Swali: Katika biblia tunasoma sehemu kadha wa kadha zikiwataja “wana wa manabii”.. Je! Hawa wana wa manabii walikuwa ni watu gani?, na kazi yao ilikuwa ni ipi? Na kwanini waliitwa hivyo?.. Na je hata leo kuna wana wa manabii?
Jibu: Ni kweli Katika Agano la kale lilikuwepo kundi la watu waliojulikana kama Wana wa Manabii. (Soma 1Wafalme 20:35, 2Wafalme 6:1, 2Wafalme 4:1, na 2Wafalme 2:5).
Watu hawa walikuwa ni “manabii wa Mungu”, ambao walijitia katika kifungo cha kujifunza juu ya Nabii zilizotangulia kabla yao..
Kumbuka sio kujifunza jinsi manabii wanavyoishi au wanavyokula au wanavyoona maono!… La! Hakuna mwanadamu yeyote anayeweza kumfundisha mtu mwingine namna ya kuona maono!…hivyo ni vipawa vya Mungu ambayo ni Mungu mwenyewe anaviweka ndani ya mtu, na hatujifunzi wala hatufundishwi.. Ni sawa na ndoto…
Hakuna mtu anayeweza kumfundisha mwenzake jinsi ya kuota!.. Ndoto zinakuja zenyewe, kwasababu ni vipawa vya asili ambavyo Mungu kaviweka kwetu sote.. Na nabii za Mungu, zinawajia watu maalumu ambao Bwana kawachagua, na si kupitia kujifunza!.
Kwahiyo hawa wana wa manabii, au kwa lugha nyingine “Wanafunzi wa manabii” walikuwa ni watu waliojikita kujifunza Nyakati na Majira, Pamoja na Nabii zilizotangulia kutolewa na manabii wengine waliowatangulia..(kumbuka walikuwa wanajulikana kama wana wa manabii, na sio wana wa NABII!)..
Na lengo la kufanya hivyo (yaani kupokea maarifa hayo) ni ili wawe salama, na wawe na uhakika wa Nabii watakazozitoa isije wakapotoka na kutoa unabii wa uongo.
Kwa mfano Nabii anaweza kuona maono au kupata ujumbe kuhusu Taifa la Israeli, sasa ili authibitishe ujumbe ule au ono lile kama kweli ni kutoka kwa Bwana, ni sharti awe na Nabii nyingine za kutosha, za waliomtangulia zinazosapoti ono lake hilo jipya!.. Na akija kugundua kuwa Nabii mwingine, mkuu aliyetangulia alishatabiri jambo kama hilo au linalokaribiana na hilo… basi ndipo Ono lake hilo linathibitika… lakini akija kukuta ono lake linakinzana na maono ambayo manabii wakuu waliyatoa, ndipo analiacha, kwasababu sio kutoka kwa Bwana… (kwasababu kamwe Bwana hawezi kujipinga katika maneno yake).
Hivyo ndio maana ilihitajika shule ya manabii, ambayo lengo lake ni kujifunza kujua Nabii zilizotangulia juu ya watu, na mataifa…
Ili tuzidi kuelewa vizuri, utakumbuka kipindi cha Nabii Yeremia wakati anatabiri kwamba Israeli watachukuliwa utumwani kwenda Babeli.. utaona Yeremia alikuwa ni mtu mwenye elimu ya kutosha kuhusu Nabii zilizotangulia, alihakiki jumbe anazozipokea katika maono, kwa nabii za waliomtangulia kama wakina Isaya, na wengineo..
Na jambo moja utaona alilojifunza ni kuwa “Manabii karibia wote, hawakuwahi kutabiri juu ya amani kwa mataifa, manabii wengi walikuwa wanatabiri juu ya Vita na Mabaya na Tauni”.. Na Yeremia alijua Mungu hawezi kujipinga.. Hivyo maono yake aliyahakiki kwa namna hiyo..
Lakini utaona alitokea mtu anaitwa Hanania, ambaye alijitokeza na kuanza kutabiri juu ya Amani kwa Israeli kwamba hawataenda utumwani, watakuwa salama, ni ilihali Taifa zima limemwacha Mungu..jambo ambalo linakinzana na Nabii Mungu alizozitoa kupitia manabii wakuu waliotangulia… Na Yeremia kuliona hilo akamwambia Hanania maneno yafuatayo…
Yeremia 28:7 “Lakini lisikilize sasa neno hili nilisemalo, masikioni mwako, na masikioni mwa watu wote,
8 MANABII WALIOKUWAKO KABLA YA ZAMANI ZANGU, NA ZAMANI ZAKO, WALITABIRI JUU YA NCHI NYINGI, NA JUU YA FALME KUBWA, HABARI YA VITA, NA YA MABAYA, NA YA TAUNI”.
Umeona jambo Yeremia alilomwambia huyu Hanania?…
Yeremia alikuwa ni Mwana wa manabii, lakini Hanania alikuwa ni mtu tu aliyejizukia na kujiita Nabii, hana elimu yoyote ya Nabii za Mungu.. na akaanza kuwafariji watu kwa maneno ya uongo!..Jambo ambalo lilimchukiza sana Mungu, na hata kumwua Hanania.
Yeremia 28:15 “Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, Sikia sasa, Ee Hanania; Bwana hakukutuma; lakini unawatumainisha watu hawa maneno ya uongo.
16 BASI BWANA ASEMA HIVI, TAZAMA, NAKUTUMA UENDE ZAKO TOKA JUU YA USO WA NCHI; MWAKA HUU UTAKUFA, KWA SABABU UMENENA MANENO YA UASI JUU YA BWANA.
17 BASI NABII HANANIA AKAFA, MWAKA UO HUO, MWEZI WA SABA”.
Lakini leo hii shetani kaligeuza hili Neno “Wana wa Manabii”. Leo hii kuna watu wamefungua vyuo vyao, wakiwa wenyewe wanajiita Manabii wakuu, na vijana wao wanawaita “wana wao (yaani wana wa manabii)”.. Lakini ukiingia katika madara yao na kusikia wanachofundishwa, ni huzuni tupu!.
Utasikia wanachofundishwa ni jinsi ya kuona maono, jinsi ya kutumia na kutengeneza mafuta na chumvi na mengineyo, utaona wanafundishwa mtindo wa maisha na mtindo wa kuongea, na kuvaa kama nabii mkuu wao, na jinsi ya kumwogopa na kumtukuza baba yao, nabii mkuu..
Na watasomea hata miaka 5 na wakitoka hapo wanapewa na vyeti, tayari wakufunzi!!!..
Ndugu! Huo ni uongo wa shetani…
Wana wa manabii katika Agano la kale, hawakufundishwa wala hawakuwa wanajifunza mitindo ya kuongea ya manabii waliowatangulia…wala walikuwa hawajifunzi jinsi ya kuona maono! (kwasababu tayari walikuwa na hiyo karama, ndio maana wakaitwa manabii)..Walichokuwa wanajifunza ni Nabii zilizotangulia zinazohusu wakati waliopo wao, na za mataifa mengine, kuanzia zilizoandikwa katika Torati ya Nabii Musa, mpaka wakati waliopo wao, ili kusudi wasije wakapotoka na maono waliyokuwa wanayapokea.
Na sisi leo hii wote ni wana wa Manabii.. ambao manabii wetu si baba zetu wa kiroho!!! Wala si maaskofu wetu, bali ni MITUME WA KWENYE BIBLIA, na MANABII WA KWENYE BIBLIA!!!...Tunatembea katika Nabii walizozitoa hao, wakina Musa, Isaya, Yeremia, Habakuki, na mitume wakina Petro, Yohana, Paulo n.k.. (Na nabii zao hazijawahi kukinzana),Kwasababu walikuwa na Roho mmoja.
Kwamfano Nabii Isaya alitoa unabii ufuatao..
Isaya 13:6 “Pigeni kelele za hofu; maana siku ya Bwana i karibu; itanyesha kama maangamizi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu”.
Nabii Yoeli naye alitoa unabii kama huo huo katika Yoeli 3:14, na manabii wengine wote walitabiri hayo hayo…
Kwahiyo ili sisi tuhesabike kuwa “Wana wa manabii” ni lazima maono yetu tunayoyaona katika ndoto, au kwa wazi, ni lazima yapatane na huo unabii wa Isaya, na Yoeli na wengineo katika biblia!… usipopatana na huo unabii wa Isaya basi hilo Ono au huo Unabii ni wa UONGO!!! Ni kutoka Kuzimu!!!...
Tukiota au tukiona maono ambayo yanatuonyesha au kutuambia kuwa “Tufurahi, tupige kelele za shangwe, kwasababu siku ya Bwana bado sana”..basi hilo ni Ono kutoka kuzimu!!!..
Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba wana wa manabii, ni manabii ambao walikuwa wamejikita katika kusoma Nabii za manabii wa Mungu waliowatangulia, ili wasifanye makosa katika kutoa nabii zao.
Na sisi ni lazima tuwe wanafunzi wa biblia, turejee biblia katika kuhakiki kila kitu, na hatupaswi kuamini tu kila jambo ambalo tunalipokea katika ndoto au maono.
Bwana Yesu na atusaidie sana.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
UJUE UCHAWI WA MANABII WA UONGO?.
Nini maana ya “Torati na manabii”?
Marko 5:12 “Pepo wote wakamsihi, wakisema, Tupeleke katika nguruwe, tupate kuwaingia wao.
13 Akawapa ruhusa. Wale pepo wachafu wakatoka, wakaingia katika wale nguruwe; NALO KUNDI LOTE LIKATELEMKA KWA KASI GENGENI, wakaingia baharini, wapata elfu mbili; wakafa baharini”.
“Genge” linalozungumziwa hapo sio lile linalotengenezwa kwaajili ya biashara za mboga mboga, au matunda..Bali Neno “genge” ni Kiswahili kingine cha “Mteremko wa mwamba”..Ipo miteremko ambayo chini ni udongo, lakini pia ipo miteremko ambayo chini ni mwamba…sasa hiyo ambayo chini ni mwamba, ndiyo inayoitwa “Genge”
Kwahiyo hapo biblia iliposema kuwa wale Nguruwe waliteremkia kwa kasi gengeni, ilimaanisha walishuka kwa kasi katika mteremko huo unaoelekea ziwani.. Na tofauti na miteremko ya kawaida na ile ya miamba..ni kwamba miteremko ya miamba INAKUWA INATELEZA!, kiasi kwamba mnyama au mtu au kitu kikianza safari ya kuelekea huko basi kwa haraka sana kitakuwa kimefika hitimisho…Ndio maana hao nguruwe biblia inataja WALISHUKA KWA KASI…
Kufunua ni jinsi gani mapepo yanavyowapeleka watu mahali ambapo si sahihi, na tena kwa haraka sana…Leo hii mtu akiingiwa na mapepo basi, hitimisho lake litakuwa ni KIFO, kama hayatamtoka. Na hakuna pepo lolote lisilotoka endapo mtu akimaanisha kuamua limtoke. Kwasababu hakuna lililo kubwa kwa Mkuu wa Uzima Yesu, na zaidi sana miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu na si mapepo. Kwahiyo tunazo haki zote za kudai uzima na haki zote za kumpokea Roho Mtakatifu endapo tutamhitaji..
Na kanuni za kupokea Roho Mtakatifu ni hii..
Matendo 2:37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie”.
Je umetubu na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu?
Maran atha!
Mada Nyinginezo:
JE UNA MATUMAINI YA KUPATA TENA KILE ULICHOPOTEZA?
Kwanini Bwana aliwalenga mbwa na nguruwe tu katika Mathayo 7:6?
Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”
Kombeo ndio hiyo hiyo teo, ni moja ya silaha ya kurusha iliyotumika zamani katika vita.
Kombeo/teo ilitengenezwa kwa Ngozi au Kamba, na jiwe lilikuwa likiwekwa katikati yake na kurushwa kumwelekea adui. Kwa ulimwengu wa sasa Silaha ya manati ndio inayotumika kama mbadala ya teo.
Hivi ni vifungu ambavyo utakutana na neno hilo;
Waamuzi 20:16 “Katika watu hao wote walikuwako watu waume mia saba waliochaguliwa, wenye shoto; kila mmoja alikuwa anaweza kuutupia unywele mawe kwa teo, wala asikose”.
Maana yake ni kuwa jeshi la Benyamini, lilikuwa na watu mia saba ambao wakuwa na shabaha ya hali ya juu sana ya kuweza kurusha mawe kwa kombeo/teo bila kukosea.. Biblia imetumia mfano wa ‘kulengwa kwa unywele’, jinsi ulivyo mdogo, kuonyesha kiwango cha shabaha cha hawa watu kilivyokuwa cha juu sana.
Utasoma pia andiko hilo katika vifungu hivi;
1Nyakati 12:2 “Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kuume na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini”.
2Wafalme 3:25 “Wakaibomoa ile miji; wakatupa katika kila mahali palipo pema kila mtu jiwe lake, wakapajaza; wakaziziba chemchemi zote za maji, wakaikata miti yote iliyo mizuri; mpaka katika Kir-haresethi tu wakayasaza mawe yake; ila wenye kombeo wakauzunguka wakaupiga”.
Lakini pia katika biblia tunaona, hii ilikuwa ni silaha maarufu aliyoitumia Daudi kumwangusha adui yake Goliathi..
1Samweli 17:40 “Akaichukua fimbo yake mkononi, akajichagulia mawe laini matano katika kijito cha maji, akayatia katika mfuko wa kichungaji aliokuwa nao, maana ni mkoba wake, na kombeo lake alikuwa nalo mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti…
49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi”.
Tunaona Daudi alipopewa, mikuki, na mapanga, na mishale, Silaha zenye ufanisi wa hali ya juu wa kivita, yeye hakutaka, bali alichagua kombeo lake na mawe matano. Alikubali kutumia silaha dhaifu, ili tumaini lake lisiwe katika silaha alizonazo bali katika Bwana ndio maana akasema..
1Samweli 17:45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. 46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti.
Hata sasa, hatupaswi kutegemea nguvu zetu, kushindana au kupambana na hali au majaribu mazito yanayotukabili mbele yetu.. Wengi wakiona hali imekuwa ngumu, wanachowaza ni moja kwa moja kutafuta fedha nyingi ili waweza kukabiliana na shida zao, ndugu ni heri umtegemee Bwana, amini katika hicho hicho kidogo ulichonacho, kwamba Bwana anaweza kukitumia hicho kukupa ushindi mkuu.
Mwingine atakuambia ukikosa elimu, hutoweza kufanikiwa, au kumtumikia Mungu. Ni kweli elimu ni nyenzo nzuri ya kukufikisha mahali Fulani pazuri, lakini isipokuwa na Mungu nyuma yake ni bure. Wewe usiyekuwa na elimu ya kutosha ukimtumikia Bwana kwa uaminifu, utafanikiwa hata Zaidi ya wale wenye elimu kubwa.
Kombeo hilo Bwana alilokupa lielekeze tu kwa Bwana, na yeye mwenyewe atakuonyesha maajabu.
Zaburi 20:7 “Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la Bwana, Mungu wetu”.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kigao ni nini? Na Je kinafunua nini kwa agano jipya?
Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?
Kibanzi na Boriti ni nini kama tunavyosoma kwenye biblia?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
Luka 8:26 “Wakafika pwani ya nchi ya Wagerasi, inayoelekea Galilaya.
27 Naye aliposhuka pwani, alikutana na mtu mmoja wa mji ule, mwenye pepo, HAKUVAA NGUO SIKU NYINGI, wala hakukaa nyumbani, ila makaburini.
28 Alipomwona Yesu alipiga kelele, akaanguka mbele yake, akasema kwa sauti kuu, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi usinitese”.
Tabia mojawapo ya mtu mwenye pepo ni KUTOKUVAA NGUO KABISA, au KUVAA NUSU UCHI!.
Ukiona unapenda kuviweka wazi viungo vya mwili wako, na hata hujisikii vibaya…fahamu kuwa hiyo ni dalili ya kuwa na Pepo ndani yako!..Na tabia nyingine ya mtu mwenye pepo ni kuwa “Anakuwa Mkali sana”..pindi anapotaka kusaidiwa..
Mathayo 8:28 “Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, WAKALI MNO, hata mtu asiweze kuipitia njia ile”.
Ukiona unachukia sana, unapoambiwa kwamba mavazi unayovaa si ya kujisitiri, basi hiyo ni dalili ya kwamba unalo pepo ndani yako!, ambalo linapaswa litoke.
Ukiona unakasirika au unakuwa mkali unapoambiwa kuwa vimini unavyovivaa, au suruali unazozivaa(mwanamke) ni dhambi, basi tafuta msaada wa haraka ili kusudi hayo mapepo yaweze kukutoka, kwasababu katika hali ya kawaida, mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa nusu tupu na akatembea hivyo barabarani na akajiona yupo sawa…
Ishara ya kwanza ya Yule mtu kutokwa na mapepo ni yeye kuvaa nguo, na kuwa akili zake timamu.
Marko 5:15 “Wakamwendea Yesu, wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, AMEVAA NGUO, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa”.
Je wewe mwanamke/mwanaume hapo kazini ulipoketi, au hapo shuleni ulipo sasa, au hapo kanisani unaposhiriki sasa je umevaa Nguo?..umejisitiri?, je kifua chako kimefunikwa au kipo wazi?..je mgongo wako umefunikwa au upo wazi?.. Je mapaja yako yamefunikwa au yapo wazi?, je tumbo lako limefunikwa au lipo wazi?.. Kama mwili wako haujasitirika! Basi ni ishara kuwa unayo mapepo na huna akili timamu (mapepo yameondoa ufahamu wako).
Lakini kama sehemu za juu za mikono yako zipo wazi, au kifua chako au mapaja yako, au umevaa nguo lakini inachora maungo yako, kiasi kwamba hauna tofauti na mtu aliye uchi kabisa, basi fahamu kuwa UNAYO MAPEPO NA PIA HUNA AKILI TIMAMU, na zaidi sana ukiona unakasirika unapoyasikia haya maneno, basi ndio uthibitisho wa mwisho kuwa Mapepo yapo ndani yako!.. na hivyo unahitaji msaada.
Na habari njema ni kwamba, msaada huo unaweza kuanza kuupata hapo hapo ulipo.
Unachopaswa kufanya sasahivi ni kudhamiria KUTAKA MSAADA WA KUTOKANA NA HAYO MAPEPO!... Na unadhamiria kwa Kumpokea Bwana Yesu maishani mwako..(Usiseme tayari nilikuwa nimeshampokea!)…Ulikuwa bado hujampokea ndio maana ulikuwa unaona upo sawa kukaa nusu uchi!!.. Bwana Yesu angekuwa ndani yako, usingekuwa hivyo ulivyo sasa!!… Wewe sasahivi ndani yako yapo mapepo ambayo yanakufanya UKAE UCHI!!.
Kwahiyo unapaswa pale ulipo ujitenge wewe binafsi, uombe toba!, kwa kudhamiria kuacha njia mbaya…kutubu dhambi maana yake ni pamoja na kuacha vyote ulivyokuwa unavifanya, maana yake leo leo nenda kachome vimini vile, na suruali zile unazozivaa, na anza kuvaa nguo kamili, kwa kufanya hivyo utakuwa umeonyesha kwa vitendo kwamba hutaki tena mapepo ndani yako, na akili itakurudia, na utaona kweli ulikuwa vifungoni.
Baada ya kufanya hivyo nenda katafute ubatizo sahihi, ubatizwe upya, na ubatizo wa kibiblia ni ule wa jina la Yesu na wa maji mengi, baada ya hapo Roho Mtakatifu atashuka juu yako na kukusafisha kabisa..
Maran atha!
Mada Nyinginezo:
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia, Neno la Mungu wetu, ambalo ni Mwanga wa njia zetu na taa iongozayo miguu yetu! (Zab 119:105).
Si watu wote waliokuwa wanamfuata Bwana au waliokuwa wanamjua Bwana walikuwa wanafunguliwa au kuponywa magonjwa yao!.. Wengi walikuwa hawafunguliwi..Na hiyo ni kwasababu walikuwa hawana HAJA YA KUPONYWA!.. aidha kutokana na kwamba hawamwamini, au walimdharau!.
Luka 9:11 “Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, AKAWAPONYA WALE WENYE HAJA YA KUPONYWA”.
Utaona pia kipindi Bwana Yesu anaenda Galilaya, hakufanya miujiza mingi huko kutokana na kwamba watu hawakumwamini..
Mathayo 13:53 “Ikawa Yesu alipoimaliza mifano hiyo, alitoka akaenda zake.
54 Na alipofika nchi yake, akawafundisha katika sinagogi lao, hata wakashangaa, wakasema, Huyu amepata wapi hekima hii na miujiza hii?
55 Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
56 Na maumbu yake wote hawapo hapa petu? Basi huyu amepata wapi haya yote?
57 Wakachukizwa naye. Yesu akawaambia, Nabii hakosi kupata heshima, isipokuwa katika nchi yake, na nyumbani mwake mwenyewe.
58 WALA HAKUFANYA MIUJIZA MINGI HUKO, KWA SABABU YA KUTOKUAMINI KWAO”.
Umeona hapo?..hakufanya miujiza mingi, kwasababu moja tu!..walimdharau na hawakumwamini!
Vile vile utakumbuka kipindi Bwana Yesu ameingia katika lile eneo lenye birika la Bethzatha..ijapokuwa mule ndani kulikuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ambao walihitaji kupona…lakini wengi wao hawakuwa na haja ya kuponywa na Bwana Yesu…wenyewe akili zao na tumaini lao lilikuwa katika yale maji yaliyoaminika kwa wakati huo kama MAJI YA UPAKO!!.
Bwana akawa anapita katikati ya wagonjwa hao…pengine akakutana na baadhi na kuwauliza kama wanataka kuponywa na pengine hata hawakumjibu neno, au walimdharau na kumfukuza..lakini alipokutana na mmoja na kumwuliza kama anataka kuwa mzima, akakiri kuwa anataka kupona lakini hakuna mtu wa kumtia birikini..Na Bwana Yesu akamwambia asimame ajitwike godoro lake aende..na alipotii na kuamini Neno hilo akawa mzima!.. Lakini wale wengine waliendelea kusubiri Maji yale yachemke..
“1 Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, ALIMWAMBIA, WATAKA KUWA MZIMA?
7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
8 YESU AKAMWAMBIA, SIMAMA, JITWIKE GODORO LAKO, UENDE.
9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo”.
Je na wewe una haja ya kuponywa roho yako na mwili wako leo?. Basi usijitumainishe katika maji wanayoyaita ya upako, au chumvi wanayoiita ya upako, au mafuta wanayoyaita ya upako.. Mwamini Bwana Yesu leo na maneno yake na pia chukua hatua ya kusimama.
Huenda umeshatumia hayo maji sana, au mafuta kwa muda mrefu lakini hujaona matokeo yoyote…leo hii yageukie maneno ya Bwana YESU katika biblia, yanayosema.. “KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA (ISAYA 53:5)” Wala usiuangalie umati..ukiona mahali pana umati mkubwa wa wagonjwa, ambao hawajapona matatizo yao lakini wanatumainia vitu kama maji, kuwaponya!..fahamu kuwa hapo ni Bethzatha kiroho!.. Uponyaji kutokea ni bahati sana (tena ni kwasababu tu ya huruma za Mungu, na wala si kwasababu vitendea kazi hivyo vina upako)…ndio maana utaona sehemu kama hizo zina msururu wa wagonjwa ambao hawajafunguliwa, lakini wenye matumaini ya kufunguliwa siku moja.. Mahali ambapo Bwana Yesu yupo, hakuna mlundikano wa wagonjwa… kwasababu yeye ni mponyaji na sio daktari!.
Leo hii kwa imani tupa hayo mafuta, tupa hayo maji, halafu liamini hili Neno la Bwana Yesu..halafu subiria uuone muujiza kwa macho yako!. Utashangaa huko kwenye maji ulikuwa unafanya nini siku zote!..
Bwana Yesu akubariki.
Mada Nyinginezo:
Nini maana ya kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua (Mithali 13:12)?.
MADHARA YA KUKOSA MAJI YA UZIMA BAADA YA KIFO.
Liwali ni mkuu wa mji au jimbo Fulani. (Gavana).
Kwamfano katika biblia tunaona, Pontio Pilato anatajwa kama Liwali wa Uyahudi sehemu ya kusini mwa Israeli,. Hivyo eneo lote la uyahudi yeye ndiye alikuwa kama mkuu wa majimbo hayo.
Mwingine ni Yusufu, biblia inasema, Farao alimweka kama Liwali wa nchi yote ya Misri.
Mwanzo 42:6 “Naye Yusufu alikuwa ni liwali juu ya nchi, ndiye aliyewauzia watu wote wa nchi. Nao ndugu zake Yusufu wakaja, wakainama kifudifudi mbele yake”.
Hivyo kazi yao haswaa ilikuwa ni sawa na ya wakuu wa mikoa wa sasa, au majimbo, ambapo kimsingi wanakuwa na mamlaka ya kuongoza shughuli zote za jimbo hilo kwa amri yao, wala hakuna chochote kinachoweza kufanyika bila idhini yao.
Hivi ni baadhi ya vifungu vya Zaida ambavyo utaweza kukutana na hilo neno;
Mathayo 27:1 “Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa liwali.
Mathayo 28:14 “Na neno hili likisikilikana kwa liwali, sisi tutasema naye, nanyi tutawaondolea wasiwasi.
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo”.
Matendo 13:6 “Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu;
7 mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno la Mungu”.
Matendo 18:12, 23:24, 26:30
Ni nini twaweza zingatia kuhusu hawa maliwali?
Bwana Yesu alisema, katika utumishi wetu, utafika wakati, tutaitishwa mbele ya mabaraza ya wafalme, na maliwali, kushitakiwa.Hivyo tukijikuta katika mazingira kama hayo hatupaswi kuogopa, kwasababu Kristo ameahidi kuwa atakuwa na sisi katika mapito yetu yote.
Mathayo 10:18 “nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa”.
19 Lakini hapo watakapowapeleka, msifikiri-fikiri jinsi mtakavyosema; maana mtapewa saa ile mtakayosema.
20 Kwa kuwa si ninyi msemao, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu”.
Bwana akubariki.
Je! Umeshamkabidhi Kristo Maisha yako?. Kama jibu ni hapana, na upo tayari kuokoka leo. Basi fungua hapa kwa mwongozo wa sala ya toba, >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA
Au tutafute kwa namba zetu hapo chini, kwa msaada huo.
+255693036618/+255789001312
Mada Nyinginezo:
Akida ni nani kibiblia, na kazi yake ni ipi? (Mathayo 8:5)
Je mwanamke Fibi, alikuwa ni askofu wa makanisa, kama mitume?
Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?
Mharabu ni nani katika biblia?
Akida ni mkuu wa majeshi ya zamani, hususani majeshi ya kirumi. Akida mmoja alikuwa anaongoza kikosi cha askari 100,. Maakida wengi walikuwa wanachaguliwa na watalawa wao wakuu moja kwa moja toka Rumi,wengine katika mabaraza, wengine kutoka kwa maliwali, na wengine moja kwa moja kwa kupandishwa vyeo, baada ya kutumika kwa muda mrefu (miaka 15-20), katika shughuli za kijeshi.
Kazi yao kubwa ilikuwa ni kusimama mstari wa mbele katika vita kuliongoza kundi lote jeshini, pia kutekeleza mauaji ya wahalifu, au washitakiwa, mfano wa hawa ni Yule akida aliye simamia mateso na mauji ya Bwana Yesu pale Kalvari
Marko 15:39 “Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu”.
Pia walikuwa wanafanya kazi ya kutoa mafunzo ya kijeshi, kugawa majukumu, kusimamia ujenzi wa ngome na kuta za ulinzi za taifa. Walifanya pia kazi ya kuwalinda wafungwa na kuwahakikishia ulinzi wao pindi wasafirishwapo, Mfano wa Hawa, soma .(Matendo 23:23, 24:23, )
Pamoja na hilo, maakida wengine walikuwa ni watu wakatili, na wapenda rushwa,
Lakini ni jambo gani Mungu anataka tujifunze nyuma ya watu hawa?
Ijapokuwa kazi hii, si kazi iliyoonekana kumrudishia Mungu utukufu, Lakini bado tunaona wapo maakida, kadha wa kadha katika biblia, waliompendeza Mungu katika utumishi wao, zaidi hata ya wayahudi wengi, waliokuwa wanajiona washika sheria na torati.
Kwamfano utaona Bwana Yesu alipokuwa katika ziara zake za kuhubiri na kufungua watu, alikutana na akida mmoja, ambaye aliustaajibisha sana moyo wake kwa imani aliyokuwa nayo, mpaka Bwana akasema hata katika Israeli,hakuna aliyekuwa na imani kubwa kama yake.
Mathayo 8:5 “Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
6 akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
7 Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
8 Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
10 Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.
11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;”
Utaona pia, kulikuwa na akida mwingine, aliyeitwa Kornelio, huyo alikuwa anatoa sadaka nyingi sana, na kuwasaidia watu, mpaka siku moja malaika wa Bwana anamtokea na kumpa maagizo ya kufanya ili aupokee wokovu kamili.
Matendo 10:1 “Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia,
2 mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima”.
Umeona? Ni nini Mungu anataka tujue?
Ni kwamba Mungu hatazami sana mahali unapotumika, lakini anatazama uaminifu wako, moyo wako, utakatifu wako, bidii yako kwake. Unaweza ukawa unafanya kazi serikalini, lakini ukamtumikia Mungu vema, kwa kukataa rushwa, na kutenda haki, na Mungu akapendezwa nawe..Mfano wa Danieli, Maadamu, upo mahali ambapo hapakinzani na sheria ya Mungu na taifa, usijisikie vibaya kutumika unachopaswa kufanya ni kumtumikia tu Mungu kwa uaminifu wote, kuangaza nuru yako ya wokovu kwa wale watu, na kumpenda yeye na kukataa njia zote mbaya zinazokinzana na Neno lake.
Kwa kufanya hivyo Basi Mungu atakutumia kutimiza kusudi lake, alilolikusudia juu yako, na watu wake, mfano wa Kornelio na Yule akida ambayo alidhubutu hata kuwajengea wayahudi sinagogi.
Bwana akubariki.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Mshipi wa dhahabu matitini ni nini?
Neno “Mashehe” tunaliona likitajwa katika biblia(Agano la kale); Hawa mashehe ni wakina nani?
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
Sifa ni kitendo cha kumshuhudia Mungu, au kuyasimulia matendo makuu ambayo ameyafanya au aliyonayo, na huwa inaambata na mguso wa ndani unaomfanya mtu arukeruke, acheze, afurahie, aimbe, ashangalie, apige kilele kwa nguvu, kwa hayo aliyoyaona kwa Mungu wake.
Kwamfano tunapoona jinsi, mbingu na nchi, jua na mwezi, na milima na bahari, vilivyoumbwa kwa uweza na ukuu wa ajabu, hapo tunapata sababu ya kumshuhudia Mungu, au kumtangaza kwa namna zote aidha kwa kumwimbia, kushangalia kwa sauti ya juu,
Au labda ulikuwa na shida Fulani labda ugonjwa, ukaponywa, au hitaji la kazi, nyumba, chakula ukapatiwa na yeye. Hapo ndipo unapopata sababu ya kuyatangaza maajabu yake, kwa kumwimbia kwa nguvu sana. Hizo ndio sifa.
Mungu anasema..
Zaburi 68:32 “Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu, Msifuni Bwana kwa nyimbo”.
Zaburi 117:1 “Haleluya. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, Enyi watu wote, mhimidin.
Zaburi 147:1 “Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu, Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri”.
Biblia inatuambia viumbe vyote na uumbaji wote, vinamsifu Mungu. Kwanini na sisi tusimwimbie yeye sifa zetu?. Embu tazama pumzi uliyopewa bure, embu tazama mapigo ya moyo yanayodundishwa ndani yako bila tozo lolote, embu tafakari jua unaloangaziwa na Yehova. Kwanini usimsifu yeye?
Bwana anaketi juu ya sifa.. (Zaburi 22:3), Na yeye pekee ndiye anayestahili kuabudiwa.
Hivyo wote wamsifuo kwa Roho na Kweli, yeye yupo juu yao. Katika sifa kuta za Yeriko zilianguka, , \vifungo vya Gereza vililegezwa Paulo na Sila walipokuwa gerezani, katika sifa maadui waliuliwa bila vita yoyote kipindi cha Mfalme Yehoshafati. Nasi pia tukiwa watu wa sifa, ni maombi tosha ya kutuweka huru na kutufungua.
Bwana atupe macho ya kuliona hilo.
Shalom.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)
Mwana haramu ni nani kibiblia? (Kumbukumbu 23:2).
Kinubi ni nini katika biblia? (1Samweli 16:16, 23)
Kuhimidi kibiblia ni kumpa Mungu sifa iliyochanganyikana na heshima na unyenyekevu wa hali ya juu sana,
Neno hili limeonekana mara nyingi sana katika biblia,
Kwamfano hivi ni baadhi ya vifungu, ambavyo utakutana na Neno hilo;
Mwanzo 14:19 “Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote”.
Waamuzi 5:3 “Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu; Mimi, naam mimi, nitamwimbia Bwana; Nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli”.
Zaburi 31:21 “Bwana ahimidiwe; kwa maana amenitendea Fadhili za ajabu katika mji wenye boma”.
Zaburi 34: 1 “Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima”.
Warumi 15:10 “Na tena anena, Furahini,Mataifa,pamoja na watu wake.
11 Na tena, Enyi Mataifa yote,msifuni Bwana; Enyi watu wote,mhimidini.
Ikiwa wewe ni mwanadamu mwenye pumzi huna budi kumuhimidi Mungu muumba wako sikuzote za maisha yako. Ni lazima ujishushe, upige magoti, na kwa kumaanisha kabisa, umsifu kwa nguvu zako zote, umtukuze kwa wema wake wako, na kuliadhimisha jina lake.
Moja ya mambo ambayo yalimfanya Daudi awe kipenzi cha Mungu, ni tabia yake, ya kumuhimidi Mungu, tena mbele ya makusanyiko ya watu.
Zaburi 26:12 “Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana”.
Bwana atusaidie sote, tuwe na matamanio kama haya. Kwasababu kama ilivyo chakula chetu sisi ni Neno la Mungu, halikadhalika chakula cha Mungu wetu ni Sifa. Hatuna budi kumlisha kila siku sifa zake, kwa kumuhimidi yeye.
Bwana akubariki.
Je umeokoka? Kama la unafahamu kuwa tunaishi katika vizazi ambacho unyakuo ni wakati wowote?. Tubu dhambi zako mgeukie Mungu, naye atakusaidia. Ikiwa utahitaji msaada ya kumkaribisha Kristo maishani mwako/ kubatizwa, basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi;
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
Wana wa Asafu ni akina nani katika biblia?
Ibada ni nini,Na je ili ikamilike inapaswa iwe na nini na nini?
Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)
Mwana-haramu, au mwana wa haramu ni mtu aliyezaliwa nje ya Ndoa Takatifu.
Zamani katika jamii ya Israeli, Mungu aliwakataza wana wa Israeli, wasioane na watu wa mataifa. (Kumbukumbu 7:2-3). Wala wasioane ndugu kwa ndugu..
Walawi 18:5 “Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na hukumu zangu; ambazo mtu akizitumia ataishi kwa hizo; mimi ndimi Bwana.
6 Mtu ye yote aliye wa kwenu ASIMKARIBIE MWENZIWE ALIYE WA JAMAA YAKE YA KARIBU ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana”.
Vile vile Bwana aliwakataza watu wasiingie kwa wake wa Jirani zao (Kumbukumbu 5:21, Kutoka 20:17).
Kwahiyo mtoto yeyote aliyepatikana kwa mojawapo ya hizo njia tatu, yaani kwa njia ya kukutana ndugu kwa ndugu, au kuoana mtu wa Israeli na mtu wa mataifa, au kwa kuzaa na mke wa Jirani yako au ambaye hamjaoana, mfano wa Yuda katika Mwanzo 38:24. Mtoto huyo aliyezaliwa aliitwa MWANA-HARAMU, Au MWANA WA HARAMU.
Na Mwana haramu, enzi za agano la kale hakuruhusiwa kuingia katika MKUTANO WA BWANA MILELE, na hata kizazi chake chote..
Kumbukumbu 23:2 “Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana; hata kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana”.
Lakini swali ni je! Mpaka sasa, wana wa Haramu,(yaani waliozaliwa nje ya ndoa, kimwili) hawakubaliwi na Bwana?
Jibu ni la!, katika Agano la kale, si tu wana haramu waliokuwa wanatengwa, bali hata walemavu na watu wenye ukoma, hawakuruhusiwa kuingia katika mkutaniko wa Bwana. Na Bwana aliruhusu vile, ili kufundisha Uana haramu wa kiroho jinsi ulivyo mbaya, ambao utakuja kufunuliwa mbeleni(katika Agano jipya). Ambao huo utatufanya sisi tusikubalike mbele za Mungu, milele!!.
Mwana wa Haramu kibiblia ni mtu ambaye Hajazaliwa mara ya Pili.
Je umewahi kujiuliza ni kwanini “Wokovu” unafananishwa na “kuzaliwa mara ya pili”.. jiulize kwanini biblia haijatumia neno “kutengenezwa upya” lakini imetumia neno “kuzaliwa mara ya pili”.. Tafsiri yake ni kwamba “hali tuliyopo” sasa ni “u-haramu”… hivyo tunapozaliwa upya, ili ule uharamu unaondoka, na kuwa wana HALALI!!.. Na hivyo tunakuwa na uwezo wa kushiriki baraka zote za Mungu kwasababu tumefanyika kuwa Watoto wa Mungu halali.
Wana wa Haramu, (ambao hawajazaliwa mara ya pili), wanafananishwa na mbegu zinazoharibika.. maana yake!, hazina uzima wa milele, lakini wana halali (yaani wale waliozaliwa mara ya pili), wanafananishwa na mbegu zidumuzo.
1Petro 1:23 “Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele”.
Na tabia ya mtoto halali, (asiye haramu), huwa baba yake anamfunza, ikiwemo pia kumwadhibu pale anapokosea..
Mtume Paulo aliliandika hilo kwa uweza wa roho na kusema…
Waebrania 12.5 “tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, Wala usizimie moyo ukikemewa naye;
6 Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.
7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye?
8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo MMEKUWA WANA WA HARAMU NINYI, WALA SI WANA WA HALALI.
9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?
10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.
11 Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani”.
Je umezaliwa mara ya pili?
Maana ya kuzaliwa mara ya pili, ni Kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi (Kwa jina la Yesu) na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. (Matendo 2:38).
Yohana 3:3 “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, MTU ASIPOZALIWA MARA YA PILI, HAWEZI KUUONA UFALME WA MUNGU.
4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili”.
Maran atha!
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
TUMEFANYIKA KUWA WANA WA MUNGU!
KWANINI YESU NI ADAMU WA PILI?