SWALI: Isaya 59:5 ina maana gani?
Isaya 59:5 Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.
JIBU: Ni mstari unaoeleza asili ya watu waovu.
Anasema huangua mayai ya fira. Fira ni aina ya nyoka wenye sumu kali sana, ambao kwa kawaida mtu akikutana nao, ni lazima awaue, au akikuta mayai yao ni lazima ayakanyage, kwasababu, asipofanya hivyo yakitotolewa wataleta madhara, Lakini mtu mwovu biblia inasema ni kinyume chake huyatotoa. Ikiwa na maana ni mtu ambaye anaona madhara Fulani yanakuja mbele kwa wengine badala ayaangamize, yeye ndio anayekuwa wa kwanza kuyakumbatia.
Mfano mmojawapo wa hawa ni manabii wa uongo, wanaojua kabisa, dhambi ina madhara, na mtu asipoishi katika utakatifu hawezi kumwona Mungu (Waebrania 12:14), lakini kwasababu hawataki kupoteza watu, kwa tamaa za pesa, hawawaonyi juu ya mambo kama hayo, kinyume chake ndio wanawasogeza kabisa kwenye mambo ya mwilini, biashara na mali, wanamsahau Mungu. Halafu wanakufa katika dhambi zao na kwenda kuzimu.
Vilevile anasema husuka wavu wa buibui. Kama vile tunavyojua buibui anaposuka wavu wake, ni kwa lengo la kunasa wadudu awale. Halikadhalika asili ya watu wa waovu ndivyo ilivyo, huandaa mazingira yote, ya wenzao kunaswa katika mambo maovu na kuangamia.
Kwamfano unapomwombea adui yako afe, ni sawa na mtu anayeunda wavu wa uangamivu. Bwana alisema tuwaombee, lakini sisi tunawatakia mauti, tena katika maombi.
Kwa ufupi, hii ni tabia ya kutengeneza kama sio kufurahia anguko la wengine.
Hivyo biblia inatuonyesha pia tukiwa na tabia kama hizo, zinatufanya na sisi Mungu asitutee na kutupa haki zetu kwa vile tumwombavyo, nasi majibu yanakuja kinyume chake.. Pale tunapotazamia jema linakuja ovu,na tunapotazamia nuru linakuja giza, tunalithitibitisha hilo katika vifungu vinavyofuata..
Isaya 59:6-9
6 Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao. 7 Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao. 8 Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani. 9 KWA SABABU HIYO HUKUMU YA HAKI I MBALI NASI, WALA HAKI HAITUFIKILII; TWATAZAMIA NURU, NA KUMBE! LATOKEA GIZA; TWATAZAMIA MWANGA, LAKINI TWAENDA KATIKA GIZA KUU.
6 Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.
7 Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao.
8 Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.
9 KWA SABABU HIYO HUKUMU YA HAKI I MBALI NASI, WALA HAKI HAITUFIKILII; TWATAZAMIA NURU, NA KUMBE! LATOKEA GIZA; TWATAZAMIA MWANGA, LAKINI TWAENDA KATIKA GIZA KUU.
Hivyo tupambane, kwa bidii zote tusiwe vyombo vya shetani vya kuunda mabaya kwa wengine.
Bwana atusaidie.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini auPiga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Injili iliyopo kwa Samaki aina ya Eeli.
Lumbwi ni nini katika biblia?
Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
Santuri ni nini? (Danieli 3:5,10)
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.
Donda-Ndugu ni nini?
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Kwanini watu watakaohukumiwa siku ile ya mwisho, wanaonekana kutofautishwa katika sehemu mbili, wengine watatokea “baharini”, na wengine katika “mauti na kuzimu”. Kwanini iwe hivyo na tofauti ya maeneo hayo ni ipi?
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 BAHARI IKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE; NA MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
Ufunuo 20:11 “Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
13 BAHARI IKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE; NA MAUTI NA KUZIMU ZIKAWATOA WAFU WALIOKUWAMO NDANI YAKE. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto”.
JIBU: Hukumu ya mwisho kabisa ni hukumu ijulikanayo kama “hukumu ya kiti cheupe cha enzi cha mwanakondoo”. Ni hukumu inayokamilisha wafu wote walioko makaburini, mbali na watakatifu.
Haitachagua wakubwa, wala wadogo, vijana au wazee. Waovu wote watafufuliwa wakati huu na kila mmoja atahukumiwa sawasawa na matendo yake, kisha atatupwa katika lile ziwa la moto, aangamie huko milele.
Lakini biblia inatuonyesha siku hiyo waovu hao watatoka sehemu kuu mbili,
Kumbuka, lugha iliyotumika hapo ni lugha ya kinabii, na sio halisi kabisa kwamba bahari inayo wafu wake. Hapana.
Je Bahari ikawatoa wafu waliokuwa ndani yake, kunamaanisha nini?.
Tukianzana na wafu waliokuwa baharini. Tabia ya bahari sikuzote ni kubwa, haina mwisho, ukipotea humo, umepotea moja kwa moja. Na kibiblia maji mengi(bahari) inamaanisha ulimwengu.
Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha”.
Hii ikiwa na maana sikuile ya mwisho, wafu wote, yaani waovu wa mataifa yote, wa lugha zote, waliokufa tangu Adamu, hadi wakati wa kurudi kwa Bwana Yesu kulinyakuwa kanisa lake (siku ya unyakuo). Wote hao watakuwa katika kundi la wafu watokao baharini. Watafufuliwa na kuhukumiwa.
Mauti na kuzimu kulifunua nini?
Lakini mara baada ya unyakuo kupita. Kuna tukio lingine litafuata, ambalo linajulikana kama dhiki kuu.
Kipindi hichi kinajulikana kama kipindi cha utawala wa shetani(mpinga-kristo), watu wengi sana watauliwa, kutokana na dhiki ambayo Mungu ataruhusu shetani aisababishe, kwa waovu wote, watakaobakia duniani. (Tukiachia mbali wale ambao watakataa chapa ya mnyama). watauawa.
Ukisoma Ufunuo 6:8 inasema.
“Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda JINA LAKE NI MAUTI, NA KUZIMU AKAFUATANA NAYE. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi”.
Umeona huyu farasi wa kijivujivu anaitwa mauti, akiambatana na kuzimu. Ambaye ni ibilisi akifanya kazi yake wakati huo. Naye atasababisha vifo vya robo ya watu waliopo duniani wakati huo. Kwamfano kwa dunia ya sasa ni Zaidi ya watu BILIONI 2, watauawa, na hiyo itakuwa ni katika mapigo ya ghadhabu ya Mungu, na vita vya Harmagedoni, na magonjwa, na wote hawa watakaokufa moja kwa moja watakuwa chini ya “Mauti na kuzimu”.
Sasa biblia inaposema Mauti na Kuzimu ikatoa wafu wake, umeshaelewa kuwa ni wafu waliokufa katika hichi kipindi cha Dhiki kuu, ambao kimsingi walikuwa chini ya mpanda farasi wanne, aliyeitwa mauti na kuzimu.
Sasa kwanini sehemu zote mbili zitajwe?
Ni kuonyesha kuwa hukumu hiyo haitambakisha mfu hata mmoja. Itakuwa ni hukumu ya ulimwengu mzima kwa wale ambao hawakunyakuliwa, Au kuikataa cha ya mnyama.
Ikiwa leo hii umekufa kama mlevi, au fisadi, au kihaba, utakapokufa utakwenda katika Habari la kiroho. Lakini ikiwa utakufa katika dhiki kuu, vilevile utakwenda katika katika mauti na kuzimu. Na wote siku ya mwisho mtafufuliwa. Na kuhukumiwa, kila mmoja kwa kipimo chake. Kisha mtatupwa katika ziwa la moto.
Ndugu, hukumu ya Mungu ni ya kuiogopa sana, kwasababu hakuna nafasi ya pili baada ya kifo. Ukifa leo ghafla, ni moja kwa moja jehanamu ukisubiria siku hiyo ya ufufuo ifike, Kwanini hayo yote yatukute? Watu walio kuzimu leo hii Ni kilio na majuto ndivyo vinavyoendelea, wanatamani wangepata hata dakika 2 za kutubu lakini hawana. Wewe muda unao. Lakini unafurahia ulimwengu.
Mgeukie Kristo, leo akusamehe dhambi zako. Tubu kwa kumaanisha kabisa kuuacha ulimwengu na tamaa zake zote. Dhamiria kumfuata Yesu, naye atakuokoa, katika dakika hizi za majeruhi. Kumbuka Unyakuo ni wakati wowote, hilo linafahamika. Muda umeisha, dalili zote zimeshatimia. Mlango wa neema kwa mataifa hivi karibuni utafungwa.
Maran Atha.
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita.
MPINGA-KRISTO
UTAWALA WA MIAKA 1000.
JE MGOGORO WA URUSI NA UKRAINE,UMETABIRIWA KIBIBLIA?
WhatsApp
SWALI: Mwandishi, alimaanisha nini, kusema Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi? (Wimbo 1:5-6)
JIBU: Tusome,
Wimbo 1:5 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. 6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda”.
Wimbo 1:5 “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda”.
Huyu ni mwanamke , anayejaribu kueleza hali yake ya nje jinsi inavyoonekana, ilivyo tofauti na uhalisia wake wa ndani. Anaanza kwa kusema mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Yaani japokuwa naonekana ni mweusi, nisiyevutia, lakini ninao uzuri wa kupendwa hata na mfalme,
Mstari wa 6 anaendelea kueleza Weusi wake, ulitokana na nini,.. Anasema, ulitokana na kazi za mashambani, ambazo aliwekwa kama mlinzi azisimamie, ikiwa na maana muda wote a jua linapochomoza jua linapozama, ni lazima awepo pale alitunze,
Wakati ndugu zake, wakiwa wamestarehe nyumbani kwenye uvuli wa makasri, wakila na kufurahi, yeye yupo mashambani anatanga na jua.
Na kwa kawaida, mtu anayekaa kwenye jua muda mrefu Ngozi yake itakuwa nyeusi tu, na vilevile itapunguza mvuto. Ndicho kilichomkuta huyu binti, aliyekuwa tofauti na mabinti wengine, kama ilivyozoeleka kuwa mabinti huwa hawakai mashambani, wala hawafanyi shughuli za ulinzi, . Lakini yeye alikuwa hivyo, na katika hayo yote anasema bado anaoozuri unaotoka ndani.
Huyu binti anafananishwa na watumishi wa Mungu, wanaotumika katika shamba la Mungu, ambao pengine kutwa kucha wanajitaabisha kuwapelekea wengine Habari njema,(Vijinini na mijini, na kwa njia mbalimbali), sasa kwa taabu hizo, kwa kawaida ni lazima watakosa vitu vingi vyema, kwasababu muda wote wapo mashambani, pengine watakuwa wadhaifu kimwili/au kimwonekano, watakuwa hawana mali, watakuwa hawana mvuto wowote. Lakini Bwana anawaona ni wazuri sana,
Mtume Paulo aliliona hilo akasema,
2Wakorintho 4:16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; 18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
2Wakorintho 4:16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
18 tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
Kuonyesha kuwa utu wetu wa nje, waweza kuchakaa kwasababu ya utumishi, lakini ule wa ndani wafanywa upya kila siku, Sehemu nyingine aliandika Maisha ya utumishi ni ya kufa kila siku, kujitoa kwa wengine na sio kwa ajili yako, kama huyu binti (1Wakorintho 15:31).
Hivyo na wewe ambaye, unamtumikia Bwana kwa uaminifu, pengine wajiuliza, mbona mwonekano wangu haupo, kama nilivyokuwa hapo nyuma simtumikii? Fahamu kuwa upo shambani, jua litakuwa ni lako, lakini uzuri wako unatoka ndani na Mungu anauona, na anapendezwa na wewe.
Siku zitakuja, utapewa mwili wa utukufu, mwili usioonja uharibifu, mwili wa milele, ndipo utakapojua kuwa wewe ulipendwa na Bwana, na hiyo haikuwa kwa mwonekano wako, lakini kwa uaminifu wako.
Shalom.
UBATILI.
KUJIPAMBA NI DHAMBI?
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”?
Kuvyaza ni nini katika biblia? (Ayubu 21:10).
KWANINI MIMI?
ANGALIA UZURI WAKO, USIGEUKE KUWA KITANZI CHAKO.
NJIA NYINGINE YA KUPATA REHEMA NA KIBALI KUTOKA KWA MUNGU.
Sulemani kwa uvuvio wa Roho alipewa kujua kati ya mambo sita yanayomchukiza Mungu, mojawapo ni mikono imwagayo damu za watu.(Mithali 6:17).
Na sehemu nyingi sana katika maandiko utaona Bwana akiwakemea watu wake kwa dhambi hii ya umwagaji damu, kwamfano ukisoma hapa utaona anasema,
Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu. 16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya; 17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane”.
Isaya 1:15 “Nanyi mkunjuapo mikono yenu, nitaficha macho yangu nisiwaone; naam, mwombapo maombi mengi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu.
16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
17 jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane”.
Soma na hapa pia;
Ezekieli 9:9 “Ndipo akaniambia, Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda ni mwingi sana, nayo nchi imejaa damu, nao mji umejaa kupotosha hukumu; maana husema, Bwana ameiacha nchi hii, naye Bwana haoni”.
Sehemu kadha wa kadha, Mungu alipowaona watu wake aliona damu nyingi mikononi mwao.. (Isaya 59:3, Yer 22:3, Eze 23:37, 45).
Sasa ni rahisi kudhani kuwa, katika mwili ni kweli walikuwa ni wauaji, wanawaua watu kwa siri au wanauana wao kwa wao ovyo . Hapana si kweli, Waisraeli hawakuwa hivyo. Kama tu vile walimwengu wengi wasasa walivyo leo.
Hivyo wenyewe hawakuelewa Mungu alikuwa anawaonaje matendo yao kwa jinsi ya Roho,
Hadi Bwana Yesu alipokuja kutufunulia jambo hilo katika agano jipya Mungu alikuwa anamaanisha nini;
Tusome.
1Yohana 3:15 “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake”.
Akaeleza, kwa undani Zaidi, jinsi mtu wa namna hii ambaye, anamchukia ndugu yake, anavyostahili adhabu sawa tu na yule Mhalifu aliyemwaga damu ya mtu.
Mathayo 5:22 “Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto”.
Ndugu unayesoma haya maneno, tufahamu kuwa, tunaweza tukawa ni waombaji wazuri, ni waalimu wazuri, ni wasaidizi wazuri, ni wachungaji wazuri, lakini mbele za Mungu tukawa watu hatari sana, tukaonekana kama wahalifu sugu kabisa, ambao tumeuwa roho za watu wengi sana, mikono yetu inabubujika damu, tumeshika visu, na mapanga, na mashoka, tunaua, na bado tunaendelea kuua watu kila siku. Sababu ni nini? Sababu ni chuki zilizopo mioyoni mwetu kwa watu wengine.
Tunapokuwa na visasi na watu, au hasira, Mungu anatuona tunastahili jehanamu ya moto. Hata sadaka yetu tunayompelekea yeye bado anaiona ni chukizo kubwa sana, ndio maana asema tusiitoe mpaka tutakapopatana kwanza na majirani zetu.
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, 24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.
Mathayo 5:23 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako”.
Hivyo, tujifunze kuachilia, ili tusiwe wauaji, na njia pekee ya kuweza kuishinda hiyo hali, ni kuwa mtu wa kutafakari sana Neno la Mungu. Kwani Neno ni tiba, inayotupa maonyo,na Faraja na ushauri, ukiona hiyo hali inakushinda, fahamu kuwa kiwango chako cha utafakariji wa maandiko ni kidogo..
Lakini tunaposoma lile Neno mfano lile andiko linalosema, ndugu yako akikusoma, mara ngapi umsamehe.. Na Bwana akajibu na kusema, hata SABA MARA SABINI.. Yaani mara 490, kwa siku moja,(Mathayo 18:22) tutagundua ni nini maana ya msamaha.. Ni Zaidi ya vile tunavyofikiria, ni Zaidi ya kuachilia mambo yote, na kukubali kuonekana mjinga, ni Zaidi ya kukubaliana na kila hali. Hapo ndipo tutakapojua hakuna sababu ya kushikamana na kila jambo ndugu zetu au marafiki, au majirani zetu wanayotufanyia, au kutuudhi kwayo.
Kwasababu katika hayo yote hawajawahi kuyarudia mara 490, kwa siku, pengine ni mara mbili tu au kumi. Hivyo tunapaswa tusamehe.
Bwana atusaidie sana, mkono yetu iwe safi kama ya mwanakondoo wake Yesu Kristo.
Ndipo tutakapomkaribia Bwana wetu na kutubariki.
Ayubu 17:19 “Lakini mwenye haki ataishika njia yake, Naye mwenye mikono safi atazidi kupata nguvu”.
RACA
KIFAHAMU KIGEZO CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU UPENDO.
Unyenyekevu ni nini?
JIFUNZE NAMNA YA KULITUMIA NENO LA MUNGU.
JE! DAMU INA UMUHIMU WOWOTE KATIKA MAISHA?
USIWE ADUI WA BWANA
MIAMBA YENYE HATARI.
Kiyama au kiama..maana yake ni ‘siku ya ufufuko’
Neno hilo linapatikana sehemu kadha wa kadha katika biblia. Kwamfano hivi ni baadhi ya vifungu ambavyo utakatana nalo;
Mathayo 22:23-28
[23] Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza, [24]wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao. [25]Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake. [26]Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba. [27]Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye. [28]Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
[23] Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,
[24]wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
[25]Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.
[26]Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.
[27]Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
[28]Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
Hapo ni mafarisayo walitaka kujua kutoka kwa Yesu siku ya ufufuo wa wafu, mambo ya ndoa yatakuwaje.?
Soma pia..Wafilipi 3:10-11
[10]ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; [11]ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
[10]ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake;
[11]ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
Akimaanisha afikie siku ya ufufuko wa wafu.
Neno hilo utalisoma pia katika vifungu hivi;
2 Timotheo 2:17-18,22
[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto, [18]walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.
[17]na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
[18]walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha.
Hivyo na sisi pia hatuna budi kuyaelekeza mawazo yetu katika ufufuo wa wafu..Tumaini hilo ni lazima liwepo ndani yetu. Na ufufuo huo utakuja siku ile ya UNYAKUO ambapo parapanda italia, kisha wafu wote waliokuwa makaburini waliompokea Kristo, watafufuliwa na moja kwa moja wataungana na sisi tuliohai kisha kwa pamoja tutapaa kumlaki Bwana Yesu mawinguni.
Swali la kujiuliza. Je, tumejipangaje kwa ajili ya siku hiyo ya kiyama? Je matendo yetu wanastahili kukubaliwa?
Majibu sote tunayo.
Tukumbuke kuwa Siku ya kiyama ipo karibuni sana.
Shalom
NINI KINATOKEA BAADA YA KIFO?
NA JINA LAKE AITWA, NENO LA MUNGU.
Je mtu akifa anakuwa hana dhambi tena?
Ufunuo 19:11-13 [11]Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. [12]Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. [13]Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Ufunuo 19:11-13
[11]Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.
[12]Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
[13]Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu.
Ulishawahi kujiuliza ni kwanini mahali hapo Yesu hajitambulishi kwa jina lake la asili tulilolizoea, bali anajiita Neno la Mungu,?.
Ipo maana kubwa sana nyuma yake ambayo wakristo wengi hatuijui.
Ni muhimu tufahamu kuwa pale Tunapomtaja YESU, tunamlenga Yesu wa pande mbili.
Wakristo wengi tunaishia kumtambua Yesu kama mtu, jinsi alivyokuwa na mamlaka, na uweza, na maajabu, jinsi alivyosulubiwa na kuzikwa na kufufuka na kupaa juu, na sasa hivi anatawala na kumiliki viumbe vyote vya mbinguni na vya duniani ..jambo ambalo ni zuri sana, kwasababu kwa kumtambua hivyo ndivyo tunavyomwamini na kupokea wokovu na kuponywa shida zetu.
Lakini kosa ni pale tunapoishia kumtambia Yesu-mtu tu, hatutaki kumtambua Yesu kama Yesu-Neno.
Utajiuliza huyu YESU-NENO ni yupi?
Ni Yesu katika maneno yake aliyokuwa anayafundisha. Leo hii ukiweza kuyaishi maneno hayo kikamilifu 100%, basi na wewe unabadilika na kuwa Yesu, mwenyewe.
Kiasi kwamba, wakati mwingine hutahitaji Yesu aje kukusaidia, bali wewe mwenyewe utaweza kufanya, kila kitu.
Wakristo wengi tunampenda Yesu tunapomsoma au kumsikia, lakini hatutaki kuwa kama yeye. Kwasababu tunaona ugumu kuyaishi maneno yake.
Tunafanana na mwanafunzi anayetegemea tu kikokoteo (calculator) kupigia mahesabu yake, lakini kichwani asiwe na maarifa yoyote ya kinachofanyika nyuma ya kikokoteo kile
lakini mtu ambaye anajua kanuni ya kikokoteo, huyo huwa anakuwa ni bora zaidi..kwasababu hata pasipo kuwa nacho anaweza tu kupiga mahesabu yake na kupata majibu. Atakihitaji kwa kurahisisha tu kazi zake, lakini pasipo hicho bado anaweza kufanya.
Lakini hiyo itamgharimu aende shule, ajifunze misingi yote ya hisabati..tofauti na yule mwingine ambaye kazi yake ni kubofya tu. “Jibu hilo hapo!”
Ndivyo ilivyo kwa wakristo wanaomtegemea Yesu-mtu tu, na sio Yesu-Neno. Wanamgeuza Bwana Yesu kama calculator wanamwita awasaidie, lakini hawataki kuyaishi maneno yake..
Sio kila wakati tutamwitaji Yesu atusaidie, wakati mwingine anataka sisi wenyewe tufanye, ndivyo alivyowazoeza pia mitume wake ambao hapo mwanzo walizoelea kumtegemea tu yeye ilihali hawazingatii maneno yake
Mathayo 17:17
[17]Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, kilichopotoka, nitakaa pamoja nanyi hata lini? Nitachukuliana nanyi hata lini? Mleteni huku kwangu.
Wakati mwingine tunamwita Yesu, atusaidie, na anakaa kimya hafanyi chochote..tunaita usiku kucha hajibu lolote. Ni kwasababu gani? Ni kwasababu hatutaki kuliishi Neno lake.
Kwamfano: mmoja anaweza akawa anafunga na kukesha kumlilia Yesu ampe mali (kwasababu anamjua Yesu-mtu anaweza yote)..lakini huku anaendelea na mambo yake ya kidunia.. Na mwingine akalizingatia lile Neno la Yesu linalosema;
Mathayo 6:32-33
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. [33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
[32]Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
[33]Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
Huyu wa pili, anaweza asimtaje Yesu wala mali mahali popote, lakini akapokea hitaji lake, kwasababu tu kajua kanuni ya roho.. Lakini yule wa kwanza kupewa/kutokupewa ni juu ya Yesu mwenyewe..sio juu yake.
Hivyo tujifunze kuyaishi maneno ya Yesu, kwamfano tunapoambiwa tusamehe huyo ndio Yesu-Neno., tunapoambiwa tusizini ndiye Yesu Neno.
Na Yesu mwenyewe alitusisitizia kwamba maneno yake yakiwa ndani yetu, basi tukiomba lolote yeye atatupa.
Yohana 15:7
[7]Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Bwana akubariki.
“Yodi” ni nini kama tunavyoisoma katika Mathayo 5:18?
BASI MUNGU ALIMWADHIMISHA MNO.
UNAMCHUKULIA YESU KWAKO KAMA NANI?
HUTATAMBUA LOLOTE, SIKU YA UNYAKUO IKIFIKA.
Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?.
SWALI: Je ni kweli, mpagani akioa au akiolewa na yule aliyeamini, na yeye pia anahesabiwa kuwa mkamilifu kulingana na mstari huu?
1Wakorintho 7:13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu
1Wakorintho 7:13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu
JIBU: Ifahamike kuwa hakuna mtu anayehesabiwa mkamilifu kwa ukamilifu wa mtu mwingine. Maandiko yapo wazi katika hilo; yanasema kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe, na kila mtu atatoa Habari zake mwenyewe siku ile, mbele za Mungu (Wagalatia 6:5, Warumi 14:12).
Lakini je! Mstari huo unamaanisha kwamba ikiwa umeolewa au kuoa mtu aliyeamini, hata kama wewe ni mtenda dhambi utahesabiwa mtakatifu kwa yeye?na ukifa utaenda mbinguni? Jibu ni hapana, ukisoma vifungu vya chini yake kidogo utaelewa vizuri..Tusome..
1Wakorintho 7:12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache. 13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe. 14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu. 15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani. 16 KWA MAANA WAJUAJE, WEWE MWANAMKE, KAMA UTAMWOKOA MUMEO? AU WAJUAJE, WEWE MWANAMUME, KAMA UTAMWOKOA MKEO”?
1Wakorintho 7:12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.
14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.
15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.
16 KWA MAANA WAJUAJE, WEWE MWANAMKE, KAMA UTAMWOKOA MUMEO? AU WAJUAJE, WEWE MWANAMUME, KAMA UTAMWOKOA MKEO”?
Paulo anamaanisha kwamba, ikiwa wewe umeamini, na mwezi wako hajaamini, hupaswi kumuacha na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine. Bali unapaswa kuendelea kuishi naye ikiwa tu bado yupo radhi kuwa nawe. Kwasababu kwa kufanya hivyo ni rahisi yeye kuvutwa kwenye Imani yako, ikiwa ataona mwenendo wako mzuri,.. Na kwa matokeo hayo Paulo anasema ni nani ajuaje na yeye atashawishwa kuokoka kama wewe?
Na ni kweli ukisikiliza shuhuda za ndoa nyingi zilivyomrudia Mungu, utasikia moja inakuambia Baba aliokoka baada ya mkewe kuwa mcha Mungu, au mama alimrudia Mungu baada ya mumewe kuokoka. Umeona? Lakini hilo haimaanishi kuwa moja kwa moja ndio tayari na yeye kaokoka,kisa tu mwenzake kaokoka hata kama ataendelea kutenda dhambi, hapana.
Wanaweza wakakaa hivyo, na bado mmoja akaendelea kutokuamini hadi kifo na kuzimu akaenda. Lakini hiyo nayo hutokea mara chache, ikiwa kweli huyo mwenzi mwingine, anaishi Maisha ya haki, na ya kumpendeza Mungu, na ya kumwombea kwa bidii mwenzake.
Lakini pia ni lazima tufahamu kuwa biblia hairuhusu, mkristo kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini. Mazingira yanayozungumziwa hapo, ni yale ambayo wokovu umemkuta tayari yupo kwenye ndoa ya namna hiyo. Leo hii kumekuwa na migogoro mingi ya kindoa, kwasababu ya maamuzi mabaya, yanayofanywa na wakristo, ambao hawazingatii maagizo ya Mungu yaliyosema tusifungwe nira Pamoja na wasioamini (2Wakorintho 6:14).
Ulinzi wa kwanza unapaswa uwe katika Imani yako, sio katika familia. Hivyo ikiwa bado hujaoa/ au hujaolewa, Imani ndio iwe ni kipimo cha kwanza cha kumtambua mwenzi sahihi. Lakini wewe ambaye tayari upo kwenye ndoa ya namna hiyo. Unalojukumu la kumvuta huyo mwenzi wako, kimatendo, kimaombi, na kimafundisho. Kwasababu huwezi jua kama atavutwa au la!.
Bwana akubariki
NDOA NA TALAKA:
KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)
NDOA NI NINI?
Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?
Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?
JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?
NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.
Wapo wanatofautisha maneno haya mawili, na wapo wanayoyaona kama ni kitu kimoja..
Ni kweli Bwana Yesu alituonyesha kuwa “maandiko na Neno” la Mungu ni kitu kilekile kimoja, na ndivyo ilivyo..
Soma Yohana 10:35
Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);
Isipokuwa tofauti yao ndogo ni kwamba maandiko yanajifunga tu katika maandishi.. lakini Neno la Mungu, ni aidha katika maandishi au kuzungumzwa.
Bwana anaweza kutoa ujumbe wake kwa sauti kinabii, vilevile anaweza kuzungumza kwa biblia (maandiko). Na zote zikawa sauti zake zenye majibu.
Lakini tulichopewa, na tunapaswa tukitegemee sana ni Neno la Mungu katika maandiko, alisema, “maandiko hayawezi kutanguka”, yaani kilichoandikwa kimeandikwa. Lakini Neno lake katika sauti anaweza kulitangua mwenyewe, au akaghahiri, au likawa la muda tu, tofauti na Neno katika maandishi.
Hivyo ukiishi kwa hilo, utakuwa salama. Lakini tukiwa wavivu wa kujifunza biblia. Tuwe na uhakika kuwa tunapoteza maisha yetu.
Marko 12:24
[24]Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?
Tupende Biblia zaidi ya chakula, tuone kuwa hatuwezi kuishi bila hilo; Daudi alisema.
Zaburi 119:140
[140]Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
Tuyapende maandiko, kwani ndio uhai wetu.
Gombo ni nini?
Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)
Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?
Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?
Nini maana ya “Torati na manabii”?
Yeshuruni ni nani katika biblia?
URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?
“Unyakuo wa kanisa umepita leo!. Hakuna tena toba”
Je taarifa hizi zimekushtua??.
Hebu jiulize Siku taarifa hizi zitakapokuwa kweli utakuwa katika hali gani? Mpaka sasa, unyakuo bado, haujatokea lakini siku utakapotokea utakuwa katika hali gani, utakapopewa taarifa kuwa watakatifu wamenyakuliwa na wewe umewachwa???..
Je utashtuka kama ulivyoshtushwa leo au utaona kawaida?.
Kama umeshtuka leo, hiyo ni kuonyesha kuwa wewe hupaswi kuwa wa ulimwengu, nyumbani kwako sio huku..ndio maana umeshtuka na kuogopa kusikia umeachwa!. Rudi leo utubu kwasababu Siku hiyo pengine utaamka asubuhi na kukutana na hizo taarifa “Unyakuo umepita”..ukikumbuka kuwa masaa kadhaa tu nyuma yaliyopita, ulisikia mahubiri na ulipuuzia.
Tubu leo hii na umpokee Yesu, kwasababu ni kweli upo karibuni kutokea.
Kama leo hii utatamani kumpa Yesu maisha yako, basi piga namba hizi, tuweze kuomba pamoja na kukuongoza sala ya Toba. 0789001312.
SWALI: Yohana alimaanisha nini aliposema..10]Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?
Je hiyo siku ya Bwana ni ipi? Na kwanini itajwe pale?
Ufunuo wa Yohana 1:10
[10]Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
JIBU: Mtume Yohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo, kwa ajili ushuhuda wa Kristo, Na kwa mara ya kwanza alipotokewa na Bwana Yesu na kuonyeshwa mambo yanayohusiana na siri za siku za mwisho na kanisa, anasema siku hiyo aliyotokewa iliangukia siku ya Bwana.
Ikumbukwe kuwa tangu awali wakristo wa kwanza, waliifanya siku ya kwanza ya juma( Yaani jumapili) kuwa ni siku ya Bwana, kufuatana na tukio la kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Na ni siku ambayo Bwana alikuwa akiwatokea wanafunzi wake (Soma Marko 16:9, Yohana 20:19 ).
Vilevile Siku hii hii ndio siku ambayo kanisa lilipokea ahadi ya Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza..Kwahiyo watakatifu wote, tangu enzi za mitume, hadi wakati wetu huu wa sasa waliifanya siku hii kuwa ni siku ya Bwana.
Soma vifungu hivi;
Matendo ya Mitume 20:7
[7]Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
1 Wakorintho 16:2
[2]Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;
Na ndio hapa sasa tunaona mtume Yohana anaeleza Kwamba alipokuwa katika Roho, siku ya Bwana (yaani jumapili) ndio alitokewa na maono hayo..
Zingatia: Mtazamo ambao siku hiyo ilikuwa ni jumamosi, si sahihi. Jumamosi, haikuwahi kuadhimishwa na wakristo wa kwanza kwa shughuli rasmi za kibada, kwa mujibu wa maandiko.
Sio kwamba Bwana anaithamini jumapili, zaidi ya siku nyingine zote, hapana au siku hiyo ni takatifu zaidi ya nyingine zote, Hapana bali anachotaka kutuonyesha ni umuhimu wa siku tunazoziweka wakfu kwa ajili yake kwamba anaziheshimu na kwamba kwa kupitia hizo, ni rahisi yeye kujifunua kwetu.
Ikiwa siku yetu kwa Bwana ni jumamosi, basi tuithamini kwa kuwa katika Roho kama vile Yohana alivyokuwa mpaka Kristo akamtembelea siku hiyo..
Kama ni jumapili, tuifanye vivyo hivyo, kama ni jumatano tuipe heshima yake. Hizi siku tusizichukulie juu juu tu,
Lakini leo hii tunapuuzia ibada kuu za kila wiki (Jumapili), tunakosa mafundisho ya biblia kanisani, au hata tukienda siku hiyo hatuwi katika roho, tunaenda ili kutimiza tu wajibu . Halafu tunataka Bwana ajidhihirishe kwetu tunapokuwa nyumbani tunaangalia tv.
Kamwe Usiruhusu, siku yako ya ibada iliwe na uvivu au mambo ya ulimwengu huu, kama vile anasa, na mihangaiko ya dunia, hata kama upo katika mazingira ambayo hayana watakatifu..Nenda milimani huko, au maporini ukasome biblia na kuomba kama Yohana..kuliko kumwachia shetani akupangie ratiba zake kwenye siku takatifu ya Bwana..
Ithamini siku ya ibada. Na kwa hakika atajidhihirisha kwako.
Ubarikiwe.
Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?
Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?
UFUNUO: Mlango wa 1
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?
JIWE LILILO HAI.