Category Archive Maana ya maneno

Kulaumu/ Lawama ni nini kibiblia?

Je! wakristo tunalaumiwa?

JIBU: Ni mashtaka au maneno  Fulani yanayotolewa dhidi yako, yanayolenga kutoridhishwa na mwenendo, au maneno au tabia yako.

Tunaweza tukawa watoto wa Mungu, na bado siku ile ya mwisho tukalaumiwa na Mungu.  Utauliza ni kwa namna gani?

Ni kweli deni letu la mashtaka limeondolewa pale msalabani kwa Kifo cha Yesu Kristo. Na kwamba mtu anapomwamini tu Yesu Kristo haukumiwi, bali anaingia uzimani. Tafsiri yake ni kuwa hana lawama la hukumu ya jehanamu (Wakolosai 1:21-22)

Lakini, kumbuka wewe “unahesabiwa” kuwa mwenye haki. Lakini kiuhalisia “huna haki ndani yako”. Yaani kwa asili wewe huna kitu chochote kizuri ndani yako mbele za Mungu, na kimsingi huo sio mpango Mungu aliokusudia kwa mwamini. Mungu anataka amwokoe mtu wake, na wakati huo huo awe mkamilifu kama yeye.

Ndio hapo hatupaswi kuichukulia NEEMA ya Mungu kama fursa ya sisi kupumzika katika dhambi, au kupuuzia matendo ya haki. Au kutokuonyesha bidii yoyote ya Kufanana na Kristo.

Maandiko yanasema watu wengi wataonekana kuwa na lawama, mbele za Kristo, kwa kushindwa tu kurekebisha baadha ya mienendo yao, walipokuwa hapa duniani.

Kwa mfano maandiko haya yanaeleza baadhi ya mienendo, hiyo; moja wapo ni  kukaa katika  Mashindano, au manung’uniko ndani ya wokovu hupelekea utumishi wako,kulaumiwa .

Wafilipi 2:14  “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano,  mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu”

Vilevile kutofikia upendo  na  Utakatifu, ni zao la lawama.

1Wathesalonike 3:12  Bwana na awaongeze na KUWAZIDISHA KATIKA UPENDO, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;

13  apate kuifanya imara mioyo YENU IWE BILA LAWAMA KATIKA UTAKATIFU mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

Tufanye nini ili tuweze kuepuka lawama, na tuwe na ujasiri, mbele za Kristo siku ile?

Ni kuitendea kazi neema ya Kristo maishani mwetu. Kwa kumtii yeye, na kumfuata kwa mioyo yetu yote, nguvu zetu zote, akili zetu zote na roho zetu zote, Ambayo inafuatana pia na bidii katika kujitenga na maovu, Ndipo itakuwa rahisi sisi kuyashinda,kwasababu ataiachilia nguvu yake ya ushindi itende kazi ndani yetu, na hivyo tutajikuta tunakaa mbali na mambo ya kulaumu.

1Wathesalonike 5:22  jitengeni na ubaya wa kila namna.

23  Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu MHIFADHIWE MWE KAMILI, BILA LAWAMA, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

Hivyo ndugu uliyeokoka, tambua kuwa kila mmojawetu atatoa hesabu yake mbele za Mungu, siku ile. Hatuna budi sasa kuishi kama watu wanaotarajia TAJI bora, na sio watu wasio na mwelekeo wowote. Bwana asije akaona “neno ndani yetu”, mfano wa yale makanisa 7  tunayoyasoma katika Ufunuo 2&3, ambayo Yesu aliyapima akaona mapungufu. Hivyo tuishi kama watu wenye malengo, sio tu wa kukombolewa, bali pia wa kukamilishwa.

2Wakorintho 6:3  TUSIWE KWAZO LA NAMNA YO YOTE KATIKA JAMBO LO LOTE, ILI UTUMISHI WETU USILAUMIWE; 4  bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida;

5  katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga;

6  katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki;

7  katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;

8  kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli.

Bwana akubariki.

Hivi ni baadhi ya vifungu vingine utakavyokutana na Neno hilo pia (1Timotheo 3:1-7, Luka 1:5-6)

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NINI KINAFUATA SIKU ILE ILE YA KUOKOKA!

Mtakatifu ni Nani?

HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

MUNGU MWENYE HAKI.

Rudi nyumbani

Print this post

Rubani ni nani katika biblia? (Ezekieli 27:8)

Swali: Je zamani marubani wanaoendesha ndege walikuwepo kama tunavyosoma katika Ezekieli 27:8?


Jibu: Turejee mstari huo..

Ezekieli 27:8 “Wakaao Sidoni na Arvadi ndio waliovuta makasia yako; wana wako wenye akili, Ee Tiro, walikuwa ndani yako, ndio WALIOKUWA RUBANI ZAKE”.

“Marubani” wanaozungumziwa hapo si Marubani wanaorusha ndege kwamaana kipindi hicho ndege zilikuwa hazijavumbuliwa…bali marubani wanaozungumziwa hapo ni wana-maji (manahodha)..Kwasababu asili ya neno hilo rubani si mwana-anga, bali ni mwana-maji.

Isipokuwa kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda na kumavumbuzi mengi kuibuka, basi maneno mengi yanakuwa yanapata maana Zaidi ya moja.

Kwamfano katika biblia yametajwa magari (Mwanzo 45:21)..sasa magari ya zamani si sawa na haya sasahivi, ingawa yote ni magari… vile vile katika biblia kuna mahali pametajwa “Risasi” (Kutoka 15:10) lakini Risasi hiyo si sawa na hii inayojulikana sasa.. Vile vile pametajwa neno “Ufisadi“ (2Petro 2:7).. Lakini ufisadi huo wa biblia ni tofauti kabisa na huu unaofahamika sasa. N.k

Kwahiyo tukirudi katika Rubani, anayetajwa hapo katika Ezekieli 27:8, ni rubani mwana-maji, na si mwana-anga. Ndio maana ukiendelea mbele Zaidi katika mstari wa 29 utaona biblia imeweka sawa…

Ezekieli 27:29 “Na wote wavutao kasia, wana-maji, na RUBANI ZOTE WA BAHARINI, watashuka katika merikebu zao, na kusimama katika nchi kavu”.

Hapo anasema “Rubani zote za baharini” ikiashiria kuwa ni wana-maji na si wana-anga.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Risasi inayotajwa kwenye Ezekieli 27:12 ni ya namna gani?

Ufisadi una maanisha nini katika biblia?

EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.

Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

Rudi nyumbani

Print this post

Neno kupomoka linamaana gani kwenye biblia?(Hesabu 16:22)

Hesabu 16:20 Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,  21 Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja.  22 Nao WAKAPOMOKA kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote?

Soma pia

Yoshua 5:13 Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? 

14 Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua AKAPOMOKA kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?

Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi baadhi; Hesabu  16:4, 16:45,

Ni Kiswahili cha zamani cha Neno kuporomoka.  Yaani kuanguka chini, kwamfano maji yanayoelekea chini kwa wingi tunasema maporomoko ya maji, au udongo unaoanguka kutoka milimani kwa wingi tunasema maporomoko ya udongo.

Hivyo, katika vifungu anaposema Musa na Haruni wakapomoka kifudifudi, anamaanisha wakaanguka chini kifudi fudi mbele za Mungu kumlilia Bwana rehema.

Je! Na sisi tuombapo rehema au  tumtakapo Bwana kwa jambo Fulani muhimu ni lazima tupomoke chini ili tusikiwe ?

Jibu lake ni kwamba sio takwa kufanya hivyo. Kwasababu Mungu anaangalia moyo, kupomoka kwetu kunapaswa kuwe moyoni. Lakini pia si vibaya kuomba kwa namna hiyo, na ni vema, kwasababu pia ni ishara moja wapo ya unyenyekevu wa moyo. Ni sawa tu na tunapopiga magoti, au kunyosha mikono juu wakati wa kumwomba Mungu, kama ishara ya unyenyekevu mbele zake.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Ni kwanini tunambariki Mungu? Je! Mungu huwa anabarikiwa?

LAANA YA YERIKO.

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2

Kuwatema farasi, maana yake ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

Kuna tofauti gani kati ya “Mwivi” na “Mwizi”?

Swali: Kwanini katika biblia lisitumike neno “Mwizi” na badala yake linatumika neno “Mwivi”…Mwivi ni nini?


Jibu: Mwivi na Mwizi ni Neno moja, lenye maana moja.. isipokuwa ni lugha mbili za nyakati mbili tofauti.

Kiswahili kilichotumika katika kutafsiri biblia ni Kiswahili cha zamani, kilichoitwa “kimvita” ambacho ndicho kimebeba maneno ambayo hatuyaoni katika Kiswahili cha sasa, na mojawapo ya maneno ndio kama hayo “Mwivi na wevi” ikimaanisha “mwizi na wezi”. Ndio maana katika biblia yote huwezi kukuta neno Mwizi, badala yake utakuta mwivi (Soma Kutoka 22:2, Ayubu24:14, Zaburi 50:18, Mithali 6:30, Yoeli 2:9, Luka 12:39 n.k )

Maneno mengine ya kimvita (Kiswahili cha zamani) ambayo mengi ya hayo hayatumiki sasa ni pamoja na “jimbi” badala ya “Jogoo”“Kiza” badala ya “Giza”….”Nyuni” badala ya “ndege”…. “Kongwa” badala ya “Nira” na mengine mengi.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba “Mwivi” na “Mwizi” ni Neno moja, lenye maana ile ile moja (ya mtu anayeiba).

Lakini mbali na hilo, maandiko yanatufundisha kuwa Bwana YESU atakuja kama “Mwivi”..

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”

Je umewahi kujiuliza ni kwanini aje kama Mwivi na si Askari?.. Kwa upana juu ya hilo basi fungua hapa >>ANAKUJA KAMA “MWIVI” NA SI KAMA “ASKARI” FANYIKA CHOMBO CHA THAMANI.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.

Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha

OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!

Nini maana ya ELOHIMU?

Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).

Rudi nyumbani

Print this post

Kalafati ni nini? (Ezekieli 27:9)

Swali: Wenye kutia Kalafati ni watu gani?

Jibu: Neno “Kalafati” limeonekana mara mbili tu katika biblia, katika Ezekieli 27:9 na Ezekieli 27:27.

Na maana yake ni “Kamba nyembamba iliyotengenezwa kwa pamba” ambayo inawekwa katikati ya mianya ya mbao za merikebu, ili kuzuia maji yasipenye katika ile miunganiko. (Tazama picha juu)

Hivyo watu wanaofanya hiyo kazi ndio waliotajwa hapo katika Ezekieli 27:9,

Ezekieli 27:9 “Wazee wa Gebali na wenye akili wake walikuwa ndani yako, WENYE KUTIA KALAFATI; merikebu zote za bahari na mabaharia wao walikuwa ndani yako, ili kubadiliana biashara yako”.

Lakini habari hii inahusu nini?

Ukisoma kitabu hicho cha Ezekieli mlango wa 27 kuanzia mstari wa kwanza, utaona ni unabii unamhusu mfalme wa Tiro. (Kwa urefu kuhusu Taifa la Tiro fungua hapa >>>Miji ya Tiro na Sidoni ni miji gani kwasasa? 

Lakini hapa ni unabii wa Mfalme wa Tiro, Kwamba kwa kiburi chake na biashara zake nyingi alizozifanya juu ya nchi na katika bahari kupitia merikebu zake, siku inakuja ambapo ataanguka na kushuka chini kwasababu ya dhambi zake nyingi.

Na biashara za baharini alizokuwa anazifanya kupitia merikebu zake kubwa ambazo ndani yake kulikuwa na wana-maji, na “watiao Kalafati” na manahodha, zitaanguka na shughuli zao hizo zitaisha!

Ezekieli 27:27 “Mali zako, na bidhaa yako, na utajiri wako, wana-maji wako, na rubani zako, na WENYE KUTIA KALAFATI WAKO, na wafanya biashara wako, na watu wako wa vita wote, walio ndani yako, pamoja na jeshi lako lote lililo ndani yako, wataanguka katika moyo wa bahari katika siku ya kuangamia kwako”.

Ufunuo kamili pia kwa anguko la ulimwengu pamoja na dini zake za uongo katika siku za mwisho..

Ufunuo Ufunuo 18:2  “Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;

3  kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake………………..

9  Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake;

10  wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja.

11  Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena;

12  bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari;

13  na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng’ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.

14  Na matunda yaliyotamaniwa na roho yako yamekuondokea; na vitu vyote vilivyo laini na vitu vya fahari vimekupotea; wala watu hawataviona tena kamwe.

15  Na wafanya biashara ya vitu hivyo, waliopata mali kwake, watasimama mbali, kwa hofu ya maumivu yake; wakilia na kuomboleza”

Je Umeokoka kwa kumwamini Bwana Yesu Kristo na kubatizwa, sawasawa na Marko 16:16?. Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho na Kristo amekaribia kurudi.

Kwa msaada Zaidi katika kumpokea Kristo fuatiliza sala hii ya Toba >>KUONGOZWA SALA YA TOBA  au wasiliana nasi kwa namba zetu zilizoanishwa mwisho wa somo hili.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KWANINI DANI ALIKAA KATIKA MERIKEBU.

EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.

Tarshishi ni mji gani kwasasa?

Mashonde ni nini? (Ezekieli 4:15).

Kuna tofauti gani kati ya  “Edeni” na “Adeni”?

Rudi nyumbani

Print this post

Makasia ni nini? (Yona 1:13).

Swali: Kuvuta Makasia maana yake nini?


Likiwa moja linatiwa ”Kasia”, yakiwa mengi ni “Makasia” … Hizi ni  “Zana” ya kukisaidia chombo kutembea juu ya maji. Zana hii kwa mwonekano ni kama “Mwiko mkubwa”, (tazama picha juu), ambapo mabaharia walipoyavuta basi chombo kilisogea mbele..

Yona 1:13 “Lakini wale watu WAKAVUTA MAKASIA kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana”.

Unaweza kusoma Zaidi kuhusu makasia katika mistari ifuatayo; Marko 6:48, Yohana 6:19,  Isaya 33:21, na Ezekieli 27:6.

Je ni nini tunajifunza katika habari ya Yona na mabaharia hawa kuvuta makasia kurudi pwani?.. Fungua hapa >>>YONA: Mlango 1

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

YONA: Mlango wa 2

HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI.

MADHARA YA KUTAFUTA ISHARA.

YONA: Mlango wa 3

YONA: Mlango wa 4

Rudi nyumbani

Print this post

Upepo wa Mbisho maana yake nini? (Mathayo 14:24)

Swali: Pepo za Mbisho ni nini?


Jibu: Turejee kuanzia mstari wa 23.

Mathayo 14:23 “Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.

24  Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; MAANA UPEPO ULIKUWA WA MBISHO.

25  Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.

26  Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu”.

Maana ya neno “Mbisho” ni “Ukinzani”. Hivyo hapo aliposema “Upepo ulikuwa wa Mbisho”, maana yake upepo ulikuwa ni wa ukinzani, (yaani ulikuwa unavuma kinyume na uelekeo waliokuwa wanauendea).

Utasoma tena aina ya upepo huu ikitajwa katika Matendo 27:4,

Matendo 27:4 ”Kutoka huko tukatweka, tukasafiri chini ya Kipro ili kuukinga upepo, kwa maana PEPO ZILIKUWA ZA MBISHO”.

Safari yoyote ya majini, ikikutana na pepo za mbisho, safari hiyo inakuwa ni ngumu sana.. Kwasababu upepo utakuwa unavuma kinyume na ile merikebu na hivyo kuchelewesha safari au hata kuirudisha nyuma.

Lakini pepo za Mbisho zinafunua nini kiroho?

Pepo za mbisho kiroho ni kila aina ya matatizo, na shida na dhiki na vikwazo kutoka kwa yule adui vinavyokawisha au kurudisha nyuma safari yetu ya Imani hapa duniani.

Ndio maana utaona katika habari hiyo ya Mathayo 14:23-36, kabla wanafunzi wa Bwana YESU kufika nchi ya Wagerasi kwaaijli ya huduma ya kufundisha na kuponya wagonjwa na kuwafungua walioteswa na shetani, adui aliwatumia “Upepo huu wa mbisho”, lengo ni ili wasifanikiwe safari yao hiyo.

Lakini BWANA YESU alipoingia ndani ya chombo kile ule upepo ukakoma na misuko suko yake, kufunua kuwa zile zilikuwa ni hila za ibilisi.

Hivyo hata sisi tunapokutana na pepo za namna hii katika Imani, suluhisho ni kuzikemea kwa Imani na kwa jina la YESU, na zitatii.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

MAJARIBU MATANO (5) YA MKRISTO.

NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?

Rudi nyumbani

Print this post

Mata ni nini (Mwanzo 27:3).

Mata ni kitu gani na imebeba  ujumbe gani kiroho?


Jibu: Turejee,

Mwanzo 27:2 “Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.

3 Basi, nakuomba, chukua MATA yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;  4 ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa”.

“Mata” Ni jina jingine la “Silaha”. Kwahiyo badala ya kutumia neno “silaha” ni sahihi pia kutumia neno “Mata”.

Kwahiyo mstari huo wa tatu (3) ni sahihi kuuweka hivi,… “chukua SILAHA yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo ”

Na silaha hiyo inaweza kuwa mkuki, mshale au upanga, lakini katika andiko hilo silaha (Mata), iliyomaanishwa pale ni “Mshale”. Na kwanini ni mshale na si upanga wala mkuki?.. ni kwasababu kuna Podo imetajwa pale na upinde..

Maana yake huwezi kubeba upanga na upinde bila mshale, hivyo ni wazi kuwa Mata iliyomaanishwa pale ni mshale, kwasababu kuna upinde na Podo.

Sasa kwa maarifa kuhusu “Podo” na ufunuo wake kiroho waweza fungua hapa >>> Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?

Sasa hizi zote ni silaha za mwili, lakini biblia inatufundisha kuwa zipo silaha za roho ambazo kila mkristo ni lazima azivae, na silaha hizo tunazisoma katika kitabu cha Waefeso 6:10-18, ambazo ni Chapeo ya Wokovu, Dirii ya Haki, Ngao ya Imani, Kweli, Upanga wa Roho, na Utayari miguuni pamoja na sala na maombi.

Na kwa silaha hizo pekee ndio tutaweza kumshinda adui yetu shetani, kwa mapana kuhusiana na silaha hizi jinsi ya kuvizaa na namna zinavyotenda kazi fungua hapa >>>MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.

JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.

KWANINI UPIGE MISHALE CHINI?

NDUGU,TUOMBEENI.

Nini maana ya  Mithali 21:1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana;

Rudi nyumbani

Print this post

Kiti cha Musa ni kipi? (Mathayo 23:2)

Swali: Biblia ina maana gani kusema Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa? Je hiki kiti cha Musa ndio kipi?



Jibu: Turejee,

Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”

“Kiti cha Musa” maana yake ni “Nafasi ya Musa”.. Leo hii tukisema mtu kaketi katika kiti cha Uraisi, maana yake ni kuwa “kachukua nafasi ya Uraisi”.

Sasa Musa alikuwa na nafasi gani?

Musa alikuwa na nafasi kuu mbili (2) mbele za wana wa Israeli.

   1) UALIMU.

Mtu wa Kwanza kuwafundisha wana wa Israeli HUKUMU, AMRI NA SHERIA za Mungu alikuwa ni MUSA.

Kumbukumbu 4: 14 “Bwana akaniamuru wakati ule NIWAFUNDISHE maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.

15 Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;

16 msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke”.

Na mahubiri yake yaliendelea kuwa msingi wa marejeo kwa vizazi na vizazi mbeleni.

2) UONGOZI.

Hii ni nafasi ya pili aliyokuwa nayo Musa mbele ya wana wa Israeli:
Maandiko yanasema Mungu alimfanya Musa kuwa “Mkuu sana” mbele ya Misri na mbele ya wana wa Israeli. Kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwake, kwa lugha nyepesi alikuwa ni kama Mfalme.

Kutoka 11:3 “…Zaidi ya hayo, huyo Musa ALIKUWA NI MKUU SANA katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake”.

Soma pia Kutoka 18:13-24, utaona nafasi ya Musa katika kuwaamua Israeli.

Sasa baada ya Musa kuondoka (yaani kufa), Mafarisayo na Waandishi wakajiweka katika nafasi yake, maana yake wao ndio wakawa WAALIMU kama alivyokuwa Musa, na pia wakajiweka kuwa VIONGOZI kama alivyoukwa Musa, kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwao.

Lakini ni heri kama wangekuwa wameketi kwenye nafasi hiyo ya Musa, na wakawa kama Musa..(yaani wacha Mungu kama Musa, au wapole kama Musa)..

Lakini wao walikuwa ni kinyume chake, walikuwa wanawatawala watu na kuwahukumu kwa sheria ya Musa lakini wao wenyewe ni wanafki mioyoni mwao.. mioyo yao ilikuwa ipo mbali na Mungu ingawa kwa nje wanaonekana ni waamuzi wazuri na viongozi wazuri wenye kusifiwa, lakini ndani yao wamejaa unafiki!.

Na Bwana YESU anatuonya tusiwe kama wao..

Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”

3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi

4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.

5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;

6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,

7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.

8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.

9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.

10 Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.

11 NAYE ALIYE MKUBWA WENU ATAKUWA MTUMISHI WENU.

12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”.

Je YESU KRISTO ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako?..Je una uhakika jina lako lipo katika kitabu cha uzima?.. Kama bado YESU hayupo maishani mwako ni heri ukampokea leo, maana saa ya wokovu na wakati uliokubali ni sasa.
Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NI KIZAZI KIPI WEWE UPO?

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

USIWE NA TAMAA YA CHAKULA KINGINE.

Rudi nyumbani

Print this post

Yahu ni nani? (Wimbo 8:6).

Jibu: Turejee,

Wimbo 8:6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni MIALI YA YAHU”.

“YAHU” ni jina lingine la “YAHWE” ambalo ndilo “YEHOVA”.

Kutoka 6:2 “Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni YEHOVA; 

3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao”.

Kwahiyo YAHU, YAHWE na YEHOVA ni jina Moja!

Lakini hapo katika Wimbo 8:6 maandiko yanasema kuwa “upendo una nguvu kama mauti”.. maana yake kama vile mauti ilivyo na nguvu kiasi kwamba wanaokufa ni ngumu kurudia uzima! Vile vile Upendo wa Mungu kwetu ni mkuu kiasi kwamba akitupenda ametupenda!, hakuna wakati atatuchukia, anaweza asipendezwe na sisi lakini si kutuchukia!.

Warumi 8:35 “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?………

38  Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,

39  wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Lakini pia anasema wivu ni mkali kuliko Ahera..Ahera ni “Kaburi”, Kwa urefu Zaidi fungua hapa >>>Ahera ni wapi? Kama tunavyosoma katika biblia.

Na miali yake ni miali ya YAHU. Maana yake ni kuwa Mungu ana upendo lakini pia anawivu, huwezi kamwe kutanganisha vitu hivi viwili, UPENDO na WIVU.

Kwahiyo kama Mungu ametupenda, basi hapendi kuona tunaabudu miungu mingine, tukifanya hivyo tunamtia yeye wivu, umbao unaweza kutupeleka kaburini (Ahera).

Kutoka 20:3 “Usiwe na miungu mingine ila mimi.

4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, NI MUNGU MWENYE WIVU; NAWAPATILIZA WANA MAOVU YA BABA ZAO, HATA KIZAZI CHA TATU NA CHA NNE CHA WANICHUKIAO, 

6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu”.

YAHU atusaidie tusimtie Wivu, lakini tumpende, na vile vile upendo wake utubidiishe katika kuyafanya mapenzi yake.

Maran atha.

Mafundisho Mengine:

Wivu ni nini na kuna aina ngapi za Wivu?

UMETEKWA NA UPENDO WA KRISTO?

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

IJUE HEKIMA YA MUNGU KATIKA KUKUINUA KIMAISHA.

WEKA KUMBUKUMBU YA MAMBO BWANA ANAYOKUFANYIA KWASABABU YATAKUFAA MBELENI.

Rudi Nyumbani:

 

Print this post