JIBU: Kibiblia ni neno linalomaanisha “mvurugano” au “mvurugiko”
Neno hilo utalisoma katika kifungu hiki;
Isaya 17:13 “Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani. 14 Wakati wa jioni, tazama, kuna hofu; Na kabla ya mapambazuko hawako; Hilo ndilo fungu lao watutekao, Na ajali yao wanaotunyang’anya mali zetu”.
Hapo ni Bwana anawahakikishia watu wake ulinzi madhubuti dhidi ya adui zao. Anasema mambo matatu yatawakumba hao wanaojaribu kuwaangamiza watu wa Mungu.
La kwanza,watakemewa na kukimbia mbali sana: Ni kama wakati wa washami kipindi cha nabii Elisha, Bwana alipowasikilizisha kelele za majeshi wakakimbia wakashindwa hata kuchukua na nyara zao nyuma(2Wafalme 7).
La pili ni “ watafanana na makapi mbele ya upepo: Kwa kawaida ngano inapopepetwa yale makapi huwa yanarushwa na upepo mbali sana, ndivyo watakavyofanywa waadui wa watoto wa Mungu wanapokaribiwa, watatoweka ghafla.
Na la tatu anasema watakuwa kama mavumbi ‘vuruvuru’ mbele ya tufani: Kwa kawaida upepo mkali wa kisulisuli au tufani inapopita juu ya ardhi iliyokuwa kavu, ule upepo wake mkali unatabia ya kuvuruga mavumbi, na kuyafanya yaruke hewani yasambae tu ovyo vyo, na hiyo husababishia hali ya hewa kuchafuka sana. Hivyo, Bwana anasema, ndivyo itakavyokuwa kwa watu hao, watavurugwa, kiasi cha kutokuelewana, kila mmoja atakuwa na lake, ni kuchanganyikiwa tu, Ndio maana ya hilo andiko.
Lakini ni nini Bwana anataka tujifunze?
Ni kwamba tuwapo ndani Kristo, hatuna haja ya kuwa na hofu, kwasababu shetani na majeshi yake, yatakutana kwanza na jeshi la Bwana kabla ya kutufikia sisi. Ndicho Elisha alichomwambia Gehazi, kwamba jeshi letu ni kubwa kuliko la kwao.
Hivyo mtakatifu yoyote unayedumu katika wokovu (usio wa mdomo bali wa roho), ulinzi huu unao. Lakini kinyume chake ni kweli ikiwa upo nje ya Kristo, huna ulinzi wowote kwa Bwana, na matokeo yake shetani anaweza kufanya lolote atakalo juu yako, hata kukuua.
Swali ni Je! Umeokoka?
Kama bado na upo tayari kufanya hivyo sasa basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo was ala hiyo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;
Je! Sulemani alienda mbinguni?
Nini maana ya uvuvio?
MZUNGUKO WAKO NI UPI?
Uga ni nini? Na kazi yake ni ipi kibiblia?
Ila atapewa mara mia sasa,Ndugu wake(Marko 10:30)
Manyoyota ni nini (Ayubu 37:6)
Rudi nyumbani
Print this post
Kweli tumtegemee Mungu kwa bidii na tusiweke hofu hata tukutanapo na majaribu ya shetani,kwa sababu tukiwa imara katika maombi tukimuomba Yesu Kristo,hakika tutayashinda majaribu
Hakika