JE! UNAWEZA KUWA NA GEUKO KAMA LA DAUDI?

JE! UNAWEZA KUWA NA GEUKO KAMA LA DAUDI?

Tunapokisoma kisa cha Daudi, cha kumwiba mke wa shujaa wake (Uria), na kumlazimisha kuzini naye kwa siri, na baadaye kumuua mumewe , (2Samweli 11) tunaishia kuona picha mbaya sana ya Daudi. Na kumshutumu, na wengi wetu kusema Daudi ni mzinzi sana, iweje apendwe na Mungu namna ile, tena awe kipenzi cha Mungu?

Ni kweli kabisa alichokifanya Daudi hakistahili kufanywa na mtu yeyote, ambaye anamjua Mungu, mfano wa Daudi. Lakini kuna funzo kubwa sana ambalo wengi wetu hatulioni nyuma ya maisha ya Daudi baada ya pale.

Daudi alipozama katika dhambi ile, na kugundua makosa yake. Alikuwa na badiliko lisilo kuwa la kawaida. Sio kule alikokuwa anaomboleza usiku kucha, Hapana, lile lingekuwa la “kufoji” tu, ambalo yoyote anaweza kulifanya hata leo. Kinyume chake Daudi alikuwa na badiliko la kimatendo. Na hilo ndilo lililomfanya apendwe sana na Mungu.

Kwa namna gani?

Sasa angalia Daudi Yule Yule ambaye alikuwa ni mzinzi, mwenye tamaa ya hali ya juu, akiona tu mwanamke mzuri hajali, huyu ni mke wa mtu au la yeye alimwiba na kuzini naye. Lakini Dakika zake za mwisho hazikuwa hivyo. Alibadilika kwelikweli baada ya dhambi ile.

Utakumbuka hata alipokuwa mzee, Wakuu wa Israeli walikwenda kumtafutia Binti mzuri bikira katika taifa lote la Israeli, ili amlalie Daudi ampe joto kwasababu nguo za joto hazikutosha. Lakini biblia inasema Daudi alipolala naye ‘hakumjua’.

Kwa jinsi ya kibinadamu, binti alale, na mtu mwenye sifa ya tamaa kama Daudi, halafu asimwingilie. Lazima kutakuwa kuna jambo lingine limetendeka ndani ya maisha ya huyo mtu.

Tusome;

1 Wafalme 1:1

 “Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto.

2 Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto.

3 Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme.

4 Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua

Ni wazi kuwa habari hiyo ilijulikana Israeli nzima, Daudi amelala na binti bikira mrembo miaka kadhaa lakini hajamwingilia. Ni shujaa kiasi gani. Hawakujua kuwa anawathibitishia Israeli kuwa yeye sio Yule wa zamani, sio Yule mzinzi mliyemzoea, ameshabadilika. Si mtu wa kulipuka lipuka tamaa ovyo kama alivyokuwa hapo mwanzo.

Hiyo ndio sababu Mungu alimpenda Daudi. Kwasababu alikuwa na badiliko la dhati Kwa Mungu wake. Je! Na sisi, tunaweza kusema tumeuacha ulimwengu kweli kweli pale tunapomgeukia Mungu, au tutakuwa na vimelea vya kidunia ndani yetu, pale tunapokutana na majaribu kama yale yale ya mwanzo. Tulipokuwa wazinzi na sasa tumeokoka, Je! Tuna ujasiri wa kuishi  maisha ya mbali na zinaa, au bado tupo nusu nusu.

Tuwe na badiliko la dhati, leo tumeanguka katika dhambi Fulani mbaya, sasa tumetubu, tusiwe tena walewale wa kuanza kuangalia angalia nyuma kama mke wa Lutu. Mungu atachukizwa na sisi na mwisho wa siku tutakuwa jiwe la chumvi kama sio kutapikwa mfano wa kanisa la Laodikia.

Tumaanishe kwelikweli kuacha mambo maovu tuliyoyazoelea. Jifunze kwa Daudi. Yule sio mzinzi kama wewe unayejitumainisha kwa visa vyake vya zamani, ukadhani kuwa utanusurika hukumu ukiendelea na tabia hiyo.

Bwana akubariki.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?(Opens in a new browser tab)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 4

Kwanini Daudi achukue mawe matano, na malaini na sio vinginevyo?

(Opens in a new browser tab)(Opens in a new browser tab)MADHIHIRISHO MATATU YA MUNGU.(Opens in a new browser tab)

Rudi nyumbani

Print this post

Rehani ni nini katika biblia?

Rehani ni nini kibiblia?, na je sisi wakristo tunaruhusiwa kuweka kitu rehani?


Rehani ni mali iliyowekwa kama dhamana kwa mkopo uliochukuliwa, maana yake mkopo usipolipwa basi mali ile inachukuliwa ili kufidia ule mkopo.

Katika biblia (Agano la kale), Rehani iliruhusiwa lakini kwa kuiangalia hali ya mtu. Kama mtu alikuwa ni tajiri mwenye uwezo basi alipokopa alipaswa aweke rehani mali itakayosimama badala ya ule mkopo endapo atashindwa kuulipa.

Lakini kama mtu alikuwa ni maskini sana, na hana kitu isipokuwa jiwe la kusagia tu na mavazi, basi hakupaswa kutozwa rehani katika hivyo alivyo navyo, ilikuwa ni dhambi kubwa kutwaa jiwe la kusagia la maskini au mavazi yake kama Rehani.

Kumbukumbu 28: 6 “Mtu awaye yote asitwae jiwe la kusagia, la juu wala la chini, kuwa rehani; kwani hivi ni kutwaa maisha ya mtu kuwa rehani”.

Kumbukumbu 24:17 “Usipotoshe hukumu ya mgeni, wala ya yatima; wala usitwae mavazi ya mjane, yawe rehani;

18 bali kumbuka ya kuwa ulikuwa mtumwa katika Misri, Bwana, Mungu wako, akakukomboa huko; kwa hiyo nakuamuru kutenda neno hili”.

Kwa urefu kwanini si sawa kutwaa jiwe la kusagia la maskini kama rehani waweza kufungua hapa >>>Kwanini jiwe la kusagia Mungu alikataza lisiwekwe rehani? (Kumbukumbu 24:6).

Sasa swali je na sisi wakristo ni sahihi kuweka kitu rehani au kupokea rehani kutoka kwa mtu tuliyemkopesha?

Jibu: Rehani haijakatazwa katika biblia, kama umemkopesha mtu kitu cha thamani, na mtu huyo si ndugu yako katika Imani (yaani mpendwa mwenzako) au si ndugu yako katika mwili (yaani mwanafamilia) waweza kupokea Rehani, ili kumhamasisha kurejesha lile deni, (ikiwa lengo lako si kumkandamiza bali kumhamasisha na kama mtu huyo uwezo huo anao). 

Lakini kama ni maskini na kaja kukopa kwako, si vizuri kuchukua rehani. Waweza kumkopa bila rehani yoyote, ni itakuwa baraka kwako.

Lakini kama ni ndugu yako katika Imani na katika damu, si vyema kumtoza rehani,  wala riba, katika mazingira yoyote yale, awe tajiri au maskini,  waweza kumkopa ukitumai kuwa atakulipa tu pasipo kutaka dhamana.

Lakini pia kama wewe ni mkopaji, (maana yake unakopa kutoka kwa mtu/taasisi kwaajili ya shughuli fulani) si dhambi kusimamisha kitu kama rehani itakayosimama kwaajili ya mkopo wako (kama mtu huyo au taasisi hiyo inahitaji hayo yote).

Bwana akubariki.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

“Humfukuza punda wake asiye baba”, nini maana ya mstari huu? (Ayubu 24:3)

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

LIONDOE JIWE.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.

Rudi nyumbani

Print this post

Rahabu kwenye biblia.

Rahabu ni nani?

Jina “Rahabu” limeonekana mara kadhaa katika biblia likiwa na maana Zaidi ya moja. Maana ya kwanza ni linamwakilisha Mwanamke wa kikanaani aliyekuwa kahaba, aliyewahifadhi wapelelezi wa kiisraeli walioingia kuipeleleza Yeriko, na maana ya pili Taifa la Misri.

Kama tu vile neno “Mharabu” katika biblia linamaanisha Jamii ya watu wa Arabia, lakini pia linamaanisha “Mtu au Malaika anayeharibu Vivyo hivyo na jina Rahabu lina maana Zaidi ya moja.

     1.RAHABU (Kahaba).

Habari ya Rahabu aliywakuwa kahaba tunaipata katika kitabu cha Yoshua mlango wa 2 na wa 6. Mwanamke huyu aliwahifadhi wapelelezi wa kiisraeli walioingia Yeriko kuipeleleza nchi ile.

Yoshua 2:1 “Yoshua, mwana wa Nuni, akawatuma watu wawili kutoka Shitimu kwa siri, ili kupeleleza, akawaambia, Enendeni mkaitazame nchi hii, na Yeriko. Wakaenda wakafika nyumbani kwa kahaba mmoja jina lake aliitwa Rahabu, wakalala huko.

2 Mfalme wa Yeriko akaambiwa, kusema, Tazama, watu wawili wa wana wa Israeli wameingia humu leo usiku, ili kuipeleleza nchi.

3 Mfalme wa Yeriko akatuma watu kwa Rahabu, akasema, Watoe watu wale waliokuja kwako, walioingia ndani ya nyumba yako, maana wamekuja ili kuipeleleza nchi.

4 Yule mwanamke akawatwaa wale watu wawili, akawaficha, akasema, Naam, wale watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka”

       2.TAIFA LA MISRI.

Jina Rahabu pia katika biblia limetumika kuwakilisha Joka kubwa la baharini ambalo ufunuo wake ni Taifa la Misri.

Isaya 30:7 “Kwa maana Misri huwasaidia bure, bila faida; Kwa hiyo nimemwita, Rahabu aketiye kimya”

Isaya 51:10 “Si wewe uliyemkata-kata Rahabu? Uliyemchoma yule joka? Si wewe uliyeikausha bahari, Na maji ya vilindi vikuu; Uliyevifanya vilindi kuwa njia, Ili wapite watu waliokombolewa?”

Zaburi 87: 4 “Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi; Huyu alizaliwa humo”

Soma pia Ayubu 26:12, na Zaburi 89:10..

Jambo kubwa na kuu tunaloweza kujifunza kwa RAHABU (Aliyekuwa Kahaba) ni IMANI.

Alikuwa na Imani juu ya mambo yatarajiwayo sawasawa na Waebrani 11:1. Aliziamini nguvu za MUNGU wa Israeli, hivyo akajua yatakayofuata baadaye kuwa ni anguko la Yeriko, hivyo akatafuta njia ya kujinusuru yeye na familia yake kwa kujiungamanisha na jamii ya Israeli.

Waebrania 11:31  “Kwa imani Rahabu, yule kahaba, hakuangamia pamoja na hao walioasi; kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi kwa amani”.

Yakobo 2:25 “Vivyo hivyo na Rahabu, yule kahaba naye, je! Hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipowakaribisha wajumbe, akawatoa nje kwa njia nyingine?

26  Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa”.

Maran atha.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

RAHABU.

LAANA YA YERIKO.

Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.

Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)

FAHAMU MAISHA YA YESU KABLA YA HUDUMA.

Rudi nyumbani

Print this post

Machukizo ni nini?

Machukizo au Chukizo ni nini? kama tunavyosoma katika biblia?


Machukizo linatokana na neno “chukizo” na chukizo ni kitu kinachosababisha chuki/hasira. Kwa Mungu kitu chochote kinachoipandisha ghadhabu yake kinaitwa “chukizo”.

Na vitu vifuatavyo ndivyo vilivyokuwa machukizo kwa MUNGU.

   1. Ibada ya Sanamu.

Sanamu ya aina yoyote ile ilikuwa ni machukizo kwa Mungu na hicho ndicho kitu cha kwanza kilichokuwa kinaletea wivu kwa Mungu.

Kumbukumbu 27:15 “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina”.

Kumbukumbu 32:16 “Wakamtia wivu kwa miungu migeni, Wakamkasirisha kwa machukizo.

17 Walitoa sadaka kwa pepo, si Mungu, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa”.

Soma pia Kumbukumbu 27:15, na 2Wafalme 23:24

   2. Uasherati na ulawiti.

Walawi 18: 22 “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo”.

Soma tena Mambo ya Walawi 20:13

   3. Mavazi yasiyopasa.

Kumbukumbu 22:5 “Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”

Mfano wa mavazi yasiyopasa, ni suruali kwa mwanamke, na nguo mfano wa magauni kwa wanaume.

   4. Sadaka yenye kasoro.

Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya Bwana, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako, yote mawili”.

Kumbukumbu 17:1 “Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng’ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako”.

Na yapo machukizo mengine mengi!.

Lakini pia lipo chukizo moja KUU na KUBWA ambalo litatokea kule YERUSALEMU, ambalo ni CHUKIZO LA UHARIBIFU, linalomhusu Mpinga-kristo.

Kwa upana juu ya CHUKIZO LA UHARIBIFU, basi fungua hapa >>CHUKIZO LA UHARIBIFU

Bwana akubariki.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.

Kemoshi ni nani? (Yeremia 48:46)

Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?

Je! Shetani anao uwezo wa kuumba, kama Mungu?

Rudi nyumbani

Print this post

Kemoshi ni nani? (Yeremia 48:46)

Swali: Huyu Kemoshi alikuwa nani, na nini tunajifunza kutoka kwake?


Jibu: Turejee,

Yeremia 48:46 “Ole wako! Ee Moabu, Watu wa Kemoshi wamepotea; Maana wana wako wamechukuliwa mateka, Na binti zako wamekwenda utumwani”.

“kemoshi” hakuwa mtu bali alikuwa ni “mungu” wa watu wa Moabu. Kumbuka kila taifa lilikuwa na mungu wake; Israeli walikuwa na MUNGU wao ambaye ni YEHOVA, Muumba wa mbingu na nchi, Tiro walikuwa na mungu wao anayeitwa “baali”, Sidoni walikuwa na mungu wao anayeitwa “ashtoreti”, wana wa Amoni walikuwa na mungu wao anayeitwa “milkomu”. N.k na hawa wana wa Moabu mungu wao ndio anayekuwa anaitwa “kemoshi” ambaye kiuhalisia ni “pepo”.

Sasa utaona Mungu aliwakataza wana wa Israeli wasiabudu miungu mingine tofauti na yeye…lakini wapo waliotii na wapo waliokaidi na kuamua kuifuata miungu hiyo ya mataifa mengine na kuiabudu na kuisujudia. Na Mfalme Sulemani alikuwa miongoni mwa waliokengeuka dakika za mwisho kwa kuifuata miungu hiyo ya mataifa, ingawa baadaye alikuja kutubu.

2Wafalme 23:13 “Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, MFALME WA ISRAELI, KWA ASHTORETHI, CHUKIZO LA WASIDONI, NA KEMOSHI, CHUKIZO LA MOABU, NA MILKOMU, CHUKIZO LA WANA WA AMONI, mfalme akapanajisi”.

Hii miungu hata leo inaabudiwa katika sehemu mbalimbali ikiwemo Africa, isipokuwa katika majina mengine tofauti na hayo.

Mila nyingi za kiafrica asili yake ni miungu hii, kwamfano mungu wa wasidoni aliyeitwa Ashtorethi alikuwa ni mtu wenye kuchongwa maumbile ya mtu, na kusujudiwa, na kufanyiwa matambiko..na sasa jamii nyingi na makabila mengi (ikiwemo na wakristo) wanafanya hayo hayo wanapokutanika katika vijiji vyao, pasipo kujua kuwa ni ibada za sanamu kama zile zile tu ambazo mataifa wasiomjua Mungu walikuwa wanazifanya.

Bwana atusaidie tuepukane na ibada hizo za sanamu.

Mistari mingine inayomtaja huyo mungu “kemoshi” ni pamoja na Hesabu 21:9, Waamuzi 11:24, 1Wafalme 11:7, 1Wafalme 11:33, Yeremia 48:7, na Yeremia 48:13.

Maran atha.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Moabu ni nchi gani kwasasa?

CHUKIZO LA UHARIBIFU

UNAMFAHAMU MUNGU WA KWELI?

MNGOJEE BWANA

USIJITUMAINISHE JUU YA SIRA YAKO ANGALI UPO KATIKA DHAMBI.

Rudi nyumbani

Print this post

Antiokia ni wapi kwasasa?

Antiokia ipo nchi gani kwa sasa? Na nini tunaweza kujifunza kupitia mji huo?


Jibu: Antiokia ni mji uliopo kusini mwa Taifa la UTURUKI na Kaskazini mwa Taifa la SIRIA.

Mji huu una historia kubwa sana ya kanisa, kwani ndicho kitovu cha jina “Ukristo”. Maandiko yanasema Wanafunzi (yaani watu waliomwamini YESU na kumfuata) waliitwa “wakristo” kwanza hapo Antiokia na si Yerusalemu kanisa lilipoanzia.

Matendo 11:26  “hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. NA WANAFUNZI WALIITWA WAKRISTO KWANZA HAPO ANTIOKIA.

27  Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia”.

Antiokia ni mji uliomiminiwa uliokuwa na Neema ya Ukristo kuliko miji mingi, lililojaa Mitume, manabii na waalimu.. kwani hata Mtume Paulo safari yake ya kuanza kuhubiri injili ilianzia pale.

Matendo 13:1 “Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli.

2  Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.

3  Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

4  Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro”.

Matendo 14:26 “Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza”.

Mji wa Antiokia kwasasa umejaa wa Islamu kutokana na Taifa hilo la Uturuki kuwa la kiislamu, ingawa kuna asilimia ndogo ya wakristo wanaoishi humo. Mahali ambapo uamsho mkubwa wa injili ulianzia sasa adui kapateka na kupafanya kuwa mji wa kipagani… Na miji mingine imenyanyuka yenye uamsho kuliko huo, sawasawa na Neno lile..

Marko 10:31 “Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza”

Hivyo hiyo ni tahadhari hata kwetu, “Tushike tulicho nacho, mpaka mwisho adui asije akatupokonya taji yetu”.

Mji wa Antiokia mwaka 2023, Februari 6 kulitokea tetemeko kubwa sana lililoua watu elfu 55, na kuharibu makazi mengi sana.

Bwana atusaidie tuwe na mwisho mwema.

Shalom.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Yerusalemu ni nini?

Ninawi ni nchi gani kwasasa?

MJI WENYE MISINGI.

Babeli ni nchi gani kwasasa?

DANIELI: Mlango wa 8

Rudi nyumbani

Print this post

JE WEWE NI ALAMOTHI?..BASI TIMIZA YAFUATAYO!

Masomo maalumu yahusuyo (Wanawake na mabinti).


Alamothi ni nini? Na nini ufunuo wake? (1Nyakati 15:20)

Jibu: Tusome,

1Nyakati 15:19 “Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu;

20 na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya SAUTI YA ALAMOTHI”

“Alamothi” maana yake ni “wanawake vijana”… Hivyo hapo anaposema vinanda vya sauti ya Alamothi, maana yake ni vinanda vya sauti za “wanawake vijana”.

Hiki ni kipindi ambacho Mfalme Daudi alikuwa analitoa sanduku la Agano la Bwana kutoka nyumbani kwa Ben-edomu na kulipandisha Yerusalemu.

Na wakati wanalipandisha Daudi aliwaandaa wana wa Asafu (watu walio hodari wa kuimba) wenye matoazi pamoja na kundi lingine la watu nane (8) viongozi wa sifa, wenye vinanda vitakavyotoa sauti kuwafuatiliza wanawake vijana waimbaji (Alamothi).

Ni nini tunajifunza?

Kikubwa tunachoweza kujifunza ni jinsi “wanawake walivyo na nafasi kubwa katika kumwimbia Mungu”. Daudi aliona, wana wa Asafu pekee haitoshi (ambao ni wanaume) …..zinahitajika pia sauti za wanawake vijana, katika kumwimbia Mungu. Na utaona jambo hilo Mungu alilikubali sana na likawa Baraka sana kwa Mfalme Daudi.

Na Mungu ni yule yule hajabadilika, kama alizikubali sifa za Daudi na kundi lake, atafanya hivyo hata leo, ikiwa tutasimama vyema katika nafasi zetu.

Ikiwa wewe ni mwanamke au binti.. fahamu kuwa sauti yako ni ya thamani sana katika kumwimbia Mungu, (ndio maana si nzito kama ya mwanaume). Hivyo chukua nafasi hiyo katika kulitimiza kusudi la Mungu ndani yako. Tafuta namna yoyote umwimbie Mungu na Bwana atakubariki.

Zaburi ya 46 ambayo iliandikwa na wana wa Kora, ni Zaburi maalumu kwa ALAMOTHI. Ni nyimbo iliyokusudiwa iimbwe na Maalamothi, yenye kumtukuza Mungu kuhubiri uweza wake.

Zaburi 46:1 “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.

3 Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.

4 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.

5 Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema.

6 Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki; Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.

7 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.

8 Njoni myatazame matendo ya Bwana, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.

9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.

10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.

11 Bwana wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu”

Bwana akubariki.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE

Kwanini wajane vijana hawakupaswa kuandikwa?

Ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda.

TATIZO LA NDANI LINALOWASUMBUA VIJANA, WALIOOKOKA.

Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza Naam, wanne walio na mwendo mzuri.

Rudi nyumbani

Print this post

Mgawanyo wa Vitabu vya Biblia

AGANO LA KALE

Vitabu vya Agano la Kale vimegawanyika katika makundi makuu manne (4)

      1. VITABU VYA SHERIA. (Tazama jedwali chini).

JINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGO/SURAMAJIRA YA UANDISHI
1.MWANZOMUSA50Jangwani
2.KUTOKAMUSA40Jangwani
3.MAMBO YA WALAWIMUSA27Jangwani
4.HESABUMUSA36Jangwani
5.KUMBUKUMBU LA TORATIMUSA34Jangwani

     2. VITABU VYA HISTORIA (Tazama Jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.YOSHUAYoshua24Kaanani
2.WAAMUZINabii Samweli21Israeli
3.RUTHUNabii Samweli4Israeli
4.1SAMWELINabii Samweli31Israeli
5.2SAMWELIEzra (Mwandishi)24Israeli
6.1WAFALMEYeremia (Nabii)22Israeli
7.2WAFALMEYeremia (Nabii)25Israeli
8.1NYAKATIEzra (Mwandishi)29Uajemi
9.2NYAKATIEzra (Mwandishi)36Uajemi
10.EZRAEzra (Mwandishi)10Israeli
11.NEHEMIANehemia13Israeli
12.ESTAMordekari10Shushani Ngomeni(Uajemi)

     3. VITABU VYA MASHAIRI (Tazama Jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.AYUBUMusa42Jangawani
2.ZABURI Daudi, Sulemani, Wana wa Asafu,Ethani, Hemani, Musa, wana wa Kora na wengine wasiotambulika.150Israeli
3.MITHALISulemani31Yerusalemu (Israeli)
4.MHUBIRISulemani12Yerusalemu (Israeli)
5.WIMBO ULIO BORASulemani8Yerusalemu (Israeli)

    4. VITABU VYA MANABII WAKUBWA (Tazama Jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.ISAYAIsaya (Nabii)66Israeli
2.YEREMIAYeremia (Nabii)52Israelil (Yerusalemu)
3.MAOMBOLEZOYeremia (Nabii)5Misri
4.EZEKIELIEzekieli (Nabii)48Babeli
5.DANIELIDanieli (Nabii)12Babeli

     5. VITABU VYA MANABII WADOGO (Tazama jedwali chini).

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.HOSEAHosea (Nabii)14israeli
2.YOELIYoeli (Nabii)3israeli
3.AMOSIAmosi (Nabii)9israeli
4.OBADIAObadia (Nabii)1israeli
5.YONA Yona (Nabii)4israeli
6.MIKAMika (Nabii)7israeli
7.NAHUMUNahumu (Nabii)3israeli
8.HABAKUKIHabakuki (Nabii)3israeli
9.SEFANIASefania (Nabii)3israeli
10.HAGAIHagai (Nabii)2israeli
11.ZEKARIAZekaria (Nabii)14israeli
12.MALAKIMalaki (Nabii)4israeli

         AGANO JIPYA

Vitabu vya Agano jipya vimegawanyika katika makundi makuu matano (5)

    1. VITABU VYA INJILI (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.MATHAYOMathayo (Mtume)28Antiokia (Siria)
2.MARKOMarko (Mwanafunzi)16Rumi au Siria
3.LUKA Luka (Mwanafunzi na, Tabibu)24Antiokia (Siria)
4.YOHANAYohana(Mtume, mwana wa Zebedayo)21Efeso (Uturuki)

   2. KITABU CHA HISTORIA (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.Matendo ya MitumeLuka (Mwanafunzi na Tabibu)28Rumi

   3. VITABU VYA NYARAKA ZA PAULO MTUME (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA SURAMAHALI KILIPOANDIKWA
1.WARUMIPaulo (Mtume)16Korintho (Ugiriki)
2.1WAKORINTHOPaulo (Mtume)16Efeso (Uturuki)
3.2WAKORINTHOPaulo (Mtume)13Makedonia (Ugiriki)
4.WAGALATIAPaulo (Mtume)6Efeso (Uturuki)
5.WAEFESOPaulo (Mtume)6Gereza
6.WAFILIPIPaulo (Mtume)4Gereza
7.WAKOLOSAIPaulo (Mtume)4Gereza
8.1WATHESALONIKEPaulo (Mtume)5Korintho (Ugiriki)
9.2WATHESALONIKEPaulo (Mtume)3Korintho (Ugiriki)
10.1TIMOTHEOPaulo (Mtume)6Makedonia (Ugiriki)
11.2TIMOTHEOPaulo (Mtume)4Rumi (Kifungoni)
12.TITOPaulo (Mtume)3Ugiriki
13.FILEMONIPaulo (Mtume)1Rumi (kufungoni)
14.WAEBRANIAinaaminika kuwa ni Paulo (Mtume)13Rumi

   4. VITABU VYA NYARAKA KWA WATU WOTE (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKWA
1.YAKOBOYakobo (Ndugu yake Bwana YESU)5Haijulikani
2.1PETROPetro (Mtume)5Babeli
3.2PETROPetro (Mtume)3Haijulikani
4.1YOHANAYohana (Mtume)5Inaaminika Efeso
5.2YOHANAYohana (Mtume)1Efeso
6.3YOHANAYohana (Mtume)1Haijulikani lakini inasadikika Efeso
7.YUDAYuda (Ndugu yake Bwana YESU)1Haijulikani

   5. KITABU CHA UNABII (Tazama jedwali chini)

N/AJINA LA KITABUMWANDISHIIDADI YA MILANGOMAHALI KILIPOANDIKIWA
1.UFUNUO WA YOHANAYohana (Mtume, mwana wa Zebedayo)22Patmo (kisiwani)

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MAJINA YA MANABII WANAWAKE

MANABII WA BIBLIA (Wanaume)

VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 13 (Kitabu cha Hosea).

MAJINA YA MITUME WA BWANA YESU

Rudi nyumbani

Print this post

Je ni Mungu au Malaika?

Swali: Je biblia inajichanganya katika Zaburi 8:4-5 na Waebrania 2:6-7. Maana sehemu moja inataja ‘Mungu’, na sehemu nyingine ‘Malaika’.


Jibu: Turejee.

Zaburi 8:4 “Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?

5 Umemfanya mdogo punde KULIKO MUNGU; Umemvika taji ya utukufu na heshima”.

Tusome tena Waebrania 2:6-7..

Waebrania 2:6 “Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie?

7  Umemfanya mdogo punde kuliko MALAIKA, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako”.

Katika Waebrania mwandishi ana nukuu maneno kutoka katika Zaburi, lakini ni kama ana nukuu kitu tofauti na kilichoandikwa kule, kwamaana yeye anataja Malaika na wakati mwandishi wa Zaburi alitaja Mungu.. Sasa swali biblia inajichanganya?.

Jibu ni La! Biblia haijichanganyi wala haijakosewa.. Isipokuwa fahamu zetu na pambanuzi zetu ndizo zinazojichanganya.

Sasa ili tuelewe ni vizuri kuzielewa kwanza lugha za kibiblia..

Si kila mahali panapotajwa Mungu, panamaanisha Mungu-muumba, La! Sehemu nyingine panamaanisha Ufalme wa Mungu (yaani jeshi la Mbinguni yaani Malaika na vyote vilivyopo kule)…Na sehemu mojawapo ambayo iliyotajwa Mungu ikimaanisha Jeshi la Mbinguni ni hii Zaburi 8:5 “…Umemfanya mdogo punde KULIKO MUNGU”.

Mungu inayotajwa hapo inamaanisha Ufalme wa Mungu (yaani jeshi la Malaika) na si MUNGU aliye Muumbaji, ambaye ni MMOJA.

Ni sawa na jina ISRAELI katika biblia,…kuna mahali linamaanisha mtu mmoja (ambaye ni Yakobo mwana wa Isaka, Mwanzo 35:10).. Lakini pia jina hili kuna mahali linamaanisha TAIFA (Ufalme, Kutoka 5:2).

Au “Yuda”, kuna mahali anatajwa kama Mtu (Mwana wa Yakobo), lakini pia kama Taifa.

Vivyo hivyo na Mungu, cheo hicho kinaweza kufunua “Ufalme” au nafasi ya MUNGU MWENYEWE kama Muumba.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba mwandishi wa kitabu cha Waebrania hajapishana na mwandishi wa Zaburi.

Kujua kwa mapana ni ufunuo uliopo nyuma ya andiko hili.. “Amefanyika bora kuliko Malaika” basi fungua hapa >>>AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

Bwana akubariki.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Ielewe kwa kina Waebrania 13:5 maana yake.

MUNGU MWENYE HAKI.

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.

JE! UNA MHESHIMU MUNGU?

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?

Rudi nyumbani

Print this post

Mbaruti ni mmea gani? (Mathayo 7:16)

Mbaruti ni nini?.(Mibaruti ni mimea ya aina gani) na umebeba ujumbe gani kiroho?.


Jibu: Turejee,

Mathayo 7:16 “Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?”

Soma pia 2Wafalme 14:9, 2Nyakati 25:18 na Hosea 10:4.

Mbaruti/Mibaruti ni jamii ya mimea yenye maua, ambayo mara nyingi inajiotea maporini. (Mimea hii inatoa matunda ambayo ina miiba inayoizunguka pande zote, kuifanya kutolika na wanyama walao nyasi). Tazama picha juu..

Katika biblia Bwana YESU alinukuu mimea huu wa mbaruti katika swali lililowahusu manabii wa uongo.. Aliuliza je watu huchuma tini katika mibaruti?,.. Maana yake ni jambo lisilowezekana kupata matunda ya “Tini“ kutoka katika jamii ya mimea hiyo ya maua ya mibaruti.

Vile vile akasema haiwezekani kuchuma zabibu kutoka kwenye miti ya miiba…

Kuonyesha kuwa Manabii wa uongo wanatoa matunda yenye MIIBA MIIBA!!.yasiyofaa kwa kuliwa bali yanaumiza na kuchoma!.

Moja ya matunda wanayotoa ni tamaa za fedha, (wakizitamani na kuwafundisha watu hizo)..ambazo biblia inasema wanaozama huko wanajichoma kwa maumivu mengi..

1Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”.

Manabii wa uongo kamwe hawahubiri wala kufundisha Toba na Utakatifu, wala safari ya kwenda mbinguni hawaihubiri kwasababu huko hawaendi!.na wao si wasafiri wa kwenda huko, hivyo mioyo yao ipo hapa hapa duniani na wanahubiri vitu vya duniani, pasipo kuweka mambo katika uwiano.

Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.

16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?

17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.

19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 7.20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua”

Bwana atusaidie.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NI SAHIHI KABISA, HUU SI WAKATI WA TINI!

SHAMBA HUWA HALIMTAMBUI WALA KUMSUBIRIA MKULIMA.

UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?

Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?

USIPOTEZWE NA MANENO YA MANABII WA UONGO.

Rudi nyumbani

Print this post