Ila atapewa mara mia sasa,Ndugu wake(Marko 10:30)

Ila atapewa mara mia sasa,Ndugu wake(Marko 10:30)

SWALI: Mbona katika Marko 10:30 Bwana Yesu anasema tutapata mara mia ‘wake’? Hii si inatupa uthibitisho kuwa ndoa za mitara ni sawa?


JIBU: Tusome kwa ukaribu vifungu vyenyewe;

Marko 10:28 “ Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.
29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au
ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,
30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, NA NDUGU WAKE, na mama,
na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza”.

Hapo hakuna mahali popote Bwana Yesu amesema tutapata mara mia ‘wake’, isipokuwa anasema tutapata mara mia  “ndugu wake”.  Akimaanisha ndugu wa KIKE, kama tu alivyosema ndugu WAUME, tutapata mara mia.

Maana yake ni kwamba mtu yeyote anayeingia gharama ya kumfuata Yesu kwa moyo wake wote, na kwa ajili ya injili yake, Bwana ameahidi kumrudishia kila kitu alichokipoteza mara100 zaidi.

Ikiwa aliwaacha dada  zake kumi(10), basi Bwana atamrudishia ndugu wadada mara mia zaidi.. yaani ndugu wadada elfu moja (1000), watakuja kuwa karibu naye.. wenye upendo kama tu ule wa wale wa kwanza   kwake.

Lakini tuseme, labda tuliacha wake zetu kwa ajili ya injili, Je! Mungu hataturudishia thawabu mara mia kwa kuwaacha wao?

Jibu ni kwamba ataturudishia pia mara mia, lakini haimaanishi kuwa tutapewa ‘wake’ tuwaoe, hapana, bali tutapewa ndugu, wenye Usaidizi kama tu wa wake.. Kumbuka, mwanamke aliumbwa kuwa msaidizi wa Adamu, hakuumbwa kuwa chombo cha starehe..

Hivyo hudumu aliyoitiwa mke duniani ni kuwa msaidizi.. Vivyo hivyo Mungu atakunyanyulia ndugu ambao watasimama kama wasaidizi kwako katika huduma, mara mia, kama wake.

Lakini haimaanishi utawaoa, hapana, kama itakavyokuwa kwa ndugu mara mia atakaokupa, hawataingia kwenye tumbo la mama yako na kuzaliwa ili wawe ndugu yako, bali watatoka nje, na kusimama kama ndugu.. Vivyo hivyo na kwa watoto na mambo mengine yote.

Lakini kwanini iwe hivyo? Ni ili kulitimiza lile neno la Bwana Yesu alilosema..

 “Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake
kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.(Luka 9.24)

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TWEKA MPAKA VILINDINI.

KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.

Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.

Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.

KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000

MADHARA YA KUTOIJUA KWELI YOTE!

KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments