Kaanani ni jina la zamani la nchi za Mashariki ya kati!..Eneo la Kaanani liliundwa na sehemu ya nchi zifuatazo, Nchi ya Israeli yote, pande za Magharibi mwa nchi ya Yordani, Kusini mwa nchi ya Lebanoni na nchi ya Palestina yote.
Nchi ya Kaanani, hapo kwanza ilikuwa inakaliwa na watu waliojulikana kama Wakaanani, ambao biblia inawataja kama watu waliokuwa wenye sifa na wenye maumbile makubwa. Ndio maana tunasoma kipindi wale wapelelezi wa Kiisraeli walipotumwa kuipeleleza nchi hiyo ya Kaanani, walirudi na ripoti ya kuogopesha, wakasema wamekutana na Wanefili ndani ya hiyo nchi.
Hesabu 13:31 “Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, HATUWEZI KUPANDA TUPIGANE NA WATU HAWA; KWA MAANA WANA NGUVU KULIKO SISI. 32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; NA WATU WOTE TULIOWAONA NDANI YAKE NI WATU WAREFU MNO. 33 KISHA, HUKO TULIWAONA WANEFILI, WANA WA ANAKI, WALIOTOKA KWA HAO WANEFILI; TUKAJIONA NAFSI ZETU KUWA KAMA MAPANZI; nao ndivyo walivyotuona sisi”.
Hesabu 13:31 “Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, HATUWEZI KUPANDA TUPIGANE NA WATU HAWA; KWA MAANA WANA NGUVU KULIKO SISI.
32 Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; NA WATU WOTE TULIOWAONA NDANI YAKE NI WATU WAREFU MNO.
33 KISHA, HUKO TULIWAONA WANEFILI, WANA WA ANAKI, WALIOTOKA KWA HAO WANEFILI; TUKAJIONA NAFSI ZETU KUWA KAMA MAPANZI; nao ndivyo walivyotuona sisi”.
Nchi ya Kaanani Mungu alimpa Ibrahimu na uzao wake wote, Ndio maana Wakaanani waliokuwa wanaishi katika nchi hiyo (Hao wanefili) Mungu alikuja kuwaondoa kwa mkono hodari..
Mwanzo 17:7 “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao”
Mwanzo 17:7 “Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao”
Baada ya Israeli kuitwaa Sehemu ya nchi ya Kaanani, waliibadilisha jina na kuiita Nchi ya Israeli. Na tangu wakati huo mpaka leo, inajulikana kama nchi ya Israeli, Ingawa si sehemu yote, sehemu nyingine ya Kaanani, Mungu hakumalizia kuwapa wana wa Israeli, kwasababu walikengeuka na kuanza kuingia maagano na wakaanani.
Waamuzi 2:1 “Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi; 2 nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani? 3 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu 4 Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia”
Waamuzi 2:1 “Kisha malaika wa Bwana alikwea juu kutoka Gilgali kwenda Bokimu. Akasema, Mimi nimewaleta ninyi mkwee juu kutoka nchi ya Misri, nami nimewaleta hata nchi niliyowaapia baba zenu; nami nilisema, Mimi milele sitalivunja hilo agano langu nililoagana nanyi;
2 nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?
3 Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu
4 Ikawa, hapo huyo malaika wa Bwana alipoyanena maneno haya, kuwaambia wana wa Israeli wote, ndipo hao watu wakainua sauti zao na kulia”
Kiroho, safari ya wana wa Israeli, kutoka Misri kwenda Kaanani, inafananishwa na safari yetu sisi ya kwenda Mbinguni (kwenye nchi yetu ya Ahadi) kutoka katika Ulimwengu wa dhambi.
Na kama jinsi safari ile ilivyokuwa na Majaribu mengi njiani, kiasi kwamba walioanza Safari kuanzia mwanzo hadi mwisho walikuwa ni wachache sana, yaani watu wawili tu (Yoshua na Kalebu). Vivyo hivyo safari ya kwenda mbinguni ni mapambano, kwasababu watakuwa wachache sana watakaoshinda…
Luka 13:22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia, 24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”
Luka 13:22 “Naye alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu. 23 Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,
24 Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze”
Hapo anasema TUJITAHITI!!..maana yake ni kwamba “JITIHADA BINAFSI PIA ZINAHITAJIKA” .. Si suala la kukaa tu na kuomba na kusubiri!…bali ni suala la kutia bidii pia!!…Wengi watakaoikosa mbingu ni kwasababu ya kutotia bidii kuutafuta ufalme wa Mungu!..(maana yake ni watu wasio na jitihada katika mambo ya kiMungu).
Sasa swali ni je!, mimi na wewe tunazo hizo jitihada za kuingia katika Kaanani yetu?.
Kama bado upo nje ya Wokovu, (yaani hujampokea Yesu) basi fahamu kuwa upo katika hatari ya kuikosa mbingu na kama tayari umeshampokea Bwana Yesu lakini unaishi maisha ya uvuguvugu, ya kutokujali, ya kusukumwa sukumwa, au kumbembelezwa bembelezwa…basi fahamu kuwa upo mbali na ufalme wa mbinguni, na siku ya kurudi kwa Bwana itakukuta kama mwivi.. kwasababu maandiko yanasema “tutie jitihada”.
Bwana akubariki.
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
NI KWA NAMNA GANI SHETANI ANAIZUIA INJILI?
MPENDEZE MUNGU ZAIDI.
Biblia ilimaanisha nini watu wasitoe vizazi vyao kwa Moleki?
Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?
Ni kweli Paulo alipuuzia maonyo aliyopewa ya kwenda Yerusalemu?
Rudi nyumbani
Print this post
Mara nyingi Bwana Yesu amekuwa akijitambulisha kwa majina mbalimbali, kwa mfano ukisoma Ufunuo 19:13 inasema jina lake anaitwa Neno la Mungu.. Hii ikiwa na maana popote palipo na Neno la Mungu, basi Kristo yupo hapo, na mtu anayeliishi hilo, basi anamuishi Kristo maishani mwake.
Ukisoma pia Isaya 9:6 inasema
“Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani”
Hapo mwishoni inasema, jina lake ataitwa mfalme wa Amani, ikiwa na maana kuwa mahali popote amani ya kweli ile idumuyo ilipo, basi Kristo naye yupo hapo pia, kwasababu yeye ndio mfalme wa hiyo.
Lakini tukirudi katika kitabu cha Ufunuo1:8, Yesu anasema maneno haya;
“Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi”.
Anayarudia tena maneno hayo hayo katika.. Ufunuo 21:6,22:13.
Maana yake ni nini?
Alfa ni herufi ya kwanza katika lugha ya kigiriki, na omega ni herufi ya mwisho ya lugha hiyo. Kwa lugha yetu ni sawa na tuseme Yesu ni “A” na Yesu ni “Z”, Maana yake ni kuwa yeye ni Neno la Kwanza na pia ni Neno la mwisho.
Lakini hajaishia hapo, anasisitizia kabisa kwa kusema yeye ni ‘Mwanzo na Yeye ni mwisho’. Jiulize kwanini hajasema yeye ni ‘juu na yeye ni chini’, au ‘yeye ni mashariki na yeye ni magharibi’ au ‘yeye ni mbele na yeye ni nyuma’, bali anasema yeye ni mwanzo na yeye ni mwisho?.. Ni muhimu sana kutafakari hili!!
Akiwa na maana kuwa, popote palipo na mwanzo, yeye anapaswa awepo hapo, na popote palipo na mwisho yeye ndio muhitimishaji. Jambo ambalo watu wengi hawalitambui, Na ndio maana inakuwa ngumu kumwona Yesu katika maisha yetu.
Kwasababu hatumtangulizi yeye, katika mwanzo wa mambo yetu, na vilevile hatuhitimishi na yeye katika mwisho wote wa mambo yetu. Tunachukulia kiwepesi wepesi tu, tunamweka Kristo katikati ya mambo yetu, tukidhani kuwa tutamwona akitembea na sisi. Hana kanuni hiyo!
Watu wote wanaoanza na Yesu na kuhitimisha na Yesu, katika mambo yao yote, angalia maisha yao, utaona ni ya ushuhuda tu kila siku.
Hivyo haya ni maeneo muhimu sana ya kuzingatia kuanza naye, ukiyachezea haya, umeshamkosa Yesu.
Hakikisha unapompa Bwana mwanao, sio unampa kwa mdomo tu, unamwacha aje kupenda mwenyewe kanisa akiwa mkubwa, bali unamgharimikia kwa Bwana mahitaji yote yanayompasa, utampa elimu, lakini zaidi elimu ya biblia kwa bidii, unamtafutia madarasa ya biblia spesheli kutoka kwa watumishi wa Mungu, unamtoa wakfu kwa Bwana, maana yake hata akikwambia mimi sitakuja kuajiriwa bali nitakuwa mchungaji, hakuna kipingamizi chochote juu yake, unamsapoti kwa furaha yote.
Ukifanya hivyo, utakuja kuvuna ulichokipanda mbeleni. Kwake huyo mtoto na kwa wazao wako wote waliosalia. Kwasababu umemfanya Yesu Alfa na Omega kwenye uzao wako.
Hivyo popote pale, hakikisha unaanza na Kristo, na unamaliza na Kristo. Na hakika tutamwona katika mambo yetu yote.
Maran Atha.
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)
Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.
Nini maana ya K.K, na B.K? (B.C na A.D).
Je tunaruhusiwa kushirikiana na wasanii wa kidunia katika kumwimbia Mungu?
Agano ni makubaliano kati ya pande mbili; Na kuna aina saba (7) za maagano kibiblia.
1)Agano kati ya “MTU NA MTU”, 2) kati ya “MTU NA KITU”, 3) kati ya “MTU NA shetani” 4) kati ya “MTU NA MUNGU” 5) kati ya “MUNGU NA MTU”, 6) kati ya “MUNGU NA VIUMBE Vyake” 7) kati ya “MUNGU, NA MWANAE”.
Kwa taratibu tuvitazame vipengele vyote hivyo vya maagano. Na kisha tutajifunza ni Agano lipi lenye nguvu kuliko yote!
Mfano wa Agano kati ya Mtu na mtu, ni lile Yakobo aliloingia na Labani..Kwamba Yakobo asiwatese wana wake huko aendako.. na wala asije akaongeza mke wake wengine zaidi ya hao wanawe aliompa..
Mwanzo 31:43 “Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu; nami naweza kuwatendea nini leo binti zangu na wana wao waliowalea 44 Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe. 45 Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo………… 50 Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe?”
Mwanzo 31:43 “Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu; nami naweza kuwatendea nini leo binti zangu na wana wao waliowalea
44 Haya! Na tufanye agano, mimi na wewe, liwe kwa ushahidi kati ya mimi na wewe.
45 Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo…………
50 Ukiwatesa binti zangu, na ukitwaa wake zaidi ya binti zangu, wala hapana mtu pamoja nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati ya mimi na wewe?”
Mfano wa mwingine wa Agano la “Mtu na mtu”..ni lile “agano la Ndoa”.. Watu wawili wanafunga ndoa, wanakuwa wameingia Agano la kuishi pamoja, mpaka kifo kitakapowatenganisha..Agano hilo linakuwa ni la mtu na mtu, mbele ya Mungu wa mbinguni. Na ikitokea mmojawapo kavunja agano hilo, basi laana itakuwa kuu yake.
2. Agano kati ya “MTU NA KITU”.
Mtu pia anaweza kuingia agano na kitu.. Kwamfano utaona Ayubu ambaye alikuwa ni mtu mkamilifu sana, aliweza kuingia agano na Macho yake, kwamba asimtazame mwanamke na kumtamani..
Ayubu 31:1 “Nilifanya agano na macho yangu; Basi nawezaje kumwangalia msichana?”
Hii ikiwa na maana kuwa hata sisi tunaweza kuweka Agano na macho yetu yasitazame ubaya, na midomo yetu isizungumze mabaya na miguu yetu isikimbilie mabaya n.k
3. Agano kati ya “MTU NA SHETANI”
Mtu anaweza kuingia Agano na shetani (miungu), na agano hili ndio baya kuliko maagano yote, kwasababu kamwe shetani hawezi kumpa mtu uzima, bali mauti!. Na maagano haya watu wanaingia aidha kwa kujua au kutokujua.. Mara nyingi Mila na Desturi!, na Kuhudhuria kwa waganga wa kienyeji na maisha ya dhambi ndiyo yanawaingiza watu kwenye maagano na mashetani bila kujua..
Kutoka 23:31 “Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hata bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.
32 Usifanye maagano pamoja nao, wala pamoja na miungu yao.
33 Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni tanzi kwako”
4. Agano kati ya “MTU NA MUNGU”.
Watu pia wanaweza kuingia maagano na Mungu wa mbingu na nchi…Mfano katika biblia utaona kipindi Israeli wamerudi nchini kwao baada ya kukaa utumwani miaka mingi, waliporudi waliweka agano na Mungu kuwa watawaacha wanawake wa kimataifa waliowaona na vile vile wataifuata torati ya Musa.
Ezra 10:3 “Haya basi! NA TUFANYE AGANO NA MUNGU WETU, kuachana na wake zetu, na wale waliozaliwa nao, tukilifuata shauri la bwana wangu, na shauri la hao wanaoitetemekea amri ya Mungu wetu; mambo haya na yatendeke kwa kuifuata torati”
5. Agano kati ya “MUNGU NA MTU”
Agano hili linakuwa thabiti, tofauti na lile ambalo mtu anaingia na Mungu, kwasababu Mungu kamwe havunjagi maagano, lakini sisi wanadamu tunavunja maagano, tunayoyaingia.. Mfano wa Agano ambalo Mungu aliingia na mtu au watu, ni lile aliloliingia na Ibrahimu, kuwa atakuwa Baba wa mataifa mengi..
Mwanzo 17: 1 “Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. 3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, 4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, 5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao. 9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako”.
Mwanzo 17: 1 “Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.
3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema,
4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi,
5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako.
7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao.
9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako”.
Agano hili ambalo Mungu aliingia na Ibrahimu, mpaka leo lina nguvu.. Ndio maana unaona ni kwanini Taifa la Israeli bado ni Taifa teule la Mungu. Na ambarikiye Israeli amebarikiwa, na amlaaniye amelaaniwa (Hesabu 24:9).
6. Agano kati ya “MUNGU NA VIUMBE”
Mungu pia anaweza kuingia agano na viumbe vyake alivyoviumba.. vilivyo na uhai na visivyo na uhai.. kama kama wanyama na mawe na miti na mabonde… Mfano wa Agano kama hili ni lile alilolifanya wakati anaigharikisha dunia, nyakati za NUHU.
Mwanzo 9:9 “Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu; 10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi. 11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi. 12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; 13 Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. 14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,
Mwanzo 9:9 “Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;
10 tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.
11 Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.
12 Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
13 Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.
14 Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,
15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. 16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi”.
15 nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.
16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi”.
Agano hili Mungu aliloingia na ardhi na wanyama kwamba hatawagharikisha tena kwa maji, lina nguvu mpaka leo, ndio maana utaona tangu wakati wa Nuhu mpaka leo hakuna gharika tena, na ule upinde tunaouna ni ishara ya agano lake hilo aliloingia nasi pamoja na viumbe vyote..
7. Agano kati ya “MUNGU, NA Mwanawe”.
Hili ndio Agano kuu, na lenye Nguvu kuliko maagano yote!.. Agano hili ndio lile aliloingia na Mwanawe mpendwa Yesu Kristo, kupitia Damu ya mwanawe. Na kwanini Agano hili lina nguvu?.. ni kwasababu Yesu Kristo ni Mungu katika mwili, hivyo Agano hili, ni Mungu kaingia na NAFSI YAKE MWENYEWE. Hivyo haliwezi kuvunjika wala haliwezi kupungua nguvu..
Agano la Mungu aliloingia na viumbe vyake kwamba havitagharikishwa kwa maji, ni kweli mpaka leo lina nguvu, lakini itakuja gharika nyingine ya moto na si ya maji, hivyo Agano la kwanza limetupa uzima lakini si wa milele, kwasababu itakuja gharika nyingine ya moto..
2Petro 3:6 “kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. 7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu”.
2Petro 3:6 “kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu”.
Lakini Agano la Damu ya Yesu ni Agano jipya, na la Mwisho, hakuna agano lingine litakalokuja katika haya maisha litakalokuwa timilifu zaidi ya hili. Kwamba kila amwaminiye Mwana wa Mungu (YESU KRISTO), anao uzima wa Milele, na anakuwa mrithi wa Baraka na ahadi za Mungu.
Kwahiyo ni muhimu sana kumpokea Yesu kila mmoja, ili tuweze kushiriki Baraka hizi za Agano jipya la Mungu.
Na damu ya Agano jipya, (yaani Damu ya Yesu), ina nguvu kuu ya kuvunja maagano yote, mtu aliyoingia na miungu, au shetani.. na kumwacha mtu kuwa huru kabisa kabisa.
Je umeingia ndani ya Agano la Damu ya Yesu?..
Kama bado, Mlango wa Neema bado upo wazi, lakini hautakuwa wazi hivyo siku zote, siku moja utafungwa na hakuna atakayeweza kuinga.. Kama unataka uzima, na kheri, basi mpokee Yesu, lakini kama hupendi uzima wala kheri basi baki kama ulivyo…
Waebrania 12:24 “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili. 25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni”
Waebrania 12:24 “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.
25 Angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa yeye aliyewaonya juu ya nchi, zaidi sana hatutaokoka sisi tukijiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni”
Watu wenye kuvunja maagano ndio watu wa namna gani? (Warumi 1:31)
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
EZEKIELI, ITABIRIE MIFUPA MIKAVU.
MJUMBE WA AGANO.
KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.
SHUSHANI NGOMENI NI WAPI KWA SASA?
Shalom, karibu tujifunze maandiko.
Kila ishara inayo sauti nyuma yake..Kwa mfano “tunapoona ishara ya mawingu kuwa meusi”..ujumbe au sauti uliopo nyuma ya hiyo ishara ni kwamba “muda si mrefu mvua inashuka”..Sasa sio kwamba mawingu yametoa sauti na kusema “mvua inakuja”..la! mawingu hayawezi kuongea.. lakini yametoa tu ishara, ambayo ndani ya hiyo ishara ipo sauti.
Hali kadhalika pia na kwa upande wa Mungu wetu, Sauti yake pia wakati mwingine ipo katika Ishara.. Mungu anaweza kuzungumza moja kwa moja tukaisikia sauti yake, lakini pia sauti yake anaweza kuiweka ndani ya ishara fulani, kwamba tutakapoona ishara hiyo, basi ni wajibu wetu kutambua sauti gani ipo nyuma ya hiyo ishara.
Na siku zote sauti ya Mungu ipo kwa lengo la kutufundisha, kutufariji na kutuonya!. Wengi Mungu kashazungumza nasi kwa njia ya Ishara..lakini hatujamsikia Mungu… Wengi tumeshaonywa sana kwa njia ya Ishara lakini hatujasikia..na huku tukidhani Mungu hajawahi kuzungumza nasi…
Neno la Mungu linasema..
Isaya 50:2 “Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu?…”
Umeona?..Kumbe Mungu huwa anatujia lakini hatujui kama ametujia, na huwa anatuita lakini hatusikii!..Ni kwanini?..ni kwasababu hatuijui Sauti ya Mungu.. Tukidhani kuwa ana njia moja tu ya kusema na sisi.
Hebu tumwangalie mtu mmoja katika biblia ambaye Mungu alizungumza naye kwa njia ya Ishara lakini aliipuuzia sauti ya Mungu, iliyokuwepo nyuma ya hiyo ishara.. Na mtu huyo si mwingine zaidi ya Mtume Petro.
Kuna wakati Bwana Yesu alimwambia Petro kuwa “kabla jogoo hajawika mara mbili atamkana mara tatu”..
Hebu tusome,
Marko 14:29 “Petro akamwambia, Hata wajapokunguwazwa wote, lakini siyo mimi 30 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu”.
Marko 14:29 “Petro akamwambia, Hata wajapokunguwazwa wote, lakini siyo mimi
30 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu”.
Hapo Bwana Yesu alimpa Petro “ishara ya jogoo” na akampa na “Sauti” moja kwa moja nyuma ya hiyo ishara, kwamba atamkana!. ..Angeweza kumwambia tu “leo utanikana” asimpe na ishara yoyote…lakini hapa utaona hapa Bwana Yesu anampa Petro “Ishara” na “sauti ya hiyo ishara”.
Na kweli wakati ulipofika, Petro akaanza kumkana Bwana Yesu, na pengine wakati anaanza tu kumkana kwa mara ya kwanza..papo hapo “Jogoo akawika”.. na Petro akamsikia Yule jogoo akiwika lakini hakutilia maanani…hakukumbuka kwamba Bwana alimwambia kabla ya jogoo kuwika atamkana!…
Hivyo kwa kuwika tu jogoo mara ya kwanza, ilitosha kumkumbusha Petro dhambi yake na kumfanya “atubu”..
Lakini Petro hakuizingatia hiyo sauti ya Mungu, iliyomwamsha roho yake atubu… badala yake akaendelea na dhambi yake!.. akaendelea kumkana Bwana tena kwa mara nyingine ya pili na ya tatu!.. Lakini kwasababu Bwana ni wa rehema, akairudia tena ishara ile ile, ya jogoo kuwika mara nyingine ya pili..
Na jogoo alipowika mara ya pili, ndipo akili zikamrudia Petro, na kutafakari..na kugundua dhambi yake ambayo tayari ameshairudia mara tatu..Na ndipo akaenda kutubu!..lakini kama asingeisikia sauti ile nyuma ya ile ishara, huenda angeendelea kumkana Bwana zaidi na zaidi na madhara yake yangekuwa makubwa mbeleni.
Umeona hapo!.. tafsiri rahisi ya kisa hicho ni kwamba.. kipindi Petro anaanza kumkana Bwana, Mungu alimtumia jogoo kumwambia Petro, “Acha Hicho unachokifanya”…usimkane Bwana!.. lakini hakusikia, “Yeye alidhani ni mlio wa jogoo tu”…Bwana akarudia tena kwa mara nyingine..Acha!..Sauti iliyotoka ni ya jogoo, lakini katika ulimwengu wa roho ni Mungu anasema acha!, ndipo Petro akapata akili.
Sasa kama Mungu alimtumia jogoo kumwonya Petro, unadhani ni mara ngani katumia watu au wanyama na viumbe kuzungumza nasi?..kutuonya tubadili njia zetu?, tutubu dhambi zetu? Tufanye hiki au kile?..
Je unadhani tukikataa leo kutubu na kulitii Neno lake siku ile tutakuwa na udhuru wowote!..je unadhani siku ile tutakuwa na cha kujitetea kwamba Bwana hajawahi kusema nasi?..Siku ya hukumu utaona ile miti uliyokuwa unadhani ni miti tu, kumbe ilikuwa ni sauti ya Mungu kwako, siku ile utaona ule ugonjwa uliokuwa unakurudia mara mbili mbili ulikuwa ni sauti ya Mungu kwako…
Siku ile utaona wale wanyama waliokuwa wanashambulia mazao yako ni sauti ya Mungu kwako,..siku ile utaona kumbe hata wale wezi waliokuibia na wale matapeli waliokudhulumu, ni Mungu alikuwa anazungumza na wewe,…. na utajuta na kusema laiti ningeisikia ile sauti na kutii!!, na wakati huo utakuwa umeshachelewa.
Na tabia ya Mungu ni kuwa “sauti yake imejificha katika vitu vinyonge tunavyovidharau sisi”… Sauti yake aliificha nyuma ya mlio wa jogoo, kwa Petro, vile vile utasoma pia kuna wakati punda aliweza kusema maneno ya Mungu mbele ya Balaamu.. Vivyo hivyo kamwe tusitegemee kuisikia sauti ya Mungu katika mambo makubwa, yeye anatumia hata vitu vinyonge kusema na sisi..
Bwana Yesu atusaidie tuitii sauti ya Mungu, iliyopo nyuma ya kila ishara yake.
Maran atha!
TEGEMEA MUNGU KUZUNGUMZA NAWE KATIKA MAMBO MADOGO
SAUTI NYUMA YA ISHARA.
ISHARA ITAKAYONENEWA
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
Nini maana ya “Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika”. Kwanini Bwana Yesu apigwe? Na kwanini kondoo wake watawanyike!… Na je! Anayempiga ni nani?.
Tusome,
Mathayo 26:31 “Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika”
Bwana Yesu alipigwa na Mungu, lakini si kwasababu ya makosa yake, (yeye hakufanya dhambi hata moja, hakufanya kosa hata moja)…Lakini lakini ni kwasababu gani alipigwa??.. ni kwaajili yetu sisi..
Kumbuka Bwana Yesu hakuja kuiondoa adhabu, ambayo tayari ilikuwa imeshatolewa juu yetu..bali alikuja kuichukua adhabu.. Kwasababu kama ingekuwa kaja kuiondoa adhabu, basi hata yeye asingepanda msalabani(asingeadhibiwa)...Adhabu juu yetu tayari ilikuwa imeshatolewa, na ilikuwa ni lazima itekelezeke(Imfikie mlengwa).. Ni sawa na mtu akutupie jiwe kutoka mbali, na jiwe lile likiwa hewani, ghafla anatokea mtu anakaa mbele yako ili lile jiwe lisikupate wewe bali limpate yeye!..
Sasa kiuhalisia mtu huyo kakuokoa wewe na madhara ya jiwe lile, lakini hajaondoa madhara ya lile jiwe..au hajazuia jiwe lile lisirushwe kutoka kwa aliyerusha!!..Ni lazima limpate tu!..yeye kachukua tu maumivu yako, maana yake atachubuka yeye badala yako wewe, ataumia yeye badala yako wewe, atapigwa yeye badala yako wewe.. Mlengwa ulikuwa ni wewe, lakini yeye kajitokeza katikati ya safari ili yeye aumie wewe upone.
Ndicho Bwana YESU alichokuja kukifanya.. si kuondoa Adhabu iliyokwisha kutamkwa juu yetu na Mungu, si kuondoa laana iliyokwisha kutamkwa juu yetu, si kuondoa dhiki na mateso na masikitiko yaliyokwisha kukusudiwa juu yetu tangu siku ile pale Edeni, bali ni kuyachukua yeye hayo masikitiko, kuyachukua yeye hayo maumivu, kuyabeba yeye hayo mapigo..
Ndio maana maandiko yanasema…
Isaya 53: 4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; LAKINI TULIMDHANIA YA KUWA AMEPIGWA, AMEPIGWA NA MUNGU, NA KUTESWA. 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, NA KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA”.
Isaya 53: 4 “Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; LAKINI TULIMDHANIA YA KUWA AMEPIGWA, AMEPIGWA NA MUNGU, NA KUTESWA.
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, NA KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA”.
Umeona hapo?.. Tulipomwona kaangikwa msalabani, tulidhania kuwa Mungu kamwadhibu kwa makosa yake..Kumbe sio!.. Mungu shabaha yake ilikuwa ni kwetu sisi wala si kwake..lakini yeye akajitokeza kuyapokea yale mapigo!..Hivyo ni sawa na kusema KAPIGWA NA MUNGU KWA MAPIGO AMBAYO SI YAKE!!
Kwahiyo alipopigwa namna hiyo na MUNGU kwa mapigo ambayo si yake.. Kwa kitambo kidogo, dunia ilikaa kimya!.. Wanafunzi wake (na wafuasi wake), walitawanyika kwasababu Mchungaji hayupo, walibaki bila mchungaji kwa kipindi cha siku tatu!..walikaa kwa huzuni na maombolezo wakati dunia inafurahia…Lakini baada ya kitambo kifupi, Bwana Yesu alipofufuka, ndipo wakakusanywa tena..
Yohana 16:19 “Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, BADO KITAMBO KIDOGO NANYI HAMNIONI, NA TENA BADO KITAMBO KIDOGO NANYI MTANIONA? 20 Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha”.
Yohana 16:19 “Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, BADO KITAMBO KIDOGO NANYI HAMNIONI, NA TENA BADO KITAMBO KIDOGO NANYI MTANIONA?
20 Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha”.
Hiyo ndio sababu ya Bwana Yesu kusema haya maneno…
Mathayo 26:31 “Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, NITAMPIGA MCHUNGAJI, NA KONDOO WA KUNDI WATATAWANYIKA”
Mungu alimpiga Bwana Yesu kwa kosa lisilo lake pale Kalvari, na kondoo wakatawanyika kwa kitambo..
Hivyo mimi na wewe baada ya kujua haya, na Mhanga, Bwana wetu Yesu Kristo aliouingia kwaajili yetu, basi tutazidi kuuheshimu wokovu wetu kuliko kawaida..
Tunapotafakari kuwa tulipaswa tufe katika huzuni, katika tabu na baada ya hapo tutupwe katika ziwa la moto milele, lakini Bwana Yesu kaja kutuzuilia hilo, kwa kuchukua yeye laana zetu..basi tunajikuta tunakuwa wanyenyekevu mbele zake, na kuzidi kumheshimu Mungu katika maisha yetu, na kudumu katika Imani na utakatifu, na usafi.
Bwana Yesu atusaidie tuzidi kuuthamini msalaba!.
JE! UNAMPENDA BWANA?
Gongo na Fimbo ni nini? Na vinawezaje kumfariji mtu? (Zaburi 23:4).
NI LIPI KATI YA MAKUNDI HAYA, WEWE UPO?
UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.
Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma.
SWALI: Shalom. Naomba kufahamu nifanye nini ili niweze kuishinda ile dhambi inayonitesa.?
JIBU: Dhambi inayomtesa mtu kwa jina lingine inaitwa “dhambi izingayo kwa upesi”, ambayo tunaisoma katika;
Waebrania 12:1
[1]Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,
Si kila dhambi, huwa inaondoka kirahisi ndani ya mtu pindi anapookoka..
Ni kweli asilimia kubwa ya dhambi mtu anajaliwa na Roho Mtakatifu kuziacha wakati ule anapotubu, na kudhamiria kumfuata Yesu kwa moyo wake wote, kwamfano mwingine alikuwa ni mwizi, mwongo, mshirikina, mzinzi n.k.
Lakini alipookoka hivi vyote akaviacha kiwepesi kabisa..Lakini ndani yake kukawa na shinikizo kubwa la kuendelea kufanya punyeto, au mawazo machafu kumtawala..hivyo hiyo hali ikawa inamtesa kwa kipindi kirefu na kumfanya akose raha, wakati mwingine amejaribu kuomba sana lakini hali ipo vilevile.
Mwingine hayo yote ameweza kuyashinda lakini dhambi ya usengenyaji imekuwa ni mzigo mzito sana kwake kuutua, mwingine ulevi, mwingine kutazama picha za ngono n.k.
Ndugu ikiwa umeokoka na unaona hiyo dhambi ni kikwazo kikubwa kwako, nataka nikuambie huna budi kushindana nayo hadi uishinde..kwasababu usipoishinda itakupeleka jehanamu.
Kaini alikuwa na dhambi ya hasira na wivu, akaipuuzia, lakini Mungu akamwambia, unapaswa uishinde
Mwanzo 4:6-7
[6]BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? [7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
[6]BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
[7]Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
Dhambi kama hizi huwa zilishatia mizizi mrefu ndani ya mtu tofauti na nyingine, hivyo kuziondoa inahitaji nguvu ya zaida..
Na njia pekee ya kuzishinda hizi ni moja tu nayo ni “kwa Kuua vichocheo vyote vinavyokupelea kuitenda dhambi hiyo”..
Mithali 26:20 Inasema;
“Moto hufa kwa kukosa kuni;..”
Moto hauwezi kuendelea muda mrefu mahali ambapo hapana kichocheo chake kama kuni au mafuta..haijalishi utakuwa na nguvu kiasi gani, mwishowe utazima tu.
Hakuna dhambi yoyote iliyo ngumu kuishinda hapa duniani endapo vichocheo vyake vitauliwa kikamilifu.
Kwa mfano kufahamu ni jinsi gani utaweza kuishinda dhambi ya uzinzi fungua hapa..>>> MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
Kwa siku za mwanzo, utaona ni shida lakini kwa jinsi siku zinavyozidi kwenda Mungu anakutia nguvu na hatimaye inakuwa ni dhambi nyepesi sana kuishinda kuliko hata zote…
Ni kawaida hata gari lililo katika mwendo kasi likichuna breki kwa ghafla, haliwezi kusimama hapo hapo…litasogea mbele kidogo, ndipo litulie japokuwa tairi tayari zilishaacha kuzunguka, kitambo kidogo.
Vivyo hivyo na wewe katika hiyo dhambi inayokuzinga kwa upesi, inayokufanya usipige mbio kwa wepesi, katika safari yako ya ukristo, kwa siku za mwanzoni itaonyesha kama kuleta ukinzani lakini kwa jinsi unavyokaa mbali na vichocheo vyake hatimaye itakufa tu ndani yako…ni kitendo cha muda.
Kwamfano kama wewe ni mvuta sigara, kiu ya kuvuta ikija, ondoka mazingira ya upatikanaji wake, vilevile wale marafiki uliokuwa unavuta nao jitenge nao waone kama kaburi, hicho kiu kitakutesa tu kwa muda mfupi, lakini uking’ang’ana utakuja kushangaa kimetoweka tu ghafla..hapo ndio tayari kimekufa..
Shindana, hadi ushinde…usikubali kusema mimi nimeshindwa kuacha hiki au kile, usikubali hiyo hali, usiwe mnyonge wa dhambi, kwasababu wanyonge wote hawataurithi uzima wa milele biblia inasema hivyo katika Ufunuo 21:27
Ikiwa ni fashion, wewe kama mwanamke ni lazima uishinde, ikiwa ni kamari, ikiwa ni miziki ya kidunia kanuni ni hiyo hiyo…Ua vichocheo vyote. Kaa mbali nayo, ulizoea kutazama picha za ngono mitandaoni, na ulipookoka mawazo yale yanajirudia rudia kwenye fahamu zako, endelea kukaa mbali na vichocheo hivyo, acha mazungumzo mabaya, left magroup yasiyokuwa na msingi kwako, epuka kutazama au kusikiliza kitu chochote chenye maudhui ya uzinzi, marafiki wazinzi waepuke, marafiki wasiokuwa na maana wa jinsi tofauti wapeuke, utafika wakati hayo mawazo machafu yatakukimbia..
Zingatia hayo, na matokeo utayaona.
JINSI YA KUSOMA BIBLIA.
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 5)
YAFUATAYO NI MAWAZO YA ADUI HIVYO USIYASIKILIZE.
CHUKIZO LA UHARIBIFU.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.
JE! NINAWEZA KUPOTEZA FURAHA YA WOKOVU?
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe. Karibu tujifunze Biblia.
Je!, wewe ni Mwanamke?..kama ndio! basi fahamu kuwa upo katika hatari kubwa ya kuingiwa na roho za mapepo kuliko mwanaume!.
Hebu tutafakari mstari ufuatao, na kisha tujiulize maswali machache!.
1Timotheo 2.11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. 12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. 13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
1Timotheo 2.11 “Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
13 Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
14 WALA ADAMU HAKUDANGANYWA, ILA MWANAMKE ALIDANGANYWA KABISA AKAINGIA KATIKA HALI YA KUKOSA”.
Hapo katika mstari wa 14, anasema “ADAMU HAKUDANGANYWA, ILA HAWA ALIDANGANYWA KABISA AKAINGIA KATIKA HALI YA KUKOSA”.
Maana yake pale Edeni, “Adamu hakudanganywa kabisa”…Adamu alikuwa anajua anachokifanya, alikubali kula lile tunda alilolipokea kutoka kwa mke wake, akiwa na akili timamu na..akijua kabisa lile ni kosa!..lakini Hawa alikuwa hajui chochote, yeye aliamini kile alichoambiwa na Nyoka ni ukweli mtupu!.hivyo alidanganywa na shetani..
Hiyo ikifunua kuwa kuna “KUNA UDHAIFU MKUBWA SANA KATIKA JINSIA YA KIKE”.
Utakumbuka tena, kipindi mfalme Sauli, alipoachwa na Mungu, kitu cha kwanza alichofikiria kukifanya ni kumtafuta mwanamke mwenye pepo la utambuzi katika nchi yake ile?
1Samweli 28:6 “Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, NITAFUTIENI MWANAMKE MWENYE PEPO WA UTAMBUZI, NIPATE KUMWENDEA NA KUULIZA KWAKE. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. 8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako”.
1Samweli 28:6 “Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.
7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, NITAFUTIENI MWANAMKE MWENYE PEPO WA UTAMBUZI, NIPATE KUMWENDEA NA KUULIZA KWAKE. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.
8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako”.
Jiulize hapo ni kwanini aseme “NITAFUTIENI MWANAMKE MWENYE PEPO, NA SI MWANAUME mwenye pepo la utambuzi”?.. Si kwamba wanaume wachawi hawakuwepo, walikuwepo!… Lakini Sauli alijua kuna utofauti wa Mwanaume mwenye pepo, na Mwanamke mwenye pepo!… Alijua mwanamke mwenye pepo, anakuwa na pepo kweli kweli!..tofauti na mwanaume!.
Utaona tena kipindi akina Paulo wapo kule Filipi, walikutana na Mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, ambaye alikuwa anawatabiria watu na kuwapatia faida mabwana zake..
Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, KIJAKAZI MMOJA ALIYEKUWA NA PEPO WA UAGUZI AKATUKUTA, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua. 17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu. 18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile. 19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji”.
Matendo 16:16 “Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali, KIJAKAZI MMOJA ALIYEKUWA NA PEPO WA UAGUZI AKATUKUTA, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.
17 Akamfuata Paulo na sisi akipiga kelele, akisema, Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye juu, wenye kuwahubiria njia ya wokovu.
18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
19 Basi bwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limewapotea, wakawakamata Paulo na Sila, wakawakokota mpaka sokoni mbele ya wakuu wa mji”.
Umeona?.. Ukizidi kujifunza biblia utakutana na maandiko yanayosema “Usimwache mwanamke mchawi kuishi (Kutoka 22:18)”… Jiulize ni kwanini inataja mwanamke na si mwanaume?…Sio kwamba haijawaona wanaume ambao ni wachawi!.. walikuwepo wanaume wachawi wengi, lakini kundi la wanawake ndilo lililokuwa limezama zaidi na ndilo lilikuwa hatari..
Sio ajabu kwanini unaona hata leo hii,..Wanawake ndio wanaoongoza kulipuka mapepo!. Hiyo ni kutokana na kwamba, ni rahisi kufungua milango ya roho zao zaidi ya wanaume!.
Maana yake ni kwamba…Kila kitu chochote kinachokuja mbele wanawake wengi ni rahisi kukiamini, pasipo kukifanyia uchunguzi wa kutosha, kila wazo linalokuja ni rahisi kulipokea bila kulifanyia uchunguzi wa kutosha, kila fundisho linalokuja ni rahisi kuliamini pasipo kulifanyia uchunguzi wa kutosha…mwisho wa siku wanajikuta wanaingiwa na roho nyingi zidanganyazo, na wanatumika na roho nyingi, pasipo wao wenyewe kujijua..
Mwanamke, si kila wazo linalotoka kwa Mume wako ni la kulipokea pasipo kulitafakari kwa kina, si kila fundisho ni la kuliamini pasipo kulichunguza mara mbili mbili.. Fahamu kuwa wewe ni lango kubwa na la kwanza dhaifu, ambalo shetani analitazama zaidi ya wanaume. Wanawake wengi wa siku hizi za mwisho ni wavivu wa kuyatafakari maandiko kwa kina.. ingawa sio wote!, lakini asilimia kubwa wapo hivyo, na pasipo kujijua kuwa wao ndio ndio windo kubwa na la kwanza la mapepo na roho zote za mashetani zaidi ya wanaume!..
Asilimia kubwa ya wanapenda kufuata mambo au kuamini mambo kwa kusikia tu!.. Kwa mfano kukizuka jambo Fulani ambalo linawafuasi wengi, wanawake wengi ni rahisi kuamini jambo hilo na kulifuata, pasipo kulichunguza kwa kina, au kulifuatilia..na huko huko ndiko wanakojikuta wameshafungua milango ya maroho ya mapepo ndani yao, bila wao wenyewe kujijua.
Baada ya kujijua kuwa wewe ni windo la roho za mapepo zaidi ya jinsia nyingine basi huna budi kuchukua tahadhari kubwa sana juu ya maisha yako, kwa kufanya jambo lifuatalo!.
JARIBU MAMBO YOTE.
Maandiko yanasema katika kitabu cha 1Wathesalonike 5:21 “ jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema”.. Hapo anasema “jaribuni” pasipo kuonyesha jinsia,.. ikiwa na maana kuwa ni jukumu la jinsia zote “kujaribu mambo”.. Na sio kujaribu jambo moja tu bali “ kujaribu yote”.. Hata ushauri unaopewa na mtu wa kazini kwako, huna budi kuujaribu, hata habari unayoletewa na rafiki yako, huna budi kuijaribu!!..Hata habari unayoisikia katika redio au Tv, ijaribu..
1Yohana 4:1 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”.
Kwanini tunajaribu kila kitu tunachokisikia?? Kwasababu “MANENO” ni “roho”..kila maneno tunayoyasikia yana roho ndani yake.. Hata Neno la Mungu ni Roho wa Mungu..tunaposikia maneno ya Mungu, maana yake tunampa nafasi Roho wa Mungu kusema ndani yetu. Sasa Utasema hilo tunalithibitisha vipi?..
Yohana 6:63 “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; MANENO HAYO NILIYOWAAMBIA NI ROHO, tena ni uzima”.
Umeona?.. Bwana Yesu anasema, maeneno ninayowaambia ni ROHO.. kadhalika tunaposikiliza mambo mengine nayo pia ni roho. Ndio maana hatuna budi kujaribu kila kitu tunachokisikia.. kama Bwana alivyosema katika..Luka 8:18 “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo….”
Na tunayajaribu mambo kupitia nini?… Si kingine zaidi ya NENO LA MUNGU.
Biblia ndio Hadubini ya maisha yetu.. ndio kipimo cha mambo yote..Maana yake kama hupendi kujifunza biblia, kamwe hutaweza kuzipima roho, kama hujizoezi kujifunza biblia mwenyewe bila kusubiria kufundisha fundisha kila mara, kamwe hutaweza kuzijaribu roho kama zinatokana na Mungu au la!..Kama wewe ni wa kusubiria tu makala Fulani iachiwe usome, au mahubiri Fulani uyasikilize, ni wa kupenda kuletewa letewa tu!…wewe mwenyewe biblia unaiona ngumu fahamu kuwa wewe ni windo bora la mapepo!.
Mwanafunzi anayeona masomo ni magumu, siku zote ni Yule ambaye hapendi kusoma, bali yule anayependa kusoma anapoona mada ni ngumu, basi anafanya bidii kupambana mpaka aielewe…na kamwe hawezi kuona masomo ni magumu… vile vile na wewe kama unaona biblia ni NGUMU miaka nenda rudi!.. Basi huo ni uthibitisho kuwa wewe si mwanafunzi wa biblia, hujawa serious!!.. ndio maana inakuwa ni ngumu kwako!.. miaka na miaka.
Hivyo kama wewe ni mwanamke, kumbuka haya, na fahamu kuwa mapepo yanakutafuta wewe zaidi zaidi ya jinsia nyingine, hivyo huna budi kuongeza umakini katika kujilinda na hizo roho.. lakini kama hutaongeza umakini kwa kuamua kujifunza BIBLIA kwa kina!!, na kupima mambo yote!!! Basi jua kuwa roho za mapepo zitakusumbua daima..na mapepo mengine yatakuingia pasipo wewe kujua, lakini utakuja kuona madhara yake baadaye sana.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
ONDOKA YESU, TUACHIE MAPEPO.
NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?
MFANYE BWANA YESU MWENYEJI MAISHANI MWAKO.
Tunaishi katika ulimwengu ambao, maadili yameporomoka sana, na bado yanaendelea kuporomoka kwa vijana na watoto..Na hiyo inatufanya tuelekeze lawama kwa watoto; tukisema watoto wa siku hizi wamebadilika sana, lakini ukweli ni kwamba wazazi ndio wamebadilika, watoto ni walewale.
Malezo ya mzazi kwa mtoto ni muhimu sana, mtoto si kama nyau, ambaye kitu pekee anachohitaji ni chakula tu na sehemu ya kulala, hata ukimwacha mwaka mzima bila kumjali kwa vingine, hakuna hasara yoyote, bado ataendelea kuwa paka..
Lakini kwa mwanadamu sivyo..yeye hafugwi, bali analelewa..na malezi ni zaidi ya chakula na nguo na mahali pa kulala.. Hapo ndipo wazazi wengi wanashindwa kuelewa.
Kwasababu mtoto atahitaji kuwa na maarifa, nidhamu, uadilifu, hekima, busara, upendo, utiifu, upambanuzi n.k. Ili aweze kuishi vema katika huu ulimwengu.
Hivi vyote hazaliwi navyo, bali anajifunza anapokuwa duniani..hivyo akikosa msaada sahihi, basi ibilisi atatumia fursa hiyo kumfundisha elimu yake na nidhamu yake hapa ulimwenguni.
Hivyo wewe kama mzazi au mlezi una jukumu kubwa sana zaidi ya lile la kumlisha na kumvisha na kumsomesha..hizo ni hatua 3 katika ya 1000, anazopaswa azijue.
Ikiwa hukupata masomo yaliyotangulia ya malezi ya watoto, basi waweza kututumia ujumbe kwa namba hii, ili tuweze kukutumia chambuzi za nyuma. Au tembelea website yetu hii www.wingulamashahidi.org. au tutumie ujumbe kwa namba hizi +255693036618
Leo tutaona njia nyingine ya kumlea mtoto vema.
Na njia yenyewe si nyingine zaidi ya kutumia KIBOKO.
Lugha hii inaweza isiwe nzuri masikioni mwa wazazi lakini ni tiba nzuri kwa malezo yao. Hata ‘panadol’ haina ladha nzuri mdomoni, lakini pale inapotutibu tunaishukuru, ndio maana tunayo siku zote majumbani kwetu.
Lakini ni kwanini utumie kiboko kwa mtoto?
Sababu zipo mbili.
Mithali 22:15
[15]Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.
Ni vizuri ukafahamu kuwa mtoto kama mtoto huwa ana ujinga mwingi ndani yake..yule si kama wewe, unapoona anang’ang’ania kitu fulani kisichopendeza halafu wewe kama mzazi unaamua tu kumwachia kisa anakililia, usidhani kuwa anaelewa matokeo ya kile anachokitaka..
Kumbuka yule hatafakari, wewe unatafakari, hivyo basi ukimsikia anatukana, usisubiri apumzike bali hapo hapo shika kiboko chapa. Ukiona unamwagiza kitu hatii, chapa..ukiona hawaheshimu watu wazima hata baada ya kuonywa mara nyingi..chapa..usiogope labda atakufa…biblia inasema kiboko cha adili hakiui..
Mithali 23:13
[13]Usimnyime mtoto wako mapigo; [14] Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Hiyo itamsaidia sana kuundoa ujinga mwingi wa kipepo ambao mwingine kwa maneno tu, peke yake au kwa kufundishwa hauwezi kutoka..
Na sababu ya pili kwanini tuwaadhibu watoto wetu kwa kiboko pale wanapokosea..ni kwasababu Mungu naye anatuadhibu sisi watoto wake.
Biblia inasema hivyo..
Waebrania 12:6-7
[6]Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. [7]Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
[6]Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
[7]Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
Umeona..Sisi hatuna hekima ya kumzidi Mungu, tengeneza picha Bwana angekuwa anatuona tunatukana wengine halafu hachukui hatua yoyote anacheka tu..si tungaangamia..Mungu alipomuona Daudi anamchukua mke wa Huria halafu anaendelea kusema wewe ni mtumishi wangu unayeupendeza moyo wangu..Daudi leo angekuwa wapi kama sio kuzimu? Lakini Mungu alimuadhibu vikali…na baadaye akatubu akapona..
Nasi pia biblia inatuambia tutakuwa wakamilifu kama Baba yetu wa mbinguni alivyomkamilifu..(Mathayo 5:48)
Mzazi unayemtazama mwanao, anafanya ujinga, unaogopa kumchapa atalia..bado hujawa mkamilifu kama Mungu.
Hivyo anza sasa kutimiza huduma hii, ili kesho mtoto huyo afanyike baraka na neema kwa ulimwengu.
Lakini zingatia: Haimaanishi kuwa umpige pige mtoto ovyo kila saa anapokosea..hapana zipo sehemu zinastahili kiboko, zipo zinazostahili maonyo, zipo zinazostahili kuelimishwa..Zote zina umuhimu wake mkubwa bila kupuuzia hata moja.
Bwana akubariki
Shalom
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
KILEMBA CHA NEEMA, JE! UMEMVIKA MWANAO?
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
NI NINI KINATOKA KINYWANI MWA MTOTO WAKO?
MALEZI YA MTOTO MCHANGA.
Wokovu na furaha ya wokovu ni vitu vinavyokwenda sambamba, palipo na wokovu ni lazima na furaha ya wokovu pia iwepo, vikipishana kidogo, basi ni tatizo kubwa sana ni sawa na chakula kilichokosa chumvi, utakula tu, ili kujaza tumbo lakini hutakifurahia hata kidogo,
Wakristo wengi sasa wameupokea wokovu, lakini , si wote wanayo furaha ya wokovu. Kuwepo katika wokovu ni suala ambalo unapaswa ufurahie, (U-enjoy), kama vile ufurahiavyo maisha ya utajiri. Lakini kama hilo jambo halipo ndani yako sasa, basi kuna tatizo kubwa.
Kuna kipindi ulikuwa unajihisi furaha, na amani na wepesi ndani ya wokovu, haukujali ni magumu kiasi gani unapitia, lakini sasa unajiona kama hiyo raha haipo tena, wokovu unakuwa kama vile wa kujilazimisha, upo tu, unasogeza siku ilimradi, kesho ije.Leo tutatazama, ni vitu gani vya kuzingatia kama mkristo, ili uweze kuirejesha ile furaha ya wokovu uliyoipoteza. Na kama hujawahi pia kuwa nayo basi zingatia kanuni hizi muhimu.
Daudi hakuwahi kupoteza furaha ya wokovu maisha yake yote, isipokuwa siku alipofanya dhambi ya makusudi, ya kuzini na mke wa askari wake (Huria), mwanzoni alidhani ni jambo jepesi tu, lakini aliponaswa katika huo mtego, alikaa muda mrefu sana, bila furaha ya wokovu, japokuwa alishasamehewa hiyo dhambi na Mungu..
Yeye ndio aliyeandika Zaburi ya 51, na katika dua zake alimwomba Mungu amrejezee furaha ya wokovu aliyoipoteza zamani.
Zaburi 51:12 “Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi”.
Nawe pia ikiwa umeokoka, halafu unaendelea kutenda dhambi, furaha hii itaondoka ndani yako, na ukristo wako utakuwa ni mzito na mgumu sana, pengine hata baada ya kutubu. Hivyo kaa mbali na dhambi.
Mahali pekee ambapo pana matumaini, faraja, nguvu ya kuendelea mbele, basi ni katika Neno la Mungu. Kama mkristo ukiwa mvivu wa kuchukua biblia yako na kusoma kila siku, huwezi kusonga mbele katika hii safari ya imani.
Kwamfano katika biblia utamsoma Ayubu, katika majaribu yake, utamsoma Ibrahimu na Sara katika kusubiri kwao, utamsoma Henoko na Eliya katika ukamilifu wao, utajifunza uvumilivu, saburi, upendo, amani, utasoma shuhuda mbalimbali za waliotendewa maajabu na Yesu n.k. Hivyo kwa maarifa hayo, ni ulinzi tosha kwako, wa kuufurahia wokovu wako.
Lakini ukiwa ni mkavu ndani, hapo ndipo ibilisi atakujaza biblia yake, ya hofu ya maisha, mashaka, wasiwasi, huzuni, wivu, chuki n.k.Penda Neno la Mungu kama upendavyo chakula.
Mithali 3:1 “Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu”.
Katika eneo ambalo hupaswi kuwa mvivu nalo basi ni hili, hapa shindana na mwili, ukikosa kuwa mwombaji, Kama Yesu alivyosema, Kesheni mwombe msije mkaingia majaribuni (Mathayo 26:41).. Ni kweli kabisa majaribu yasiyokuwa na msingi yatakukuta, na hivyo utakuwa unaishi kila siku maisha ya kujikwaa kwaa..
Ibada ni muhimu sana kwa mkristo, ikiwa umeokoka halafu huna desturi ya kuhudhuria ibadani, kujumuika na watakatifu wengine, utaikosa furaha ya wokovu wako..Bwana alisema..
Waebrania 10:25 “wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia”.
Pia maandiko yanasema..
Mithali 27:17 “Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake”.
Vipo vitu ambavyo utavipata kwa juhudi zako mwenyewe, lakini vipo ambavyo utaongezewa na wengine, kuna mahali utaishiwa nguvu, mwingine atakushika mkono hata tu kwa karama yake. Binafsi nimeona nikitengenezwa ukristo wangu kwa sehemu kubwa sana nilipokuwa na wengine, zaidi ya nilivyokuwa mwenyewe.
Ibadani pia ni mahali ambapo, utapata fursa ya kumwimbia na kumwabudu Mungu, kwa nafasi na uhuru zaidi kuliko mahali ulipo mwenyewe. Na ukikosa ibada ya Sifa, pia furaha ya wokovu haiwezi kumiminika ndani yako.Sifa huponya mioyo yetu. Huondoa uchungu na mizigo yetu,.Jaribu kudumu muda mrefu katika sifa, utaona badiliko kubwa sana moyoni mwako.
Ukiridhika na hiyo hiyo hali ya kiroho muda mrefu, tatizo hili ni lazima likukute.. lilishawahi nikuta mimi, na likanisumbua sana.. Embu tengeneza picha mtoto ameshafikisha miaka 5, bado anategemea tu, maziwa ndio yawe chakula chake, Je! atafurahia chakula hicho kama alivyokuwa na miezi 5?, jibu ni la, kinyume chake ndio atadhoofika.
VIvyo hivyo na wewe ikiwa umeokoka, na kitambo sasa kimepita, hakikisha kila siku unapiga hatua mpya, katika kujifunza, kuacha dhambi, na zaidi sana, kushuhudia habari njema kwa walio nje.Moja ya mambo ambayo yananipa furaha moyoni ya wokovu, ni pale napoona siku yangu haijapita bure bure bila kufanya kitu fulani kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Lakini nikipitisha muda fulani mrefu, nipo nahangaika hangaika tu na mambo ya kiulimwengu, huwa furaha hiyo inapotea kabisa, najiona kama Roho Mtakatifu ameniondoka.
Hivyo wewe kama mkristo hakikisha, kila siku unapiga hatua, anza kuwahubiria na wengine na bila shaka utaufurahia mwenyewe wokovu wako.
Hivyo katika mambo hayo matano (5), angalia ni wapi umezembea, kisha uchukue hatua nyingine ili usife kiroho, kwasababu ukiendelea nayo hiyo hali muda mrefu hatma yake itakuwa ni kurudi nyuma au kufa kiroho kabisa. Kubali kuanza upya na Bwana.Kumbuka tatizo sio wokovu wetu, tatizo lipo katika mienendo yetu.Bwana atusaidie.
Furaha ni nini?
IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.
KIFO CHA MTAKATIFU POLIKAPI (Policarp).
Nini maana ya wokovu watoka kwa Wayahudi? (Yohana 4:22)
Nini maana ya ombeni kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi wala siku ya sabato?.
VIPINDI VINNE VYA MAISHA VILIVYO VIGUMU MTU KUMKUMBUKA MUUMBA WAKE.
Swali: Je! Roho Mtakatifu anaweza kuondoka juu ya Mtu?.Kulingana na Zaburi 51:11?
Zaburi 51:11 “Usinitenge na uso wako, Wala Roho yako mtakatifu usiniondolee“.
Jibu rahisi la swali hili ni ndio!, anaweza kuondoka juu ya mtu, na mtu akabaki kama alivyo…
Mfano wa mtu katika biblia ambaye aliondokewa na Roho Mtakatifu juu yake ni Mfalme Sauli.
1Samweli 16: 14 “Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua. 15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua”
1Samweli 16: 14 “Basi, roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua.
15 Nao watumishi wa Sauli wakamwambia, Angalia, sasa roho mbaya kutoka kwa Mungu inakusumbua”
Na sababu pekee iliyosababisha Roho wa Mungu kuondoka juu ya Sauli ni tabia ya Sauli ya kutokujali na vile vile kutoyatii maagizo ya Mungu, na kumdharau.
1Samweli 15:22 “Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu”. 23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”.
1Samweli 15:22 “Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu”.
23 Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme”.
Na madhara ya mtu aliyempoteza Roho Mtakatifu, ni KUONDOKEWA NA FADHILI ZA MUNGU JUU YA MAISHA YAKE.
Sauli aliondokewa na Fadhili za Mungu, baada tu ya Roho wa Mungu kuondoka juu yake..
2Samweli 7:14 “Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu; 15 LAKINI FADHILI ZANGU HAZITAMWONDOKA, KAMA VILE NILIVYOMWONDOLEA SAULI, niliyemwondoa mbele yako”.
2Samweli 7:14 “Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu;
15 LAKINI FADHILI ZANGU HAZITAMWONDOKA, KAMA VILE NILIVYOMWONDOLEA SAULI, niliyemwondoa mbele yako”.
Mtu aliyeondokewa na Fadhili za Mungu, anakuwa anaipoteza ile Amani ya KiMungu kipindi amempokea Roho, hali kadhalika ile furaha ambayo ilikuwa ndani yake inapotea!..ile raha aliyokuwa anaipata alipokuwa ndani ya wokovu, inapotea!…Ule utulivu aliokuwa anaupata kipindi Roho yupo juu yake, unapotea….kile kibali alichokuwa nacho kipindi cha mwanzo kinaondoka..anakuwa ni mtu wa kuhangaika, na kusumbuliwa na roho chafu za wivu, hasira, uchungu, na nyinginezo, kama ilivyokuwa kwa Sauli.
Maandiko yanasema Roho wa Mungu alipomwacha tu Sauli, pale pale roho mbaya ikaanza kumsumbua…akaanza kumwonea wivu Daudi, akaanza kuwa mkatili kwa kuwaua makuhani wa Mungu..
1Samweli 22:11 “Ndipo mfalme akatuma watu waende kumwita Ahimeleki, kuhani, mwana wa Ahitubu, na jamaa yote ya baba yake, hao makuhani, waliokuwako huko Nobu; nao wakaenda kwa mfalme wote pia”.
Hizo ndizo hasara za kumpoteza Roho Mtakatifu.. Mfalme Sauli alipoasi, Fadhli za Mungu zilimwondoka, na akawa mtu wa kukosa amani, furaha, kujiamini, na wivu…
Lakini kumbuka pia, kuondokewa na Roho Mtakatifu si kuacha kunena kwa lugha, au kufanya miujiza, au kutoa pepo. Mtu aliyeondokewa na Roho Mtakatifu bado anaweza kutoa pepo, bado anaweza hata kunena au kwa lugha..
Kwasababu matunda ya Roho Mtakatifu ndani ya mtu sio Kunena kwa lugha, au kutabiri, au kuona maono, bali ni yale yanayotajwa katika kitabu cha Wagalatia 5:22 “ Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,”.. Mambo hayo ndio yanayopotea ndani ya mtu, pindi Roho Mtakatifu anapoondoka ndani yake.. Na si kunena kwa lugha, au kuona maono, au kutabiri.. Mtu anaweza kunena na kutabiri lakini Roho Mtakatifu akawa hayupo ndani yake..
Utauliza hilo tunalithibitisha vipi?.. Maandiko yanaonyesha Sauli hata baada ya Roho wa Mungu kuondoka ndani yake, bado aliendelea kutabiri..
1Samweli 18:10 “Ikawa siku ya pili yake, roho mbaya kutoka kwa Mungu ikamjilia Sauli kwa nguvu, NAYE AKATABIRI NDANI YA NYUMBA. Basi Daudi alikuwa akipiga kinubi kwa mkono wake kama siku zote; naye Sauli alikuwa na mkuki mkononi mwake”.
Umeona?.. Matunda ya Roho ni tofauti kabisa na kazi za Roho.. Kazi za Roho kama miujiza, unabii, ishara, zinaweza kufanyika kupitia yeyote yule. Bwana alimtumia Punda kuona maono ya malaika mbele ya Balaamu, atashindwaje kumpa maono mwenye dhambi?..
Kwahiyo maono au kunena kwa lugha, sio uthibitisho wa kwanza wa mtu aliye na Roho Mtakatifu, uthibitisho wa kwanza wa mtu mwenye Roho Mtakatifu ndani yake ni hayo matunda tunayoyasoma katika Wagalatia 5:22, ambayo ni Upendo, amani, furaha, Fadhili, kiasi..yaani kwaufupi ni utakatifu (Waebrania 12:24). Ndio maana Bwana Yesu alisema wengi watakuja siku ile na kusema Bwana Bwana hatukutoa pepo kwa jina lako, na kufanya unabii, lakini Bwana atawafukuza kutoka mbele zake.
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Mathayo 7:22 “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu”.
Hata sasa Roho Mtakatifu anaweza kuondoka juu ya Maisha yetu!.. na tukazipoteza Fadhili za Mungu. Na ataondoka endapo TUTAMHUZUNISHA, au KUMZIMISHA.
TUNAMHUZUNISHAJE?
Maandiko yanasema katika Waefeso 4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi”.
Tabia za kutokujali Neno la Mungu, kama alivyokuwa Sauli ndizo za kwanza zitakazoweza kusababisha Roho Mtakatifu kuondoka juu yetu..Tunapolisikia Neno halafu hatulitii.. badala yake tunaendelea na mambo yale yale mabaya, hapo tunamhuzunisha Roho mtakatifu aliye ndani yetu…
Tunapoendelea kufanya mambo machafu, ambayo tunajua kabisa ni kinyume na Neno la Mungu, hapo tunamhuzunisha na hivyo ni rahisi kutuacha na tukaingiliwa na maroho mengine.
TUNAMZIMISHAJE?
Maandiko yanasema katika kitabu cha 1Wathesalonike 5:19 kuwa “Msimzimishe Roho”.. Maana yake Roho Mtakatifu anaweza kuzimika ndani yetu.
Na tunamzimisha Roho kwa sisi kuacha kuomba, kuacha kufunga, kuacha kufanya ibada, kuacha kuifanya kazi ya Mungu, kuacha kumtolea, kuacha kumtukuza na kumsifu na kuifanya kazi yake na kuacha kuishi Maisha matakatifu. Mambo haya yanamfanya Roho Mtakatifu kuzimika ndani yetu, na hata kuondoka kabisa na kutuacha.
Bwana Yesu atusaidie tuzidi kudumu katika Neema yake na kuitunza zawadi nzuri ya Roho aliyotupatia (Matendo 2:39).
Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.
Mtakatifu ni Nani?
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?
AKAZIDI KUENDELEA KATIKA HEKIMA NA KIMO.