UMEONDOLEWA DHAMBI?

UMEONDOLEWA DHAMBI?

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu lililo taa ya miguu yetu na mwanga wa njia yetu. (Zab. 119:105).

Kuna tofauti ya Msamaha wa dhambi na Ondoleo la dhambi.

Mtu anapokukosea  labda amekutukana au kukuibia na akikuomba msamaha unaweza kumsamahe  (ukamwachilia kabisa moyoni mwako) lakini kumsamehe kwako hakumfanyi yeye kuacha ile tabia.. Maana yake ni kwamba kama ile tabia haitaondoka ndani ya huyo mtu basi ni wazi kuwa atarudia lile kosa siku nyingine. Atapumzika siku mbili au tatu na baadaye atarudia lile kosa. Sasa mtu kama huyu kapata msahama lakini si ondoleo la ile tabia.

Vile vile kwa Mungu tunaweza kupata msamaha wa makosa yetu na dhambi zetu, lakini kama hatutapata Ondoloe la dhambi hizo (Maana yake kama ule mzizi wa dhambi ndani yetu hautang’olewa) basi tutabaki vile vile, kila mara tutarudia makosa yale yale. Na mzizi wa dhambi ni lazima uondoke maishani mwetu kwasababu ndicho kitu kilichomleta Bwana Yesu duniani.

Bwana Yesu hakuja tu kuleta msamaha wa dhambi bali pia ondoleo la dhambi..Kwasababu msamaha wa dhambi ulikuwepo hata kabla ya Bwana Yesu kuja duniani, watu waliomba msamaha mbele za Mungu na wakasamehewa makosa yao, lakini Ondoleo la dhambi halikuwepo, Dhambi hazikuondolewa katika kumbukumbu za Mungu (zilifunikwa tu) na vile vile hazikuondolewa ndani ya mtu, bado watu waliendelea kurudia makosa yale yale, baada ya Bwana Yesu kuja watu ndipo wakapata ondoleo la dhambi, ndani yao (utumwa wa dhambi ukakoma kwa wale wote waliompokea).

Sasa tunapataje ondoleo la dhambi?.. kiasi kwamba dhambi haitupelekeshi tena wala kututawala?

Kwanza ni kwa kutubu mbele za Mungu, na kukiri kwamba sisi ni wakosaji, (hapa unatubia makosa yako yote ambayo umeyafanya kwa kujua, na kwa kutokujua mbele za Mungu, kwa tendo hilo Bwana atakusamehe ikiwa toba hiyo imetoka kweli ndani ya moyo na kwamba umekusudia kubadilika kabisa..)

Sasa hatua inayofuata ili Dhambi zako ziondolewe (ule mzizi wa dhambi ndani yako uondoke) baada ya kutubu ni wewe kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi…  Hiki ni kipengele cha muhimu sana ambacho si cha kupuuzia hata kidogo..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU

Ubatizo sahihi unakamilisha toba na hivyo mtu anayefanya hayo Mungu anampa zawadi ya Roho Mtakatifu pamoja na Ondoleo la dhambi, jambo ambalo ni muhimu sana.

Mtu huyu kama toba yake imetoka ndani ya moyo kabisa basi ule uzinzi uliokuwa unamsumbua mara kwa mara unakufa, anajikuta anaushinda uasherati na haurudii tena, kwasababu dhambi imeondolewa ndani yake, zile tabia zilizokuwa zinamwendesha mara kwa mara zinaondoka ndani yake kwasababu ule mzizi wa dhambi umeondolewa ndani yake n.k n.K

Na kumbuka ni muhimu sana kubatizwa ubatizo ulio sahihi, kwasababu si kila batizo zinaondoa dhambi.. nyingine utabatizwa lakini utabaki vile vile. Na ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Matendo 19:10)!.

Je unataka usiendelee kuwa mtumwa wa dhambi?.. Tumia kanuni hiyo ya Matendo 2:27-37. Na Mungu ni mwaminifu atafanya sawasawa na Neno lake.

Maran atha.

Ikiwa hujabatizwa bado na unahitaji msaada wa kupata ubatizo sahihi, basi waweza kuwasiliana nasi kwa namba zetu na tutakusaidia kwa hilo.

Shalom

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

AGIZO LA TOBA LINAENDANA NA UBATIZO!.

NINI MAANA YA KUTUBU

Dameski ni wapi kwasasa?

BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.

Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?

Rudi nyumbani

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments