Ni jambo la kawaida katika familia yoyote, si Watoto wote watakuwa na mahusiano sawa na wazazi wao. Wapo ambao wataonekana kuaminiwa Zaidi ya wengine, wapo ambao watapendwa Zaidi ya wengine, pia wapo ambao watategemewa na wazazi wao kuliko wengine, n.k. Lakini hilo haliwafanyi wale wengine wasiwe Watoto wa wazazi wao.
Inatokea hivyo, kutokana na aidha tabia zao, ujuzi au nafasi walizonazo. Vivyo hivyo na kwa Mungu katika familia yake ya watakatifu (Waliookoka), Si watakatifu wote watakuwa vipenzi wa Mungu, si wote wataaminiwa na Mungu, na si wote watategemewa na Bwana. Lakini hayo hayawafanyi hao wengine wasiwe Watoto wa Mungu.
Leo tutatazama mambo ambayo tukiwa nayo, basi tujue tutakuwa Watoto ambao tutapendwa sana na Mungu. Hivyo Ili tufahamu hayo tutaangalia katika biblia, mifano ya watu watatu (3) ambao, walipendwa na Mungu, ili na sisi tuige tabia kama zao tupendwa na Mungu.
Upendo ndio tabia ya kwanza itakayokuzogeza karibu na Mungu, na upendwe sana. Kati ya mitume 12 wa Bwana Yesu, Mtume Yohana peke yake ndiye aliyependwa na Yesu sana. Mpaka akawa muda wote anaegemea kifuani pake.
Yohana 21:20 “Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?) 21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?
Yohana 21:20 “Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)
21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?
Lakini lililomfanya apendwe na Yesu, ni upendo ambao aliuiga kutoka kwake. Na ndio maana utaona injili zake zote anahimiza upendo, kwasababu Mungu mwenyewe ni Upendo. Hivyo ili na sisi tupendwe na Bwana, hatuna budi kuonyesha bidii katika kupendana,
Na tabia za upendo tunazisoma katika 1Wakorintho 13:4-8….ambazo ni hizi;
13.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 13.5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 13.6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 13.7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 13.8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
13.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
13.5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
13.6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
13.7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
13.8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Maana yake, ni kuwa tayari kukataa mambo yote yanayoweza kukukosesha na Mungu bila kujali gharama/hasara gani utakayoingia kwa kutokufanya hivyo. Huo ndio uthabiti wa moyo Mungu anaoutaka. Ambao alikuwa nao Danieli, ndio uliomfanya Mungu ampende sana.
Danieli 10:11 “Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.
Soma pia Danieli 10:19,
Unaona Danieli, alikuwa ni mtu aliyependwa sana. Hiyo yote ni kutokana na moyo wake wa msimamo, tangu alipoingia kule Babeli wakati wayahudi wote, wapo vuguvugu, akiwa bado ni kijana mdogo alipoitwa akae katika milki za mfalme hakusita kutaa vyakula najisi vya kifalme..Na hata bado akiwa mzee, walipotaka kumzuia asimwabudu Mungu wake, bado aliendelea kumwabudu kutwa mara tatu, bila kuogopwa kutupwa katika tundu la simba.
Moyo kama huo unaonyesha upendo mkamilifu kwa Mungu wake, hivyo Mungu naye angeonyesha upendo wake tu. Na ndio maana Danieli kila alipotembelewa na Malaika alianza kwa kuambiwa mtu upendwaye sana.
Vivyo hivyo na sisi, katika mambo yetu, Ikiwa boss wako/ kazi yako vinakuzuia usiwe karibu na Mungu wako kwa ule muda unaokupasa umwabudu. Ukionyesha uthabiti, kwamba ni lazima ukamtumikie Bwana wako, ukamfanyie ibada, Bwana atakupenda..Ikiwa kazini kwako wanakulazimisha uvae suruali na vimini wewe kama binti uliyeokoka, ukakataa na kusema Imani yangu hainiruhusu bila kuogopa kufukuzwa kazi, basi ujue, upo katika njia ya kupendwa na Mungu kama Danieli.
Sulemani, ni mtu mwingine ambaye biblia inatuambia alipendwa na Mungu. Tunalithibitisha hilo katika,
Nehemia 13:26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. TENA ALIPENDWA NA MUNGU WAKE, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Ni kwasababu gani? Ni kwasababu yeye hakuwa kama wafalme wengine, kama Sauli, ambao akili zao zilielekea katika kutawala tu, na vita dhidi ya maadui. Bali yeye alitamani kupata njia ya namna ya kuyatengeneza mambo kwa hekima, watu wa Mungu wafurahi katika Bwana na kumtimikia katika utulivu. Ndipo Mungu akasikia ombi lake, akampatia. (1Wafalme 3:1-15)
Ndio hapo utaona hata vile ambavyo hakuomba, kama vile Mali Mungu alimpatia, kwasababu alipendwa sana na Mungu kwa kile alichokitamani. Na kama isingekuwa yeye mwenyewe kuja kukengeuka mwishoni, basi angekuwa ni mfano mkubwa sana wa kuigwa katika biblia nzima.
Vivyo hivyo na wewe, ukiitafuta hekima, ujue unatafuta kupendwa na Mungu, na hekima ya Mungu ipo katika Neno lake. Ukiwa ni mtu wa kujifunza biblia, na sio msomaji tu, kama gazeti, Hekima hiyo itaingia yenyewe moyoni mwako (Mithali 2:10). Na Mungu atakusaidia kuwapa wengine neema hiyo. Na mwisho wa siku utapendwa na Mungu.
Hekima zote za kimaisha, za kiutumishi, za kifamilia, za kijamii, zipo katika Neno la Mungu. Hivyo hakuna namna utaweza kuishi bila kusoma biblia.
Hivyo mambo hayo matatu tukiyachanganya. Yaani UPENDO, UTHABITI WA MOYO, NA HEKIMA.
Basi tujue kupendwa na Mungu, ni lazima kutatokea tu kwetu, . Na faida yake ni kuwa, tutaonyeshwa na mambo makubwa Zaidi ya tunayoyajua. Danieli na Yohana ndio waliopewa siri za nyakati za mbeleni. Na mpaka sasa tunagemea sana nabii zao ili kutambua nyakati na majira ya siku za Mwisho. Vilevile hata na vyote tunavyovisumbukia vya mwilini, ikiwa tutapendwa na Mungu basi yeye mwenyewe atavisogeza karibu na sisi. Kama alivyofanya kwa mtumwa wake Sulemani, na Danieli.
Bwana akubariki, na nikutakie kupendwa kwema na Bwana.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
Donda-Ndugu ni nini?
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
Moabu ni nchi gani kwasasa?
Kigao ni nini? Na Je kinafunua nini kwa agano jipya?
Rudi nyumbani
Print this post
Kukana ni kitendo cha kumkataa mtu aliyekaribu nawe, kwa hofu/shinikizo Fulani pengine aidha kwa hofu ya kuaibishwa, au kudharauliwa, au kuuliwa au kutengwa, au kuchekwa n.k. Lakini kimsingi sio kwamba humpendi au huyo mtu hana thamani yoyote kwako.
Lakini kusaliti, ni jambo baya Zaidi, kwasababu linahusisha, kumkataa mtu Fulani aliye karibu nawe kwa hiari yako mwenyewe, pasipo shinikizo lolote, kwa maslahi yako binafsi, ni kitendo cha moyo-baridi kabisa.
Kwamfano Petro alimkana Bwana, kutokana na shinikizo la hofu ya yeye kukamatwa na kwenda kupigwa kama Bwana..Lakini hapo nyuma utaona, alidhubutu kumuhakikisha kabisa Bwana kwamba hata wenzake wote wajapomkana, yeye hatofanya hivyo (Mathayo 26:33-35)
Utaona tena hata baadaya ya kutubu kwake baadaye, alipokutana na Bwana kule baharini bado alimuhakikisha mara tatu kuwa anampenda yeye..(Yohana 21:15-17). Kuonyesha kuwa ni shinikizo ndio lililompeleka kufanya vile, lakini moyo wake bado upo kwa Yesu.
Lakini Yuda tangu mwanzo alikuwa hampendi Bwana, japokuwa yeye alipendwa sana, mahali pengine mpaka Yesu akawa anampa siri zake za ndani japokuwa alikuwa mwizi, biblia inasema hivyo katika Zaburi 41:9
9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.
Lakini kinyume chake akarudisha mabaya badala ya mema. Utaona yeye mwenyewe kwa hiari yake akawafuata wakuu wa makuhani bila shinikizo lolote, akawaambia mtanipa nini, nikiwapa Kristo!. Wakamuahidia Pesa. (Mathayo 26.14-16)
Usaliti unafanana na mtu ambaye yupo tayari kumuua au kumletea madhara mzazi wake, kwa faida zake mwenyewe, pengine mali, au cheo, au heshima. Bila kujali kuwa yeye ndiye aliyemnyonyesha, aliyemtunza tangu akiwa tumboni, ndiye aliyemsomesha na kumvisha n.k.
Lakini kibiblia, vyote viwili yaani “kukana na kusaliti” hatupaswi kuwa navyo kwa Bwana wetu.
Leo hii wapo watu wanaomsaliti Bwana..Ndio hawa manabii na makristo wa uongo. Ambao wanajua kabisa waliokolewa kwa thamani, walitolewa chini matopeni, lakini wanapokuzwa kidogo, wanaanza kumgeuza Kristo kuwa biashara yao. Wanaacha utumishi walioitiwa, wanatumia fursa ya Kristo, kuyashibisha matumbo yao tu… Hawa ndio wakina Yuda.
Wafilipi 3:18 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; 19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Wafilipi 3:18 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Lakini Wakanaji, ni wakristo wote, ambao mioyo yao haipo kikamilifu kwa Bwana..wapo nusu nusu, ndio wale wakipitia dhiki kidogo, wapo tayari kumwacha Kristo, kisa ndugu, au wazazi, au shughuli, au ujana au anasa..hali na mazingira yanawafanya wamkane Bwana wao moja kwa moja, kwa matendo yao.
Na hii ni mbaya sana Bwana Yesu mwenyewe alisema..
Mathayo10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. 35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; 36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. 37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. 39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.
Mathayo10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.
39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.
Umeona?..Lipi bora, uchukiwe na ulimwengu leo, lakini siku ile utukuzwe na Yesu, au leo hii umkane halafu siku ile ukwane naye? Majibu yanajulikana.
Hatupaswi kuogopa kuonekana washamba kisa tumeokoka, hatupaswi kuogopa kupigwa, au kuchekwa, au kuonekana tumerukwa na akili sababu ya Yesu, mwokozi wetu. Bali tumkiri yeye kwa matendo yetu, kwasababu hata yeye mwenyewe alidharauliwa lakini akayapuuzia maradhau yao (Isaya 53:3).
Hivyo sote tujifunze kujitwika misalaba yetu tumfuate Kristo. Ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu,.
Bwana atubariki.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Je! Yuda atahukumiwa na Mungu kwa dhambi yake ya usaliti?
Chapa zake Yesu ni zipi hizo?
WAPENZI, MSIIAMINI KILA ROHO.
Neno ‘Kima’ linamaanisha nini Katika biblia? (Mathayo 27:9 )
Je! Ni kanisa lipi sahihi kumuabudia Mungu?
Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).
Ijumaa kuu ni ijumaa ya mwisho kabisa ya Bwana wetu Yesu Kristo kuwepo hapa duniani, ni siku ile ambayo alipitia mateso mengi, na kusulibiwa, na kufa na kisha kuzikwa. Siku hii huadhimishwa na wakristo wengi ulimwengu, kama kukumbuka la mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo kila mwaka.
Lakini swali ni kwanini iitwe ijumaa kuu na sio ijumaa ya mateso au ya huzuni? Kwanini iwe kuu? Wakati siku hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana ya mamlaka ya giza, ya huzuni na masumbufu ya Yesu mwokozi wetu?
Ni kweli kwa jicho la nje! Ni siku isiyo nzuri, lakini kwa jicho la Roho ni siku ya furaha sana tena sana kwetu sisi wanadamu, Kwani ni siku ambayo kwa mara ya kwanza tulifutiwa mashtaka yetu ya hukumu, tangu tulipopoteza uzima pale Edeni. Kwani asingekufa Yesu, tusingepata msamaha wa dhambi.. Hivyo kifo chake, kilileta ukombozi mkuu sana kwetu, na matokeo yake hatupaswi kulia, kinyume chake tufurahie, kwani siku kama ya leo, karibia miaka 2000 iliyopita, tuliwekwa huru…Hivyo ni sahihi kuitwa ijumaa kuu na sio ijumaa ya mateso.
Ni sawa na mfano wa Samaki anayevuliwa, yeye kwa upande wakw kweli atapitia mateso ya kufa, lakini yule anayemvua atafurahia kupata kitoweo. Hivyo tunaweza kusema ni uchungu kwa Samaki lakini furaha kwa mvuvi..
Kifo cha Bwana wetu Yesu kilikuwa ni faida kubwa kwetu, kwasababu kama damu yake isingemwagika, tusingepata ondoleo la dhambi zetu (Waebrania 9:22).
Jibu ni La, desturi ya kutokula nyama (ya wanyama-damu moto), ni pokeo tu la kanisa katoliki, ambao kwa mujibu wao, wanafanya hivyo kwa heshima ya Kristo, kuutoa mwili wake, kama sadaka kwetu, kwasababu nyama ni chakula cha starehe, hawafanyi hivyo ili kuyatafakari mateso ya Bwana, na sio tu katika siku ya ijumaa kuu, bali pia siku ya jumatano ya majivu, pamoja na ijumaa nyingine zote, zinazofuata katika mfungo hawali nyama .
Lakini agizo hilo halipo mahali popote katika maandiko. Kama ukila haufanyi makosa, au usipokula vilevile haufanya makosa.
Jibu ni la!, Biblia haijatupa agizo wala katazo la mtu kuiadhimishi siku Fulani kwa Mungu wake.
Ni kwa jinsi yeye anavyoamini tu!.
Warumi 14:5 “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe. 6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu”.
Warumi 14:5 “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu”.
Hivyo ikiwa wewe hauoni kama siku ya ijumaa kuu inafaida yoyote kwako, basi usimuhukumu yule ambaye anaiadhimisha kwa Mungu wake, lakini pia wewe ambaye unaidhimisha usimuhukumu yule ambaye haiadhimishi. . Ikiwa unaona mfungo huo kwa kipindi hicho cha pasaka hauna maana kwako, hufanyi kosa, lakini pia usimuhukumu yule ambaye anafunga kwa ajili ya Bwana wake aliyemfia msalaba.Ndivyo ilivyo
Shalom.
Easter ni nini?. Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?
PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA PASAKA?
Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?
Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3
WhatsApp
Mtu ni kiumbe cha kwanza kilichoumbwa na Mungu duniani, chenye mfano wake na sura yake, kilichoumbiwa utashi na ujuzi ndani yake, kilichotofautishwa na wanyama wote na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu duniani Ndicho kinachoitwa mtu.
Tunasoma hilo katika,
Mwanzo 1:26
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Lakini jina Binadamu/mwanadamu, ni neno lililozuka kufuatana na jina la mtu wa kwanza aliyeitwa Adamu.
Jina hilo alipewa na Mungu..Hivyo watu wote waliozaliwa na yeye waliita “wana wa Adamu”kwa kifupi “wanadamu” ambapo jina hilo kwa kiharabu linatamkwa “bin-Adam” ambapo sisi tunatamka “Binadamu”
Lakini ni mtu yule yule..isipokuwa asingeweza kuitwa binadamu siku ile ya kwanza alipoumbwa kwasababu alikuwa bado hajapewa jina, na pia halikuwa hana baba wa mwilini.
Ni sawa na Neno mwebrania na mwisraeli… kabla ya Yakobo kubadilishwa jina lake wana wote wa Ibrahimu hata Ibrahimu mwenyewe aliitwa Mwebrania..(Mwanzo 14:13)
Lakini Yakobo alipobadilishwa jina na kuitwa Israeli, utaona uzao wake wote baada ya pale ulizoeleka na kuitwa waisraeli mpaka leo. Lakini bado mahali pengine waliendelea pia kuitwa waebrania kwa asili yao.
Ndivyo ilivyo kwa mtu na mwanadamu. Ni yule yule kulingana na majira.
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
Pango la Makpela ni lipi, je lina umuhimu wowote kwetu?
Uru wa Ukaldayo ni nini?
MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.
Utasi ni ugonjwa gani? (Marko 7:32).
Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?
Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
Tofauti na “Kima” mnyama ambaye anajulikana (jamii ya nyani), ukirudi katika biblia Neno hili lina maana nyingine pia.
Kima maana yake ni “thamani ya kitu katika pesa”.
Kwa mfano tukisema kima cha nazi ni Tsh. 1000. Maana yake ni kuwa thamani ya nazi ni sh. 1000.
Kwamfano Neno hilo utalipata katika vifungu hivi;
Mithali 31:10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani”.
Yaani thamani mke mwema, inazidi thamani ya madini ghali ya Marijani (Ruby).
Mathayo 27:9 “Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima;” Walawi 27: 11 “Na kama ni mnyama ye yote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa Bwana, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani; 12 na kuhani atamtia kima, akiwa mwema akiwa mbaya; kama wewe kuhani utakavyomtia kima, ndivyo itakavyokuwa. 13 Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako. 14 Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa Bwana ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa”.
Mathayo 27:9 “Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima;”
Walawi 27: 11 “Na kama ni mnyama ye yote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa Bwana, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani;
12 na kuhani atamtia kima, akiwa mwema akiwa mbaya; kama wewe kuhani utakavyomtia kima, ndivyo itakavyokuwa.
13 Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako.
14 Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa Bwana ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa”.
Soma pia Walawi 27:23, Ayub 18:28, Matendo 7:16
Je, kipo kima kinachozidi thamani ya Bwana Yesu?
Yuda alijaribu, kumsaliti Bwana kwa kima cha fedha, lakini Pamoja na kupokea mapesa yote, bado mwisho wa siku aliona, thamani yake hailinganishwi na utajiri wowote wa ulimwengu, ijapokuwa alikuwa ni mwizi lakini utaona alirudisha fedha zao zote, na kwenda kujinyonga.
Sasa Ikiwa watu waovu wanauona uthamani wa Bwana, hadi kwenda kujiua, iweje wewe uone kazi ni bora kuliko Bwana Yesu, anasa ni bora kuliko ibada?.
Je! thamani ya Bwana wako inazidi thamani ya huu ulimwengu? Bwana Yesu alisema Itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima halafu upate hasara ya nafsi yako? Itakufaidia nini?
Tubu mgeukie Bwana..
Ikiwa hujampa Bwana Yesu Maisha yako, na upo tayari kufanya hivyo leo, kwa kumaanisha kabisa, basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa Sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Konde la Soani ni nini? (Zaburi 78:12,43)
Deraya ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 59:17
Bushuti ni nini?
Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?
Tunguja ni nini katika biblia? (Mwanzo 30:14).
Hisopu/ Hisopo ni nini katika biblia?(Zaburi 51:7)
Kuhusuru ni nini kibiblia? (Luka 19:43)
Kujuzu ni nini kama tunavyosoma katika 2Wakorintho 12:4?
Ni eneo la pango ambalo lilikuwa karibu na mji wa Israeli unaoitwa Hebroni, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa mtu mmoja aliyeitwa Efroni, kwa ajili ya maziko ya mke wake Sara.
Mwanzo 23:13 “Akamwambia Efroni, na watu wa nchi wanasikiliza, akisema, Tafadhali unisikilize; nitatoa kima cha shamba, nawe ukipokee kwangu, nami nitamzika humo maiti wangu. 14 Efroni akamjibu Ibrahimu, akamwambia, 15 Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n’nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako. 16 Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara”.
Mwanzo 23:13 “Akamwambia Efroni, na watu wa nchi wanasikiliza, akisema, Tafadhali unisikilize; nitatoa kima cha shamba, nawe ukipokee kwangu, nami nitamzika humo maiti wangu.
14 Efroni akamjibu Ibrahimu, akamwambia,
15 Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n’nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako.
16 Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara”.
Eneo hilo baadaye lilikuja kugeuka kuwa kaburi la kifamilia, kwani hapo hapo ndipo Ibrahimu alipokuja kuzikwa na watoto wake, halikadhalika, ndipo Yakobo na Esau walipomzikia baba yako Isaka,
Na wakati wakiwa kule Misri, Yakobo aliwaagiza Watoto wake,pia wakamzike katika kaburi hilo la familia, la Makpela.
Mwanzo 49:29 “Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti; 30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia. 31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea; 32 shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi”.
Mwanzo 49:29 “Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;
30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;
32 shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi”.
Eneo hilo kwasasa, pale Israeli limejengwa msikiti, ujulikanao kama “msikiti wa Ibrahimi”, japo wote wayahudi na waislamu, hakuna hata mmoja anaweza kusema anao umiliki wa moja kwa moja wa hapo.
Lakini Je pango la makpela lina umuhimu kwetu hadi sasa au kwa Wayahudi?
Pango hili, au lolote lile ambalo lilizikiwa watakatifu, halina umuhimu wowote katika Imani yetu, Zaidi ya mambo ya kihistoria tu. Myahudi au mkristo yoyote ukizikwa karibu na eneo hilo, hakutakufanya uende mbinguni, Wapo wengine wanafikiri, wakienda Yerusalemu na kuomba kwenye ule ukuta wa Nehemia wa maombolezo, ndio maombi yao yatasikiwa. Au wakienda kubatizwa katika mto Yordani kama Bwana Yesu ndio ubatizo wao utapokelewa, jambo ambalo sio kweli.
Halikadhalika na Pango hilo la makpela halina umuhimu wowote, kwa mtu yeyote, kuzikiwa pale.
Watoto wa Ibrahimu/Wana wa Ibrahimu walikuwa ni wangapi?
Je! ni halali kwa mtu wa Mungu kutumia njia za uzazi wa mpango,ikiwamo mipira?
Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.
MWENGE WAKO WA UHURU UPO WAPI?
Kuna njia kuu sita(6)
Ni vema ukazifahamu hizi njia Mungu anazozungumza na watu, ili usitegemee tu njia moja uifahamuyo wewe, matokeo yake ukakosa shabaha ya kuzisikia sauti za Mungu kila siku maishani mwako zinapozungumza na wewe.
Hii ni Aidha kwa Sauti, ndoto, au maono,
Ni mojawapo ya njia ambayo Mungu anazungumza na watu. Na ndio inayojulikana na kutegemewa na wengi.
Ayubu 33:14-15
[14]Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. [15]Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;
Katika maisha yetu kwa namna moja au nyingine Mungu alishazungumza nasi kwa njia hii. Unaweza usione, maono au usisikie sauti lakini kila mtu huwa anaota. Na kwa njia hiyo Mungu huzungumza.
Hii ndio sauti ya Mungu namba moja ambayo inazungumza na mtu moja kwa moja na kwa wakati wote..ni sauti ambayo hailinganishwi na sauti nyingine zozote.
Ukiwa ni msomaji mzuri wa Neno, utamsikia Mungu katika nyanja zote za Maisha akikufariji, akikuonya, akikushauri, akikuongoza n.k. Ni pakeji iliyojitosheleza., ambayo hailinganishwi na njia nyingine yoyote.
2Timotheo 3:16 “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;”
Ikiwa wewe umeokoka, na umejazwa Roho Mtakatifu, basi ujue mara nyingi sana Mungu atatumia amani yake moyoni mwako kuamua mambo mengi..
Na ndio maana Bwana Yesu alisema..
Mathayo 10:11-13
[11]Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka. [12]Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni. [13]Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
[11]Na mji wo wote au kijiji cho chote mtakachoingia, tafuteni ni nani humo aliye mtu mwaminifu; mkae kwake hata mtakapotoka. [12]Nanyi mkiingia katika nyumba isalimuni.
[13]Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
Wakolosai 3:15a “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu;..”
Kuonyesha kuwa amani itokayo kwa Roho ni sauti ya Mungu kutuongoza, ikiwa umepoteza amani ghafla katika mazingira fulani kuwa makini sana hapo. Wakati mwingine ni Mungu anazungumza.
Hapa anaweza akachagua aidha apitie mtu mwovu au mtu mwema. Mara nyingi sana Mungu anazungumza na watu kupitia watumishi wake, yaani wahubiri, waalimu, wainjilisti n.k.
Yeremia 25:4
[4]Naye BWANA ametuma kwenu watumishi wake wote, hao manabii, akiamka mapema na kuwatuma, lakini ninyi hamkusikiliza, wala hamkutega masikio yenu, msikilize.
Na mara nyingine tena anaweza kutumia watu wa kidunia kukuonya..kama vile maaskari, wakuu wa hii dunia n.k.
Hivyo ni kuzingatia sana unachokisikia au kufundishwa au kuonywa na watu, hususani watumishi wa Mungu..Mara nyingine sauti ya Mungu ipo nyuma yao.
Mazingira yanaweza yakawa ya kimaisha, au ya kihali…kwa mfano Mungu akitaka uelewe jambo fulani, wakati mwingine hatumii sauti ya moja kwa moja, kwasababu pengine unaweza kulichukulia juu juu tu au usimwelewe, hivyo atakupitisha katika maisha fulani au mazingira fulani, na kwa kupitia hayo utajua kabisa hapo ni Mungu alikuwa akisema na wewe.
Mfano wa watu kama hawa alikuwa ni Nebukadreza, yeye alionywa na Mungu, awe mnyenyekevu na amche Mungu, lakini hakusikia, kinyume chake akapuuzia ule unabii aliopewa na Danieli. Matokeo yake baada ya miezi 12, akageuzwa kuwa kama mnyama, akawa anaishi huko misituni akila majani kama ng’ombe..mpaka siku alipoelewa somo kuwa aliye juu ndiye anayetawala falme zote za duniani. Ndipo akajinyenyekeza ,hivyo Mungu akamrudishia ufalme wote wa dunia. (Danieli 4)
Sauti ya Mungu imejificha sana katika vitu vinavyotuzunguka na asili, kiasi kwamba tungefahamu vema basi tusingekuwa na ugumu wa kumwelewa Mungu.
Embu fikiri Bwana Yesu alivyotuambia..tafakarini Kunguru?..hawapandi hawavuni wala hawana maghala ya chakula lakini wanakula..Je sisi si mara nyingi zaidi ya hao? (Luka 12:24)
Hili ni neno ambalo lilikwepo tangu enzi na enzi kiasi kwamba watu wangekuwa wanalitafakari kabla hata ya Yesu, wasingekuwa na hofu ya maisha pale wanapotaka msaada kutoka kwa Mungu.
Vivyo hivyo utazamapo, bahari, milima, miti, zipo sauti nyingi sana za Mungu nyuma yake .. Chukua muda mwingi kutafakari, utaisikia sauti ya Mungu waziwazi.
Mungu alimwambia Ibrahimu angalia juu tazama nyota za mbinguni na mchanga wa baharini upate imani kwangu.
Hivyo ni vizuri ukapata maarifa haya usije ukaangamia kwa kutomwelewa Mungu. Leo hii watu wanategemea njia moja tu..ile ya moja kwa moja..yaani kusikia sauti, au kuona maono au kuota ndoto. Na kusahau hizi nyingine.. Ndio hapo utasikia wakisema nimeomba sana, nimelia sana Mungu aseme na nini, lakini sijawahi kumsikia.
Ni kwanini? Nikwasababu wanalazimishia njia hiyo hiyo moja Mungu aseme nao..
Hawajui kuwa Mungu hapangiwi fomula ya kuzungumza.Hivyo wewe uombapo..kuwa mtulivu, soma sana Neno mtafakari Mungu..subiri azungumze kwa jinsi apendavyo yeye. Atakujibu tu aidha kwa Neno lake, au mtumishi wake, au amani moyoni mwako, au kwa kutazama mambo ya asili, ukiona hivyo basi ujue ni Mungu huyo.
Hivyo kaa katika utulivu wa Roho, zingatia kusoma Neno..kwasababu maarifa kama haya utayapata katika biblia na sio kwa kuota au kuona maono.
Yohana 8:32 “tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”.
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
NJIA SAHIHI YA KUFUNGA.
Unyenyekevu ni nini?
ALITOKA HUKO, AKAENDA MAHALI KARIBU NA JANGWA.
SWALI: Naomba kufahamu maombolezo ya Hadadrimoni tunayoyasoma katika Zekaria 12:11 ni maombolezo gani hayo?
Zekaria 12:11 “Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido”.
JIBU: Hadadrimoni ni eneo lililokuwa sehemu ya bonde lijulikanalo kama Megido huko Israeli. Bonde hili lilisifika kwa vita, na Zaidi sana kuuawa kwa baadhi ya viongozi wakubwa. Hivyo kupelekea maombolezo makubwa sana kwa watu waliouliwa viongozi wao.
Mfano katika Habari hii, inamlenga mfalme Yosia, ambaye ndiye aliyekuwa tumaini la mwisho la Taifa la Israeli. Kama wewe ni msomaji wa biblia utakumbuka, Yosia alikuwa mfalme aliyemcha Mungu sana kuliko wafalme wote wa Israeli,tukimwondoa Daudi, na yeye ndiye aliyefanikiwa kuondoa sanamu zote Israeli kipindi kile, Na ndiye mfalme ambaye kuzaliwa kwake kulitabiriwa miaka mingi sana kabla hajazaliwa.
Hivyo waisraeli walimwona kama ndiye tumaini pekee waliobakiwa nalo.
Lakini siku moja alitoka kwenda kupigana vita na mfalme wa Misri aliyeitwa Neko. Na kinyume na matazamio yake, aliuliwa, na mahali alipouliwa palikuwa ni hapo Hadadrimoni katika bonde la Megido.
Israeli nzima iliposikia, ilimwombolezea maombolezo makubwa sana, taa ya Israeli kuzima ghafla, mpaka wakamwekea kumbukumbuku lake la kila mwaka akumbukwe.
2Wafalme 23:29 “Katika siku zake, Farao-neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana na mfalme wa Ashuru, akafika mto Frati; naye mfalme Yosia akaenda kupigana naye; naye mfalme wa Misri akamwua huko Megido, hapo alipoonana naye”.
2Nyakati 35:25 “Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote waume kwa wake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hata leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika maombolezo”.
Hivyo Mungu akatumia kivuli hicho kueleza jinsi taifa la Israeli litakavyokuja kuomboleza huko mbeleni, siku watakapopewa neema ya kumtambua Kristo. Biblia inasema wayahudi watamwombolezea Yesu waliyemchoma, watalia kama vile mtu aliyefiwa na mwana wake wa pekee, mfano wa pigo la wamisri la kuuliwa wazaliwa wao wa kwanza, jinsi walivyokuwa na maombolezo makuu.
Kama vile, maombolezo ya Yosia katika bonde la Hadadrimoni, Waisraeli walivyombolezea mfalme wao, kwa uchungu mwingi, ndivyo itakavyokuwa siku hiyo watakapomwagiwa neema ya kumtambua Kristo..
Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza. 11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, KAMA MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI KATIKA BONDE LA MEGIDO. 12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao; 13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. 14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Zekaria 12:10 “Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, KAMA MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI KATIKA BONDE LA MEGIDO.
12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.
Ndugu, Kipindi si kirefu hii neema inayochezewa leo hii, itageuka na kuwarudia wayahudi. Kipindi hicho unyakuo utakuwa umeshapita, na Roho Mtakatifu hayupo tena kwetu sisi watu wa mataifa, bali kwa watu wake Israeli. Dunia itastaajabia, kuona watu hawa wametolea wapi moyo huo wa kujuta kwa ajili ya Yesu ambaye leo hii wanamkataa.
Kwani wayahudi hawa wakati huo, biblia inasema watajitenga, familia kwa familia, ukoo kwa ukoo, kila moja atakuwa na maombolezo yake makuu sana haradharani na sirini, kudhihirisha kazi ya Roho Mtakatifu juu yao. Sasa wakati huo ndio Mungu atakuwa anawaandaa ili kuwarudishia ufalme ambao waliutazamia kutoka kwa masihi wao, sawasawa na lile ulizo la mitume (Matendo 1:6)
Ndugu, ukishaona mabadiliko haya kwa wayahudi, ujue umeshaachwa katika unyakuo, vilevile hii dunia itakuwa na kipindi kifupi sana kisichozidi miaka 7 hadi iishe. Leo hii tumeshaona Israeli imekuwa taifa, wote wamesharudi kwao. Unadhani wanachosubiria ni nini kama sio kurudiwa wakati wowote.
Bwana Yesu alisema,
Mathayo 24:32 “Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu”;
Mtini unawakilisha taifa la Israeli (Yer 24), Hivyo tuonapo Israeli leo hii inachipuka, tujue kuwa wakati wa mavuno umeshafika.
Je!, unalitambua hilo? Bado unaipuuzia hii neema ambayo hatuna nayo muda mrefu?. Una Habari kuwa unyakuo ni wakati wowote, na hatua zake tayari zimeshaanza?. Wakati tulionao sasa si wakati wa kubembelezewa wokovu, Injili imeshazagaa kila mahali, watu wote wameshasikia, ni wakati wa kujitakasa, wewe ambaye tayari umeshaokoka. Lakini kama bado upo nje ya neema kipindi hichi? Utakuwa ni wa ajabu kweli.
Unasubiria siku Fulani, neema ikufikie? wakati neema ya wokovu ipo tayari kila mahali, unasubiria ikufikieje tena? Tambua kuwa njia imeshasonga, na wengi wanatamani waingie wanashindwa, kwasababu upotofu mwingi upo duniani, na wewe bado tu unaisubiri.. Ni kuwa makini sana. Neema inakimbilia Israeli sasa, jicho la Bwana linaelekea kule sasa, kwani muda wetu umeshakwisha.
Bwana atusaidie.
SIKU YA TAABU YA YAKOBO.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.
SWALI: Shalom… Pastor naomba kuuliza je ni sahihi mtumishi kuongoza kanisa hajafunga ndoa? na anaweza kubatiza washirika? Amina.
JIBU: Kigezo cha mtu kuwa Kiongozi wa kanisa, na kufanya kazi zote za madhabahuni, ikiwemo kubatiza, kuwawekea watu mikono ya utumishi, n.k. vimetolewa katika kitabu cha 1Timotheo 3:1-7
1 Timotheo 3 : 1-16
1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.
2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha;
4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu;
5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?)
6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Askofu maana yake ni mwangalizi wa kanisa, Hivyo yeyote anayelichunga kanisa, awe ni mchungaji, mwalimu, Mtume, maana yeye ndio mwangalizi basi vigezo hivyo vinamuhusu.
Lakini katika vigezo hivyo vyote, hakuna hata kimoja, kinachosema, ni lazima aoe.. Isipokuwa anasema Askofu ni lazima awe ni mume wa mke mmoja..Akiwa na maana kwamba ikiwa ni mwana-ndoa basi, anapaswa awe ni mume wa mke mmoja, na si Zaidi, kama anao wake wawili au watatu, tayari ameshakidhi vigezo vya kutostahili kuitwa mchungaji.
Lakini ikiwa ni mtu ambaye, hajaoa lakini ameshika vigezo vyote, hivyo, yaani, ni mtu asiyelaumika, si mlevi, mpole, si mpenda fedha, aliyeshuhudiwa na watu ni mwema, amekomaa kiroho. Basi huyo anavigezo vyote vya kuwa mchungaji, au kiongozi yoyote wa kanisa.
Mtume Paulo hakuwa ameoa, lakini alikuwa ni mwangalizi wa makanisa yote yaliyokuwa Asia, na mataifa mengine, Na Zaidi sana yeye ndiye aliyetoa mwongozi wa mafundisho ya ndoa.
Hivyo kuoa/ kutokuoa, si takwa, la kuwa askofu.
Kinyume chake mtume Paulo,alishauri watu wote wawe kama yeye (yaani wasioe), kwasababu watu wasiooa inawapa wigo mpana wa kumtumikia Mungu bila kuvutwa na mambo mengine, ikiwa wamemaanisha kweli kujikita kwa Bwana.
1Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”.
1Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”.
Lakini ikiwa huwezi kuishi Maisha hivyo, kwa jinsi ulivyoitwa, basi hakikisha unatumika kiuaminifu, hapo utakuwa umekidhi vigezo vya kulichunga kundi , kubatiza, n.k.
Ndoa na Talaka
Ndoa ya serikali ni halali?
Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?
Uvuvi bora hauchagui wa kuvua.
Askofu na mchungaji mkuu ni nani?
WANA-NDOA: Baba Mkwe, Na mama Mkwe.
Nakusalimu katika jina la mwokozi wetus Yesu Kristo, sifa na utukufu vina yeye milele na milele. Amina.
Unafahamu kuwa shetani ambaye ni adui yetu, si kila wakati anafanya mambo yake kwa kutegemea jitihada zake tu, anajua kabisa mambo mengine huwa hayatoki isipokuwa kwa kufuata kanuni ambazo tayari Mungu alishaziweka.
Na huwa anazitumia hizo kanuni, kutuharibu sana, lakini sisi kama wana wa ufalme, hatuzitumii kumuharibu yeye.
Kwamfano madhara aliyopanga kumletea Ayubu, alitambua kuwa haiwezekani kwa njia ya kawaida kuyatekeleza ,. Ndipo akatumia njia ya juu Zaidi ya kujishusha, kwa kwenda KUJIHUDHURISHA mbele za Mungu,.
Akashusha kiburi chake hadi chini kabisa, akaungana na Malaika watakatifu wa Mungu, kupanda mbinguni, akaenda mbele ya uwepo wa Mungu, kwa unyenyekevu wote, akitumaini kuwa kwa kutenda kule, ni lazima tu Mungu atamwangalia, kwasababu Mungu ni Mungu wa uumbaji wote.
Na kweli baadaye Mungu alipomwona anatembea tembea mbele ya uwepo wake kwa muda mrefu, akaanzisha mazungumzo naye, Akamuuliza unatoka wapi shetani, akasema duniani, katika mizunguko yangu, ndipo shetani akatumia fursa hiyo ya mazungumzo, kupeleka na mashataka yake yote. Na mwisho wa siku akapatiwa haja yake.
Akashuka chini, akamfanya Ayubu kama alivyoweza kumfanya..
Ayubu 1:6 “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. 7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. 8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu”.
Ayubu 1:6 “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao.
7 Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo.
8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu”.
Tunachopaswa tujue ni nini, Ikiwa mungu wa dunia hii, anajua siri ya mafanikio ya uharibifu wake, haitegemei tu nguvu zake mwenyewe, bali pia kwa kujihudhurisha mbele za Mungu ..Unategemea vipi wewe na mimi tusiwe watu wa namna hiyo?
Shetani anatushangaa sana, tunapomkimbia Mungu, anatushangaa sana tunapokwenda mbali na uwepo wa Mungu, kwa visingizio visivyokuwa na maana, hatutaki kwenda kumfanyia Mungu ibada hata mara moja kwa wiki tunasema tumechoka, kwasababu jumatatu tunakwenda kazini hivyo hatuna budi tulale!! Ndugu ukitegemea nguvu zako kuyaongoza haya Maisha jihesabie tu wewe ni MKIA Maisha yako yote. Ndivyo ilivyo..
Hilo shetani alijaribu akaona halifai, na wewe unalijaribu, alijua si kila wakati nitajiamulia tu mimi mwenyewe, kwa nguvu zangu..Lazima niwe na muda wangu wa kwenda kujinyenyekeza, tena kwa muda mrefu mbele za Mungu.
Ikiwa tunaona mikesha ni shida, hata mara moja kwa mwezi, tusahau Mungu kuanzisha mazungumzo yoyote na sisi. Ikiwa hatujizoezi kusali mara kwa mara, na kuutafuta uso wa Mungu hata kwa mifungo wakati mwingine, tujue tu mambo mengi sana tutafeli kuyatimiza maishani mwetu.
Faida za kujihudhurisha mbele za Bwana ni zipi?.
Tunapokuwa uweponi mwa Bwana muda mrefu, Mungu mwenyewe ataanzisha mazungumzo na sisi, atatuuliza, unasumbukia nini, una haja gani, unatafuta nini? Kama tu alivyofanya kwa shetani…Lakini akitutazama hatupo uweponi mwake, Tunazunguka zunguka tu duniani, na masumbufu ya Maisha haya kila wakati, siku saba kwa juma, siku 365 za mwaka, na yeye ataendelea na mambo yake, atatuacha tutaabike wenyewe..
Biblia inasema..
Yakobo 4:8 “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi..”
Ndugu tujizoezi, kumkaribia Mungu kila siku, ibada inayotoka rohoni iwe ni sehemu ya Maisha yetu, Na bila shaka tutaanza kumuona Mungu akisema na roho zetu.
Kumbuka uanzapo kufanya mambo kama hayo kwa bidii, hutasikia sauti kama sauti ikisema na wewe, bali rohoni Mungu atakuwa anazungumza na Maisha yako. Na mara utaona yote uliyokuwa unamwomba, au unayatamani yatendeke tangu zamani, Mungu anakufanikisha kwa njia ambazo hujazitazamia. Hivyo ndivyo Mungu anavyozungumza na watu.
Tukiijua kanuni hii, shetani atatuchukia sana, kwasababu tutakuwa tumeshajua siri ya mafanikio yetu, kama yalivyokuwa yake katika huu ulimwengu.
Kama wewe ni mtakatifu, anza sasa kumpa Mungu muda wako wa kutosha, huko ndiko kujihudhurisha mbele zake, usiwe na udhuru wa kutokwenda ibadani, usiwe na udhuru wa kutohudhuria mikesha na wenzako, usiwe na udhuru wa kutokufunga na kuomba, na kujifunza Neno kila siku. JIHUDHURISHE kwa kadiri uwezavyo mbele za Mungu.
Ndivyo Mungu atakavyoanzisha mazungumzo na wewe.
Ikiwa bado upo nje ya Kristo, kumbuka kuwa, hatuna muda mrefu hapa duniani, Unyakuo ni wakati wowote, kulingana na kutimia kwa dalili zote zilizotabiriwa katika maandiko, na kama hilo halitoshi fahamu kuwa mlango wa neema, umeshaanza kufungwa, usipoiamini injili, leo, kesho itakuwa ni ngumu Zaidi, na siku moja hutaiamini kabisa. Kwasababu neema haidumu milele, maandiko yanasema hivyo!.
Hivyo tubu dhambi zako kwa kumaanisha leo, mgeukie Kristo, injili tuliyobakiwa nayo sasa sio ya kubembelezwa, ni wewe mwenyewe uone hali halisi, umgeukie muumba wako.
Maran Atha.
TUSIRUHUSU MAMBO YA KUSUBIRISHA, YAVURUGE MUDA WETU NA MUNGU.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
“Vya Kaisari mpeni kaisari” ni vipi hivyo tunavyopaswa tumpe?.