Title January 2024

MAOMBI YA KUOMBEA WATOTO.

(Masomo maalumu kwa wazazi na walezi)

Marko 9:21 “Akamwuliza babaye, Amepatwa na haya tangu lini? Akasema, TANGU UTOTO

Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno lo lote, utuhurumie, na kutusaidia

23  Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye”.

Kuna umuhimu Mkubwa sana wa kuwaombea watoto, KILA SIKU (ZINGATIA HILI: KILA SIKU!!!!). Kwanini kila siku?..kwasababu adui naye anawatafuta kila siku, kwamaana anajua imeandikwa (Uzao wako utamponda kichwa (Mwanzo 3:15))

Vifuatavyo ni vipengele vya Maombi kwaajili ya mtoto/watoto.

        1.WOKOVU/NEEMA.

Mwombee mtoto wako Neema ya kumjua Mungu, na kuzungumza naye tangu akiwa tumboni, na ikiwa ulichelewa kuanza kufanya hivyo, basi bado unayo nafasi ya kumwombea hata sasa.

Andiko la kusimamia: 1 Timotheo 3:15  “na ya kuwa TANGU UTOTO umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu”

     2. UTII NA HESHIMA

Mwombee mtoto wako/watoto wako roho ya Utii..Ili wapate miaka mingi ya kuishi na ya kheri.

Andiko la kusimamia: Waefeso 6:1 “Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.

2  Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, 6.3  Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.

       3. ULINZI

Waombee watoto wako ulinzi wa kiroho na kimwili,  Wakiroho- wasivamiwe wala kutumiwa na nguvu za giza angali wakiwa wadogo na hivyo kuaathirika tabia zao, vile vile wasiharibiwe na dunia wala wasijengeke katika misingi isiyofaa.

Andiko la kusimamia: 1Yohana 5:21  “Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu”

      4. UKUAJI (KIROHO NA KIMWILI)

Waombee watoto wako wakue katika kumjua Mungu, vile vile wasipate shida yoyote ya kiafya itakayowaletea ulemavu au udumavu. Akili zao zikue vizuri na wawe na afya bora, vile vile magonjwa yasiwapate iwe ya kuambukiza au kurithi.

Andiko la kusimamia: Luka 2:39 “Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti.

40  Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake”.

       5. ELIMU

Waombee watoto wako wawe watu wa kupenda kusoma, na pia kufanya vizuri katika Elimu ya dunia.

Andiko la kusimamia: Mithali  4:13 “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako”

      6. ROHO MTAKATIFU.

Waombee watoto wako wajazwe na Nguvu za Roho Mtakatifu katika nyakati zote, wakiwa tumboni kama Yohana Mbatizaji (Luka 1:15) na hata baada ya kuzaliwa na katika vipindi vyote vya ukuaji wao.

Andiko la kusimamia: Matendo 2:38 “ Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.

Kama ukiweza kutumia muda wa kutosha kumwombea Mtoto wako/watoto wako katika vipengele hivyo (KILA SIKU, Asubuhi na jioni)  basi utamweka utawaweka katika nafasi nzuri sana kiroho na mafanikio katika wakati ujao.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?

FAIDA ZA MAOMBI YA USIKU

Nini maana ya “Andiko huua, bali Roho huhuisha (2Wakorintho 3:6)

MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.

NI YESU YUPI UNATEMBEA NAYE?

Rudi nyumbani

Print this post

Jicho kucheza ni ishara ya nini?

Jicho kucheza cheza maana yake nini?.. au inaashiria nini kiroho?..Je ni ishara ya kwamba kuna mtu ananisema au kuna jambo baya linakwenda kutokea?.


Jibu: Jicho kucheza ni kitendo cha kope ya jicho moja kutikisika.. Hali hii inawatokea watu wengi, katika vipindi tofauti tofauti (Na ni tendo lisilo la hiari).

Katika biblia hakuna mahali popote panaonyesha kuwa jicho kutikisika ni ishara ya jambo Fulani lijalo, wala hakuna mtu aliyewahi kufunuliwa jambo  lolote (lijalo au lililopita) kwa njia hiyo katika biblia…

Isipokuwa kuna vipindi vichache ambavyo hisia za rohoni zinaweza kujidhihirisha katika mwili… Kwamfano mtu anaweza kushukiwa na nguvu za Mungu akahisi mwili wote kutetemeka..mwingine akahisi masikio yanawaka moto, mwingine miguu, mwingine mikono, mwingine jasho mwili mzima n.k Hii inatokea lakini si kwa watu wote, bali kwa wachache… lakini jicho kucheza ni jambo ambalo linawatokea wengi!.

Mwingine akaingia mahali penye mamlaka nyingine mwili ukaishiwa nguvu au akapata msisimko Fulani..Hiyo inaweza kutokea kwa baadhi ya watu ila si wote..L akini katika suala la jicho kucheza si jambo geni, au la watu wachache…bali ni jambo ambalo linawatokea  wengi sana (Zaidi ya asilimi 90 ya watu).

Hivyo si tendo la ajabu kwamba ni ishara ya jambo Fulani lijalo… bali ni misisimko tu ya misuli ya mwili ambayo inaweza kutokea sehemu nyingine yoyote katika mwili, wengine inawatokea katika misuli ya mikono (misuli inaanza kucheza tu yenyewe), wengine katika miguu na sehemu nyingine za mwili. Inapotokea hali kama hii huwa inaisha yenyewe baada ya muda fulani kupita.

Lakini ikiwa kuna kitu ambacho Roho Mtakatifu anataka kukufunulia kupitia hisia za mwili, au kiungo chako…basi kitu hicho kitakuwa Dhahiri kwako atakuambia, lakini pia kumbuka siku zote Roho Mtakatifu hana kanuni moja maalumu ya kusema na mtu kwamba leo akitumia ishara hiyo ya mwili basi kesho atarudia tena kusema na wewe kwa njia hiyo hiyo (inakuwa ni nadra sana).

Shukrani kwa washirika wetu, http://www.swisswatch.is unaweza kupata mtandaoni ili kukidhi kila mapendeleo na bajeti, kutoka kwa bajeti hadi mifano ya maridadi ya hali ya juu.Maana yake kama leo Bwana kakupa ufunuo kwa ishara ya jicho usitegemee kesho jicho litakapocheza basi ni Bwana anataka kusema na wewe (kamwe usiende katika hayo mazoea)Looking for an affordable yet stylish timepiece? Look no further than our Replica hublot 44mm collection, where luxury meets affordability. These Cheap Diamond Replica Hublot 44mm watches, all under $39, exude elegance and sophistication without breaking the bank. Crafted with precision and attention to detail, our replicas capture the essence of the original Hublot design, making them a perfect choice for those who appreciate quality without the hefty price tag. Experience the allure of a Hublot 44mm watch today and elevate your style effortlessly.. Mahali pekee ambapo unaweza kutafuta kupokea ufunuo mara kwa mara kwa njia hiyo hiyo moja, ni KWENYE BIBLIA.

Kila utakapoishika biblia na kutafuta kuisoma katika utulivu na kumaamisha basi utaisikia sauti ya MUNGU, lakini si kila jicho linapocheza, au mwili unapochemka, au mikono inapowaka moto, au nywele zinaposisimka.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Kijicho ni nini? (Marko 7:22)

Kucheza karata ni sahihi kwa Mtu aliye MKRITO?

TAA YA MWILI NI JICHO,

Je biblia inatuhubiria kucheza Mieleka au kuitazama? (Mwanzo 32:24)

Je ushabiki wa mpira ni dhambi?

Rudi nyumbani

Print this post

Mistari ya biblia kuhusu maombi.

Ifuatayo ni mistari michache ya biblia inayohusu maombi.


Zekaria 10:1 “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.”

Mathayo 7:7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

8  kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”

Marko 13:33 “Angalieni, kesheni, [ombeni], kwa kuwa hamjui wakati ule utakapokuwapo”

Luka 22:40 “ Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni.”

Yohana 15:7 “Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

Yohana 16:24 “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu”

Wafilipi 4:6 “Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu”.

Marko 11:24  “Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu”.

Wakolosai 4:2 “Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani”

Waefeso 6:18  “kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”

1Wathesalonike 5:17 “ombeni bila kukoma;”

1Yohana 5:14  “Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia”.

1Timotheo 2:1 “Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote”

Yakobo 5:16  “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii”

Kwa mwongozo wa maombi ya kujikuza kiroho  fungua hapa >> MWONGOZO WA MAOMBI YA KUJIKUZA KIROHO.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.

MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA

MISTARI YA BIBLIA YA FARAJA.

IFAHAMU FAIDA YA KUMKIRI KRISTO UKIWA HAPA DUNIANI.

Rudi nyumbani

Print this post

Mistari ya biblia kuhusu kibali.

Ifuatayo ni baadhi ya mistari ambayo itamsaidia mtu kupata kibali aidha KWA MUNGU au kwa WANADAMU, au KWA WAKUU Au vyote kwa pamoja (Mungu pamoja na wanadamu).

KIBALI CHA MUNGU:

Mwanzo 4:6 “Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?

7 Kama ukitenda vyema, HUTAPATA KIBALI? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde”

1Samweli 1:17 “Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.

18 Naye akasema, Mjakazi wako na AONE KIBALI MACHONI PAKO. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukukunjamana tena”. 

KWA WATU:

Kutoka 11:3 “Bwana akawapa watu hao KIBALI MACHONI PA WAMISRI. Zaidi ya hayo, huyo Musa alikuwa ni mkuu sana katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake”

Esta 2:15 “Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona”

KWA WAKUU NA WAFALME:

Mwanzo 39:21 “Lakini Bwana akawa pamoja na Yusufu, akamfadhili, AKAMPA KIBALI machoni pa mkuu wa gereza.

22 Mkuu wa gereza akawatia mkononi mwa Yusufu watu wote waliofungwa, waliomo gerezani; na yote yaliyofanyika humo ndiye aliyeyafanya”

1Samweli 16:22 “Kisha Sauli akapeleka watu kwa Yese, akasema, Tafadhali, mwache Daudi asimame mbele yangu; maana AMEONA KIBALI machoni pangu”.

1Samweli 27:5 “Daudi akamwambia Akishi, Sasa kama nimeona KIBALI MACHONI PAKO na nipewe mahali katika miji hii mmojawapo mashambani, nipate kukaa huko; mbona mtumwa wako akae katika mji wa kifalme pamoja na wewe?”

Nehemia 2:4 “Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni.

5 Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, NIMEPATA KIBALI MACHONI PAKO, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga”

Esta 5:2 “Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye AKAPATA KIBALI machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo”

KWA MUME:

Ruthu 2:10 “Ndipo aliposujudia, akainama mpaka nchi, akamwambia, Jinsi gani NIMEPATA KIBALI machoni pako, hata ukanifahamu, mimi niliye mgeni?

11 Naye Boazi akajibu, akamwambia, Nimeelezwa sana yote uliyomfanyia mkweo, tangu alipokufa mumeo; na jinsi ulivyowaacha baba yako na mama yako, na nchi yako uliyozaliwa, ukawafikilia watu usiowajua tangu hapo”.

Esta 2:17 “Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye AKAPATA NEEMA NA KIBALI machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti”

KWA MUNGU PAMOJA NA WANADAMU:

1Samweli 2:26 “Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa Bwana, na kwa watu pia”

Mithali 3:4 “Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe”

BWANA AKUBARIKI.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.

Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)

MAPAMBO YA WANAWAKE WALIOUKIRI UCHAJI WA MUNGU.

WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU

JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?

Rudi nyumbani

Print this post

Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.(Yakobo 5:9)

SWALI: Biblia inamaana gani inaposema “Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango”.

Yakobo 5:9  Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.


JIBU: Neno la Mungu halitoi nafasi ya sisi, kunung’unikiana kwasababu yoyote. Aidha ya kuonewa, au kudhulumiwa, kuaibishwa au kufanyiwa jambo ambalo halikupasa utendewe, Manung’uniko ni zao la kutokuwa na uvumilivu. Na kwamba tukifanya hivyo basi, tafsiri yake ni kuwa tunamfanya Mungu naye aghahiri uvumilivu wake kwetu.

Lakini anatoa, suluhisho, kwamba hayo tuyaache mikononi mwake. Kwasababu yeye ndio mwamuzi wetu. Na kwamba, sio tu mwamuzi lakini  ni mwamuzi ambaye yupo mlangoni. Akiwa na maana kuwa Kristo yupo karibu sana na maonevu, au dhuluma hizo, na kwamba yeye mwenyewe atalipa, wala hatakawia, kwasababu yupo mlango.

Atalipa aidha kwa wakati huu huu duniani,  au siku ile ya mwisho wa Hukumu. Kwake yeye ni lazima haki itendeke. Pia kwa upande mwingine anataka uogope kwasababu ukinung’unika yeye hayupo mbali kukusikia.

Wafilipi 4:5  Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa, popote tusimamapo kutoa malalamiko, laumu, kuhesabu makosa, n.k. basi tutambua kuwa Kristo yupo hapo hapo katikati yetu kutusikia. Hivyo tusiwe wepesi ya kunena, bali tujifunze kuwa wavumilivu katika mambo yote. Ili Mungu atuachilie neema yake.

Bwana akubariki.

Je! Umeokoka? Je, umebatizwa katika ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo? Kama ni hapana, basi wakati ndio huu, tubu dhambi zako, kwa kumwamini Yesu upokee ondoleo la dhambi zako, Na Bwana atakupa kipawa cha Roho wake Mtakatifu.

Ikiwa upo tayari kumkabidhi leo maisha yako. Basi  fungua hapa kwa mwongozo huo. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MWAMUZI WA KWELI:

“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?

Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini kusema Marko 2:19″walioalikwa harusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao?”

MBINGUNI YUPO NANI SASA?

Rudi nyumbani

Print this post

NI YESU YUPI UNATEMBEA NAYE?

NI ALIYEFIFIA MAVAZI AU MWENYE MAVAZI MEUPE?

Yesu anajifunua kwa watu kulingana na jinsi mtu huyo anavyotembea naye. Wapo watu wanatembea na Bwana Yesu katika mng’ao wake wa ajabu. Lakini wapo wanaotembea naye katika hali ya kawaida sana. Utajiuliza kwa namna gani.

Wakati mwingi sana, Yesu alipokuwa na wanafunzi pamoja na makutano. Zaidi ya asilimia 98 ya maisha yake, alikuwa hana tofauti na watu wengine wowote. Kiasi kwamba akijichanganya kati ya watu 10, huwezi mtofautisha na yoyote, kimwonekano. Ndio maana wengi, walishindwa kumngundua, alipokuwa na watu soma (Yohana 18:7).

Lakini kuna wakati, alibadilika sura, mpaka mwonekano wake. Tutaona ni nini kilichomfanya awe vile jambo lililowafanya mitume wake kumchukulia kitofauti sana tangu ule wakati.

Marko 9:2  “Hata baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani, peke yao; akageuka sura yake mbele yao; 3  mavazi yake yakimeta-meta, meupe mno, jinsi asivyoweza dobi duniani kuyafanya meupe.

4  Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu. 5  Petro akajibu, akamwambia Yesu, Rabi, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu, kimoja chako wewe, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. 6  Maana, hakujua la kunena, kwa kuwa waliingiwa na hofu nyingi.

7  Kisha likatokea wingu, likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, msikieni yeye. 8  Mara hiyo walipotazama huku na huku, hawakuona mtu pamoja nao ila Yesu peke yake.

9  Na walipokuwa wakishuka mlimani aliwakataza wasimweleze mtu waliyoyaona, hata Mwana wa Adamu atakapokuwa amefufuka katika wafu”.

Sababu iliyowafanya Petro, Yohana, na Yakobo, kumwona Bwana katika mwonekano ule. Ni mahali walipokwenda naye. Walikwenda naye mlimani “KUOMBA”. Maombi ndio yaliyopelekea, Yesu abadilike ghafla mbele yao na kuwa na ule utukufu wake wa asili.

Vivyo hivyo na sisi ili tumwone Kristo katika utukufu wake mkamilifu katika maisha yetu, Tupende maombi. Ukiwa mvivu katika kuomba, Yesu atakuwa ni wa kufifia maishani mwako. Hutafurahia uweza wake mtimilifu katika maisha yako, hutafurahia wokovu wako. Mfanye awe kama JUA kwako, ang’ae kweli kweli, mpe nafasi kwasababu yeye ndio Nuru ya ulimwengu. Penda maombi, kila siku omba, kutana naye hapo, hudhuria mikesha sana, omba kwa bidii, ondoa uvivu.

 Usipomruhusu Yesu akupangie maisha yako, kimaombi, shetani atakusaidia kuyapanga.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

Tofauti kati ya maandiko na Neno ni ipi?

MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.

FAIDA ZA MAOMBI.

USIYAACHE MAVAZI YAKO NA KWENDA UCHI!

Rudi nyumbani

Print this post

JE! MWAMBA HALISI NI NINI KULINGANA NA BIBLIA?

Je! Umejengwa kweli juu yake?

Ukimuuliza mtu, mwamba ni nini, ni rahisi kukujibu YESU. Jibu ambalo ni sahihi, maandiko yanatuthibitishia hilo Yesu kuwa Yesu ni mwamba (Mathayo 21:42, 1Wakorintho 10:4). Lakini lazima ufahamu pia  MWAMBA mwenye anasemaje, kuhusu yeye mwenyewe alivyo.

Ni maneno ambayo tunayasoma lakini si rahisi kuyatafakari kwa ukaribu, embu tusome tena, halafu utaona mwamba alimaanisha nini. (Zingatia vifungu vilivyo katika herufi kubwa) Soma kwa utulivu.

Mathayo 7:24  Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na KUYAFANYA, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

25  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26  Na kila asikiaye hayo maneno yangu ASIYAFANYE, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27  mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.

28  Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29  kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.

Umeelewa? Vema hayo maneno?

Kumbe mtu  yeyote anayesikia maneno ya Yesu. Hapo hapo huwa anaanza ujezi.

Lakini tofauti inakuja mahali anapokwenda kujengea,. Yule aliyejenga kwenye mchanga tafsiri yake Yesu anasema, anasikia, lakini hayatendei kazi (Hayafanyi), aliyoyasikia. Hivyo hapo Mchanga, ni KUTOTENDA.

Lakini Yule mwingine aliyekwenda kwenye mwamba tafsiri yake ni anasikia lakini pia anatenda. Hivyo MWAMBA, ni kutenda.

Mwamba sio kumjua Yesu ndugu, mwamba sio kusoma sana biblia na kujua mafumbo na siri zote zilizo katika biblia, mwamba sio kujua kujua tafsiri zote za kigiriki na kiebrania kwenye maandiko, mwamba sio kujua kufundisha vema biblia,.. Sio hivyo vyote.

Mwamba ni KULITENDEA KAZI NENO, Unalolisikia kwake. Hilo tu. Sio kumjua Yesu.

Hatari iliyopo leo, miongoni mwa wakristo wengi, ni kwamba tumejengwa juu ya mafundisho mengi. Lakini hatujajengwa juu ya kutendea kazi mafundisho tunayofundishwa. Ndugu fundisho halikusaidii kuyashinda majaribu, au tufani za mwovu, au dhoruba, au pepo, hapo unafanya kazi ya kuchosha tu,kudumu katika kusikia, kusoma, kusikiliza, bado si suluhisho, kusema nimebarikiwa, nimefunguliwa ufahamu, bado hakukufikishi popote, kama HUTALIISHI hilo Neno.

Ukiwa ni wa kufanya bidii kuliishi NENO moja, wewe ni imara sana kuliko Yule mwenye kujiona anaijua biblia yote

Penda Utakatifu, penda usafi wa moyo, penda kupiga hatua rohoni. Penda matendo mema.

Bwana akubariki.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

NAYAJUA MATENDO YAKO.

Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)

Ngome ni nini?  Kwanini Mungu anafananishwa na ngome?

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?

Rudi nyumbani

Print this post

Kuna tofauti gani kati ya “Mwivi” na “Mwizi”?

Swali: Kwanini katika biblia lisitumike neno “Mwizi” na badala yake linatumika neno “Mwivi”…Mwivi ni nini?


Jibu: Mwivi na Mwizi ni Neno moja, lenye maana moja.. isipokuwa ni lugha mbili za nyakati mbili tofauti.

Kiswahili kilichotumika katika kutafsiri biblia ni Kiswahili cha zamani, kilichoitwa “kimvita” ambacho ndicho kimebeba maneno ambayo hatuyaoni katika Kiswahili cha sasa, na mojawapo ya maneno ndio kama hayo “Mwivi na wevi” ikimaanisha “mwizi na wezi”. Ndio maana katika biblia yote huwezi kukuta neno Mwizi, badala yake utakuta mwivi (Soma Kutoka 22:2, Ayubu24:14, Zaburi 50:18, Mithali 6:30, Yoeli 2:9, Luka 12:39 n.k )

Maneno mengine ya kimvita (Kiswahili cha zamani) ambayo mengi ya hayo hayatumiki sasa ni pamoja na “jimbi” badala ya “Jogoo”“Kiza” badala ya “Giza”….”Nyuni” badala ya “ndege”…. “Kongwa” badala ya “Nira” na mengine mengi.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba “Mwivi” na “Mwizi” ni Neno moja, lenye maana ile ile moja (ya mtu anayeiba).

Lakini mbali na hilo, maandiko yanatufundisha kuwa Bwana YESU atakuja kama “Mwivi”..

Ufunuo 16:15 “(Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake)”

Je umewahi kujiuliza ni kwanini aje kama Mwivi na si Askari?.. Kwa upana juu ya hilo basi fungua hapa >>ANAKUJA KAMA “MWIVI” NA SI KAMA “ASKARI” FANYIKA CHOMBO CHA THAMANI.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.

Nini maana ya Mithali 6:30 Watu hawamdharau mwivi, Akiiba ili kujishibisha

OKOA BADALA YA KUANGAMIZA!

Nini maana ya ELOHIMU?

Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).

Rudi nyumbani

Print this post

Ipi tofauti kati ya Kalvari na Golgotha?

Swali: Je Neno “Kalvari” tunalisoma wapi katika biblia?, na tofauti yake na Golgotha ni ipi?


JIbu: Katika biblia ya Kiswahili hakuna neno “Kalvari”, bali kuna neno “Golgotha” ambalo tunalisoma katika kitabu cha Yohana 19:17

Yohana 19:17 “Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, GOLGOTHA.

18  Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati”.

Maana ya Neno “Golgotha”, tayari biblia imeshatoa tafsiri yake hapo  kwenye mstari wa 17 kuwa ni “Fuvu la Kichwa”

Sasa neno “Kalvari” maana yake ni nini?

Neno Kalvari linapatikana katika tafsiri chache za lugha ya kiingereza, ambalo asili yake ni lugha ya Kilatini “CALVARIAE” lenye maana ile ile ya “Fuvu la kichwa cha mtu”.

Hivyo “Kalvari” na “Golgotha” ni Neno moja lenye maana moja, isipokuwa lugha tofauti, ni sawa na neno  “church” na “kanisa” ni kitu kimoja ila lugha tofauti.

Kufahamu kwa upana ufunuo uliopo nyuma ya Golgotha, (Fuvu la kichwa), basi fungua hapa >>>FUVU LA KICHWA.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)

Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?

AMELAANIWA AANGIKWAYE MSALABANI.

ALIFANYIKA SADAKA KWA AJILI YETU!

Biblia inaposema Yesu ameketi mkono wa kuume inamaana gani?

Rudi nyumbani

Print this post

Wale waliowekewa tayari ufalme ni akina nani?. (Mathayo 20:23).

Swali: Je wale waliowekewa tayari ni akina nani na kwanini Bwana Yesu aseme maneno yale?


Jibu: Tuanzie kusoma mstari wa 20..

Mathayo 20:20 “Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.

21  Akamwambia, Wataka nini? Akamwambia, Agiza kwamba hawa wanangu wawili waketi mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika ufalme wako.

22  Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza.

23  Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, SINA AMRI KUWAPA, BALI WATAPEWA WALIOWEKEWA TAYARI NA BABA YANGU”.

Ili tuelewe vizuri, hebu tafakari mfano huu.. “wanafunzi wawili wamemfuata mwalimu wao wa darasa na kumwomba washike nafasi ya kwanza kitaifa na mwingine ashike ya pili kitaifa katika mitihani yao ya mwisho wa kuhitimu”.. Unadhani jibu la mwalimu litakuwa ni lipi?..

Bila shaka mwalimu atawauliza.. je! Mtaweza kusoma kwa bidii??.. Na kama wale wanafunzi watajibu NDIO!.. Bado Mwalimu hataweza kuwapa hizo nafasi, bali atawaambia mimi sina mamlaka ya kuwapa bali “Wasahishaji watakaosahisha mitihani ya wote ndio watakaotoa majibu ya mitihani yenu na kuwapanga kama mmestahili hizo nafasi au la”..

Ndicho Bwana YESU alichowaambia hawa wana wa Zebedayo!.. ambao walienda kumwomba nafasi ya kuketi pamoja naye katika kiti chake.. na jibu la Bwana YESU likawa, ni “kukinywea kikombe”.. maana yake kukubali mateso kwaajili yake!.. Na wao wakajibu “wataweza”.. Lakini jibu la Bwana likawa “Nafasi hizo watapewa waliowekewa tayari”..maana yake waliostahili.

Na hao waliostahili ni akina nani?

Ni wale watakaofanya vizuri Zaidi ya wengine wote katika mambo yafuatayo.

   1. KUKINYWEA KIKOMBE.

Kikombe alichokinywea Bwana Yesu ni kile cha Mateso ya msalabani (Soma Mathayo 26:39), kutemewa mate, kupigwa Makonde, kuvikwa taji ya miiba, na kugongomelewa misumari mikononi..

Na yeyote ambaye atakubali kuteswa kwaajili ya Kristo, na si kwaajili ya mtu au kitu kingine chochote, basi yupo katika daraja zuri la kumkaribia Kristo katika siku ile kuu.

  2. KUBATIZWA UBATIZO WA BWANA YESU.

Marko 10:38  “Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au KUBATIZWA UBATIZO NIBATIZWAO MIMI?”

Swali Ubatizo aliobatizwa Bwana YESU KRISTO ni upi?…. si mwingine Zaidi ya ule wa kufa, kuzikwa na siku ya tatu kufufuka, na kupaa juu (soma  Luka 12:50), Na ubatizo huu mpaka sasa hakuna rekodi ya wazi ya yoyote aliyeupitia..

Ubatizo tubatizwao sasa ni ule wa maji mengi, ambao ni ishara ya kufa na kufufuka na Kristo (Wakolosai 2:12), kwamba tunapozamishwa katika maji mengi na kuibuka juu, ni ishara ya kufa pamoja na Kristo na kufufuka pamoja naye… Lakini Ule hasa wa kufa na kufufuka na kupaa, hakuna rekodi ya wazi ya aliyeupitia.

Isipokuwa unawezekana ndio maana tunasoma katika Ufunuo 11, kuwa wale washahidi wawili, ni miongoni mwa watakaoupitia..

Ufunuo 11:10 “….Nao wakaao juu ya nchi wafurahi juu yao na kushangilia. Nao watapelekeana zawadi wao kwa wao, kwa kuwa manabii hao wawili waliwatesa wao wakaao juu ya nchi.

11  NA BAADA YA SIKU HIZO TATU U NUSU, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.

12  WAKASIKIA SAUTI KUU KUTOKA MBINGUNI IKIWAAMBIA, PANDENI HATA HUKU. WAKAPANDA MBINGUNI KATIKA WINGU, ADUI ZAO WAKIWATAZAMA”.

Je umempokea YESU?, Fahamu kuwa tunaishi katika siku za mwisho, na Kristo yupo mlangoni.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mafundisho mengine:

USIWE ADUI WA BWANA

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA

JE! UNAYO NAFASI MBINGUNI?

UWE KIKOMBE SAFI 

Nini maana ya kikombe cha maji ya baridi(Mathayo 10:42)?

Rudi nyumbani

Print this post