Title July 2024

VIASHIRIA VINGINE VYA ROHO MTAKATIFU KUWEPO NDANI YAKO.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu, (Mkuu wa Uzima na Mfalme wa wafalme), YESU KRISTO libarikiwe. Karibu tujifunze Neno la Mungu wetu lililo taa na Mwanga wa njia zetu (Zab. 119:105).

Kiashiria cha Kwanza ni UTAKATIFU:

kwamba Roho Mtakatifu yupo ndani yako (au umebatizwa na Roho Mtakatifu) ni UTAKATIFU, angalia maisha yako, je dhambi imekuwa hafifu kiasi gani, ukijilingalisha na kipindi cha nyuma.. Ukiona kuna nguvu kubwa ndani yako ya kushinda dhambi, basi tambua kuwa si wewe, bali ni uwepo wa nguvu za Roho Mtakatifu ndani yako.

Kiashairia cha Pili ni KARAMA:

Karama maana yake ni ile shauku/msukumo  wa kumtumikia Mungu katika eneo Fulani, ambao unakutofautisha na mwingine.. Ukiona una shauku kubwa ya kumtumikia Mungu, na ukiangalia shauku hiyo huioni kwa mwingine aliye karibu na wewe, au ukijaribu kumweleza mwingine ni kama hakuelewi, basi fahamu kuwa hiyo shauku si wewe, bali ni Nguvu/msukumo wa Roho Mtakatifu ndani yako. (ndio maana zinaitwa karama za roho, 1Wakorintho 12:1)

Kiashiria cha Tatu ni KUCHUKIWA/KULAUMIWA BILA SABABU:

Si kila lawama ni ishara mbaya: Ukiona kila unalolifanya la KiMungu linazua lawama, au shida mahali ulipo..basi hiyo pia ni ishara nyingine ya uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako..

1Petro 4:14 “MKILAUMIWA kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia”.

Kiashiria cha Nne: KUPUNGUA KWA HOFU NDANI YAKO.

Ukiona hofu imeisha ndani yako, kiasi kwamba wakati  wengine wana wasiwasi kuhusiana na mambo Fulani wewe huna wasiwasi hata kidogo, na unajihisi kabisa kuwa Mungu yupo na wewe, basi fahamu kuwa kuna uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu ndani yako, na si wewe kwa akili zako (kwasababu kwa akili za kawaida, hakuna mtu mwenye akili timamu asiyetishwa na misukosuko ya maisha).

Kiashiria cha Tano: FURAHA.

Ukiona kuna furaha isiyoelekeza ndani yako kila unapofikiria habari za YESU, na wakati mwingine unatamani kumweleza mwingine, na ukijaribu ni kama haoni kama unavyoona, basi fahamu kuwa si wewe hisia zako, bali ni nguvu za Roho Mtakatifu ndani yako, Wagalatia 5:22.

Kiashiria cha Sita: MFULULIZO WA MAFUNUO.

Ukiona kila unapotembea unamwona YESU katika neno lake, au unauona uweza wa YESU, ambao unakuletea changamko Fulani, na msisimko wa kipekee, ambao huoni kwa mwingine, basi tambua kuwa ni kazi za Roho Mtakatifu hizo ndani yako.. kwani kwa kawaida macho yaliyofumbwa hayawezi kumwona YESU popote wala kuuona uweza wake.

Vile vile ishara hii inaambatana na kupata ufahamu wa maandiko kwa namna ya kipekee sana.

SASA UFANYE NINI UNAPOGUNDUA KUWA ROHO MTAKATIFU YUPO NDANI YAKO?

  1. USIMZIMISHE ROHO (1Wathesalonike 5:19)

Kumzimisha Roho Mtakatifu ni kitendo cha kumfanya Roho Mtakatifu aondoke ndani yako na kukaa mbali nawe aidha kwa muda kwa muda au moja kwa moja.. na vitu vinavyomzimisha Roho Mtakatifu ni dhambi za makusudi…kama uzinzi, wizi, ibada za sanamu na kupenda mambo ya kidunia.

Mambo haya mtu akiyafanya Roho Mtakatifu anaondoka ndani yake, na ile nguvu ya kushinda dhambi inaondoka ndani yake, vile vile ile nguvu ya kushinda hofu pia inaondoka ndani yake.

  1. USIMHUZUNISHE ROHO (Waefeso 4:30)

Kumhuzunisha Roho sawasawa na Waefeso 4:30, ni kitendo cha kumfanya Roho Mtakatifu asifurahiwe na wewe, na matokeo ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu kwa muda mrefu, ni kuondoka ndani ya mtu.

Mambo yafuatayo yanaweza kuwa sababu ya Roho Mtakatifu kuhuzunika ndani yetu..

1. Tabia ya kukosa Imani…kama vile Bwana YESU alivyohuzunishwa na wanafunzi wake mara kadhaa, pale walipokuwa wanapungukiwa na Imani, mpaka kufikia hatua ya kuwaambia mara kwa mara “Imani yenu iko wapo”

Vile vile na sisi tunapopungukiwa na Imani katika mazingira tukutanayo hiyo Roho Mtakatifu anaugua ndani yetu, hivyo hatuna budi kuwa watu wa Imani daima.

Na Imani chanzo chake ni kusikia Neno la Mungu, (ambayo tafsiri yake ni kusoma na kujifunza biblia). Neno la MUNGU linapokaa kwa wingi ndani yetu pamoja na maombi basi viwango vyetu vya Imani vinakuwa na hivyo tunakuwa katika hali ya kumpendeza Roho Mtakatifu.

2. Tabia ya uvivu wa kiroho.. Ukiwa mlegevu kutenda yakupasayo, Roho Mtakatifu anaugua kwasababu hutumii kile ulichopewa,

Kama viashiria hivyo havipo ndani yako basi huenda Roho MTAKATIFU bado hajaingia ndani yako, au amesogea pembeni, na hiyo si kwasababu wewe ni mbaya, au una kasoro, au wengine ni bora kuliko wewe mbele zake, LA!..bali ni kwasababu bado hujafungua mlango, au ulikuwa hujui jinsi ya kuufungua mlango..kwasababu yeye anatamani aingie ndani yako Zaidi hata ya wewe unavyotamani.

Sasa swali la msingi, unaufunguaje mlango ili aingie ndani yako?

Kanuni ni rahisi sana, isiyogharimu hata theluthi ya senti moja.. na kanuni  yenyewe ni kukiri tu makosa yako, kwamba wewe ni mwenye dhambi na hivyo unahitaji msaada wake (kutubu) kwa kumaanisha kabisa kuacha mambo yote mabaya.., na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana YESU, kama bado ulikuwa hujabatizwa, baada ya hapo yeye mwenyewe ataingia ndani yako, na utaona matunda hayo na mengine Zaidi ya hayo..

Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”

Kama haujabatizwa na utahitaji msaada huo, basi waweza wasiliana nasi kwa namba zilizoanishwa hapa chini na tutakusaidia juu ya hilo.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

FAHAMU VIASHIRIA VYA MTU ALIYESAMEHEWA DHAMBI ZAKE.

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.

IMANI “MAMA” NI IPI?

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

UJIO WA BWANA YESU.

Rudi Nyumbani

Print this post

Wakrete ni watu gani na walikuwaje  waongo? (Tito 1:12)

Swali: Biblia inasema wakrete walikuwa ni waongo na walishuhudiwa na nabii wao, je walikuwaje waongo  (walidanganya nini), na huyo nabii wao alikuwa nani?


Jibu: Wakrete ni jamii ya watu waliokuwa wanaishi mahali paitwapo “Krete” na Krete ni kisiwa kilichokuwepo katika nchi ya Ugiriki.

Sasa Mtume Paulo alimwandikia Tito waraka huu kumpa maagizo na maelekezo machache kuhusu kanisa na viongozi (katika uteuzi).. Kwa urefu kuhusiana na kitabu hiki cha Tito na maaelekezo Paulo aliyompa Tito kwa uongozo wa Roho Mtakatifu fungua hapa >>> MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.

Lakini kwa ufupi ni kwamba tabia mojawapo waliyokuwanayo watu wa Krete, ni UONGO, Walikuwa wanasifa ya kusema Uongo katika viwango vikubwa, kiasi kwamba mpaka mtu wa kwao, ambaye ni nabii wao wenyewe aliandika kuhusiana na tabia hiyo waliyonayo waKrete ya Uongo, pamoja na ulafi na uvivu.

Biblia haijamtaja huyo Nabii ni nani, na wala haijaandika kuhusu huo waraka, lakini hapa tunaona Mtume Paulo ana unukuu…”

Tito 1:12 “..MTU WA KWAO, NABII WAO WENYEWE, AMESEMA, WAKRETE NI WAONGO SIKU ZOTE, HAYAWANI WABAYA, WALAFI WAVIVU

Sasa tukirudi katika historia, alikuwepo mwana filosofia wa KRETE aliyeitwa “EPIMEDINES”.. Huyu alikuwa ni Nabii wa mungu wa kigiriki aliyeitwa “zeu”..ambaye anatajwa katika Matendo 14:12-13.

Huyu Epimedines pamojana na kuwa alikuwa ni nabii wa mungu huyo wa kigiriki, lakini pia alikuwa ni mwandika mashairi. Moja ya shairi lake aliloliandika (ambalo aliliandika kwa kumtukuza huyo mungu wao wa kigiriki aliyeitwa zeu) lilikuwa linasema hivi..

…“Walikutengenezea kaburi, takatifu, uliye juu (zeu), Wakrete, waongo siku zote, wanyama wabaya, wavivu wa tumbo. Lakini wewe hukufa: unaishi na unakaa milele. Kwa maana ndani yako tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai wetu”…

Ni shari la kumtukuza mungu wao (zeu), lakini lilikuwa maarufu Krete kote kwani huyu Epimedines aliaminika na  wakrete wote kuwa ni nabii. Na Paulo kwasababu ni msomaji, aliujua huu ushairi, na hivyo katika kusisitiza dhambi ya wakrete ya Uongo kuwa ni kweli, ndio ananukuu hayo maneno ya nabii wao aliyewashuhudia kuwa ni waongo.

Lengo la Mtume Paulo si kumthibitisha nabii wao huyo La!.. bali kuthibitisha Uongo wa wakrete ambao watu wote wanauona hata walio wa Imani ya mbali… Hivyo ndio anamwonya Tito aukemee huo!.

Tunachoweza kujifunza ni kuwa UONGO ni mbaya, kwani biblia inashuhudia kuwa ibilisi ndiye baba wa Uongo, hivyo wote wadanganyi wote ni watoto wa ibilisi.

Yohana 8:44 “ Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo”.

Bwana atusaidie tushinde dhambi.

Maran atha!

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

WANNE WALIO WAONGO.

Mzushi ni nani kibiblia? (Tito 3:10).

UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.

Mungu anachukia kuachana (Malaki 2:16)

UNAWAFAHAMU MANABII WA UONGO?

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini Mungu aliwazuia walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake?(Walawi 21:16-24)

SWALI: Kwanini katika agano la kale Mungu aliwazua walemavu wasimtumikie madhabahuni kwake? Ikiwa Mungu hana upendeleo kwanini aliliagiza hili litendeke?


Mambo ya Walawi 21:16-24

[16]Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

[17]Nena na Haruni, umwambie, Mtu awaye yote wa kizazi chako wewe katika vizazi vyao, aliye na kilema, asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

[18]Kwa kuwa mtu awaye yote aliye na kilema hatakaribia; mtu kipofu, au kiwete, au mtu aliye na pua iliyoharibika, au aliye na kitu kilichozidi vimpasavyo mwili,

[19]au mtu aliyevunjika mguu, au aliyevunjika mkono,

[20]au aliye na kijongo, au aliye kibeti, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;

[21]mtu awaye yote wa kizazi cha Haruni kuhani aliye na kilema asikaribie kuzisongeza sadaka za BWANA kwa njia ya moto; ana kilema huyo asikaribie kusongeza chakula cha Mungu wake.

[22]Atakula chakula cha Mungu wake, katika hicho kilicho kitakatifu sana, na hicho kilicho kitakatifu.

[23]Lakini hataingia ndani ya pazia, wala asikaribie madhabahu, kwa sababu ana kilema; ili kwamba asipanajisi patakatifu pangu; kwa kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye.

[24]Basi Musa akanena na Haruni na wanawe, na wana wa Israeli wote.

JIBU: Agano la kale lilikuwa ni taswira ya agano jipya (la rohoni) jinsi litakavyokuwa baadaye (Wakolosai  2:17).

lile lilikuwa ni agano la mwilini, hivyo mambo mengi yalipaswa yadhihirishwe kwanza ki-mwilini ili kufunua au kufundisha kwa urahisi mambo ya rohoni yatakayokuja baadaye, lakini kiuhalisia haikuwa mpango wa Mungu mkamilifu yachukiliwe vilevile kwa majira yote.

Kwamfano mtoto mdogo anapoanza kujifunza hesabu, huwezi kumwambia  moja jumlisha na tatu ni nne. hatakuelewa. Bali utachukua kitu chenye umbo, (labda vijiti). utampa kimoja, kisha utachukua tena vijiti vingine vitatu utampa. halafu utamwambia avichanganye avihesabu atoe jumla.  atavihesabu vyote..na hapo hapo anakuambia nimepata vinne.

Sasa yeye atadhani hesabu ni vijiti. Lakini anapokuwa mtu mzima anagundua alipewa tu maumbo ili aelewe vizuri. Lakini hesabu ni uelewa wa akilini sio vijiti.

Vivyo hivyo na sisi tulipoanza kuelezwa makusudi makamilifu ya Mungu, tulifananishwa na watoto (Wagalatia 4:1-6). Mungu hakutaka kumleta Kristo moja kwa moja afe, amwage damu yake, ndipo sisi tuondolewe dhambi zetu kwa hiyo damu. Ukweli ni kwamba tusingemwelewa Mungu, vema.

Hivyo alitanguliza agano la kale kwanza, la mwilini, la mambo ya nje. Tuelewe kitaswira jinsi ilivyo sawa na isivyo sawa. ndipo baadaye atumie mifano hiyo kueleza ya rohoni.

kwamfano walikatazwa kula nguruwe, sababu alikuwa hacheui, mnyama asiyecheua ni yule asiyeweza kurejesha chakula akakitafuna na kukimeza tena kama ng’ombe. Sasa lengo la Mungu sio kwasababu nguruwe alikuwa ana magonjwa. kiuhalisia nguruwe ni mboga nzuri tu, lakini ni kwasababu ya ile sifa, ya kutocheua, ambayo rohoni sisi tunafundishwa hatupaswi kuwa nayo. maana yake ukishindwa kutafakari, yale uliyotendewa na Mungu nyuma, au uliyofundishwa na Mungu, wewe ni sawa na kiumbe najisi, mfano wa nguruwe. kwasababu hutaweza kuwa mtu wa shukrani, hutaweza kuwa mtu wa imani. Wana wa Israeli walionyesha tabia hii, wakati wanavuka habari ya shamu. walimnung’unikia Mungu wakisema unatuua, kwasababu hawana chakula. hawakukumbuka miujiza mikubwa aliyowatendea kipindi kifupi nyuma. Lakini Daudi alipokutana na Goliati hakulia wala kuogopa alisema yule Bwana aliyeniokoa na dubu na simba ataniokoa na mfilisti huyu asiyetahiriwa. alicheua akala tena akapata nguvu ya kuendelea mbele, kumshinda adui. Hakutaka kuwa nguruwe.

sasa tukirudi pia katika mambo ya madhabahuni kufuatana na swali letu.  Kumbuka waliopewa nafasi ya kuhudumu hekaluni walikuwa ni jamii ya makuhani tu, wazao wa Lawi. Mtu mwingine yeyote hakuruhusiwa. Vilevile hata yule mlawi ikiwa ni mlemavu wa aina yoyote pia hakuruhusiwa.

Kuonyesha kuwa hawakutengwa wao tu, hata watu wa kabila nyingine, haijalishi ni manabii au wanamtumikia Mungu kiasi gani ikiwa wewe si mlawi hukuruhusiwa hata na wanawake wote, hawakuwa tofauti na vilema katika suala la kuhudumu. Kwahiyo hawakutengwa walemavu tu. Bali na makundi mengine yote.

Sasa kwanini Mungu akataze walemavu na wenye madhaifu wasihudumu. Kwasababu Mungu alikuwa.anaonyesha picha ya rohoni ni jinsi gani watumishi wake, wahudumu.wa madhabahuni wanavyopaswa wawe, kwamba wasiwe watu wenye kasoro mbele zake. Yaani wawe watu wakamilifu sio walemavu rohoni.

Huo ndio ulikuwa ujumbe wa Mungu, hakuwa na Neno lolote baya na walemavu. Wala hakuwachukia.

Na ndio maana tunapokuja agano jipya tunaona vipofu, viwete, mabubu wanamjia Mungu, anawaponya. Na isitoshe Yesu alikuwa anakwenda kukaa kwao na kula nao (Marko 14:3).

Mungu hashughulika na ulemavu wa mwilini, bali ule wa rohoni. Ambao ukiwa mdhaifu huko, wewe ni najisi mbele zake. pitia somo hili ufahamu zaidi juu ya ulemavu wa rohoni upoje.

>>> UKOMA NA UJANE ULIO NDANI YAKO, UMEUPATIA TIBA?

wapo walemavu wengi, ambao wengine Mungu mwenyewe ameruhusu wawe vile kwa ushuhuda wake, na wanamtumikia kwa namna isiyo ya kawaida na wanafanya miujiza mikubwa, wanaponya watu na kuwafungua, utauliza kwanini Mungu asiwaponye? mawazo ya Mungu si mawazo yetu, Elisha alikufa na ugonjwa wake, lakini mifupa yake ilifufua wafu.

fuatilia ushuhuda huu ukujenge…. >>> USHUHUDA WA RICKY:

Hii ni kutuonyesha kuwa,  wakati wa sasa mbele za Mungu hakuna mwanamume, au mwanamke, au mlemavu au mtumwa wote ni makuhani wake na tumestahilishwa na Yesu Kristo kuingia patakatifu pa patakatifu kwa damu yake sisi tuliomwamini….

Haleluya. Upendo wake ni wa ajabu kwetu.

Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Mimbari ni nini? Je tofauti kati ya Mimbari na madhabahu ni ipi?

NITAONGEZAJE NGUVU ZANGU ZA ROHONI?

Ulimwengu wa Roho ni nini? Na mtu anawezaje kuwa wa rohoni?

CHAKULA CHA ROHONI.

Rudi Nyumbani

Print this post

JE! NI CHEMCHEMI IPI INATOKA NDANI YAKO, YA MITO AU YA KISIMA?

Mtu yeyote aliyeokoka, ndani ya moyo wake kunatokea chemchemi ya maji  yaliyo hai (Mithali 4:23). Na maji hayo huwa hayakauki, kwasababu yanatoka kwenye chanzo chenyewe  halisi ambacho ni Yesu Kristo,

Na Kama vile tunavyojua maji hufanya kazi zisizopungua nne.

  1. kukata kiu,
  2. kumeesha,
  3. kusafisha,
  4. na kugharikisha pale yanapozidi,

Ndivyo ilivyo kazi ya maji haya  katika moyo wa mtu, hukata kiu ya mambo maovu(Ufunuo 21:6, Yohana 4:14), humeesha mambo mema ya Mungu , husafisha moyo wa mtu, lakini pia  hugharikisha kazi za Yule  mwovu.

Ndio maana maandiko yanasema pepo limtokapo mtu hupitia mahali pasipo na maji, ni kwanini? Ni kwasababu eneo lenye maji  rohoni, pepo hawezi kukaa anaona gharika, na mafuriko makubwa hawezi kusogelea hapo. Na eneo lenye maji ni moyo wa mtu aliyeokoka.

Luka 11:24  Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,

25  Nitairudia nyumba yangu niliyotoka

26  Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza

Sasa wengi wetu hatujui kuwa hayo maji, yanakuwa kama maji ya “KISIMA” tu, ambayo hutulia pale pale, ni neema ya bure ambayo kila mwamini amepewa. Lakini ili ayafanye maji hayo kuwa “MITO” yaani yatiririke mbali. Si jambo la kusema tu nimeokoka. Bali kitu cha ziada lazima kifanyike kwenye maisha ya mtu.

Kama tunavyojua mito, huenda mbali kuwasaidia, hata watu wasiojua chanzo chake kilianzia wapi, Kwamfano mamilioni ya  wakazi wa mji wa Kilimanjaro, kutegemea maji yanayotiririka kutoka katika mlima wa Kilimanjaro, Na ni wazi wengi wao hawajui chanzo ni mwamba gani. Lakini wananufaika. Hata Pale Edeni Mungu alitoa mto katikati ya bustani, lakini haukuishia pale bali ulitoka mpaka nje ya bustani, kuyanufaisha mataifa. (Mwanzo 2: 10-14)

Vivyo hivyo ili na wewe yale maji uliyoyapokea siku ulipookoka, kama chemchemi ya kisima, unataka yatoke nje, huna budi kufanya jambo lingine la ziada.

Ndio maana mitume walishindwa kulitoa lile pepo sugu, wakijiuliza kwanini, ndipo   Bwana Yesu alisema maneno haya

Mathayo 17:21  [Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.]

Ni nini hiyo haitoki?

Ni maji yaliyo ndani yako. Kubadilika na kuwa mito, ni lazima uingie gharama za kuwa mwombaji. Si kuomba tu bali Kuomba bila kukoma. Mwombaji yoyote huuvutia uwepo wa Mungu maishani mwake. Maombi ni ‘pump ‘ya Mungu inayoyavuta yale maji nje! Yakawasaidie wengine. Huwezi kuwa mtu wa mafunuo kama huna desturi ya kuomba, huwezi kuwasaidia wengine rohoni, hata kuwaombea wasaidike, kama wewe si mtu wa kuomba. Unatazamia mumeo aache pombe, halafu sio mwombaji, utapona tu wewe peke yako, lakini hutaweza kumponya mwingine. Unatazamia familia yako iokoke, halafu wewe mwenyewe huingii gharama za mifungo na maombi, yasiyo koma, mara kwa mara, zitakuwa ni ndoto tu, labda Mungu awaguse kwa njia zake mwenyewe, lakini sio kwa matamanio yako.

Na si tu katika eneo la kuwasaidia wengine, bali hata katika maeneo ya maisha yako ambayo unataka uone maingilio Fulani ya Mungu makubwa. Huna budi kuyatoa hayo maji yaende kuponya hayo maeneo.

Maandiko yanasema imetupasa kumwomba Mungu sikuzote bila kukata tamaa (Luka 18). Hiyo ndio njia pekee itakayoleta majibu.

Yohana 7:38  Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.

Na Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NI WAPI UTAKUTANA NA MALAIKA WA BWANA?

Mruba ni mdudu gani kwenye biblia?(Mithali 30:15)

Mto Frati upo nchi gani, Umuhimu wake katika biblia ni upi?

Rudi Nyumbani

Print this post

HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU.

Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU”.

Je unaelewa maana ya kuwa Mwanafunzi?

Zifuatazo ni sifa za mwanafunzi.

   1. KUFUNDISHWA

   2. KUJIFUNZA.

   3. KUFANYA MITIHANI.

   4. KUHITIMU.

Mtu akikosa hizo sifa basi sio mwanafunzi.

Na kwa upande wa BWANA wetu YESU KRISTO ni hivyo hivyo (Tutazame moja baada ya nyingine).

       1. KUFUNDISHWA

Hakuna mwanafunzi yoyote anayejifundisha mwenyewe, ni lazima awe na mwalimu

Na vile vile Ili ukidhi vigezo vya kufundishwa na BWANA YESU mwenyewe ni “lazima ujikane nafsi”.. Na matokeo ya kukosa kufundishwa na Bwana ni kushindwa mitihani ya maisha ikiwemo VIPINDI VYA KUPUNGUKIWA na VIPINDI VYA KUWA NA VINGI.

Katika biblia tunaona mtu aliyefundishwa Vizuri na Bwana YESU na kuelewa ni Paulo… Yeye alifundishwa jinsi ya kuishi vipindi vyote vya (njaa na kutokuwa na njaa, vya kupungukiwa na kuongezekewa).

Wafilipi 4:12 “Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.

13  Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”

2. KUJIFUNZA.

Hii ni sifa ya pili ya Mwanafunzi yoyote, ni lazima awe anajifunza. Na kwa upande wa Imani ni lazima kujifunza kama mwanafunzi wa Kristo…

Na tukitaka tuweze kujifunza biblia na kuielewa  vizuri ni lazima tujikane Nafsi na kubeba misalaba yetu na kumfuata Bwana YESU. (hakuna njia nyingine tofauti na hiyo).

Si ajabu leo hii inakuwa ngumu sana kuweza kuielewa biblia, pindi tuisomapo…sababu pekee ni kutojikana nafsi na kubeba msalaba na kumfuata Bwana YESU, tunapenda ule ukristo laini laini, ambao hauna matokeo yoyote kiroho.

   3. KUFANYA MITIHANI.

Hii ni sifa ya tatu ya mwanafunzi yoyote anayesoma, ni lazima awe na vipindi vya kujaribiwa kwa mitihani.

Vivyo hivyo ili tuwe wanafunzi wa YESU wa Bwana ni lazima tupitishwe katika vipindi vya kujaribiwa na Bwana YESU mwenyewe….. Na lengo la mitihani hiyo (au majaribu hayo) ni kumwimarisha mtu huyo kiimani.

Yakobo 1:2 “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;

3  mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi”.

Na madhara ya kukosa kujaribiwa kwa mitihani ya BWANA YESU ni kushindwa kuhitimu na hatimaye kukosa cheti.

    4. KUHITIMU.

Mwanafunzi anayehitimu ni yule aliyemaliza mitihani yote na kufaulu, (huwa anapewa cheti) kile cheti ni kibali maalumu, na fursa  pamoja na heshima ya daima kwa mwanafunzi yule.

Vile vile na mtu aliye mwanafunzi wa BWANA YESU, akiisha kumaliza majaribu yote na kuyashinda, atahitimu kwa kupewa cheti ambacho ni TAJI YA UZIMA..

Yakobo 1:12 “ Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao”.

Jiulize je wewe ni Mwanafunzi wa BWANA YESU au ni mfuasi tu?…. Waliokuwa wanamfuatilia Bwana YESU ni wengi lakini waliomfuata na kuwa wanafunzi wake walikuwa wachache sana.. Wengine wote walikuwa ni washabiki tu aidha wa miujiza au wa siasa, lakini waliojiunga na chuo cha Bwana YESU walikuwa ni wachache sana.

Na kanuni ya kujiunga na chuo hicho cha Bwana YESU na kuwa mwanafunzi wake si nyingine Zaidi ya hiyo ya “KUJIKANA NAFSI NA KUBEBA MSALABA”.

Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, HAWEZI KUWA MWANAFUNZI WANGU”.

Na kumbuka hakuna tafsiri nyingine ya UKRISTO au kuwa MKRISTO Zaidi ya UANAFUNZI..

Matendo 11:26  “….Na WANAFUNZI waliitwa WAKRISTO kwanza hapo Antiokia”.

Hivyo ukitaka kujijua kama wewe ni Mkristo au la!.. sipime tu kama umeshakuwa Mwanafunzi wake, kama huna sifa hizo hapo juu za uanafunzi bado hujawa MKRISTO.

Bwana YESU atusaidie.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?

Bwana alimaanisha nini kusema “Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake”?

Mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu?

NITAJUAJE KUWA NIMEITWA ILI KUMTUMIKIA MUNGU?

TOA HUDUMA ILIYO BORA.

Rudi Nyumbani

Print this post

JIFUNZE JAMBO KWENYE UKOO WA YESU, UWE NA AMANI

Leo hii kumekuwa na hofu nyingi katikati ya watu, juu ya historia na machimbuko ya familia zao.  Wengine wameona maisha yao au tabia zao za sasa zimeathiriwa na chimbuko la familia zao, au koo zao, au mababu yao. Na hivyo hawajui wafanyeje.

Lakini ukweli ni kwamba hakuna hata mmoja wetu ambaye, chimbuko lake halijaathiriwa, Tukianzia na la Bwana wetu Yesu Kristo, na ndio maana biblia imeandikwa tukapewa, ili kutuonyesha sisi njia, ya kusimama na shindana na nguvu za Yule mwovu kwa ujasiri wote bila woga.

Kitabu cha Mathayo, kinaanza na kueleza ukoo wa Yesu. Kulikuwa na sababu ya kutangulizwa historia ya ukoo wake, ili Mungu kutufundisha sisi jambo. Watu wengi wakiangalia ule mtiririko, wanadhani Mungu anatuonyesha jinsi Yesu alivyotokea katika ukoo hodari, mashuhuri. Lakini Hapana. Ukweli ni kwamba hakukuwa na umuhimu wowote, kwa wengi walioorodheshwa katika ukoo wake.

Lakini nataka tuone, jinsi ukoo ule ulivyovurugwa, kiasi kwamba kama Mungu angetazama usafi basi, usingestahili hata kidogo kumleta mkombozi duniani. Katika ukoo wake hakukuwa tu na wema, lakini kulikuwa na  “makahaba” kulikuwa na pia “wazinzi-waliokubuhi”, kulikuwa na “makafiri” . Kwamfano Yule Rahabu, alikuwa ni kahaba, tena kahaba kweli kweli. Tena Kulikuwa na Ruthu, mwanamke wa kimataifa, ambaye Mungu aliwakataza kwa nguvu sana, wayahudi wasitwae wanawake wa kimataifa kuwaoa, mbegu takatifu zisichangamane na mbegu nyingine (Ezra 9:2) ni unajisi, lakini hapa ikawa tofauti, mwanamke wa kimataifa akaingizwe kwenye ukoo. kama huyo haitoshi alikuwepo mzinzi  Tamari, ambaye, yeye alifanya hila akalala na mkwe wake, kumzaa Peresi,..Jambo lisilofikirika kiakili, vilevile, alikuwepo Bersheba  mke wa wizi, wa Mfalme Daudi, ambaye miongoni mwa wake halali wa Daudi hakuwepo, lakini alichaguliwa yeye, kuupitisha uzao wa Kristo, na wale wasafi wakaachwa.

Tusome..

Mathayo 1:1  Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.

2  Ibrahimu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;

3  Yuda akamzaa Peresi na Zera KWA TAMARI; Peresi akamzaa Esromu; Esromu akamzaa Aramu;

4  Aramu akamzaa Aminadabu; Aminadabu akamzaa Nashoni; Nashoni akamzaa Salmoni;

5  Salmoni akamzaa Boazi KWA RAHABU; Boazi akamzaa Obedi KWA RUTHU; Obedi akamzaa Yese;

6  Yese akamzaa mfalme Daudi. Daudi akamzaa Sulemani KWA YULE MKE WA URIA ;

7  Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;

8  Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia;

9  Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia;

10  Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia;

11  Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli.

12  Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;

13  Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori;

14  Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi;

15  Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo;

16  Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.

17  Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vine.

Hivyo ukoo wa Bwana wetu Yesu Kristo, ulivurugwa-vurugwa, tunaweza kusema haukuwa msafi,  kulinganisha na koo za wayahudi wengine. Lakini huyo ndiye aliyekuja kumpendeza Mungu kuliko wote, ijapokuwa alitokea katika chimbuko lililokorongoka, huyo ndiye aliyekuja kuwa mkombozi, huyo ndiye aliyekuja kuwafungua watu na kukata mizizi yote ya laana, na kuwa Baraka kwa ulimwengu.

Ni kutufundisha nini?

Usiogope, yawezekana kweli, chimbuko lenu ni bovu, ni makahaba tu, ni walevi tu, mna magonjwa ya kurithi yanatembea, mnaudhaifu Fulani, maskini wa kupindukia, hamuoelewi, hamzai. Nataka nikuambie wacha kuhangaika kuufikiria ukoo wako. Kwasababu hata iweje hakuna aliyewahi kutokea mwenye chimbuko safi hapa duniani. Wewe mtazame  Kristo tu, aliyemaliza yote pale msalabani. Amini tu kazi yake aliyoimaliza kwako.

Unapookoka, huna laana yoyote ndani yako, haijalishi ukoo mzima walizindika, haijalishi mna mizimu na mikoba ndani.. Hiyo ndio bye! Bye!, imeisha!. Haina nguvu ndani yako, wala usiipe kibali, mwamini Yesu aliyekukomboa.

Usiwe mtu wa kuzunguka huku na huko kuvunja laana za ukoo, utavunja ngapi? Ni mababu wangapi wamepita huko nyuma, itakupasa basi urudi sasa mpaka Adamu. Uvunje laana zote. Hivyo kua kiroho, mwamini Yesu aliyekukomboa. Matatizo ya kifamilia mliyonayo, wanayo hata wale watumishi wa Mungu, isipokuwa kwa namna tu nyingine. Lakini wao wamemwamini Kristo aliyewakomboa, ndio maana hawana laana yoyote. Lakini kaulizie huko kwao kukoje watakuambia. Ndugu ukiokoka, Ya kale yamepita tazama, yamekuwa mpya. Unachopaswa kufanya baada ya kuokoka tu , ni kuendelea kumjua zaidi Kristo ili uwe na amani,sio kuchimbua tena ya kale, jifunze kwa ukoo wa Yesu .

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Kwanini  vizazi vya ukoo wa Yesu vinajipinga katika Mathayo na Luka.

KUVUNJA MAAGANO YA UKOO.

UMUHIMU WA KUISHI MAISHA YAMPENDEZAYO MUNGU SASA.

Rudi Nyumbani

Print this post

Mungu anachukia kuachana (Malaki 2:16)

(Masomo maalumu kwa wanandoa)


Kama unafikiria kuachana na huyo ulifunga naye ndoa ni jambo la busara,  basi fahamu kuwa unafanya jambo linalomchukiza BWANA MUNGU. Kwanini???.. ni kwasababu Mungu anachukia kuachana.

Malaki 2:16 “Maana mimi NAKUCHUKIA KUACHANA, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana”

Utauliza vipi kwa sababu ile ya Uasherati iliyotajwa katika Mathayo 5:32.

Mathayo 5:32 “lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini”.

Ni kweli Uasherati ndio sababu pekee ya uhalali wa ndoa kuvunjika, lakini bado biblia haijatoa amri au sharti kuwa pale uasherati unapotokea basi ndoa hiyo ivunjike..(kwamba haipaswi kuendelea) inapaswa ivunjwe!.. La! Biblia haitufundishi hivyo hata kidogo…badala yake biblia inatufundisha kusamehe!..

Bwana wetu YESU KRISTO alikuwa na sababu zote za kutotusamehe, lakini alitusamehe hivyo hivyo, vipi mimi na wewe!, tusipokuwa watu wa kusamehe tutawezaje kumpendeza Mungu au sisi wenyewe kusamehewa?

Hivyo suala la ndoa ni kusameheana na kuvumiliana kwa mambo mengi.. Sisemi kuwa uasherati uvumiliwe au upaliliwe ndani ya ndoa, la!.. bali pale mmoja anapoonekana kuvutwa na ibilisi ni wajibu wa mwingine kumrudisha kwenye mstari kwa kumvumilia na kumwombea pamoja na kumtengeneza kwa neno la Mungu mpaka atakaporejea katika mstari sahihi wa Imani.

Usimwache Mume/mke kwasababu ya zinaa, (Ni kweli ni jambo linaloumiza lakini jifunze kuvumilia na kusamehe na kutafuta namba ya kutengeneza)…itakufaidia nini kumwacha huyo na kwenda kuanza familia nyingine na huku tayari mna watoto?..

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya magomvi ya hapa na pale, itengeneze nyumba yako kwa maombi na mafunzo ya Neno la Mungu.

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya hali ya Uchumi.. tafuta namna ya kuyatengeneza na si kukimbia.

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya ndugu zako au ndugu zake, marafiki zako au marafiki zake.

> Usimwache Mume/mke kwasababu ya Uzee au magonjwa au madhaifu aliyonayo.

Na kumbuka: Mume na Mke wanaozungumziwa hapa ni wale waliohalalishwa na Neno la Mungu, (maana yake waliofunga ndoa) na si wale wanaoishi kihuni (wamechukuana na kuishi kwenye chumba/nyumba, na hata wengine wamezaa watoto)..hao si wanandoa bali ni wahuni..Hao haya maandiko haya na mashauri haya hayawahusu kabisa.. badala yake wanapaswa waachane mara moja na watubu na kila mmoja akae kivyake!!!!, kwasababu wanafanya Uasherati.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako.

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.

Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?

Pale mwanandoa mmoja anaposhindwa kutimiza wajibu wake ufanyaje?

Rudi Nyumbani

Print this post

Je mkristo anaruhusiwa kuchangia damu?

Swali: Je mkristo anaruhusiwa kuchangia damu kwa mgonjwa aliye katika uhitaji huo, kwaajili ya kuokoa maisha yake?


Jibu: Biblia inasema maneno yafuatayo…

1Yohana 3:16 “Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; IMETUPASA NA SISI KUUTOA UHAI WETU KWA AJILI YA HAO NDUGU.

17  Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo”

Maadamu mtu akiondolewa damu kiasi kidogo mwilini mwake, Hafi!!.. na vile vile mtu anayepokea damu mwilini mwake pia Hafi!, kinyume chake ndio anapata UZIMA! (wa mwilini).. basi ni wazi kuwa si dhambi kuchangia damu kwa mtu mwingine…..Zaidi sana ni jambo la upendo, ikiwa hakuna njia nyingine ya kumsaidia mhitaji huyo zaidi ya hiyo ya kumchangia damu.

Kwanini si dhambi!.. ni kwasababu hata sehemu ya damu tulizonazo tumepokea kutoka kwa wazazi wetu!…HAKUNA MTU ANAYEZALIWA DUNIANI NA DAMU YAKE MAALUM (Special), wote tunazipokea kutoka kwa wazazi wetu ndio maana zinamfanano na hao!, na zinamfanano na ndugu zetu tuliozaliwa nao familia moja.

Kwahiyo kumchangia damu mgonjwa si dhambi!… Maana utamchangia atapona!, na kwa njia hiyo yaweza kuwa sababu ya kumvuta kwa KRISTO, (akiona upendo wako namna hiyo).. lakini kama ukimnyima na akifa katika hali yake ya kutokuamini hakuna faida yoyote wewe unayoipata…

Kwahiyo ni afadhali utafute namna ya kuokoa roho kwa njia hiyo, kwasababu hakuna hasara yoyote unayopata katika mwili wako utoapo kiasi kidogo hiko cha damu na kumpatia mwingine!.. ni lita ngapi za damu umepoteza wakati wa mzunguko wako (wewe mwanamke) na bado unaendelea kuishi.

Ni lita ngapi za damu umepoteza wewe mwanaume ulipopata majeraha au ulipofyozwa na hao mbu kutandani mwako siku zote za maisha yako?.. Kwa kutafakari hayo yote hakuna sababu ya kumnyima damu ndugu yako, ikiwa kuna ulazima huo, na wala hakuna sehemu yoyote kwenye biblia iliyokataza kuchangia damu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

Je!Sisi kama wakristo Tunaruhusiwa kuchangia ujenzi wa Imani nyingine?

Je mama mjamzito anaruhusiwa kufunga?

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

Nini maana ya Mithali 27:21  inaposema “mtu hujaribiwa kwa sifa zake?”

JE UMEUFIKIA ULE UTUKUFU HALISI WA MANA? 

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini kuna mrudio wa uumbaji kwenye Mwanzo sura ya pili?

Swali: Tukisoma Mwanzo sura ya kwanza tunaona Mungu akimaliza kazi yote ya uumbaji kwa zile siku saba, lakini tukirudi kwenye Sura ya pili tuona ni kama tena Mungu anarudia uumbaji anamuumba mwanadamu,  na pia mimea, je kulikuwa na uumbaji wa aina mbili ulitokea pale. Na ni nini tunajifunza pale?


JIBU: Jibu ni hapana, uumbaji wa Mungu ulikuwa ni ule ule mmoja, tofauti na baadhi ya watu wanavyodhani. isipokuwa Sura ya kwanza Mungu anaeleza ‘kwa taswira ya ujumla’, lakini katika sura ya pili anaeleza jinsi ‘utaratibu wa uumbaji wake ulivyokuja kutokea’, mpaka kuileta hiyo picha ya ujumla.

Kwamfano katika Sura ya kwanza anasema Mungu alimuumba mwanamke na mwanaume..

Mwanzo 1:27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

Lakini katika sura ya pili anaonyesha jinsi alivyoanza kumuumba  kwa kumtoa ardhini mpaka alivyompulizia pumzi ya uhai, hadi utaratibu wake wa kutawala.

Mwanzo 2:4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi

5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.  7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.

8 Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.

Umeona,? Vilevile ukisoma Mwanzo 1:11&12, utaona Mungu anaumba mimea yote . Lakini hapo kwenye sura ya pili anaonyesha  jinsi mime hiyo inavyokuja kutokea, anaeleza kwanza inaanza  katika mbegu, kisha inyeshewe mvua, ikue baadaye ndio iwe mche kamili wenye matunda.

Hivyo, Kulikuwa na umuhimu wa kuwekwa sura zote mbili, ili tuelewe  kanuni za Mungu za utekelezaji wa mipango yake. Maana kama tungeishia tu sura ya kwanza tusingeelewa ni kwa namna gani mambo yanaendelea kama yalivyo leo.

Ni fundisho gani lipo hapo?

Hata sasa Mungu anasema jambo. Lakini pia huna budi kuelewa mpango wake wa utekelezaji wa hilo jambo! Ili usiudhike, au usikate tamaa, au usijikwae, au usiwe na mashaka. Unatafakari ni kweli Mungu alimuumba mwanamke tangu awali, lakini kutokea kwake kulikuja baadaye sana, tena sio ardhini bali ubavuni mwa Adamu. Kama hilo tusingelifahamu, tusingeelewa kwanini tunaambiwa sisi wote ni mwili mmoja.

Kama tusingejua kuwa  ili mti ufikie matunda, kama Mungu alivyoukusudia, ni lazima uanze kwanza kama mbegu, ioze ardhini, kisha ipate mvua, imee, itoke katika jani, hadi shina, hadi mti. Tungesema hii si sawa, kuna shida, mbegu kuoza ardhini, hakuna mmea hapo?.

Halikadhalika hata sasa Mungu amekuahidi pengine, atakupa jambo Fulani. Sasa usitarajie lije ghafla tu, pengine litapitia hatua Fulani, huwenda likaonekana kama limetoweka kabisa,kama vile mbegu inayooza ardhini, lakini mwishowe itakuja kutokea tu, kama tu Yusufu alivyoonyeshwa kuwa ndugu zake watamwinamia, Au Ibrahimu kuonyeshwa atakuwa  baba wa mataifa mengi, lakini mapito yao unayajua, Yusufu kuuzwa utumwani, kutupwa gerezani, Ibrahimu kuwa tasa. Lakini mwisho utaona yale waliyoahidiwa yalikuja kutokea vilevile.

Tunapaswa tumwelewe sana Mungu ili tuwe na amani, Neno la Mungu linaposema, kwa kupigwa kwake sisi tumepona, amini kuwa umepona kwa kifo cha Yesu, hata kama utahisi maumivu mengi kiasi gani leo, daktari atakuambia huwezi kupona ugonjwa wako hautibiki. Wewe amini, tu hilo jambo litatokea, haijalishi litachukua wakati gani, utapitia mateso mengi kiasi gani leo, mwisho wa siku utakuwa tu mzima.

Usiishi tu na mwanzo sura ya kwanza, ishi pia na sura ya pili. Utamwelewa Mungu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

NGUVU YA MUNGU YA UUMBAJI

Kwanini Bwana achukizwe na mtumwa yule aliyeficha talanta yake ardhini? (Mathayo 25:26-30)

Ni maneno gani Bwana Yesu aliyokuwa anayaandika ardhini? (Yohana 8:7).

Rudi Nyumbani

Print this post

Kwanini biblia ni neno la Mungu?

Swali: Je ni kweli biblia ni Neno la Mungu?


Kabla ya kujibu kwanini biblia ni Neno la Mungu, na si kitabu kingine chochote?… hebu tujiulize kwanza na tujadili kwanini

Biblia ni Neno la Mungu kwasababu lina maneno yaliyo hai..

Vivyo hivyo biblia ni kitabu cha Mungu, kwasababu kimebeba taarifa sahihi kumhusu Mungu.. Na taarifa KUU ndani ya kitabu hiko kitukufu, ni taarifa ya mwanadamu kuondolewa dhambi kupitia YESU KRISTO (Hiyo ndiyo taarifa kuu) ambayo inaleta “UZIMA WA MILELE KWA MTU”..Na ndio karama kuu ya MUNGU kwetu.

Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.

Vitabu vingine vyote vilivyosalia havijabeba suluhisho lolote la ondoleo la dhambi za Mtu, badala yake zimebeba tu taarifa za maadili, au staha, mambo ambayo yanapatikana hata katika vitabu vya sheria za nchi.

Lakini taarifa na njia ya ondoleo la dhambi zipo katika BIBLIA TU PEKE YAKE!!!..

Kwasababu “dhambi” ndio sumu pekee ya mwanadamu, na hiyo ndio kizuizi kikubwa cha mtu kumkaribia Mungu, hivyo mtu akiondolewa hiyo anakuwa ameokoka! Hata kama maisha yake hapa duniani bado yanaendelea.

Na ni kwa njia gani mtu anaondolewa dhambi zake moja kwa moja??

Matendo 2:36 “ Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.

37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

38 Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, NANYI MTAPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU”.

Kanuni ya kuondolewa dhambi, ni kutubu na kubatizwa (Marko 16:16). Na toba halisi ni ile inayotoka moyoni yenye madhamirio ya kugeuza mwelekeo moja kwa moja. Na ubatizo sahihi ni ule wa maji mengi (Yohana 3:23) na kwa jina la BWANA YESU (Matendo 8:16, na Matendo 19:5).

BWANA YESU AKUBARIKI.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Mafundisho mengine:

JIPE NAFASI KATI YA TAARIFA UNAYOIPOKEA NA MAAMUZI UNAYOYATOA.

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

UPEPO WA KUSI HULETA MVUA;

NENO LA MUNGU KATIKA UTIMILIFU WOTE.

UWEZA WA MUNGU NJE YA WAKATI.

Rudi Nyumbani

Print this post