Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.
Swali la msingi: Kwanini Kristo afe, si angekuja tu kuhubiri na kufundisha njia ya wokovu na kisha apae zake kurudi juu alipotoka, kulikuwa na sababu gani ya kufa?. Leo tutajifunza sababu chache za kifo cha Bwana Yesu. Kwa kuchunguza vitu vya asili, kumbuka vitu vingi vya asili vinahubiri injili, Ndio maana sehemu kadhaa Bwana Yesu alikuwa anasema maneno haya..
Luka 13:18 “Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? NAMI NIUFANANISHE NA NINI? 19 Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake. 20 Akasema mara ya pili, NIUFANANISHE NA NINI UFALME WA MUNGU?”.
Luka 13:18 “Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? NAMI NIUFANANISHE NA NINI?
19 Umefanana na punje ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake.
20 Akasema mara ya pili, NIUFANANISHE NA NINI UFALME WA MUNGU?”.
Maana yake ufalme wa mbinguni, umeandikwa katika vitu vya asili, umeandikwa katika Maisha ya kawaida tunayoishi, katika shughuli tunazozifanya n.k
Sasa Umuhimu wa Kifo cha Bwana Yesu, pia tunaweza kuupata kwa kupitia vitu hivi hivi vya asili, kama tukivitafakari kwa hekima.
Zifuatazo ni sababu chache za Umuhimu wa Kifo cha Bwana Yesu.
Yohana 12:24 “Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi”.
Hapo Bwana alikifananisha kifo chake na jinsi chembe ya ngano, inavyopandwa…Siku zote ukichukua mbegu yeyote, ile ya mahindi, au maharage, ukiifunga ndani ya gunia mahali ambapo haitaingiliwa na wadudu, ile mbegu inaweza kukaa hata miaka 5, bila kuharibika, na bila kumea chochote… Lakini utakapoichukua na kuitupa ardhini, ikazama chini ya udongo, ikapatwa na umande wa ardhini, ikaoza, wadudu wakaitembelea kidogo, wakala gamba lake la nje, ikanuka kidogo..Ndipo hapo itaanza kumea, na mwishoni kuwa mche mkubwa au hata mti, na kuzaa matunda mengi, yenye mbegu nyingi…Lakini isipopitia hizo hatua haitazaa chochote.
Na hiyo ndio sababu ya Kristo kufa..Kristo asingekufa na kufufuka, Injili isingefika duniani kote, Mataifa tusingepata wokovu…Lakini baada ya kufa, akatuletea nguvu ya Roho Mtakatifu juu yetu, kwa uweza na nguvu..Neno lake likasambaa duniani kote mpaka leo. Hivyo ilikuwa ni muhimu sana Kristo afe.
Kumbuka kuwa Kristo alibeba dhambi zetu, laumu zetu alizibeba, kwaufupi mbele za Mungu alikuwa ni mwenye hatia kwaajili yetu. Kutokana na dhambi zetu kuwa nyingi, Baba yake (ambaye ndio Baba yetu) aliuficha uso wake kwa muda ule alipokuwa pale msalabani, ndio maana akalia..Mungu wangu..Mungu wangu mbona umeniacha?..
Wagalatia 3:13 “ Kristo alitukomboa katika laana ya torati, KWA KUWA ALIFANYWA LAANA KWA AJILI YETU; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti”.
Kwahiyo suluhisho pekee ya kuitoa hiyo laana juu yake ilikuwa ni KUFA, Asingekufa ile laana ingeendelea kukaa juu yake, Mungu angeendelea kujitenga naye vile vile siku zote.. Hivyo pale alifanyika najisi/laana kwaajili yetu.. Kwa dhambi zetu, ikasababisha Mungu kujitenga naye..
Sasa kifo kimefananishwa na usingizi, Siku zote mtu akiwa amechoka sana, hata uumpe pesa kiasi gani, hawezi kuundoa ule uchovu, hata umpe chakula cha aina gani hawezi kuundoa ule uchovu, suluhisho la kumfanya mtu arudie ukakamavu wake ni kulala..Akishalala akiamka, ule uchovu wote utakuwa umetoweka, na atarudi ukakamavu upya.
Na kifo kazi yake ni hiyo hiyo, ilikuwa haina budi Kristo, afe ili azike uchovu wa dhambi zetu, na afufuke akiwa katika upya.
Pia tunaweza kujifunza kwa vifaa vichache tunavyovitumia kama simu au computer… Simu ikileta usumbufu (imeganda, au imekuwa slow sana)..mara nyingi suluhisho ni kuizima na kuiwasha (kui-restart).
Kristo alipokufa na kufufuka ndipo akaenda kuketi mkono wa kuume wa Mungu Baba, mamlaka yote na urithi wote akawa amekabidhiwa rasmi…
Waebrania 9:16 “Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. 17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya”
Waebrania 9:16 “Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya.
17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya”
Sasa ni kwa namna gani kifo kihusiane na urithi?
Turudi kwenye mfano ule ule wa kifaa kinachoitwa simu au computer..kama wewe ni mtumiaji wa simu, zinazojulikana kama simu-jacha (smartphone) au computer.. Utakuwa unajua kwamba ili kila unapotaka kuongeza program nyingine, ili ifanye kazi, inakuambia ukizime na kukiwasha kifaa chako..ili kile ulichokiongeza kiweze kufanya kazi.
Ukitaka simu yako iwe na uwezo kutumia internet, huna budi kutumiwa zile settings na shirika la huo mtandao, na kisha wakishakutumia watakuambia zima simu yako na kuiwasha. Sasa unaweza kujiuliza ni kwanini wakwambie uzime na kuiwasha..Kwanini wasikwambie tu, endelea kuitumia hivyo hivyo.
Na Kristo, ni hivyo hivyo, alikabidhiwa mamlaka na Baba akiwa hapa duniani sawasawa na Marko 28:18, lakini Mamlaka hayo ili yaweze kuwa na nguvu zaidi, hana budi Bwana Yesu, kufa na kufufuka.
Kwahivyo kwa hayo machache, Ilikuwa ni lazima Kristo afe, na kufufuka ili Mamlaka yake iwe na nguvu. (Kwa urefu wa habari hiyo fungua hapa >> FAHAMU KINACHOMGHARIMU MUNGU, KUTOA URITHI WAKE.
Bwana atusaidie Mauti ya Yesu iwe na nguvu kwetu pia. Biblia inasema tunapomwamini Yesu, tunatakiwa tufe pamoja naye na kufufuka pamoja naye na kuketi pamoja naye katika roho..
Na tunakufa na kufufuka pamoja na Kristo kwa njia ya Ubatizo..Utauliza hiyo inapatikana wapi kwenye biblia..?
Warumi 6:3 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 BASI TULIZIKWA PAMOJA NAYE KWA NJIA YA UBATİZO KATIKA MAUTI YAKE, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima”.
Warumi 6:3 “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake?
4 BASI TULIZIKWA PAMOJA NAYE KWA NJIA YA UBATİZO KATIKA MAUTI YAKE, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima”.
Ndio maana ubatizo sahihi ni wa muhimu sana, ni kitu kidogo cha dakika moja lakini shetani hakipendi milele. Atamfanya mtu apende kuogelea katika fukwe za bahari masaa hata matano, lakini hatamruhusu aingie kwenye maji hayo hayo abatizwe kwa dakika mbili tu, kwa jina la Yesu. Hataruhusu hilo kamwe!..atahakikisha anamletea huyo mtu mapepo ya kumshawishi, na kuona kile kitu hakina maana au ni kutumiza matakwa ya mwanadamu na si Mungu.
Kwasababu anajua mtu yule akiingia kwenye yale maji kwaajili ya ubatizo, na huku moyoni ametubu kabisa kwa kudhamiria kuziacha dhambi zake, anajua atakapoingia kwenye yale maji, basi maisha yake yatabadilika na kuketi karibu na Kristo katika ulimwengu wa roho, kwasababu atakuwa kafufuka pamoja na Kristo.. Jambo ambalo hawezi kuliruhusu hata kidogo.
Ndugu kama ni wewe mmojawao ambaye ulishawishika na shetani namna hiyo, leo hii mpinge, katafuta kubatizwa, ubatizo sahihi wa maji tele na kwa jina la Yesu Kristo popote pale na kwa gharama zozote, usikubali kuendelea kubaki nyuma kiroho.
Ikiwa utahitaji kubatizwa, basi wasiliana nasi kwa namba hizo hapo chini, au tutafute inbox.
Pia kama hujampokea Yesu maishani mwako, hiyo ndio hatua ya kwanza unayotakiwa uifanye, KUMBUKA YESU NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA. Hakuna njia nyingine zaidi yake yeye. Hivyo mpokee leo moyoni mwako na katafute ubatizo sahihi, na utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako.
Bwana akubariki.
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
Jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP
Mada Nyinginezo:
KWANINI NI YESU KRISTO WA NAZARETI?
YESU MPONYAJI.
RABI, UNAKAA WAPI?
WAKAKAA KWAKE SIKU ILE. NAYO ILIKUWA YAPATA SAA KUMI.
USINIE MAKUU.
Rudi Nyumbani:
Aina za dhambi ni zipi?
Dhambi zimegawanyika katika makundi makuu manne:
Hizi ni dhambi ambazo mtu anajua kabisa biblia imekataza kuzifanya lakini yeye anakwenda kuzitenda hivyo hivyo . Mfano wa dhambi hizi ni kama uzinzi, wizi, uuaji, aubuduji sanamu, ushirikina, rushwa n.k.
Luka 12:47 “Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana”.
Hesabu 15:30 “Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake. 31 Kwa sababu amelidharau neno la Bwana, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake”.
Hesabu 15:30 “Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
31 Kwa sababu amelidharau neno la Bwana, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake”.
Hizi ni dhambi ambazo mtu anafanya kwa kupuuzia wajibu wake au majukumu yake yeye kama mtu wa Mungu. Hizi zimegawanyika katika mafungu matatu;
1Samweli 12:23 “Walakini mimi, hasha! NISIMTENDE BWANA DHAMBI KWA KUACHA KUWAOMBEA NINYI; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka”
Ezekieli 3:18 “Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. 19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako. 20 Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako. 21 Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako”.
Ezekieli 3:18 “Nimwambiapo mtu mbaya, Hakika utakufa; wewe usimpe maonyo, wala husemi na huyo mtu mbaya ili kumwonya, kusudi aache njia yake mbaya na kujiokoa roho yake; mtu yule mbaya atakufa katika uovu wake; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
19 Lakini ukimwonya mtu mbaya, wala yeye hauachi ubaya wake, wala njia yake mbaya, atakufa katika uovu wake; bali wewe umejiokoa roho yako.
20 Tena mtu mwenye haki aiachapo haki yake, na kutenda uovu, nami nikiweka kikwazo mbele yake, atakufa; kwa sababu hukumwonya, atakufa katika uovu wake, wala matendo yake ya haki aliyoyatenda hayatakumbukwa; lakini damu yake nitaitaka mkononi mwako.
21 Bali ukimwonya mwenye haki, kwamba yule mwenye haki asitende dhambi, tena ikiwa yeye hatendi dhambi, hakika ataishi, kwa sababu alikubali kuonywa; nawe umejiokoa roho yako”.
Siku ile ya Mwisho, Kristo atakapokuja biblia inasema atawatenganisha kondoo na mbuzi. Kondoo ni wale watu ambao walitimiza wajibu wao wa kuwasaidia watakatifu waliohudumu katika kazi ya Mungu wakiwa hapa duniani, na mbuzi ni wale ambao walipuuzia na kudharau, hawakujua wajibu wao, wa kutoa vitu Mungu alivyowabariki kuwasaidia watenda kazi wa Mungu.
Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Mathayo 25:31 “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele”.
Mfano wa dhambi hizi ni kama; Mtu amepandwa na hasira, sasa kutokana na hasira zile ukampiga mwenzake na kumuua, lakini lengo lake lilikuwa sio kumuua, au kumpiga n.k. Hiyo ni aina ya dhambi ambayo mtu akifanya anapaswa akatubu, asipotubu, ni kosa litakalompeleka motoni.
Walawi 4:1 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 2 Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo Bwana amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo; 3 kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa Bwana ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi. 4 Naye atamleta huyo ng’ombe na kumweka mlangoni pa hiyo hema ya kukutania, mbele za Bwana; naye ataweka mkono wake kichwani mwake ng’ombe, na kumchinja huyo ng’ombe mbele za Bwana. 5 Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng’ombe, na kuileta ndani ya hiyo hema ya kukutania;
Walawi 4:1 “Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
2 Haya, nena na wana wa Israeli, uwaambie, Kama mtu ye yote akifanya dhambi pasipo kukusudia, katika neno lo lote ambalo Bwana amelizuilia lisifanywe, na kutenda neno lo lote la maneno hayo;
3 kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa Bwana ng’ombe mume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.
4 Naye atamleta huyo ng’ombe na kumweka mlangoni pa hiyo hema ya kukutania, mbele za Bwana; naye ataweka mkono wake kichwani mwake ng’ombe, na kumchinja huyo ng’ombe mbele za Bwana.
5 Kisha huyo kuhani aliyetiwa mafuta atatwaa baadhi ya damu ya huyo ng’ombe, na kuileta ndani ya hiyo hema ya kukutania;
Ni dhambi ambazo mtu anafanya kwa kutokujua kama anachofanya ni kosa au la.
Luka 12:48 “Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi”.
Utajiuliza ni kwanini, mtu wa namna hii aadhibiwe? Jibu ni kwamba kutojua sheria, haimaanishi kuwa sheria haitakuhukumu, ni kama tu ilivyo katika sheria za kidunia, mtu akivunja sheria kwa kisingizio cha kutoijua sheria haimfanyi mtu huyo asishitakiwe. Huwezi kwenda kumbaka mtoto mchanga, na ukasema sikujua kama sheria inakataza kitendo hicho, na adhabu yake ni kali hivyo, uachwe huru.. Unaona ni wajibu wako kuijua sheria. Ndivyo ilivyo katika sheria za Mungu.
Mtu mwovu siku ile hawezi kujitetea kwa chochote, ikiwa leo hii itaendelea na uovu wake, haijalishi atasema simjui Mungu kwa namna gani.
Bwana atusaidie tuzikwepe dhambi hizo zote kwa neema yake. Hakika tutashinda ikiwa tutadumu tu katika neema ya Roho Mtakatifu.
Je umeokoka? Je! Unajua kuwa hizi ni nyakati za mwisho, na hukumu ya kiti cheupe che enzi cha mwanakondoo ipo karibuni? Kama upo nje ya wokovu unangoja nini, embu leo fanya uamuzi mwema wa kumgeukia muumba wako. Kumbuka biblia inatuambia;
Warumi 6:23 “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”.
Ikiwa upo tayari kutubu dhambi zako na kumpokea Bwana leo, basi fungua hapa kwa ajili ya kupata maelekezo muhimu ya kufanya. >>> SALA YA TOBA
Maran Atha.
Nini maana ya “kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi?”
KWANINI NI LAZIMA TUFE KWA HABARI YA DHAMBI?.
TOBA IGUSAYO MOYO WA BWANA.
AKIJUA YA KUWA ANA WAKATI MCHACHE TU”.
Nini Maana ya Hosana?
WhatsApp
Kitabu cha waraka wa pili wa Yohana ( 2 Yohana ) ndicho kitabu kifupi kuliko vyote katika biblia nzima, kina sura moja tu na mstari 13, kinapatikana katika agano jipya. Ili kujua ujumbe wake ni nini, fungua hapa >>> WARAKA WA PILI WA YOHANA.
Lakini tukirudi katika agano la kale, kitabu kilicho kifupi kuliko vyote ni Kitabu cha Obadia, (japo sio kifupi kuliko vyote katika biblia nzima) chenyewe kina sura moja tu na mistari 21,
Kitabu hichi kinaeleza mambo mabaya yaliyofanya nchi ya Edomu kwa ndugu zao wayahudi. Edomu ni taifa lililozaliwa na Esau yule ndugu yake Yakobo. Hivyo mataifa haya mawili yangepaswa yawe ni ndugu na kushirikiana katika shida na raha.
Lakini ilipotekea shida katika Israeli, wakati ule wanachukuliwa utumwani na Nebukdreza, na miji yao kuchomwa na kuteketezwa, hawa Waedomu huwakuja kuwasaidia ndugu zao waisraeli, badala yake walikuwa wanafurahia kwa kilichokuwa kinatendeka, Na kibaya zaidi walikuwa wanawasapoti maadui wa ndugu zao kufanya hivyo.
Obadia 1:11 “Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao. 12 LAKINI USIITAZAME SIKU YA NDUGU YAKO, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.
Obadia 1:11 “Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao.
12 LAKINI USIITAZAME SIKU YA NDUGU YAKO, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.
Hivyo Mungu akaliona hilo ndipo akatumia kinywa cha nabii Obadia, kuitamkia hukumu Edomi, akasema nchi yao nayo itaangamizwa, na wageni wataitawala,
Obadia 1:4 “Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana”.
Na zaidi ya yote Mungu atawarejesha wana wa Israeli tena, na kuwamilikisha nchi hiyo. Lakini wao wataangamizwa, kwasababu hawakuona uchungu juu ya ndugu yao wa damu.
Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao. 18 Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo”.
Obadia 1:17 “Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.
18 Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo”.
Tunajifunza nini?
Tunapaswa tuoneane huruma sisi kwa sisi, na kusaidiana kinyume chake tukiwa tunafurahia mabaya yawapate wapendwa wetu, na kibaya zaidi tunashirikiana na wale wanaowaangamiza tujue kuwa Mungu anaweza kutugeuzia kibao na sisi kama alivyofanya kwa Waedomi. Atamwokoa yule ndugu yako, lakini wewe atakuangamiza.
Vilevile inatufundisha kuwasaidia wale walio wadhaifu wa imani, Ikiwa tutaona mtu fulani anashida ya kiroho, na shetani anataka kumwangamiza, na sisi, hutaki kuchukua hatua yoyote kwenda kumfundisha au kumuhubiria, hilo nalo ni kosa kama walilolifanya waedomi.
Hivyo Bwana atusaidie tuwe na moyo wa kusaidiana kama kitabu hichi Obadia kinavyotufundisha. Ni kitabu kifupi lakini kina ujumbe mzito sana kwetu.
Shalom.
Kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312 / 0693036618.
VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Biblia ina vitabu vingapi?
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
USIIGEUZE NYUMBA YA MUNGU KUWA PANGO LA WANYANG’ANYI.
SWALI: Kwanini Mtume Paulo, alimkataza Timotheo asiwaandike wajane vijana? Je wajane vijana hawapaswi kusaidiwa au?
Jibu: Kabla ya kwenda kwenye jibu la swali letu, kuna mambo muhimu ya kufahamu kwanza ya utangulizi.
Katika kanisa la kwanza kulikuwa na utaratibu wa kuwasaidia wazee, hususani wale wenye umri mkubwa sana. Ambao hawawezi kufanya kazi wala hawana mtu wa kuwasaidia, kama Watoto au wajukuu.
Sasa haikuwa kila mzee tu, anayejiunga na kanisa alikuwa anasaidiwa la! Haikuwa hivyo, Kulikuwa na vigezo au sifa za wazee waliokuwa wanastahili kusaidiwa. Na sifa hizo tunazisoma katika kitabu cha Timotheo..
1Timotheo 5:9 “Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja; 10 naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema”.
1Timotheo 5:9 “Mjane asiandikwe isipokuwa umri wake amepata miaka sitini; naye amekuwa mke wa mume mmoja;
10 naye ameshuhudiwa kwa matendo mema; ikiwa amelea watoto, ikiwa amekaribisha wageni, ikiwa amewaosha watakatifu miguu, ikiwa amewasaidia wateswao, ikiwa amefuata kwa bidii kila tendo jema”.
Maana yake ni kwamba kama sio mjane, anaye mume..basi huyo tayari anaweza kuhudumiwa na Mume wake, kwa mahitaji yake, hivyo asiandikwe kwenye orodha ya wanaostahili kusaidiwa na kanisa ili kanisa lisije likalemewa.
Maana yake ni kwamba akiwa chini ya umri huo, bado anayo nguvu za kufanya kazi za kujipatia kipato, hivyo anaweza kuendelea kufanya kazi zake za mikono huku akiendelea na kazi ya kuhudumu katika kanisa..Ili kanisa lisije likalemewa.
Maana yake ni kwamba kabla ya mume wake kufa, awe na rekodi ya kuwa na huyo huyo mume mmoja, na sio awe na rekodi ya kuwa na wanaume wengi. Mwanamke yeyote mwenye hiyo rekodi ya kuwa na wanaume wengi, hana sifa ya kuandikwa kwenye orodha ya wanaohitaji kusaidiwa.
Maana yake ni kwamba sio tu mtu, kazeeka hivyo anaona sehemu ya kwenda kumalizia pensheni ya uzeeni ni kanisani, hivyo anakwenda kujiunga ili tu awe ana hudumiwa. Biblia imesema watu wa namna hiyo wasiandikwe..Watu wanaopaswa kuandikwa ni lazima wawe na rekodi ya kuifanya kazi ya Mungu katika kanisa Pamoja na matendo mema, na utakatifu.
Sasa hapo biblia imeruhusu watu wenye sifa hizo kusaidiwa, lakini haikusema kila mwanamke anayefikia umri wa miaka 60 au Zaidi na ni mjane, ni lazima aandikwe kwenye orodha ya watakaosaidiwa. Hapana!!.. Kama mjane ana miaka Zaidi ya 60, na una uwezo mzuri wa kiuchumi, hapaswi kuandikwa, vile vile kama anao Watoto, au ndugu ambao wanaweza kumtunza vizuri, ni mume tu ndio hana, vile vile hapaswi kuandikwa. Wanaondikwa ni wale wajane kweli kweli ambao hawana mtu yeyote waliyebakiwa naye wa kuwasaidia, wamebaki wenyewe. Na tumaini lao lote lipo kwa Bwana, hao ndio wanaopaswa kuwekwa kwenye orodha ili kanisa lisilemewe.
1Timotheo 5:3 “Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. 4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu. 5 Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku”
1Timotheo 5:3 “Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli.
4 Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.
5 Basi yeye aliye mjane kweli kweli, ameachwa peke yake, huyo amemwekea Mungu tumaini lake, naye hudumu katika maombi na sala mchana na usiku”
1Timotheo 5: 16 “Mwanamke aaminiye, akiwa ana wajane, na awasaidie mwenyewe, Kanisa lisilemewe; ili liwasaidie wale walio wajane kweli kweli”.
Sasa tukirudi kwenye swali, ni kwanini wajane vijana hawapaswi kuandikwa?.
Sababu ya kwanza tumeshaiona hapo juu, ni ili kanisa lisilemewe, kwasababu wanao nguvu na uwezo wa kufanya kazi, hivyo fungu hilo la posho, ni heri likawasaidie wale ambao hawana uwezo kabisa wa kufanya kazi, wenye umri mkubwa, ambao hawana tumaini kabisa.
Sababu ya pili ndiyo hiyo tunayoisoma katika 1Timotheo 5:11-15.
Tusome..
1Timotheo 5:11 “Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa; 12 nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza. 13 Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa. 14 Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu. 15 Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani”
1Timotheo 5:11 “Bali wajane walio vijana ukatae kuwaandika hao, maana, wakizidiwa na tamaa kinyume cha Kristo, wataka kuolewa;
12 nao wana hukumu kwa kuwa wameiacha imani yao ya kwanza.
13 Tena, pamoja na hayo, hujifunza kuwa wavivu, wakizunguka-zunguka nyumba kwa nyumba; wala si wavivu tu, lakini ni wachongezi na wadadisi, wakinena maneno yasiyowapasa.
14 Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu.
15 Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani”
Ni ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya wanawake ni “watu wa kupenda udadi, au umbea, kutafuta tafuta kujua mambo ya watu wengine”.. Na wengi wa hao ni wale ambao hawana shughuli maalumu za kufanya, na wenye umri kati ya miaka 20-45 na wengine hadi 50. Mwanamke wa rika hili, akishakosa shughuli ya kufanya, na Zaidi akiwa hajaolewa, ni rahisi sana kuchukuliwa na hiyo roho ya udadisi dadisi. Na wivu wivu, tofauti na mwanamke ambaye ameolewa au mwenye shughuli maalumu ya kufanya. Kwasababu mwanamke aliyeolewa atakuwa akili yake yote ipo katika kuiendesha familia yake na kuitunza na kuangalia Watoto wake.
Sasa katika kanisa pia wapo wanawake, ambao ni wa rika hilo, Ambao baada ya waume zao kufa wamekuwa wajane, hivyo na wenyewe wanajiweka kwenye kundi hilo la wanawake wajane ambao kazi yao ni kudumu katika sala na maombi na kuhudumu kanisani siku zote (tumaini lao lote lipo kwa Bwana 1Timotheo. 5:5)… Hivyo na wao wanajiweka katika kundi la watu wanaohitaji kusaidiwa na kanisa.
Lakini tatizo lilionekana kwamba wengi wa wanawake hawa ambao ni vijana, wanakuja kugeuka tabia siku za mbeleni na kuanza kujiingiza kwenye mahusiano yasiyo rasmi, na tabia hizo za udadisi. Na hivyo hivyo wanakuwa wameiacha Imani ambayo walikuwa nayo hapo kwanza. Na hivyo kujiingia kwenye hukumu, kwasababu wameiacha Imani.
Kuacha Imani ya kwanza, maana yake kuacha njia ya haki waliyokuwa wanaiendea hapo kwanza.
Kwahiyo wanawake hawa, biblia imesema wasiandikwe, badala yake ni vizuri wakaolewa tena, ili wazae Watoto, wawe na majukumu, kwasababu watakapokuwa na majukumu na watakapokuwa na Watoto, watakuwa busy na familia zao, hivyo si rahisi kushawishika kuwaka tamaa na kuwa wadadisi, tofauti na wakitanga tanga bila kuwa na majukumu, ni rahisi kuchukuliwa na tamaa za kila namna.
Lakini pia kumbuka si wanawake wote ambao ni wajane na ni vijana, wana tabia hizo…Hapana!..Hapo biblia imemaanisha ni wengi wao, lakini si wote. Wapo ambao ni wajane vijana, au hawajaolewa lakini wanaishikilia Imani, Ingawa wapo wachache sana. Katika biblia alikuwepo mwanamke aliyeitwa Ana, ambaye aliishikilia Imani bila kuiacha tangu mume wake alipokufa angali akiwa bado binti mdogo, na mpaka akiwa na miaka 80, hakuiacha Imani. Na Mungu akampa neema ya kumjua mtoto Yesu kuwa ndiye Masihi katika uchanga ule. Wakati wengine hata Yesu alipokuwa mtu mzima bado hawakumwamini.
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. 38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”.
Luka 2:36 “Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake”.
Bwana atubariki
Maran atha.
Wanaowachukua wanawake wajinga mateka ni akina nani?
Je! Mungu anaupendeleo kwa wanaume zaidi ya wanawake?
TUJIFUNZE JAMBO KWA WANAWAKE HAWA WAWILI:
Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?
CHUKI ULIZO NAZO KWA MAADUI ZAKO, SIZO ALIZONAZO MUNGU JUU YAO.
Nguo za magunia( au mavazi ya magunia) ndiyo mavazi ya namna gani ?
Magunia kama biblia inavyotafsiri ni tofauti na inavyotafsiriwa sasa, Leo hii ukizungumzia magunia unamaanisha labda mifuko aina ya Salfeti (Sulphate) ambayo yanatumika sana sana katika kuhifadhia nafaka, au utakuwa unazungumiza magunia yaliyoshonwa kwa nyuzi za katani.
Lakini mavazi ya magunia, biblia haiyatafsiri kama mavazi yaliyotengenezwa kwa mojawapo ya malighafi hizo (salfeti au nyuzi za katani). Bali mavazi ya magunia yaliyozungumziwa kwenye biblia ni mavazi yaliyotengenezwa kwa MANYOYA YA MBUZI.
Nguo hizo zilitengenezwa mahususi, kuashiria aidha vitu hivi viwili Maombolezo au Toba
1. Maombolezo.
Watu zamani za biblia waliopitia misiba, au majanga walikuwa wanavaa nguo hizo za magunia kuonyesha hali ya maombolezo, kuonyeshwa kuguswa na tatizo hilo, na kwamba wapo katika huzuni na si furaha..
Mfano wa hao ni Rispa aliyeomboleza baada ya kufiwa na wanawe.
2Wafalme 21:10 “Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku”
Tunaona mfano mwingine ni wana wa Israeli, baada ya kupata msiba wa kupelekwa utumwani..biblia inasema iliwapasa wavae mavazi ya magunia kwa maombolezo..
Yeremia 4: 8 “Kwa sababu hiyo jifungeni NGUO ZA MAGUNIA; ombolezeni na kulia kwa uchungu; kwa maana hasira kali ya Bwana haikugeuka na kutuacha”
Yeremia 6:26 “Ee binti wa watu wangu, ujivike NGUO YA MAGUNIA, na kugaagaa katika majivu; fanya maombolezo, kama maombolezo kwa ajili ya mwana wa pekee, maombolezo ya uchungu mwingi; maana mwenye kuteka nyara atakuja juu yetu ghafula”.
Mifano mingine watu waliovaa mavazi ya magunia, kuashiria maombolezo unaweza kuisoma katika mistari ifuatayo (2Wafalme 6:30, 2Wafalme 19:1)
2. Toba
Watu pia walipotaka kujisongeza mbele za Mungu, kwa toba..walivaa nguo za magunia, kuashiria hali ya unyenyekevu, na kujishusha, kwamba wao si kitu mbele ya Mungu mkuu, na hivyo kutaka rehema kutoka kwake. Mfano wa watu hao ni nabii Danieli.
Danieli 9:3 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na KUVAA NGUO ZA MAGUNIA na majivu. 4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake”
Danieli 9:3 “Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na KUVAA NGUO ZA MAGUNIA na majivu.
4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake”
Na mfano mwingine ni watu wa Ninawi..
Yona 3: 5 “Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, WAKAJIVIKA NGUO ZA MAGUNIA, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. 6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, AKAVUA VAZI LAKE, AKAJIVIKA NGUO ZA MAGUNIA, na kuketi katika majivu”
Yona 3: 5 “Basi watu wa Ninawi wakamsadiki Mungu; wakatangaza kufunga, WAKAJIVIKA NGUO ZA MAGUNIA, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo.
6 Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, AKAVUA VAZI LAKE, AKAJIVIKA NGUO ZA MAGUNIA, na kuketi katika majivu”
Na wengine mfano wa hao, unaweza kuwasoma katika mistari ifuatayo (2Wafalme 19:1, Nehemia 9:1).
Je wakristo sasa Nasi pia tunapaswa kuvaa mavazi ya magunia pindi tunapotubu kwa Mungu wetu au tunapomboleza pindi tunapopitia na misiba?.
Huo ni uchaguzi wa mtu avae au asivae. Lakini biblia haijatoa amri kwamba lazima mtu avae magunia anapotubu.. Ilichotia msisitizo ni hichi..
Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; 13 RARUENI MIOYO YENU, WALA SI MAVAZI YENU, MKAMRUDIE BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya”
Yoeli 2:12 “Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;
13 RARUENI MIOYO YENU, WALA SI MAVAZI YENU, MKAMRUDIE BWANA, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya”
Hapo inasema turarue mioyo yetu na si mavazi yetu…Kumbuka mavazi yanayozungumziwa hapo ndio hayo ya magunia, na si vile vimini, au mavazi yasiyo ya heshima yanayovaliwa na wadada. Hayo mtu anapookoka hapaswi kabisa kuendelea kuyavaa.
Je umeurarua moyo wako kwa Bwana? Kama bado Ni vyema ukafanya hivyo mapema
MAVAZI YA NDANI NA YA NJE.
MAVAZI YAPASAYO.
JE KUVAA PETE NI DHAMBI?
MWANAMKE ULIYEKOMAA KI-UMRI, ITAMBUE HUDUMA YAKO.
JE! UNAYATUNZA MAVAZI YAKO?
Jina la Bwana wetu Yesu libarikiwe. Unapomkiri Yesu kwa Kinywa, au unapojisalimisha kwa Yesu, kwa kudhamiria kabisa, dakika hiyo hiyo..Shetani anaangushwa juu yako, kama umeme…Na anawekwa chini ya miguu yako na unakabidhiwa mamlaka, juu yake.
Luka 10: 18 “Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni KAMA UMEME. 19 Tazama, NIMEWAPA AMRI YA KUKANYAGA NYOKA NA NGE, NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”
Luka 10: 18 “Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni KAMA UMEME.
19 Tazama, NIMEWAPA AMRI YA KUKANYAGA NYOKA NA NGE, NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”
Hapo kuna vitu vitatu ambavyo unapewa amri juu ya hivyo.
Amri ya kukanyaga NYOKA. 2). amri ya kukanyaga NGE na 3). amri ya kukanyaga NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI.
Nyoka ni kiumbe anayeuma (au anayeng’ata kwa kutumia mdomo)..Silaha yake kubwa ni mdomo na mate yake, hana silaha nyingine kiasi kwamba ukikibana kile kichwa hakuna atakachoweza kufanya ili kukudhuru. Nyoka ni mfano wa Watu wanaotumika na shetani, kwa kujua au kwa kutokujua kukudhuru wewe kupitia maneno wanayoyazungumza…Yaani kwaufupi silaha yao ni maneno..
Zaburi 143:1 “Ee Bwana, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri. 2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita. 3 Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao”
Zaburi 143:1 “Ee Bwana, uniokoe na mtu mbaya, Unihifadhi na mtu wa jeuri.
2 Waliowaza mabaya mioyoni mwao, Kila siku huondokesha vita.
3 Wamenoa ndimi zao kama nyoka, Sumu ya fira i chini ya midomo yao”
Fira ni nyoka aina ya KOBRA, Sasa hao Biblia imesema tumepewa amri juu yao..”kuwakanyaga”…Sasa hatuwakanyagi na sisi kwa kuwarudishia maneno.. Hapana, tukifanya hivyo na sisi tutakuwa ni nyoka kama hao. Lakini tunakanyaga vichwa kwa kuyapuuza maneno yale, na kuyazuia yasiingie moyoni mwetu..
Kwasababu ukiyaruhusu yaingie moyoni mwako, yatakuwa sumu kwako na yatakudhuru.. Hivyo unayapuuzia yale maneno na kuyapiga mateke, hiyo ni silaha kubwa sana..Ambayo kwa hiyo utaweza kuwakanyaga nyoka wote.. (Kumbuka nyoka hapo ni lugha ya rohoni, usimwite kamwe ndugu yako nyoka hata kama ni mbaya kiasi gani kwako).
Nge ni mdudu anayeuma kwa kutumia MKIA, na si Mdomo kama nyoka. Hawa ni jamii ya watu ambao wanatumika na shetani pasipo kujua au kwa kujua. Ambao kwa mbele ni wazuri lakini kwa nyuma wanatumia mkia kukudhuru, na kama unavyojua mkia wa nge, umepanga juu ukazunguka lengo lake ni kukuchoma wewe kwa nyuma, pasipo kujua ni nani kakudhuru.
Hivyo shetani anaweza kutumia watu wanaoonekana ni wazuri kwa nje lakini kumbe ni wenye madhara juu yako, watu wa namna hiyo tumepewa amri ya kuwakanyaga..Hatuwakanyagi kwa kuwachukia wala kufanya nao vita bila wao kujijua, tukifanya hivyo na sisi tutakuwa nge, ambao hatungati kwa mdomo lakini tunang’ata kwa mkia..Hivyo na hawa tumepewa silaha ya kushughulika nao, na hiyo si nyingine Zaidi ya MIGUU YETU, Maana yake kutotafuta tafuta wanachokiwaza juu yetu wala kukifikiri juu yako wanatuwazia nini, maana yake wewe unasonga mbele, hufuatilii wewe unaendelea mbele na mambo yako unayoyafanya.
Kama vile watu wanavyolikanyaga neno la Mungu chini, maana yake ni kwamba wanalipuuzia, wanaendelea na mambo yao, vivyo hivyo na wewe unakanyaga maneno yao, au hila zao…kwa kuzipuuzia, na kwajinsi unavyozidi kuzipuuza ndivyo zinavyozidi kuishiwa nguvu, kwasababu utakuwa umempa Mungu nafasi kubwa ya kukupigania, na mwisho wa siku watatubu na kushawishika kumwamini Mungu wako, na utakuwa umeokoa roho zao.
Kipengele hicho ndio cha mwisho na cha Muhimu sana..Ambacho shetani hataki watu wakijue wala wakielewe, kwasababu kinamhusu yeye mwenyewe na mapepo yake, na wala hakiwahusu watu anaowatumia..
Shetani anapenda kuwaaminisha watu kuwa yeye ana nguvu sana, na hivyo akishika mahali ni ngumu yeye kutolewa..Hivyo watu wengi wamefungwa na nguvu za Ibilisi kwa muda mrefu kwasababu tu ya Imani hiyo ndani yao. Utakuta mtu anaumwa, au anapitia tatizo Fulani, na lile tatizo ndani yake kashalikuza na kuwa kubwa mno, na kuamini kuwa inahitajika nguvu nyingi sana za rohoni kuliondoa, au upako mwingi kuliondoa..Wengine wanatokewa kabisa na mapepo wazi, wangine yanawajia katika ndoto, wengine wananyanyaswa na mashetani usiku, kiasi kwamba hata wanaogopa kulala wenyewe. Wengine wanatishiwa na kusumbuliwa na shetani kwa namna ambayo hata wanashindwa kusimulia, mwisho wa siku wanakata tamaa hata ya kuishi. Na kundi hili lipo kubwa sana.
Sasa watu kama hawa, shetani amewashika kwa kutumia Imani yao kupata nafasi ya kuwatesa.
Biblia inasema hapo, tumepewa Amri ya KUKANYAGA… Unaelewa maana ya kukanyaga???…Kukanyaga maana yake ni KULIPOTEZEA JAMBO!!..Kulishusha hadhi, kulipunguza nguvu, kuliabisha, kulidhalilisha, kulidharau. Hiyo ndio maana ya kukanyaga, wala kukanyaga sio kuingia kwenye maombi ya mifungo ya masafa, hapana hiyo sio maana yake.. Maana yake ni kuliweka chini yako jambo. Kama tu vile watu wanavyolikanyaga chini neno la Mungu, wanafanya hivyo kwa kulidharau…Kitendo cha kukidharau kitu tayari umekikanyaga chini.
Waebrania 10.28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu. 29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Waebrania 10.28 “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?”
Umeona hapo?. Watu wote wanaoihesabia damu ya agano la Yesu kuwa ni kitu ovyo, na kumdharau (au kwa lugha ya sasa, ni kuipotezea), watu hao ndio wanahesabika kama wamemkanyaga Mwana wa Adamu.
Ni hivyo hivyo, mtu anayehesabia kazi za shetani kuwa ni kitu ovyo, hapo anakuwa amemkanyaga chini, ya miguu yake.
Hivyo kwa silaha ile ile tunayotumia kukanyaga nyoka na nge, ndiyo hiyo hiyo tunayotumia KUZIKANYAGA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI. Wala hakuna silaha nyingine, shetani asikuogopeshe ikiwa upo tayari ndani ya Kristo..
Maana yake ni hii.
Baada ya kumkiri Yesu, kama ulikuwa unaumwa na kuamini kwamba ni ngumu kupona ugonjwa ulio nao, HILO wazo unaanza kulidharau ndani yako, kuanzia sasa (unalikanyaga!)..
> Shetani alikuwa amekutishia kwamba dhambi yako haisameheki, unalidharau hilo wazo, na kulipoteza kwenye akili yako..
> Mapepo yalikuwa yanakuhubiria kwamba utakufa kila siku kwenye mawazo yako, unayapotezea hayo mawazo na kuyadharau, na kusema hilo halipo..kwa jinsi unavyozidi kuyashusha hadhi hayo mawazo ya shetani, na uongo wake huo…ndivyo na yenyewe yanavyozidi kukosa nguvu juu yako na hatimaye kupotea kabisa.
> Maroho yalikuwa yanakukaba usiku, Hizo sauti zinazokuambia kwamba yatarudi tena huzitilii maanani..acha kabisa kuyapa hayo mapepo heshima kubwa kiasi hicho!, yashushe hadhi..
> Mandoto ya ajabu ajabu shetani alikuwa anakutumia, anza kuyapotezea wala usiyatafakari tafakari, wala usitafute kujua maana zake, yaache yapite…yakanyage chini!.. usiyakuze, kwenye kichwa chako kana kwamba ni kitu cha muhimu sana.
> Mawazo shetani anayokuletea kwamba mapepo yatakudhuru, hayo mawaza anza kuacha kuyawaza, yakanyage chini, badala yake huo muda tumia kutafakari mambo mengine, tumia kutafakari Maneno ya Mungu, hapo utakuwa unammaliza nguvu shetani kwa kasi sana..Maana shetani kazi yake ni kukutisha wewe ili uanze kumfikiria yeye na kumkuza kwenye akili yako, ndipo apate nguvu juu yako..sasa wewe nenda kinyume naye.
>Shetani alikuwa amekuaminisha kwamba ni lazima kila siku aje akutese, yakatae hayo mawazo, wala usiyatafakari, tena yasahau kabisa kwenye kichwa chako, na wala usipate ratiba ya kufikiri jinsi anavyokutesaga..kwa jinsi unavyozidi kumpotezea, naye anapotea..
Kwasababu Miguu yetu ni silaha kubwa na ina nguvu kuliko vichwa vya nyoka, ina nguvu kuliko mikia ya nge, na ina nguvu kuliko nguvu za adui shetani.
Likumbuke hili neno..Luka 10: 18 “Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni KAMA UMEME. 19 Tazama, NIMEWAPA AMRI YA KUKANYAGA NYOKA NA NGE, NA NGUVU ZOTE ZA YULE ADUI, wala hakuna kitu kitakachowadhuru”
Kama hujaokoka kumbuka hizi ni siku za mwisho na Yesu anakaribia kurudi, biblia inasema itatufaidia nini tukiupata ulimwengu mzima na kupata hasara za nafsi zetu?..Tafakari neno hilo kwa makini, hivyo kama utaamua leo kumpa Kristo Maisha yako, utakuwa umefanya jambo la busara sana, ambalo hutakaa ujutia katika maisha yako, hivyo kwa msaada Zaidi na maombezi fungua hapa >> SALA YA TOBA.
Maran atha!
MKUU WA UZIMA AKUWEKE HURU.
SALA YA UPONYAJI/MAOMBI YA UPONYAJI.
UPONYAJI WA ASILI
KWA KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA.
WEWE NI BWANA UNIPONYAYE.
Shalom, leo tutajifunza madhara ambayo tunaweza kuyapata pale tunapoukataa ule upendo wa mwisho kabisa wa Yesu Kristo.
Yuda alikuwa ni mtume wa Yesu, lakini kama tunavyojua habari yake, alikuwa mwizi, na pia hakuwa na upendo wa dhati kwa Bwana.. Tunaona katika biblia hali hiyo ya uasi aliendelea nayo kwa muda mrefu sana, lakini katika kipindi hicho chote haikuleta madhara yoyote katika maisha yake, aliendelea kutembea na Yesu, aliendelea kushiriki baraka zote za Yesu kama mmojawapo wa mitume wengine..
Mpaka anafikia hatua ya kwenda kupatana na wakuu wa makuhani ili kumsaliti Yesu bado, nafasi alikuwa nayo ya kuahirisha mawazo yake, uwezo huo alikuwa nao, isitoshe alikuwa anaona Yesu akimpa viashiria vingi kuwa anavyovifanya anaweza kuviahirisha, lakini hilo halikumwingia moyoni mwake. Mpaka siku ile walipokuwa wameketi chakulani jioni na Yesu akaanza kuwatawadha miguu, kuonyesha upendo wake kwao, akamtawadha na Yuda miguu yake, huku Yuda akiyatazama macho ya Emanueli yenye upole, yasiyo na kosa lolote, akisikia kabisa rohoni anashuhudiwa kuwa anachojaribu kukifanya sicho sawa..aghahiri mawazo yake, haoni mpaka Bwana wake amekuja kumuosha miguu yake, kumthibitishia kuwa miguu yake haitakiwi kuwa myepesi kukimbilia maovu.. Lakini hilo halikuwa kitu kwa Yuda.
Mpaka dakika ya mwisho kabisa tuona Kristo anaonyesha Upendo wake wa mwisho, wa kuchukua chakula chake cha heshima na kumgawia Yuda peke yake, kama heshima ya kipekee, tusome;
Yohana 13:21 “Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti. 22 Wanafunzi wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye. 23 Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda. 24 Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye? 25 Basi yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani? 26 Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. 27 NA BAADA YA HILO TONGE SHETANI ALIMWINGIA. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi. 28 Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo. 29 Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu. 30 Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku”.
Yohana 13:21 “Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.
22 Wanafunzi wakatazamana, huku wakiona shaka ni nani amtajaye.
23 Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.
24 Basi Simoni Petro akampungia mkono, akamwambia, Uliza, ni nani amtajaye?
25 Basi yeye, hali akimwelekea Yesu kifua chake, akamwambia, Bwana, ni nani?
26 Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote.
27 NA BAADA YA HILO TONGE SHETANI ALIMWINGIA. Basi Yesu akamwambia, Uyatendayo yatende upesi.
28 Wala hakuna mtu katika wale walioketi chakulani aliyeijua sababu ya kumwambia hivyo.
29 Kwa maana wengine walidhania, kwa kuwa Yuda huchukua mfuko, ya kwamba Yesu alimwambia kama, Nunua mnavyovihitaji kwa sikukuu; au kwamba awape maskini kitu.
30 Basi huyo, akiisha kulipokea lile tonge, akatoka mara hiyo. Nako kulikuwa ni usiku”.
Sasa Tonge sio ule mkate wa Pasaka, au sio ule mkate aliowapa wanafunzi wake kama mwili wake waule siku ile, hapana, Tonge ni chakula cha heshima kilichokuwa kinaandaliwa na wayahudi zamani, ambacho kinaweza kikawa na mkate au kitu kingine, lakini sana sana kilitumika mkate, ambacho hicho mtu alikuwa anampa Yule mtu anayemuheshimu sana, au wa muhimu kwake, ili kuinyesha thamani yake. Hivyo aliyeuandaa aliuchua mkate huo na kuuchovya katika mboga iliyoandaliwa pamoja na huyo mtu aliyemwandalia.
Utaliona Hilo katika kipindi cha Ruthu, alivyoitwa na Boazi kwake..
Ruthu 2:14 “Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza”.
Soma pia Ayubu 31:16, na Mithali 23:6, utaliona neno hilo.
Sasa alichokifanya Bwana ndicho hichi, kumpa Yuda heshima ya kipekee, wa kuchovya donge lake pamoja naye,. Kuonyesha upendo wake wa kipekee kwake.
Lakini mara baada ya kula tu, angali moyo wake bado hujaiacha nia ya kumsaliti biblia inatuambia shetani akamwingia saa hiyo hiyo …Akawa amefikia “point of no return”. Hii Ikiwa na maana kuwa sasa shetani anayo nafasi ya kumchukua huyu mtu asilimia 100, anaweza kumwendesha kwa jinsi anavyotaka, (amepata hati miliki maalumu) na ndio hapo utaona akawaendea wale makuhani na kuwapa mikakati yote ya kumkamata Yesu. Na Mwisho wa siku yeye mwenyewe akajiua, kwasababu tayari alikuwa ameshavaliwa na pepo mkuu mwenyewe ibilisi.
Na sisi vivyo hivyo, Kristo anapotuonyesha upendo wake kwetu, na hatuoni jambo lolote baya likitokea kwenye maisha yetu pale tunapofanya dhambi kwa makusudi, pengine unazini na upo kanisani, na huoni jambo lolote baya likikutokea, na saa nyingine unamwomba Yesu akutendee jambo Fulani na anakutendea, na wewe unadhani itaendelea hivyo hivyo kila siku..
Upo wakati atakuonyesha upendo mkubwa zaidi ya huo, (atakumegea Tonge lake) na kama usipojua nini maana ya Upendo huo kwamba anakutaka wewe utubu, wewe ukadhani anafurahishwa na unachokifanya, na ndio maana kukubariki, ujue tayari mwisho wako umefika. Ibilisi anakuingia na hapo ndipo unapokuwa mwisho wako.
Hivyo tusipumbazwe na rehema za Kristo. Tukiona hatuadhibiwi kwa makosa yetu, tuogope kwasababu utafika wakati tutakabidhiwa shetani moja kwa moja.
Hizi ni nyakati za mwisho Je! Umeokoka? Je! Umepokea Roho Mtakatifu. Kumbuka Yesu ndio mwokozi wa ulimwengu. NA HUO NDIO UKWELI PEKEE ULIODUMU DUNIANI KWA WAKATI WOTE.
BIRIKA LA SILOAMU.
Sikukuu ya kutabaruku ni ipi?
CHAPA YA MNYAMA
MTUMWA SI MKUU KULIKO BWANA WAKE.
Bwana Yesu aliposema pesa za bindoni alimaanisha pesa za mfukoni.. mfuko unaozungumziwa ni ule wa kuvaa kiunononi ambayo ndio ilitumika zamani. tazama picha.
Marko 6:7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu; 8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni”;
Marko 6:7 “Akawaita wale Thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu;
8 akawakataza wasichukue kitu cha njiani isipokuwa fimbo tu; wala mkate, wala mkoba, wala pesa za bindoni”;
Ni kwanini Bwana Yesu alisema hivyo?
Ieleweke kuwa Bwana Yesu hakumaanisha kuwa injili haihitaji fedha, wala mahitaji hapana, injili inahitaji fedha, tena sana ili isonge mbele.…Lakini hapo alikuwa halengi kazi ya injili bali aliwalenga wale wapeleka injili. Kwamba hao ndio wanapaswa wasifikiri kuwa inahitajika maandalizi mengi au makubwa ili wao wamtumikie Mungu.
Bwana aliwatuma wao kama wao, na mambo mengine yote aliwapa huko mbele ya safari. Na ndio maana sehemu nyingine aliwauliza hapo nilipowatuma hamna kitu Je! Mlipungukiwa na chochote? Wakasema hapana.
Luka 22:35 “Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La!
Hiyo ni kuonyesha kuwa mahitaji ya muhimu aliwapatia. Huko walipoenda. Hata na sisi, tunapaswa tujue kuwa tunapotaka kumtumikia Mungu tusifikirie sana hali zetu, labda tutaanzia wapi,au tuna nini, au hatuna nini, hilo wazi tuliondoe, Ni kweli wazo hilo ni gumu kulipokea lakini ndio maagizo ya Bwana.. tunapaswa tuyaamini, na kwamba yeye mwenyewe atatupatia.
Fitina maana yake nini kwenye biblia?
Kijicho ni nini? (Marko 7:22)
MZAZI, JALI MAISHA YA KIROHO YA MTOTO WAKO.
Kwanini wale dubu waliowauwa vijana wa Elisha walikuwa wa kike?
Fitina ni nini?
Katika biblia Fitina maana yake ni “kufanya mageuzi au mapinduzi”. Mtu ambaye anataka kufanya mapinduzi labda ya kimamlaka, kutokana na kwamba labda hakubaliani na serikali yake, au mamlaka yake, na hivyo akakusanya watu kadhaa na kutafuta kuiangusha serikali, kwa lugha ya kibiblia mtu huyo anafanya fitina.
Katika biblia (Agano la kale) tunaona mifano ya watu kadhaa waliofanya fitina katika biblia..
Huyu Shalumu, alimng’oa Mfalme Zekaria kwenye kiti chake kwa hila, na yeye akatawala mahali pake
2Wafalme 15: 10 “Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake…… 15 Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na fitina aliyoifanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-chatarehe cha wafalme wa Israeli.”.
2Wafalme 15: 10 “Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake……
15 Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na fitina aliyoifanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-chatarehe cha wafalme wa Israeli.”.
Huyu naye alimng’oa madarakani mfalme Peka wa Israeli kwa kumuua na kutawala mahali pake.
2Wafalme 15:30 “Na Hoshea mwana wa Ela akafanya fitina juu ya Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.”
Na wengine wengi ambao unaweza kuwasoma katika mistari hii..(2Wafalme 17:4, 2Wafalme 21:23, 2Nyakati 13:6)
Katika agano jipya pia tunaona mifano ya baadhi ya watu waliofanya fitina.
Huyu Baraba, alipanga kunyanyuka kinyume na mamlaka iliyokuwa inatawala, akataka kufanya mapinduzi…Na pia aliua watu kadhaa katika harakati zake hizo za mapinduzi..
Luka 23: 18 “Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba. 19 Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya FITINA iliyotokea mjini, na kwa uuaji”
Luka 23: 18 “Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba.
19 Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya FITINA iliyotokea mjini, na kwa uuaji”
Na katika kanisa la Kristo pia kuna fitina za shetani.
Fitina ndani ya kanisa la Kristo ipoje?..Ni pale mtu anapotaka KULIPINDUA NENO LA MUNGU, na kulisimamisha lake.
Warumi 16:17 “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale WAFANYAO FITINA na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. 18 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu”.
Warumi 16:17 “Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale WAFANYAO FITINA na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
18 Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu”.
Asilimia kubwa ya watu WANAOLIPINDUA NENO LA MUNGU, na kulisimamisha lao, ni ili tu wapate faida Fulani, labda fedha, ndio biblia inasema hapo, watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo bali matumbo yao. Hawa wanaweza kuupindua Uponyaji wa Yesu uliopo katika JINA LAKE, na kulazimisha uwe katika Maji, au mafuta..lengo lao wala si kwasababu wana huruma sana, lengo lao ni ili wauze hayo maji na mafuta mengi wapate pesa, ndio maana yanawekwa kwa kiwango kidogo lakini bei kubwa.
Tumeonywa tujihadhari nao.. tusichukuliwe na fitina zao.
Hali kadhalika wapo wahubiri wanaomfitini Kristo, na kutafuta kuchukua nafasi yake, ili waabudiwe au waonekane ni miungu-watu, hawa nao pia tumeonywa tujiepushe nao.
Je umeokoka?. Kama bado unasubiri nini tubu leo na kumpokea Kristo, unyakuo upo karibu
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312
Nini tofauti kati ya Husuda, faraka na uchafu?
Hazama ni nini katika biblia?(Ezekieli 16:12, Kutoka 24:47)
MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU
RUDI KUMPA MUNGU UTUKUFU.
KITABU CHA UZIMA
KITABU CHA UCHAWI.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu katika uchambuzi wa vitabu vya biblia, tumekwisha jifunza vitabu kadhaa vya mwanzo, kama utakuwa hujavipitia na ungependa kufanya hivyo, basi unaweza kufungua hapa>> VITABU VYA BIBLIA: Sehemu ya 1
Na leo tutazidi kusonga mbele, kwa kutazama kitabu kimoja Zaidi ambacho ni kitabu cha Ayubu.
KITABU CHA AYUBU.
Kitabu cha Ayubu ndio kitabu kikongwe kuliko vitabu vyote vya biblia, Kitabu hichi kiliandikwa kabla ya kuandikwa kitabu cha Mwanzo. Kitabu cha Mwanzo kiliandikwa na Nabii Musa, kadhalika na kitabu hichi cha Ayubu, ni nabii Musa huyo huyo ndiye aliyekiandika.
Nabii Musa alikiandika kwanza kitabu hichi kisha ndio vikafuata vitabu vingine vingine vya torati kama kitabu cha Mwanzo, kutoka n.k.. Sasa sio kwamba Musa alikuwepo wakati Ayubu anaishi duniani na akawa ananakili Maisha aliyokuwa anayapitia hapana!.. Ayubu aliishi miaka mingi sana kabla ya Nabii Musa kutokea, na mambo yote Ayubu aliyoyapitia yalinakiliwa na Ayubu mwenyewe Pamoja na watu waliomzunguka Ayubu (maana yake marafiki zake na ndugu zake). Hivyo hata baada ya kufa Ayubu, historia ya Maisha yake iliendelea kuwepo, lakini haikuwepo katika mpangilio bora, Sasa Musa alipokuja kutokea miaka mingi baadaye, kwa uongozo wa kiMungu alikusanya Pamoja taarifa zote za Ayubu kwa usahihi na kuziweka kwenye mfumo wa kitabu, ndio kikatokea hicho kitabu cha Ayubu tunachokisoma leo katika biblia.
Kitabu cha Ayubu kinaanza na Historia ya Ayubu mwenyewe mahali alipozaliwa na uelekevu wake kwa Mungu. Ayubu alizaliwa katika nchi ya “Usi”. Nchi ya Usi kwasasa ni maeneo ya kusini mwa nchi ya YORDANI. (kufahamu nchi ya Yordani ilipo, unaweza kutazama ramani).
Ayubu aliishi kabla ya Ibrahimu, hivyo hakuwa Mwisraeli. Lakini alimjua Mungu wa kweli wa mbingu na nchi na alimcha yeye, kutoka kwa mababu zake (akina Nuhu)
Kitabu cha Ayubu kimegawanyika katika Sehemu kuu 4.
Tukianza na sehemu ya kwanza:
Sehemu hii ni ile milango miwili ya mwanzo, na ndio milango iliyo mirahisi kuieleweka kuliko milango mingine yote inayofuata. Hapa inaelezea Ayubu jinsi alivyokuwa Mkamilifu na mwelekevu mbele za Mungu, kwamba alikuwa ni mcha Mungu na ni mtu aliyejiepusha sana na uovu.
Lakini pia katika Sura hizi mbili za Mwanzo ndizo Sura pekee katika biblia nzima zilizotupa, taswira kamili ya kinachoendelea katika katika mamlaka yaliyopo juu yetu sisi wanadamu. Sura hizi ndizo zimetufumbua macho na kuelewa kuwa kumbe wakati sisi tunaendelea na Maisha yetu, kuna mmoja anatushitaki mbele za Mungu, na ndiye sababu ya majaribu yetu yote tunayoyapitia. Ni ukurasa mmoja tu katika biblia lakini umekuwa muhimu sana kwetu. Inaeleza jinsi sababu ya mwenye haki wakati mwingine kupitia majaribu. Sasa ili kujua kwa urefu ni kwa namna gani mashitaka hayo yanaendelea juu mbinguni dhidi yetu, unaweza kufungua hapa na kusoma upatapo nafasi >>> JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU. Kwasasa hatutaingia sana huko.
Sehemu ya Pili:
Sehemu hii ni kuanzia ule mlango wa 3 hadi wa 38, Sehemu hii ni imeelezea majibizano kati ya Ayubu na Rafiki zake watatu, walioitwa ELIFAZI, BILDADI, na SOFARI.
Marafiki hawa walikuwa ni marafiki wa Ayubu wa kitambo kirefu, na walikuwa wamejaa hekima ya ki-Mungu ndani yao. Na waliposikia Rafiki yao kapatwa na majanga yale, na misiba ile walitoka huko walipokuwepo kuja kumliwaza na kumshauri.
Rafiki zake hawa walikuja na Mashauri yao, lakini hawakujua kuwa Mashauri yao hayakuwa yaliyonyooka mbele za Mungu. Wenyewe katika akili zao waliamini asilimia mia moja kwamba Ayubu kuna mahali atakuwa alimkosea Mungu ndio maana akapatwa na majanga yale, walitumia mitazamo yao tu, hawakujua kuhusu vita vilivyokuwa vinaendelea mbinguni. Hivyo walikuja kwa nia moja tu, KUMWAMBIA AYUBU ATUBU!!, Atubie dhambi zake zote alizozifanya kwa siri, zilizompelekea apate majanga yote yale. Kwasababu walimwambia hakuna mtu anayeweza kukutwa na majanga yale, kama hajamkosea Mungu.
Na Ayubu alipowaambia kwamba hajafanya chochote kilicho kibaya cha siri, bado hawakumwamini Ayubu..waliendelea kumwambia kwamba amemkosea Mungu. Hivyo ikawa mlolongo mrefu wa mashauriano, kila mmoja akitumia hekima yake kutoa Mashauri yake dhidi ya Ayubu. Ayubu naye akitumia hekima zake kuwajibu kuwa hajafanya kosa lolote..mazungumzo yakawa marefu mno, mwishoni wakachoka kumshauri Ayubu, kwasababu alionekana anajihesabia haki machoni pake mwenyewe. Akatokea kijana mmoja aliyeitwa Elihu, naye pia akajaribu kutoa Mashauri yake kwa Ayubu na Rafiki zake watatu.
Na katika mazungumzo yao wote wanne (yaani Ayubu na Rafiki zake watatu, yalikuwa yamfikia Mungu juu pasipo wao kujua, na Mungu alikuwa anawasikiliza. Sasa kwa urefu pia kuhusu huduma za hawa Rafiki zake Ayubu, Na kufahamu jinsi, shetani anavyoweza kuwatumia watu wanaoitwa watumishi wa Mungu kuwamaliza watumishi wengine wakamilifu, fungua hapa kwa ajili ya somo hilo kwa urefu >> HUDUMA YA ELIFAZI, BILDADI NA SOFARI,
Sehemu ya Tatu:
Baada ya mazungumzo yao yote, Mungu anamjibu Ayubu kwa upepo wa kisulisuli, maana yake kwa Tufani, jambo ambalo Ayubu hakuwahi kuliona hapo kabla, na anaanza kwa kumuuliza.
Ayubu 38:1 “Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, 2 Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa?”
Ayubu 38:1 “Ndipo Bwana akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
2 Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa?”
Maana yake ni “Ni nani huyo anayehoji kazi zangu kwa maneno ya upumbavu”…Swali hilo Mungu alimwuliza Ayubu, akimlenga Ayubu na marafiki zake watatu.. Kutokana na maneno waliyokuwa wanazungumza, juu ya Mungu alichomfanyia Ayubu.
Na ukiendelea kusoma mpaka huo Mlango wa 41, utaona Bwana anaendelea kumuuliza maswali Ayubu, kuhusu utukufu wake, ambayo maswali hayo hayana majibu mpaka sasa..(Ili Ayubu ajue kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kuzihoji kazi zake wala kuzipatia majibu)…Mfano wa swali moja Mungu alilomuuliza Ayubu ni ili..
Ayubu 38:4 “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. 5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?”
Ayubu 38:4 “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?”
Hili swali hakuna mtu anaweza kutoa jibu lake. Na maswali mengine mengi aliyoulizwa unaweza kuyasoma mpaka mlango ule wa 41.
Sehemu ya Nne:
Na baada ya Mungu kumuuliza Ayubu hayo maswali. Ayubu alikosa majibu, na akajinyenyekeza akatubu, naye akajiona alikosea sana katika kunyanyua mdomo wake kuzihoji hoji kazi za Mungu, Pamoja na marafiki zake, ijapokuwa hakuzihoji kwa ubaya, lakini kitendo cha kushindana tu, tayari alitambua lilikuwa ni kosa. Hivyo akatubu mbele za Mungu kwa kuvaa nguo za magunia, na kufunga mdomo wake. Utasoma habari hiyo katika ule mlango wa 42.
Ayubu 42:1 “Ndipo Ayubu akamjibu Bwana, na kusema. 2 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. 3 Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? KWA MAANA, NIMESEMA MANENO NISIYOYAFAHAMU, MAMBO YA AJABU YA KUNISHINDA MIMI, NISIYOYAJUA. 4 Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie. 5 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. 6 Kwa sababu hiyo NAJICHUKIA NAFSI YANGU, NA KUTUBU KATIKA MAVUMBI NA MAJIVU”.
Ayubu 42:1 “Ndipo Ayubu akamjibu Bwana, na kusema.
2 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.
3 Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? KWA MAANA, NIMESEMA MANENO NISIYOYAFAHAMU, MAMBO YA AJABU YA KUNISHINDA MIMI, NISIYOYAJUA.
4 Sikiliza, nakusihi, nami nitanena; Nitakuuliza neno, nawe niambie.
5 Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.
6 Kwa sababu hiyo NAJICHUKIA NAFSI YANGU, NA KUTUBU KATIKA MAVUMBI NA MAJIVU”.
Na baada ya Ayubu kujinyenyekeza na kujua kosa lake, Bwana aliwageukia wale Rafiki zake watatu, Elifazi, Bildadi na Sofari, ambao ndio waliomfanya Ayubu, azungumze maneno mengi, na zaidi ya yote, maneno yao ndio yaliyozihoji vibaya kazi za Mungu kuliko hata Ayubu. Hivyo Mungu akawakasirikia na kutaka kuwaadhibu.
Ayubu 42:7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu. 9 Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile Bwana alivyowaamuru; naye Bwana akamridhia Ayubu”.
Ayubu 42:7 “Basi ikawa, baada ya Bwana kumwambia Ayubu maneno hayo, Bwana akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira zangu zinawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili; kwa kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
8 Basi sasa, jitwalieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, mkamwendee mtumishi wangu Ayubu, mjisongezee sadaka ya kuteketezwa; na huyo mtumishi wangu Ayubu atawaombea ninyi; kwa kuwa nitamridhia yeye, nisiwatende sawasawa na upumbavu wenu; kwani ninyi hamkunena maneno yaliyonyoka katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu.
9 Basi Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya kama vile Bwana alivyowaamuru; naye Bwana akamridhia Ayubu”.
Na mwisho, katika kitabu hichi tunaona, tunaona Mungu akimuhurumia Ayubu na kumbariki tena na kumpa mara dufu ya vile alivyokuwa navyo.
Kuonyesha jinsi mwisho wa Mungu ulivyo mwema.
Kwa hitimisho katika kitabu hichi tunajifunza mambo yafuatayo:
1 . Kumcha Bwana na kuepukana na uovu kama Ayubu:
2. Uvumilivu wakati wa majaribu: (Yakobo 5: 11 Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.)
3. Kuishi Maisha ya usafi: kwasababu mshitaki wetu ibilisi, anapeleka mashitaka kuhusu sisi kila siku. Kama alimshitaki Ayubu kwa uzuri wake, unadhani tukiwa wabaya atakuwa anapeleka nini mbele za Mungu kama si kutuchongea tuangamizwe.
4. Kutokuwa na mashindano ya dini (hata kama unajua kitu, sio busara kulumbana na mtu asiyetaka kuamini unachokiamini) Ayubu alijua yupo sahihi, na marafiki zake hawapo sahihi, lakini kitendo cha kujibizana vile, ikawa tayari ni jambo lisilompendeza Mungu. Hivyo na sisi hatupaswi kuwa hivyo (Tito 3:9, 2Timotheo 2:14).
5. Mwenye haki kupitia mateso, haimaanishi Mungu hayupo naye; Tofauti na mitazamo ya watu wengi leo hii, wakishaonekana tu mtu aliyeokoka, anapitia hali Fulani mbaya labda ni hali ngumu ya kifedha, au ni magonjwa, basi moja kwa moja wanahitimisha kuwa Mungu amemwacha, au Mungu hayupo pamoja naye.
6. Kuwaombea Rafiki zetu na maadui zetu. (Hapo tunaona japokuwa Ayubu aliudhiwa na kukoseshwa na marafiki zake hao, lakini mwishoni aliwaombea rehema kwa Mungu, na wala hakuwalaani, na kwa kufanya vile {yaani baada ya kuwaombea tu}ndio ikafungua mlango wa baraka zake za mwisho).
Ayubu 42:10 “Kisha Bwana akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; Bwana naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza”.
Hivyo na sisi tukitaka kufungua milango ya baraka hatuna budi kuwapenda adui zetu, na kuwaombea wale wanaotuudhi sawasawa na maneno ya Bwana wetu Yesu aliyotuasa katika..
Luka 6:27 “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, 28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi”
Luka 6:27 “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi,
28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi”
Je umeokoka? Kama bado unasubiri nini ndugu?..Kristo anarudi, je akirudi leo kulichukua kanisa utakuwa wapi?..hayo Maisha ya uasherati, ulevi na anasa yanakusaidia nini sasa? Zaidi ya kukuharibu tu?.
Kama leo utaamua kuokoka utakuwa umefanya uamuzi bora ambao hautaujutia, ni vizuri ukafanya hivyo sasa, na wala usingoje kesho…kwamaana hujui yatakayozaliwa ndani ya siku moja.. Hivyo kama upo tayari kutubu leo na kumpokea Kristo fungua hapa kwa msaada Zaidi >>> SALA YA TOBA.
Usikose mwendelezo wa vitabu vinavyofuata.
Kwa maombezi/ Ushauri/ Ratiba za Ibada/Maswali/ Whatsapp/ Piga namba hizi: +255693036618/ +255789001312
MAMBO YA KUJIFUNZA KATIKA KITABU CHA RUTHU:
DANIELI: Mlango wa 1
UTAWALA WA MIAKA 1000.
SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?