Swali: Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma jua na mwezi viliumbwa katika siku ya 4 , sasa napenda kujua kabla ya hapo siku zilihesabiwaje, maana jua ndilo linalotenga mchana na usiku…na maandiko yanatuonyesha kuwa lilikuja kuumbwa siku ya 4?
Jibu: Ni kweli jua na mwezi viliumbwa siku ya 4, tena baada ya miti na miche ya kondeni kuumbwa (Mwanzo 1:14).
Lakini ukisoma kuanzia mstari wa pili katika kitabu hiko cha Mwanzo, utaona Mungu tayari alikuwa ameshaumba mchana na usiku na ameshatenga giza na nuru.
Mwanzo 1:1 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; MUNGU AKATENGA NURU NA GIZA.
5 MUNGU AKAIITA NURU MCHANA, NA GIZA AKALIITA USIKU. IKAWA JIONI IKAWA ASUBUHI, SIKU MOJA”.
Umeona?..kumbe tayari Mungu alikuwa ameshaumba mchana na usiku kabla hata ya kuumba jua. Maana yake hata kama asingeumba jua bado majira na mchana na usiku yangekuwepo kwasababu yeye mwenyewe ndio Nuru ya ulimwengu (mwilini na rohoni).
Yohana 8:12 “Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima”.
Ndio maana katika ile mbingu mpya na nchi mpya hakutakuwepo na jua na bado Nuru itakuwepo.
Ufunuo 21:23 “Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo”.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa Mungu aliumba mchana na usiku, kabla ya kuliumba jua..na hiyo ni kuonyesha utukufu wake yeye, na pia kuonyesha kuwa yeye ndiye Nuru halisi Na ndio chanzo cha Nuru yote.
Je umempokea Bwana Yesu aliye Nuru ya kweli? Kama bado fahamu kuwa bado upo gizani ijapokuwa jua linakumulika…kwahiyo ni vyema ukafanya maamuzi thabiti leo ya kumpokea na kuokoka.
Yohana 12:46 “Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani”
Soma pia Yohana 9:5 na Yohana 11:9.
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je! mwanadamu wa kwanza kuumbwa ni yupi?
NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.
Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?
SWALI: Mtume Paulo alikuwa na maana gani aliposema “nimeaminiwa uwakili”?
1Wakorintho 9:16 “Maana, ijapokuwa naihubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimewekewa sharti; tena ole wangu nisipoihubiri Injili! 17 Maana nikiitenda kazi hii kwa hiari yangu nina thawabu; ila ikiwa si kwa hiari yangu, nimeaminiwa uwakili”.
JIBU: Mtume Paulo aliifanya kazi ya Mungu, kana kwamba ni muajiwa/kibarua aliyepewa dhamana ya kusimamia kazi zote alizowekewa chini yake kwa uangalifu, kana kwamba akipoteza chochote au akileta hasara ya jambo lolote atawajibishwa, na boss wake utakapofika muda wa mahesabu.
Tofauti na mtu aliyejitolea tu kazi, kama kusaidia, mtu wa namna hiyo hata akiacha wakati wowote, hawezi kuwajibishwa zaidi sana atapewa shukrani, kwa kutoa mchango wake katika shughuli hiyo, na kupewa viposho.
Ndio maana ya hiyo kauli, “nimeaminiwa uwakili”..kwa lugha nyepesi “nimeamiwa kazi ya mtu mwingine niisimamie kama kijakazi” Na hiyo ndiyo iliyompelekea Mtume Paulo, kusema mimi ni ‘mtumwa na mfungwa’ wa Yesu Kristo (Warumi 1:1,Waefeso 3:1).. Kwasababu hiyo akaitenda kazi ya Mungu kwa uaminifu wote, na kwa umakini wote, hata zaidi ya mitume wengine.
Ni funzo gani tunalipata.
Nasi pia tukiichukulia kazi ya Mungu kama sio jambo la hiari, au la kujitolea tu, bali kama ndio sehemu ya kazi yetu tuliyoajiriwa na Mungu hapa duniani, na kwamba tusipoifanya kwa uaminifu tukaleta hasara, tutatolea hesabu yake siku ya mwisho,..
Yaani tukimtumikia Mungu kama vile tuzitumikiavyo kazi zetu maofisi, bila kuwa na udhuru wowote.
basi tutajifunza kuitenda bila ulegevu Na mwisho wake utakuwa ni kupewa thawabu kubwa na kutukuzwa sana na Bwana Yesu tutakapofika kule mbinguni.
Lakini kama tutajitoa kwa Mungu pale tunapojisikia tu, au tunapokuwa na nafasi, au tunapokumbushwa, au tunapofanikiwa sisi si watumwa au wafungwa wa Yesu Kristo, bali ni watumishi wake tu. Hatujafikia hatua hiyo ya kuitwa watumwa wake.
Bwana atujalie utumishi bora, kama huo, wa kuaminiwa uwakili
Shalom
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JIFANYIE RAFIKI KWA MALI YA UDHALIMU.
Mungu alikuwa anaongea na nani aliposema na “Tumfanye mtu kwa mfano wetu”
Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?
Pesa za bindoni ni nini?(Marko 6:8)
Kutazama Nyakati mbaya ni kufanyaje?.
UTAMBUE UJUMBE WA SAA UNAYOISHI.
Yerusalemu, ni Neno la kiyahudi linalomaanisha “Mji wa amani” au “msingi wa amani” .
Kabla ya mji huu kupata sifa tunayoifahamu sasahivi, awali ulikuwa ni mji wa wakaanani, waliojulikana kama wayebusi, kipindi ambacho wayahudi bado hawajaimiliki nchi yao.
Hivyo baada ya wana wa Israeli kuiteka nchi ya kaanani, eneo ambalo lilikuwepo huu mji, liligawanya kwa kabila la Yuda. Lakini hawa wayebusi hawakuondolewa moja kwa moja katika mji huo wa Yerusalemu, bado ukaendelea kuwa chini ya milki yao.
Mpaka baadaye, Daudi alipouvamia na kuwaondoa wayebusi. Ndipo Mji huo ukaitwa “Mji wa Daudi”.(2Samweli 5:6-10) Baadaye akalihamishia Sanduku la Mungu la agano, mpaka mji huo, hivyo kidogo kidogo ukaanza kupokea sifa ya kuwa kiini cha dini (2Samweli 6:1-19). Daudi akaazimia kumjengea Mungu hekalu ambalo, atamwekea Mungu agano lake huko. Lakini hakuruhusiwa kwasababu ya mauaji mengi aliyoyasababisha, Mpaka mtoto wake Sulemani, alipokuja kulijenga, Hapo ndipo wana wote wa Israeli wakapafanya Yerusalemu kuwa kitovu cha kumwabudia Mungu. Na Mungu pia akapabariki na kupachagua pawe mji wake mtakatifu, kati ya miji yote, ambapo ataliweka jina lake, lijulikane kwa mataifa yote ya ulimwengu..
Japokuwa eneo la mji huu, lilibomolewa na kujengwa mara kadhaa, lakini hapo ndipo mfalme wetu Yesu Kristo atakapokuja kutawalia dunia yote katika ule utawala wa miaka 1000 kama mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana, atakaporudi mara ya pili.
Lakini biblia inatuonyesha kuwa upo mji mwingine wa kimbinguni, ambao Mungu amewaandalia watu wake,..ujulikanao kama YERUSALEMU MPYA.
Umechukua jina la Yerusalemu hii ya duniani, ili kutupa picha tuelewe vizuri utakavyokuwa. Mji huo utashuka kutoka mbinguni kwa Mungu mwenyewe na kuja hapa duniani. Ndani ya mji huo maandiko yanasema “hakitaingia chochote kilicho kinyonge”. Isipokuwa watu maalumu sana wajulikanao kama bibi-arusi wa Kristo.. Kumbuka si kila atakayepokea uzima wa milele, atakuwa na daraja sawa na mwenzake..Uaminifu wako, na utumishi wako sasa, vinaeneleza wewe utastahili kukaa wapi utakapofika kule ng’ambo. Wapo ambao watastahili kukaa ndani ya mji, na wapo ambao watakaa nje ya mji huo mtakatifu. Japo wote watakuwa ni watakatifu.
Ndani ya huo mji ndio yatakuwa makao mapya ya Mungu milele (Ufunuo 21:3), Mambo yaliyopo huko ni mazuri biblia inasema jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia(1Wakorintho 2:9). Kwa ufupi ni kwamba kila mmoja wetu atajuta, kwanini hakujibidiisha kwa Mungu sana kwa uzuri atakaokutana nao huko.
Huu ndio mji ambao Ibrahimu aliuona..ukamfanya aishi kama mpitaji tu hapa duniani, japokuwa alikuwa na mali nyingi na utajiri mwingi..
Waebrania 11:9 “Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.
10 Maana alikuwa AKIUTAZAMIA MJI WENYE MISINGI, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu”.
Tafakari maandiko haya;
Ufunuo 21:1 “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure.
7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Je! Na wewe utakuwa na sehemu ndani ya mji ule?
Maran atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.
Hisopu/ Hisopo ni nini katika biblia?(Zaburi 51:7)
Neno ‘Kima’ linamaanisha nini Katika biblia? (Mathayo 27:9 )
SWALI: Nini maana ya maandiko haya?
Mithali 25:28 “Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta”.
JIBU: Mstari huu unatupa picha jinsi mtu asiyeweza kuitawala roho yake anavyoonekana rohoni.Hapo anasema, roho yake imefanana na mji uliobomolewa usio na kuta..
Zamani, miji mikubwa ilipojengwa ilikuwa ni lazima izungushiwe kuta kubwa na ndefu.. Yerusalemu ulizungushiwa kuta, Babeli ulizungushiwa kuta, Yeriko ulizungushiwa kutwa n.k. Na lengo la kufanya vile ilikuwa ni kuulinda mji dhidi ya wavamizi, na wapepelezi, wasiingie kokote tu watakako na kuushambulia mji.
Ni vijiji na vimiji vidogo tu ndivyo vilikuwa havina kuta zinazozunguka..lakini miji yote ilikuwa ni lazima iwe na sifa hiyo.
Sasa na rohoni ndivyo ilivyo, ikiwa na maana, kama wewe si mtu wa kuitawala roho yako, ni sawa na ule mji usio na kuta..Na matokeo yake ni kuwa upo hatarini kuvamiwa na kila aina ya maadui zako wa rohoni.
Ukishindwa kuizuia roho yako na tamaa za huu ulimwengu..Kwamba kila kitu unachojisikia kukifanya, wewe unafanya, kijisikia kuzini unakwenda kuzini, ukijisikia kunywa pombe unakunywa.. ukijisikia kuvaa vimini unavaa, ukijisikia kuvaa suruali unavaa, ukijisikia kutumia mkorogo unatumia, fahamu kuwa, utakuwa ni makao ya mapepo yote mabaya duniani.
Kwasababu roho yako haina ulinzi. Ndugu si kila kitu unachokiona, ukifanye, au ukiangalie, au ukisikilize, unapokesha muda wote kwenye tamthilia, kwenye simu unachati, lakini muda wa kuomba huna, muda wa kujifunza Neno huna.. Wewe ni mji usiokuwa na ukuta..
Utaombewa leo, mapepo yatatoka, lakini kesho yatarudi tena mengine mengi tu, tatizo ni hilo, umefungua malango kwa kila roho inayojisikia kukuingia ..kwasababu umeshindwa kuitawala roho yako. Leo rafiki yako anakuja kukwambia tukabeti, na wewe bila kufikiri unakimbilia huko, unatazama picha za ngono, unasikiliza miziki ya kidunia, ni lazima uvamiwe na mapepo.
Mithali 4:23 “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima”.
Hivyo ni lazima tujifunze kuzitawala roho zetu, sawasawa na maandiko yanavyotasa.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI YA KUUHARIBU UJANA WAKO.
Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
Swali: Katika 1Wakorintho 7:36 Mtume Paulo anafundisha kuwa Mtu akiona hamtendei vyema mwanamwali wake basi aruhusu waoane”.. Je alikuwa ana maana gani kusema hivyo? (Au kwa ujumla mstari huo unamaanisha nini)?.
Jibu: Labda tuanze kusoma kuanzia juu kidogo mstari wa 34.
“1Wakorintho 7:34 “Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
35 Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.
36 Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.
37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.
38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema.”
Hapa Paulo kwa kuongozwa na roho anatoa USHAURI WA KITUME, juu ya watu wanaotaka kuoa na wale wasiotaka kuoa, au wa wale wanaotaka kuolewa na wasiotaka kuolewa.
Ukisoma kuanza juu zaidi utaona anashauri kuwa ni “Ni heri mtu akae bila kuoa kabisa, au kutoolewa kabisa kwaajili ya Bwana, kuliko kuoa au kuolewa”.. lakini hiyo sio sharti au Amri, bali chaguzi la mtu!!. Maana yake ni kuwa Mtu atakayeoa atakuwa hafanyi dhambi, na vile vile atakayeolewa atakuwa hafanyi dhambi… Lakini mtu ambaye atakaa bila kuoa au kuolewa, huyo ana faida mara nyingi zaidi kwasababu atakuwa atajishughulisha zaidi na mambo ya Mungu pasipo kuvutwa, au kusongwa na mambo mengine ya kifamilia.
1Wakorintho 7:32 “Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje Bwana;
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe”
Lakini Paulo hajaishia tu kutoa ushauri kwa Watu wanaotaka kuoa au kuolewa, bali alienda mpaka kwa wazazi wenye mabinti majumbani kwao ambao ni mabikira (wanawali).
Akashauri kuwa ikiwa Mzazi, anaye binti au mabinti ambao bado hawajaolewa, Na mzazi huyo anatamani mabinti wake wamtumikie Mungu pasipo kuvutwa na mambo mengine, zaidi sana na yeye mwenyewe ana uwezo wa kuyatawala mapenzi yake (Yaani sio kigeugeu, cha kutamani kupata wajukuu au kuitwa mkwe), basi anaweza kuwadumisha wanawe (mabinti wake) katika kuishi maisha ya kutotamani kuolewa, ili wamtumikie Mungu vyema, pasipo kuvutwa na mambo mengine..kama wale mabinti wane wa Filipo waliokuwa manabii, wanatabiri..
Matendo 21:8 “Asubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.
9 Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri”.
Kuwalea mabinti kwa namna hiyo kuna faida kubwa sana…kwasababu biblia inasema katika Mithali 22: 6 “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee”. Ikiwa na maana kuwa msingi ambao mtoto wako utakaomwekea tangia akiwa mdogo huo hawezi kuuacha mpaka atakapokuwa mtu mzima. Na msingi mmojawapo ambao ni mzuri ndio huo wa Kutokuja kuolewa/kuoa, ili kusudi wamtumikie Mungu pasipo kuvutwa na mambo mengine, katika siku za mbeleni.
Sasa Paulo hajatoa amri kwamba ni lazima wazazi wote wafanye hivyo kwa mabinti zao… bali ni “Ushauri tu wa kitume anaoutoa”.. Lakini pia anaendelea kusema, ikiwa mzazi anaona kuwa binti yake (Mwanamwali wake), hamtendei jinsi ipasavyo (maana yake binti yake anatamani kuolewa na yeye mzazi ni kikwazo) basi hapaswi kuendelea kumshikilia huyo binti kwa kumzuia kuolewa, bali amruhusu aolewe, na kwa kufanya hivyo pia atakuwa hatendi dhambi..
1Wakorintho 7:36 “Lakini mtu awaye yote akiona ya kuwa hamtendei mwanamwali wake vipendezavyo, na ikiwa huyo amepita uzuri wa ujana wake, na ikiwapo haja, basi, afanye apendavyo, hatendi dhambi, na awaruhusu waoane.
37 Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.
38 Basi, hivyo na amwozaye mwanamwali wake afanya vema; na yeye asiyemwoza atazidi kufanya vema”.
Ni nini tunajifunza?
Kama mzazi, mojawapo ya mafundisho au msingi wa kuwawekea wanao ni pamoja na huo wa kutafakari au kufikiri kutokuja kuoa au kuolewa huko mbeleni (kwaajili ya Bwana).. Kumbuka “sio kumzuia mwanao kuoa au kuolewa” la! bali kumfundisha au kumwekea msingi huo, ili atakapokuja kufikia umri wake mwenyewe aone kila sababu za yeye kuishi kama alivyo kwaajili ya Bwana na utumishi wake..
Ushauri huu unaweza kuonekana kama mpya na wa ajabu lakini ndio ushauri wa kitume. (Paulo, aliye baba yetu wa kiroho alilihakiki hilo kwa msaada wa roho) hivyo na sisi tukitaka tupate faida nyingi za kiroho basi tusikilize ushauri huo. Lakini si Lazima, wala si sharti.(hatujalazimishwa)
1Timotheo 2:7 “Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli”.
Bwana akubariki.
Ikiwa kama unapenda kujua zaidi kama ni Sharti mchungaji kuoa au kutokuoa katika utumishi wake basi unaweza kufungua hapa>> Je! Mtu ambaye hajaoa anaruhusiwa kulichunga kundi?
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JE NI HALALI KUOA WAKE WENGI, AU KUTOA TALAKA?
Wanafunzi wa Yesu, walimaanisha nini kusema kama “Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa”?
Biblia inasema Bwana Yesu alifundisha kwa mifano. Naomba kuelewa hiyo mifano ni nini? Na dhumuni lake lilikuwa ni lipi?
Mifano, ni hadithi zinazoambatanishwa na habari husika, ili kueleza uhalisia zaidi wa ukweli huo.
Bwana Yesu alitumia mfumo huu, wa hadithi za kidunia ili kueleza uhalisia wa mambo ya ufalme wa mbinguni. Na takribani mafundisho yake yote yalitegemea mifano.
Mathayo 13:34 “Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno;
35 ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali”.
Mpaka ikafikia wakati Fulani wanafunzi wake wanamuuliza kwanini unapenda kutumia mifano kufundisha watu?(Mathayo 13:10)
Kwamfano alipotaka kueleza habari ya madhara ya kutokusamehe, alitumia hadithi ya yule mtu aliyedaiwa talanta elfu kumi, ambaye alikuwa karibuni na kuuzwa kwa kukosa cha kulipa, lakini bwana wake akamuhurumia akamsemehe deni lote, lakini yeye alipokutana na mtumwa wake aliyemdai dinari 100 tu hakutaka kumsamehe, matokeo yake bwana wake aliposikia tabia yake hiyo akamkamata na kumtupa gerezani, mpaka na yeye atakapolipa yote(Mathayo 18:21-35).
Hivyo mtu unaposikia hadithi hiyo, inakupelekea kuelewa zaidi jinsi Mungu naye anavyojisikia pale tunaposhindwa kuwasamehe watu makosa yao .
Katika Biblia ni mifano zaidi ya 30 Bwana Yesu aliisema, lakini ni mingi zaidi ya hiyo aliifundisha, ambayo haijaandikwa kwenye biblia, (Yohana 21:25)
Madhumuni na mifano hiyo yalikuwa ni mawili:
Bwana Yesu alipoizungumza kwa waliokuwa na kiu ya kusikia, aliieleza kwa uwazi wote bila maficho yoyote.
Lakini alipokutana na kundi la watu ambao hawakuwa na nia ya kujifunza, watu wenye wivu, mafarisayo na waandishi ambao walimkufuru Roho Mtakatifu pamoja na maherodi, alikuwa anatumia mifano ya mafumbo, ili wasielewe chochote. Na alipokuwa peke yake alihakikisha anawafunulia mafumbo hayo wale ambao walikuwa na kiu ya kuujua ukweli.
Mathayo 13:13 “Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya”.
Hivyo mfumo huu hata sasa Bwana anautumia rohoni.. ukiwa kweli na nia ya kumjua Mungu, atakufundisha sana, na kutumia hata mifano halisi ya kimaisha ili mradi tu ahakikishe unayaelewa mapenzi yake, vema na kwa ufasaha wote. Lakini ikiwa mwovu, na unajifanya unamjua Mungu, ukweli ni kwamba hutamwelewa, atakuja kwako kwa mafumbo mengi tu.. Utakuwa kila siku ni mtu wa kutomwelewa Mungu, na kumtumikia kidini tu.
Bwana Yesu atusaidie tuwe na kiu ya kweli kwake. Kwasababu hii biblia haijakusudiwa kila mtu aielewe bali wale wenye nia tu ya dhati kwa Bwana..walio maskini wa roho.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KWA WALE WALIO NJE “YOTE” HUFANYWA KWA MIFANO
Kwa aibu yako mwenyewe, na kwa aibu ya uchi wa mama yako.
MAKABURI YAKAFUNUKA; IKAINUKA MIILI MINGI YA WATAKATIFU WALIOLALA;
Ni kwanini Yesu alisema “Na wakisikia wasikie, wasielewe Wasije wakaongoka?”
Biblia inamaana gani iliposema “Dhambi ilipozidi, Neema ilizidi kuwa nyingi Zaidi”.
Swali: Napenda kujua tunampendaje Bwana Mungu wetu kwa mioyo yetu yote, kwa roho zetu zote, kwa nguvu zetu zote, na kwa akili zetu zote kulingana na Marko 12:30.
Jibu: Tuanze kusoma kuanzia mstari wa 28..
Marko 12:28 “Na mmojawapo wa waandishi akafika, akawasikia wakisemezana naye, akatambua ya kuwa amewajibu vema, akamwuliza, Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?
29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;
30 nawe mpende Bwana Mungu wako KWA MOYO WAKO WOTE, na KWA ROHO YAKO YOTE, na KWA AKILI ZAKO ZOTE, na KWA NGUVU ZAKO ZOTE.
31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi”.
Awali ya yote ni vizuri tukajua tofauti ya “OMBI” na “AMRI”. Ombi ni kitu ambacho unaombwa ukifanye, na endapo usipokifanya basi huwezi kuhesabiwa makosa, kwasababu ni Ombi, (lina uchaguzi wa kukubali au kukataa) lakini AMRI ni kitu ambacho mtu unaamriwa kukifanya (iwe unapenda au hupendi, ni sharti ukifanye), na endapo usipokifanya basi inakuwa ni kosa!.
Sasa hapo Bwana Yesu aliposema kuwa “AMRI” ya kwanza ni kumpenda Bwana Mungu kwa moyo wote, roho yote, akili zote na nguvu zote, Hiyo Ni AMRI na si OMBI. Maana yake mtu yeyote asiyempenda Bwana Mungu wake kwa viwango hivyo, basi mtu huyo kavunja amri ya Kwanza na ataenda kuhukumiwa!.
Ndio maana Mtume Paulo kwa uweza wa Roho aliandika maneno haya..1Wakorintho 16:22 “Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha”.
Maana yake kutompenda Bwana ni laana kubwa!.. kwasababu ni kuvunja amri ya kwanza.
Sasa tukirudi kwenye swali letu, Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo wote, roho zote, akili zote na nguvu zote?
1.KWA MOYO WOTE
Kufanya kitu kwa moyo maana yake ni kukifanya kitu kwa hiari.. pasipo kuwa na mambo au mawazo mengine ya kando kando, kama malalamiko, manung’uniko, majivuno, au pasipo kusukumwa sukumwa.
Kwahiyo maana ya kumpenda Mungu kwa Moyo wote, maana yake ni kumpenda Mungu pasipo masharti.. Maana yake kama unamtolea Mungu zaka, au sadaka basi unamtolea kwa kupenda wewe mwenyewe,na si kwasababu umeshurutishwa au kwasababu biblia inasema tumtolee…hapana bali unamtolea kana kwamba hakuna sheria yoyote iliyokuambia ufanye hivyo..
Vile vile kama unamtumikia, katika kuhubiri, kumwimbia, kusaidia wengine n.k basi unapaswa umtumikia kwa moyo, kana kwamba hakuna sheria iliyokuambia ufanye hivyo…
Luka 17:10 “Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya”
2. KWA ROHO YOTE
Roho siku zote ni chumba cha IBADA… Na mtu anayefanya ibada kwa Mungu maana yake anamwabudu Mungu, kwasababu neno lenyewe “Ibada” limetokana na Neno “kuabudu”..
Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba KATIKA ROHO NA KWELI. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu”.
Ukimpenda Bwana kwa Roho yote, maana yake kila wakati utatafakari na kutafuta kumfanyia Mungu ibada iliyo kamilifu… hutafanya ibada iliyo nje na Kweli ya Mungu.. Kila siku utahakiki ibada unayoifanya kama ni katika roho na katika Kweli ya Mungu (Neno la Mungu), na utaifanya hivyo kwa bidii sana. Hutamchanganya Mungu na sanamu!, wala hutamchanganya Mungu na matambiko ya kimila, wala hutakuwa vuguvugu katika Imani yako…utajituma kufika ibadani siku zote, utajituma kuomba siku zote na mambo yote ya kiibada yatakuwa ni mambo ya kwanza katika maisha yako.
3. KWA NGUVU ZAKO ZOTE.
Wakati wa kuwa na NGUVU ni wakati wa “Ujana”.. Hiki ndicho kipindi ambacho watu wote wanapaswa watie bidii katika kumtafuta Mungu.
1Yohana 2:14b “… Nimewaandikia ninyi, vijana, KWA SABABU MNA NGUVU, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu”.
Wakati wa ujana ni wakati ambao roho zetu zinakuwa na uwezo mkubwa wa kutunza maneno ya Mungu, kuliko wakati wa uzee.. Kiasi kwamba mtu anayeyasoma maandiko katika ujana ni rahisi maandiko yale kukaa ndani yake kwa muda mrefu na kuzaa matunda zaidi ya mtu mzima (mzee), jambo ambalo shetani analiogopa sana!.. Ndio maana hapo maandiko yanasema.. “Nimewaandikia ninyi, vijana, KWA SABABU MNA NGUVU, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, NANYI MMEMSHINDA YULE MWOVU”.
Vile vile katika kitabu cha Mhubiri 12:1 maandiko yanasema “Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo”.
Maana yake itafika kipindi (utakapokuwa mzee) utatamani Neno la Mungu likae na kudumu ndani yako lakini halitakaa na hivyo utakosa furaha, kwasababu Nguvu zako zitakuwa zimeisha.
Kwahiyo maana ya kumpenda Bwana kwa nguvu zote maana yake ni kumpenda BWANA katika ujana wako wote; unatumia muda mwingi katika kuomba maadamu unazo nguvu za mwili, vile vile unatumia muda mwingi katika kwenda kuhubiri maadamu unayo miguu yenye nguvu, pia unatumia muda mwingi katika kujifunza Neno la Mungu katika miaka ya ujana ambayo unazo nguvu katika roho za kuyatunza maneno ya Mungu.
Wengi wanasema nitamgeukia Mungu na kumtumikia nikiwa mzee.. kamwe usijaribu kuwaza hivyo!..biblia inasema kama unamkataa Mungu leo, utakapofikia uzee hutakuwa na Furaha wala Nguvu (Mhubiri 12:1).
Na pia Bwana Yesu alimwuliza Petro mara tatu, kama anampenda angali akiwa kijana..na akamwambia ukweli kuwa kama hatajishughulisha sasa katika kumtafuta yeye, na kumtumikia angali akiwa kijana, basi asitegemee ataweza akiwa mzee, kwasababu wakati wa uzee hatakuwa na hizo nguvu, bali atapelekwa huku na huko mahali asipopataka..
Yohana 21:15 “Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni Petro, Je! Simoni wa Yohana, WEWE WANIPENDA KULIKO HAWA? Akamwambia , Naam ,Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu.
16 Akamwambia tena mara ya pili, Simoni wa Yohana, WANIPENDA? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.
17 Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, WANIPENDA? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu.
18 Akasema, Amin, amin, nakuambia, WAKATI ULIPOKUWA KIJANA, ulikuwa ukijifunga mwenyewe na kwenda utakako; lakini utakapokuwa mzee, utainyosha mikono yako, na mwingine atakufunga na kukuchukua usikotaka
4. KWA AKILI ZAKO ZOTE.
Akili ni utashi wa kufanya mambo na kuyarahisisha yale yanayoonekana kuwa ni magumu… Kila mtu anazo akili za mwili alizojaliwa na Mungu, (Ingawa dhambi inaweza kumfanya mtu aonekane hana akili kabisa mbele za Mungu).
Hivyo kama umejiepusha na dhambi basi unazo akili, Hivyo katika hizo ulizopewa zitumie katika kumtumikia Mungu na kumtafuta.
Kwamfano katika dunia ya sasa, huwezi kusema utamtafuta Mungu halafu umkose, ikiwa umedhamiria kweli kumtafuta kwa akili zetu zote.. Yeye (Mungu) anasema tukimtafuta tutamwona (Yeremia 29:13).
Hebu tafakari Leo hii kuna simu nyingi feki kuliko orijino masokoni, lakini pamoja na kwamba feki ni nyingi mno kuliko orijino, lakini utaona kuna mtu anaitafuta orijino mpaka anaipata!.. Utaona anaulizia huku na huku, na kufanya uchunguzi huu na ule, mpaka anafikia kujua vimelea vya orijino na feki, na hatimaye anaipata iliyo orijino na kuiacha feki. (hapo ametumia akili zake zote kuitafuta simu orijino mpaka kaipata).
Lakini katika kumtafuta Mungu, utasikia mtu anakuambia “siku hizi manabii wa uongo wengi, sijui tumwamini yupi tumwache yupi” Hivyo anaamua tu!, kuacha kumtafuta Mungu, au kwenda kanisani..kwasababu tu manabii wa uongo wengi, au kwasababu tu, upotofu ni mwingi..
Mtu kama huyu hajaamua kutumia akili yake yote katika kumtafuta Mungu!! Ni mvivu wa akili.. kwasababu anao uwezo wa kutumia akili yake yote kutafuta simu orijino katikati ya feki, lakini si kuutafuta ukweli wa Mungu katikati ya uongo.
Lakini kama angeamua kutumia akili yake kidogo tu, na kuanza kuchambua hao wa uongo kupitia neno la Mungu, na kutafuta huku na huko, na kuulizia ulizia, na kutafiti tafiti, ni wazi kuwa siku moja angefika katika ukweli, na angewasaidia pia na wengine..
Lakini anadhani kwa yeye kutomtafuta Mungu siku ile atatoa udhuru mbele za Mungu, pasipo kujua kuwa anaivunja amri ya kwanza ya Mungu, ya kumpenda yeye kwa akili zote.
Ndugu Dada/Kaka.. Usipomtafuta Mungu sasa katika nyakati hizi, usipompenda kwa moyo wako wote na roho yako yote, na nguvu zako zote na akili zako zote, fahamu kuwa siku ya mwisho hutakuwa na udhuru, wala hakuna mwanadamu yoyote atakayekuwa na udhuru.
Bwana Yesu atusaidie tumpende yeye kwa vitu hivyo vinne kwa bidii sana.
Maran atha!.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
ILI TUONEKANE SAFI MBELE ZA MUNGU TUFANYE NINI?
Mtu asiye na akili ni nani kibiblia?
Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
Swali: Je kuna tofauti gani ya Mola na Mungu, na je sisi wakristo ni sahihi kutumia Jina Mola badala ya Mungu?
Jibu: Neno Mola, limeonekana mara kadhaa katika biblia…
Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, MOLA, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo”
Yuda 1:4 “Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake MOLA, na Bwana wetu Yesu Kristo”.
Ufunuo 6:10 “Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, EE MOLA, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi”.
Maana ya MOLA ni “Mungu-Mtawala”…
Neno ‘Mungu’ maana yake ni “Muumbaji”, yaani aliyeumba vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana.. lakini jina Mola limeingia ndani zaidi, kumtaja Mungu kama Mtawala, Ni sawa na mtu anayesema “Mungu mwenyezi” badala ya “Mungu” au Mtu anayesema “Mungu mwenye Nguvu” badala ya “Mungu tu”. Mtu anayeomba kwa kumtaja Mungu pamoja na na sifa yake nyingine, hoja zake zinakuwa na Nguvu zaidi kuliko Yule anayetaja Mungu tu.
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba, sisi wakristo ni sahihi kabisa kutumia neno Mola katika maombi yetu, kwasababu ni jina linaloelezea zaidi uweza wa Mungu, Ndio maana Wanafunzi walipokusanyika na kuomba baada ya Petro na Yohana kufunguliwa kutoka gerezani, maandiko yanasema pale walipokuwepo palitikiswa na wote wakajazwa Roho Mtakatifu na wakanena Neno la Mungu kwa ujasiri.
Matendo 4:24 “Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
25 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?………………..
31 HATA WALIPOKWISHA KUMWOMBA MUNGU, MAHALI PALE WALIPOKUSANYIKA PAKATIKISWA, WOTE WAKAJAA ROHO MTAKATIFU, WAKANENA NENO LA MUNGU KWA UJASIRI”.
Bwana Yesu akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
USIMLAANI KIZIWI, WALA USITIE KWAZO MBELE YA KIPOFU.
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, WALA MTU ATAZAMAYE NYAKATI MBAYA, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu”.
Kutazama Nyakati mbaya kunakozungumziwa hapo ni “KWENDA KUTAFUTA SABABU YA ISHARA FULANI AMBAZO ZINAAMINIKA KUWA NI MBAYA”.. Mfano wa mtu akipishana na mbwa mweusi, au paka mweusi njiani au akimwona bundi juu ya bati lake, huwa inaaminika kuwa ni ishara mbaya au ya jambo fulani baya linalokuja.. Au mtu akijikwaa anaamini kuwa kuna mtu anamzungumzia vibaya…Hivyo mtu kama huyo unakuta anaenda kwa mganga, au kwa mnajimu, kutafuta maana ya ishara hiyo, au mbaya anayemfuatilia, sasa mtu huyo ndiye anayetafsirika kama “mtu atazamaye Nyakati mbaya”
Katika biblia Bwana Mungu aliwakataza wana wa Israeli, tabia ya kutazama nyakati mbaya. Kwasababu kwasababu ni imani potofu, ambayo inamwelekeza mtu kamwamini na kumwabudu shetani.
Kumbukumbu 18:13 “Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.
14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na kutazama bao; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Jambo hilo hilo Mungu analikataa hata sasa, kwasababu yeye ni Yule Yule jana na leo na hata milele (Waebrania 13:8).
Ukiwa ndani ya Kristo, viumbe na wanyama si kitu kwako, bundi na popo kwako watakuwa ni ndege wa kawaida, huna haja ya kuwaogopa wala kuwatazama hao kama ishara ya jambo fulani lijalo…. Ishara ya mambo mabaya yajayo ni dhambi maishani mwetu!.
Ukiwa msengenyaji, au mwasherati, au ulevi, au muabuduji wa sanamu basi hiyo ndio ishara tosha ya Majanga yajayo!.. Lakini tukiwa wasafi na dhamiri zetu zikiwa safi mbele za Mungu, hatuna haja ya kutafuta kuangalia nyakati mbaya kwasababu hakuna mabaya yoyote yatakayotujia, tunakuwa tunalindwa na kuzungukwa na Nguvu za Mungu.
Lakini ukitoka kwenda kwa mganga kutafuta hatima ya kesho yako, kutokana na ishara uliyoiona, ambayo unaamini kuwa ni ishara mbaya, basi fahamu kuwa unafanya machukizo mbele za Mungu, na siku ya mwisho utasimama hukumuni.
Bwana atusaidie tuepukane na hayo yote.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MUNGU ATAKUUA UKIWA MBAYA MACHONI PAKE.
NYAKATI SABA ZA KANISA NA WAJUMBE WAKE.
UTAYAFIKIAJE MANENO SAFI YA MUNGU?
Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu ATAZAMAYE BAO, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,
11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako……………….
14 Maana mataifa haya utakaowamiliki huwasikiliza wanaoshika nyakati mbaya na KUTAZAMA BAO; bali wewe, Bwana, Mungu wako, hakukupa ruhusa kutenda hayo”.
Kutazama bao ni aina ya uchawi, ambayo inahusisha kuwasiliana na wafu, au miungu kwa njia ya kipande kidogo cha Ubao..
Katika Nyakati za kale, na hata nyakati za sasa katika baadhi ya sehemu, aina hii ya uganga bado inaendelea kufanyika…ambapo, watu Fulani maalum (ambao ni wachawi/waganga) wanakuwa na “Ubao” na huo ubao unakuwa umeandikwa maandishi fulani, pamoja na tarakimu, na alama fulani zisizoeleweka.
Ambapo mtu/watu wanapotaka kujua mambo yaliyopita au yanayoendelea sasa, au yatakayokuja, basi wanaketi kuuzunguka ubao huo, na kisha kuweka vidole vyao katika sehemu mojawapo ya huo ubao kufuatia maelekezo ya huyo mganga, na kisha wanapokea taarifa wanazozihitaji kutoka kwa hiyo miungu kupitia mganga huyo, au kupitia wao wenyewe.
Katika karne ya 19, uliibuka ubao mmoja maarufu ujulikanao kama “Ubao wa Ouija”. Ubao huu ulipata umaarufu katika bara la Ulaya na baadaye katika bara la Marekani, ulitumika na wachawi wengi maarufu na watu wengi waliutumainia ikiwemo watu maarufu, ukiaminika kutoa taarifa nyingi za mambo yasiyojulikana, Ubao huo hata sasa unatumika lakini si maarufu kama ilivyokuwa katika karne hiyo ya 19.
Katika biblia Bwana Mungu aliwakataza wana wa Israeli “kutazama Bao” na ‘anatukataza hata sisi leo’. Kwasababu ni aina ya uchawi, na aliye nyuma ya ubao huo ni “shetani mwenyewe”.. akiwadanganya kuwa “ni wafu”. Hivyo ilikuwa ni kosa kubwa kwenda kutazama bao, ili kupata taarifa fulani zilizojificha.
Katika biblia tunamsoma mfalme mmoja wa Israeli aliyeitwa Manase, alikuwa ni mtu wa kutazama sana bao, jambo ambalo Mungu alishalikataza, na matokeo yake akajisababishia matatizo makubwa sana, kwani Mungu kumtoa katika ufalme kwa muda mpaka alipotubu.. na hata alipotubu bado madhara ya alichokuwa anakifanya hayakuondoka yote, kwani aliwakosesha Israeli na kuwafanya na wao kuwa watu wa kutazama bao. Na hivyo ikawa pia ni mojawapo ya sababu ya Mungu kuwapeleka utumwani Babeli.
2Wafalme 21:1 “Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba.
2 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli.
3 Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.
4 Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu.
5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana.
6 Akampitisha mwanawe motoni, AKATAZAMA BAO, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
7 Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;
8 wala sitawapotosha Israeli miguu watoke katika nchi niliyowapa baba zao; wakiangalia tu na kufanya sawasawa na yote niliyowaamuru, na kwa kuishika torati yote aliyowaamuru mtumishi wangu Musa.
9 Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.
Mstari wa 6 hapo, unasema “AKATAZAMA BAO” Maana yake lolote lililokuwa linaendelea asilolijua, hakutaka kumwuliza Mungu, ajibuye kwa njia ya ndoto, au manabii wake, badala yake yeye “alikimbilia kutazama bao”.. Na hivyo akadanganywa pakubwa sana na shetani..akawa anafanya machukizo mengi, ikawa dhambi kubwa sana kwake.
Na jambo lilolomchukiza Mungu kipindi hicho, linamchukiza hata leo..
Leo hii idadi kubwa ya watu wanaohudhuria kwa waganga wa kienyeji na kupewa maagizo ya kuweka viganja vyao juu ya vibao, au vibuyu, au mashuka, na kuambiwa mambo yao, hawajui kuwa wanafanya dhambi kama tu hiyo ya kutazama bao. Vile vile watu wanaobashiri (wanaoBET), nao pia ni watu wanaotazama Bao.
Ndugu, kama unataka kuweka sawa mambo yako ya kiroho na ya kimwili, suliuhisho ni moja tu!, mpokee Yesu maishani mwako, huyo ndiye suluhisho, kwasababu yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
JINSI YA KUPOKEA UPONYAJI, TUNAPOMWOMBA BWANA ATUGUSE MARA YA PILI.
MADHARA YA KUTOIJUA KWELI YOTE!
NI KIPI KINAMZUIA MUNGU KUZUNGUMZA NA SISI?