Nakusalimu katika jina la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tujifunze maneno ya uzima.
Ipo tabia ambayo tunapaswa tujifunze kuhusu Mungu. Kama tunavyojua, alipomaliza kuumba vitu vyote ndani ya zile siku saba, zoezi la mwisho kabisa lilikuwa ni Mungu kupanda bustani mashariki mwa Edeni. Tengeneza picha, bustani hiyo ilikuwaje! Bila shaka ilikuwa ni nzuri sana. Mungu alifanya kazi ya kuchukua Ua hili, Ua lile, ukoka huu, ukoka ule, mti huu wa kivuli, mti ule wa matunda kila moja mahali pake stahiki.. Yaani kwa ufupi Edeni ni bustani ambayo iliundwa kwa kila aina ya mmea, lakini katika mpangilio bora. Jambo lililoifanya bustani ile kuwa tofauti na maeneo mengine yote duniani.
Kwani huko kwingine kulijiotea otea, bila mpangilio maalumu. Japo pia napo kulikuwa pazuri lakini sio kama Edeni, kwasababu ile ni bustani iliyopandwa sio kujiotea. Lakini tunaona, asili ya ile Bustani. Ni kwamba ilihitaji kulimwa na matunzo baada ya pale ili iendelee kuwepo vilevile katika ubora wake. Hii ikiwa na maana kama isingetunzwa na kulimwa, ingepotea kabisa, na kufanana tu na sehemu nyingine yoyote ya dunia.
Mwanzo 2:8 “Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya…15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Watunza bustani wanaelewa jambo hili, mahali ambapo wanazipanda, huwa ni lazima mara kwa mara, wawepo kung’oa majani-shambulizi yanayojitokeza, wanafyeka ukoka unapozidi kimo, wanatia mbolea panaposua sua, na wanainyeshea bustani kila siku, na wakati mwingine kuiwekea uvuli. Hivyo ni kazi ambayo inamgharimu mtunza bustani kuwepo pale wakati mwingi.
Ndivyo ambavyo Mungu alimpa jukumu hilo Adamu, kwamba aitunze bustani na kuilima, kwasababu hilo halikuwa jukumu lake tena. Tafsiri yake ni kwamba ili aendelee kukaa katika mahali pazuri pa nchi. Hana budi kupalima na kupatunza. Asipofanya hivyo pataendelea kuwa kama sehemu nyingine tu ya dunia.
Lakini Adamu, hakuweza kudumu katika bustani ile kwasababu aliyakaidi maagizo ya Mungu.
Kila mtu ameandaliwa Edeni yake hapa duniani, ambayo atamfurahia Mungu wake katika hiyo. Si kila mazingira Mungu amekuwekea wewe kumfurahia yeye, si kila mahali ni Edeni yako. Ipo sehemu maalumu, ambapo hapo Mungu anakuundia kisha wewe unapatunza baada ya hapo.
Na sehemu yenyewe ni ndani ya Kristo.
Maana yake ni kuwa ukishaokoka, tayari Mungu amekuwekea mema yako mbeleni. Hivyo kuanzia huo wakati huna budi kuanza kuistawisha bustani yako kwa kuitilia mbolea mara kwa mara, kuinyeshea maji, kuipalilia, kuichonga n.k.. Ndio hapo, linakuja suala la Maombi ya mara kwa mara, mikesha, mifungo, kutafakari Neno, kufanya ibada za sifa, kutoa sadaka, kujitenga na dhambi, na kushuhudia.
Unapokuwa mtu wa namna hii ndivyo unavyoifanya bustani yako kupendeza siku baada ya siku rohoni, ndivyo inavyojitofautisha na sehemu nyingine za dunia, kwa uzuri wake. Matokeo yake ni kuwa Dunia yako itakuwa ya neema sikuzote yenye furaha, Amani na mafanikio, yenye kububujika maziwa na asali. Lakini ukikaa tu ukasubiri, ukasema Mungu atatenda, huku huyatunzi maneno ya Mungu ndani yako, sahau kuona mabadaliko yoyote maisha yako yatakuwa hayana tofauti na yale ya kale, kwasababu kazi ya utunzaji sio ya Mungu bali ni yako. Wewe umemsubiria Mungu, wakati Mungu alishamaliza kazi yake.
Litunze sana Neno la Mungu, kwa kuliishi sio kulisikia tu. Kwani wanaofanya hivyo wanafungua milango mingi sana ya kiroho, Kanisa la Filadelfia ndio kanisa pekee lililopendwa na Kristo kwasababu liliyatunza maneno yake, na matokeo yake likafunguliwa mlango wa mafanikio mbele yake.
Ufunuo 3:8 “Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe UMELITUNZA NENO LANGU, wala hukulikana jina langu”.
Hivyo anza sasa kujibidiisha kulitendea kazi Neno la Mungu. Kwa jinsi unavyolitunza ndivyo utakavyoona mabadiliko yako.
Bwana akubariki.
Je! Umeokoka? Je, unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho? Tunaishi katika dakika za nyongeza tu? Dalili zote zilizotabiriwa kuhusiana na kurudi kwa pili kwa Yesu zimeshatimia?. Wasubiri nini? Ukifa leo utajibu nini mbele ya kiti cha enzi cha Mungu? Tubu sasa ukabatizwe, upokee ondoleo la dhambi zako. Ikiwa bado hujafanya hivyo, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi kwa msaada huo; +255693036618/+255789001312
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kuna tofauti gani kati ya “Edeni” na “Adeni”?
UNAWAZA NINI SASA, JUU YA UFALME WA MBINGUNI?
EDENI YA SHETANI.
SISI TU MANUKATO YA KRISTO.
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
Kwanini Mungu hakumuua Nyoka, akamwacha Hawa ajaribiwe katika bustani ya Edeni?
Kwa jina lake Ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.
AKAPITA KATIKA LILE SHAMBA AMBALO YAKOBO ALIMPA YUSUFU MWANAWE
Rudi nyumbani
Print this post
Jina la Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia!.
Usipoujua ufunuo umhusuo Yesu hutaona sababu ya kumwamini wala kumfuata, vile vile usipopata ufunuo wa kutosha uhusuo ubatizo hutaona umuhimu wa kubatizwa! (utaona ni habari tu ya kawaida, kwamba ukibatizwa au usipobatizwa vyote ni sawa tu).
Nataka nikuambie ndugu, ubatizo ni tendo la muhimu sana kuliko wengi tunavyodhani. Na leo nataka tuone ni jinsi gani agizo la Ubatizo lilivyoambatana na Toba, kwamba baada ya kutubu ni lazima kubatizwa.
Hebu tuyasome maneno yafuatayo ya Bwana Yesu..
Luka 24:46 “Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote “WATAHUBIRIWA KWA JINA LAKE HABARI YA TOBA NA ONDOLEO LA DHAMBI, kuanza tangu Yerusalemu”.
Luka 24:46 “Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;
47 na kwamba mataifa yote “WATAHUBIRIWA KWA JINA LAKE HABARI YA TOBA NA ONDOLEO LA DHAMBI, kuanza tangu Yerusalemu”.
Nataka tuone na kuutafakari kwa kina huo mstari wa 47 unaosema kuwa mataifa yote watahubiriwa “KWA JINA LAKE HABARI YA TOBA NA ONDOLEO LA DHAMBI”
Hili ni agizo ambalo Bwana Yesu aliwapa wanafunzi wake kwamba watu wote ni lazima wahubiriwe habari ya toba na ondoleo la dhambi kwa jina lake.
Mitume walilisikia hili agizo la Bwana, na walilishika sasa hebu tuangalie ni kwa namna gani walilitekeleza,..je walikwenda kuwaambia tu watu “watubu waondolewe dhambi zao au kuna la ziada walilifanya ”
Tusome kitabu cha Matendo 2:36-38
Matendo 2:36 “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Matendo 2:36 “Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.
37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Umeona hapa! Petro anawaambia watu “watubu na kubatizwa kwa jina lake Yesu, wapate ondoleo la dhambi zao”.. na sio tu “Tubuni mpate ondoleo la dhambi”….. sasa linganisha na yale maagizo Bwana aliyowapa akina Petro kuwa “wakawahubirie watu wote kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi”.
Kumbe kuhubiriwa habari ya Toba na ondoleo la dhambi ni pamoja na ubatizo!.. Maana yake ili mtu apate ondoleo kamili la dhambi zake ni lazima pia akabatizwe (Katikati ya Toba na ondoleo la dhambi, kuna ubatizo ambao shetani kawafumba watu macho wasiuone)..Ndio maana ni ngumu leo hii wengi kushinda dhambi, kwasababu mzizi wa dhambi katika maisha yao haujaondolewa, kwasababu wameukosa ubatizo sahihi.
Mitume sehemu zote walihubiri hivi, kwamba watu baada ya kutubu ni lazima wakabatizwe ili dhambi zao ziondolewe… na mitume kamwe wasingeweza kufanya kitu chochote kilicho kinyume na maagizo ya Bwana Yesu…ikiwa na maana kuwa walimwelewa sana Bwana pale aliposema kuwa wakawahubirie mataifa yote kwa jina lake, kwamba ubatizo pia kwa jina lake ni sehemu ya mahubiri yao.
Swali ni je!, na wewe umebatizwa kwa maji mengi na katika ubatizo sahihi wa jina la Bwana Yesu?.. Kumbuka, kama ulibatizwa utotoni basi fahamu kuwa watoto wachanga hawabatizwi kwasababu bado hawajatubu, (kujitambua hawajajitambua watawezaje kutubu?) ni sharti kwanza wahubiriwe wamwamini Mwokozi na kujijua kuwa wao ni wenye dhambi ndipo watubu na kubatizwa. Bwana akubariki.
Tafuta ubatizo sahihi kama bado hujabatizwa, na kama utahitaji msaada Zaidi wa namna ya kupata ubatizo karibu na mahali ulipo basi utawasiliana nasi kupitia namba zetu hapa chini.
Maran atha!
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.
TOFAUTI YA UBATIZO WA YOHANA NA UBATIZO WA BWANA YESU
HUNA SHIRIKA NAMI.
BASI TUENDELEE KUMJUA MUNGU,NAYE ATATUJILIA KAMA MVUA YA VULI.
Boazi na Ruthu.
Atukuzwe Yesu Kristo Bwana wetu na mwokozi wetu, Nakukaribisha tuzidi kuzitafakari siri za ufalme wa mbinguni.
Awali ya yote tukumbuke kuwa mahusiano ambayo Yesu anayatengeneza kwa kila mwaminio sio mahusiano kama ya rafiki na rafiki, au ndugu na ndugu, hapana, bali kama ya Bwana-arusi na Bibi-arusi.
Ni vema hilo ukalifahamu mapema, kwasababu kitakachotufanya tuende mbinguni, ni Ndoa, na sio urafiki. Hivyo yeye kama Mfalme ndio Bwana-arusi, na sisi ni Bibi-arusi wake. Tunapojiunganisha naye, ni lazima tuonyeshe tabia za bibi-arusi wa kweli, vinginevyo hatutapata kibali cha kuwepo katika karamu ya Arusi yake, atakayoifanya mbinguni kwa wateule wake kwa tukio linalojulikana kama Unyakuo.
Mimi na wewe hatua budi kuhakikisha tunakuwa bibi-arusi safi wa Kristo, na sio masuria, ili tupate kibali cha kukubaliwa na yeye siku ile ya mwisho.
Leo wa neema za Bwana, tutajifunza kwa kupitia maisha ya Boazi na Ruthu. Kumbuka hadithi zote unazozisoma katika biblia zina ufunuo wa Kristo na kanisa lake. Hivyo usomapo hakikisha unamwomba Roho Mtakatifu akufunulie, ili biblia kwako isiwe kama vitabu vingine vya hadithi.
Sasa kama wewe ni mwanafunzi wa Biblia utakuwa umeshawahi isoma habari ya Ruthu. (Kama hujasoma nashauri ukakisome kwanza hicho kitabu, ndipo utaelewa vema, kiini cha somo hili, kwasababu hatutakichambua chote).
Utakumbuka, Boazi alikuwa ni shemeji wa yule mwanamke mjane aliyeitwa Naomi. Biblia inasema Boazi alikuwa ni tajiri sana, na mkuu katika mji ule. Lakini huyu Naomi alikuwa pia na mkwe wake aliyeitwa Ruthu.
Ruthu naye alikuwa mjane, kwani alifiwa na mume wake kabla hajapata mtoto. Hivyo wote wawili walikuwa ni wajane yaani Naomi na Ruthu, isipokuwa Ruthu alikuwa bado ni kijana aliyekidhi vigezo vya kuoelewa tena, lakini Naomi alikuwa ameshakuwa mkongwe hawezi kuolewa tena.
Lakini siku moja Naomi, akaona si vema mkwe wake Ruthu abakie kama yeye. Akaanda mazingira ya kumpatia mkwe wake mume mwingine, ndipo akachunguza na kuona kuwa Boazi ndiye amfaaye. Hivyo akaunda mpango aliokuwa na uzoefu nao, akamfundisha Ruthu namna ya kumwingia, na kwa kupitia njia ile basi Ruthu atapata kibali, kwa mtu huyu tajiri na mkuu wa mahali pale.
Embu tuutazame mpango wenyewe, tunaousoma katika ile sura ya 3, kisha tuone kanuni na sisi ya kukubaliwa na Kristo.
Ruthu 3:1 “Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema? 2 Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani. 3 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa. 4 Nayo itakuwa wakati atakapolala, utapaangalia mahali alalapo, nawe uingie, uifunue miguu yake ujilaze hapo; na yeye atakuambia utakalofanya. 5 Akamwambia, Hayo yote unenayo mimi nitayafanya. 6 Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza”
Ruthu 3:1 “Kisha Naomi akamwambia mkwewe, Je! Mwanangu, si vizuri nikutafutie raha, ili upate mema? 2 Basi na huyu Boazi, je! Siye wa mbari yetu, ambaye ulikuwapo pamoja na wasichana wake? Tazama, usiku wa leo atakuwa akipepeta shayiri pale ugani.
3 Basi wewe oga, ujipake mafuta ujivike mavazi yako, kisha uende kwenye uga; walakini usijionyeshe kwake mtu yule, ila atakapokwisha kula na kunywa.
4 Nayo itakuwa wakati atakapolala, utapaangalia mahali alalapo, nawe uingie, uifunue miguu yake ujilaze hapo; na yeye atakuambia utakalofanya.
5 Akamwambia, Hayo yote unenayo mimi nitayafanya.
6 Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza”
Ukichunguza hapo utaona, Ruthu anapewa hatua tano za kupitia.
Naomi alijua uchafu, haupatani na bibi-arusi yoyote. Hakuna mume anayependa mwanamke mchafu, ni sharti awe msafi tena kwelikweli. Ndipo hapo sasa utaona akamwambia Ruthu akaoge kwanza awe safi. Ikifunua kuwa mkristo yoyote kabla ya kukubaliwa na Kristo, ni sharti kwanza awe safi kwa maji, yaani Ubatizo, ambao unaleta ondoleo la dhambi zake. Kama hujabatizwa, ni sharti ubatizwe katika maji ya kuzama, na kwa jina la Yesu Kristo, ili dhambi zako ziondolewe, Ndipo ukidhi hatua ya pili ya kumkaribia Kristo.
Kuoga tu peke yake haikutosha aliambiwa pia ajipake mafuta, Ikifunua kuwa Mkristo yoyote ni lazima awe na mafuta rohoni mwake. Na mafuta hayo ni Roho Mtakatifu. Ukikosa Roho Mtakatifu kamwe huwezi kukubaliwa na Kristo.
Matendo 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”
Ruthu alikuwa na mavazi yake ya kawaida, lakini hapa Naomi anampa shauri avae mavazi mengine yanayofanana na ya bibi-arusi, meupe safi, aonekane tofauti na wanawake wengine, apendeze, avutie machoni pa Boazi atakapoenda kujionyesha kwake.
Maana yake ni kuwa kila mkristo lazima awe na vazi la arusi, na vazi lenyewe ni Utakatifu. Kama tunavyosoma katika Ufunuo 19:8.Ukipoteza utakatifu, kamwe Kristo hawezi kukupokea, haijalishi utasema nimeokoka.
Ugani ni mahali wanapopepeta nafaka, Hivyo Boazi alikuwa ni mtu wa kazi, muda wote utamkuta yupo kazini kwake, si mtu aliyekuwa mlegevu, Ukitaka kumpata sharti na wewe pia uingie ugani kwake. Hivyo Ruthu ilimpasa aende vilevile, lakini alipewa maagizo kwamba iwe kwa siri, asijulikane na mtu yoyote yule.
Ikifunua kuwa, pamoja na kwamba, utakuwa umeokoka, huna budi kujishughulisha na kazi ya Bwana. Na wewe pia uwepo shambani mwake, lakini ukiwa na vazi lako la thamani(yaani Utakatifu). Na wakati uwapo huihitaji, kutenda kazi yake kama mtu wa mshahara bali kama mtumwa asiyekuwa na faida, uhakikishe upo kama mtu asiyetambulika na Kristo. Unatumika ndipo baadaye yeye mwenyewe aone vema kujifunua kwako.
Luka 17:5 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani. 6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. 7 Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? 8 Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? 9 Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? 10 Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya
Luka 17:5 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.
6 Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
7 Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
8 Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
9 Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? 10 Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya
Na hatua ya mwisho aliyopewa Ruthu na Naomi ni kujilaza miguuni pa Boazi. Maana yake ni kujivika unyenyekevu, Unakubali kulala kwenye miguu yenye mavumbi ya Bwana wako. unathamini cha Bwana ambacho kinadharauliwa, unathamini watu wa Mungu, .. Hapo ndipo pawe makazi yako daima, penye unyenyekevu.
Hivyo baada ya kutimiza, hatua zote hizo 5, yaani kuoga, kujipaka mafuta, kuvaa vazi la bibia-arusi, kudumu ugani na kulala chini ya miguu ya Yesu. Fahamu kuwa Kristo atajidhihirisha kwako, kama Boazi wa Ruthu.
Kumbuka maagizo hayo yote, Ruthu hakujiamulia tu, bali aliyapokea, kwa mkwe wake mzoefu aliyeitwa Naomi. Na sisi Naomi wetu ni Mitume na Manabii, yaani Biblia Takatifu. Tukiipenda, kuyashika yaliyoandikwa mule, basi tutakuwa bibi-arusi wa Kristo kwelikweli. Mtume Paulo aliandika hivi;
2Wakorintho 11:2 “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi. 3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo”.
2Wakorintho 11:2 “Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo”.
Zingatia: Kama wewe si bibi-arusi, huwezi kwenda kwenye Unyakuo. Hizi ni siku za mwisho, wakati wowote Yesu anarudi, Je! umejiandaaje? Utajibu nini siku ile, utakapoulizwa kwanini hukuitii injili? Wakati ni mchache sana tunaishi katika dakika za nyongeza tu, Tengeneza maisha yako sasa, huu sio wakati wa kuhubiriwa injili ya kubembelezwa, ni wewe mwenyewe uone uhalisia utubu. Yesu yupo mlangoni.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.
INAYOENDELEA SASA NI HUDUMA YA RUTHU.
EWE MKE! HESHIMA YAKO IPO KWA WAKWE ZAKO.
KAMA MKRISTO FAHAMU ZIPO HATUA UTAPIGISHWA NA MUNGU.
Jina la Bwana Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu.
Warumi 6:8 “Lakini tukiwa TULIKUFA PAMOJA NA KRISTO, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye”
Kabla ya kujitathmini kama kweli tulikufa pamoja na Kristo hebu kwanza tukitafakari kifo cha Bwana Yesu.
Tunasoma kifo cha Mwokozi wetu hakikuwa cha ugonjwa, au cha uzee, au cha ajali… bali kilikuwa ni kifo cha mateso, Bwana Yesu alibeba msalaba wake mpaka Golgotha, na pale akatundikwa msalabani kwa dhihaka nyingi na maumivu makali na kwa masaa mengi.
Lakini pamoja na hayo alisema kuwa “mtu yeyote akitaka kumfuata, ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake ndipo amfuate..
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate”.
Nataka tutafakari kwa undani mambo hayo matatu (3), kujikana, kubeba msalaba na kumfuata Yesu…
1. Ajikane mwenyewe.
Maana ya kujikana, ni kukataa mapenzi yako na kujiachilia kwa mapenzi ya mwingine, hivyo Kristo anataka mtu yeyote anayetaka kumfuata ni lazima ayaache yale anayoyapenda na kuyafuata yale yeye (Kristo) anayoyapenda.
2. Ajitwike Msalaba wake.
Kujitwika msalaba maana yake ni kubeba kitu ambacho utakwenda Kuteswa nacho. Kristo alibeba msalaba wake na akaenda kusulubiwa juu ya huo, na ndivyo sisi nasi tunapaswa tubebe misalaba yetu..
3. Anifuate
Amfuate wapi?…amfuate kila mahali atakapokwenda… na mwisho wa safari ya Yesu ni Golgotha, katika Kifo!….na kifo cha Bwana Yesu kilikuwa juu ya ule msalaba alioubeba, na si juu ya kitu kingine chochote, vile vile na sisi tunaposema tumekufa pamoja na Kristo ni lazima kifo chetu kiwe juu ya misalaba yetu tuliyoibeba na si juu ya kitu kingine chochote.
Je umeubeba msalaba wako?
Kama hukuubeba msalaba wako utasemaje basi ulikufa pamoja Kristo?.. Kama hujajikana nafsi utasemaje kuwa umekufa pamoja na Kristo?, Kama mapenzi ya baba yako yana nguvu kuliko mapenzi ya Mungu utasemaje ulikufa pamoja na Kristo?.. Kama unamwogopa mama yako kuliko kumwogopa Mungu utasemaje ulikufa pamoja na Kristo?… Kama kazi yako ina nguvu kuliko ibada za Kristo utasemaje ulikufa pamoja na Kristo?, kama kumkiri Kristo tu mbele ya watu ni ngumu utasemaje ulikufa pamoja naye?, kama maisha yako yamejaa uchafu wa kila aina utasemaje basi ulikkufa pamoja na Kristo?.. Wengi wamekufa pamoja na Yuda katika roho lakini si pamoja na Kristo, waliokufa pamoja na Kristo ni watu waliobeba misalaba yao..
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, 26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27 MTU YE YOTE ASIYEUCHUKUA MSALABA WAKE NA KUJA NYUMA YANGU, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU”.
Luka 14:25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,
26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
27 MTU YE YOTE ASIYEUCHUKUA MSALABA WAKE NA KUJA NYUMA YANGU, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU”.
Na wote waliokufa pamoja na Kristo na kuzikwa pamoja naye ndio watakaoishi pamoja naye kama maandiko yanavyosema…
Je wewe umekufa pamoja na nani?.. na umekufa juu ya nini?….Ishara ya kufa pamoja na Kristo ni msalaba, je wewe unao huo msalaba katika maisha yako?
Tofuati kati ya kifo na mauti ni ipi?
BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.
Je! Bwana Yesu alisulubiwa juu ya msalaba au juu ya mti uliokuwa wima?
UTHAMINI WITO WA PILI WA YESU ZAIDI YA ULE WA KWANZA.
Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?
Tunaona kuna baadhi ya watu ambao majina yao yameongezwa vionjo kwa mbele, kwa mfano Simoni Petro, Yuda Iskariote, Tomaso pacha, Simoni mkananayo, Yohana Mbatizaji n.k
Watu hawa ambao majina yao yanaonekana kuongezewa vionjo mbele yake ni kwa lengo la kuwatofautisha na watu wengine wenye majina kama ya kwao. Na vionjo hivyo vilivyokuwa vinawekwa ni aidha kulingana na mahali (miji) wanayotokea, au majina ya wazazi wao, au matendo/huduma wanazozifanya.
Wafuatao ni baadhi ya majina ya watu yaliyoongezewa vionjo kulingana na Matendo waliyokuwa wanayafanya;
Kulingana na Mahali walipotokea;
Kwahiyo ili kumtofautisha na Simoni Petro au Simoni mwingine yeyote, ndipo huyu akaitwa Simoni Mkananayo au Simoni Zelote.
Kulingana na majina ya Wazazi/ Ndugu
1 .Yakobo wa Alfayo: Yakobo alikuwa ni mtoto wa Mtu aliyeitwa Alfayo, Aliitwa hivyo ili kumtofautisha na akina Yakobo wana wa Zebdayo na wengine waliokuwepo kwa wakati huo.(Marko 3:18).
2. Yuda mwana wa Yakobo: Huyu alikuwa ni mwanafunzi wa Bwana Yesu ambaye pia aliitwa kwa jina lingine “Thadayo”(Marko 3:18). Ili kumtofautisha na Yuda aliyemsaliti Bwana Yesu, ndipo kwa jina lingine akajulikana hivyo kama Yuda wa Yakobo au Thadayo.
3. Tomaso aitwaye Pacha (Yohana 20:2)– Ni kuonyesha Tomaso kuwa alikuwa na Pacha lakini hakutajwa katika maandiko huyo pacha wake alikuwa ni nani, ila aliitwa hivyo ili kumtofautisha na wakina Tomaso wengine waliokuwepo pale.
Je jina lako ni nani? Na linabeba ujumbe gani?… >>JINA LAKO NI LA NANI?
Maran atha
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
MAANA YA MAJINA NA TAFSIRI ZAKE.
Kwanini mtu afanye miujiza na bado asiende mbinguni?
Yeremia alikuwa na umri gani alipoitwa?
NGUVU YA UPENDO WA KRISTO.
(Masomo maalumu kwa Wakristo, Je! Unajijua nafasi yako?.. je unajijua kuwa wewe ni manukato yanayokubalika na pia yasiyokubalika kwa upande mwingine?).
Manukato ni neno lingine la “Marashi”.. Na kazi ya manukato/Marashi ni kukifanya kitu kivutie, hakuna mtu anayejipaka marashi ili mtu amkimbie. Lakini changamoto ni kwamba haijalishi marashi yatakuwa ni mazuri kiasi gani, ni lazima kwa upande mwingine kuna mtu yatamtia kichefuchefu tu. (Si kila marashi yaliyo mazuri kwa mtu, yatakuwa mazuri kwa watu wote).. ni lazima upande mmoja utayakosoa tu.
Na siku zote, marashi yaliyokosolewa huwa yanatia kichefuchefu na hata wakati mwingine kumuumiza Yule anayeyasikia..
Kadhalika biblia inasema kuwa sisi ni Manukato ya Kristo. Na kama ni manukato ni lazima upande mmoja yatakubalika na upande mwingine yatakatalika.. Na siri ya manukato ya Kristo ni kwamba wengi wanayachukia zaidi ya wale wanayoyapenda..
2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu. 15 KWA MAANA SISI TU MANUKATO YA KRISTO, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; 16 katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo? 17 Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo”.
2Wakorintho 2:14 “Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
15 KWA MAANA SISI TU MANUKATO YA KRISTO, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;
16 katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo?
17 Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo”.
Wakristo wengi wanadhani kuwa wanapookoka bali wataanza kupendwa, na kukubalika na kupokea kibali kila mahali. Ni kweli hayo yanaweza kutokea kwasababu kwa Mungu yote yanawezekana.. Lakini fahamu kuwa wewe ni marashi mazuri lakini yenye kuleta harufu mbaya kwa wanaopotea..
Maisha ya usafi na ukamilifu unayoishi ni harufu nzuri kwa wanaookolewa, (Maana yake ni mfano mzuri wa kuigwa, kwa waongofu wapya na waaliookoka), kuomba kwako na kufunga kwako na kuhubiri kwako ni harufu nzuri kwa waliookoka kama wewe.
Lakini kwa wale ambao hawamtaki Yesu, fahamu kuwa maisha yako ni kichefuchefu kwao….ni lazima watakupinga tu, ni lazima watakuletea vita tu, ni lazima watakukosa tu, ni lazima watakurushia mishale tu..Kwasababu kwao wewe ni manukato yenye harufu mbaya, tena harufu inayoleta mauti kabisa…yaani maisha yako yanawahukumu..
Hili ni jambo la kufahamu wewe uliyempokea Kristo na kuokoka!.. Kamwe usifikiri kuwa utaendelea furaha yako ndani ya Kristo ni jambo linalovutia machoni pa wengine… Ukristo ni vita, unapoamua kuwa mkristo ni kama mtu aliyevaa kombati na kuingia vitani.. Kwahiyo tegemea kukumbana na maadui wa imani, watakaokukosoa na kukutatisha tamaa..
Yohana 15:18 “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. 20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu”.
Yohana 15:18 “Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi.
19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu”.
Marhamu ni nini? Na Manukato ni nini?
Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?
USICHELEWE KUMPAKA BWANA MARHAMU!
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 1: Upande wa wanaume)
Nini tofauti ya Uwezo na Uweza kibiblia?
Mithali 25:14 “Kama mawingu na upepo pasipo mvua; Ndivyo alivyo yeye ajisifiaye karama kwa uongo”.
Njia nyingine shetani anayoitumia kuwaangusha watu na kudanganya watu, ni kupitia “karama za uongo”.. Hii inatokea pale ambapo mtu anajipandikiza karama ambayo hana, na anajitangaza kuwa anayo kwa wote, jambo ambalo lina madhara makubwa sana kiroho.
Zifuatazo ni ishara za karama ya kweli ndani ya Mtu, maana yake mtu akikosa hizi ishara basi huenda hiyo karama hana au anayo lakini imeshambuliwa na kutumiwa na adui.
Mtu mwenye karama ya kweli ya Mungu, ni lazima atakuwa na msukumo wa kuwafanya watu wazidi kukamilika katika Utakatifu, na kumcha Mungu…hata kufikia viwango ambavyo Mungu anataka (Waebrania 12:14), maana yake kila siku atakuwa anatafuta kutatua kasoro zinazofanya watu au yeye mwenyewe asiwe mkamilifu kwa Mungu..Lakini kama karama ya mtu inazidi kumfanya yeye mwenyewe asiwe mkamilifu, au kuwafanya watu wasiwe wakamilifu kwa Mungu, au wasihamasike kumtafuta Mungu zaidi, au kujitakasa… badala yake inawahamasisha kutafuta mambo ya kidunia, basi huyo mtu haijalishi anajiita Mchungaji au Mtume, au nabii kiuhalisia hana hiyo karama..
Utauliza tunalithibitisha vipi hilo kimaandiko… hebu tusome maandiko yafuatayo..
Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; KWA KUSUDI LA KUWAKAMILISHA WATAKATIFU….”
2. IPO KWA LENGO LA KUWAHUDUMIA WATU NA SI KUJIHUDUMIA YENYEWE.
Karama yoyote ya kweli ni lazima iwe na HUDUMA, na huduma maana yake ni kutoa msaada kwa wengine, na msaada tulioagizwa sisi wakristo tu utoe ni ule wa kiroho na usio na gharama.. Maana yake hatujaagizwa kuwatoza watu vitu ili wapokee kutoka kwetu.
Hiyo ikiwa na maana kuwa kama mtu yeyote anajiita Mchungaji, au Nabii, au Mwinjilisti au Mwimbaji, au halafu huduma yake anaitoa kwa malipo, ni wazi kuwa hana hiyo karama, haijalishi anajua kuimba kiasi gani au anajua kuhubiri kiasi gani, au anatoa unabii kiasi gani… Kama hatakuwa mtu wa kutoa Huduma bila kutazamia malipo, huyo atakuwa anahudumu kwa roho nyingine ya adui.
Utasema tunalithibithisha vipi hili nalo kimaandiko… Tuendelee na mstari ule wa 12..
Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, HATA KAZI YA HUDUMA ITENDEKE….” 3. IPO KWA LENGO LA KUUJENGA MWILI WA KRISTO.
Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, HATA KAZI YA HUDUMA ITENDEKE….”
3. IPO KWA LENGO LA KUUJENGA MWILI WA KRISTO.
Mwili wa Kristo unajengwa kwa viungo vyote na si kimoja au viwili.. Kristo alipokuwa hapa duniani hakuwa mlemavu.. wala hata baada ya kufa hakuwa mlemavu (maandiko yanaonyesha mifupa yake haikuvunjwa pale msalabani).. Na sisi ni viungo vya Kristo, hivyo ili tuujenge mwili mkamilifu wa Yesu ni lazima tuwepo wote pamoja..
Mtu akijiona Nabii, au Mtume, au Mwalimu na hayupo katika ushirika na viungo vingine katika kanisa, ni yeye tu kama yeye, mtu huyo si kiungo cha Kristo, na hana hiyo karama anayojivunia..
1Wakorintho 12:14 “Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. 15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo? 16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo? 17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa? 18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. 19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. 21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi”.
1Wakorintho 12:14 “Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.
15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?
16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?
17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?
18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.
19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja.
21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi”.
Tunazidi kulithibitsha hili katika mstari ule ule wa 12..
Waefeso 4:11 “Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, HATA MWILI WA KRISTO UJENGWE”
12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, HATA MWILI WA KRISTO UJENGWE”
Kama Karama haiujengi mwili wa Kristo ni karama ya uongo.
Kwahiyo ni lazima kila mtu mwenye karama Fulani ya Roho awe na sifa hizo, lakini kama hana hizo sifa basi huenda hana hiyo karama anayojivunia kuwa anayo au alikuwa nayo lakini sasa imeshambuliwa na inatumiwa na adui.
Na watu wote wanaojivunia karama za Uongo, biblia imesema ni kama mawingu yasiyo na maji.
Maana yake ni watu wanaotoa matumaini ya kusitawisha jambo lakini mwisho wao ni ukame tu.. Hivyo si wakuaminiwa.
Bwana atusaidie karama zetu ziwe za kweli.
Karama ya pili inayozungumziwa katika 2Wakorintho 1:15 ndio ipi?
ICHOCHEE KARAMA YAKO.
Nini tofauti kati ya Kipawa na Karama?
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.
Karibu katika mafunzo ya biblia.
Kwanini tunasema kuwa hili ni kanisa la Mwisho la Laodikia?, Je ni viashiria gani vinavyotutambulisha kuwa hali ya kanisa la Laodikia lile la saba ambalo Mtume Yohana alionyeshwa kwenye Maono katika kitabu cha Ufunuo ndio hali halisi ya kanisa letu la siku za mwisho?.
Awali ya yote hebu tujikumbushe historia ya yale makanisa saba, tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo Mlango wa 2 na wa 3.
Makanisa saba tunayoyasoma katika kitabu cha Ufunuo ni makanisa ambayo yalikuwa katika miji 7 tofauti tofauti. (Efeso, Smirna, Pergano, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia, Ufunuo 1:11).
Hivyo na makanisa hayo yalijulikana kwa majina ya miji hiyo, na Yote ilikuwa inapatikana katika eneo lijulikanalo kama “Asia Ndogo” ambapo kwasasa ni nchi ya “Uturuki”.
Sasa kila kanisa lilikuwa na tabia yake, kulingana na huo mji (unaweza kusoma tabia hizo katika Ufunuo 2-3). Na kanisa la Mwisho kabisa kutajwa ambalo ndio la saba lililoitwa Laodikia lilikuwa na tabia nyingine ya kipekee ambayo kwa hiyo ndiyo tutajua kuwa kanisa letu la sasa linafanana na kanisa la huo mji au la!.
Sasa kabla ya kwenda kusoma tabia za kanisa hilo katika kitabu cha Ufunuo, hebu kwanza tuweke msingi mwingine wa kuelewa jambo lingine, ambalo litatusaidia kuelewa hili vizuri.
Katika biblia maandiko yanatabiri kuwa dalili za siku za mwisho ni Maasi kuongezeka katika kiwango cha miji ya Sodoma na Gomora, au miji ya Nyakati za Nuhu (Soma Luka 17:26-28).
Maana yake ni kuwa kama hali ya maovu haijafikia kile kiwango cha maasi ya Sodoma na Gomora, basi bado ule mwisho utakuwa upo mbali, lakini kama hali ya mji itafikia kile kiwango cha maasi ya Sodoma na Gomora basi ni wazi kuwa ule mwisho umefika.
Kwahiyo ni sahihi kusema kuwa Miji ya Sodoma na Gomora ni ishara au alama ya miji ya siku za mwisho, Hivyo tukitaka kujua kuwa tupo siku za mwisho basi tujilinganishe na miji ya Sodoma na Gomora. (2Petro 2:6 na Yuda 1:7).
Na sasa tunaona kabisa kuwa kizazi chetu ni kama kile cha Sodoma na Gomora na hata huenda kimepita, kwasababu katika miji ya Sodoma na Gomora kulikuwa na mwingiliano wa ndoa za jinsia moja..vile vile na sasa hali ni hiyo hiyo, ushoga upo kila mahali, mauaji, dhuluma n.k kwahiyo tupo siku za mwisho.
Vile vile na kanisa la Mji wa Laodikia, ambao ulikuwepo katika enzi za kanisa la Kwanza, lilikuwa ni Ishara ya kanisa la siku za mwisho. Maana yake ni kuwa tukitaka kujua kuwa tunaishi katika kanisa la mwisho, basi tunapaswa tujilinganishe kanisa letu na lile la Laodikia. Tukiona yanafanana kitabia basi tujue kuwa hili ndio kanisa la mwisho na unyakuo umekaribia.. lakini tukiona kuwa bado hatujafikia viwango vya kanisa lile basi tujue kuwa ule mwisho huenda bado sana.
Sasa hebu tusome tabia za kanisa la Laodikia katika biblia.
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
15 NAYAJUA MATENDO YAKO, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; INGEKUWA HERI KAMA UNGEKUWA BARIDI AU MOTO. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
15 NAYAJUA MATENDO YAKO, YA KUWA HU BARIDI WALA HU MOTO; INGEKUWA HERI KAMA UNGEKUWA BARIDI AU MOTO.
16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.
17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi”.
Umeona tabia za kanisa la Laodikia?..Biblia inasema ni kanisa ambalo lilikuwa vuguvugu, si moto wala si bariki.. mfano kamili wa kanisa la wakati huu. (Kumbuka hapa tunazungumzia kanisa na si watu wa ulimwengu, watu wa ulimwengu ishara yao ni miji ya Sodoma na Gomora na sisi kanisa ishara yetu ni kanisa la mji wa Laodikia).
Kanisa la wakati huu utaona mtu mguu mmoja nje mguu mmoja ndani, leo yupo kanisani kesho disco, leo anamwabudu Bwana kesho anasikiliza miziki ya kidunia, simu yake nusu ina nyimbo za injili nusu nyimbo za kidunia, kabati lake nusu lina nguo za kujisitiri nusu lina nguo za nusu uchi, maneno yake nusu ya heshima nusu ya kihuni, biashara yake nusu ni halali nusu ni haramu, duka lake nusu lina bidhaa njema nusu lina bidhaa haramu (pombe, na sigara), leo atatoa sadaka kesho anaonga/ anaogwa.n.k
Hiyo ndiyo ilikuwa hali ya kanisa la Laodikia na ndio hali ya kanisa la Sasa tulilopo.
Hiyo ndiyo alama pekee inayotutambulisha siku si nyingi unyakuo wa kanisa utatokea. Kwasababu hakutakuwa na kanisa lingine litakalotokea lenye tabia nyingine, hili la Laodikia biblia imetabiri ndio kanisa la Mwisho baada ya hapo ni unyakuo ndio maana utaona pale, baada ya ujumbe wake kumalizika kilichofuata ni Yohana kuchukuliwa juu mbinguni.
Ufunuo 4:1 “Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo”.
Wakati kanisa hili la Laodikia limechafuka hivi, Bwana analiandaa kundi lake dogo, na kuliambia litoke huko, kama vile alivyowaokoa Nuhu na Luthu..Vile vile kanisa la Laodikia litaingia katika dhiki kuu kwasababu ni kanisa vuguvugu lakini kundi dogo ambalo litakuwa safi na litakuwa Moto na si Vuguvugu hilo litaenda na Bwana katika unyakuo.
Ndugu unyakuo umekaribia sana, Yesu yupo Mlangoni kurudi, ondoka katika uvuguvugu, wa kidunia, kuwa Moto.. Ukiamua kumfuata Kristo basi mfuate kwelikweli, usiige desturi za kidunia, ukiamua kuwa mtu wa kujisitiri fanya hivyo kikweli kweli usiwe nusu nusu, ukiamua kumfuata Yesu basi jikane kweli kweli.
Uvuguvu Kristo anauchukia kuliko hata Yule mtu aliye baridi kabisa.. kwasababu yeye mwenyewe anasema ni heri mtu awe moto au baridi kuliko vuguvugu..
Bwana atusaidie.
AGENDA KUBWA YA SHETANI KWA KANISA HILI LA LAODIKIA.
SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO, LAKINI MIKONO NI YA ESAU.
Babewatoto ni nani katika biblia?(Isaya 34:14).
Babeli ni nchi gani kwasasa?
JE NI KWELI SAMAKI NGUVA YUPO?
Karibu tujifunze biblia.
Matendo 3:22 “ Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi. 23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake”
Matendo 3:22 “ Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.
23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake”
Unabii huo unamhusu Bwana Yesu Kristo, lakini swali la Msingi hapa, je! Ni wakati gani ambao “watu wataangamizwa na kutengwa” kwa kutomsikiliza huyu Masihi…Kwasababu ni wengi leo hawamsikilizi wala kumtii lakini hawaangamizwi wala kutengwa na watu wao.
Hapo kuna mambo mawili ambayo yatatimia kwa pamoja.. 1) KUANGAMIZWA, na 2) KUTENGWA.
Haya ni mambo mawili ambayo yatatimia kwa wakati mmoja kwa wote ambao hawatamsikiliza Masihi.Sasa swali, ni hili unabii huo utatimia lini wa watu kuangamizwa na kutengwa?
Tusome,
2Wathesalonike 1:7 “na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; WAKATI WA KUFUNULIWA KWAKE BWANA YESU kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake 8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; 9 watakaoadhibiwa kwa MAANGAMIZI ya milele, KUTENGWA na uso wa Bwana na UTUKUFU WA NGUVU ZAKE;”
2Wathesalonike 1:7 “na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; WAKATI WA KUFUNULIWA KWAKE BWANA YESU kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake
8 katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;
9 watakaoadhibiwa kwa MAANGAMIZI ya milele, KUTENGWA na uso wa Bwana na UTUKUFU WA NGUVU ZAKE;”
Umeona hapo?. Kumbe wote wasioitii injili, leo siku ya mwisho (ya kufunuliwa Bwana Yesu) wataangamizwa!, na sio tu kuangamizwa, bali pia “watatengwa na uso wa Mungu” na “kutengwa na utukufu wa nguvu zake”…Maana yake wataanza kwa kutengwa kutoka kwa ndugu zao (wakati wa kutenganishwa kondoo na mbuzi Mathayo 25:31-35) na pia watatengwa na vitu vyote Mungu alivyoviumba ikiwemo dunia na kila kitu…sawasawa na Mithali 2:21-22.
Mithali 2:21 “Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake. 22 Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang’olewa”
Mithali 2:21 “Maana wanyofu watakaa katika nchi, Na wakamilifu watadumu ndani yake.
22 Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang’olewa”
Ni jambo baya sana kutengwa na uso wa Mungu na kuangamizwa!..Wengi leo wanamkataa Yesu na kuikataa Injili wakidhani ipo njia nyingine ya kufika mbinguni.. Bwana Yesu yeye mwenyewe alisema kwa kinywa chake kuwa..
Yohana 14:6 “..Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi”.Hakuna njia nyingine ya kumfikisha mtu mbinguni isipokuwa njia ya Msalaba!.. Usidanganyike kwa vyovyote vile.
Mwisho wa dunia unakuja, Mpokee Yesu leo, Itii injili yake inayosema… usizini, usiibe, usivae mavazi ya nusu tupu, usivae mavazi yapasayo jinsia nyingine, usijichore mwili, usitukane n.k
Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa >> WHATSAPP-GROUP
Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?
Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)
Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?
Wana wa Manabii walikuwa ni watu gani?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe daima, karibu tujifunze Biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na Mwanga wa njia yetu (Zab.119:105).
Maandiko yanatuonyesha kuwa si lazima watu wote wanene kwa lugha (1Wakorintho 12:30 na 14:23), kana kwamba ndio uthibitisho pekee wa mtu kuwa wa kiroho…lakini pia kuna faida kubwa ya kunena kwa lugha ikiwa mtu atajaliwa hilo.
Na pia kunena kwa lugha si jambo ambalo mtu anaweza kuamua, kwamba sasa naanza kunena, la! Kunena kwa lugha ni msukumo ambao Roho Mtakatifu anaushusha ndani ya mtu pasipo mtu kutaka au kupanga!.. Ni kama mtu anavyopokea unabii, au anavyopokea ndoto au maono.. hakuna mtu anayeweza kupanga unabii au maono au ndoto (labda awe nabii wa uongo)!.. kwani mambo hayo yanakuja tu yenyewe kutoka kwa Mungu, kwajinsi apendavyo Mungu… Na kunena kwa lugha ni hivyo hivyo, si lazima iwe kila siku au kila saa, bali ni wakati maalumu tu ambao Roho atalishusha jambo hilo ndani ya mtu.
Sasa zipo lugha za wanadamu, na vile vile za Malaika (Soma 1Wakorintho 13:1), Zozote kati ya hizo mtu aliyejazwa Roho anaweza kuzinena. Na zote zina faida katika kuzinena… Katika kunena lugha za wanadamu ni pale ambapo mtu haijui lugha Fulani ya jamii fulani ya watu, lakini ghafla anajikuta anaanza kuizungumza ile lugha vizuri sana.. Vile vile katika kunena lugha za malaika, ni pale ambapo anajikuta anazungumza lugha ambayo ni mpya kabisa isiyotumiwa na wanadamu mahali popote.
Na maneno anayoyazungumza yanakuwa aidha ni maneno ya unabii, au maonyo au ya kumsifu Mungu.. kwahiyo kama ni ujumbe kwa kanisa ni lazima awepo mfasiri..
Vile vile kama ni lugha Mpya inayozungumzwa, maana yake ambayo haitumiki na jamii yoyote ya wanadamu, na ni ujumbe kwa kanisa, basi anahitajika pia mfasiri, lakini kama mtu yupo katika maombi yake binafsi na lugha hiyo ikamjia ndani yake, basi hapo hahitaji mfasiri bali anakuwa ananena maneno ya siri na Mungu wake.
Na leo tutaangalia faida moja kubwa ya kunena lugha mpya, uwapo wewe binafsi katika maombi yako ya faragha.
MAZUNGUMZA YAKO YANAKUWA NI YA SIRI.
Hii ndio faida kuu na ya kwanza. Kikawaida mazungumzo ya siri yanakuwa na upinzani mchache kuliko mazungumzo ya wazi!.. na njia mojawapo ya kuficha mazungumzo ni kutumia lugha nyingine!..
Kwamfano utaona Waarabu wawili, au Wachaga wawili, au wamasai wawili, au wasukuma wawili, wanapokutana mahali Fulani ili waongee kwa uhuru zaidi utaona wanatumia lugha zao za asili , lengo ni kuficha mazungumzo na pia kuzungumza mambo yao yale mambo ya ndani kwa uhuru zaidi.. watu walio kando kando inakuwa ngumu kuelewa na hivyo wazungumzaji wanakuwa wamefunga milango mingi.
Na sisi tunapozungumza na Mungu wetu, KUNA WAKATI TUNAHITAJI USIRI.. Maneno yetu tunayoyazungumza si lazima yaeleweke na watu wa kando yetu au na mapepo katika ulimwengu wa roho. Ili kuzuia vita visivyokuwa na msingi.
Shetani asipoelewa kile tunachoomba kwa Mungu, inamwia vigumu kwake kupanga mashambulizi, kwasababu hajui ni nini tunamwomba Mungu kwa wakati huo, hivyo anabaki tu hapo katikati, lakini akisikia unamwomba Mungu akupe Amani, au akupe riziki Fulani, tayari na yeye kashajua ni eneo gani aende kukupiga vita ili usipokee kile ulichomwomba Mungu. Ndio maana Mtume Paulo kwa ufunuo wa roho aliliona hilo na akawaandikia watakatifu..
1Wakorintho 14:2 “Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye; lakini anena mambo ya siri katika roho yake”.
Hivyo usijizuie kunena kwa lugha kama umejaliwa hilo.. itakusaidia kuzuia vita vingi katika ulimwengu wa mwili na wa roho.
Je kunena kwa Lugha mpya kukoje?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
SEMA KWA LUGHA NYINGINE.
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.