Title August 2020

Nini maana ya “wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto”?

SWALI: Biblia inaposema “Na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto” Ina maana gani? (Yuda 1:22).


JIBU: Ukisoma kitabu chote cha Yuda kwa utulivu ambacho ni sura 1 tu, utaona maudhui kubwa iliyoandikwa pale ilikuwa ni kulionya kanisa juu ya kuishindania Imani ambayo walikabidhiwa mara moja tu, (soma binafsi kwa utaratibu utaliona hilo), Na hiyo ni kutokana na kuwa tangu ule wakati  kulizukua wimbi kubwa la manabii wa uongo, ambao walifananishwa na Kora na Balaamu, Pamoja wa watu waovu, mfano wa Sodoma na Gomora na watu wasio na imani (aliowaitwa makafiri), waliojiingiza kwa siri katikati ya kanisa la Mungu, ambao kazi yao ilikuwa ni kuleta  matengano ndani ya kanisa.

Hivyo mtume Yuda alilionya sana kanisa kuhusu watu hawa, na ndipo mwishoni kabisa katika waraka wake akalisihi kanisa, kila mmoja kwa nafasi yake, afanye kazi ya kuwarejesha wengine katika Imani kwa bidii, na ndio hapo akasema..

Yuda 1:22  “Wahurumieni wengine walio na shaka,

23  na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto; na wengine wahurumieni kwa hofu, mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”.

Unaona jambo la kwanza aliwaambia wawahurumie walio katika shaka: Maana yake ni kwamba kuna wapo watu ambao walishaathiriwa na mafundisho ya watu hao waongo, mpaka wakawa na mashaka na Imani, Hivyo watu kama hao aliwasihi, wawahubirie kwa kuwajengea misingi ya Imani tena, ili wasimame, na wasiyumbishwe na uongo unaozagaa huko.

Lakini pia akawaambia..

“na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto”. Hii ikiwa na maana kuwa wapo wengine ambao walikuwa tayari wameshazama kabisa katika udanganyifu wao wa mauti, ni kama vile unamuona mtu ambaye yupo motoni, wewe unadhani njia rahisi kumtoa pale itakuwa ni ipi? Ni wazi kuwa haitakuwa ya kumsihi, au kumwomba, hapana, utatumia maneno ya nguvu na vitendo, kwa kumnyakua kutoka kule motoni ili tu apone kwanza,

Ndivyo ilivyo katika kuwahubiria watu wengine ambao wameshakuwa sugu wa Habari za wokovu (Shetani ameshawapofusha macho), Inapofikia wakati kama huo, injili za upendo na huruma za Kristo hazitawafaa, bali injili za hukumu na ziwa la moto, na mateso ya milele, na dhiki kuu, zinazowangoja watu waovu, ndizo zitakazowatafakarisha Zaidi na kuwageuza.

Kuna watu wanasema, hatupaswi kuhubiri Habari za dhiki kuu, na jehanum ya moto kufanya hivyo ni kuwatisha watu, hivyo inawafanya wawe waoga, wampokee Yesu kwa sababu wanaogopa kwenda kuzimu na sio kwasababu wanampenda.

Ndugu, Ni heri aokoke kwa hofu ya Jehanum, kuliko, upotelee huko milele. Na huko ndiko kuwaokoa wengine kwa kuwanyakua kutoka moto, sio kwa kuwahubiria maneno ya kuwapendezesha, bali kuwaonya na hatari watakayoikuta mbeleni..Na hata hivyo sio uongo, bali ni kweli ndivyo ilivyo kwa watu wote ambao hawatatubu.

Kama biblia inavyosema.

2Wakorintho 5:10 “ Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.

11 BASI TUKIIJUA HOFU YA BWANA, TWAWAVUTA WANADAMU; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia”

Ni kweli kabisa yapo makundi yanayostahili kufundishwa sana juu ya Upendo wa Kristo, kwa mfano watu waliokata tamaa ya Maisha, au mtu aliye katika dhiki na mateso na vifungo vya shetani, au mtu ambaye hamjui Mungu kabisa, au mwenye shauku ya kumjua Mungu, lakini hajui ni wapi pa kuanzia,..Hawa wanastahili injili za Upendo wa Mungu..Ndizo zitakazowafungua na kuwapeleka viwango vingine..

Mathayo 11.28  “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29  Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30  kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Lakini lipo kundi lingine ambalo, limeshahubiriwa, na linafahamu kila kitu, lakini bado lipo katika dhambi, pengine ili kuliokoa (kulinyakua kutoka huko liliko) injili inayolifaa ni ile ya Ziwa la Moto wa milele, Na bado tutaendelea kuzihitaji kwa wakati huu wa siku za mwisho.

Ubarikiwe.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312


Mada Nyinginezo:

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

HATARI YA KUHUBIRI INJILI TOFAUTI NA ILIYOANDIKWA KWENYE BIBLIA.

JE KIFO NI NINI? NA JE KUNA AINA NGAPI ZA VIFO?

JE NI LAZIMA MKRISTO AOE/AOLEWE?

KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUOTA UPO KANISANI.

Kuota upo kanisani inamaanisha nini kimaandiko?


Hiyo ni ndoto njema itakayo kwa Mungu. Kamwe shetani hawezi kukuotesha ndoto ya namna hiyo..

Kama umeota ndoto hii kuna mawili. La kwanza ikiwa wewe ni mkristo uliyeokoka na umesimama imara, Hapo ni Mungu anakuonyesha kuwa upo katika njia sahihi, hivyo endelea kumtafuta Bwana kwa bidii Zaidi kwasababu Upo uweponi mwake..Daudi alisema..

Zaburi 122:1 “Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana”.

Kwasababu huko ndipo Mungu alipo. Kanisani na nyumbani mwa Bwana, kwahiyo ukiota upo kanisani ni ishara kuwa inaishi kwa Mungu.

Lakini ikiwa umeiota ndoto hii upo kanisani, na huku nyuma unajijua kabisa hauna mahusiano yoyote na Mungu, au hata kanisani huendi, Maisha yako ni ya dhambi..

Basi ujue hiyo ni sauti ya Mungu, anayokuvuta kwake,..Anakuonyesha kuwa hapo ndipo unapopaswa uwepo, hapo ndipo nyumbani kwako.. Wewe sio wa ulimwengu huu.

Hivyo itii sauti ya Mungu, mgeukie yeye, kwasababu huwezi jua ni kwanini afanye hivyo kwako leo… Kumbuka duniani hapa sisi ni wapitaji pengine kesho inayodhani itakuwepo inaweza isiwe yako.

Hivyo fanya uamuzi haraka wa kutubu dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuucha ulimwengu moja kwa moja, na ukifanya hivyo YESU atakusamehe, Fahamu hiyo ndoto inatoka kwa kwa Mungu kabisa hivyo usiipuuzie. Mungu huwa anazungumza na watu wakati mwingine hata Zaidi ya mara moja.

Ayubu 33: 14 “Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

15 Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani”;

Pengine Mungu alishazungumza na wewe kwa njia mbalimbali utubu dhambi zako umgeukie. Leo hii usiifanye shingo yako kuwa ngumu.

Kama upo tayari kuokoka na kuanza Maisha mapya na Yesu Kristo basi huo utakuwa ni uamuzi wa busara sana kwako..Unaweza kusema mimi mboni ni muislamu, haijalishi wewe ni nani, Mungu anakuita, kwasababu amekuchagua wewe na anakupenda, na anataka kukuokoa upate uzima wa milele..Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa  Sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na hayo mengine yaliyosalia Bwana atakusaidia kuyashinda.

Group la whatsapp Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

KUOTA UPO UCHI.

Hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge.(Ufu 21:27)

FAHAMU TAFSIRI ZA NDOTO MBALIMBALI.

Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?

Rudi Nyumbani:

Print this post

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

Hili ni moja ya swali lenye mtafaruku mkubwa sana miongoni mwa wakristo, na wengi hata wameishia mpaka kugombana kabisa!..Wapo wanaoamini kanisa litapitia dhiki kuu ndipo linyakuliwe na wapo wanaoamini kanisa halitapita dhiki kuu, yaani utaanza kwanza unyakuo ndipo dhiki kuu ifuate.

Kuna kitu kimoja cha kimaandiko ambacho hakijulikani na wengi..nacho ni Mgawanyiko wa ujio wa Kristo;

Ujio huu umegawanyika katika vipengele vikuu 3, mtu akishindwa kuvielewa vipengele hivi basi biblia itamchanganya. Na vipengele hivyo ni kama ifuatavyo.

  1. UJIO WA KWANZA WA KRISTO:

Huu ni ule wakati Kristo alipozaliwa na Bikira Mariamu, na kuishi kwa miaka 33 na nusu na kisha kufa, na kufufuka na kupaa mbinguni alikotoka.

  1. UJIO WA PILI:

Huu utahusisha Kristo kuwapokea wateule wake mawinguni katika tendo maarufu lijulikanalo kama unyakuo. Wakati huo, wafu waliopo makaburini watafufuka wataungana na watakatifu walio hai na kwa pamoja watakwenda mawinguni kumlaki Bwana. Katika Ujio huu Kristo hatashuka duniani, atabaki mawinguni, watakaonyakuliwa ndio watakaokwenda mawinguni kumfuata na kwenda naye mbinguni kwenye makao waliyoandaliwa.

Katika hatua hii ndio litatimia lile neno.. la kwenye Luka 17:34

“Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 

35 Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. 

36 Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa”.

Vilevile lile Neno “atakuja kama mwivi usiku”, ndio litatimia katika hatua hii..Pengine utakuwa umelala na mume wako/mke wako aliyeokoka  na ghafla! utapoamka asubuhi hutamkuta kitandani. n.k. 

Huu hautakuwa ujio wa kila jicho kumwona Yesu, kwasababu hatakuja kwa hukumu bali kwa ajili ya kuwachukua wateule wake na kwenda nao mbinguni kwenye karamu aliyowaandalia, ili kuwaepusha na dhiki ambayo itakwenda kuanza duniani muda sio mrefu. Dhiki ambayo inajulikana kwa jina lingine kama saa ya kuharibiwa ulimwengu!.

Ufunuo 3:10 “Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi”.

Sasa huo sio wakati wa kila jicho kumwona Yesu mawinguni, wakati wa kila jicho kumwona utakuwa ni wakati wa ujio wa tatu, ambao tutauona mbele kidogo.

Sasa kabla ya kwenda hatua ya mwisho ya Ujio wa tatu, hebu tujiulize maswali machache juu ya huu ujio wa pili.

  • Hebu jiulize kama Ujio huu wa pili wa Kristo (yaani unyakuo wa kanisa) utahusisha kila jicho kumwona Yesu, vipi kuhusu hao waliolala vitandani wakati wa kuja kwake?..Je wakati wa kuja kwake, watazinduka usingizini na kumwona Bwana mawinguni?..kama ndivyo basi sentensi hii itakuwa haina maana>> “wawili watakuwa wamelala mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa”. 

Na wakati wa kila jicho kumwona Kristo, biblia inasema Mataifa yote wataomboleza..na milima itahama na visiwa, kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi, na jua litazima na mwezi utakuwa mwekundu kama damu. Kwa ufupi mwisho wa dunia utakuwa umefika..Sasa kama mambo hayo yote yatatokea katika siku ile ya unyakuo, ni nani atakuwa amelala kitandani, au yupo shambani analima, katikati ya dhiki kubwa namna hiyo, huyo mpinga-Kristo atatokea wapi na atawapa watu chapa muda gani?.. 

Kwahiyo ni wazi kuwa siku ya unyakuo ni nyingine na siku ya Ujio wa Kristo ambao kila jicho litamwona nayo ni nyingine. Haiwezekani siku ya unyakuo ndio iwe siku hiyo hiyo ya kila jicho kumwona, na visiwa na milima kuhama.

Sasa twende hatua ya mwisho ya tatu.

UJIO WA TATU:

Baada ya unyakuo kupita katika ujio wa pili, baadhi ya watu watatoweka, na dunia haitaelewa chochote, wengi watahisi watu wamepotea tu, kama ilivyo kawaida ya watu kupotea potea na kupatikana, na wengine wengi watajua ni habari za kuzusha tu!..taarifa chache zitafika vituoni, lakini mwisho zitaishia kupuuziwa… Kama baadhi ya taarifa za watu kupotea zinavyopuuzwa leo. Pasipo kujua kuwa Kristo tayari kashalinyakua kanisa lake (kundi dogo). Na siku hiyo hakutakuwa na ishara yoyote angani, wala jua halitazima..kutakuwa na ukimya tu kama wa siku zote.

Sasa katikati ya hicho kipindi, ndio utakuwa wakati wa mpinga-kristo kunyanyuka…Ndani ya miaka mitatu na nusu ya kwanza (yaani miezi 42), utakuwa ni wakati wa mpinga-kristo kuwadanganya watu waipokee chapa yake..wengi wataipokea chapa pasipo kujua, wakidhani ni mfumo mpya tu! Wa kimaendeleo umezuka, ambao utasaidia watu kutambulika kirahisi..Utakubalika duniani kwa muda mfupi sana, kiasi kwamba mtu atakayeukataa atakuwa anaenda kinyume na serikali, hivyo atatafutwa na kusingiziwa mambo yasiyofaa.

 Wachache sana wataipokea kwa kujua, kwa kujua kabisa kwamba hii ni chapa, lakini wengi hawatajua..kwasababu mpinga-kristo hatakuwa mtu mwenye mapembe kama watu wanavyofikiri, bali atakuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana wa kisiasa, kidini, kiuchumi na kijeshi, na anatakua ni mtu anayeshika biblia!. Hivyo hatajulikana na wengi kuwa ndiye mpinga-kristo mwenyewe, kwasababu ataheshimika kama kiongozi wa dini, atakayeleta amani..hivyo atapewa nguvu na dunia nzima.

Baada ya miaka mitatu na nusu  ya kwanza kuisha, wale wachache ambao wataikataa chapa  yake hiyo ndio watakaoanza kuipitia DHIKI KUU, wengine hawataguswa!..wataendelea na shughuli zao za KUUZA NA KUNUNUA bila usumbufu!…Lakini walioikataa  watajaribu kujificha lakini watakamatwa na kupewa shutuma za uongo na hivyo kukusanywa katika magereza maalumu ya mateso…wakiwa humo watateswa mateso ambayo hayajawahi kutokea tangu dunia kuumbwa…na watamani kufa lakini wale waliowafunga hawatawaua mapema!!…

Lakini mwisho wa siku watakufa wote….na karibia na mwisho  ya hiyo miaka mitatu na nusu ya mwisho, wataisha wote…Ndipo Mungu ataanza kuwapiga wanadamu wote waliopokea hiyo chapa ya mnyama kwa yale mapigo ya VITASA SABA, tunayoyasoma katika ufunuo 16. Kwahiyo DHIKI KUU, itaongezewa juu yake vitasa saba..Na Mwisho kabisa, miaka hiyo ya dhiki na vitasa itakapoisha, biblia inasema Jua litatiwa giza, na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, Ishara ya mwana wa Adamu itaanza kuonekana mbinguni..

Bwana Yesu mwenyewe Mfalme wa wafalme  atatokea mawinguni pamoja na jeshi kubwa na watakatifu walionyakuliwa…Atashuka kwa ajili ya vita vya Harmagedoni, na kwaajili ya utawala wa miaka elfu duniani.

Sasa siku hii kwa wale wachache ambao watakuwa wamesalia duniani, ambao waliipokea chapa lakini hawakufa katika mapigo ya vitasa saba..Wataona umeme ukimulika kutoka mashariki hata magharibi!..na dunia yote itakuwa giza ghafla (jua litazimwa)!…Na watamwona Kristo mawinguni, uso wake uking’aa kuliko jua…Hofu kuu itawaangukia wataomboleza kwa hofu, biblia inasema watatamani milima iwaangukie..

Mathayo 24:29 “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 

30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi 

31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.”.

Soma tena…

Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; JUA LIKAWA JEUSI KAMA GUNIA LA SINGA, MWEZI WOTE UKAWA KAMA DAMU, 

13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 

14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 

15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 

16 WAKIIAMBIA MILIMA NA MIAMBA, TUANGUKIENI, TUSITIRINI, MBELE ZA USO WAKE YEYE AKETIYE JUU YA KITI CHA ENZI, NA HASIRA YA MWANA-KONDOO. 

17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.

Sasa utauliza hao wateule ambao Bwana atawakusanya wakati wa kutokea mawinguni kwa utukufu mwingi ni wakina nani?

Hao watakuwa ni Wayahudi 144,000, waliotiwa muhuri wa Mungu baada ya kuisikia ile injili ya manabii wawili wa kwenye Ufunuo 11, hivyo walifichwa mbali na mpinga-kristo na dhiki ya vitasa (Ufunuo 12:14-15). Kundi hili la wayahudi 144,000 ambao walifichwa mbali na yule joka…Ndio wanaoitwa wateule..

Hawa wakati Kristo atakaokuja ndio watakaokusanywa kutoka pepo nne, na kuletwa juu ya mlima Sayuni uliopo pale Israeli..(Ufunuo 14:1 “ Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao”). 

Kwahiyo sio kanisa ambalo litakusanywa kutoka pembe nne, bali ni wayahudi hao 144,000, ambao waliisikia ile injili iliyohubiriwa na wale manabii wawili katika Ufunuo 11, na kutiwa muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao…Kanisa tayari lilikuwa utukufuni, na ndio linalorudi na Kristo hapa!.

Sasa upo utata mmoja maarufu katika Ufunuo 7:9-16..Tusome 

“ 9  Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;

 10  wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo…………………………

13 Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? .

14  Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.

15  Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. 

16  Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote”

Mstari huu ndio unaowafanya wengi wahitimishe kwamba dhiki kuu itaanza ndipo tuende mbinguni…Lakini hebu soma vizuri mstari huo wa 9 unasema “nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi”.

Hapa ni mbinguni baada ya unyakuo…na sio kundi moja la watu Fulani tu! Bali ni la watu wote (sio tu walio hai) bali hata waliokufa katika Kristo katika vizazi vyote vya nyuma, wakina Petro waliokatwa vichwa, wakina Stephano waliopigwa mawe, wakina Perpetua waliopitia dhiki za kuwekwa kwenye maarena na kufunguliwa Wanyama wakali, wakina Polikapi waliochomwa moto, wakina Antipa na wengine wengi na hata wakristo wote wanaopitia dhiki za kiimani hata sasa ambao watakuwa hai mpaka ile siku ya kunyakuliwa….

Sasa wote hawa kwa pamoja ndio wanaolijenga hilo jeshi kubwa hapo juu la Ufunuo 7…Kwahiyo hilo sio kundi moja tu la watu Fulani tu wachache!..bali ni la watu wa vizazi vyote waliokufa katika Kristo(Na mbele za Mungu, ni washindi wa dhiki za ulimwengu, kama Bwana Yesu alivyosema “ulimwenguni mnayo dhiki”). Mbinguni hakutakuwa na makundi mawili; ya waliopitia dhiki na ambao hawajapitia dhiki, ndio maana unaona hapo hakuna makundi mawili, bali kundi moja tu!.

Huo ni ufupisho tu kwa yatakayotokea siku za mwisho…Hivyo kwa hitimisho ni kwamba kanisa halitapitia Dhiki kuu ya mpinga-kristo… “litaepushwa na saa ya kuharibiwa”..watakaopitia dhiki kuu ya mpinga-kristo ni wale watakaoachwa kwenye unyakuo..na watauawa na mpinga-kristo (na hawatakuwa miongoni mwa watakaokwenda mbinguni), wataikosa karamu ya Mungu mbinguni ingawa wakati wa Kristo kurudi na watakatifu, watafufuliwa na kuingia katika utawala wa miaka elfu hapa duniani.

Na siku ya unyakuo sio siku ya kila jicho kumwona Yesu mawinguni, sio siku ya mataifa yote kuomboleza.

Sasa ni kitu gani kinachowafanya watu wachanganyikiwe?

Ni kwasababu ya kutoelewa kalenda ya Neno la Mungu…Ni wachache sana wanalijua na kulielewa andiko la kwenye Warumi 11, linalozungumzia Upofu waliopigwa Wayahudi (yaani waisraeli). Upofu huo walipigwa wasimwamini Masihi, Yesu Kristo ili sisi watu wa mataifa tupate Neema (hebu tenga muda binafsi soma taratibu Warumi 11 yote).

Kutokana na upofu waliopigwa iliwafanya wasimwamini kabisa Yesu, na kujikuta wakimtazamia Masihi mwingine. Na sisi watu wa Mataifa ikawa ni nafasi kwetu kumwamini, kwani wale mitume ambao walipaswa watumwe kwa wayahudi walikuja kwetu na sisi tukamwamini Yesu, macho yetu yakafunguliwa..tukaipokea hiyo neema. Na tumekaa na hiyo neema sasa kwa Zaidi ya miaka 2,000, ndio maana huoni ugumu leo kuhubiri injili ya Yesu na watu wakamwamini kirahisi tu!..Neema hii haipo kwa Waisraeli unaowaona leo!..Ukienda Israeli ukiwaeleza Habari za Yesu, wanakuona ni mwendawazimu…wanakupinga kabisa!..ni wachache sana wanaomwamini, lakini Zaidi ya asilimia 90 ya waisraeli wanamkataa Yesu. Na hiyo ni kutokana na upofu waliopigwa..yaani neema waliyopokonywa ili tupewe sisi.

Lakini biblia inasema katika hiyo hiyo warumi 11…kwamba hawatakuwa katika hiyo hali ya kutomwamini Yesu milele. Itafika siku ambapo macho yao yatafumbuliwa..Siku hiyo itakuwa ni zamu ya watu wa mataifa kupitia ukame wa rohoni kama wanayoipitia sasa waisraeli.

Siku hiyo itakuwa ni siku ya Neema ya wokovu kuondoka kwa watu wa Mataifa milele na kuhamia Israeli. Sasa Neema hiyo itahitimishwa na tukio la unyakuo. Kristo atakapolinyakua tu kanisa lake, na Mlango wa Neema siku hiyo hiyo utakuwa umefungwa kwa watu wa Mataifa na kubakia kwa waisraeli peke yao. Huku hata mtu aombe vipi, hakuna rehema. Roho Mtakatifu atahamia kwa Waisraeli, watahuzunika sana na kujilaumu ilikuwaje kuwaje mpaka wakamkataa Masihi kwa miaka yote hiyo…

Kwa kupitia injili ya wale manabii wawili, ndio watapatikana idadi ile 144,000 (Haijulikani kama ndio namba kamili,  au ni ya kuwakilishi tu, kwamba idadi inaweza kuwa kubwa Zaidi ya hiyo). Lakini hao tu ndio watakaosalimika, ndio wateule,  na watakusanywa katika Mlima Sayuni.

Warumi 11:25  “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili. 

26  Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake. 

27  Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.

Sasa hapa kwenye WAKATI WA MATAIFA na WAKATI WA WAYAHUDI, ndiko kunakowafanya watu washindwe kuuelewa ujio wa Bwana.  Asilimia kubwa ya watu hawajui kuwa kuna wakati wa Wayahudi kurudiwa na kumwamini  mwokozi…wengi wanajua tu! Kuna unyakuo basi!…kwamba baada ya unyakuo hakuna chochote kitakachoendelea, na wanaamini kuwa mbinguni tutakaa huko milele, wala hakuna wakati tutarudi tena huko..Hawajui kwamba kuna utawala wa miaka elfu wa kutawala na Kristo duniani unatungoja. N.k

Tukiyajua hayo..huu sio wakati wa kucheza na Neema tuliyopewa sisi watu wa mataifa hata kidogo…Sasahivi unaweza kusikia injili, ukaikataa kwa mdomo lakini moyoni mwako ukashuhudiwa kwamba ni kweli yanayozungumzwa…Hicho kinachokushuhudia ndani yako ni sauti ya wito wa Mungu (Ni neema ya Mungu bado inatuita)..Itafika kipindi itaondoka kabisa…itahamia Israeli.. na hiyo sauti ya Roho Mtakatifu itakapoondoka..Ndipo mpinga-kristo atafunuliwa.

2Wathesalonike 2:7  “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. 

8  Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake”

Bwana atubariki.                  

Group la whatsapp Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako au Whatsapp tutumie ujumbe kwenye box la maoni chini au piga namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

MAJONZI YA MTUME PAULO KWA NDUGU ZAKE.

YONA: Mlango wa 3

NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.

Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?

YAKINI NA BOAZI.

NEEMA YA MZALIWA WA PILI.

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

JINSI SODOMA NA GOMORA ILIVYOKUWA INAVUTIA SANA..

Rudi Nyumbani:

Print this post

KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

Kuota umechomwa kisu au Kuota umepigwa risasi kuna maanisha nini?


Awali, ni vyema kujua kuwa si kila ndoto aotayo mtu, ina maana katika maisha yake, Hilo ni vizuri ukalifahamu, Ndoto nyingi tunazoziota kila siku zinatokana na shughuli zetu za kila siku (Mhubiri 5:3), au mazingira yanayotuzunguka, au mambo ambayo tunayawaza mara kwa mara, au  tulishawahi kuyaona, au kuyapitia sehemu Fulani katika maisha yetu (Isaya 29:8)..

Naweza kusema asilimia 90 ya ndoto tunazoziota kila siku zinaangukia katika kundi hili,.Hapo ndipo watu wengi wanaposhindwa kuelewa, wanataka kila ndoto wapate tafsiri ya rohoni, au maishani, hilo jambo halipo, utaishia kudanganywa, au kujidanganya mwenyewe, Kumbuka kinachoweza kueleza hatma ya maisha yetu kwa ufasaha wote, sio ndoto tunazoziota usingizini, bali Neno la Mungu tunaloliishi kila siku.

Mungu anaziita ndoto kama makapi ukifananisha na Neno lake(Yeremia 23:28-29). Akiwa na maana kuwa mtu Yule anayeishi kwa kulishika Neno lake, Ni bora kama ngano, kuliko yule anayetafuta maana za ndoto zilizofananishwa na makapi.

Ni mara chache, ndoto zinabeba ujumbe, ili kutambua ndoto yako inatoka kwa Mungu au kwa shetani, au kwako mwenyewe, basi fungua hapa usome kwanza>>> Nitajuaje kama ndoto ni ya Mungu au ya Shetani?

KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

Hivyo ukiwa umeshasoma, na unao uhakika kabisa kuwa ndoto uliyoota, si ya kawaida, imekujia kwa uzito mwingine wa kitofauti, imekushtua sana, imeonekana kama ni jambo la halisi kabisa, basi upo ujumbe wa rohoni.

Sasa kwa namna ya kawaida, ukishaona mpaka mtu amefikia hatua ya kukuchoma kisu, au amekupiga risasi ni wazi kuwa kuna jambo ulilifanya, au unalifanya sasa hivi, ambalo  limemchukiza sana, kiasi cha kufikia  uamuzi wa kuona kufa kwako ni bora kuliko kuishi.

Vivyo hivyo katika ndoto ukiona umepigwa risasi, au umechomwa kisu, au upanga, au mkuki,au kitu chenye ncha kali, hiyo  ni ishara kuwa maishani mwako, lipo jambo ambalo unalifanya, halifurahiwi na wengine, aidha ni zuri au baya,

Katika biblia tunasoma habari ya mtu mmoja, aliyeitwa Egloni mfalme wa Boabu, huyu, aliwatumikisha Israeli kwa muda wa miaka 18, na hiyo yote ilikuwa ni kutokana na makosa yao wenyewe(Israeli)..Lakini walipomlilia Mungu, awaokoe kutoka katika utumwa na mateso ya mfalme huyu, Mungu akawasikia ndipo akawapelekea mwokozi aliyeitwa Elihu.

Huyu Elihu alijifanya kama mjumbe, aliyeituwa na Israeli, kumbe hila zake zilikuwa ni kwenda naye katika chumba cha siri, ili wakiwa wao wawili peke yao achomoe upanga wake na kumchoma tumboni, Tusome kidogo..

Waamuzi 3:20 “Basi Ehudi akamwendea; naye alikuwa anaketi peke yake katika chumba chake cha baridi. Ehudi akasema, Mimi nina ujumbe utokao kwa Mungu kwako wewe. Basi akainuka katika kiti chake.

21 Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kuume, akamtia tumboni mwake;

22 hicho kipini nacho kikaingia ndani pamoja na huo upanga wenyewe; nayo mafuta yakashikamana tena juu ya upanga, kwani hakuutoa tena upanga tumboni; nao ukatokea kwa nyuma.

23 Ndipo Ehudi akatoka nje barazani, akamfungia milango ya hicho chumba na kuifunga kwa ufunguo.

24 Basi alipokuwa amekwisha toka nje, hao watumishi wake wakaenda; wakaona, na tazama, hiyo milango ya chumba ilikuwa imefungwa kwa ufunguo; nao wakasema, Hapana budi amejifunika miguu yake ndani ya chumba cha baridi.

25 Wakangoja hata wakatahayari; na tazama, hakuifungua milango ya chumba; basi wakatwaa ufunguo, na kuifungua; na tazama, bwana wao alikuwa ameanguka nchi, naye amekufa”.

Umeona? Sasa huyu Elgoni alichomwa kutokana na makosa yake, lakini, pia wapo wengine waliochomwa kutokana na haki zao, mfano mmojawapo ni Bwana wetu YESU KRISTO..Yeye alichomwa mkuki pale msalabani, sio kwasababu alikuwa mwovu hapana.

Hivyo na wewe jiangalie ni wapi katika maisha yako, pana vita kwa wengine, wewe umesimama, Ikiwa upo ndani ya Kristo basi, ujue maadui wa imani wapo, lakini huna haja ya kuogopa, Kwasababu Mungu atakupigania, kikubwa unachopaswa ufanye ni kuzidi kuwa mwombaji.

Lakini kama upo nje ya Kristo, ukweli ni kwamba, licha tu kuzungukwa na hatari za maadui, lakini, maisha yako ya rohoni yapo hatarini.. Mungu anaweza kweli kukuepusha na hatari za mwilini, lakini zile za rohoni za ibilisi hawezi kukuzuia kutokana na kwamba wewe ni milki ya ibilisi.

Jiulize ukifa leo ghafla katika dhambi utakuwa mgeni wa namna huko uendako?

Hivyo ndugu ikiwa unahitaji kumpa leo YESU maisha yako..Basi uamuzi huo utakuwa ni busara sana kwako, Kama upo tayari kufanya hivyo, moja kwa moja fungua hapa, kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Na hayo mengine yaliyosalia Mungu atakujalia rehema zake.

Bwana akubariki.

Kwa mafundisho zaidi ya Neno la Mungu.

Whatsapp: +255 789001312

Group la whatsapp 

  Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

 

Mada Nyinginezo:

Kuota unafanya Mtihani.

KWANINI TUNAPASWA TUJIZUIE?

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA.

HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?

NILIMWONA SHETANI, AKIANGUKA KUTOKA MBINGUNI.

ZIFAHAMU HUDUMA KUU (10) ZA SHETANI DUNIANI.

Rudi Nyumbani:

Print this post

ZABURI 91, NI ZABURI YENYE NGUVU NYINGI.

Zaburi 91, Ni Zaburi iliyo ya kipekee sana yenye nguvu, Na shetani analijua hilo, ukitaka kuamini jiulize, ni kwanini Shetani aliitumia Zaburi hii kumjaribu Bwana,? Kiasi kwamba mtego wake ungekubali basi Zaburi hii ndio ingekuwa silaha ya kumwangushia Bwana.

Ni kwanini ainukuu Zaburi 91? Shetani aliijua nguvu na ulinzi Mungu aliouweka juu ya wampendao..Lakini wengi wetu hatuifahamu…Alimwambia hivi Bwana..

Mathayo 4:6 “akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake; Na mikononi mwao watakuchukua; Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako”.

Unaona, alijua kuwa mtu yeyote aliyempendeza Mungu, huwa anaachiliwa ulinzi wa kipekee, Mungu anamuagizia mpaka malaika zake, wamlinde, asijikwae,..

Hivyo kama wewe umeokoka  na umesimama vizuri basi fahamu Zaburi 91, Ni salaha yako madhubuti ya kummaliza shetani na vitisho vyake, na majeshi yake..Isipokuwa tu usiitumie hiyo kwa lengo la kumjaribu Mungu, vinginevyo utampa shetani nafasi ya kukuangusha kama alivyojaribu kufanya kwa Bwana Yesu.

Embu tuisome,

ZABURI 91

1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

2 Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.

3 Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji, Na katika tauni iharibuyo.

Bwana anasema, atakuepusha na mitego ya mwindaji(Shetani), na tauni iharibuyo..akiwa na maana atakulinda na magonjwa hatari mfano wa Tauni kama Corona..Unaona ikiwa wewe ni mtakatifu, huna haja ya kuwa na hofu.

Anaendelea kusema…

Zaburi 91:4 Kwa manyoya yake atakufunika, Chini ya mbawa zake utapata kimbilio; Uaminifu wake ni ngao na kigao.

5 Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,

6 Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,

Ndugu uliyeokoka, Bwana atakulinda tu, huna haja ya kuogopa, iwe ni mchana au usiku atakuwa na wewe kukulinda na mikono ya magonjwa na maadui.

Zaburi 91:7 Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.

8 Ila kwa macho yako utatazama, Na kuyaona malipo ya wasio haki.

9 Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako.

10 Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.

Haijalishi utaona ni wangapi, wanadondoka, au wanashindwa pembeni yako, wameanguka, lakini wewe Bwana atakuwa na wewe wakati wote kuhakikisha hushindwi wala hupatwi na mabaya hayo yote, hata kama utaonekana kama unashindwa,lakini mwisho wa siku ushindi utakuwa ni wako tu,

Zaburi 91:11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote.

12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

13 Utawakanyaga simba na nyoka, Mwana-simba na joka utawaseta kwa miguu.

Unaona zaidi ya hiyo, Malaika wa Bwana watakuwa na wewe kukulinda kila wakati, usijikwae, na mabaya..Na hiyo yote ni kwasababu gani? Ni kwasababu, umempenda Mungu na umemtafuta kwa bidii, umemfanya yeye kuwa tegemeo lako, na ndio maaana anasema..

Chapisho hili limefadhiliwa na https://www.swisswatch.is/ washirika wetu.

Zaburi 91:14 Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.

15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;

16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu.

Maneno ya faraja sana na yanayotia nguvu, lakini  mpaka Mungu kukutamkia hivyo ujue ni lazima kwanza uwe ni mwana wake mpendwa, vinginevyo, hakuna ulinzi wowote, utaokao kwake utakufikia..

Ili Mungu akulinde na tauni (Corona) isikuue, au magonjwa mengine ya kutisha yaliyozuka duniani leo hii, ni lazima uwe mwana wake mpendwa, ili Mungu akulinde na maadui (mapepo na wachawi), Ili Mungu akuagizie malaika zake watembee na wewe kila wakati kama alivyofanya kwa Elisha..basi ni lazima kwanza ufanyike mwana wake.

Ndipo hapo nawe utakapoitamka Zaburi 91 kwa ujasiri wote, na iwe kweli na maana kwako. Kumbuka  Zaburi hii ilimwingia sana shetani kichwani, na ndio maandiko pekee aliyoyatamka kwa kinywa katika biblia nzima, hiyo ni kuonyesha kuwa ni jinsi gani anaona wivu, kuona watoto wa Mungu wanapokea ulinzi wa kipekee kutoka kwa Mungu.

Maana yake ni kuwa ukimkosa leo Kristo, basi huwezi mshinda shetani, kwasababu ulinzi wa Mungu haupo juu yako.. Hivyo kama upo tayari leo kumpa Yesu maisha yako, basi uamuzi utakaofanya ni mzuri na wa busara sana..Kama ni hivyo fungua hapa kwa ajili ya maelekezo juu ya sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Tafadhali Share na wengine,

Whatsapp: +255789001312

Mada Nyinginezo:

TAZAMA, NASIMAMA MLANGONI.

AGANO LAKO LINABEBWA NA NANI?.

WEWE NI BWANA UNIPONYAYE.

KIAMA KINATISHA.

JIFUNZE KUJITOA KWA MUNGU NA KUWA MKARIBISHAJI.

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani:

Print this post