Karibu katika darasa fupi, linalohusu vijana na mahusiano.
Yapo maswali kadhaa ya kujifunza kwa kijana kabla ya kuanza mahusiano ya aina yoyote ile, na mambo yenyewe ni haya;
1. Je ni wakati gani ulio sahihi wa kuanza mahusiano?
2. Je ni mtu gani sahihi wa kujiingiza naye katika mahusiano?
3. Je mambo gani ninapaswa niyafanye na yapi sipaswi kuyafanya ninapoingia katika uhusiano?
Awali ya yote ni muhimu kufahamu kuwa darasa hili linawahusu/linawafaa zaidi vijana wa kiume na wa kike ambao tayari wameshaokoka!, yaani wametubu na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu na wanaitazamia mbingu mpya na nchi mpya. Kama bado hujampokea Bwana Yesu basi mafunzo haya yanaweza yasikusaidie, hivyo ni vyema kwanza ukampokea Bwana Yesu (ukaokoka), na ndipo mambo mengine yafuate baadaye.
Mahusiano yamegawanyika katika sehemu kuu (2), Yapo Mahusiano kabla ya Ndoa, na Mahusiano baada ya Ndoa. Mahusiano kabla ya ndoa, yanaitwa Uchumba ambayo tutajikita sana kujifunza juu ya haya katika siku ya leo.
1. Ni wakati gani ulio sahihi wa kuanza mahusiano Kwa kijana wa kiume:
Kama wewe ni kijana wa kiume na umeokoka, wakati sahihi wa kuanza mahusiano ni wakati ambao tayari unajitegemea mwenyewe. Maana yake una sehemu yako mwenyewe ya kuishi na una kipato chako mwenyewe, haumtegemei mzazi au ndugu!, kwasababu hatua ya uchumba ndio hatua ya awali kabla ya kuoa, na huwezi kuoa ukiwa bado hata wewe mwenyewe huwezi kujitunza, utamtunzaje huyo mke anayekuja?.
Kwasababu hiyo basi si wakati sahihi wa kuanza mahusiano yoyote ukiwa bado ni Mwanafunzi, au ukiwa bado upo kwa wazazi wako, au ukiwa huna shughuli yoyote ya kukuingizia kipato!.
Ni umri gani sahihi wa kuanza Mahusiano, kwa kijana wa kiume?
Hapa inategemea na umri ulioanza kujitegemea mwenyewe, katika zama hizi vijana wengi wa kiume kuanzia miaka 25 na zaidi ndio wanaanza kujitegemea na hiyo ni kutokana na mifumo ya Elimu. Mtu atamaliza shule akiwa na zaidi ya miaka 20, na kujikuta kuanza kufanya kazi za mikono akiwa na zaidi ya miaka hata 25, wakati huo unaweza kuwa wakati sahihi wa kuanza uchumba.
Wapo wengine wanawahi kuanza kujitegemea wenyewe kabla ya umri huo!, hao wanaweza kuwahi kuanza mahusiano..lakini mahusiano ya mapema ni hatari sana, kwasababu akili ya kijana bado haijakomaa vizuri katika kujua mambo mengi ya kimaisha na wengi wanaingia huko kutokana na tamaa za kimwili tu!,.. Hivyo Ni vizuri kijana wa kiume akaanza mahusiano zaidi ya miaka 25.
Kwa kijana wa kike:
Wakati sahihi wa kuanza mahusiano kwa kijana wa kike, si wakati upo shule, bali wakati ambao umemaliza shule,
Vile vile umri sahihi wa kuanza mahusiano ni miaka 20 na zaidi!.. Zamani kidogo ilikuwa ni mapema, lakini zama hizi, shule zimewafanya watu wachelewe kuanza maisha yao kujitegemea. Lakini vijana wengi wa kike walio chini ya miaka 20 sasa wanaojiingiza kwenye mahusiano ya uchumba wengi wanaongozwa na tamaa tu!, aidha kwa kujua au kwa kutokujua. Na wengi wa hao wakifikisha miaka 30, akili zao zinapofika hatua ya kupevuka wanajigundua kuwa walikuwa wanafanya vitu vya kitoto na vya kipumbavu.
Kwa kijana wa kiume:
Mtu sahihi wa kuanza naye mahusiano sio yule uliyeoneshwa na Nabii, au Mchungaji, au uliyechaguliwa na mtu. Kamwe usianze mahusiano na mtu yeyote ambaye umesaidiwa kuchaguliwa. Uchaguzi utachagua wewe!, Yule Bwana aliyekuchagulia atakuja kwako na wewe utajikuta unampenda, anakidhi vigezo vyako!..Hivyo ndivyo Bwana anavyowapa watu wenza wao na sio kuchaguliwa na mchungaji au Nabii, au kuoteshwa ndoto.
Vile vile usianze mahusiano na msichana/ mwanamke yeyote ambaye yeye ndiye anayekuomba au kukulazimisha umwoe!.
Kwa kijana wa kike mtu sahihi wa kuanza naye mahusiano si mwanafunzi, haijalishi anaonesha kukupenda kiasi gani, bado sio mtu sahihi, hapa sizungumzii wale watu ambao ni wafanyakazi lakini wanajiongezea elimu ya juu (hili tayari ni kundi la watu wazima wanaojitambua), wanafunzi tunaowazungumzia hapa ni wale wa sekondari, na wale waliotoka sekondari na moja kwa moja chuo.
4. Je mambo gani napaswa niyafanye na yapi sipaswi kuyafanya ninapoanza mahusiano?
Fanya mambo yafuatayo unapoanza mahusiano.
Kwa kijana wa kiume!
Mfahamu huyo mtu kwanza, na kama ameokoka anza naye urafiki kama wa dada na kaka tu Kama hajaokoka au si mtu wa imani moja nawe!, mhubirie kwanza aokoke, akimkubali Bwana Yesu, atakukubali na wewe, akimkataa Bwana Yesu hawezi kukukubali na wewe!. Usimwahidi kwamba utamwoa endapo akiokoka maana kwa kufanya hivyo atakukubali ilimradi tu aolewe na wewe!, hivyo mvute kwa Kristo kama unavyowavuta wengine wote.
Akikubali kumtii Kristo na kumpata Roho Mtakatifu ambaye umempokea wewe, na hata kushiriki kanisa moja nawe, hapo unaweza kuanza naye urafiki kama wa kaka na dada tu!, wa kuheshimiana, wakati huo unaweza kuongeza kumjali zaidi kuliko wengine wote wanaomzunguka, kwa kufanya hivyo atakuwa ameshaanza kujua kuwa unamjali, na hivyo atakupenda na hapo ni rahisi kuendelea na hatua nyingine.
Kwa kijana wa kike!
Kwasababu ni mwanaume ndiye anayemchagua mwanamke!, kijana wa kike hupaswi kujiweka au kujitangaza kwamba unatafuta mchumba.. Kaa katika hali yako ya asili, umri usikuogopeshe wala kukutatanisha, wapo wanaoolewa hata na miaka 60, na wanakuwa na furaha, hivyo usijitafutishe mchumba.. usijipendekeze sana kwa vijana wa kiume!, bali dumu katika usafi wa Rohoni na wa Mwilini, jiweke katika mazingira ya usafi na ya upole!, Bwana atakuletea mtu sahihi ambaye atakuheshimu, kwa wakati sahihi. (www wingulamashahidi org).
Hali kadhalika utakayemwona anakuja kwako kuwa naye makini, kwasababu Matunda mazuri si mtu tu anayeyapenda bali hata nyani, na ndege na popo na bundi wanayapenda!, (maana yake hata watu waovu wanawapenda wanawake wanaojiheshimu na watakatifu), hivyo kuwa makini, Kama hajaokoka mkaribishe kanisani, na jitahidi usimhubirie wewe, kwamaana ni rahisi kukubali kuokoka ili akupate!, bali mwunganishe na mchungaji wa kiume kanisani, au na mtu yeyote aliyesimama pale kanisani, kama akimsikiliza huyo na kumkubali Kristo, ni rahisi kuwa mtu sahihi Bwana aliyekukusudia, lakini kama hataki kujihusisha na mchungaji au mtu yeyote kanisani, jitenge naye, usitazame uzuri wake au fedha zake, ni pando la adui, anakutafuta kwa faida zake tu!
Mambo yafuatayo usiyafanye unapokuwa katika Mahusiano ya uchumba!
Kwa kijana wa kiume/kike.
1/ Usikutane kimwili na huyo uliyeanza naye mahusiano, wala msishikane wala kubusiana, (Kujaliana tayari ni ujumbe tosha kwamba kila mmoja anampenda mwenzie, na sio kufanya hayo mambo)
2/ Usimtembelee huyo kijana/binti nyumbani kwake akiwa peke yake, tafuta mwenzako muwe wawili ndipo umtembelee, hiyo itaongeza heshima yenu na vile vile shetani hatapata nafasi. Vile vile tafuta masomo mazuri yanayohusu mahusiano, yaliyofundishwa na watumishi wa Mungu wa kweli, mshirikishe mwenzio asikilize mafundisho hayo, au asome, au ahudhurie semina ili aanze kujiandaa na kuwa mume au mke.
Baada ya kuhakiki kuwa huyu mwenzangu ananifaa kimaisha na vile vile ananifaa kiroho, vile vile amekukubali uwe mwenza wake, basi hatua ya ndoa inaweza kufuata. Mambo yafuatayo yatakufaa baada ya mwenzako kukubali kufunga ndoa naye.
1. Tangaza kwa wazazi: Kumbuka unapoenda kutangaza isiwe ni jambo la kushtusha kwa wazazi wako au walezi, ni vizuri wawe wanamjua huyu mwenza wako hata kabla ya hapo, ili wawe na amani naye.
2. Baada ya kutangaza kwa wazazi, Ndoa inapaswa itangazwe kanisani. Baada ya kanisa kujua na kupewa taratibu zote za ndoa, Mahari zitapangwa (Ni lazima kijana wa kiume ulipe mahari, ikiwa kubwa sana omba upunguziwe au kopa mahali ulipe), ni kinyume na maandiko kijana wa kiume kutolipa mahari, Kristo aliingia Gharama kutukomboa sisi (ndio damu yake) ambayo inafananishwa na mahari kwetu sisi bibiarusi wake, kwahiyo ni lazima kijana ulipe mahari.
3. Baada ya Mahari na ndoa kutangazwa na kufungwa, kanisani. Hapo Mmekuwa Bwana arusi na Bibi-Arusi, mnaweza kufanya mambo yote yanayowahusu wana-ndoa. Hampaswi kuishi kama wachumba tena.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.
JINSI YA KUUHARIBU UJANA WAKO.
MAMA, TAZAMA, MWANAO.
kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
Rudi nyumbani
Biblia inasema;
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo”.
Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo”.
Mistari hiyo kwa namna nyingine tunaweza kusema; Tukikosa amani, na watu wote, tukikosa utakatifu pia basi tutapungukiwa na neema ya Mungu, na matokeo yake ni kuwa shina la uchungu litachipuka ndani, na kuwasababishia watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Ni kweli mstari huu unalenga watakatifu wa Mungu..
Tukikosa, mambo hayo mawili, yaani Amani na watu wote, na Utakatifu, kuna uwezekano mkubwa sana wa hili shina la uchungu kuchipuka ndani yetu.
Jiulize kama wewe ni Mtakatifu je, una amani na watu wote? Ikiwa na maana una amani na watakatifu wenzako na watu wengine wa nje?..Ni jambo la kujitahidi sana, hata kama ni gumu ni lazima ujitahidi kama biblia inavyosema, kwasababu ukiukosa tu huo, matokeo yake ni kuwa UCHUNGU uchungu utaanza kuchipuka ndani yako.
Kibiblia Uchungu, ni hali ambayo inakuwa na mchanganyiko wa hasira, kinyongo, wivu, chuki, ghadhabu, na maumivu kwa mtu mwingine.
Na biblia inatuonyesha huwa linaanza kama mbegu, mpaka baadaye linachupuka na kuota mizizi mpaka kuwa shina nene. Na likishafikia hatua hiyo ya kuwa shina, kuliondoa ndani yako ni ngumu sana, litakusumbua kwa muda mrefu kweli, kwasababu tayari limeshakita mizizi kwenye moyo wako.
Hili shina limewasumbua sana wapendwa, hivyo tujitahidi sana tusilipe nafasi mioyoni mwetu..
Mfano mmojawapo katika biblia wa mtu aliyesumbuliwa na shina hili ni Mfalme Sauli.
Lilimwanza pale alipomwacha Mungu, na Mungu kuuhamisha ufalme wake kwenda kwa Daudi. Utaona alipojua hilo alianza kumchukia Daudi kidogo kidogo, badala akatae ile hali, akaendelea kumchukia Daudi kwa kila kitu mpaka baadaye akaonyesha kwa nje sasa yale yaliyokuwa ndani ya moyo wake, akaanza kuweka mikakati ya kumwinda na kumfukuza maporini na majeshi yake ili amuue, bila sababu yoyote. Ikawa ni ngumu tena, kulishinda lile shina la uchungu lililokuwa ndani yake.
Hata alipojaribu kutubu mara ya kwanza na ya pili juu ya jambo hilo la kumwinda Daudi bado alishindwa, kwasababu shina hilo limeshakita mizizi mkubwa ndani yake (1Samweli 24).
Hivyo na sisi, tumeonywa, tujitahidi sana, tena sana tuwe na amani na kila mtu, ni jukumu la kila mtakatifu, kila mshirika, kila mtumishi, si mchungaji, si nabii, si mtume, wote, jukumu hili ni letu, kuwa na amani na watu wote, tusiruhusu chuki, hasira, vinyongo, na wapendwa wenzetu, au ubaya wowote, vilevile na watu wa nje wa kidunia, tusigombane nao.
Kama wewe ni mchungaji, hakikisha huna neno na mshirika yoyote, au mchungaji mwenza, kama wewe ni mtendakazi kanisani, ondoa uadui wa siri na mtendakazi mwenzako, hata kama hakupendezi, jitahidi kwa upande wako uwe na amani na kila mtu kanisani.
Hiyo itatufanya tuwe mahali salama. Tuliepuke hili shina baya la adui mioyoni mwetu.
Yakobo 3:14 “Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. 15 Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani. 16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya. 17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki”.
Yakobo 3:14 “Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli.
15 Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.
16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.
17 Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki”.
Waefeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; 27 wala msimpe Ibilisi nafasi”.
Waefeso 4:26 “Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;
27 wala msimpe Ibilisi nafasi”.
Shalom.
KIFAHAMU KIGEZO CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.
Nini maana ya “Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati”
TULITAFUTE KWA BIDII TUNDA LA ROHO.
SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO.
Tunaishi katika ulimwengu ambao, ukisimama tu kuhubiri, au kukemea dhambi, moja kwa moja utaambiwa UNAHUKUMU, Ukimweleza mtu madhara ya dhambi ya uzinzi kuwa mwisho wake, ni motoni, atakuambia, wewe ni nani mpaka utoe hukumu hiyo.
Wakati Fulani nilizungumza na watu Fulani ambao walikuwa wanatetea dhambi ya ushoga, nikawaambia watu wanaofanya matendo kama hayo, mwisho wao ni jehanamu walinishambulia, kisha wakanipa andiko, lile, ambalo linamzungumzia yule mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, ambapo mafarisayo walimpeleka kwa Yesu, kwa lengo la kumjaribu, kama na yeye ataridhia kupigwa mawe, lakini mambo yakawa tofauti badala ya kuwaruhusu wampige mawe akawaambia, “Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe”. Basi wote wakatawanyika wakamwacha yule mwanamke akiwa na Bwana peke yake.( Yohana 8:1-11)
Hivyo kwa Habari hiyo hawa watu nao wakaniambia, kama wale watu hawakumtupia yule mwanamke mawe, wewe ni nani utuhukumu sisi kwa tunachokifanya, humwogopi Yesu?.
Nikawaambia mimi siwezi kuwatupia ninyi mawe, lakini Yesu mwenyewe atawatupia ninyi mawe, wakati wenu ukifika.
Watu wanadhani Kristo atakuwa katika kiti chake cha rehema milele, kuchukuliana na dhambi zetu,, hawajui kuwa atasimama kama hakimu siku moja kuwahukumu na kuwaadhibu waovu wote,..Wanadhani, Bwana anafurahia uasherati wa mtu, au uzinzi wa mtu, wanadhani alifurahia pia Uzinzi wa yule mwanamke, ndio maana hakufanya chochote.
Nataka nikuambie ikiwa yule mwanamke angeendelea katika uzinzi wake, ni kweli angekwepa mawe ya wanadamu kwa wakati ule, lakini angekutana na mawe ya Kristo siku ile ya hukumu.
Wakati huo hakutakuwa na huruma yoyote katika macho ya Bwana Yesu, haijalishi wewe ni mtoto au mlemavu, au mzee, kama ulikufa katika dhambi, utahukumiwa na kutupwa motoni milele.
Hata kabla ya siku ya hukumu yenyewe kufika, siku ile ambayo atakuwa anarudi katika mawingu kuja kutawala kama mfalme, biblia inasema, ulimwengu mzima utamwombolezea (Ufunuo 1:7).. Na utamwombolezea kwasababu gani, kwasababu ya hayo mapigo atakayokuwa anawamwagia waasi wote katika huuu ulimwengu.
Inatisha sana kwasababu, Bwana Yesu atawaua watu wengi sana, wasiokuwa na idadi. Soma hapa;
Isaya 66:15 “Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto. 16 Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; NAO WATAKAOUAWA NA BWANA WATAKUWA WENGI”.
Isaya 66:15 “Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.
16 Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; NAO WATAKAOUAWA NA BWANA WATAKUWA WENGI”.
Siku hiyo Wazinzi, mashoga, wafiraji, walevi, washirikina, watatamani milima iwaangukie, ili tu waiepuke hiyo ghadhabu ya Bwana Yesu, lakini haitakuwa hivyo; watashiriki tu mapigo yake.
Ufunuo 6:15 “Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama”?
Ufunuo 6:15 “Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama”?
Ndugu, yangu, huu wakati usitamani ukukute, kwasababu hata baada ya kupokea mapigo hayo makali kutoka kwa Bwana Yesu, bado utasimama katika kiti chake cha hukumu na kutoa hesabu ya mambo yote uliyokuwa unayafanya hapa duniani yasiyompendeza Mungu, na baada ya hapo utatupwa katika lile ziwa la moto uangamie milele na milele.
Tukiyatafakari haya kwa umakini, ndio tutajua ni kwa namna gani Bwana Yesu hapendezwi na dhambi hata kidogo, Kuona leo hii unatoa mimba hafanyi chochote, unatazama picha za ngono, hachukui hatua yoyote, unaiba hakuadhibu, unazini, unalewa, unaabudu sanamu, bado hajishughulishi na wewe..usipumbazike ukadhani, hali hiyo itaendelea hivyo hivyo milele, hata baada ya kufa.
Waebrania 10:31 “Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai”.
Ni heri ukayasalimisha Maisha yako leo kwa Bwana Yesu maadamu neema ipo, Wakati umekaribia, mambo yatabadilika ghafla, parapanda italia, kisha watakatifu wataondoka..Wewe ambaye utabakia katika huu ulimwengu, ndio utakayekutana na huo upande wa pili wa shilingi wa Bwana Yesu, ni kilio na kusaga meno!. Hutaamini kama huyu ndio yule Bwana aliyekuwa ananililia kila siku niache dhambi kwa sura ya upole, nikawa namdharau. Atakuuwa mwili na roho.
Mathayo 10:28b “… afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum”.
Bwana atusaidie sana, ikiwa hujaokoka, embu anza Maisha yako upya na Kristo leo. Tubu dhambi zako kwa kumaanisha kuziacha, kisha tafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na uwe katika jina la Bwana Yesu Kristo, ili upokee ondoleo la dhambi zako, na baada ya hapo Bwana atakusaidia. Hatuna muda tena, Yesu anarudi wakati wowote.
Kwa msaada ya kumpokea Yesu, basi wasiliana nasi kwa namba hizi; +255789001312 /+255693036618
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
UNYAKUO.
KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU KINAJAA…TUBU UMGEUKIE MUNGU
UPENDO WA MUNGU.
“Nikolai” ni neno la kigiriki lenye maana ya “Kuteka madhabahu”.
Katika kanisa la kwanza kulikuwa na kundi dogo la watu lililonyanyuka, ambalo lilikuwa linateka madhabahu.
Na kuteka madhabahu kunakozungumziwa sio kuteka nyara vitu vya madhabahuni au watu wanaosimama madhabahuni, hapana!.
Bali kuteka kunakozungumziwa hapo, ni kusimamisha mfumo ambao unaondoa uongozi wa Roho Mtakatifu ndani ya kanisa, na kusimamisha uongozi wa wanadamu.
Kikawaida kanisa linapaswa liongozwekwa karama za Roho Mtakatifu, yaani Uinjilisti, uchungaji, unabii, aualimu, karama za lugha, miujiza, imani n.k (1Wakorintho 12).
Hizo ndizo zinazoliongoza kanisa, na ndizo zinazojenga mwili wa Kristo,lakini enzi za kanisa la kwanza liliinuka kundi la watu wasio na Roho, na kutaka kuliongoza kanisa kibinadamu.
Maana yake badala Roho Mtakatifu anene, apange, afundishe, aamue, na afanye jambo kupitia karama alizoziweka ndani ya watu wake..kinyume chake wakainuka watu wakawa wao ndio wanapanga, wananena, wanafundisha na wanaamua kupitia falsafa zao, hekima zao, vyeo vyao, heshima zao katika jamii, umaarufu wao, elimu zao, ujuzi wao, mwonekano wao, na si tena kupitia karama za Roho.
Ratiba za masomo ya kufundisha zikawa zinapangwa na wanadamu, inaweza kutolewa kalenda hata ya mwaka mzima, masomo ya kufundisha tayari yameshaandaliwa.
Hivyo ubinadamu ukawa umeteka madhabahu ya Bwana badala ya Roho Mtakatifu. Huo ndio “Unikolai”.
Na katika kanisa la kwanza maandiko yanasema unikolai ulianza kama Matendo tu, Yaani watu hao ambao yalikuwa ni mapando ya adui shetani, walikuwa wanafanya hayo lakini sio kuwafundisha watu.
Ufunuo 2:6 “Lakini unalo neno hili, kwamba wayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo na mimi nayachukia”.
Lakinibaadaye unikolai ulikuja kubadilika na kuwa “Mafundisho”, yaani watu wakawa sio tu wanatenda unikolai, bali wakawa wanafundisha wengine kuutenda unikolai, (yaani kuunyanyua uongozi wa kibinadamu na kuushusha chini uongozi wa Roho Mtakatifu).
Ufunuo 2:15 “Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. 16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu”.
Ufunuo 2:15 “Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile.
16 Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu”.
Matendo na mafundisho ya Wanikolai katika nyakati hizi za mwisho ndio yameshika hatamu.
Leo hii hakuna tena uongozo wa Roho mtakatifu ndani ya kanisa, ni Liturjia, na malokeo ndio yanayoongoza… kiasi kwamba hata ikitokea mtu kafunuliwa jambo jipya na Roho Mtakatifu la kwenda kufundisha, hawezi kupata nafasi kwasababu tayari kalenda ya nini cha kufundisha mwaka mzima imeshawekwa, na lazima aifuate hiyo!.
Leo hii ili uaminike kuwa wewe mchungaji au mtumishi wa Mungu ni lazima uwe umepitia chuo cha biblia na theolojia, ukisema unao wito wa Roho Mtakatifu bila kupitia mambo hayo huwezi kueleweka. (Huo ni unikolai), ambao Bwana Yesu kasema anauchukia!!!.
Unikolai hautaki kabisa Uongozo wa Roho Mtakatifu, unampinga Roho Mtakatifu siku zote.
Na shetani anajua kanisa linaloongozwa na Roho Mtakatifu ni hatari sana katika ufalme wake. Na yeye hataki watu waende mbinguni.
Hivyo atafanya juu chini kumzimisha Roho ndani ya kanisa, lakini ashukuriwe Mungu, katikati ya giza nene ipo Nuru mahali.
Bwana anao watu wake mahali fulani katika kila Taifa, ambao hawajamzimisha Roho.
Bwana atusaidie na sisi tuwe miongoni mwa hao ambao hawajamzimisha Roho.
1 Wathesalonike 5:19 “Msimzimishe Roho”
Maran atha!
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
Kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu?
AHADI YA ROHO ILIYOSALIA SASA KWA KIPINDI CHETU.
UFUNUO: Mlango wa 3 part 3
Tusome,
1 Yohana 2:16 “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
1 Yohana 2:16 “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”.
Kiburi cha Uzima ni kiburi mtu anachokipata kutokana na vitu alivyonavyo vya kidunia (hususani mali).
Watu ambao hawajamjua Mungu, uzima wao wameuweka kwenye mali, wanapokuwa na mali nyingi ndipo wanapojiona waoni watu (wanao uzima), wakikosa wanajiona wao si kitu.. hivyo inapotokea wanapata mali hizo zinawapa kiburi na kuwafanya wabadilike tabia mbele za Mungu na wanadamu.
Lakini Bwana Yesu alisema maneno haya..
Luka 12:15 “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. 16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; 17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. 18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. 19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. 20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? 21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu”.
Luka 12:15 “Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
16 Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; 17 akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
18 Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu.
19 Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
21 Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu”.
Je na wewe uzima wako umeuweka wapi? Je ni kwenye nyumba ulizozijenga? Je ni hizo ndizo zinazokupa kiburi hata kumdharau Mungu na kuwadharau wengine?, Je ni fedha ulizonazo?, au Magari?, au Vyeo? Inazokufanya uone injili ni habari zilizopitwa na wakati?..kama ndio basi unacho kiburi cha uzima pasipo kujijua, ambacho maandiko yanasema hakitokani na Mungu, kwasababu mali ni kama maua leo ipo kesho haipo, hivyo si ya kujitumainisha nayo, kamwe isituletee kiburi.
Je umejitajirisha wapi leo? Mbinguni au duniani, umejiwekea hazina yako wapi?, Mbinguni au duniani?
Bwana atusaidie tusiwe na kiburi cha uzima.
FANYA BIDII ZOTE ULE MATUNDA YA UZIMA.
KARAMA YA MUNGU NI UZIMA WA MILELE.
JE WEWE NI LAZARO YUPI, WA KWANZA AU WA PILI?
Imekuwa changamoto kubwa kwa mtu anayeokoka mara ya kwanza, au kwa yule mtu ambaye anahitaji kumwabudu Mungu katika njia sahihi, kutambua kanisa sahihi la kumfanya yeye amwabudu Mungu wake katika Roho na kweli.
Hiyo ni kutokana na kuzuka kwa imani nyingi potofu, na watu wenye nia mbaya, ambao lengo lao ni kuwapoteza watu na sio kuwaokoa.
Hivyo wewe kama mkristo huna budi kuwa mchunguzi sana, na Mungu pia ameruhusu tuwe watu wa namna hiyo sawasawa na (1Timotheo 4:1 )..kwasababu hizi ni zama za uovu.
Lakini pamoja na kwamba kuna makanisa na imani nyingi za uongo ulimwenguni, bado suluhisho sio kukaa nyumbani..kwasababu ni agizo la Bwana kwamba tusiache kukusanyika pamoja na wengine, kumwabudu yeye(Waebrania 10:25)..Na faida zake ni nyingi sana, tofauti na utakavyokwenda mwenyewe mwenyewe, wakati wote. Hata ukutanapo na jiwe katika chakula haikufanya wewe umwage chakula chote..utalitoa lile jiwe utaendelea kula..Vivyo hivyo na katika habari ya makanisa.
Lakini pia kumbuka kujiunga na kanisa sio tiketi ya wewe moja kwa moja kwenda mbinguni..lakini kanisa sahihi lina sehemu kubwa sana ya kukusaidia wewe kufika mbinguni.
Makanisa yanafananishwa na SHULE. Kwamfano mwanafunzi anayehitimu shule ya msingi..akienda sekondari, huwa anakutana na chaguzi nyingi sana za shule zikimwita..na kila shule inajinadi kuwa ina ufauluji mzuri, na mazingira mazuri ya kusomea..
Hivyo ni wajibu wa mwanafunzi mwenyewe kufanya uchunguzi wake mwenyewe je, ni kweli shule hiyo ina vigezo vya kumsaidia kufaulu? .Uchaguzi wa shule mbaya utamweka katika hatari kubwa sana ya kufeli haijalishi atakuwa na akili nyingi kiasi gani.
Lakini pamoja na kwamba shule itakuwa na ubora na ufauluji mzuri, bado bidii ya mwanafunzi mwenyewe binafsi inahitajika..
Hivyo vyote viwili vinasaidiana na vina umuhimu, na vinakwenda sambamba. Tengeneza picha mwanafunzi anayesema mimi siendi shule..nitatafuta tu namba yangu ya mtihani wa mwisho siku hiyo ikifika nikafanye.. nitakuwa najisomea peke yangu nyumbani kwa miaka yote hiyo.. Jiulize mwanafunzi kama huyo atafaulu kweli..lengo la shule kuwekwa ni kumsaidia mwanafunzi ufauluji wake, kwa kukutanishwa na waalimu wa kumsaidia na kumpa nidhamu ya usomaji bila kuvutwa na mambo mengine..
Halikadhalika ukristo na kanisa ni vitu vinavyokwenda sambamba, na ni wajibu wako kuchagua kanisa sahihi litakalokusaidia kufanikisha safari yako ya wokovu hapa duniani.
Mpaka hapo naamini umepata picha..hivyo vifuatavyo ni vigezo muhimu sana vya kuukusaidia kutambua kanisa sahihi ni lipi
1) YESU KRISTO ndio kiini cha imani hiyo.
Tunapouzungumzia ukristo, tunamzungumzia Yesu Kristo, kanisa lisilomfanya Kristo peke yake ndio msingi wa imani hiyo. Ni kanisa la uongo. Ukiona halimtaji Kristo kwa kila kitu..Kimbia hilo kanisa..ikiwa jina la nabii au kiongozi ndio linatamkwa na kupewa heshima kubwa kuliko Kristo..ondoka haraka sana hapo..
Vilevile ukiona Bwana Yesu analinganishwa na watakatifu wengine, kana kwamba na wenyewe ni wapatanishi wa dhambi zetu kama yeye..mfano wa Yosefu na Maria. Ondoka pia hapo, haijalishi litakuwa na wafuasi wengi au zuri kiasi gani.
Wakolosai 2:18-19 [18]Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; [19]wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua Kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.
2) Pili, kanisa la kweli Linaamini Biblia Takatifu tu ndio mwongozo wake.
Ni lazima liamini Biblia yenye vitabu 66, na si zaidi wala pungufu..yapo madhehebu ambayo yameongeza vitabu vya Apokrifa katika biblia na kuifanya iwe na vitabu 73.
Ukiona dhehebu hili ondoka hapo, vitabu vyovyote nje ya vile vinavyojulikana yaani 66 havijaviviwa Roho Mtakatifu.
Ufunuo wa Yohana 22:18 [18]Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Halikadhalika yapo mengine yanaamini katika mapokeo, kama vile waaminivyo bibila takatifu hayo pia yakimbie ni upotevu na udanganyifu mwingi upo ndani yake.
Utapotezwa tu..
3) Tatu linafundisha mafundisho yanayolenga ufalme wa mbinguni.
Yohana mbatizaji alipoanza kuhubiri alisema tubu kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia..Bwana Yesu naye alihubiri kwa kusema tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia(Mathayo 3:2, 4:17)…mitume nao walihubiri na kufundisha vivyo hivyo.
Nasi pia tujue ukristo, ni habari za ufalme wa mbinguni na sio ufalme wa duniani..Ikiwa utakuwepo mahali unafundishwa na kushinikizwa tu juu ya mambo ya ulimwenguni wakati wote..yaani mali, na vitu vya ulimwenguni..hiyo ni ishara kuwa kanisa hilo ni la uongo..hivyo ondoka hapo.
Ndio zipo nyakati, hayo nayo yatafundishwa katika kanisa lakini sehemu yao iwe ndogo sana, yasiwe kiini cha mtu kuwepo kanisani kumwabudu Mungu. Kanisa ni habari za ulimwengu ujao.
4) Utakatifu na Upendo:
Huu nao ni msingi mwingine wa kanisa hai la Kristo, kufundishwa utakatifu na Upendo ambavyo vyote viwili ndio vinatajwa kama malango ya kumuona Mungu sawasawa na (Waebrania 12:14, na 1Yohana 4:7-8 ).
Kanisa ambalo, watu wake wanamwabudu Mungu watakavyo, wanawake na vijana wanavaa hohe hahe, wanaenda kanisani kama vile disco na hawaambiwi chochote, hawakemewi dhambi, hawaonywi..hilo sio kanisa hai.
5) Karama za Roho:
Alipo Roho Mtakatifu, atadhihirisha na uwepo wake pia, kama kanisa haliruhusu karama kama za uponyaji wa Roho, unabii, uinjilisti, lugha, maombi n.k. ni dalili kuwa hilo sio kanisa la Kristo.
Yapo ambayo yanaamini lakini hayahimizi, haya yanaweza yasiwe na shida..lakini yapo ambayo hayaamini kabisa kiasi kwamba lolote likitokea waweza fukuzwa kanisani..haya ndio uyakimbie, kabisa kwasababu yatakuua kiroho, ushindwe kumtumikia Mungu kwa karama aliyoiweka ndani yako.
1 Wakorintho 12:7-11 [7]Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. [8]Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; [9]mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; [10]na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; [11]lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
Hivyo kwa vigezo hivyo, naamini utakuwa umepata mwanga wa kujua kanisa la kweli ni lipi.
Hivyo chukulia kwa uzito suala hili, lipime kanisa lako, kwasababu wengi wameshafungwa katika kamba za makanisa ya uongo na bado wanaendelea nayo..Usiogope kutoka kwasababu atakayehukumiwa ni wewe sio hilo dhehebu.
Nikitakie uchaguzi mwema.
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
FUNDISHO KUU LA NEEMA YA MUNGU KWETU.
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
Kama jina lake lilivyo “Maji ya Farakano”…maana yake ni maji yanayoondoa mafarakano.
Mtu yeyote katika Israeli ambaye alikuwa amejitia unajisi kwa kugusa maiti ya mtu, alikuwa amejifarakanisha na Mungu, hivyo hana budi kujitakasa, ili akubalike mbele za Mungu.
Na kitu pekee kilichokuwa kinaweza kumtakasa ni maji hayo maalumu, yaliyojulikana kama MAJI YA FARAKANO.
Maji hayo yalikuwa yanatengenezwa kwa majivu ya Ng’ombe mwekundu, ambaye hajazaa bado, wala hajatiwa nira, wala hajakamuliwa maziwa.
Ng’ombe huyu alikuwa ni maalumu kwa ajili ya upatanisho Wa dhambi za wana wa Israeli.
Baada ya kuchinjwa na kuteketezwa, majivu yake yalihifadhiwa na kuchanganywa na maji safi, sasa maji hayo ya majivu ya huyo ng’ombe ndio yaliyoitwa maji ya Farakano.
Endapo mtu yeyote atagusa maiti basi atajitakasa kwa kunyunyiziwa maji hayo ya farakano na atakuwa safi. Na mtu yeyote asiyejitakaswa na maji hayo sheria ilikuwa ni kuuawa.
Hesabu 19:1 “BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado; 3 nanyi mtamleta kwa Eleazari kuhani, naye atakwenda naye nje ya kambi, na mtu mmoja atamchinja mbele yake; 4 kisha Eleazari kuhani atatwaa katika damu yake kwa kidole chake, na kuinyunyiza damu yake kuelekea upande wa mbele wa hema ya kukutania mara saba; 5 kisha mtu mmoja atamchoma moto huyo ng’ombe mbele yake; ngozi yake, na nyama yake, na damu yake, pamoja na mavi yake pia atachoma moto; 6 kisha kuhani atatwaa mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, na kuvitupa katika huo moto unaomchoma ng’ombe. 7 Ndipo kuhani atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, kisha baadaye ataingia kambini, naye kuhani atakuwa najisi hata jioni. 8 Na huyo aliyemchoma moto ng’ombe atazifua nguo zake majini, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa najisi hata jioni. 9 Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng’ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi. 10 Na yeye ayazoaye majivu ya huyo ng’ombe atazifua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; na jambo hili litakuwa amri ya milele, kwa wana wa Israeli, na wa mgeni akaaye kati yao. 11 Mtu agusaye maiti ye yote atakuwa najisi muda wa siku saba; 12 naye atajitakasa kwa yale maji siku ya tatu, na siku ya saba atakuwa safi; lakini kama hajitakasi siku ya tatu, ndipo na siku ya saba hatakuwa safi. 13 Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado”.
Hesabu 19:1 “BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,
2 Hii ndiyo amri ya sheria BWANA aliyoagiza, akisema, Waambie wana wa Israeli wakuletee ng’ombe mke mwekundu asiye na kipaku, mkamilifu, ambaye hajatiwa nira bado;
3 nanyi mtamleta kwa Eleazari kuhani, naye atakwenda naye nje ya kambi, na mtu mmoja atamchinja mbele yake;
4 kisha Eleazari kuhani atatwaa katika damu yake kwa kidole chake, na kuinyunyiza damu yake kuelekea upande wa mbele wa hema ya kukutania mara saba;
5 kisha mtu mmoja atamchoma moto huyo ng’ombe mbele yake; ngozi yake, na nyama yake, na damu yake, pamoja na mavi yake pia atachoma moto;
6 kisha kuhani atatwaa mti wa mwerezi, na hisopo, na sufu nyekundu, na kuvitupa katika huo moto unaomchoma ng’ombe.
7 Ndipo kuhani atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, kisha baadaye ataingia kambini, naye kuhani atakuwa najisi hata jioni.
8 Na huyo aliyemchoma moto ng’ombe atazifua nguo zake majini, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa najisi hata jioni.
9 Kisha mtu mmoja aliye safi atayazoa majivu ya huyo ng’ombe, na kuyaweka yawe akiba katika mahali safi nje ya kambi, nayo yatatunzwa kwa ajili ya mkutano wa wana wa israeli, kuwa ndiyo maji ya farakano; ni sadaka ya dhambi.
10 Na yeye ayazoaye majivu ya huyo ng’ombe atazifua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; na jambo hili litakuwa amri ya milele, kwa wana wa Israeli, na wa mgeni akaaye kati yao.
11 Mtu agusaye maiti ye yote atakuwa najisi muda wa siku saba;
12 naye atajitakasa kwa yale maji siku ya tatu, na siku ya saba atakuwa safi; lakini kama hajitakasi siku ya tatu, ndipo na siku ya saba hatakuwa safi.
13 Mtu awaye yote agusaye maiti wa mtu aliyekufa, asijitakase, yuatia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atakatiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ukali juu yake bado”.
Lakini katika agano jipya hatuna sheria hiyo, kwamba tukigusa maiti tunakuwa najisi mpaka tunyinyuziwe maji hayo.
Unajisi katika agano jipya sio kushika maiti, wala si kula bila kunawa, si kukaa bila kuoga, wala si kuingia kanisani bila kutawadha..ni vizuri kufanya hayo kwa lengo la usafi tu!, Lakini haitusogezi karibu na Mungu n.k.
Bali unajisi hasa ambao unatuweka mbali na Mungu ni kutoa maneno machafu mdomoni mwetu, na kuwaza mabaya moyoni mwetu.
Marko 7:15,18-23 “Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu….. 18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; 19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. 20 Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, 22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. 23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”
Marko 7:15,18-23 “Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu…..
18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi;
19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
20 Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.
21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi”
Mambo haya ndio yanayotufarakanisha sisi na Mungu na kutufanya kuwa najisi mbele zake.
Na unajisi huo hautakaswi kwa Maji ya Farakano, bali kwa Neno la Mungu.
Waefeso 5:25 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”.
Waefeso 5:25 “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa”.
Na neno la Mungu, ambalo ndio maji yatutakasayo linasema..
Matendo ya Mitume 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
Matendo ya Mitume 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”
Hilo ndilo Neno la Mungu litusafishalo na kutuondolea UNAJISI WOTE!. Na ndio maji yetu ya Farakano katika agano jipya.
Je umetubu na kubatizwa kwa jina lake Yesu Kristo?..Je umepokea Roho Mtakatifu?..Kama bado unangoja nini?.
Hizi ni siku za mwisho na Bwana yu karibu kurudi, na walio najisi wote hawataurithi uzima wa milele.
Maran atha!.
Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?
Nini maana ya usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka!.(Kumbukumbu 25:4)
JIEPUSHE NA UNAJISI.
TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.
WhatsApp
Ni wapi katika biblia panaonyesha kuwa suruali ni vazi la kiume tu? Na vipi juu ya kanzu!, mbona kama ni mfano wa gauni lakini linavaliwa na wanaume, kwanini Suruali isivaliwe pia na wanawake!
Jibu: Vazi la Suruali mara ya kwanza katika biblia lilivaliwa na Makuhani.
Mungu aliwapa amri makuhani watengeneze suruali ambazo zilitofautiana kimaumbile, waliambiwa watengeneze suruali fupi (yaani kaptula), Na vile vile walikuwa wanavaa zile ndefu ambazo zilifika kabisa mpaka chini kwenye viiko vya miguu.
Kutoka 28:41 “Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani. 42 Nawe wafanyie SURUALI ZA NGUO YA KITANI, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani; 43 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake”.
Kutoka 28:41 “Nawe mvike huyo nduguyo Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.
42 Nawe wafanyie SURUALI ZA NGUO YA KITANI, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;
43 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake”.
Na katika Israeli hakukuwa na Kuhani Mwanamke!, Makuhani wote walikuwa ni wanaume. Hivyo lilikuwa ni vazi la kiume. (Soma pia Kutoka 39:27, na Walawi 6:10)
Vile vile tunaweza kulithibitisha hilo kipindi kile cha akina Shedraka, Meshaki na Abednego. Wakati Mfalme Nebukadneza alivyowatupa katika lile tanuru la moto, maandiko yanasema walitupwa kule hali wamevaa suruali zao na kanzu zao na joho zao.
Danieli 3:21 “Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa SURUALI ZAO, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto. 22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego”.
Danieli 3:21 “Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa SURUALI ZAO, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.
22 Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na ile tanuru ilikuwa ina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego”.
Sasa Shedraka, Meshaki na Abednego hawakuwa wanawake, bali wanaume!, na hakuna popote katika biblia panataja au kuonyesha mwanamke kavaa suruali, kama hawa wakina Shedraki au kaagizwa kuvaa suruali kama hawa Makuhani.Hakuna!!. Ikifunua kuwa hilo ni vazi la kiume!
Maandiko yanasema.
Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.
Mwanamke yeyote kuvaa suruali ni machukizo mbele za Mungu, Suruali sio vazi la kumsitiri mwanamke, hakuna mwanamke yeyote anayevaa suruali na kuonekana kama kajisitiri, badala yake ataonekana kama kajidhalilisha au kajifunua..Na maandiko yanasema wanawake na wavae mavazi ya kujisitiri.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani”
Hivyo mwanamke yeyote hapaswi kuvaa suruali, wala vimini wala nguo zozote zinazochora maungo yake.
Na pia Kanzu, halikuwa vazi la kike!, kanzu lilitumika kama vazi la Nje!, kama vile mtu anavyovaa koti!.. Ndio maana utaona hapo wakina shedraka, Meshaki na Abednego walikuwa wamevaa suruali na kanzu kwa nje. Kwahiyo Kanzu halikuwa gauni, Gauni ni vazi la kike lililotengenezwa mahususi kufuatia maumbile ya mwanamke!. Na ndilo wanawake wa kikristo wanapaswa walivae.
Sasa inawezekana ulikuwa hulijui hili kuwa hilo ni vazi la kiume, lakini leo umejua na ndani ya kabati lako kumejaa suruali, nataka nikuambie, usingoje kesho, leo leo zitoe kazichome moto!, wala usimpe mtu!.. zichome na tafuta magauno au sketi ndefu!, usiogope kuonekana mshamba mbele ya ulimwengu!. Ni heri uonekane mshamba lakini unakwenda mbinguni kuliko kuonekana wa kisasa lakini sehemu yako ni katika lile ziwa la moto!.
USIYAACHE MAVAZI YAKO NA KWENDA UCHI!
Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?
PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.
VAZI LA YESU HALIGAWANYWI.
Kibiblia mzushi ni mtu anayezusha jambo au mada ambazo lengo lake ni kuleta MIGAWANYIKO!.
Mtu anayezuka katikati ya kanisa na kuzusha mada ambazo anajua kabisa zitaishia kuleta migawanyiko ndani ya kanisa la Kristo, mtu huyo ni Mzushi kibiblia. Kwa lugha ya kiingereza (divisive person).
Na biblia imetoa maelekezo juu ya watu hao, kwamba tuwakatae, (maana yake tusiwape nafasi).
Tito 3:10 “Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; 11 ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe”.
Tito 3:10 “Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae;
11 ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe”.
Mfano wa mada zinazoleta migawanyiko ndani ya kanisa ndio hizo Mtume Paulo alizoziorodhesha katika Tito 3:9..
Tito 3:9 “Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana”.
Mashindano ya dini, hayo yanasababisha kiburi na mwishowe migawanyiko katika kanisa kwasababu yanawaharibu wale wanaosikia…
Kwasababu ndani ya kanisa kuna ambao pia bado ni wachanga katika Imani, sasa endapo wakisikia watu wanashindana (kila mmoja anajiona mjuzi) ni rahisi Imani zao kudhoofika na hata kuiacha ile Imani, au kuegemea upande mmoja na kuudharau mwingine, hivyo tayari migawanyiko imeshaingia.
2Timotheo 2:14 “Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao”.
1Timotheo 6:4 “..amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya”
Na sisi kama wakristo hatuna budi kujihadhari na Uzushi, vile vile watu ambao ni wazushi katika kanisa, baada ya kuwaonya mara ya kwanza na ya pili, na hawataki kubadilika maandiko yametupa ruhusu ya kujiepusha nao!, maana yake kutowapa nafasi yoyote ya kusema au kuchangia chochote!, wabaki kimya au wazungumze wao wenyewe.
UFUNUO Mlango wa 2: Sehemu ya pili.
KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.
Neno “Uchungu wa mauti” lina maana gani kibiblia?
TWAENENDA KWA IMANI NA SI KWA KUONA.
Hizi ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kuuharibu ujana wako kwa wepesi.
Wahuni ni ndio wawe marafiki zako, wazinzi ndio wawe kampani yako, walevi ndio wawe watu wa kukupa raha, wanawake wasengenyaji ndio wawe wajoli wako, njia hii ukiitumia vizuri itakufanikisha haraka sana kwenye malengo yako. Huna haja ya kukaa na vijana wenye hekima, wanaomcha Mungu ya nini?
Ukiliondoa neno hili katika akili yako utafanikiwa..
Zaburi 1:1 Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Wakati wale vijana wengine washamba wanajibidiisha kumpendeza Mungu, sawasawa na
Zaburi 119:9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
Basi wewe, nenda kinyume tu, kataa kulifuata neno la Mungu. Tafuta namna nyingine ya kuisafisha njia yako, Pale unapoambiwa usizini, ona kama huo ni udhaifu, kazini na kila kahaba au mwanamume unayemwona, kwasababu wewe ni mrembo sana, si ndio? kijana maji ya moto.
Kile roho yako inapenda, huna haja ya kujizuia. Usijizuie wala usiwe na kiasi, Ukijisikia kwenda Disko nenda, ukijisikia kuvuta sigara vuta, ukijisikia utukane, fanya hivyo, ukijisikia kutembea nusu uchi barabarani tembea, ukijisikia kujichubua tumia mikorogo yote, kwasababu andiko linalokusapoti kufanya hivyo;
Mhubiri 9:8 Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose marhamu. 9 Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua. 10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; KWA KUWA HAKUNA KAZI, WALA SHAURI, WALA MAARIFA, WALA HEKIMA, HUKO KUZIMU UENDAKO WEWE.
Mhubiri 9:8 Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose marhamu.
9 Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote za maisha yako ya ubatili, ulizopewa chini ya jua; siku zote za ubatili wako, kwa maana huo ni sehemu yako ya maisha; na katika taabu zako ulizozitaabika chini ya jua.
10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; KWA KUWA HAKUNA KAZI, WALA SHAURI, WALA MAARIFA, WALA HEKIMA, HUKO KUZIMU UENDAKO WEWE.
Kati ya watu 7,00,000,000 waliopo duniani leo, zidi kufikiri hakukuwahi kuwa na warembo zaidi yako wewe, na wakajuta, wazuri kupita wewe, wote hao waliokufa walikuwa wadhaifu sana, endelea kudharau maonyo ya waliokutangulia, ona mawazo yao ni ya kizee,
Hata hili andiko usilizingatie,
Mhubiri 12: 12 Tena, zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo;..”
Biblia iendelee kuwa kwako ni kitabu cha wazee,
Kwasababu kujishughulisha na kazi ya Mungu ni ushamba kwako, basi hata na mambo mengine, hayana haraka sana, si umri bado mdogo, utasoma tu siku moja, sasahivi ponda starehe, utafanya kazi tu siku moja, kesha kwenye muvi, chat instagramu, zururazurura, ruka ruka tu huku na huko, kwasababu muda bado upo, .
Wale wanaolishika hili neno achana nao.
Waefeso 5:15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
Ukiyafanikisha haya kwa bidii ,mafanikio yako yapo mbioni.
Liondoe kabisa neno hili akilini mwako, utafanikiwa..
Basi wewe, nenda kinyume tu, kataa kulifuata neno la Mungu. Njia yako utaisafisha vizuri sana, Pale unapoambiwa usizini, ona kama huo ni udhaifu, kadange na kila kahaba au mwanamume unayemwona, kwasababu wewe ni mrembo sana, si ndio? kijana maji ya moto.
Kile roho yako inapenda, huna haja ya kujizuia. Ukijisikia kwenda Disko nenda, ukijisikia kuvuta sigara vuta, ukijisikia utukane, fanya hivyo, ukijisikia kutembea nusu uchi barabarani tembea, ukijisikia kujichubua tumia mikorogo yote, kwasababu andiko linalokusapoti ni hili;
Kati ya watu 7,00,000,000 waliopo duniani leo, zidi kufikiri hakukuwahi kuwa na warembo zaidi yako wewe, wazuri kupita wewe, wote hao waliokufa walikuwa wadhaifu sana, endelea kudharau maonyo ya waliokutangulia, ona mawazo yao ni ya kizee, Kwasababu wewe ni wewe..
Biblia ni kitabu cha wazee,
Kwasababu kujishughulisha na kazi ya Mungu ni ushamba kwako, basi hata na mambo mengine, hayana haraka sana, si umri bado mdogo, utasoma tu siku moja, sasahivi ponda starehe, utakuja kufanya kazi tu siku moja, kesha kwenye muvi, chat instagramu, zururazurura, ruka ruka tu huku na huko, kwasababu muda bado upo, .
Ukiyafanikisha haya kwa bidii bado,mafanikio yako yapo mbioni.
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
Je! Ni dhambi kwa kijana aliyeokoka kuvaa suruali za kubana (model), kunyoa mitindo (mfano kiduku), ?
AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.