Title March 2023

Haini ni mtu gani? Mithali 13:2

Tusome,

Mithali 13:2 “Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake; Bali nafsi ya mtu haini itakula jeuri”

Haini ni jina lingine la mtu ambaye ni “Msaliti”, mtu anayefanya usaliti juu ya mwingine ni sawa na kafanya “Uhaini”. Mtu anayeisaliti nchi yake mtu huyo ni Mhaini, vile vile  mtu anayeisaliti Imani yake yenye kumfikisha mbinguni, kwa kurudia mambo machafu mtu huyo anafanya uhaini kwa Mungu wake.

Zaburi 78:57 “Bali walirudi nyuma, wakahaini kama baba zao; Wakaepea kama upinde usiofaa

 58 Wakamkasirisha kwa mahali pao pa juu, Wakamtia wivu kwa sanamu zao.

 59 Mungu akasikia, akaghadhibika, Akamkataa Israeli kabisa.”.

Na maandiko yanazidi kuonyesha kuwa Wahaini wote wa imani watapata adhabu..

Zaburi 119:158 “Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako”.

Mithali 22:12 “Macho ya Bwana humhifadhi mwenye maarifa; Bali huyapindua maneno ya mtu haini.”

Soma pia Mithali 13:15 na Zaburi 25:3.

Kama tayari ulikuwa umeyakimbia machafu ya ulimwengu, na sasa umeyarudi nyuma fahamu kuwa huo unafanya uhaini mbele za Mungu, kimbia haraka sana msalabani ukatubu,  kama ulikuwa umeacha uzinzi na sasa umeurudia, tubu kwa machozi sana mbele za Bwana, leo hii ni nafasi yako ya kutubu na kumgeukia Mungu, usingoje kesho, na hakikisha unatubu kwa kumaanisha kabisa kutofanya hayo uliyoyafanya au unayoyafanya, na Bwana atakupokea lakini ukizidi kukawia upo hatarini sana…

 Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

Je ni kweli kila nafsi itaonja mauti kulingana na (Zaburi 89:48)?

Sifa ni nini?

USIMFANYIE JEURI ROHO WA NEEMA.

MAGONJWA YAKUPATAYO MARA KWA MARA.

Rudi nyumbani

Print this post

YESU KATIKA USINGIZI WAKE.

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo.

Naamini kuwa ulishawahi kusoma katika maandiko kuwa kuna mahali Yesu alilala. Lakini ulishawahi kujiuliza ni kwanini habari ile iandikwe kulikuwa na umuhimu gani?

Kumbuka kila tukio lililoandikwa katika biblia limebeba somo kwetu sisi watakatifu.

Jambo pekee lililomfanya Yesu alale usingizi  mzito namna ile, sio kuchoka kama wengi wanavyodhani, kuna nyakati nyingi Yesu alikuwa anachoka kuliko hata hapa, lakini alikuwa halali, anapanda mlimani kuomba…lakini ni nini kilichompelekea alale?

Jambo lililompa Yesu usingizi mzito, ni ile DHORUBA iliyoanza kule baharini.

Marko 4:36-39

[36]Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye.

[37]Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji.

[38]Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia?

[39]Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

[40]Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado?

Umeona hapo, hakuna mahali popote biblia inarekodi Yesu alipitiwa na usingizi,  isipokuwa hapo kwenye dhoruba kuu.

Wakati wengine wanahangaika na matatizo, hawapati usingizi, wanapambana na changamoto zao..upande wa pili wa Yesu mambo ni tofauti,kule kuyumba kwa chombo kumbe ndio kulikuwa kunavuta usingizi vizuri.

Lakini ni nini Bwana anataka tujifunze juu ya tabia hii ya Kristo?

Ni kwamba hata yeye akiwa amejaa vizuri ndani yetu, tutadhihirisha tabia kama zake.

Ni kwanini leo hii tuna hofu ya maisha, tuna hofu ya kesho, tutaishije, tutakula nini, tutavaa nini? tuna hofu ya wezi, tuna hofu na kufukuzwa kazi, tuna hofu ya magonjwa?

Ni kwasababu Kristo hajajaa ndani yetu vizuri, ni kwasababu hatujapokea uhakika wa kuwa salama daima.

Wakristo wengi, wakiwa kwenye matatizo, mbalimbali hawana raha, wanapoteza utulivu..wanahangaika huku na kule kama wakina Petro. Hii ni hali ya kawaida ya kibinadamu. Lakini Yesu anaweza kukupa usingizi katikati ya tufani na dhoruba..endapo atajaa ndani yako vizuri.

Unachopaswa kufanya ni jiachie tu kwa Yesu, mwache yeye ahangaike na hiyo tufani, itaisha tu yenyewe, haitadumu muda mrefu, atakufungulia mlango wa kutoka katika hilo jaribu, haijalishi ni kubwa kiasi gani.

Jiachie tu kwa Yesu mtafakari yeye muda wote, muwaze yeye na uweza wake, Kama hujaokoka, hakikisha unafanya hivyo sasa, hivyo kwa jinsi utakavyokuwa unaendelea kumsogelea yeye ndivyo atakavyokupa wepesi kwa kukabiliana na mambo yote, na changamoto zote unazokutana nazo..Na hatimaye zitaisha tu bila hata kusumbuka kwasababu yeye yupo kazini.

Mkaribie Yesu sasa acha kuzitegemea akili zako mwenyewe..Naye atakusaidia, yeye mwenyewe anasema;

Mathayo 11:28-29

[28]Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

[29]Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu

Anasema pia..

Mathayo 6:31-34

[31]Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

[34]Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.

Mkaribie Yesu, Akutue mizigo. Akupe uzingizi, akupe raha.

Zaburi 127:2 “Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi”

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

FAHAMU JINSI KRISTO ANAVYOPONYA WATU ROHO.

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

NA WATU WOTE WALIKUWA WAKIAMKA MAPEMA, WAENDE HEKALUNI.

Dia ni nini katika biblia? (Mithali 13:8)

SABATO ILIFANYIKA KWAAJILI YA MWANADAMU NA SI MWANADAMU KWAAJILI YA SABATO!

KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

Rudi nyumbani

Print this post

Dia ni nini katika biblia? (Mithali 13:8)

Jibu: Tusome,

Mithali 13:8 “Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”.

Dia ni Kiswahili kingine cha neno “Fidia”, Kwahiyo hapo biblia inaposema “Dia” ya nafsi ya mtu ni utajiri wake, na maskini hasikii ogofyo lolote, maana yake ni kwamba “Fidia ya mtu anapokutana na matatizo ni itatoka katika vitu alivyonavyo” ikiwa na maana kuwa mtu anapokutwa na tatizo labda kasababisha hasara Fulani au kafanya kosa Fulani katika jamii, lililomsababishia apigwe faini, au kakutana na watu na kaingiliwa na wahalifu katika nyumba yake, basi Mali alizo nazo zinaweza kuwa fidia kwaajili ya uhai wake, maana yake anaweza kuwapa wale watu sehemu ya mali zake na akaisalimisha roho yake.

Lakini mtu asiye na kitu kabisa (yaani Yule maskini kikweli kweli), huwa hawezi kupokea vitisho vyovyote, hakuna jambazi yeyote anayefikiria kwenda kuvunja nyumba ya maskini akiwa na mtutu ili amwibie mali zake.. Ikiwa na maana kuwa, maskini siku zote yupo huru!.. hafuatiliwi na mtu, wala hakuna mtu ana habari na maisha yake (hapokei ogofyo lolote).

Ni hekima gani tunaipata hapo? Au ni nini tunajifunza hapo?

Ili tuelewe ni nini tunajifunza hapo, hebu tuanzie kusoma kuanzia mstari wa 7

Mithali 13:7 “Kuna mtu mwenye kujitajirisha, lakini hana kitu; Kuna ajifanyaye kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.

8 Dia ya nafsi ya mtu ni utajiri wake; Bali mtu maskini hasikii ogofyo lo lote”

Hii ni hekima ambayo inaweza kutusaidia kuwa salama..sio lazima tuwapo na mali, tujionyeshe kuwa na mali kwa watu!, ndio maana hapo biblia inasema “kuwa maskini, lakini ana mali nyingi.”.. Unapokuwa mtu wa kujionyesha mbele za watu mali ulizo nazo, unajiweka katika hatari ya kutoa DIA (Fidia) kwaajili ya uhai wako, kwasababu kila mtu atatamani hizo mali ulizo nazo, utavutia watu waovu na wasio waovu, utavutia majambazi, utavutia wenye mamlaka na watu  wapendao rushwa n.k

Hivyo hekima ni kujiweka katika maisha ya wastani, hata kama unazo mali nyingi, si lazima ujulikane wewe ni tajiri kuliko wote.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?

Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

Nini maana ya ampokeaye Nabii atapata thawabu ya Nabii? (Mathayo 10:41).

MWIMBIE BWANA ZABURI KATIKA NYAKATI ZA FURAHA.

Rudi nyumbani

Print this post

Je watu wa kale walitumia vifaa gani kuandikia?

Watu wa kale walitumia wino, na kalamu pamoja na karasati kuweka kumbukumbu zao kama tunavyofanya sasa..

Isipokuwa wino wao, kalamu zao na karatasi zao zilikuwa tofauti na hizi tunazotumia sasa..

Mtume Yohana katika nyaraka zake aliandika hivi; 

3 Yohana 1:13

[13]Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu. 

Kuonyesha kuwa unandishi wao ulitegemea wino na kalamu, kama tu huu wetu.

Je! Wino wa kale ulitengenezwaje?

Tofauti na huu wa kwetu unaotengenezwa na kemikali mbalimbali..wino wa zamani ulikuwa unatengenezwa na MASINZI. Masinzi hayo yalikuwa yanavunwa aidha kutoka  katika mafuta yaliyochomwa au kuni pale yanapoganda katika chombo kama sufuria kwa pembeni.

Wino wa kale

Sasa yalipokusanywa kama poda, baadaye yanachanganywa na gundi inayotoka katika mmea wa mpira..lengo la kufanya hivyo ni kuufanya wino huo ushikamane vizuri ili  wakati wa uandishi wino usitapakae ovyo.

Hivyo mwandishi anapoununua wino huo anachofanya ni kuchanganya na maji, kisha kutumia kalamu yake kuchovya na kuandika katika hilo karatasi lao.

Je! Kalamu zao ziliundwaje

Tofauti na kalamu zetu hizi, ambazo zinatengenezwa kwa mirija ya pastiki na chuma. Kalamu za zamani ziliundwa na mmea ujulikanao kama MWANZI ambayo hata huku sehemu kadhaa hutumika.. Mianzi hii ilichongwa kwa pembeni kuacha ncha. Ili kuruhusu wembamba wa uandishi katika karatasi  kama tu kalamu zetu za kisasa zilivyo.Tazama picha.

Kalamu za kale

Je karatasi za kale zilikuwaje?

Karatasi za zamani zilifanana hizi isipokuwa zenyewe zilikuwa ni nene, ziliundwa na mmea ujulikanao kama mafunjo(Ayubu 8:11).

Mmea huu ulichongwa kulingana na ukubwa wa karatasi, kisha kuchanjwa chanjwa katika vipisi vidogo, ambavyo baaadaye vililowekwa katika maji ili vilainike..kisha vinawekwa katika ubao ulionyooka, kisha vinalazwa kipisi kimoja baada ya kingine, na vingine kupita kwa kukatiza..kisha panawekwa ngozi ya mnyama kwa juu , na baada ya hapo kukandamizwa, ili vipisi hivyo vishikane,

Na kuachwa siku kadhaa, baadaye wakitoa, tayari karatasi hiyo nene hutokea… ngumu na imara kuliko hata hizi tulizonazo sasa. Ndizo walizotumia watu wa kale kuandikia.

karatasi za kale

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka? Je! Unatambua kuwa unyakuo wa kanisa upo karibu? Umejiandaaje? Ikiwa bado hujafanya hivyo na unahitaji msaada huo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;

Maran Atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?

Yerusalemu ni nini?

Kaniki ni nini katika biblia? (Yeremia 8:21).

Karismatiki ni nini?

KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.

Rudi nyumbani

Print this post

Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.

Zaburi 147:3 Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao.  4 Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.  5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.

Ukitazama juu unaona nyota nyingi sana zisizo na idadi, mbali na hizo zilizo ndani ya upeo wa macho yetu, lakini pia zipo nyingine tusizoziona ambazo idadi yake ni mabilioni kwa mabilioni, matrilioni kwa matrilioni,..

Lakini hapa Mungu anatupa siri ya uweza wake, anasema zote hizo amezihesabu na kuzipa majina,..

Sasa Kwanini atuambie jambo kama hilo?

Ni kutuaminisha kuwa ikiwa anazifahamu  nyota zote zilizo mbali, nje-ndani, atashindwaje kutufahamu sisi? Atashindwaje kuziona taabu zetu na shida zetu, atashindwaje kuyaona mateso yetu na majeraha yetu?

Hivyo hapo anaposema ‘Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuziganga jeraha zao’. Anamaanisha, huweza kutufanya upya, endapo tutamkaribia.

1Petro 5:7  ‘huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu’.

Mkaribie Kristo akuponye kwasababu yeye yupo karibu sana na wewe zaidi ya nyota za angani.

Utukufu na uweza vina yeye milele na milele amina.

Maombi Yangu:

“Baba mwema, tumeona uweza wako, juu ya ulimwengu wako uliouumba, kwamba hakuna lolote usilolijua,wala usiloliweza, na sasa ninakukaribia Baba wa Upendo, kama ulivyoahidi kwenye Neno lako kwamba utaziganga jeraha zangu, Naomba sasa niponye moyo wangu, na mwili wangu, nifanye upya tena, nisimame mbele zako, nikutumikie. Ni katika jina la Yesu naomba nikuamini. Amen.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NYOTA ZIPOTEAZO.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?

MUNGU WETU, JINSI LILIVYO TUKUFU JINA LAKO DUNIANI MWOTE!

UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?

Agano ni nini? na kuna aina ngapi za maagano?

Mofa ni nini? na inafunua nini kiroho?(1Samweli 28:24).

NIMEOKOKA, ILA MUNGU NDIYE ANAYEJUA NITAKWENDA WAPI.

Rudi nyumbani

Print this post

Ni kosa gani alilolifanya Eli, ilihali aliwaonya watoto wake?

SWALI: Kwanini Mungu alimuadhibu Eli kwa kosa la kutowaonya watoto wake, angali tunasoma katika maandiko aliwaonya hapo kabla?

Tusome;

1Samweli 2:22 Basi Eli alikuwa mzee sana; naye alisikia habari za mambo yote ambayo wanawe waliwatenda Waisraeli; na jinsi walivyolala na wanawake waliokuwa wakitumika mlangoni pa hema ya kukutania. 

23 Akawaambia, Mbona mnatenda mambo kama hayo? Maana nasikia habari za matendo yenu mabaya kwa watu hawa wote.  24 Sivyo hivyo, wanangu, kwa maana habari hii ninayoisikia si habari njema; mnawakosesha watu wa Bwana. 

25 Mtu mmoja akimkosa mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosa Bwana, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu Bwana amekusudia kuwaua.

Lakini Hapa Mungu anasema…

1Samweli 3:12 Siku hiyo nitayatimiza maneno yale yote niliyoyasema juu ya Eli katika habari za nyumba yake, tangu mwanzo hata mwisho. 

13 Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye HAKUWAZUIA. 

14 Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.


JIBU: Kibiblia “Kuonya” sio tu kusema kwa mdomo, bali pia kuchukua hatua stahiki, endapo maonyo hayatatekelezwa. Eli ni kweli aliwaonya watoto wake, kwa dhambi walizokuwa wanazifanya madhabahuni pa Mungu, lakini aliendelea kuwaangalia, wakifanya mambo yao maovu bila kuwaondoa katika nafasi zao. Ndio maana hapo kwenye 2Samweli3:13 Mungu anamwambia Samweli, kwamba HAKUWAZUIA. Hakuwaondoa katika kazi ya utumishi, Pengine kwasababu ni watoto wake, warithi wake, akawastahi zaidi ya  Mungu. Hivyo wakati wa adhabu ulipofika yeye naye alishiriki adhabu ile.

Hili ni funzo, pia kwa viongozi wote wa imani, nyakati hizi tunazoishi, kanisa limegeuzwa kama mahali pa kila mtu kujiamulia jambo lake, na viongozi wanaona wanafumbia macho. Utakuta mchungaji ni mzinzi, lakini askofu akipata taarifa, badala wamwondoe katika ofisi ile, wanamwonya tu, kisha wanamuhamisha dayosisi, wanamstahi, na akifika kule anaendelea na maovu yake, anahamishwa tena dayosisi.

Utakuta watoto wa wachungaji, ni walevi, hawana maadili, lakini wanaendelea kubaki katika nafasi za wazee wa kanisa au waimbaji kwaya. Mchungaji akiambiwa, anachokifanya ni kuwaonya tu, lakini bado wanaendelea kushika nafasi hizo za madhabahuni. Hii ni hatari. Mungu anataka hatua stahiki zifuatane na maonyo kama hakuna mabadiliko.

Hivyo kama wewe ni kiongozi, kumbuka maonyo yako ni lazima yaambatane na vitendo.

Bwana atusaidie.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini Kuhani wa Mungu Eli alikufa kwa kuvunjika shingo?

IKABODI MAANA YAKE NI NINI?

NA NENO LA BWANA LILIKUWA ADIMU SIKU ZILE.

NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA PILI WA YOHANA.

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

Rudi nyumbani

Print this post

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA

Baraka ni karama ya Mungu, na kila mmoja wetu aliyekombolewa na Yesu, ahadi hiyo ni yake. Baraka zimegawanyika mara mbili, zipo baraka za mwilini, na baraka za rohoni. Lakini kubwa zaidi ni zile za rohoni. Hivi ni baadhi ya vifungu vinavyoeleza Baraka za Mungu. Lakini pia ikiwa utapenda kupata vifungu mbalimbali, pamoja na mafundisho mazuri ya Neno la Mungu, bofya link hii uweze kujiunga na kundi letu la Whatsapp>>> WHATSAPP GROUP

Wafilipi 4:19  “Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu”

Yakobo 1:17  “Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka”.

Hesabu 6: 24 “Bwana akubarikie, na kukulinda;  25 Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili;  26 Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani”

3Yohana 1:2  “Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo”

2Wakorintho 9:8  “Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;”

Kumbukumbu 28:2 “na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.  3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.  4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.  5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.  6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo”.

Waefeso 1:3 ” Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;”

Mathayo 6:30 ” Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31  Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32  Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33  Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34  Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake”

Malaki  3:10 “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la”.

Zaburi 20:4 “Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako, Na kuyatimiza mashauri yako yote”.

Mathayo 5:6  “Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa”.

Mithali 16:3 “Mkabidhi Bwana kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika”

Yeremia 17:7 “Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake”

Pia Kwa wokovu/ maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU KIFO.

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

MISTARI YA BIBLIA YA UPONYAJI.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..

HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

Dina akatoka kuwaona binti za nchi. (Mwanzo 34:1)

Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Huu ni mfululizo wa masomo maalumu kwa ajili ya wanawake: Ikiwa hukupata chambuzi nyingine za nyuma basi fungua link hii  uweze kuzipitia >>>   MAFUNDISHO KWA WANAWAKE

Mwanzo 34:1-3 Inasema..

“Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, AKATOKA KUWAONA BINTI ZA NCHI.  2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri.  3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri”

Dina alikuwa ni binti wa Yakobo, aliyejitunza na kujiheshimu, alikaa chini ya Mama zake akifundishwa desturi za uzao wa Ibrahimu unavyopaswa uwe. Akafahamu kuwa uzao wao haupaswi kuchanganywa na uzao wa ukoo mwingine, Ili Baraka ya Ibrahimu aliyoahidiwa kwa uzao wake isiingiliwe na doa.

Lakini Tunaona, jambo moja alilolifanya Dina, ambalo pengine hakujua mwisho wake utampelekea pabaya. Na jambo lenyewe “ni yeye kutoka na kwenda kuonana na mabinti wa nchi”. Kama msichana alipoona mabinti wa mataifa mengine, wanaishi maisha ya kidunia, maisha ya anasa, maisha ya ukisasa. Na yeye naye akatamani kwenda kuunga urafiki nao, bila kujua mwisho wake utakuwaje.

Hivyo kidogo kidogo, akaanza kuchukuliwa na desturi za wanawake wa kidunia, akaanza kujichanganya, siku ya kwanza, siku ya pili, wiki ya kwanza wiki ya pili, mwezi wa kwanza, mwezi wa pili. Kidogo kidogo wale mabinti wa kidunia waanza kumfundisha tabia mbaya..Pengine wakaanza kumwambia “Mbona wewe ni mrembo, hadi sasa huna boyfriend”..Mbona una shepu zuri, embu vaa hizi nguo fupi uonekane na wanaume..Embu twende leo disco, tukakutane na vijana wenzetu, tule maisha, ujana maji ya moto..

Akawa anawasikiliza, na huko ndipo akakutana na huyo Shekemu, akamlaghai, kisha akambikiri..Taarifa zikawafikia ndugu zake, wakakasirika sana Simeoni na Lawi, hadi kufikia kitendo cha kwenda kuwaua watu wote wa huo ukoo. Kwasababu waliona tendo alilofanya Dina, ni chukizo kubwa sana kwa jamii yao. Kuuchafua uzao uliobarikiwa, kuvunja maagano ya Mungu.

Nini Bwana anataka mabinti na wanawake wajifunze?

Kabla ya kuanguka katika dhambi, ushawihi huwa unaanza kwanza kwa marafiki wanaokuzunguka.  Angalia ni watu wa namna gani uliozoena nao, au uliounga urafiki nao, au unaokaa nao muda mrefu. Mabinti wengi waliookoka, hawajafundishwa kuvaa vibaya na wanaume wazinzi, bali na mabinti wenzao, hawajafundishwa kwenda disco au kunywa pombe na wanaume, bali mabinti wenzao. Hawajafundishwa kwenda kwa waganga na kaka zao, bali wanawake wenzao, hawajafundishwa kusengenya na jamii, bali ni wanawake wenzao wanaokutana nao masaluni na mabarazani.

Hawa ndio maadui wa kwanza. Dina hakutoka kwenda kumtafuta Shekemu, alitoka kuwatazama mabinti  tu wa kidunia na huko huko wakamuunganishia Shekemu. Laiti angetulia nyumbani akakaa na wale wabinti wenzake wa ukoo mmoja hata kama ni washamba, angekuwa salama.

Wewe kama mwanamke usipende kuunga urafiki na wanawake ambao hawajaokoka, ambao hawana habari na Mambo ya ufalme wa mbinguni, upo chuo, upo shuleni, upo kazini, ni heri ubaki kivyako vyako, kuliko kujiingiza hatarini. Siku zote uangamivu unavyokuja huwa unaanzia mbali sana, hivyo kuwa makini, tafuta watu waliodhamiria kuishi maisha matakatifu, hao ndio wawe marafiki zako wa karibu, washauri wako, uige tabia zao, kataa kampani za kipepo, acha wakuone mshamba, lakini roho yako ipo salama, acha upitwe na fashion, acha upitwe na uzuri lakini jina lako lipo katika kitabu cha uzima.

Majira tunayoishi ni ya kung’ang’ania kwa nguvu wokovu tuliopewa, ni kuwa siriazi kweli kweli, kwasababu maelfu kwa maelfu ya watu wanaangamia, wanashindwa kumaliza mwendo wao salama hapa duniani wanaponzwa na marafiki, Unadhani na sisi tukiwa walegevu, tunadhiria kila kitu tu kinachokuja mbele yetu, tutawezaje kupona. Njia imesonga, mlango ni mwembamba, tunajiingiza kwa nguvu, isitoshe muda tuliobakiwa nao ni mchache. Hivyo hatupaswi kuwapa nafasi watu wakidunia katika maisha yetu.

Tujifunze kwa Dina. Tuwe salama. Kataa, kampani za kipepo!

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

MAFUNDISHO KWA WANAWAKE

FUNGUO WALIZOKUWA NAZO MABINTI WATANO WA SELOFEHADI!

MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.

Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Nifanyeje niwe mwombaji mzuri, wa masafa marefu?

Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; (Mithali 11:16)

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

Rudi nyumbani

Print this post

KAMA MTUMISHI WA MUNGU, TAFUTA MAARIFA KWA BIDII.

Huu ni mfululizo wa Masomo maalumu kwa Watumishi wa Mungu (Wahubiri wa Injili, Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu, Manabii na Waimbaji wote).

Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”.

Tunaona hapa Bwana anaanza  kama kwa kulaumu!.. sasa anamlaumu nani? Si wana wa Israeli bali anawalaumu  MAKUHANI wake! (Yaani watu waliowekwa kwa lengo la kuwafundisha wana wa Israeli njia ya kumcha Bwana)… ambao kwasasa wanafananishwa na (Wachungaji, Wainjilisti, Waalimu, Mitume, Manabii na wahubiri wote)

Watu hawa Bwana anawalaumu kwa kuwa “wameyakataa maarifa” (maana yake hawataki kujishughulisha kutafuta maarifa yatakayowasaidia wao pamoja na wengine), na hivyo kusababisha Israeli yote kukosa maarifa.. kwasababu laiti wakiyapata maarifa hayo ya kiMungu ya kutosha, basi wangeweza kuwafundisha Israeli nzima na hivyo Israeli yote ingeponyeka..

Lakini kinyume chake, Makuhani hawa hawayataki maarifa!, wanaridhika kukaa katika ujinga, hawataki kusoma maandiko,  na hivyo kusababisha Israeli yote kukosa maarifa na kuangamia, jambo ambalo ni DHAMBI KUBWA SANA MBELE ZA MUNGU!, Kwasababu wao ndio chanzo cha Israeli yote kukosa maarifa..

Na tunaona madhara yake ni nini… Bwana AKAWAKATAA wasiendelee kuwa makuhani, na akawakataa na WATOTO WAO pia.

Ni jambo baya sana, Bwana kukukataa kuwa KUHANI.. kwani unakuwa Umenyang’anywa Neema yote iliyokuwa juu yako.. utalazimisha kuendelea na Mungu, lakini yeye atakuwa yupo mbali na wewe kama ilivyokuwa kwa Sauli..

1Samweli 15:23 “Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”

Hili ni jambo baya sana na linaloendelea sasa miongoni mwa watumishi.. Ni heri tukataliwe na wanadamu wote, lakini tusikataliwe na Mungu..

Kama mtumishi wa Mungu tafuta maarifa!!!… kwasababu utumishi wako unapimwa!.. Bwana anategemea kuona watu wake wanajaa maarifa ya kumjua yeye pindi wanapokuja katika kanisa unalohudumu, wanapokuja katika maskani unayo hudumu…. hataki kuona watu wake wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, ili hali wewe (unayejiita mtumishi wa Mungu) ndiye ambaye ungepaswa uwape hayo maarifa.!

Bwana akiona watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa, usidhani wewe utabaki salama!.. Bwana atakukataa wewe na pia atawakataa watoto wako..

Usifurahie kuona watu walio chini yako, hawaelewi kanuni ya Imani, wanatanga tanga huku na kule kutafuta  maji, au mafuta au kuufananisha ukristo na uganga wa kienyeji…

Chukua jukumu la kujifunza biblia kwa kina ili ujae maarifa yatakayokusaidia wewe na ukawasaidie na watu wako!!!!!…soma, tafiti, chunguza maandiko kila siku, hakiki mambo yote, acha kutafuta umaarufu na sifa zisizokuwa na maaana kutoka kwa watu wako…. hiyo itathaminisha utumishi wako mbele za Mungu.. wape watu Maarifa ya kiMungu, hayo ndiyo yatakayowalinda wasije wakaangamia!… Kumbuka siku zote kuwa Bwana hataki watu wake waangamizwe kwa kuyakosa hayo!.

Kama unaona uvivu kutafuta maarifa na kuwapa watu hayo, acha hiyo kazi ya kuhubiri, sio wito wako!, nenda katafuta kazi nyingine, kafanye biashara na Mungu atakubariki huko!, lakini usiwaongoze watu katika njia ya upotevu, kwa kuwajaza elimu za mambo ya ulimwengu huu na elimu za kichawi badala ya kuwapa elimu na maarifa ya ufalme wa mbinguni.. utajitafutia laana badala ya Baraka!.

Bwana Yesu na atusaidie sana.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TAFUTA KWA BIDII KUWA MTAKATIFU.

NJAA ILIYOPO SASA.

Je! Mungu anaupendeleo kwa wanaume zaidi ya wanawake?

UFANYE WEMA WAKO KATIKA MAARIFA.

Tofauti kati ya Hekima, ufahamu na maarifa, ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya andiko hili  “Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.(Yohana 5:37)”

Jibu: Tusome,

Yohana 5:37  “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. SAUTI YAKE HAMKUISIKIA WAKATI WO WOTE, WALA SURA YAKE HAMKUIONA.

38  Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.”

Hapa Bwana Yesu hamaanishi kwa Wayahudi hawajawahi kuisikia sauti ya Mungu, wala kuliona umbile lake!. Hapana bali andiko hilo linamaansha kuwa Mungu alijidhihirisha kwao kimaumbile lakini hawakumwona na vile vile alijidhihirisha kwao kisauti lakini hawakumsikia.

Sawasawa kabisa na alivyosema katika Kitabu cha Isaya

Isaya 50:2 “Basi, NILIPOKUJA, MBONA HAPAKUWA NA MTU? NILIPOITA, MBONA HAPAKUWA NA MTU ALIYENIJIBU? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu”.

Umeona hapo?.. kumbe kuna wakati Bwana anatujia kimaumbile lakini hatumwoni?… Sasa utauliza ni wakati gani anatujia hatumwoni, na ni wakati gani anapaza sauti yake hatuisikii??

Kupitia watumishi wake wa kweli, wanapotujia kama wageni na kutuletea habari njema, ujio wao unafananishwa kabisa na ujio wa Kristo kwetu kimaumbile, haihitaji yeye Mungu atutokee ndio ihesabike kuwa tumeliona umbile lake, bali watumishi wake tu kutujia tayari hao ni umbile lake…… utasema hilo tunalithibitisha vipi kimaandiko??

Mathayo 25:41 “Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;

42  kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;

43  nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.

44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?

45  Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, KADIRI MSIVYOMTENDEA MMOJAWAPO WA HAO WALIO WADOGO, HAMKUNITENDEA MIMI.

46  Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.

Umeona?.. Vile vile tusiposikiliza sauti za watumishi wake, ni sawa na hatujaisikiliza sauti yake!.. Ndio maana hapo katika Isaya 52:2 anasema “nilipoita mbona hamkuitika?”.. maana yake ni kwamba wenyewe walidhani sauti wanayoisikia ni ya mwanadamu kumbe ni ya Mungu.. vile vile walidhani umbile walionalo mbele yao ni la mwanadamu kumbe ndio umbile la Mungu, kwahiyo wakayadharau maneno ya Mungu aliyoyazungumza kupitia watumishi wake..

Na hapa Kristo anarudia tena maneno hayo hayo ya Isaya na kusema… “Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. SAUTI YAKE HAMKUISIKIA WAKATI WO WOTE, WALA SURA YAKE HAMKUIONA.”.. Maana yake Mungu alizungumza nao mara nyingi, na kuonekana kwao mara nyingi lakini hawakuwahi kumsikia wala kumwelewa wala kumfahamu hata mara moja, kwasababu mioyo yao ilikuwa mbali naye.

Na sisi tunajifunza kuwa sauti ya Mungu haiji kwetu kama sisi tunavyotaka au tunavyopanga, wala Mungu hatujii kimaumbile kama sisi tunavyotaka!..

Ni wengi sana wanafunga na kukesha ili kwamba Mungu awatokee, na waisikie sauti ya Mungu kama vile redio,..kama unafanya hivyo nataka nikuambie kuwa “unapoteza muda wako”.. kwasababu hiyo sio Njia ya MUNGU kuzungumza na sisi, hizo ni njia zetu sisi wanadamu za kuwasiliana..Mungu yeye anazo njia zake, ni lazima tuzijue hizo, tusilazimishe atumie zetu… “atafanya hivyo akipenda”, lakini si kanuni yake!.

Ukitaka kuisikia sauti ya Mungu vizuri, soma Neno na kulitafakari, Sikiliza mahubiri ya watumishi wa Mungu wa kweli, na ishi maisha matakatifu. Hapo utamwona Mungu sana katika maisha yako na utamsikia sana.

Bwana atusaidie na kutubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)

WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.

Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?

Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?

FAHAMU JINSI MUNGU NA SHETANI WANAVYOZUNGUMZA NA WATU.

Rudi nyumbani

Print this post