MISTARI YA BIBLIA KUHUSU KIFO.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU KIFO.

Mistari ya biblia kuhusu kifo.


Kifo ni jambo lisilozoeleka kwa mtu yeyote, Lakini pamoja na hayo lipo tumaini la uzima tena, kwa wale waliomwamini Bwana Yesu Kristo. Na ndio maana mtume Petro aliwatia moyo waaminio wote wa wakati ule, akiwaambia wasistaajabie sana, msiba huo utakapowapata kwa ghafla kama jaribu la moto, kinyume chake wafurahie kwasababu lipo tumaini tena la uzima siku ile ya ufufuo..Kwasababu watafufuliwa tena, na kuwaona wapendwa wao.

1Petro 4:12 “Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.

13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe”.

Hivyo na wewe unapoipitia mistari hii naomba uitafakari kwa utulivu, itakuponya sehemu Fulani.

Kwababu biblia inasema tena..

Mhubiri 7:2 “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.

3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo”.

Na pia Bwana Yesu alisema…

Mathayo 5:4 “Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika”.

Na bado biblia inaendelea kusisitiza na kusema..

Mhubiri 7: 1 “Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa”.

 

1Wathesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.”.

 

Zaburi 23:4 “Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji”.

 

Warumi 14:8 “Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana”.

 

Luka 23:43 “Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.

 

Yohana 11:26 “naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo”?

 

Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.

2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.

3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.

4 Nami niendako mwaijua njia”.

 

Zaburi 116:15 “Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake”.

 

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

 

Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2 Wakati wa kuzaliwa, na wakati wa kufa; Wakati wa kupanda, na wakati wa kung’oa yaliyopandwa;

3 Wakati wa kuua, na wakati wa kupoza; Wakati wa kubomoa, na wakati wa kujenga;

4 Wakati wa kulia, na wakati wa kucheka; Wakati wa kuomboleza, na wakati wa kucheza”;

 

1Wakorintho 15:26 “Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti”.

 

Ufunuo 21:4 “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita”.

 

2Wakorintho 5:1 “Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni”.

 

Wafilipi 3:20 “Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;

21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.

 

2Wakorintho 12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.

10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.

 

Warumi 5:12 “Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi”

Lakini tukishafahamu hayo, tukishafahamu kuwa haya maisha ni ya kitambo tu,  yanayeyuka kama mvuke, swali linakuja je! Wewe umejiwekaje kipindi hichi kifupi ulichobakiwa nacho duniani?

Yakobo 4:14 “walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka”.

Jiulize ukifa na wewe leo ghafla, utakuwa upande gani?.Ukiona moyoni mwako huna jibu la uhakika ni wazi kuwa ukifa huwezi kwenda mbinguni..Kwasababu wanaokwenda mbinguni Yesu Kristo anauweka uhakika huo moyoni mwao. Lakini kama wewe ni mwenye dhambi, biblia inasema, mauti  ya pili inakuongojea huko mbeleni, hata baada ya kifo hichi cha kawaida.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”

Embu yatafakari vizuri maisha yako, hata ukipata kila kitu, na pesa zote duniani ujue ipo siku isiyokuwa na jina utakuwa ni vumbi tu..

Mhubiri 12:7 “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa”.

 

Mhubiri 9: 5 “kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa”.

 

Zaburi 146: 4 “Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea”.

Ndio kifo kitakukuta, lakini Bwana hapendi ufe katika hali ya dhambi, kwasababu hutakuwa na tumaini tena la maisha baada ya hapo.

Ezekieli 18:32 “Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi”.

Inawezekana upo katika msiba wa mtu wako wa karabu, fahamu kuwa wakati mwingine Bwana anaruhusu uyapitie hayo, au uyaone hayo ili kukumbusha jambo la muhimu unalotakiwa kulifikiria kwanza.

Mhubiri 7: 14 “Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake”.

Unaona?

Lakini ukimpa leo Yesu maisha yako, atakupa tumaini la kweli, atakuondolea hofu la mauti, atakuponya roho yako na wewe utakuwa na amani wakati wote, hata ikitokea umekufa leo, unaouhakika wa kwenda mbinguni.. anasema..

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha”.

Wokovu ni bure, kwa wakati wote, na unapatikana wakati wowote mtu anapoufungua moyo wake. Kwanini usimkaribishe Yesu mwokozi maishani mwako?

Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.

Hivyo ikiwa leo umeguswa ndani yako na unasema sitaki tena kuishi maisha ya kubahatisha, sitaki kuishi maisha ya mguu mmoja ndani mwingine nje, nataka kuwa upande wa Yesu moja kwa moja. Basi uamuzi huo ni wa busara sana kwako, Kwasababu yeye anasema wote wajao kwangu sitawatupa nje kamwe.. Hivyo fungua hapa kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba na Bwana akubariki. >>>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Maran Atha.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?

USIUZE URITHI WAKO.

VIFUNGO VYA GIZA VYA MILELE.

UNYAKUO.

Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia..!!

MIHURI SABA

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments