Jibu: Turejee Isaya 9:6,
Isaya 9:6 “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; NA UWEZA WA KIFALME UTAKUWA BEGANI MWAKE; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani”.
Katika jeshi lolote lile, liwe la Ulinzi au la wananchi, kunakuwa na vyeo. Si askari wote wanafanana kimadaraka, wapo wenye madaraka makubwa na wapo wenye madaraka madogo. Na utaona ili kumtofautisha askari mmoja na mwingine kimadaraka, wanakuwa na sare ambazo zina alama Mabegani mwao, alama hizo ni maarufu kama “Nyota”.
Sasa nyota zile mabegani si ‘urembo’ bali zinafunua mamlaka Fulani/cheo cha yule askari.. ndio utaona wale wenye nyota nyingi basi wanakukuwa na Vyeo vikubwa Zaidi na mamlaka makubwa Zaidi.
Kwamfano utaona “Jenerali wa Jeshi” ndiye mtu mwenye cheo kikubwa Zaidi katika jeshi, na mara nyingi anakuwa ameshapitia ngazi zote za chini kama Ukoplo, Brigedia Jenerali, meja-Jenerali, au luteni-Jenerali.
Na mpaka amefikia ngazi hiyo ya Ujenerali, maana yake ndiyo ngazi ya juu na hakuna nyingine. Na anatofuatishwa na Askari mwingine si kwa sura, jinsia au kimo, bali anatofautishwa na “ule uwezo uliopo begani mwake” (yaani zile nyota nne begani mwake). Askari wengine waonapo zile nyota mabegani basi watapiga saluti na kutii..
Sasa serikali nyingi za kidunia zimenakili baadhi ya mambo kutoka katika Serikali iliyo juu (yaani ya mbinguni).
Kama yupo Jenerali wa jeshi la wanadamu, vile vile yupo JENERALI MKUU WA JESHI LA MBINGUNI, na huyo si mwingine Zaidi ya BWANA YESU KRISTO!. Ambaye ana nyota zi kifalme begani mwake, nazo ndizo hizo zilizotajwa (MSHAURI WA AJABU, na MUNGU MWENYE NGUVU, na BABA WA MILELE na MFALME WA AMANI).
Hiyo ndio maana biblia inamtaja BWANA YESU KRISTO kama BWANA WA VITA, na MFALME WA WAFALME, Kwasababu yeye ni Jenerali Mkuu.
Ufunuo 17:14 “Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu”.
YESU pekee ndiye njia ya UZIMA, na Bwana wa vita, na Mfalme wa Wafalme, ambaye hana wa kulinganishwa naye, kwasababu ndiye mwenye mamlaka yote ya mbinguni na duniani (Mathayo 28:18).
Je umemwamini Huyu Mkuu (YESU)?.. Je bado hujaona tu kuwa hakuna wokovu kwa mwingine yoyote isipokuwa yeye?..bado hujaona tu kuwa hakuna mwenye nguvu nyingi Zaidi yake yeye?.
Yeye pekee yake ndiye mwenye uwezo wa kufungua na kufunga, leo hii kama utampokea Basi atakufungua katika vifungo vya dhambi na mizigo yote ya adui shetani (Mathayo 11:28), vile vile atakufungua na vifungo vyote vinavyokutesa, kwasababu Bega lake linahubiri UWEZA MKUU.
Isaya 22:22 “Na ufunguo wa nyumba ya DAUDI NITAUWEKA BEGANI MWAKE; yeye atafungua wala hapana atakayefunga; naye atafunga wala hapana atakayefungua.”
Bwana akubariki.
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?
Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?
Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.
Je ni kweli hakuna aliyepaa mbinguni zaidi ya Mwana wa Adamu? (Yohana 3:13)
SWALI: Nini maana ya kumsulibisha mwana wa Mungu mara ya pili, na kumfedhehi kwa dhahiri?
JIBU: Neno hilo tunalisoma katika kifungu hiki;
Waebrania 6:4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
Anazungumzia kundi la watu ambao walishapitishwa katika hatua zote tano (5), za uzuri wa Mungu na matendo makuu ya Mungu ndani ya maisha ya mwaminio. yaani.
i)Kupewa nuru ya injili,
ii)kuonja kipawa cha mbinguni,
iii) kufanywa mshirika wa Roho Mtakatifu,
iv) kulionja Neno zuri la Mungu,
v) na kuonja nguvu za zamani zijazo.
Kwamba watu wa namna hii wakianguka, kamwe haiwezekani kuwafanya wakatubu upya.
Lakini halengi kundi la watu walio wachanga kiroho, au waliorudi nyuma kwa kukosa maarifa, au kudanganywa au kwasababu nyingine zozote, bali kundi la watu ambao wanamjua vema Mungu wao, na wanaelewa kabisa wanachokwenda kukifanya ni nini, Ni watu ambao wameshaonja Baraka na neema zote za Bwana, hawa ndio haiwezekani kuwageuza upya wakatubu pale wanapoanguka. Biblia inasema wanachofanya ni sawa na kumsulibisha Yesu mara ya pili.
> Sasa swali linakuja wanamsulibishaje mwana wa Mungu mara ya pili, na wanamfedhi kwa namna gani?
Tengeneza, picha mume amemfumania mke wake katika uzinzi. Sasa kutokana na yale maumivu ya kusalitiwa akataka kumfukuza, lakini Yule mwanamke akamlilia kwa kumwomba msamaha, akikiri kuwa hatarudia tena uovu ule, asamewapo. Basi Yule mwanamume akamsamehe, na kuachilia uchungu wote, maisha yakaendelea. Lakini baada ya kipindi kupita Yule muma akamfumania tena mke wake katika uzinzi, Unadhani kitendo kile kitanyanyua hisia gani kwa Yule mwanaume?
Bibla shaka ataona ni kama ametoneshwa majeraha ambayo yalishapona zamani kwa gharama kubwa alizoingia kumsamehe wakati ule. Ni sawa, anakumbushwa yale maumivu ya mwanzo. Ndivyo ilivyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo, pale unapoacha wokovu ambao umeshaujua uzuri wake, kisha ukarudia yale yale maisha ya kale, ni sawa na kumrudishia Kristo maumivu aliyoyapata pale msalabani siku ile alipokusamehe dhambi zako. Unamsulibisha mara ya pili. Unampa mateso ambayo tayari alishayamaliza, unakuwa huna tofauti na wale waliompiga pale masalabani.
>Lakini hapo anaposema unamfedhehi kwa dhahiri. Anamaana ya unamzalilisha kwa wazi (yaani hadharani).
Chukua tena mfano; Mtu ameingia gharama ya kukupikia chakula kizuri cha heshima, akitarajia kuwa utakapokula utakifurahia na kukipenda. Lakini ulipopewa kukila ulionyesha kukipenda pale mwanzoni, mara ghafla ukakichukia na kukitema mbele yake, na baadaye ukakimwaga, na baada ya hapo ukaenda kununua chakula chako kingine,ukala tena mbele yake. Jiulize Yule mpishi wako atajisikiaje?
Ataona umemfedhi, umemzalilisha, kama vile kazi aliyoifanya kwako ni bure, . Ndivyo Bwana, anavyoona, wale wanaorudi nyuma. Wanamdhalilisha, kuifanya kama vile kazi ya msalaba, inamapungufu fulani, ni ujinga tu uliofanyika pale, Roho Mtakatifu ni uongo, nguvu za Mungu ni dhaifu. Na ndio maana umeamua kugeukia mambo ya kidunia uliyokuwa umeyaacha zamani.
Hivyo hatua kama hii, ni mbaya sana. Vifungu hivi ni kutufundisha zipo hatari nyingi kwa mkristo anayerudi nyuma kwa makusudi. Kamwe usiruhusu jambo hilo maisha mwako.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?
Mata ni kitu gani na imebeba ujumbe gani kiroho?
Jibu: Turejee,
Mwanzo 27:2 “Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.
3 Basi, nakuomba, chukua MATA yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; 4 ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa”.
“Mata” Ni jina jingine la “Silaha”. Kwahiyo badala ya kutumia neno “silaha” ni sahihi pia kutumia neno “Mata”.
Kwahiyo mstari huo wa tatu (3) ni sahihi kuuweka hivi,… “chukua SILAHA yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo ”
Na silaha hiyo inaweza kuwa mkuki, mshale au upanga, lakini katika andiko hilo silaha (Mata), iliyomaanishwa pale ni “Mshale”. Na kwanini ni mshale na si upanga wala mkuki?.. ni kwasababu kuna Podo imetajwa pale na upinde..
Maana yake huwezi kubeba upanga na upinde bila mshale, hivyo ni wazi kuwa Mata iliyomaanishwa pale ni mshale, kwasababu kuna upinde na Podo.
Sasa kwa maarifa kuhusu “Podo” na ufunuo wake kiroho waweza fungua hapa >>> Podo ni nini na umuhimu wake ni upi rohoni?
Sasa hizi zote ni silaha za mwili, lakini biblia inatufundisha kuwa zipo silaha za roho ambazo kila mkristo ni lazima azivae, na silaha hizo tunazisoma katika kitabu cha Waefeso 6:10-18, ambazo ni Chapeo ya Wokovu, Dirii ya Haki, Ngao ya Imani, Kweli, Upanga wa Roho, na Utayari miguuni pamoja na sala na maombi.
Na kwa silaha hizo pekee ndio tutaweza kumshinda adui yetu shetani, kwa mapana kuhusiana na silaha hizi jinsi ya kuvizaa na namna zinavyotenda kazi fungua hapa >>>MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
UTHABITI WA AGANO LA MUNGU KWA MKRISTO.
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.
Nini maana ya Mithali 21:1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana;
SWALI: Na je! Walawi na makuhani katika kanisa la sasa ni watu wa namna gani?
JIBU: Mungu alilichagua kabila moja kati ya kumi na mbili liwe kabila lake takatifu litakalosimama katika kazi na shughuli zote za kidini na ibada Israeli.
Sasa katikati ya hawa walawi ndipo walipotolewa makuhani ndani yake. Hivyo makuhani wote walikuwa ni walawi lakini walawi wote si makuhani.
Kwasasa, kila mkristo, ni Mlawi. Kwasababu tayari ameshapewa uwezo ndani yake na karama, ya kuifanya kazi ya Mungu pale tu anapookoka. Kila mmoja ni kiungo kwa mwenzake ndani ya kanisa. Lakini mkristo anabadilika kutoka kuwa mlawi mpaka kuwa kuhani pale anaposimama hasaa kwa ajili ya huduma/kazi ya Mungu kwa watu wake.
Anapobeba maono Fulani, labda tuseme kulichunga kanisa, huyo ni kuhani wa Mungu, na hivyo anaposimama na kuwabariki watu basi Baraka hizo huwafikia watu moja kwa moja kutoka kwa Mungu, mfano tu wa makuhani wa agano la kale. Au anapotumika katika kuwafundisha, kuwaombea wengine, kuwasimamia wengine, haijalishi ngazi aliyopo, au mahali au jinsia, huyo rohoni ni kuhani wa Mungu.
Hivyo kila mkristo anaouwezo wa kuwa kuhani wa Mungu, kwasababu lengo la Mungu ni sote tuwe makuhani wake, sio tu walawi, Na Yesu Kristo Bwana wetu akiwa ni kuhani Mkuu.
1Petro 2:9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Je! Kristo yupo moyoni mwako?
Kama ni hapana, basi wakati ndio huu, mgeukie, akusamehe dhambi zako, kwa kutubu na kumaanisha kabisa kuziacha, naye atakukomboa. Ikiwa upo tayari kwa ajili ya mwongozo huo, basi waweza fungua hapa kwa mwongozo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Shalom.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kwa namna gani tumefanyika Makuhani na Ufalme?.(Ufunuo 1:6)
WALAWI WALIKUWA WENYE MIOYO YA ADILI KWA KUJITAKASA KULIKO MAKUHANI.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Kwanini Yesu aliwaambia wale wakoma wakajionyeshe kwa makuhani?
SWALI: Nini maana ya Kumbukumbu 25:11
Kumbukumbu 25:11 “Washindanapo waume wao kwa wao, akakaribia mke wa mmojawapo, ili kumwokoa mumewe katika mkono wa ampigaye, yule mke akatoa mkono wake, na kumkamata tupu yake; 12 umkate ule mkono wake, lisiwe na huruma jicho lako”
JIBU: Bwana asifiwe, Haya ni mafundisho maalumu wayahusuyo wana-ndoa. Lakini pia kanisa la Kristo.
Kama ukiutafakari mstari huu, utaona picha ya mwanamke mwenye huruma, ambaye, ameona mume wake, anapigana na adui yake, na pengine alikuwa anakaribia kushindwa. Hivyo kwasababu ya upendo wake kwa mumewe, akaamua kwenda kumwokoa. Lakini tunaona njia aliyoitumia badala imletee alilolitarajia, ikamletea matatizo yeye mwenyewe.
Kwasababu gani? Kwasababu alikwenda kugusa sehemu zake za siri, Na hiyo ikawa kosa kwake, lililostahili adhabu ya kukatwa mkono. Laiti kama angemkamata mahali pengine labda tuseme mguuni, au penginepo, ni wazi kuwa kusingekuwa na adhabu yoyote au adhabu iliyo kali namna ile.
Ni mipaka ya mwanamke awapo ndani ya ndoa yake. Fikiria hata kwa adui ya mume wake huyu mwanamke, hukupaswa kuvuka mipaka ya kindoa, si zaidi kama angefanya hivyo kwa rafiki wa karibu wa mume wake ndio ingekuwa kosa kubwa kabisaa?. Leo hii kumekuwa na migogoro mingi ndani ya ndoa, na ukitazama utagundua tabia ya wanawake kutojiwekea mipaka yao, wakutanapo na wanaume wengine wa nje.
Kwamfano mwanamke yupo kazini. Halafu Boss wake/ mfanyakazi mwenzake anazungumza mazungumzo ya mizaha, ya kizinzi, utaona na yeye analiridhia hilo, au kulifurahia au anaona ni kawaida tu. Anashindwa kujiwekea mipaka, Anaipoteza nidhamu yake, anaruhusu mazoea yaliyopitiliza ambayo hayampasi mtu kama yeye kuwa nayo. Sasa hiyo ni hatari kubwa.
Wewe kama mwanamke unapaswa ujiwekee mipaka ya hali ya juu. Ukiona migororo inaendelea baina ya wanaume, jiwekee mipaka ya kitabia na kimwenendo. Uwe salama, ili mkono wako usifike kusikostahili. Uvaaji wako, usemi wako, uwe kama mtu aliye kwenye “KIFUNGO” cha ndoa. Watu wakuheshimu, wenye mizaha wakuonapo wakae kimya. Usiruhusu kabisa mazungumzo yako na mtu mwingine yafike kwenye maeneo ya sirini, iwe kwenye simu, ofisini, njiani, shuleni, mtaani, nyumbani, au popote pale. Weka MLANGO mkubwa wenye makomeo ya chuma . Mazungumzo hayo yawe na mume wako tu, na sio mwingine yoyote.
Halikadhalika inatupa na picha ya rohoni pia. Sisi kama kanisa ni lazima tufahamu kuwa wote ni “WAKE” wa Bwana wetu Yesu Kristo. Na hivyo anataka tuwe na tahadhari tuendapo kumuhubiri yeye kwa watu wa nje, tujichunge tusijaribiwe wenyewe, kwa vitendo vyao. Kwasababu itatugharimu kinyume chake.
Tukutanapo na wazinzi kuwahubiria, tusivutwe kwenye uzinzi wako, tukutanapo wa watukanaji, tusirudishe matusi, tukutanapo na wenye fedha, tusigeuzwe injili yetu. Bali tubaki kwenye mipaka yetu ile ile.
Wagalatia 6:1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Nini maana ya Mithali 16:30 Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka;
Maana ya Mithali 29:21 “Amtunduiaye mtumwa wake tangu utoto, Mwisho wake atakuwa ni mwanawe”
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU NDOA.
USIONDOE ALAMA YA MPAKA ILIYOWEKWA NA MABABA.
Kwanini kuwe na kitabu Cha kumbukumbu la Torati na kwanini kiitwe vile?
Swali: Kwani kulikuwa na ubaya gani, wa bwana yule kurudisha talanta ile moja?, kwani hakupoteza kitu wala hajaleta hasara yoyote?..je kulikuwa na sababu gani ya yeye kuhukumiwa vile?.
Jibu: Ili tuweze kuelewa vizuri sababu ya mtumwa yule kuhukumiwa vile, tuisome habari yenyewe kwa uchache..
Mathayo 25:14 “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita WATUMWA WAKE, akaweka kwao MALI ZAKE.
15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri”.
Nataka tuzingatie hayo maneno mawili “Watumwa wake” na “Mali zake”.
Kwa haraka tukiisoma habari hii tunaweza kutafakari kuwa huyu mtu aliwekeza mali zake kwa “rafiki zake” au “ndugu zake”..
Ingekuwa heri kama ingekuwa ni “rafiki zake” au “ndugu zake” kwani hata wasingeleta faida yoyote angeweza kuwaelewa lakini aliwekeza mali zake kwa “watumwa wake” ambao ni watu anaowalipa mshahara huenda kila siku au kil amwisho wa mwezi.
Sasa ili tuelewe vizuri, tengeneza picha una biashara yako (labda duka) halafu umeajiri mfanya kazi pale na kukubaliana naye mshahara, na ukaondoka na kurudi jioni na kukuta hajafanya kazi yoyote na Zaidi anakuambia fedha zako za mtaji zipo pale pale hajazigusa.
Bila shaka utachukizwa naye..kwanini?..cha kwanza ulitegemea kupata faida ndio maana wewe ukamweka pale, pili mshahara wake unatokana na faida katika hiyo kazi, kwa utendaji wake..
Kwahiyo kama hatafanya kazi yoyote na mwisho wa mwisho wa siku au mwezi atataka mshahara je utamlipa nini?…maana utakapofika mwisho wa mwezi atakudai mshahara, na wewe umeshaingia naye mkataba wa kumlipa..
Kwahiyo ni wazi kuwa ni lazima utakasirika, kwasababu kutokufanya kwake kazi ni hasara kwako, kwasababu mwisho wa siku ni lazima utamlipa, hivyo anakurudisha nyuma hata kama hajagusa mtaji wako, lakini mwisho wa siku utaathirika wewe katika wakati wa kumlipa mshahara..Hivyo ni hasara!!!
Ndicho kilichowatokea yule mtumwa aliyeficha talanta aliyopewa na bwana wake, maana yake ni kweli kairudisha ile talanta kama ilivyo, lakini mwisho wa mwezi atataka mshara (kwasababu yeye ni mwajiriwa na si ndugu/rafiki).. sasa bosi wake atatolea wapi fedha ya kumlipa ikiwa hajazalisha chochote?..
Ndio maana bwana wake akamwambia ni heri hata angeipeleka kwa watoa riba kuliko kuificha ardhini.
Hili ni fundisho kamili kwa wakristo kwamba vipawa na karama na uwezo tuliojaliwa na Bwana basi tutumie katika kumtumikia Mungu pasipo udhuru, kwasababu sisi ni watumwa wake!, ametuweka kwa faida yake…
Bwana atusaidie tusifiche talanta zetu ardhini bali tuzitendee kazi au tuzipeleke kwa watoa riba.
Mathayo 25:27 “basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”
Kufahamu kwa mapana maana ya “kupeleka fedha kwa watoa riba”, basi fungua hapa >>>Watoao riba ni akina nani? (Mathayo 25:27)
Maran atha!
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
JINSI YA KUISHINDA HALI YA MSONGO WA MAWAZO.
BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”
Swali: Je Bwana alimaanisha nini kusema “ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba” Je alikuwa na maana gani kusema vile?
Jibu: Mathayo 2:27 “basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
28 Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi”
Ukisoma habari hiyo kuanzia juu utaona ni mfano uliokuwa unazungumzia watumwa ambao Bwana wao aliwapa talanta, na yule aliyepokea talanta tano, alizalisha nyingine tano, huenda kwa biashara aliyoifungua…na yule aliyepokea talanta mbili naye pia akazalisha nyingine mbili huwenda kutokana biashara aliyoifungua..
Lakini yule aliyepokea Moja, hakuenda kuifanyia kazi badala yake alienda kuificha chini ya ardhi, na siku ya mwisho akamrejeshea Bwana wake talanta ile ile moja aliyoipokea kutoka kwa Bwana wake, Lakini tunasoma Bwana wake akamkemea na kumwambia kuwa ni mtumwa “mbaya na mlegevu”.
Maana yake kama ameshindwa kabisa kwenda kuifanyia kazi basi angalau angeiweka kwa watoao riba, ..maana yake akakopeshe watu ambao wao wataenda kuizungusha ile fedha na hatimaye kumrejeshea iliyo yake na faida yake, lakini huyu mtumwa hakufikiri hata hilo, badala yake alienda kuifukia chini ya ardhi..
Sasa kiroho talanta zinafananishwa na “kipawa au uwezo” wowote ambao mtu kapewa na Mungu, unaomtofautisha yeye na mwingine.
Sasa kama mtu si Mtumishi wa madhabahuni, si mchungaji, si mwalimu, si mwinjilisti wa kwenda huku na kule kuhubiri habari njema… wala haoni kama anaweza kufanya kazi moja wapo ya hizo, lakini Mungu kamjalia kauwezo Fulani cha kifedha,
Basi kuliko kukaa bila kufanya kazi yoyote ya Mungu, ni afadhali fedha zake hizo ziwe chache au nyingi, aziwekeze katika injili (maana yake awape wanaokwenda kuieneza injili huku na kule) ili matunda yatakayopatikana kupitia injili watakaohubiri wengine kwa sapoti yake, basi na yeye awe mshirika wa matunda hayo kwasababu kachangia injili hiyo.. (Hiyo ndio maana ya kuweka fedha kwa watoa riba). Yeye hajahubiri lakini kapeleka nguvu zake kwa wanaohubiri.
Lakini kama haubiri, haufanyi uinjilisti wowote, si mwalimu, si mchungaji, na hutaji hata moja ya fedha zako kuipeka kwenye injili, mwisho wake utakuwa kama wa huyu aliyeificha talanta yake ardhini.
Luka 16:9 “Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele”.
Bwana atusaidie tutumie talanta zetu vizuri.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
talanta ni nini
BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.
TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO.
Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
Swali: Biblia ina maana gani kusema Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa? Je hiki kiti cha Musa ndio kipi?
Jibu: Turejee,
Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”
“Kiti cha Musa” maana yake ni “Nafasi ya Musa”.. Leo hii tukisema mtu kaketi katika kiti cha Uraisi, maana yake ni kuwa “kachukua nafasi ya Uraisi”.
Sasa Musa alikuwa na nafasi gani?
Musa alikuwa na nafasi kuu mbili (2) mbele za wana wa Israeli.
1) UALIMU.
Mtu wa Kwanza kuwafundisha wana wa Israeli HUKUMU, AMRI NA SHERIA za Mungu alikuwa ni MUSA.
Kumbukumbu 4: 14 “Bwana akaniamuru wakati ule NIWAFUNDISHE maagizo na hukumu, mpate kuzitenda katika nchi ile mtakayoivukia ili kuimiliki.
15 Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yo yote siku ile Bwana aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;
16 msije mkajiharibu nafsi zenu, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa sura yo yote, mfano wa mwanamume au mwanamke”.
Na mahubiri yake yaliendelea kuwa msingi wa marejeo kwa vizazi na vizazi mbeleni.
2) UONGOZI.
Hii ni nafasi ya pili aliyokuwa nayo Musa mbele ya wana wa Israeli:
Maandiko yanasema Mungu alimfanya Musa kuwa “Mkuu sana” mbele ya Misri na mbele ya wana wa Israeli. Kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwake, kwa lugha nyepesi alikuwa ni kama Mfalme.
Kutoka 11:3 “…Zaidi ya hayo, huyo Musa ALIKUWA NI MKUU SANA katika nchi ya Misri, machoni pa watumishi wa Farao, na machoni pa watu wake”.
Soma pia Kutoka 18:13-24, utaona nafasi ya Musa katika kuwaamua Israeli.
Sasa baada ya Musa kuondoka (yaani kufa), Mafarisayo na Waandishi wakajiweka katika nafasi yake, maana yake wao ndio wakawa WAALIMU kama alivyokuwa Musa, na pia wakajiweka kuwa VIONGOZI kama alivyoukwa Musa, kiasi kwamba maamuzi ya mwisho yalikuwa yanatoka kwao.
Lakini ni heri kama wangekuwa wameketi kwenye nafasi hiyo ya Musa, na wakawa kama Musa..(yaani wacha Mungu kama Musa, au wapole kama Musa)..
Lakini wao walikuwa ni kinyume chake, walikuwa wanawatawala watu na kuwahukumu kwa sheria ya Musa lakini wao wenyewe ni wanafki mioyoni mwao.. mioyo yao ilikuwa ipo mbali na Mungu ingawa kwa nje wanaonekana ni waamuzi wazuri na viongozi wazuri wenye kusifiwa, lakini ndani yao wamejaa unafiki!.
Na Bwana YESU anatuonya tusiwe kama wao..
Mathayo 23:2 “Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa”
3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi
4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.
5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
6 hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi,
7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.
8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.
9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.
10 Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.
11 NAYE ALIYE MKUBWA WENU ATAKUWA MTUMISHI WENU.
12 Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa”.
Je YESU KRISTO ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako?..Je una uhakika jina lako lipo katika kitabu cha uzima?.. Kama bado YESU hayupo maishani mwako ni heri ukampokea leo, maana saa ya wokovu na wakati uliokubali ni sasa.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Upo umuhimu mkubwa wa kuliita Jina la Bwana
Warumi 10:12 “Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao;
13 kwa kuwa, KILA ATAKAYELIITIA JINA LA BWANA ATAOKOKA”
Kuna umuhimu mkubwa wa kuliitia jina la Bwana kiusahihi, na kuna hatari kubwa ya kuliita au kulitaja jina la Mungu kimakosa.
Kutoka 20:7 “Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure”.
Kwahiyo kama kwa kulitaja jina la Mungu bure ni dhambi, vile vile kinyume chake ni kweli kwamba tukilitaja inavyopaswa na kwasababu muhimu basi ni Faida kubwa kwetu.
Kwanini?, ni kwasababu jina la Mungu lina nguvu kuliko mwonekano wake…amelitukuza jina lake kuliko umbile lake, ndio maana amependa kutujulisha jina lake Zaidi ya sura yake.
Mithali 18:10 “Jina la Bwana ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama”
Leo kwa neema zake tutatazama njia sahihi ya kulitaja jina la Bwana Mungu kulingana na mazingira tunayopitia ili tupate wokovu, tumaini, faraja, ushindi, Amani na Nguvu!.
1.Katika kipindi cha mahitaji-Mwite YEHOVA-YIRE.
Yehova-Yire maana yake ni Mungu-Mpaji, (Mungu anayetoa kimiujiza)..Asili ya jina Yehova-Yire, ni kipindi Ibrahimu anakwenda kumtoa Isaka mwanae kama sadaka kwa Mungu, akiwa njiani mwanae Isaka alimwuliza Ibrahimu baba yake kuwa kuni zipo na moto pia upo lakini yupo wapi mwanakondoo?..Ndipo Ibrahimu kwa Imani alimjibu.. “Mungu atajipatia (Mwanzo 22:7-8)”.
Na walipofika katika mlima Moria ndipo wakamkuta kondoo ambaye tayari Bwana alikuwa amewaandalia. Ibrahimu akamwita Bwana YEHOVA-YIRE.
Vile vile na sisi tuwapo katika hali ya kuhitaji jambo Fulani (kama hitaji) tumwite Mungu kama YEHOVA-YIRE, itakuwa na mashiko Zaidi mbele zake kuliko kumwita au kumwomba tu kama MUNGU-MWENYEZI.
2. Katika nyakati za Magonjwa- Mwite YEHOVA-RAFA
Yehova-Rafa maana yake ni “Mungu-atuponyaye”. Wakati wana wa Israeli wanaelekea Kaanani, Bwana Mungu aliwaahidi “kutowaletea magonjwa yale aliyowapiga nayo wamisri” endapo wakidumu katika sheria zake na amri zake.. Hivyo wana wa Israeli baada ya kusikia hivyo wakawa wanamwita Mungu YEHOVA-RAFA, kipindi walipopitia magonjwa na maradhi, na Mungu alikumbuka ahadi yake hiyo na aliwaponya na magonjwa yao.
Kutoka 15:26 “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye”.
Vile vile upitiapo magonjwa au maradhi, mwite Mungu kama YEHOVA-RAFA, na utauvuta uponyaji kirahisi Zaidi..ndivyo walivyofanya wana wa Israeli katika nyakati za magonjwa.
3. Katika Nyakati za vita- Mwite YEHOVA-NISI
Yehova-Nisi maana yake ni “Bwana ni Mungu wa vita”. Kipindi wana wa Israeli wanashambuliwa na Waamaleki, Mungu alimwambi Musa anyanyue mikono yake miwili juu, na aliponyanyua Israeli walishinda na aliposhusha waamaleki walishinda, na mwisho wa vita vile Israeli walishinda kwasababu Haruni aliitegemeza mikono ya Musa kuanzia asubuhi mpaka jioni (Kutoka 17:8-16).
Ndipo wana wa Israeli wakamwita Bwana YEHOVA –NISI, maana yake “Mungu wa Vita” (bendera yao).. Kwahiyo Nyakati za Vita walimwimbia Bwana, na kumsifu kama YEHOVA NISI na si Yehova Yire, na Bwana aliwaonekania.
Na sisi tukutanapo na vita mbele yetu viwe vya kiroho, kiimani au kiuchumi.. basi ni vizuri tukamwita Mungu wetu kama Yehova Nisi, tukamsifu na kumwimbia kwa jina hilo, na vita mbele yetu atavifanya maji!.. kwasababu yeye anaketi katika sifa.
4. Katika vipindi vya Hatari- Mwite YEHOVA–ROHI.
Yehova-Rohi maana yake ni “Bwana ndiye mchungaji wangu”. Daudi alipopita vipindi vya hatari, alimwita Bwana kama mchungaji wake, Yehova-Rohi na kumsifu kwa jina hilo (Zaburi 23). Na Bwana daima alionekana mbele yake alimwokoa na hatari za kifo na dhiki zilizopo mbele yake.
Vile vile na sisi tuonapo hatari, au tuhisipo hatari, jina jema la kumwita Bwana na kumtukuza nalo, na kumsifu nalo ni YEHOVA-ROHI.
5.Katika kipindi cha mambo yasiyowezekanika –Mwite YEHOVA-EL – SHADAI.
Yehova-Elshadai maana yake “Bwana ni Mungu-Mwenyezi” (anayeweza kufanya mambo yote).
Kipindi ambacho Ibrahimu anaona uwezekano wa kupata mtoto haupo kutokana na umri wa mke wake Sara, Bwana alijidhihirisha kwake kama Mungu mwenye uwezo wote (Mungu mwenyezi), na Sara akapata mimba, Hivyo Ibrahimu na Israeli wote wakaendelea kumwomba BWANA kama YEHOVA-ELSHADAI Katika vipindi vya mahitaji yaliyo magumu, kama utasa, ukame n.k
6. Katika nyakati za Upweke- Mwite YEHOVA-SHAMA.
Yehova-Shama maaana yake “Mungu yupo hapa” (Ezekieli 48:35). Nyakati ambazo unajiona upo peke yake, mwambie Bwana wewe upo hapa, YEHOVA-SHAMA, na uwepo wa kipekee utakufunika, ndivyo Israeli walivyomwita Bwana nyakati za upweke.
7. Nyakati za kukosa Amani- Mwite YEHOVA-SHALOM.
Yehova-Shalom, maana yake ni “Mungu Amani yangu”. Gideoni alipotokewa na yule malaika alihisi atakufa, lakini malaika yule alimwambia “hutakufa” na Gideoni akapata “amani”akamwita Mungu Yehova-Shalom.. Mungu ni Amani yangu.
Waamuzi 6:22 “Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa Bwana; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona Bwana uso kwa uso.
23 Bwana akamwambia Amani iwe pamoja nawe; usiogope; hutakufa.
24 Ndipo Gideoni akamjengea Bwana madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu; hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri”.
Na sisi vitokeapo vipindi vya Amani ya moyo kupotea na hofu kutawala, hususani hofu ya kifo, basi tumwite Mungu kama Yehova-Shalom, na amani yake itatufunika.
8. Nyakati za kutamfakari Mungu kwa matendo yake- Mwite YEHOVA-ADONAI.
Yehova-Adonai maana yake ni “Mungu mwenye enzi yote(mfalme)” aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Sifa kwa ADONAI zina nguvu kama zikitajwa kwa maarifa hayo..
9.Katika vipindi vya Kupotea na kuhitaji wokovu- Mwite YEHOVA-MWOKOZI (YESU KRISTO)
Maana ya YEHOVA-MWOKOVU ni YESU,… Tafsiri ya jina YESU ni Yehova-Mwokozi. Hili ndilo jina lenye nguvu katika vipindi karibia vyote. Na ndilo jina la ukombozi, na hakuna jina lingine litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa jina hili la YESU, (Matendo 4:12).
Ikiwa umepotea dhambini, liite jina la YESU naye atakusaidia, ikiwa hutajabatizwa ili ukamilishe wokovu sawasawa na andiko la Marko 16:16, na ukabatizwe kwa jina la YESU, (Matendo 2:38, Matendo 19:5 na Matendo 10:48).
Yapo na majina mengine mengi yafaayo kumwita Bwana wetu katika nyakati hizo, lakini hayo yatoshe kusema tu, kuwa Mungu wetu anatupenda na anataka tupate faida, na faida moja wapo ni hiyo ya kulitumia jina lake wakati wa mahitaji.
Lakini katika hayo yote fahamu jambo moja kuwa unapoamua kuanza kulitaja jina la Bwana ili uvute msaada kutoka kwake, hakikisha unaacha UOVU..
2Timotheo 2:19 “Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, KILA ALITAJAYE JINA LA BWANA NA AUACHE UOVU”
Je umempokea Yesu Kristo, na kusafishwa dhambi zako kwa damu yake?
Kumbuka tunaishi majira ya kurudi kwa YESU mara ya pili, na shetani anafanya bidii nyingi kuhakikisha watu wanaenda katika lile ziwa la moto pamoja naye.
Bwana atusaidie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
ZIFAHAMU NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE SABA.
HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA.
Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.
JE UMEJIANDAA KUTIMIZA UNABII UPI?
Jibu: Tusome,
Walawi 19:27 “Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu”.
“Denge” ni mtindo wa kunyoa nywele kwa kuziacha nyingi upande wa juu (katikati) na kuziacha chache au kuzimaliza zote kwa upande wa chini (kuzunguka kichwa), kwa lugha ya sasa ni maarufu kama “Panki”.
Zamani sana nyakati za biblia mtindo huu waliokuwa wananyoa walikuwa ni watu wanaoabudu miungu, (wakiamini kwa kunyoa vile basi watajikinga na madhara Fulani ya kiroho), lakini siku zilivyozidi kwenda mtindo huu ulikuwa unatumiwa na watu wa ulimwengu kama fasheni, kiasi kwamba walionyoa hivyo basi walikuwa wanajulikana kama “wahuni” (wenye lengo la kupalilia zinaa na uasherati) , lakini zama hizi mtindo huu unatumiwa na watu wote, hadi wachungaji!!, na hauonekani kuwa ni tatizo.
Sasa swali ni je! Ni dhambi kunyoa denge/panki?
Jibu ni Ndio!..na itabaki kuwa ndio pasipo kujalisha ni watu wangapi wanafanya hivyo..
Na kwanini ni kosa?…kwasababu ile ile ya kuchanja chale..
Walawi 19:27 “Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
28 MSICHANJE CHALE YO YOTE katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi Bwana”.
Mtu anayenyoa denge, na anayechanja chale.. NI MAMOJA! Zote ni alama katika mwili ambazo zilitambulisha ibada Fulani, na mpaka leo zinafanya kazi hiyo hiyo… ni agano kamili katika mwili wa mtu linalohubiri ibada za miungu, haijalishi mtu huyo anajua au hajui..ndio maana kuna umuhimu mkubwa sana wa kufuatilia historia ya kitu kabla ya kukitumia kitu hicho/ mtindo huo…
Kwasababu si kila mtindo unaokubaliwa na wengi ni wa kiMungu, wala si kila desturi inayokubaliwa na kutumiwa na wengi ni ya kiMungu, nyingi ya tamaduni, desturi na mitindo ya kimaisha asili yake ni adui.
Na huwezi kukitumia kidonge chenye lengo la matibabu kama PIPI kwasababu tu kina utamu, halafu kisiwe na madhara kwako, vile vile huwezi kutumia elimu ya shetani au malighafi za shetani na kuzifanya mtindo, au urembo, halafu zisiwe na madhara kwako!..
Chale ni tiba ya shetani, denge ni tiba ya shetani, mitindo hiyo ilibuniwa na yeye kufanya tiba za kishetani… hivyo zinapotumiwa kama urembo! au fasheni! Ni kweli zitaleta mvuto kwa macho ya nje ya kibinadamu lakini zitabaki kubeba madhara yale yale katika kiroho. Ndio maana biblia ikakataza tusinyoe denge!.
Na hii sio sheria, kwamba ni agano la kale..na sasa tupo agano jipya hivyo kila kitu ni ruksa… Suala la ibada kwa miungu migeni litabaki kuwa katazo kwetu kwa nyakati zote.. Na denge, pamoja na chale ni ibada hizo…kama vile unavyoikimbia chale vile vile ikimbie kimbia denge.
Wala usiseme “ni nywele tu hazina maana”…Nywele zako zinamaana sana kiroho, ndio maana Bwana amekukataza usinyoe denge.. Bwana YESU alisema maneno yafuatayo..
Mathayo 10:30 “lakini ninyi, hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote”
Na tena alisema katika Luka..
Luka 21:18 “Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu”
Sasa kama nywele za vichwa vyetu Mungu hazitazami wala hashughuliki nazo..basi atakuwa mwongo aliposema hapo kuwa “zimehesabiwa zote na tena hakuna hata moja itakayopotea”.. Lakini kama Mungu ni kweli, basi pia nywele zetu ni lazima tuziweke kama atakavyo..
Ukizipunguza punguza kama unavyotaka wewe unaharibu mahesabu ya kimbingu, ukizisuka suka na kuziongezea marasta unaharibu mahesabu ya kimbingu, na hivyo unajiingiza katika mahesabu ya kishetani.
Hivyo usinyoe denge mtu wa Mungu, wala usisuke marasta…kama miaka ya zamani (katika biblia)mtu aliyenyoa denge alionekana ni mshirikina, iweje leo dunia ikuhubirie wewe ni mtakatifu?..kama miaka ya nyuma tu mtu aliyenyoa denge(panki) alionekana muhuni, iweje leo hii dunia ikuambie kuwa sio ni urembo?.. Huoni kama kuna udanganyifu mkubwa unaondelea sasa kutoka kwa adui..
Usiangalie ni idadi kubwa kiasi gani ya watu wananyoa denge, au wanasuka rasta na kuamini kuwa ni sawa, wewe liangalie Neno la Mungu..kwani nyakati tunazoishi ni za hatari.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Ikiwa bado hujaokoka fahamu kuwa Siku ya Wokovu ni leo, wala usingoje kesho.. kwa msaada wa kuongozwa sala ya kumkiri BWANA YESU basi fungua hapa >>>KUONGOZWA SALA YA TOBA
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine:
Je kwa mkristo aliyeokoka, ni dhambi kunyoa ndevu zake?
Nini maana ya mbingu na nchi zitapita lakini maneno yangu hayatapita kamwe? (Mathayo 24:35).