SWALI: Naomba kuelewa kwa undani Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
JIBU:
Sehemu nyingi Biblia inaposema mbinguni, huwa inamaanisha moja kwa moja kule Mungu alipo Pamoja Malaika zake, Kule ambako Bwana Yesu alikwenda kutuandalia makao. Mahali ambapo sisi kama watakatifu bado hatujafika hata mmoja.
Ndio mbingu ya Tatu, ambayo Mtume Paulo alinyakuliwa kuonyeshwa baadhi ya vitu vilivyopo kule vipo kule ambavyo havielezeki kibinadamu, kwasababu upeo wetu ni mdogo. (2Wakorintho 12:1-4)
Ni juu sana, ambako, hatuna maelezo ya kutosha kupaelezea, mpaka tutakapofika.
2Nyakati 6:18 “Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; siuze nyumba hii niliyoijenga!”
Ni mbingu ya mangojeo, ambayo sio makazi yetu ya kudumu. Mtakatifu anayekufa sasa hivi anakwenda mahali panapoitwa Peponi/Paradiso, akisubiria, siku ya unyakuo ifike, arudi kaburini achukue mwili wake, kisha aungane Pamoja na wale watakatifu watakaokuwa hai wakati huo, na moja kwa moja safari ya kwenda mbinguni ianze, kule Bwana Yesu alipo.
Yule mwizi pale msalabani, Bwana alimwambia maneno hayo;
Luka 23:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. 43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Luka 23:42 “Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi”.
Wengine wanaiita mbingu ya pili, lakini vyovyote vile iitwavyo, bado ni mahali pa mangojeo pa watakatifu, Ndio kifuani pa Ibrahimu, yule maskini Lazaro alikwenda (Luka 16:19-31), ndio kule ambazo zile Roho zilizo chini ya madhahabu zilikuwa zinalia, zikiomba zilipiziwe kisasi kwa watesi wao.
Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. 10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? 11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Ufunuo 6:9 “Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.
10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?
11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao”.
Vilevile huku ndio kule wale wafu waliofufuka na Bwana Yesu walipoelekea kwa mara ya kwanza. (Mathayo 27:52-53)
Hivyo leo, hii ukifa katika Kristo, basi unakwenda katika eneo hili la mbingu, ambalo ni lizuri sana. Ukisubiri ufufuo wa mwisho.
Kuzimu kibiblia ni Neno lililomaanisha makao ya wafu Au kaburini. Ambapo, waovu na wema walikuwa wanakwenda kabla ya Kristo kuja duniani, kuwatenganisha moja kwa moja kimakao,
Ayubu anasema
Ayubu 14:13 “Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka!”
Daudi pia alipazungumzia, (Zaburi 16:10), kwamba Bwana hatomwacha huko milele.
Lakini baada ya Bwana Yesu kuja, wakatifu walitoka huko makaburini, na kwenda peponi/ Paradiso. Mahali pa raha Zaidi pa juu na si makaburini tena. Hivyo wanaobakia makaburini au kuzimu ni waovu.
Ni mahali pa mangojeo pa waovu, ni mahali pa mateso, kama vile Paradiso palivyo mahali pa raha pa mangojeo kwa watakatifu, vivyo hivyo jehanamu nako, ni mahali pa mangojeo pa watu waovu wanaokufa sasa. Wanaadhibiwa huko, wakingojea siku ile ya hukumu ya mwisho ifike. Ili wapewe hukumu yao, katika hukumu ya kile kiti cheupe cha enzi cha mwanakondoo, kisha wakatupwe kwenye lile ziwa la moto, ambalo ndio mauti ya pili ilipo.
Ni sawa na mhalifu anayekamatwa sasa hivi, kabla ya kuhukumiwa kifungo, huwa anawekwa kwanza mahabusu, akisubiria siku ya kupandishwa kizimbani ifike, ahukumiwe kisha akatumikie kifungo chake Jela, Ndivyo ilivyo kwa watu waovu wanaokufa sasa, na waliokufa zamani. Wanakwenda katika sehemu hii ya mateso, ambayo si ya kawaida.
Bwana Yesu alisema..
Marko 9:45 “Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [ 46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]”
Marko 9:45 “Na mguu wako ukikukosesha, ukate; ni afadhali kuingia katika uzima, u kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jehanum; [
46 ambamo humo funza wao hafi, wala moto hauzimiki.]”
Swali, la kujiuliza ni Je! Tukifa leo, au Unyakuo ukitukuta leo, mimi na wewe tutakuwa wa upande upi? Katika mambo ambayo hupaswi kuyachukulia juu juu tu, basi ni mambo ya Maisha yako ya milele. Kwasababu ukishakufa hakuna nafasi ya pili tena. Kama umestahili Jehanamu basi utaendelea kuishi humo milele.
Ni heri ukamgeukie Kristo, maadamu muda mchache bado unao. Acha kutazama, mambo ya ulimwengu, kwani huwa yanapumbaza sana, kukufanya usione kama kuna mabaya yanakuja mbele, Moja ya hizi siku utajutia Maisha yako, uliishije endapo hukumpa Kristo Maisha yako leo.
Tubu dhambi zako, maanisha kumfuata Yesu.
Bwana atusaidie, kuyafahamu haya.
Shalom.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Mada Nyinginezo:
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?
Je! kuna maombi yoyote ya kumtoa mtu aliyekufa kwenye mateso ya kuzimu?
MILANGO YA KUZIMU.
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)
Rudi nyumbani
Print this post
Eneo ambalo mji wa Babeli ulikuwepo, ni maeneo ya nchi ya IRAQ kwa sasa, Mji huu ndio uliokuwa maarufu kwa kuwa na “bustani zinazoelea”, lakini kwasasa mji huu haupo tena, wala maajabu yake hayapo!!,
kwasababu mji huo ulikuwa mji wa kishetani na ulifanya dhambi nyingi, na Mungu akauadhibu.. mahali ulipokuwepo pamebakia tu mbuga!!, sawasawa na unabii Mungu alioutoa juu ya mji huo.
Isaya 13:19 “Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza. 20 Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko. 21 Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko. 22 Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka”..
Isaya 13:19 “Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.
20 Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.
21 Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani; na nyumba zao zitajaa bundi; mbuni watakaa huko; na majini watacheza huko.
22 Na mbwa-mwitu watalia ndani ya ngome zake; na mbweha ndani ya majumba ya anasa; na wakati wake u karibu kufika, na siku zake hazitaongezeka”..
Kwahiyo leo hii hakuna kilichosalia pale!, pamebakia tu kuwa sehemu ya makumbusho ya kale.
Kumbuka shetani aliinyanyua Babeli ya kwanza, ambayo Mungu aliiharibu kwa kuchafua lugha za wajenzi wao!, na kazi ya ujenzi ikaishia pale! (Mwanzo 11), Lakini hakukata tamaa bali aliitengeneza Babeli nyingine, ambayo ndiyo iliyokuja kuangushwa na falme za Umedi na Uajemi, ikawa jaa!!
Lakini sasa shetani katengeneza Babeli nyingine ambayo ni ya KIROHO, hii iliyopo sasa ndio mbaya kuliko mbili zilizotangulia, na ndio kitovu cha machukizo na machafuko yote yan chi (sawasawa na Ufunuo 17).
Kwa urefu juu ya Babeli hiyo ya rohoni iliyopo sasa, fungua hapa >>> BABELI YA ROHONI.
Maran atha!
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.
JE WEWE NI LAZARO YUPI, WA KWANZA AU WA PILI?
Ninawi ni nchi gani kwasasa?
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 12 (Kitabu cha Isaya)
TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.
Tunasoma Matendo 2:38, kuwa watu walibatizwa kwa jina la YESU. Lakini biblia haijataja Yohana Mbatizaji alitumia jina gani kumbatizia Bwana Yesu, Pamoja na makutano waliomjia ili awabatize?.
Jibu: Yohana Mbatizaji hakutumia jina lolote katika Ubatizo. Ubatizo wake ulikuwa ni ubatizo wa Toba, ambapo baada ya watu kusikia mahubiri yake na kutubu, aliwazamisha kwenye maji mengi kwa ishara ya kuoshwa dhambi zao kwa maji. (Hakuna jina lolote lililohusika).
Lakini baada ya Bwana Yesu kuja, maandiko yanasema mambo yote tunayafanya kwa jina lake (Jina la Yesu).
Wakolosai 3:17 “Na kila mfanyalo, KWA NENO au KWA TENDO, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye”.
Umeona hapo?.. anasema lolote lifanyikalo kwa “Neno” au kwa “Tendo”.
Mfano wa mambo yafanyikayo kwa neno, ni kuomba, kutoa pepo, kubariki, kuimba, kutoa unabii n.k Hayo yote tunayafanya kwa jina la YESU. Ndio maana leo Pepo linatoka kwa jina la Yesu, vile vile tunapoomba tunatumia jina la YESU, n.k Mambo haya hapo kabla hayakuwepo, kwamba pepo linamtoka mtu kwa kutaja tu jina la mtu Fulani!.. Lakini yamekuja kuwezekana kwa mmoja tu, ambaye ni Bwana YESU, kwa jina lake tunafanya yote!.
Lakini sio hilo tu, bali maandiko yanasema pia, lolote tufanyalo kwa TENDO. Sasa mfano wa tendo, ndio huo Ubatizo!.) Kwamba tunazamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU. Yohana hakutumia jina la Yesu, ndio maana ubatizo wake ukakoma, lakini ubatizo wa jina la Yesu umedumu siku zote!! Na ndio unaoondoa dhambi!.
Matendo 19:1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; 2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3 AKAWAULIZA, BASI MLIBATIZWA KWA UBATIZO GANI? WAKASEMA, KWA UBATIZO WA YOHANA. 4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu 5 WALIPOSIKIA HAYA WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”.
Matendo 19:1 “Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko;
2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.
3 AKAWAULIZA, BASI MLIBATIZWA KWA UBATIZO GANI? WAKASEMA, KWA UBATIZO WA YOHANA.
4 Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu
5 WALIPOSIKIA HAYA WAKABATIZWA KWA JINA LA BWANA YESU.
6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.”.
Umeona hapo?. Watu hao walirekebisha ubatizo wao, wakabatizwa tena kwa jina la BWANA YESU
Na sisi leo hii hatuna budi kubatizwa kwa jina la Bwana Yesu ili tupate ondoleo la dhambi.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.
Ubatizo ni nguzo muhimu sana na ya awali katika Ukristo, (Kila Mtu aliyemwamini Yesu ni lazima abatizwe). Na kumbuka lengo kuu la ubatizo sio wewe kupewa jina jipya. Hilo sio lengo la ubatizo, lengo la ubatizo ni kuzikwa kwa utu wako wa kale, na kufufuka katika upya.
Swali ni Je! umebatizwa inavyopaswa kwa kuzamishwa na kwa jina la Bwana Yesu? Kama bado unasubiri nini?..Fanya hima ubatizwe ili uitimize haki yote!.na kumbuka pia ubatizo sio wa kunyunyiziwa wala wa uchangani, bali ni maji mengi! Na wa utu uzima.
Hivyo kama ulibatizwa pia utotoni, huna budi kubatizwa tena sasa, baada ya kujitambua, kwasababu wakati ule hukuwa umeokoka!, hukuwa umetubu..lakini sasa umejitambu, hivyo huna budi kubatizwa.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga Namba hizi…
JE! UMEBATIZWA UBATIZO SAHIHI?
Je! Bwana Yesu alibatiza akiwa hapa duniani?
FUMBO ZA SHETANI.
UFUNUO: Mlango wa 1
Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni ipi?
Dameski ni mji ambao mtume Paulo alitokewa na Bwana Yesu, wakati akiwa anaelekea kuwaua wakristo ndani ya mji huo (Matendo 9:2-7). Mji wa Dameski mpaka leo upo!.. Ni moja ya miji ambayo haijabadilika jina lake mpaka leo, mingine mfano wa hiyo ni Yerusalemu na Bethlehemu.
Mji wa Dameski upo katika nchi ya SYRIA kwasasa. Tamaduni za watu waliopo Dameski ni tofauti na za watu wa enzi za kale… Hivyo mji upo Pamoja na watu, lakini tamaduni ni nyingine si ile ya zamani.
Nabii Isaya alipewa ufunuo juu ya mji huo kuja, kuondolewa kabisa katika siku za mwisho..
Isaya 17:1 “Ufunuo juu ya Dameski. TAZAMA, DAMESKI UMEONDOLEWA USIWE MJI, NAO UTAKUWA CHUNGU YA MAGOFU. 2 Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu. 3 Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema Bwana wa majeshi”.
Isaya 17:1 “Ufunuo juu ya Dameski. TAZAMA, DAMESKI UMEONDOLEWA USIWE MJI, NAO UTAKUWA CHUNGU YA MAGOFU.
2 Miji ya Aroeri imeachwa; itakuwa kwa makundi ya kondoo, nao watajilaza huko wala hapana atakayewatia hofu.
3 Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema Bwana wa majeshi”.
Pia vita vya Ezekieli 38, vilivyotabiriwa kuja kupiganwa kati ya Israeli na mataifa ya kandokando Pamoja na Gogu, itaifuta kabisa mji huo.
Kwasababu kwasasa ni mji unaopinga Yerusalemu kama mji mtakatifu wa Mungu mwenyezi na urithi wa Israeli, na unafanya vita dhidi ya Taifa h. Kwasababu hiyo utaondolewa Pamoja na miji mingine baadhi kulingana na biblia.
Isaya 49:23 “Habari za Dameski. Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia; Maana wamesikia habari mbaya; Wameyeyuka kabisa; Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia. 24 Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake. 25 Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu? 26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi. 27 Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi”.
Isaya 49:23 “Habari za Dameski. Hamathi umetahayarika, na Arpadi pia; Maana wamesikia habari mbaya; Wameyeyuka kabisa; Huzuni iko baharini, haiwezi kutulia.
24 Dameski umedhoofika; Umejigeuza kukimbia; tetemko limeushika; Dhiki na huzuni zimeupata, Kama za mwanamke katika utungu wake.
25 Imekuwaje mji wa sifa haukuachwa, mji wa furaha yangu?
26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika njia kuu zake, na watu wote wa vita watanyamazishwa katika siku hiyo, asema Bwana wa majeshi.
27 Nami nitawasha moto katika ukuta wa Dameski, nao utayateketeza majumba ya Ben-hadadi”.
Tarshishi ni mji gani kwasasa?
Bwana Yesu alizaliwa mwaka gani?
MAMA, TAZAMA, MWANAO.
Nyungu ni nini kibiblia?(Ayubu 41:20,31, Waamuzi 6:19)
Tarshishi ni mji uliokuwepo nchi ijulikanayo kwasasa kama Lebanoni. Taifa la Lebanoni katika nyakati za kale ndio Taifa lililokuwa linaongoza kwa uzalishaji wa miti aina ya MIEREZI (Kujua Mierezi ni miti gani fungua hapa >> MIEREZI).
Mji mkuu wa Taifa la Lebanoni, ndio ulikuwa Tarshishi. Mji huu wa Tarshishi ndio uliokuwa unaongoza kwa wafanya biashara, na ndio uliokuwa kitovu cha biashara ulimwenguni. Nabii Yona alikimbilia mji huu kwasababu ulikuwa na fursa nyingi. (Kwa urefu juu ya mji wa Tarshishi na biashara zake na Taifa hilo linafunua nini kiroho, fungua hapa >>Tarshishi).
Asili ya mji wa Tarshishi ni mwana wa Yafethi aliyeitwa Yavani, ambaye huyu Yavani ndiye aliyewazaa wenyeji wa Tarshishi.
Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika. 2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. 3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. 4 NA WANA WA YAVANI NI ELISHA, TARSHISHI, Kitimu, na Warodani”.
Mwanzo 10:1 “Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
2 Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
3 Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
4 NA WANA WA YAVANI NI ELISHA, TARSHISHI, Kitimu, na Warodani”.
Ashuru ni nchi gani kwa sasa?
MADHARA YA KUFUATA MAMBO YAKO TU!
Je Elisha alimdanganya Ben-hadadi kuwa hatakufa kwa ugonjwa wake?
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
Ninawi ni wapi?
Ninawi ni mji uliokuwepo kaskazini mwa Taifa la Iraq kwasasa. Mji huu kwasasa haupo, ila mahali pale ulipokuwepo mpaka leo pako!. Na mji huu ndio uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru. (Kujua Taifa la Ashuru ni wapi kwasasa fungua hapa> ASHURU).
Mji wa Ninawi ndio Mji Nabii Yona aliagizwa na Mungu akahubiri Injili, ili watu wa mji ule watubu, lakini alikataa na kukimbilia mji wa Tarshishi. Kujua Mji wa Tarshishi kwasasa ni nchi gani basi fungua hapa> TARSHISHI.
Mji wa Ninawi haukuwa mji wenye watu wengi sana lakini ulikuwa umeendelea sana. Kipindi Nabii Yona anatumwa kwenda kuhubiri huko, biblia inarekodi mji ule kuwa na watu 120,000 tu!.
Yona 4:10 “Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; 11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”
Yona 4:10 “Bwana akamwambia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuuotesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja;
11 na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?”
Ijapokuwa Mungu alikusudia kuuadhibu mji huu lakini wenyeji wake walitubu kwa mahubiri ya Yona. Na Bwana Yesu alikuja kutoa unabii kwa vizazi hivi vya siku za mwisho kuwa..
Mathayo 12:41 “Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; KWA SABABU WAO WALITUBU KWA MAHUBIRI YA YONA; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona”.
Na sisi tunapaswa tutubu kwa mahubiri ya Bwana Yesu, ili tusije kuangukia hukumu siku ya Mwisho.
Babeli ni nchi gani kwasasa?
NINI MAANA YA KUTUBU
YONA: Mlango wa 4
Ashuru ni wapi?
Ashuru ilikuwa ni nchi iliyokuwepo maeneo ya Iraq, Uturuki, na Syria..Mataifa haya matatu yamechangia sehemu ya nchi hiyo ya Ashuru, kama vile mataifa matatu (Kenya, Uganda na Tanzania), yalivyo na sehemu katika ziwa Victoria, kadhalika na Iraq, Uturuki na Syria ni sehemu ya Taifa hilo liliokuwa linaitwa Ashuru.
Lakini kwasasa duniani hakuna Taifa linaloitwa Ashuru. Kwani baada ya mataifa hayo matatu kuzaliwa hilo la Ashuru likafa.
Na Uliokuwa mji mkuu wa Taifa la Ashuru, uliitwa NINAWI. Ninawi ndio mji Nabii Yona alioambiwa akahubiri Injili, lakini kinyume chake akakimbilia Tarshishi..Kujua Ninawi ni wapi kwa sasa fungua hapa>NINAWI.
Vile vile kujua Tarshihi ni wapi kwasasa fungua hapa > TARSHISHI.
Asili ya Taifa la Ashuru kibiblia ni kutoka kwa Nimrodi..
Mwanzo 10:8 “Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. 9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana. 10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari. 11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala; 12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa”.
Mwanzo 10:8 “Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
9 Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
10 Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
11 Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
12 na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa”.
Lakini Taifa la Ashuru ndilo lililowachukua Israeli na kuwapeleka utumwani katika Taifa hilo. Lakini baadaye walirudi katika Taifa lao chini ya amri ya Koreshi Mwajemi.
Bwana Yesu alisema “Baba uwasamehe kwakuwa hawajui walitendalo (Luka 23:34)”. Je kwa kusema hivyo ina maana wote walisamehewa dhambi zao, kiasi cha kwamba hata wangekufa pale wangeenda mbinguni?.
Jibu: Dhambi waliyosamehewa ni hiyo ya kumsulibisha Bwana, na Bwana Yesu aliwasamehe kutoka moyoni, na hivyo Baba aliwasamehe pia. Lakini kusamehewa kosa hilo, haimaanisha wamesamehewa na mengine yote..haimaanishi wamesamehewa uuaji waliofanya jana, au matusi waliyotukana juzi, au mauaji waliyoyatekeleza wiki iliyopita, au wizi walioufanya mwezi uliopita.
Hapana!..walichosamehewa ni hicho kimoja tu!..yaani kosa hilo la kumsulubisha Bwana Yesu!.
Ni sawa na wewe leo umsamehe mtu aliyekutapeli jana, na hivyo ukaghairi kumpeleka polisi, hiyo haimaanishi kasamehewa dhambi zake zote za utapeli alizowafanyia na wengine. Wewe umemsamehe kweli na Mungu pia kamsamehe.
Lakini hatia za makosa mengine aliyowafanyia wengine bado hajasamehewa mpaka atakapotubu.
Vile vile na waliomsulubisha Bwana walisamehewa tu dhambi hiyo moja ya kumsulubisha Bwana, nyingine zilizosalia walipaswa watubu.(Waungame dhambi zao zote, ndipo wawe salama).
Zaidi sana kama walikufa bila kumwamini Yesu, vile vile watahukumiwa kwa dhambi hiyo, hatakama walisamehewa ile kumsulubisha Bwana.
Yohana 3:18 “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. 19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.
Yohana 3:18 “Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
19 Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu”.
Hivyo kama Bwana Mungu alipanga kuwapiga kwa kosa la kumsulibisha Bwana, alighairi na kuyaondoa hayo madhara, lakini ghadhabu ya makosa mengine waliyoyafanya ilikuwa pale pale, na zaidi sana ghadhabu ya wao kutomwamini Bwana bado haikuondolewa. Hiyo inaondolewa kwa mtu kuyasalimisha maisha yek kwa Yesu.
Hiyo ikitufundisha kuwa tunapaswa tuungame dhambi zetu zote kwa Bwana.
1 Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”. Maran atha!
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
FUATILIA NDOTO HII, UTAJIFUZA KITU.
HUYU MELKIZEDEKI NI NANI?
YANAYOENDELEA SASA KATIKA MADHABAHU YA MUNGU ROHONI.
Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?
Ni kawaida mwanadamu anapopitia matatizo mengi au shida nyingi, huwa anatamani hata afanane na mnyama asiyejua shida, anatamani angekuwa kama ndege apae zake aende mbali na makao ya watu akaishi humo.
Ndivyo Daudi alivyosema..kipindi ambacho anafukuzwa na Sauli huko majangwani, alisema..
Zaburi 55:5-8[5]Hofu na tetemeko limenijia, Na hofu kubwa imenifunikiza.[6]Nikasema, Ningekuwa na mbawa kama njiwa, Ningerukia mbali na kustarehe.[7]Ningekwenda zangu mbali, Ningetua jangwani.[8]Ningefanya haraka kuzikimbia Dhoruba na tufani.
Lakini jinsi Mungu alivyotuumba, kamwe hatuwezi kuzitoroka dhoruba na tufani za maisha…fahamu kuwa watu wanaokuudhi ndio hao hao utaendelea kuishi nao, na kama hutaishi nao nyumba moja, basi kuna kipindi mtakutana tu katika nukta fulani ya maisha..
Maadui zako, watesi wako, pamoja na wachawi hakuna siku Mungu atakutenga nao akupeleke katika dunia yako mwenyewe uishi huko kwa starehe, hicho kipindi hutakaa ukifikie haijalishi wewe ni mtakatifu kiasi gani.
Mungu anachokifanya kwetu ni kutulinda na kutuepusha tu na madhara yao, yasitufikie. Lakini kuishi katikati yao ni jambo endelevu mpaka mwisho.Bwana Yesu alisema;
Yohana 17:15[15]Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
Wakati mwingine, Mungu anapotaka kukupa rizki, anatumia hata njia ya hao hao, unakula katikati yao wakikuona..
Zaburi 23:5[5]Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
Hivyo ndugu uliyeokoka, acha kutaabika kwa ajili ya wanadamu, wala usipeleke akili zako mbali sana, ukidhania kuwa hao watu walio na wewe kama mwiba kuna siku watatoweshwa milele, uishi peke yako kwa starehe..Kanuni hiyo Mungu hajaichagua japo tunaitamani.
Zaidi sana jifunze kuyatimiza mapenzi ya Mungu katikati yao. Utakuwa na furaha katika maisha.Kumbuka Mbawa kama za njiwa hatujapewa wanadamu.
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Kwanini wakristo wengi ni maskini?.
ALAMA KATIKA VIPAJI VYA NYUSO.
KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?
Swali: Kurushwa upesi kunakozungumziwa katika Danieli 9:21 ndio kupi?
Wokovu wa kweli ni upi?
Je unaposema umeokoka, ni nini kinakupa uhakika huo?
Fahamu ni nini Bwana anataka kuona kwako, pindi tu unapookoka.
Ni kweli katika Warumi 10:9 biblia inasema;
“Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka”.
Lakini kukiri kunakozungumziwa hapo, sio sawa na inavyotafsiriwa sasa. Zamani, kukiri kulimaanisha kutangaza vita na ulimwengu, Pamoja na kuhatarisha Maisha yako pia . Kwani ukristo ulijulikana kama ni dini asi, dhidi ya Imani za kipagani.
Soma,
Yohana 9:22 “.. kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi”.
Hivyo watu wengi walikuwa wanauliwa, wengine wanafukuzwa mbali na jamii, kwa jambo hilo tu moja, la kumkiri Yesu hadharani. Kwahiyo mtu yeyote kabla ya kwenda kumtangaza Yesu hadharani kuwa ndiye mwokozi wake, alijifikiria mara mbili kwanza.
Sasa jambo kama hili linatokea kweli sehemu baadhi ulimwenguni, lakini sio kote. Kwani sisi tuliopo katika mazingira mchanganyiko kama haya. Neno kukiri tu kwa kinywa, sio kipimo tosha kwamba wewe umemfuata Yesu, kwasababu mtu yeyote anaweza kufanya hivyo hata mpagani, kwasababu hakuna hatari yoyote inaweza kumtokea kama akifanya hivyo. Kwasababu anakuwa ni kama tu kaongea.
Na ndio maana leo hii kuna idadi kubwa sana ya watu wanajiita wakristo wanasema wameokoka. Ukiwauliza wameokokaje watakuambia, kwasababu walimkiri Yesu kwa vinywa vyao, hilo tu.Na huku ukiangalia Maisha yao, hayana tofauti na watu wa kidunia.
Ndugu usidanganyike, wokovu wetu ili ufanane na ule wa watu wa zamani, hatuna budi tumkiri Yesu KWA MATENDO YETU. Tunaukataa ulimwengu na mambo yake yote, kivitendo.
Bwana Yesu alitabiri kuwa siku za mwisho, wengi watamwita ‘Bwana, Bwana’, kwa midomo tu, lakini matendo yao yapo mbali naye, lakini anasema atawafukuza Dhahiri.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Mathayo 7:21 “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.
Umeona? Ikiwa hao atakaowafukuza wanafanya miujiza mikubwa, na kutoa ishara nyingi, jiulize wewe ambaye hutendi lolote, na bado unatenda dhambi, unadhani utamwonga Mungu, kisa uliongozwa sala ya toba?
Ndugu, ni kuwa makini sana nyakati hizi, Ukisema umeokoka, uthibitishe wokovu wako kwa matendo kwamba umeuacha ulimwengu kweli kweli. Unaacha hivyo vimini, hizo suruali uvaazo binti,Uzinzi, anasa, punyeto, picha za ngono utazamazo mitandaoni.
Kuongozwa sala ya toba mara nyingi, sio tiketi ya kwenda mbinguni, bali badiliko lako ndilo litakalokuoa.
Bwana atufumbue macho yetu tulione hilo.
WhatsApp