SWALI: Naomba kufahamu maana ya mawe matano ya kombeo na jiwe la kwanza maana yake nini na la pili hata la tano, na kwa nini mawe laini asingeokota jiwe ni jiwe tu?
JIBU: Daudi alipokutana na Goloathi maandiko yanatuambia akashuka katika kijito Cha maji akayaokota mawe matano malaini, kama silaha yake ya kumwangusha Goliathi.
1 Samweli 17:40
[40]Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti.
Lakini Swali linakuja, Kwanini yawe matano, na je yanafunua Nini rohoni? Na pia Kwanini yawe malaini?
Baadhi ya watu wanaamini pengine Daudi hakuwa na Imani ya kutosha Kwa Mungu ya kuamini kuwa jiwe Moja tu lingetosha kumwangusha Goloathi, ndio maana akachukua matano. Lakini uhalisia ni kwamba Daudi alikuwa na Imani, hata kitendo tu Cha kukataa kubeba silaha za vita alizopewa na mfalme ilikuwa ni Imani kubwa.
Wengine wanaamini mawe Yale matano, yanafunua mambo matano ambayo Daudi alikuwa nayo yaani 1) Imani, 2) utiifu, 3)utumishi, 4)maombi na 5) Roho Mtakatifu.
Wengine wanaamini kuwa yanasimama kuwawakilisha wale watoto 5 wa Yule jitu aliyeitwa Refai, ambapo, Goliathi akiwa mmojawapo.(2Samweli 21:15-22). Hivyo Daudi alionyesha kuwa wote atawaangamiza.
Wengine wanaamini kuwa mawe yale matano yanafunua zile huduma tano (5), Waefeso 4:11. Ambazo hizo zinasimama kama msingi wa kumuangusha shetani katika kanisa.
Lakini tukirudi katika muktadha wa habari yenyewe, kiuhalisia ni kuwa Daudi alichukua mawe matano, akiamini kuwa la kwanza likimkosa bado la pili lipo atarusha tena, na kama la pili likimkosa basi bado lipo la tatu atarusha tena..Kufunua jinsi gani alivyokuwa na akiba ya imani. Bwana Yesu alisema, Imetupasa kuomba sikuzote bila kukata tamaa, (Soma Luka 18:1-8), Upo wakati utaomba jambo kwa Bwana, halafu usijibiwe muda huo huo, je! Utakata tamaa kesho tena usiombe? Yesu anatuambia tuombe bila kukoma. Daudi aliamini hata ikitokea jiwe la kwanza limegonga dirii ya chuma, sio wakati wa kuvunjika moyo, ni kuvuta lingine, na kuendelea na mapambano. Vivyo hivyo na sisi yatupasa tuwe watu wenye akiba nyingi ya imani ndani yetu. Tunaomba tena na tena na tena, kwasababu hatujui ni jiwe lipi litaleta majibu, kama ni la kwanza au la katikati au la mwisho.
Lakini pia utaona hekima nyingine Daudi aliyoitumia ni kwenda kuyachukua mawe yake kwenye kijito cha maji. Jiulize ni kwanini iwe kwenye maji na sio penginepo? Kwasababu kimsingi mawe yapo kila mahali. angeweza kuokota tu ardhini.
Ni kufunua nini? Daudi alitambua VIJITO VYA MAJI YA UZIMA, ndipo wokovu ulipo. Ambavyo ni Yesu Kristo (Yohana 7:28). Usalama wa imani yake uliegemea kwa Mungu. Hata sasa Bwana anataka imani yetu iegemee kwa Yesu Kristo, huko ndiko asili ya nguvu zetu ilipo, Kama mkristo usipolitambua hili ukawekeza imani yako kwenye elimu, au mali, au vitu vya ulimwengu huu, tambua kuwa huwezi mpiga adui yako ibilisi, kwa lolote.
Na mwisho kabisa Daudi aliyatwaa mawe laini kwanini yawe malaini. Hata katika maji, yapo mawe ya maumbile mbalimbali, yapo makubwa yapo madogo, yapo yenye ncha, yapo malaini. Lakini alitambua kuwa jiwe litakalokaa katika kombeo lake, na litakalopaa vizuri na kumwangusha adui yake, sio kubwa, wala lenye ncha, wala zito sana. Bali laini, la mviringo. Kufunua nini.. Hauhitaji imani kubwa ya kuhamisha milima ili kumwangusha ibilisi. Bali kipimo cha imani yako, ukikitumia vema kinatosha kabisa kumdondosha Shetani.
Warumi 12:3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. 4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake.
Ukitumia vema nafasi yako uliyopewa na Mungu. Katika udogo wako, unyonge wako, umaskini wako, utamwangusha adui. Kila mmoja wetu amepewa nguvu hizo na Mungu. Hivyo usisubiri uwe Fulani ndio udhani utauangusha ufalme wa shetani. Hapo hapo ulipo ikiwa umeokoka, jiwe lako Kristo amekutolea. Litumie vizuri, lirushe vema, Goliathi atalala chini.
Bwana akubariki
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Je! aliyemwua Goliathi ni Daudi au Elhanani.
WALA HAKUACHA MTU ACHUKUE CHOMBO KATI YA HEKALU.
LIONDOE JIWE.
YESU NDIYE ATAKAYEKURUSHIA MAWE, USIPOTUBU.
JIWE LILILO HAI.
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya Mithali 27:21 inaposema “Kalibu ni kwa fedha, na tanuru kwa dhahabu; Na mtu hujaribiwa kwa sifa zake”
JIBU: Kalibu na tanuru hizi ni sehemu za moto, ambapo, madini kama ya shaba, fedha, au dhahabu yanapitishwa na kuyeyushwa ili kutenganisha uchafu uliogandamana na madini hayo. Hivyo hakuna namna nyingine ambayo unaweza kuifanya dhahabu au fedha ing’ae isipokuwa kuvipitisha kwenye matanuru hayo makali ya moto yaliyotengenezwa, na baadaye yatokee katika uzuri wake.
Vivyo hivyo na hapo anasema, ili kuupima moyo wa Mtu, kama ni kweli ndivyo alivyo au sivyo si katika kitu kingine chochote bali katika SIFA zake?
Ni vitu ambavyo vinavyoweza kumfanya asifiwe katika hivyo, Kwamfano, labda kipaji chake, cha kuimba. Ukimwona mtu hakengeushwi na kipawa hicho, yaani kiburi hakinyanyuki, staha inadumu, nidhamu na unyenyekevu unakaa naye, ijapokuwa ni maarufu, lakini viwango chake vya kiroho ni vilevile. Basi huyu ni mtu aliyekamilika kweli.
Au mwingine, Bwana kamjalia kupata pesa nyingi hivyo amekuwa tajiri sana na kuwazidi wengi. Lakini utajiri wake, haumfanyi adharau wengine, haumfanyi asimwabudu Mungu, haumfanyi achague watu wa kuishi nao, haumfanyi asiwasaidie wengine. Huyu ujue ni dhahabu safi kwelikweli, tabia yake ya mwanzo ilikuwa ni kweli.
Utakuta Mwingine labda kapata Elimu kubwa kuwazidi wengine, akabadilika tabia, akawa tena hajichanganyi na walio chini yake, kama ilivyokuwa zamani, hana muda wa kupokea simu za watu ambao anawaona hawamsaidii, hana nafasi ya kuhudhuria kwenye makanisa ambayo hayana wasomi, tofauti na alipokuwa hana elimu kubwa aliishi na kila mtu. moto wake umemtambulisha kwa sifa zake.
Vivyo hivyo kila jambo ambalo utasifiwa kwalo, iwe ni uzuri wako, hapo ndipo patakapoeleza tabia zako. Unajiwekaje wekaje, je! Hiyo ndio sababu ya wewe kutembea na vimini barabarani na suruali, au ndio sababu ya wewe kujisitiri.
Hivyo hekima inatupa kipimo sahihi cha kumtambua mtu alivyo rohoni. Sio katika mazungumzo yake, au kutenda kwake sasa, bali katika vitu vitakavyompa Sifa. Hapo paangalie sana. Utakuta ni mtumishi wa Mungu kweli kweli na huduma yake ilipokuwa changa, alikuwa ni mnyenyekevu, mwombaji, anahubiri kweli ya Neno la Mungu, anawasaidia watu wote. Lakini pindi ilipokuwa na imejulikana sana, au huduma ipo katika daraja lingine, amebadilika, na kuwa kama mtu spesheli kama kiongozi wa nchi, mpaka umwone, lazima uwe na kadi yako ya mwaliko tena wa kiwango Fulani cha fedha, mafundisho anayoyahubiri ni ya kujinadi, au kujisifia yeye. Hapo ndipo panapoeleza tabia halisi ya huyo mhubiri, na sio kule chini alipokuwepo. Kule alikuwa anaigiza tu.
Hivyo, kila mmoja ajichunguze, je! Nitakaposifiwa, au nitakapopandishwa viwango vingine, nitabakia kuwa yeye Yule kama Bwana wetu Yesu alivyokuwa. Nikipata kazi, nitapoa kimaombi? Nikiolewa nitawadharau ambao hawajaolewa?.
Bwana atusaidie.
Je! Upo ndani ya Kristo? Kama ni la! Unangojea nini? Tambua kuwa tupo katika dakika za majeruhi, usiishi kama mnyama ambaye anaamka asubuhi anachowaza ni kula tu, ikifika jioni ni kurudi bandani. Wewe umewekewa kusudi la kufanya hapa duniani, na lenyewe ni kuyatenda mapenzi ya Mungu, na sio kula na kunywa na kujenga nyumba. Embu geuka sasa mkabidhi YESU maisha yako, ili parapanda ya mwisho itakapolia uwe na uhakika wa kwenda naye katika unyakuo. Ikiwa upo tayari kutubu dhambi zako leo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Kalibu maana yake nini? (Mathayo 6:30).
Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?
HEKIMA NI NINI? NA UFAHAMU UNAPATIKANA WAPI?
Nini maana ya Mithali 5:15-18 anaposema Unywe maji ya birika lako mwenyewe?
Fahamu maana ya Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
Shetani anaishi wapi, Je! Amefungwa au yupo kuzimu?
Swali: Tunaona Yakobo alishindana mweleka na Malaika wa Mungu (Mwanzo 32:24), je kuna ubaya wowote na sisi kutazama mieleka kwenye Tv?.
Jibu NI La! Biblia haijawahi kutufundisha wakati wowote kuipenda dunia, Zaidi sana imesema tusiipende dunia, wala mambo yaliyomo duniani na kama tukiipenda dunia na mambo yake basi upendo wa Mungu haupo ndani yetu. (1Yohana 2:15).
Na Mieleka ni moja ya mambo ya kidunia, pamoja na mipira!.
Sasa utajiuliza mbona Yakobo alipigana Mieleka katika Mwanzo 32:24?
Yakobo hakuketi na kupanga mechi na yule Malaika, kana kwamba walikuwa wanaburudishana au kupimana nguvu.. La! Haikuwa hivyo.. Kilichotokea ni kwamba Malaika wa Mungu alimtembelea Yakobo katika mwili wa kibinadamu, na baada ya kumaliza kilichompeleka pale, wakati anataka kuondoka, Yakobo alimzuia asiondoke, lengo ni kutaka kupokea Baraka kutoka kwa Malaika yule.
Sasa wakati Malaika anataka kuondoka, Yakobo anamvuta na kumrudisha nyuma mwisho ukageuka kuwa mweleka, lakini si wa lengo la kujiburudisha wala kudhuriana, wala kupimana nguvu bali la kuzuiana!!!
Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. 25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye. 26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki. 27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo. 28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda. 29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko. 30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka”. Lakini Mieleka inayoonekana kwenye Luninga zama hizi za mwisho ni Mapando ya shetani asilimia mia, Ndio maana utaona wanaocheza michezo hiyo wanakuwa wapo nusu uchi!. na wanatangaza vitu vya kiulimwengu.
Mwanzo 32:24 “Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
29 Yakobo akamwuliza, akasema, Niambie, tafadhali, jina lako? Akasema, Kwa nini waniuliza jina langu? Akambariki huko.
30 Yakobo akapaita mahali pale, Penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso kwa uso, na nafsi yangu imeokoka”.
Lakini Mieleka inayoonekana kwenye Luninga zama hizi za mwisho ni Mapando ya shetani asilimia mia, Ndio maana utaona wanaocheza michezo hiyo wanakuwa wapo nusu uchi!. na wanatangaza vitu vya kiulimwengu.
Hivyo na sisi hatupaswi kupigana Mieleka ya kidunia isiyo na maana, badala yake tupigane Mieleka ya kiroho ambayo matokeo yake ni sisi kubarikiwa. Tung’ang’anie baraka zetu zilizoandikwa katika NENO LA MUNGU, (biblia). Na pia tushidane kwa kumponda yule adui yetu shetani chini ya miguu yetu.
Waefeso 6:12 “Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama”
Maran atha!
Kucheza karata ni sahihi kwa Mtu aliye MKRITO?
Je ushabiki wa mpira ni dhambi?
MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.
Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?
Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?
Swali: Tukisoma Mwanzo 2:23, tunaona Mwanamke Hawa pekee ndiye aliyetajwa kama “Nyama na mfupa wa Adamu” kwasababu alitwaliwa kutoka kwa Adamu..lakini tukiruka mpaka kwenye kitabu hicho hicho cha Mwanzo 29:14, tunaona Labani anamtaja Yakobo kama “Nyama yake na mfupa wake”. Sasa swali Yakobo atakuwaje nyama na damu ya Labani, ukilinganisha na kauli hiyo ya Adamu aliyomwambia Hawa?
Jibu: Tusome mistari hiyo..
Mwanzo 2:22 “na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. 23 Adamu akasema, Sasa huyu ni MFUPA KATIKA MIFUPA YANGU, NA NYAMA KATIKA NYAMA YANGU, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume”
Mwanzo 2:22 “na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.
23 Adamu akasema, Sasa huyu ni MFUPA KATIKA MIFUPA YANGU, NA NYAMA KATIKA NYAMA YANGU, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume”
Turejee tena..Mwanzo 29:12-14
Mwanzo 29:12 “Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni NDUGU WA BABAYE, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari. 13 Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote. 14 Labani akamwambia, Ndiwe kweli MFUPA WANGU NA NYAMA YANGU. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja”.
Mwanzo 29:12 “Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni NDUGU WA BABAYE, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari.
13 Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote.
14 Labani akamwambia, Ndiwe kweli MFUPA WANGU NA NYAMA YANGU. Naye akakaa kwake muda wa mwezi mmoja”.
Kauli ya “Mfupa na Nyama”, haipo tu kufunua au kuwakilisha mahusiano ya mke na mume, bali pia mahusiano ya kindugu.
Watu waliozaliwa familia moja, hao ni watu wenye mfupa mmoja na nyama moja, hata vipimo vya kibinadamu (vya kibaolojia) vinathibitisha hilo. Sasa Hawa alitwaliwa kutoka katika ubavu wa Adamu hivyo ni lazima atakuwa tu uhusiano wa kibaolojia na Adamu, na tukirudi katika hiyo habari ya Labani na Yakobo, tunasoma walikuwa ni mtu na mjomba wake, hivyo walikuwa ni ndugu (nyama moja na damu moja na mfupa mmoja).
Kwahiyo kwa hitimisho ni kuwa kauli ya “nyama moja na mfupa mmoja” Haikutumika tu kwa Adamu na Hawa bali pia kwa watu wenye mahusiano ya kidamu, na inatumika mpaka leo, ni sawa tu na kauli ya Mungu aliyosema kuwa “alimwumba mtu kwa mfano wake na sura yake (Mwanzo 1:26-27)” haikumfunga kwamba itumiwe na yeye tu, kwani tunaona Adamu alipomzaa Sethi katika Mwanzo 5:3 alisema maneno yanayokaribia kufanana na hayo kuwa “alizaa mwana kwa sura yake na mfano wake”. Hivyo hata sisi ni sura na mfano wa wazazi wetu, licha tu ya kuwa na sura na mfano wa Mungu.
Na watu wote waliookoka, ni wa Damu moja na mfupa mmoja na nyama moja (mwili mmoja) na Yesu Kristo.
Wakolosai 3:15 “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa KATIKA MWILI MMOJA; tena iweni watu wa shukrani”. Waefeso 4:4 “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja”
Wakolosai 3:15 “Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa KATIKA MWILI MMOJA; tena iweni watu wa shukrani”.
Waefeso 4:4 “Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja”
Na wote walio damu moja na Kristo ndio ndugu zake Kristo, na hao ndio watakaorithi pamoja naye, kwasababu agano la urithi siku zote lipo kwa watu wenye undugu wa kidamu.
Je umefanyika kuwa mrithi wa ahadi za Mungu?.. Kumbuka tunafanyika kuwa warithi kwa njia ya kumwamini Bwana Yesu Kristo na kubatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu.
Bwana akubariki.
HAPANA MFUPA WAKE UTAKAOVUNJWA.
Kwanini Raheli aliiba miungu ya Baba yake, (Labani) Mwanzo 31:19.
MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
JE UMEKUFA PAMOJA NA NANI?
Mithali 5:15 “Unywe maji ya birika lako mwenyewe, Na maji yenye kububujika katika kisima chako. 16 Je! Chemchemi zako zitawanyike mbali, Na mito ya maji katika njia kuu? 17 Yawe yako mwenyewe peke yako, Wala si ya wageni pamoja nawe. 18 Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako”
JIBU: Mstari huu unawalenga wanandoa, na unafananisha tendo la ndoa kama kisima ambacho kila mwanandoa amekichimba kunywea maji yake hapo ili kukata kiu ile ya mwili. Na kwamba mtu anapoingia katika hali hii, hawezi kunywa maji ya visima vingine na mwingine hawezi kuja kunywa maji ya kisima chake. Kwani vimeundwa mahususi kwa wale tu waliovichimba yaani wanandoa, mwingine yoyote atakayeshiriki ni mauti.
Jambo ambalo ni kweli, madhara ni mengi ambayo mtu anayapata anapotoka nje ya ndoa yake na kukutana na watu wengine kuzini nao, migogoro mingi ya kindoa inayozuka hata kupelekea kuvunjika kwa ndoa zao, wengine hata kuuana ni kwasababu ya tabia hii ya kuingilia ndoa za watu au kutoka nje ya ndoa. Magonjwa yasiyotibika kama ukimwi huingia kwa namna hii.
Na zaidi ya yote mtu afanyaye mambo kama haya ni anakwenda kinyume na agizo la Mungu ambalo litampelekea kuhukumiwa na kutupwa katika ziwa la moto atakapokufa; Maandiko yanasema.
Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.
Kaa mbali na uzinzi, chimba kisima chako mwenyewe, (Oa au Olewa na mke au mume mmoja). Utulie hapo, epuka tamaa. Siku hizi ni za mwisho Yesu anakaribia kurudi, mlango ni mwembamba unaoelekea uzimani imekuwa kawaida, kwa mtu kuwa na wake kando, wakidhani kuwa ndio wamekamilika, hawajui kuwa ibilisi ameshawanasa, ulinzi wa Mungu umeshaondoka ndani yao, wapo hatarini kufa, kuzimu ikiwangojea, Je! Umejiandaaje na jambo hilo? Ikiwa upo tayari kutubu leo dhambi zako na kuachana na hizo tabia za ibilisi, ili Yesu akusaidie kushinda dhambi basi uamuzi huo ni wa busara, waweza kufungua hapa kwa mwongozo huo wa kuokoka >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MAFUNDISHO YA NDOA.
BIRIKA LA SILOAMU.
Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.
Kisima cha joka na lango la jaa ni nini?(Nehemia 2:13)
Biblia inamaana gani inaposema ‘tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao’?
“Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia;Achukiaye mambo ya dhamana yu salama
Swali: Biblia inasema katika Yakobo 4:9 kwamba kucheka kwetu kugeuzwe kuwa maombolezo, je Mungu hapendi tuwe tunafurahi? Au maana yake ni nini mstari huu?
Jibu: Turejee
Yakobo 4:9 “Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu”.
Kicheko kinachozungumziwa hapo ambacho kinapaswa kigeuzwe kuwa maombolezo sio kicheko cha mambo mazuri, kwamba umeona watu wameokoka na ukafurahi na kushangilia na kucheka, kwamba ndio kicheko hicho kibadilike kiwe maombolezo!.
Hapana! Bali kicheko kinachozungumziwa hapo ambacho ni sharti kibadilike na kuwa maombolezo ni kicheko cha mambo mabaya (yaani dhambi). Mtu anapocheka baada ya kupata fedha za dhuluma, kicheko hicho ndicho biblia inachosema kuwa kinapaswa kibadilike kuwa huzuni, Kicheko mtu anachokipata baada ya kumwumiza mwingine au kuiba, au kula rushwa au kudhulumu au kufanya jambo lingine lolote baya hicho kicheko kinapaswa kibadilike na kuwa huzuni.
Maana yake mtu anapogundua makosa yake hapaswi tena kufurahia mabaya anayoyafanya au aliyokuwa anayafanya, badala yake anapaswa aomboleze, mtu aliyekuwa anazifurahia pesa haramu na kuzichekelea pale anapomjua Yesu, anapaswa asiendelee kufurahia maisha anayoishi bali aomboleze kwa kutubu na kujutia alichokuwa anakifanya.
Na kwanini ni muhimu kuomboleza na kutubu kwa mabaya, badala ya kucheka na kufurahia katika mabaya?
Ni kwasababu Bwana Yesu alisema ole wao wachekao sasa maana wataomboleza na kulia..
Luka 6:25 “… Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, kwa kuwa mtaomboleza na kulia”.
Kwahiyo ni heri leo kuomboleza kwaajili ya dhambi na maovu ili tupate rehema na siku za mwisho tuweze kuokolewa na lile ziwa na moto, kuliko leo kucheka na kufurahia mambo mabaya halafu mwisho wa siku tunatupwa katika ziwa liwakalo moto.
Swali ni je! Mimi na wewe leo tunafurahia nini na kuombolezea nini?
Je ni anasa ndizo unazozifurahia?, ni uzinzi na uasherati ndio unaoufurahia?, je ni mali za dhuluma ndizo zinazokupa kicheko?, je ni wizi ndio unaokuburudisha? Je ni kuanguka kwa wengine ndiko kunakokuchekesha.
Kumbuka neno la Mungu litabaki kuwa lile lile siku zote kuwa “ole wao wanaocheka sasa maana watalia”
Tubu ukaoshwe dhambi zako leo kwa kumwamini Yesu Kristo na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo.(Matendo 2:38).
Yakobo 4:7 “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. 8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. 9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. 10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.
Yakobo 4:7 “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu.
10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza”.
Maran atha.
KUWA MWOMBOLEZAJI.
Nini maana ya neno ‘mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena’?
MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.
Nini maana ya huu mstari; Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”
Nini maana ya huu mstari Ayubu 23:10 ‘Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’?
Ayubu 23:10 “Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu”
Kila mmoja kaandaliwa mapito yake na Mungu, ijapokuwa hatima yetu ni moja lakini mapito kamwe hayawezi kufanana. Na anafanya hivyo kwasababu ya utofauti wa wito na huduma, aliopewa kila mmoja katika kusudi lake aliloitiwa duniani.
Hivyo unapookoka anachokifanya Mungu ni kuitazama njia yako, kisha kukupitisha katika mitihani yake ili uweze kufuzu kulitimiza kusudi lake alilokuwekea mbele yako. Hivyo hii mitihani kwa jina lingine ndiyo yanainaitwa majaribu. Tofauti na baadhi wanavyotafsiri kwamba majaribu ni mitego ya dhambi Mungu anayompitishia mtu. Jibu ni hapana, Kama ni hivyo basi maandiko yangekuwa yanakinzana pale yanaposema, Mungu hamjaribu mtu, bali mtu mwenyewe anajaribiwa na tamaa zake mwenyewe (Yakobo 1:13-15)
Kwahiyo sasa lengo la mitihani hii ni kukuimarisha zaidi. Kwamfano labda wewe umewekewa huduma ya uponyaji ndani yako. Wakati mwingine Mungu anaweza kuruhusu upite mapito kama ya kuumwa sana, ili utambue umuhimu wa kuwajali na kuchukuliana na wagonjwa wenye hali mbaya kama hizo, watakaokuja kwako kuhitaji msaada mbeleni.
Ndio maana ya hili andiko ‘yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’
Kwamfano katika biblia utaona mitume walipitia vipindi vingi mbalimbali vya kuvua samaki, lakini asilimia kubwa ya hivyo hawakuwa wanapata chochote baada ya kutaabika usiku kucha, yamkini wengine walikuwa wanapata lakini wao hawapati chochote, lakini walipokutana na Yesu walipata kirahisi. Ni nini Bwana alikuwa anawafundisha? Ni uvumilivu katika kuwavua watu wake, na kwamba watakapoanza huduma watambue kuwa wokovu unatoka kwa Bwana na sio katika uweza wa nguvu zao.
Vivyo hivyo na wewe utapitishwa katika pito lako la moto, ili kujaribiwa lengo ni kuimarishwa. Wengine wanafanywa watumwa wa kuteswa sana ili watakapofanywa mabwana waweze kuwastahi watoto wa Mungu kwa upole watakaokuja chini yao, wakikumbuka mateso yaliyowakuta wao hayapaswi kwenda kwa wengine.
Mwingine katika utasa, mwingine katika vifungo, mwingine katika ujane, lakini madarasa yao yakishakamilika, basi taabu hizo zinawaacha. Na hivyo wanakuwa tayari kwa ajili ya utumishi wa Bwana.
Halikadhalika na wewe pia ikiwa umeokoka, na unajikuta katika madarasa ya Mungu, yakupasa useme kama Ayubu ‘yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu’. Na mwisho wako utakuwa ni mkuu sana kuliko mwanzo. Kwasababu siku moja utayafurahia mapito ya Mungu na kumtukuza sana (Yeremia 29:11).
Lakini kama hujaokoka, usiseme unafundishwa na Mungu, hayo ni mafundisho yako au ya ibilisi. Kwasababu Mungu hawezi kumpa mitihani mtu ambaye si mwanafunzi wake. Ni heri ukafanya uamuzi wa busara leo kwa kumkaribisha Yesu Kristo moyoni mwako. Unasubiri nini usifanye hivyo?
Ikiwa upo tayari kufanya hivyo basi bofya hapa kwa mwongozo huo >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
Ubatizo wa moto ni upi?
MAJARIBU 10 WANA WA ISRAELI WALIYOMJARIBU MUNGU.
Kupwelewa maana yake nini? (Matendo 27:26).
Kwanini biblia inaitaja mara kwa mara dhahabu ya Ofiri?
KWA KUWA WASEMA MIMI NI TAJIRI.
Mhubiri 10:20 Usimlaani mfalme, la, hata katika wazo lako; Wala usiwalaani wakwasi chumbani mwako; Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari
JIBU: Ni vema kutambua kuwa aliyeandika habari hii alikuwa ni mfalme, hivyo alitambua vema alichokiandika, na kwa hekima ya Ki-Mungu akazinakili ili ziwe onyo na angalizo kwetu . Ni wazi kuwa aliwahi kukutana na taarifa nyingi za uasi zilizowahi kupangwa kinyume chake kwa siri, au maneno ya unafiki, au ya dhihaka zilizosemwa kwa siri kinyume chake. Na yote hayo yakamfikia kwa haraka sana, kinyume na matarajio ya wale waliyoyapanga. Na huwenda wakawa wanabakiwa na maswali mengi, ni nani anayetoboa siri zao?.Wakakosa majibu
Sasa ni kwanini iwe hivyo?
Ni kwasababu Utawala wowote wa wakuu, unaundwa pia na ulinzi wake maalumu, (unaojulikana na ule wa siri usiojulikana). Kiasi kwamba chochote utakachokipanga kinyume chake kwa siri , tambua tu kitamfikia. Ndio maana hapo anasema usiwalaani katika wazo, au katika chumba chako cha siri.. Akiwa na maana hata wazo lako usiliruhusu kufanya hivyo, kwasababu mtu anayanena yaujazayo moyo wake. Kabla uasi haujatokea nje, unaanzia kwanza rohoni.
Halikadhalika wakwasi wanaozungumziwa hapo, ni watumishi wa wafalme, aidha mawaziri, au maakida, au maliwali ambao kikawaida huwa ni matajiri, vivyo hivyo na wao usijaribu kufanya hivyo ukidhani taarifa hazitawafikia. Zitawafikia, Mhubiri anatumia mfano wa ndege anasema.. ‘Kwa kuwa ndege wa anga ataichukua sauti, Na mwenye mabawa ataitoa habari’. Yaani kwa jinsi ndege wanavyoweza kusafiri kwa haraka, sehemu moja hadi nyingine, kwa wepesi wao na safari yao ya anga isivyo na vikwazo, ndivyo watu usiowajua watakavyoifikisha habari kwa wakuu wao, kinyume na matazamio yako.
Ndivyo ilivyokuwa kipindi cha mfalme Ahasuero, kulitoka watu wawili waliopanga mikakati kwa siri kumuua, lakini taarifa zilimfikia haraka mfalme kwa kinywa cha Mordakai mlinzi wa mlangoni, na wale watu wakagundulikana wakauliwa mara moja. (Esta 2:21-23)
Hakuna jambo lolote la siri ambalo halitajulikana kwa wakuu.
Tunaye Mfalme wa Wafalme, YESU KRISTO ambaye ndiye anayepaswa kuogopwa na watu wote ulimwenguni. Na kwamba hatupaswi kufanya jambo lolote kinafki, au kwa-siri mbele zake, linalokinzana na ufalme wake duniani. Kwasababu yote yatakuja kufichuliwa na kuwekwa wazi siku ile ya mwisho ya hukumu.
Yeye mwenyewe alisema;
Luka 12:2 “Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana. 3 Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari”
Hivyo uonapo kazi ya Mungu ya kweli inatendeka, kuwa makini sana na kinywa chako, uyapinge hata hayo mawazo yanayotaka kukwambia utukane, au ukufuru, au upinge. Vilevile wewe kama mhudumu wa kazi ya Bwana, tumika kwa uaminifu na kwa hofu ukijua kabisa mambo yako yote yanaonekana wazi mbele za Mungu, hakuna maficho.
Tuwe makini sana na ufalme wa Yesu Kristo duniani.
Je! Upo ndani ya Kristo? Je! Unatambua kuwa hizi ni nyakati za hatari, Yesu yupo mlangoni sana kurudi kulichukua kanisa lake? Unaishi maisha ya namna gani, ukifa leo huko uendako utakuwa mgeni wa nani? Embu tubu dhambi zako mgeukie Bwana akutakase, umtumikie yeye katika kipindi hichi kifupi tulichobakiwa nacho, itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima kisha ukapata hasara ya nafsi yako?. Ikiwa upo tayari kufanya hivyo leo, Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala hiyo ya toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
YESU NI MFALME WA AINA GANI KWAKO?
Nini maana ya Mhubiri 10:16, inaposema Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana?
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Uasherati wa Kiroho maana yake nini?
JINA LAKO NI LA NANI?
SWALI: Naomba kufahamu maana ya hili andiko;
Mithali 9:13 “Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu”.
JIBU: Kupiga kilele kunakozungumziwa hapo ni zaidi ya ile ya ‘kupaza sauti ya juu’ bali hapo anamaanisha pia ‘Kulazimisha jambo lake lionekane, ambalo limeshindikana kwa namna ya kawaida, hivyo anatumia njia nyingine za usumbufu.(Ndio makelele)
Kwamfano, labda amejiona havutii mbele za watu, anachofanya, ni kusambaza picha za uchi-uchi mitandaoni, au kuvaa nguo za ajabu na kukatiza mitaani, ili wanaume wamwone wamtamani wamfuate. Hizo ni kilele za mwanamke mpumbavu.
Na ndio maana ukiendelea kusoma vifungu vinavyofuata vinamlenga mwanamke wa namna hii, tusome..
Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu. 14 Hukaa mlangoni pa nyumba yake, Juu ya kiti mahali pa mjini palipoinuka, 15 Apate kuwaita wapitao njiani, Waendao moja kwa moja katika njia zao. 16 Kila aliye mjinga na aingie humu. Tena amwambia mtu aliyepungukiwa na akili, 17 Maji yaliyoibiwa ni matamu, Na mkate ulioliwa kwa siri hupendeza. 18 Lakini huyo hajui ya kuwa wafu wamo humo; Ya kuwa wageni wake wamo chini kuzimuni
Na ndio huyu huyu anayezungumziwa katika Mithali 7:10-11
Ni mwanamke ambaye akiona, hapendezi anakwenda kujichubua na kwenda kujipamba na kujiwekea makucha marefu na kuvaa viatu vilivyoinuka kama kwato, aonekane kama mdoli barabarani, Ili watu wamwangalie wamsifie, au wamfuate wamwoe au walale naye.
Tofauti na mwanamke mwenye busara, biblia inasema huwa ni MTULIVU, na Mpole, na anazingatia sana kuufunika mwili wake. Hana tabia ya kujikweza zaidi ya alivyoumbwa na Mungu, hana makelele, mwenendo wake umenyooka, huwezi mwona anajianika kwenye mitandao ya kijamii, kila tukio yumo na yeye aonekane mrembo, akipost picha zake za uchi-uchi, huwezi mpata hapo.
1Timotheo 2:9 “Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna”
Je! Wewe ni mwanamke mwenye makelele? Au mtulivu. Kumbuka heshima yako na thamani yako ipo katika sitara yako. Ukishindwa kujithamini utaitwa ‘mjinga’, na’ usiyejua kitu’ Kama maandiko yanavyosema hapo.
Jitambue.
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.
Nini maana yake, mpumbavu kuwa na fedha mikononi mwake ya kununulia hekima, Ikiwa hana moyo wa ufahamu?
Nini maana ya Mithali 27:6 “Jeraha utiwazo na rafiki ni amini;
Kwanini Mungu anajifanya kama hajui mambo?
Ni kwa namna gani baraka ya Bwana haichanganyi na huzuni, nyuma yake?
Mithali 10:22 “Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo”
JIBU: Kwanza ni vema kufahamu hapo anaposema ‘Baraka ya Bwana hutajirisha’ hamaanishi kuwa kipimo cha kuwa umebarikiwa na Bwana ni utajiri unaofuata baada ya hapo, hapana, Kwasababu wapo watu ambao si wakristo na hawamchi Mungu lakini ni matajiri, na wapo ambao si matajiri na wengine ni maskini kabisa lakini ni matajiri kwa Bwana.
Ufunuo 2:9 “Naijua dhiki yako na umaskini wako, (lakini u tajiri) najua na matukano ya hao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sinagogi la Shetani”.
Baraka ya Bwana haipimwi kwa mali, bali kwa mwitikio wa wokovu ndani ya mtu.
Lakini katika mstari huo, anaeleza tofauti iliyopo kati ya utajiri unaopatikana kwa Mungu na ule unaopatikana penginepo. Kwamba ule wa ki-Mungu Hauchanganyi huzuni ndani yake. Lakini ule wa kwingine unafuatana na huzuni nyingi nyuma yake.
Kwamfano mtu amepata mali kwa njia ya biashara ya madawa ya kulevya. Ni wazi mtu kama huyu hawezi kuwa na raha, kwasababu wakati wote atakuwa katika kujilinda, na mashaka ya kukamatwa na vyombo vya dola. Au mwingine kapata utajiri kwa njia ya rushwa, atakuwa na hofu sikumoja kukamatwa na vyombo vya dola kwa kosa la kuhujumu uchumi. Au mwingine kwa njia ya uganga, atapewa masharti, atoe wengine kafara, au alale chooni sikuzote za maisha yake, ili utajiri wake uendelee.
Hivyo utajiri wowote nje ya ule unaopatikana na Mungu, unavimelea vingi vya mateso. Visasi, vinyongo, wivu, hofu, mashindano n.k. Kwa kifupi ni kuwa hauna raha, Hivyo Bwana anatushauri kama kufanikiwa tufanikiwe kwake ambapo kunaendana na kanuni ya kumcha yeye kwa bidii (Kumbukumbu 28), kufanya kazi halali, na kuwa mtoaji. Na utakapobarikiwa basi Bwana atakupa raha katika vitu hivyo.
Bwana awe nawe.
Je! Upo ndani ya Kristo? Kama ni la! Wakati ndio sasa, geuka upokee ondoleo la dhambi zako kwasababu muda ni mchache tuliobakiwa nao, tubu pokea wokovu sasa Parapanda inakaribia kulia. Ikiwa upo tayari kutubu leo, basi fungua hapa kwa mwongozo huo. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
USINIPE UMASKINI WALA UTAJIRI. (Mithali 30)
KANUNI RAHISI YA KUPOKEA BARAKA MARA DUFU.
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
USIIKARIBIE DHAMBI, KAA NAYO MBALI.
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU BARAKA
Ni sahihi kwa mkristo kupokea fedha kutoka kwa mtu anayefanya kazi haramu?