SWALI: Kwanini wayahudi walimwambia Yesu kuwa hawajawahi kuwa watumwa wa mtu yeyote angali tunajua kuwa walishawahi kuwa watumwa kule Misri kwa miaka 400?
JIBU: Tusome;
Yohana 8:31 “Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; 32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. 33 Wakamjibu, Sisi tu uzao wake Ibrahimu, wala hatujawa watumwa wa mtu wakati wo wote; nawe wasemaje, Mtawekwa huru? 34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. 36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”.
Kauli ya hawa wayahudi haikuwa kauli ya kweli bali ya uongo uliowazi, Na lengo la majibu yao halikuwa kutafakari Yesu anayoyasema bali kumpinga tu, Na ndio maana hawakuona shida kuzungumza uongo wa wazi, kwani vitabu vyao vinaeleza walishawahi kuwa watumwa Misri,Babeli, Ashuru na sehemu kadha wa kadha walishawahi kutumikishwa na mataifa hata wakiwa katika taifa lao wenyewe.
Lakini Yesu hakulenga utumwa wa mwilini kama wao walivyodhani, bali ule wa rohoni, wa dhambi, yaani tamaa, wivu, uongo, mawazo mabaya, hasira n.k. Mambo ambayo walikuwa hawana.Lakini kwasababu lengo lao lilikuwa ni kumpinga waliendelea bado kusema uongo hata juu yake..Kwamfano ukisoma vifungu vinavyofuata katika mazungumzo yao, ule mstari wa 48 utaona wanasema kwamba yeye ni msamaria tena ana pepo. Jambo ambalo ni uongo mwingine wa makusudi. Kwani Walijua kabisa Yesu ni myahudi, na wazazi wake Yusufu, na ndugu zake wote wapo nao, mpaka kazi yao ya useremala waliyoifanya waliijua, tena wakamwita Rabi sehemu nyingine, lakini kwasababu wapo kibishi wakazusha uongo na kusema yeye ni msamaria, tena mwenye pepo.
Na ndio maana Bwana Yesu katika mazungumzo hayo hayo (Mstari wa 44) akawaeleza wazi kuwa wao ni wa Baba yao ibilisi kwasababu “hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo ”. kwasababu ya uongo wao.
Hii ni kutufundisha nini?
Tuipende kweli, Kwasababu tusipolipenda Neno la Mungu, shetani atatutumia kulipinga Neno hilo hilo kwa kushuhudia habari za uongo uliowazi na wala hututaona shida, kama ilivyokuwa kwa wayahudi hawa.
Je! Umeokoka, je! Unahakika wa maisha yako ya milele baada ya kifo? Je! Unatambua kuwa hizi ni siku za mwisho, na roho ya mpinga-Kristo inatenda kazi ndani ya watu ambao hawajaokolewa leo? Unasubiri nini usimgeukie muumba wako, tamaa za dunia zitakufikisha wapi?umefungwa Rohoni upo chini ya Utumwa wa dhambi, anayeweza kukuweka huru ni Yesu tu peke yake. Ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618 / +255789001312, kwa ajili ya mwongozo huo bure.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Ni kosa gani lililowafanya wana wa israeli wawe watumwa miaka 400 Misri?.(
WANA WA MAJOKA.
EPUKA MUHURI WA SHETANI
YULE JOKA WA ZAMANI.
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?
Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)
Je! Mwendo wa Sabato ulikuwaje kibiblia?(Matendo 1:12)
Rudi nyumbani
Print this post
Jibu: Iskariote sio jina la mtu fulani, au la mzazi wa Yuda, bali ni jina lenye maana ya “Mtu wa Keriothi/ Kariote”…
Neno Iskariote ni neno la kigiriki lililoungwa na maneno mawili: “Is” ambalo maana yake ni “mwana wa” na la pili ni “Kariote”..likimaanisha mji wa Kariote au KeriothiKwahiyo ukiunganisha maneno hayo mawili maana yake ni “Mwana wa Keriothi”
Na Keriothi ni mji uliokuwepo katika Nchi la Moabu, ambayo kwasasa ni maeneo ya nchi ya Jordani.Na Wamaobu walikuwa ni watu wa mataifa, hawakuwa waIsraeli, kwa urefu kuhusu Taifa hili unaweza kufungua hapa >>> MOABU NI WAPI
Sasa swali ni je! Kwanini Yuda aitwe hivyo, na asiitwe tu Yuda! Kwanini atambulike kama Mwana wa Keriothi(Iskariote)?… kulikuwa na umuhimu gani yeye kutajwa kwa jina hilo?.
Jibu rahisi ni kwamba, alitajwa vile ili kumtofautisha na wakina Yuda wengine, kwasababu kulikuwa na watu wengi wanaoitwa Yuda ambao pia walikuwa wanafuatana na Yesu. Na Kuna mwingine alikuwa mdogo wake Yesu.
Kwa mfano utaona kuna wanafunzi wawili wa Bwana Yesu waliokuwa na majina yanayofanana..wote walikuwa wanaitwa Simoni, sasa ili kuwatofautisha ndio mmoja akajulikana kama Simoni Petro na mwingine Simoni Mkananayo. (Mathayo 10:2-4).
Vile vile kulikuwa na wanawake wengi waliomfuata Bwana walioitwa Mariamu, sasa ili kuwatofautisha hao akina Mariamu, ndipo hapo wengine wakatajwa kulingana na miji waliyotokea mfano Mariamu aliyetolewa pepo saba alijulikana kama Mariamu Magdalene, kufuatia mji aliotokea ujulikanao kama Magdalene. (Luka 8:2).
Na Yuda Iskariote aliitwa hivyo kufiatia mji ambao Baba yake alitokea (Keriothi).
Yohana 6:71 “Alimnena Yuda, mwana wa Simoni Iskariote; maana huyo ndiye atakayemsaliti; naye ni mmojawapo wa wale Thenashara”.
Soma pia Yohana 13:2, na Yohana 13:26, huenda baba yake Yuda alikuwa ni myahudi lakini mwenyeji wa Kerioth pamoja na Yuda mwanae.
Kuhusiana na mji wa Keriothi au Kariote, pitia mistari ifuatayo; Amosi 2:2, Yeremia 48:24, na Yoshua 15:25.
Na sisi Bwana anatujua majina yetu kulingana na tabia zetu.
Kutoka 33:17 “BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako”
Mbele za Mungu kila mtu anajulikana kwa tabia yake…fulani mcha Mungu, fulani mwombaji, fulani mkaribishaji, fulani mwizi, fulani mzinzi, fulani msengenyaji.
Bwana atujalie tujulikane kwa majina mazuri na mema mbele zake ili tupate neema.
Maran atha
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
ILI NIWE KIELELEZO KWA WALE WATAKAOMWAMINI BAADAYE.
JINA LA MUNGU NI LIPI?
TUUTAFUTE USEMI MMOJA. TUUJENGE MNARA WA MUNGU
Jibu: Kulikuwa na tukio zaidi ya moja la Bwana Yesu kupakwa mafuta…Tukio la kwanza ni hilo tunalolisoma katika injili tatu, (Mathayo 26:6-13 na Marko 14:3-8 na Yohana 12:1-3), ambapo biblia inaonyesha moja kwa moja kuwa ni Mariamu ndugu yake Lazaro, ndiye aliyempaka Bwana Marhamu siku sita kabla ya pasaka.
Tusome,
Yohana 12:1 “Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu. 2 Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye. 3 Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu”.
Yohana 12:1 “Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu.
2 Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye.
3 Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu”.
Lakini tukirudi katika Injili ya Luka, tunasoma tukio lingine ambalo linakaribia sana kufanana na hili la Bethania, ambapo biblia inasema alitokea mwanamke mmoja mwenye dhambi na kuanguka miguuni pake na kulia huku akimpaka mafuta.
Jibu: Turejee..
Luka 7:36 “Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani. 37 Na tazama, mwanamke MMOJA WA MJI ULE, ALIYEKUWA MWENYE DHAMBI, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu. 38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.”
Luka 7:36 “Mtu mmoja katika Mafarisayo alimwalika ale chakula kwake; akaingia katika nyumba yake yule Farisayo, akaketi chakulani.
37 Na tazama, mwanamke MMOJA WA MJI ULE, ALIYEKUWA MWENYE DHAMBI, alipopata habari ya kuwa ameketi chakulani katika nyumba ya yule Farisayo, alileta chupa ya marimari yenye marhamu.
38 Akasimama nyuma karibu na miguu yake, akilia, akaanza kumdondoshea miguu machozi yake, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake, akiibusu-busu miguu yake na kuipaka yale marhamu.”
Sasa ni viashiria gani vinatuthibitishia kuwa yale yalikuwa ni matukio mawili tofauti?
Hivyo kwa hitimisho ni kuwa haya ni matukio mawili tofauti, yaliyotokea kukaribiana na biblia haikumtaja Yule mwanamke wa Galilaya alikuwa ni nani?.. labda huenda alikuwa ni Yule Yule Mariamu alimpaka mara mbili, au ni mwanamke mwingine ambaye biblia haijamtaja jina lake.
Lakini hayo yote si ya muhimu sana kuyajua, (kwamba ni nani, au ni matukio mangapi) lililo la muhimu kulijua ni tendo hilo la kiimani wanawake hawa waliloyoyafanya.. sasa kujua kwa undani Siri iliyokuwepo katika kumpaka Bwana mafuta fungua hapa >>> AKAKIVUNJA KIBWETA AKAIMIMINA KICHWANI PAKE.
Bwana atubariki.
SWALI: Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani? Ni mpangalio wake upoje kulingana na mwandishi?
JIBU: Kitabu Cha Zaburi hakikuandikwa na mtu mmoja, Bali ni mjumuisho wa waandishi mbalimbali. Kitabu hiki ndio kilichoandikwa na waandishi wengi kuliko vyote kwenye biblia.
Kiliandikwa katika nyakati mbalimbali Kwa kipindi Cha miaka elfu moja na zaidi..kitabu hiki kimebeba mashahiri, maombolezo, nyimbo na maombi.
Mfalme Daudi ndiye aliyeandika Kwa sehemu kubwa kitabu hichi;
Jumla Zaburi zilizojuliakana kuwa zimeandikwa na Daudi ni 73. Lakini pia zipo nyingine 2 ambazo hazikutajwa moja Kwa moja lakini waandishi wengine katika nyaraka zao walinukuu baadhi ya maneno kwenye Zaburi, na kusema ni ya Daudi.
Ambazo ni Zaburi 2 ambayo sehemu ya maandishi hayo yanatajwa katika Matendo 4:25,
Na Zaburi 95 Waebrania 4:7
Hivyo kudhaniwa kuwa Daudi aliandika Zaburi 75;
Hizi ndio orodha ya hizo Zaburi 73 alizoziandika yeye;
3-9
11-32
34-41
51-65
68-70
86
101
103,
108-110
122
124
131
133
138-145
2. SULEMANI
Mwandishi mwingine ni Sulemani yeye aliandika Zaburi mbili tu..ambazo ni Zaburi 72 na Zaburi 127″
3. ETHANI na HEMANI
Nyingine zimeandikwa na Ethani na Hemani, Hawa ni watu ambao waliokuwa na hekima nyingi mfano wa Mfalme Sulemani, wanatajwa katika vifungu hivi;
1 Wafalme 4:30-31
30 Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.31 Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.
Ethani aliandika Zaburi moja tu nayo ni Zaburi 89
Hemani pia aliandika Zaburi moja ambayo ni Zaburi 88
4. MUSA
Mwandishi mwingine alikuwa ni Musa yeye pia aliandika Zaburi 1 ambayo ni ya 90.
5. ASAFU
Zaburi nyingine 12 ziliandikwa na Asafu na familia yake.
Ambazo ni
50, 73-83
6. WANA WA KORA
Wana wa Kora, waliandika Zaburi 11
42, 44-49,84-85, 87-88
7. WASIOTAMBULIKA
Na Zaburi nyingine 48, zilizobakia hazijulikani waandishi wake.
Hivyo Kwa ufupisho ni kwamba Daudi aliandika Zaburi 73, Sulemani 2, Musa 1, Ethani 1, Hemani 1, Asafu 12, Wana wa Kora 11, wasiotambulika ni 48.
Ikiwa utapenda kupata uchauzi zaidi ya kitabu Cha Zaburi pitia link hii >> https://wingulamashahidi.org/2020/11/27/vitabu-vya-biblia-sehemu-ya-9-kitabu-cha-zaburi/
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 11 (Mithali, Wimbo ulio bora, Mhubiri)
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.
Mwanazuoni ni mtu gani kibiblia?
NA TAA YA MUNGU ILIKUWA BADO HAIJAZIMIKA
JINSI YA KUPIGANA MAOMBI YA VITA.
MASOMO MAALUMU KWA WANAWAKE.
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
Neno hili limetajwa mara moja katika biblia, kwenye kitabu cha;
Matendo 1:12 “Kisha wakarudi kwenda Yerusalemu kutoka mlima ulioitwa wa Mizeituni, ulio karibu na Yerusalemu, wapata mwendo wa sabato”.
Ni mwendo ambao ulitengwa maalumu wa mtu kusafiri siku ya sabato, ambao urefu wake ulikuwa ni dhiraa elfu mbili (2000), ambao ni sawa na Kilometa moja kwa makadirio.
Kutoka mlima wa mizetuni mpaka mjini Yerusalemu, ni umbali uliokuwa ndani ya hiyo kilometa moja, ndio huo walisafiri mitume wa Bwana siku hiyo.
Lakini Je! Agizo hilo tunalipata wapi katika agano la kale?
Hakuna andiko la moja kwa moja katika torati ya Musa linaloeleza kuwa mwendo wa sabato, ulipaswa uwe ndani ya hizo dhiraa elfu mbili. Bali Marabi wa kiyahudi baadaye walidhani hivyo kulingana na uhalisia wa maandiko haya.
Kutoka 16:29 “Angalieni, kwa kuwa Bwana amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba
Kwamba anaposema Usiondoke mahali pako, anamaanisha ndani ya mipaka ya mji wako, hii ikiwa na maana ukiwa ndani ya mipaka uliruhusiwa kutembea, utakavyo. Na kama ikitokea unatoka, basi hupaswi kusafiri Zaidi ya hizo dhiraa elfu 2000.
Na hiyo waliirithi kufuatana na sheria ya malisho ya nje ya mji ambayo walipewa walawi katika..
Hesabu 35:4 “Na yale malisho ya miji mtakayowapa Walawi, ukubwa wake utakuwa tangu ukuta wa mji kupima kiasi cha dhiraa elfu pande zote. 5 Nanyi mtapima hapo nje ya mji upande wa mashariki dhiraa elfu mbili, na upande wa kusini dhiraa elfu mbili, na upande wa magharibi dhiraa elfu mbili, na upande wa kaskazini dhiraa elfu mbili, huo mji ulio katikati. Hayo ndiyo yatakayokuwa kwao malisho ya miji”.
Hivyo kwa kurejea sheria hizo, wakahitimisha kuwa mwendo wa mtu kusafiri nje ya mji siku ya sabato ni hizo dhiraa elfu mbili(2000) au kilometa moja . Ndio Wakauita mwendo wa Sabato. Lakini hakukuwa na sheria ya moja kwa moja inayoeleza mwendo huo ulipaswa uwe katika vipimo hivyo.
Lengo la kufanya vile ni kuwafanya watu wasitawanyike mbali na eneo la kuabudia, ndani ya mji, siku hiyo ya Bwana.
Hata sasa. Ni lazima Kila mmoja wetu awe na mwendo wake wa sabato katika siku ya Bwana..kumbuka jumapili ni siku ya Bwana, hupaswi kwenda mbali na uwepo wa Mungu, siku hiyo sio siku ya kufanya biashara, sio siku ya kwenda kwenye mihangaiko isiyokuwa na lazima, Bali ni siku maalumu Kwa ajili ya ibada..penda kuwepo kanisani, mikutanoni, kwenye semina, kwenye mafundisho redioni,mitandaoni, kwenye vitabu vya kiroho.n.k.
Shalom
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
IMESALIA RAHA YA SABATO KWA WATU WA MUNGU.
Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
EPUKA KUCHELEWA IBADA.
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?
NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?
Je ni kweli Yesu peke yake ndiye aliyepaa mbinguni, na Eliya hakupaa wala Henoko? Kulingana na Yohana 3:13?
Jibu: Tusome,
Yohana 3:13 “Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”
Mstari huu lengo lake si kutoa taarifa za waliopaa mbinguni au ambao hawajapaa!, tukiusoma kwa lengo hilo basi ni rahisi kuchanganyikiwa, na kuona biblia inajichanganya…
Mfano mtu anaweza kusikika akitoa kauli hii “hakuna mtu aliyewahi kuja kwangu kunitazama, isipokuwa mtoto wangu tu”.. Kauli hiyo mtu asipojua kwanini imezungumzwa vile, anaweza kutafsiri kuwa “hakuna mtu yeyote aliyewahi kufika nyumbani kwake huyo ndugu, iwe mgeni au mwenyeji, isipokuwa mtoto wake tu…..maana yake anaishi tu peke yake peke yake, au nyumba yake ipo mafichoni mahali ambapo watu hawawezi kufika, au pengine amefunga mlango kwa wageni hivyo hakuna mtu yeyote anayeweza kumtembelea”…
Lakini kumbe hakumaanisha hivyo, yule aliyemsikia hakuanza kusikiliza mwanzo wa maneno yake bali alichukua kipande cha mwisho cha maneno yake… lakini kumbe maneno yake hasa yalianza hivi….. “Tangu nilipoanza kuugua, mpaka nilipopona hakuna mtu aliyewahi kuja kwangu kunitazama isipokuwa mtoto wangu tu “
Na kauli ya Bwana Yesu, aliposema hakuna aliyepaa juu ila aliyeshuka, ina mantiki hiyo hiyo…
Sasa Ili tuelewe vizuri, tuanzie kusoma mstari ule wa 12.
Yohana 3:12 “Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? 13 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”
Yohana 3:12 “Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni?
13 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”
Hapa tunaona ni Bwana Yesu anampa Nikodemu taarifa kuwa “yeye pekee ndio mwenye taarifa za mbinguni, yaani siri za ufalme wa mbinguni” asizozijua mtu mwingine yeyote.
Na kwanini siri hizo anazo yeye tu peke yake?, na si mwingine yeyote?..Kwasababu ni yeye tu pekee ndiye aliyetokea mbinguni, wengine wote asili yao ni hapa duniani, hivyo hawawezi kujua mambo ya mbinguni wala siri za ndani za mbinguni, kwasababu hawakutokea huko. Lakini Yesu asili yake sio duniani..yeye alikuwepo mbinguni kabla hajazaliwa na Mariamu.
Nabii Eliya alipaa mbinguni lakini hakutokea mbinguni, hivyo hawezi kuyajua ya mbinguni, kwasababu asili yake ni duniani, yeye alizaliwa hapa duniani kama wanadamu wengine wote, mbinguni alienda kama tu sehemu ya mwaliko.. Kama sisi tutakavyoalikwa siku ile ya mwisho ya parapanda.. Tutaenda kama wageni waalikwa, lakini Kristo si mgeni mwalikwa bali Mwalikaji/naye ni mwenyeji.
Ni sawa na Mtoto wa mfalme wa Taifa fulani, aje aishi Tanzania na baada ya muda arejee nchini mwake, halafu kuna kijana mwingine raia wa Tanzania, mzaliwa wa Tanzania apewe mwaliko wa kwenda kuishi Huko kwenye huo ufalme, kipindi chote cha maisha yake.. Je huyu kijana aliyealikwa anaweza kuwa sawa na yule kijana aliye mwana wa Mfalme?.. Au watakuwa na uelewa sawa kuhusiana na mambo ya huo ufalme?.
Jibu ni la! Ni wazi kuwa Huyu kijana wa Mfalme atakuwa anajua siri nyingi za Taifa lake, kuliko huyu kijana aliyealikwa, kwasababu ni mzaliwa wa kule, na zaidi sana ni mwana wa mfalme, lakini huyu aliyealikwa hatajua sana mambo ya ufalme ule, kwasababu yeye ni kama mwalikwa tu.
Ni hivyo hivyo kwa Eliya na Henoko.. Hao ni waalikwa tu mbinguni, lakini hawakuwa wenyeji wa kule,
Lakini Yesu ni Mwalika, na tena ni mfalme.. hivyo Kristo pekee ndiye ajuaye mambo yote ya mbinguni, siri zote za Ufalme wa mbinguni, kwasababu yeye ni mwana wa Mfalme na pia asili yake ni kwenye huo ufalme.
Ndio maana sasa biblia inasema hapo… “Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, wala hamsadiki, mtasadiki wapi niwaambiapo mambo ya mbinguni? Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu”.
Maana yake hakuna mtu aliepaa mbinguni kwenda kuzichukua siri na kutujuza sisi, isipokuwa Yule aliyeshuka kutoka kule, ambaye ni Yesu Kristo mwenyewe, Mwana wa Adamu.
Maran atha.
Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
MJUE SANA YESU KRISTO.
Ni kweli hakuna mtu aliyewahi kuuona uso wa Mungu Zaidi ya Bwana Yesu?
Uishi kwa furaha pamoja na mke umpendaye, siku zote
Mithali 17:16 “Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?”.. Hili andiko lina maana gani?
Mithali 17:16 “Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?”..
Hili andiko lina maana gani?
Jibu: Awali ni vizuri kufahamu hekima inayozungumziwa hapo ni hekima gani?
Hekima inayozungumziwa hapo si hekima ya ki Mungu, kwasababu hekima ya Mungu haipatikani kwa fedha…bali hekima inayozungumziwa hapo ni ile ya kiulimwengu, ambayo hiyo inaweza kupatikana kutoka kwa watu,na kwa njia ya kununuliwa (kwa njia ya kwenda katika shule za wenye hekima)…ambapo mtu atalipa kiasi fulani cha Ada na kisha kufundishwa hiyo hekima.
Mfano wa shule za hekima, ni hizi tulizonazo sasa, ambapo mtu atajiunga na shule fulani na kwenda kupewa Maarifa katika eneo fulani la maisha, ambayo yatamfanya aishi vizuri na kupata mafanikio katika maisha.
Kwahiyo hapo biblia iliposema… “Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mkononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?”
Tafsiri yake kwa lugha nyepesi ni hii………. “ina maana gani mpumbavu kuwa na fedha ya kulipia elimu yake na ikiwa hana Moyo wala Nia ya kuipata hiyo hekima?”
Ni jambo ambalo kweli halina Maana,…kwasababu hata akienda kutafuta kuinunua hiyo hekima hataipata kwasababu moyo wake haupo huko, hivyo ataenda kupoteza fedha tu…
Andiko hili linatufundisha umuhimu wa kufanya kitu kwa moyo (iwe cha kimwili Au cha kiroho)… Kama hujanuia kufanya kitu kwa moyo basi ni heri usikifanye kabisa kwasababu ni sawa na kupoteza muda au fedha.
Kwanini maombi kwa Marehemu si sahihi kibiblia?
“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama
TAFUTA HEKIMA, MAARIFA, UFAHAMU NA BUSARA.
Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?
WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE
Je Bwana Yesu alimtokea Yuda baada ya kufufuka kwake?.. maana tunasoma katika 1Wakorintho 15:5 kuwa aliwatokea wale Thenashara ambao mmojawao alikuwa ni Yuda.
Jibu: Kwanza ni muhimu kujua maana ya Neno “Thenashara”.. Tafsiri ya Thenashara ni “kumi na mbili”. Maana yake popote biblia inapotaja neno hilo, iliwalenga wale Mitume 12 wa Bwana Yesu.
Na katika kipindi cha huduma ya Bwana Yesu, Yule Yuda aliyemsaliti alikuwa miongoni mwa hao Thenashara. Lakini tunaona baada ya kufa walibaki Mitume 11 tu..na kipindi Bwana Yesu anafufuka Yuda tayari alikuwa ni Marehemu kwani alijinyonga kabla hata ya Bwana kufufuka, hivyo hakuuona ufufuo wa Bwana, Lakini tukienda mbele katika kitabu cha 1Wakorintho 15:3 tunasoma kuwa Bwana aliwatokea wote 12.. Je ni kwamba biblia inajichanganya au la?
Tusome..
1Wakorintho 15:3 “Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 5 na ya kuwa alimtokea Kefa; TENA NA WALE THENASHARA; 6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala”
1Wakorintho 15:3 “Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;
4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;
5 na ya kuwa alimtokea Kefa; TENA NA WALE THENASHARA;
6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala”
Ni kweli Bwana aliwatokea wale Thenashara (yaani Mitume 12), lakini Yule wa 12 hakuwa Yuda kwasababu biblia inasema nafasi yake ilichukuliwa na mtu mwingine aliyeitwa Mathiya.
Tusome.
Matendo 1:23 “Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. 24 Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, 25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye AKAHESABIWA KUWA PAMOJA NA MITUME KUMI NA MMOJA”
Matendo 1:23 “Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. 24 Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili,
25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye AKAHESABIWA KUWA PAMOJA NA MITUME KUMI NA MMOJA”
Hapo anasema Mathiya akahesabiwa kuwa pamoja na Mitume 11, maana yake yeye alikuwa wa 12. Kwahiyo Mathiya alihesabika miongoni mwa Thenashara, na ndio maana hapo katika 1Wakorintho 15:5 Mtume Paulo kataja kumi na Mbili, lakini Yule wa 12 hakumlenga Yuda bali Mathiya.
Thenashara ni nini? (Marko3:16)
Je ni halali kupiga kura kanisani kuchagua viongozi?
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?
Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?
Jibu: Katika biblia hakuna mahali popote panapoonyesha marehemu waliombewa..isipokuwa katika sehemu moja tu inaonyesha Marehemu mmoja aliyekuwepo katika mateso ya kuzimu aliomba ndugu zake walio hai wakahubiriwe injili ili wasife katika dhambi na kwenda kule aliko, lakini tunaona maombi yake hayo hayakuwa na matokeo yoyote.Hebu tuisome hiyo habari..
Luka 16:27 “Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu,28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso.29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao.30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu.31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishiwa hata na mtu akifufuka katika wafu”
Umeona?..Huyu Tajiri alijaribu kuwaombea watu walio hai wasifike alipo lakini maombi yake yalizuiliwa, halikadhalika Sisi tulio hai hatuwezi kuwaombea watu waliokufa kwamba watolewe katika mateso ya kuzimu.
Kama kuna maombi ya kuwaombea wafu watoke katika mateso ya kuzimu na kuingia paradiso, basi vile vile yatakuwepo pia maombi au sala za kuwatoa watu peponi na kuwapeleka kuzimu.. Lakini kama hakuna maombi ya mtu kumtoa mtu peponi(yaani paradiso) na kumpeleka kuzimu…vile vile hakuna maombi yoyote ya kuweza kumtoa mtu kuzimu na kumpeleka peponi.
Utasema tunazidi kulithibitisha vipi hilo kimaandiko?
Hebu tuzidi kuisoma hiyo habari ya Tajiri na Lazaro…Tuangalie maombi mengine aliyoomba kuhusiana na yeye kutolewa kule.
Luka 16:23 “Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu.24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa.26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ILI WALE WATAKAO KUTOKA HUKU KWENDA KWENU WASIWEZE; WALA WATU WA KWENU WASIVUKE KUJA KWETU”.
Hapo mwisho anasema..kati Yao (hao walio kuzimu na walio peponi)..KUMEWEKWA SHIMO KUBWA kama mpaka, ili walio kuzimu wasiweze kuvuka kuingia peponi na walio peponi wasivuke kwenda kuzimu..Ikiwa na maana kuwa hakuna mwingiliano wowote wa walio kuzimu na walio peponi..Hilo shimo katikati yao lipo mpaka sasa.
Hivyo kwa hitimisho, maombi ya kuwaombea heri Marehemu au kuwaombea wapunguziwe adhabu ni maombi yasiyo ya kimaandiko na hayana matokeo yoyote… Vile vile sala za kuwaomba watakatifu waliofariki watuombee halipo kimaandiko.
Ni vizuri kutengeneza maisha yetu hapa duniani kabla ya kufa, kwa kumwamini Bwana Yesu na kutubu dhambi, kwasababu tukishakufa hakutakuwa na nafasi nyingine ya pili.
Yohana 8:24 “Kwa hiyo naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu”.Bwana atusaidie.
Je sisi wakristo tunaruhusiwa kufanya 40 za marehemu?
MATESO YA KUZIMU.
KUNA AINA NGAPI ZA MAOMBI?
USIRUHUSU INZI WATUE JUU YA ROHO YAKO.
Jibu: Kushuhudia kunatokana na neno “Ushuhuda”. Mtu anayetoa taarifa ya jambo fulani alilolishuhudia au aliloshuhudiwa basi hapo anatoa ushuhuda.
Kwamfano mtu anaweza kuona ajali ya gari na akaenda kuwaelezea watu wengine tukio zima jinsi lilivyokuwa, hapo ni sawa na ametoa ushuhuda au amewashuhudia watu ajali ile.
Vile vile katika Ukristo, mtu anayewaelezea wengine mambo aliyoyaona au kuyasikia kumhusu Yesu…yani wema wake aliomtendea, au aliowatendea watu wengine, hapo ni sawa na kusema anawatolea ushuhuda au anawashuhudia wengine habari za Yesu.
Lakini tukija katika neno “Kuhubiri”…lenyewe ni neno pana linalojumuisha kushuhudia, kufundisha, kuonya, na kutoa maoni.
Kwamfano mtu aliyeshuhidia tukio la ajali ya gari na akaenda kulielezea/kulishuhudia kwa watu.. na baada ya hapo akaanza kutoa mafundisho na tahadhari kuhusiana na ajali kama hizo na jinsi ya kuziepuka..mtu huyo anakuwa ameihubiri ile habari za ajali.
Vile vile mtu anayeenda kutoa ushuhuda wa wema wa Yesu na habari za kufa na kufufuka kwake na mwishoni akaanza kuelezea faida za kumpokea Yesu, na hasara za kutompokea…ni nini Yesu anataka na nini hakitaki…Mtu huyo anakuwa amevuka kutoka hatua ya kushuhudia mpaka ya kuhubiri.Na sisi kama wakristo ni lazima tuzishuhudie habari za Yesu na pia tuzihubiri
2 Timotheo 4:5 “Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako”
Je kauli ya Bwana Yesu inajichanganya? Katika Yohana 8:14 na Yohana 5:31?
UTARATIBU WA KUTOA FUNGU LA 10 UPOJE?.
KUOTA AJALI, KUNAMAANISHA NINI?
Je! Mungu anasababisha ajali au Majanga?
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?