Category Archive maswali na majibu

Unyenyekevu ni nini?

Unyenyekevu ni nini, kibiblia, ili mtu awe ni mnyenyekevu anapaswa aweje?


Tafsiri ya Unyenyekevu ni Kujishusha. Pale unapokuwa na uwezo wa kutumia   nguvu, au sauti, au mamlaka,kuhimiza jambo, lakini unajishusha chini, kana kwamba wewe si kitu, huo ndio unaitwa unyenyekevu.

Unyenyekevu sio kushushwa, bali kujishusha. Na kinyume cha Unyenyekevu ni kiburi, yaani kujipandisha juu, kujiona wewe unaweza yote, wewe ni bora kuliko vyote, wewe una nguvu kuliko wote, wewe una sauti zaidi ya wote.

Unyenyekevu ni mgumu sana kuufikia, kwasababu asili ya mwanadamu ni kutaka kujipandisha juu. Lakini ukiupata unyenyekevu basi umepata mpenyo mkubwa sana wa kumfikia Mungu.

Kiwango cha unyenyekevu kinatofautiana, kwa jinsi mtu unavyoterekema ngazi moja chini, ndivyo kiwango chake cha unyenyekevu kinavyokuja juu, na pale anapoongeza ngazi nyingine na nyingine ndivyo unyenyekevu wake unavyofikia kilele cha juu sana.

Ni kwanini tuwe wanyenyekevu?

  1. Ni kwasababu Kristo naye alikuwa mnyenyekevu;

Wafilipi 2:6 “ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho;

7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;

8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba”.

2) Kwasababu Mungu anawapinga wenye kiburi

Yakobo 4:6 “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu”.

Mungu ni adui mkubwa kwa kiburi, hivyo tukilijua hilo ni kujitahidi sana tuwe mbali na kitu hicho.

Faida za kuwa wanyenyekevu ni zipi?

  1. Mungu anakuwa karibu nasi:

Mungu alikuwa karibu na Bwana Yesu, kuliko mtu mwingine yeyote, na hiyo yote ni kwasababu ya unyenyekevu wake:

Mathayo 11:28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

     2) Mungu anatukweza juu;

Utaona baada ya Bwana Yesu kujishusha, Mungu alimkweza juu Zaidi ya vitu vyote ulimwenguni.

Wafilipi 2:8 “tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;

11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba”.

Tunakuwaje wanyenyekevu?

  1. Kumuhesabu mwenzako ni bora kuliko nafsi yako mwenyewe.

Wafilipi 2:3 “Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake”.

     2) Kuuzuia ulimi:

Kuwa wa mwisho kunena, na kuzuia hasira zako, usiotoe maneno ya majigambo;

Yakobo 3:5 “Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum”.

  3) Kutojihesabia haki, mbele za Mungu:

Luka 18:9 “Akawaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote.

10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.

11 Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.

12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote.

13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi”.

14 Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

     4) Kukubali kujishughulisha na mambo manyonge

Warumi 12:16 “Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili”.

Si lazima, kila jambo la juu tung’ang’anie kulifanya. Bwana Yesu alikuwa ni Mungu, lakini akaona kule kuwa sawa naye sio kitu cha kushikamana nacho. Akawa kama mtumwa..Vivyo hivyo na sisi tupende utumwa kuliko ukubwa.

Mwisho kabisa tukumbuke kuwa Unyenyekevu kibiblia, upo kwa namna mbili; Unyenyekevu wa sisi kwa sisi, na unyenyekevu kwa Mungu. Vyote viwili vinakamilisha Unyenyekevu wa ki-Mungu. Kama vile ulivyo upendo. Ili tukamilike katika huo ni sharti, tupendane sisi kwa sisi, na vilevile tumpende Mungu.

Ndio maana Bwana Yesu aliwatawaza miguu watakatifu wake, akatupa na sisi kielelezo kuwa tunyenyekeane sisi kwa sisi, kama yeye alivyofanya.

Hivyo tuizingatie sana nguzo hii muhimu katika ukristo wetu. Ili tumfurahie Mungu wetu.

Bwana akubariki.

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.

Mada Nyinginezo:

Upole ni nini?

Furaha ni nini?

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

TUMAINI NI NINI?

Jehanamu ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post

Nini maana ya “wanawake saba watamshika mtu mume mmoja”

SWALI: Isaya 4:1 na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe lakini tuitwe  tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetun. Je; andiko hili linamaanisha nini?


Kwanini wanawake? Kwanini wawe saba? Kwanini chakula chao na nguo zao na sio za mume wao? maanake mume akioa moja ya majukumu ya kwake kufanya kwa mkewe ni kumlisha na kumvika sasa hawa wanakula na kuvaa vya kwao ni kitu gani hawa wanawake?

JIBU: ufunuo wa mstari huo ni huu..wanawake saba ni makanisa saba (katika vipindi saba vya kanisa kama inavyooneka katika ufunuo 2 & 3)..

Mtu mume mmoja ni Yesu Kristo,.Lakini hao wanawake wote 7 wanasema watakula chakula chao wenyewe na kuvaa nguo zao wenyewe bali waitwe tu kwa jina la yule mtu mume mmoja ambaye ni Yesu Kristo.Jambo hili la kusema tutakula chakula chetu na kuvaa nguo zetu wenyewe ni tabia za hayo makanisa yote 7 yalivyokuwa, kila kanisa lilikuwa na tabia yake pekee, na yote yanatafuta kumpendeza Yesu Kristo lakini kwa njia zao wenyewe,

kwahiyo hicho “chakula” kinachozungumziwa hapo ni mapenzi yao wenyewe, na mienendo yao wenyewe hawataki chakula cha Bwana wao,(ambalo ni neno la Kristo lisiloghoshiwa), wala hawataki “mavazi” ya Bwana wao (Ambao ni utakatifu na matendo mema soma ufunuo 19:8,) bali waitwe tu kwa Jina la Bwana Yesu aibu yao iwaondoke hii aibu ina maana waiepuke hukumu itakayokuja na ndio maana yale makanisa yote hayakuweza kuoana na Kristo kikamilifu yalikuwa na mapungufu yake, na sisi pia tupo katika kanisa la mwisho la saba la LAODIKIA ni kanisa vuguvugu,na ndilo lililomkinai Bwana wake kuliko mengine yote yaliyotangulia soma..

ufunuo 3:14-22,”14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.

15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto.

16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.

17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi.

18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.

19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.

20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”

Lakini tunapaswa wote tushinde ili tuvuke kutoka kuwa masuria na kuwa bibi-arusi safi wa Yesu Kristo waliokubaliwa tayari kwenda kwenye arusi ya mwanakondoo itakayofanyika mbinguni kwa Baba.Kumbuka bibi-arusi sio sawa na suria.Kwahiyo ndugu watakaoshiri karamu ya mwanakondoo ni bibi-arusi tu, je! wewe ni bibiarusi? umepokea Roho Mtakatifu? umejiweka tayari kumpokea Bwana wako atakaporudi? matendo yako yanastahili wokovu? jibu lipo moyoni mwako. Tubu sasa umgeukie Bwana kumbuka tunaishi kizazi ambacho kitashuhudia kuja kwa pili kwa Kristo.

ufunuo 19: Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.

Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.


Mada Nyinginezo:

KWANINI UNAPASWA UWE BIBI ARUSI NYAKATI HIZI ZA MAJERUHI?

NAMNA YA KUMTAMBUA BIBI ARUSI WA KWELI WA KRISTO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Utii ni nini? na ni nani tunayepaswa kumtii au kutokumtii?

Utii ni nini kibiblia?


Utii ni kitendo cha kukubali kufanya maelekezo au maagizo unayopewa na aliye na mamlaka ya juu Zaidi yako wewe bila kujali  linakubaliana na maamuzi yako au la!.

Lakini pamoja na hayo watu wengi hawajui kuwa utii unaweza pia kutanguliwa na isihesabiwe kuwa ni dhambi ya kutokutii mbele za Mungu, Lakini hiyo ni katika mazingira maalumu ambayo tutajifunza mbele kidogo katika somo letu hili.

Ili kujua ni wakati gani tunapaswa tusitii Ni vizuri kwanza tukawajua watu ambao biblia imetuagiza tuwatii wakati wote:

1 Utii kwa wazazi wetu:

Wakolosai 3:20  “Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana”

Hili ni agizo la Mungu kwa kila mwenye baba, au mama au mlezi, Mungu ametuagiza tuwatii wazazi wetu, kwa kila wanachotuelekeza kufanya. Na zipo baraka nyingi  katika kufanya hivyo  ikiwemo kupewa upendeleo wa kuishi umri mrefu hapa duniani

Kutoka 20:12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

https://www.high-endrolex.com/12

Hata Bwana wetu Yesu Kristo alikuwa na utii huu ukisoma Luka 2:51 inasema .. “Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.

Vivyo hivyo na sisi tunapaswa tuwe na huu utii kwa faida zetu wenyewe. Na pia kuyatimiza maagizo ya Mungu.

2 Utii kwa Mume:

Wake wamepewa maagizo ya kuwatii waume zao kwa kila namna.

1Petro 3:1 ” Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; ……5  Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 6  Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote”

Soma pia Wakolosai 3:18 utaliona jambo hilo hilo.. Ikiwa wewe ni mke, halafu huisikii sauti ya mume wako labda kwasababu anakipato cha chini au anamapungufu fulani, au ni mwenye dhambi usidhani kuwa Mungu yupo upande wako. Unapaswa umtii na ujishushe kwasababu hayo ndiyo maagizo ya Mungu.

#3 Utii kwa wazee:

1Petro 5:5  “Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu,..”

Mungu ametupa maagizo kama vijana, kuwathamini wazee, katika kanisa na vilevile katika jamii. Wanapotoa Mashauri hatupaswi kuwapinga au kujibishana nao,..Tukifanya hivyo tusidhani kuwa Mungu yupo upande wetu. Tunapaswa tuwape heshima kama vile wazazi wetu wenyewe ndivyo Mungu atakavyotufanikisha.

1Timotheo 5:17  Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha

1Timotheo 5.1  Mzee usimkemee, bali umwonye kama baba; na vijana kama ndugu;

#4 Utii kwa viongozi wetu wa Imani:

Bwana anatuagiza, tuwatii wale wanaotungoza katika njia ya wokovu. Na ndio maana Paulo alimwandikia Filemoni maneno haya:

Filemoni 1:21  “Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo”

Lakini tukipashana nao kauli au kuwavunjia heshima, au kutowasikiliza, basi tujue kuwa tunampinga Mungu, na Hivyo Mungu hawezi kuwa upande wetu hata katika huduma zetu.

#5 Utii kwa mabwana zetu (ma-boss):

Waefeso 6:5  “Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;

6  wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;

7  kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;

8  mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.”

Ikiwa utamvunjia heshima boss wako, ukafukuzwa kazi, usidhani kuwa Mungu atakuwa na wewe hata katika hiyo kazi nyingine mpya utakayokwenda kuitafuta. Haijalishi wewe ni mkristo au la..Maadamu umewekwa chini ya boss wako, basi huna budi kutii yale yote anayokuagiza kufanya bila unafiki..

#6 Utii kwa wenye mamlaka (Serikali):

Tito 3:1  “Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; 2  wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.

Serikali na mamlaka zote zinafanya kazi ya Mungu, hivyo pale inapotuagiza tulipe kodi tunapaswa kufanya hivyo, inavyotuagiza tusifanye hiki au kile tunapaswa tutii..Lakini kama tutakwenda kinyume na serikali, kwa kiburi chetu wenyewe basi tujue kuwa Mungu hapo nasi hawezi kuwa na sisi.

#7 Utii kwa Mungu:

Huu ndio utii ulio wa juu Zaidi kuliko wote.. Biblia inatuambia katika Yakobo 4:7  “Basi mtiini Mungu…”.. Utii huu tunaweza kuuona  ukijidhihirishwa katika ukamilifu wote kwa Bwana wetu Yesu Kristo.

Wafilipi 2:7  “bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8  tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa MTII hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9  Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10  ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11  na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

Inatuambia tena…

Waebrania 5:7  Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;

8  na, INGAWA NI MWANA, ALIJIFUNZA KUTII kwa mateso hayo yaliyompata;

9  naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;

Vivyo hivyo na sisi kila mmoja Maisha yetu yanapaswa yawe ya utii, tukilitii Neno la Mungu, kila tunapoagizwa tulifanye.

Lakini sasa Je! ninapaswa kuwatii wote hawa hata kama mmojawao anachoniambia kinakinzana na maagizo ya Mungu?

Biblia imeweka wazi kabisa katika hali kama hiyo tunapaswa tusitii maagizo ya mtu yeyote bali ya Mungu kwanza..Ukisoma katika biblia utaona kuna wakati mitume walizuiliwa kuhubiri injili na wenye mamlaka na viongozi wa Dini lakini mitume walewale waliosema watiini wenye mamlaka ndio wakawa wa kwanza kusema..Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu,

Matendo 5:27  “Walipowaleta, wakawaweka katika baraza. Kuhani Mkuu akawauliza,

28  akisema, Je! Hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili? Nanyi, tazameni, mmeijaza Yerusalemu mafundisho yenu, na mnataka kuileta damu ya mtu yule juu yetu.

29  Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu”

Leo hii mama au baba yako anaweza kukwambia ufanye mila za matambiko, Na huku wewe unajua kabisa jambo hilo linakinzana na maandiko, hapo hupaswi kumtii mzazi wako hata kama itaonekana amewavunjia heshima kiasi gani…

Wazazi

Au wazazi wanakushurutisha unywe pombe, au ufanye dhambi, hapo unaruhusiwa kutowatii kwasababu utii huo hautokani na Mungu na hivyo mbele za Mungu hutahesabika kuwa hajawatii wazazi wako.. Maandiko yanathibitisha hilo (Mathayo 10:37)

Serikali

Vilevile, Serikali imekupiga marufuku usiabudu. Au usihubiri injili, Hapo unapaswa usiitii serikali hata kama ni Mungu ndiye aliyeruhusu tutii mamlaka hizo. Ilimtokea Danieli, lakini yeye alihesabu mamlaka na Mungu ni kubwa kuliko mamlaka zote, hivyo alichofanya ni kufungua madirisha kabisa watu wote wamwone akiabudu, bila woga wowote, Na sisi vivyo hivyo hatupaswai kuogopa kuyashika maagizo ya Mungu Zaidi ya wanadamu.

Mume.

Au Mume, anakushurutisha mfanye tendo la ndoa kinyume cha maumbile, hapo hupaswi kumtii, mume wako, kwasababu maagizo hayo yanakinzana na Neno la Mungu..Hata kama akikutisha kukuacha, mwache aende, utiifu wa Mungu ni Zaidi ya utiifu mwingine wowote.

Au boss wako anakulazimisha uingie katika mikataba ya rushwa, Na huku unajijua kabisa kuwa unachofanya kinakinzana na Imani yako, hapo hupaswa kumkubalia, au anakulazimisha ufanya naye uzinzi, hapo pia hupaswa kumkubalia haijalishi ni boss wako anayeheshimika kiasi gani. Au maandiko yamekuagiza uwatii hao kiasi gani.

Hivyo UTIIFU wowote ni lazima upatane na maagizo ya Mungu, kama haukinzani na Neno la Mungu hapo unapaswa utii yote unayoelekezwa kwa moyo wote bila kiburi..Na ndivyo Mungu atakavyokufanikisha..

Kwasababu kinyume na hapo, ukosefu wa utiifu wowote, ni kazi ya shetani ambayo siku hizi za mwisho ndio umekita mizizi..

2 Timotheo 3:1  Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.2  Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, WASIOTII WAZAZI WAO, wasio na shukrani, wasio safi.

Je! Umeokoka?

Je ndani yako kiburi kimekaa? Je unajua kuwa watu wa namna hiyo hawataurithi uzima wa milele? Je Unafahamu kuwa tunaishi katika kanisa la mwisho lijulikanalo kama Laodikia, na hatutakuwa na kanisa lingine Zaidi ya hili, Na unyakuo ni wakati wowote kwasababu dalili zote zimeshatimia?.. Kwanini usimpe leo Kristo Maisha yako.? Kwanini usiwe na uhakika wa kwenda mbinguni hata ukifa leo?

Kama upo tayari kufanya hivyo sasahivi.. basi uamuzi unaoufanya ni wa busara sana ambao hautakaa uujutie maisha yako yote kama ilivyokuwa hata kwetu sisi. Unachopaswa kufanya, hapo ulipo, chukua muda mchache ujitenge peke yako. Kisha piga magoti, kisha fuatisha sala hii kwa Imani, ukijua kuwa Mungu yupo hapo karibu na wewe pembeni yako kukusikia..Kisha ukiwa sasa katika utulivu Sema sala hii kwa sauti.

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, .
NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa ikiwa umefuatisha sala hiyo kwa Imani ..Hatua iliyobakia kwako ni kuithitisha toba yako kwa Vitendo ikiwa ulikuwa unafanya mambo yote ambayo hayampendezi Mungu, unatii sasa kwa kunayaacha na kujitenga nayo, Na Mungu akishaona umegeuka kwa vitendo basi toba yako anaipokea na atakuja ndani yako wakati huo huo na kufanya makao ya milele kwako. Vile vile unahitaji, kutafuta kanisa la kiroho ambalo utajumuika na wakristo wengine katika kumwambudu Mungu, na kujifunza biblia ili uukulie wokovu. Na vilevile ili upate ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako.

Ubarikiwe sana.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia masomo haya kwa njia ya email yako piga namba hii 0789001312

Group la whatsapp Kwa mgawanyo bora wa masomo download App hapa>> App wingu la mashahidi

Mada Nyinginezo:

MAAGIZO AMBAYO HAYAJAAGIZWA!

LISHIKILIE SANA LILE AGIZO LA KWANZA.

MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA TITO.

KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Rudi Nyumbani:

Print this post

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA).

Musa alipewa maagizo na Mungu atengeneze nyoka wa shaba, amning’inize ili wale wote waliomuasi Bwana watakapomtazama nyoka Yule wapone saa ile ile.

Hesabu 21: 8 ‘’Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.

9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi’’.

Lakini Mungu hakuwahi kuwaagiza Wana wa Israeli kuwa wakati wowote watakapokutana na madhara au matatizo basi wamsimamishe nyoka wa shaba wamtazame ili wapone, hakuwahi kufanya hivyo, lakini wana wa Israeli walitazama wakagandua SIRI ndani yake, wakasema ni lazima kutakuwa na uponyaji Fulani kwenye nyoka wa shaba kama sivyo Mungu asingemwagiza Musa kuiunda, hivyo ngoja tujijengee utaratibu wetu, wa kuifanyia ibada, na kumwomba Mungu kupitia ile naye Mungu atatusikia dua zetu..

Hivyo hilo jambo lilikuja kuendelea hivyo kwa mamia ya miaka mbeleni, mpaka likajengewa madhabahu kubwa na kuwa jambo maarufu sana Israeli, watu wakawa wanakwenda kuiinamia ile sanamu ya nyoka na kumwomba Mungu wa Israeli kupitia ile awaponye matatizo yao, wakaifukizia uvumba..

Hawakujua hilo lilikuwa ni chukizo kubwa sana kwa Mungu ndilo lililowapelekea hata kukumbana na matatizo yote yale ikiwemo kuchukuliwa utumwani tena.. Ndipo sasa baada ya miaka mingi sana kupita akatokea mfalme mmoja anayeitwa Hezekia yeye ndiye aliyefanikiwa kuliona hilo chukizo mara moja, Tusome:

2 WAFALME: 18:1 ‘’Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea, mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia, mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.

2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka ishirini na kenda katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Abiya, binti Zekaria.

3 Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya Daudi, baba yake.

4 Alipaondoa mahali pa juu, akazibomoa nguzo, akaikata hiyo Ashera; akaivunja vipande vipande ILE NYOKA YA SHABA ALIYOIFANYA MUSA; maana hata siku zile wana wa Israeli walikuwa wakiifukizia uvumba; naye akaiita jina lake NEHUSHTANI

5 Alimtumaini Bwana, Mungu wa Israeli; hata baada yake hapakuwa na mfano wake katika wafalme wote wa Yuda, wala katika hao waliomtangulia’’.

Embu jaribu kutafakari kwa utulivu uone kitu hapo! AGIZO lilikuwa ni la Mungu mwenyewe lakini sasa linageuka kuwa kitanzi na kikwazo kikubwa sana kwa watu…Tunaweza kuwalaumu wale tukasema walipungukiwa na akili lakini nataka nikuambie sisi wa kizazi hiki ndio tuliopungukiwa akili zaidi ya wale..Tutaona ni kwa namna gani tunafanya makubwa zaidi ya wao.

Mungu alimwagiza Musa achonge nyoka wa shaba kama ISHARA tu! ya kitu Fulani tu rohoni, nacho ndicho tunakuja kukiona sisi watu wa agano jipya, kuwa tendo lile Mungu aliliruhusu lifanyike vile kumfunua Bwana wetu Yesu Kristo atakapotundikwa msalabani kwamba kila mtu atakayemwamini aokolewe, hilo tunalithibitisha kwa maneno yake mwenyewe..

Yohana 3:14 ‘’Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyohivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye’’.

… lakini hakukuwa na kitu chochote cha maana ndani ya ile SHABA, uponyaji halisi haukuwa ndani ya shaba ile bali ulitoka kwa Mungu mwenyewe..matokeo yake watu wakaacha kumtazama Mungu ambaye ni mponyaji wao wakaigeukia shaba isiyoweza kusema, wala kunena, wala kuzungumza..

Leo hii tunajua ni kweli Mungu alimwagiza Elisha achukue CHUMVI na kuitia katika chemchemi ya maji iliyokuwa inazaa mapooza..Na baadaye maji yale yakawa matamu,.Lakini kumbuka sio chumvi iliyotibu maji bali ni Mungu ndiye aliyefanya vile, lakini ni kwanini leo hii tunaihusisha chumvi na mambo ya ibada ikiwa hatujaongozwa kuitumia?.Nasi tunasema vile vile kama wana wa Israeli, Mungu kaweka uponyaji wa kiungu ndani ya chumvi,..tunasema kuna nguvu fulani ndani ya chumvi kama sivyo kwanini Mungu alimwagiza Elisha aiweke katika maji?…Tunamtia Mungu wivu pasipo sisi kujijua..

Halikadhalika tunayapa MAJI heshima, na kusema maji yana nguvu ya kusafisha mtu ndani yake, na kumtakasa, Tunamweka nyuma Mungu tunayapa maji heshima, ndugu Huko ni sawa kuiabudu sanamu ya Shaba.

Vivyo hivyo na vitu vingine vyote, tunasema UDONGO unabeba uhai, kwahiyo tukiumwaga kwenye biashara zetu, utazifufua, huku tukishikilia kile Bwana Yesu alichokifanya alipotengeneza TOPE ardhini na kumpaka Yule kipofu machoni, na macho yake kufumbuka, tunasema kama udongo usingekuwa na uponyaji Fulani Yesu asingeagizwa kutengeneza tope na kumpa kipofu..na kibaya zaidi mpaka tumeshavipa majina kama VITENDEA KAZI VYA KIROHO.

Tunahusisha MISALABA katika Ibada zetu. Kama unapenda msalaba wako kwanini usiunig’inize nyumbani kwako kama kumbukumbu lako la Bwana kukufia msalabani, lakini ni kwanini unakwenda kuuinamia, kuomba kupitia huo, unadhani unampa Mungu heshima hujui kuwa ni ASHERA hilo umeiweka moyoni mwako.

Na mambo mengine mengi, tunayafanya hatujui kuwa ndivyo tunavyomtia Mungu wivu. Fumbua macho yako, utoke kwenye uchanga wa kiroho, ikiwa Mungu amekuongoza kutumia mojawapo ya vitu hivyo kama ishara ya kitu Mungu anachokifanya rohoni ni sawa, kama amekuongoza kutumia maji tumia, amekuongoza kutumia mafuta tumia, na uthibitisho wa kuwa umeongozwa na Mungu kufanya hivyo, ni kwamba hakitakuwa unakirudia rudia,….Elisha halikuwa hatumii chumvi kila tatizo linalokuja mbele yake…Wala sio kila mgonjwa aliyekuja mbele yake alikuwa anamwambia akaoge mto Yordani mara saba. Alikuwa anafanya vile pale alipokuwa anaongozwa tu! Na sisi tunapaswa tuwe hivyo hivyo.

lakini kama tunageuza Imani yetu kutoka katika nguvu ya uweza wa DAMU YA YESU inayoweza kufuta na kuondoa kila kitu na kuvipa vitu hivyo visivyo na uhai heshima Fulani ya kiroho kwamba vina nguvu Fulani au uwezo Fulani wa wa kusababisha mambo, basi tujue moja kwa moja tunamfanyia ibada shetani. Na Mungu anachukizwa nazo kupindukia kwa namna ile ile anavyochukizwa na waabudu baali na Jua.

Na madhara yake ni kwamba, Mungu atatupiga kwa kukosa kwetu maarifa, wakati mwingine badala ya tatizo kuisha ndivyo litakavyoongezeka, kwasababu biblia inasema ni heri ungekutana na ghadhabu ya Mungu kuliko WIVU wake, na ibada zote za sanamu zinaleta wivu mbele za Mungu.

Mithali 27:4 ‘Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya WIVU’.

Wimbo uliobora 8: 6“………….wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu.”

Huu ni wakati wa kutubu (yaani kugeuka), na kumwabudu yeye katika Roho na Kweli.

Jina la Bwana wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele. Amin.

 Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa  Maombezi, Ushauri au Ratiba za Ibada Wasiliana nasi kwa namba

+225693036618/ +225789001312



Mada Zinazoendana:

FIMBO YA HARUNI!

HISIA YA MUNGU ILIYO MBAYA KULIKO ZOTE.

MWISHO WA HAO WAMSAHAUO MUNGU.

FAHAMU ZA WATU HUWA ZINAONDOLEWA NA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post