SWALI: Mstari huu una maana gani?
Mithali 27:10 “Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali”
JIBU: Ni mstari unaolenga umuhimu wa marafiki wema katika maisha yetu. Hapo anaanza kwa kusema usimwache rafiki yako mwenyewe, lakini haishii tu kwa rafiki yako, anaendelea kusema pia hata rafiki wa baba yako. Kwasababu wanaweza wakawa msaada kwako wa karibu kuliko ndugu wakati mwingine.
Kauli hiyo haimaanishi kuwa ndugu hawana msaada, hapana, lakini kutegemea tu ndugu peke yake, na kuwapuuzia marafiki wema kwaweza kukukwamisha, kwamfano umezidiwa na ugonjwa chumbani kwako, na unahitaji huduma ya kwanza, hapo huwezi kumpigia simu ndugu yako aliye mkoa mwingine, au wilaya nyingine aje kukusaidia, ni wazi kuwa msaada wa kwanza utauhitaji kutoka kwa jirani yako.
Ndio maana ya huo mstari, usimwache rafiki yako mwenyewe, yaani usimpuuzie, wala usimpuuzie rafiki wa Baba yako hata kama sio rafiki yako. Marafiki wa ndugu zetu, mara nyingi hufanyika msaada mkubwa kwetu wakati mwingine, Hili ni jambo la kawaida katika jamii, mara nyingi tumeona marafiki wa wazazi, au wa ndugu zetu wakitumika kutusaidia kwa sehemu moja au nyingine.
Lakini tukiwa ndani ya Kristo, tunapata marafiki ambao ni zaidi hata ya ndugu, kwasababu wao, husukumwa na upendo wa Kristo ambao umezidi wote. Bwana ameahidi hivyo kwamba tukiacha vyote kwa ajili ya jina lake, basi hayo yote atatujalia (Marko 10:30).
Je! Umeokoka? Je! Unatambua kuwa hizi ni nyakati za mwisho, na Yesu yupo mlangoni kurudi? Maisha yako yapo kwa nani. Kama upo nje ya Kristo ni heri ukatubu sasa, kwasababu mlango wa neema unakaribia kufungwa, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kama hukubatizwa, ili upate ondoleo la dhambi na upokee kipawa cha Roho Mtakatifu, ikiwa utahitaji msaada huo basi wasiliana nasi kwa namba zetu hizi +255693036618 / +255789001312.
Bwana akubariki.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
USIWE ADUI WA BWANA
Rafiki hupenda sikuzote; Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.
Usimwache mwanamke mchawi kuishi! Biblia ilimaanisha nini?
BASI, IWENI NA HURUMA, KAMA BABA YENU ALIVYO NA HURUMA
Je ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko wote duniani?
KWA HIYO NDUGU, VUMILIENI, HATA KUJA KWAKE BWANA.
NDUGU,TUOMBEENI.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Kwanini Biblia inakataza kula asali nyingi, nini maana ya mstari huu kiroho?
Mithali 25:16 “Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika”.
Pia sehemu nyingine inasema..
Mithali 25:27 Haifai kula asali nyingi mno; Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.
JIBU: Asali hufananishwa na Neno la Mungu,
Ezekieli 3:1 Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli. 2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo. 3 Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.
Soma pia Ufunuo 10:10. Utalithibitisha hilo.
Na kila mmoja wetu anashauriwa alisome Neno la Mungu (alile) sana kwasababu ndio uzima wetu (Mathayo 4:4).
Mithali 24:13 Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo
Lakini katika maandiko hayo tunaona tena biblia inatuasa tusile nyingi mno kupita kiasi, ikaja kutuletea madhara..Sasa maana yake ni nini? Je! Tulipende Neno la Mungu kwa kiasi au la?
Jibu ni kwamba hapo haimaanishi tulisome/ tujifunze neno la Mungu kwa kiasi hapana.. Bali analenga katika Suala la NIA zetu.. Ni kawaida yetu sisi watoto wa Mungu, kuwa na NIA inayopitiliza hususani pale tunapolifahamu sana Neno la Mungu.
Kwamfano, tunaposoma juu ya neema ya Mungu iliyokuwa inatembea juu ya Eliya, Kisha tunaposoma kitabu cha Malaki4:4-5, kwamba ahadi imetolewa kuwa Roho ya Elia itarudi tena katika siku za mwisho. Baadhi ya watu wanajiweka katika nafasi hizo, na wanaamini kuwa Mungu anakwenda kuwaandaa kwa roho hiyo ili waje kuionya dunia kwa mapigo na ishara kama za kwake.
Au Musa kafunga siku 40 bila kunywa wala kula, akaongeza na nyingine 40 na yeye bila uongozi wa Roho Mtakatifu anasema na mimi lazima nifunge hivyo.
Wapo wengine wanasema na mimi nisipotokewa na Yesu kama Paulo alivyotokewa kule Dameski, bado sitakwenda kuhubiri injili, hivyo wanasubiriwa kwa miaka watokewe wapewe maagizo, kwa kufunga na kuomba. Sasa Hali kama hizi zina hatari kwasababu mwisho wa siku zinamfanya asiwe mtu wa matunda kwa kungojea jambo ambalo huwenda Mungu hajalikusudia katika maisha yao, kwasababu amenia makuu kuliko kipimo kile alichopimiwa na Mungu.
Mtume Paulo aliyasisitiza sana makanisa juu ya jambo hilo akasema..
Warumi 12:16b “.. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili
Na hapa pia anasema..
1Wakorintho 7:17 “Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote. 18 Je! Mtu fulani ameitwa hali amekwisha kutahiriwa? Asijifanye kana kwamba hakutahiriwa. Mtu fulani ameitwa hali hajatahiriwa bado? Basi asitahiriwe. 19 Kutahiriwa si kitu, na kutokutahiriwa si kitu bali kuzihifadhi amri za Mungu. 20 Kila mtu na akae katika hali ile ile ambayo alikuwa nayo alipoitwa. 21 Je! Uliitwa u mtumwa? Usione ni vibaya lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia. 22 Kwa maana yeye aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo.
Ikiwa Bwana kakupa kipimo cha ushemasi, tembea katika hicho kwa uaminifu usilazimishe uwe nabii wa mataifa yote kama Yeremia. Bwana amekuokoa, tumika katika kipimo hicho hicho, ikiwa itampendeza kukunyanyua juu zaidi, basi atafanya kwa wakati wake, lakini kwasasa tujishughulishe na mambo manyonge,
Lakini si hayo tu, wakati mwingine katika kufahamu sana maandiko, hupelekea tabia za majivuno, kujiona unafahamu, kukataa kushauriwa kunazalika ndani ya mtu. Hivyo hupelekea kujifungia mwenyewe milango ya Mungu kuendelea kusema naye. Hivyo ili kuepuka kuitapika asali iliyo nzuri na njema, ni vizuri haya yote tukajiepusha nayo, tunapojifunza kwa bidii Neno la Mungu kila siku.
Tule asali kwa kadiri ya kututosha tusije tukashiba tukaitapika, kwa kukosa shabaha ya maandiko.
Maran Atha.
Shalom.
NJAA IPO?, USIACHE KULA ASALI.
Kwanini iwe ni nchi ibubujikayo maziwa na asali?
Je! Ni sawa kuingia katika shamba la mtu mwingine na kula jinsi utakavyo?
Kula uzao wa tumbo lako maana yake nini? (Kumbukumbu 28:53)
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Aibusu midomo atoaye jawabu la haki (Mithali 24:26)
Wewe umemwaga damu nyingi,
Kuna wakati Daudi aliingiwa na wazo la kumjengea Mungu nyumba, hivyo wazo hilo likawa jema sana machoni pa Mungu, likamfurahisha sana Bwana mpaka akamwahidia Baraka tele katika ufalme wake..Lakini tunasoma Mungu alimzuia Daudi asiijenge hiyo nyumba, bali mwana wake Sulemani ndiye aje kuijenga, sio kwamba Mungu alikuwa hatamani Daudi aijenge, hapana Mungu alimpenda sana, na alikuwa kipenzi chake, lakini kulikuwa na kikwazo kilichomkwamisha..
Embu tusome…
1 Nyakati 22:7-8 [7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu. [8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;
1 Nyakati 22:7-8
[7]Daudi akamwambia Sulemani mwanawe, Kwangu mimi nia yangu ilikuwa kujenga nyumba kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wangu.
[8]Lakini neno la BWANA likanijia, kusema, Wewe umemwaga damu nyingi, na vita vikubwa umevifanya; wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu;
Sababu yenyewe Mungu ameitoa hapo kwamba Daudi “amemwaga Damu za watu wengi”..Daudi hakujua kuuwa kwakwe watu sio jambo ambalo lilikuwa linavutia machoni pa Bwana, japokuwa Mungu alikuwa pamoja naye wakati wote, hakujua kuwa kuua kule kulikuwa kunapeleka harufu mbaya mbele za Mungu aliye mtakatifu na msafi.
Hivyo wakati anapeleka ombi lake la kumjengea hekalu, Mungu akamkataza kwasababu alimuona ananuka damu za watu wengi, Na sikuzote Mungu hawezi kuruhusu mikono yenye damu, kushiriki katika kujenga vitu vitakatifu.
Ni nini Bwana anataka tujifunze.
Sisi kama wakristo, zipo dhambi au makosa ambayo tunayazoelea kuyafanya mara kwa mara, lakini hatujui kuwa tunamkosea Mungu, wakati mwingine tunapumbazika, kuona rehema na fadhili zake zinatufuata kila mahali, lakini ndani ya mioyo yetu tunamwaga damu kila kukicha kama Daudi.
Kwamfano, katika agano jipya, hatuui kwa Upanga au kwa mkuki, maandiko yanasema..
1Yohana 3:15 “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
Kitendo tu cha kuwa na chuki, na jirani yako, au ndugu yako, kumbe rohoni unatafsirika kama mwuaji, hivyo chuki hizo zinavyoendelea na kuzidi wakati baada ya wakati, zinavyozidishwa kwa watu wengine kadha wa kadha, ndivyo mtu huyo anavyoonekana anamwaga damu nyingi.
Na madhara yake utakuja kuyaona mbeleni, wakati ambapo unamwomba Mungu kibali cha kutenda jambo Fulani jema kwa ajili yake, anakuzuia, unataka Mungu atembee na wewe katika viwango Fulani vya juu, anakuzuia, kwasababu umeendekeza makosa au dhambi hizo kwa muda mrefu.
Hivyo, tunapaswa, kila inapoitwa leo, tuangalie ni wapi tumezoelea kupafanya ambapo hapampendezi Mungu, kisha tuache mara moja, ili isije kutuletea madhara mbeleni, Kama ni katika usengenyaji, tuache mara moja, kama ni katika uongo, rushwa, udhuru, wivu, manung’uniko tuache mara moja.
Bwana atusaidie
KWANINI DAUDI ALIKUWA NI MTU ALIYEUPENDEZA MOYO WA MUNGU?
EPUKA KUCHELEWA IBADA.
NAAM, HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA.
Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?
KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?
KIFAHAMU KIGEZO CHA KUSAMEHEWA NA MUNGU.
SWALI: Nini maana ya huu mstari?
Mithali 25:23 Upepo wa kusi huleta mvua; Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu.
JIBU: Maandiko yanasema Upepo wa kusi huleta mvua, hapo hasemi ‘upepo’ huleta mvua hapana bali anasema ‘Upepo wa kusi’, Maana yake ni kuwa kila aina ya upepo hubeba tabia yake, kwa mfano upepo wa Kaskazi, hauleti mvua, bali unaleta joto. Vivyo hivyo na pepo nyingine zote, hubeba tabia zao.
Hii ni kufunua nini?
Na sisi wanadamu huwa tunavumisha pepo zetu..Na ndio maana utasikia Neno “UVUMI” wa jambo Fulani, na taarifa hizo husambazwa kwa maneno ya vinywa vyetu, Hivyo kila jambo unalolitoa na kulipeleka kwa mtu mwingine au kwa jamii, huo ni upepo, na ni lazima uwe makini nao sana, kwasababu mwisho wa siku ni lazima ulete faida au madhara.
Na ndio maana hapo katika sehemu ya pili ya mstari huo anasema.. “Vile vile asingiziaye huleta uso wa ghadhabu”. Kusingizia ni neno linalojumuisha usengenyaji, au mtu anayechukua taarifa zisizo za kweli na kuzipeleka kwa mwingine, Watu kama hawa, mwisho wa siku watavuna ghadhabu tu, au kuchukiwa, au kusababishiwa madhara na wale waliotolewa taarifa zao. Kwasababu kila uvumi unamatokeo yake.
Lakini tukiwa watu wa kupeleka habari njema, watu wa kuhubiri habari za Kristo, Maana yake ni kuwa Upepo tunaovumisha ni wa heri sikuzote, hivyo tufahamu kuwa mwisho wake utakuwa ni mzuri, utatuletea neema badala ya ghadhabu, kupendwa badala ya kuchukiwa, kusaidiwa badala ya kufukuzwa.
Hivyo tuwe makini na taarifa, au maneno yanayotoka katika vinywa vyetu, biblia inasema..
1 Petro 2:1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote. 2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
Epuka masengenyo, na kuwazungumzia wengine vibaya.
Kuwaogopa wanadamu huleta mtego,(Mithali 29:25)
NA UPEPO WA KUSI ULIPOANZA KUVUMA KIDOGO,
JIPE NAFASI KATI YA TAARIFA UNAYOIPOKEA NA MAAMUZI UNAYOYATOA.
IEPUKE GHADHABU YA MUNGU.
Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela.
Kwanini mtu afanye miujiza na bado asiende mbinguni?
Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.
SWALI: Naomba nieleweshwe maana ya huu mstari
Mithali 24:27
[27]Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba yako.
JIBU: Zamani enzi za biblia, kilimo kilikuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa watu wengi kama ilivyo sasa katika baadhi ya jamii.
Hivyo ilikuwa ni ajabu mtu kutumia rasilimali zake katika kununua au kujenga vitu visivyo na umuhimu sana, kama vile nyumba, nguo za kifahari, magari ya farasi n.k.angali shambani kwake hajajiwekeza vya kutosha.
Watu walikuwa wanakusanya kwanza chakula cha kutosha kujihakikishia shibe kwa miezi au miaka kadhaa, ndipo baada ya hapo hufikiria kutumia hazina zao katika kujenga, au kujiendeleza..lakini hawakujiendeleza kabla ya kuhakikisha mashamba yao yamewanufaisha..
Na ndio hapo Sulemani utaona anatoa ushauri ule ule..
Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba tengeneza kwanza mambo yako uwe imara ndipo yale mengine ya ziada yafuate baadaye.
Ni kawaida ya mwanadamu kupenda, vitu vizuri kwanza kabla hajavitaabikia..
Alikuwepo Gehazi, mtumwa wa Elisha, yeye aliona kusubiri wakati wa Mungu ni kujichelewesha, kutumika kama mtumwa asiye na faida ni kupoteza muda, hivyo, zile zawadi zenye thamani nyingi zilizoletwa na Naamani, na Elisha kuzikataa, yeye akamwona kama alikuwa hapendi mema..lakini Elisha alimwambia maneno haya..
2 Wafalme 5:26
[26]Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi?
Alimuuliza Je huu ndio wakati? ..kumbe kulikuwa na wakati lakini haukuwa ule..
Watu wanataka kula vitu vya Bwana lakini hawataki kutengeneza kwanza kazi zao huko mashambani, hawana muda wa kuifikiria kazi ya Mungu, hawana muda na kuhubiri injili ya kweli,wanachokifiria ni matumbo, na kwamba watapata faida gani..
1 Timotheo 6:5-6
[5]… huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. [6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
[5]… huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida.
[6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
.Vilevile hata katika maisha ya kawaida, hekima hizi zinamafunzo, mtu atataka anunue simu ya milioni 2, lakini hana shughuli yoyote ya kumwingizia kipato, badala aitumie kama mtaji, kisha kile akipatacho kama faida ndio atumie kununua hayo mengine..
Bwana atusaidie, katika kuyapangalia maisha yetu ya rohoni na mwilini
TENGENEZA NYAVU ZAKO, OSHA NYAVU ZAKO.
Nini maana ya vifungeni viuno vya Nia zenu? (1Petro 1:13).
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
Nini maana ya Ukuta uliopakwa chokaa (Matendo23:3)?
Uchaga ni nini? (Luka 12:24)
Pale unapotubu, kwa kumaanisha kabisa kuacha maovu, na maisha ya kale ya dhambi, wakati huo huo Mungu anakusamehe dhambi zako kabisa kabisa. Lakini hutasikia, hisia Fulani, au badiliko Fulani la wakati huo huo, kwani fikra zako za dhambi za zale bado zitaendelea kuzunguka kwenye akili yako. Hivyo wengi wakishaona hivi wanadhani kuwa Mungu hajawasamehe, na hivyo wanaendelea kubaki katika mashaka, au kurudia rudia kumlilia Mungu awasamehe.
Na hapa shetani ndipo anapata nafasi ya kuwatesa, na kuwakandamiza, wengine wanajikuta kila siku wanaomba Toba Mungu nisikie unisamehe!, Mungu nisikie unisamehe!, kumbe tayari Mungu alishawasamehe tangu siku ile ya kwanza walipomaanisha kweli kweli kugeuka na kukataa kurudia dhambi zao.
Ndugu, fahamu hata kama wewe utakuwa na kumbukumbu la nyuma la dhambi zako, lakini kwa Mungu ni tofauti, yeye akisamehe anasahau kabisa.
Waebrania 8:12 “Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena”.
Unapokwenda mbele za Mungu, lazima uamini kwa moyo wako wote umeshasamehewa, vita vya kimawazo vinavyoanza kuja tangu huo wakati, huna budi kuvishinda, kwa kuvipinga, ukisikia moyoni mwako unaambiwa, aah! Wewe dhambi zako ni nyingi, ile dhambi ulishamkufuru Roho Mtakatifu, pinga, kataa sema mimi nimeshasamehewa kwa damu ya Yesu Kristo.
Kisha unavyozidi kufanya hivyo baada ya kipindi Fulani utaona amani ya Mungu imekuvaa.
Lakini pia ni lazima ukumbuke kuwa yapo mambo yanayochangia pia kusamehewa dhambi zetu, na yenyewe ni sisi kuwasamehe waliotukosea kama wapo.
Bwana Yesu alisema..
Mathayo 6:14 “Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu”.Hivyo uombapo msamaha zingatia kuwa moyo wako ni mweupe kwa wengine.
Bwana akubariki
NINI MAANA YA KUTUBU
Nini maana ya kumpenda Bwana kwa moyo,roho, akili na nguvu zetu zote?
TAFUTA MSAMAHA HALISI, NA SI MSAMAHA TU!
KUONGOZWA SALA YA TOBA
Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).
1Timotheo 5:23 “Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara”
Haya ni maneno ya mtume Paulo kwa mtoto wake wa kiroho Timotheo, Ni rahisi kuyachukulia juu juu, lakini ukitazama kwa undani utaona jinsi watu wa kale walivyojitoa kwa Bwana,bila kuruhusu hali zao za mwilini kuwakwamisha.
Kama tunavyosoma, Timotheo alikuwa ni kijana mwenye bidii sana, aliyetumika na Mtume Paulo katika kuineza injili sehemu kubwa ya dunia, lakini kijana huyu hakuwa vizuri sana kiafya kama tunavyodhani, alikuwa anasumbuliwa na tumbo, lakini kama hilo halitoshi, alikuwa pia anapatwa na magonjwa ya MARA KWA MARA, tena katika ujana na sio uzee. Ni heri magonjwa hayo yangekuwa ni ya siku moja, bali ya mara kwa mara. Paulo aliishi naye kwa muda mrefu hivyo alikuwa anamwelewa sana, anashangaa leo yupo sawa, kesho, ni mgonjwa, wiki hii yupo sawa, wiki ijayo tumbo linamsumbua sana.
Lakini katika yote hayo, hakuwa kama Dema ambaye alimwacha Paulo, akaurudia ulimwengu, yeye aliendelea kuitenda kazi ya Bwana katika madhaifu yake ya mwili, Ni mtu tu pekee ambaye Paulo alijiona amani kumwachia hata huduma yake aiendeleza duniani. Alikuwa kama Elisha kwa Eliya.
Hivyo mwishoni kabisa mwa huduma, tunaona hapa Paulo anamwandikia waraka huu na kumsisitiza, asinywe maji tu peke yake, bali na mvinyo kidogo kwa ajili ya magonjwa hayo ya mara kwa mara, Paulo hapa anampa ushauri wa kitabibu, zaidi ya ule wa kiroho, kwani zamani mvinyo , ulitumika kwa ajili ya baadhi ya magonjwa, lakini sasa kwa wakati wetu tunazo dawa za hospitalini. Unaweza kujiuliza Paulo ambaye Mungu alimtumia kwa ishara na miujiza ya kupita kawaida, angepaswa amweke, mikono, na kukemea magonjwa hayo ya mara kwa mara yamwachie, lakini alitambua kuwa si kila wakati hali itakuwa hivyo, mambo mengine Mungu anayaruhusu yatokee kwa sababu zake.
Ni kama Elisha, ambaye, alisumbuliwa na ugonjwa ambao ulikuja kumuua, lakini hakumwacha Bwana, na kusema Mungu gani huyu hanioni, aliendelea kuwa nabii wa Mungu,
2Wafalme 13:14 “Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatelemka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!”
Ni nini Bwana anataka tujifunze?
Katika madhaifu yetu, kamwe tusipunguze spidi ya kumtumikia Mungu, kwasababu mambo tunayoyapitia sisi walishayapitia watakatifu wengine waliotutangulia. Kijana Timotheo, alikuwa ni mdhaifu sana kimwili, lakini aliichapa injili ya Kristo, bila kujali yamsibuyo. Alisafiri huko na huko.
Yawezekana na wewe, ni mhubiri au mtumishi wa Bwana, lakini vidonda vya tumbo, haviishi ndani yako ijapokuwa umemwomba sana Bwana aviondoe lakini bado huoni matokeo yoyote, endelea hivyo hivyo kutumika usisubiri upone, una magonjwa Fulani ya kichwa ambayo yanakuja na kuondoka, yanakuja na kuondoka, yasikukwamishe, mkumbuke Timotheo, kunywa dawa za hospitalini, songa mbele, unasumbuliwa na saratani, unasumbuliwa na sukari, inapanda, inashuka, kila siku ni kuchoma sindani, Usingoje kwanza Bwana akuponye, endelea, kwani huzijui njia za Bwana, hujui ni kwanini leo upo hivyo, huwenda amekusudia, uishi maisha marefu kuliko zaidi ya wengine katika hali hiyo hiyo ili jina lake litukuzwe, na uwaponye wengi wanaosumbuliwa na maradhi kama hayo, Elisha baada ya kufa katika ule ugonjwa wake, tunaona bado mifupa yake ilifufua wafu, Hivyo kuugua si kikwazo cha Mungu kutokututumia sisi.
Tujipe moyo tusonge mbele, Bwana anatupenda, kwani yeye mwenyewe alisema, pale tuwapo dhaifu ndipo tulipo na nguvu.
2Wakorintho12:9 “Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. 12.10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu”.
UWEPO WA BWANA HATA KATIKATI YA MATESO.
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.
Nini maana ya..“wakiwazuia watu wasioe” (1Timotheo 4:1)
AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!
MAUMIVU NYUMA-YA-HUDUMA.
NINI TOFAUTI KATI YA KARAMA, UTENDAJI KAZI NA HUDUMA.
KANSA/SARATANI INATIBIKA.
Kuna wakati Bwana Yesu alianza safari ya kuchosha ya kutembea kutoka Yerusalemu kuelekea Galilaya..lakini maandiko yanatuonyesha katika safari yake yote hiyo hakuona mahali popote pa kupumzika, japo alikatiza katika vijiji na miji midogo midogo.
Lakini alipofika Samaria mahali ambapo hapakai wayahudi, aliingia katika eneo ambalo, huwenda alihisi amani nyingi ya Mungu ikibubujika ndani yake, na hapo hapo akaona kisima cha maji akatulia apumzike kidogo.
Lakini maandiko yanatupa uelewa eneo hilo lilikuwa ni la namna gani mpaka likamfanya Yesu avutiwe nalo…yanasema..mahali pale palikuwa ni karibu na Shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe..
Yohana 4:3-8
[3]aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya.
[4]Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria.
[5]Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe.
[6]Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
[7]Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.
[8]Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula.
Yesu aliiona ardhi ile katika roho, aliona mbaraka ule wa Yakobo kwa mwanawe Yusufu unavyomkaribisha pale, hivyo hakuweza kupita hivi hivi bila kutenda jambo…aliiona haki ya Yusufu inamlilia shambani kwake.. Kumbuka Israeli yote ilikuwa ni Milki ya wana wote 12 wa Yakobo, lakini si kila shamba la mwana wa Yakobo Yesu alipumzika.
Hivyo kitendo cha Yesu tu kutulia pale, kama tunavyojua habari watu wengi wa Samaria wakapokea wokovu akawaokoa watu ambao hawakustahili wokovu kabisa (yaani wasamaria).
Unaweza kujiuliza ni wakati gani Yakobo alimpa Yusufu shamba hilo? Waweza kusoma habari hiyo katika..Mwanzo 48:21-22
Utaona akipewa sehemu mara dufu ya wenzake.. Na hiyo yote ni kwasababu Yakobo alimpenda Yusufu kwa tabia zake njema.
Ile Tabia ya Yusufu ya kumcha Bwana alipokea thawabu sio tu za wakati ule alipofanyika kuwa waziri mkuu wa Misri.. Lakini tunaona pia hadi kipindi cha Bwana Yesu baraka zake bado zilitembea.
Leo hii ukimcha Mungu wewe kama kijana, utawasababishia wengine kupokea neema ya wokovu hata wakati ambapo haupo hapa duniani.. Kumcha Mungu ni uwekezaji mkubwa sana zaidi ya mali.
Bwana akikubariki uzao, basi huwenda vitukuu vyako vikawa majeshi hodari ya Kristo, kwasababu Yesu anapita kuangalia ni wapi mbaraka wa Yusufu upo ili apumzike? akakuona wewe.
Akikubariki mashamba au mali, siku za mbeleni aidha uwapo hai au ufapo, Kristo atapita hapo na patakuwa kitovu cha madhabahu nyingi za Mungu.
Chochote kile ukiachacho duniani, kama sio mali, kama sio shamba, kama sio vitu..basi Mungu atatumia hata mifupa yako kuwaponya wengine.. Ndivyo Mungu alivyofanya kwa Elisha baada ya kufa na miaka mingi kupita ameshasahaulika, amebakia tu mifupa, kaburini, lakini maiti ilipoangukia mifupa yake, ile maiti ikafufuka.
Je ni tabia gani unaionyesha kwa Mungu sasa, hadi akupe shamba lake spesheli ambalo Kristo atakuja kupumzikia hapo siku za mbeleni? Watoto wako, vijukuu vyako, vitabarikiwaje kama wewe hutamcha Mungu sasa?
Tafakari maisha ya Yusufu, kisha fananisha na yako utapata majibu. Yatupasa tuichukie dhambi, tuchukie uasherati, tuchukie wizi, tuwe waaminifu, tuishi maisha yanayompendeza Mungu sikuzote.
Na hatimaye na sisi tutakuwa wokovu kwa vizazi vyijavyo.
Bwana atuponye..Bwana atusaidie.
Shalom
WALA HAKUSIMAMA MTU PAMOJA NAYE, YUSUFU ALIPOJITAMBULISHA KWA NDUGUZE
Je! habari ya Yusufu, inabeba ujumbe gani kwa agano jipya?
UVUMILIVU NA MIKAKATI YA ABSALOMU, INA FUNZO NYUMA YAKE.
Kuiaua Nchi ni kufanya nini? (Waamuzi 18:2).
Injili iliyopo kwa Samaki aina ya Eeli.
Huu ni mwendelezo wa Mafundisho maalumu yawahusuyo wanawake.
Mithali 11:16
[16]Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; ..”
Ujumbe huu ni kwako wewe binti/Mama/ ambaye unapenda kuheshimiwa na Mungu pamoja na wanadamu.
Kumbuka heshima inatafutwa na si wote wanayo, kwasababu inagharama yake kuipata…heshima sio uzuri, heshima sio elimu, sio u-kisasa, wala sio pesa..Ni thamani yako ya ndani, inayoonwa na wengine.
Dada Ukitaka kufahamu ni nini kitakupa heshima usiwafuate mabinti wenzako,la! Hata na akili zako pia usizifuate, Bali mtafute aliyekuumba ili akupe siri ni nini kitakuthaminisha hapa duniani kwa wanadamu.
Inatia huruma kuona, mabinti wengi wanadhani wanaheshimiwa kwa urembo wao..hivyo hubuni kila namna ya kujipamba, na kujichubua ngozi zao, wanavaa mawigi na makucha ya bandia, kisha kwa ujasiri wanatembe mbele ya watu..wakidhani kuwa ndio wanaonekana watu wa maana sana kwenye jamii..Ukifanya hivyo Binti umepotea!
Wanadhani kuonyesha miili yao barabarani, na kujifanya wakisasa ni heshima, dada hapo huheshimiwi unasanifiwa tu. Unachofanya ni kujiongezea nafasi tu ya kuwa kiburudisho cha macho ya wahuni..na ndio maana watakupigia miluzi na kukutazama tazama.mara mbili ili kesho urudie kufanya hivyo tena, wajiburudishe macho yao, lakini zaidi ya hapo wewe ni FELIA…
Hivyo fahamu heshima yako inatoka wapi..
Biblia inaeleza heshima ya mwanamke inakuja katika mambo haya saba
Yote haya utayasoma katika vifungu hivi:
Mithali 31:30
[30]Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke AMCHAYE BWANA, ndiye atakayesifiwa.
1 Timotheo 2:9-11
[9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na ADABU nzuri, na MOYO WA KIASI; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; [10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. [11]Mwanamke na ajifunze katika UTULIVU, AKITII kwa kila namna.
[9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na ADABU nzuri, na MOYO WA KIASI; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
[10]bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
[11]Mwanamke na ajifunze katika UTULIVU, AKITII kwa kila namna.
1 Petro 3:3-4
[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; [4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya UPOLE NA UTULIVU, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya UPOLE NA UTULIVU, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
Ukiyazingatia haya binti/mwanamke, heshima itakufuata yenyewe…na lolote ulitamanilo kwa Mungu utalipata tu..Kama ni mume bora Mungu atakuletea, tena zaidi ya matarajio yako kama Ruthu alivyoletewa Boazi,
Kama ni kibali, utakipata tena cheo kikubwa zaidi ya wengi, ikiwa ni utumishi, Bwana ataizidisha karama yako pakubwa sana..Na zaidi ya yote una uzima wa milele. Hata ukienda mbinguni unawekwa kundi moja na akina Sara na Ana na Debora, Mariamu, na wanawake wote mashujaa walioishindania imani ipasavyo.
Lakini kinyume chake ni kweli, usipoyashika hayo, utafanana tu na Yezebeli na ukienda kuzimu utawekwa kundi moja na yeye.
Usiiuze heshima yako.
Jithamini.
NAFASI YA MWANAMKE KATIKA KANISA
MWANAMKE, BINTI, MAMA.( Sehemu ya 1)
USHAURI KWA MWANAMKE WA KIKRISTO.
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?
Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?
SWALI: Mstari huu unamaana gani?
Mithali 23:1-3
[1]Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako. [2]Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi. [3]Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila.
[1]Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako.
[2]Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi.
[3]Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila.
JIBU: Sulemani akiwa kama mfalme alielewa sana tabia za wafalme zilivyo na hivyo kwa uzoefu wake hapa anatoa mapendekezo yake kwa mtu yeyote ambaye ataitwa na mfalme au mtu yeyote mkuu kula chakula pamoja nao.
Anasema chukua tahadhari “Mwangalie sana”..uwe na kiasi na hizo zawadi zake akupazo, hapo ametumia lugha ya vyakula, lakini yaweza kuwa uongozi, fursa, pesa, n.k..anasema uwe na kiasi, kwasababu nyingi za hizo huwa ni za hila.
Kwasababu mfalme hawezi kumwalika mtu, kama haoni kuna faida fulani anaweza kuipata kwake, ingekuwa ni hivyo angekuwa anamwalika kila mtu tu, ikulu na kushiriki naye.
Mfano wa wazi tunauona, kwa malkia Esta alipomwalika Hamani, kama Hamani angelielewa andiko hili, angetafakari mara mbili mbili ni kwanini apewe tu yeye kipaumbele cha juu zaidi ya wengine..Lakini alikuwa anacheka na kufurahia tu mialiko, na matokeo yake yakawa ni kujipeleka mwenyewe kitanzini.
Ni kawaida ya shetani akishaona una hatari ya kuupindua ufalme wake, haji kwa hasira au kiboko, atakuja kwa anasa, alifanya hivyo kwa Bwana Yesu, na kumwambia “hivi vyote nitakupa, endapo utaanguka na kunisujudia”..Bwana akamkemea, na kumfukuza, wakati mwingine mfalme Belshaza alimwita Danieli, amtabirie vizuri juu ya ufalme wake akamuahidi atakuwa mtu wa tatu kwenye ufalme wake, Danieli hakupumbazika na kukaa pamoja naye katika utawala wake wa dhambi, kinyume chake akakataa akatabiri na kuondoka zake..Lakini usiku huo huo kumbe ndio ulikuwa mwisho wa mfalme Belshaza, akavamiwa na wamedi, na kuuawa, sasa kama Danieli angekutwa pale anafanya anasa nao naye pia habari yake ingeishia pale.
Watumishi wengi wa Mungu wakubwa, wamepoozwa moto wao wa injili au utumishi wao kwa ujumla na watu wakuu au wa mamlaka, kwa kukosa kwao kiasi.
Hivyo mstari huu unatupa tahadhari, katika ngazi yoyote ile, iwe ni ngazi ya chini, katika kampuni,au shirika, au katika serikali, tualikwapo, tuwe makini, kuchunguza ni mashauri gani yapo nyuma yake.
Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?
Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.
Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?
WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU
NUHU WA SASA.