Swali: Kucheza Magemu kwenye komputa au simu ni sahihi? Mfano magemu ya mpira, vita, kupigana, karata, magari, pool-table, zuma, na mengineyo ni dhambi?..
Jibu: Kabla ya kujibu swali hili, ni muhimu kwanza kujua michezo hiyo kama ni sahihi kuishiriki au la!
Awali ya yote mkristo aliyeokoka, hapaswi kushiriki michezo ya kupigana, iwe awanjani (ndondi) au vitani (iwe kwa nia ya kifursa au burudani) kwasababu biblia inasema kushindana kwetu si juu ya damu ya nyama bali juu ya falme na mamlaka za mapepo katika ulimwengu wa roho (Waefeso 6:10-13 na vita vya kiroho dhidi ya mapepo si vya kujiburudisha au kujifurahisha).
Vile ile mkristo hapaswi kucheza pool-table kwasababu ni mchezo wa ibilisi na unaochezwa na watu wasio na Roho wa Mungu.. ndio maana meza zake zipo maeneo yafanyikapo anasa kama disko, au bar… huwezi kukuta poo-table kanisani.
Vile vile mkristo hapaswi kushiriki michezo mingine yote ya kidunia iliyojishonesha na mifumo ya kidunia ikiwemo mipira na basket.
Sasa kama hapaswi kushiriki wala kushabikia michezo hiyo, vile vile Magemu yanayoshabikia mambo hayo hapaswi kushiriki, kwasababu hakuna tofauti ya kushabikia ukiwa uwanjani na kucheza magemu yake.. (kwasababu ile shangwe unazaliwa moyoni kutokana na kile unachokiona au kishiriki).
Hivyo si sahihi kwa mkristo kucheza magemu katika kompyuta au simu au katika kifaa kingine chochote ikiwemo PS (Play station).
Lakini yapo magemu yaliyotengenezwa pasipo kuhusisha michezo ya damu na nyama, (hayo ndio hatari kabisa) kwasababu yamebuniwa kutoka katika mambo yanayoendelea rohoni.
Kwamfano utaona kuna magemu ya Nyoka,.. joka linazunguka na kumeza vitu, sasa mambo haya hayapo katika ulimwengu wa mwili, lakini yapo katika ulimwengu wa roho.. sasa kwasababu shetani anataka kuendeleza mahusiano kati yake na wanadamu kwa hata njia ya mwili, ndio yanakuja haya magemu.
Mtu anapocheza game la kumwongoza nyoka kumeza vitu, au anapocheza game la kukumbizwa na joka, au kukimbizwa na viumbe visivyojulikana, basi anashiriki basi anathibitisha mambo hayo katika roho, na hivyo maisha yake yataendeshwa na hayo maroho kwa kupenda au kutokupenda. (Hata ndoto zake zitakuwa zimejaa hayo mambo).
Roho ya kupenda na kucheza magemu inaongezeka kwa kasi siku hizi za mwisho, na hasa kwa njia ya simu.. zamani ilikuwa ni agenda ya kupanda msingi wa maroho kwa watoto, lakini siku hizi hata watu wazima, hivyo ni kuongeza umakini sana.
Biblia inasema tusiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani, kwani mtu akiipenda dunia hata kumpenda Baba hakupo ndani yake.
1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.
16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia
17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele”
Na tena inasema yoyote yaliyo yenye kupendeza na yaliyo ya staha na kweli tutayafakari hayo (Wafilipi 4:8)
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
LENGO LA SHETANI KWA WATOTO WA KIZAZI HIKI.
Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?
Je kumwimbia Mungu kwa kucheza ni sahihi kibiblia?
Jicho kucheza ni ishara ya nini?
Neno la Mungu linatufundisha kuushinda “Ubaya kwa wema”..
Warumi 12:20 “Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21 USISHINDWE NA UBAYA, BALI UUSHINDE UBAYA KWA WEMA”.
Maana yake ukifanyiwa ubaya, usilipe ubaya, bali Lipa “Wema”, ili yule aliyekufanyia ubaya ajione yeye ndiye mwenye makosa na hivyo baadae arejee na kutubu.
Lakini pia biblia hiyo hiyo inazidi kutufundisha kuwa WEMA wetu pia usitajwe kwa UBAYA
Warumi 14:16 “Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya”.
Kumbe pia “Wema” unaweza kutajwa kwa “Ubaya”
Unaweza kweli usirudishe Ubaya kwa ubaya, na ukarudisha wema kwa ubaya…lakini bado huo wema ulioufanya ukaonekana ni “mbaya”.
Hivyo ni lazima pia “tuutakase wema wetu”.. Hata Maji ijapokuwa yanaweza kutumika kusafisha nguo, lakini nayo pia yanaweza kuchafuka.. hata sabuni pia ijapokuwa inatumika katika kutakasa, lakini nayo pia inaweza kuchafuka!..
Vile vile na “Wema” ijapokuwa ni mzuri na unahitajika lakini pia unaweza pia Kuchafukana na kuonekana “mbaya”.
Sasa ni Kitu gani kinchouchafua Wema wetu?
1. Nia
Nia ni kitu kimoja kinachoweza kuufanya Wema wetu usiwe tena wema bali UNAFIKI… Kwamfano utaona mtu anaweza kufanya “wema”..lakini Nia yake ni ili ASIFIWE na watu, au aonekane ni mtu wa kidini, aliyesimama kiimani! Na wala ndani yake hamna upendo wala dhamiri njema!. Sasa wema wa namna hii ndio “Wema unaotajwa kwa Ubaya”.
Mathayo 23:28 “Vivyo hivyo ninyi nanyi, kwa nje mwaonekana na watu kuwa wenye haki, bali ndani mmejaa unafiki na maasi”.
2. Roho ya KISASI
Roho ya kisasi ni ile hali ambayo mtu atarudisha wema… Lakini moyoni anawaza kisasi (kwa kusema Mungu ampige).. Ndugu ikiwa umefanyiwa ubaya, epuka kauli hii “Namwachia Mungu atampiga”… Kauli hii inaonekana ni njema sana na ya busara, lakini nataka nikuambie, busara yake haijakamilika (hiyo kauli ina kasoro).. Ni kweli umefanya wema, baada ya wewe kutendewa mabaya,
Sasa kuliko umtakie mabaya kutoka kwa Mungu ni heri umwombee rehema ili yamkini Mungu amsamehe (hiyo itakupandisha thamani sana mbele za Mungu, kwasababu sifa ya Kwanza ya Mungu ni rehema kabla ya visasi).. …tunalithibitisha vipi hili kibiblia?
Mithali 24:17 “Usifurahi, adui yako aangukapo; Wala moyo wako usishangilie ajikwaapo,
18 Bwana asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake”
Kama Bwana ataamua kumlipa kisasi kwa aliyoyafanya kwako basi hiyo ni juu yake (Bwana) na si juu yako wewe, kwani kisasi ni juu yake yeye (Warumi 12:19-2), na hatuwezi kumshauri juu ya visasi..
kwani kuna waliojaribu kumshauri na ikashindikana…wapo waliomwombea kisasi Sauli kwa kuwaua watakatifu wa Kristo, lakini kisasi walichomwombea au walichomtakia (kwamba apigwe na Mungu) kiligeuka kuwa Wokovu kwa Sauli na Kuwa Paulo Mtume, kwahiyo masuala ya visasi si juu yetu sisi wakristo, hiyo ni juu ya Mungu, tunachopaswa kufanya ni kufanya wema na kuwaombea rehema maadui zetu, kwamba Bwana awasamehe, mengine tunamwachia yeye..
Jambo hili ni kama mtihani mkubwa lakini ndio NENO LA MUNGU!!..wala sio “ulemavu wa akili, wala sio unyonge”..bali ni Neno la Mungu lenye nguvu na linaloishi…
Luka 6:27 “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, WATENDEENI MEMA wale ambao wawachukia ninyi,
28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie”.
Bwana atusaidie… WEMA WETU UTAJWE kwa uzuri na si kwa Ubaya.
Maran atha!
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
UFANYE WEMA WAKO KATIKA MAARIFA.
AINA SABA (7), ZA SIFA KIBIBLIA.
Nini maana ya ‘kuhuluku’ kama tunavyosoma katika biblia?
TEMBEA NDANI YA SUKOTHI YAKO.-Maafundisho maalumu kwa watumishi
Mithali 13:20 Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
Tulipokuwa watoto wazazi wetu walitufundisha kubagua baadhi ya marafiki tuliokuwa nao, na cha ajabu vigezo walivyotumia havikuwa hata rangi zao, au kimo chao, au afya zao, bali tabia zao na akili zao. Wale watoto waliokuwa na nidhani, na akili shuleni wazazi wetu walitushurutisha sana kukaa nao karibu, kwasababu waligundua kuwa na sisi tutaambukizwa tabia zao, lakini wale waliokuwa watukutu, hata tulipokutwa tunacheza nao tu, tuliadhibiwa, sisi tuliona kama ni uonevu usio kuwa na tija, lakini baadaye tulipokuwa watu wazima, na kuona hatma ya wale watoto, ndio tulijua ni nini wazazi wetu walikuwa wanakiona.
Vivyo hivyo katika maisha ya rohoni, tunaambiwa.
Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.
Ni watu waliookoka, wenye hofu ya Mungu ndani yao.
Mtu yeyote aliyemwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake, huku akiendelea katika kumcha Mungu kwelikweli, huyo ni wa kukaa karibu naye sana. Kwasababu na wewe utajifunza njia za wokovu, utaambukizwa kuomba, utaambukizwa mifungo, utaambukizwa upendo wa ki-Mungu, lakini pia na maarifa ya Neno la Mungu, pamoja na uinjilisti.
Watu hawafahamu kuwa hata hekima ya mwokozi wetu Yesu haikuja tu kwa kutegemea hekima kutoka juu kwa baba yake, hapana, ilichangiwa pia na watu aliowachagua kukaa nao karibu, tangu alipokuwa mdogo, tunalithibitisha hilo pindi alipokuwa amekwenda Yerusalemu na wazazi wake kwa ajili ya kuila sikukuu, kama kijana angeweza kukaa na wenzake, kujifunza uchezaji wa kamari, au kutembea mitaani kutafuta wasichana, au kwenda kwenye dansi na sinema, na kujiunga na makundi ya wavuta bangi. Lakini, haikuwa hivyo kwake, yeye alichagua watu ambao wangekuwa ni wa muhimu kwake, ndio wale viongozi wa imani na waalimu waliotwa marabi, akawa akiwasikiliza hao na kuwauliza maswali, na ghafla akaambukizwa tabia zao, mpaka akawa yeye ndio RABI wao mkuu.
Luka 2:40 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. 41 Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka.
42 Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu;
43 na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari.
44 Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao;
45 na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. 46 Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, AMEKETI KATIKATI YA WAALIMU, AKIWASIKILIZA NA KUWAULIZA MASWALI.
47 Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. 48 Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.
49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? 50 Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia
Mambo mengine hutaweza kuyaacha, au tabia nyingine hutaweza kuziondoa ndani yako. Kama hutaweka machaguzi ya watu sahihi wa kuongozana nao. Utakuta ni mkristo analalamika ni mzito wa kuomba, au kushuhudia, au kufunga. Ukiangalia kampani ya watu wake muda wote, ni wafanyakazi wenzake wa ofisini, ni marafiki zake wa chuo, ni majirani zake hapo mtaani. Lakini wapendwa, au watumishi wa Mungu waaminifu, ni jumapili tu kukutana nao kanisani, hata anapotafutwa, kukumbushwa wajibu wake kiroho, anawakwepa. Na wakati huo huo anatumainia awe moto kiroho. Hapo ni kujidanganya.
Tunahitaji kupashana moto, kamwe huwezi simama kipeke yako, haijalishi wewe ni nani, au unamjua Mungu kwa ukubwa kiasi gani. Tembea na waombaji ili uwe mwombaji, tembea na washuhudiaji ili uweze kushuhudia, kaa na waalimu ili uwe mwalimu. Nje ya hapo utageuzwa na ulimwengu,.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako.
NGUVU YA HEKIMA NA AKILI
IVUMBUE INJILI YA KRISTO KUTOKA KATIKA KILA JAMBO.
Rudi Nyumbani
SWALI: Nini maana ya hii Mithali 10:25
Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena; Bali mwenye haki ni msingi wa milele.
JIBU: Mstari huo unajifafanua vizuri kwenye ule mfano Bwana Yesu aliutoa kuhusiana na watu wanaoyasikia maneno yake, halafu hawayatendi. Tusome.
Mathayo 7:24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa.
Hivyo tukirejea katika vifungu vile vya kwenye mithali. Unaweza kuelewa mtu asiye haki hasaa ni nani?
Ni Yule ambaye anaisikia injili, halafu hatii. Mtu Yule anayesema ameokoka, lakini zao la wokovu halionekana ndani yake. Rohoni anaonekana hana tofauti na yule ambaye hajamjua Mungu kabisa. Wote hao huitwa wasio haki. Bado wapo dhambini, hawajakombolewa na damu ya Yesu Kristo.
Hawa wataonekana kwa nje kama vile ni watakatifu. Lakini kinapokuja tu kisulisuli aidha cha majaribu, shida, dhiki, udhia,au mapigo kwa ajili ya Kristo, mara ghafla wanarudi nyuma, wanakuwa kama watu ambao hawajawahi kumjua Mungu kabisa, kwasababu hakujikita katika mwamba. Wengine sio majaribu ya shida, bali yale ya mafanikio makubwa, ndio hapo anasa zinawazidi wanamsahau Mungu, wanaiaga imani, kwani walimfuata Yesu kwasababu ya shida tu. Wengine ndoa, elimu, vyeo wakishavipata, huwaoni tena kwa Yesu.
Lakini mtu anayeyasikia maneno ya Kristo na kuyatii, ni kinyume chake, huitwa msingi wa milele. Huyo hatikiswi na wimbi, kisulisuli au dhoruba yoyote. Kwasababu yupo juu ya mwamba.
Okoka, upokee msamaha wa dhambi, kisha ishi kufuata na toba yako, ili uhakika wa kusimama uwe nao wakati wote.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
SWALI: Nini maana ya Mithali 28:28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
JIBU: Mithali hii hulenga hasaa watawala, iwe ni serikalini, kwenye mataasisi, makanisa n.k. endapo waongozao ni waovu, basi hufanya hata watu (hususani wale wema) kujificha, Au kutoonekana kabisa.
Ndio kama ilivyokuwa katika kipindi cha mfalme Ahabu, alipoiharibu nchi yote ya Israeli kwa kuweka miungu migeni, akichochewa na mkewe Yezebeli. Wakati huo Manabii wengi wa Mungu waliuliwa, na wale waliosalia walijificha wasionekane kabisa, wakabakia tu makuhani wa baali na wenye dhambi. Kiasi kwamba Eliya akadhani ni yeye tu peke yake nabii aliyebakia Israeli. Kuonyesha ni jinsi gani wenye haki, walivyokuwa adimu wakati huo. Lakini Mungu alimwambia Eliya, nimejisazia watu elfu saba wasiopigia goti baali.
Warumi 11:3 Bwana, wamewaua manabii wako, wamezibomoa madhabahu zako, nami nimesalia peke yangu, nao wananitafuta roho yangu.
4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali.
5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.
Ni kama leo tu ulimwenguni, tunavyoona kiwango cha watenda maasi na maasi kinavyozidi kuongezeka, ndivyo inavyokuwa ngumu kukutana na watakatifu halisi, na hiyo inaweza pelekea pengine ukajidhani mpo wachache, au hakuna kabisa kama wewe.
Ukiwa katika mazingira kama haya usipumbazike, ukafanana na ulimwengu. Bali fahamu kuwa wapo, isipokuwa Mungu amewaficha tu. Siku watakapoondolewa waovu duniani ndipo utajua kuwa Mungu anao watakatifu wake, wengi.
Ndio maana ya hilo neno Bali “waangamiapo wasio haki, wenye haki huongezeka”.
Binti ambaye unatembea kwa kujisitiri barabarani, na huwenda huoni aliye kama wewe mtaa mzima, usife moyo, ni kwasababu wasio haki ni wengi. Kijana uliyeamua kuishi maisha ya mbali na uzinzi na anasa usijidhani upo peke yako, songa mbele tambua, ni Mungu amewaficha tu watu wake.
Kwasababu ni Neno la kweli kabisa wasio haki wastawipo, wenye haki hujificha, (sio kwamba wamekufa, bali wapo). Wakati utafika waovu wataondolewa, na sisi tutamiliki na kuangaza. Usiwe mfauta wimbi, nyakati hizi ni za hatari. Ni sawa na kichuguu tu, waweza kudhani hakina kumbikumbi ndani, kina huoni chochote kinachotoka humo, lakini wakati wa mvua, unastaajabia wingi wao umetoka wapi. Vivyo hivyo na wewe endelea kutembea kwa ujasiri katika wokovu wako. Unyakuo umekaribia. Tambua Bwana analo jeshi lake.
Mithali 28:28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha; Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Rudi Nyumbani
SWALI: Nini maana ya Mithali 27:15 Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi, Na mwanamke mgomvi ni sawasawa;
JIBU: Neno Kutona-tona kama lilivyotumika hapo, ni “maji yanayovuja darini”.
Hivyo anaposema Kutona-tona daima siku ya mvua nyingi. Anamaanisha kitendo cha kuvuja sana kwa dari siku ya mvua nyingi, na kitendo cha kukaa na mwanamke mgomvi ndani ni sawasawa.
Kwa namna gani?
Tunajua ukikaa kwenye nyumba ambayo dari lake halikujengwa vizuri, mvua kubwa inaponyesha maji mengi huchuruzika na kuingia ndani. Wakati umelala utashangaa maji yanakudondekea kitandani mwako, yanachuruzikia kwenye makochi, yanakwenda mpaka kwenye makapeti, jambo ambalo litakufanya usitulie hata kidogo humo ndani utakuwa tu bize, kusogoza vitu ovyo ovyo visilowe, na mbaya ni pale mvua inapokuwa kubwa, na maji kuongezeka ndani, mwisho huwa ni kutoka kabisa nje na kuiacha nyumba.
Ikiwa umeshawahi kupitia changamoto kama hiyo ya kuvujiwa nyumba, unaelewa ni kero kiasi gani.
Ndivyo anavyofananisha kutendo hicho na kuishi na mwanamke mgomvi. Ikilenga hasaa wanandoa. Kumbuka aliyeandika mithali hizi ni Sulemani, alikuwa anatambua anachokisema, kwasababu aliishi na wanawake elfu moja(1000) kama wake zake, na alijua masumbufu yao. Alikutana na changamoto za baadhi yao.
Mwanamke mgomvi, kibiblia ni Yule asimheshimu mumewe, ni Yule anayemwendesha mumewe, anayemkaripia, asiyekuwa msikivu, kila jambo analolifanya mumewe ni kulikosoa tu, mwenye kiburi na mwenye maneno mengi, asiye na staha.
Wanawake wa namna hii, huwataabisha waume zao sana, na hatimaye wengine huwafanya wahame kabisa nyumba, kukaa mbali na familia zao. Ni dari linalovuja utawezaje kukaa kwenye nyumba hiyo?
Andiko hilo limerudiwa pia katika;
Mithali 19:13 Mwana mpumbavu ni msiba kwa babaye; Na ugomvi wa mke kama kutona-tona daima.
Uonapo familia zenye migogoro ya namna hii ni kuziombea sana Bwana aziponye.
Maandiko hayo yamewekwa sio kuonyesha mabaya kwa jinsia ya kike, hapana, bali imetoa tahadhari ili yasitokee kwa wanawake wa kikristo.
Biblia imetoa mwenendo wa mwanamke halisi wa kikristo, inasema awe ni wa kumtii mume wake. Awe ni mwenye kiasi, na MPOLE, na adabu. Akifanya hivyo atasimama vema kwenye nyumba yake, badala ya kuiharibu kinyume chake ataijenga.
1Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
Soma pia.
1Petro 3:1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;
2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, ROHO YA UPOLE NA UTULIVU, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.
Hivyo wewe kama mwanamke ukitembea katika hayo, utakuwa katika upande salama wa Mungu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>
https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Wokovu wa milele/ Ulinzi wa daima (eternal security) Je! ni neno la kimaandiko?
Rudi Nyumbani
May the name of the Lord and the Great Savior JESUS CHRIST be praised, let us learn the Bible, the living Word of our God, which is the lamp and the light of our way to heaven (Ps. 119:105).
One of the biggest and oldest sermons of the devil is to preach to people that “GOD DOESN’T FORGIVE AND HATES PEOPLE”.
This doctrine is a great weapon to make a person not try to seek God, or even if he had already started the steps to seek God’s face, then he should give up on the way. He knows that if a person knows that he can be forgiven by God, then he will not find him again, and he wants people to continue in sin so that they will eventually miss eternal life as he did.
Now one of the main characteristics of GOD who created heaven and earth is FORGIVENESS. It means “he gives forgiveness even to a person who does not deserve to be forgiven”.. And this is the first attribute that makes him (GOD) scary!.. and not only the miraculous deeds he did in Egypt, or that he continues to do even now, which we basically think that that’s what makes God scary.
The Great and the first miracle that makes God fear, is FORGIVING SINS, and COMPLETELY REMOVING THEM FROM A PERSON.
Psalm 130:3 “Lord, if You counted the evils, O Lord, who would stand?
4 But for you there is forgiveness, SO THAT YOU SHOULD BE FEARED”.
What? Do you feel that you are a sinner, and you feel that your sin cannot be erased??…know that GOD has forgiveness, and not only forgiveness but also remission of sin, so much so that after being forgiven, God removes the foundation of that sin, so much so that sometimes there will be no power over you.
Do you feel that the murder you committed cannot be forgiven?, do you feel the thoughts you thought or are thinking are unforgivable?, do you feel the act you did and repeated many times is unforgivable?..if those thoughts are in you then know that it is the enemy who is telling you that.
Everything you have done is forgivable if you want the Lord to forgive you! All you have to do is repent by meaning to stop what you are doing, if you truly repent by meaning, then with FAITH believe that God will forgive you, you don’t need an angel to tell you that you are forgiven, just believe, because that’s what the Bible teaches us that “let’s go by faith and not by to see” (2 Corinthians 5:7).
And once you believe in that way, then God will forgive you the mistake or the mistakes you made, even if you made them repeatedly 100 times, he will already forgive you all your debt. But remember forgiveness is not forgiveness!.. Someone can forgive you for the insult you insulted, but if the spirit of insulting has not left you then you can repeat the same insults tomorrow and the day after tomorrow.
Therefore, so that the mistake does not repeat itself again in your life, it needs to be removed from its roots in you. Now the principle of removing the root of sin is what the devil has blinded people to.
But thanks be to God because it is clear in the scriptures.
let’s read
Acts 2:37 “When they heard this, their hearts burned, and they said to Peter and the other apostles, What should we do, our brothers?
38 Peter said to them, REPENT AND BE BAPTIZED EACH OF YOU IN THE NAME OF JESUS CHRIST, GET FORGIVENESS OF YOUR SINS, and you will receive the gift of the Holy Spirit”.
Here Peter shows these congregations, the principle of REMOVING the ROOT of sin in them, after they REPENT of sin, that THEY BE BAPTIZED IN THE NAME OF JESUS CHRIST. As a symbol of taking off the old personality and putting on a new personality, and with that water symbol, then the root of sin will leave them, the sins of repeating themselves will stop, so the man of God remains free from sin.
And again our God with his love adds to us the gift of the Holy Spirit, in us as the Seal of God for what we have repented of.
Are you still holding on to your sins? Why don’t you confess today by repenting and being baptized? And remember that the correct confession is that of repentance by meaning, and the correct baptism is that of a lot of water and in the name of the LORD JESUS CHRIST.
May the Lord bless you.
If you need help in leading the prayer of Repentance, or baptism then you can contact us and we will help you in that.
Maran atha!
Please share this message with others;: +255789001312 au +255693036618
Sisi tuliookolewa pamoja na Bwana wetu Yesu Kristo, tunafananishwa na mti mmoja alioupanda Mungu mwenyewe ulimwengu. Na wote tunayo sehemu katika mti huo, na tumewekewa wajibu wa kufanya.
Bwana wetu Yesu Kristo anafananishwa na shina la mti, halafu sisi tunafananishwa na matawi.
Shina ni kuanzia kwenye mizizi, hadi mahali matawi yanapotokea. Hivyo Bwana wetu Yesu, ndiye anayechukua uhai wetu moja kwa kutoka kwa Mungu na kutuletea sisi. Lakini sisi ni kuanzia kwenye matawi mpaka kwenye matunda.
Yohana 15:1-2,5
[1]Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima.
[2]Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa….
[5]Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Sasa wengi wetu tunachoona katika mashina ni matunda tu peke yake. lakini leo ni vema tuone jambo hili kwa ndani. Kwa kawaida tawi huundwa na vitu viwili, cha kwanza ni majani, na cha pili ni matunda.
na vyote viwili vinapaswa vionekane katika shina.
Hivyo mimi na wewe kama watakatifu, ni lazima tujiulize je majani yapo? na je matunda yake pia yapo?
Matunda ni nini?
Tafsiri ya awali ya matunda kama ilivyozungumziwa kwenye mfano ya mti, sio kuwavua watu kwa Kristo, kama inavyodhaniwa, hapana bali ni Kutoa tunda la wokovu wako. Yaani tunda la toba.
Yohana mbatizaji kwa uvuvio wa Roho alilifafanua vema..Tusome.
Mathayo 3:7-10
[7]Hata alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?
[8]Basi zaeni matunda yapasayo toba;
[9]wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto.
[10]Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.
Aliwaona mafarisayo ambao walikiri kwa ujasiri wao ni wajumbe wa Yehova, uzao wa Ibrahimu, lakini mioyoni mwao, maovu na machafu ya kila namna yamewajaa. Hivyo wakaonekana ni miti isiyo na matunda.
Matunda ndio yale yanayojulikana kama tunda la Roho, ambayo kila mwamini anapaswa afanye bidii kuyatoa moyoni mwake katika maisha yake yote ya wokovu, awapo hapa duniani. Ambayo ni;
Wagalatia 5:22
[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu
[23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Mtu yeyote anayefanya bidii kuonyesha wokovu wake kimatendo, mtu huyo humzalia Mungu matunda, ambayo ndio chakula cha Roho wa Mungu. Na hivyo hufurahishwa sana na sisi..
Lakini kama tulivyosema shina huundwa na majani pamoja na matunda. Sasa majani, ni utumishi ambao kila mmoja wetu amepewa wa kuwavuta wengine kwa Kristo, kwa karama aliyopewa ndani yake.
Tuliagizwa na Bwana tuenende ulimwenguni kote, tukahubiri injili na kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi wake (Mathayo 28:19),
Unapowashuhudia wengine, ni kwamba majani yako yanawaponya mataifa, na hivyo unawaokoa. Kumbuka majani kimsingi hayana ladha, mara nyingi hutumika kama tiba. Ndicho Bwana anachokifanya kwa wenye dhambi kupitia sisi, tunapowashuhudia.
Ufunuo wa Yohana 22:1-2
[1]Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,
[2]katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na MAJANI YA MTI HUO NI YA KUWAPONYA MATAIFA.
Umeona? Kumbe majani yake, ni lengo la kuwaponya mataifa, watu wasiomjua Mungu. Tujiulize je na sisi tunayaponya mataifa kwa kuhubiri injili?
Wewe kama mkristo uliyemshirika wa mti wa uzima huna budi kuwa mhubiri wa injili usikae tu, hivi hivi ukasema tayari nimeokolewa inatosha, fanya jambo kwa Bwana. Waeleze wengine habari za Yesu, waponywe. Usijidharau ukasema siwezi, kumbuka aitendaye kazi hiyo ni Kristo ndani yako, wewe ni tawi tu. washuhudie wengine.
Lakini si kuhubiri tu, halafu maisha yako yapo kinyume na Kristo, hapana hilo nalo ni hatari, ukiwa na majani tu, halafu huna matunda ya wokovu moyoni mwako..Utalaaniwa.
Marko 11:13
[13]Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; maana si wakati wa tini.
[14]Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia.
Umeona hawa ni watu, wanaodhani kumtumikia Mungu tu yatosha hakuna haja ya kuishi maisha matakatifu. wanakutwa na majani tu peke yake.
Tuhakikishe tuna majani, lakini vilevile tuna matunda kwasababu sisi ni shina, ndani ya mti wa uzima. Na neema ya Mungu itatusaidia.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Tafsiri ya Mithali 27:18 Yeye autunzaye mtini atakula matunda yake;
KWANINI MTINI KATIKATI YA MIZABIBU?
UMEIZALIA MATUNDA MIAKA 4 YA NEEMA ULIYOPEWA?
Rudi Nyumbani
Swali: Je kazi ya udalali ni dhambi, na Mkristo anaruhusiwa kuifanya?
Jibu: Dalali ni yule mtu anayeuza kitu kwa niaba ya mwingine na kisha kuchukia asilimia fulani ya faida ya kile kilichouzwa.
Au pia dalali anaweza kuwa mtu mwenye kutafuta soko la bidhaa ya mtu mwingine na kisha kuchukua asilimia ya faida inayopatikana.
Kama hiyo ndio maana au tafsiri ya udalali, basi mtu akiifanya “SI DHAMBI”, Kwani hata ununuaji wa bidhaa kiwandani na uuzaji masokoni kwa namna moja au nyingine ni “Udalali”, kwani utanunua kwa gharama ndogo na kuuza kwa gharama kubwa na kisha kuichukua ile faida….Hapo tayari umeshakuwa dalali wa wenye kuitengeneza ile bidhaa..
Kwahiyo udalali si dhambi ikiwa tu haujahusisha mambo yafuatayo.
1. UONGO.
Labda umepewa kazi ya kutafuta mteja wa bidhaa husika, halafu ukampata na kumwekea kiwango cha juu sana nje na mapatano na yule aliyekupa bidhaa (lengo la kufanya hivyo ni ili wewe upate faida kubwa na ya haraka)…
Au mteja amehitaji bidhaa au nyumba na wewe ukamlaghai kwa uongo na kumpa kitu ambacho kiko chini ya viwango na huku ukijua kabisa kuwa kitu hiko hakistahili hiyo gharama, Huo wote ni Uongo na udalali huo ni haramu.
2.Dhuluma.(Utapeli).
Unapomdhulumu mtu fedha au bidhaa yake, aidha kwa kumlipa kisasi au kwasababu nyigine yoyote udalali huo ni haramu.
3. Haifanyiki ndani ya nyumba ya Mungu..
Udalali unaofanyika ndani ya Nyumba ya MUNGU ni haramu..
Utaona Bwana YESU aliwafukuza wale madalali wote waliokuwa wanabadili fedha ndani ya nyumba ya MUNGU.
Yohana 2:15 “Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;”
Vivyo hivyo kanisani si sehemu ya minada, na udalali, ni sehemu ya Ibada takatifu ya roho na kweli.
Swali lingine je?…Fedha ya udalali inaweza kutolewa sadaka ikiwemo Zaka?.
Jibu ni Ndio!.. kama udalali huo haujahusisha mambo hayo hapo juu, basi inaweza kutolewa sadaka ikiwemo Zaka(yaani fungu la Kumi), na ikakubalika mbele za Mungu.
Na je mkristo anaweza kufanya kazi ya udalali??..
Jibu ni Ndio! Anaweza kufanya, ikiwa hatatumia Uongo, au dhuluma, au rushwa, au kufanya ndani ya kanisa la Mungu.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
KAMA MHUBIRI USIWE MFANO WA DIOTREFE.
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE
Nakusalimu katika jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo, Tukijua kuwa ule mwisho unakaribia, hatuna budi siku baada ya siku tujichunguze je! Tumekamilika vema? ili siku ile tusionekane na mawaa mbele zake. Tulipokee taji timilifu tuliloandaliwa mbinguni na mwokozi wetu Yesu Kristo kwa neema zake.
Leo, napenda tufahamu juu ya wimbo mpya. Kama wewe ni msomaji mzuri wa kitabu cha Ufunuo. Utagundua zimetajwa nyimbo kuu tatu.
Swali ni je! Hizi nyimbo ni zipi na zinatimiaje?
Wimbo wa Musa na wa mwanakondoo tunazisoma, katika Ufunuo 15:2-3
Ufunuo 15:2 Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.
3 Nao WAUIMBA WIMBO WA MUSA, MTUMWA WA MUNGU, NA WIMBO WA MWANA-KONDOO, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa
Wimbo wa Musa, ni injili ya Musa, ambayo iliwafanya watu wa kale, kutembea katika hiyo ili wamkaribie Mungu, ndiyo ile torati, ambayo wale waliokuwa katika agano la Ibrahimu kwa uzao, walirithi neema hiyo. Hivyo wana wa Israeli wote walikuwa wanauimba wimbo wa Musa. Yoyote ambaye hakuwa hana wimbo huo, basi wokovu au kumkaribia Mungu hakukuwezekana kwake.
Lakini wimbo wa Musa haukuwa na ukamilifu wote kwasababu ulikuwa ni wa mwilini, na wa kutarajia ahadi ya mwokozi mbeleni. Hivyo Mungu akaleta wimbo mwingine mpya kwa wanadamu wote. Ndio huo wimbo wa mwana-kondoo.
Ambayo ni injili ya neema iliyoletwa na Bwana wetu Yesu Kristo na kuhubiriwa na mitume wake. Kwa ufupi sisi wote tuliomwamini Yesu Kristo katika agano hili jipya, kwa pamoja tunauimba wimbo wa mwana-kondoo. Ndio maana kiini cha imani, na wokovu wetu ni Yesu Kristo. Mtu yeyote ambaye hajaoshwa dhambi zake kwa damu ya Yesu, hawezi kumwona Mungu, wala kamwe hataweza kumwelewa, haijalishi ataonyesha bidii zake nyingi kiasi gani. Kwasababu ndio utimilifu wote.
Lakini upo wimbo mwingine wa Tatu ndio huo wimbo mpya.
Wimbo huu, si wote watakaoweza kuuimba, lakini watakaoweza kuuimba watakuwa karibu sana na mwana-kondoo (Yesu Kristo), baada ya maisha haya. Ndio wale washindao, Ndio wale Yesu aliosema atawakiri mbele ya Baba na malaika zake, ndio wale watakaoketi pamoja naye katika viti vya enzi, ndio wale watakaotoka mashariki, magharibi, kaskazini na kusini, kula mkate naye mezani pake. Na vigezo amevianisha pale. Anasema..
Ufunuo 14:1 Kisha nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.
2 Nami nikasikia sauti kutoka mbinguni, kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi kuu. Na hiyo sauti niliyoisikia ilikuwa kama sauti ya wapiga vinubi, wakivipiga vinubi vyao;
3 na KUIMBA WIMBO MPYA mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele ya wale wenye uhai wanne, na wale wazee; WALA HAPANA MTU ALIYEWEZA KUJIFUNZA WIMBO ULE, ila wale mia na arobaini na nne elfu, WALIONUNULIWA KATIKA NCHI.
4 HAWA NDIO WASIOTIWA UNAJISI PAMOJA NA WANAWAKE, KWA MAANA NI BIKIRA. Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako. Hawa wamenunuliwa katika wanadamu, malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.
5 NA KATIKA VINYWA VYAO HAUKUONEKANA UONGO. MAANA HAWANA MAWAA
Kama tunavyoweza kuona hapo tabia za wale walioweza kuuimba wimbo huo ni mbili;
Hapo hamaanishi kuwa hawakuwa wazinzi, hapana, (ni kweli uzinzi sio jambo lao) bali anamaanisha hasaa uzinzi wa rohoni, yaani Kumwabudu Mungu pamoja na sanamu. Na sanamu kwa wakati wetu si tu vile vinyago vya kuchonga tu, bali pia ni kitu chochote kinachochukua nafasi ya Mungu wako moyoni. Wengine mali, wengine tv, wengine mipira, wengine elimu, wengine ma-magemu, wengine ushirikina, wengine udhehebu. Hizo ni sanamu, unapozidhibiti wewe kama mkristo hiyo ni hatua mojawapo ya kuweza kuuimba wimbo huo mpya.
Lakini anasema..
Ni watu walionena kweli yote ya Mungu (injili ya Kristo), wala hawakuibatilisha kwa ajili ya fedha, au maslahi, au cheo, au unafki au wafuasi. Bali waliitetea kweli yote ya Mungu na kuiishi pia, . Maana yake mimi na wewe tukiinena kweli ya Kristo na kuiishi, basi vinywani mwetu tunakuwa hatuna uongo.
Na matokeo ya mtu wa jinsi hii, ni kwamba anakuwa nafasi maalumu sana mbinguni(Ufunuo 5:8-9), Ni sawa na leo unajisikiaje unapoitwa uishi ikulu na raisi wako? Unajisikiaje kila mahali aendapo na msafara wake wewe upo pamoja naye. Anapopokea heshimu, na wewe unapokea naye.
Hivyo bidii ina malipo. Nyakati tulizonazo sio kusema nimeokoka hiyo inatosha!.. Ni nyakati za kujifunza wimbo huu mpya kwa bidii. Kutijahidi kumpendeza Bwana. Na yeye mwenyewe ameahidi neema yake itatusaidia.
Bwana akubariki.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Kwa mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.
Mafundisho mengine:
Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule(Kutoka 12:4)
Rudi Nyumbani