Gidamu ni nini? Kwanini Yohana alisema hastahili kuzilegeza gidamu za Yesu?

Gidamu ni nini? Kwanini Yohana alisema hastahili kuzilegeza gidamu za Yesu?

SWALI: Kwanini Yohana alisema hastahili kulegeza gidamu ya viatu vya Yesu, gidamu ni nini?

Gidamu ni mikanda maalumu ya viatu,

Viatu vya zamani vilikuwa havina muonekano kama tulionao sasa hivi, ambao vingi vinatengenezwa kwa muundo wa kutumbukiza tu mguu,, vya zamani vilikuwa zinashikiliwa na mikanda maalumu, au kamba maalumu, ambazo zinazungushwa kwenye miguu, ili kuwezesha kiatu kisitoke, sasa hiyo mikanda ndio inayoitwa Gidamu. tazama picha juu..

Neno hilo utalipata kwenye vifungu hivi;

Marko 1:7 “Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake.

8 Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu”.

Luka 3:16 “Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”;

Mathayo 3.11 “Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto”.

Tukirudi kwenye swali kwanini Yohana Mbatizaji alisema hastahili kulegeza gidamu ya viatu Yesu?

Zamani na hata sasa kazi ya kufunga na kufungua mikanda/kamba za viatu ni kazi zinazofanywa na watumwa wa chini sana,  Wanachofanya ni kumwandalia bwana wao viatu, kisha kumvisha, na baadaye kuwavua tena pindi watakaporudi kutoka katika mihangaiko yao, na kuvichukua viatu hivyo mpaka sehemu ya usafi na kuhakikisha  wanaviosha, vinakuwa maridadi, kisha wanarudi kuwavisha tena bwana zao, hiyo ndio inakuwa ni kazi yao muda wote, siku zote.

Kwa desturi wa wayahudi kazi kama hii haikufanywa na mtumwa wowote wa kiyahudi, kwasababu ni kazi nyonge, dhaifu na ya kudharaulika, ilikuwa inafanywa na wakaanani tu(Watu wa mataifa mengine waliokuwa wanaishi Israeli wakati ule).

Sasa Yohana kusema hastahili kulegeza hata gidamu ya viatu vya Yesu, ni kuonyesha kutostahili kwake, kuifanya hata ile kazi ndogo sana ya Yesu Kristo, kwasababu Kristo ni mkuu kupita kiasi. Hivyo hata ile kazi inayoonekana ni ya kudharaulika sana kwake ni kubwa sana, kiasi cha kumfanya ajione hastahili kuifanya. Huo ni unyenyekevu wa hali ya juu sana na hofu aliyokuwa nayo Yohana kwa ajili ya Bwana wake Yesu Kristo.

Na matokeo yake, hatushangai ni kwanini Bwana Yesu alimfanya kuwa mtangulizi wake, na zaidi ya yote akamshuhudia kuwa katika uzao wa wanawake hakuwahi kutokea mtu aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni kuliko yeye. Hiyo yote ni kwasababu aliithamini sana hata ule wito mdogo sana wa Bwana Yesu.

Je na sisi tunaweza kuwa kama Yohana mbatizaji?..Kama tutashindwa kupiga deki kanisa la Bwana, au kuosha choo,  tutawezaje, kufanywa watangulizi wake..Tutawezaje kuonyeshwa siri za ndani za ufalme wa mbinguni kama alivyoonyeshwa Yohana, kama tutazidharau hata zile kazi zake ndogo.

 Thamini Gidamu za Yesu!

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?

Mtu mwenye “kitango” ni mtu wa namna gani kibiblia?

UFUNUO: Mlango wa 1

Amri zilizo ndogo alizozizungumzia Yesu ni zipi?

Bwana Yesu alikufa akiwa na umri gani?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments