1.) DUNIANI (miaka 33 na nusu)
2) KUZIMU (Siku tatu)
3) MBINGUNI (Miaka elfu mbili na …)
4) DUNIANI TENA (Miaka 1000)
Ni vema tukaifahamu hii migawanyo kwa kina ili tujue huduma ya Bwana wetu Yesu sasa ni ipi kwa watu wake.
Bwana aliposhuka duniani, aliishi miaka thelathini na tatu na nusu, ndani ya miaka hii alikuwa na lengo la kuwafundisha na kuwakomboa wanadamu wote kutoka katika laana ya dhambi na mauti. Na siku ile alipokwenda msalabani, ndipo akakamilisha kusudi hili. Ndio pale aliposema IMEKWISHA. Akiwa na maana kuwa kuanzia huo wakati na kuendekea kila mwanadamu atakayemwamini yeye ni lazima aokolewe.
Kusudi lake la kwanza likawa limekwisha.
Kusudi la pili lilikuwa ni kuzimu.
Pindi tu alipokufa hakwenda mbinguni moja kwa moja bali alishuka kuzimu. Kuzimu ni mahali pa wafu. Hivyo zamani wafu wote waliokuwa wema na waovu, wote walikuwa wapo makaburini, isipokuwa waovu walitengwa mahali pao mbali na wema. Waovu walikuwa katika vifungo vya hukumu. Lakini wema walikuwa sehema salama.
Sasa Bwana Yesu aliposhuka kuzimu, alifanya huduma kwa makundi yote mawili. Kwamfano lile Kundi la waovu alikwenda kulihubiria makosa yao, ni kwanini wamestahili hukumu, Soma..
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
1Petro 3:19 “ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;
20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji”.
Maana yake ni kuwa hata sasa, ikiwa utakufa katika dhambi, ni moja kwa moja utakwenda huku wafu hawa walipo ambapo hapana raha, ndio Jehanamu yenyewe iliyopo chini ya dunia.
Lakini walio wema Bwana Yesu aliwachukua na kuwafungua kutoka katika vifungo vya kaburi, na kuwahamishia mahali pazuri sana pajulikanapo kama peponi.
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. 51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;”
Mathayo 27:50 “Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;”
Hivyo ikiwa wewe ni mtakatifu ukifa sasa, hutajiona ukishuka makaburini, bali utajiona ukichukuliwa juu, mbinguni. Lakini sio kule Kristo alipokwenda,(huko tutafika baadaye) bali katika mbingu ya katikati, ambayo hiyo utakaa huku ukisubiria ule ukombozi wa miili yetu, Siku ile ya Unyakuo. Ambapo kwa pamoja utaungana na watakatifu walio hai, na moja kwa moja kwenda mbinguni kule Kristo alipo kwenye karama ya mwana-kondoo. Hivyo hudumu hii ya Yesu iliishia pale siku ile alipofufuka.(1Wakorintho 15:51-55)
Hii ndio huduma ambayo mpaka sasa inaendelea ya mwokozi wetu. Alisema mwenyewe maneno haya..
Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”.
Yohana 14:1 “Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo”.
Mpaka anasema ninakwenda kuwaandalia makao, maana yake ni kuwa hapo kabla sisi hatukuwa na makao yoyote mbinguni. Hivyo makao haya ndio ile Yerusalemu mpya, ambayo itashuka kutoka kwa Mungu mbinguni, baada ya utawala wa miaka 1000 kuisha.
Haya ni makao ya milele, hivyo hatushangai ni kwanini hadi sasa Bwana anatuandalia. Bwana atusaidie tusiikose ile mbingu mpya na nchi mpya ambayo Yerusalemu mpya ipo ndani yake. Ni makao ambayo jicho halijawahi kuona wala sikio kusikia. Huko tutamashangaa Mungu sana, kwa kipindi kisichokuwa na mwisho.
Huu ndio wakati wa ule utawala wa miaka elfu moja, ambao Kristo atakuja kutawala na watakatifu wake, hapa duniani, ndio kule kurudi kwa pili kwa Yesu Duniani, akiwa kama Mfalme wa wafalme, na Bwana wa Mabwana. Ni wakati wa sabato ya watakatifu wote. Utajiuliza kulikuwa na umuhimu gani Mungu kuipitisha kwanza hii miaka 1000, na sio tuingie moja kwa moja kwenye Yerusalemu yake iliyo ndani ya mbingu mpya na nchi mpya?
Ni kwasababu Bwana anataka kuwahakikishia watu wake kuwa hakuna chochote walichokipoteza pindi walipokuwa wanataabika kwa ajili yake hapa duniani, pindi walipojikana, kwa kuacha kila kitu, na kudharauliwa,.hivyo ili kuwaonyesha hakuna walichokipoteza, atawarudishia hiyo miaka ya raha, na wenyewe watakuwa wafalme na Mabwana duniani. Wakati huo dunia haitakuwa kama hii tena, bali itarejezwa hata zaidi ya Edeni, na amani itakuwepo duniani.(Soma Ufunuo 20:1-4). Watatawala pamojanna Kristo kwa amani na furaha isiyoelezeka.
Ndugu, tukiyaona haya, tunatambua sasa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana. Siku yoyote unyakuo utapitia, mlango wa neema utafungwa, dalili zote zimeshatimia Jiulize Je, umejiandaaje? Au umejiwekaje tayari kumpokea Bwana Yesu. Na hata kama hatarudi wakati wako. Ukifa leo hii, huko uendako utakuwa ni mgeni wa nani?
Yesu yupo mlangoni kurudi, tubu dhambi zako ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la YESU KRISTO, upate ondoleo la dhambi zako. Hizi ni siku za mwisho. Tunachokisubiri sasa ni unyakuo tu, dalili zote zimeshatimia.
Maran Atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
MBINGU MPYA NA NCHI MPYA. (Sehemu ya 3)
Je mbinguni itakuwa ni kuimba tu wakati wote?.
KWANINI KUWE NA UTAWALA WA MIAKA 1000
MAUMIVU NYUMA-YA-HUDUMA.
DHIKI KUU INAKUJA NA UNYAKUO UPO KARIBU.
Rudi nyumbani
Print this post
Mungu kamwe hajatuweka hapa duniani tutafute “dunia njema”, Dunia ambayo tutaishi mbali na hatari, mbali na majanga, mbali ni watu wabaya au waovu, hapana, hili ni jambo ambalo kila mtu aliyempokea Kristo au aliyeokoka anapaswa alijue, hata tujitahidi vipi kutafuta mahali ambapo patakuwa pazuri kwetu bado hatutapaona…
Kwasababu duniani hii ilishaharibika tangu Adamu alipoasi, na iliendelea kuwa hivyo hivyo, na hata sasa itakuwa hivyo hivyo ya hatari hadi mwisho wake, hakuna mahali utaenda au utakaa na kusema hapa hakuna ukinzani, hakuna masumbufu.., ni kitendo cha muda tu, ukiyashazoelea hayo mazingira mapya utavumbua shida nyingine nyingi na hatari zilizopo hapo,ambazo kule hukuziona, nenda kote ulimwenguni ndio uhalisia ulivyo..
Kitu Mungu anachokifanya ni kutufanya tuwe salama katika mazingira haya mabaya, lakini sio kubadili mazingira yawe mbingu kwetu. Anachofanya ni kutuandalia meza, tule tunywe, katikati ya watu waovu, katikati ya wachawi, katikati ya waganga, katikati ya wauaji, katikati ya wapagani.. Lakini tusidhuriwe na wao..Na anafanya hivyo ili tumaini letu liwe kwake tu.
Daudi alilijua hilo akasema maneno haya katika Zaburi..
ZABURI 23
1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. 2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza. 3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji 5 WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
1 Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
2 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, Kando ya maji ya utulivu huniongoza.
3 Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.
4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji
5 WAANDAA MEZA MBELE YANGU, MACHONI PA WATESI WANGU. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
Umeona, anasema waandaa meza mbele yangu machoni pa watesi wangu.. Machoni pa wafanyakazi wenzangu wanaonionea wivu, machoni pa wafanya-biashara wenzangu wanaoniendea kwa waganga, machoni pa majirani zangu wanaoniundia visa kila kukicha..Hapo ndipo Mungu anapokuletea chakula chako, anapokuchunga, anapokupa faraja..Kamwe usitazamie atakupeleka mbinguni, kukupa rizki, au Baraka zako.
Usihangaike kumwomba Mungu akubadilishie mazingira akupe mengine, au akubadilishie watu akupe wengine, au akubadilishie majirani, au wafanyakazi, au akuhamishe mahali ulipo akusogeze kwingine kwasababu hapo ulipo ni pabaya sana.. Mungu atakusogeza wakati wake ukifika, lakini fahamu kuwa hata huko uendako, hata hao watu wengine uwakutao, matatizo yanaweza kuzuka hata makubwa kuliko ya kwanza.. Lakini mwombe Bwana katika mazingira yoyote akusaidie,, Hilo linatosha yeye awe mchungaji wako, awe mwamba wako, awe jemedari wako wa vita, ndio maombi anayotaka kuyasikia, na huwa anayajibu upesi, maombi ya namna hii. Mwombe akufanikishe hapo hapo ulipo, akupe amani na faraja hapo hapo ulipo..
Bwana Yesu alimwomba Mungu maneno haya..
Yohana 17:15 “Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu”.
Si mapenzi ya Bwana, wewe ukae mbali na walimwengu, bali katikati yao, mpaka wakati wa Bwana utakapofika ndio akuondoe na kukupeleka pengine. Wakristo wengi wameathiriwa na mazingira yanayowazunguka, wanapoona hatari nyingi mbele yao au nyuma yao. Badala waweke tegemeo lao kwa Bwana awasaidie watimize mapenzi ya Mungu, wanabakia kuyalaumu mazingira, wakisema, ni kwasababu ya hiki, ni kwasababu ya kile..Yule ananipiga vita ndio maana sina muda na Mungu..Laiti ningeondoka hapa na kwenda kule ningetumika vizuri zaidi n.k…
Ndugu, Dunia hii iliyoanguka haina mahali utakuta pana unafuu, zaidi ya pengine, hapatakuwa na wachawi lakini patakuwa na magonjwa, hapatakuwa na magonjwa lakini patakuwa na uzito kiroho, au mwitikio wa watu kwa Mungu ni mdogo, hapatakuwa na maskini lakini patakuwa na majanga,..Hivyo hatari zipo na zitaendelea kuwepo kwasababu mkuu wa ulimwengu huu yupo kote.
Lakini tukiegemea kwa Bwana, na kumlilia yeye atembee nasi, atulinde, atuokoe, atupe amani, atupe faraja,atupiganie, na sio kuyalaumu mazingira, tutakuwa salama.
Wakati Fulani Mungu alinionyesha usiku katika ndoto, nilijikuta nimeingia katika jumba Fulani, lakini sikufahamu kama ni milki ya adui..Hivyo nikiwa kule nikawa kuzungumza na mama mmoja ambayr alikuwa kama kafungwa, lakini ghafla, mahali pale palibadilika,nikaanza kuwaona watu wanaotumiwa na ibilisi ndani ya mazingira yale, nikagundua uwepo wa pale sio wa ki-Mungu, bali ni milki ya ibilisi, basi nikawa natafuta mlango wa kutoka niondoke, lakini milango yote ilikuwa imepotea, basi nikawa nazunguka zunguka kwenye lile jumba lenye mazingira ya kutisha, kutafuta mlango wa kutokea sioni, kila nikiingia kwenye mlango mmoja, nakutana na chumba kingine, nikifungua kile huku nikitazamia ndio mlango wa kutoka nje, ndio kwanza nazama katika vyumba vya ndani zaidi..
Lakini nikiwa huko ndotoni, nikajikuta Napata hisia nyingine, nikasema Bwana ndiye ngome yangu ninahofu ya nini..Nikasema sitahangaika tena kutafuta mlango wa kutokea, nitatulia tuli, niendelee kumwangalia Bwana wangu, nikasema hapa nitatoka tu nisiwe na hofu..Na muda huo huo ghafla , nikawaona wenzangu wakiwa katika chumba kimoja wapo ndani ya hilo jumba, tukakutana wote tukiwa na amani sana kana kwamba pale sio ndani ya jumba la shetani, tukawa tunakula na kunywa, halafu tukaanza kuimba nyimbo nzuri za kumsifu Mungu, nakumbuka mahali pale niliona uwepo mzuri wa Bwana kana kwamba tulikuwa kanisani,
Na ghafla nikashutuka, ndipo Mungu akanifundisha neno hili..
Zaburi 23:5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. 6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
Zaburi 23:5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika.
6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele.
Hivyo tuondoe hofu ya watu, tumtazame Bwana. Na yeye atatuokoa.
Shalom.
Au jiunge na makundi yetu ya mafundisho ya kila siku kwa kwa njia ya Whatsapp kwa kubofya hapa >>>> WHATSAPP GROUP
Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;(Mithali 16:2)
Je ni lazima kushiriki Meza ya Bwana?
YESU ANAKWENDA KUIBADILISHA OFISI YAKE.
SALA YA BWANA. (Namna ya kuiomba)
MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU.
Mahali pa juu palikuwa ni wapi kama tunavyosoma katika biblia?
Ni miaka mingapi ya njaa Daudi aliyoambiwa achague? Ni miaka 7 au miaka 3?
karismatiki maana yake nini?
Karismatiki ni neno la kiyunani lenye maana ya “Zawadi za neema”.. Au kwa lugha nyepesi zaidi, tunaweza kusema, “vipawa vya neema”. Ambavyo hivyo hutolewa na Roho Mtakatifu mwenyewe na sio mwanadamu. Neno hili utalisikia sana vinywani vya madhahebu mbalimbali ya kikristo.
Ni mkondo ambao ulianza, mwanzoni mwa karne ya ishirini, (1906), kule Azusa Marekani, wakati ambapo dhehebu la Pentekoste lilipoanza. Lililoamini kuwa uthibitisho wa Mungu kuwepo katikati ya watu basi ni kuonekana kwa zile karama za Roho Mtakatifu, ambazo zinazungumziwa katika kitabu cha 1Wakorintho 12.
Kwamba kanisa ili liwe hai, ni sharti vipawa vya Roho kama vile Kunena kwa lugha, kutoa unabii, uponyaji na miujiza, vidhihirike ndani yake. Ikumbukwe kuwa tangu kanisa la kwanza la mitume kupita, vipawa hivi vilionekana kama vimekufa, havipo tena, lakini, viliibuliwa tena na Roho Mtakatifu mwanzoni mwa hiyo karne ya ishirini, ambapo baadhi ya wakristo walikaa chini na kufunga na kumwomba Mungu ajifunue kwa namna hiyo kama ilivyokuwa katika kanisa la kwanza la mitume. Na kweli wakiwa katika maombi hayo, Roho Mtakatifu alishuka, watu wengi wakaanza kunena kwa lugha, na karama mbalimbali kuonekana.
Ni jambo ambalo lilikuwa gheni, kwa madhehebu mengi makongwe, ambayo yalikuwa tayari yameshajikita katika mifumo ya kidini kwa muda mrefu. Kama vile Katoliki, Lutheran, Angalican, Moravian n.k.
Hivyo basi mvuto wa vipawa hivi, ulivyoendelea kuwa mkubwa, mpaka kufikia miaka ya 1980, madhehebu mengine mengi yakaanza kurithi mfumo huu wa karismatiki, ikiwemo dhehebu kama Katoliki, ( wakaitwa Karismatiki Katoliki), mengine ni Lutheran, na Anglikana, n.k. ijapokuwa yamekuwa na upishano kati ya wao kwa wao katika mifumo ya imani hii .
Hivyo kwa ufupi tunaweza kusema kanisa lolote linalosisitiza udhihirisho wa vipawa/karama za Roho, kama vile uponyaji, unabii, kunena kwa lugha, huitwa Kanisa la Karismatiki.
Ni nini tunapaswa tufahamu kuhusu vipawa vya Roho(Karismatiki).
Ni kweli kanisa linalokosa vipawa hivi, ni kanisa lililo nusu-mfu, au mfu kabisa. Kwasababu Mungu sio sanamu, ambaye anapokea tu ibada, lakini hatoi vipawa/zawadi kwa watu wake. Hayupo hivyo. Lakini pia ukengeufu mkubwa umeingia na kuvichafua vipawa vya Mungu, ikiwa na maana, kuwa mkristo usipokuwa makini utajikuta unapokea Roho nyingine na sio Yule wa Mungu.
Ni kuwa makini katika siku hizi za mwisho, wimbi kubwa la manabii wa uongo, linazukia huku, mafunuo yasiyo ya ki-Mungu yanaibuka na kuwapoteza watu kutoka huku, matumizi ya visaidizi kama maji, na chumvi za upako, vimewapoteza wengi,..Hivyo kumetokea mvurugano mkubwa sana. Mtu atanena kwa lugha leo, kesho atakwenda kuzini, jiulize ni roho gani ameipokea huyo?
Ni nini tunapaswa tufanye?
Nyakati hizi za mwisho, Tujitahidi sana kuitegemea BIBLIA kwa kila kitu tunachokitenda, au tunachoongozwa kukifanya, Ikiwa ni karama hakikisha haikinzani na kanuni za msingi za Neno la Mungu, hiyo ndio njia pekee ya kuthibitisha kuwa kipawa hicho ni cha ki-Mungu. Lakini nje ya hapo utapotea. Ikiwa utapokea ufunuo, au unabii, usiupokee tu, ilimradi ni fulani kasema, kisa kaona maono, hakikisha kwanza katika biblia, Je! Ndivyo ilivyo? Au La!. Kwasababu shetani ameingilia sana mikusanyiko mingi, ajaribu kuiangusha kwa namna hii.
Haiwezekani, useme mimi nimepokea Roho Mtakatifu, ninanena kwa lugha, ninaimba kwa Roho, Halafu anakuacha uendelee kuabudu sanamu la mtakatifu Fulani,sanamu la Mariamu au uombe sala za wafu. Huyu sio Roho Mtakatifu, haijalishi atajiita ni Karismatiki namna gani.
Hivyo ni kuwa makini, tusije pokea roho nyingine isiyokuwa ya Mungu. Hizi ni zama za uovu.
1Yohana 4:1 “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani”
Nini tofauti kati ya Kipawa na Karama?
JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?
HATA ILIPOTIMIA SIKU YA PENTEKOSTE.
SEMA KWA LUGHA NYINGINE.
NA VIUNGO VYETU VISIVYO NA UZURI VINA UZURI ZAIDI SANA.
ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.
UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU.
Makanda ni neno lingine la KAPU.
Ambalo hutumika kuhifadhi au kubebea vitu mbalimbali hususani vyakula au nafaka.
Katika biblia Neno hilo utakutana nalo katika vifungu kadha wa kadha, mfano wapo ni hivyo ni hivi;
Mathayo 15:37
[37]Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.
Marko 8:8
[8]Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.
Luka 16:6-7
[6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. [7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
[6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini.
[7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
Luka 16:5-7
[5]Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu? [6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. [7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.
[5]Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu?
Ni nini twapaswa kujua nyuma ya makanda ya mikate waliyoyakusanya wanafunzi wa Yesu ambayo baadaye waliyasahau mpaka wakaanza kulalamikiana na kulaumiana..Hadi Yesu akawakemea..(Marko 8:14-21)
Ni kwamba waliweka mioyo yao katika makapu yao, katika hazina zao, hata waliposahau wakapaniki.
Ni hali iliyopo sasa miongoni mwetu sisi, tuliookolewa. Tunafikiri sana makapu yetu yana nini, kwa miezi 10 mbele, kwa miaka 3 ijayo..na pale tunapopungukiwa hata uhusiano wetu na Mungu unakufa..Lakini Bwana Yesu anatuambia tusiwe wasiwasi, wala tusiyasumbukie hayo..bali tuutafuta kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine atatuzidishia..kwasababu maisha ni zaidi ya chakula.
Bwana akubariki.
Ila atapewa mara mia sasa,Ndugu wake(Marko 10:30)
JE! UNAMPENDA BWANA?
Mtu akizaa watoto mia, lakini nafsi yake haikushiba mema;
MASWALI NA MAJIBU: YAHUSUYO NDOA- Sehemu ya 2.
WAKINYAMAZA HAWA, MAWE YATAPIGA KELELE.
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WAONGOFU WAPYA.
Ulishawahi kujiuliza ni nini Mungu anafundisha wana wa Israeli nyuma ya agizo hili? Tunalolisoma katika Kumbukumbu 22:6
“Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda; 7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.
Bwana aliwapa agizo, endapo mtu yeyote akipita, njiani au karibu na kichaka, kisha akakutana na kiota cha ndege koo kimelala pale karibuni, kinatekeka kirahisi, kiasi kwamba unaweza kuwachukua wote, bila nguvu yoyote.Basi hapo, walipewa sharti, wasiwe na tamaa ya kuwachukua wote, bali wamwache koo aende zake akaendeleze uzao, lakini wale makinda anaweza kuwachukua na kuwafanya wake. Hivyo kwa kitendo hicho tu, mtu anajiongezea siku za kuishi duniani.
Ufunuo wake ni upi Katika Ukristo na katika maisha?
1) Katika Maisha.
Ni mara ngapi tunaona watoto wa jamaa zetu, wamekuwa mayatima, au wazazi wao wapo katika hali ya kutojiweza kupitiliza, mpaka wanashindwa kuwamudu watoto wao, lakini sisi tunapita hatuna muda nao kisa tu sio sisi tuliowazaa . Tunawaona watoto wale wakiangamia pamoja na wazazi wao. Bwana anatushauri, tusifanye hivyo, ni heri tusiwajali wale wazazi, tuwaache, tusiwape kitu chochote, lakini wale watoto tuwahurumie, kwani tukifanya hivyo, Mungu atatubariki na kutuongezea siku za kuishi duniani.
Watu wengi tunadhani, kuwaheshimu tu wazazi, ndio tunapata siku nyingi za kuishi, lakini ukweli ni kwamba, ukiwajali pia watoto wa asiyejiweza, utajiongezea siku pia za kuishi duniani.
2) Katika ukristo.
Vilevile katika ukristo. Ipo mikusanyika mingi, Yapo makanisa mengi, zipo huduma nyingi, ambazo haziwaweki watu katika mstari wa wokovu wa kweli, viongozi wao ni vipofu, hivyo na wale wanaoongozwa pia watakuwa ni vipofu, na mwisho wa siku wote watatumbukia shimoni. Sasa ikiwa wewe ni mchungaji au mkristo, na unaona mwenzako mahali alipo anapotezwa..Usikae kimya, na kusema wale sio washirika wangu, au wale sio wa dhehebu langu, au wale sio wa dini yetu..Bali unapaswa kuwaeleza ukweli, uwavute katika mahali sahihi ili uokoe roho zao..
Yawezekana ikawa ni ngumu kumgeuza kiongozi, hivyo usihangaike naye sana ikiwa utashindwa kumfikia, lakini wale makinda hakikisha unawajuza njia sahihi. Hiyo itakuongezea siku zako za kuishi hapa duniani.
Katika siku hizi za mwisho, watu wengi wamewekwa sehemu za hatari, wengine wameaminishwa katika watu, wengine vitu, wengine katika dini, wengine taasisi..lakini Kristo hayupo kabisa mioyoni mwao. Hawamjui, hawalifahamu Neno, hawajui nyakati wanazoishi, dini walizopo ni za kipagani. Sasa hii ni hatari sana, tunapoona wakiendelea katika kudanganywa na viongozi wao ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao. Hivyo sisi tuwe wa kwanza kulihubiria hili kundi la Mungu, litoke huko lirudi kwenye Neno.
Bwana atusaidie shalom.
KOIKOI ANGANI AJUA NYAKATI ZAKE ZILIZOAMRIWA.
Uzima wa milele ni nini?
MISTARI YA BIBLIA KUHUSU WATOTO.
NINI MAANA YA SISI KUWA WATOTO WA MUNGU?
Watu wenye ulemavu wa akili, wataenda mbinguni?
Afadhali mtu akutwe na dubu aliyenyang’anywa watoto wake.
MTEGO HUTEGWA BURE, MBELE YA MACHO YA NDEGE YE YOTE.
Thenashara ni nini? (Marko3:16)
SWALI: Naomba kufahamu vifungu hivi tunavyovisoma katika Isaya 24:18-20 vinamaana gani?
Isaya 24:18 “Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika. 19 Dunia kuvunjika, inavunjika sana; dunia kupasuka, imepasuka sana; dunia kutikisika, imetikisika sana. 20 Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka, wala haitainuka tena.”
JIBU: Mstari hiyo inatupa picha ya dunia ilivyosasa katika hali ya roho. Imefananishwa na mlevi ambaye amelewa sana, na hivyo hawezi kujimudu tena.
Kama tunavyofahamu, mlevi kabla ya kudondoka mtaroni na kulala hapo hapo, huwa unayumba yumba sana, anapepesuka sana, hatua moja mbele, kumi nyuma, kwenda kulia, kwenda kushoto, hiyo yote ni anatafuta uwiano lakini anaukosa kwasababu kichwa chote kimeshatiwa uzito, kila kitu kilichombele yake anakiona kama kimegeuzwa juu chini..
Hivyo kutembea kwake, hakuhusishi tena ubongo, bali uzoefu, na hatari zaidi pale atakapo jikwaa tu kidogo na kuanguka, basi safari yake inakuwa imeishia hapo, hawezi tena kunyanyuka, mpaka atakapolevu asubuhi.
Ndivyo dunia, ilivyo rohoni, nyakati hizi tulizopo, imelevywa sana kwa dhambi za wanadamu, na hivyo imepoteza muhimili wake, tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo, hatushangai sikuhizi kuona, majangwa mengi, ukame uliopitiliza, matetemeko makubwa ya ajabu, magonjwa ya kutisha kama Korona, Ebola kuzuka, mambo ambayo hapo zamani hayakuwepo. Sasa haya yote hayajajizukia hivi hivi tu, bali ni kuleweshwa kwa dunia kwa dhambi zinazoendelea kuwa nyingi.
Ndugu yangu, tupo katika hatari kubwa; Hatari ya “hofu, mashimo, na mitego”, kama hayo maandiko yanavyosema, Ikiwa na maana kama tupo nje ya Kristo tujiandae, kukutana na mambo haya katika maisha yetu. Mtu ambaye hajaokoka, ni kwa neema za Mungu tu anaishi hadi sasa kwenye dunia hii inayowaya-waya kama machela.
Lakini kama tumeokolewa Bwana ameahidi kutuepusha nayo. Kwasababu unyakuo wa kanisa upo karibuni sana kutokea. Na baada ya hapo, ndipo huu ulimwengu utaanguka kabisa..
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu, 13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi. 14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake. 15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Ufunuo 6:12 “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
13 na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?.
Je! Unasubiri nini, usimkaribishe maishani mwako? Je! Unauhakika wa kesho? Vipi ikiwa utakufa leo, au Kristo amerudi ghafla sasa hivi utasema nini rafiki.. Kumbuka mipango yote ya mpinga-Kristo ipo tayari, injili imeshahubiriwa duniani kote, dakika tulizonazo ni za nyongeza tu, wakati wowote, parapanda italia, na hali halisi ilivyo tusidhani tuna miaka mingi mbele, muda umeisha kwelikweli, usipumbazwe na mambo ya ulimwengu ukadhani, Yesu harudi hivi karibuni. Ni kwasababu husomi biblia ndio maana unadhani hivyo. Injili ya sasa sio ya kubembelezwa tena, ni mtu mwenyewe kuona na kugeuka, na kuyasalimisha maisha yako. Sio wakati wa kutanga tanga, na maisha bali ni kumtafuta Mungu.
Bwana atusaidie.
Maranatha.
UNYAKUO.
MFALME ANAKUJA.
TABIA ZITAKAZOMTAMBULISHA MPINGA-KRISTO AJAYE.
MWENDO UNAOSHANGAZA SANA!
Je! Bwana Yesu alikunywa kileo mpaka watu wakasema ni mlafi na mlevi? Kulingana na Mathayo 11:19?
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. Ni siku nyingine tena yenye neema za Bwana.
Napenda leo tujifunze, ni nini kwanza Bwana anahitaji kuona kwetu kabla ya yeye kuachilia neema zake katika mambo tumwombayo au tuyatafutayo. Embu tusome habari hii kwa mara nyingine tena..
Luka 5:4 “Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki. 5 Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu. 6 Basi, walipofanya hivyo walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika; 7 wakawapungia mikono washirika wao waliokuwa katika chombo cha pili, waje kuwasaidia; wakaja, wakavijaza vyombo vyote viwili, hata vikataka kuzama. 8 Simoni Petro alipoona hayo, alianguka magotini pa Yesu, akisema, Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana. 9 Maana alishikwa na ushangao, yeye na wote waliokuwa pamoja naye, kwa sababu ya wingi wa samaki walioupata;”
Kumbe Bwana Aliona taabu ya Petro usiku ule ilivyokuwa, aliona kule kutafuta kwake usiku kuchwa pasipo mafanikio kulivyokuwa. Alipokuwa anatupa nyavu hapati, anajaribu tena hapati, anasogea sehemu nyingine avue ndio anakosa kabisa mpaka kunapambazuka, haambulii chochote..
Na ndio maana hatushangai jambo la kwanza Yesu alilomwambia Petro mara baada ya kuhubiri kwake, sio Petro twende shambani kwako nikakubariki, au twende tukahubiri injili, ..Hapana bali tweka vilindini ukavue samaki, nikabariki kwanza kwa kile ulichokuwa unakisumbukia kwa muda mrefu..
Hata sasa Kristo ni Yule Yule, kabla ya kutupigisha hatua yoyote kiroho..Hatuna budi kwanza tufanye kazi ya kuchosha usiku kucha, wakati mwingine bila mafanikio yoyote. Watu wengi wanataka Mungu atembee nao kwa viwango vya juu zaidi, lakini hawapo tayari kutaabika kwanza, hawapo tayari kutumika kwanza, katika utumishi wa Mungu kwa muda mrefu, tena ule ambao hauonyeshi matunda yoyote ya awali, lakini tunataka tulale, tuamke kesho tuwe kama Musa.
Huduma nyingi zimekufa kwa namna hii, pale wanapoona hakuna maendeleo au hatua zozote, mwishowe wanakata tamaa ya kumtumikia Mungu, wanavunjika moyo, wanaghahiri, wanakwenda kutafuta shughuli nyingine.
Ndugu, Hatuna budi kufahamu wakati mwingine ni desturi ya Mungu kutuacha kwanza, kwa kipindi Fulani, atupime uaminifu wetu, lakini pia atutengeneze, si kila wakati mambo yote yatakuja papo kwa papo kama wengi wanavyosema, yaweza kuchukua mwaka kama sio miaka, lakini tukivumilia, siku isiyokuwa na jina tutashangaa vile tulivyovitamani, tunavipata kwa urahisi sana, tena bila kusumbukia, wala kuchukua muda kama ilivyokuwa hapo mwanzo, Hatua kama hiyo ukishaifikia, ujue tayari Kristo ameshaona utumishi wako. Lakini lazima tufanye kazi ya kuchosha usiku kucha.
Waweza kusema, jambo kama hili alilifanya siku hiyo tu ya kwanza alipokutana na Petro, lakini utaona mwishoni kabisa mwa huduma yake kuwa nao, baada ya kufufuka kwake, mitume kwa mara nyingine tena walienda kuvua samaki, lakini usiku ule wote hawakupata kitu, ilipofika asubuhi wakamwona Yesu amesimama pwani, ndipo akawauliza wanangu mna kitoweo? Wakasema hapana, akawaambia watupe jarife upande wa kulia watapata (Yohana 21:1-13)
Na kweli samaki ambapo waliwasumbukia usiku kuchwa, wakawapata kwa dakika tano, tena sio kule vilindini bali pale pale pwani. Unataka Mungu aikuze huduma yako, tumika kwanza kwa Bwana, fanya uinjilisti sana, hata kama huoni mtu yeyote ameokoka leo au kesho, wakati wa Bwana ukifika, utaona maajabu. Lakini ukikata tamaa, ukasema sioni chochote, Kristo atasema hustahili kupokea neema.
Wewe ni mwimbaji wa Injili, imba sana, dumu kwa uaminifu kufanya mazoezi, tunga, jifunze kwa moyo wako wote, nyimbo za utakatifu, na kuponya,bila ulegevu, hata kama utaambiwa hujui kuimba,wewe imba sana, hata kama miaka 10 itapita bila kuona kazi yako inamponya mtu..endelea tu, wakati utafika wa Bwana kuachilia neema yake, ataibariki sauti yako, na kuwa msaada ya maelfu ya watu duniani. Sauti itakuwa ni ileile lakini itajazwa neema na nguvu.
Kuna wakati ambao Yesu alipowalazimisha wanafunzi wake wapande mashuani, waende ng’ambo, usiku ule bahari iliwachafukia, lakini maandiko yanatuambia Yesu aliwaona wakitaabika katika kuvuta makasia, lakini hakufanya chochote, mpaka usiku sana wa manane ndio akawafuata akiwa anatembea juu ya maji. Ndipo akawatulizia dhoruba yao. (Marko 6:45-52).. Katika habari ile utajiuliza ni kwanini Yesu awaache wataabike, muda wote ule bila kuchukua hatua..jibu ni kuwa alikuwa anawajengea ushuhuda. Nasi pia Kabla ya Yesu kuzimisha dhoruba katika maisha yetu, na kutupa amani daima, yatupasa tuwe wastahimilivu sasa katika majaribu mengi na shida kwa ajili ya jina lake.
Luka 6:21 “Heri ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashiba. Heri ninyi mliao sasa, kwa sababu mtacheka”.
Jambo lolote la ki-Mungu unalopenda kulifanya, litende kwasababu Mungu anataka kuona kwanza kiu yako kwenye hilo jambo. Vilevile kama unataka Mungu akubariki, penda kutoa bila kutazamia malipo yoyote sasa, toa tu, hata kama ni kwa miaka, unaona unapata hasara tu, usikate tamaa, malipo yake utayaona wakati Fulani mbeleni, Bwana atakapoachilia neema zake.
Hii ni kanuni ya Ki-Mungu, aliitumia kwa, kwa Ibrahimu, Kwa Yusufu, kwa Musa, hata na kwetu pia anaitumia ikiwa tutakubali kwanza kufanya kazi ya kuchosha isiyokuwa na faida kwa muda mrefu.
Usikate tamaa, Bwana awe nawe.
Shalom
KAMA MWIZI USIKU WA MANANE.
RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.
Je! Siku ilihesabiwaje kabla ya jua na mwezi kuumbwa?
REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.
USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.
Biblia inamaanisha nini iliposema “wakidhania kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa;?
NI NINI TUNAJIFUNZA KWA YOANA NA MANAENI?
Sehemu ya 1
Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya”.
Nakusalimu katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, karibu tujifunze maneno ya uzima; Huu ni mfululizo wa makala, zinazochambua baadhi ya maneno au vifungu, ambavyo vimekuwa vigumu kwetu sisi kuvielewa kuhusiana na Mungu. Na hiyo imepelekea hadi baadhi ya watu wasimwamini kabisa Mungu na wengine kusema inakuwaje Mungu mwenye uwezo afanye vitendo kama hivi, au aruhusu mambo kama haya?
Hivyo katika makala hizi, tutaangazia uhalisia wa vifungu hivyo; Na tutapata amani katika hayo.
Kuna wakati Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno haya;
Yohana 13:7 “Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye”.
Ikiwa na maana kuna mambo ambayo Mungu anayafanya , kamwe hatutakaa tuyaelewe kwa sasa, bali baadaye sana. Na “Baadaye”, inaweza kumaanisha kipindi kirefu kijacho, au wakati wa baada ya haya maisha.
Hivyo basi, hakuna mwanadamu anayeweza kutolea majibu kila jambo analolisoma kuhusu Mungu, isipokuwa tu tunapapasa-pasaka, na kuelewa yale tuliojaliwa kuelewa na Roho Mtakatifu kwa sasa (Matendo 17:27).
Leo kwa sehemu tutaona, kwanini Mungu alisema maneno haya.
Sehemu: Mithali 16:4 “Bwana amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya”.
Swali linaloulizwa hapo, Je! Ni kweli Mungu aliwaumba wabaya ili kutimiza kusudi la ubaya?
Jibu ni ndio kama ilivyoandikwa.
Utauliza, ni kwanini sasa aseme yeye ni Mungu wa upendo, apendezwaye na haki? . Jibu ni lile lile, afanyalo leo hatutalijua, sasa lakini tutalijua vizuri baadaye. Na mawazo yake si mawazo yetu.
Ni vichache tu tunaweza kujua kwanini amewaumba watu wabaya kama ibilisi na mapepo yake, na waovu kama akina Kaini, kora, Belshaza? Ili wafanye mabaya duniani?
Majibu tuliyopewa kuyaelewa, ni ili kutimiza makusudi yake matatu makuu;
Kwamfano tunapoona hatma ya ibilisi na matendo yake maovu, hakuna hata mmoja anapendezwa na tabia kama zile, hivyo na sisi tutajilinda na dhambi ya uasi, kwa gharama zote, kwasababu tunajua mwisho wake utakuwa wapi. Hivyo yeye na watu wabaya wamekuwa funzo kubwa kwetu sisi, juu ya madhara ya dhambi.
Kama wasingekuwepo, tusingejua uzuri wa haki. Huwezi kujua sukari ni tamu kama hujawahi kuonja kitu kichungu, huwezi kujua hili ni joto kama hujawahi kuhisi baridi kabisa. Vilevile hatuwezi kujua Mungu ni wa upendo kama hatujakaa na watu wabaya, kama vile wauaji, wabinafsi n.k
Vilevile ameruhusu kwa lengo la kuadhibu, pale tumkoseapo Mungu. Anaruhusu watu kama akina Nebukadreza wa Babeli, kutuadhibu, kama wafilisti kwa Israeli walipomkosea Mungu. Hivyo wanasimama pia kama fimbo ya Mungu kwa watu wake kuwafunza.
Na vilevile kuwapa sababu zote hao watu wabaya kwanini wanastahili hukumu siku ile ya mwisho kwa matendo yao.
Pia sababu ya tatu ni ili kudhihirisha uweza wake mwingi. Mungu huwa anaruhusu wachawi kama Yane na Yambre washindane naye ili atoe maajabu yake yote, anaruhusu watu kama Farao wawe na mioyo migumu ili aonyeshe uweza wake mkuu wa uokozi, aliruhusu taifa lake Israeli lizungukwe na maadui zake aonyeshe jinsi anavyoweza kuokoa.
Soma hapa;
Warumi 9:17 “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu. 19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi? 21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima? 22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;”
Warumi 9:17 “Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote.
18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
19 Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake? 20 La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi?
21 Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?
22 Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;”
Hivyo basi, hizi ni baadhi ya sababu, lakini zipo nyingine zaidi ya hizo ambazo tutakuja kuzifahamu baadaye.
Ni kutufundisha unyenyekevu, tukubali kufanyika watu wema, ili tusiwe vyombo vya ubaya, Kwasababu kila jambo unaloliona duniani, liwe baya liwe jema, lipo chini ya makusudi ya Mungu, hakuna linalotokea kwa bahati mbaya, na ndio maana mengi ya hayo bado hayajaondolewa yote. Lakini utafika wakati yataisha.
Kumbuka hatuna miaka 100 tu ya kumjua Mungu, bali tuna umilele mbeleni, Hivyo kwa kipindi hichi kifupi hatuweza kutoa habari zote za Mungu, na kumuuliza kwanini umeruhusu haya, au yale..tuwe watulivu.
Tupende mema tuwe salama, tumpe Kristo maisha yetu ili tusiwe vyombo vya ghadhabu kama Farao, bali vya heshima.
Mwendelezo unakuja..
JE! UMECHAGULIWA TANGU ASILI?
KITABU CHA UZIMA
NGUVU YA UPOTEVU.
YESU NI NANI?
TOFAUTI YA MITUME, MANABII, WAINJILISTI, WACHUNGAJI NA WAALIMU NI IPI?
HATARI! HATARI! HATARI!
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
Shalom…Bwana wetu Yesu Kristo atukuzwe milele. Karibu tujifunze maneno yake ya uzima.
Lipo la kutafakarisha sana, katika ile habari ya yule mtu aliyesafiri, na kuwaita watumwa wake watatu na kumpa kila mmoja talanta ya Fedha wakafanyie biashara.
Kama tunavyoijua habari yule wa kwanza aliyepewa talanta tano, akaleta faida ya talanta nyingine tano, Vilevile yule aliyepewa talanta mbili akachuma nyingine mbili…lakini yule aliyepewa moja..maandiko yanatuambia hakuchuma chochote…
Na sababu iliyomfanya ashindwe kufanya vile si nyingine zaidi ya “WOGA”…Tusome..
Mathayo 25:24-30
[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;[25]basi NIKAOGOPA, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.[29]Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
[25]basi NIKAOGOPA, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
[29]Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.
[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Aliogopa nini?
Aliogopa atakapojaribu kuifanyia biashara ataipoteza…aliogopa kupata hasara..hivyo akaona ni heri aihifadhi tu..mahali fulani mpaka Bwana wake atakaporudi amrudishie kilicho chake wamalizane..
Aliogopa kuchekwa, na kudharauliwa, na kudhihakiwa, alijiona hawezi kuzalisha kile alichopewa, hana uzoefu na biashara..hakutaka kujitosa kama wale wenzake…ambao wao pia waliijua hatari ya biashara kwamba kuna kupata na kupoteza, lakini hawakutaka kuzipa kipaumbele… lakini yeye akasema sitaki kupata magonjwa ya moyo..wacha niihifadhi tu..kwani nini! , maadamu sijamtapeli..akirudi nitamrudishia kilicho chake.
Ndugu hii hali ipo kwa wakristo wengi hadi sasa..hawataki kupiga hatua moja mbele kuuzalia matunda wokovu wao kisa tu HOFU, ya kupata hasara..
Hasara ya nini?
Hasara ya ndugu kuwatenga, kama ndugu zao wakisikia kaokoka, wakiwatenga itakuwaje?
Hasara ya kuonekana wamerukwa na akili,..
Hasara ya marafiki kuwacheka, kuwaona ni washamba, wamepitwa na wakati..kwasababu wameacha mtindo fulani wa maisha.
Hasara ya kufukuzwa kazi, au kushushwa cheo kazini, kisa tu hawali rushwa tena.
Hasara ya kuachwa na mke/mume kisa tu wamejitwika msalaba wao na kuwafuata..
Hivyo hofu kama hizi na nyingine nyingi zimekuwa kigezo cha wakristo wengi kufukia talanta zao chini..wanasubiria tu siku ya kufa, Kristo aje na kuwauliza mmezalisha Nini kwenye Wokovu niliowapa siku ya kwanza…wenyewe waseme hakuna zaidi tu ya kuokoka..
Hii ni hatari kubwa sana…na jambo la kuhuzunisha..Ni lazima tujue “hakuna hatua moja mbele kama hakuna kujikana” Yesu aliye Bwana wetu alikubali kuchukiwa, kutengwa, kuonekana karukwa na akili, hadi kuuliwa, ili tu amzalie Mungu matunda yaliyo bora..(Yohana 7:5)
Marko 3:21
[21]Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.Na yeye mwenyewe akatuambia tusipojitosa kama yeye hatuwezi kuwa wanafunzi wake…
[21]Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.
Na yeye mwenyewe akatuambia tusipojitosa kama yeye hatuwezi kuwa wanafunzi wake…
Luka 14:26-27
[26]Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.[27]Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
[26]Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
[27]Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Akasema pia..ili mbegu ya ngano iweze kuzaa na kuleta matunda mengi haina budi kuoza kwanza chini ya ardhi, ndipo baadaye ichipuke na kukukua na kuzaa..(Yohana 12:24)
Ni lazima tuonekane tumekufa kwanza ndipo tuzalishe talanta zetu..tuonekane tumepotea kwa ajili ya Kristo ndipo tupate karama zake, tukilikimbia hili, tujue hatutazalisha chochote, ukristo wetu utakuwa ni ule ule wa miaka nenda, miaka rudi.
Ndugu/dada umedhamiria kumfuata Yesu, embu acha udunia kwa moyo wako wote..acha vimini, acha marafiki wasiofaa, acha miziki, na tamaa za ujanani, mtafute Mungu kwa moyo wote, elekeza nguvu zako zote huko..Epuka kuwa mkristo-jina…yule wa kusema nimeokoka-nampenda Yesu, halafu maisha yako hayana ushuhuda hata chembe..
Maanisha sasa..kwasababu siku zinavyozidi kwenda, siku moja utakufa na utatolea hesabu wokovu uliopewa, ukauchezea kwa hofu za wanadamu na ulimwengu.
Bwana atusaidie..
Maran atha.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)
Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)
Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”
ANGALIA JINSI USIKIAVYO:
Yesu alifundisha kwa mifano. Je hiyo mifano maana yake nini?
HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO.
SWALI: Naomba nifahamishwe mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?
JIBU: Si kweli, Nguvu za giza huwa hazichagua, hali ya mtu ya kimaisha, zinawavaa matajiri vilevile vinawavaa maskini, zinawavaa wanaume, zinawavaa wanawake, zinawatesa watoto (Marko 9:21), vilevile zinawaathiri mpaka wanyama (Soma Mathayo 8:31 )..Kwasababu kazi ya shetani sikuzote ni kuuharibu mpango mzima wa Mungu kwa viumbe vyake vyote.
Hivyo usidanganyike kuwa matajiri hawawezi kuwa na mapepo, huwenda ni kwasababu wewe hujakutana na visa hivyo, lakini vipo vingi. Pia katika maandiko walikuwepo matajiri ambao walisumbuliwa na mapepo.
Soma..
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye, 2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba, 3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”
Luka 8:1 “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,
2 na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
3 na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”
Umeona hapo, Hao wanawake wanaotajwa wote walikuwa ni matajiri, hakuna maskini, tukianzia na huyo Mariamu Magdalena, ambaye alitoa marhamu yake yenye thamani ya mamilioni ya pesa akammwagia Kristo miguuni pake, mpaka kwa Yoana mkewe Kuza, wakili wa Herode.
Mawakili kwa zamani ni sawa tu na mawaziri wakuu na wakuu wa majeshi sasahivi, hivyo huyu mke wa waziri mkuu alikuwa akimfuata Yesu, huwezi kusema ni maskini, alikuwa tajiri na wanawake wengine hapo wakitajwa walikuwa wakimuhudumia kwa mali zao.
Hivyo, hakuna mtu aliye na ofa kwa Mungu au kwa shetani, kwasababu ya hali yake ya kimaisha. Sote tunahitaji wokovu, tunahitaji msaada kwa Kristo sawasawa, tunahitaji kufunguliwa na yeye.
Tahadhari:
Epuka mahubiri yanayopigia kampeni utajiri, ambayo ndio yanayoendelea sikuhizi za mwisho kana kwamba ndio uhai wa mtu ulipo, yatakupoteza. Mkimbilie Kristo akupe uzima wa milele.
Efatha.
Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?
MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.
SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.
JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 4)
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?