Neno kupiga kite limeonekana mara kadhaa katika biblia.
Maana ya “kupiga Kite” ni kutoa pumzi nje, kuashiria aidha kushangazwa, kupata unafuu au kukata tamaa.
Kwamfano mwanafunzi aliyekuwa anasubiria matokeo ya mtihani alioufanya, na wakati anaangalia matokeo kwenye orodha na kuona amefaulu basi unaweza kuona anashusha pumzi. (Kitendo hicho cha kushusha pumzi, kana kwamba kapunguza presha ndani yake, kitendo hicho ndicho kinachoitwa kupiga Kite).
Au mtu aliyejaribu kufanya jambo fulani kwa muda mrefu, asifanikiwe na kuazimia kujaribu kwa mara moja ya mwisho, kama tumaini lake la mwisho, na wakati anangojea kupata tumaini zuri, ghafla yanakuja matokeo mabaya ya kuvunja moyo, mtu wa namna hiyo pia utaona anashusha pumzi, kuashiria kukata tamaa (kitendo hicho pia ni kupiga kite).
Limetumika neno “kupiga” na sio “kufanya”...kwasababu matendo hayo ya kuvuta pumzi au kutoa, yanatamkwa kwa kuanza na neno “kupiga”..kwamfano “kupiga miayo”, huwezi kusema “kufanya miayo”.
Katika biblia Neno hilo limeonekana mara kadhaa.
Maombolezo 1:11 “Watu wake wote hupiga kite, Wanatafuta chakula; Wameyatoa matamaniko yao wapate chakula Cha kuihuisha nafsi; Ee BWANA, tazama, uangalie; Kwa maana mimi nimekuwa mnyonge”.
Pia,
Maombolezo 1:4 “Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu”.
Unaweza kusoma pia 9, utaona Neno hilo hilo.Unaweza kusoma pia Maombolezo 1:21, na Zaburi 90:9 , utaona Neno hilo hilo.
Je umemwamini Bwana Yesu?..kumbuka ulimwengu huu unapita na mambo yake yote, miaka yetu inapukutika kama kite, anaanza na matumaini inaishia na huzuni na kukata tamaa, lakini kama tukiwa ndani ya Yesu itaanza na huzuni lakini itaishia na furaha.
Zaburi 90:9 Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako, Tumetowesha miaka yetu kama kite.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
Je kupiga miayo ni ishara ya mapepo?
TAFUTA KUIFANYA KAZI YA MUNGU KWA HUDUMA MUNGU ALIYOIWEKA NDANI YAKO.
Amwimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.
Rudi nyumbani
Podo ni kimfuko au kibegi kidogo aidha cha ngozi au malighafi nyingine, ambacho hutumika kubebea mishale.
Utalisoma Neno hilo katika vifungu hivi;
Mwanzo 27:1-3[1]Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.[2]Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.[3]Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
Soma pia Ayubu 39:23, Isaya 49:2, Yeremia 5:16
Lakini Hiyo inafunua nini rohoni? Sikuzote askari makini huwa habebi mchale mmoja anapokwenda vitani..atahitaji Furushi la mishale kujihakikishia ushindi wake dhidi ya adui zake. Na ndio hapo atahitaji podo la kuihifadhia hiyo mishale yake.
Ni kama mwanajeshi, hawezi kutegemea risasi moja kujihakikishia ushindi atakuwa na mkanda wa risasi, ili adui yake ajapo amshindilie vya kutosha..
Halikadhalika na sisi kama wakristo, hatuna budi kuwa na podo zetu zenye mishale mingi ya kumpiga yule adui.Hatumpigi shetani kwa maombi tu peke yake, vinginevyo tutakwama mahali.. tutampiga kwa mshale wa kuhibiri injili pia, kwa mshale wa kutenda matendo mema, kwa mshale wa kumtolea Mungu sadaka, kwa mshale wa kuwasaidia wenye uhitaji, kwa mshale wa utakatifu n.k.
Hapo ndipo tutakuwa tumezijaza podo zetu silaha.
Embu soma kwa makini vifungu hivi;
Zaburi 127:4-5[4]Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.[5]Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.
Nasi tujitahidi kujaza podo zetu silaha nyingi ili shetani asipate upenyo wa kutushambulia kirahisi.
Bwana akubariki
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pomboo ni nini katika biblia?(Kutoka 25:5, Ezekieli 16:10)
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?
Je ni kweli miaka yetu ya kuishi ni 80 tu (kulingana na Zaburi 90:10).
KUWA RAFIKI WA DUNIA NI KUWA ADUI WA MUNGU.
Mjoli ni mfanyakazi-mwenza, Ni mtu unayefanya naye kazi moja inayofanana.. Kwamfano kama wewe ni mwalimu, ukakutana na mwalimu mwenzako huyo ni mjoli wako…Kama wewe ni mhubiri ukakutana na mhubiri mwenzako huyo ni mjoli wako, kama wewe ni mkulima ukakutana na mkulima mwenzako huyo ni mjoli wako..
Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi kwenye biblia..
Mathayo 18:23-35[23]Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.[24]Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talantaelfu kumi.[25]Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni.[26]Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.[27]Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.[28]Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinarimia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho.[29]Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.[30]Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni.[31]Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.[32]Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;[33]nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?[34]Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.[35]Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
Wafilipi 4:3[3]Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
Soma pia..Wakolosai 1:7 ,4:7, Ufunuo 19:10, 22:9.
Vivyo hivyo na sisi watakatifu ulimwenguni kote tuliookolewa na Yesu Kristo, kila mmoja ni mjoli kwa mwenzake. Hivyo hatuna budi kupendana, kutumikiana, kusameheana.. Maadamu tupo katika shamba moja na kazi moja, tunapaswa kuujenga ufalme wa Mungu kwa nguvu zetu zote. Huku tukizingatia misingi ya Biblia, na sio ya kidhehebu au kidini
Yule aliyemzuia Yohana asimsujudie alikuwa ni Mwanadamu au Malaika?
Makuruhi ni nini, kama tunavyosoma katika biblia?
JINSI YA KUEPUKA KUUMIZWA MOYO KUSIKOKUWA NA SABABU.
EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.
Maandiko yanasema siku zetu za kuishi ni miaka70 tukiwa sana na nguvu ni miaka 80, sasa swali mbona kuna wengine wanaizidi hiyo miaka na kufikisha hata miaka 90?
Tusome,
Zaburi 90:10 “Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Na kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana chapita upesi tukatokomea mara”.
Tunapaswa pia tujiulize kwanini kuna watu hawaifikii hiyo miaka 70 au 80, ambayo Mungu amesema mwanadamu ataiishi, badala yake wanakufa katika umri mdogo na hata wengine katika uchanga kabisa?..Je Mungu ni mwongo?.
Jibu ni la! Mungu si mwongo, alipotaja umri huo wa miaka 70-80 kama ndio umri wa mwanadamu hakumaanisha kuwa ndio amri/sheria kwamba kila mtu ni lazima aufikie huo, na asizidi hapo, hapana! bali alitaja huo umri kama Wastani wa maisha ya mtu.
Maana yake wastani wa umri wa mwanadamu ni kati ya miaka 70 hadi 80. Ikiwa na maana kuwa wanadamu wengi watakufa katikati ya huo umri. Lakini hiyo haimaanishi kuwa ni wote!.. bali wengi wao.
Wapo watakaofika miaka 90 au hata 100, lakini ni wachache sana, ukilinganisha na wanakaokufa kati ya umri wa miaka 70-80. Na wapo watakaokufa chini ya umri huo.
Na kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda ni kama wastani huo wa umri wa wanadamu unazidi kushushwa kutokana na kuongezeka kwa maasi.
Wanadamu wa kwanza walikuwa wanaishi hata miaka elfu, lakini wastani wa miaka hiyo ilikuja kushushwa hadi miaka 120, baada ya gharika..Na ikaja kushushwa zaidi hadi miaka 80 wakati wa Daudi, na sasa pengine wastani huo umeshushwa zaidi, kulingana na uhalisia wa takwimu za watu wanaokufa sasa, ni wachache sana wanaofika hata hiyo miaka 70.
Lakini yote katika yote iwe tunaishi miaka 50 au 80 au 100, maisha yetu duniani bado ni mafupi tu! ukilinganisha na umilele ambao unakuja mbele yetu baada ya kifo.
Itatufaidia nini tuishi miaka 120 ya dhambi hapa duniani halafu tukatumikie mamilioni ya miaka katika ziwa la moto?.
Ni heri tuishi miaka 80 au 100 katika kumtumikia Mungu, na mwisho tukaishi mamilioni ya miaka ya raha katika mbingu mpya na nchi mpya.
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
Binadamu wa kwanza aliishi miaka mingapi?
Nuhu alipataje ujuzi wa kuwatambua wanyama wale wote na kuwaweka ndani ya Safina?
SHUSHANI NGOMENI NI WAPI KWA SASA?
WhatsApp
Ni wale wa wayahudi wa kimwili au kiroho?, yaani ni wale wazaliwa wa Uyahudi au wale walimomwamini Kristo Yesu na kufanyika kuwa wayahudi kwa namna ya rohoni. (Ufunuo 2:9, ufunuo 3:9)?.
Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani. 10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”.
Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani.
10 Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima”.
Wayahudi wanaozungumziwa hapo ni wayahudi kwa kuzaliwa kabisa, ambao walikuwa wanajiona kama wao ndio Wayahudi kweli kweli, yaani uzao wa Mungu mteule, lakini Mungu alikuwa anawaona tofauti, kwasababu walikuwa wanaipinga injili ya Masihi, yaani Yesu Kristo, ambaye alitabiriwa katika torati yao hiyo hiyo (Matendo 3:20-24 na Yohana 5:39).. Mfano wa hao ni Mafarisayo na Masadukayo, ambao walikuwa ni wayahudi kwa kuzaliwa lakini walikuwa wanaenda kinyume na maneno ya uzima ya Bwana YESU.
Katika nyakati za kanisa la kwanza, waliokuwa maadui wa kwanza wa Injili ya Bwana Yesu, walikuwa ni wayahudi, ambao walikuwa wanaona wivu wanapowaona watu wengine hususani wa Mataifa wanamgeukia Mungu wa Israeli.
Sasa Kundi hilo la wayahudi wasioamini Injili ya Bwana Yesu na kuipiga vita, ndio Bwana anawaita “sinagogi la shetani”..Na wayahudi hawa walikuwa wamezagaa sehemu nyingi duniani kote, kila walipowaona watu wa mataifa wanamwamini Yesu, walikuwa wanaitumia torati yao kuwavunja moyo na kuwaaminisha mambo yaliyo kinyume na injili ya Kristo.
Matendo 14:1 “Ikawa huko Ikonio wakaingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi; na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na la Wayunani wakaamini. 2 Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa Mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu”.
Matendo 14:1 “Ikawa huko Ikonio wakaingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi; na kwa vile walivyonena, kundi kubwa la Wayahudi na la Wayunani wakaamini.
2 Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa Mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu”.
Ni heri kama wangekuwa hawaiamini tu!, lakini walikuwa wanaipiga vita injili ya Bwana Yesu..mfano wa hao ni Mafarisayo na Masadukayo. Mitume waliwatahadharisha sana watu wa mataifa wajihadhari na wayahudi hao, (Kitabu cha Wagalatia chote ni waraka wa Mtume Paulo kwa wakristo wa Galatia, akionesha kuhuzushwa kwake kwa jinsi walivyogeuzwa nia kirahisi na kundi hilo la wayahudi wa uongo, na hata kuiacha injili ya kweli).
Myahudi kweli kweli ni yule anayemwamini Bwana Yesu Kristo na maneno yake kama torati ilivyotabiri.
Kumbukumbu 18:15 “Bwana, Mungu wako, atakuondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.”
Sasa hao ndio waliokuwa maadui wa Injili katika kanisa la kwanza, lakini katika siku za hizi za Mwisho vita ni vikali Zaidi, kwasababu shetani hawatumii tena hawa wayahudi kufanya vita na Ukristo. Bali anawatumia wanaojiita wakristo, (ambao kiuhalisia ni wakristo wa uongo) kuuangamiza ukristo wa kweli.
Leo hii ukihubiri injili kamili ya kimaandiko au ukiuishi utakatifu, vita vya kwanza vitatoka kwa “wanaojiita wakristo”.. shetani anawatumia Zaidi wanaojiita wakristo kuliko watu wa mataifa.
Ni kipindi cha kuwa macho sana na kuyasoma maandiko, ili tuweze kuushinda upotofu wa shetani.
TOFAUTI KATI YA HEKALU, SINAGOGI NA KANISA NI IPI?
NI NANI ALIYEKUPA MAMLAKA HII UYATENDE HAYA?
Kwanini Paulo aungane na wale watu wanne wenye nadhiri?
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
MAWE YALIYOKWISHA KUCHONGWA MACHIMBONI.
SWALI: Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.” (Marko 9:49)
JIBU: Kama tunavyofahamu kazi kubwa ya chumvi ni kiungo, kiasi kwamba chakula kinaweza kikawa ni kizuri kweli, kinavutia kwa macho, kina harufu nzuri, lakini kikikosa chumvi huwa kinapoteza ladha yote, haijalishi kilitengenezwa kwa viungo vingi kiasi gani.
Vivyo hivyo na sisi kwa Mungu, ili tuwe tumestahili kuingia katika ufalme wake wa mbinguni, ni lazima tuwe kama chakula kilichokamilika kwake, tukikosa ladha tu ya chumvi yake, kamwe hatuwezi kuuingia ufalme wake.
Sasa ili kuelewa vizuri chumvi hiyo tunaipate, au inakujaje kujaje ndani yetu, tusome Habari yenyewe, kuanzia vifungu vya juu yake kidogo, ili tupate picha kamili;
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika; 44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [ 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.] 47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum; 48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki. 49 KWA SABABU KILA MTU ATATIWA CHUMVI KWA MOTO. 50 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi”.
Marko 9:43 “Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima u kigutu, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehanum, kwenye moto usiozimika;
44 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
45 Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [
46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]
47 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum;
48 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.
49 KWA SABABU KILA MTU ATATIWA CHUMVI KWA MOTO.
50 Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi”.
Umeona, baada ya maagizo hayo, mwishoni kabisa Kristo ndio anasema na sisi tutatiwa chumvi lakini si kwa kitu kingine bali kwa MOTO.
Na moto wenyewe ndio huo, aliokuwa anauzungumzia hapo juu, kwamba kiungo chako kimoja kikikukosesha kikate, unapokata kiungo chako, utasikia maumivu kweli, lakini ndio tiba ya kukufikisha mbinguni, ndio chumvi yenyewe inayokufanya ulete ladha mbele ya Mungu.
Hiyo ikiwa na maana kuwa, hata wewe, binafsi unafahamu kabisa vipo vitu ambavyo vinakukosesha vinakufanya usimrudie Mungu wako kikamilifu, inawezekana ni kazi Fulani, au kampani ya marafiki zako walevi, au wahuni, au wadada wenzako wadadisi, au ndugu zako, au binti yule, au kijana yule. Kumbuka Bwana amekupa amri hii, ikiwa wanakufanya uikose mbingu, Achana nao, haraka sana bila kuangalia nyuma.. wakatae..
Ni kweli inauma,unapoviacha hivyo vitu, au unapowaacha ni moto utausikia, lakini ndivyo unavyotiwa chumvi na Bwana. Kwasababu usipoukubali moto huo sasa, utakutana nao siku ile utakaposhuka Jehanum ukifa.
Huu si wakati, wa kuikumbatia dhambi hata kidogo, si wakati wa kumwangalia mtu Fulani anasema nini juu ya Maisha yako ya milele, mbinguni utakwenda peke yako, vilevile usipotubu jehanumu utakwenda peke yako. Ni heri upitie shida hapa duniani, kule ukaishi milele kwa rah a na Mungu, kuliko kupitia raha za kitambo hapa duniani, halafu kule ukaishia motoni milele.
Hivyo ndugu yangu kubali kutiwa chumvi sasa, kwa kukubali kuacha yale ambayo yameshikamana sana na wewe kwa wakati huu wa siku za mwisho.
Waebrania 12:1 “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu”,
Bwana akubariki.
“Ninyi ni chumvi ya dunia” Andiko hilo lina maana gani?
OLE WAKO KORAZINI NA BETHSAIDA.
Nini tofauti kati ya moyo na roho?
UNYAKUO.
SWALI: Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake”?
JIBU: Ukisoma kuanzia mstari wa juu yake kidogo anasema;
Luka 6:39 “Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili? 40 Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake”.
Luka 6:39 “Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili?
40 Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake”.
Akiwa na maana kuwa, Yule anayeongozwa hawezi kumzidi maarifa kiongozi wake, kama akiwa ni kipofu hata Yule anayeongozwa atakuwa ni kipofu pia, na mwisho wao wote utakuwa ni shimoni tu, Kama alikuwa na maarifa fulani kidogo, hata Yule anayeongozwa atakuwa na maarifa hayo hayo madogo, kama alikuwa na mengi, vivyo hivyo na mwanafunzi wake atakuwa nayo. Lakini hawezi kumzidi kimo.
Halikadhalika katika kanisa la Kristo, ikiwa Kiongozi anayelichunga kanisa, atakuwa anafundisha mafundisho potofu, hakuna namna washirika wake wataacha kuyaishi na kufundisha mafundisho hayo hayo kwa wengine, haiwezekani wakafundishe mafundisho ya haki. Kwasababu Mwanafunzi hampiti mwalimu wake,
Hiyo ni kututahadharisha, tuwe makini na viongozi tunaowachagua watuongoze. Ikiwa viongozi wetu hawatuhimizi kuishi katika utakatifu, na maisha ya haki, na ya ufalme wa mbinguni. Tujue kuwa tutafanana na wao, tutakuwa mfano wa watu wa ulimwengu huu, na mwisho wetu utakuwa ni jehanamu tu pamoja na wao.
Lakini Bwana Yesu aliendelea kusema.. “lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake”. Ikiwa na maana mwanafunzi mzuri anayezingatia, huwa anafikia kiwango cha kulingana na mwalimu wake, Na hapo ndipo Bwana alipokuwa anapataka, lakini si zaidi yake.
Swali la kujiuliza Je! Ni kiongozi yupi uliyemchagua akuongoze?
Bwana Yesu mahali pengine alisema maneno hayo hayo kwa namna nyingine.. Alisema,
Mathayo 10:24 “Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. 25 Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake”?
Mathayo 10:24 “Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake.
25 Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake”?
Ikiwa kama sote ni wanafunzi wa Bwana Yesu, tufahamu pia, Kristo alichukiwa na kudhihakiwa, na kutukanwa na kuitwa Beelzebuli, lakini ikiwa sisi wakati wote ni wakupendwa na dunia na kusifiwa, ni lazima tujiulize, kwanini hatujawa kama mwalimu wetu.
Sehemu nyingine, mwalimu wetu Yesu Kristo, aliwatawadha wanafunzi wake miguu, kama ishara ya unyenyekevu, japokuwa yeye alikuwa ni mkuu kuliko wao, akasema.
Yohana 13:14 “Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. 16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. 17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda”
Yohana 13:14 “Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.
17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda”
Kwahiyo, tukiishi kama Kristo alivyoishi duniani, tutapita njia ile ile aliyoipitia yeye. pale alipostahili kupendwa na sisi tutapendwa, pale alipostahili kuchukiwa na sisi tutachukiwa, Pale aliponyenyekea na sisi tutanyenyekea.
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Je ni sahihi kumwita mtu “Mkuu”?
Tofauti kati ya mtume na mwanafunzi ni ipi kibiblia?
Zaburi 89:48 “Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?”
Awali ya yote ni vizuri kufahamu kuwa Mwandishi aliyeandika maneno haya, alikuwa katika mazingira gani, Mwandishi alikuwa katika mazingira ya Sala (yaani kuomba) na si kuhubiri au kutoa mahusia kama Zaburi nyingine. Kuna maneno ya kuzungumza na Mungu na ya kuzungumza na Watu.
Tunapozungumza na Mungu katika sala, ni kawaida yetu kujishusha..huwezi kujiinua mbele za Mungu kwamba wewe unafaa, hata kama kweli unafaa, huwezi kusema wewe unastahili hata kama kweli unastahili, ni lazima uwe si kitu mbele za Mungu. (Soma Luka 18:11-14).
Vile vile Mwandishi alikuwa anamjua HENOKO mtu wa Saba, baada ya Adamu, ambaye hakuonja mauti, bali alitwaliwa na Mungu bila kufa!.
Hivyo kama angekuwa amemaanisha kuwa kila mtu ni lazima afe, basi atakuwa amesema uongo, maana anamjua Henoko kwamba hakufa. (Na biblia sio kitabu cha uongo!)
Kwahiyo maana yake ni kwamba, Mwandishi hakumaanisha kama watu leo wanavyoutafsiri huo mstari, kwamba kila mtu ni lazima afe, bali alisema vile akiwa na maana nyingine kabisa.
Zaburi hiyo ya 89, yote ni Zaburi ya sala ya unyenyekevu, ambapo mwandishi anasali huku akimwinua Mungu, na kujishusha yeye.. na si Zaburi ya mahubiri wala maonyo!, ndio maana ukianzia mstari wa juu kidogo utaona anasema..
“46 Ee Bwana, hata lini? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto? 47 Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu; Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu! 48 Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?”
“46 Ee Bwana, hata lini? Utajificha hata milele? Ghadhabu yako itawaka kama moto?
47 Ukumbuke jinsi mimi nisivyo wa kudumu; Kwa ubatili gani umeiumba jamii ya wanadamu!
48 Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?”
Sasa ili tuelewe vizuri, hebu chukua mfano umsikie mtu aliye mgonjwa sana anaomba hivi.. “Ebwani nisaidie mimi niliye mdhaifu, niliye karibia na kufa, ni mwanadamu gani leo hii anaweza kuishi bila kufa?”
Bila shaka kwa kuomba huko, atakuwa hajamaanisha kuwa hakuna mtu anaweza kuishi bila kufa!, bali amemaanisha kuwa yeye ni mdhaifu, na wanadamu wote ni wadhaifu na hakuna mtu anaweza kuishi bila kufa kwa nguvu zake na uwezo wake mwenyewe”.
Ndicho mwandishi alichokuwa anakimaanisha hapo?..
Alikuwa katika sala, kuzungumza na Mungu na hivyo kujionyesha kuwa yeye ni mavumbi tu, na wanadamu wote tu mavumbi tu, na ni dhaifu, ndio ikamfanya aombe sala ya namna hiyo ya unyenyekevu, lakini Hakuwa anatoa mahubiri au mafundisho, au mashauri kwa watu kuwa kila mtu ni lazima afe, bali alikuwa katika sala!, anamweleza Mungu na si mwanadamu!..kuonesha ishara ya kujishusha na unyenyekevu mbele za Mungu.
Kwahiyo kwa hitimisho Si kila mtu atakufa!, Henoko hakufa, Nabii Eliya hakufa, kadhalika kuna watu watanyakuliwa wakiwa hai wakati Bwana Yesu atakapokuja mara ya pili (kwenye tukio maarufu lijulikanalo kama unyakuo).
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; HATUTALALA SOTE, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.
1Wakorintho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; HATUTALALA SOTE, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika”.
Hapo anasema “hatutalala sote” maana yake “hatutakufa wote”..Unyakuo utawakuta wengine wakiwa hai, hivyo watakuwa hawajakionja kifo, na vile vile katika maandiko hakuna mahali popote panaposema kuwa kila nafsi itaonja mauti, msemo huo ni maarufu sana lakini kiuhalisia haupo katika biblia.
Lakini kufa si hoja, au kutokufa.. Hoja ni je! Tutakuwa wapi baada ya kifo, au siku ile ya unyakuo itatukutaje?, kama tukifa katika dhambi basi tutangamia milele katika lile ziwa la moto, lakini kama tukifa katika Kristo tutadumu milele Pamoja na Bwana. Vile vile kama tukiwa hai ndani ya Kristo mpaka unyakuo utakapofika basi tutanyakuliwa na kwenda naye mawinguni, lakini kama unyakuo ukitukuta huku tuko nje ya Kristo, basi tutabaki hapa katika dhiki kuu ya Mpinga Kristo.
Na Unyakuo wa kanisa ni siku yoyote! Na wakati wowote!.. Je umejiandaaje?, umempokea Kristo na kubatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu ndani yako?
Bwana yu karibu!
Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki;
SALA YA ASUBUHI
Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?
SALA YA UPONYAJI/MAOMBI YA UPONYAJI.
Biblia inamaana gani inaposema “Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu?”
Katika maandiko tunasoma kwamba Mungu alimshuhudia Musa kuwa ndiye mtu mpole kuliko watu wote duniani, lakini tunaona huyo Musa mbeleni (katika Hesabu 31:15) anakuja kuonekana kama mkatili sana?, hapo sijaelewa!.
Hesabu 31:14 “Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita. 15 MUSA AKAWAULIZA, JE! MMEWAPONYA WANAWAKE WOTE HAI? 16 Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana. 17 Basi KWA AJILI HIYO MWUENI KILA MUME KATIKA HAO WATOTO, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Hesabu 31:14 “Musa akawakasirikia majemadari wa jeshi, na hao maakida wa elfu elfu, na wakuu wa mia mia, hao waliorudi kutoka katika kupiga vita.
15 MUSA AKAWAULIZA, JE! MMEWAPONYA WANAWAKE WOTE HAI?
16 Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana.
17 Basi KWA AJILI HIYO MWUENI KILA MUME KATIKA HAO WATOTO, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Tusome tena..
Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”.
Bwana Mungu hawezi kusema uongo, ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko watu wote duniani, lakini hakuzaliwa hivyo, maandiko yanatuambia pia Musa hapo kwanza alikuwa mtu Hodari wa maneno na matendo.(maana yake hakuwa mpole), ndio maana alikimbia Misri baada ya kugundulika kuwa kaua mtu.
Matendo 7:22 “Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo”.
Sasa unaweza kujiuliza upole alikuja kuutolewa wapi?
Baada ya Musa kumkimbia Farao, alikwenda nchi ya Midiani, akiwa huko Mungu alikishusha kiburi chake, akamnyenyekeza kutoka kuwa Mwana wa kifalme mpaka mchunga mbuzi na kondoo, alichunga mifugo ya Yethro mkwewe kwa miaka mingi sana (Takribani miaka 40), hivyo kile kiburi chake chote kikaisha, yale majivuno yake yote yakaisha, ule ujuzi wake wote wa kuzungumza ukaisha, akawa ni mtu mpole sana, asiyeweza kuongea sana. Na ndipo katika wakati huo Mungu akamtokea na kumwagiza ashuke Misri akawaokoe ndugu zake. (Kwahiyo ni Mungu ndiye aliyemfanya mpole).
Lakini swali ni je! Kama tayari Mungu kamfanya mpole kwanini mbeleni tunaona tena anatoa mashauri ya kuua watu?
Hesabu 31:17 “Basi KWA AJILI HIYO MWUENI KILA MUME KATIKA HAO WATOTO, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Jibu ni kwamba, Musa hakutoa amri ya kuua kwa matakwa yake yeye, au kwa agizo lake yeye, BALI KWA AGIZO LA MUNGU. Mungu ndiye aliyetoa maagizo ya kuua watu wote wa Midiani, bila kubakisha yeyote, kutokana na kosa la wamidiani kumtoa Balaamu, na kumtuma kwa Balaki mfalme wa Moabu, ili awalaani Israeli, hivyo Mungu akaikasirikia nchi ya Midiani na kumwagiza Musa akawaue watu wote.
Na Musa alipowatuma majemedari wa Israeli wakaue, kwa agizo hilo la Bwana, wale majemedari wakaua kweli wanaume na wafalme lakini wakawaacha hai wanawake!, jambo ambalo ni kinyume na maagizo Bwana aliyoyatoa.
Tusome tena,
Hesabu 31:7 “Nao wakapigana na Midiani kama Bwana alivyomwagiza Musa; nao wakamwua kila mume. 8 Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga. 9 Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng’ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara. 10 Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza kwa moto. 11 Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama. 12 Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko. 13 Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago. 14 MUSA AKAWAKASIRIKIA MAJEMADARI WA JESHI, NA HAO MAAKIDA WA ELFU ELFU, NA WAKUU WA MIA MIA, HAO WALIORUDI KUTOKA KATIKA KUPIGA VITA. 15 MUSA AKAWAULIZA, JE! MMEWAPONYA WANAWAKE WOTE HAI? 16 Tazama, hawa ndio waliowakosesha wana wa Israeli, kwa shauri la Balaamu, wamfanyie Bwana dhambi katika hilo jambo la Peori, na kwa hivyo pigo lilikuwa katika mkutano wa Bwana. 17 Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Hesabu 31:7 “Nao wakapigana na Midiani kama Bwana alivyomwagiza Musa; nao wakamwua kila mume.
8 Nao wafalme wa Midiani wakawaua pamoja na watu wengine waliouawa; Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao wafalme watano wa Midiani; Balaamu mwana wa Beori naye wakamwua kwa upanga.
9 Wana wa Israeli wakawachukua mateka wanawake wa Midiani na watoto wao; na ng’ombe zao wote, na kondoo zao wote, na mali zao zote, wakachukua nyara.
10 Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na marago yao yote wakayateketeza kwa moto.
11 Nao wakatwaa hizo nyara zote, na mateka yote, ya wanadamu na ya wanyama.
12 Nao wakawaleta mateka ya wanadamu, na mateka ya wanyama, na hizo nyara, na kuyaweka mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wa wana wa Israeli, hapo maragoni katika nchi tambarare za Moabu, zilizo karibu na Yordani hapo Yeriko.
13 Basi Musa, na Eleazari kuhani, na wakuu wote wa huo mkutano, wakatoka nje kwenda kuwalaki nje ya marago.
14 MUSA AKAWAKASIRIKIA MAJEMADARI WA JESHI, NA HAO MAAKIDA WA ELFU ELFU, NA WAKUU WA MIA MIA, HAO WALIORUDI KUTOKA KATIKA KUPIGA VITA.
17 Basi kwa ajili hiyo mwueni kila mume katika hao watoto, na kila mwanamke aliyemjua mume kwa kulala pamoja naye”.
Hivyo Musa aliendelea kuwa mpole vile vile, kuliko watu wote, lakini alikuwa anayashika maagizo ya BWANA bila kupindisha, kile Bwana atakachokisema anakitekeleza kama kilivyo ili ampendeze Mungu, na aliwaamuru watu kuyafanya maagizo ya Bwana bila kuyapindisha.
Tunachoweza kujifunza na sisi ni kwamba, hatuna budi kuyatekeleza maagizo ya Bwana kama yalivyo, bila kuyapindisha, haijalishi tutaonekanaje!
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
SWALI: Je Wakati Mfalme Nebukadreza anawatupa Shadraka, Meshaki na Abednego kwenye tanuru la Moto, Danieli alikuwa wapi?
JIBU: Kwasababu biblia haiandiki kila habari, bali inachagua yale matukio muhimu tu, yatakayotusaidia, ndivyo ilivyo katika habari hii, haielezi habari za Danieli kwa wakati huo, alikuwepo wapi, lakini katika sintofahamu hiyo, tuna la kujifunza. Hivyo hapo mambo matatu yanawezekana,
La kwanza ni aidha Danieli hakuwepo, wakati huo, ambapo Nebudreza, anatoa amri, kwasababu utakumbuka kuwa yeye aliyewekwa juu ya waganga wote, na wenye hekima (Danieli 5:11). Hivyo kuna uwezekano, alipewa jukumu lingine la kwenda kulifanya nje ya Babeli kwa wakati huo , na mbio ilipopigwa yeye hakuwepo.
La pili, ni aidha, watu waliokuwa pamoja na mfalme agizo hilo halikuwahusu, kwasababu ukichunguza utaona, Nebukadreza, aliwaita wakuu wake wote waliokuwa katika majimbo yake yote ulimwenguni. Na lengo la kuwaita, lilikuwa ni kuwapima utiifu wao kwa serikali yake moja ya ulimwengu. Ndio maana akawalazimisha wakuu wote ambao wapo mbali naye waje kuisujudia sanamu yake. Hivyo kwasababu Danieli alikuwa katika jumba la mfalme agizo hilo halikumuhusu.
Danieli 2:49 “Tena, Danielii akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danielii alikuwa akiketi katika lango la mfalme”.
Na mwisho, ni kwamba Danieli, tangu mwanzo alisimama katika misingi ya Imani yake, utakumbuka, walipoitwa na kutaka kulishwa Divai, pamoja na vyakula najisi, moja kwa moja walivikataa yeye pamoja na hao wenzake watatu. (Danieli 1:8-16) Hivyo uwezekano pia wa Danieli kumweleza mfalme misimamo wake, ulikuwepo, na mfalme akamwelewa, akamwacha peke yake asiisujudie miungu yake.
Lakini kusema kwamba alitii amri ya mfalme, hilo jambo halipo, wala lisingewezekana kwa Danieli, kwasababu utakumbuka, hata baadaye sana, jaribio kama hilo lilitaka kufanyika, la kumzuia asimwabudu Mungu wake, lakini alikaidi amri yao bila kujali nani kasema, au adhabu gani imetolewa.
Lakini habari hii ya kutokuwepo kwa Danieli inatufundisha nini? Ni kwamba, upo wakati Mungu atakuepusha na majaribu ambayo nafasi ya kuyakwepa ni ndogo sana, lakini pia upo wakati Mungu atakupitisha katika majaribu ya adui. Mwanzoni kikombe kile hakikumuhusu Danieli, lakini mwishoni, alishiriki kikombe cha kutupwa katika tundu la Simba.
Nasi pia, kuna nyakati ngumu zitapita mbele yetu katika eneo la imani yetu, na Mungu atatuvusha salama bila hata ugumu wowote, lakini pia zipo nyakati ataziacha zipite juu yetu. Lakini yote katika yote, tunapaswa tuwe katika msimamo wetu kama vile Danieli.
Nyakati zote za mvua, na joto, misingi ya imani yetu isitikiswe.
DANIELI: Mlango wa 1
UMEDI NA UAJEMI ZILITAWALAJE?
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Nini maana ya kuutia moyo ufahamu? (Danieli 10:12)