu ya roho zetu inayohusika na upambanuzi wa roho za uadui, Bwana anaziongoza yeye, tunajikuta tunakuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua mabaya na kuyashinda, kadhalika mambo yote mabaya ambayo ni sumu kwetu, tunakuwa tunauwezo wa kuyapambanua.. kama vile Figo na Ini zilivyokuwa na uwezo huo.
Hivyo kuna umuhimu pia mkubwa sana wa kumtolea Bwana, hususani tunapomtolea kwa hiari na si kwa kulazimishwa, kuna baraka nyingi sana za kiroho.
Maran atha!
Kwanini Mungu awachome watu kwenye ziwa la moto na hali yeye ndiye aliyewaumba?
UTAWALA WA MIAKA 1000.
TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.
Je ni wanyang’anyi wawili waliomtukana Bwana Yesu au mmoja?
Sadaka ya amani, ilikuwa ni sadaka inayotolewa kwa Mungu kutokana na amani mtu aliyoipata; Tofauti na ambavyo ingeweza kutafsirika kuwa ni sadaka ambayo mtu angeitoa kwa Mungu ili kupatana naye! (yaani kurejesha amani na Mungu), lakini sivyo, haikuwa na maana hiyo!.
Wana wa Israeli walitoa aina hii ya sadaka, pale ambapo ndani yao walipata amani. Na amani hiyo ilitokana na Mungu kuwafanyia jambo Fulani zuri katika Maisha yao labda kuwafanikisha, au kuponywa magonjwa au kupatanishwa na maadui zao n.k.
Hivyo kutokana na amani hiyo walimtolea Bwana sadaka ya kumshukuru, ndio iliyojulikana kama sadaka ya Amani. (Na sadaka Hii ilikuwa ni sadaka ya hiari na haikuwa ya amri, maana yake mtu hakulazimishwa kumtolea Mungu, ni kwajinsi atakavyojisikia yeye, kama ameona kuna sababu ya kumshukuru Mungu kwa amani basi alimtolea, kama aliona hakuna sababu basi aliacha!, hakulazimishwa).
Tofauti na sadaka nyingine ambazo mtu akipeleka mbele za Bwana, kama ni ng’ombe au mbuzi au kondoo au njiwa, mnyama yule anakuwa anateketezwa wote juu ya madhabahu baada ya kuchunwa, lakini sadaka hii ya Amani ilikuwa tofauti kidogo!, kwani baada ya mtu kumleta mbele za Bwana katika hema, kuhani alimchuna yule mnyama, na kutoa baadhi ya viungo vichache vya ndani tu!, ambavyo ni FIGO, MAFUTA YAFUNIKAYO MATUMBO, na KITAMBI KILICHOPO KATIKA INI. Na viungo hivyo ndivyo alivyokuwa anaviteketeza juu ya madhahabu, sehemu iliyobakia yaani nyama ya mwili, ilikuwa ni kwaajili ya makuhani, na mara chache sana iliteketezwa kwa moto.
Walawi 3:1 “Na matoleo yake kwamba ni SADAKA ZA AMANI; kwamba asongeza katika ng’ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana. 2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote. 3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo, 4 NA FIGO ZAKE MBILI, NA MAFUTA YALIYOSHIKAMANA NAZO, YALIYO KARIBU NA KIUNO, NA HICHO KITAMBI KILICHO KATIKA INI, PAMOJA NA HIZO FIGO; HAYO YOTE ATAYAONDOA. 5 Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana”.
Walawi 3:1 “Na matoleo yake kwamba ni SADAKA ZA AMANI; kwamba asongeza katika ng’ombe, mume au mke, atamtoa huyo aliye mkamilifu mbele ya Bwana.
2 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.
3 Naye atasongeza katika sadaka hiyo ya amani, dhabihu kwa Bwana itakayofanywa kwa njia ya moto; yaani, mafuta yafunikayo matumbo, na mafuta yote yaliyo juu ya matumbo,
4 NA FIGO ZAKE MBILI, NA MAFUTA YALIYOSHIKAMANA NAZO, YALIYO KARIBU NA KIUNO, NA HICHO KITAMBI KILICHO KATIKA INI, PAMOJA NA HIZO FIGO; HAYO YOTE ATAYAONDOA.
5 Na wana wa Haruni watayateketeza kwa moto juu ya madhabahu, juu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika kuni zilizo juu ya moto; ni dhabihu ya kusongezwa kwa njia ya moto, harufu ya kupendeza kwa Bwana”.
Sadaka hii inatufundisha nini sisi watu wa agano jipya?
Je inatufundisha na sisi tukachune ng’ombe na kuwatoa sadaka ya kuteketezwa?.. La!, haitufundishi hivyo, bali inatufundisha kuzijali Fadhili za Bwana.
Kama Bwana amekupa amani katika Taifa unaloishi huna budi kumshukuru kwa matoleo yako kwa chochote kile angalau kila mwaka au kila mwezi..(Hiyo ni sadaka ya amani kwako kwa Bwana, usipomtolea hutendi dhambi ila pia hupati thawabu).
Vile vile kama Bwana kakupa Amani na nyumba yako, au ndoa yako..basi mshukuru kwa chochote, mtolee sadaka hiyo ya amani, naye ataona umemheshimu, na utapata baraka.
Kama Bwana amekupa amani mahali unapoishi, au unapofanyia kazi, au unapomtumikia yeye.. basi mtolee sadaka ya Amani, sadaka ya namna hiyo inaugusa sana moyo wa Mungu kwasababu anaona unazithamini Fadhili zake.
Na eneo lingine lolote la Maisha yako ambalo unaona umepata amani kwalo, mtolee chochote yeye.. Na kipeleke kwenye nyumba ya Mungu.
Na katika matoleo kumbuka jambo hili siku zote!, sadaka za amani zinapelekwa kwenye nyumba ya Bwana au kwenye utumishi wa Bwana, usipeleke kwa maskini, wala kwa ombaomba barabarani!!..
Israeli kulikuwa na maskini wengi, lakini Bwana alimwagiza Musa na Haruni kuwa wawaambie Israeli wote wapeleke sadaka zao NYUMBANI KWAKE!..sio kwamba Mungu alikuwa hawaoni maskini!, aliwaona lakini alikuwa na sababu kubwa kwanini awaambie wapeleke nyumbani kwake!.. Ni kwasababu nyumbani kwake ndipo kunapotoka uzima!, ndipo ibada za kuwaombea Israeli wote zinapofanyika!, (ikiwemo na maskini ndani yake), ndipo walipokuwepo makuhani wa Bwana ambao muda wote wanafanya kazi ya Mungu, kuwapatanisha na kuwarejesha kwa Mungu wao!. Pasipo ile hema kuwepo ya kufanya upatanisho, Israeli ingeshafutika kitambo..Hiyo ndio maana Bwana alisema sadaka zote ziende pale, ili ule utumishi wa ukuhani uendelee kuwepo, usife wala kupotea.
Hivyo ukiwa na chochote tofauti na sadaka ya shukrani, wapelekee maskini, na wasiojiweza mitaani, lakini sadaka! Ipeleke madhabahuni kwa Bwana!..itakuletea matokeo makubwa Zaidi.
Usianze kusema, wala kufikiri sadaka yako inaliwa na wachungaji!, hiyo sio kazi yako, mwachie Bwana yeye anajua kushughulika na madhahabu yake, aliwaadhibu wana wa Eli waliokuwa makuhani kwa kuidharau sadaka ya Bwana, pasipo kusaidiwa na mtu, atashughulika na viongozi wa namna hiyo hiyo siku hizi za mwisho, lakini wewe uliyetoa hutakuwa na hatia, thawabu yako ipo pale pale.
Hivyo usisikilize uongo wa shetani uliozagaa kila mahali unaosema..nikipata sadaka napeleka kwa mayatima na ombaomba, kwasababu wachungaji ni wahuni!! Utajipunguzia thawabu zako!..Toa sehemu nyingine na kuwapa hao, lakini sadaka yako ambayo itaambatana na shukrani na maombi, ipeleke madhabahuni kwa Bwana. (HIYO NI KULINGANA NA NENO LA MUNGU!!).
Bwana atusaidie tuzijali Fadhili za Bwana.
Maran atha
Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?
Sadaka ya kuinuliwa ni sadaka ya namna gani?
SHINA LA UCHUNGU, LISICHIPUKE NDANI YETU.
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”
Mshahara wa Mbwa ni upi? Kama tunavyousoma katika Kumbukumbu 23:18
Kigao ni aina ya silaha inayofanana na ngao,
Inachokitofautisha kigao na ngao ni kwamba kigao ni kidogo na chepesi, rahisi kubebeka, na huwa kinafungwa mkononi, lakini ngao huwa ni kubwa na nzito kidogo.
Mara nyingi katika vita vikubwa vya zamani, askari walikuwa wanakwenda vitani na ngao kubwa kwasababu vita vile, vilikuwa ni vya wengi, na mishale, mingi ilirushwa kutoka kila mahali, hivyo palihitajika kifaa kikubwa kidogo cha kujilinda, hapo ndipo ngao ilibebwa.
Lakini katika hali ya kawaida si kila mahali askari walitembea na ngao kubwa, hivyo walibeba vigao vyepesi na umuhimu wake ulikuwa ni pale, walipojikuta katika vita vya mtu na mtu, vya kurushiana mapanga, hapo kigao kilikutumika, kupangua mapanga na sio ngao, kwasababu ngao ni nzito, mahususi kwa kuzuia mishale ya mbali, lakini kwa vita vya mtu na mtu ni ngumu, kidogo ilihitaji kifaa chepesi..Ndio hicho kilichojulikana kama kigao.
Tazama picha juu..
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia;
Zaburi 35:1 “Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami. 2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie”.
Zaburi 35:1 “Ee Bwana, utete nao wanaoteta nami, Upigane nao wanaopigana nami.
2 Uishike ngao na kigao, Usimame unisaidie”.
Zaburi 91:3 “Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo. 4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao. 5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana”,
Zaburi 91:3 “Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.
4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana”,
1Wafalme 10:17, 2Nyakati 9:16
Je! Kigao kinafunua nini kwa agano jipya?
Sisi kama watakatifu Bwana anatushauri, tuvae silaha zote za haki ili tuweze kuzipinga hila za shetani (Waefeso 6:11). Na moja ya silaha hizo zilizozungumziwa hapo ni Ngao., Ikimaanisha na kigao.
Ambayo biblia inasema, ndio IMANI. Hivyo Imani yetu inapaswa isimame katika vita vikubwa, na katika vita vidogo, katika mapambano makubwa na katika mapambano madogo, tushike NGAO NA KIGAO.
Yeremia 46:3 “Tengenezeni kigao na ngao, mkakaribie ili kupigana”.
Mara nyingi tunadhani shetani atatuangusha kwa mamilioni ya majeshi ya mapepo atakayotutumia.. Lakini, anaweza kutumia askari wake mmoja wa giza akatuondolea Imani yetu kwa Bwana kabisa, akaturudisha nyuma.
Hivyo ni kuwa makini, tuwe na Ngao Pamoja na vigao vyetu rohoni. Imani yetu ithibitike kotekote. Kwasababu Imani ni kitu cha msingi sana kukilinda. Na hiyo tumeambiwa tuishindanie kwasababu tumekabidhiwa tu MARA MOJA tukiipoteza basi kuipata tena ni ngumu..
Yuda 1:3 “Wapenzi, nilipokuwa nikifanya bidii sana kuwaandikia habari ya wokovu ambao ni wetu sisi sote, naliona imenilazimu kuwaandikia, ili niwaonye kwamba mwishindanie imani waliyokabidhiwa watakatifu mara moja tu”.
Ndugu kama umeokoka, shikilia wokovu kwa nguvu zote, usirudishwe nyuma na mwanadamu mmoja au majeshi ya maadui. Simama imara na Bwana atakusaidia.
Silaha za Mkono wa kuume na za mkono wa kushoto ni zipi
Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?
MJUMBE WA AGANO.
Ufunuo 12 inaelezea vita vya wakati upi?
Je kama mtu hataki au hajisikii kushiriki meza ya Bwana, na akaamua maisha yake yote kutokufanya hivyo, lakini amri nyingine anashika, je ataokolewa siku ya mwisho?.
Jibu: Shalom.
Yapo maandiko ambayo ni hiari kwetu kuyafanya na yapo ambayo ni maagizo, ambayo ni lazima kila anayejiita mkristo ayafanye.
Mfano wa maandiko ambayo ni hiari sisi kuyafanya au kutoyafanya ni “Ndoa”. Biblia imetoa maagizo ya ndoa lakini haijaweka ulazima wa jambo hilo, maana yake si lazima kuoa au kuolewa, mtu akiamua kukaa bila kuoa au kuolewa hajavunja sheria. (1Wakorintho 7:1-2).
Lakini yapo maandiko ambayo ni maagizo ya lazima kwa kila mkristo, na mojawapo ya hayo ni KUSHIRIKI MEZA YA BWANA.
Mengine ni ubatizo, na kuoshana miguu. Agizo la ubatizo si la hiari bali ni la lazima.
Ni lazima kila mtu baada tu ya kuamini akabatizwe, na si kubatizwa tu!..bali kubatizwa katika ubatizo sahihi.
Na pia ni lazima kila mtu baada ya kuokoka awe mshirika wa meza ya Bwana, maana yake ni lazima ashiriki mwili na damu ya Yesu. Hii ni lazima kama vile agizo la ubatizo lilivyo, haijalishi wewe si mpenzi wa Mkate au divai. Ni lazima ushiriki, kwasababu ni kiwango kidogo tu kinachohitajika kwako sio sufuria nzima ya mikate wala chupa nzima ya divai.
Sasa kwanini ni agizo la lazima?.
Ni kwasababu tusiposhiriki meza ya Bwana Yesu alisema hatuna UZIMA NDANI YETU!.
Yohana 6:53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho”.
Yohana 6:53 “Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho”.
Sasa tukirudi kwenye swali, je! Tusiposhiriki Meza ya Bwana, baada ya kuokoka tutaokolewa? Jibu ni hilo hapo juu kwamba hatutaokolewa, kwasababu hatutakuwa na uzima, maana yake hatutakwenda kwenye unyakuo na hata tukifa hatutafufuliwa! Kulingana na maandiko hayo!.
Hiyo ikifunua kuwa Neno la Mungu hatulitimizi kama tutakavyo sisi, bali kama atakavyo yeye.
Bwana akisema tushiriki hiyo ni amri kwetu, sio suala la kusema nasikia kichefuchefu, (au sipendagi ngano)..Huna budi kula hivyo hivyo hata kama hupendi. Kadhalika Bwana akisema tukabatizwe, sio suala la kutoa mapendekezo yetu au hisia zetu, kwamba tunaogopa maji, au tunaogopa kuzamishwa, au hatupendi kuzamishwa..ni lazima kufanya kama Bwana alivyosema, kama tunataka kuokoka.
Lakini kama hutaki siku ile kufufuliwa na kuurithi uzima wa milele, au kama hutaki kunyakuliwa usibatizwe wala usishiriki meza ya Bwana na huku tayari umeshajua umuhimu wa kufanya hayo.
Watakaopata neema ya kuokoka ni wale ambao hawakuwahi kujua wala kusikia juu ya haya, tunayoyasikia sisi..lakini kwa wewe na mimi ambao tayari tumeshayasikia na kujua hivi..tusiposhiriki meza ya Bwana kwa makusudi hatuna udhuru.
Lakini pia hatushiriki tu kama tutakavyo sisi, bali biblia inatuonya tujitakase kwanza, na tujipambanue nafsi zetu kama kweli tunastahili kushiriki, maana yake kama maisha yetu ni ya dhambi, hatuna budi kwanza kumpokea Yesu ndipo tushiriki..
1 Wakorintho 11:27 “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. 28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe. 29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili. 30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala. 31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa”.
1 Wakorintho 11:27 “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.
28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.
29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.
30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.
31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa”.
Bwana atubariki.
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Je tunapaswa tushiriki Meza ya Bwana mara ngapi?
NI NINI BWANA ANATAZAMIA KILA TUNAPOSHIRIKI MEZA YAKE.
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
MFANYE BWANA YESU MWENYEJI MAISHANI MWAKO.
SWALI: Kulingana na Hesabu 9:11 Je! kuna sikukuu za pasaka mbili kwa mwaka?
Hesabu 9:11 “mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;”
JIBU: Mungu aliwaagiza wana wa Israeli kila tarehe kumi na nne (4) ya mwezi wao wa kwanza, itakuwa ni sikukuu ya pasaka kwao, ambayo wataila kama kumbukumbu la siku ambayo Mungu aliwatoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa.
Hivyo kila inapokaribia tarehe hiyo ya mwezi wa kwanza wayahudi wote walijitakasa na kukusanyika pamoja ili kuila pasaka hiyo..Na ilikuwa ni sheria na lazima.
Lakini tunaona hapo katika kitabu cha Hesabu kuna mwezi mwingine ambao ni wa pili, tarehe kama hiyo hiyo ya 14, wayahudi walikuwa wanakusanyika tena waile pasaka..
Swali ni Je kulikuwa na pasaka nyingine ya pili?
Jibu ni ndio Mungu aliruhusu iwepo pasaka nyingine ndogo.. Na ni kwanini aliruhusu, ni kwasababu kulikuwa na watu ambao kipindi cha sikukuu ya kwanza hawakuweza kufika kwa wakati kutokana na umbali wa safari…na wengine walikuwa wamenajisika kwa kushika maiti, ambayo iliwagharimu muda wa siku saba mpaka wawe safi(Hesabu 19:11)..Na sheria ilikuwa hauruhusiwi kwa namna yoyote kuingia katika kusanyiko lolote la watakatifu mpaka utakapokuwa safi kabisa.
Kwahiyo kulikuwa na kundi kubwa la watu ambao walishindwa kuila sikukuu hiyo ya pasaka kwa kwasababu hizo zilizoorodheshwa.
Hivyo kwa makundi kama haya ya watu, walipewa nafasi yao ya kipekee na Mungu ili kusudi kwamba sikukuu hii isiwapite kabisa katika mwaka huo.
Hesabu 9:10-12 [10]Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA; [11]mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu; [12]wasisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.
Hesabu 9:10-12
[10]Nena na wana wa Israeli, kuwaambia, Mtu wa kwenu, au wa vizazi vyenu, ye yote atakayekuwa na unajisi kwa ajili ya maiti, au akiwako mbali katika safari, na haya yote, ataishika Pasaka kwa BWANA;
[11]mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;
[12]wasisaze kitu chake cho chote hata asubuhi, wala wasimvunje mfupa wake; kama hiyo sheria yote ya Pasaka ilivyo ndivyo watakavyoishika.
Hiyo ndio sababu ya kuwepo kwa sikukuu nyingine ndogo ya pasaka..iliyofanyika mwezi mmoja baadaye.
Lakini Je hadi sasa tunayo maagizo kama haya ya kuzishika sikukuu za pasaka?
Katika agano jipya hatusheherekei tena sikukuu za pasaka kwa jinsi ya mwili, bali kwa jinsi ya Roho tukikumbuka kuwa pasaka wetu Yesu Kristo tayari alishachinjwa zamani..
Hivyo wakati wote tupo katika pasaka yake.
Lakini leo hii wengine wanaifananisha siku hii na siku ya Valentino (Valentine’s day)..yaana siku ya wapendanao duniani kama wanavyosema ambayo huwa inaadhimishwa kila tarehe 14 mwezi wa 2 duniani kote..Jambo ambalo halihusiani kabisa na Sikukuu hii ya Bwana.
Kwanza mwezi wa pili wa kiyahudi sio sawa na mwezi wetu wa pili wa kalenda ya Gregory..
Pili Upendo uliotangazwa na Valentino.Hauhusiani kabisa na Upendo uliotangazwa na Yehova Mungu wetu katika maandiko yake matakatifu.
Hivyo hatupaswi kuyalinganisha mambo ya kimbinguni na sherehe za kidunia. Sisi kama wakristo hatusheherekei Valentine’s day. Ni sikukuu ya kipagani. Tunaisheherekea pasaka ya Bwana kila siku katika Roho.
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?
Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
UNYAKUO.
Kuna siku Fulani nikiwa nasafiri kwenye gari, nikamsikia mtu fulani kwenye redio akisema “Rafiki wa adui yako ni Adui yako”..akimaanisha kuwa “mtu yeyote ambaye atashirikiana na yule mtu anayekupinga wewe, au anayekuchukia au anayekupiga vita basi huyo naye pia ni adui yako”..Haijalishi hakujui wewe wala hajawahi kukutana na wewe, wala hajawahi kukuona..kitendo tu cha kuwa Rafiki wa adui yako, tayari ni yeye kashafanyika kuwa adui wako.
Usemi huo ni wa kidunia lakini una kauhalisia fulani ndani yake..
Hebu tusome maandiko yafuatayo..
Yakobo 4:4 “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu”
Hapo maandiko yanasema.. “Kuwa rafiki wa dunia” tayari wewe ni adui wa Mungu…Maana yake haijalishi hujawahi kumwona Mungu wala kumsikia, au kukutana naye, haijalishi hujawahi kulikufuru jina lake, wala kumtukana. Kitendo cha wewe tu kuwa Rafiki wa ulimwengu tayari umeshakuwa adui yake!.
Na hiyo ni kwanini?
Kwasababu ulimwengu upo kinyume na Mungu siku zote, anasa zote zinautukuza ufalme wa giza, Fahari zote za kidunia zinautukuza ufalme wa giza ambao upo chini ya shetani, na ufalme wa giza wote upo kinyume na ufalme wa Nuru wa Mungu.
Luka 4:5 “Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. 6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo”.
Luka 4:5 “Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja.
6 Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo”.
Ndugu fahamu kuwa unapokuwa Rafiki wa mambo ya kidunia tayari wewe ni umeshakuwa adui wa Mungu. Unapokuwa Rafiki wa tamthilia za kidunia tayari wewe ni adui wa Mungu, haijalishi kinywani unakiri wewe ni Rafiki wa Mungu… Neno lake linasema wewe tayari ni adui yake.
Unapokuwa Rafiki wa filamu za kidunia, wewe ni adui wa Mungu, Unapokuwa Rafiki wa michezo ya kidunia kama kubeti, kupambana ndondi, karate, mipira, n.k wewe ni adui wa Mungu kwasababu michezo hiyo ipo kinyume na Mungu, na inamtukuza shetani.
Unapokuwa rafiki wa miziki ya kidunia, wewe tayari ni adui wa Mungu, haijalishi hujawahi kumtukana Mungu kinywani mwako, tayari wewe ni adui yake, kadhalika unapokuwa Rafiki wa starehe na anasa zote za kidunia umeshajifanya mwenyewe kuwa adui wa Mungu. Huhitaji kutangaza kinywani kwamba wewe ni adui wa Mungu, kitendo tu! Cha kuwa Rafiki wa ulimwengu, wewe tayari ni adui yake.
Na madhara ya kuwa adui wa Mungu, ni kuitazamia ghadhabu ya Mungu itakayoijia ulimwengu na hata baada ya ulimwengu katika ziwa la moto.
Yeremia 46:10 “Maana hiyo ni siku ya Bwana, Bwana wa majeshi, SIKU YA KISASI, ILI AJILIPIZE KISASI JUU YA ADUI ZAKE; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, Bwana wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati”.
Na tena linasema..
Nahumu 1:2 “Bwana ni Mungu mwenye wivu, naye hujilipiza kisasi; Bwana hujilipiza kisasi, naye ni mwingi wa hasira; BWANA HUJILIPIZA KISASI JUU YA ADUI ZAKE, HUWAWEKEA ADUI ZAKE AKIBA YA HASIRA”.
Umeona? Bwana ameahidi kuwaharibu maadui zake.. Na maadui zake ni akina nani?.. Ni wale wote walio “Rafiki wa ulimwengu”.
Je wewe ni adui wa Bwana kwa kuupenda kwako ulimwengu?.. Kama ndio kwanini leo usifanyike Rafiki wa Bwana kwa kujitenga mbali na ulimwengu, na anasa zake zote, na Fahari zake zote?.. Bwana Yesu aliukataa ulimwengu mbele ya shetani!, na sisi hatuna budi kuukataa Dhahiri, na Bwana huyo huyo, aliyeukataa ulimwengu mbele ya shetani, alituachia na sisi Neno hili la kutafakari..
Marko 8:36 “Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?”
Kama leo hii umeamua kuisalimisha roho yako kwa Kristo, basi uamuzi utakaouchukua ni mwema, ambao hautaujutia Maisha yako yote. Basi hapo ulipo jitenge binafsi, sehemu ya utulivu. Kisha piga magoti na kufuatisha sala hii fupi ya Imani.
Sema Bwana Yesu, ninakuja leo mbele zako, nimetambua mimi ni mwenye dhambi, na nilikuwa adui yako pasipo kujijua, leo hii ninatubu dhambi zangu zote nilizotangulia kuzifanya, na zile nilizokuwa nimepanga kuzifanya. Natubu kwa kumaanisha kuziacha!, ingia ndani yangu leo. Ninakiri kuwa wewe ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yangu!, na kwamba ulikuja kufa kwaajili yangu, ukafufuka na utarudi tena kuwachukua wateule wako, nisaidie niwe miongoni mwa wale utakaokuja kuwachukua siku ile.
Leo hii ninamkataa shetani na kazi zake zote!.. ninaukataa ulimwengu na kazi zake zote!..ninakataa anasa, na ushabiki wa mambo yote ya kiulimwengu!, na urafiki wa mambo yasiyofaa, yanayoniweka mbali nawe Bwana wangu.
Roho Mtakatifu karibu ndani yangu leo, nisaidie na niongoze katika kuijua kweli yote na kuushinda ulimwengu. Asante Bwana Yesu kwa kunisamehe na kuniingiza katika neema yako.
Amen!
Ikiwa umefuatisha sala hii yote kwa Imani, tayari Bwana Yesu kaingia ndani yako, kuanzia sasa yupo tayari kukupeleka katika hatua nyingine kiimani. Unachopaswa kufanya ni kujitenga mbali na vichocheo vyote vya dhambi, mfano kama simu yako ina miziki, au mipira, tamthilia, filamu, picha za ngono au link za kubet, zifute zote wakati huu, ili umpe Roho Mtakatifu nafasi ya kukupeleka viwango vingine, kadhalika kama ulikuwa na kampani za marafiki zipunguze, au anza kuzungumza nao Habari za wokovu tu!.
Na mwisho kabisa unapaswa ubatizwe ili ukamilishe hatua ya mwisho ya wokovu wako, ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, Hivyo mapema sana tafuta mahali sahihi ukabatizwe, na kama utahitaji msaada huo wa ubatizo basi wasiliana nasi kwa namba hizo hapo chini, tutakusaidia kwa hilo.
Na mwisho kabisa unapaswa ubatizwe ili ukamilishe hatua ya mwisho ya wokovu wako, ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, Hivyo mapema sana tafuta mahali sahihi ukabatizwe, na kama utahitaji msaada huo wa ubatizo basi wasiliana nasi kwa namba hizo
hapo chini, tutakusaidia kwa hilo.
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13).
KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.
Je kualikwa kwenye sherehe za watu ambao si wakristo ni dhambi?
Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu, utukufu na ukuu vina yeye milele na milele amina.
Huu ni mwendelezo wa mafundisho ya wana-ndoa.
Ustawi bora wa ndoa, hautegemei tu, mume au mke kutimiza wajibu wao wa mwilini,. Hiyo ni sehemu moja wapo, lakini pia ipo nyingine ambayo ni ya muhimu sana, na shetani pia anaifahamu, na kuipiga vita sana, na wewe kama mwanandoa, ukikosa jicho hilo la rohoni kulitambua, yapo mambo mengi sana mazuri utayakosa katika maisha yako ya ndoa.
Kama vile mafanikio ya mtoto yanavyochangiwa na kuwaheshimu na kuwasikiliza wazazi wake. Vivyo hivyo mafanikio bora ya ndoa yanategemea sana, utii na heshima, na kuwasikiliza wakwe zako. Leo tutaona kibiblia ni kwa namna gani hili jambo lilivyo na nguvu nyingi sana katika ustawi mzuri wa ndoa.
MAMA-MKWE.
Ikiwa wewe ni binti uliyeolewa, fahamu kuwa baraka zako za kimaisha, hazipo tena kwa mama yako mzazi, bali zipo kwa mama-mkwe wako.
Vilevile ikiwa wewe ni kijana uliyeoa, fahamu pia, ubora na ustawi mzuri wa boma lako, hautegemei tena, wazazi wako, bali Baba-mkwe wako.
Ni ngumu kupokea, na ndio hapa, vita vinapokuwepo, lakini ndivyo Mungu alivyopenda iwe.
Ukisoma kitabu cha Ruthu kinaeleza kwa marefu, jinsi mama-mkwe alivyokuwa msingi wa Ruthu kufanikiwa na kupendwa na Mungu, kiasi kwamba hadi leo hii, tunakisoma kitabu hiki, ni kwasababu ya siri aliyoitambua kwa mkwe wake Naomi, utasoma, wakati Ruthu amefiwa na mume wake, hakutaka kuachana na mkwe wake, na kwenda kuolewa tena kwao, lakini alienda naye mpaka nchi ya ugenini, akakubali kuwa kama kijakazi wake, akakubali kuwa kama bibi mjane, japokuwa alikuwa kijana, lakini hakuachana naye hata kwa nukta moja, wakati mke-mwenza Orpa karudi kwao kuolewa, tena yeye hakumwacha mkwe wake Naomi kama tunavyosoma Habari, Lakini mwisho wa siku tunajua ni nini alikutana nacho Ruthu..Badala ya unyonge, ikiwa furaha. Hadi kupewa neema ya uzao wa Bwana Yesu kupitia kwake, angali hakuwa hata mwanamke wa kiyahudi bali wa kimataifa.
Kwa maelezo marefu juu ya Habari hiyo fungua link hii, >> https://wingulamashahidi.org/2020/02/19/ewe-mke-heshima-yako-ipo-kwa-wakwe-zako/
Au nitumie msg inbox nikutumie somo lake kwa urefu..
Hiyo ni kuonyesha kuwa mwanamke yeyote uliyeolewa, hatua kubwa za mafanikio yako, ipo kwa mkwe-wako. Shusha kiburi chako, jinyenyekeze, utamwona Bwana, hata kama ni mbaya bado, lipo zuri utalipata tu kwake ambalo ndio litakuwa chanzo cha kupanda juu kwako.
BABA-MKWE
Lakini leo nataka tuone pia baraka zilizo kwa Baba-Mkwe. Na hii hasaa inamuhusu mwanamume. Kamwe usimdharau baba wa mke wako, hata kama atakuwa ni mnyomge kiasi gani, lipo zuri moja tu atakuwa nalo, ambalo huwezi kulipata mahali pengine popote isipokuwa kwake, ambalo litakufaa sana.
Embu mtafakari Musa, alikuwa ni mtu aliyezungumza na Mungu uso kwa uso, akitaka jambo lolote kutoka kwa Mungu alikwenda moja kwa moja kuzungumza naye, Mungu alimpa Musa idadi kubwa ya watu, ili awachunge, lakini katika kuwachunga kule, kulikuwa hakuna utaratibu maalumu, watu walikuwa wanaenda tu, hivyo hivyo,kwa foleni kama vile hospitalini, na wakati wote huo, Mungu hakuwahi kuzungumza na Musa juu ya jambo hilo.
Sio kwamba alikuwa halioni, alikuwa analiona, lakini ni utaratibu wa Mungu, si kila jambo atakuagiza ufanye au atazungumza na wewe moja kwa moja, haijalishi wewe ni nani.. Hata wakati wote Mungu alipokuwa anazungumza na wana wa Israeli, hata siku moja hakuwahi kuwaambia mbona mnaniweka katika mahema yenye giza aliwaacha tu hivyo hivyo,.Lakini utaona miaka mingi sana baadaye Daudi aliligundua hilo, akasema nitamjengea Mungu nyumba. Na Mungu alipoona Daudi kawaza vile akapendezwa naye sana akambariki.(2Samweli 7)
Ndivyo ilivyokuwa kwa Musa, Kusanyiko lote, hakuweza kulimudu, hakuweza kulichunga ipasavyo, lakini Mungu alikuwa anazungumza naye kila siku, lakini sio kwa Habari hizo. Ndipo siku moja Baba-mkwe wake (yaani baba wa mke wake), alipomtembelea kule jangwani, akaona jambo ambalo, Musa wala Israeli hawakuliona. Tusome;
Kutoka 18:14 “Mkwewe Musa alipoyaona yote aliyowafanyia watu, akasema, Ni jambo gani hili uwatendealo hao watu? Kwani wewe kuketi hapo peke yako, na watu wote kusimama kwako tangu asubuhi hata jioni? 15 Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu; 16 wakiwa na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri za Mungu, na sheria zake. 17 Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema. 18 Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako. 19 Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao; 20 nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya. 21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi; 22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe. 23 Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani. 24 Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia. 25 Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi. 26 Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe. 27 Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe”.
Kutoka 18:14 “Mkwewe Musa alipoyaona yote aliyowafanyia watu, akasema, Ni jambo gani hili uwatendealo hao watu? Kwani wewe kuketi hapo peke yako, na watu wote kusimama kwako tangu asubuhi hata jioni?
15 Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu;
16 wakiwa na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri za Mungu, na sheria zake.
17 Mkwewe Musa akamwambia, Jambo hili ufanyalo si jema.
18 Huna budi utadhoofika wewe, na hawa watu walio pamoja nawe pia; maana jambo hili ni zito mno kwako; huwezi wewe kulitenda peke yako.
19 Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;
20 nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya.
21 Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;
22 nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.
23 Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani.
24 Basi Musa akasikiza neno la mkwewe, akayafanya yote aliyokuwa amemwambia.
25 Musa akawachagua watu wenye uwezo katika Israeli yote, akawaweka wawe vichwa juu ya watu, wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi.
26 Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe.
27 Kisha Musa akaagana na mkwewe; naye akaenda zake, mpaka nchi yake mwenyewe”.
Umeona? Alichokifanya Musa, kilileta matokeo makubwa sana kwake na kwa wale aliowachunga. Hata sasa, wewe ni Baba, una familia ndogo au kubwa, usimdharau mkwe wako, kama yupo hai, kaa naye, msikilize kwa makini, hata kama atakuwa mjinga, usione shida kumwomba ushari wa kindoa, lipo moja litakusaidia kwa ustawi bora wa familia yako. Halikadhalika na mwanamke pia, shikamana na mama-mkwe wako.
Hizo ni kanuni za kiroho, zizingatie kwa afya ya maisha yako ya kindoa.
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
MAFUNDISHO YA NDOA.
NDOA NI NINI?
NDOA NA HARUSI TAKATIFU.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
Karibu tujifunze Biblia.
Je umewahi kujiuliza ni NEEMA IPI MARIAMU ALIYOPEWA NA MUNGU?
Luka 1:28 “Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, ULIYEPEWA NEEMA, Bwana yu pamoja nawe. 29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? 30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, KWA MAANA UMEPATA NEEMA KWA MUNGU”.
Luka 1:28 “Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, ULIYEPEWA NEEMA, Bwana yu pamoja nawe.
29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani?
30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, KWA MAANA UMEPATA NEEMA KWA MUNGU”.
Kwa haraka haraka ni rahisi kufikiri kuwa Neema Mariamu aliyopewa na Mungu ni yeye kumzaa BWANA YESU!.. Lakini nataka nikwambie kuwa hiyo sio neema ambayo Mungu alimpatia Mariamu. Kumzaa Bwana Yesu ni matokeo tu, ya Neema aliyopewa.
Neema kuu Mungu aliyompatia Mariamu ni “YEYE KUYAAMINI MANENO YA MUNGU”, hiyo ndio Neema kubwa ambayo hata sisi sote tunaihitaji.
Kikawaida si jambo rahisi kukubali au kuamini mtu anayekujia na kukwambia maneno ambayo hujayatazamia au kuyategemea na kuyaamini!. Lakini ilikuwa ni kinyume chake kwa Mariamu, kwani yeye aliyaamini maneno yale magumu, aliamini kuwa “ROHO MTAKATIFU ANAWEZA KUJA JUU YAKE NA AKAPATA MIMBA KIMIUJIZA PASIPO HATA KUMKARIBIA MWANAUME”. Hiyo ndiyo neema Mariamu aliyopewa!!. Si jambo rahisi kuamini hilo!.. Ukitaka kuamini kuwa si jambo rahisi mkumbuke Zekaria, baba yake Yohana Mbatizaji.
Malaika huyo huyo aliyemtokea Mariamu, alimtokea kwanza Zekaria na kumpa taarifa kama hizo hizo alizompa Mariamu, tena zake zilikuwa ni nyepesi kuliko za Mariamu, kwasababu yeye aliambiwa tu!, atakutana na mke wake Elizabeth na katika uzee wao watapata mtoto kama vile Ibrahimu na Sara walivyopata mtoto katika uzee wao.
Lakini ijapokuwa Zekaria alikuwa ni kuhani, ambaye angepaswa awe na Imani kubwa kuliko Mariamu, na tena ijapokuwa anao ushuhuda kama huo katika maandiko (Habari ya Ibrahimu na Sara), lakini tunaona bado hakumwamini Gabrieli? Mwishowe Malaika yule akakasirika na kumpiga Ububu, mpaka lile neno lilipotimia.
Hebu tusome kidogo..
Luka 1:7 “Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. 8 Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, 9 kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba. 10 Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba. 11 Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. 12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. 13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. 14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake……….. 18 Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi. 19 Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. 20 Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake”.
Luka 1:7 “Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana.
8 Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu,
9 kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba.
10 Na makutano yote ya watu walikuwa wakisali nje saa ya kufukiza uvumba.
11 Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia.
12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia.
13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.
14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake………..
18 Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi.
19 Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.
20 Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake”.
Hapo Zekaria hakuambiwa kuwa “mke wake atachukua mimba kimiujiza” kama alivyoambiwa Mariamu.. lakini ilikuwa ni kizaazaa, hakumwamini yule Malaika mpaka akapigwa ububu!!… sasa hebu jiulize kama yule Malaika angempa taarifa ngumu kama za Mariamu kuwa “mke wake atachukua mimba kimiujiza bila kukutana naye” ingekuwaje!..si angeweza hata kumlaani yule Malaika pale pale, na pengine Zekaria angepigwa kwa pigo kubwa kuliko hilo la ububu!!.
Kwahiyo unaweza kuona Neema Mariamu aliyopewa ni “KUYAAMINI MANENO YA MUNGU KWA ASILIMIA ZOTE”..Jambo ambalo ni Zuri sana!.
Walikuwepo mabikira wengi pale Yerusalemu na Nazareth, lakini Malaika Gabrieli hakutumwa kwao, kwasababu taarifa hizo zilikuwa ni ngumu kuaminika!..
Bwana Yesu alisema maneno haya mahali Fulani..
Luka 4:24 “Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe. 25 Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; 26 WALA ELIYA HAKUTUMWA KWA MMOJAWAPO, ILA KWA MJANE MMOJA WA SAREPTA KATIKA NCHI YA SIDONI”.
Luka 4:24 “Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe.
25 Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima;
26 WALA ELIYA HAKUTUMWA KWA MMOJAWAPO, ILA KWA MJANE MMOJA WA SAREPTA KATIKA NCHI YA SIDONI”.
Mwanamke wa Sarepta anafananishwa na Mariamu. Kwani Mwanamke wa Sarepta aliyaamini maneno ya Nabii Eliya kwa asilimia zote, aliamini kwamba inawezekana kabisa Mungu kumlisha kwa unga mdogo uliobakia kwa kipindi cha miaka mitatu au hata 10..kama vile Mariamu alivyoamini kuwa inawezekana yeye kupata ujauzito kimiujiza.
1Wafalme 17:8 “Neno la Bwana likamjia, kusema, 9 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe. 10 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa. 11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12 Naye akasema, KAMA BWANA, MUNGU WAKO, AISHIVYO, SINA MKATE, ILA KONZI YA UNGA KATIKA PIPA, NA MAFUTA KIDOGO KATIKA CHUPA; NAMI NINAOKOTA KUNI MBILI ILI NIINGIE NIJIPIKIE NAFSI YANGU NA MWANANGU, TUULE TUKAFE. 13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao. 14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, LILE PIPA LA UNGA HALITAPUNGUKA, WALA ILE CHUPA YA MAFUTA HAITAISHA, HATA SIKU ILE BWANA ATAKAPOLETA MVUA JUU YA NCHI”.
1Wafalme 17:8 “Neno la Bwana likamjia, kusema,
9 Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.
10 Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.
11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako.
12 Naye akasema, KAMA BWANA, MUNGU WAKO, AISHIVYO, SINA MKATE, ILA KONZI YA UNGA KATIKA PIPA, NA MAFUTA KIDOGO KATIKA CHUPA; NAMI NINAOKOTA KUNI MBILI ILI NIINGIE NIJIPIKIE NAFSI YANGU NA MWANANGU, TUULE TUKAFE.
13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.
14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, LILE PIPA LA UNGA HALITAPUNGUKA, WALA ILE CHUPA YA MAFUTA HAITAISHA, HATA SIKU ILE BWANA ATAKAPOLETA MVUA JUU YA NCHI”.
Huyu Mwanamke wa Sarepta alipata Neema kama tu ya Mariamu.
Sasa ni kitu gani kiliwafanya hawa wanawake wapate Neema ya kumwamini Mungu, kuliko wanawake wote walio waliokuwepo Israeli?.
Biblia inatupa majibu katika…
1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote JIFUNGENI UNYENYEKEVU, mpate kuhudumiana; kwa sababu MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI, LAKINI HUWAPA WANYENYEKEVU NEEMA. 6 BASI NYENYEKEENI CHINI YA MKONO WA MUNGU ULIO HODARI, ILI AWAKWEZE KWA WAKATI WAKE; 7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu”.
1Petro 5:5 “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote JIFUNGENI UNYENYEKEVU, mpate kuhudumiana; kwa sababu MUNGU HUWAPINGA WENYE KIBURI, LAKINI HUWAPA WANYENYEKEVU NEEMA.
6 BASI NYENYEKEENI CHINI YA MKONO WA MUNGU ULIO HODARI, ILI AWAKWEZE KWA WAKATI WAKE;
7 huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu”.
Umeona hapo, kanuni ya kupata Neema kutoka kwa Mungu?… ni KUJIFUNGA UNYENYEKEVU!!!.. Kujishusha siku zote!, mbele za Mungu na wanadamu, unakuwa mdogo kuliko wote!, unakuwa tayari kuwatumikia wengine Zaidi ya wewe kutumikiwa!!
Mariamu alikuwa anazo hizo sifa!.. Biblia haijaeleza kwa urefu Maisha yake, lakini tunaweza kupata dondoo chache za jinsi Maisha yake yalivyokuwa katika mistari ifuatayo..(Zingatia vipengele vilivyoanishwa kwa herufi kubwa).
Luka 1:46 “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, 47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; 48 Kwa kuwa AMEUTAZAMA UNYONGE WA MJAKAZI WAKE. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; 49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu. 50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha. 51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; AMEWATAWANYA WALIO NA KIBURI KATIKA MAWAZO YA MIOYO YAO; 52 AMEWAANGUSHA WAKUU KATIKA VITI VYAO VYA ENZI; NA WANYONGE AMEWAKWEZA. 53 Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu”.
Luka 1:46 “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
48 Kwa kuwa AMEUTAZAMA UNYONGE WA MJAKAZI WAKE. Kwa maana, tazama, tokea sasa Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, Na jina lake ni takatifu.
50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.
51 Amefanya nguvu kwa mkono wake; AMEWATAWANYA WALIO NA KIBURI KATIKA MAWAZO YA MIOYO YAO;
52 AMEWAANGUSHA WAKUU KATIKA VITI VYAO VYA ENZI; NA WANYONGE AMEWAKWEZA.
53 Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu”.
Hebu tuyajadili haya maneno ya Mariamu kwa ufupi ili tujue kama kweli alikuwa mnyenyekevu au la!! (Hapo yapo mambo makuu matatu!).
1. AMEUTAZAMA UNYONGE WA MJAKAZI WAKE:
Kwa maneno haya, kumbe Mariamu alikuwa anaonekana mnyonge mbele za watu, hakuwa mwanamke aliyejikweza..
2. AMEWATAWANYA WALIO NA KIBURI KATIKA MAWAZO YA MIOYO YAO.
Maana yake Mariamu yeye hakuwa na kiburi!, ndio maana kasema maneno hayo.. na maandiko yanasema, Mungu huwapinga wenye kiburi na kuwapa wanyenyekevu Neema.(Rejea 1Petro 5:5).
3. AMEWAANGUSHA WAKUU KATIKA VITI VYAO VYA ENZI; NA WANYONGE AMEWAKWEZA.
Maneno haya yanathibitisha tena kuwa Mariamu alikuwa mnyonge!, ndio maana Mungu akamkweza.
Hivyo Kwa hitimisho ni kwamba ili na sisi tupewe NEEMA kama ya Mariamu, au kama ya wengine wengi ya KUYAAMINI MANENO YA MUNGU, na hatimaye kufanya makubwa..hatuna budi tuwe wanyenyekevu. Tukubali kujihusisha na mambo manyonge, mambo madogo!.. Tusijione sisi ni bora mbele za Mungu, tukiwa watu wa namna hiyo basi Mungu atatuongezea NEEMA ZAIDI, na tutajikuta tunafanya makubwa sana.
Unapokuwa kanisani, jifunze kujishughulishe na yale mambo ambayo yanayoonekana yanadharaulika kuliko yote!, siku moja utaona matokeo yake, Zekaria alikuwa anajulikana na wakuu, tena anafanya kazi ya ukuhani lakini maneno ya Gabrieli yalimchanganya…wakati huo huo Mariamu ambaye pengine alikuwa anadumu tu katika kusali na kuomba!, na kujisitiri na kujishusha, na kuwaombea wengine, anakuja kupewa Neema kubwa ya kuyaamini maneno makuu ya Mungu.
Bwana atusaidie, Bwana atupe unyenyekevu, Bwana atuongezee Neema yake.
Bwana wetu yu aja!.
HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?
MAMA, TAZAMA, MWANAO.
ZIKUMBUKE FADHILI ZA MUNGU