Je Sipora, mke wa Musa alikuwa Mkushi mwenye ngozi nyeusi?, Kulingana na Hesabu 12:1? Na ni kwanini Miriamu na Haruni wamkasirikie Musa kwa kumwoa mwanamke Mkushi?, na kama alikuwa Mkushi mbona maandiko sehemu nyingine yanasema Yethro baba yake Sipora alikuwa ni Mmidiani na sio Mkushi?.. Au je! Musa alikuwa na mke mwingine tofauti na Sipora?
Jibu: Hapana! Maandiko hayaonyeshi kuwa Musa alioa mwanamke mwingine zaidi ya Sipora.
Sasa ili tujue kama Sipora alikuwa Mkushi au hebu kwanza tusome mistari ifuatayo..
Hesabu 12:1 “Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. 2 Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. 3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”
Hesabu 12:1 “Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.
2 Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.
3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi”
Sasa Kushi lilikuwa ni Taifa gani?
Kushi ni taifa lijulikanalo kama Ethiopia kwasasa, Taifa hili lipo kaskazini mwa nchi ya Kenya, na kusini-mashariki mwa nchi ya Sudani. Wenyeji wa Taifa la Kushi(Ethiopia) ni watu wenye ngozi nyeusi tangu zamani za biblia na hata sasa. Tunalithibitisha hilo katika Yeremia 13:23.
Yeremia 13:23 “Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoa-doa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya”
Umeona?.. hapo inamtaja Mkushi pamoja na ngozi yake, kwamba haiwezi kubadilika.. Kwahiyo mpaka hapo tumeshajua ngozi ya Sipora ilikuwaje?.. kwamba ilikuwa ni ngozi ya Kikushi.
Sasa swali ni je! Kama alikuwa ni Mkushi, kwanini biblia iseme baba yake alikuwa ni Mmidiani, Taifa la mbali kabisa, lililopo Mashariki ya kati, tena lenye watu wenye ngozi ijulikanayo kama nyeupe?.. na zaidi sana hata Sipora mwenyewe Musa alimpatia akiwa huko huko Midiani na sio Kushi?.
Jibu ni kwamba Yethro, baba yake Sipora, alikuwa ni Mmidiani kwa kuzaliwa, lakini kwaasili hakuwa mmidiani bali alikuwa ni Mkushi.
Ni sawa na Mzungu,au Mchina, au Mhindi aliyezaliwa katika Taifa la Tanzania, akakulia Tanzania, akaishi na watanzania, akasoma shule za kitanzania, na hata lugha ya Kiswahili ya kitanzania akawa anaiongea.. kwa utambulisho wake ataitwa mtanzania, na atapata haki zote za kiraia…lakini kwa asili sio Mtanzania bali ni Mzungu, au Mchina au Mhindi.
Ndivyo alivyokuwa Yethro, baba yake Sipora, alikuwa ni Mkushi kwaasili lakini Mmidiani kiuraia..(au kwa lugha rahisi, ni kwamba alikuwa ni Mkushi ambaye hakuzaliwa Kushi bali Midiani).
Ni sawa na Musa kipindi anakutana na hao mabinti wa Yethro, walikwenda kumtaja mbele ya baba yao kama Mmisri, lakini kiuhalisia Musa hakuwa Mmisri, bali mwebrania… Hivyo walimwita Mmisri kwasababu huenda aliwaambia katokea Misri.. Jambo ambalo ni kweli, Musa alikuwa ni Mmisri, kwa kuzaliwa, na kiuraia lakini hakuwa mwenye asili ya waMisri.
Kutoka 2:15 “Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima. 16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao. 17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao. 18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo? 19 Wakasema, MMISRI MMOJA ALITUOKOA KATIKA MIKONO YA WACHUNGAJI, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi. 20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula. 21 Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora. 22 Huyo akamzalia mwana, akamwita jina lake Gershomu, maana alisema, Nimekuwa mgeni katika nchi ya ugeni”
Kutoka 2:15 “Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.
16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.
17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao.
18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo?
19 Wakasema, MMISRI MMOJA ALITUOKOA KATIKA MIKONO YA WACHUNGAJI, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.
20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula.
21 Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora.
22 Huyo akamzalia mwana, akamwita jina lake Gershomu, maana alisema, Nimekuwa mgeni katika nchi ya ugeni”
Swali lingine; Ni kwanini Miriamu na Haruni, wakamkasirikie Musa kwasababu ya Mwanamke, Mkushi aliyemwoa?.. Je ni kwasababu alikuwa mweusi? Na ngozi nyeusi imelaaniwa?.
Jibu ni La!.. Hawakumkasirikia Musa kwasababu ya Rangi ya mke wake!..kwamba alikuwa mweusi na wao hawaipendi ngozi nyeusi,… la! Hiyo haikuwa sababu….
Sababu iliyowafanya wakasirike, ni kwasababu Yule alikuwa ni mwanamke wa kimataifa…
Maana yake ni kwamba hata kama asingekuwa Mkushi, lakini ni Mmisri, bado wangemkasirikia… vivyo hivyo hata kama angekuwa ni mzungu Yule mwenye uso mweupe kuliko wote, bado Miriamu na Haruni wangenung’unika.. kwasababu wayahudi na mataifa hawachangamani(kuoana).. Na mataifa walikuwa ni watu wote, nje na Taifa la Israeli.
Sasa swali la mwisho.. Kwanini Musa amwoe mwanamke wa kimataifa, na ilihali anajua kabisa haitakiwi kuwa hivyo?
Musa alimpata Sipora kabla ya sheria. Na ilipokuja sheria kuwa si ruhusa wao kuoa wanawake wa kimataifa, tayari Musa alikuwa na Sipora, hivyo asingeweza kumwacha!!!… na kipindi Mungu anatoa hiyo sheria ya kutooa wanawake wa kimataifa, ndio hicho hicho kipindi ambacho Musa na Haruni walinyanyuka kumlaumu. Kabla ya hapo utaona hawakuongea chochote.
Ni nini tunajifunza hapo?
Kwanza tunajifunza kuwa biblia haijichanganyi ni fahamu zetu ndizo zinazojichanganya.. Pili tunajifunza kuwa si sawa kumwacha mke wako baada ya wewe kuokoka, hata kama huyo mwanamke ni mpagani kiasi gani, wala si sawa kumwacha mume wako baada ya wewe kuokoka hata kama huyo mwanaume ni mpagani kiasi gani.. Ndicho biblia inachotufunza pia katika…
1Wakorintho 7:12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. 13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu”
1Wakorintho 7:12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu”
Lakini hiyo pia haitupi ruhusa kuoa wanawake wa kipagani, ikiwa tumeshaokoka tayari na tunataka kuoa, vile vile haitoi ruhusa kuolewa na mwanaume wa kipagani kama bado hujaolewa na unataka kuoelewa..
Kama umeshaokoka, na umesimama na unataka kuoa/kuolewa.. ni sharti uolewe au uoe mtu mwenye imani moja na wewe, Bwana mmoja, roho mmoja, na Ubatizo mmoja. Ukienda kutafuta binti wa kidunia na kumwoa hapo utakuwa umejifunga nira na wasioamini, jinsi isivyo sawa(2Wakorintho 6:14)..na unafanya machukizo yale yale walioyafanya watu wa kipindi cha Nuhu, yaliyowasababishia kuangamizwa kwa gharika (kwani wana wa Mungu waliowaona binti za wanadamu, wakawatamani na kuwaoa).
Hizi ni siku za Mwisho, kama hujampokea Yesu, fahamu kuwa hata uwe na maarifa kiasi gani, bado utapotea tu!, hivyo wokovu ni lazima!, kama unapenda maisha.
Maran atha!
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Midiani ni nchi gani kwasasa?.
MKUMBUKE MKE WA LUTU.
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI.
MJUMBE ASIYEKUWA NA UJUMBE.
BWANA alimaanisha nini kwenye mstari huu Marko 2:21″ Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kukuu?
Rudi nyumbani
Print this post
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAENEO YA IBADA: Sehemu ya 2
EPUKA KUCHELEWA IBADA.
Jambo la kuchelewa ibada sio tu linamvunjia Mungu heshima yake, lakini pia linaweza kukupelekea mauti. Utajiuliza hili linawezekanikaje. Embu tufuatilie kisa hiki cha Anania na mkewe Safira, kisha tuone ni jambo lipo nyuma yake.
Matendo ya Mitume 5:1 “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, 2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. 3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu. 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. 6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika. 7 Hata MUDA WA SAA TATU BAADAYE MKEWE AKAINGIA, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. 8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. 9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe. 10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe. 11 Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya”.
Matendo ya Mitume 5:1 “Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali,
2 akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume.
3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja?
4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.
5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.
6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika.
7 Hata MUDA WA SAA TATU BAADAYE MKEWE AKAINGIA, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.
8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo.
9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.
10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.
11 Hofu nyingi ikawapata kanisa lote na watu wote walioyasikia haya”.
Katika habari hiyo tunaona mke wa Safira hakuwepo ibadani wakati ibada inaanza, alikuja kutokea SAA TATU baadaye. Hii ikiwa na maana kwamba kama ibada inaanza saa tatu kamili asubuhi yeye alifika saa sita mchana.. Na matokeo yake hakuelewa chochote kilichotokea kwamba tayari mume wake alishakufa saa nyingi na kuzikwa.
Tengeneza picha angekuwepo pale muda ule ule, ingekuwa rahisi yeye kutubu, alipomuona mume wake ameanguka na kufa, lakini hakuwepo, alidhani kama ilivyokuwa jana, ndivyo ilivyo na leo. Hata sasa wapo watu ambao Mungu anawaua kiroho, kwa kuiendekeza tabia hii. Hawapo kwenye vipengele vingi vya maombi, hawajua kuwa wakati mwingine Mungu anaachilia rehema, mwanzoni kabisa mwa ibada, lakini wao wanakosa halafu wanakuja baadaye kushiriki na wale wengine bila kutakaswa dhambi zao, mwisho wa siku wanapigwa na Mungu.
Ndugu zipo Baraka mtu anazozipata kila mwanzo na kila mwisho wa ibada, nilisiliza ushuhuda wa mpendwa mmoja, anasema alionyeshwa kuna malaika maalumu wanaogizwa na Bwana wasimame, kila mwanzo na kila mwisho wa ibada, kazi yao mahususi ni kutoa Baraka.
Hivyo mtu anapochelewa ibadani tayari ameshapoteza Baraka zake, na vilevile mtu anayeondoka kabla ya ibada kuisha jambo ni lile ile. Na ndivyo ilivyo wewe sio mgeni rasmi kwa Mungu..Mungu ndiye anayepaswa awe mgeni rasmi kwako, anatukuta tayari tupo ibadani tunamsubiria yeye. Mungu ni zaidi ya raisi, ni zaidi ya mfalme yeyote. Kama unakuwa mwaminifu na ratiba ya kazini kwako, ambayo inakupasa kila siku uwahi kuamka ufike, kwanini usiwahi ibadani, unachelewa bila sababu yoyote ya msingi?
Unapokosa, kipengele kimoja wapo, ni sawa na umekosa ibada nzima, hata 1000, haiwezi kuitwa elfu moja kama haijakamilika.. haijalishi utakuwa na kiwango cha 999.99 kinachoikaribia.. Kama senti moja itakosekana bado itaitwa tu mia tisa, na sio elfu moja.
Na ndivyo ilivyo ibada yoyote ya Mungu, kama, utakosa kile kipengele cha kwanza cha kufungua ibada, usidhani kuwa siku hiyo ulifanya ibada yoyote. Mungu anaona umepunguka. Anasema yeye ni alfa na omega, mwanzo na mwisho. Maana yake ni kuwa ili akamilike kwako ni lazima mwanzo wako uwe naye pia na mwisho wako.
Jijengee desturi nusu saa kabla ya ibada yoyote kuanza uwe umeshafika maeneo ya uweponi mwa Bwana. Kwa kufanya hivyo kamwe hutakaa uchelewe. Na utapokea Baraka nyingi badala ya laana.
Shalom.
KATAA KUWA EUTIKO, WA KUSINZIA IBADANI.
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
Nini maana ya “saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada?”
Ni muda gani Bwana Yesu alisulibiwa. Je! Ni saa 3 au saa 6?
Kwanini Mungu aseme “Alaaniwe azuiaye upanga wake usimwage damu” (Yeremia 48:10).
Je! Mtu ambaye hajaoa anaruhusiwa kulichunga kundi?
ALAMA ZA BENDERA YA ISRAELI ZINAWAKILISHA NINI?
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, WALA MTU ATAZAMAYE NYAKATI MBAYA, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu”.
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, WALA MTU ATAZAMAYE NYAKATI MBAYA, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu”.
Kutazama Nyakati mbaya kunakozungumziwa hapo ni “KWENDA KUTAFUTA SABABU YA ISHARA FULANI AMBAZO ZINAAMINIKA KUWA NI MBAYA”.. Mfano wa mtu akipishana na mbwa mweusi, au paka mweusi njiani au akimwona bundi juu ya bati lake, huwa inaaminika kuwa ni ishara mbaya au ya jambo fulani baya linalokuja.. Au mtu akijikwaa anaamini kuwa kuna mtu anamzungumzia vibaya…Hivyo mtu kama huyo unakuta anaenda kwa mganga, au kwa mnajimu, kutafuta maana ya ishara hiyo, au mbaya anayemfuatilia, sasa mtu huyo ndiye anayetafsirika kama “mtu atazamaye Nyakati mbaya”
Katika biblia Bwana Mungu aliwakataza wana wa Israeli, tabia ya kutazama nyakati mbaya. Kwasababu kwasababu ni imani potofu, ambayo inamwelekeza mtu kamwamini na kumwabudu shetani.
Kumbukumbu 18:13 “Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako. 14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Kumbukumbu 18:13 “Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.
14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Jambo hilo hilo Mungu analikataa hata sasa, kwasababu yeye ni Yule Yule jana na leo na hata milele (Waebrania 13:8).
Ukiwa ndani ya Kristo, viumbe na wanyama si kitu kwako, bundi na popo kwako watakuwa ni ndege wa kawaida, huna haja ya kuwaogopa wala kuwatazama hao kama ishara ya jambo fulani lijalo…. Ishara ya mambo mabaya yajayo ni dhambi maishani mwetu!.
Ukiwa msengenyaji, au mwasherati, au ulevi, au muabuduji wa sanamu basi hiyo ndio ishara tosha ya Majanga yajayo!.. Lakini tukiwa wasafi na dhamiri zetu zikiwa safi mbele za Mungu, hatuna haja ya kutafuta kuangalia nyakati mbaya kwasababu hakuna mabaya yoyote yatakayotujia, tunakuwa tunalindwa na kuzungukwa na Nguvu za Mungu.
Lakini ukitoka kwenda kwa mganga kutafuta hatima ya kesho yako, kutokana na ishara uliyoiona, ambayo unaamini kuwa ni ishara mbaya, basi fahamu kuwa unafanya machukizo mbele za Mungu, na siku ya mwisho utasimama hukumuni.
Bwana atusaidie tuepukane na hayo yote.
Kutazama bao ni kufanya nini?
MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
UTAYAFIKIAJE MANENO SAFI YA MUNGU?
Je ushabiki wa mpira ni dhambi?
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu ATAZAMAYE BAO, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. 12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako………………. 14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na KUTAZAMA BAO; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu ATAZAMAYE BAO, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako……………….
14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na KUTAZAMA BAO; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Kutazama bao ni aina ya uchawi, ambayo inahusisha kuwasiliana na wafu, au miungu kwa njia ya kipande kidogo cha Ubao..
Katika Nyakati za kale, na hata nyakati za sasa katika baadhi ya sehemu, aina hii ya uganga bado inaendelea kufanyika…ambapo, watu Fulani maalum (ambao ni wachawi/waganga) wanakuwa na “Ubao” na huo ubao unakuwa umeandikwa maandishi fulani, pamoja na tarakimu, na alama fulani zisizoeleweka.
Ambapo mtu/watu wanapotaka kujua mambo yaliyopita au yanayoendelea sasa, au yatakayokuja, basi wanaketi kuuzunguka ubao huo, na kisha kuweka vidole vyao katika sehemu mojawapo ya huo ubao kufuatia maelekezo ya huyo mganga, na kisha wanapokea taarifa wanazozihitaji kutoka kwa hiyo miungu kupitia mganga huyo, au kupitia wao wenyewe.
Katika karne ya 19, uliibuka ubao mmoja maarufu ujulikanao kama “Ubao wa Ouija”. Ubao huu ulipata umaarufu katika bara la Ulaya na baadaye katika bara la Marekani, ulitumika na wachawi wengi maarufu na watu wengi waliutumainia ikiwemo watu maarufu, ukiaminika kutoa taarifa nyingi za mambo yasiyojulikana, Ubao huo hata sasa unatumika lakini si maarufu kama ilivyokuwa katika karne hiyo ya 19.
Katika biblia Bwana Mungu aliwakataza wana wa Israeli “kutazama Bao” na ‘anatukataza hata sisi leo’. Kwasababu ni aina ya uchawi, na aliye nyuma ya ubao huo ni “shetani mwenyewe”.. akiwadanganya kuwa “ni wafu”. Hivyo ilikuwa ni kosa kubwa kwenda kutazama bao, ili kupata taarifa fulani zilizojificha.
Katika biblia tunamsoma mfalme mmoja wa Israeli aliyeitwa Manase, alikuwa ni mtu wa kutazama sana bao, jambo ambalo Mungu alishalikataza, na matokeo yake akajisababishia matatizo makubwa sana, kwani Mungu kumtoa katika ufalme kwa muda mpaka alipotubu.. na hata alipotubu bado madhara ya alichokuwa anakifanya hayakuondoka yote, kwani aliwakosesha Israeli na kuwafanya na wao kuwa watu wa kutazama bao. Na hivyo ikawa pia ni mojawapo ya sababu ya Mungu kuwapeleka utumwani Babeli.
2Wafalme 21:1 “Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba. 2 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli. 3 Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. 4 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu. 5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. 6 Akampitisha mwanawe motoni, AKATAZAMA BAO, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 7 Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele; 8 wala sitawapotosha Israeli miguu watoke katika nchi niliyowapa baba zao; wakiangalia tu na kufanya sawasawa na yote niliyowaamuru, na kwa kuishika torati yote aliyowaamuru mtumishi wangu Musa. 9 Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.
2Wafalme 21:1 “Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba.
2 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli.
3 Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.
4 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu.
5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana.
6 Akampitisha mwanawe motoni, AKATAZAMA BAO, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
7 Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;
8 wala sitawapotosha Israeli miguu watoke katika nchi niliyowapa baba zao; wakiangalia tu na kufanya sawasawa na yote niliyowaamuru, na kwa kuishika torati yote aliyowaamuru mtumishi wangu Musa.
9 Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.
Mstari wa 6 hapo, unasema “AKATAZAMA BAO” Maana yake lolote lililokuwa linaendelea asilolijua, hakutaka kumwuliza Mungu, ajibuye kwa njia ya ndoto, au manabii wake, badala yake yeye “alikimbilia kutazama bao”.. Na hivyo akadanganywa pakubwa sana na shetani..akawa anafanya machukizo mengi, ikawa dhambi kubwa sana kwake.
Na jambo lilolomchukiza Mungu kipindi hicho, linamchukiza hata leo..
Leo hii idadi kubwa ya watu wanaohudhuria kwa waganga wa kienyeji na kupewa maagizo ya kuweka viganja vyao juu ya vibao, au vibuyu, au mashuka, na kuambiwa mambo yao, hawajui kuwa wanafanya dhambi kama tu hiyo ya kutazama bao. Vile vile watu wanaobashiri (wanaoBET), nao pia ni watu wanaotazama Bao.
Ndugu, kama unataka kuweka sawa mambo yako ya kiroho na ya kimwili, suliuhisho ni moja tu!, mpokee Yesu maishani mwako, huyo ndiye suluhisho, kwasababu yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima.
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
MADHARA YA KUTOIJUA KWELI YOTE!
NINI MAANA YA UCHAWI?
NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAENEO YA IBADA: Sehemu ya 1
Kuna mambo ambayo yanaonekana madogo, lakini yana madhara makubwa sana rohoni. Watu hawafahamu kuwa wanaweza kufa kabisa kiroho kwa tabia ya kuendekeza USINGIZI ibadani..
Embu tusome habari ya Eutiko, tuone ni jambo gani Bwana anataka tufahamu nyuma ya matukio yaliyokuwa yanaendelea pale..
Tusome.
Matendo ya Mitume 20:7-10
[7]Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane. [8]Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika. [9]Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa. [10]Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake.
[7]Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
[8]Palikuwa na taa nyingi katika orofa ile tulipokuwa tumekusanyika.
[9]Kijana mmoja, jina lake Eutiko, alikuwa ameketi dirishani, akalemewa na usingizi sana; hata Paulo alipoendelea sana kuhubiri, akazidiwa na usingizi wake akaanguka toka orofa ya tatu; akainuliwa amekwisha kufa.
[10]Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake.
Nataka tuyatathimini hayo mazingira..kwanza walipokuwa wanasilizia injili ni katika gorofa, na gorofa yenyewe si ya kwanza bali ni ya tatu..
Pili japokuwa mahali pale ilikuwa ni usiku lakini biblia inatuambia kulikuwa na taa nyingi sana..maana yake ni kuwa mazingira yote yalikuwa yanaonekana, yapo wazi hivyo mahali pa hatari palionekana, na mahali salama pia palionekana.
Lakini tunaona huyu Eutiko alichagua kwenda kukaa katika dirisha la gorofa, akijua kabisa mahali pale si salama kukaa endapo akiteleza kidogo na kuanguka..
Lakini hakujali hilo, baada ya muda kidogo akasinzia.. Na matokeo yake akaanguka kutoka katika ile gorofa ya tatu. Na alipofika chini alikuwa tayari ameshakufa..
Ni kwanini habari hii iandikwe hapa? Kumbuka kila hadhithi inayoandikwa katika biblia inafundisho kubwa sana nyuma yake.
Sasa kitendo cha kuwepo katika gorofa ya tatu.
Inamaanisha kuwa mahali popote Neno la Mungu, linahubiriwa, au ibada inaendelea, iwe ya jumapili, au fupi ya maombi au mikesha, Rohoni mnakuwa mmechukuliwa mpaka mbingu ya Tatu (ndio ile gorofa ya tatu), juu sana mahali ambapo Mungu yupo na kiti chake cha enzi kilipo.
Na huko kuna Nuru nyingi, kama tulivyoona jinsi taa nyingi zilivyokuwa pale gorofani. Ikiwa na màana kuwa wakati unajaribu kuchagua kusogea mbali na uwepo wa Mungu utatambua kabisa mahali ulipo si salama..
Tabia ya kusinzia inakutuma ukae dirishani mwa uwepo wa Bwana na sio ukumbini. Ni kuonyesha jinsi gani usivyo “siriazi” na Mungu.
Na hatimaye unaanguka kutoka uweponi mwa Bwana..na kufa moja kwa moja kiroho.
Leo imekuwa ni desturi na mtu/watu wengi kila wafikapo nyumbani kwa Mungu ni lazima wasinzie, na wenyewe wanaona ni kawaida, wanadhani pale ni sawa na ofisini kwao, au shuleni kwao, ambapo hakuna jambo lolote la rohoni linalokuwa linaendelea.
Wanasahau kuwa wamepewa neema ya kupandishwa hadi kwenye kiti cha enzi cha Mungu, lakini wanakaa madirishani.
Ndugu ikiwa wewe ni mmojawapo wacha hii tabia, ukiindekeza utaanguka na kufa kabisa kiroho. Nimeona watu wengi wenye tabii hii, wakirudi nyuma ulimwenguni, wengine wakichuliwa na mawimbi ya ibilisi.
Kuwa siriazi na Mungu wako, tambua kilichokupeleka pale, unapoona wengine hawasinzii, haimaanishi kuwa hawahisi usingizi kama wewe, wanahisi lakini watalalaje mbele ya kiongozi wao mkuu? Wanaogopa kumvunjia heshima yake. Vilevile wanataka wapokee kikamilifu kile kilichowapeleka pale,
Hivyo kataa usingizi na wenyewe utakukimbia, na hiyo inakuja kwa kuzingatia kwa makini kile kinachoendelea pale, mawazo yako yote yakiwa pale, ukijua kabisa kila siku ni mpya nyumbani kwa Bwana, na Mungu anatembea.
Lakini kama utaenda kwa desturi na mazoea, au kukamilisha ratiba, utakuwa ni mtu wa kulala lala na siku moja utakufa kabisa kiroho kwasababu uwepo wa Mungu umekwisha kukuacha. Mheshimu Mungu.
Bwana atasaidie sana.
MIMI NI ALFA NA OMEGA.
DHAMBI YA MAUTI
YESU ANA KIU NA WEWE.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.
SWALI: Naomba kufahamu kumpenda Mungu kukoje, Je tufanyeje ili tuonekane tunampenda?
JIBU: Tofauti na sisi tunavyotafsiri upendo, kwamba ni kuonyesha hisia zilizo nzuri kwa mwingine, Kwamfano kuhurumia, kujali, kuthamini, kuhudumia, kusifia, kujitoa n.k.
Lakini kwa Mungu ili tuonekane tunampenda yeye, ni zaidi ya kuonyesha hisia.. Kwani waweza kuwa na hisia nzuri kwa Mungu, mpaka ukatoa machozi, unapotafakari matendo yake makuu, Unapotazama wema wake na fadhili zake, na uumbaji wake wote, vikakufanya ujihisi kumpenda sana Mungu.
Lakini hili mbele za Mungu linaweza lisihesabike, kwasababu si kile Mungu anachotaka kukiona kwetu..
Hivyo ni vizuri kufahamu mambo haya makuu matatu (3), ambayo ukifanya bidii kuyatenda, bila hata kuonyesha hisia Fulani kubwa, Mungu atakuona unampenda sana, na matokeo yake atajidhihirisha kwako. Mambo yenyewe ni haya;
Amri zake ni pamoja na kukaa mbali na dhambi, halikadhalika, kupendana sisi kwa sisi.
Biblia inasema..
1Yohana 5:3 “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. 4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”.
1Yohana 5:3 “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
4 Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu”.
Umeona, Bado Bwana Yesu analirudia tena hilo hilo neno katika
Yohana 14:15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Yohana 14:15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Na amri yake iliyo kuu aliyotupa, ni kupendana sisi kwa sisi, kama nafsi zetu (Yohana 13:34), na zaidi kuwapenda mpaka wale wanaotuchukia. Tukizingatia hayo mambo mawili, huku tukijilinda na dhambi, kwa maisha ya utakatifu, hiyo ni dalili ya kwanza inayofunua upendo wetu wa kweli kwa Mungu.
Kuupenda ulimwengu kunakwenda kinyume na kumpenda Mungu, biblia inasema hivyo katika;
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
Ukisema unampenda Mungu, halafu, bado unapenda fashion, unapenda anasa, unapenda party party, na tafrija tafrija, mipira, muvi muvi kila wakati, miziki ya kidunia, kampani za wenye dhambi, vijiwe vijiwe visivyo na maana.
Basi ufahamu upendo kwa Mungu hautakaa uwepo ndani yako, Biblia inasema hivyo. Jitenge na mambo ya kiulimwengu kwa jinsi uwezavyo, tafuta ndugu katika Bwana ndio wawe watu wako wa karibu, biblia ndio iwe novel yako, nyimbo za sifa ndio ziwe mziki wako, kanisani ndio pawe kijiweni pako. Ukizingatia hayo kwa bidii, basi kidogo kidogo, upendo kwa Mungu usio wa kinafki utaingia ndani yako. Na Mungu atauona.
Marko 12:29 “Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; 30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote”.
Marko 12:29 “Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote”.
Hapo hajasema, “mpende tu Bwana Mungu wako”, halafu basi, bali anasema utampenda kwa mambo yote manne, yaani roho, moyo, mwili na akili.
Mungu hataki kupendwa kwenye roho tu, bali hata kwenye akili zako, na nguvu zako. Ikiwa unafikiria Mungu anataka umtafute tu siku za ibada, umwabudu halafu basi, bado hujakamilisha kumpenda, bali anataka nguvu zako unazokwenda kuzisumbukia huko katika kutanga tanga kwako ziishie kwake, Mali zako, kujitoa kwako katika kuujenga ufalme wa Mungu, na kusambaza habari zake.
Vilevile akili yako yote uitumie kwake, ubuni utafiti ni kwa jinsi gani, unaweza kuifanya kazi ya Mungu iwe bora zaidi, kama vile unavyofikiri kila siku ni jinsi gani unavyoweza kuyafanya maisha yako kuwa bora kwake, sio tu kumwachia mtumishi Fulani,au mchungaji Fulani afanye yeye kila kitu, angali vingine vipo ndani ya uwezo wako wewe.
Kwa kuzingatia mambo hayo matatu, basi utakuwa umempenda Mungu, na yeye atalijua hilo, na matokeo yake ni kujidhihirisha kwako, na kukuhudumia. Huko ndio kumpenda Mungu.
Zaburi 91:14 “Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu. 15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza; 16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu”.
Zaburi 91:14 “Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
15 Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu”.
Bwana akubariki.
TAFUTA UZIMA WA MILELE NA SI UZIMA TU!.
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
SWALI: Mbona katika Marko 10:30 Bwana Yesu anasema tutapata mara mia ‘wake’? Hii si inatupa uthibitisho kuwa ndoa za mitara ni sawa?
JIBU: Tusome kwa ukaribu vifungu vyenyewe;
Marko 10:28 “ Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, aundugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, NA NDUGU WAKE, na mama,na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza”.
Hapo hakuna mahali popote Bwana Yesu amesema tutapata mara mia ‘wake’, isipokuwa anasema tutapata mara mia “ndugu wake”. Akimaanisha ndugu wa KIKE, kama tu alivyosema ndugu WAUME, tutapata mara mia.
Maana yake ni kwamba mtu yeyote anayeingia gharama ya kumfuata Yesu kwa moyo wake wote, na kwa ajili ya injili yake, Bwana ameahidi kumrudishia kila kitu alichokipoteza mara100 zaidi.
Ikiwa aliwaacha dada zake kumi(10), basi Bwana atamrudishia ndugu wadada mara mia zaidi.. yaani ndugu wadada elfu moja (1000), watakuja kuwa karibu naye.. wenye upendo kama tu ule wa wale wa kwanza kwake.
Lakini tuseme, labda tuliacha wake zetu kwa ajili ya injili, Je! Mungu hataturudishia thawabu mara mia kwa kuwaacha wao?
Jibu ni kwamba ataturudishia pia mara mia, lakini haimaanishi kuwa tutapewa ‘wake’ tuwaoe, hapana, bali tutapewa ndugu, wenye Usaidizi kama tu wa wake.. Kumbuka, mwanamke aliumbwa kuwa msaidizi wa Adamu, hakuumbwa kuwa chombo cha starehe..
Hivyo hudumu aliyoitiwa mke duniani ni kuwa msaidizi.. Vivyo hivyo Mungu atakunyanyulia ndugu ambao watasimama kama wasaidizi kwako katika huduma, mara mia, kama wake.
Lakini haimaanishi utawaoa, hapana, kama itakavyokuwa kwa ndugu mara mia atakaokupa, hawataingia kwenye tumbo la mama yako na kuzaliwa ili wawe ndugu yako, bali watatoka nje, na kusimama kama ndugu.. Vivyo hivyo na kwa watoto na mambo mengine yote.
Lakini kwanini iwe hivyo? Ni ili kulitimiza lile neno la Bwana Yesu alilosema..
“Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yakekwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha”.(Luka 9.24)
TWEKA MPAKA VILINDINI.
KALAMU YENYE UONGO YA WAANDISHI IMEIFANYA KUWA UONGO.
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000
KIASI NI NINI KATIKA UKRISTO?
Ipo hekima ambayo Mungu anaitumia, pindi anapotaka kututoa katika hatua moja ya kimaisha kwenda nyingine.
Kiasili, nafsi zetu sisi wanadamu zinapenda kupokea majibu ya maombi pale tu tunapoomba… Lakini hekima ya Mungu wakati mwingine si kutupa kile tunachokiomba wakati ule ule tunapoomba… Wakati mwingine inaweza kuchukua muda mrefu kupokea majibu, na bado ikawa ni mapenzi ya Mungu.
Yapo mambo ambayo tukimwomba Mungu, ni rahisi kupokea majibu papo kwa hapo, lakini yapo ambayo yatachukua muda kujibiwa!..Sasa si kwasababu Mungu hawezi kujibu papo hapo! La!, anaweza kwasababu hakuna kinachomshinda yeye, lakini anapoyachelewesha wakati mwingine kwa faida yetu.
Hebu tengeneza picha, mtoto wa miaka 6 ambaye hajui hata kusoma, anamwomba Baba yake ambaye ni tajiri sana, ampe gari!.. Ni kweli Baba yake anao uwezo wa kumpa gari pale pale alipoomba, lakini hawezi kumpa kwasababu bado hajajua hata kusoma, atawezaje kuendesha hilo gari?..kwasababu aendapo akipewa gari katika akili hiyo aliyonayo, kitakachofuata ni Ajali!.. na mzazi atakuwa amemwua mtoto wake, badala ya kumpa uzima!..
Kwahivyo Ni sharti kwanza aende darasani akafundishwe kusoma na kuandika, na hesabu.. halafu akishajua hayo yote, ndipo aende kwenye shule ya udereva, akajifunze kanuni za uendeshaji magari, na baada ya kuhitimu na kupata leseni, ndipo baba yake ampe gari!..
Hivyo zoezi zima hilo la kusoma mpaka kupata leseni mpaka siku ya kukabidhiwa gari, linaweza kuchukua miaka hata 10. Kwahiyo ni sawa na kusema kwamba, mtoto kajibiwa ombi lake la kupewa gari baada ya miaka 10.
Lakini endapo mtoto Yule angeomba “peremende” kwa Baba yake, ni dhahiri kuwa “angepatiwa muda ule ule alioomba”.
Na kwa Mungu wetu ni hivyo hivyo, yapo mambo ambayo tukiomba tutajibiwa wakati huo huo, lakini yapo mambo mengine yatachukua muda mrefu sana, hata miaka kadhaa kujibiwa!!…
Hivyo kama umezoea kumwomba Mungu jambo na kupokea majibu yake saa hiyo hiyo, na ukamwomba jambo lingine ukaona hujajibiwa muda huo huo kama unavyotaka wewe!!.. Fahamu kuwa sio kwamba Mungu kakunyima hilo jambo, au kwamba hajasikia maombi yako!.. Amesikia maombi yako, na tayari majibu kashayaachia, lakini yatakuja kudhihirika siku nyingi za mbeleni endapo ukidumu katika kuishikilia ahadi hiyo.
Hebu tujifunze mfano mmoja juu ya wana wa Israeli, kipindi wanatoka Misri..
Tunasoma katika maandiko kuwa, kipindi wanaingia Kaanani, Mungu hakuwatoa wakaanani katika ile nchi ndani ya siku moja, au ndani ya mwaka mmoja, biblia inasema ilichukua miaka kadhaa, Mungu kuwaondoa Wakaanani na wengineo waliokuwa wanaikalia ile nchi ya Ahadi.
Sasa ni kwasababu gani Mungu hakuwaondoa Wakaanani wote na wahivi wote ndani ya siku moja??..Jibu: Si kwasababu hakuwa na uwezo huo, alikuwa nao tele, lakini kwafaida ya watoto wake Israeli, ilikuwa hana budi kuwapa urithi huo kidogo kidogo!…kwasababu angewapa siku ile ile, basi yangezuka matatizo mengine, ambayo tunayasoma katika mistari ifuatayo…
Tusome,
Kutoka 23: 27 “Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. 28 Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako. 29 SITAWAFUKUZA MBELE YAKO KATIKA MWAKA MMOJA; NCHI ISIWE UKIWA, NA WANYAMA WA BARA WAKAONGEZEKA KUKUSUMBUA. 30 NITAWAFUKUZA KIDOGO KIDOGO MBELE YAKO, HATA UTAKAPOONGEZEKA WEWE, NA KUIRITHI HIYO NCHI”
Kutoka 23: 27 “Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao.
28 Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.
29 SITAWAFUKUZA MBELE YAKO KATIKA MWAKA MMOJA; NCHI ISIWE UKIWA, NA WANYAMA WA BARA WAKAONGEZEKA KUKUSUMBUA.
30 NITAWAFUKUZA KIDOGO KIDOGO MBELE YAKO, HATA UTAKAPOONGEZEKA WEWE, NA KUIRITHI HIYO NCHI”
Umeona hapo?..Sababu ya wao kutopewa Nchi yote ndani ya siku moja, ni lli wanyama wasiongezeke juu ya nchi, na kuwaletea madhara.. Kwasababu kipindi wanatoka Misri, walikuwa wachache.. halafu wanakwenda kupewa nchi kubwa!.. ni lazima sehemu kubwa ya nchi hiyo itakuwa MAPORI!.. Kwasababu hakuna watu wa kuijenga wala kukaa juu yake..na hivyo Nyoka wataongezeka, chatu na fisi wataongezeka, watakaokula mifugo yao..hali kadhalika samba na mbu!, watakuwa wengi kwasababu ya wingi wa mapori, na hivyo itanyanyuka shida nyingine..
Kwahiyo hekima ya Mungu, ikaamua maadui wa Israeli wasifukuzwe wote, bali waachwe kwanza kwa kitambo kifupi, waendelee kufyeka mapori, mpaka idadi ya Israeli itakapoongezeka, kufikia kiwango cha kuweza kuitawala nchi nzima, ndipo maadui wote waondolewe!.
Na sisi ni nini tunajifunza hapo?…tunajifunza kuwa wavumilivu, na kuwa na Subira katika ahadi za Mungu na kwamba si kila ombi litajibiwa siku tunayoitaka sisi.
Ikiwa wewe ni binti au kijana, na umemwomba Mungu akupe mwenza wa maisha, na unaona hujibiwi kwa wakati unaotaka wewe, huenda ni kwasababu wakati wake haujafika! Aidha Umri wako ni mdogo, au pengine akili yako bado haijakuwa vya kutosha, bado haijafundishwa vya kutosha maisha ya ndoa,.. Na ili Mungu asikupoteze ndio maana hakupi unachotaka kwa wakati huo huo.
Vile vile Ukimwomba Mungu mali na huku akili yako inawaza kwenda kujionyesha mbele za watu, fahamu kuwa Mungu ameshasikia maombi yako, lakini hutapokea saa hiyo hiyo, ulipopmba…badala yake utakwenda kwanza kwenye madarasa yake ambayo atakufundisha maisha ukiwa na mali, (huenda yakachukua hata miaka 20), inategemea na akili yako, na ukifaulu madarasa yake! basi atakupatia!..kwasababu utakuwa umeshajengeka vya kutosha, kiasi kwamba mali haziwezi kukuangusha wala kukurudisha nyuma kiroho, wala kuwaharibu wengine.
Na maombi mengine yote ni hivyo hivyo..yanayo hatua mpaka tuone matokeo, hivyo tuwe wavumilivu na watu wa subira..
Bwana Yesu atubariki.
IJUE SIRI YA UTAUWA.
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
Tofauti kati ya lijamu na hatamu ni ipi kibiblia?
Kigao ni nini? Na Je kinafunua nini kwa agano jipya?
Tofauti kati ya Hekima, ufahamu na maarifa, ni ipi?
Kaanani ni jina la zamani la nchi za Mashariki ya kati!..Eneo la Kaanani liliundwa na sehemu ya nchi zifuatazo, Nchi ya Israeli yote, pande za Magharibi mwa nchi ya Yordani, Kusini mwa nchi ya Lebanoni na nchi ya Palestina yote.
Nchi ya Kaanani, hapo kwanza ilikuwa inakaliwa na watu waliojulikana kama Wakaanani, ambao biblia inawataja kama watu waliokuwa wenye sifa na wenye maumbile makubwa. Ndio maana tunasoma kipindi wale wapelelezi wa Kiisraeli walipotumwa kuipeleleza nchi hiyo ya Kaanani, walirudi na ripoti ya kuogopesha, wakasema wamekutana na Wanefili ndani ya hiyo nchi.
Hesabu 13:31 “Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, HATUWEZI KUPANDA TUPIGANE NA WATU HAWA; KWA MAANA WANA NGUVU KULIKO SISI. 32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; NA WATU WOTE TULIOWAONA NDANI YAKE NI WATU WAREFU MNO. 33 KISHA, HUKO TULIWAONA WANEFILI, WANA WA ANAKI, WALIOTOKA KWA HAO WANEFILI; TUKAJIONA NAFSI ZETU KUWA KAMA MAPANZI; nao ndivyo walivyotuona sisi”.
Hesabu 13:31 “Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, HATUWEZI KUPANDA TUPIGANE NA WATU HAWA; KWA MAANA WANA NGUVU KULIKO SISI.
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; NA WATU WOTE TULIOWAONA NDANI YAKE NI WATU WAREFU MNO.
33 KISHA, HUKO TULIWAONA WANEFILI, WANA WA ANAKI, WALIOTOKA KWA HAO WANEFILI; TUKAJIONA NAFSI ZETU KUWA KAMA MAPANZI; nao ndivyo walivyotuona sisi”.
Nchi ya Kaanani Mungu alimpa Ibrahimu na uzao wake wote, Ndio maana Wakaanani waliokuwa wanaishi katika nchi hiyo (Hao wanefili) Mungu alikuja kuwaondoa kwa mkono hodari..
Mwanzo 17:7 “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao”
Mwanzo 17:7 “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao”
Baada ya Israeli kuitwaa Sehemu ya nchi ya Kaanani, waliibadilisha jina na kuiita Nchi ya Israeli. Na tangu wakati huo mpaka leo, inajulikana kama nchi ya Israeli, Ingawa si sehemu yote, sehemu nyingine ya Kaanani, Mungu hakumalizia kuwapa wana wa Israeli, kwasababu walikengeuka na kuanza kuingia maagano na wakaanani.
Waamuzi 2:1 “Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; 2 nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? 3 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu 4 Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia”
Waamuzi 2:1 “Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;
2 nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?
3 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu
4 Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia”
Kiroho, safari ya wana wa Israeli, kutoka Misri kwenda Kaanani, inafananishwa na safari yetu sisi ya kwenda Mbinguni (kwenye nchi yetu ya Ahadi) kutoka katika Ulimwengu wa dhambi.
Na kama jinsi safari ile ilivyokuwa na Majaribu mengi njiani, kiasi kwamba walioanza Safari kuanzia mwanzo hadi mwisho walikuwa ni wachache sana, yaani watu wawili tu (Yoshua na Kalebu). Vivyo hivyo safari ya kwenda mbinguni ni mapambano, kwasababu watakuwa wachache sana watakaoshinda…
Luka 13:22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”
Luka 13:22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”
Hapo anasema TUJITAHITI!!..maana yake ni kwamba “JITIHADA BINAFSI PIA ZINAHITAJIKA” .. Si suala la kukaa tu na kuomba na kusubiri!…bali ni suala la kutia bidii pia!!…Wengi watakaoikosa mbingu ni kwasababu ya kutotia bidii kuutafuta ufalme wa Mungu!..(maana yake ni watu wasio na jitihada katika mambo ya kiMungu).
Sasa swali ni je!, mimi na wewe tunazo hizo jitihada za kuingia katika Kaanani yetu?.
Kama bado upo nje ya Wokovu, (yaani hujampokea Yesu) basi fahamu kuwa upo katika hatari ya kuikosa mbingu na kama tayari umeshampokea Bwana Yesu lakini unaishi maisha ya uvuguvugu, ya kutokujali, ya kusukumwa sukumwa, au kumbembelezwa bembelezwa…basi fahamu kuwa upo mbali na ufalme wa mbinguni, na siku ya kurudi kwa Bwana itakukuta kama mwivi.. kwasababu maandiko yanasema “tutie jitihada”.
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
MPENDEZE MUNGU ZAIDI.
Biblia ilimaanisha nini watu wasitoe vizazi vyao kwa Moleki?
Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Mara nyingi Bwana Yesu amekuwa akijitambulisha kwa majina mbalimbali, kwa mfano ukisoma Ufunuo 19:13 inasema jina lake anaitwa Neno la Mungu.. Hii ikiwa na maana popote palipo na Neno la Mungu, basi Kristo yupo hapo, na mtu anayeliishi hilo, basi anamuishi Kristo maishani mwake.
Ukisoma pia Isaya 9:6 inasema
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani”
Hapo mwishoni inasema, jina lake ataiwa mfalme wa Amani, ikiwa na maana kuwa mahali popote amani ya kweli ile idumuyo ilipo, basi Kristo naye yupo hapo pia,kwasababu yeye ndio mfalme wa hiyo.
Lakini tukirudi katika kitabu cha Ufunuo1:8, Yesu anasema maneno haya;
“Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi”.
Anayarudia tena maneno hayo hayo katika.. Ufunuo 21:6,22:13.
Maana yake ni nini?
Alfa ni herufi ya kwanza katika lugha ya kigiriki, na omega ni herufi ya mwisho ya lugha hiyo. Kwa lugha yetu ni sawa na tuseme Yesu ni “A” na Yesu ni “Z”, Maana yake ni kuwa yeye ni Neno la Kwanza na pia ni Neno la mwisho.
Lakini hajaishia hapo, anasisitizia kabisa kwa kusema yeye ni ‘Mwanzo na Yeye ni mwisho’. Jiulize kwanini hajasema yeye ni ‘juu na yeye ni chini’, au ‘yeye ni mashariki na yeye ni magharibi’ au ‘yeye ni mbele na yeye ni nyuma’, bali anasema yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho?.. Ni muhimu sana kutafakari hili!!
Akiwa na maana kuwa, popote palipo na mwanzo, yeye anapaswa awepo hapo, na popote palipo na mwisho yeye ndio muhitimishaji. Jambo ambalo watu wengi hawalitambui, Na ndio maana inakuwa ngumu kumwona Yesu katika maisha yetu.
Kwasababu hatumtangulizi yeye, katika mwanzo wa mambo yetu, na vilevile hatuhitimishi na yeye katika mwisho wote wa mambo yetu. Tunachukulia kiwepesi wepesi tu, tunamweka Kristo katikati ya mambo yetu, tukidhani kuwa tutamwona akitembea na sisi. Hana kanuni hiyo!
Watu wote wanaonza na Yesu na kuhitimisha na Yesu, katika mambo yao yote, angalia maisha yao, utaona ni ya ushuhuda tu kila siku.
Hivyo haya ni maeneo muhimu sana ya kuzingatia kuanza naye, ukiyachezea haya, umeshamkosa Yesu.
Hakikisha unapompa Bwana mwanao, sio unampa kwa mdomo tu, unamwacha aje kupenda mwenyewe kanisa akiwa mkubwa, bali unamgharimikia kwa Bwana mahitaji yote yanayompasa, utampa elimu, lakini zaidi elimu ya biblia kwa bidii, unamtafutia madarasa ya biblia spesheli kutoka kwa watumishi wa Mungu, unamtoa wakfu kwa Bwana, maana yake hata akikwambia mimi sitakuja kuajiriwa bali nitakuwa mchungaji, hakuna kipingamizi chochote juu yake, unamsapoti kwa furaha yote.
Ukifanya hivyo, utakuja kuvuna ulichokipanda mbeleni. Kwake huyo mtoto na kwa wazao wako wote waliosalia. Kwasababu umemfanya Yesu Alfa na Omega kwenye uzao wako.
Hivyo popote pale, hakikisha unaanza na Kristo, na unamaliza na Kristo. Na hakika tutamwona katika mambo yetu yote.
Maran Atha.
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)
Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.
Nini maana ya K.K, na B.K? (B.C na A.D).
Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?