Kabla ya kuwafahamu wana wa Asafu, ni vizuri kumfahamu Asafu mwenyewe alikuwa ni nani.
Asafu alikuwa ni mmoja wa walawi ambao, mfalme Daudi alimuweka kama kiongozi wa mbele wa sifa, atakayesimama mbele ya sanduku la Mungu daima kumsifu Mungu. (Soma 1Nyakati 6:31-32, 39).
1 NYAKATI: MLANGO 16
1 Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. 2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana. 3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. 4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli; 5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;
1 Wakaliingiza sanduku la Mungu, na kuliweka katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake; wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.
2 Na Daudi alipokwisha kuitoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Bwana.
3 Kisha akawagawia kila mtu wa Israeli, waume kwa wake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu.
4 Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la Bwana, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, Bwana, Mungu wa Israeli;
5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Matithiya, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;
Kulingana na maandiko, biblia inasema huyu Asafu hakuwa tu mwimbaji, bali Mwonaji pia,
2Nyakati 29:30 “Tena Hezekia mfalme na wakuu wakawaamuru Walawi, wamwimbie Bwana sifa kwa maneno ya Daudi, na ya Asafu mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama vichwa, wakaabudu”.
Baadaye, uzao wake uliendeleza nyayo zake, na wote wakawa waimbaji katika hekalu la Mungu lililokuja kujengwa baadaye, na hata baada ya ule uhamisho wa Babeli, waliporudi bado waliweza kuwekwa katika kazi hiyo hiyo ya Sifa..
Soma, Ezra 2:41 “Waimbaji; wana wa Asafu, mia moja ishirini na wanane”.,
Pia Nehemia 7:44
Halikadhalika kuna baadhi ya Zaburi zilijulikana kama Zaburi za Asafu,Ambazo ni Zaburi 50 na ya 73-83. (Baadhi ya tafsiri zinaonyesha hivyo). Hiyo ni kuonyesha kuwa Mungu alimtumia yeye na uzao wake kwa njia ya uimbaji, kutoa nabii ambazo zinatusaidia hadi sasa.
Lakini kwasasa wana wa Asafu ni akina nani? Na tunapata funzo gani?
Wana wa Asafu ni watu wote wanaotumikia madhabahuni pa Bwana katika huduma ya kumsifu na kumwimbia Mungu. Watu hawa wanatenda kazi kubwa inayompendeza Mungu na kwa kupitia wao, Mungu huwa anapitisha, jumbe zake nyingi, na nabii nyingi zinazookoa na kuponya watu kama ilivyokuwa kwa wana wa Asafu, hii ikiwa na maana, kwamba wakitumika vema katika kazi yao, basi ni utumishi mkubwa sana, hata Zaidi ya huduma nyingine zote.
Lakini, watu hawa walijua kanuni ya kumwimbia Mungu, walimwimbia Mungu katika “uzuri wa utakatifu”, sawasawa 1Nyakati 16:29. Tofauti na sasa, waimbaji wengi, wamekuwa wasanii, wanageuza uimbaji wa injili kuwa Sanaa na sio wito na huduma ya Kristo Yesu.
Wanasahau kuwa huduma yao ndio ya kwanza kabisa inayomkaribia Mungu Zaidi ya nyingine zote,..Huduma ya Maserafi na Makerubi malaika watakatifu wasimamao mbele ya Mungu daima
Lakini kinyuma chake, Mwimbaji wa injili, utamkuta anakata mauno, anavaa vimini, anapamba uso kama Yezebeli, anaimba kwa staili za wasanii wa kidunia.. Twategemea vipi Mungu atasema au atawaponya, au atawafungua na watu wake kupitia uimbaji huo?, Haiwezekani..Inasikitisha kuona, kanisa la sasa, kundi kubwa la watu walioharibikiwa linatoka kwa wanakwaya na waimbaji.
Kumbuka Sababu iliyowafanya wana wa Israeli,wapelekwe utumwani haikuwa tu kuabudu maashera hapana, ilikuwa pia ni hiyo ya unafki katika kumwimbia.
Amosi 6:5 “ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi pamoja na sauti ya vinanda, na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi, kama vile Daudi;”
Bwana anatuonya vikali, na sisi pia atatuadhibu vikali kama tutakuwa na tabia kama za wao, anataka anapoimbiwa aimbiwe katika “uzuri wa utakatifu” (1Nyakati 16:29)..Maana yake ni kwamba wewe mwongoza sifa, wewe mwimbaji, wewe mpiga kinanda,wewe mpiga gitaa, uwe kielelezo kuanzia mavazi yako, usemi, hadi tabia, mbele za watu. Utakatifu ndio uwe leseni yako, ya kumwimbia Mungu.
Kama utashindwa utakatifu, ni heri uache tu, ukafanye kazi nyingine, kwasababu utakuwa unajizombea laana badala ya baraka.
Mahali Mungu anasifiwa na kuabudiwa ni kuwa makini sana.. wengine walipoteza Maisha walipojaribu kuvuruga utaratibu pindi Mungu anapokuwa anasifiwa (Soma 2Samweli 6:1-11 ), Vivyo hivyo na wewe mwimbishaji kanisani, usipokuwa siriazi na huduma yako, uwezekano wa kukutwa na hayo upo mkubwa sana.
Bwana anataka sote tuwe wana wa Asafu, ili atutumie kumtukuza yeye, Pamoja na kuzungumza na watu wake, ili aziponye roho za watu..
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MAOMBI YA YABESI.
NI KITU GANI TUNAJIFUNZA KWA RISPA, BINTI AYA?
SOMO no.02 (BINTI WA YEFTHA).
Gongo na Fimbo ni nini? Na vinawezaje kumfariji mtu? (Zaburi 23:4).
Nini maana ya “Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi”?
NI SALAMA ROHONI MWANGU Lyrics
WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.
Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri.
Rudi nyumbani
Print this post
Maongeo ni maongezeko,
Kwa mfano Neno hilo utalisoma katika vifungu hivi;
Kutoka 23:10 “Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake; 11 lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni”.
Kutoka 23:10 “Utapanda mbegu katika nchi yako muda wa miaka sita na kuyavuna maongeo yake;
11 lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni”.
Soma pia Walawi 19:24
Maana yake ni kuwa kwa muda wa miaka sita Mungu aliwaruhusu wana wa Israeli wapande na kuvuna, hata na vile vinavyoongeza katika mavuno yao. Lakini ufikapo mwaka wa saba, hawakuruhusiwa kuvuna chochote bali waviache kwa ajili ya maskini na Wanyama wa kondeni.
Isaya 9:7 “Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo”.
Maana yake ni kuwa maongezeko ya enzi yake, na amani hayatakuwa na mwisho yataendelea kuongezeka na kuongezeka milele. Na anayezungumziwa hapo si mwingine Zaidi ya Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakolosai 2:18 “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; 19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu”.
Wakolosai 2:18 “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;
19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu”.
Hapo anaposema, “hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu”, ana maana kuwa, mwili huo(ambao ndio kanisa la Kristo) ukishakwisha kushikamanishwa Pamoja viungo vyote.. Basi hukua, kwa maongezeko (maongeo), yatokayo kwa Mungu..Sio maongezeko yatokayo kwa mwanadamu.
Hii ikiwa na maana hata sisi kama wakristo, tukishikama Pamoja na Kristo tukamfanya kuwa kichwa chetu, basi, tutakuwa katika ukuaji (maongezeko )unaotoka kwa Mungu mwenyewe..
Lakini kinyume chake ni kweli tukimkataa Kristo, kama kichwa cha kanisa, na kuwafanya wanadamu kuwa ndio vichwa vyetu, basi hatutakuwa na maongezo yoyote ya rohoni au mwilini, na hata kama tukiwa nayo, basi yatakuwa hayatokani na Mungu bali ibilisi.
Hivyo hatuna budi kumfanya Kristo kichwa cha kila kitu.. kwasababu ufalme wake unadumu milele. Lakini tukifanya tunajua kujenga ngome zetu au falme zetu, tufahamu kuwa taabu zetu zitakuwa ni bure mwisho wa siku.
Ukuaji wetu wa ndani na nje, unamtegemea Yesu Kristo tu, zaidi yake hakuna mwingine.
Sifa heshima na utukufu vimrudie yeye milele na milele daima.
Bwana atusaidie.
Shalom..
Sadaka ya kinywaji ilikuwaje? Na inawakilisha nini?
Mkatale ni nini katika biblia? (Matendo 16:24)
SIFONGO NA SIKI NI NINI?
Pakanga ni nini?
Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Bushuti ni nini?
Donda-Ndugu ni nini?
Pango la Makpela ni lipi, je lina umuhimu wowote kwetu?
Katika biblia (Agano la kale), kimiminika kilichokuwa kinatolewa sadaka ni “Divai” na si kitu kingine,
Walawi 23:13 “Na sadaka yake ya unga itakuwa sehemu za kumi mbili za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, ni kafara iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto kuwa harufu ya kupendeza; na SADAKA YAKE YA KINYWAJI ITAKUWA NI DIVAI, robo ya hini”.
Unaweza kuona pia sadaka hii ya Kinywaji ikitajwa katika kitabu cha Kutoka 29:40, Kutoka 30:9, na Walawi 23:18, Hesabu 6:15, Hesabu 15:6 na Hesabu 28:17..
Sasa swali linakuja kwanini IWE DIVAI na si kitu kingine?
Sasa Sadaka ya kinywaji (Divai) iliyokuwa inapelekwa katika madhabahu haikuwa kwa kazi ya Ulevi, bali kwa matumizi ya Nishati.
Katika sheria za Musa, Bwana aliagiza pia wana wa Israeli watoe sadaka ya kinywaji, ambayo ilikuwa ni DIVAI. Na divai hiyo ilipelekwa kwa kuhani, na kuhani aliingia nayo ndani ya hema, na kuitwaa sehemu ndogo ya ile Divai, na kisha kuimimina juu ya madhahabu Pamoja na unga mwembamba, na kuwasha moto juu yake.
Asili ya sadaka hii ni wapi?
Matoleo ya sadaka ya kinywaji yalianzia kwa Yakobo kipindi alipotokewa na Mungu kule Betheli, kama vile sadaka ya Zaka ilivyoanzia kwa Ibrahimu kipindi anakutana na Melkizedeki na hatimaye ikaja kuwa sheria kwa Israeli yote. Vivyo hivyo na sadaka ya kinywaji.
Mwanzo 35:9 “MUNGU AKAMTOKEA YAKOBO TENA, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, AKAMIMINA JUU YAKE SADAKA YA KINYWAJI, AKAMIMINA MAFUTA JUU YAKE.15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.”
Mwanzo 35:9 “MUNGU AKAMTOKEA YAKOBO TENA, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.
10 Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.
11 Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
12 Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.
13 Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
14 Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, AKAMIMINA JUU YAKE SADAKA YA KINYWAJI, AKAMIMINA MAFUTA JUU YAKE.
15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.”
Sasa Sadaka ya Kinywaji inawakilisha nini katika Agano jipya?
Sadaka ya kinywaji katika Agano jipya inawakilisha damu ya YESU, ambayo ilimwagika/kumiminwa kwaajili yetu, mara moja tu! (kumbuka damu ya Yesu, inafananishwa na Divai), Bwana Yesu alilisema hilo wazi..
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, INAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU”.
Luka 22:19 “Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU, INAYOMWAGIKA KWA AJILI YENU”.
Umeona hapo! Kile kikombe (Divai) kilikuwa ni Damu ya Yesu iliyotiririka na iliyomwagika pale Kalvari, na ni ufunuo wa Ile sadaka ya kinywaji ambayo ilikuwa inamiminwa juu ya madhabahu. Na pia ni ufunuo wa meza ya Bwana.
Bwana Yesu akubariki
Maran atha!
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
Sadaka ya kutikiswa ilikuwaje?
Nini maana ya.. “Utoapo sadaka mkono wako wa kuume usijue ufanyalo mkono wako wa kushoto”
NI NINI BWANA ANATAZAMIA KILA TUNAPOSHIRIKI MEZA YAKE.
BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?
Biblia inatuonyesha baada ya tukio la unyakuo, ambapo watakatifu watakwenda mbinguni kwenye karamu ya mwana-kondoo kwa kipindi cha miaka saba, ..watarudi tena duniani wakiwa na Bwana Yesu ili kutawala naye kwa muda wa miaka 1000.
Sasa utajiuliza ni kwanini Bwana Yesu asiwe nao milele mbinguni bali arudi tena dunia kutawala nao. Makusudi ya Bwana ni yapi?
Sasa leo hatupo kueleza kwa urefu, huo utawala utakujaje kujaje na wakati gani..ikiwa utapenda kupata somo lake kwa urefu basi fungua link hii >>> UTAWALA WA MIAKA 1000.
Lakini nataka tuone sababu za kuwepo kwa utawala huo…
Sababu zipo mbili kuu
Raha hiyo inajulikana kama raha ya sabato..
Waebrania 4:9-11
[9]Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. [10]Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. [11]Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.
[9]Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.
[10]Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.
[11]Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.
Hichi ndicho kipindi ambacho Bwana atawarejeshea vyote watumwa wake walivyovipoteza kwa ajili yake walipokuwa hapa duniani kwa kuwapa ufalme ulio bora wenye nguvu na wa kudumu. (Yoeli 2:25)
Watatawala kama wafalme na mabwana, na makuhani,..na Yesu Kristo mwenyewe akiwa kama Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme.
Kipindi hicho dunia hii itarejeshwa na kuwa nzuri sana hata zaidi ya ilivyokuwa Edeni. Dunia yote itajawa na amani..kwasababu kipindi hicho ibilisi atakuwa amefungwa kwa muda wa miaka 1000,
Ikiwa wewe iliishi maisha ya kujikana na huu ulimwengu wa kitambo unaopita, basi kule utakuwa na nafasi kubwa sana kwa Yesu Kristo, tutakuwa na miili mipya ya utukufu isiyougua wala kuzeeka, utaburudishwa kwelikweli,
Na raha isiyo na kifani itatawala nyuso za watu wa Mungu, mtu ambaye ulionekana umerukwa na akili kwa kumtumikia kwako Mungu, binti ulionekana mshamba kwa kujisitiri kwako, Bwana atakupa heshima na faraja yako ya kumiliki.
Wote waliotaabika kwa ajili ya injili ya Kristo kwa namna moja au nyingine huo ndio utakuwa wakati wa kuburudishwa na kuyafurahia maisha.. Ni lazima Bwana Yesu afanye hivi, ili kuwathibitishia watu wake kwamba hakuna chochote walichokipoteza walipokuwa hapa duniani walipomfuata yeye.
ambapo wa mwisho atakuwa ni mauti.
1 Wakorintho 15:24-26
[24]Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. [25]Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. [26]Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
[24]Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.
[25]Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.
[26]Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
Kumbuka hata katika utawala ule watu watakuwa wanaendelea kufa, wale ambao walizaliwa humo..lakini sisi hatutakufa kwasababu tutakuwa na miili ya utukufu tuliyotoka nayo mbinguni.
Hivyo Bwana Yesu atadhibiti maadui zake waliosalia (wa rohoni) na wa mwisho wao atakuwa ni mauti,
Kwasasa, bado maadui baadhi wa Bwana Yesu hawajadhibitiwa, na ndio maana bado utaona watu wanakufa, lakini mambo hayo yote, atayamaliza ndani ya huo utawala wa amani wa miaka 1000.
Hivyo mpaka utalawa unakwisha..mambo yote mabaya yatakuwa yamekwisha kabisa kabisa.
Na baada ya hapo sasa ndio inakija mbingu mpya na nchi mpya..huko hakutakuwa na kilio wala mateso, wala huzuni, wala mauti, kwasababu tayari vilishakomeshwa na Yesu Kristo vyote katika utawala ule.
Na ile Yerusalemu itakushuka sasa kutoka mbinguni, ambapo Mungu kwa mara ya kwanza atafanya maskani pamoja na wanadamu.(Ufunuo 21&22)
Yaani kwa ufupi ni kwamba Mungu atahamishia makao yake hapa..
Uzuri na mambo yaliyopo huko..biblia inasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia,
Jua na mwezi havitakuwepo..ulimwengu huu utageuzwa na kuwa sehemu ya tofauti kabisa..
Lakini ikiwa wewe upo nje ya wokovu, unayo hasara ya mambo mengi, ya kwanza ni karamu ya mwana-kondoo mbinguni, ya pili ni utawala wa miaka 1000 na mwisho mbingu mpya na nchi mpya.
Hivyo itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima kisha upoteze roho yako.
Kumbuka kwa jinsi hali ilivyo hichi ni kizazi kitakachoshuhudia tukio la unyakuo, hatuweki siku lakini kwa dalili zinavyoonyesha hatuna muda mrefu Kristo anarudi..labda pengine leo usiku.
Hivyo tuanze kuelekeza mawazo yetu mbinguni, tuachane na mambo haya ya kitambo ya ulimwengu. Yesu ameshatuandalia makao, ambayo atakuja kutuburudisha kwa kipindi cha miaka 1000. Tutubu dhambi zetu kwa kumaanisha kabisa kuziacha. Na Bwana atatupokea na kutusamehe.
Bwana akubariki
IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.
UMUHIMU WA KUBATIZWA.
Kiyama ni nini?
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.
USICHELEWE KUMPAKA BWANA MARHAMU!
Kupiga ramli ni nini katika biblia?
WhatsApp
Kifo ni ile hali ya uhai kutoka ndani ya kiumbe hai chochote. Kifo kinaweza kumtokea mtu, mnyama, bakteria, kirusi, mmea, jani n.k. Vyote hivi maadamu vina uhai ndani yao, vinapotokwa tu huo uhai basi vinakuwa vimekufa.
Lakini Mauti ni nini?
Mauti ni kile kile kifo, isipokuwa ni mahususi tu kwa mwanadamu.. Huwezi kusema “mti” umekumbwa na mauti, au “mbwa” amepatwa na mauti.. Bali utasema, mti umekufa au mbwa amekufa. Ni mwanadamu tu ndiye anayekumbwa na mauti.
Lakini kwanini Kifo kitofautishwe na mauti?
Ni kuonyesha uzito wa hali hiyo kwa mwanadamu.. Kwamfano “Kilio” kinaweza kutokea kwa mtu yeyote yule, iwe ni mtoto au mtu mzima Lakini kikiwa kwa mtu mzima, hakiwezi kuchukuliwa kama kile cha mtoto, kwasababu kama vile wasemavyo wanajamii, “ukiona mtu mzima analia basi ujue kuna jambo”
Maana yake ni kuwa hadi mtu mzima anatoa machozi, ujue hayajaja bure bure tu, bali yana sababu nyuma yake, na matokeo mbele yake, kwasababu si desturi ya mtu mzima kulia. Nyuma yake utagundua aidha kuna msiba, au magonjwa, au kuumizwa moyo kusikoelezeka, kusalitiwa au kupoteza mali zake nyingi, au vitu, n.k.. Lakini mtoto mdogo anaweza akalia kwasababu zisizokuwa na maana au msingi wowote.
Vivyo hivyo katika kifo na mauti ni tendo lilelile..kuondoka kwa uhai.. isipokuwa linapokuja kwa mtu, linakuwa na uzito wa namna yake, kwasababu mwanadamu hakuumbiwa kifo, halidhalika kwa sifa yake na heshima na akili alizopewa na Mungu, jambo kama hilo ni anguko kubwa sana kwake..Mauti ni pigo kwa mwanadamu.
Sababu ya mauti kumpata mtu ni nini?
Ni dhambi..
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Sisi wanadamu tulipoasi, adhabu hii ya mauti ilitukumba.. Hilo ni pigo kubwa sana kwetu, tofauti na Wanyama, wenyewe hawajui chochote, wala hawaelewi, kufa na kupotea kwao ni kitu cha kawaida, lakini sisi tunajua kwamba ipo siku uhai utatutoka..
Lakini heri ingekuwa ni kifo cha miili yetu tu halafu basi.. Lakini Huko mbeleni pia baada ya kifo, kuna adhabu ya kifo cha roho. Hiyo ndio inayoitwa mauti ya pili..Ambazo roho hizi zitamalizwa kabisa katika lile ziwa la moto..Hapo ndipo utaona, tofauti ya kifo cha mnyama, na kile cha mwanadamu.
Ndugu, ukikumbwa na mauti sasa, toa yale mawazo kwamba utakuwa kama mnyama tu.. Hapana, ukifa katika dhambi, utanyoshea moja kwa moja hadi jehanamu, ukisubiri siku ya ufufuo ifike uhukumiwe kisha utupwe katika ziwa la moto milele na milele.
Lakini Habari njema ni kwamba, Bwana Yesu alikuja kukomesha mauti kwa mwanadamu, na kwamba yeyote amwaminiye yeye, anakuwa amevuta kutoka katika mauti na kuingia kwenye uzima..
Yohana 5:24 “Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani”.
Umeona? Yaani Yesu akikuoa mauti inakuwa haina nguvu tena ndani yake..
Hivyo ndugu, wasubiri nini, leo usimkaribishe Yesu moyoni mwako.? Kumbuka hakuna mtu mwenye garantii ya kuishi milele. Au anayeijua kesho yake kama atakuwa duniani au la. Ukifa katika dhambi ni nani atakayekuponya na mauti ya roho yako? Huko utakapokwenda utakuwa mgeni wa nani. Kama huna uhakika, unajisikiaje kubaki katika hali hiyo?
Lakini nafasi sasa unayo, Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, yaani kuongozwa sala ya toba ya kumpokea Yesu.. Basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo huo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa kifo kinampata kiumbe hai chochote, lakini mauti ni mahususi kwa mwanadamu, kwasababu yenyewe inabeba maana kubwa zaidi ya kifo cha kutoka uhai tu. Mauti imebeba uchungu, majuto, masononeko, hukumu, nyuma yake, jambo ambalo kifo hakina.
jiunge kwenye group la whatsapp la mafundisho ya kila siku kwa kubofya hapa >>> WHATSAPP
Jehanamu ni nini?
Kuna hukumu za aina ngapi?
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
UNYAKUO.
DHAMBI YA MAUTI
BALI WANA WA UFALME WATATUPWA NJE!.
Ni muhimu kujua kanuni za kuomba, ili tusije tukajikuta tunapiga mbio bure, kwa kuomba maombi yasiyokuwa na majibu. Kwanza ni muhimu kumjua unayemwomba ni Mungu wa namna gani.. Usipozijua tabia za unayemwomba, na ukienda kumwomba..unaweza ukamchukiza badala ya kumpendeza.
Sasa zipo hoja nyingi, ambazo ni harufu mbaya mbele za MUNGU wetu, lakini leo tutajifunza hoja moja ambayo ni hoja inayoonekana kama Nzito, machoni petu, lakini mbele za Mungu wetu ni harufu mbaya..
Na hoja yenyewe ni ya KUWASHITAKI WALE TUNAOWAONA KUWA MAADUI ZETU, MBELE ZA MUNGU.
Hebu tusome kisa kifuatacho, kisha tujifunze tabia ya Bwana Yesu ambayo shetani katupiga upofu tusiijue…
Luka 12:13 “Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, MWAMBIE NDUGU YANGU ANIGAWIE URITHI WETU. 14 Akamwambia, MTU WEWE, NI NANI ALIYENIWEKA MIMI KUWA MWAMUZI AU MGAWANYI JUU YENU?”
Luka 12:13 “Mtu mmoja katika mkutano akamwambia, Mwalimu, MWAMBIE NDUGU YANGU ANIGAWIE URITHI WETU.
14 Akamwambia, MTU WEWE, NI NANI ALIYENIWEKA MIMI KUWA MWAMUZI AU MGAWANYI JUU YENU?”
Kikawaida hata mimi nilitegemea Bwana Yesu, angesuluhisha hii KESI!, Kwa kuwaweka mezani na kuzungumza na pande zote mbili, ili yule anayestahili HAKI apewe, na yule asiyestahili AONYWE!!.. Lakini ilikuwa kinyume chake!… Bwana Yesu anaanza kushughulika kwanza na huyu aliyeleta Mashitaka!… na kumwuliza..NI NANI ALIYEMWEKA YEYE AWE MWAMUZI JUU YAO, AU MGAWANYI!!!.. Ni kama vile Bwana anazikataa hizo mada!, ni kama vile havutiwi nazo, ni kama vile zinampotezea muda!!!. Ndio maana hata mashitaka ya Martha juu ya ndugu yake Miriamu hayakuwa kama alivyotegemea. (Luka 10:40-42).
Sasa maandiko yanasema Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele, hajabadilika, na hatabadilika (Waebrania 13:8)… kama aliyakataa mashitaka ya huyu mtu hadharani, dhidi ya adui yake, basi atakayataa hata na mashitaka yetu katika SALA!!!.. Kwasababu ni yeye yule, habadiliki.
Ni kweli umedhulumiwa kiwanja chako!, ni kweli umeonewa, ni kweli umestahili haki…Ila unapokwenda kwenye maombi, kamwe usimshitaki huyo unayemwona kama adui yako, kwasababu hutaambulia chochote!…maombi yako ni kama kichefuchefu tu kwa Bwana!..
Ni vizuri kumjua unayemwomba ana tabia gani kabla ya kumwomba!.. hii ndio shida kubwa inayosababisha watu wengi kutojibiwa maombi yao, na hawajui ni kwanini. Tatizo ni kwamba hawamjui wanayemwomba ana tabia gani.. Ndugu, Bwana Yesu hana tabia kama uliyonayo wewe, au niliyo nayo mimi na wala hutuwezi kumfundisha tabia zetu..na kamwe hawezi kufuata tabia zetu..na wala hana cha kujifunza kutoka kwetu.. sisi ndio tuna cha kujifunza kutoka kwake, na tunapaswa tuige tabia yake ili tufanikiwe.
Sasa tabia yake ni hii..
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39 Lakini mimi nawaambia, MSISHINDANE NA MTU MWOVU; LAKINI MTU AKUPIGAYE SHAVU LA KUUME, MGEUZIE NA LA PILI. 40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. 41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Mathayo 5:38 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, MSISHINDANE NA MTU MWOVU; LAKINI MTU AKUPIGAYE SHAVU LA KUUME, MGEUZIE NA LA PILI.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili”.
Maana yake ni kwamba kama mtu Kakupiga shavu moja bila kosa lolote, badala ya kwenda KUPIGA MAGOTI KUMSHITAKI KWA BWANA!.. wewe Mpe shavu la pili, alipige na hilo halafu nenda kapige magoti! Mshukuru Mungu kwakuwa umefanikiwa kumpa na shavu la pili alipige…Utakuwa umeyatenda mapenzi ya Mungu…na umeomba maombi yenye hoja… HALAFU SASA SUBIRIA MAJIBU YAKE!!!.
Mtu kakudhulumu kipande kidogo cha ardhi, mwongeze na mita kadhaa..halafu mshukuru Mungu..Hapo utakuwa umeukosha moyo wa Bwana Yesu kuliko unavyodhani!!!… Na utaona matokeo yake.. Ndani ya kipindi kifupi, utaona jinsi Bwana atakavyomtengeneza yule mtu, kwasababu atamgusa moyo na atajiona ni mkosaji, na utashangaa anakurudishia ile sehemu ya ardhi aliyokudhulumu, ndivyo maandiko yanavyosema.. kuwa Njia za mtu zikimpendeza Bwana, humpatanisha na maadui zake..
Mithali 16:7 “Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye”.
Kwasababu Bwana anataka Nuru yetu iangaze…kwamba watu wanapoyatazama matendo yetu mema, jinsi gani tulivyo wema..ndipo wapokee neema ya wokovu..lakini tukiwa watu wakaidi, wakushindana wa kutupiana maneno, wakushitakiana mchana kutwa na usiku kucha..bila shaka sisi hatutakuwa na utofauti wowote na shetani… maana tafsiri ya jina shetani ni MSHITAKI, AU MCHONGEZI. Usiku na mchana anatushitaki mbele za Mungu (Soma 1Petro 5:8 na Ufunuo 12:10). Sasa na sisi tusiwe mashetani wengine!!..kwa kupeleka mashitaka mbele za Mungu.
Ndugu, ukitaka baraka basi mwabudu na msikilize Bwana Yesu Kristo wa kwenye biblia, ambaye yupo hai sasahivi..na Bwana Yesu wa kwenye biblia ni huyu mwenye maneno yafuatayo..
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki”.
Na watumishi wake pia watakuwa na maneno hayo hayo…lakini pia yupo yesu mwingine asiyekuwa wa kwenye biblia, huyo anakuambia Mpige adui yako mchukie adui yako, ukimfuata huyo au ukiwafuata watumishi wake basi jua unaenda kuzimu.
2Wakorintho 11:4 “Maana yeye ajaye akihubiri YESU MWINGINE ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye!”
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
VITA DHIDI YA MAADUI
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
UMUHIMU WA KUZALIWA MARA YA PILI.
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
Mathayo 8:11 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; 12 bali WANA WA UFALME WATATUPWA KATIKA GIZA LA NJE, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Mathayo 8:11 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
12 bali WANA WA UFALME WATATUPWA KATIKA GIZA LA NJE, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”.
Je umewahi kujiuliza ni kwanini Bwana Yesu aseme maneno hayo??, kuwa Wana wa Ufalme watatupwa nje?. Watakuwaje wana wa Ufalme halafu tena watupwe nje?…hao si ndo wangepaswa waingie ndani??.. Je Bwana Yesu alikosea?
Jibu ni la!, hakukosea..bali ni kweli Wana wa Ufalme watatupwa nje!!.
Sasa ili tuwajue hawa wana wa Ufalme ni akina nani?. Hebu tuutafakari mfano mwingine wa Bwana alioutoa mahali pengine.
Mathayo 22:1 “Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema, 2 Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. 3 Akawatuma watumwa wake WAWAITE WALIOALIKWA KUJA ARUSINI; nao wakakataa kuja. 4 Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, WAAMBIENI WALE WALIOALIKWA, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini. 5 Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake; 6 nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua. 7 Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. 8 Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, LAKINI WALE WALIOALIKWA HAWAKUSTAHILI. 9 Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini. 10 Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi IKAJAA WAGENI”.
Mathayo 22:1 “Yesu akajibu, akawaambia tena kwa mithali, akisema,
2 Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi.
3 Akawatuma watumwa wake WAWAITE WALIOALIKWA KUJA ARUSINI; nao wakakataa kuja.
4 Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, WAAMBIENI WALE WALIOALIKWA, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng’ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.
5 Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake;
6 nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua.
7 Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao.
8 Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, LAKINI WALE WALIOALIKWA HAWAKUSTAHILI.
9 Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini.
10 Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi IKAJAA WAGENI”.
Katika mfano huo utaona kuna makundi mawili, kundi la kwanza ni WAALIKWA, (ambao tunaweza kuwaita kama “wana wa Harusi”, au waliostahili kuingia harusini, ambao walipewa kadi zao maalumu za mwaliko na waliandaliwa viti kabisa, na wanafahamiana na Bwana harusi).. Lakini wapo ambao hawakupewa kadi kabisa…wala walikuwa hawajaalikwa, kwaufupi hawakuwa kwenye bajeti yoyote, wala walikuwa hawafahamiani na Bwana harusi.
Lakini mwishoni tunaona wale WANA WA HARUSI, ambao walikuwa na nafasi harusini, ambao walifahamiana sana na Bwana harusi, ambao ni ndugu zake, na jamaa zake na Bwana harusi, waliokuwa wamekusudiwa hiyo sherehe, yaani kwaufupi karamu ilikuwa ni kwaajili yao na furaha yao…mwisho wa siku hakuna hata mmoja, aliyeingia katika hiyo karamu..badala yake walitokea wengine wakaingia katika karamu..ambao hawakustahili, wasiojuana hata na Bwana harusi, waliotoka kutoka njia panda za barabarani, kutoka mitaani, kutoka masokoni na kutoka sehemu mbali mbali…wakaingia karamuni..harusi ikajaa WAGENI.. (Zingatia hilo neno wageni!)
Kupitia mfano huu tayari tutakuwa tumeshajua ni kwanini Bwana Yesu aseme haya…
Mathayo 8:11 “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; 12 bali WANA WA UFALME WATATUPWA KATIKA GIZA LA NJE, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”
12 bali WANA WA UFALME WATATUPWA KATIKA GIZA LA NJE, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno”
Leo hii wana wa Ufalme duniani ni wengi sana… Kwa ufupi wote ambao wameisikia Injili, na injili inajirudia rudia masikioni mwao, lakini wanaitolea udhuru kila mara, hawapo tayari kujikana nafsi na kumfuata Yesu, hao tayari ni WANA WA UFALME, ambao Bwana anawaalika lakini hawaalikiki!!!.
Pamoja na kwamba wamehubiriwa uzuri wote wa mbinguni, na faida za kiroho watakazozipata endapo wakiamua kubadilisha Maisha yao, na kuishi kulingana na Neno la Mungu na mapenzi ya Mungu, Pamoja na kuwa wamejihakikishia kuwa ni kweli wanaishi nyakati za kurudi Bwana wao… lakini bado watatoa udhuru..
Utasikia wanasema.. “Ni kweli natamani kusimama kiimani lakini kazi zangu zinanibana, nakosa muda wa kusoma biblia” .. “Ni kweli natamani kuwa mwombaji na kuhudhuria ibadani lakini kazi ni nyingi, nakuwa bize mpaka jumapili”… “Ni kweli natamani kuacha pombe, na kuacha kuvaa kikahaba na kihuni ila naamini sikumoja tu nitaacha”.. “Ni kweli Neno linanufundisha kubatizwa, lakini siwezi kwasasa, kwasababu mchungaji wangu na familia yako hawaamini hilo” n.k n.K.
Sasa hili ndio kundi la WANA WA UFALME, ambao siku ile, biblia imetabiri WATATUPWA NJE, Kutakakowako KILIO NA KUSAGA MENO!!.
Ndugu usifurahie tu kulisikia Neno, au kulisoma Neno na kulielewa, bali furahia na kushangilia UNAPOLITENDA NENO. Biblia sio kitabu cha taarifa, au simulizi..bali ni kitabu cha MAELEKEZO ya Nini cha kufanya!..Maana yake tunapaswa tukitendee kazi kile tunachoelekezwa kwenye biblia, sio tukisome tu!!..au tuhubiriwe tu!..
Leo tunaishi katika kizazi cha watu wanaopenda sana kusikiliza mahubiri, wanapenda sana kuhubiriwa, wanaopenda sana kufundishwa biblia, lakini si wanaopenda KUTENDA KILE WANACHOKISIKIA AU WANACHOKISOMA AU WANACHOFUNDISHWA!!!!.
Yakobo 1:22 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, HALI MKIJIDANGANYA NAFSI ZENU. 23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, HUYO ATAKUWA HERI KATIKA KUTENDA KWAKE.
Yakobo 1:22 “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, HALI MKIJIDANGANYA NAFSI ZENU.
23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, HUYO ATAKUWA HERI KATIKA KUTENDA KWAKE.
Vile vile usifurahie kuwa Mtu wa UDHURU!.. Ukidhani Udhuru ni wako ndio utakaomfanya Bwana akuhurumie siku ile, la!.. Yeye siku zote analiangalia Neno lake alitimize na si udhuru zetu..
Luka 9:61 “Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. 62 Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu“.
Luka 9:61 “Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu.
62 Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu“.
Mathayo 10:37 “Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. 39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.
Mathayo 10:37 “Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.
39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.
Jikane nafsi mtu wa Mungu… Unyakuo wa kanisa upo Karibu!
NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.
USIMPE NGUVU SHETANI.
GHARAMA YA UFALME WA MBINGUNI.
Tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na ufalme wa Mungu ni ipi?
Hapo ndipo, atakapompa Mungu Baba ufalme wake.
MWANANCHI WA UFALME WA MBINGUNI
Bwana Yesu asifiwe,
Ufukufu na Heshimu ni vyake milele na milele. Amina.
Napenda tutafakari, Pamoja kwa makini maneno haya ambayo Bwana Yesu alimfunulia mtume wake Petro, ni maneno ambayo yatakufaa sasa wewe kijana ambaye bado una nguvu za kufanya utakalo hivi sasa..
Embu Tusome;
Yohana 21:18 “Akasema, Amin, amin, nakuambia, Wakati ulipokuwa kijana, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na MWINGINE atakufunga na kukuchukua usikotaka”.
Hii kauli ni ya kuitafakari sana, sio ya kuichukulia juu juu, Hapa Bwana anamweleza Petro jinsi ujana wake unavyoweza kumpa uhuru wa ‘nani wa kujifunga chini yake’, na kumtumikia, mfano akiamua, ajifunge na kuwa mtumwa wa mali, uamuzi ni wake, akitaka ajifungue kisha ajifunge kwa mwingine tena, bado uwezo huo anao, leo anaweza akajifunga kwa Mungu, kesho kwa shetani, ni jinsi apendavyo kwasababu nguvu hizo anazo rohoni.
Hapo ndipo lile neno linalosema, “nimewaandikia ninyi vijana kwasababu mna nguvu ya kumshinda yule mwovu”(1Yohana 2:14), linapotimia, maana yake, uwezo wa kujifungua au kujifunga kwa shetani, unao, angali bado una nguvu..
Lakini tunaona Bwana Yesu anampa angalizo lingine na kumwambia, utakapokuwa mzee, “MWINGINE”..Atakufunga na kukuchukua usikotaka..
Sasa ulishawahi kutafakari huyo ‘mwingine’ ni nani?
Huyo mwingine ni Aidha “Mungu” au “Shetani”.. Maana yake ni kuwa utafika wakati, ambapo kama hutajiweka chini ya Mungu tangu sasa, shetani atakuweka chini yake kipindi hicho, penda usipende,..yaani utamilikiwa na shetani asilimia mia ya Maisha yako, na kukufanyia chochote apendacho juu yako..
Ukishafikia hii hatua, kamwe huwezi tena kumgeukia Mungu, wala hata kuzielewa Habari za Mungu, kwasababu tayari wewe ni mfungwa wa shetani.
Hali kadhalika kinyume chake ni kweli, unapofanyika chombo cha Mungu sasa angali una nguvu..utafika wakati huna nguvu, Mungu atakuchukua moja kwa moja na kukupeleka atakapo yeye.. Huko ndipo wakati ambapo uzee wako unaishia vema..hata kama ni kwa kifo kwasababu ya ushuhuda, lakini kamwe hutakaa upotee tena milele..kwasababu umeshafungwa tayari na Mungu, hivyo hakuna namna yoyote utakaa upotee au uanguke mikononi mwa shetani.
Ndio maana biblia inasema..
Mhubiri 12:1 “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.
Maana yake ni kwamba usipomkumbuka muumba wako leo, wakati una nguvu (wakati wa ujana wako) utafikia wakati, utapoteza furaha yako yote ya maisha.. Hicho ndicho kipindi cha kufungwa na ibilisi, na kupelekwa usipotaka..Angalia vema utaona wazee wengi ambao wamekuwa wakipuuzia injili tangu ujanani, mwisho wao huwa hauwi mzuri, kunakuwa na ugumu mkubwa sana kuwashawishi kwa Habari ya wokovu. Huwa wanapitia wakati mgumu sana kiroho kwasababu tayari “mwingine” ameshawafunga na kuwachukua wasipotaka..
Hivyo Bwana Yesu alikuwa anamtahadharisha Mtume Petro, sio tu kwa Habari ya kifo chake, lakini pia kwa maamuzi anayoyachukua sasa..lazima yawe ya busara.. Utumwa anaouchagua sasa, ndio utakaomuhifadhi baadaye..
Kama ni Kristo, basi Kristo atamwokoa, lakini kama ni shetani basi shetani atampeleka alipo yeye..
Ndugu, siku hizi ambazo waweza kusikia injili, na ukashawishika moyoni, ndizo siku zako za ujana, embu sasa anza kujiweka chini ya Kristo, akuongoze, achana na ulimwengu na mambo yake, wanadamu hawawezi kukufaidia chochote kwa siku zijazo.
Anza kuisafisha njia yako sasa, kama vile biblia inavyotushauri katika..
Zaburi 119:9 “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako”.
Kumbuka, ni kipindi kifupi sana tumebakiwa nacho hadi kurudi kwa Bwana Yesu mara ya pili, Kama unadhani, Unyakuo bado sana, fikiria mara mbili, dalili zote zimeshatimia, injili inayoendelea sasa sio ya kubembelezewa wokovu, bali ni ya kujiingiza katika ufalme kwa nguvu. Huna sababu ya kuendelea kufichwa uhalisia, dakika hizi ni za majeruhi, siku yoyote, parapanda inalia, PARAPANDA INALIA!!
Shalom.
PETRO AKAMWAMBIA YESU “BWANA NA HUYU JE”?
NI YESU YUPI UMEMPOKEA?, NI ROHO IPI UMEIPOKEA? NA INJILI IPI UMEIPOKEA?
Je! Ni kanisa lipi sahihi kumuabudia Mungu?
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.
Ni sahihi kusema sikuitiwa kuhubiri ubatizo kama Paulo alivyosema (1Wakorintho 1:17)?.
LAKINI WAKATI WA TAABU WATASEMA, SIMAMA UKATUOKOE.
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
Katika 1Wakorintho 1:17, Paulo anasema hakuitiwa kubatiza, Je na mimi kama sijaitiwa kubatiza, bali nimeitiwa kuhubiri watu waokoke tu!, nitakuwa na hatia, nisipohubiri suala la ubatizo wala kuligusia kabisa?
Jibu: Ni muhimu kufahamu kuwa kila mtumishi wa kweli wa Mungu, haijalishi awe nani, ameitiwa KULIHUBIRI NENO LA MUNGU KATIKA UKAMILIFU WOTE, pasipo kubagua kipengele chochote katika maandiko. Huo ndio wito tuliopewa..
Tutatofautiana tu namna ya kuhubiri, kwasababu tunazo karama mbali mbali lakini INJILI NI MOJA KWETU WOTE!, Na wote tutahubiri kitu kimoja.. Hakuna mahali tumepewa maagizo ya kuhubiri tofauti tofauti au kulipunguza Neno la Mungu.
Sasa tukirudi kwenye swali, ni kwanini Paulo aseme sikuitiwa kubatiza?
Hebu tusome, mstari huo kwa utarati kisha tuendelee..
1Wakorintho 1:17 “Maana Kristo HAKUNITUMA ILI NIBATIZE, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika”.
Hapa hakusema “MAANA KRISTO, HAKUNITUMA NIHUBIRI UBATIZO,” lakini badala yake anasema “KRISTO HAKUNITUMA NIBATIZE”. Maana yake kuhubiri Ubatizo Paulo alikuwa anauhubiri kama kawaida,(Soma Matendo 19:1-5 utalithibitisha hilo), lakini kitendo cha kufanya Ubatizo hakuwa anakifanya sana, bali mara moja moja sana… Ndio maana tukirudi juu kidogo katika mistari hiyo tunaona yeye mwenyewe anajishuhudia kubatiza watu baadhi..
1Wakorintho 1:14 “Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ILA KRISPO NA GAYO; 15 mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16 TENA NALIWABATIZA WATU WA NYUMBANI MWA STEFANA; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine”.
1Wakorintho 1:14 “Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ILA KRISPO NA GAYO;
15 mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu.
16 TENA NALIWABATIZA WATU WA NYUMBANI MWA STEFANA; zaidi ya hao, sijui kama nalimbatiza mtu ye yote mwingine”.
Umeona hapo anasema aliwabatiza Krispo, na Gayo Pamoja na watu wa nyumbani mwa Stefana.. Kuashiria kuwa alikuwa anabatiza, lakini hakuwa anaifanya hiyo huduma mara kwa mara, kulinganisha na huduma ya kwenda kuzunguka huku na huko kuhubiri Neno kwa watu aliyokuwa anaifanya.. Na wote walioamini injili yake aliwaongoza katika makanisa wabatizwe au watu maalumu wakabatizwe!..ili yeye apate nafasi ya kuendelea kuhubiri injili sehemu nyingine…Na ilipotokea hakuna mtu wa kuwabatiza kwa mahali hapo, basi alichukua yeye hilo jukumu la kuwabatiza!. kama hapo kwenye Matendo 19:2-6.
Ni sawa na jinsi Mitume walivyogawanya jukumu la kuwahudumia wajane, kwa wale Mashemasi 7 ili wao wadumu katika kulihubiri Neno.
Matendo 6:2 “Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, HAIPENDEZI SISI KULIACHA NENO LA MUNGU NA KUHUDUMU MEZANI. 3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; 4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno. 5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; 6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao”.
Matendo 6:2 “Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, HAIPENDEZI SISI KULIACHA NENO LA MUNGU NA KUHUDUMU MEZANI.
3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;
4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.
5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;
6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao”.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba, Hakuna mtu yeyote ambaye ameitiwa kufundisha Neno moja la kwenye biblia na kuliacha lingine…Wote tunapaswa tuhubiri injili yote, iliyo kamili, yaani injili ya toba, ubatizo, Imani, Roho Mtakatifu, na mambo mengine yote ya kiimani, pasipo kupunguza chochote wala kuongeza. sawasawa na (Ufunuo 22:18-19).
Sababu kuu inayowafanya asilimia kubwa ya wahubiri wabague baadhi ya maneno kwenye biblia na kufundisha baadhi tu, ni kwasababu wanaogopa kuumiza hisia za watu au kupoteza waumini!, na wala si kitu kingine!!.. Jambo ambalo ni la hatari sana!.. kuacha kuhubiri Neno la Mungu kwasababu ya kohofia hisia za mtu, atajisikiaje, au atakuonaje.
Ni heri kuonekana hufai, lakini umelizungumza Neno la Mungu katika ukamilifu wote, Ni heri mtu ahuzunike moyoni kwasababu ya kweli ya Neno uliyomweleza, kwasababu itamuumiza moyo sasa, lakini baadaye itakuwa ni tiba kwake na atakuja kumshukuru Mungu sana kwaajili yako..
2Wakorintho 7:10 “Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti”.
Lakini unajua kabisa ubatizo aliobatizwa sio sahihi, mavazi anayovaa sio ya kiimani, kazi anayoifanya sio halali, na kwasababu unaogopa usiumie utakapomwambia ukweli, unaishia kumfariji kuwa wewe hujaitiwa kuhubiri ubatizo au Mavazi au kazi mtu anayoifanya, wewe umeitiwa kumhubiria amwamini Yesu tu!.. Fahamu kuwa ndio unazidi kumpoteza huyo mtu!.
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.
Kuhubiri injili kwa husuda na fitina ndio kupi?
Ulishawahi kukutana na kundi la watu ambao linakutafuta tu wakati wa shida, kama ndio, kuna hali Fulani unajisikia ambayo sio nzuri, ni kweli wapo ambao mazingira yanawabana washindwe kukutafuta nyakati nyingine, lakini wapo ambao wewe kwao ni mtu wa kuwatatulia tu matatizo, Habari nyingine na wewe hawana..
Kuna mtu mmoja alikuwa ananifuata nimtatulie tu matatizo yake, lakini baada ya hapo ukimpigia hata simu umsalimie, hapokei, na anabadilisha line ya simu moja kwa moja ili usimpate, baadaye anakuja kukutafuta tena, na jambo linalofuata hapo ni kuomba msaaada..
Unajua hata kama utamsaidia, lakini utasema kwanini iwe hivi, kwanini tusiwe na mahusiano hata na nyakati nyingine zote..
Sasa hiyo hali ndiyo ambayo Mungu anapitia sasahivi kwa wanadamu wengi duniani, biblia inasema..
Yeremia 2:27 “waliambiao gogo la mti, Wewe u baba yangu; na kuliambia jiwe, Ndiwe uliyenizaa; kwa maana wamenipa mimi visogo, wala hawakunielekezea nyuso zao; LAKINI WAKATI WA TAABU WATASEMA, SIMAMA UKATUOKOE”.
Umeona, wanadamu wengi sasa kinachowapeleka kwa Mungu, si kingine Zaidi ya kuomba, wafunguliwe, kuomba waponywe, kuomba wafanikishwe kiuchumi, kuomba kazi, n.k.
Lakini ukiangalia mahusiano waliyonayo na Mungu ni hafifu sana au hakuna kabisa.. Hana muda wa kusoma biblia kuyajua mapenzi ya Mungu ni nini katika Maisha yake, kumaliza hata dakika 20 kila siku katika kutafakari Neno la Mungu hawezi, kuomba kunamshinda, kwenda ibadani ni mara moja kwa mwezi, ikizidi sana mara mbili, na hata akienda ni ili Mungu amjibu lile ombi lake alilomuomba lakini sio kumwabudu katika Roho na Kweli.
Anachokiona kirahisi kwake, ni kwenda kununua maji ya upako na mafuta, ili amwage kwenye biashara zake, ili mambo yake yaende sawa.. Au pale anapopitia hali mbaya sana ya magonjwa ndipo anapomfuata Mungu ili amsaidie,. Hapo ndipo atafunga na kuomba, na kusoma Neno kila siku kwa bidii..Lakini siku nyingine zote anaishi maisha ya dhambi.
Ndugu, tujue kabisa Mungu hapendezwe na huo mfumo wetu wa Maisha, Mungu ametuzira watu wengi sana na sisi hatujui, ndio maana inakuwa ngumu sana kusaidiwa na Mungu kwasababu, Maisha yetu ni ya kinafki mbele zake.
Lakini ukiendelea kusoma pale Bwana anasema..
Yeremia 2:27 “waliambiao gogo la mti, Wewe u baba yangu; na kuliambia jiwe, Ndiwe uliyenizaa; kwa maana wamenipa mimi visogo, wala hawakunielekezea nyuso zao; lakini wakati wa taabu watasema, Simama ukatuokoe. 28 LAKINI WAKO WAPI MIUNGU YAKO ULIOIFANYA? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawasawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda. 29 MBONA MNATAKA KUTETA NAMI? Ninyi nyote mmeniasi, asema Bwana”.
Yeremia 2:27 “waliambiao gogo la mti, Wewe u baba yangu; na kuliambia jiwe, Ndiwe uliyenizaa; kwa maana wamenipa mimi visogo, wala hawakunielekezea nyuso zao; lakini wakati wa taabu watasema, Simama ukatuokoe.
28 LAKINI WAKO WAPI MIUNGU YAKO ULIOIFANYA? Na wasimame hao, kama wakiweza kukuokoa wakati wa taabu yako; kwa maana hesabu ya miungu yako ni sawasawa na hesabu ya miji yako, Ee Yuda.
29 MBONA MNATAKA KUTETA NAMI? Ninyi nyote mmeniasi, asema Bwana”.
Umeona tusimgeuze Mungu kama ni sehemu ya kutatulia matatizo yetu tu, ili hali Maisha yetu hayaendani na wokovu. Tusitete na Mungu, Mambo hayo kayafanye kwa waganga wa kienyeji lakini usifanye kwa Mungu, kwasababu utajikuta unaangukia tu laana badala ya baraka.
Hivyo tuanze sasa, kumtafuta Mungu nyakati zote, tuhakikishe tunayatenda mapenzi yake, tuonyeshe bidii zetu kwake, kwamba tunampenda sio kiunafiki, bali kwa mioyo yetu kweli. Tunamtafuta sio atufanye kuwa mabilionea, bali atufanye kuwa wana wake kama Yesu Kristo. Na ndio sasa hata hayo mengine atasaidia bila hata kutumia nguvu wala kumwomba..
Kumbuka katika nyakati hizi za mwisho, watakaokwenda kwenye UNYAKUO, sio kila mtu asemaye ninamwamini Mungu tu, halafu basi,..Bali ni watu wayatendao mapenzi ya Mungu kikamilifu sawasawa na Neno la Kristo.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”
Bwana atupe jicho la kuona, na kuyatendea kazi.
USIJARIBU KUMGEUZA MUNGU MGANGA WA KIENYEJI,UTAKUFA.
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
WAKATI ULIOKUBALIKA NALIKUSIKIA
JINSI UNAJISI UNAVYOMGHARIMU MTU.