SWALI: Yakobo 5:14 inasema, wazee wa kanisa wakitaka kumwombea mgonjwa wampake mafuta, je! yale ni mafuta ya upako au?. Na kama sio, ni mafuta gani yanayozungumziwa pale?.
Yakobo 5:14 “Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana”.
JIBU: Kabla hutujaona ni mafuta gani yanayozungumziwa pale..Tuutazame kwanza kwa ukaribu mstari huo, ukiungalia vizuri utaona umegawanyika katika vipengele viwili.. utaona baada ya hao wazee wa kanisa kuitwa, hatua ya kwanza ni wanamuombea, (hicho ni kipengele cha kwanza kilichotenganishwa na alama ya mkato), na hatua ya pili inayofuata sasa baada ya hapo ni kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
Watu wengi hawalioni hilo, wanayaunganisha hayo maneno mawili pamoja, na ndio hapo wanadhani, mafuta Fulani ya chupa ndio maombezi yenyewe, .. Jambo ambalo si sahihi?. Kilichomaanishwa pale ni kuwa maombi yakishakwisha, kinachofuata ni kupakwa mafuta…Ukisoma biblia kwa haraka haraka ni rahisi kupoteza shabaha ya maandiko mengi.
Sasa tukirudi kwenye swali ni mafuta gani yale yaliyomaanishwa?..
Biblia inasema..
1Yohana 2:20 “Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote”.
Roho Mtakatifu ndiye anayepaka watu mafuta, na mafuta yenyewe ni Neno lake (Yohana 16:13). Hivyo mtu aliye na Neno la Mungu kwa wingi ndani yake, mtu huyo ana mafuta mengi sana ya kumsaidia.
2Wakorintho 1:21 “Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu. 22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.”
2Wakorintho 1:21 “Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu.
22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.”
Sasa mitume na wazee wa kanisa kwa kujua mafuta hasaa na halisi ni yapi, ilikuwa ni desturi yao mara baada ya kuwaombea wagonjwa, jambo linalofuata na kuwaimarisha kwa Neno, ,Kwasababu walijua hicho ndicho kinachoweza kumfanya mtu asimame na kuweza kufanya mambo yote mwenyewe, hata baada ya kutoka pale.
1Yohana 2:27 “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake”.
Vivyo hivyo, na sasa, tunapaswa tuendeleze desturi hiyo, si kuwaombea tu wagonjwa matatizo yao, sio kufanyia tu kuwafanyia maombi ya ukombozi peke yake halafu hakuna cha ziada baada ya hapo, bali pia, tuwapake mafuta ya Roho wa Bwana..Tuwape chakula cha uzima..ambacho hata wakitoka pale, wanaweza kusimama wao wenyewe, pindi wanapokumbana na matatizo kama hayo na hata kumshinda shetani.
Huo ndio uponyaji hasaa, Lakini kama mtu atatolewa mapepo kwa kuombewa, halafu hatiwi mafuta,(Yaani hufundishwi au ajifunzi maneno ya uzima), akitoka pale, ataendelea na dhambi zake, na yale mapepo yatamrudia baada ya kipindi kifupi, tena yenye nguvu mara saba zaidi, na hali yake ya mwisho itakuwa mbaya kuliko ile ya kwanza kama biblia inavyosema. Na kazi inakuwa ni bure, Hivyo jitathmini na wewe kama mhubiri je unafanya hivyo?.
Kwahiyo mafuta yanayozungumziwa pale, sio mafuta ya chupa, bali ni Neno la Mungu, linalomiminwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani ya mtu..
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
Kwanini Mungu alisema hakuna mtu awazaye kuuona uso wake akaishi?
PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA PASAKA?
Roho Mtakatifu ni nani?.
Rudi Nyumbani:
Print this post
Amen Asante kwa somo zuri