SWALI: Kaini baada ya kumuua ndugu yake Abeli, alikimbilia katika nchi ya Nodi, Naomba kufahamu Je! Huko alipatia wapi mke na kuzaa naye watoto? (Mwanzo 4:16).
JIBU: Ukisoma Mwanzo 5:1-5 utaona inasema….
“1Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
4 Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, AKAZAA WANA, WAUME NA WAKE
5 Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na the lathini, naye akafa.”
Sasa kwenye Mstari huo wa 4 utaona kuwa kumbe mbali ya Kaini na Abeli kuzaliwa na Adamu kulikuwa na wana wengine wa kike na wakiume waliokuja kuzaliwa kwenye familia yao pia, na ndio huko huko Kaini alipojitwalia mke.
SWALI: Kama KAINI alitwaa mke ambae alizaliwa na Adamu na Hawa ambao ni wazazi wake kwahiyo alimuoa dada yake je,kwahiyo nihalali kumuoa mwanamke ambae ni dada yangu wa damu?”.
JIBU: Kumbuka hata Adamu mwenyewe hakwenda kumtwaa mke kutoka kwenye familia nyingine, bali katika ubavu wake mwenyewe, hivyo kama ni undugu basi Adamu na hawa wana undugu mkubwa zaidi ya Dada na kaka…
Unaona? Mungu aliruhusu iwe hivyo mwanzoni kwa ajili ya uzazi, ili watu waongezeke, lakini baadaye Mungu alitoa maagizo kuwa ni makosa mtu kutwaa ndugu wake wa karibu na kumfanya kuwa mke wake..
Mambo ya walawi 18:6 “Mtu ye yote aliye wa kwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi Bwana”.
Na pia mstari wa 9 unasema…
9″ Utupu wa umbu lako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, kwamba alizaliwa nyumbani mwenu au kwamba alizaliwa kwengine, utupu wa hao usifunue”.
Kwahiyo ni machukizo kuoa ndugu yako yoyote yule wa karibu.
Ubarikiwe
Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Mada Nyinginezo:
MTI WA UZIMA NA MTI WA MAARIFA.
SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
JIBU: Mungu alimpa maagizo nabii Hosea kuoa mke aliye kahaba, sio kwasababu Mungu, anahalalisha usherati, hapana! Kusudi la Mungu kufanya vile ni kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli ni jinsi gani wao wanavyofanya uasherati katika roho zao mbele zake kwa kuyaacha maagizo yake.. Kwahiyo nabii Hosea alipooa mke wa uzinzi, ilikuwa kama ishara ya Bwana kutaka kuwaonyesha wana wa Israeli mambo wanayoyafanya mbele zake…
Sasa Bwana alitaka endapo watu watakapomwuliza Hosea kwanini ameoa mke ambaye ni mzinzi…ndipo Hosea awajibu, kama mimi ninavyoudhiwa na huyu mwanamke mzinzi ndivyo na ninyi (wana wa Israeli) mnavyomuudhi Bwana kwa kufanya uzinzi mbele zake kwa kulihalifu agano lake na kuabudu miungu migeni, ukisoma habari ile yote kwa urefu utaona jambo hilo.
Sio mara ya kwanza Bwana kutoa ishara kupitia maisha ya watu, ukisoma biblia mahali pengine utaona Nabii ezekieli Bwana anamwagiza ale kinyesi, mahali pengine akate nywele zake kwa upanga azigawanye sehemu tatu….sehemu nyingine anaambiwa ahame nyumba yake kwa kutoboa ukuta, huku amejifunika macho kumwonyesha Mfalme wa Yuda Sedekia kwamba wakati majeshi ya wakaldayo yatakapouzingira mji kwa miaka miwili, yeye atatoroka kwa njia ya kutoboa ukuta wa mji, na hatimaye watamkamata na kumtoboa macho yake sawasawa na nabii Ezekieli alivyoonyesha…
Ezekieli 12:1 Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.
3 Basi, mwanadamu, funga tayari vyombo kwa uhamisho, ukahame wakati wa mchana mbele ya macho yao; nawe utahama toka mahali pako hapa mpaka mahali pengine mbele ya macho yao; labda watafahamu, wajapokuwa ni nyumba iliyoasi.
4 Nawe utatoa vyombo vyako, wakati wa mchana, mbele ya macho yao, kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa; nawe mwenyewe utatoka, wakati wa jioni, mbele ya macho yao, kama watu watokavyo katika kuhamishwa.
5 Toboa mahali ukutani mbele ya macho yao, ukachukue vitu kwa kuvipitisha pale.
6 Mbele ya macho yao utajitwika begani pako, na kuvichukua nje gizani; utafunika uso wako, hata usiione nchi; kwa maana nimekuweka uwe ishara kwa nyumba ya Israeli.
7 Nikafanya vile vile kama nilivyoamriwa; nalitoa vyombo vyangu wakati wa mchana kana kwamba ni vyombo vya kuhamishwa, na wakati wa jioni nikautoboa ukuta kwa mkono wangu; nikavitoa gizani, nikavichukua begani, mbele ya macho yao.
8 Asubuhi neno la Bwana likanijia, kusema,
9 Mwanadamu, nyumba ya Israeli, je! Nyumba ile iliyoasi, hawakukuambia, Unafanya nini wewe?
10 Waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Ufunuo huu wamhusu mkuu wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao.
11 Sema, Mimi ni ishara kwenu; kama mimi nilivyotenda, wao nao watatendwa vile vile; watahamishwa, watakwenda kufungwa.
12 Naye mkuu aliye kati yao atachukua begani katika giza; naye atatoka kwenda zake; watatoboa mahali ukutani, wapate kuvichukua vyombo vyao nje; atafunika uso wake, kwa sababu hataiona nchi kwa macho yake.
13 Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, angawa atakufa huko.
14 Nami nitawatawanya kwa pepo zote wote wamzungukao ili wamsaidie, na vikosi vyake vyote; nami nitaufuta upanga nyuma yao.
15 Nao watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana; nitakapowatawanya kati ya mataifa, na kuwatupa-tupa katika nchi zote”
Ukizidi kusoma utaona mahali pengine Nabii mmoja Bwana alimwagiza amwambie mtu ampige mpaka atoke majeraha.
1 Wafalme 20: 35 “Basi, mtu mmoja wa wana wa manabii akamwambia mwenzake kwa neno la Bwana, Nipige, nakusihi. Akakataa yule kumpiga.
36 Akamwambia, Kwa sababu hukuisikiliza sauti ya Bwana, angalia, mara ukitoka kwangu simba atakuua. Na mara alipotoka kwake, simba alimwona, akamwua.
37 Ndipo akaona mtu mwingine, akasema, Nipige, nakusihi. Yule mtu akampiga, hata kumpiga na kumtia jeraha.”
Sasa mambo haya yote ni ishara ya Bwana kutaka kuzungumza na wana wa Israeli kwa kupitia maisha ya watu, kwahiyo hiyo ndio sababu ya Mungu kumwambia Nabii Hosea akaoe mke wa kikahaba..na pia kumbuka Hosea mwenyewe hakuwa mzinzi ni yule mwanamke aliyeambiwa amwoe ndiye aliyekuwa ni kahaba. Kwa jinsi hiyo hiyo mambo hayo yanavyochukiza mbele za watu ndivyo hivyo hivyo yanavyochukiza mbele za Mungu, pale watu wanapoasi maagano yake.
Ubarikiwe!
Mada zinazoendana:
MADHARA YA DHAMBI YA UASHERATI.
JIBU: Biblia haituelezi kuwa kama kuna mtu yeyote anayejuwa mawazo ya mtu isipokuwa mtu mwenyewe na Mungu peke yake basi. Mungu peke yake ndio yupo kila mahali, yeye peke yake ndio anajua kila kitu, na yeye peke yake ndiye anayeweza mambo yote..Kwasababu yeye ndio muumba wa vyote. Hilo tunalithibitha katika vifungu hivi vya maandiko.
Zaburi 139: 1 “Ee Bwana, umenichunguza na kunijua.
2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote.
4 Maana hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, Bwana.
5 Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako.
6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia. 7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako?
8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko.
9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari;
10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.
11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; 12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu”.
Unaona ni sawa tu! na mtu ambaye anamiliki account ya facebook,sasa mwenye uwezo pekee wa kuiingia na kutoka ni mmiliki wa account hiyo na aliyetoa account hiyo ambao ni facebook basi! Hao wawili tu ndio wenye uwezo wa kufanya lolote juu ya account hiyo lakini mtu mwingine wa nje! hata kama na yeye atakuwa anamiliki shirika kubwa kiasi gani linaloweza kufanana na facebook, hawezi hata kidogo kuwa na uwezo wa kudukua taarifa za account yako ya facebook, labda wewe umfunulie au shirika la facebook lenyewe limpe taarifa zako.
Vivyo hivyo moyo wa mwanadamu shetani hawezi kuuingia wala kufahamu mawazo yaliyopo ndani yake, isipokuwa wewe mwenyewe umfunulie au Mungu.
Lakini pia kumbuka biblia inamwita shetani lile joka la zamani, Hii ikiwa na maana kuwa amekuwepo duniani tangu zamani na hiyo inampa faida kuwatazama wanadamu kwa muda mrefu na kuelewa baadhi ya tabia walizonazo, hivyo anaweza akawa anauwezo wa kuhisi mawazo ya mtu yakoje na haraka akamuundia njia ya kumwangamiza kulingana na anachokitamani, lakini kufahamu moja kwa moja fikra za mtu kama vile Mungu hilo hawezi, uwezo huo wa kuyasoma mawazo ya mtu mwingine hata sisi wanadamu tumepewa,..unaweza ukamuangalia mtu katika mazingira Fulani ukajua anachowaza, lakini huwezi kuingia ndani ya kichwa chake na kujua kila kitu ndani yake.
Na ndio maana utaona shetani alipokuwa anamjaribu hata Yesu alikuwa anamwambia ikiwa wewe ndiwe! Kuonyesha kuwa alikuwa hana hata uhakika wa uhusiano wa Yesu na Baba yake ulivyo maana kama angelijua hilo asingepoteza hata muda wake kumuuliza Bwana maswali yaliyoonekana kuwa ni ya kitoto kwa Bwana .
Lakini pia shetani anaowezo wa kutuma fikra zake ndani ya mtu, anaweza akatuma kwa kupitia ndoto, kwa kutumia mawazo, au hata kwa njia ya maono. Na hayo huwa yanakuja na nguvu Fulani kukushawishi kufanya mambo yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Kama mtu akiwa anaendelea kuyatafakari badala ya kuyakataa basi ndivyo anavyompa shetani wigo mpana wa kuyamiliki maisha yake.
Na ndio maana biblia inasema inatupaswa tuwe na uwezo wa kuteka kila fikra ipate kumtii Kristo. Jambo lolote linalokuja kwenye mawazo yetu, au ndoto, au chochote kile kama kinapingana na kanuni za Mungu ni kutokipa nafasi, kukikataa kwa nguvu, na chenyewe mwisho wa siku kitaondoka.
2 Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)
5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;”.
Hivyo, kuhusu shetani kufahamu mawazo ya mtu kana kwamba anasikia radio, hilo jambo haliwezi, japo anao uwezo wa kuhisi mtu au anachokiwaza au kumsoma mawazo yake kwa kuchunguza tabia za huyo mtu na mienendo yake, na mazungumzo yake mara kwa mara.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
TUNAMWABUDU MUNGU ALIYE HAI ,JE! WALE WANAOMWABUDU SHETANI SIO MUNGU WAO ALIYE HAI?
JE! UKRISTO UNAMPA MTU DHAMANA YA KUWA TAJIRI?
JIBU: Ndio atamuhukumu kama mkosaji, na ndio maana utaona zile adhabu zote zilimpata!! Hata kufiwa na mtoto wake wa kwanza…Na baada ya kufa kama hakupewa moyo wa kutubu, basi bado ataenda jehanamu ya moto. Kumbuka Moyo wa kutubu na moyo wa kumtafuta Mungu, ni Mungu mwenyewe ndio anaotoa sio sisi tunaoamua kwa juhudi zetu..ndio maana Bwana Yesu alisema katika
“Yohana 6:44 Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka;”
Umeona hapo? Nguvu ya mtu kumfuata Mungu ni Mungu mwenyewe ndiye anayekujalia..vinginevyo haiwezekani kumtafuta Mungu wala kumfuata.Sasa Kwanini Mungu amjalie Musa moyo mlaini wa kumkubali na Farao ampe moyo mgumu wa kumkataa??..hatujui na wala hatuwezi kumuuliza Mungu hayo maswali, ndivyo ilivyompendeza yeye, ni sawa na tumuulize Mungu alitokea wapi?? Hayo ni maswali tusiokuwa na majibu nayo….Yapo juu ya upeo wa fikra zetu. Na ndio maana mtume Paulo alisema katika..
Warumi 9.13 “Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!
15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.
16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.
17 Kwa maana maandiko YASEMA JUU YA FARAO, ya kwamba, nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.
18 BASI, KAMA NI HIVYO, ATAKAYE KUMREHEMU HUMREHEMU, NA ATAKAYE KUMFANYA MGUMU HUMFANYA MGUMU.
19 Basi, utaniambia, MBONA ANGALI AKILAUMU? Kwa maana NI NANI ASHINDANAYE NA KUSUDI LAKE?
20 La! Sivyo, Ee binadamu; WEWE U NANI UMJIBUYE MUNGU? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?”
Unaona hapo? Biblia inasema pia wapo watu ambao hawajakusudiwa uzima wa milele, watu ambao majina yao hayajaandikwa katika kitabu cha uzima kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu (Ufunuo 17:18 na Ufunuo 13:8)..Swali ni Ni wakina nani hao?? Jibu ni kwamba Hatuwajui, Mungu ndie anayewajua…sisi sio kazi yetu kuwafahamu, jukumu tulilopewa ni kuhubiri injili kwa kila kiumbe kana kwamba wote wote wamekusudiwa uzima wa Milele,…Na kujitahidi kuishi kulingana na maagizo yake na amri zake,ili tuwe na uhakika sisi sio miongoni mwa hilo kundi lililoandikiwa kupotea milele.Kwasababu dalili kuu inayotambulisha kuwa umekusudiwa uzima wa milele ni pale mtu anapoitii na kubadilika, kadhalika dalili kubwa inayoweza kumtambulisha kama mtu huyo hajakusudiwa uzima wa milele, ni pale anapoupinga wokovu ndani ya moyo wake.
Ubarikiwe!
Mada zinazoendana:
MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU:
WALIPO WAWILI AU WATATU KWA JINA LANGU
JIBU: Shalom!, Kwa hali ya kawaida tunafahamu sanduku kazi yake huwa ni kuhifadhi vitu Fulani, inaweza ikawa ni fedha,vito,nguo, hazina, miili n.k. na ndio maana tukirudi kwenye biblia tunaona biblia inataja masanduku ya aina mbali mbali, kwa mfano pale Yusufu alipokufa biblia inatuambia mwili wake waliuweka kwenye sanduku (Mwanzo 50:26), hivyo kuna masanduku ya miili. Hali Kadhalika kulikuwa na masanduku ya kuhifadhia sadaka, ambayo yaliitwa masanduku ya sadaka au masanduku ya hazina, mahususi kwa kazi ya sadaka tu!. (Marko 12:41).
Vivyo hivyo na masanduku mengine yalikuwepo, ya fedha, ya vito n.k.. Sasa tukirudi kwenye sanduku la agano lililokuwepo Israeli katika agano la kale, mpaka limeitwa sanduku la agano ni wazi kuwa ndani yake lilikuwa limehifadhi maagano Fulani. Na kama ukisoma biblia utaona ndani ya sanduku lile ambalo Musa alipewa maagizo alichonge lilikuwa na vitu vitatu: kimoja ni zile mbao zenye zile amri 10 Mungu alizompa Musa akiwa mlimani, zilizoandikwa kwa kiganja cha Mungu mwenyewe, cha pili ni ile mana, na cha tatu ni ile fimbo ya haruni iliyochipuka.
Na kila mojawapo hapo ilikuwa na maana yake. Musa aliagizwa avitunze vitu hivyo vitatu kwenye sanduku lile liwe kama kumbukumbuku la agano Mungu alilofanya na wana wa Israeli tangu walipotoka Misri mpaka walipoingia katika nchi ya ahadi. Vitu hivyo aliagizwa vikae kwenye sanduku kwa vizazi vyote kama ukumbusho.
Waebrania 9:2 “Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
3 Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,
4 yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano;
5 na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja”.
Fimbo ile ikimaanisha ukombozi wao waliopewa na Mungu kwa njia ya mti ule, Mungu alitumia kipande kile cha mti ule kumwadhibu Farao mpaka kuwaachilia watoke katika utumwa ule mgumu ambao kwa namna ya kawaida ilikuwa haiwezekani wao kutoka Kwahiyo fimbo ya Haruni ndio ile ile fimbo ya Musa).
Kadhalika amri zile kumi zikufunua sheria zote na maagizo yote Mungu aliowapa wana wa Israeli walipokuwa jangwani kwamba waziendee hizo siku zote za maisha yao.
Na mana, inafunua chakula cha kiroho Mungu alichokuwa anawapa kule jangwani kilichoshuka kutoka mbinguni, ambacho kiliwapa nguvu ya kusonga mbele katika hali zozote walizokuwa wanapitia. Sasa tukirudi katika agano jipya kama swali lilivyoulizwa Sanduku la agano linawakilisha nini katika agano jipya?.
Jibu ni kuwa mambo yote yaliyotendeka katika mwili kwenye agano la kale yalikuwa yanafunua mambo yanayoendelea katika roho kwenye agano jipya sasa. Hivyo sisi sote tunaoishi katika agano jipya, Na sisi pia Mungu aliingia agano na sisi na kutugawia FIMBO, AMRI, na MANA. Na hizo zote akazihifadhi katika sanduku lake moja litembee nasi. Na sanduku hili si lingine zaidi ya BIBLIA neno la Mungu.
Fimbo yetu ni msalaba ule ambao kwa huo Mungu aliutumia kumpiga shetani siku ile pale Golgotha, siku ile Bwana aliposema IMEKWISHA! Baada ya damu yake kumwagika Basi siku hiyo ulikuwa mwisho wa kila kitu kwa shetani, Bwana aliyotuweka huru mbali na utumwa na vifungo vya shetani (Farao).
Kadhalika amri zile ni maagizo yote tuyasomayo katika Biblia Bwana aliyotupa,kila siku tuyafuate na Mana na ufunuo wa Roho ambao huo unashuka moja kwa moja kutoka mbinguni kwa Baba kutupa sisi nguvu ya kudumu katika IMANI. Hivyo vitu hivyo vitatu vinakamilisha agano jipya na vyote hivyo vipo katika sanduku moja nalo ndio BIBLIA TAKATIFU.
Na kama vile mahali popote wana wa Israeli walipoenda sanduku la agano lilifuatana nao kadhalika mtu yeyote aliye mkristo na anakaa mbali na biblia maneno ya Mungu ni wazi kabisa bado hajaingia kwenye hili agano jipya la damu ya Yesu Kristo.
Ubarikiwe.
Mada Nyinginezo:
MAJARIBU MATATU YA YESU KRISTO
MUNGU KUSEMA NA WEWE PEKEE, HAITOSHI KUKUPA USHINDI.
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA WARAKA WA TATU WA YOHANA.
KWANINI SAMWELI ALIRUHUSUIWA KUHUDUMU HEKALUNI KAMA VILE WALAWI WAKATI YEYE NI MU-EFRAIMU?
NINI MAANA YA HUU MSTARI “NIMEVIPIGA VITA VILIVYO VIZURI, MWENDO NIMEUMALIZA, IMANI NIMEILINDA;”?
JIBU: Hii ni kuonyesha kuwa Bwana hakuja kukomboa roho zetu tu basi, bali hata miili yetu pia..Na aliposema hata unywele mmoja wa vichwa vyenu hautapotea, alikuwa anaamanisha kuwa hata kile kinachoonekana kuwa hakina thamani katika mwili wetu hakitapotea..vyote vitarejeshwa tena, ..Ikiwa ni mwamini alikufa hana mguu, basi siku ile ya ufufuo mguu wake utarejeshwa ikiwa alikufa na upara juu ya kichwa chake, basi nywele zake zote zitarejea katika siku ile na kuwa kama kijana. Na baada ya kurejeshwa ndipo miili mipya ya utukufu kutoka mbinguni ambayo asili yake ni mbinguni na sio ardhini itakuja kuivaa hii miili yetu ya ardhini. Kuonyesha kuwa hakuna kilichopotea hata kimoja…
1Wakoritho 15:51 “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 MAANA SHARTI HUU UHARIBIKAO UVAE KUTOKUHARIBIKA, NAO HUU WA KUFA UVAE KUTOKUFA.
54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?”
Lakini pia ikiwa Bwana anasema “Walakini HAUTAPOTEA hata Unywele” alimaanisha kuwa wapo ambao UTAPOTEA..Na hao ndio wale wanampinga YESU mfalme wa uzima sasa hivi wakijua kabisa yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuokoa roho zao na miili yao. Siku ile wakifa katika dhambi basi miili yao na roho zao vyote kwa pamoja zitateketea katika lile ziwa la Moto milele. Watapotea milele wala hakutakuwa na kumbukumbu kama hata hao watu walishawahi kuishi duniani.
Ubarikiwe
Mada zinazoendana:
UTALIPWA KATIKA UFUFUO WA WENYE HAKI.
TUZO UTAPEWA KULINGANA NA NAFASI YAKO.
MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.
NI MAONO YAPI HAYO UNAYOSUBIRIA?
SWALI: Shalom!.Ndugu zangu Biblia inatuambia kuhusu kazi yakutoa jasho aliyopewa Nuhu ya”KUVIINGIZA KATIKA SAFINA”VIUMBE VIRUKAVYO-Vya kiume na vyakike kwa jinsi yake” “KILA NAMNA YA WANYAMA-Wakiume na Wakike kwa jinsi yake” .
Swali Ni je! Nuhu Alipata wapi ujuzi huo wa kuvitambua hivyo viumbe vyote, na je! Hao wanyama wote aliwatolea wapi?
JIBU: Ukisoma mstari wa 20 sura ya 6 wa kitabu kile cha Mwanzo Biblia inasema : 20 Katika vyote virukavyo kwa jinsi yake, na kila namna ya mnyama kwa jinsi yake, kila kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake, wawili wa kila namna WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI. Unaona hapo, hilo neno WATAKUJA KWAKO ILI UWAHIFADHI
Ni kuthibitisha kuwa sio wanyama wote Nuhu alikwenda kuwachunguza kujua jinsia zako au kuwakamata, hapana wengine walikuja wenyewe Mungu ndiye aliyewaleta,isipokuwa wale wa kufungwa, lakini wengi wa hao waliosalia Mungu aliwaleta mwenyewe kwa Nuhu, kazi ya Nuhu ilikuwa ni kuwaingiza tu ndani.
Ubarikiwe.
Mada zinazoendana:
JE! VIUMBE VINATAZAMIAJE KWA SHAUKU KUFUNULIWA KWA MWANA WA MUNGU?
JE! VITABU VYA BIBLIA VILIWEZAJE KUKUSANYWA PAMOJA?
HATUA ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUTUONGOZA.
SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.
JIBU: Ili kupata jibu ya swali hilo, ni vizuri pia tujiulize baadhi ya maswali ambayo ni rahisi kabisa kuyajibu yanayoonekana katika maisha yetu ya kila siku. Tuchukulie mfano Leo hii nikimuuliza daktari je! Utanithibitishiaje kuwa kama kuna kitu kinachoitwa kirusi au bacteria.?..
Tunafahamu hataniita na kuniambia angali kwa makini utaviona hewani , vikielea, vinginevyo nitamuona ni mwendawazimu lakini yeye kama daktari atajua kabisa kwa macho yangu ya asili siwezi kuviona virusi au bacteria hivyo jambo yeye atakalolifanya ni moja kwa moja kunichukua na kunipeleka mahabara na kunionyesha KIFAA maalumu kinachoitwa HADUBINI (Microscope), ambacho hicho kimeundwa mahususi kwa ajili ya kuvuta vitu visivyoonekana kwa macho. Hivyo pale nitakapoitazama labda tusema damu kwenye hadubini hiyo na kuona vijidudu vidogo vidogo vikitembea ndipo hapo nitakapoamini kuwa kuna viumbe vinaitwa Bacteria au virusi.
Kadhalika leo hii mtaalamu wa masuala ya Anga, akaniambia kuna sayari inayoitwa Pluto inayofanana na dunia, ni wazi kuwa siwezi kuamini kwasababu kwa macho yangu hayalithibitishi hilo lakini pindi atakapotumia kifaa chake maalumu kinachoitwa DARUBINI (Telescope). Ambacho hicho ni mahususi kwa kuvuta magimba yote yaliyo angani ndipo nitakapoamini kuwa kweli kuna sayari inayoitwa Pluto kwasababu ninaiona kwenye darubini. Vivyo hivyo na mambo ya rohoni, hatuwezi kuyatambua kwa jinsi ya mwilini biblia inatuambia hivyo katika
1Wakoritho 2: 14 “Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni”.
Hivyo ili sasa tuweze kujua kuwa kuna mbingu au kuzimu basi yatupasa nasi pia tutumie kifaa maalumu kinachoweza kuvuta mambo ya rohoni na hicho si kingine zaidi ya BIBLIA TAKATIFU. Tatizo linakuja ni pale watu wasipotaka kuliamini NENO LA MUNGU na huku bado wanataka wamwone Mungu, ni sawa na mtu anayetaka kuona kirusi na huku bado haiamini Hadubini. Iamini kwanza biblia, ndipo utakapopata uthibitisho kweli kama kuna mbingu au kuzimu vinginevyo hata mtu atoke mbinguni au kuzimu akuambie hutaamini wala hutaweza kulithibitisha hilo.
Ubarikiwe sana.
Mada zinazoendana:
JE! MBINGUNI KUTAKUWA NA KULA NA KUNYWA?
NIFANYE NINI ILI NIIKWEPE HUKUMU.
JIBU: Shalom! Maana ya Neno ongoka ni KUGUEUKA.
Hivyo biblia inaposema mtu ni mwongofu inamaanisha kuwa ni mtu aliyegeuka na kuacha mienendo aliyokuwa anaiendea hapo mwanzo. Embu tutazame baadhi ya vifungu kwa kupitia hivyo tutajifunza kwa uelewa mrahisi zaidi:
Mathayo 18.3 “akasema, Amin, nawaambia, MSIPOONGOKA na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni”.
Hapo Bwana alikuwa anamaanisha MSIPOGEUKA na kuwa kama vitoto, yaani wasipogeuzwa fikra zao na kuwa kama watoto wadogo hawawezi kuuingia katika ufalme wa mbinguni. Kadhalika tukisoma..
Marko 4: 11 “Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa mifano,
12 ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije WAKAONGOKA, na kusamehewa.”
Tunaona hapo Bwana alimaanisha wale watu wasije WAKAGEUKA na kuacha njia zao mbaya, ambapo kama wakifanya hivyo Mungu atawasemehe, na kuwaachilia neema ya kusamehewa dhambi zao. Tukisoma pia..
1Timotheo 3.6 “Wala asiwe mtu ALIYEONGOKA karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.”
Hapo Mtume Paulo aliposema mtu aliyeongoka hivi karibuni, alimaanisha kuwa mtu Yule aliyegeuka na kuacha njia zake mbovu, hivi karibuni, asije akapewa kazi ya uaskofu kwasababu mtu kama huyo bado hajaweza kuijua imani vizuri, na kuweza kuzitambua hila za shetani kwani bado ni mchanga wa imani.
Hivyo ukitazama na vifungu vingine utaliona jambo hilo kwa muda wako unaweza ukavipitia baadhi ninavyokuorodheshea hapa (Mathayo 13:15,Luka 22:32, Matendo 15:3).
Kwa hiyo tunaweza kusema mtu anaweza akawa ni mwongofu, lakini bado hajaokoka. Tutalitazama hilo kwa undani tutakapojua kwanza maana ya kuokoa pia.
Kuokoka na wokovu ni kitu kile kile..Kuokoka ni kitenzi cha nomino Wokovu. Hivyo mtu mpaka awe ameokoka ni lazima kwanza awe amehusishwa na anayemwokoa mwenyewe (yaani mwokozi). Katika ukristo huwezi kusema umeokoka mwenyewe kama Yesu Kristo hajayageuza maisha yako, kama maisha yako hajahusianishwa na Kristo moja kwa moja, basi utakuwa umepokea wokovu mwingine tofauti na ule unaozungumzwa kwenye biblia.
Warumi 10:9 “ Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, “”utaokoka””.
10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”.
Na pia inasema: “AAMINIYE na KUBATIZWA “ataokoka”; asiyeamini, atahukumiwa.(Marko 16:16)”. Zingatia hivyo vifungu viwili vya mistari, vitakuja kutusaidia huko mbeleni. Kwasababu vyote viwili vinahusianishwa na suala la wokovu kwa mwanadamu. Kama tulivyosema suala la kuokoka ni jambo la kuingia moja kwa moja katika mahusiano ya karibu na Yule anayekuokoa. Upo udanganyifu mkubwa unaoendelea duniani sasahivi, watu wadhaniao kuwa wokovu ni jambo la Kuzungumza tu kwenye kinywa halafu basi wewe tayari utakuwa umeokoka. Hivyo imepelekea kila mtu duniani anasema ameokoka hata kama ni mlevi kisa tu tayari alishakiri yale maneno alipokuwa anaangozwa sala ya toba.
Watumishi wa Mungu wameyaacha na yale mwengine na kuona kuwa hayana umuhimu wowote. Hii ni kutokana na kwamba Kushindwa kuelewa maana ya Neno KUKIRI, ndiyo inayopelekea wokovu kuonekana ni kitu cha ajabu sasa duniani. Ndiyo inayopelekea watu kutoona nguvu za wokovu zikitenda kazi ndani yako. Wanakiri wameookoa, wameokoka.. lakini ukweli ni kwamba Wapo mbali na wokovu kuliko wao wanavyodhani. Biblia inaposema kwa kinywa mtu Hukiri “HATA” kupata wokovu..zingatia hilo Neno “HATA”..Ikiwa na maana kuwa ni tendo ENDELEVU. Sio kuzungumza tu siku moja halafu basi, Pia ili neno KIRI liwe na uweza na nguvu ni lazima pia neno KANA liwepo..
Kwa Watakatifu wa kale ilikuwa mtu akionyesha tu kumkiri Yesu kuwa ni mwokozi ilikuwa adhabu yake ni kufa au kutengwa na jamii pamoja na sinagogi. (Soma Yohana 3&9). Hivyo watu wa wakati ule ilikuwa kukiri tu vile, basi wewe ulikuwa umeshajihalalisha si wa kwao, na hivyo unawekwa mbali na watu wote wanamchukia Kristo. Lakini kukiri kwetu sisi mazingira tuliyopo mazingira ya kukana hayapo basi hilo neno halina nguvu kwa kinywa pekee.
Tunamkiri Kristo kwa maisha yetu na matendo yetu kuonyesha kuwa ni kweli Kristo alikufa, na kufufuka pamoja na sisi, kwanza kwa kubatizwa katika maji mengi na katika jina la YESU KRISTO kama maandiko yasemavyo pindi tu tuaminipo kama ishara ya kuamini kuwa alikufa akafufuka pamoja na sisi kuuonyesha ulimwengu tumekuwa milki halali ya Bwana. Na Pili ni kukubali kuishi maisha yanayomkiri Kristo kila siku.
Hapo ndio mtu anakuwa tayari kuingia gharama zote ikiwemo kuwa tayari kutengwa, kuchukiwa, kuachwa, kudharauliwa kwa ajili ya KRISTO, kwa ajili ya kumfuata Kristo. Sasa hapo ndipo mtu amemkiri Kristo. Na wokovu kwake ni jambo la lazima. Fananisha maneno hayo na vifungu hivi Bwana Yesu alivyowaambia makutano:
Mathayo 10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu; 36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.
37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.
38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.”
Pia ni vizuri kufahamu kuwa wapo watu wanaosema kuwa tukiwa hapa duniani hatuwezi kukoka mpaka tutakapokwenda mbinguni. Huo nao ni uongo. Biblia inasema 2 Wakoritho 6: 2 “Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama SIKU YA WOKOVU NI SASA)”.
Siku ya wokovu ni sasa. Tunaokolewa tukiwa hapa duniani hivyo mtu kusema nimeokoka ikiwa kweli amezingatia vigezo vyote vilivyotelewa na huyo amwokoaye.
Hana budi kujithibitishia hilo kuwa tayari ameshaokoka. Na hivyo siku ile ya kwenda mbinguni ni kukamilishwa tu kwa wokovu wake. Kumbuka raha ya wokovu inaanzia hapa hapa duniani pindi tu pale mtu anapomwamini Yesu Kristo, matunda ya wokovu yanaanzia duniani mbinguni ni kukamilishwa tu. Hivyo, kwa kuhitimisha tunaweza kusema mtu aliyeongoka ni tofauti na aliyeokoka. Japo aliyeokoka tayari alishaongoka ndani yake, lakini aliyeongoka haitupi uhakika kuwa ameokoka, kwasababu Neno lenyewe kuongoka ni KUGEUKA na sio KUOKOLEWA. Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp
Ubarikiwe sana.
Mada zinazoendana:
JE! UMECHAGULIWA KABLA YA KUWEKWA MISINGI YA ULIMWENGU?
KAMA MHUBIRI NI WOKOVU UPI UNAUPELEKA KWA WATU?
UKIAMINI NA UKIMKIRI YESU KWA KINYWA CHAKO, UTAOKOKA.
JISHUSHE ILI MUNGU AKUHUDUMIE.
KANUNI RAHISI YA KUFANIKIWA.
SWALI: KUFUKIZA UVUMBA ndio kufanyaje? Na tena wana wa Israel walimfukizia uvumba Malkia wa mbinguni, ndio yupi huyo?
JIBU: Uvumba ni aina Fulani ya manukato, yanayotengenezwa kwa viungo mbalimbali ambavyo baada ya kutengenezwa pamoja, huwa yanachomwa na kutoa harufu Fulani iliyo nzuri. Sasa katika biblia (Agano la Kale) wana wa Israeli walipokuwa jangwani kabla ya kufika nchi ya Ahadi, walipewa maagizo na Mungu mwenyewe watengeneze UVUMBA, na makuhani watakuwa wanauchoma huo kila siku ndani ya ile Hema waliyoambiwa waitengeneze..
Na ni makuhani peke yao ndio waliokuwa wanaruhusiwa kufanya hiyo kazi ya kuvukiza uvumba. Hivyo Makuhani waliuchukua huo uvumba na kuuchoma kila siku ndani ya ile hema ya kukutania katika madhabahu ndogo iliyokuwemo kule ndani, Na ilikuwa ni amri ya daima ni lazima wafanye hivyo kila siku..Na Bwana aliwaagiza wana wa Israeli wasitengeneze uvumba wowote kwa viungo hivyo kwa ajili ya mambo yao..Fomula ya kutengeneza huo uvumba ni kwa ajili ya Bwana tu!
Kutoka 30:34 “Bwana akamwambia Musa, Jitwalie MANUKATO MAZURI, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja;
35 nawe UTAFANYA UVUMBA WA VITU HIVYO, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu;
36 nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.
37 Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili ya Bwana”.
Sasa swali ni kwanini Bwana aliwapa hayo maagizo ya kuchoma uvumba ndani ya nyumba yake??
Jibu ni kwamba kila kitu kilichokuwemo ndani ya ile Hema ya kukutania kilikuwa ni lugha ya picha ya jambo linaloendelea rohoni….kwamfano kile kinara cha taa saba ndani ya nyumba ya Mungu kiliwakilisha makanisa saba katika ufunuo sura ya 2 na ya 3, kadhalika Yule kuhani mkuu anayeingia patakatifu pa patakatifu na Damu ya mwanakondoo ili kufanya upatanisho, anamwakilisha Yesu Kristo, ambaye ndiye kuhani wetu mkuu aliyeingia patakatifu pa patakatifu kwa damu yake mwenyewe mara moja tu!
Kadhalika na ule UVUMBA, kwa jinsi ulivyokuwa unachomwa ndani ya Nyumba ya Mungu, na moshi wake kukijaza kile chumba, na kupaa juu mbinguni..Jambo lile lilikuwa linafunua jinsi gani maombi ya watakatifu yanavyomfikia Mungu, kwanza yanakuwa yameandaliwa kulingana na Neno lake, pili yanapaa juu kama moshi na kumfikia Mungu mbinguni, kwani tunajua kitu pekee kinachopaa juu chenyewe ni moshi..Hivyo kwasababu yametengenezwa na viungo vinavyoendana na Neno la Mungu, maombi ya watakatifu yanakuwa ni harufu nzuri ya kuvutia mbele za Mungu, yanakuwa kama perfume mbele zake. Na ndio maana Daudi alisema maneno haya..
Zaburi 141: 2 “SALA YANGU IPAE MBELE ZAKO KAMA UVUMBA, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.”
Kwasababu hiyo basi katika agano jipya hatuchomi ubani tena, wala hatuvukizi uvumba kwasababu hayo yalikuwa ni mambo ya mwilini yanayofunua mambo ya rohoni, HIVYO UVUMBA WETU NI MAOMBI YETU TUNAYOMWOMBA MUNGU KILA SIKU YANAYOENDANA NA NENO LAKE.Ndio maana pia tunasoma hayo katika kitabu cha Ufunuo..
Ufunuo 5:8 “ Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, NA VITASA VYA DHAHABU VILIVYOJAA MANUKATO, AMBAYO NI MAOMBI YA WATAKATIFU.”
Ufunuo 8:4 “NA MOSHI WA ULE UVUMBA UKAPANDA MBELE ZA MUNGU PAMOJA NA MAOMBI YA WATAKATIFU, kutoka mkononi mwa malaika.”
Lakini pamoja na hayo shetani naye huwa anapenda kuiga na kugeuza mambo, na kuwadanganya watu kuwa mambo hayo kwasasa yanapaswa yaendelee kufanyika, kama anavyowadanganya watu kuwa kwasababu agano la kale kondoo na mbuzi walikuwa wanachichwa kwa ajili ya upatanisho, vivyo hivyo na sasa kondoo na mbuzi wanapaswa wachichwe kwa ajili ya kuondoa mikosi katika mtu, au jamii au ukoo, hivyo watu badala wapone ndio wanajiongezea roho juu ya roho..
Vivyo hivyo leo hii Bado shetani anawadanganya watu juu ya kuvukiza uvumba, ndio utasikia watu wanaambiwa wakachome ubani manyumbani mwao kufukuza mapepo, na zaidi hata makanisani watu wanavukiza uvumba, jambo ambalo ni machukizo kwa Mungu wa mbinguni…. Na kuhusu MALKIA WA MBUNGUNI. Hakuna mahali popote biblia imesema kuna malkia mbinguni, isipokuwa imeeleza miungu ya kipagani, inayojulikana kama malkia wa Mbinguni, hivyo biblia ilipotaja malkia wa mbinguni mahali popote ilikuwa inamaanisha miungu ya kipagani inayojulikana na watu kama malkia wa mbinguni, Ni sawa na leo atokee mtu atengeneze kinyago chake halafu akiite Malkia wa mbinguni, kiuhalisia sio kweli kwamba ni malkia wa mbinguni, mbinguni Mungu aliko hapana bali kimeitwa vile kutokana na watu wanakiita chenyewe malkia wa mbinguni.
Ubarikiwe!
Mada zinazoendana:
ZILE TUNU (DHAHABU, UVUMBA NA MANEMANE) MAMAJUSI WALIZOZITOA KWA BWANA ZILIWAKILISHA NINI?
HUYU AZAZELI NI NANI TUNAYEMSOMA KATIKA(WALAWI 16:8)
JE! SISI NI WAFALME NA MAKUHANI KWA NAMNA GANI?