Haki maana yake ni kitu ambacho mtu anastahili kukipata. Kwamfano kuishi ni haki ya Kila mwanadamu, Hakuna mtu anayepaswa kumzuia mwingine kuishi, kisa ni mwanamke au ni mfupi, au ni kichaa, au mlemavu. Maadamu tu amekuwa mwanadamu tayari anayo haki ya kuishi.
Mfano mwingine wa haki, ni mtu aliyesoma ukahitimu katika shahada Fulani labda tuseme ya utatibu, mtu kama huyo tunasema ana haki ya kuitwa daktari kwasababu amesomea jambo Hilo.
Vivyo hivyo katika Roho. Mungu naye anayo haki yake, katika kutoa vitu vyake.
Mwanzoni ilikuwa Ili kumkaribia Mungu na kupata kibali kwake na mema yote na baraka zote ilikupasa kwanza uishike Sheria yake yote. Hivyo yoyote aliyeweza kufanya hivyo alipatiwa haki hiyo. Soma Kumbukumbu 28
Lakini Kwa bahati mbaya hakukuwa na mtu aliyestahili kumkaribia Mungu kwasababu Hakuna mwanadamu aliyekwenda katika maagizo yote ya Mungu Kwa ukamilifu wote, bila kosa. Kwahiyo tangu zamani hakukuwa na mwanadamu hata mmoja aliyefanikiwa kumkaribia Mungu. Wote walitenda dhambi (Zaburi 14:3)
Hivyo Mungu akabuni mpango mwingine wa kumwokoa mwanadamu ili awe amestahili kupokea mambo yote ya rohoni ya Mungu, ikiwemo uzima wa milele na kumkaribia yeye.
Ndipo akamleta Yesu duniani, Ili Kila amwaminiye asipotee Bali apokee kuhesabiwa haki bure, bila kutegemea Tena matendo ya Sheria. Kwasababu Kwa matendo ya Sheria hakukuonekana aliyestahili.
Hivyo Mimi na wewe tunapomwamini Kristo kama ndiye Bwana na mwokozi pekee wa maisha yetu na kuukubali msamaha wake wa dhambi, basi tunahesabiwa tumestahili kuitwa watakatifu, na hivyo tunamkaribia Mungu katika ukamilifu wote, kumwomba yeye na kupokea vyote kutoka kwake bila sharti. Haleluya!
Warumi 3:21-24
[21]Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; [22]ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; [23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; [24]wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
[21]Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii;
[22]ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;
[23]kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
[24]wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
Hivyo ikiwa umekombolewa na Yesu Kristo, basi unapaswa uwe na ujasiri wote kumkaribia Mungu, bila kutegemea ukamilifu wako,Bali Kristo tu, na hivyo utapokea mema, yote kutoka Kwa Mungu.
Waebrania 4:16
[16]Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Hiyo Ndio inaitwa “HAKI itokayo Kwa Mungu” ambayo tunaipata kwa kupitia Yesu Kristo tu peke yake.
Kwa Yesu tunapokea uzima wa milele bure. Kwa Yesu Tunapokea majibu ya mahitaji yetu yote bure. Kwa Yesu tunaitwa watakatifu.
Lakini Swali ni je! Umemwamini Kristo? Kumbuka kamwe huwezi kumpendeza Mungu Kwa matendo yako pekee, Kila mwanadamu chini ya jua anamuhitaji Kristo.
Ikiwa Bado hajaokoka basi mlango upo wazi Leo. Tubu mgeukie Bwana akuponye. Ikiwa upo tayari kupokea msamaha wa dhambi Leo, na kufanywa kiumbe kipya, basi fungua hapa Kwa Mwongozo huo. >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618
Mafundisho mengine
TUNAHESABIWA HAKI BURE KWA NJIA YA IMANI.
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
SI KWA MATENDO BALI NEEMA.
NJONI, NUNUENI MLE NA MNYWE.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Nini maana ya Mithali 16:30
Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya.
JIBU: Mstari huo haumaanishi mtu anayefumba macho yake, Huwa anaishia kuwaza mawazo mabaya, hapana kama ni hivyo basi, tungekuwa tunafanya makosa kufumba macho tunapoomba.
Zaidi sana mtu mwenye hekima huwa anapoona jambo la kutisha ovu, au lenye aibu Ndio anayekuwa wa kwanza kufumba macho yake asiruhusu kuona kinachoendelea.. kama vile walivyofanya watoto wa Nuhu.(Mwanzo 9:23)
Hali kadhalika anaposema mtu aikazaye (aifumbaye), midomo yake. Haimaanishi mtu asiyezungumza-zungumza, Huwa anaishia kuyazungumza maneno yasiyofaa. Kama ni hivyo biblia isingesema;
Mithali 21:23
[23]Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, Atajilinda nafsi yake na taabu.
Lakini je? Vifungu hivyo vilimaanisha Nini?
Hapo anaposema afumbaye macho yake ni kuwaza yaliyopotoka,..alimaanisha afumbaye macho asitazame kweli (ambayo ni Neno la Mungu), linapomfundisha au kumwonya. Mtu huyo lengo lake ni kuendelea katika mawazo yake mabaya ya dhambi. Mfano aambiwapo kuishi na mke ambaye si wako ni uzinzi, na wazinzi sehemu Yao ni Katika ziwa la moto, lakini hataki kuliona au kulisikia Hilo andiko, jibu lake ni kuwa anataka kuendelea katika matendo yake ya giza.
Ndicho kilichokuwa Kwa waliompinga Yesu., Ndio maana akasema maneno haya;
Mathayo 13:15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Mathayo 13:15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema,
Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
Vilevile anaposema “Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya”
Anamaanisha, aizuiaye midomo yake kusema maneno ya uzima, ya staha, ya kujenga, ya adabu, ya maarifa, ya busara n.k.. Mwisho wake utakuwa ni kunena maneno mabaya tu.
Bwana alisema..
Luka 6:45
[45]Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.
Vivyo na hivyo na sisi, hatuna budi tujipime na kujichunguza…macho yetu hutazama Nini, vinywa vyetu vimejawa na maneno gani.? Lakini fahamu kuwa huwezi kushinda jicho lako, au ulimi wako ikiwa Kristo hajaumbika ndani yako.
Je! Unataka msaada Kwa Yesu Kristo? Kama jibu ni Ndio, basi unachopaswa kufanya cha kwanza ni kuyaachilia maisha yako kwake. Ili akusamehe dhambi zako. Ndipo akupe nguvu ya kushinda dhambi.
Hivyo bofya hapa Kwa ajili ya Mwongozo wa Sala ya Toba.>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Mafundisho mengine:
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
NI WAKATI UPI UTAUONA USO WA KRISTO?
MWANANGU, NIPE MOYO WAKO;
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
JE! JICHO LAKO LINAONA NINI KATIKATI YA MAJARIBU?
Kama mwanamke uliyeokoka. Fahamu kuwa una wajibu wa kujiombea wewe, kuombea jinsia yako, na kuliombea Kanisa la Kristo kwa ujumla. Huu ni mwongozo wa kipengele muhimu vitakavyokusaidia katika maombi yako. ambavyo kama utakuwa ni mwombaji wa mara kwa mara katika maeneo hayo, basi unajijengea mazingira ya kuwa mwanamke bora, mama bora, na zaidi sana mtumishi bora wa Bwana katika mwili wa Kristo.
Mwongozo huu unaweza kuutumia pia muwapo wanawake wawili au watatu katika kikundi chenu cha maombi, au kanisani. Na hivyo kila kipengele tenga muda wa kutosha kuomba.
NANGA: Zaburi 68:11 “Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;”
Mfano wa wanawake hawa alikuwa ni Loisi.
NANGA: 2Timotheo 1:5 nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo
NANGA: Yeremia 9:17 Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; 18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji. 19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.
NANGA: Luka 10:39 Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.
NANGA: 1Petro 3:4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
NANGA: 1Petro 3:6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote
NANGA: 1Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani
NANGA: Luka 8:3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao
NANGA: Mwanzo 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye
NANGA: Luka 1:6 Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila lawama. 7 Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana
NANGA: Kutoka 15:20 Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza. 21 Miriamu akawaitikia,Mwimbieni Bwana ,kwa maana ametukuka sana;Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini
NANGA: Soma – 2Samweli 21, yote
NANGA: Luka 24:22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, 23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai
PIA OMBA…
NANGA: 2Yohana 1:1 Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
NANGA: (Soma Kutoka 1:15-19)
NANGA: Ruthu 1:16 Naye Ruthuu akasema, Usinisihi nikuache, Nirejee nisifuatane nawe; Maana wewe uendako nitakwenda, Na wewe ukaapo nitakaa. Watu wako watakuwa watu wangu, Na Mungu wako atakuwa Mungu wangu; 17 Pale utakapokufa nitakufa nami, Na papo hapo nitazikwa; Bwana anitende vivyo na kuzidi, Ila kufa tu kutatutenga wewe name
NANGA: Luka 2:36 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 2.37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba
NANGA: Luka 2:51 Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. 51 Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake
NANGA: Luka 10:40 “Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi;..”
NANGA: Waamuzi 4:4 Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule. 5 Naye alikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue
NANGA: Luka 15:8 Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? 15.9 Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
NANGA: Soma (Marko 12:42, 1Wafalme 17:12, Luka 7:11)
OMBA PIA…
PIA OMBA HIZI TABIA ZIONDOKE NDANI YAKO NA WANAWAKE WOTE…
Kwa ushauri/ Msaada/ Maombezi /Ratiba za ibada, wasiliana nasi kwa mawasiliano haya;
Na, Mwl Denis & Devis Julius
KANUNI YA KUOMBA NA KUPOKEA.
MWONGOZO WA MAOMBI YA WAHUDUMU/ WASIMAMAO MADHABAHUNI.
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
NIFANYE NINI ILI MUNGU AYAJIBU MAOMBI YANGU?
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)
SWALI: Nini maana ya Mithali 21:1
“Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo”.
JIBU: Kuna mithali inayosema “maji hufuata mkondo”. Ikiwa na maana, palipo na mfereji kule kule unapoelekea ndipo maji nayo huelekea. Mfano ukielekeza mrefeji shambani mwako, basi maji yale yataelekea huko si kwingineko, ukielekezea mfereji nyumbani mwako, basi maji yatakuja ndani mwako. Kamwe maji hayajiamulii pa kuririkia.
Vivyo hivyo na Mungu, ndivyo anavyofananisha mamlaka yake juu ya wafalme na wakuu wa dunia hii. Kwamba mashauri yao, hawajiamulii tu peke yao kwa kujitakia. Kwamfano utakumbuka kuna wakati Mungu alimnyanyua Moyo Koreshi mtawala wa Uajemi ili awape ruhusu wayahudi warudi katika nchi yao wakamjengee nyumba.
Ezra 1:1 Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema, 2 Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; 3 Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Bwana, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu. 4 Na mtu awaye yote aliyesalia mahali po pote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu
Mungu huyo huyo ndiye aliyemfanya mfalme Nebukadreza kuwa na moyo mkatili ili awachukue watu wake utumwani kwasababu ya makosa yao.(Yeremia 27:6, 43:10)
Mungu anaweza kuwatumia watawala kuadhibu taifa, au kuwabariki watu wake. Hii ni kuonyesha kuwa hakuna tawala yoyote katika hii dunia inamilikiwa na fikra za mwanadamu asilimia 100, bali mengi ya mashauri ya wakuu hutoka juu mbinguni, au yameruhusiwa na Mungu. Wao ni kama maji tu yanayofuata mkondo wa kusudi la Mungu.
Ndio jambo ambalo Mungu alimwambia Mfalme Nebukadreza kwamba “aliye juu ndiye anayetawala”(Danieli 5:21) lakini yeye alidhani ni uongo, mpaka siku alipoondolewa kwenye ufalme wake kwa miaka 7, na kurudishwa baadaye.
Hivyo, jambo hili, sio tu la viongozi wa kidunia, lakini pia hata wa kanisani. Ikiwa kanisa ulilopo linasimamia kweli na utakatifu na Kristo Yesu ndio kiini cha fundisho lao, basi waheshimu sana viongozi wako, kwasababu si kila shauri linalotoka kwenye vinywa vyao, ni wao wamefikiria. Wao ni kama maji tu yaliyomwagwa kwenye mfereji, ili kukuongoza wewe. ukishandana nao, au ukipuuzia kuongozwa nao, wakati mwingine unapingana na maamuzi ya Mungu wako bila kujijua.
Waheshimu viongozi wako wanaokulea kiroho, kama vile unavyowaheshimu watawala ya kidunia.
Shalom
Fahamu maana ya Mithali 29:4 “Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.
Ni kwa namna gani Kristo analitakasa kanisa kwa Maji katika Neno? (Waefeso 5:26)
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
ITAMBUE KARAMA YA MUNGU.
Swali: Biblia inasema katika Ufunuo 1:6 kuwa kupitia Bwana Yesu tumefanyika kuwa ufalme na makuhani, je tumefanyikaje kuwa hivyo?
Jibu: Awali ya yote tusome maandiko yafuatayo,
1 Yohana 4:17 “Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, KAMA YEYE ALIVYO, NDIVYO TULIVYO NA SISI ULIMWENGUNI HUMU”.
Hapo anasema “kama yeye alivyo ndivyo na sisi tulivyo”. Ikiwa na maana kuwa katika roho sisi tunafanana na Kristo kwa kila kitu.
Maana yake kama Kristo ni mwana wa Mungu basi na sisi ni wana wa Mungu sawasawa na Warumi 8:16.
Warumi 8:16 “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu”.
Vile vile kama Kristo alikufa na kufufuka na kuketi katika kiti cha enzi, vile vile na sisi katika roho tulikufa pamoja naye kwa njia ya ubatizo (sawasawa na Warumi 6:4 na Warumi 6:8) kwa njia ya ubatizo
Warumi 6:4 “Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima”.
Na vile vile kama Kristo alifufuka na sisi pia tulifufuka pamoja naye na sasa tumeketi pamoja naye katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 2:6 “Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu”.
Kwahiyo kwa ufupi ni kwamba watu waliookoka kikamilifu wanafanana na Kristo kwa kila kitu, na hii ndio sababu kwanini shetani pamoja na mapepo yake yanawaogopa watu wa YESU KRISTO, ni kwasababu yanamwona Yesu Kristo ndani yao.
Sasa nafasi nyingine ya YESU iliyo kuu ni nafasi ya “ukuhani” na tena si kuhani tu, bali “KUHANI MKUU”.
Waebrania 8:1 “Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni”.
Na kama Kristo alivyokuwa Kuhani, vile vile na sisi ni makuhani.
Na kumbuka kazi ya Makuhani ilikuwa ni kuwapatanisha watu na Mungu wao kwa njia ya SADAKA NA MAOMBI NA MAFUNDISHO.
Mfano Samweli, alifanya kazi ya kuwapatanisha Israeli kupitia sadaka zao , vilevile na kuwaombea na kuwafundisha njia iliyo sahihi..
1 Samweli 12:23 “Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka”
Na Kristo ni hivyo kama Kuhani amesimama kutupatanisha na baba kwa njia ya kutuombea..
1 Yohana 2:1 “Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki”.
Soma pia Warumi 8:34, utaona jambo hilo hilo.
Na pia Yesu anatupatanisha kwa Baba kwa njia ya sadaka ya mwili wake alioutoa kwaajili yetu.
Na sisi pia kwakuwa tunafanana na yeye katika roho sawasawa na hiyo 1 Yohana 4:1, basi na sisi ni makuhani kama yeye na tunaweza kuzifanya kazi zile zile anazozifanya yeye sasa za kikuhani.
Na kazi hizo ni kuwapatanisha watu na Baba kwa njia ya MAOMBI, MAFUNDISHO NA SADAKA. Hivyo tumepewa na sisi huduma ya upatanisho kama aliyonayo Bwana wetu YESU KRISTO.
Utauliza tunalithibitisha vipi hilo kibiblia?…Tusome maandiko yafuatayo..
2 Wakorintho 5:18 “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye ALITUPA HUDUMA YA UPATANISHO;
19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; NAYE AMETIA NDANI YETU NENO LA UPATANISHO”
Ndio maana tunaweza kuombeana na Mungu akasikia (Yakobo 5:16) kwasababu na sisi ni makuhani kama yeye, Vile vile kwa kujitoa miili yetu na vitu vyetu kama sadaka tunaweza kujipatanisha na kuwapatanisha wengine na Mungu.
Na hiyo yote ni kwasababu Kristo ametufanya na sisi kuwa makuhani kama yeye sawasawa na Ufunuo 1:6.
Tofauti ya Kristo na sisi ni kwamba Kristo yeye ni KUHANI MKUU, na sisi tunabaki kuwa makuhani, (yeye ni mkuu wa makuhani, utukufu na heshima zinabaki kwake, Bwana wa mabwana, mwamba imara!!!).
Na ni kwa namna gani sisi ni UFALME?.
Ni kwa namna ile jinsi Kristo alivyo…Yeye ni Mfalme, na tena si mfalme tu, bali Mfalme wa wafalme.
Ufunuo 19:16 “Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA”
Na kama yeye ni Mfalme wa wafalme, maana yake anao wafalme anaowatawala ambao nao pia ni wafalme na hao si wengine zaidi ya wale wanaomwamini.. (Kwamaana hawezi kuitwa mfalme wa wafalme kama hana wafalme chini yake anaowatawala).
Na utukufu wa ufalme tulionao sasa utakuja kudhuhirika zaidi katika ule utawala wa amani wa miaka 1000 wa YESU KRISTO.
Ufunuo 20:6 “Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; BALI WATAKUWA MAKUHANI WA MUNGU NA WA KRISTO, NAO WATATAWALA PAMOJA NAYE HIYO MIAKA ELFU”
Je umeziona faida za kuwa ndani ya Kristo?.. Tunakuwa makuhani na tena wafalme…
Je! Tayari Umemwamini yeye?.
Kama bado unasubiri nini?..kumbuka tunaishi majira ya kurudi kwa Yesu mara ya pili.
Shalom..
Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Je! Kutamani kwa namna yoyote hakufai?
Mathayo 5:27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
JIBU: Ukitafakari hapo utaona mazingira Bwana anayoyazungumzia hapo ni ya uzinzi. Uzinzi ni kitendo cha kutoka nje ya mpango wa ki-ndoa katika eneo la kukutanika kimwili. ambao chanzo chake ni tamaa.
Sasa Bwana anaweka wazi kuwa uzinzi huanzia ndani kwenye mawazo ya mtu, moyoni mwake, tofauti na vile inavyodhaniwa kuwa mpaka wakutane dhahiri.
Lakini swali linaloulizwa je! Hatupaswi kutamani kabisa? Na kama tukitamani tutakuwa tunafanya kosa.
Kila kitu Mungu amekiweka katika utaratibu wake. Ni sawa na kusema kwanini ulafi ni dhambi, wakati Mungu ametuwekea ndani yetu hamu ya kula. Au kwanini nisile udongo wakati, najisikia hamu ya kuula mimi kama mjamzito, Au kwanini nisinywe pombe wakati ninajiona kabisa nina kiu nayo?. Kama Mungu angekuwa hapendi kwanini ameniwekea kiu hiyo?
Lakini unajua kabisa ukizidisha kula kuna madhara mwilini, pia ukila/ukinywa kitu kisichopasa utajisababishia madhara mwenyewe.
Vivyo hivyo katika tamaa. Haijawekwa, iwe ni “kutamani-tamani”, kila kitu kinachokatiza mbele. Bali Mungu aliiumba hiyo mahususi kwa wanandoa. Hivyo ikiwa upo humo huna budi kuzielekeza kwa mkeo/mumeo tu, na kama bado hujaingia humo, unapaswa uweze kuzitawala. Na hiyo inawezekana kabisa, usipozitengenezea mazingira, haziwezi kuamka na kukusumbua. Kwasababu maandiko yanasema moto hufa kwa kukosa kuni.
Ufanyeje.
Ni kujiepusha na mazingira yote, yatakayoweza kukupelekea kulipuka tamaa. Kwamfano, mazungumzo-zungumzo yasiyokuwa na maana na mtu wa jinsia nyingine, (kuchati), na kutazama video au picha zenye maudhui ya kizinzi, kuzungumza-zungumza habari hizo na marafiki zako, kuwa katika mazingira yasiyo ya kujishughulisha, kwamfano upo tu huna kazi yoyote umekaa, ni rahisi kupelekwa kwenye mawazo hayo na adui. Lakini pia kuwa msomaji wa Neno na mwombaji. Vitakusaidia sana kuwa mtu asiyetawaliwa na tamaa.
Na hivyo hata adui akitaka kukupeleka kwenye hali ya kutamani, kujengea picha, kutafakari, basi unaweza kuyakataa hayo mawazo haraka, na ukaendelea kuwa salama, bila ya kuzini moyoni mwako. Kwasababu umevidhibiti.
Pia kumbuka jambo hili, si la wanaume tu, bali kwa jinsia zote. Hatupaswi kuishi maisha ya tamaa.
MOTO HUFA KWA KUKOSA KUNI.HATA UASHERATI NAO
Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?
WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU
Biblia imemaanisha nini iliposema “hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu”
Bwana aliposema “sikuja kutangua torati bali kuitimiliza” alikuwa anamaanisha nini?
SWALI: Ni mateka yapi hayo aliyoyateka..na ni vipawa gani alivyowapa wanadamu.?
Waefeso 4:8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.
JIBU: Ufalme wa Mbinguni umefananishwa na ngome Fulani, yenye hazina kubwa sana ambayo hupiganiwa na watu wengi kumilikiwa.
Na Ndio maana Bwana Yesu aliyasema maneno haya;
Mathayo 11:12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.
Umeona unafananishwa na kitu cha kutekwa, sio kitu cha kuombwa, au kubembelezwa Fulani. Inahitaji kupambania.
Hivyo Kwa maneno hayo utaelewa kuwa hata Bwana wetu Yesu Kristo, alikuwa katika operesheni hiyo ya kuuteka huo ufalme.
Na hiyo ilikuja kutimia siku ile aliposhinda pale Kalvari Kwa kifo chake na kufufuka katika wafu aliweza kumiliki vyote vya mbinguni na vya duniani…vyote viliwekwa chini yake.
Waefeso 1:20-23 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; [21]juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; [22]akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo [23]ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Sasa kwasababu ameteka Kila kitu cha mbinguni, aliteka pia na ‘uweza wote wa kiungu’ na kutupa sisi wanadamu, ndio vipawa au karama za Roho Mtakatifu, alizozitoa Kwa lengo la kuujenga mwili wa Kristo, kuhubiri injili, na kuhudumu.
Ndio hapo akawafanya wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine wainjilisti, wengine, wachungaji na wengine waalimu.(Waefeso 4:11)
Pamoja na karama zile 9, tunazozisoma katika 1Wakorintho 12.
1 Wakorintho 12:8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; [9]mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; [10]na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; [11]lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
Mambo ambayo hayakuwahi kuonekana zamani, hata za manabii..lakini Sasa twaziona zikidhihirika katika kanisa la Kristo.
Hivyo kumbuka Yesu hajateka mateka tu mbinguni. ni mpaka duniani. Maana yake ni kuwa sisi tuliomwamini hatuna budi pia kuwa watekaji. Hivyo popote pale uendapo kuhubiri injili, usiogope Wala usiwe mnyonge, vamia, hubiri Kwa ujasiri na hakika watu watabadilika kwasababu nguvu hizo tumepewa katika Kristo Yesu
2 Wakorintho 10:4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Bwana akubariki
Wakaldayo ni watu gani?
TUNA JUKUMU LA KWENDA KUTEKA MATEKA.
MLANGO MWINGINE WA ADUI KUTULETEA MAJARIBU.
TABIA ZA NJIA YA MUNGU KWA MKRISTO
MBINGUNI YUPO NANI SASA?
Vyemba kama lilivyotumika hapo ni mkuki.
Absalomu mwana wa Daudi alipomwasi baba yake, na kusababisha vita vikubwa katika Israeli, Tunasoma, alipokuwa vitani, akiwa amepanda mnyama wake, alipita chini ya mti mmojawapo akanaswa, mnyama alipoendelea mbele yeye akabaki ananing’inia pale pale, pasipo mafanikio yoyote ya kujinasua, baadhi ya askari wa Daudi walipomwona waliogopa kumuua, kufuatana na kiapo cha Daudi alichowaagiza wasimuue. Lakini jemedari wa mfalme aliyeitwa Yoabu yeye alikaidi amri, na kwenda kumwua kumpiga hivyo vyemba vitatu, moyoni. Kisha akamaliziwa na wasaidizi wake.
2Samweli 18:14 Ndipo Yoabu akasema, Siwezi kungoja na kusema nawe hivi. Akachukua vyemba vitatu mkononi mwake, akamchoma Absalomu moyoni, alipokuwa akali hai katikati ya ule mwaloni. 15 Kisha vijana kumi, waliomchukulia Yoabu silaha zake wakamzunguka, wakampiga Absalomu, na kumwua
Hivyo Yoabu alimchoma mikuki mitatu Absalomu kifuani mwake.
Lakini katika habari hii tunajifunza nini?
Upendo wa Daudi kwa mwanae ni sawa na Upendo wa Mungu kwetu sisi. Ijapokuwa Absalomu alimuudhi sana baba yake mpaka kumvunjia heshima ya kulala na wake zake, na kuuasi ufalme wake mtukufu, Daudi bado moyo wake ulikuwa kwa Absalomu kutaka atubu. Lakini Absalomu mwenyewe hakutaka, na hivyo alikutana na majeshi yakamwangamiza kwa tabia zake za uasi ulioendelea. Laiti angekuwa mtoto mtii, asingekufa kwasababu baba yake angeweza kumlinda.
Tunapomwasi Mungu, tunajitenga na rehema zetu wenyewe, Kama vile Yona alivyosema katika (Yona 2:8),. Kamwe usimwasi Mungu ndugu, tembea katika njia zake, kwasababu hakika huko unapokimbilia kifo kipo. Na utakapovamiwa na adui yako ibilisi Mungu hataweza kukutetea kwa lolote. Utakufa na kuangamia milele kwa vyemba hivyo rohoni.
Nje ya Kristo hakuna usalama. Mrudie Mungu wako, kwa kumfuata Bwana Yesu, Tubu dhambi zako leo, ubatizwe, upokee ondoleo la dhambi zako. Uishi maisha ya neema siku zote ndani ya pendo lake. Acha uasi, neema haitadumu kwako daima kukulinda katika hiyo mitego adui anayokutegea kila siku akuue.
Je ungependa kuupokea wokovu leo? Kwa Yesu kuwa mwokozi wako na mtetezi? Kama ni ndio basi fungua hapa kwa mwongozo huo wa Sala ya Toba >>>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Bwana akubariki. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
ANGALIA UZURI WAKO, USIGEUKE KUWA KITANZI CHAKO.
UVUMILIVU NA MIKAKATI YA ABSALOMU, INA FUNZO NYUMA YAKE.
MJUMBE ASIYEKUWA NA UJUMBE.
NI WAKATI GANI SHETANI ANAPENDA KUMSHAMBULIA MWAMINI?
Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.
Msongo wa mawazo ni nini? Ni shinikizo au mfadhaiko wa kiakili, unaomkumba mwanadamu, pale anapokutana na matatizo, au taabu, au dhiki au shida Fulani. Hivyo inapotokea mtu huyu anashindwa kuzitatua changamoto hizo, ndipo msongo huo huja.
Kwamfano labda mtu amegundulika, ana ugonjwa usiotubika, na kaambiwa na daktari hawezi kupona, mtu kama huyu ni rahisi kukumbwa na msongo wa mawazo,
Au labda mwingine hana kazi na akiangalia familia inamtegemea, na bado hajafikia malengo yake kulinganisha na umri alionao, moja kwa moja mtu kama huyu ni rahisi kukumbwa pia na msongo wa mawazo. N.k.
Na kama tiba isipopatikana matokeo yake yanaweza kuwa mtu huyo, kupata matatizo ya kiafya, wengine kuchanganyikiwa, wengine kujitenga na watu, wengine kujifungia ndani kulia tu usiku kucha, wengine kutenda vitendo viovu,hata kujiua.
Je! Mkristo anaweza kuwa na msongo wa kimawazo? Jibu ni ndio anaweza kuwa nao. Lakini tiba imeshatolewa. Tutaona katika somo hili kwa namna gani, kwasababu yawezekana wewe ni mmoja wapo ambaye unakutana na hali hii na hujui cha kufanya.
Embu tuone kwanza baadhi ya watu katika maandiko ambao walipitia misongo ya mawazo
Eliya wakati amemaliza kuwaua manabii wa Baali, akatazama huku na huku na kujiona kama ni yeye peke yake ndiye nabii wa Mungu aliyebaki, hivyo ikampelekea ajitenge, na kukimbilia jangwani, akae huko mpaka afe. Lakini Mungu alikuja kumtokea baada ya siku 40, akampa majibu ya faraja, kwamba asidhani yupo peke yake kuna wengine 7,000 amejisazia, rudi Israeli, kanitumikie.(1Wafalme 18-19)
Alikumbwa mara nyingi na msongo wa mawazo katika maficho yake alipokuwa anawindwa na mfalme Sauli. Mara nyingi alifikia hatua ya kukata tamaa ya maisha. Embu tafakari haya maneno aliyoyasema Daudi.
Zaburi 69:1 Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu. 2 Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha. 3 Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu. 4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua. 5 Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu
Baada ya kupotelewa na mali zake, na watoto wake, hadi mwili wake kubaki mifupa tu. Mkandamizo ulimjia. Ayubu anasema;
Ayubu6:2 Laiti uchungu wangu ungepimwa, Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja! 3 Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari; Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka
Mpaka akanza kusema maneno magumu, ya kulaana siku aliyozaliwa. Mtu kama huyu alikuwa katika hali mbaya sana kifikra na kiakili.
Petro na Yuda walipitia jambo moja, kukana na kusaliti, ni dhambi pacha. Isipokuwa Yuda alikwenda kujinyonga kwasababu msongo wa mawazo ulimshinda, lakini Petro hakujinyonga. Yeye alikwenda kujificha na kulia sana kwa “majonzi”. Tengeneza picha ni wewe unamkana Mungu wako, tena kwa maneno ya dhihaka mbele za watu. Hali hiyo unadhani itakufanya ujionaje kama sio mateso ya kiakili baada ya hapo?. Wengine wanapitia hali kama hizi, wanapojiona wamemtenda Mungu dhambi kubwa sana, isiyosameheka, wakidhani kuwa Mungu hawajali tena, hawathamini.(Mathayo 26:75)
Baada ya Bwana Yesu kufa, hofu ya wayahudi ikawavaa mitume, wakiona kuwa wao ndio wanaofuata kuuliwa baada ya kiongozi wao kufa.. Hivyo hiyo ikawapelekea kujifungia ndani, wasitoke. Msongo mkubwa sana wa mawazo uliwavaa, kutoka kwa wayahudi.(Yohana 20:19-29)
Itoshe tu kutumia mifano hiyo michache, kwani wapo wengine wengi sana katika biblia waliopitia hali kama hizi, mfano ni Musa, Yusufu, Yeremia, Nebukadreza, Hana(mamaye Samweli), Danieli, Mtume Paulo wote hawa ukisoma habari zao katika biblia utayathibitisha hayo.
Utagundua, walipopotia taabu zao, walilikumbuka TUMANI la Mungu. Ndilo lililowapa nguvu ya kuweza kuvuka nyakati hizo mbaya walizozipitia. Waliyazingatia haya maneno;
1Petro 5:6 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; 7 HUKU MKIMTWIKA YEYE FADHAA ZENU ZOTE, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.
Na lile alolilisema Yesu..
Mathayo 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha
Pale akili zilipogoma, fikra kuzima, moyo kuwa baridi, walijifunza kumtwika Mungu, huzuni zao, mateso yao, shida zao. Hata pale ambapo hazikutatulika kwa wakati walioutarajia, lakini waliendelea na mwisho wa siku Bwana alikuja kuyaweka yote sawa. Kwasababu yeye mwenyewe alisema.
Yeremia 29:11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi TUMAINI siku zenu za mwisho
Hivyo ndugu, ikiwa na wewe upo katika hali hii ya msongo wa kimawazo, katika eneo lolote lile, iwe la kiroho, kihuduma, kifamilia, kikazi, kiafya, kimaendeleo. Umeshindwa kuendelea mbele, Usiogope. Kwa Mungu lipo TUMAINI, zaidi ya Matumaini yote ya kibinadamu.
Haijalishi msongo huo, umekupata kutokana na dhambi zako, au kutokana na hali zilizo nje ya uwezo wako. Usiogope. Mponyaji, mfajiri, mtatuaji wa matatizo yupo. Huyu si mwingine zaidi ya YESU KRISTO mwokozi.
Mungu akikupa tumaini, ujue ni lazima litokee, lakini mwanadamu akikupa tumaini, ni kusudi tu kukufariji, lakini tatizo linaweza kubaki palepale. Yesu hayupo hivyo. Mtazame tu yeye. Wakati wa shida, ndio wakati wa kukimbilia chini ya mbawa zake, sio kuwakimbilia wanadamu.
JE! UFANYEJE?
Na hakika, katika muda fulani, utaona Mungu anakuvusha, anakuponya, anakufariji, anakuondolea huo mzigo. Huo ni uhakika sio makisio. Usiache tu kuendelea na Bwana..
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Mafundisho Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255789001312 au +255693036618. Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
TUMAINI NI NINI?
UKIOKOKA,HIZI FIKRA ZIKIJA NDANI YAKO, ZIKATAE.
VITA VYA KIFIKRA BAADA YA KUZALIWA MARA YA PILI
TUUTAFUTE UMOJA WA ROHO.
Je shetani ana uwezo wa kujua mawazo ya mtu?
Tofauti kati ya ndoto na Maono ni ipi?
Huu ni mwendelezo wa Mafundisho maalumu yawahusuyo wanawake.
Mwanamke aliyepoteza shilingi moja.
Luka 15:8 Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione? 9 Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
Bwana Yesu alipenda kutumia mifano halisi ya kimaisha kutufundisha habari za rohoni. Kwamfano katika habari hiyo tunafahamu mfano huo ulikuwa analenga mambo ya ufalme wa mbinguni, jinsi Mungu anavyomthamini mtu wake mmoja aliyepotea katika dhambi, pindi atubupo na kurejea. Kwamba tendo hilo linamfanya yeye pamoja na malaika zake mbinguni kufurahi sana.
Lakini leo nataka tujifunze kuhusu mfano huo katika uhalisia wake wa kimaisha kama ulivyoandikwa. Kuna maswali lazima ujiulize kwanini amtaje mwanamke na sio mwanaume. Kisha aipoteze shilingi yake pale NYUMBANI kwake, na sio sehemu nyingine, labda barabarani au sokoni? Tofauti na mfano uliotangulia ambao unamzungumzia Yule mtu aliyepotelewa na kondoo mmoja akawaacha wale 99 akaenda kumtafuta Yule mmoja huko maporini.
Na hatua ambazo alitumia kuitafuta shilingi ile hadi kuipata, kuna funzo gani pia?.
Kumbuka kimaandiko aliyekabidhiwa nyumba aisimamie ni mwanamke, ndio maana biblia inasema,
Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Na hazina yake inapatikana humo, lakini pia ikipotea, basi hupotelea humo humo.
Tukisema nyumba hatumaanishi, gorofa, na sebule na jiko. Hapana, bali tunamaanisha wale waliomo mule. Hao ndio hazina yake hasaa.
Sasa katika mfano huo mwanamke huyu alikuwa na shilingi 10, labda tuseme hao ni watoto 10, au ndugu 10, lakini mmoja akapotea, huwenda akawa mtundu, au mwizi, au kibaka, au shoga, au jambazi n.k. Lakini Mwanamke huyu hakukata tamaa na kukaa chini na kusema, Ahh! Ninao hawa 9, wenye kujitambua na wenye nidhani. Embu ngoja niachane na Yule pasua kichwa mtukutu, mwenye kiburi, asinipe presha, nifarijiwe na hawa wanangu 9 wazuri. Hapana, bali alilazimika kufanya jambo ili kuhakikisha amempata na Yule.
Hivyo kama tunavyosoma, hakukaa tu hivi hivi, na kuzungumza. Bali alichukua hatua fulani, na hatua zenyewe ndio hizi tatu.
Hii ikiwa na maana gani? mpaka anafikia hatua ya kuwasha tamaa, maana yake ni kuwa chumba hicho kilikuwa na giza, hivyo asingeweza kuipata shilingi yake katika mazingira yale. Tafsiri yake ni nini? Alimkaribisha Kristo. Ambaye ndio Nuru ya ulimwengu katika nyumba yake.
Hivyo hatua ya kwanza katika kutatua tatizo lake, alimtambua Kristo kwenye nyumba yake. Na sasa Nuru ilipomulika ndipo akatambua kuwa nyumba ilikuwa chafu. Kama asingewasha taa, kamwe asingeweza kugundua kuwa Vitu havipo katika mpangalio wake. Hivyo ikampasa aanze kwanza kuifagia nyumba ile, aipangilie vizuri. Makombo yaliyodondoka sakafuni ayafagie, vikombe na vijiko vilivyokaa hoe hae, aviweke mahali pake, nguo ambazo hazijakunjwa aziweke kabatini, uwazi uwepo. Hakukimbilia kuitafuta shilingi yake katika hatua hiyo. alijua hawezi kuipata katika mazingira yale, machafu, imejificha sana.
Hivyo ikamchukua muda Fulani mrefu kuisafisha nyumba yake, mpaka hatimaye, pengine baada ya saa 6, ikawa safi. Kila kitu kikawa katika mpangilio wake.
Ndipo sasa akaenda katika hatua ya mwisho ya “kuitafuta kwa bidii ile shilingi”. Akaanza kupita eneo moja baada ya lingine, hakutoka nje ya nyumba kwenda kuitafuta barabarani, hapana bali pale pale ndani kwasababu alijua fedha zake hazijawahi kutoka nje ya nyumba.
Na hatimaye akaipata. Na mwisho wa siku akawaalika na marafiki zake, wakafurahi pamoja. Kwasababu ilimgharimu kuipata tena.
Hii ni kufunua nini?
Wanawake wengi wanapoona aidha ndugu zao nyumbani, au watoto wao, au ndoa zao zimeharibika,. Wengine wanakimbilia kwa waganga ili wasaidike, hapo umepotea, wengine wanakimbilia kwa washauri wa kijamii, bado hujapata suluhisho. Suluhisho pekee ni Nuru ya ulimwengu. Yesu Kristo, aimulikie kwanza nyumba yako.
Na Yesu anachokifanya ni kukuonyesha madhaifu uliyokuwa nayo, uchafu uliomo nyumbani mwako, ili urekebishe (ndio ufagie). Sasa wengine wanapofikia hatua hii, wanapoona wanahubiriwa waishi maisha ya utakatifu, wawe watu wa ibada majumbani mwao, wawe waombaji, wafungaji, wafukuze tabia zisiojenga majumbani mwao, waweke mipaka Fulani kwenye familia zao. Wanaona kama wanatwikwa mzigo juu ya mzigo. Wanamkimbia Kristo, wanabakia kulia tu, na kuhuzunika..
Wanachofikiria tu, ni utatuzi wa tatizo, mume aache pombe (aokoke), watoto wawe wasikivu, nyuma iwe na amani, n.k. lakini hawataki wao wenyewe kurekebisha baadhi ya mambo makwao. Hapo ndugu ukikwepa hatua hii, sahau kukipata unachokitafuta. Hata upewe bahari nzima ya mafuta ya upako, na pipa la chumvi. Unapoteza muda, hutatui jambo lolote.
Kristo anataka usafi kwanza, ndipo akupe jicho la kuiona shilingi yako iliyopotea. Sasa ikiwa utatimiza mambo hayo mawili yaani KRISTO ndani yako, na usafi wako. Kinachofuata ni kutafuta ulichokipoteza.
Hii ndio hatua sasa ya kumuhubiria, kumshauri, kumwonya, kumvuta kwa Bwana. Sasa ukiendelea hivyo hivyo, muda si mwingi utampata kiwepesi sana haijalishi alikuwa amepotea kiasi gani, au alikuwa sugu namna gani. Hakuna linaloweza kujificha mbele ya Nuru. Tatizo lolote sugu unalolijua wewe la kifamilia, kwa kufuata kanuni hizo litatatulika tu.
Hivyo wewe kama mwanamke, itambue huduma hii iliyopewa na Bwana, laiti kama wanawake wote, wangekuwa ni wa kujiwajibisha kwa namna hii, jamii zetu na familia zetu zisingekuwa na migogoro mingi,wala injili isingekuwa ngumu sana kuihubiri kwasababu tayari walishatangulia walioweka misingi bora nyuma. Hii ni huduma kubwa sana kwa mwanamke na Bwana anaithamini sana.
Simama katika nafasi yako wewe kama mama, wewe kama Dada, nyumba au familia itasimama, endapo wewe utasimama.
Shalom.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255789001312 au +255693036618 Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group
MAFUNDISHO KWA WANAWAKE
MWANAMKE ABIGAILI ANAFUNZO GANI KWA WANAWAKE?
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
BADO TUTAHITAJI TU KUSAIDIANA.
Je Mungu anaketi katika giza? (1Wafalme 8:12)
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 1)