Category Archive Home

RUDIA, TENA NA TENA KUMWOMBA MUNGU USIKATE TAMAA.

Nilipokuwa mdogo, kulikuwa na wakati kaka yetu mara nyingi alikuwa kila akitoka shule ni lazima arudi na zawadi siku nyingine alikuwa anapitia bakery anatuletea sambusa za nyama n.k., sasa alikuwa anamnunulia kila mtu ya kwake, lakini mimi na mwenzangu tulikuwa na tabia moja, alipotugawia za kwetu, tulikuwa tunazila haraka haraka, ili ziishe haraka tuanze kuwaomba wengine kabla za kwao hazijaisha…mpaka tunamrudia Yule aliyetuletea zawadi, mwanzoni anatufukuza kabisa tusimkaribie, lakini sisi tulikuwa hatuachi kumsumbua unaona kabisa amekasirika, kaudhika lakini tunazidi kumwomba tu, anatuambia tukiendelea kumsumbua sasa atatupiga, lakini tulikuwa hatuachi kumsumbua kama vile nzi, anatuonya tena, na tena kwa ukali na hasira kuwa atatupiga huku hasira zikiwa zimemjaa, lakini sisi tukiwa katika hatari ya kupigwa hatuachi kumwomba atugawie kidogo, mwisho wa siku anaona bora acheke tu, anasema haya njooni, anaigawanya sambusa mara mbili nusu anampa mmoja na nusu mwingine.

Alianza kwa hasira lakini mwisho wa siku anaishia kwa kucheka tu, anasema ngoja niwape wasizidi kunisumbua, hizi ni kanuni ambazo zipo katika maisha yetu, unapokazana kung’ang’ania kitu Fulani utakipata tu hata iweje, ndio maana hata Bwana alitoa mfano unaofanana na huo na kusema.,

Luka 18.1 “Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.

2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.

3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.

4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,

5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.

6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.

7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?

8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?”

Unaona, mfano mwingine ni huu:

Luka 11:5 “Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,

6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake;

7 na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?

8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.

9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.”

Hivyo na wewe, leo uliyempa Kristo Maisha yako na kumwishia yeye katika Kanuni zake nataka nikuambie, usikate tamaa katika kumwomba Mungu, wala usimwekee mipaka kwa kile umwombacho..Wapo wengine wanaogopa kumwomba Mungu vitu vikubwa wakidhani kuwa Mungu hawezi kuwatendea, unavyomchukulia Mungu ndivyo atakavyojifunua kwako, yeye atakupa kwa kiwango kile kile ulichompimia yeye..Bwana alisema ombeni lolote kwa jina langu nami nitalifanya(Yohana 14:13), hakutoa masharti ya jambo hilo uliombalo maadamu lipo sawasawa na mapenzi yake..

Hata kama utaona leo wala kesho hujibiwi, usiache kuomba, hata kama itapita miezi, miaka usiache kumsumbua sumbua Mungu, kwani wakati utafika atakupa hitaji lako, kwasababu anasema kila aombaye, kila atafutaye, na kila abishaye, atafunguliwa..hiyo ni lazima, hajasema labda atapata,au labda ataona, badala yake anasema kila aombaye atapata.Kuonyesha ni kauli ya AMRI.

Yakobo 5:16 ‘’………. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.

18 Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake’’

Hivyo tumia fursa hiyo kumwomba Mungu, bila kuvunjika moyo, usije ukafika kule, ukasema laiti ningejua nilipokuwa duniani ningemwomba Mungu hiki au kile..Nafasi ipo wazi kwako sasa, mwombe Mungu KARAMA zilizo kuu yaani kipawa vyake vya rohoni, mwombe Mungu akupe ROHO WAKE MTAKATIFU kama bado hujapokea, (hilo ndio jambo kubwa ambalo mwanadamu anaweza kumwomba Mungu) maana huyo ndio chanzo cha vyote ukimpata huyo umeupata ulimwengu mzima.. mwombe bila kukata tamaa, naye atakupa kwa wakati wake. Alisema

Mathayo 11.13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa ROHO MTAKATIFU HAO WAMWOMBAO?.”

Kumbuka Roho Mtakatifu ndio muhuri wa Mungu, na Roho Mtakatifu ni zaidi ya Kunena kwa Lugha.

Ubarikiwe. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

FAIDA ZA MAOMBI.

ELIYA ALIOMBA KWA BIDII HADI AKASIMAMISHA MVUA KUNYESHA KWA MIAKA 3 NA NUSU JE! KUOMBA KWA BIDII NI KUOMBA KWA NAMNA GANI?

AYUBU ALITESEKA KATIKA MAJARIBU KWA MIAKA MINGAPI?

NI JAMBO GANI LINALOMTAMANISHA SANA BWANA TUMWOMBE BILA KUKATA TAMAA?

Rudi Nyumbani

Print this post

MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA!

Luka 3:7 ‘’Basi, aliwaambia makutano ya wale waliomwendea ili awabatize, Enyi wazao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?

8 Basi, TOENI MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu Watoto.

9 Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni’’.

Maneno hayo Yohana aliwaambia Wayahudi, ambao kwa kipindi kirefu walikuwa wanajua kuwa wao ndio Taifa teule la Mungu, uzao wa Ibrahimu wana wa Ahadi…Kwamba katika dunia nzima wao pekee ndio walioteuliwa na Mungu kuwa Taifa la Mungu…Na kweli ndivyo walivyokuwa kulingana na ahadi Mungu aliyomwahidia Ibrahimu. Na wapo baadhi waliokuwa wanaishi Maisha ya kumpendeza Mungu lakini wengi wao waliobweteka na kusema ‘sisi ni uzao wa Mungu hata tukifanya hiki au kile Mungu hatatutupa milele’ na hiyo ikawafanya  wawe wanaishi Maisha ya uvuguvugu.

Lakini hapa Yohana anatokea kutoka nyikani akiwaambia…. ‘enyi kizazi cha nyoka’…kumbuka wao wanajijua kuwa ni kizazi cha Ibrahimu, lakini Yohana anawaambia hapa ‘enyi kizazi cha nyoka’…Na wakati huo ilikuwa inajulikana na watu wote hata Yohana mwenyewe mbatizaji alikuwa anajua kuwa ‘ailaaniye Israeli amelaaniwa’…Kwasababu Mungu alimwambia Ibrahimu akulaaniye amelaaniwa, na akubarikiye amebarikiwa (Mwanzo 12:3)…Hivyo kuwaita ‘wana wa Israeli, uzao mteule wa Mungu kuwa ni uzao wa Nyoka ni kama kuilaani Israeli’.

Lakini Yohana hakuishia hapo, aliendelea kuwaambia…’msiseme mioyoni mwenu kuwa tunaye baba ndiye Ibrahimu.. kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu Watoto’’….

Yaani kwa lugha nyepesi hiyo sentensi ili ieleweke tunaweza kuiweka hivi; ‘Enyi wazao wa nyoka msijidhanie kuwa ni nyie tu ndio watu pekee wa Mungu na kwamba Mungu hawezi kuwa na watu wengine zaidi yenu…msifikiri hivyo hata kidogo…kwamaana hata kutoka kwenye vitu vinavyodharaulika visivyokuwa na uhai kama haya mawe Mungu anaweza kuwanyanyua watu wake wengine wa ahadi wanaompendeza’’.

Na kama ni msomaji mzuri wa Biblia utakuja kuona kuwa hayo mawe Yohana aliyokuwa anayazungumzia hapo ni sisi watu wa mataifa..Baada ya wayahudi (yaani waisraeli) kuikataa Neema iliyoletwa na Bwana wetu Yesu Kristo, Na kuyakataa maonyo haya ya Yohana Mbatizaji…Neema hiyo ilitoka kwao na kuhamia kwetu sisi watu wa mataifa…Sisi ndio hayo mawe tuliounuliwa kuwa Watoto wa Ibrahimu.

Matendo 13:46 ‘’Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza[yaani kwa waisraeli]; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa.

47 Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.

48 Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini’’.

Kwahiyo Kazi moja wapo Yohana Mbatizaji aliyokuja kuifanya ni ‘kuondoa mawazo potofu’ katikati ya wayahudi kuwa wao ni watu bora kuliko wote…Na kwamba Mungu hawezi kuwaacha kwa namna yoyote ile…Hivyo hata wakiendelea na Maisha yao machafu, Mungu atakuwa nao tu milele!! Kwasababu ni Waisraeli tu, Taifa la Mungu, uzao wa Ibrahimu…

Lakini Yohana akawaambia kwa uweza wa Roho, kuwa wasipozaa matunda yapatanayo na Toba zao…watakatwa (maana yake Mungu atawaacha na kuigeuzia Neema yake kwa watu wengine).Na wenyewe wataachwa ukiwa..Lakini hawakutaka kusikia na yakawakuta yaliyotabiriwa.

Kadhalika Neema imekuja kwetu sisi, Ujumbe ni ule ule kwetu pia..Tusijidhanie kuwa kwasababu Neema ipo, kwasababu tuna damu ya Yesu, na kwamba tunaweza kuomba toba wakati wowote na kupata msamaha..basi tukabweteka na kutokuzaa matunda yapatanayo na Toba! Na sisi pia tutakatwa na kutupwa motoni. Kama Mungu hakuwahurumia watu wake Israeli, unadhani sisi tutasalimikaje?

Warumi 11:19 “Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.

20 Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.

21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.”

SASA MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA NI YAPI?.

Kumbuka hapa Yohana hakuwaambia wayahudi, watubui dhambi zao….hapana bali aliwaambia wazae matunda yapatanayo na toba zao…Ikiwa na maana kuwa Walishatubu! Lakini walikuwa hawazai matunda yapatanayo na toba zao….Siku zote baada ya toba..hatua inayofuata ni kutenda na kuishi kulingana na ulichokitubia…Kama Mtu alikuwa ni mwasherati anatubia kwanza uasherati wake, na akiisha kutubu anaizalia matunda ile Toba…Yaana anaanza kuishi Maisha ya usafi na anaacha uasherati kabisa, sio anatubu leo baada ya siku mbili anatenda tena ile dhambi, halafu anatubu tena na kufanya tena.. kama anacheza danadana..Hapana! hapo huzai matunda yoyote ndugu..Yohana alichowaambia kama sauti ya mtu aliaye nyikani ni kwamba ‘watu wazae matunda yapatanayo na Toba, au waishi Maisha yanayoendana na walichokitubia’…Hivyo ndicho alichokuwa anakisisitiza Yohana.

Watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli lakini ukweli ni kwamba, Ukitubu halafu hujakusudia kuacha kile ulichokitubia..hapo ni unamkufuru Mungu!…Na unapokwenda kushiriki Meza ya Bwana, au kubatizwa na huku ndani ya moyo wake hujakusudia kuacha dhambi…ni bora usifanye hivyo tena, au usiende kubatizwa kabisa…kwasababu utakuwa unakwenda kujitafutia laana badala ya baraka.

Usijaribu kabisa kushiriki meza ya Bwana, kama hujakusudia kuacha dhambi zako, kama bado ni mwasherati, au mlevi, au mtazamaji wa pornography au mtukanaji.. kuna hatari kubwa sana…hata wakati mwingine ya kupoteza Maisha….Chagua kuwa baridi kabisa au moto ogopa uvuguvugu.

1 Wakoritho 11:22 ‘ Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.

28 Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.

29 Maana alaye na kunywa, hula na kunywa hukumu ya nafsi yake, kwa kutokuupambanua ule mwili.

30 Kwa sababu hiyo wako wengi kwenu walio hawawezi na dhaifu, na watu kadha wa kadha wamelala.

31 Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu, tusingehukumiwa.”

Wala usijihusishe na maagizo yoyote ya Bwana Yesu kama kuhubiri, kubatiza, kubatizwa, kushiriki kwenye vikundi vya maombi ya ndani, kutawadha au kutawadhwa miguu n.k kama hujakusudia kuacha dhambi….sisemi kutubu peke yake!! Bali Nazungumzia KUACHA! Au kwa lugha ya kibiblia KUZAA MATUNDA YAPATANAYO NA TOBA YAKO! Kama Yohana alivyozungumza kwa uweza wa Roho.

Je! Unazaa hayo matunda leo?…Tangu usikie kuwa uasherati ni dhambi, umetubu mara ngapi dhambi hiyo lakini bado unaendelea kuifanya?..tangu usikie kuwa ulevi, utazamaji wa pornography, utukanaji, ulaji rushwa, usengenyaji, wizi, usagaji, ushoga, uchawi, ulawiti, ufanyaji masturbation ni dhambi lakini bado unaendelea kufanya?…Yohana aliwaita watu hao kuwa ni KIZAZI CHA NYOKA! Ingawa wao walijiona kuwa ni uzao wa Ibrahimu..Bwana Yesu aliwaita kuwa ni kizazi cha Nyoka ingawa walijitetea kwake kuwa ni uzao wa Ibrahimu…Wao walijihesabia haki lakini mbele za Mungu walionekana wamestahili kwenda jehanamu ya moto.

Ndugu unapoambiwa ukweli sio kwamba unahukumiwa..Yohana alipowaita wayahudi uzao wa nyoka sio kwamba aliwalaani au kuwahukumu…hapana alijua kabisa lile andiko linalosema (amlaaniye Israeli naye amelaaniwa) bali aliwaambia ukweli kwa lengo la wao kutubu kutubu sio kwa lengo la kuwashutumu au kuwahukumu….kwasababu ndivyo walivyokuwa wanaonekana mbele za Mungu…Kadhalika leo unapousikia ukweli usikimbilie kufikiria kuwa unahukumiwa …bali ufikirie kugeuza njia zako na kufurahia umeambiwa ukweli.

Biblia inatuonya tuzae matunda yapatanayo na Toba! Hilo ndio Neno la Leo.

Ikiwa hujampa Bwana Maisha yako, hujachelewa kabisa…ingawa umechelewa!! Hivi sasa bado unyakuo hujapita, lakini kipindi sio wakati mrefu kuanzia sasa utatokea, na mambo mabaya yataikumba dunia nzima… hivyo hapo ulipo tenga dakika chache, peke yako tubu dhambi zako zote na kisha baada ya kutubu dhamiria kuacha yote uliyoyatubia…unakuwa hufanyi tena hizo dhambi hata iweje..unaziacha kuanzia leo na kuendelea! shetani asikudanganye kuwa huwezi…unaweza! Hivyo kusudia kuzaa matunda yapatanayo na ulichokitubia..Na baada ya hapo nenda katafute ubatizo sahihi wa kuzamishwa katika maji mengi na kwa jina la BWANA YESU KRISTO (Matendo 2:38) kwaajili ya ondoleo la dhambi zako. Na Bwana mwenyewe atafanya yaliyosalia..kukupa wewe Roho Wake Mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi, na kuyaelewa maandiko, na kukulinda mpaka siku ya unyakuo itakapofika ili uwende naye mawinguni.

Bwana akubariki sana kwa kudhamiria kwako kumfuata Mungu. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

UZAO WA NYOKA NI UPI?

UBATIZO SAHIHI NI UPI?

TUNAMHITAJI SANA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUYAELEWA MAANDIKO.

SAMEHE KUTOKA NDANI YA MOYO WAKO

NITASHINDAJE HALI YA KUUMIZWA NA MANENO YA WATU!

Rudi Nyumbani

Print this post

NINAJUA MAWAZO NIKUWAZIAYO:

Shalom mpendwa wa Bwana, karibu katika kuyafakari maandiko matakatifu, Na leo tutajifunza somo ambalo tunaweza kuliona nyuma wa wana wa Israeli kukaa Babeli miaka 70, Ni kwanini Mungu aliamua kuweka bayana kuwa watakaa utumwani miaka ile 70 , na kuwaambia kuwa wakifika kule kama ni kuzaa waendelee kuzaa watoto, wawaoze binti zao, wapende bustani, wajenge, n.k….yaani kwa ufupi tunaona Mungu hakuwa na haja ya Dua zao za kuomba warudishwe katika nchi ya Israeli kwa wakati ule, utaona hakuwashauri hata waishi kama wapitaji kule Babeli watakapofika, badala yake aliwaambia waendelee na shughuli zao za kawaida kama tu vile walivyokuwa wanaishi Israeli.. Ukisoma Yeremia 29 yote utaliona hilo.

Lakini ukweli ni kwamba hata ingekuwa ni wewe leo hii yamekukuta mambo kama hayo , mtu kaja kuiua familia yako yote, na ukoo wako wote halafu anakuchukua mateka kukupeleka nchi ya mbali na kukwambia baada ya miaka 70 nitakurudisha nchini mwako, kwahiyo ukifika kule wewe jenga, panda , uishi maisha ya furaha, JE! Ni kweli utakuwa na Furaha hiyo nchi ya ugenini unayoiendea ambayo huijui hata ikoje, wala hujui utakutana na watu wa aina gani huko?, Ni wazi kuwa Mawazo yako kila siku yatakuwa nyumbani,katika majozi ukitumaini siku yoyote utarudi lakini sio baada ya miaka 70.

Hiyo ndio hali iliyowakuta wana wa Israeli, Walipomkosea Mungu, kupita kiasi, mpaka Mungu kukata tamaa juu yao, Mungu alimruhusu Nebukadneza mfalme wa Babeli, aje kuwachukua utumwani, Hivyo lile kundi la kwanza lililoenda utumwani, lilipokuwa kule lilitamani sana lirudi nyumbani Israeli, mpaka kukatokea manabii wa uongo wakawa wanawadanganya kwa kuwafariji kuwa watakaa kule miaka 2 tu kisha Mungu atawarudisha nchi yao tena, lakini Mungu alizungumza nao kwa kinywa cha Nabii Yeremia na kuwaambia kuwa watakaa utumwani kwa muda wa miaka 70 mizima haitapungua wala haitaongezeka, na hivyo wasijitaabishe hata kidogo kufikiri hiyo itakuwa ni habari ya hivi karibuni, kikubwa tu waendelee kuoa, wapande na wajenge, wawatikie na mema hao maadui zao, siku zote watakazokuwa huko. na ndiyo tunasoma iliyompelekea hata Nabii Yeremia kupitia matatizo makubwa namna ile hata kufikia hatua ya kutaka kuuliwa na wayahudi, kwa taarifa mbaya alizokuwa anazileta, kwasababu Iko wazi kuwa hakuna mtu anayependa kufia utumwani,

Ni habari za kukatisha tamaa sana kwa namna moja au nyingine,wakikumbuka utumwa ule wa Misri jinsi walivyoteswa ndio wanaokwenda kukutana nao tena, kufanyishwa kazi ngumu,kutumikishwa, kuchapwa.Lakini tunasoma pamoja na hayo kuna maneno Mungu alizungumza nao kwa kinywa cha Yeremia..Na maneno yenyewe ndio haya:

Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho”.

Wengi wetu tunasoma huu mstari lakini hatujui ni kwanini Mungu alizungumza maneno hayo…Maneno hayo Mungu aliwaambia wana wa Israeli wakati wanachukuliwa utumwani, Babeli.

Kwa kweli ni maneno ya faraja ambayo hata sisi mstari huu tunapenda kuutumia tunapopitia matatizo. Lakini habari yao inatufundisha nini?.Ndugu wana wa Israeli wanafananishwa na watoto wa Mungu sasa, yaani wale waliomwamini Kristo na baadaye wakarudi nyuma, wale walioujua ukweli wakaupinga..wale ambao Mungu amekuwa akiwaonya mara nyingi waache njia zao mbaya kwa mahubiri wanayosikia kila siku, lakini hawakusikia, mpaka imefikia hatua wamezama katika matatizo makubwa ambayo hawajui watatokaje, wengine wamezama kwenye uzinzi na sasa wamepata ukimwi, na leo hii kweli umetubu na kuacha uzinzi kabisa unataka Mungu akuponye, nataka nikuambie, kila mtu atavuna alichopanda, umemwomba Mungu akuponye lakini huoni mabadiliko yoyote, kesi yako wewe ni sawa na hii ya wana wa Israeli.

Hivyo nataka leo nikuambie kulingana na maandiko wala usihuzunike kujikuta umekaa katika hiyo hali kwa muda mrefu sana.. kama yalivyowakuta wana wa Israeli kwa makosa yao, ndivyo yalivyokukuta na wewe. Wao walikaa miaka 70 lakini siku moja walitoka….Na wewe usisahau Neno hili kuwa.. Mungu anayajua mawazo anayokuwazia wewe, ni mawazo ya amani wala sio mabaya kukupa tumaini siku zako za mwisho.

Umekuwa mwizi au mbakaji na sasa umefungwa, ni kweli umeshatubu kabisa kwa kudhamiria kuacha, umekuwa mtoto mzuri wa Mungu, huibi tena wala huna nia za Yule adui tena moyoni mwako…lakini unajiuliza ni kwanini mpaka sasa bado upo kifungoni Mungu hakutoi huko?, nataka nikuambie, kusamehewa ni kitu kingine, na kufutiwa adhabu ni jambo lingine, cha msingi ukijikuta katika hali kama hiyo, wewe kuwa tu mtulivu kuwa mtu mwema huko gerezani, mtumikie Mungu wako kwa uaminifu wote, ifanye kazi ya Mungu huko huko uliko, fanya shuhuli zote zinazokuja mbele yako, kana kwamba vile hutoki leo wala kesho, kwa kuwa Mungu anayajua mawazo anayokuwazia wewe ni kukupa tumaini katika siku zako za mwisho.

Sasa kumbuka wana wa Israeli walipofika Babeli japo walitubu na kulikuwa na watu wa Mungu wengi tu mfano wa Ezekieli, na akina Danieli, lakini hakuwaacha wateseke kama kwa utumwa ule wa Misri, aliwanyanyulia watu hodari na wenye hekima kama Danieli, Meshaki, Shedraki na Abednego, na kuwaweka katika jumba la kifalme mbele ya Nebukadreza, na kwa kupitia hao Mfalme aliwapa heshima wayahudi wote waliokuwa Babeli pamoja na Mungu wao , wamwabudu kwa uhuru na amani, waliishi kweli utumwani lakini hawakuwa kama watumwa muda wote waliokuwepo kule, ni kama vile Yusufu na ndugu zake, japo wote walikuwa utumwani lakini waliishi vizuri zaidi hata wa Wamisri waliokuwa kule ndivyo ilivyokuwa kwa wale waliokwenda Babeli.

Na baada ya ile miaka 70 ya adhabu kupita Mungu aliwafungulia mlango mkubwa wa kurudi katika nchi yao, lakini hawakurudi mikono mitupu walirudi pamoja na zawadi nyingi walizopewa kule Babeli, na hata wale waliosalia huko Babeli na kwenye nchi za mataifa kwa hiyari yao na wale ambao walikuwa wamesambaa duniani kote tunaona Mungu aliwanyanyulia tena watu kama Mordekai na Esta, kwenye viti vya enzi vya Uajemi, hawa nao waliwafanya wayahudi wapate heshima mara dufu duniani kote, waliogopeka na kuheshimiwa sana, japo walikuwa katika nchi za ugenini. Unaona jinsi mawazo ya Mungu yalivyokuwa mema juu yao mwisho wa siku, licha ya kutumikia adhabu lakini pia alipenyeza kusudi lake katika adhabu zao.

Hivyo na wewe ambaye ulimkosea Mungu na sasa umekutana na mabaya, mpaka sasa upo shimoni, na kwa bahati nzuri ulitubu dhambi zako, na uliziacha kabisa, ni wazi kuwa Mungu alikusamehe siku ile ile ulipogeuza Nia yako na njia zako.., lakini bado unaona hujatoka katika hilo shimo ulilozama, iadha la magonjwa, au vifungo, au shida, au taabu, nataka nikuambie usivunjike moyo, endelea kumtumikia Mungu katika hali uliyopo, haijalishi itakuchukua wiki, au mwezi au miaka mpaka kufunguliwa kabisa, lakini wewe endelea kumtumikia katika hali uliyopo na yeye atakubariki atakuongeza atakufundisha , atakuzidisha huko ulipo, na wakati wake ukifika atakufungua moja kwa moja..shetani asikudanganye kuwa Mungu amekuacha, au anakuchukia. Kutumikia adhabu haimaanishi kuwa Mungu hakupendi..

Isaya 44: 21 “Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi”.

Mithali 3:11 “Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kurudiwa naye”.

Na pia kama hujatubu dhambi zako ukihofia kwamba Mungu hatakusamehe…Hiyo ni sauti ya Ibilisi inazungumza na wewe..inayotaka kukupeleka ukajinyonge kama Yuda! Mungu anataka utubu akusamehe dhambi zako zote bure kwasababu yeye ni mwenye rehema…Anataka utubu ukiwa kwenye hayo hayo madeni ya kupindukia, anataka utubu katika hali hiyo hiyo ya magonjwa na vifungo, katika hali hiyo hiyo ya ushirikina na uchawi uliyopo, katika hali hiyo hiyo ya uuaji na utapeli uliyopo, katika hali hiyo hiyo ya ukahaba na usagaji.Tubu leo naye atakusamehe! Na kukubadilisha kwa maana anakuwazia mawazo mema sana huko mbeleni, kukupa wewe tumaini.

Mwisho kabisa nataka umalizie kwa kuyatafakari maneno haya:

Zaburi 103: 11 “Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.

12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

13 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo Bwana anavyowahurumia wamchao.

14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

15 Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo.

16 Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko! Na mahali pake hapatalijua tena.

17 Bali fadhili za Bwana zina wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana;

18 Maana, wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye”.

Ubarikiwe.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine na utakuwa umefanya kazi ya kuipelekea injili mbele.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

JE! UNA MASIKIO YANAYOSIKIA?

Yohana 2:13 ‘’Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

17 Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.

18 Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya? 19 Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.

20 Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?

21 Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.

22 Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.’’

Tukisoma kisa hichi ni rahisi kuwahukumu Makuhani na Mafarisayo na Wayahudi kuwa walikuwa watu wasiofikiri…watu wanaoona miujiza lakini hawaamini…ni kweli kuna mambo ya kulaumiwa lakini si yote…. hebu leo kwa sehemu tuchunguze kama ni kweli walikuwa hawafikiri wakati wote..

Jaribu kuchukua mfano wewe ni mtumishi wa Serikali, labda unatumika kwenye shirika fulani la Umma..halafu siku moja anatokea mtu usiyemjua anaingia mahali mnapofanyia kazi na kuanza kuvuruga vuruga nyaraka na hati muhimu..huku anawapazia sauti na kuwaambia…msigeuze serikali ya Raisi wangu kuwa pango la mafisadi….na mnapojaribu kumzuia na kumwuliza yeye ni nani na nani kamtuma kufanya vile, anawajibu…jiuzuluni wote na mwachie ngazi leo na baada ya siku tatu nitalinyanyua hili shirika upya.

Unafikiri ni kitu gani..kitagonga kwenye akili…Moja kwa moja aidha utajua huyo mtu karukwa na akili..Na pili jambo litakalofuata ni kutafuta njia ya kwenda kumshitaki haraka…Kwasababu anakuja kuharibu kazi na kuzungumza vitu visivyoeleweka…eti atalinyanyua shirika ndani ya siku tatu!!…Shirika hili mpaka kulifikisha hapa tumetumia miaka Zaidi ya 20 wewe unataka kulinyanyua ndani ya siku tatu!..

Hebu fikiria huyo mtu hata akienda mahakamani atashindaje kesi?..kwasababu amesikiwa na watu wote kwa kinywa chake akisema atalinyanyua shirika kwa siku tatu.

Na ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu mahali Fulani, alipowakuta wayahudi wanafanya biashara kule Hekaluni,aliwaambia wasigeuze nyumba ya Baba yake kuwa pango la wanyang’anyi lakini walipomuhoji kwa ishara gani unafanya haya? Akawaambia libomoeni hekalu hili na ndani ya siku tatu nitalisimamisha.

Sasa wayahudi walidhani wamemsikia vizuri na kumwelewa…kumbe hawajamwelewa ingawa wamemsikia,..ndio maana Neno linasema ‘kusikia mtasikia lakini hamtaelewa..Kutazama mtatazama lakini hamtaona (Mathayo 13:14)’…Walidhani hekalu litakalobomolewa na kusimamishwa ndani ya siku tatu ni hilo la mawe wanaloliona mbele yao..kumbe kulikuwa na hekalu lingine ambalo lilikuwa ni mwili wa Bwana Yesu.

Na waliendelea na huo upofu mpaka siku ya mwisho, pale walipomsulibisha

Walisema maneno haya:

Mathayo 27:40 ‘’Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako; ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, shuka msalabani’’.

Lakini tunaona waliokuja kumwelewa ni wanafanzi wake tu! Tena dakika za mwisho, Wale waliokuwa wanatembea naye kila siku. Ndio waliopewa neema ya kumwelewa Bwana Yesu alikuwa anamaanisha nini katika maneno yake. Sio kila mtu tu alikuwa anamwelewa Bwana Yesu.

Ndugu huo upofu mpaka leo upo! Unaendelea kwa watu wengi wasio wanafunzi wa Yesu Kristo..Bwana hana wanafunzi 12..alianza na wanafunzi 12, lakini sasa anao wanafunzi wengi…Na hao ndio anaowafunua macho ya kuyaelewa maneno yake…wengine walio nje maneno ya Yesu yatakuwa ni mafumbo kwao…wataona wanamwelewa sana Bwana Yesu lakini kumbe hawamwelewi..

Watadhani kwasababu Bwana aliyageuza maji kuwa divai basi alihalalisha unywaji wa pombe, lakini hawaelewi kuwa Pia kitendo cha Bwana kula na makahaba na wenye dhambi lengo lake halikuwa kuhalalalisha ukahaba wao wala dhambi zao…Alifanya vile ili kutafuta njia ya kuwavuta watubu kwa upendo wake….Na watu walipomwita kuwa mlevi haikumaanisha kuwa yeye kweli ni mlevi..wewe unaweza kuitwa mlevi na maadui zako lakini isiwe ni mlevi kweli…kadhalika walipomwita yeye ni mlafi haikumaanisha Bwana Yesu alikuwa ni mlafi kweli…

Alipomwita Herode Mbweha!..hakumaanisha kumtukana!!…ingekuwa ndio hivyo, basi yeye mwenyewe amejitukana sana…alipokuwa anajiita mwanakondoo?..au anapowafananisha watu wake na kondoo..kwa wale wafugaji wanaelewa ni afadhali mtu akuite mbwa kuliko kondoo.

Kadhalika aliposema mkawabatize watu wote kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu hakumaanisha hivyo vyeo bali alimaanisha ni jina moja ambalo ndio la Baba, na ndio hilo hilo la Mwana na ndio hilo hilo la Roho Mtakatifu na hilo sio lingine Zaidi ya Jina la YESU (Matendo 2:38).

Na aliposema…’’aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele’’..hakumaanisha tukamkamate na kumchinjwa na kunywa damu yake kama simba…bali alimaanisha kuula katika roho na kuinywa damu yake katika roho..Na chakula cha Roho zetu ni Maneno tunayosikia…Yakiwa ni Maneno ya Mungu, basi ni chakula bora cha uzima wa milele, na yakiwa maneno ya yule mwovu basi ni chakula kisichofaa cha mauti.

Kwahiyo Biblia inatufundisha tuwe na masikio yanayosikia, na macho yanayoona..ili kwamba tunaposoma Biblia tuielewe…Na hayo tutayapata kwa kuwa wanafunzi wa Yesu tu!..kwasababu hao ndio Bwana alikuwa anawapa kuelewa maneno yake…

Na vigezo vya kuwa mwanafunzi ni hivi..

Luka 14:25 ‘’Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,

26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

27 MTU YE YOTE ASIYEUCHUKUA MSALABA WAKE NA KUJA NYUMA YANGU, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,

30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.

31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?

32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.

33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu’’.

Je! Umeuchukua msalaba wako?..je! umewachukia ndugu zako, baba yako na mama yako?…kuchukia kunakozungumziwa hapo sio kuchukia mtu kwa hasira au chuki ya moyo…hapana! Bali ni kitendo cha kuyakataa na kuyachukia maamuzi ya wazazi wako au ndugu zako yanayopingana na mapenzi ya Mungu kwako, na kuamua kuyafuata yale mapenzi ya Mungu tu!..Huko ndio kuwachukia kunakozungumziwa hapo juu!!…kama baba yako ni mlevi na anakutaka na wewe uwe kama yeye…hapo unayachukia hayo maamuzi na kusema hapana!..kama ni msengenyaji hivyo hivyo..kama ni mlarushwa na wewe anataka uwe kama yeye unasema No! kama ni mchawi au Mwenda kwa waganga..na anataka kukufundisha na wewe uwe kama yeye..hapo unasema hapana! N.k. 

Na pia ili uwe mwanafunzi biblia inasema unapiga gharama!! Ukristo sio jambo la kujaribu na kutoka! Biblia inasema utachekwa….Ukiamua kumfuata Bwana Yesu, hesabu kuwa kuna kuonekana mpumbavu, kuonekana mshamba…wakati mwingine kuonekana umerukwa na akili…Na pia ukristo sio mteremko muda wote…piga hesabu kuwa kuna wakati Bwana anaweza kukuacha kwa kipindi Fulani kirefu pasipo kuzungumza na wewe kwa njia unayotaka! Je! Utaendelea kuwa naye!…utakapopitia shida, dhiki na wakati mwingine misiba utamwacha?

Pia piga gharama! Je asipokupa vile vitu unavyohitaji! Utaendelea kuwa naye?.

Na mwisho anasema ‘mtu yeyote asiyeacha vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu’..Kuacha vyote ulivyonavyo ni mfano wa wakina Petro…waliacha vyote walivyo navyo na kumfuata Bwana…Kuacha vyote ulivyo navyo sio lazima kwenda kuuza mali zako au hazina yako…bali ni kuishi kana kwamba hivyo vitu sio vya kwako…kiasi kwamba hata ikitokea kimepotea hakipo kwenye akili yako…umeshakiacha siku nyingi…akili yako imetawaliwa na kutenda mapenzi ya Mungu na kuyaishi…hakina chochote katika moyo wako…kiwepo au kisiwepo vyote kwako ni sawa sawa tu.

Ukishapiga hizo gharama, na kujitwika msalaba wako, biblia inasema umekuwa mwanafunzi wake…ambao wamepewa Neema ya kuzijua siri za ufalme wa mbinguni…

Hivyo kama hujampa Kristo Yesu Maisha yako, ni vizuri ukafanya hivyo leo… Na ili uwe mwanafunzi wake piga gharama za kumfuata…na Bwana akusaidie katika hilo.

Mungu akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

JIANGALIENI BASI JINSI MSIKIAVYO;

SAUTI AU NGURUMO?

IELEWE SAUTI YA MUNGU.

INJILI KULINGANA NA TEKNOLOJIA

Mungu akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

NINI MAANA YA KUISHI KWA KUUKOMBOA WAKATI?.

Shalom mwana wa Mungu, ikiwa Mungu amekupa neema ya kuiona siku hii ya leo, basi usipuuze kujifunza ni kitu gani anataka kutoka kwako leo?, Kukutana na ujumbe huu si kwa bahati mbaya bali Mungu anakusudi na wewe juu ya wakati aliokupa hapa duniani.

Tukisoma Waefeso 5:15-18 biblia inatuambia hivi.. “15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

16 MKIUKOMBOA WAKATI kwa maana zamani hizi ni za uovu.

17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;”.

Nataka leo tujifunze nini maana ya kuukomboa wakati kimaandiko. Tunajua tafsiri rahisi ya hili neno kuukomboa wakati ni “kuutumia muda vizuri”, tulipokuwa shuleni moja ya vitu ambavyo vilikuwa vinawachukiza sana walimu,ni pale walipokuwa wanaona wanafunzi wanautumia muda wao vibaya (hawaukomboi wakati), Hususani pale mwalimu anapotazama muda aliobakiwa nao mbeleni jinsi ulivyo mchache, topics bado ni nyingi za kusoma, halafu mwanafunzi, anaruka ruka hajisomei, anapiga kelele darasani, hazingatii masomo, haudhurii darasani, inawatia sana hasira waalimu pamoja na wazazi. Vivyo hivyo na katika mambo mengine.

Lakini pia katika upande wa maandiko, tunafundishwa tuukomboe wakati, kwasababu biblia imeweka wazi kabisa kuwa zamani hizi ni za UOVU, na tunauokomboa wakati kwa namna gani? Biblia inasema ni kwa kutaka kufahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Mungu kwetu.Huko ndiko kuukomboa wakati kuliko na maana mbele za Mungu.

Ndugu huu ulimwengu una mambo mengi na mahangaiko mengi, Ni kweli tunafahamu kwa sehemu moja au nyingine hatuwezi kuepuka mihangaiko kama ipo lakini tunaonywa tuishi kama watu wenye hekima, na sio wajinga, tukijua kuwa sisi ni wapitaji tu hapa duniani, na siku zetu zinakimbia kwa kasi sana, biblia inasema sisi ni kama MVUKE uonekanao kwa kitambo kisha kutoweka (Yakobo 4:14), Mvuke sio kama moshi ambao unaweza walau ukauona ukipaa mawinguni, mvuke wenyewe hata kwenye dari haufiki umeshapotea, ndivyo maisha yetu yalivyo. Biblia inasema na mwanadamu ni kama maua ambayo hayo hayana maisha marefu,(Zaburi 103:15 ”Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo).

Hata kama tutaishi miaka 60 tu au miaka 120 bado siku zetu zitabakia kuwa ni chache sana. Hivyo swali tunalopaswa kujiuliza tukifa leo huko tunapokwenda ni kitu gani cha maana kitaoneka tumekifanya hapa duniani?. Kwasababu kule hatutaulizwa tulikuwa na majumba mangapi, au magari mangapi, au biashara ngapi, au watoto wangapi,wala hatutaulizwa tulikuwa maskini kiasi gani LA! Tutaulizwa ni kitu gani tumeongeza katika ufalme wa mbinguni..Tukiliweka hilo akilini basi itatusaidia sana kuishi kwa uangalifu.

Tunamwona Bwana wetu Yesu alijua nini maana ya kuukomboa wakati, angalia alichowaambia wanafunzi wake..Yohana 9:4 ”Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi…”

Unaona Japo alikuwa ni Mungu katika mwili alijua nini maana ya muda, kuwa kuna kipindi kinachoitwa usiku (KIFO) ambacho mtu yoyote atatamani kufanya kazi ya Mungu asiweze, Na tunamwona Bwana wetu japo aliishi miaka 33 tu lakini kazi aliyoifanya ina matunda makubwa mpaka sasa tunayafaidi. Hiyo ni kwasababu aliukomboa muda wake vizuri hapa duniani ipasavyo. Wakati mwingine hakuwa na muda hata wa kula. Alipoletewa chakula.

NA SISI JE! TUNAWEZAJE KUUMBOA WAKATI WETU?

Tujijengee utaratibu wa kila siku mpya inapoanza tumwombe Mungu atusaidie tufanya kitu ambacho kitakuwa na manufaa katika ufalme wa mbinguni na katika maisha yetu ya rohoni… tuzitazame siku zetu ikiwa inaweza kupita siku nzima, wiki, mwezi bila kuona kitu chochote cha maana tulichokifanya kwa ajili ya maisha yetu ya rohoni au kwa ajili ya ufalme wa Mungu, basi tujue hatuukomboi muda haijalishi tunatengeneza mabilioni pa pesa kiasi gani kwa siku. Ndugu huu ndio wakati wa kuanza kuitengeneza njia yako upya mbele za Mungu, kabla ya siku ile kufika.

Muda ambao unautumia kuchati kwenye magroup ya whatsapp, au kusoma habari zisizokuwa na maana mitandaoni, komboa wakati kwa kutumia muda huo kujifunza Neno la Mungu, au kusoma mahubiri au mafundisho ya Neno la Mungu. hayo ndio mapenzi ya Mungu kwako, au tumia muda huo kukaa katika utulivu kumsifu na kumwimbia Mungu wako..peke yako au pamoja na wakristo wengine..

Tukiwa makazini kwetu, tumwombe Mungu atusaidie, sio wakati wote, tutakuwa buzy na shughuli, au kuongea na wafanyakazi wenzetu mambo ya kikazi, tutumie muda wetu wakati mwingine kuwashirikisha habari za Yesu, huku tukiwaelekeza katika vyanzo vizuri vya kupata habari za Mungu, kwa kufanya hivyo pia tutakuwa tumeukomboa wakati na siku yetu kuwa na maana mbele za Mungu.

Muda ambao tumekaa hatuna shughuli yoyote, tunaweza tumia muda huo kwenda kuomba, hata kama hatutakuwa na mahitaji wakati huo mbele za Mungu, lakini pia tumeagizwa kuwaombea wengine, hivyo tumia muda huo kuwaombea watu wengine, kuna ndugu zako, rafiki zako, jamaa zako, taifa lako, kanisa n.k..Kwa kufanya hivyo utakuwa umeukomboa wakati. Na pia maombi yanasaidia kuepukana na majaribu.

Kama biblia inavyosema Mungu utusaidie kuzihesabu siku zetu tupate mioyo ya hekima (Zab 90:12). Hivyo na sisi tupate leo hekima ya kujua kuwa muda unakwenda sana, na jukumu bado ni kubwa mbele yetu na mtihani ulio mbele yetu bado hatujauvuka. Basi tusiwe kama wajinga, tukaze mwendo, tuanze kutumia muda wetu sasa kwa vitendo kujifunza kwa bidii Neno la Mungu kuliko jana, tuombe, na tuifanye kazi yake pia kana kwamba hatuna tena mwaka mbele. Maana usiku waja asioweza mtu kuitenda kazi. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

MIISHO YA ZAMANI.

SEHEMU YA MAANDIKO ILIYOFICHWA.

JINSI MWISHO ULIVYOKARIBIA.

MWEZI NI ISHARA GANI KWETU?

Rudi Nyumbani

Print this post

CHANZO CHA MAMBO.

Jina kuu la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe. karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa iongozayo njia zetu. Biblia inasema “Mjue sana Mungu ili uwe na Amani (Ayubu 22:21)”..Siku zote ukijua sababu ya jambo Fulani basi unapata amani. Amani inakuja baada ya kujua sababu ya jambo Fulani.

Leo tutajifunza juu ya vyanzo vya matatizo, na namna ya kuyatatua. Kama tunavyojua wengi wetu vyanzo vya matatizo mengi ni shetani..huo ni ukweli usiopingika. Lakini je! Shetani analetaje matatizo?.

Tukijifunza Mfano wa Ayubu, tunaweza kupata majibu baadhi, tunaona shetani alimshambulia Ayubu baada ya kupata kibali maalumu kutoka kwa Mungu, hiyo ikifunua kwamba shetani hawezi kumgusa mtu yeyote wa Mungu pasipo ruhusa yeyote kwa Mungu..

Hivyo Mungu anaporuhusu mtu ajaribiwe…anachokifanya ni kutoa ulinzi wake juu ya Yule mtu, na akishatoa ulinzi wake maana yake shetani anapata nafasi ya kumwingia. Hivyo anamshambulia.

Na shetani huwa ana njia kuu mbili za kuwashambulia watu.

1) Anatumia mapepo…Katika njia hii mtu atajikuta tu ameingia matatizoni pasipo kujua chanzo ni nini. Kumbe ni majeshi ya mapepo wabaya yamemvamia.

2) Na njia ya pili anatumia watu..(Na watu atakaowatumia ni aidha watumishi wake wa uongo wanaovaa mavazi ya kondoo lakini ndani ni mbwa-mwitu wakali…au atatumia wachawi na waganga)….atatumia watumishi wa uongo kuwajaribu wale wanaomjua Mungu, na atatumia wachawi na waganga kuwajaribu wale wasiomjua Mungu…au wakati mwingine atatumia vyote viwili kuwajaribu wale watu wanaomjua Mungu.

Sasa tukirudi kwenye mfano wa Ayubu..baada ya ulinzi wa kiMungu kuondoka juu yake…shetani alimletea majaribu wengi… Kama haikuwa ni kazi ya mapepo moja kwa moja basi kuna uwezekano mkubwa sana shetani alitumia watu Fulani kumfanyia Ayubu yale mambo…Alichofanya shetani baada ya kuona ukingo wa kiMungu umeondoka juu ya Ayubu ni pengine aliwatupia roho ya wivu watu baadhi waliokuwa wanamzunguka…na ile roho ilipowaingia pengine ikawasukuma kumwendea hata kwa waganga… labda walikwenda kwa mganga fulani maarufu kwa kipindi hicho mwenye nguvu, wakaenda na picha yake na za watoto wake..na nyayo zake labda..Na wakiwa kule wakaona wanafanikiwa kumwona kwenye kioo chao cha kichawi, na pengine huyo mganga akafanya mambo yake na kutuma kimbunga cha kichawi juu ya watoto wake wakiwa karamuni, na kwasababu ulinzi wa kiMungu umeondoka juu ya Ayubu jambo lile likafanikiwa na Kuwaua watoto wake wote. Na magonjwa ni hivyo hivyo ni kikundi Fulani cha maadui zake Ayubu kilihusika kumletea yale magonjwa.

Sasa labda baada ya tukio hilo pengine Ayubu aliona tabia Fulani za watu wanaomzunguka kufurahi..na pengine walisema vimaneno Fulani kuonyesha kuwa wao ndio walifanya vile. Sasa kwa jicho la haraka haraka kama Ayubu angekuwa sio mtu wa rohoni…angesema maadui zake wamemfanyia visa..Lakini Bwana alimpa jicho la Mbali kujua mwanzo wa Matatizo yake hayakuwa ni wale watu..bali alijua yalikuwa ni Mungu mwenyewe…kutoa ulinzi juu yake. Ndio maana aliishia kusema “Bwana alitoa na Bwana alitwaa, jina lake libarikiwe”…Alijua maisha yake ni makamilifu isipokuwa ni Mungu tu katoa ulinzi juu yake kwa makusudi Fulani. Angalia jinsi alivyouamini uhusiano wake na Mungu, kiasi cha kwamba hakuweza kuyumbishwa ni kitu chochote, na sisi je! tunaweza tukawa hivyo?.

Na mambo hayo hayo yanaendelea leo hii, watu wanatumiwa na shetani kukuharibu, pengine ni wachawi au waganga…na kushindwa kuelewa chanzo cha mambo yote ni nini?…chanzo cha mambo yote sio watu kukuonea wivu, au wachawi kukuchukia hapana!..chanzo cha matatizo yote ni Ulinzi wa kiMungu kuondoka juu yako..Usianze kupambana na watu wanaokuchukia, anza kutafuta mzizi wa tatizo ni wapi..kama Ayubu.

Ayubu alijua chanzo cha matatizo yake, kuwa ni Bwana ndiye kayaruhusu hayo lakini njia zake ni kamilifu…alijua sio dhambi ndani yake iliyosababisha ulinzi wa kiMungu uondoke juu yake.

Kadhalika na sasa tunapaswa tujitathmini, kama kuna jambo Fulani limetokea ambalo halipo sawa…chanzo chake ni nini?..Je! ni kama Ayubu? (Njia zetu ni kamilifu isipokuwa ni Bwana anatujaribu tu) au ni kwasababu ya dhambi zetu, kwasababu kitu pekee kinachotoa ulinzi wa kiMungu juu ya mtu ni dhambi…

Ukiwa mwasherati magonjwa yatakusumbua na wachawi watakusumbua sana, mapepo yatakusumbua sana hakuna namna utaweza kuwashinda, hata uombewe kiasi gani hakuna namna utaweza kuchomoka mikononi mwao…ukiwa mtazamaji wa pornography na mfanyaji wa masturbation ni hivyo hivyo…ukiwa ni mzinzi, ni shoga ni msagaji ni hivyo hivyo, watakusumbua na hakuna namna utaweza kuwashinda…Usidanganywe kuwa kuna mchungaji yeyote duniani mwenye uwezo wa kukuombea wachawi au mapepo yasikufikie wala kukudhuru, wala usidanganyike kuwa kuna maji yoyote au mafuta yoyote ya upako yanayowazuia wachawi wasiweze kufika nyumbani kwako…Usidanganyike kabisa ndugu…

Kitu pekee kinachoweza kufukuza na kuzishinda nguvu za giza juu ya maisha yako ni MAISHA YA UTAKATIFU katika Kristo Yesu, Uhusiano wako na Mungu ni wa kiwango gani, hicho tu! Wala hakuna kingine….Maisha unayoishi ndio yanayoamua ulinzi wa kiMungu uwe juu yako au uondoke.

Fanya uamuzi sahihi leo, usitazame wachawi, wala waganga, kama ndio chanzo cha matatizo yako…wala usiende kutafuta suluhisho kwa kuombewa, wala kupakwa mafuta..Suluhisho lipo kwako ambalo ndio chanzo cha mambo yote…suluhisho ni KUBADILIKA na kuishi maisha ya utakatifu, ambayo hayo yanakuja kwa kutubu kwanza dhambi zako zote, na kudhamiria kuziacha kabisa kuanzia sasa na kuendelea na kwenda kubatizwa na kisha kupokea Kipawa cha Roho Mtakatifu ambaye atakusaidia kushinda dhambi.

Ukifanya hivyo, ulinzi wa kiMungu utakuwa juu yako, haihitaji wewe kwenda kuombewa wala kupakwa mafuta, wala kuwaogopa wachawi…Utaishi kwa Amani sana, na wala hakuna chochote kitakachokugusa. Kwasababu nguvu iliyopo ndani yako ni kubwa kuliko ya kwao..Bwana Yesu alisema..

Luka 6.17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;…… watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;…”

Bwana akubariki sana. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

JINSI WATU WANAVYOZAMA KATIKA USHIRIKINA NA UCHAWI.

HUDUMA YA (ELIFAZI, BILDADI, NA SOFARI).

JE! MUNGU ANASABABISHA AJALI?

Rudi Nyumbani

Print this post

WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA;

Jina Bwana wetuYesu libarikiwe. Ni siku nyingine tena Bwana ametupa neema kuiona hivyo nakukaribisha ndugu popote pale ulipo tushiriki pamoja Baraka Bwana alizotuandalia leo.

Tukisoma Zekaria 12:9-14, inasema. 

“ 9 Hata itakuwa siku hiyo, ya kwamba nitatafuta kuwaangamiza mataifa yote watakaokuja kupigana na Yerusalemu. 

10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.

11 Siku hiyo kutakuwa na maombolezo makuu huko Yerusalemu, kama maombolezo ya Hadadrimoni katika bonde la Megido.

12 Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;

13 jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.

14 Jamaa zote zilizosalia, kila jamaa peke yake, na wake zao peke yao”.

Watu wanaozungumziwa hapo ni wayahudi (yaani Waisraeli) , Embu leo jiulize tu Israeli ni Taifa dogo sana kama mkoa wa njombe, ni taifa ambalo huwezi hata ukaenda na kukutana na vitu vya kuvutia huko au vya kushangaza kama mataifa mengine makubwa, lakini ni kwanini leo hii imekuwa ni JICHO LA DUNIA?. Wapo mbali na Mungu lakini ni watu wenye akili na wenye mafanikio makubwa duniani, jiulize siku wakiwa karibu na Mungu itakuwaje?

Hayo maandiko hapo juu ni lazima yatime, utafika wakati biblia inasema Roho ya neema itaachiliwa juu yao na watamwamini huyu Yesu ambaye sasa hawamwamini, Siku hiyo Watalia na kuomboleza baada ya kugundua makosa yao kuwa Yule waliyemsulibisha na KUMCHOMA MKUKI miaka 2000 iliyopita kumbe ndiye Masiya waliokuwa wanamsubiria kwa miaka mingi..Ile roho ya ufarisayo na usadukayo itaondoka juu yao.

Kama vile biblia inavyotabiri kutakuwa na maombolezo makubwa sana huko Yerusalemu wakitubu makosa yao.

Sasa hicho ndio kile kipindi ambacho mtume Paulo alikiandika katika

 Warumi 11:25 “Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili [anasema na sisi watu wa mataifa]; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.

26 Hivyo Israeli wote wataokoka; kama ilivyoandikwa, Mwokozi atakuja kutoka Sayuni; Atamtenga Yakobo na maasia yake.

27 Na hili ndilo agano langu nao, Nitakapowaondolea dhambi zao”.

Unaona hapo unabii huo utatimia katika hiyo siku?, Huo wakati wa Israeli kurudiwa na kutengwa na maovu yao upo karibuni sana, na utakapoanza tu basi ujue utimilifu wetu sisi mataifa utakuwa umeshawasili yaani kwa lugha nyingine neema kwetu itakuwa imeshaondoka na kurudi tena Israeli, na hiyo itaambatana na tendo KUU la UNYAKUO.

Sasa wayahudi ambao leo hii utawaona wanalia usiku na mchana pale kwenye ule Ukuta wa maombolezo (wailing wall). wakimwomba Mungu wa Ibrahimu baba yao aje kuwaokoa na maadui zao na kuleta utawala wa masihi duniani, ipo siku hayo maombolezo yatakoma, na ndipo Mungu atawarudia kwa kuwafumbua macho na kumwona YESU, Kumbuka Mungu aliwapofusha kwa makusudi kabisa wasimwamini Kristo ili sisi mataifa tuipate neema vinginevyo huyu Yesu wa thamani ambaye leo hii tunaifurahia neema yake, tungemsikilizia tu kwa wayahudi, sisi tungeendelea kuwa waabudu miti,vinyago, na wachawi. Na hata hivyo dunia ungekuta imeshakwisha siku nyingi, wakati ule ule tu Yesu aliokuwa ndio ungepaswa uwe ni wakati wa wao kurejeshewa ufalme wa dunia na Yesu.

Unakumbuka mitume walimuuliza Yesu baada ya kufufuka je! Huu ndio wakati wa kuwarudishia Israeli ufalme? Yesu akawaambia, sio kazi yenu kujua nyakati wala majira.(Matendo 1:6), Hii ikiwa na maana kuna wakati utafika watarudishiwa na huyu huyu masihi Yesu Kristo.

Hivyo huo wakati unafika, Pale Mungu atakaposimama tena upande wa Israeli na kuwashindania kwa nguvu nyingi kama alivyokuwa anafanya zamani, pale mataifa yote ulimwenguni yatakapoungana ili yaje kujaribu kuisambaratisha Israeli katika ile vita ya Harmagedoni ndipo hapo Kristo atakawapigania toka juu kwa nguvu na uweza mwingi…damu nyingi itamwagika sana, maadui wote wa Israeli watakufa kama kuku waliochinjwa wakaachwa, wakati huo Bwana atakapolipigania Taifa lake…. Tunalisoma hilo katika..

Zekaria 14:1 “Tazama, siku moja ya Bwana inakuja, ambayo mateka yatagawanyika kati yako.

2 Kwa maana nitawakusanya mataifa yote walete vita juu ya Yerusalemu; na huo mji utapigwa, nazo nyumba zitatekwa, nao wanawake watatendwa jeuri; na nusu ya watu wa mji watatoka kwenda utumwani; ila mabaki ya watu wa mji hawatakatiliwa mbali.

3 Hapo ndipo ATAKAPOTOKEA BWANA, naye atapigana na mataifa hayo, kama vile alipopigana zamani siku ya vita.

4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.

5 Nanyi mtakimbia kwa njia ya bonde la milima yangu; kwa maana bonde lile la milima litaenea hata Aseli; naam, mtakimbia, kama vile mlivyokimbia mbele ya tetemeko la nchi, siku zaUzia, mfalme wa Yuda; na Bwana, Mungu wangu, atakuja, na watakatifu wote pamoja naye.

Kwahiyo tusifurahie tu kuona leo hii Israeli inazidi kufanikiwa lakini badala yake tuogope na tujiulize maswali je! Wewe tumejiandaaje sasa?, neema ndio hivyo inaondoka kwetu, tazama hata hali ya ukristo sasa hivi duniani sio kama ile ya zamani, tazama mataifa ya ulaya ambayo ndio yalikuwa ya kwanza kutuleta injili lakini sasa jinsi yanavyozidi kujitenga na ukristo kwa kasi, hiyo ni dalili kuwa neema inaondoka kwa mataifa, inakimbilia Israeli..Itafika wakati mataifa yote yataenda kinyume na taifa teule la Mungu hata hili taifa letu vilevile litaungana na yule mpinga-Kristo ili kuiangamiza Israeli.

Zekaria 12: 3 “Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata jeraha nyingi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake”.

Ndugu wakati huo sio wa kuutamani kwanini tusubirie mpaka hayo yote yatukute kwa ghafla wakati tunayo nafasi sasa? Neema inamalizikia AFRIKA, usiiche ikupite, chukua hatua ya kumwamini Yesu ayasafishe maisha yako, ili uwe tayari kwa unyakuo ulio karibuni kutokea.

Bwana akubariki. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

MAMBO YATAKAYOTOKEA ISRAELI SIKU ZA HIVI KARIBUNI.

WAISRAELI WENGI SANA WANARUDI KWAO SASA.

MZEITUNI HALISI UTAKAPOPACHIKWA.

“WOKOVU WETU U KARIBU NASI KULIKO TULIPOANZA KUAMINI”

UNYAKUO.

Rudi Nyumbani

Print this post

WATAMTAZAMA YEYE AMBAYE WALIMCHOMA;

Jina Bwana wetu Yesu libarikiwe. Ni siku nyingine tena Bwana ametupa neema kuiona hivyo nakukaribisha ndugu popote pale ulipo tushiriki pamoja Baraka Bwana alizotuandalia leo.

Bwana akubariki.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Print this post

MAANDALIZI YA UJENZI WA HEKALU LA TATU YAPO TAYARI.

Jicho la Mungu kidogo kidogo linaanza kuondoka kwa mataifa na kurejea Israeli. Wakati wowote Hekalu la tatu nitaanza kujengwa pale Yerusalemu kwani maandalizi yote yapo tayari.Kilichobaki ni amri tu kutolewa, Na kumbuka ujenzi wa sasa hivi sio kama ule wa zamani, haitachukua tena miaka 7 au 20 kukamilika, itakuwa ni kitendo cha wiki kadhaa tu, au miezi kadhaa tu, kila kitu kitakuwa kimeshakamilika. Na tunafahamu likishakamilika tu, Mungu ataliweka JINA LAKE HAPO kama alivyomwahidia mtumishi wake Daudi na Sulemani zamani (1Wafalme 9:3), na mahali popote jina la Mungu lilipo basi WIVU wake utakuwepo pia.

Na biblia inatuambia mpinga-kristo akishaliona hilo ataondoka moja kwa moja na kwenda kutaka kuketi pale kama Mungu kupatia unajisi ili Mungu atiwe wivu alete uharibifu duniani kote ndio maana kimaandiko huyu mpinga-kristo anajulikana kama (CHUKIZO LA UHARIBIFU), Yeye ndio atakayeleta dhiki kuu, wakati huo unyakuo wa kanisa utakuwa umeshapita.

2Wathesalonike 2:3 “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu;

4 yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.

5 Je! Hamkumbuki ya kuwa wakati nilipokuwapo pamoja nanyi naliwaambieni hayo?

6 Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake.

7 Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.

Unadhani muda tuliobakiwa nao sasa ni mwingi?.Uzuri ni kwamba hatuna haja ya kuelezeana kila kitu kwani mambo yote yapo wazi kwenye TV na Internet siku hizo zitakapofika.. Huu ni wakati wa kujifunga mkanda UNYAKUO upo mbioni.

Maran Atha.jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Zinazoendana:

UFUNUO: Mlango wa 11

UNYAKUO. 

CHUKIZO LA UHARIBIFU NI NINI?

MPINGA-KRISTO AU YULE MWANA WA KUASI NI NANI?

Rudi Nyumbani

Print this post