UMEJIANDAAJE KWA NYAKATI ZA KUWA PEKE YAKO?

UMEJIANDAAJE KWA NYAKATI ZA KUWA PEKE YAKO?

Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tuyatafakari maneno ya neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Sisi kama wakristo hatuna budi kutambua kuwa yapo majira mbalimbali tutapishana nayo angali tukiwa hapa duniani katika safari yetu ya imani. Leo tutaona mojawapo ya majira ambayo, huna budi kupishana nayo sehemu Fulani katika maisha yako. Na watakatifu wengi wanapofikia hatua hii, huwa wanavunjika moyo, na wengine kudhani Mungu amewaacha. Lakini la! Ni moja ya mapito ambayo Bwana anayaruhusu kwasababu zake maalumu.

Na majira hayo ni ya kuondolewa msaada, au usaidizi, au ukaribu, au faraja ya  ndugu, ya marafiki, au ya wapendwa. Yategemea na pito la mtu mwenyewe. Na sio kwamba ni wabaya, hapana, ni Mungu tu peke yake kaamua kufunga milango hiyo. Ili abaki yeye na Mungu wake tu, katika chumba cha siri cha rohoni.

Tujifunze kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ambaye, alikuwa mashuhuri sana, na kila mahali alipokwenda alizingirwa na makutano mengi, wakati mwingine alijificha ili watu wasimwone, kwasababu walikuwa wanamsonga sana, hata nafasi ya kula ilikosekana, maelfu ya watu walitamfuata popote alipokwenda.

Lakini kuna majira, hata wale waliokuwa karibu naye (yaani mitume) walimkimbia akabaki yeye peke yake, na hilo aliliona mapema akawaambia wanafunzi wake, ili wasije wakajisikia vibaya.

Yohana 16:32  Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.

33  Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Na ilikuja kutokea hivyo (Soma Marko 14:27-51). Kwasababu ilikuwa ni sehemu ya pito la mwana wa Mungu.

Halikadhalika yupo mtume Paulo, kama tunavyojua yeye ndio alikuwa kama askofu-kiongozi wa makanisa ya mataifa. Alikuwa na marafiki wengi, alikuwa na wapendwa wengi waliomsapoti na kumfariji, katika utumishi wake. Lakini upo wakati alijikuta peke yake. Mpaka akaandika sehemu ya waraka huo na kumtumia Timotheo. Jambo ambalo huwezi dhani linawezekana kwa askofu wa makanisa.

2Timotheo 4:16  “Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. 17  Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. 18  Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina”

Hivyo, hii sio bahati mbaya, ijapokuwa tunazungukwa na wapendwa, na familia, na watoto, na marafiki, lakini kuna wakati Bwana atataka ubaki peke yako na yeye. Na hivyo katika kipindi hicho utakachojikuta, upo mbali nao, au huoni msaada wowote kutoka kwao kama ilivyokuwa kule mwanzo, au hawakuulizii tena, huna mtu wa kucheka naye, kuimba naye. Usijione mpweke, bali mtazame Kristo, elekeza mawazo yako kwake, kwasababu kuna jambo anataka kukufundisha.

Na wakati huo ukiisha, utaona tena anakurejeshea, faraja yako, wapendwa wako, rafiki zako, ndugu zako, na safari inaendelea. Kama alivyofanya kwa Ayubu.

Ayubu 42:10 “Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza.  11 Ndipo wakamwendea nduguze wote, waume kwa wake, nao wote waliojuana naye hapo zamani, wakala chakula pamoja naye katika nyumba yake; nao wakamlilia na kumtuza moyo katika habari za huo uovu wote Bwana aliouleta juu yake; kila mtu akampa kipande cha fedha, na pete ya dhahabu kila mmoja”.

Hivyo weka akiba ya wakati huo, kwasababu hutaukwepa ikiwa wewe ni mwana wa Kristo.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618

Mada Nyinginezo:

WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA; NAO WATAMWOMBOLEZEA.

RABI, UNAKAA WAPI?

HIZI NI NYAKATI ZA KUFUNGA NA KUOMBA.

NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?

NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.

Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?

JE UTII WAKO KWA MUNGU UMETIMIA?.

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Moses
Moses
7 days ago

Nimejengwa sana na huu ujumbe. Asante.