Dhambi inafananishwa na mnyama mkali sana wa porini, kama vile simba au chui, au chatu. Utagundua tabia moja waliyonayo hawa wanyama pale wanapowinda ni kuwa hawana papara, Wanakuwa wavumilivu sana mbele ya kitoweo chao, hawakurupuki ovyo kwa kuanza kukikimbiza kutokea mbali, hapana, bali utaona wanajisogoza karibu navyo, taratibu na kwa upole sana, na kwa kuvizia,kana kwamba hawana habari navyo, kiasi kwamba yule anayewindwa, hawezi kugundua chochote.. Hadi pale anapokaribiwa sana, na kurukiwa, au kikimbizwa kwa ghafla ndipo anapogundua haa, kumbe adui yangu alikuwa karibu sana na mimi. Akiwa anajiandaa kukimbia tayari ameshakamatwa..
Na ndivyo ilivyo dhambi tabia yake, haina papara.. Wakati ule kabla Kaini hajamuua ndugu yake Habili, kuna maneno ambayo Mungu alimwambia, embu tusome..
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? USIPOTENDA VYEMA DHAMBI IKO, INAKUOTEA MLANGONI, NAYO INAKUTAMANI WEWE, WALAKINI YAPASA UISHINDE, 8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.”.
Mwanzo 4:3 “Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? USIPOTENDA VYEMA DHAMBI IKO, INAKUOTEA MLANGONI, NAYO INAKUTAMANI WEWE, WALAKINI YAPASA UISHINDE,
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.”.
Unaona? Kumbe dhambi ilikuwa imeshamsogelea sana Kaini mlangoni kama chui, lakini yeye hakuiona, ilikuwa inasubiria tu afungue mlango Fulani katika maisha yake, kisha yenyewe imrukie kwa ghafla, na habari yake iwe imekwisha. Hivyo Mungu akamtahadharisha mapema lakini yeye hakusikia, Na kama tunavyosoma biblia, Kaini hakutubu na kugeuka kuachana na mahasira zake na wivu, badala yake, siku moja akamwambia ndugu yake twenda huko maporini, walipofika kule, alishangaa nguvu ya ajabu ya kuua imemwingia ndani yake kwa ghafla, na moja kwa moja, akachukua kisu akamchinja ndugu yake bila hata huruma.
Jiulize swali ni nani alimfundisha Kaini kuua?, hakuna aliyemfundisha bali ni ile dhambi iliyomnasa ndio ilitekeleza hayo yote. Unapoona mauaji ya kikatili yanatekelezwa na watu usidhani kuwa ni akili zao ziliwatuma hivyo,.Unapoona Yuda anakwenda kumsaliti Bwana wake, tena kwa kumbusu macho makavu, usidhani mwanadamu wa kawaida anaweza kufanya kitendo kama kile hapana, bali dhambi ikishakaba koo, huwezi kunasuka tena, ni sharti utimize mapenzi yake.
Ndugu yangu, leo hii, tabia ya dhambi bado ni ile ile.. Unapohubiriwa utubu dhambi, sio kwa faida ya mchungaji wako, au mwalimu wako, ni kwa faida yako mwenyewe. Kwasababu mimi na wewe sasa hivi tunawindwa vikali sana,..Na kama tutafungua milango yetu kuruhusu kila aina ya dhambi ituchezee tu, tufahamu kuwa mwisho wetu upo mlangoni.
Dhambi ina shinikizo kubwa sana, ikishafanikiwa kukuvaa kama Kaini, au Yuda, ujue hutoki tena, hutajali kifo, hutajali chochote. Kama unaendelea kutoka nje ya ndoa yako, kumbuka upo hatarini kufa, kama unazini zini ovyo, ujue dhambi imeshakuandalia mauti yako. Hatujui itakuwa ni kwa njia ya ukimwi, au kifo, au mapepo, lakini safari yako ipo ukingoni.
Hatupaswi kumwogopa shetani hata kidogo, lakini tunapaswa tuiogope dhambi kweli kweli. Kwasababu yeye ndio yule mnyama atuwindaye. Shetani kazi yake ni kututengenezea mazingira ya sisi kunaswa na dhambi, lakini yeye hana nguvu yoyote ya kukushinda.
Hivyo, tuwe makini, kama hujatubu, ni heri ukatubu sasa, na sio kesho. Hakuna wokovu wa kesho au ule wa “siku moja nitaokoka”. Wokovu wa namna hiyo haupo, wala hautakaa uje milele. Tubu mpendwa ukabatizwe, ukaoshwe dhambi zako, upokee na Roho Mtakatifu, hizi si zama za kutanga tanga na huu ulimwengu wa dhambi, mitandao inawaharibu watu wengi sana. Yesu alituambia, tumkumbuke mke wa Lutu. Tukitaka kuziponya nafsi zetu tutaziangamiza, na tukiziangamiza kwa ajili yake tutaziponya.
Acha mambo ya dunia yakupite, acha fashion zikupitie, acha anasa zikupite, ipoteze nafsi yako kwa Mungu, lakini mwisho wa siku utapona, kuliko kuupata ulimwengu mzima halafu baadaye unakwenda kuzimu milele itakusaidia nini?. Dhambi ni mnyama katili sana.
Bwana atusaidie sana.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali.Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
pia kama utapenda uyapate mafundisho haya kwa njia ya Whatsapp au email basi tutumie ujumbe kwenye namba hizo hizo.
jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mafundisho mengine:
Mada Nyinginezo:
SI KWA UWEZA WALA KWA NGUVU BALI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA.
NI VIZURI SISI KUWAPO HAPA.
Je aliyezungumza na Musa kule jangwani ni Mungu mwenyewe au malaika wake?
UTAKUWA MTORO NA MTU ASIYE NA KIKAO DUNIANI.
HUDUMA YA UPATANISHO.
Rudi nyumbani
Print this post
Tofauti na makabila mengine 11 ambayo Yakobo aliyabariki kama tunavyosoma katika kitabu cha Mwanzo ile sura ya 49. Kabila la Isakari ndio kabila, lililokubali utumishi, tena sio utumishi tu ilimradi utumishi bali utumishi kama wa Punda kwa watu wa Mungu. Unaweza kusema wana wa Isakari walikuwa wajinga, kuongozwa na roho ya punda kama wasemavyo watu sasa hivi. Lakini maandiko yanatuambia, walifanya hivyo kwasababu waliona ni nini kipo mbele yao. Waliona nchi nzuri ya utukufu ikiwangojea, waliona mahali pa mapumziko ya milele pako mbele yao panawasubiri, na hivyo ili kufikia nchi hiyo ni sharti leo hii watumike sana. Soma..
Mwanzo 49:14 “Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo; 15 Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu”.
Mwanzo 49:14 “Isakari ni punda hodari, Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;
15 Akaona mahali pa raha, kuwa pema, Na nchi, ya kuwa ni nzuri, Akainama bega lake lichukue mizigo, Akawa mtumishi kwa kazi ngumu”.
Unaona, alikubali kujishusha, ili awe mtumishi wa kazi ngumu. Kama vile Punda moja anayebeba chakula cha kondoo wengi zizini. Ndivyo alivyojiona kwa wengine. Na matokeo yake biblia inatuambia, wana wa Isakari walikuja kuwa wenye akili nyingi za kujua majira ya nyakati Zaidi ya wote. Ndio waliokuwa wanategemewa na Israeli nzima, kutoa taarifa juu ya nyakati za neema na hukumu zilizoamriwa na Mungu. Akili hizo na hekima hizo walipewa na Mungu mwenyewe.
1Nyakati 12:32 “Na wa wana wa Isakari, watu wenye akili za kujua nyakati, kuyajua yawapasayo Israeli wayatende; vichwa vyao walikuwa watu mia mbili na ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao”.
Je! Na sisi tunaweza kufananishwa na wana wa Isakari? Unajua ni kwanini leo watu hatutaki kumtumikia Mungu, ni kwasababu hatuoni yaliyo mbele yetu, tunaona ya hapa hapa tu, hatuona majira ya neema yanayokuja huko mbeleni, hatuioni Yerusalemu mpya na nchi mpya tuliyoahidiwa na Mungu. Hatuoni Karamu ya mwanakondoo ambayo Yesu alikwenda kutuandalia kwa miaka 2000 sasa ipo karibuni kuanza. Na ndio maana hatutaki leo hii kujitia katika utumishi wa Mungu. Tunachojua ni kujitia katika utumishi wa kusumbukia maisha, tupate magari, tupate majumba, mashamba, tuwe mabilionea., hayo tu, Mambo ambayo fahari yake inaishia hapa hapa duniani.
Hata kuhudhuria ibada tunaona ni mzigo mzito, lakini tupo radhi kufanya kazi siku 365 bila kuchoka, usiku na mchana, tupo radhi kutazama Tv kila siku, lakini kusoma aya moja ya biblia na kuitafakari ni mtihani kwetu..Kama hayo yakitushinda tutawezaje, kuwa watumishi wa Mungu?
Wana wa Isakari waliitambua ile kauli ya Bwana Yesu kabla hata ya yeye mwenyewe kuja..kwamba ukubwa katika ufalme wa mbinguni, sio kuwa na sifa, na ujuzi, na vyeo, na kutumikiwa, hapa duniani, bali ni katika utumishi kwa wengine.. ndio maana wao wakaamua kuwa vile.
Mathayo 20:25 “Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. 26 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;”
Mathayo 20:25 “Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.
26 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu;
27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu;”
Je! Na sisi tunaiona sawasawa hiyo nchi nzuri na ya kumeta meta kule ng’ambo? Kama ndivyo basi tuwe radhi kuwa Punda kwa kondoo wa Mungu, kama ilivyokuwa kwa wana wa Isakari. Tukubali kumtumikia Mungu,bila kutafuta faida zetu wenyewe. Tukubali kuwatanguliza wengine, na sio sisi tu wenyewe na matumbo yetu, kila siku. Ili siku ile Kristo akaketi pamoja na sisi katika kiti chake cha enzi mbinguni.
Kumbuka hizi ni siku za kumalizia, wakati tuliobakiwa nao ni mfupi sana,Injili tuliyonayo sio ya kuliliwa liliwa tena uokoke. Kwasababu muda wake umeshaisha, tumebakiwa na injili ya Ushuhuda tu. Ili siku ile watu wasije wakasema hawakuhubiriwa injili. Embu jiulize wewe ambaye upo kwenye mawazo mawili mawili, ni ujasiri gani unapata kuishi maisha ya namna hiyo?
Unyakuo ukipita leo hii usiku na ukaachwa utamweleza nini Kristo? Au kifo kikikuta ghafla, huko unapokwenda utakuwa mgeni wa nani? Kuzimu ipo na haishi watu kama maandiko yanavyosema. Na ibilisi anataka uendelee katika hali hiyo hiyo, ili mabaya yakukute kwa ghafla, kama yalivyowakuta wenye dhambi wote waliotangulia kuzimu.
Tubu dhambi zako, na Zaidi sana ukawe mtumishi wa Mungu, ufanye kusudi lake hapa duniani. Kwasababu hilo ndilo uliloitiwa.
Bwana akubariki.
WAENDEE WANA WA ISAKARI, UWE SALAMA.
UFUNUO: Mlango wa 17
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Wibari ni nani?(Mithali 30:26)
SWALI: Shalom naomba kujua nini maana ya huu mstari “Roho za manabii huwatii manabii? (1Wakorintho 14:34)
JIBU: Labda tusome kuanzia juu kidogo ili tupate picha kamili mstari huo ulikuwa unamaana gani..
1Wakorintho 14:26 “Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga. 27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. 28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu. 29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue. 30 Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze. 31 Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe. 32 NA ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII. 33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu”.
1Wakorintho 14:26 “Basi, ndugu, imekuwaje? Mkutanapo pamoja, kila mmoja ana zaburi, ana fundisho, ana ufunuo, ana lugha, ana tafsiri. Mambo yote na yatendeke kwa kusudi la kujenga.
27 Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.
28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
29 Na manabii wanene wawili, au watatu, na wengine wapambanue.
30 Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno, yule wa kwanza na anyamaze.
31 Kwa maana ninyi nyote mwaweza kuhutubu mmoja mmoja, ili wote wapate kujifunza, na wote wafarijiwe.
32 NA ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII.
33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu”.
Ukisoma hapo utaona kuna ustaarabu ulizuka miongoni mwa wakristo wa kanisa la Korintho. Walipokuwa kutanika kanisani, kila mtu alikuwa na neno la kusema, kila mtu alikuwa na wimbo wake spesheli wa kumwabudu Mungu, kila mtu alikuwa na ufunuo wake, kila mtu alikuwa na fundisho lake jipya la kuliwasilisha kanisani, kila mtu alikuwa na lugha na tafsiri yake mwenyewe..
Embu tengeneza picha, kila mtu kanisani anazo karama zote, wote wanataka kufundisha kwasababu wamepokea mafunuo, wote wanataka kutabiri kwasababu ni manabii, wote wanataka kufasiri lugha, wote wanataka kuwa waongozaji kwaya n.k…
Utagundua jambo kama hilo likiwepo kanisani, ni wazi kuwa hakutakuwa na kujengana tena, bali mavurugano tu, kwasababu hakuna utaratibu, hivyo hata kuielewa sauti ya Mungu itakuwa ni shida.
Kwamfano tengeneza picha umeenda kwenye shule yenye waalimu wengi, halafu kila mwalimu anataka afundishe masomo yote, hesabati, yeye, kemia yeye, baolojia yeye, na mwingine hivyo hivyo, jiulize wanafunzi wataelewaje? Hawawezi kuelewa bali watachanyikiwa, ni wapi wajifunze, au mwalimu yupi wamsikilize…
Halikadhalika na katika kanisa la wakorintho, Paulo aliwaagiza, wasiwe na utaratibu huo, hata kama imetokea watu 10 au 20 au 50 katika kanisa wamepewa ufunuo kwa wakati mmoja, hawapaswi wanene wote, bali wawape ruhusa walau wawili au watatu tu, na hao wengine wabakie kupambanua..
Na kama ikitokea hao ambao hawajapewa nafasi ya kunena na bado wanang’ang’ania tu wanene na wao, wanapaswa wakumbuke huo msemo wa Paulo kwamba “ROHO ZA MANABII HUWATII MANABII”
Maana yake ni kuwa kama wao ni manabii, wanapaswa watii utaratibu wa manabii wenzao uliowekwa. Hata kama wao hawajapewa nafasi. Kwasababu Mungu sio Mungu wa machafuko,. Na vilevile kama ikatokea mwingine aliyeketi amefunuliwa jambo kubwa zaidi, basi yule wa kwanza, anapaswa awe radhi kumpisha mwenzake, na yeye atulie, kwasababu mambo yote yanafanywa kwa lengo la kulijenga kanisa, na sio kwa lengo la mashindano, au kwa lengo la kutoa mafunuo mengi, ambayo yatafanya kanisa likose shabaha ya kujua kusudi la Mungu ni nini.
Hata sasa, utaratibu huu unapaswa uwe mwendelevu katika makanisa, sio maono yote au mafunuo yote watu waanaoonyeshwa na Mungu yanapaswa yafundishwe ndani ya kanisa kwa wakati huo huo, hapana, vinginevyo tutazama kwenye machafuko na mikanganyiko mingi, bali vichaguliwe viungo viwili au vitatu katika vyenye karama hiyo, kisha sisi wengine tubakie kupambua, na hao wengine wapewe nafasi wakati mwingine..Ili tuweze kumwelewa Mungu.
Lakini kama ikitokea mmojawetu anataka kujiona na yeye ni lazima ya kwake isemwe, akumbuke usemi ule..”Roho za Manabii, huwatii manabii”. Awe tayari kuwatanguliza wenzake kwanza, Kwasababu Mungu si Mungu wa machafuko bali wa utaratibu.
Bwana akubariki
Kwa maombezi/Ratiba za ibada/ Ushauri/ Maswali. Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mafundisho mengin
Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; Mstari huu unamaana gani?.
MATARAJIO YA KILA MWANADAMU DUNIANI NI YAPI?
JE UNAIFANYA KAZI YA MUNGU?
HAKUNA MTU ANIONDOLEAYE, BALI MIMI NAUTOA MWENYEWE
WhatsApp
Kama leo hii Mungu akikutoa katika utumwa wa dhambi (Yaani kuokoka), basi weka akilini kuwa unapopelekwa kutakuwa ni nje ya matarajio yako, na pengine pasiwe ni pa kuvutia kabisa katika macho yako. Ni vizuri tukafahamu njia za Mungu, ili pale tunapokutana nazo tusiwe ni watu wa kulaumu laumu, au kuuliza uliza ni kwanini hivi, kwanini vile?
Kipindi kile Mungu alipowatoa wana wa Israeli katika nchi ya Misri, walitazamia kupitishwa katika NJIA kuu ya mataifa yote, iliyojulikana kama njia ya wafilisti. Njia hiyo ilikuwa ni ya haraka na ya chap chap, kiasi kwamba kama wangeipitia hiyo, ingewachukua wiki kadhaa tu wangeshafika Kaanani. Lakini Mungu alikuwa na sababu ya wao kutowapitisha njia ile..Tusome..
Kutoka 13:17 “Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri; 18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha”.
Kutoka 13:17 “Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, Wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita, na kurudi Misri;
18 lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa silaha”.
Unaona wana wa Israeli walipitishwa katika njia ngeni kabisa machoni pao, njia yenye ukingo wa mbeleni ya bahari, njia ya vichakani, isiyopitwa na watu, njia ya upweke..Mpaka biblia inatuambia hicho ndicho kilichomvutia Farao, kuwafuatilia tena ili wawateke nyara wawarudishe Misri. Lakini hawakujua kuwa Mungu yupo kule kuwatetea.
Kutoka 14:1 “Bwana akasema na Musa, akamwambia, 2 Waambie wana wa Israeli, kwamba warudi na kupiga kambi yao mbele ya Pi-hahirothi, kati ya Migdoli na bahari, kukabili Baal-sefoni; mtapanga mbele yake karibu na bahari. 3 Naye Farao atasema katika habari za wana wa Israeli, Wametatanishwa katika nchi, ile jangwa imewazuia wasitoke. 4 Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Basi wakafanya hivyo. 5 Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena? 6 Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye;”
Kutoka 14:1 “Bwana akasema na Musa, akamwambia,
2 Waambie wana wa Israeli, kwamba warudi na kupiga kambi yao mbele ya Pi-hahirothi, kati ya Migdoli na bahari, kukabili Baal-sefoni; mtapanga mbele yake karibu na bahari.
3 Naye Farao atasema katika habari za wana wa Israeli, Wametatanishwa katika nchi, ile jangwa imewazuia wasitoke.
4 Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Basi wakafanya hivyo.
5 Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena?
6 Akaandalia gari lake, akawachukua watu wake pamoja naye;”
Hata sasa, wapo watu wanapookoka, na ghafla kuona mambo yanakwenda kinyume na matazamio yao, wanapolazimika kuishi staili nyingine ya maisha, wanageuka na kurudi nyuma na kuuacha wokovu. Na tena pale wanapoona, kuna ukigo mzito mbele yao na kwamba wakiendelea na njia hiyo ya wokovu watakwama ndio kabisa wanakimbia kwa miguu yote miwili, na kusema huyu si Mungu.
Pengine mwingine atapitia shida kidogo, au dhiki kutoka kwa ndugu, au kupungukiwa, jambo ambalo ni kinyume na matarajio yake, wakati hapo mwanzo yeye alidhani akimpokea Kristo siku hiyo hiyo mambo yataanza kuwa safi, sasa anapoona kumetokea mitikisiko Fulani katika maisha, anamwacha Mungu anasema huyu sio Mungu.
Ndugu ikiwa kweli umetubu dhambi zako, na umejitwika msalaba wako kumfuata Kristo, umesema mimi na ulimwengu ndio kwaheri, kamwe usitazame nyuma, pale unapoona mambo yanakuja kinyume na matarajio yako, wewe songa mbele. Ni Mungu ndiye kakusudia kukupitisha hapo, usianze kulaumu laumu au kunung’unika, na kusema kwanini mimi, maadamu Kristo yupo ndani ya moyo wako, songa mbele. Unapoona njia hiyo imekuwa ndefu sana, kama vile huielewi itaisha lini? Bado usiwe mwepesi wa kutazama nyuma. Wewe endelea mbele maadamu unamwona Kristo kila siku katika maisha yako. Kumbuka iliwachukua miaka 40 wana wa Israeli kuifikia Kaanani yao.
Nawe pia upo wakati Bwana aliouweka atakufikisha katika Kaanani yako ya hapa duniani na mbinguni. Ni wewe tu, kutambua kuwa njia za Mungu sio njia zetu. Jambo ambalo wengi wetu hatulijua pale tunaposema tumemfuata Kristo, na huku tunamtaka Mungu atatupitisha kwa njia ya wengi.
Kamwe tuondoe hayo mawazo. Yeye ana njia zake, na wanadamu wana njia zao. Hilo tulifahamu. Na pia tukumbuke mtoto yoyote wa Mungu, atapitishwa tu kwenye njia hizo, haijalishi ni mjanja, au hodari, au tajiri au maskini kiasi gani, ni lazima atakutana tu na njia hizi zisizoeleweka za Mungu, kwasababu madarasa ya Mungu hayarukwi. Na tabia ya hizi njia ni kuwa zinaambatana ni miujiza mingi ya Mungu, ikiwa na maana mtu anaweza kufikia mahali anaona amekwama, ghafla anashangaa amepitaje pitaje mazingira hayo, huo ndio uthitibisho kuwa yupo katika njia hiyo ya Mungu.
Lakini kama akistahimili, basi ajue, licha tu ya kuupokea uzima lakini mwisho wako atakuwa ni wa mafanikio na wa Baraka sana hapa duniani.
NJIA YA ‘UTAJIRI MKUU’ KWA KIJANA.
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 2
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
MUNGU HATAZAMI MOTO WA KIGENI,KUWA MAKINI!
Mathayo 24:14 “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja”.
Bwana Yesu asifiwe ndugu mpendwa..
Ukitaka kujua kuwa mambo yote sasa yameshakamilika, kinachongojewa ni UNYAKUO tu, angalia hali ya mavuno shambani mwa Bwana. Embu fananisha watu waliokuwa wanamjia Kristo kipindi cha mitume, na watu wanaookoka sasa katika kipindi chetu hichi.
Kipindi kile injili ilipokwenda kuhuburiwa mahali kwa mara ya kwanza, mwitikio wa watu wa kumgeukia Kristo ulikuwa ni wa kustaajabisha sana, utakumbuka baada ya Pentekoste tu, kanisa lilikuwa likijiongeza kwa idadi ya maelfu, kwa injili ndogo sana. Na ndio maana kwa kipindi kifupi sana, ukristo ulienea ulimwenguni kote, na sio kuenea tu, badi kuhubiriwa (Wakolosai 1:6, 1Wathesalonike 1:8).Hiyo ni kuonyesha kuwa kweli ule ulikuwa ni wakati wa mavuno.
Lakini angalia sasa, mambo ni tofauti hakuna mtu asiyeifahamu injili, au kuzijua habari za Kristo, wote tunazifahamu, lakini jiulize kwanini, watu hawataki kuokoka, kinyume chake ndio wanakwenda mbali kabisa na Ukristo..Hiyo ni kuonyesha kuwa mavuno yameshakwisha shambani, kilichobaki ni magugu tu.
Na hiyo imepelekea sasa injili kubadilika sio tena ya kuwavuta watu, bali ni ya ushuhuda. Unapoona, injili imekufikia hapo ulipo kitandani kwako ukiwa umeishika simu yako na kusoma, ujue hiyo sio ya kukuvuta wewe, hiyo ni ya ushuhuda tu, ukiona injili imekufikia hapo sebuleni kwako unapotazama tv na familia yako, injili inakufikia kwenye hivyo vipeperushi unavyovisoma huko mitaani. Unapewa biblia bure ya kwenye simu yako, mambo ambayo hata zamani hayakuwepo. Basi ujue hiyo sio injili ya kukuvuta tena kwa Kristo ndugu. Ni injili ya USHUHUDA Tu. Ili utakapokufa katika dhambi zako, usiwe na sababu ya kusema sikuwahi kusikia, au kuona, au kuambiwa.
Wewe jiulize tu, ni kwanini pamoja na mahubiri yote hayo uliyohubiriwa na kuyasikia siku zote za maisha yako, na bado huna badiliko lolote ndani yako. Unadhani ni jambo la kawaida? Hapana, kwa kawaida Neno moja tu lingetosha kukufanya uwe mtakatifu sawasawa na Waebrania 4:12. Lakini hujageuka kwasababu wewe sio Ngano bali ni gugu tu.
Kilichosalia sasa hivi ni Mungu anatazama walau kama yatakuwepo masalia salia machache ayaokoe. Lakini nataka nikuambie, moja ya hizi siku ambazo zinahesabika, tutashuhudia mabadiliko makubwa sana duniani. Tutashuhudia tendo kuu la Unyakuo wa kanisa.
Ndio yale maneno ambayo Bwana Yesu alisema, .(Mathayo 24:40-42) yatatimia hapo. Usiku huo wawili watakuwa wamelala mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wanasaga(ikimaanisha watakuwa katika biashara zao), mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa. Wale watakaoachwa, huku duniani kitakachokuwa kinaendelea ni vilio na kusaga meno. Wakijuta kwanini kipindi kile hawakuitii sauti ya Mungu, ilipokuwa inawavuta kwake kwa upole. Watalia na kuomboleza, kweli kweli, ndugu usiwe mmojawapo.
Lakini watakaokuwa wamenyakuliwa, moja kwa moja wataelekea mbinguni wakiwa na miili yao ya utukufu, katika ile karamu ya mwana-kondoo. Kwenye raha isiyokuwa na kifani. Wakifutwa machozi kwa taabu zao walizokuwa wanapitia huku duniani kwa ajili ya Kristo.
Ndugu mambo haya unaweza kuona kama ni hadithi, au mambo yatakayotokea miaka elfu 5 mbeleni, usijidanganye. Yesu aliposema TUBUNI, kwa maana ufalme wa mbinguni UMEKARIBIA. Alikuwa hasemi uongo. Ni kweli ufalme wa mbinguni ulikuwa umekaribia, jiulize sisi wa sasa hivi tusemeje?.
Maanisha kugeuka, unaposikia injili kwa wakati huu.
Shalom.
UNYAKUO.
KUMBE MUNGU ANAWEZA KUKULIPA KWA USICHOSTAHILI!
MWANZO WA INJILI YA YESU KRISTO.
UFUNUO: Mlango wa 14
Kuwiwa maana yake nini katika biblia?
Je watu ambao hawajasikia kabisa injili watahukumiwa?
Katika ukristo ogopa sana ile kauli ya kusema “Huu si wakati”… “Bado kidogo”…. “Wakati wake utafika tu siku moja”… Ogopa sana kauli kama hizo, tena ziogope kuliko ukoma.
Kwanini ninakuambia hivyo? Ni kwasababu wakati ambapo unafikiria majira yake bado, huo ndio wakati Kristo anatazamia kuona matunda kwako. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na asili. Hana tabia ya kutafuta matunda wakati wa msimu. Haongozwi na misimu.
Embu kitafakari vizuri kitendo alichokifanya siku ile alipokuwa anakwenda Yerusalemu kutokea Bethania, alipokutana na ule mtini njiani, alifanya nini!. Utaona alikwenda moja kwa moja na kutafuta matunda juu yake, Na alipokosa akaulaani na kunyauka saa ile ile , pasipo kujali kuwa ule haukuwa hata msimu wake wa kuzaa..
Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa. 13 Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; MAANA SI WAKATI WA TINI. 14 Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”.
Marko 11:12 “Hata asubuhi yake walipotoka Bethania aliona njaa.
13 Akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili labda aone kitu juu yake; na alipoufikilia hakuona kitu ila majani; MAANA SI WAKATI WA TINI.
14 Akajibu, akauambia, Tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunzi wake wakasikia”.
Hili ni jambo ambalo watu wengi hawalifahamu, wanapoangalia mazingira Fulani, wanaona kama vile wakati wake bado, pale mtu unapomuambia biblia inasema “saa ya wokovu ni sasa, na wakati uliokubalika kuokoka ni leo (2Wakorintho 6:2 )” yeye atasema, ngoja kwanza, siku moja nitaokoka tu!, ngoja nimalize chuo, ngoja nioe kwanza, ngoja nipate kazi, ngoja nitoke kwanza kwa wazazi wangu..Ngoja nijenge nyumba yangu kwanza..
Huku akitazamia kweli siku moja akishavipata hivyo vitu ndio atatulia afikirie sasa kumtumikia Mungu. Lakini hajui wakati amekaa akiungojea huo wakati ufike Kristo anatokea ghafla kwenye maisha yake, kutafuta matunda, anayakosa, hatua inayofuata kwake ni KULAANIWA MILELE.
Maana yake ni kuwa kamwe asahau WOKOVU katika maisha yako, na ndio maana watu kama hao ambao wana tabia ya kusubiri, subiri, kujivuta vuta, mwisho wa siku unawakuta mpaka wanakufa hawajaokoka haijalishi kuwa wameshapata kila kitu. Sio kwamba kulikuwa na ugumu wowote. Hapana lakini kwasababu walishalaaniwa na Yesu tangu zamani, walipotazamiwa wamzalie Kristo matunda wakashindwa.
Hivyo ndugu, tambua kuwa jicho lako sio jicho la Yesu. Wewe unatazama misimu, Yesu hajui msimu. Wewe unatazama nyakati, Kristo hajui nyakati. Wakati wowote anataka ajapo akukute, ukiwa na matunda. Akukute unamzalia matunda ya Roho. Lakini ukiwa ni mtu wa kusubiria siku Fulani ifike ndio ufanye maamuzi. Upo katika hatari kubwa sana ya kulaaniwa.
Wana wa Israeli, kuna wakati nao pia walijibunia utaratibu kama huo, wakati ambapo Mungu alishawapa tamko la kwenda kumjengea nyumba, Lakini walipopokea vitisho kutoka kwa mfalme aliyefuata kwamba waache ujenzi, wao nao wakasikiliza sauti yake kweli wakaacha. Ukisoma pale utagundua kuwa Kilichofuata ni Mungu kuwalaani, akawapiga kwa umaskini na shida zisizokuwa za kawaida. Mpaka siku walipogundua kosa lao, na kwenda kumjengea tena Mungu nyumba, walijutia mawazo yao.
Hagai 1:2 “Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya Bwana. 3 Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, 4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika”?
Hagai 1:2 “Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Watu hawa husema, Huu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujenga nyumba ya Bwana.
3 Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,
4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika”?
Leo hii, mtu akishazuiwa na wazazi wake, au boss wake, au mume wake, basi hiyo ndio inakuwa tiketi ya yeye kuukimbia kabisa wokovu au utumishi wa Mungu, akijitetea kuwa pengine haukuwa wakati sahihi na ndio maana vikwazo kama hivyo vimetokea. Nataka nikuambie, ondoa hayo mawazo kuanzia leo, kwasababu hata kwa Yesu hayapo, utalaaniwa.
Upokee wokovu leo, tubu dhambi zako leo, kuwa tayari kubatizwa katika ubatizo sahihi leo, anza kuishi maisha matakatifu yampendezayo Mungu, bila kujali mazingira, watu, hali, au msimu,..Na baada ya hapo yeye mwenyewe atakupokea na kukujalia kuzaa matunda wakati huu huu, unaoonekana kama haufai kwako.
Kumbuka hizi ni siku za mwisho, wakati wa mavuno umekaribia sana, dalili zote zinaonyesha kizazi chetu tunachoishi kitashuhudia tukio halisi la kurudi kwa Bwana Yesu duniani mara ya pili, kulinyakua kanisa lake. Jiulize Ikiwa atarudi leo usiku utakuwa na lipi la kujitetea, ikiwa hukumpa maisha yako? Au ukifa leo utamweleza nini huko uendako kama Yesu si mwokozi wa maisha yako.
Usizifiche dhambi zako, ikiwa upo tayari kuokoka leo, basi uamuzi huo utakuwa ni wa busara sana kwako. Basi popote pale kama utahitaji msaada huo wasiliana nasi kwa namba hizo hapo chini, au tafuta kanisa la kiroho lililo karibu na wewe, wakusaidie kupokea wokovu.
Kisha hakikisha unatafuta ubatizo sahihi wa kuzamishwa kwenye maji mengi, na kwa jina la YESU KRISTO (Zingatia sana hilo), kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako. Na yeye mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu.
Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita..
AINA TATU ZA WAKRISTO.
UFUNUO: Mlango wa 22
JE UNAYAFANYA MAPENZI YA MUNGU?
Mlima wa Mizeituni unaumuhimu gani kwetu?
VAZI LA YESU HALIGAWANYWI.
Kuna silaha ambazo nataka ufahamu shetani anazozitumia kwa watu ambao wanakaribia kuokoka, au waliookoka lakini bado ni wachanga katika imani. Silaha hizo, zimewafanya watu wengi waishi katika hofu, na misongo mikubwa ya mawazo, mimi nikiwa mmojawapo kabla sijaokoka.
Nataka nikuambie mawazo haya yakikujia, yakatae kwa nguvu zako zote, kwasababu ni vita vya kifikra ambavyo shetani na majeshi yake ya mapepo wanavyoleta ili kukuangusha uiche imani, au usisonge mbele. Narudia tena usiruhusu hata kidogo mawazo hayo yakutawale;
1) Umemkufuru Roho Mtakatifu:
Hii ndiyo silaha ya ibilisi ya kwanza ; Anakuletea mawazo kuwa wewe huwezi kusamehewa, kwani dhambi yako ni ya kumkufuru Roho Mtakatifu. Na anaweza kukurushia mpaka hayo mawazo ya namna hiyo ili ujione wewe tayari dhambi yako imeandikwa kwa kalamu ya chuma.
Nataka nikuambie, huo ni uongo tu, dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu haiji hivyo. Na kamwe mtu aliyemkufuru Roho hata hofu na Mungu hana ndani yake, ni mfano wa mafarisayo na masadukayo ambao walikuwa wanazipinga kazi za Roho Mtakatifu wazi wazi na kuzishuhudia hadharani kuwa ni za mapepo wakati wanaujua kabisa ukweli kwamba na Roho Mtakatifu ndiye aliyekuwa anafanya kazi zile (Mathayo 12:24-32).
Sasa jiulize wewe ni lini ulishawahi kwenda kuzipinga kazi za Roho Mtakatifu huku ukajua kabisa ndio yeye, halafu ukatoa maneno ya kufuru na kusema zile ni kazi ya mapepo..Ulishawahi kufanya jambo kama hilo mbele ya kadamnasi? Ni wazi kuwa hujawahi kufanya.. Sasa hayo mawazo ya wewe umemkufuru Roho Mtakatifu yametoka wapi kama sio kwa shetani?
Watu wengi, nimewasiliana nao, wamekuwa wakisumbuliwa na mawazo mkandamizo kama hayo, Lakini leo nataka nikuambie Usiogope, hiyo ni ishara kuwa Mungu yupo karibu na wewe sana, unachopaswa kujua ni kufahamu ile kweli, ili ikuweke huru kweli kweli.
2) Bado hujaokoka:
Unaweza ukawa umetubu kweli dhambi zako kwa kudhamiria kuziacha, na ukabatizwa katika ubatizo sahihi, na baada ya hapo ukaanza kuishi maisha yanayompendeza Mungu, Lakini kipindi fulani kikapita shetani akakuletea mawazo kwamba bado hujaokoka, wanaookoka hawawi kama wewe. Mawazo kama haya, yakatae, Bwana Yesu alisema, “Hakuna mtu anayeweza kwenda kwake, kama Baba yake hajamvuta kwake (Yohana 6:44)” Hivyo mpaka wewe umefikia hatua ya kutubu, na kubatizwa na kuanza kuonyesha bidii ya kuishi sawasawa na mapenzi yake, haikuwa kwa akili zako, bali ni Yesu mwenyewe alikuvuta.
Hivyo songa mbele, zidi kujitakasa siku baada ya siku, mpaka kuufikia ukamilifu kwasababu Yesu yupo pamoja na wewe.
3) Umeshachelewa:
Hili ni jambo lingine ambalo, limewadhoofisha wengi. Wanadhani elimu ya kidunia ni sawa na elimu ya ufalme wa mbinguni. Elimu ya kidunia, ukishakuwa mtu uzima na hujaenda shule, unaweza ukaonekana kama umeshachelewa. Duniani ukifikisha umri fulani hujaolewa, au hujapata kitu fulani umeshachelewa. Lakini kwa Mungu haiendi hivyo, maadamu pumzi ya uhai ipo ndani yako bado hujachelewa kumtumikia yeye.
Mungu anakutazama, ufanye vizuri isipokuwa tu uonyeshe bidii, ili ufanye vizuri kuliko hata wale ambao walikuwepo tangu zamani. Embu mkumbuke mtume Paulo, hakuwa miongoni mwa wale 12, wala siku ile ya Pentekoste hakuwepo. Lakini alikuja kufanya kazi kubwa kuliko wote waliomtangulia.
Ukumbuke pia ule mfano wa mwajiri na waajiriwa ambao Bwana Yesu aliutoa, akasema kulikuwa na wengine ambao walikutwa jioni kabisa hawana kazi yoyote, wakaambiwa waende shambani, na kule shambani walipomaliza shughuli yao, wakalipwa sawa sawa na wale wengine, ambao walikuwa tangu asubuhi shambani.(Mathayo 20:1-16). Na ndio maana Bwana Yesu akamalizia na kusema “wapo walio wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wale wa kwanza watakuwa wa mwisho”.
Vivyo hivyo na wewe, ikiwa umeitwa kwenye miaka ya 20, au 30 au 40 au 50 au 80. Hujachelewa popote pale. Mtumikie Bwana kwa moyo wako wote na kwa uaminifu. Na thawabu yako inaweza kuwa kubwa kama tu ile ya mitume.
4) Mungu hawezi kupendezwa na wewe:
Haya mawazo yanakuja hususani pale ambapo pengine hukutumiza wajibu wako fulani uliloambiwa na Mungu ufanye, au ulifanya dhambi fulani ambayo ilikuwa ni ya makusudi kabisa kwa Mungu, pengine ulivunja viapo vya ndoa yako ukaenda kuzini, au uliua mtu, au uliiba n.k..
Nataka nikuambie kama umetubu tayari kwa kumaanisha kutoka katika moyo wako. Basi usiruhusu tena hayo mawazo yawe ndani yako, kukutawala. Mrudie Mungu wako, mtumikie kwa bidii, kwani kumpendeza tena kunawezekana, na akawa rafiki yako, zaidi hata ya pale mwanzo kama utatii. Daudi alizini ni mke wa Uria, lakini alitubu, hata baada ya kuadhibiwa na Mungu, aliendelea kumtafuta Mungu wake, na mwisho wa siku bado akawa mtu ambaye ameupendeza moyo wa Mungu.
5) Fulani ni bora kuliko wewe mbele za Mungu:
Haya ni mawazo mengine ya ibilisi, kukukandamizi tu usipige hatua, kwamba fulani ni zaidi yako wewe mbele za Mungu. Hilo jambo halipo, Mungu hana utaratibu huo wa kulinganisha watu.Yeye huwa anasimama katika utaratibu wake. Ni sawa na mwalimu anayesahihisha mitihani, hasahishi kwasababu fulani ni machachari kuliko wengine, hapana, bali kwasababu amejibu sawasawa na alichotaka.
Ndivyo ilivyo kwa Mungu, hana habari na sura ya mtu, ikiwa wewe utatembea katika njia zake, basi atakuwa rafiki kwako, wala hakulinganishi na mtu mwingine aliye juu yako au aliye chini yako, na Yule mwingine hamlinganishi na wewe, bali wote anawalinganisha na Neno lake, kila mmoja kivyake.
Hivyo na wewe tembea katika njia yako, na Mungu wako, acha kujilinganisha na fulani, jilinganishe na biblia. Vinginevyo shetani atakuletea mikandamizo ya mawazo ukashindwa kumtumikia Mungu kwa ufanisi, kwa kumwona fulani tayari ni mtiwa mafuta wa Bwana, wewe huwezi kumfikia yeye.
Mawazo kama hayo yakatae.
Kumbuka, kuingia katika wokovu ni kurahisi sana, lakini kudumu kunakuwa kugumu, na hiyo yote inasababishwa na shetani na mapepo yake, Na dawa ya shetani sio tu kuomba, bali pia kulijua NENO. Nikisema Neno, sio kukariri vifungu vya biblia hapana, bali kupata ufunuo wa Neno la Mungu katika maisha yako ya kila siku.
Bwana Yesu alimshinda shetani kwa Neno kule jangwani, vivyo hivyo na wewe. Mungu anaweza akawa ameshakupa uhuru, lakini kama hutakuwa na maarifa ya kutosha ya kuupigania uhuru wako, bado ibilisi atakusumbua hata kama umeokoka. Maombi ya kufunguliwa pekee hayawezi kukufanya kuwa huru.. Kama ni hivyo Bwana Yesu asingesema..Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru” (Yohana 8:32)Umeona kinachokamilisha uhuru wa mtu ni KWELI, na KWELI ni Neno la Mungu. (Yohana 17:17)
Hivyo jitahidi sana, uwe mtafakariji wa Neno. Ili ujue nafasi yako kwa Mungu ni ipi, wakati huu ni wakati wa vile VITA vikali ambavyo, Danieli alionyeshwa, katika (Danieli 10:1). Si vita tena vya kimwili, bali vita vya kifikra vinavyoletwa na ibilisi na mapepo yake.
Kama hujatubu, nafasi bado unayo. Tubu sasa mgeukie muumba wako, kisha ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi zako, ikiwa hukufanya hivyo. Na baada ya hapo Mungu atakupa Roho wake Mtakatifu atakayekusaidi kuifahamu kweli yote ili uwe huru (Yohana 16:13).
Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
NAMNA YA KUITAMBUA SAUTI YA MUNGU INAPOZUNGUMZA NA WEWE
Nakusalimu katika jina kuu sana la mwokozi wetu Yesu Kristo. Karibu tuyatafakari maandiko maadamu siku ile inakaribia.
Tukitazama matukio yaliyokuwa yanaendelea pale msalabani yapo mambo kadha wa kadha tunaweza kujifunza. Kwamfano siku ile utaona walimvua nguo zake zote, wakazigawanya mafungu manne, kila askari fungu lake. Hii ikiwa na maana kuwa Bwana Yesu alisulibiwa akiwa uchi kabisa, hakutuonea haya sisi, iweje sisi tumwonee haya yeye?
Lakini wale askari walipofika kwenye Kanzu yake nayo, kwasababu ilikuwa ni ya Tano, na wenyewe walikuwa ni wanne, na kila mmoja alitaka apate sehemu ya vazi lile..Wakaona njia rahisi ni kuligawanywa, walau kila mtu apate kipande chake.
Lakini lile vazi lilikuwa ni la kitofauti sana, lilikuwa halijashonwa kwa kuunganishwa vipande mbalimbali hapana.Bali Lote tokea juu hadi chini lilikuwa ni vazi moja, kiasi kwamba kulikuwa hakuna sehemu lilikuwa na kipande kilichojitegemea kikaunganishwa nalo hapana. Unaweza kutazama mfano wa vazi hilo kwenye picha juu.
Hivyo wale askari walipotafuta walau, maungio ya vazi lile ili wawezi kukata wagawane kila mtu kipande chake hawakuona. Pengine walitafuti kwenye mikono hawakuona, kwenye kola hawakuona, kwenye mfuko hawakuona. Mwishoni wakaona ni heri walipigie tu kura, ili liwe la mmojawapo.
Yohana 19:23 “Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. 24 Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari”.
Yohana 19:23 “Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu.
24 Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari”.
Lakini tunaposoma habari hiyo ni jambo gani Mungu anataka tujue? Je! Ni mambo ya mavazi yake tu kupigiwa kura tu au ni nini?
Ujumbe mkuu Mungu anataka tuone hapo ni kwamba VAZI LA YESU HALIGAWANYI.. Kwasababu halija ungwaungwa, kama mengine yalivyo. Kama utalihitaji ni sharti ulichukue lote, au uliharibu kabisa, hakuna namna..
Hata sasa, mtu yeyote anayeamua kuwa mkristo, hana budi alivae vazi hili. Ambalo haliungwi ungwi.. Ndilo linalojulikana kama VAZI LA WOKOVU, Tunalolisoma katika
Isaya 61:10 “Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana AMENIVIKA MAVAZI YA WOKOVU, AMENIFUNIKA VAZI LA HAKI, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Unapolivaa vazi hili ni lazima UUISHI wokovu wote, huwezi kuyakwepa maisha ya utakatifu.. Wakristo wengi wanatafuta kuligawanya vazi la wokovu wawe nalo kwa sehemu tu, hawataki kujitoa kikamilifu kwa Mungu pale wanapookoka. Wanataka waitwe wanakwaya, lakini bado waendelee na uzinzi kwa chini chini, wanataka waitwe vijana waliokoka, lakini waendelee kwenda disco, wavae vimini, na milegezo, na viduku, Wanadhani, hilo jambo linawezekana katika wokovu. Ni kweli litawezekana kwenye dini zao, na madhehebu yao, lakini kwa KWA YESU hilo jambo halipo.
Ndugu, watakaokwenda kwenye UNYAKUO, watakuwa wale tu walio tayari kulichukua vazi lote la Yesu, hao ndio wanaojulikana kama BIBI-ARUSI wa Kristo. Lakini tukijidanganya kuwa tumeokoka, halafu bado tupo nusu nusu, hatueleweki sisi ni wa upande upi, ipo wazi kuwa wakati ule tatabaki tu hapa duniani kwenye dhiki kuu ya mpinga-Kristo, na kama hutakuwa hai, basi utaendelea kubakia makaburini mpaka siku ile ya ufufuo itakapofika uhukumiwe uende motoni.
Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. 8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; KWA MAANA KITANI NZURI HIYO NI MATENDO YA HAKI YA WATAKATIFU”.
Ufunuo 19:7 “Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.
8 Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing’arayo, safi; KWA MAANA KITANI NZURI HIYO NI MATENDO YA HAKI YA WATAKATIFU”.
Naamini utakuwa unatambua kuwa tunaishi katika kanisa la Laodikia, na uvuguvugu na tabia ya kanisa hili ni kuwa lipo Vuguvugu, tofauti na yale mengine. Hivyo Bwana atuepushe na uvuguvugu huu uliopo duniani leo.
Maran atha.
PINDO LA VAZI LAKE SASA LIMEREFUSHWA.
Nini maana ya “mkilichukia hata vazi lililotiwa uchafu na mwili”?
kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?
WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.
SWALI: Biblia inamaana gani kusema “vipo sita, naam saba”. Kwanini isingesema tu mara moja saba, mpaka ianze sita,halafu tena saba?
JIBU: Ni lugha ya zamani, iliyotumika kuwekea msisitizo kitu hususani kile cha mwisho, yaani, kama inadhaniwa ni sita, basi kipo na cha saba ambacho ndio zaidi.
Kwa mfano ukisoma ile Mithali 6:16 inayozungumzia mambo sita ambayo Mungu anayachukia utaona anaongezea na kingine cha saba, ambacho ni “kupanda mbegu ya fitina katika ya ndugu” ikiwa na maana hicho ndio kibaya zaidi..
Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake. 17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia; 18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; 19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu”.
Mithali 6:16 “Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana; Naam, viko saba vilivyo chukizo kwake.
17 Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;
18 Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu;
19 Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu”.
Ukisoma pia Mithali 30:18 “utaona Sulemani anasema tena kati ya mambo ambayo yanamshangaza mienendo yao, yapo matatu lakini lile la nne ndio zaidi, ambalo ni mwendo wa kijana pamoja na msichana.
Mithali 30:18 “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu. 19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana”.
Mithali 30:18 “Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna manne nisiyoyafahamu.
19 Mwendo wa tai katika hewa; Na mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu pamoja na msichana”.
Vivyo hivyo, ukisoma Mithali 30:29, Sulemani anasema pia vipo vitu vitatu vyenye mwendo wa kupendeza lakini akakiongezea na cha nne chenye mwendo wa kupendeza zaidi nacho ni mfalme asiyehasika.
Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri. 30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote; 31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki”.
Mithali 30:29 “Kuna watatu wenye mwendo wa kupendeza, Naam, wanne walio na mwendo mzuri.
30 Simba aliye hodari kupita wanyama wote; Wala hajiepushi na aliye yote;
31 Jimbi aendaye tambo; na beberu; Na mfalme ambaye haasiki”.
Soma, pia vifungu hivi;
Mithali 30:15 “Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi! 16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!”
Mithali 30:15 “Mruba anao binti wawili, Waliao, Nipe! Nipe! Kuna vitu vitatu visivyoshiba kamwe, Naam, vinne visivyosema, Basi!
16 Kuzimu; na tumbo lisilozaa; Nchi isiyoshiba maji; na moto usiosema, Basi!”
Ayubu 5:19 “Yeye atakuokoa na mateso sita; Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.
Amosi 1:3 “Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma”;
Soma pia Amosi 1:4.
Na hata sasa, katika mambo saba(7) ambayo biblia inasema yanamkamilisha mwanadamu, lipo la nane(8) ambalo ndio kuu zaidi linaloitwa UPENDO.
Tusome.
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, 6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, 7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, UPENDO. 8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
2Petro 1:5 “Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa,
6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa,
7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, UPENDO.
8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.
Ni vizuri tukawa na hayo mengine yote, lakini tukikosa upendo wa Ki-Mungu, basi bado hatujakamilishwa.
Je! Upendo wa AGAPE upo ndani yako?
Ili kufahamu tunaupate upendo wa namna hii, fungua link hii>>
https://wingulamashahidi.org/2020/12/21/nitaupataje-upendo-wa-ki-mungu-ndani-yangu/
UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?
NI NINI KITAKACHOTUFANYA TUPIGE MBIO BILA KUPUNGUZA MWENDO?
UFUNUO: Mlango wa 1
Je! kuna madhara kuchukiwa na kila mtu kwasababu huna mali?. Kama biblia inavyosema katika Mithali 14:20?.
Mpumbavu ni nani katika biblia? (Zaburi 14:1, Mithali 10:14)
JIBU: Ukisoma katika kitabu cha Kutoka, utaona kuna habari kama inajichanganya kuhusiana na baba-mkwe halisi wa Musa, Kwamfano Kutoka 2:18 Inasema aliitwa Reueli, lakini sehemu nyingine zote zilizosalia kama vile Kutoka 3:1,4:18, inamtaja kama ni Yethro. Je kuna makosa ya kiuandishi?
Embu tusome baadhi ya vifungu hivyo;
Kutoka 2:15 “Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima. 16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao. 17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao. 18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo? 19 Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi. 20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula. 21 Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora.
Kutoka 2:15 “Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima.
16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.
17 Wachungaji wakaja wakawafukuza; lakini Musa akasimama, akawasaidia, akalinywesha kundi lao.
18 Walipofika kwa Reueli baba yao, akasema, Imekuwaje hata mkarejea mapema leo?
19 Wakasema, Mmisri mmoja alituokoa katika mikono ya wachungaji, tena zaidi ya hayo, akatutekea maji, akalinywesha kundi.
20 Akawaambia binti zake, Yuko wapi basi? Mbona mmemwacha mtu huyo? Mwiteni, ale chakula.
21 Musa akawa radhi kukaa kwake mtu yule, naye akampa Musa binti yake, Sipora.
Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu”.
Jibu ni kuwa hakuna hitilafu, yoyote ya kiuandishi isipokuwa zamani ilikuwa ni jambo la kawaida mtu mmoja kuwa na jina zaidi ya moja, Kwamfano tukimtazama Yakobo, Mungu alimwambia utaitwa Israeli, Hivyo majina yake yote mawili utayakuta yakiandikwa sehemu mbalimbali katika biblia Lakini mtu ni Yule Yule mmoja.
Vivyo hivyo na Yethro mkwewe Musa, aliitwa pia Reueli, na kwasababu alikuwa ni kuhani, hatushangai kuona akiwa na majina mawili, moja la kwake la asili na lingine la kikuhani.
Mafundisho mengine
UTAJI ULIOKUWA JUU YA USO WA MUSA.
Je Musa yupo anawashitaki watu..kulingana na Yohana 5:45?
Je Musa kumwoa Sipora, Mkushi alifanya dhambi?
USIKATE TAMAA UNAPOPITIA MAGONJWA.