SWALI: Kwanini watu watakaohukumiwa siku ile ya mwisho, wanaonekana kutofautishwa katika sehemu mbili, wengine watatokea “baharini”, na wengine katika “mauti na kuzimu”. Kwanini iwe hivyo na tofauti ya maeneo hayo ni ipi?
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 BAHARI IKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE; NA MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 BAHARI IKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE; NA MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
JIBU: Hukumu ya mwisho kabisa ni hukumu ijulikanayo kama “hukumu ya kiti cheupe cha enzi cha mwanakondoo”. Ni hukumu inayokamilisha wafu wote walioko makaburini, mbali na watakatifu.
Haitachagua wakubwa, wala wadogo, vijana au wazee. Waovu wote watafufuliwa wakati huu na kila mmoja atahukumiwa sawasawa na matendo yake, kisha atatupwa katika lile ziwa la moto, aangamie huko milele.
Lakini biblia inatuonyesha siku hiyo waovu hao watatoka sehemu kuu mbili,
Kumbuka, lugha iliyotumika hapo ni lugha ya kinabii, na sio halisi kabisa kwamba bahari inayo wafu wake. Hapana.
Je Bahari ikawatoa wafu waliokuwa ndani yake, kunamaanisha nini?.
Tukianzana na wafu waliokuwa baharini. Tabia ya bahari sikuzote ni kubwa, haina mwisho, ukipotea humo, umepotea moja kwa moja. Na kibiblia maji mengi(bahari) inamaanisha ulimwengu.
Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha”.
Hii ikiwa na maana sikuile ya mwisho, wafu wote, yaani waovu wa mataifa yote, wa lugha zote, waliokufa tangu Adamu, hadi wakati wa kurudi kwa Bwana Yesu kulinyakuwa kanisa lake (siku ya unyakuo). Wote hao watakuwa katika kundi la wafu watokao baharini. Watafufuliwa na kuhukumiwa.
Mauti na kuzimu kulifunua nini?
Lakini mara baada ya unyakuo kupita. Kuna tukio lingine litafuata, ambalo linajulikana kama dhiki kuu.
Kipindi hichi kinajulikana kama kipindi cha utawala wa shetani(mpinga-kristo), watu wengi sana watauliwa, kutokana na dhiki ambayo Mungu ataruhusu shetani aisababishe, kwa waovu wote, watakaobakia duniani. (Tukiachia mbali wale ambao watakataa chapa ya mnyama). watauawa.
Ukisoma Ufunuo 6:8 inasema.
“Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda JINA LAKE NI MAUTI, NA KUZIMU AKAFUATANA NAYE. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi”.
Umeona huyu farasi wa kijivujivu anaitwa mauti, akiambatana na kuzimu. Ambaye ni ibilisi akifanya kazi yake wakati huo. Naye atasababisha vifo vya robo ya watu waliopo duniani wakati huo. Kwamfano kwa dunia ya sasa ni Zaidi ya watu BILIONI 2, watauawa, na hiyo itakuwa ni katika mapigo ya ghadhabu ya Mungu, na vita vya Harmagedoni, na magonjwa, na wote hawa watakaokufa moja kwa moja watakuwa chini ya “Mauti na kuzimu”.
Sasa biblia inaposema Mauti na Kuzimu ikatoa wafu wake, umeshaelewa kuwa ni wafu waliokufa katika hichi kipindi cha Dhiki kuu, ambao kimsingi walikuwa chini ya mpanda farasi wanne, aliyeitwa mauti na kuzimu.
Sasa kwanini sehemu zote mbili zitajwe?
Ni kuonyesha kuwa hukumu hiyo haitambakisha mfu hata mmoja. Itakuwa ni hukumu ya ulimwengu mzima kwa wale ambao hawakunyakuliwa, Au kuikataa cha ya mnyama.
Ikiwa leo hii umekufa kama mlevi, au fisadi, au kihaba, utakapokufa utakwenda katika Habari la kiroho. Lakini ikiwa utakufa katika dhiki kuu, vilevile utakwenda katika katika mauti na kuzimu. Na wote siku ya mwisho mtafufuliwa. Na kuhukumiwa, kila mmoja kwa kipimo chake. Kisha mtatupwa katika ziwa la moto.
Ndugu, hukumu ya Mungu ni ya kuiogopa sana, kwasababu hakuna nafasi ya pili baada ya kifo. Ukifa leo ghafla, ni moja kwa moja jehanamu ukisubiria siku hiyo ya ufufuo ifike, Kwanini hayo yote yatukute? Watu walio kuzimu leo hii Ni kilio na majuto ndivyo vinavyoendelea, wanatamani wangepata hata dakika 2 za kutubu lakini hawana. Wewe muda unao. Lakini unafurahia ulimwengu.
Mgeukie Kristo, leo akusamehe dhambi zako. Tubu kwa kumaanisha kabisa kuuacha ulimwengu na tamaa zake zote. Dhamiria kumfuata Yesu, naye atakuokoa, katika dakika hizi za majeruhi. Kumbuka Unyakuo ni wakati wowote, hilo linafahamika. Muda umeisha, dalili zote zimeshatimia. Mlango wa neema kwa mataifa hivi karibuni utafungwa.
Bwana atusaidie.
Maran Atha.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.
MPINGA-KRISTO
UTAWALA WA MIAKA 1000.
JE MGOGORO WA URUSI NA UKRAINE,UMETABIRIWA KIBIBLIA?
Rudi nyumbani
Print this post
Injili ya Yesu Kristo imejificha katika viumbe vya asili. Bwana mahali biblia inamfananisha Bwana Yesu na Mwanakondoo, sehemu nyingine kama Simba, sehemu nyingine Bwana Yesu anafanishwa na “Jiwe” , mahali pengine Roho Mtakatifu anafanishwa na Huwa (njiwa).
Lakini pia kuna mahali Bwana Yesu alituwaambia tuwatazame kunguru pamoja na Maua ya kondeni (Luka 12:24), na sehemu nyingine aliufananisha mbinguni na Wafanya biashara, na sehemu nyingine wakulima, na sehemu nyingine aliufananisha na wavuvi wanaokwenda kuvua..Na sehemu nyingine aliwafananisha watu kama samaki wanapaswa kuvuliwa.
Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba Injili ya Bwana Yesu Kristo imejificha pia katika viumbe vya asili. i.
Hivyo wakati mwingine hatuna budi kujifunza juu ya baadhi ya viumbe, na kupata hekima..
Leo tutamtazama Samaki mmoja aitwaye Eeli.
Je unamjua Samaki aina ya Eeli? Je unayajua maajabu yake?, na Injili gani imejificha nyuma ya Maisha yake?
Eeli ni Samaki ambao ni familia moja na Kambale. Samaki hawa wanaishi katika maji mafupi, . Lakini Samaki hawa maajabu yake ni kwamba wanatengeneza umeme mkubwa sana katika miili yao, ambao umeme huo wanautumia kujilinda dhidi ya maadui na kujitafutia vitoweo.
Eeli anapokumbana na hatari mbele yake, labda Samaki mwingine aliye mkubwa kuliko yeye, au kiumbe kingine chenye kutishia usalama wake, basi huitoa shoti hiyo na kumpiga adui yake.
Na kiwango cha umeme Samaki Eeli mmoja anachoweza kuzalisha kwa pigo moja ni mpaka Volti 650, na wakati Volti za 150 tu zinatosha kumuua Mwanadamu, lakini yeye hutoa hadi volti hizo 650, ambazo kama zikimfikia mwanadamu, sio tu kumuua papo kwa hapo, bali pia zinaweza kumuunguza viungo vyake vya ndani.
Lakini Pamoja na kwamba Samaki huyu, anayo silaha hatari namna hiyo kuliko samaki wote, ambayo inaweza kumuua mtu au kiumbe hai chochote ndani ya dakika moja, lakini bado ni Samaki mpole sana, bado hayupo katika orodha ya viumbe au viumbe hatari duniani. Hayupo hata 100 bora ya viumbe hatari, hata samaki sangara kamzidi kwa ukali!.
Ni samaki ambaye ni hatari sana lakini anayejihadhari sana na maadui zake, na asiyetumia uwezo wake wote kiasi kwamba hata ikitokea kakanyagwa na mtu ndani ya maji kwa bahati mbaya, yeye hutoa kiwango kidogo tu cha shoti, ambacho kitamshtua adui yake, amwache au akae mbali naye lakini si kumuua kabisa.
Tofauti na Samaki wengine kama samaki jiwe, au jelly au papa ambao hawana silaha kali kama hiyo, lakini ni wakorofi mno, kiasi kwamba akipita adui mbele yao, au akihisi hatari basi ana uwezo wa kutumia uwezo wake wote, kudhuru.
Laiti Eeli angekuwa mwenye hasira kama za Papa, au samaki mwingine yeyote, leo hii angeshika nafasi ya kwanza kwa viumbe hatari ulimwenguni. Kwasababu hakuna kiumbe chochote chenye silaha kali kama hiyo, hata nyoka ijapokuwa sumu yake ni kali na inayoua kwa haraka, kama mtu hajapatiwa matibabu..
Eeli yeye silaha yake ya shoti, inaua papo kwa hapo endapo akitumia uwezo wake wote. Na kutokana na maisha yake hayo imemfanya kuwa moja ya samaki wanaoishi muda mrefu sana, mpaka kufikia miaka 85.
Ni nini tunajifunza kwa Eeli?
Na sisi kama watu wa Mungu, tunazungukwa na nguvu za Mungu, kwa kiwango kikubwa sana… Lakini Nguvu hizi hatupaswi kuzitumia kuharibu wengine, nguvu hizi zimo ndani yetu, kutulinda tu na mishale ya yule adui, lakini si kutufanya tuonekane watofauti duniani.
Hebu tumtazame mmoja aliyekuwa kama huyu Samaki Eeli, ambaye alikuwa na nguvu nyingi kuliko wote, lakini hakuutumia uwezo wake wote..
Tusome,
Luka 9:51 “Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu; 52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. 53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. 54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? 55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] 56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”.
Luka 9:51 “Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;
52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.
53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.
54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine”.
Hapo Bwana Yesu alikuwa ana uwezo wa kushusha moto, na ndani ya dakika moja wale wale wasamaria wangekufa wote, bila kubakia hata mmoja lakini, hakuutumia uwezo wake huo, bali aliwarehemu kwasababu alikuwa anajua hawajui watendalo. Soma tena kisa kama hicho hicho katika Mathayo 26:51-53.
Na sisi pia hatuna budi kuwa kama Bwana Yesu..Bwana Yesu alipigwa lakini hakurudishwa, ingawa alikuwa na uwezo wa kurudisha mapigo makali, alitukanwa lakini hakurudisha matusi, aliambishwa lakini hakuabisha, ingawa alikuwa na uwezo wa kuabisha..n.k.
Alikuwa mfano wa Eeli ambaye anao uwezo mwingi lakini ni pole..
Wafilipi 4:5 “Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu”.
Hatupaswi kuwalaani watu kwa jina la Bwana, hata kama wanatumia nguvu za giza, tunachopaswa kukilaani na kukiharibu ni zile kazi wanazozifanya, na tunazilaani kwa kuomba, kuhubiri, kusoma Neno na kuishi maisha matakatifu..
Tuwe kama Eeli.
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
Je! Ni kweli kuna samaki mtu (Nguva) Baharini.
UVUVI BORA HAUCHAGUI, CHA KUVUA.
Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?
SWALI: Mwandishi, alimaanisha nini, kusema Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi? (Wimbo 1:5-6)
JIBU: Tusome,
Wimbo 1:5 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. 6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda”.
Wimbo 1:5 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda”.
Huyu ni mwanamke , anayejaribu kueleza hali yake ya nje jinsi inavyoonekana, ilivyo tofauti na uhalisia wake wa ndani. Anaanza kwa kusema mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Yaani japokuwa naonekana ni mweusi, nisiyevutia, lakini ninao uzuri wa kupendwa hata na mfalme,
Mstari wa 6 anaendelea kueleza Weusi wake, ulitokana na nini,.. Anasema, ulitokana na kazi za mashambani, ambazo aliwekwa kama mlinzi azisimamie, ikiwa na maana muda wote a jua linapochomoza jua linapozama, ni lazima awepo pale alitunze,
Wakati ndugu zake, wakiwa wamestarehe nyumbani kwenye uvuli wa makasri, wakila na kufurahi, yeye yupo mashambani anatanga na jua.
Na kwa kawaida, mtu anayekaa kwenye jua muda mrefu Ngozi yake itakuwa nyeusi tu, na vilevile itapunguza mvuto. Ndicho kilichomkuta huyu binti, aliyekuwa tofauti na mabinti wengine, kama ilivyozoeleka kuwa mabinti huwa hawakai mashambani, wala hawafanyi shughuli za ulinzi, . Lakini yeye alikuwa hivyo, na katika hayo yote anasema bado anaoozuri unaotoka ndani.
Huyu binti anafananishwa na watumishi wa Mungu, wanaotumika katika shamba la Mungu, ambao pengine kutwa kucha wanajitaabisha kuwapelekea wengine Habari njema,(Vijinini na mijini, na kwa njia mbalimbali), sasa kwa taabu hizo, kwa kawaida ni lazima watakosa vitu vingi vyema, kwasababu muda wote wapo mashambani, pengine watakuwa wadhaifu kimwili/au kimwonekano, watakuwa hawana mali, watakuwa hawana mvuto wowote. Lakini Bwana anawaona ni wazuri sana,
Mtume Paulo aliliona hilo akasema,
2Wakorintho 4:16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; 18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
2Wakorintho 4:16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
Kuonyesha kuwa utu wetu wa nje, waweza kuchakaa kwasababu ya utumishi, lakini ule wa ndani wafanywa upya kila siku, Sehemu nyingine aliandika Maisha ya utumishi ni ya kufa kila siku, kujitoa kwa wengine na sio kwa ajili yako, kama huyu binti (1Wakorintho 15:31).
Hivyo na wewe ambaye, unamtumikia Bwana kwa uaminifu, pengine wajiuliza, mbona mwonekano wangu haupo, kama nilivyokuwa hapo nyuma simtumikii? Fahamu kuwa upo shambani, jua litakuwa ni lako, lakini uzuri wako unatoka ndani na Mungu anauona, na anapendezwa na wewe.
Siku zitakuja, utapewa mwili wa utukufu, mwili usioonja uharibifu, mwili wa milele, ndipo utakapojua kuwa wewe ulipendwa na Bwana, na hiyo haikuwa kwa mwonekano wako, lakini kwa uaminifu wako.
Shalom.
UBATILI.
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?
Kuvyaza ni nini katika biblia? (Ayubu 21:10).
KWANINI MIMI?
ANGALIA UZURI WAKO, USIGEUKE KUWA KITANZI CHAKO.
NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.
Donda-Ndugu ni nini?
Je unajua ubatizo unaua na vile vile unaokoa?.
Ipo siri kubwa sana katika ubatizo ambayo laiti watu wengi wangeijua wangeutafuta kwa bidii zote.
Hebu tusome mistari ifuatayo,
1 Petro 3:20 “watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, WALIOKOKA KWA MAJI. 21 MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO, UNAOWAOKOA NINYI PIA SIKU HIZI; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo”.
1 Petro 3:20 “watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, WALIOKOKA KWA MAJI.
21 MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO, UNAOWAOKOA NINYI PIA SIKU HIZI; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo”.
Hapo kuna vitu 3 vya kuzingatia katika mistari hiyo..na tutatazama kipengele kimoja baada ya kingine.
1. WATU WANANE WALIOKOKA KWA MAJI.
Hapa tunachoweza kuona ni kwamba..“kumbe maji ni njia ya wokovu?”. Nuhu pamoja na mkewe na wanawe watatu na wake zao, jumla nafsi 8, waliokoka kwa maji!!!!!
Wakati wengine wasioamini wanaangamia kwa maji, Nuhu aliyeamini, maji hayo hayo yanamwokoa na ghadhabu ya Mungu. Hili ni jambo la kwanza la kuzingatia…hebu tulitazame jambo la pili.
2. MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO, UNAOWAOKOA NINYI PIA SIKU HIZI.
Kumbe kama Nuhu alivyookoka kwa Maji zamani hizo, na sisi siku hizi hatuna budi kuokoka kwa kupitia maji hayo hayo? Yaani kwa Kubatizwa. Si ajabu Bwana Yesu alisema katika Marko 16:16 kuwa..“Aaminiye na kubatizwa ataokoka”..na si “atakayeamini tu peke yake”
Huu ni ufunuo mkubwa sana ambao Mtume Petro alifunuliwa na Roho Mtakatifu..
Kumbe wakati sisi tunasoma habari za gharika ya Nuhu kama gazeti, kumbe nyuma yake kuna ufunuo wa ubatizo..
Si ajabu na Yohana Mbatizaji pengine naye alitolea ufunuo wa ubatizo humu humu. Unapomwamini Yesu (Ni sawa na umeingia ndani ya safina kama Nuhu)..unapobatizwa kwa kuzamishwa katika maji mengi na kuibuka juu (Ni sawa na umeingia kwenye gharika ukiwa ndani ya safina na umetoka salama).
Na kama vile baada ya gharika Mambo yote yakawa mapya kwa Nuhu, akaingia katika ulimwengu mpya na kuanza maisha mapya, yale ya kwanza yenye shida na dhuluma na maasi yamepita. (Kwa ufupi uchafu wote wa kwanza ukaondoka).
Vivyo hiyo na sisi tunapobatizwa katika roho tunaondoa uchafu wote unaozunguka maisha yetu ya kiroho… Yale maisha ya kale yanazikwa, zile dhambi za kale zinaisha nguvu, kile kiburi cha kale kinafifia n.k Faida hii kuu inatupeleka katika kipengele cha tatu na cha mwisho.
3. SIYO KUWEKEA MBALI UCHAFU WA MWILI, BALI JIBU LA DHAMIRI SAFI MBELE ZA MUNGU.
Kumbe lengo la ubatizo sio kuondoa uchafu wa mwilini kama JASHO au VUMBI..bali ni kuondoa uchafu wa rohoni ambao huo ndio jibu la Dhamiri zetu safi mbele za Mungu.
Swali ni Je! umebatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu kulingana na Matendo 2:38?.
Kama bado unasubiri nini na tayari umeshajua faida zote hizi?..Haraka sana katafute ubatizo sahihi, kwa gharama zozote baada ya wewe kumwamini Bwana Yesu na kutubu dhambi zako.
Kama unapata ugumu kupata sehemu ya ubatizo, basi unaweza kuwasiliana nasi kwa namba zilizopo chini ya somo, tutakusaidia, kukuelekeza mahali karibu na ulipo.
Bwana akubariki.
UBATIZO NI NINI NA ULIO SAHIHI NI UPI?
KWANINI UBATIZO NI WA MUHIMU.
Je! Ni kweli ubatizo wa maji hatuuhitaji tena?
Je! Unaweza kubatizwa na usipokee Roho Mtakatifu?. Na Je! Unaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono?
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
Sulemani kwa uvuvio wa Roho alipewa kujua kati ya mambo sita yanayomchukiza Mungu, mojawapo ni mikono imwagayo damu za watu.(Mithali 6:17).
Na sehemu nyingi sana katika maandiko utaona Bwana akiwakemea watu wake kwa dhambi hii ya umwagaji damu, kwamfano ukisoma hapa utaona anasema,
Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. 16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; 17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane”.
Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane”.
Soma na hapa pia;
Ezekieli 9:9 “Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, naye Bwana haoni”.
Sehemu kadha wa kadha, Mungu alipowaona watu wake aliona damu nyingi mikononi mwao.. (Isaya 59:3, Yer 22:3, Eze 23:37, 45).
Sasa ni rahisi kudhani kuwa, katika mwili ni kweli walikuwa ni wauaji, wanawaua watu kwa siri au wanauana wao kwa wao ovyo . Hapana si kweli, Waisraeli hawakuwa hivyo. Kama tu vile walimwengu wengi wasasa walivyo leo.
Hivyo wenyewe hawakuelewa Mungu alikuwa anawaonaje matendo yao kwa jinsi ya Roho,
Hadi Bwana Yesu alipokuja kutufunulia jambo hilo katika agano jipya Mungu alikuwa anamaanisha nini;
Tusome.
1Yohana 3:15 “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake”.
Akaeleza, kwa undani Zaidi, jinsi mtu wa namna hii ambaye, anamchukia ndugu yake, anavyostahili adhabu sawa tu na yule Mhalifu aliyemwaga damu ya mtu.
Mathayo 5:22 “Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto”.
Ndugu unayesoma haya maneno, tufahamu kuwa, tunaweza tukawa ni waombaji wazuri, ni waalimu wazuri, ni wasaidizi wazuri, ni wachungaji wazuri, lakini mbele za Mungu tukawa watu hatari sana, tukaonekana kama wahalifu sugu kabisa, ambao tumeuwa roho za watu wengi sana, mikono yetu inabubujika damu, tumeshika visu, na mapanga, na mashoka, tunaua, na bado tunaendelea kuua watu kila siku. Sababu ni nini? Sababu ni chuki zilizopo mioyoni mwetu kwa watu wengine.
Tunapokuwa na visasi na watu, au hasira, Mungu anatuona tunastahili jehanamu ya moto. Hata sadaka yetu tunayompelekea yeye bado anaiona ni chukizo kubwa sana, ndio maana asema tusiitoe mpaka tutakapopatana kwanza na majirani zetu.
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, 24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.
Hivyo, tujifunze kuachilia, ili tusiwe wauaji, na njia pekee ya kuweza kuishinda hiyo hali, ni kuwa mtu wa kutafakari sana Neno la Mungu. Kwani Neno ni tiba, inayotupa maonyo,na Faraja na ushauri, ukiona hiyo hali inakushinda, fahamu kuwa kiwango chako cha utafakariji wa maandiko ni kidogo..
Lakini tunaposoma lile Neno mfano lile andiko linalosema, ndugu yako akikusoma, mara ngapi umsamehe.. Na Bwana akajibu na kusema, hata SABA MARA SABINI.. Yaani mara 490, kwa siku moja,(Mathayo 18:22) tutagundua ni nini maana ya msamaha.. Ni Zaidi ya vile tunavyofikiria, ni Zaidi ya kuachilia mambo yote, na kukubali kuonekana mjinga, ni Zaidi ya kukubaliana na kila hali. Hapo ndipo tutakapojua hakuna sababu ya kushikamana na kila jambo ndugu zetu au marafiki, au majirani zetu wanayotufanyia, au kutuudhi kwayo.
Kwasababu katika hayo yote hawajawahi kuyarudia mara 490, kwa siku, pengine ni mara mbili tu au kumi. Hivyo tunapaswa tusamehe.
Bwana atusaidie sana, mkono yetu iwe safi kama ya mwanakondoo wake Yesu Kristo.
Ndipo tutakapomkaribia Bwana wetu na kutubariki.
Ayubu 17:19 “Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu”.
RACA
KIFAHAMU KIGEZO CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.
Unyenyekevu ni nini?
JIFUNZE NAMNA YA KULITUMIA NENO LA MUNGU.
JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA?
USIWE ADUI WA BWANA
MIAMBA YENYE HATARI.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, libarikiwe.
Zipo njia nyingi za kuvuta rehema za Mungu, juu yako.. baadhi ya hizo ni kuwa Mwombaji, mtoaji, na mtu wa kusamehe.
Lakini ipo njia nyingine ambayo tukiijua basi, siku zote tutakuwa watu wa kupata rehema kutoka kwa Bwana na hata kama kuna mabaya tuliyofanya mbele za Mungu, basi anatusamehe na kughairi kutuadhibu.
Na njia hiyo si nyingine Zaidi ya “kutojilipiza kisasa” au kutofurahia “anguko la wanaofanya vita nawe”.
Watu wengi leo hususani Wakristo, wanakosa maarifa kwa kudhani kuwa Mungu anapendezwa sana na anguko la maadui zao. Hivyo kila siku, na kila saa wanawaombea shari maadui zao, na kila siku wanakaa wakisubiria anguko lao ili wafurahi.. (Kama vile Nabii Yona alivyokaa chini ya mtango, akingoja kuona Ninawi inaangamizwa).
Na hiyo yote ni kutokana na jinsi tulivyofundishwa au kujifunza. Pasipo kujua kuwa hayo sio mapenzi ya Mungu kabisa.. Ingekuwa Mungu ana hasira sana na adui yako, nadhani asingemuumba kabisa.. Lakini mpaka unamwona anaishi, jua ni mapenzi ya Mungu yeye awepo pale..
Sasa hebu tujifunze mstari ufuatao ili tuweze kuelewa vizuri..
Mithali 24:17 “Usifurahi adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo; 18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.
Mithali 24:17 “Usifurahi adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo;
18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”.
Umeona hapo?..Anasema usifurahi, ukimwona adui yako anaanguka!.. kwasababu Bwana kamwangusha kwa lengo la kumnyenyekeza na si kwa lengo la kumwangamiza kabisa!, kama wewe unavyofikiri..
Hivyo unaposhangilia anapoadhibiwa na Mungu, jambo hilo halimpendezi kabisa Mungu… na Bwana akiona unashangilia kuanguka kwake, basi anaghairi ule ubaya na kukugeukia wewe. (Kwasababu na wewe sio kwamba ni mkamilifu mbele zake, kwamba haustahili adhabu yoyote, unazo kasoro nyingi sana, isipokuwa Mungu ni mvumilivu kwako).
Vile vile, watu wanaofanya vita na wewe na kukushutumu, kukusengenya, kukulaumu, kukuudhi, kukuumiza, au hata kukutesa pasipo hatia yoyote, usijaribu kamwe kuwarudishia mabaya, wala kuwashitaki mbele za Mungu, wewe waombee rehema…na kubali mashutumu yao..Kwasababu kwa kufanya hivyo, Mungu, sio kwamba utakuona wewe ni mjinga mbele zake, kinyume chake utaonekana mwenye busara na hivyo utapata rehema Zaidi na kibali mbele zake.
Usichukizwe na laana watu wanazokulaani, kwasababu laana hizo kwako, ndio baraka kwako, mashutumu hayo unayoshutumiwa, Mungu anayasikiliza na yanamhuzisha, hivyo Bwana atakupa wewe rehema kwa mashutumu hayo, atakuhurumiwa kwa masengenyo hayo…N.k
Daudi aliijua hii siri, ndio maana kamwe hakuwahi kutoa Neno la laana kwa waliokuwa wanamlaani, wala hakuwahi kufurahia kuanguka kwa waliokuwa wanaitafuta roho yake, ndio maana utaona alilia sana, siku Sauli alipokufa, vile vile alilia sana Absalomu, mwanae alipokufa!..ambao hawa wote walifanyika maadui zake.
Sasa ni kwanini hakuwalaani waliokuwa wanamlaani?, ni kwasababu alijua KUWA KULAANIWA KWAKE NA WATU NDIO KUBARIKIWA KWAKE NA BWANA.
Utakumbuka wakati Fulani alipokuwa anamkimbia Mwanae Absalomu, alikutana na mtu mmoja aliyeitwa Shimei, mtu huyo alianza kumlaani, lakini Daudi hakurudisha laana hata moja, wala hakumwua ingawa alikuwa anao huo uwezo.
2 Samweli 16:5 “Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; ALITOKA, AKALAANI ALIPOKUWA AKIENDA. 6 Tena akamtupia Daudi mawe, na watumishi wote wa mfalme Daudi; na watu wote na mashujaa wote walikuwako mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto. 7 Na Shimei alipolaani, alisema hivi, NENDA ZAKO! NENDA ZAKO! EWE MTU WA DAMU! EWE MTU USIYEFAA! 8 Bwana amerudisha juu yako damu yote ya nyumba ya sauli ambaye umetawala badala yake; naye bwana ametia ufalme katika mkono wa absalomu mwanao; kisha, angalia, wewe umetwaliwa katika uovu wako mwenyewe, kwa sababu umekuwa mtu wa damu. 9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, Mbona mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake. 10 Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu Bwana amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya? 11 Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; si zaidi Mbenyamini huyu sasa? MWACHENI ALAANI, KWA SABABU BWANA NDIYE ALIYEMWAGIZA. 12 LABDA BWANA ATAYAANGALIA MABAYA YALIYONIPATA, NAYE BWANA ATANILIPA MEMA KWA SABABU YA KUNILAANI KWAKE LEO. 13 Basi wakaendelea njiani Daudi na watu wake; SHIMEI NAYE AKAAENDELEA JUU YA UBAVU WA KILE KILIMA, KWA KUMKABILI, HUKU AKIENDELEA, AKILAANI, AKIMTUPIA MAWE, NA KURUSHA MAVUMBI”.
2 Samweli 16:5 “Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; ALITOKA, AKALAANI ALIPOKUWA AKIENDA.
6 Tena akamtupia Daudi mawe, na watumishi wote wa mfalme Daudi; na watu wote na mashujaa wote walikuwako mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto.
7 Na Shimei alipolaani, alisema hivi, NENDA ZAKO! NENDA ZAKO! EWE MTU WA DAMU! EWE MTU USIYEFAA!
8 Bwana amerudisha juu yako damu yote ya nyumba ya sauli ambaye umetawala badala yake; naye bwana ametia ufalme katika mkono wa absalomu mwanao; kisha, angalia, wewe umetwaliwa katika uovu wako mwenyewe, kwa sababu umekuwa mtu wa damu.
9 Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, Mbona mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake.
10 Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu Bwana amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya?
11 Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; si zaidi Mbenyamini huyu sasa? MWACHENI ALAANI, KWA SABABU BWANA NDIYE ALIYEMWAGIZA.
12 LABDA BWANA ATAYAANGALIA MABAYA YALIYONIPATA, NAYE BWANA ATANILIPA MEMA KWA SABABU YA KUNILAANI KWAKE LEO.
13 Basi wakaendelea njiani Daudi na watu wake; SHIMEI NAYE AKAAENDELEA JUU YA UBAVU WA KILE KILIMA, KWA KUMKABILI, HUKU AKIENDELEA, AKILAANI, AKIMTUPIA MAWE, NA KURUSHA MAVUMBI”.
Je na sisi leo hii tunaweza kukubali mashutumu namna hii?.. kiasi kwamba wanaotusengenya na sisi hatuwarudishii masengenyo, wala kuwalaumu?.. kiasi kwamba tunahuzunika kuanguka kwa wanaoshindana nasi?
Tukifikia hatua hii tutapata kibali sana Mbele za Mungu. Unaona Daudi hapo baada ya kukubali mashutumu na laana anasema.. “MWACHENI ALAANI, KWA SABABU BWANA NDIYE ALIYEMWAGIZA. LABDA BWANA ATAYAANGALIA MABAYA YALIYONIPATA, NAYE BWANA ATANILIPA MEMA KWA SABABU YA KUNILAANI KWAKE LEO. ”
Daudi alijua ili kupata Mema, hana budi kukubali laana, ili kupata kibali hana budi kukubali mashutumu. Na si Daudi peke yake, utaona pia na Ayubu, katika Maisha yake yote anasema hajawahi kufurahia anguko la wanaomchukia au wanaoshindana naye.. jambo lililomfanya apate kibali kikubwa sana mbele za Mungu, na kuonekana kuwa mkamilifu kuliko watu wote waliokuwepo chini ya jua katika kipindi chake..
Ayubu 31:29 “Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu; 30 (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);”
Ayubu 31:29 “Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu;
30 (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);”
Na sisi ili tupate rehema na kibali na baraka, na Mema kutoka kwa Mungu, hatuna budi kuwa kama Daudi na Ayubu..Ni kanuni inayoonekana kama ni ngumu, lakini ndio iliyokubalika mbele za Mungu. Injili za kupiga maadui, na kutwa kuchwa kushindana na maadui zako na kusubiria kuona shari yao ili ufurahie nataka nikuambie ni injili za kuzimu, ingawa kwa nje zinaonekana kama zina hekima.. Bwana Yesu Mkuu wa uzima alisema maneno haya..
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44 lakini mimi nawaambia, WAPENDENI ADUI ZENU, WAOMBEENI WANAOWAUDHI, 45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?”
Mathayo 5:43 “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, WAPENDENI ADUI ZENU, WAOMBEENI WANAOWAUDHI,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?”
Unataka Rehema?, unataka kibali?, unataka Mema kutoka kwa Mungu??.. huna budi kukubali mashutumu, kwasababu Kristo naye alikubali mashutumu na kejeli na kudharauliwa lakini sasa ana utukufu kuliko vitu vyote.
Bwana YESU ANARUDI!!
VITA DHIDI YA MAADUI
KUTUBU SIO KUOMBA REHEMA.
NJIA MUNGU ALIYOIWEKA KWA KILA JAMBO.
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
Jina la Bwana Yesu Kristo, Mkuu wa Uzima, libarikiwe.. karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu, ambalo ni taa iongozayo miguu yetu na mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Je unajua ni kwanini baadhi ya watu waovu, Mungu anaruhusu wafanikiwe katika ulimwengu huu, ijapokuwa wanalikufuru jina lake? Siri ipo katika mistari ifuatayo..
Mathayo 13:24 “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake; 25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu. 27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu? 28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? 29 AKASEMA, LA; MSIJE MKAKUSANYA MAGUGU, NA KUZING’OA NGANO PAMOJA NAYO. 30 VIACHENI VYOTE VIKUE HATA WAKATI WA MAVUNO; NA WAKATI WA MAVUNO NITAWAAMBIA WAVUNAO, YAKUSANYENI KWANZA MAGUGU, MYAFUNGE MATITA MATITA MKAYACHOME; BALI NGANO IKUSANYENI GHALANI MWANGU”.
Mathayo 13:24 “Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake;
25 lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.
26 Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
27 Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
29 AKASEMA, LA; MSIJE MKAKUSANYA MAGUGU, NA KUZING’OA NGANO PAMOJA NAYO.
30 VIACHENI VYOTE VIKUE HATA WAKATI WA MAVUNO; NA WAKATI WA MAVUNO NITAWAAMBIA WAVUNAO, YAKUSANYENI KWANZA MAGUGU, MYAFUNGE MATITA MATITA MKAYACHOME; BALI NGANO IKUSANYENI GHALANI MWANGU”.
Nataka tuone huo mstari wa 30 unaosema.. “VIACHENI VYOTE VIKUE”..
Hili ni Neno kubwa sana.. Yaani Mungu anaruhusu Magugu yasitawi ndani ya shamba lake?.. Si ajabu leo unaona waovu wanasitawi katika dunia yake, si ajabu unaona leo wachawi wanavuna, wauaji wanafanya biashara na kufanikiwa, waabudu sanamu wanaishi miaka mingi, walevi wanastawi katika dunia hii hii, wanayoishi watu wanaomcha Mungu.
Ukiona hivyo usishangae, kwasababu ni Mungu karuhusu wasitawi, wao ni magugu kati ya Ngano, ndani ya shamba lake, na Mungu kazuia wasiondolewe kwanza bali wakue Pamoja na Ngano, hata wakati wa mavuno, maana yake zile baraka za kumwagiwa maji na kuwekewa mbolea wacha nao wazifaidi mpaka wakati wa mavuno, na utakapofika wakati wa mavuno zitangamizwa milele..(Kwahiyo kumbe lengo la kuacha magugu yakue Pamoja na ngano, ni ili mwisho wa siku magugu hayo yale kuangamizwa)
Ndio maana sasa Daudi akasema maneno haya…
Zaburi 92:7 “Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele”
Na Sulemani mwanae pia akasema…
Mithali 1:32 “…kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”
Katika siku hizi za mwisho shetani anawafanya watu waangalie hali zao za kimaisha, na kuzifanya kuwa kipimo cha kwanza cha hali zao za kiroho. Kwamba ukipata mafanikio mengi basi ni Mungu kakubariki, na vile vile usipokuwa na mafaniko basi kuna tatizo, kwamba upo mbali na Mungu, Kufuatia 3 Yohana 1:2.
Ni kweli hali za kimaisha ni kipimo cha hali ya kiroho, lakini kipimo hichi si thabiti asilimia mia, kwasababu kuna matajiri wengi watakuwepo kuzimu, na vile vile kuna maskini wengi watakuwepo mbinguni (kasome Luka 16:19-31).
Hivyo kukubaliwa kwetu na Mungu hatukupimi kwa mafanikio, kwasababu yeye mwenyewe alisema “VIACHENI VYOTE VIKUE PAMOJA”. Ili wakati wa mavuno viangamizwe.
Sasa swali kama Mafanikio sio kipimo thabiti cha kukubaliwa na MUNGU, je kipimo thabiti kitakuwa ni kipi?
Kipimo kamili ni UTAKATIFU….Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, NA HUO UTAKATIFU, ambao hapana MTU ATAKAYEMWONA BWANA ASIPOKUWA NAO”.
Hicho ndio kipimo ambacho, kipo thabiti asilimia mia..Maana yake ukiwa mtakatifu utamwona Mungu, usipokuwa mtakatifu hutamwona Mungu, hakuna ambaye ataenda kuzimu akiwa mtakatifu..wala hakuna ambaye ataenda mbinguni kama si mtakatifu.. Tofauti na kipimo cha kwanza ambacho hakieleweki sana..kwasababu wapo matajiri kuzimu, na maskini mbinguni.
Kama ni hivyo, basi huu si wakati wa kutafuta kwanza mafanikio ya mwilini, bali wa kutafuta kwanza Utakatifu, ili tukae mbali na dhambi..kwasababu dhambi ndiyo itakayotutenga na Mungu milele.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.
Wagalatia 5:19 “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU”.
Maran atha!
UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU.
Je! Ni kweli Yesu alirejesha kila kitu kama pale Edeni?
MAVUNO NI MENGI
MWISHO WA MAVUNO, NI MWISHO WA DUNIA.
Ayubu 21:10 “Fahali wao HUVYAZA wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba”.
Kuvyaza ni lugha ya “kuzaliana” inayotumika kwa Wanyama wa kiume. Badala ya kusema “Ng’ombe dume anapanda”, lugha nzuri ni kusema “ng’ombe anavyaza” . Neno hili limeonekana mara moja tu katika biblia..
Ayubu aliiona njia ya wasio haki, kwamba mali zao zinapongezeka, na mafahali yao YANAPOVYAZA na, na ng’ombe wao wa kike wanavyozaa kwa wingi, na huku wanamkataa Mungu.. mwisho wao utakuwa ni kushuka kuzimu kwa ghafla.
Ayubu 21:7 “Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu? 8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao. 9 Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi. 10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba. 11 Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza. 12 Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi. 13 SIKU ZAO HUTUMIA KATIKA KUFANIKIWA, KISHA HUSHUKA KUZIMUNI GHAFULA. 14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako. 15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?”.
Ayubu 21:7 “Mbona waovu wanaishi, Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?
8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao, Na wazao wao mbele ya macho yao.
9 Nyumba zao zi salama pasina hofu, Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.
10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu; Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.
11 Huwatoa kama kundi watoto wao. Na watoto wao hucheza.
12 Huimba kwa matari na kwa kinubi, Na kuifurahia sauti ya filimbi.
13 SIKU ZAO HUTUMIA KATIKA KUFANIKIWA, KISHA HUSHUKA KUZIMUNI GHAFULA.
14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee; Kwani hatutaki kuzijua njia zako.
15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie? Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?”.
Vile vile Daudi naye aliliona hilo hilo, kuwa mafaniko ya Mtu mwovu, mwisho wake ni kuangamia.
Na Sulemani naye aliliona hilo na kwa uweza wa Roho akasema..
Mithali 1:32 “…kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza”.
Hii ikifunua kuwa mafanikio sio uthibitisho wa kwanza kwamba tumekubaliwa na Mungu, ukilima na kuvuna na huku moyoni umemwacha Mungu jua hayo mafaniko, yatakuangamiza..Ukifanya biashara na ukafanikiwa sana, sio uthibitisho wa kwanza kwamba njia zako ni sawa mbele za Mungu.. Zaidi sana Bwana Yesu alisema, itamfaidia nini mtu akiupata ulimwengu mzima, na kisha akapata hasara ya nafsi yake?.. kumbe inawezekana mtu akaupata hata ulimwengu mzima, lakini bado akapotea!. Hivyo mafanikio sio kitu cha kwanza cha kutafuta, bali tuutafute kwanza ufalme wake na haki yake.
Na ufalme wake na haki yake ni kumwamini Yesu, na kutubu na kubatizwa na kuishi Maisha matakatifu.
KUOTA UNA MIMBA.
Je! Daudi hakuwa mtoto wa ndoa wa Yese? (Zab 51:5)
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
Maji ya Farakano ni nini katika biblia?
Nini maana ya usimfunge ng’ombe kinywa apurapo nafaka!.(Kumbukumbu 25:4)
Kiyama au kiama..maana yake ni ‘siku ya ufufuko’
Neno hilo linapatikana sehemu kadha wa kadha katika biblia. Kwamfano hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakatana nalo;
Mathayo 22:23-28
[23] Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, [24]wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. [25]Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. [26]Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. [27]Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. [28]Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
[23] Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,
[24]wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
[25]Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.
[26]Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.
[27]Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
[28]Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
Hapo ni mafarisayo walitaka kujua kutoka kwa Yesu siku ya ufufuo wa wafu, mambo ya ndoa yatakuwaje.?
Soma pia..Wafilipi 3:10-11
[10]ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; [11]ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
[10]ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;
[11]ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
Akimaanisha afikie siku ya ufufuko wa wafu.
Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi;
2 Timotheo 2:17-18,22
[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, [18]walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.
[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
[18]walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.
Hivyo na sisi pia hatuna budi kuyaelekeza mawazo yetu katika ufufuo wa wafu..Tumaini hilo ni lazima liwepo ndani yetu. Na ufufuo huo utakuja siku ile ya UNYAKUO ambapo parapanda italia, kisha wafu wote waliokuwa makaburini waliompokea Kristo, watafufuliwa na moja kwa moja wataungana na sisi tuliohai kisha kwa pamoja tutapaa kumlaki Bwana Yesu mawinguni.
Swali la kujiuliza. Je, tumejipangaje kwa ajili ya siku hiyo ya kiyama? Je matendo yetu wanastahili kukubaliwa?
Majibu sote tunayo.
Tukumbuke kuwa Siku ya kiyama ipo karibuni sana.
Shalom
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
Je mtu akifa anakuwa hana dhambi tena?
Ufunuo 19:11-13 [11]Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. [12]Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. [13]Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Ufunuo 19:11-13
[11]Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
[12]Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
[13]Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini mahali hapo Yesu hajitambulishi kwa jina lake la asili tulilolizoea, bali anajiita Neno la Mungu,?.
Ipo maana kubwa sana nyuma yake ambayo wakristo wengi hatuijui.
Ni muhimu tufahamu kuwa pale Tunapomtaja YESU, tunamlenga Yesu wa pande mbili.
Wakristo wengi tunaishia kumtambua Yesu kama mtu, jinsi alivyokuwa na mamlaka, na uweza, na maajabu, jinsi alivyosulubiwa na kuzikwa na kufufuka na kupaa juu, na sasa hivi anatawala na kumiliki viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani ..jambo ambalo ni zuri sana, kwasababu kwa kumtambua hivyo ndivyo tunavyomwamini na kupokea wokovu na kuponywa shida zetu.
Lakini kosa ni pale tunapoishia kumtambia Yesu-mtu tu, hatutaki kumtambua Yesu kama Yesu-Neno.
Utajiuliza huyu YESU-NENO ni yupi?
Ni Yesu katika maneno yake aliyokuwa anayafundisha. Leo hii ukiweza kuyaishi maneno hayo kikamilifu 100%, basi na wewe unabadilika na kuwa Yesu, mwenyewe.
Kiasi kwamba, wakati mwingine hutahitaji Yesu aje kukusaidia, bali wewe mwenyewe utaweza kufanya, kila kitu.
Wakristo wengi tunampenda Yesu tunapomsoma au kumsikia, lakini hatutaki kuwa kama yeye. Kwasababu tunaona ugumu kuyaishi maneno yake.
Tunafanana na mwanafunzi anayetegemea tu kikokoteo (calculator) kupigia mahesabu yake, lakini kichwani asiwe na maarifa yoyote ya kinachofanyika nyuma ya kikokoteo kile
lakini mtu ambaye anajua kanuni ya kikokoteo, huyo huwa anakuwa ni bora zaidi..kwasababu hata pasipo kuwa nacho anaweza tu kupiga mahesabu yake na kupata majibu. Atakihitaji kwa kurahisisha tu kazi zake, lakini pasipo hicho bado anaweza kufanya.
Lakini hiyo itamgharimu aende shule, ajifunze misingi yote ya hisabati..tofauti na yule mwingine ambaye kazi yake ni kubofya tu. “Jibu hilo hapo!”
Ndivyo ilivyo kwa wakristo wanaomtegemea Yesu-mtu tu, na sio Yesu-Neno. Wanamgeuza Bwana Yesu kama calculator wanamwita awasaidie, lakini hawataki kuyaishi maneno yake..
Sio kila wakati tutamwitaji Yesu atusaidie, wakati mwingine anataka sisi wenyewe tufanye, ndivyo alivyowazoeza pia mitume wake ambao hapo mwanzo walizoelea kumtegemea tu yeye ilihali hawazingatii maneno yake
Mathayo 17:17
[17]Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu.
Wakati mwingine tunamwita Yesu, atusaidie, na anakaa kimya hafanyi chochote..tunaita usiku kucha hajibu lolote. Ni kwasababu gani? Ni kwasababu hatutaki kuliishi Neno lake.
Kwamfano: mmoja anaweza akawa anafunga na kukesha kumlilia Yesu ampe mali (kwasababu anamjua Yesu-mtu anaweza yote)..lakini huku anaendelea na mambo yake ya kidunia.. Na mwingine akalizingatia lile Neno la Yesu linalosema;
Mathayo 6:32-33
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. [33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Huyu wa pili, anaweza asimtaje Yesu wala mali mahali popote, lakini akapokea hitaji lake, kwasababu tu kajua kanuni ya roho.. Lakini yule wa kwanza kupewa/kutokupewa ni juu ya Yesu mwenyewe..sio juu yake.
Hivyo tujifunze kuyaishi maneno ya Yesu, kwamfano tunapoambiwa tusamehe huyo ndio Yesu-Neno., tunapoambiwa tusizini ndiye Yesu Neno.
Na Yesu mwenyewe alitusisitizia kwamba maneno yake yakiwa ndani yetu, basi tukiomba lolote yeye atatupa.
Yohana 15:7
[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
“Yodi” ni nini kama tunavyoisoma katika Mathayo 5:18?
BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?.