Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, libarikiwe!…karibu tujifunze Biblia, Neno la Mungu wetu. Neno la Mungu ni Taa iongozayo hatua za miguu yetu na Mwanga unaoongoza Njia yetu.
Huu ni mwendelezo wa ufupisho wa vitabu vya Biblia, Tumeshavitazama vitabu kadhaa nyuma, kama bado hujapitia uchambuzi huo, basi Unaweza kufanya hivyo kwa kufungua link hii>>VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1. Au ukawasiliana nasi kupitia namba zilizopo mwisho wa somo hili, au katika tovuti yetu, ili tuweze kukutumia masomo hayo kwa njia ya Whatsapp.
Vile vile ni muhimu kujua kuwa huu ni Ufupisho tu!, na muhtasari, ambao utakuwezesha kuvielewa vitabu hivi kiurahisi, hivyo baada ya kusoma ufupisho huu ni vizuri kwenda kusoma kitabu husika, ili ukajazilishe vile vichache ulivyovitapata huku. Kwa kusoma ufupisho huu pekee yake bila kushika biblia, hakuna chochote utakachonufaika nacho, Zaidi sana ni afadhali kuisoma biblia bila ufupisho wowote, kuliko kusoma hapa na kutoishika kabisa biblia.
KITABU CHA HOSEA.
Kitabu cha Hosea, kimeandikwa na Hosea Mwenyewe na maana ya jina Hosea ni “Wokovu”.. Hosea alikuwa ni Nabii wa Mungu, kama vile alivyokuwa Yeremia, Isaya au Danieli.. Kitabu cha Hosea, kinakadiriwa kuandiwa kwa muda wa miaka 40. Ndani ya muda huo Hosea alipokea mfululizo wa maono kutoka kwa Mungu na akayaandika katika kitabu hicho chenye sura/milango 14.
Nabii Hosea ni moja ya manabii watatu ambao Bwana aliyatumia Maisha yao kama Ishara… Wengine ni Nabii Isaya, ambaye kuna wakati aliambiwa atembee uchi (kuelewa zaidi kwanini aambiwe atembee uchi fungua hapa >> KWANINI NABII ISAYA ALIAGIZWA KUHUBIRI UCHI? ), na mwingine ni Ezekieli ambaye aliambiwa ale mikate iliyookwa juu ya kinyesi cha Mwanadamu, na vile vile alale kwa upande mmoja kwa siku nyingi, kuwa ishara juu ya wana wa Israeli.
Lakini Nabii Hosea yeye Mungu aliyafanya Maisha yake kuwa ishara, kwa namna nyingine, na namna hiyo ni “katika eneo la Ndoa”.. Kwa kawaida Bwana hakuwahi kuwapa watu maagizo ya kuoa watu wazinzi au makahaba. Lakini Hosea aliambiwa akaoe mwanamke “Kahaba”..Mwanamke ambaye tabia yake si kutulia na mwanaume mmoja, Ambaye hawezi kukaa na mwanaume mmoja. Huyo ndio Bwana alimpa maagizo Hosea akamwoe kwa sababu maalumu..
Lengo la kumpa maagizo hayo ni ili kuwafundisha Israeli ni kwajinsi gani wanaonekana mbele zake, kwamba mbele za Mungu wanaonekena kama Mwanamke kahaba, ambaye hatulii ni mume wake mmoja. Na Taifa la Israeli katika roho linafananishwa na mwanamke, na Mungu ni kama MUME wake.
Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, INGAWA NALIKUWA MUME KWAO, asema Bwana”.
Yeremia 31:31 “Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, INGAWA NALIKUWA MUME KWAO, asema Bwana”.
Umeona hapo?.. anasema tangu siku ile aliyowatoa Misri, yeye alikuwa ni MUME KWAO, lakini walilivunja agano lake..pia Yeremia 3:14, inazungumzia jambo hilo hilo…
Yeremia 3:14 “Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana; maana mimi ni MUME WENU; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni”
Kwahiyo Kwajinsi Israeli walivyokuwa wanamwacha Mungu, kiroho ni kama walikuwa wanamsaliti MUME WAO, ambaye ni Mungu. Na matendo yote mabaya waliyokuwa wanayafanya kiroho yalitafsirika kama UASHERATI.
Kwahiyo Hosea kuambiwa vile aoe kahaba, ni kuwapa ujumbe Israeli kuwa kama vile yeye (Hosea) anavyosumbuliwa na mwanamke Kahaba, (leo yupo na yeye ndani, kesho katoroka kwenda kufanya ukahaba)…ndivyo na Israeli inavyomsumbua Mungu kwa uzinzi wa kiroho inaoufanya..
Sasa ili kuzidi kuelewa kwa undani, juu ya Agizo hili Hosea alilopewa unaweza kufungua hapa >>> Kwanini MUNGU Anampa Nabii Hosea maagizo ya Kumuoa mwanamke kahaba?
Kwahiyo baada ya Israeli yote kuona Hosea kaoa mwanamke mzinzi na tabu anazozipata kwa mwanamke huyo, na jinsi Hosea alivyowapa majibu, baadhi ya wana wa Israeli walitubu, na kumgeukia Mungu, lakini wengine walishupaza shingo.
Kitabu cha Hosea tutakigawanya katika sehemu kuu 8.
SEHEMU YA KWANZA (mlango wa kwanza na wa pili).
Unahusu maelekezo ya Bwana kwa Hosea, juu ya kutafuta MKE WA KIKAHABA ALIYEITWA GOMERI, na kuzaa naye Watoto watatu, mtoto wa Kwanza, ambaye atakuwa wa kiume atamwita YEZREELI (Yezreeli ulikuwa ni mji ya mfalme wa Israeli, aliyeitwa Ahabu na mkewe Yezebeli). Ndipo palipokuwa kitovu cha maasi yote ya Isreali.
Na mtoto wa pili ambaye atakuwa wa kike ataitwa Lo-ruhama, ambayo tafsiri yake ni “Asiyehurumiwa”. Na mtoto wa tatu, ambaye ni wa kiume atamwita Lo-Ami, maana yake ni “Si watu wangu”.
Kupitia Watoto hao watatu, Pamoja na Mama yao, Mungu alipitisha ujumbe mzito sana kwa Israeli yote na Yuda. (Unaweza kupitia sura hizo mbili binafsi, kwa msaada wa Roho).
SEHEMU YA PILI (mlango wa tatu).
Unahusu maelekezo ya Bwana, kwa Hosea kuhusu kuoa mwanamke mwingine wa kizinzi, lakini huyu wa sasa, anapaswa akamchukue ambaye tayari anapendwa na mtu mwingine, lengo la kufanya hivyo ni kuwaonyesha ni jinsi gani, wana wa Israeli watatwaliwa na Mfalme Nebukadreza na kukaa siku nyingi mbali na uwepo wa Mungu aliye mume wao.
Hosea 3:1 “Bwana akaniambia, Enenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile Bwana awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu. 2 Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri; 3 nami nilimwambia, Utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya ukahaba, wala hutakuwa mke wa mtu awaye yote; nami nitakuwa hali iyo hiyo kwa ajili yako. 4 Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago; 5 baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho”.
Hosea 3:1 “Bwana akaniambia, Enenda tena, mpende mwanamke apendwaye na rafiki yake, naye ni mzinzi; kama vile Bwana awapendavyo wana wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine, na kupenda mikate ya zabibu kavu.
2 Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri;
3 nami nilimwambia, Utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya ukahaba, wala hutakuwa mke wa mtu awaye yote; nami nitakuwa hali iyo hiyo kwa ajili yako.
4 Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago;
5 baada ya hayo wana wa Israeli watarejea, na kumtafuta Bwana, Mungu wao, na Daudi, mfalme wao; nao watamwendea Bwana na wema wake kwa kicho siku za mwisho”.
SEHEMU YA 3 (mlango wa 4-5).
Bwana anatoa OLE juu ya Israeli kutokana na dhambi zao wanazozifanya.
SEHEMU YA 4 (Mlango wa wa 6).
Bwana anatoa Shauri la Toba kwa Israeli, kwamba watubu naye atawarehemu..
Hosea 1 ‘Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. 2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake. 3 Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi”.
Hosea 1 ‘Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu.
2 Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.
3 Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi”.
SEHEMU YA 5 (Mlango wa 7-9).
Bwana anazidi kumwonyesha Nabii Hosea, makosa ya Israeli na jinsi wanavyoyategemea Mataifa kama Misri na Ashuru katika kupata msaada, zaidi ya kumtegemea Bwana.
Hosea 7:10 ‘Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote. 11 Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru. 12 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia. 13 Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu. 14 Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi”.
Hosea 7:10 ‘Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.
11 Naye Efraimu amekuwa kama njiwa mpumbavu, asiye na fahamu; humwita Misri, huenda Ashuru.
12 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.
13 Ole wao! Kwa kuwa wamenikimbia; uharibifu na uwapate! Kwa kuwa wameniasi; ingawa ninataka kuwakomboa, hata hivyo wamenena uongo juu yangu.
14 Wala hawakunililia kwa moyo, lakini wanalalamika vitandani mwao; hujikutanisha ili kupata nafaka na divai; huniasi mimi”.
SEHEMU YA 6 (Mlango wa 10).
Unabii wa Israeli kuchukuliwa mateka kwenda Ashuru.
Kumbuka Israeli ilikuja kugawanyika katika sehemu kuu 2, kaskazini na kusini, kaskazini palibaki kuitwa Israeli lakini upande wa kusini kuliitwa Yuda. Sasa huu upande wa Kaskazini ulikuja kuchukuliwa mateka mpaka Taifa la Ashuru lililopo Kaskazini..kutokana na maasi kuwa mengi, lakini kabla ya kupelekwa huko Bwana alituma manabii wengi kuwaonya watubu, waache maasi, wairudie sheria ya Mungu, na mmojawapo wa manabii hao, Bwana aliowatuma kuwaonya Israeli ni huyu Nabii Hosea!.. aliwaambia maneno haya…
Hosea 10:5 “Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-Aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka. 6 NAYO ITACHUKULIWA ASHURU, IWE ZAWADI KWA MFALME YAREBU; EFRAIMU ATAPATA AIBU, NA ISRAELI ATALIONEA HAYA SHAURI LAKE MWENYEWE. 7 Katika habari za Samaria, mfalme wake amekatiliwa mbali, kama povu usoni pa maji. 8 Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni. 9 Ee Israeli, umefanya dhambi tangu siku za Gibea; huko ndiko walikosimama; ili vita vilivyokuwa juu ya wana wa uovu visiwapate katika Gibea”.
Hosea 10:5 “Wakaao Samaria wataona hofu kwa ajili ya ndama za Beth-Aveni; kwa maana watu wa mji huo wataulilia, na makuhani wake walioufurahia, kwa sababu ya utukufu wake; kwa maana umetoweka.
6 NAYO ITACHUKULIWA ASHURU, IWE ZAWADI KWA MFALME YAREBU; EFRAIMU ATAPATA AIBU, NA ISRAELI ATALIONEA HAYA SHAURI LAKE MWENYEWE.
7 Katika habari za Samaria, mfalme wake amekatiliwa mbali, kama povu usoni pa maji.
8 Mahali pa Aveni palipoinuka, yaani, dhambi ya Israeli, pataharibika; mwiba na mbigili itamea juu ya madhabahu zake; nao wataiambia milima, Tusitirini; na vilima, Tuangukieni.
9 Ee Israeli, umefanya dhambi tangu siku za Gibea; huko ndiko walikosimama; ili vita vilivyokuwa juu ya wana wa uovu visiwapate katika Gibea”.
SEHEMU YA 7 (Mlango wa 11-12).
Bwana anawakumbusha Israeli Huruma zake (Jinsi alivyowahurumia kipindi wakiwa katika nchi ya utumwa ya Misri), lakini sasa wamemwacha, na hawajui kama wapo kwenye hatari.
Hosea 11:1 “Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, nikamwita mwanangu atoke Misri”.
SEHEMU YA 8 (Mlango wa 12-14).
Bwana anazidi kuwapa shauri Israeli la kumrudia yeye kutubu, vile vile anawatahadharisha juu ya Hukumu ijayo.
Hosea 14:1 “ee israeli, MRUDIE BWANA, MUNGU WAKO; MAANA UMEANGUKA KWA SABABU YA UOVU WAKO. 2 chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie bwana; mkamwambie, ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe”.
Hosea 14:1 “ee israeli, MRUDIE BWANA, MUNGU WAKO; MAANA UMEANGUKA KWA SABABU YA UOVU WAKO.
2 chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie bwana; mkamwambie, ondoa maovu yote, uyatakabali yaliyo mema; na hivyo ndivyo mtakavyotoa sadaka za midomo yetu kana kwamba ni ng’ombe”.
Kwa hitimisho ni kwamba kitabu cha Hosea ni kitabu cha Maonyo ya Israeli kumrudia Mungu, na kwamba, watubu..
Na sisi (watu wa Mungu) tunafananishwa na Mwanamke, tena Bibi-arusi..na Yesu Kristo ni Bwana wetu..
2Wakorintho 11:2 “Maana nawaonea wivu, WIVU WA MUNGU; KWA KUWA NALIWAPOSEA MUME MMOJA, ILI NIMLETEE KRISTO BIKIRA SAFI. 3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo”.
2Wakorintho 11:2 “Maana nawaonea wivu, WIVU WA MUNGU; KWA KUWA NALIWAPOSEA MUME MMOJA, ILI NIMLETEE KRISTO BIKIRA SAFI.
3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo”.
Kama Bibiarusi wa Kristo, unapofanya anasa kwa makusudi, katika roho unatafsirika kuwa unafanya uasherati mbele za Bwana, kama ni mtukanaji, mwizi, mlevi, na huku unajiita umeokoka jua kuwa unamtia Bwana wivu, kwa uasherati huo wa kiroho unaoufanya.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 2
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)
KIELELEZO CHA MWANAMKE KATIKA NYUMBA.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Je ni kweli, mpagani akioa au akiolewa na yule aliyeamini, na yeye pia anahesabiwa kuwa mkamilifu kulingana na mstari huu?
1Wakorintho 7:13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu
1Wakorintho 7:13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu
JIBU: Ifahamike kuwa hakuna mtu anayehesabiwa mkamilifu kwa ukamilifu wa mtu mwingine. Maandiko yapo wazi katika hilo; yanasema kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe, na kila mtu atatoa Habari zake mwenyewe siku ile, mbele za Mungu (Wagalatia 6:5, Warumi 14:12).
Lakini je! Mstari huo unamaanisha kwamba ikiwa umeolewa au kuoa mtu aliyeamini, hata kama wewe ni mtenda dhambi utahesabiwa mtakatifu kwa yeye?na ukifa utaenda mbinguni? Jibu ni hapana, ukisoma vifungu vya chini yake kidogo utaelewa vizuri..Tusome..
1Wakorintho 7:12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. 13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. 15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. 16 KWA MAANA WAJUAJE, WEWE MWANAMKE, KAMA UTAMWOKOA MUMEO? AU WAJUAJE, WEWE MWANAMUME, KAMA UTAMWOKOA MKEO”?
1Wakorintho 7:12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
16 KWA MAANA WAJUAJE, WEWE MWANAMKE, KAMA UTAMWOKOA MUMEO? AU WAJUAJE, WEWE MWANAMUME, KAMA UTAMWOKOA MKEO”?
Paulo anamaanisha kwamba, ikiwa wewe umeamini, na mwezi wako hajaamini, hupaswi kumuacha na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine. Bali unapaswa kuendelea kuishi naye ikiwa tu bado yupo radhi kuwa nawe. Kwasababu kwa kufanya hivyo ni rahisi yeye kuvutwa kwenye Imani yako, ikiwa ataona mwenendo wako mzuri,.. Na kwa matokeo hayo Paulo anasema ni nani ajuaje na yeye atashawishwa kuokoka kama wewe?
Na ni kweli ukisikiliza shuhuda za ndoa nyingi zilivyomrudia Mungu, utasikia moja inakuambia Baba aliokoka baada ya mkewe kuwa mcha Mungu, au mama alimrudia Mungu baada ya mumewe kuokoka. Umeona? Lakini hilo haimaanishi kuwa moja kwa moja ndio tayari na yeye kaokoka,kisa tu mwenzake kaokoka hata kama ataendelea kutenda dhambi, hapana.
Wanaweza wakakaa hivyo, na bado mmoja akaendelea kutokuamini hadi kifo na kuzimu akaenda. Lakini hiyo nayo hutokea mara chache, ikiwa kweli huyo mwenzi mwingine, anaishi Maisha ya haki, na ya kumpendeza Mungu, na ya kumwombea kwa bidii mwenzake.
Lakini pia ni lazima tufahamu kuwa biblia hairuhusu, mkristo kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini. Mazingira yanayozungumziwa hapo, ni yale ambayo wokovu umemkuta tayari yupo kwenye ndoa ya namna hiyo. Leo hii kumekuwa na migogoro mingi ya kindoa, kwasababu ya maamuzi mabaya, yanayofanywa na wakristo, ambao hawazingatii maagizo ya Mungu yaliyosema tusifungwe nira Pamoja na wasioamini (2Wakorintho 6:14).
Ulinzi wa kwanza unapaswa uwe katika Imani yako, sio katika familia. Hivyo ikiwa bado hujaoa/ au hujaolewa, Imani ndio iwe ni kipimo cha kwanza cha kumtambua mwenzi sahihi. Lakini wewe ambaye tayari upo kwenye ndoa ya namna hiyo. Unalojukumu la kumvuta huyo mwenzi wako, kimatendo, kimaombi, na kimafundisho. Kwasababu huwezi jua kama atavutwa au la!.
Bwana akubariki
NDOA NA TALAKA:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
NDOA NI NINI?
Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?
Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?
JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?
NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.
Wapo wanatofautisha maneno haya mawili, na wapo wanayoyaona kama ni kitu kimoja..
Ni kweli Bwana Yesu alituonyesha kuwa “maandiko na Neno” la Mungu ni kitu kilekile kimoja, na ndivyo ilivyo..
Soma Yohana 10:35
Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
Isipokuwa tofauti yao ndogo ni kwamba maandiko yanajifunga tu katika maandishi.. lakini Neno la Mungu, ni aidha katika maandishi au kuzungumzwa.
Bwana anaweza kutoa ujumbe wake kwa sauti kinabii, vilevile anaweza kuzungumza kwa biblia (maandiko). Na zote zikawa sauti zake zenye majibu.
Lakini tulichopewa, na tunapaswa tukitegemee sana ni Neno la Mungu katika maandiko, alisema, “maandiko hayawezi kutanguka”, yaani kilichoandikwa kimeandikwa. Lakini Neno lake katika sauti anaweza kulitangua mwenyewe, au akaghahiri, au likawa la muda tu, tofauti na Neno katika maandishi.
Hivyo ukiishi kwa hilo, utakuwa salama. Lakini tukiwa wavivu wa kujifunza biblia. Tuwe na uhakika kuwa tunapoteza maisha yetu.
Marko 12:24
[24]Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?
Tupende Biblia zaidi ya chakula, tuone kuwa hatuwezi kuishi bila hilo; Daudi alisema.
Zaburi 119:140
[140]Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
Tuyapende maandiko, kwani ndio uhai wetu.
Gombo ni nini?
Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)
Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
Nini maana ya “Torati na manabii”?
Yeshuruni ni nani katika biblia?
URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?
Jibu: Tuisome Habari nyenyewe…
Yohana 8:3 “Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati. 4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini. 5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje? 6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, AKAANDIKA KWA KIDOLE CHAKE KATIKA NCHI. 7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe. 8 Akainama tena, AKAANDIKA KWA KIDOLE CHAKE KATIKA NCHI. 9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati. 10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia? 11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]”.
Yohana 8:3 “Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi, wakamweka katikati.
4 Wakamwambia, Mwalimu, mwanamke huyu amefumaniwa alipokuwa akizini.
5 Basi katika torati, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii; nawe wasemaje?
6 Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, AKAANDIKA KWA KIDOLE CHAKE KATIKA NCHI.
7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe.
8 Akainama tena, AKAANDIKA KWA KIDOLE CHAKE KATIKA NCHI.
9 Nao waliposikia, wakashitakiwa na dhamiri zao, wakatoka mmoja mmoja, wakianzia tangu wazee hata wa mwisho wao; akabaki Yesu peke yake, na yule mwanamke amesimama katikati.
10 Yesu akajiinua asimwone mtu ila yule mwanamke, akamwambia, Mwanamke, wako wapi wale washitaki wako? Je! Hakuna aliyekuhukumu kuwa na hatia?
11 Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]”.
Katika tukio hilo maandiko, hayajasema wala kutaja ni kitu gani Bwana Yesu alichokuwa anakiandika ardhini, ikifunua kuwa SIO KITU CHA MUHIMU SANA SISI KUKIJUA, maana ingekuwa ni cha muhimu sana kukijua basi Mtume Yohana asingeacha kukiandika kwa faida yake na yetu pia, au Marko au Mathayo, wangeviandika… Lakini hakikuwa kitu cha muhimu sana kwetu kukijua…Ni sawa tutafute ni aina gani ya udongo, Bwana aliyoitengenezea tope, kwaajili ya kumponya yule kipofu.
Yohana 9:6 “Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho”.
Unaona?..kujua ni aina gani ya udongo iliyotumika hapo kutengenezea tope, haitusaidii sana, vile vile kujua ni aina gani ya Mti ulitumika kumsulubisha Bwana pale msalabani, pia haitusaidii chochote, kwamba tujue ule mti ulikuwa ni Mkoko, au Mtini, au Mpingo, au Mwerezi au Mwaloni haitusaidii chochote kiroho.. Ndio maana maandiko hayaeleza aina ya mti huo.
Vile vile ni maneno gani Bwana Yesu aliyokuwa anayaandika ardhini sio jambo la muhimu kulijua.. Wengi wanasema Bwana Yesu alikuwa anaandika dhambi za wale Mafarisayo na Masadukayo ardhini, kufuatia andiko la Yeremia 17:13..
Yeremia 17:13 “Ee Bwana, tumaini la Israeli, wote wakuachao watatahayarika. WAO WATAKAOJITENGA NAMI WATAANDIKWA KATIKA MCHANGA, kwa sababu wamemwacha Bwana, kisima cha maji yaliyo hai”.
Lakini bado hoja hii haina nguvu, kwasababu Bwana Yesu angekuwa kutwa kuchwa anashinda kuandika tu dhambi za watu mchangani, kwasababu waliokuwa wanamkataa ni wengi.
Hivyo alichokuwa anakiandika sio cha Muhimu kukifaham, lakini kilicho cha muhimu kujua ni KWANINI ALIKUWA ANAANDIKA ARDHINI, WAKATI WATU WANAMWONGELESHWA!. Hicho ndio cha muhimu kujua..
Sababu kuu ya Bwana Yesu kushuka na kuanza kuandika chini, ilikuwa ni kwa “LENGO LA KUWAPA NAFASI YA KUJITAFAKARI na YA KUCHUKUA MAAMUZI THABITI”.
Ili tuelewe vizuri, tuutafakari huu mfano mrahisi.
“Mtu Fulani unayemjua amekuja kwako kukuuliza swali la mtego, au swali ambalo anayo majibu yake..na wewe ukajua anayo majibu yake…Hivyo ukaamua kukaa kimya, usimjibu swali lile, huku ukianza kuchezea chezea shilingi iliyopo mezani, pako mbele yako, au ukaendelea kuchezea simu…Na baadaye akazidi kukuhimiza umjibu… wewe ukamjibu, jibu fupi, la kumtafakarisha..na baada ya kumjibu ukaendelea kuchezea chezea ile shilingi iliyopo mezani au ukaendelea kuchezea simu yako”.
Je kwa tukio hilo kuna lolote la kujifunza katika hiyo shilingi au hiyo simu?.. kwamba tuanze kutafuta kujua ni shilingi ngapi uliyokuwa unaichezea, au ni mizunguko mingapi uliyokuwa unaizungusha au tuanze kutafuta kujua ni nini ulikuwa unakitazama kwenye simu wakati unaongeleshwa?.
Jibu ni la!.. wewe ulikuwa unarusha rusha ile shilingi, au unachezea simu ile kwa lengo la kumpa yule mtu nafasi ya kujitafakari swali alilouliza, hali kadhalika baada ya kumjibu kwa ufupi na kuendelea kuchezea simu yako ni ili kumpa nafasi ya nafasi ya kuondoka, na kutafakari ulichomwambia.. asiendelee kukuuliza maswali ambayo anayo majibu yake. (Na kwa njama hiyo fupi, basi utafanikiwa kumwondoa huyo mtu mbele yako, bila kutumia nguvu nyingi).
Ndicho Bwana Yesu alichowafanyia Mafarisayo, lengo lake ni kuwapa muda wa kujitafakari na kuacha kuuliza maswali ambayo wanayo majibu yake, na vile vile kuondoka pale. Lakini si kuandika dhambi zao ardhini.
Hivyo hiyo ni Hekima Bwana aliyoitumia kufupisha majadiliano marefu, na hoja zisizokuwa na Msingi.
Na sisi tunachoweza kujifunza hapo ni kuwa, sio kila hoja ni za kushiriki, nyingine ni kuzikatisha kwa Hekima.. Si kila swali ni la kujibu kwa urefu, na si kila mazungumzo ni ya kuyakumbatia kwa muda mrefu. Mazungumzo ambayo ni ya mashindano ya dini, hayo Mtume Paulo kwa ufunuo wa Roho alimwonya Timotheo na makanisa yote Kristo, kwamba wajiepushe nayo..
1Timotheo 6:20 “Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na maneno yasiyo ya dini, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo”
2Timotheo 2:14 “Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao”
Bwana Yesu alipopelekwa mbele ya Makuhani na mbele ya Pilato, hakuwa mtu wa maneno mengi, mara zote alipoulizwa maswali ambayo hayana maana yoyote alikaa kimya!!..
Marko 15:4 “Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi. 4 Pilato akamwuliza tena akisema, HUJIBU NENO? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki! 5 Wala Yesu HAKUJIBU NENO TENA, hata Pilato akastaajabu”.
Marko 15:4 “Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi.
4 Pilato akamwuliza tena akisema, HUJIBU NENO? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki!
5 Wala Yesu HAKUJIBU NENO TENA, hata Pilato akastaajabu”.
Nasi pia pia hatuna budi kuwa watu wa maneno machache na watu wa kujiepusha na mashindano, ya dini.. Umeona, kwa matendo hayo mawili tu ya Bwana kuacha kuwazungumza na wale mafarisayo na kuendelea kuandika chini, ilitosha kuwaondoa Mafarisayo wale, Zaidi hata angetumia maneno mengi, lakini kwa maneno yale machache na tendo lile moja, alivifunga vyinywa vyao.
Tito 3:9 “Lakini maswali ya upuzi ujiepushe nayo, na nasaba, na magomvi, na mashindano ya sheria. Kwa kuwa hayana faida, tena hayana maana”.
Maran atha!
Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?
Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?
NEEMA YA MUNGU KWA MARIAMU.
Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?
Kwanini Yakobo na Yohana waliitwa “Wana wa Ngurumo”?
SWALI: Yohana alimaanisha nini aliposema..10]Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?
Je hiyo siku ya Bwana ni ipi? Na kwanini itajwe pale?
Ufunuo wa Yohana 1:10
[10]Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
JIBU: Mtume Yohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo, kwa ajili ushuhuda wa Kristo, Na kwa mara ya kwanza alipotokewa na Bwana Yesu na kuonyeshwa mambo yanayohusiana na siri za siku za mwisho na kanisa, anasema siku hiyo aliyotokewa iliangukia siku ya Bwana.
Ikumbukwe kuwa tangu awali wakristo wa kwanza, waliifanya siku ya kwanza ya juma( Yaani jumapili) kuwa ni siku ya Bwana, kufuatana na tukio la kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Na ni siku ambayo Bwana alikuwa akiwatokea wanafunzi wake (Soma Marko 16:9, Yohana 20:19 ).
Vilevile Siku hii hii ndio siku ambayo kanisa lilipokea ahadi ya Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza..Kwahiyo watakatifu wote, tangu enzi za mitume, hadi wakati wetu huu wa sasa waliifanya siku hii kuwa ni siku ya Bwana.
Soma vifungu hivi;
Matendo ya Mitume 20:7
[7]Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
1 Wakorintho 16:2
[2]Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
Na ndio hapa sasa tunaona mtume Yohana anaeleza Kwamba alipokuwa katika Roho, siku ya Bwana (yaani jumapili) ndio alitokewa na maono hayo..
Zingatia: Mtazamo ambao siku hiyo ilikuwa ni jumamosi, si sahihi. Jumamosi, haikuwahi kuadhimishwa na wakristo wa kwanza kwa shughuli rasmi za kibada, kwa mujibu wa maandiko.
Sio kwamba Bwana anaithamini jumapili, zaidi ya siku nyingine zote, hapana au siku hiyo ni takatifu zaidi ya nyingine zote, Hapana bali anachotaka kutuonyesha ni umuhimu wa siku tunazoziweka wakfu kwa ajili yake kwamba anaziheshimu na kwamba kwa kupitia hizo, ni rahisi yeye kujifunua kwetu.
Ikiwa siku yetu kwa Bwana ni jumamosi, basi tuithamini kwa kuwa katika Roho kama vile Yohana alivyokuwa mpaka Kristo akamtembelea siku hiyo..
Kama ni jumapili, tuifanye vivyo hivyo, kama ni jumatano tuipe heshima yake. Hizi siku tusizichukulie juu juu tu,
Lakini leo hii tunapuuzia ibada kuu za kila wiki (Jumapili), tunakosa mafundisho ya biblia kanisani, au hata tukienda siku hiyo hatuwi katika roho, tunaenda ili kutimiza tu wajibu . Halafu tunataka Bwana ajidhihirishe kwetu tunapokuwa nyumbani tunaangalia tv.
Kamwe Usiruhusu, siku yako ya ibada iliwe na uvivu au mambo ya ulimwengu huu, kama vile anasa, na mihangaiko ya dunia, hata kama upo katika mazingira ambayo hayana watakatifu..Nenda milimani huko, au maporini ukasome biblia na kuomba kama Yohana..kuliko kumwachia shetani akupangie ratiba zake kwenye siku takatifu ya Bwana..
Ithamini siku ya ibada. Na kwa hakika atajidhihirisha kwako.
Ubarikiwe.
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?
UFUNUO: Mlango wa 1
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
JIWE LILILO HAI.
Kwa kawaida Mawe, hayaishi.. ni vitu visivyo na uhai.. Kwasababu tabia mojawapo ya viumbe hai ni kukua, na nyingine ni kuzaliana na kuwa na hisia (yaani muitikio kwa mazingira ya nje).
Lakini Mawe tunayoyaona yote hayazai.. Hakuna jiwe linaloweza kuzaa..wala mawe hayakui, yapo vilevile siku zote..kwahiyo ni vitu visivyo hai.
Lakini biblia inasema lipo Jiwe moja la kipekee ambalo LINAISHI!!.. Hilo ni tofauti na mawe mengine, mawe mengine ni magumu lakini hayaishi, ni mazuri kimwonekano lakini hayana uhai, ni ya gharama sana, lakini hayana uzima, hayakui, hayazai, hayaongezeki. Lakini lipo jiwe moja la gharama sana, na gumu sana, na lililo hai, linalokua na kuzaa..na jiwe hilo si jingine zaidi ya YESU KRISTO.
1Petro 2:4 “Mmwendee yeye, JIWE LILILO HAI, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima”.
Jiwe hili lilianza dogo sana, katika tumbo la Bikira Mariamu.. likazidi kukua katika uweza na nguvu. Mpaka kufikia miaka 33 na nusu, liliongezeka nguvu, na thamani baada ya kushinda mauti, na sasahivi limeunuliwa juu sana, na siku moja litarushwa kutoka juu mpaka chini duniani na kuvunja vunja falme zote za ulimwengu, na litakuwa Mlima mkubwa, na litazaa milima mingine mingi, ambayo ndiyo sisi.
Danieli 2:34 “Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande……………………
36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme.
44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni ATAUSIMAMISHA UFALME AMBAO HAUTAANGAMIZWA MILELE, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali UTAVUNJA FALME HIZI ZOTE VIPANDE VIPANDE NA KUZIHARIBU, NAO UTASIMAMA MILELE NA MILELE.
45 NA KAMA VILE ULIVYOONA YA KUWA JIWE LILICHONGWA MLIMANI bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.”.
Jiwe hilo lililo hai ni YESU KRISTO. Linaishi, ndio maana unaona hapo katika maandiko, linaonekana kukua na kuwa mlima mkubwa, na hatimaye kuzaa mawe mengine na hayo mawe kuwa milima mingine mingi… na milima hiyo ndio sisi tuliomwamini, ambao tutakaokuja kutawala pamoja naye katika utawala wa miaka elfu.
1Petro 2:5 “NINYI NANYI, KAMA MAWE YALIYO HAI, MMEJENGWA MWE NYUMBA YA ROHO, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo”
Lakini wote ambao hawatamwamini Yesu katika maisha haya, Jiwe hili litakuja kuwaponda ponda..
1Petro 2:6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika. 7 BASI, HESHIMA HII NI KWENU NINYI MNAOAMINI. BALI KWAO WASIOAMINI, JIWE WALILOLIKATAA WAASHI, LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBENI. 8 TENA, JIWE LA KUJIKWAZA MGUU, NA MWAMBA WA KUANGUSHA, KWA MAANA HUJIKWAZA KWA NENO LILE,WASILIAMINI,NAO WALIWEKWA KUSUDI WAPATE HAYO”.
1Petro 2:6 “Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 BASI, HESHIMA HII NI KWENU NINYI MNAOAMINI. BALI KWAO WASIOAMINI, JIWE WALILOLIKATAA WAASHI, LIMEKUWA JIWE KUU LA PEMBENI.
8 TENA, JIWE LA KUJIKWAZA MGUU, NA MWAMBA WA KUANGUSHA, KWA MAANA HUJIKWAZA KWA NENO LILE,WASILIAMINI,NAO WALIWEKWA KUSUDI WAPATE HAYO”.
Litumainie hili jiwe lililo hai, mengine yote yana thamani lakini hayana uzima, Wafalme wa dunia wana thamani lakini hawana uhai, ni mawe yasiyoishi, Wakuu na wenye mamlaka ni mawe magumu kama almasi yenye thamani nyingi lakini hayana uhai…(kwasababu almasi ijapokuwa ni ya thamani kuliko mawe yote, lakini si kitu kinachoishi). Lakini Yesu ni Jiwe lililo hai, tena lenye thamani, na linaloharibu. Hilo ndilo la kulitumainia na kulitafuta.
Kama umelipata hilo, basi wewe nawe ni jiwe kama yeye Bwana Yesu alivyo, katika ulimwengu wa roho unavunja vunja na kuponda ponda ufalme wa giza na kuharibu na kuteka nyara kila kitu. Na unao uwezo wa kuzaa mawe mengine, kwasababu nawe ni jiwe lililo hai.
Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika..
CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.
Roho, Nafsi, na Mwili vina utofauti gani?
Je Lutu alikwenda kuwahukumu watu wa Sodoma na Gomora? Kulingana na Mwanzo 19:9?
JIWE LA KUSAGIA
Ni jambo la kawaida katika familia yoyote, si Watoto wote watakuwa na mahusiano sawa na wazazi wao. Wapo ambao wataonekana kuaminiwa Zaidi ya wengine, wapo ambao watapendwa Zaidi ya wengine, pia wapo ambao watategemewa na wazazi wao kuliko wengine, n.k. Lakini hilo haliwafanyi wale wengine wasiwe Watoto wa wazazi wao.
Inatokea hivyo, kutokana na aidha tabia zao, ujuzi au nafasi walizonazo. Vivyo hivyo na kwa Mungu katika familia yake ya watakatifu (Waliookoka), Si watakatifu wote watakuwa vipenzi wa Mungu, si wote wataaminiwa na Mungu, na si wote watategemewa na Bwana. Lakini hayo hayawafanyi hao wengine wasiwe Watoto wa Mungu.
Leo tutatazama mambo ambayo tukiwa nayo, basi tujue tutakuwa Watoto ambao tutapendwa sana na Mungu. Hivyo Ili tufahamu hayo tutaangalia katika biblia, mifano ya watu watatu (3) ambao, walipendwa na Mungu, ili na sisi tuige tabia kama zao tupendwa na Mungu.
Upendo ndio tabia ya kwanza itakayokuzogeza karibu na Mungu, na upendwe sana. Kati ya mitume 12 wa Bwana Yesu, Mtume Yohana peke yake ndiye aliyependwa na Yesu sana. Mpaka akawa muda wote anaegemea kifuani pake.
Yohana 21:20 “Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?) 21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?
Yohana 21:20 “Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)
21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?
Lakini lililomfanya apendwe na Yesu, ni upendo ambao aliuiga kutoka kwake. Na ndio maana utaona injili zake zote anahimiza upendo, kwasababu Mungu mwenyewe ni Upendo. Hivyo ili na sisi tupendwe na Bwana, hatuna budi kuonyesha bidii katika kupendana,
Na tabia za upendo tunazisoma katika 1Wakorintho 13:4-8….ambazo ni hizi;
13.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 13.5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 13.6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 13.7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 13.8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
13.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
13.5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
13.6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
13.7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
13.8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Maana yake, ni kuwa tayari kukataa mambo yote yanayoweza kukukosesha na Mungu bila kujali gharama/hasara gani utakayoingia kwa kutokufanya hivyo. Huo ndio uthabiti wa moyo Mungu anaoutaka. Ambao alikuwa nao Danieli, ndio uliomfanya Mungu ampende sana.
Danieli 10:11 “Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.
Soma pia Danieli 10:19,
Unaona Danieli, alikuwa ni mtu aliyependwa sana. Hiyo yote ni kutokana na moyo wake wa msimamo, tangu alipoingia kule Babeli wakati wayahudi wote, wapo vuguvugu, akiwa bado ni kijana mdogo alipoitwa akae katika milki za mfalme hakusita kutaa vyakula najisi vya kifalme..Na hata bado akiwa mzee, walipotaka kumzuia asimwabudu Mungu wake, bado aliendelea kumwabudu kutwa mara tatu, bila kuogopwa kutupwa katika tundu la simba.
Moyo kama huo unaonyesha upendo mkamilifu kwa Mungu wake, hivyo Mungu naye angeonyesha upendo wake tu. Na ndio maana Danieli kila alipotembelewa na Malaika alianza kwa kuambiwa mtu upendwaye sana.
Vivyo hivyo na sisi, katika mambo yetu, Ikiwa boss wako/ kazi yako vinakuzuia usiwe karibu na Mungu wako kwa ule muda unaokupasa umwabudu. Ukionyesha uthabiti, kwamba ni lazima ukamtumikie Bwana wako, ukamfanyie ibada, Bwana atakupenda..Ikiwa kazini kwako wanakulazimisha uvae suruali na vimini wewe kama binti uliyeokoka, ukakataa na kusema Imani yangu hainiruhusu bila kuogopa kufukuzwa kazi, basi ujue, upo katika njia ya kupendwa na Mungu kama Danieli.
Sulemani, ni mtu mwingine ambaye biblia inatuambia alipendwa na Mungu. Tunalithibitisha hilo katika,
Nehemia 13:26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. TENA ALIPENDWA NA MUNGU WAKE, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.
Ni kwasababu gani? Ni kwasababu yeye hakuwa kama wafalme wengine, kama Sauli, ambao akili zao zilielekea katika kutawala tu, na vita dhidi ya maadui. Bali yeye alitamani kupata njia ya namna ya kuyatengeneza mambo kwa hekima, watu wa Mungu wafurahi katika Bwana na kumtimikia katika utulivu. Ndipo Mungu akasikia ombi lake, akampatia. (1Wafalme 3:1-15)
Ndio hapo utaona hata vile ambavyo hakuomba, kama vile Mali Mungu alimpatia, kwasababu alipendwa sana na Mungu kwa kile alichokitamani. Na kama isingekuwa yeye mwenyewe kuja kukengeuka mwishoni, basi angekuwa ni mfano mkubwa sana wa kuigwa katika biblia nzima.
Vivyo hivyo na wewe, ukiitafuta hekima, ujue unatafuta kupendwa na Mungu, na hekima ya Mungu ipo katika Neno lake. Ukiwa ni mtu wa kujifunza biblia, na sio msomaji tu, kama gazeti, Hekima hiyo itaingia yenyewe moyoni mwako (Mithali 2:10). Na Mungu atakusaidia kuwapa wengine neema hiyo. Na mwisho wa siku utapendwa na Mungu.
Hekima zote za kimaisha, za kiutumishi, za kifamilia, za kijamii, zipo katika Neno la Mungu. Hivyo hakuna namna utaweza kuishi bila kusoma biblia.
Hivyo mambo hayo matatu tukiyachanganya. Yaani UPENDO, UTHABITI WA MOYO, NA HEKIMA.
Basi tujue kupendwa na Mungu, ni lazima kutatokea tu kwetu, . Na faida yake ni kuwa, tutaonyeshwa na mambo makubwa Zaidi ya tunayoyajua. Danieli na Yohana ndio waliopewa siri za nyakati za mbeleni. Na mpaka sasa tunagemea sana nabii zao ili kutambua nyakati na majira ya siku za Mwisho. Vilevile hata na vyote tunavyovisumbukia vya mwilini, ikiwa tutapendwa na Mungu basi yeye mwenyewe atavisogeza karibu na sisi. Kama alivyofanya kwa mtumwa wake Sulemani, na Danieli.
Bwana akubariki, na nikutakie kupendwa kwema na Bwana.
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)
NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?
Donda-Ndugu ni nini?
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU
Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?
Moabu ni nchi gani kwasasa?
Kigao ni nini? Na Je kinafunua nini kwa agano jipya?
Gumegume ni jamii ya miamba ambayo ni migumu sana, inapatikana huko maeneo ya mashariki ya kati sana sana nchi ya Palestina. Zamani ilitumika katika kutengeneza vifaa, kama nyundo, mashoka, visu, majembe, ncha za mikuki na michale n.k. hiyo yote ni kwasababu ya sifa ya ugumu wake.
Neno hili limetumika sehemu kadha wa kadha katika biblia kama tunavyoweza kulisoma katika vifungu hivi;
Yoshua 5:2 “Wakati huo Bwana akamwambia Yoshua, Haya, jifanyie visu vya mawe ya gumegume, watahiri tena wana wa Israeli mara ya pili.
Ayubu 28:9 “Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake; Huipindua milima hata misingi yake”.
Isaya 5:28 “Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika; Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume; Na gurudumu zao kama kisulisuli”;
Ezekieli 3:9 “Kama almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji chako; usiwaogope, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi”.
Kumbukumbu 32:13 “Alimpandisha mahali pa nchi palipoinuka, Naye akala mazao ya mashamba; Akamnyonyesha asali iliyotoka jabalini, Na mafuta yaliyotoka katika mwamba wa gumegume;”
Lakini je Neno hili/ Mwamba huu unafunua nini rohoni?
Mungu anataka na sisi tuwe na mioyo ya gumegume kwake,(yaani mioyo migumu isiyokengeuka haraka), Kama ilivyokuwa kwa mwanawe mpendwa Yesu Kristo, ambaye tunamsoma unabii wake katika Isaya 50:7, akielezewa jinsi moyo wake ulivyokuwa mgumu kwa Bwana kama gumegume, licha ya kuwa alipitia mateso makali namna ile.
Isaya 50:5 “Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma. 6 Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate 7 Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, KWA SABABU HIYO NIMEKAZA USO WANGU KAMA GUMEGUME, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Isaya 50:5 “Bwana MUNGU amenizibua sikio langu, wala sikuwa mkaidi, wala sikurudi nyuma.
6 Naliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate
7 Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, KWA SABABU HIYO NIMEKAZA USO WANGU KAMA GUMEGUME, nami najua ya kuwa sitaona haya.
Umeona, Bwana Yesu, japokuwa alipitia mateso makali, lakini bado moyo wake haukugeuka nyuma. Nasi pia ndivyo Mungu anavyotaka atuone.
Mtume Paulo pia alikuwa ni mtu wa namna hii, mpaka akadhubutu kusema hakuna jambo lolote linaloweza kumtenga yeye na upendo wa Kristo.
Warumi 8:38 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Warumi 8:38 “Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo,
39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Swali la kujiuliza, je! Na sisi, mioyo yetu ni ya gumegume kwa Bwana? Au ya Udongo?
Je! Dhiki na mateso vitakapotujia, bado tutaweza kung’ang’ana na Bwana?
Bwana atusaidie, tuwe watu na namna hii.
Shalom.
Shinikizo ni nini?
MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.
Tofauti kati ya kukana na kusaliti ni ipi?
Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).
Bwana Yesu alimaanisha nini kusema “Saa yangu haijawadia?”
Kwanini Bwana Yesu alivikwa taji ya miiba?
Tusome,
2Timotheo 2:16 “Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu, 17 na neno lao litaenea kama DONDA-NDUGU. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, 18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha”.
2Timotheo 2:16 “Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,
17 na neno lao litaenea kama DONDA-NDUGU. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha”.
Donda-ndugu ni kidonda kinachotokana na damu kuacha kupita katika kiungo kimojawapo cha mwili, husuani katika vidole au katika viungo vya ndani ya mwili kama Maini, na hivyo kusababisha kusababisha kiungo hicho kitengeneza kidonda kisichopona..
Na kiungo hicho kisipoondolewa basi kidonda hicho kinasambaa mwili mzima, na kusababisha matatizo mengine makubwa zaidi. Ugonjwa wa donda-ndugu hauna tofauti na ugonjwa wa Kansa. Na suluhisho la kutibu ugonjwa huo ni kukikata hicho kiungo.
Mtume Paulo alifananisha mafundisho ya uongo ya Himenayo na Fileto na ugonjwa huo wa Donda-Ndugu.
FILETO na HIMENAYO walianza kuwafundisha watu kuwa Kiyama kimeshapita. Hakuna tena kiyama kinachokuja mbeleni, unyakuo umeshapita zamani, na hautakuja tena..
Na kwasababu mafundisho hayo ni mafundisho hatari, maana yake yasipokataliwa na kuzuiliwa vikali ni rahisi kusambaa kwa watu wengi na kusababisha imani za watu wengi kuvurugika na watu wengi kufa kiroho.
Watu wakishaamini kuwa hakuna tena unyakuo unaokuja, kitakachofuata ni kupoa na kuendelea na dhambi na anasa, hata kama watajiita bado ni wakristo, lakini ndani yao hakuna tena tumaini lolote la maisha yanayokuja. Utaona tena Mtume Paulo, analionya kanisa la Thesalonike juu ya mambo hayo hayo..
2Thesalonike 2:1 “Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, 2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. 3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; 4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu. 5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo? 6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake”.
2Thesalonike 2:1 “Basi, ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake,
2 kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.
3 Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;
4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.
5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?
6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake”.
Hata sasa Unyakuo bado haujatokea, lakini siku yoyote kuanzia sasa, kanisa litaondolewa, na watakatifu wakweli walioukataa ulimwengu na kujitakasa kwa Neno, watanyakuliwa juu katika utukufu, na duniani kitakachokuwa kimesalia ni dhiki kuu ya Mpinga-Kristo.
Sasa hivi kuna mafundisho mengi yamezalika ndani ya Imani ya Kikristo, wapo wanaosema kwamba hakuna unyakuo wa kanisa, wapo wanaosema kuwa unyakuo umeshapita, na sasa tupo katika utawala wa miaka elfu moja, Wengine wanaamini kuwa mamlaka ya Bwana Yesu imeshapita, sasa tupo mamlaka nyingine, ya Mungu Baba na mafundisho mengine mengi sana…
Na mafundisho haya katika siku hizi za mwisho yameenea kama donda-ndugu kiasi kwamba hata kuwabadilisha tena watu wayarudie maandiko inakuwa ni ngumu.
Je! Siku ya unyakuo watoto wachanga watanyakuliwa?
TOFAUTISHA KATI YA MAFUNDISHO YA YESU, NA YA WAANDISHI.
Je ni lazima kupitia mafundisho ya muda mrefu kabla ya kubatizwa?
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
WhatsApp
Kukana ni kitendo cha kumkataa mtu aliyekaribu nawe, kwa hofu/shinikizo Fulani pengine aidha kwa hofu ya kuaibishwa, au kudharauliwa, au kuuliwa au kutengwa, au kuchekwa n.k. Lakini kimsingi sio kwamba humpendi au huyo mtu hana thamani yoyote kwako.
Lakini kusaliti, ni jambo baya Zaidi, kwasababu linahusisha, kumkataa mtu Fulani aliye karibu nawe kwa hiari yako mwenyewe, pasipo shinikizo lolote, kwa maslahi yako binafsi, ni kitendo cha moyo-baridi kabisa.
Kwamfano Petro alimkana Bwana, kutokana na shinikizo la hofu ya yeye kukamatwa na kwenda kupigwa kama Bwana..Lakini hapo nyuma utaona, alidhubutu kumuhakikisha kabisa Bwana kwamba hata wenzake wote wajapomkana, yeye hatofanya hivyo (Mathayo 26:33-35)
Utaona tena hata baadaya ya kutubu kwake baadaye, alipokutana na Bwana kule baharini bado alimuhakikisha mara tatu kuwa anampenda yeye..(Yohana 21:15-17). Kuonyesha kuwa ni shinikizo ndio lililompeleka kufanya vile, lakini moyo wake bado upo kwa Yesu.
Lakini Yuda tangu mwanzo alikuwa hampendi Bwana, japokuwa yeye alipendwa sana, mahali pengine mpaka Yesu akawa anampa siri zake za ndani japokuwa alikuwa mwizi, biblia inasema hivyo katika Zaburi 41:9
9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.
Lakini kinyume chake akarudisha mabaya badala ya mema. Utaona yeye mwenyewe kwa hiari yake akawafuata wakuu wa makuhani bila shinikizo lolote, akawaambia mtanipa nini, nikiwapa Kristo!. Wakamuahidia Pesa. (Mathayo 26.14-16)
Usaliti unafanana na mtu ambaye yupo tayari kumuua au kumletea madhara mzazi wake, kwa faida zake mwenyewe, pengine mali, au cheo, au heshima. Bila kujali kuwa yeye ndiye aliyemnyonyesha, aliyemtunza tangu akiwa tumboni, ndiye aliyemsomesha na kumvisha n.k.
Lakini kibiblia, vyote viwili yaani “kukana na kusaliti” hatupaswi kuwa navyo kwa Bwana wetu.
Leo hii wapo watu wanaomsaliti Bwana..Ndio hawa manabii na makristo wa uongo. Ambao wanajua kabisa waliokolewa kwa thamani, walitolewa chini matopeni, lakini wanapokuzwa kidogo, wanaanza kumgeuza Kristo kuwa biashara yao. Wanaacha utumishi walioitiwa, wanatumia fursa ya Kristo, kuyashibisha matumbo yao tu… Hawa ndio wakina Yuda.
Wafilipi 3:18 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; 19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Wafilipi 3:18 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;
19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Lakini Wakanaji, ni wakristo wote, ambao mioyo yao haipo kikamilifu kwa Bwana..wapo nusu nusu, ndio wale wakipitia dhiki kidogo, wapo tayari kumwacha Kristo, kisa ndugu, au wazazi, au shughuli, au ujana au anasa..hali na mazingira yanawafanya wamkane Bwana wao moja kwa moja, kwa matendo yao.
Na hii ni mbaya sana Bwana Yesu mwenyewe alisema..
Mathayo10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga. 35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; 36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake. 37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili. 38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. 39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.
Mathayo10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;
36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.
39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.
Umeona?..Lipi bora, uchukiwe na ulimwengu leo, lakini siku ile utukuzwe na Yesu, au leo hii umkane halafu siku ile ukwane naye? Majibu yanajulikana.
Hatupaswi kuogopa kuonekana washamba kisa tumeokoka, hatupaswi kuogopa kupigwa, au kuchekwa, au kuonekana tumerukwa na akili sababu ya Yesu, mwokozi wetu. Bali tumkiri yeye kwa matendo yetu, kwasababu hata yeye mwenyewe alidharauliwa lakini akayapuuzia maradhau yao (Isaya 53:3).
Hivyo sote tujifunze kujitwika misalaba yetu tumfuate Kristo. Ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu,.
Bwana atubariki.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Je! Yuda atahukumiwa na Mungu kwa dhambi yake ya usaliti?
Chapa zake Yesu ni zipi hizo?
WAPENZI, MSIIAMINI KILA ROHO.
Neno ‘Kima’ linamaanisha nini Katika biblia? (Mathayo 27:9 )
Je! Ni kanisa lipi sahihi kumuabudia Mungu?