Title September 2019

Je! sisi kama watakatifu tunaowezo wa kuamuru hukumu?

SWALI: Tumeambiwa sisi (Watakatifu) tutahukumu, Je! baada ya kuhukumu tutaweza kuwaamurisha malaika wawachukue wale tuliowahukumu na kuwatupa kwenye ziwa la moto?


JIBU: Ubarikiwe kwa swali zuri, lakini kuna jambo la kujifunza zaidi hapo, siku ile tutakapoketi na Bwana kuhukumu, sisi ndio tutafanana na yeye lakini hukumu ya mwisho atatoa yeye peke yake YESU KRISTO. Sisi tutakuwa kama mawakili. Kwa mfano siku ile atasimamishwa mtu aliyekuwa anafanya uasherati, na huku anasema ameokoka, na Bwana atamwuliza kwanini ulikuwa unafanya vile, labda atasema kwasababu kizazi chetu kilikuwa na simu zenye internet hivyo ilikuwa ni ngumu kujizuia, sasa utaitwa wewe Michael ambaye saa hiyo utakuwa pembezoni mwa Bwana, na Bwana atakuuliza ilikuwaje wewe uliushinda uasherati katika kizazi cha internet, utatoa sababu pale, sasa zile sababu zako utakazozitoa wewe mtakatifu ndizo zitakazo muhukumu yule mkosaji Unakumbuka yale maneno Bwana Yesu aliyoyasema katika..

Mathayo 12:41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.

42 Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani”.

Kwa namna hiyo ya malkia wa sheba atakavyokihukumu kizazi kile, ndivyo na sisi tutakavyokihukumu kizazi hichi.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

JE NI KWELI TUTAWAHUKUMU MALAIKA? SAWASAWA NA 1WAKORINTHO 6:2

HUDUMU YA MALAIKA WATAKATIFU.

KUNDI LA MALAIKA WALETAO MABAYA.

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.

JE! BAADA YA ULIMWENGU HUU KUISHA MALAIKA WATAKUWA NA KAZI GANI TENA?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.

SWALI: Yesu alikuwa na maana gani alipomwambia yule Mama kwamba chakula cha watoto hawapewi mbwa?

JIBU: Tusome,

Mathayo 15: 21 “Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni.
22 Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
27 Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani pa bwana zao.
28 Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile”.

Kumbuka Bwana Yesu alipokuja duniani, hakutumwa kwanza kwa watu wa mataifa, hapana kwasababu wao hawakuwa wanamtazamia mwokozi yeyote, kadhalika watu wa mataifa walikuwa ni watu wasiokuwa ni dini, wapagani, wasiomjua Mungu, walikuwa wanaabudu miungu,na ndio maana Bwana akawafananisha na mbwa katika mfano huo…

Lakini wayahudi ni watu wa Mungu tangu zamani uzao wa Ibrahimu, pamoja na hayo kwa miaka mingi walikuwa wanalitazamia taraja la wokovu wao ambalo lingeletwa tu na MASIHI mwenyewe atakayeshuka kutoka mbinguni, Hivyo kwa kuwa wale ni uzao wa Mungu, uzao wa Ibrahimu, sasa ulipofika wakati wa Mungu kuwatimizia haja yao waliyokuwa wanaisubiria kwa muda mrefu, ndio akamleta Bwana Yesu duniani aje kuwakomboa..

Na ndio maana sasa tunamwona Bwana Yesu alipokuwa duniani, hakuhubiri katika nchi yoyote ya mataifa, kadhalika hakuwatuma hata wanafunzi wake katika mji au kijiji chochote cha mataifa, kwasababu hakutumwa kwao, bali kwa wale waliomtazamia (yaani wayahudi).

Lakini hapa tunamwona huyu mwanamke ambaye ni mtu wa Tiro, (mwanamke aliyekuwa wa kimataifa), asiyekuwa na dini wala Imani katika Mungu wa kweli, alipomwona Bwana akipita kando kando ya miji yao, akamfuata ili ahudumiwe naye, lakini Bwana hakuonyesha kumjali kwa namna yoyote ile, lakini kwa vile alivyokuwa akimsumbua sumbua, ndipo Bwana akamwambia sikutumwa [kwa watu wa mataifa] ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (yaani wayahudi)..lakini alipozidi kumsumbua sumbua, aliongezea na kumwambia “si vema kutwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa”..yaani akiwa na maana kuwa si vizuri kuiondoa ile neema ya wokovu kwa wale waliostahili kuipokea(yaani wayahudi) na kuwapatia watu ambao hawakustahili kuipokea au kuitazamia(watu wa mataifa).

Lakini pamoja na hayo tunakuja kuona baadaye, ile neema ililetwa kwetu sisi mataifa, baada ya wale ambao waliostahili kuipokea kuikataa, hivyo sisi sasa sio mbwa tena bali tumefanywa kuwa wana wa Mungu kwa damu ya Yesu Kristo.

Hiyo ndio siri iliyokuwa imefichwa tangu zamani kwamba sisi watu wa mataifa tumehesabiwa kuwa warithi wa wokovu sawa na wayahudi kwa njia ya Yesu Kristo. Haleluya. Hivyo ndio maana Mtume Paulo akasema katika..

Waefeso 3: 4 “Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.
5 Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
6 ya kwamba MATAIFA NI WARITHI PAMOJA NASI WA URITHI MMOJA, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;”

Hivyo somo la kujifunza, hapo ni lipi?. Tumwendeapo Mungu, kwa haja ihusuyo wokovu wetu, hata kama ni kweli tutakuwa hatustahili mbele za Mungu, pengine njia zetu zimekuwa mbaya sana, na tumeomba mara ya kwanza, na ya pili na ya tatu hatujajibiwa…Hatupaswi kukataa tamaa, tuzidi kuomba tuzidi kuomba kama yule mwanamke..Kwasababu Bwana Yesu alishatupa mfano unaofanana na huo, juu ya yule kadhi dhalimu, aliyekuwa hamchi Mungu, lakini yule mwanamke mjane alivyomwendea mara ya kwanza hakupewa haki yake, lakini kwa jinsi alivyokuwa akimwendea endea mara kwa mara, alimpatia haki yake, japo hamchi Mungu, ili asije akamsumbua daima…(Luka 18:1-8)

Vivyo hivyo na sisi tusiache kumwomba Mungu neema ya wokovu, neema ya uponyaji, mahitaji binafsi, hata kama hatutaona dalili zozote za kujibiwa maombi yetu. Kwasababu Mungu anapendezwa na mtu aombaye kwa bidii.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

JINSI YA KUITUMIA VYEMA NEEMA YA MUNGU ILIYO JUU YANGU.

MPAKA UTIMILIFU WA MATAIFA UTAKAPOWASILI.

MADHARA YA KUUPIZIA MAAGIZO YA MSINGI MUNGU ANAYOKUPA.

NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?

CHANZO CHA MAMBO.

MAVAZI YAPASAYO.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! sheria ilikuwaje dhaifu kwasababu ya mwili? (Warumi 8:3)

Warumi 8:3 “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili”;


JIBU: Sheria peke yake haiwezi kuondoa dhambi ndani ya mtu, kwamfano Mungu alipotoa amri usizini, Ni kweli wengi waliijitahidi kuishika kwa kutokuzini kabisa maisha yao yote mpaka kifo, lakini ukweli ni kwamba ile tamaa ya kutamani kuzini ilikuwepo ndani yao. Walijizuia vile ni kwasababu sheria ilisema hivyo, lakini sio kwamba ilitoka moyoni mwao kabisa kuchukia uasherati, Na ndio maana sheria hapo inaonekana kuwa dhaifu, kwasababu yenyewe kama yenyewe haiwezi kuondoa dhambi, bali ni kama inazuia tu kwa muda… wanaitumikisha miili kwa nguvu hata hivyo haisaidii kuondoa tamaa za mwili.

Lakini sheria ya Roho wa Mungu huondoa dhambi ndani ya moyo wa mtu kabisa, pale mtu anapozaliwa mara ya pili, ile kiu ya kutamani dhambi Mungu anaiua mwenyewe ndani ya mtu, hivyo mtu wa namna hiyo hata kama Mungu asingesema usizini, yeye mwenyewe kwa kuwa mafuta ya Roho wa Mungu yanakaa ndani yake, ataona kuwa kile kitendo ni kibaya, kadhalika kutamani nako ataona ni kubaya, kumchukia ndugu ni kubaya n.k….unaona hapo, utagundua kuwa zile sheria zote za Mungu zinatimilika zenyewe ndani ya moyo wa Mungu bila hata shuruti.

Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.

Na ndio maana Bwana Yesu alisema, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Mtu hawezi kushinda dhambi kwa nguvu zake mwenyewe, nje ya Roho Mtakatifu. Wapo wanasema zishike amri kumi tu, basi inatosha kumpendeza Mungu…Lakini hawajui kuwa wapo wayahudi waliozikisha vizuri Zaidi ya wao lakini bado wakawa wanajiona kuwa hawana uzima ndani yao. Ni kwasababu gani?. Kwasababu sheria wanaishika kwa njia ya mwili lakini sio kwa njia ya Roho.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

UTIMILIFU WA TORATI.

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

UFALME WA MUNGU HAUPATIKANI KIRAHISI.

UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

JINSI ITAKAVYOKUWA KATIKA SIKU ILE

FUVU LA KICHWA.

ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.

 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Mungu anasababisha ajali au Majanga?

SWALI: Je! Mungu anasababisha ajali au majanga, kwamfano ajali ya kivuko cha MV Nyerere kuzama?


JIBU: Mungu hasababishi ajali yoyote ile, japo Mungu anaweza akamwadhibu mtu kwa makosa yake. Shetani ndiye mwenye lengo siku zote la kuangamiza hata wakati ambapo mtu hana makosa, kama alivyofanya kwa Ayubu, kwasababu biblia inasema yeye alikuwa ni muuaji tangu mwanzo.(Yohana 8:44).

Asilimia kubwa ya ajali na majanga yanaletwa na shetani. Na pia biblia inasema yapo majanga mengine yanaletwa na Mungu mwenyewe, na mpaka imefikia hivyo ujue ni adhabu kutokana na makosa ya watu wenyewe, na pia Bwana anasema huwa hafanyi jambo lolote bila kuwafunuliwa hao watumishi wake manabii, kuwaonya kama tunavyoona alivyofanya kwa watu wa Ninawi.

Leo hii mtu anamuudhi Mungu labda ni muuaji, lakini kabla Mungu hajamwadhibu atamwonya pengine kwa kumtumia Mtumishi wa Mungu au kwa kusikia mahubiri, na akajua kabisa Mungu anamwonya atubu utakuta pengine alisikia Neno likisema “Uaye kwa upanga, atauawa kwa upanga”..

Lakini yeye akapuuzia na kuendelea na tabia yake ya kuuiba na kuua watu pasipo hatia.. Sasa mtu kama huyo inatokea mazingira labda siku moja amekutana na kundi la wanyang’anyi usiku, na kwa bahati mbaya wakamvamia na kumchoma kisu, kisha na kufa..Sasa kwa nje unaweza ukasema ni shetani lakini sio shetani bali ni Mungu mwenyewe kamlipizia kisasi juu yake.

Hivyo zipo ajali zinazotoka kwa Mungu mwenyewe. Kadhalika zipo pia zinazotengenezwa na shetani, ambazo hizo ndio nyingi kuliko zile zinazotoka kwa Mungu.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

NI NANI ANAYETAWALA DUNIA KATI YA MUNGU NA SHETANI?

KWANINI MUNGU ANARUHUSU WATU WAPITIE SHIDA?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA JIKANE MWENYEWE?

JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?

MPENDEZE MUNGU ZAIDI.

Jehanamu ni nini?

RAHABU.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Paulo hakumsamehe Marko, pindi walipotaka kwenda tena kazini?

Matendo 15:37 ″Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao.

38 Bali Paulo HAKUONA VEMA kumchukua huyo aliyewaacha huko pamfilia,asiende nao kazini.

39 Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana….”

JIBU: Ukisoma kitabu cha Matendo 13:13 utaona Yohana, aliwaacha wakina Paulo na Barnaba huko Pamfilia, inaonekana aliogopa dhiki itakayokwenda kuwakuta mbeleni, kwasababu Paulo bado mzigo wa kupeleka injili duniani kote alikuwa nao, hivyo walipomsihi waende pamoja alikataa, lakini sasa baadaye tunakuja kumwona tena akikutana na mtume Paulo na Barnaba na kutaka kujumuika nao katika kwenda kuipeleka injili, na ndio hapo tunaona mtume Paulo hakukubali jambo hilo kwasababu kama alishindwa kuandamana nao wakati wa tabu za awali,

kadhalika hataweza kushikamana nao katika dhiki zinazofuata, hivyo sio kwamba Paulo hakumsamehe, alimsamehe lakini hakutaka kuambatana naye tena ili asiwe kikwazo cha injili kwenda mbele.

Ni mfano tunaopaswa tujifunze na sisi [watumishi wa Mungu], kazi ya Mungu si ya kuifanya kirafiki tu, hapana bali wale watakaoitenda kazi kiuaminifu ndio tuambatane nao na kuwatambua hata kama watakuwa si watu wetu wa karibu sana. Lakini ikiwa ni ndugu halafu anaipuuzia kazi ya Mungu, hapo ni kumweka kando, Biblia ilishasema

Wafilipi 2:12 “…utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu”

Mungu akubariki.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP

Mada zinazoendana:

Paulo alikuwa na maana gani aliposema “nimeaminiwa uwakili”

DHAMBI YA MAUTI

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

KWANINI PALE BWANA ALICHUKUA HATUA YA KUMSAMEHE DHAMBI KWANZA KABLA YA KUMPONYA YULE MTU MWENYE KUPOOZA?.

UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

AGIZO LA UTUME.

USIPIGE MATEKE MCHOKOO!


Rudi Nyumbani:

Print this post

BWANA ailaze roho ya marehemu mahali pema PEPONI.

SWALI: Ni sahihi kwa Mkristo mtakatifu kumwambia BWANA ailaze roho ya mtu aliyekufa mahali pema PEPONI?


JIBU: Sio sahihi, kwasababu ameshakufa. Tumepewa amri ya kuombeana sisi kwa sisi, yaani tunapokuwa tunaishi hapa duniani, baada ya kufa hatujapewa amri ya kuombeana. Hakuna maombi yoyote yanayoweza kubadilisha hatima ya mtu aliyekufa, kilichobakia kwa mtu aliyekufa ni hukumu tu! (Waebrania 9:27).

Mazishi ya watu wasioamini ni tofauti na mazishi ya watu waliomwamini BWANA wetu Yesu Kristo, wasiomwamini wao hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na mambo yatakayofuata baada ya kifo, ndio maana wanasema maneno hayo, lakini sisi tulioamini ndio tunaoelewa kwamba kama ndugu yetu amekufa katika Bwana, basi tunalo tumaini la kukufuka tena kwasababu ni kama amelala tu!.. Lakini kama mtu amekufa katika dhambi na hakumpokea Kristo basi huyo hana tumaini la uzima wa milele, hivyo hawezi kuokolewa kwa maombi yoyote yale. Kwasababu Bwana Yesu alitupa maagizo ya kuenenda ulimwenguni kote kuihubiri injili, AAMINIYE NA KUBATIZWA ATAOKOKA, hakutupa agizo la kuenenda ulimwenguni kote kuwaombea wafu waokoke au walazwe mahali pema peponi.

Kwahiyo saa ya wokovu ni sasa katika maisha haya, baada ya maisha haya ni hukumu.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

WALE WATAKATIFU WALIOFUFUKA NA BWANA YESU KWAO JE! WALIKUWA PEPONI AU WAPI?

KUNA UMUHIMU WOWOTE WA KUWEKA MSALABA MAKABURINI?

JE! NI SAHIHI KUWAOMBEA WAFU?

UFUFUO WA UZIMA NA WA HUKUMU.

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO?

 KUWAHUDUMIA MALAIKA PASIPO KUJUA.


Rudi Nyumbani:

Print this post

“Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU”(Yohana12:32).

SWALI: Nini maana ya haya maandiko “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU”(Yohana12:32)?.

JIBU: Tunaona wana wa Israeli baada ya kumkosa Mungu kule jangwani, Bwana aliwapiga kwa pigo la nyoka wa moto, na ndipo Musa akaambiwa atengeneze nyoka wa shaba na kumwinua juu ya nchi, ili kila amtazamaye apate kupona. Sasa Bwana wetu Yesu Kristo alifananishwa na yule nyoka wa shaba juu ya ule mti, kwamba na yeye aliinuliwa juu (Pale Kalvari) ili kila amtazamaye (kwa macho ya rohoni na kumwamini) apate uzima wa milele, na ndio maana alisema katika…

Yohana 3:14 ” Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.”

Kwahiyo hapo Bwana aliposema “Nami nikiinuliwa juu ya nchi,NITAWAVUTA WOTE KWANGU” alimaanisha kuwa “baada ya kusulibiwa pale msalabani” kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu, itaachiliwa nguvu kubwa ya watu wengi kuvutwa kwake, na ndio maana ukiendelea kusoma mstari unaofuata utaona ameweka wazi kuwa kuinuliwa kunahusu mauti ya mwili wake..

Yohana 12:32 “Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
33 Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa”.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

MUNGU NDIYE ANAYEISHAWISHI MIOYO.

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

AYUBU 28 : HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?

MAJI YA UZIMA.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?

Kumbukumbu 23:24 Uingiapo katika shamba la mizabibu la jirani yako, utaweza kula zabibu za kukushibisha, kama upendavyo; ila usitie katika chombo chako. 25 Uingiapo katika mmea wa jirani yako waweza kuyapurura masuke kwa mkono wako; ila usisongeze mundu katika mmea wa jirani yako.

Kwa hio nikiingia katika shamba la jirani yangu, napaswa kula matunda na kushiba, bila, ila nisiweke katika kapu?


JIBU: Hapo unapaswa uelewe haizungumzii tu kuingia katika shamba la mtu mwingine wakati wowote unaojisikia wewe na kuanza kula kwasababu tu maandiko yamesema tule ila tusibebe chochote hapana!!.. Jambo kama hilo linakuja pale unapokuwa katika mazingira ambayo umeshikwa na njaa, na hauna chakula, na ukiangalia hauna chochote mfukoni kwa wakati huo, na mfano ukiendelea mbele katika hali hiyo unaweza ukazimia kwa njaa njiani…Sasa katika mazingira kama hayo hapo mbele za Mungu unaweza kuingia kwenye shamba la mwingine na kula pasipo kuhesabiwa hatia yoyote mbele za Mungu..isipokuwa usijifungashie mazao yake na kuondoka nayo.

Lakini pia jambo la kukumbuka ni hili, sheria hizo walipewa wayahudi , hivyo utamaduni kama huo ulikuwa kwa wayahudi tu peke yao, kwasababu hiyo basi ilikuwa hata mtu akimwona mgeni kaingia katika shamba lake kwa dharura na kuanza kula, hamfanyi chochote kwasababu anajua agizo la Mungu juu ya masuala kama hayo. Lakini kwa mazingira ya watu wa mataifa kama sisi tuliyopo, huwezi tu kuingia katika shamba la mtu asiyemjua Mungu na kuanza kula mazao yake pasipo hata idhini yake, vinginevyo itakuwa ni kujitafutia tu matatizo..Ni rahisi kuingia katika shamba la mtu wa imani moja na wewe(Ndugu yako katika Kristo) kuliko la mtu asiyemjua Mungu,cha msingi ni kutumia hekima ya kwenda kuomba. Na ukikatazwa ondoka utafute pengine.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

JE! NI VEMA KWA MKRISTO KWENDA HOSPITALI AU KUTUMIA MITI SHAMBA ANAPOUGUA?

KANUNI JUU YA KANUNI.

NAOMBA KUJUA WATAKAOENDA MBINGUNI JE! NI WENGI AU WACHACHE?

JE! KUNA DHAMBI KUBWA NA NDOGO?

JE! INAWEZEKANA MTU AKAWA ANAFANYA MIUJIZA NA KUTOA PEPO NA BADO ASINYAKULIWE?

JE! UNAMPENDA BWANA?


Rudi Nyumbani:

Print this post

Je kuna andiko linalomruhusu mwanamke kuwa sister?

JIBU: Nadhani utakuwa unazungumzia ma-sisters mfano tunaowaona katika  dini ya Kikatoliki. Ni wazi kuwa hakuna andiko lolote au mahali popote kwenye biblia linasema hivyo. Lakini mwanamke anaweza akajizuia asiolewe kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, biblia imesema hivyo katika

1Wakorintho 7: 34 “Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane”.

Hivyo mwanamke yeyote anayejizuia kuolewa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni, hafanyi vibaya kulingana na maandiko lakini amaanishe kweli kufanya hivyo vinginevyo kama atakuwa anaishi kwa kulipuka tamaa, basi atakuwa anajitafutia mwenyewe hukumu..

Pia lipo andiko lingine linasema..

1 Timotheo 4 :1 Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wenginewatajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani;

2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;

3WAKIWAZUIA WATU WASIOE, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.

Unaona hapo inasema “wakiwazuia”..ikiwa na maana kuwa wanahaja ya kuoa lakini wanalazimishwa kufanya hivyo kutokana labda na utaratibu wa dini zao au madhehebu yao..kwamba ili wapewe nafasi fulani inawapasa wawe hivyo…lakini haimaanishi kuwa mtu yeyote ambaye ametaka kumtumikia Mungu pasipo kuoa au kuolewa anakwenda kinyume na maandiko.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA.

MARIAMU

TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:

RABONI!

MKUMBUKE MKE WA LUTU.

MAANA YA KUISHI NA MKE KWA AKILI.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post

Yohana mbatizaji alibatizwa na nani?

JIBU: Biblia haijaeleza mahali popote ni nani aliyembatiza Yohana mbatizaji, lakini kwa hekima tunaweza kufahamu kuwa yeye naye alibatizwa kama alivyokuwa anawabatiza wengine, kwasababu ni sharti kwanza uwe kielelezo wa jambo ambalo unalifanya ndipo uwafundishe na wengine vinginevyo utakuwa ni mnafki, huwezi kuwatangazia watu uhuru wakati wewe mwenyewe bado upo vifungoni…

Lakini sasa swali linakuja ni nani aliyembatiza Yohana?..Jibu ni kwamba miongoni mwa watu aliwahubiria suala la ubatizo na kuamini, mmojawapo kati yao ndiye aliyembatiza Yohana. Kumbuka suala la ubatizo, halimtilii mkazo sana mbatizaji kama linavyomtilia yule anayebatizwa, nikiwa na maana kuwa mbele za Mungu yule anayebatizwa ndiye mwenye uwezo wa kuufanya ule ubatizo kuwa batili au la, na sio mbatizaji..Na ndio maana tunakuja kumwona Bwana Yesu, yeye hakustahili kubatizwa na Yohana kwasababu yeye ndiye mwenye haki kuliko yeye, lakini yeye alimwambia fanya hivyo kwa sasa, ni kwasababu gani? Ni kwasababu hakukuwa na mwenye haki Zaidi yake atakayeweza kufanya vile…

Vivyo hivyo,na kwa Yohana kwa kuwa hakukuwa na mtu mwingine aliyeupokea ufunuo ule, pengine aliwaambia wale wafuasi wake, wafanye hivi kwa sasa (yaani wambatize), ili atimize haki yote.

Mfano huo huo pia tunaweza kujifunza kwa Ibrahimu, Mungu alipompa ufunuo wa TOHARA kwa uzao wake wote, na Mungu akamwambia awatahiri watoto wake na watu wa nyumbani mwake,. Tunaona pia yeye naye hakujitenga kana kwamba haumuhusu hapana, bali yeye baada ya kuwatahiri watu wake, kadhalika yeye naye akatahiriwa na wao. soma

Mwanzo 17: 23 “Ibrahimu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Ibrahimu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.
24 Naye Ibrahimu alikuwa mwenye umri wa miaka tisini na kenda alipotahiriwa nyama ya govi lake.
25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake.
26 Siku ile ile akatahiriwa Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe”.

Unaona hapo sasa kwa mifano hiyo hiyo tunaweza kufahamu kuwa Yohana naye baada ya kumbatiza mmoja wa wafuasi wake, yeye naye akabatizwa na wao, ili haki yote itimizwe, Amen.

Ubarikiwe.

Ikiwa utahitaji msaada zaidi ya mafundisho ya kila siku/maombezi/ubatizo/ushauri basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618/+2557890001312

Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP


Mada zinazoendana:

NINI MAANA YA KIPAIMARA?..NA JE! NI JAMBO LA KIMAANDIKO?

NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.

LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.

AMIN! NAWAAMBIA KIZAZI HIKI HAKITAPITA

CHAGUA NI JIWE LIPI LITAKALO KUFAA KWA UJENZI.


 

Rudi Nyumbani:

Print this post