Category Archive maswali na majibu

Je! habari ya muda aliotawala Mfalme Yekonia inajichanganya? (2Wafalme 24:8 na 2Nyakati 36:9).

Jibu: Kabla ya ufafanuzi tuisome mistari hiyo..

2Wafalme 24:8 “Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala MIEZI MITATU katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani wa Yerusalemu”.

Tusome tena,

2Nyakati 36:9 “Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu MIEZI MITATU NA SIKU KUMI; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana”.

Hapa tunaona mwandishi wa kitabu cha Wafalme anataja miezi aliyotawala Yekonia ni mitatu (3) lakini mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati ameongeza siku kadhaa mbele yake (miezi 3 na siku 10).

Swali, je! Ni yupi yupo sahihi na yupi hayupo sahihi?.. au je biblia inajichanganya?. Au ina makosa katika uandishi?

Jibu ni la! Biblia haijichanganyi mahali popote na haijawahi kujichanganya, na wala haina makosa mahali popote kwasababu endapo ikijichanganya au ikikosewa, basi yote itakuwa ni uongo na sio Neno la Mungu, lakini tunaona maneno yaliyoandikwa kule ni nguvu ya Mungu, na ni uweza wa Mungu, na tena ni Roho, na hayana makosa…

Sasa tukirudi katika hiyo habari ya muda aliotawala Yekonia, je! Mwandishi yupi yupo sahihi?.

Jibu ni kwamba wote wapo sahihi, hakuna aliyekosea.

Mtu akikwambia nitakuja kukutembelea mwezi wa 3 halafu akaja mwezi huo wa 3 tarehe 10 je atakuwa amekudanganya?..bila shaka atakuwa hajakudanganya kwasababu hiyo tarehe ipo ndani ya huo mwezi wa tatu (haijatoka ndani ya huo mwezi wa 3).. hata kama atakuja tarehe 20 au 21 au 25 atakuwa bado hajakudanganya kwasababu bado tarehe hizo zipo ndani ya mwezi wa huo wa tatu.

Hali kadhalika Mwandishi wa kitabu cha Samweli kasema tu “Yekonia katawala miezi 3” ingawa alikuwa anajua na siku alizotawala lakini kapenda tu kufupisha, hajapenda kutaja na siku wala masaa wala dakika wala sekunde lakini kafupisha tu! Miezi 3.

Lakini mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati kapenda kutaja Miezi Mfalme Yekonia aliyotawala na Siku alizotawala, lakini hajapenda kutaja na masaa wala dakika wala sekunde… Huwenda angetokea na mwandishi mwingine angetaja Miezi aliyotawala, na siku na masaa na sekunde!.. na bado asingekuwa ametoa taarifa sahihi ambazo hazikinzani na za wale waliofupisha!.

Kwahiyo biblia haijajichanganya hapo!.wala haijichanganyi mahali popote. Tazama pia muda wana wa Israeli waliokaa Misri je ni miaka 400 au 430?..kujua hilo kwa urefu fungua hapa >>> Je! Miaka Israeli waliokaa Utumwani ilikuwa mingapi? (miaka 400 au 430) kulingana na Mwanzo 15:13 na Kutoka 12:40-42?, Je biblia inajichanganya?

Je unajua kuwa dhiki kuu itakuja baada ya unyakuo wa kanisa na unyakuo upo karibu?..tutumie ujumbe inbox kwa maelezo marefu juu ya hili.

Maran atha!

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

Mwandishi wa kitabu cha Zaburi ni nani?

MIEZI 13 YA KIYAHUDI.

UWEZA WA MUNGU UNAONEKANA WAPI?

TUSIIFUATISHE KAWAIDA YA ULIMWENGU HUU.

Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?

Rudi nyumbani

Print this post

Swali: Je idadi ya askari waliohesabiwa katika 1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9 inajichanganya?.

Swali: Katika 1Nyakati 21:5 tunasona waliohesabiwa kwa Israeli na Yuda jumla ni  askari 1,570,000 lakini tukirudi  katika 2Samweli 24:9 tunaona jumla ya  idadi ya askari waliohesabiwa walikuwa ni 1,300,000 kwa Yuda na Israeli, je biblia inajichanganya?.

Jibu: Turejee,

1Nyakati 21:5 “Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu elfu mara elfu, na mia elfu, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu mia nne na sabini elfu, wenye kufuta panga”.

Tusome tena…

2Samweli 24:8 “Nao walipokwisha kuzunguka nchi yote, wakaja Yerusalemu mwisho wa miezi kenda na siku ishirini. 

9 Naye Yoabu akamtolea mfalme jumla ya hesabu ya watu; nao walikuwa wa Israeli mashujaa wenye kufuta panga mia nane elfu; nao wa Yuda walikuwa watu mia tano elfu”.

Ni kweli katika mistari hii miwili, inaonyesha tofauti ya Askari waliohesabiwa, tunaona kitabu kimoja kinataja idadi ya juu sana, na kingine kinataja idadi ya chini, sasa swali ni je! biblia inajichanganya?

Jibu ni la! Biblia haijichanganyi kwasababu ni kitabu kilichovuviwa na Roho Mtakatifu. Fahamu zetu zinaweza kujichanganya katika kuielewa biblia  lakini kamwe biblia haijawahi kujichanganya, hususani panapotokea habari moja kunukuliwa na waandishi wawili tofauti, kwasababu kama biblia itakuwa na makosa sehemu yoyote, basi kitabu kizima kitakuwa na mapungufu na hivyo hakiwezi kuwa kitabu kitakatifu.

Lakini mpaka Roho Mtakatifu aruhusu kidumu kwa nyakati zote na vizazi vyote ni wazi kuwa biblia yenye vitabu 66 ni maandishi matakatifu na ya kuaminiwa asilimia 100, kwaajili ya maarifa sahihi ya kiMungu, na haina makosa yoyote.

Sasa tukirudi katika hiyo habari tunayoisoma katika vitabu hivyo viwili (1Nyakati 21:5 na 2Samweli 24:9) kila mwandishi alijaribu kunukuu aina ya askari waliohesabiwa..

Mwandishi wa kwanza wa kitabu cha 2Samweli 24:9 alinukuu idadi ya Askari ambao walikuwa ni MASHUJAA TU! Ambao idadi yao ilikuwa ni hiyo 1,300,000 Na Mwandishi wa pili wa kitabu cha 1Nyakati 21:5 alinukuu idadi ya Askari wote kwa ujumla (Waliokuwa mashujaa na wasio mashujaa)..ndio maana utaona idadi imeongezeka mpaka kufikia hiyo 1,570,000. Kwahiyo biblia haijichanganyi.

Ilikuwepo tofauti ya Askari wa kawaida na waliokuwa Mashujaa, waliokuwa mashujaa na wale waliokuwa wakongwe na wazoefu katika vita wenye uwezo mkubwa wa kupambana, kwamfano utaona Mfalme Uzia biblia inaonyesha alikuwa na Askari wa kawaida na waliokuwa mashujaa, waliozoea vita, wepesi na hodari wa vita.

2Nyakati 26:11 “Zaidi ya hayo Uzia alikuwa na jeshi la watu wa kupigana, waliokwenda vitani vikosi vikosi, sawasawa na hesabu walivyohesabiwa na Yeieli mwandishi, na Maaseya msimamizi, chini ya mkono wa Hanania, mmojawapo wa maakida wa mfalme. 

12 Hesabu yote ya wakuu wa nyumba za mababa, WATU MASHUJAA, ILIKUWA ELFU MBILI NA MIA SITA.

13 Na chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la askari, mia tatu na saba elfu, na mia tano, ambao walipigana vita kwa nguvu nyingi, kumsaidia mfalme juu ya adui”.

Je unajua Bwana Yesu alisema kuwa ”Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni (Mathayo 7:19 )??”

Je ni matunda gani unayozaa?..Mazuri au mabaya..

Mathayo 7:17 “Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.

18  Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.

19  Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni”

Maran atha.Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

LIPO LA KUJIFUNZA KWA WALE MASHUJAA 37 WA DAUDI.

Je Kauli ya Mungu katika Warumi 11:4 na 1Wafalme 19:18 inajichanganya?.

Nini maana ya Dirii, Chapeo na Utayari?

USIZITEGEMEE NGUVU ZAKO KUKUSAIDIA!

KUNA NGUVU YA ZIADA KATIKA KULING’ANG’ANIA KUSUDI LA MUNGU.

Rudi nyumbani

Print this post

Kanaani ililaaniwa (Mwanzo 9:20-25,) kwanini Mungu awapeleke wana wa Israeli katika nchi iliyolaaniwa?

Jibu: Turejee,

Mwanzo 9:20 “Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;

21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.

22 Hamu, BABA WA KANAANI, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. 

23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. 

24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.

25 Akasema, NA ALAANIWE KAANANI; Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake”.

Kumbuka hapo kwanza “Kaanani” halikuwa jina la Nchi, bali lilikuwa ni jina la ‘Mtu’. Na mtu huyo alikuwa ni mtoto wa nne (4) wa Hamu..

Mwanzo 10: 6 “Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani”.

Hatujui kwa undani mtoto huyu (Kanaani) alikuwa na tabia gani?..lakini ni wazi kuwa matendo yake yalikuwa kama ya baba yake Hamu, ndio maana akabeba laana ya moja kwa moja ya baba yake.

Sasa huyu Kanaani ndiye aliyelaaniwa na baadaye alikuja kuzaa watoto na uzao wake ukaitwa Uzao wa Kanaani, kufuatia jina la Baba yao, na walipotawanyika usoni pa nchi yote katika ule utawanyiko wa Babeli (Mwanzo 11:8-9) ndipo wakaenda kuishi mahali wana wa Israeli walipowakuta.

Kipindi wanaishi, ardhi ile ilijulikana kama nchi ya Wakanaani. Na kilichokuwa kimelaaniwa na Mungu si ile ardhi/nchi bali ni watu, (ambao ndio hao wakaanani)..ikiwa na maana kuwa hata kama wasingeishi katika ile ardhi na kwenda kuishi katika ardhi nyingine bado wangekuwa chini ya laana.

Kwahiyo wana wa Israeli wakati wanatoka Misri, Mungu aliwatoa Wakanaani kwenye ile ardhi na kuwaweka wana wa Israeli, kwasababu kilicholaaniwa katika Mwanzo 9:5 si ardhi bali ni watu, hivyo watu wanaweza kuondolewa na ardhi ikaendelea kutumika na wengine na ikawa nchi ya Baraka tu, ndio maana baada ya pale haikuitwa tena nchi ya wakanaani bali nchi ya Israeli.

Lakini swali ni je! Hawa Wana wa Hamu mpaka leo wamelaaniwa?.. Maana miongoni mwao kuna Kushi ambaye uzao wake ni watu weusi.

Jibu ni la! Kristo alikuja kuondoa laana zote pale Kalvari, na hivyo hakuna tofauti ya Myahudi na Mmisri, Mkushi na mwisraeli, mbele za Mungu… kama tumeokoka wote tunahesabiwa sawa mbele zake. Lakini kama hatutazaliwa mara ya pili kwa maji na kwa roho wote mbele zake ni kama tuliolaaniwa.

Wakolosai 3:10 “mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.

11  Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote”.

Waefeso 2:16  “Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba”

Je umezaliwa mara ya pili?..

Yohana 3:3  “Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.

4  Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

5  Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu”.

Bwana Yesu anarudi!Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Wakaanani walikuwa ni watu gani?

TUMEFANYA KAZI YA KUCHOSHA USIKU KUCHA.

NI KWANINI WATU WENGI WANASHINDWA KUMWELEWA MUNGU?

Moabu ni nchi gani kwasasa?

Je ni kweli Isaka alifarijika kwa kifo cha mamaye? (Mwanzo 24:67).

Rudi nyumbani

Print this post

Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule(Kutoka 12:4)

SWALI: Bwana yesu apewe sifa, Naomba kufahamu, Kwanini Wana wa Israeli walimuhifadhi mwana-kondoo siku nne kabla ya kuchinjwa katika sikukuu ya pasaka.Je Kuna ufunuo gani tunaweza kupata katika Tendo hilo (Kutoka 12:6)


JIBU: Tusome..

Kutoka 12:3-7

[3]Semeni na mkutano wote wa Israeli, mkawaambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa mwana-kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana-kondoo kwa watu wa nyumba moja;

[4]na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.

[5]Mwana-kondoo wenu atakuwa hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.

[6]Nanyi mtamweka hata siku ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli watamchinja jioni.

[7]Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti cha juu, katika zile nyumba watakazomla.

Bwana aliwapa agizo la kuwatenga wana-kondoo Kutoka katika kundi siku ya 10, Kisha  siku ya 14 kuchinja.

Maana yake ni kuwa sadaka/dhabihu Yao, ilipaswa itambulike mapema Kisha ikatengwa. Kama wangekaidi agizo hilo na kuchagua mwanakondoo siku Ile Ile ya kuchinja au hata siku moja kabla  ilikuwa ni kosa mbele za Mungu.

Kufunua nini?

Na sisi pia Bwana anapendezwa na dhahibu zenye maandalizi, ambazo zimetengwa mapema…Kwamfano unapokwenda ibadani jijengee desturi ya kumwandalia Mungu sadaka zako mapema..hata ikiwezekena siku kadhaa kabla..Kwa jinsi unavyoandaa mapema ndivyo inavyokuwa na utukufu mwingi zaidi..

Lakini pia Unahakikisha unaitenga kabisa na hesabu zako nyingine..(yaani haiguswi), mpaka siku ya kumtolea. 

Hiyo itaifanya sadaka Yako ipokelewe Kwa furaha na Mungu, kuliko kufikiria kumtolea Mungu muda huo huo wakati ulikuwa na nafasi ya kufanya maandalizi. Ndio ufunuo ulio nyuma ya agizo hilo la Pasaka.

Bwana akubariki.Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Makerubi wenye sura nne, ni kweli wapo? na je! wanyama wataenda mbinguni?

Kwanini Kristo aitwe Mwana-kondoo. (Yohana 1:29)

Tofauti kati ya zaka na sadaka ni ipi?

TUUTAFUTE USEMI MMOJA. TUUJENGE MNARA WA MUNGU

NI SAA KUMI NA MBILI (12) TU, ZA KRISTO KWAKO.

Bahari mbalimbali zilizoorodheshwa kwenye biblia.

Konzo la Ng’ombe ni nini? (Waamuzi 3:31).

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini Bwana Yesu ajulikane kama ‘Amina’ (Ufunuo 3:14)

Jibu: Turejee,

Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye ‘ALIYE AMINA’, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu”

Neno Amina maana yake ni “Na iwe hivyo”.. Neno hili kwa lugha ya kiingereza ni “Amen” Hivyo Popote panapotajwa “Amina” au “Amen” maana yake ni “na iwe hivyo”.

Sasa kwanini Bwana Yesu ajitambulishe kwa neno hilo?..

Ni kuyatofautisha maneno yake na wengine! Kwamba maneno yake ni Thabiti.

Sasa ili tuelewe vizuri, turejee pale Bwana Yesu aliposema kuwa “Mimi ndimi Njia, na Kweli na Uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia yangu mimi (Yohana 14:6)”.

Tukiunyambua huo mstari vizuri, tunapata sentensi mbili 1. Yeye ndiye Njia, 2. Mtu haji kwa Baba ila kwa njia yake yeye.

Hapo Bwana anajiita kuwa yeye “Njia” anajifananisha yeye na kitu kisicho na uhai..lakini anazidi kufafanua ni kwa jinsi gani yeye ni njia kwa kuendelea kusema… “mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye” ikiwa na maana kuwa, kwa maneno ya Yesu na maisha yake, tukiyafuata hayo tutafika mbinguni (hayo ndio njia)… Njia zipo nyingi, lakini zote hizo hazimpeleki mtu mbinguni, isipokuwa njia ya Yesu tu! Ambayo ni Neno lake.

Sasa tukirejea tena hapo Bwana aliposema yeye  ni “Amina” utaona mbele kidogo anaendelea kufafanua ni kwa namna gani yeye ni “Amina”.

Ufunuo 3:14  “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, SHAHIDI ALIYE MWAMINIFU NA WA KWELI, MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU”.

Anasema yeye ni Amina, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. Maana yake maneno yake ni hakika!, akisema amesema ni lazima iwe hivyo!.. Amina yake ni amina kweli.. wengine wanazo amina lakini zinaweza zisitimie kama walivyoseme. Lakini yeye (Yesu) maneno yake ni hakika!.. akisema basi ni lazima “ITAKUWA HIVYO KAMA ALIVYOSEMA” Ndio maana anaitwa Shahidi mwaminifu.. hajawahi kusema jambo halafu lisitimie..Ni mwaminifu kwa maneno yake siku zote.

Tusome,

Marko 13:31 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.

2Wakorintho 1:20 “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi”.

Je umemtumainia huyu ambaye Maneno yake hayapiti?. Alisema “Aaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16)” je unadhani kutakuwa na kanuni nyingine Zaidi ya hiyo?.. Alisema wadhalimu, na wachawi, na wazinzi, na walevi hawataurithi ufalme wa mbinguni, je unadhani anadanganya??..ni kweli itakuwa hivyo!, maneno yake kamwe hayapiti, Amina yake ni amina kweli..

Je umempokea Yesu?, je umebatizwa kwa maji na kwa Roho Mtakatifu?.. Kama bado basi tafuta kufanya hivyo mapema.

Maran atha?Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

UAMINIFU NI KIGEZO KIKUBWA CHA KUTUMIWA NA MUNGU.

Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake, Ni ndugu yake aliye mharabu

Je Henoko aliyeenda na Mungu alikuwa ni mwana wa Kaini? (Mwanzo 4:16)

Vifungu vya biblia kuhusu Uongozi.

HUDUMA YA WALE MASHAHIDI WAWILI.

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini Kristo aitwe Mwana-kondoo. (Yohana 1:29)

Yohana 1:29 “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”.

Bwana Yesu sehemu nyingine anajulikana hivi kama Mwana-kondoo kufuatia tabia ya kondoo ilivyo.

Kondoo ni mnyama mpole sana na mnyenyekevu, tofauti na Mbuzi.. Kondoo Anapokatwa manyoya yake huwa hajigusi anatulia sana, na pia hawezi kujichunga mwenyewe huwa anamtegemea mchungaji asilimia mia. Tofauti na mbuzi au Ng’ombe.

Lakini pamoja na hayo kondoo aliyekomaa ambaye tayari kashaota pembe ijapokuwa ni mpole lakini kuna vipindi vichache vichache anakuwa na hasira hususani wakati wa mvua, na pia anapokutana na kondoo mwingine aliye wajinsia kama yake. Hivyo Bwana Yesu hajajifananisha na kondoo aliyekomaa, kwasababu anazo kasoro nyingi.. bali anajifananisha na kondoo mchanga, (mwana-kondoo) ambaye bado hata hajaota pembe, ambaye hawezi kupambana, aliye mnyenyekevu na mpole.

Bwana Yesu naye ni mpole mfano wa huyo.. Maandiko yanamshuhudia hivyo..

Mathayo 21:5  “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, MPOLE, naye amepanda punda, Na mwana-punda, mtoto wa punda”.

Na yeye mwenyewe anajishuhudia hivyo  katika Mathayo 11:28.

Mathayo 11:28  “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29  Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; KWA KUWA MIMI NI MPOLE na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30  kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi”.

Je umemfuata Yesu aliye mpole?..yeye anayeongea nawe kwa sauti ya upole moyoni mwako, kwamba utubu dhambi?.

Kama bado unasubiri nini?

Okoka leo na ukabatizwe na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu nawe utapata ondoleo la dhambi…na jina lako litaandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana kondoo na utakuwa na nafasi katika mji ule, mbingu mpya na nchi mpya.

Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo”.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

Upole ni nini?

LISHA KONDOO WANGU, LISHA WANA-KONDOO WANGU.

Je ni kweli Musa alikuwa mtu mpole kuliko wote duniani?

JE! UNAMPENDA BWANA?

MWANANGU, NIPE MOYO WAKO;

Rudi nyumbani

Print this post

Je Henoko aliyeenda na Mungu alikuwa ni mwana wa Kaini? (Mwanzo 4:16)

Jibu: Turejee,

Mwanzo 4: 16 “Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.

17 Kaini akamjua mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Henoko; akajenga mji akauita Henoko, kwa jina la mwanawe”.

Henoko aliyeenda na Mungu hakuwa mwana wa Kaini, kwasababu Uzao wa Kaini wote ulilaaniwa, na hivyo hakutoka nabii yeyote wala mtu yeyote mwenye rekodi ya kumpendeza Mungu katika huo uzao, bali uzao wote uligharikishwa na ile gharika.

Swali kama ni hivyo kwanini Henoko aonekane hapa kama ni uzao wa Kaini?.

Jibu ni kwamba Huyu Henoko anayetajwa hapa katika (Mwanzo 4:16) sio yule aliyeenda na Mungu, bali alikuwa ni Henoko mwingine, kwasababu jina hilo ‘Henoko’ hakuwa nalo mtu mmoja tu!, bali ni wengi waliitwa kwa jina hilo, kama tu leo majina yetu yanavyoweza kuwa ya watu wengine mahali pengine.

Lakini yule Henoko, aliyekuwa mtumishi wa Mungu, na aliyempendeza Mungu alitokea katika Uzao wa Sethi na habari zake tunazisoma katika Mwanzo mlango wa 5.

Mwanzo 5:18 “Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko. 

19 Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.

20 Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa. 

21 Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 

22 Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.

23 Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.

24 Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa”.

Huyo ndio Henoko aliyeenda na Mungu, ambaye alikuwa mwana wa Yaredi wa uzao wa Sethi, na alikuwa ni mtu wa saba kutoka kwa Adamu (Yuda 1:14). Lakini yule mwingine alikuwa mwana wa Kaini.

 Ni sawa Lameki aliyetajwa katika Mwanzo 4:18-19, ambaye alioa wake wawili, na yule aliyetajwa katika Mwanzo 5:28-31 ambaye alikuwa ni baba yake Nuhu… Hawa walikuwa ni Lameki wawili tofauti wenye tabia mbili tofauti, ingawa majina yao yalifanana…ndivyo ilivyo pia kwa hawa Henoko wawili tuliojifunza habari zao.

Sasa Ni jambo gani tunaloweza kujifunza kwa Henoko aliyeenda na Mungu?

Alikuwa ni mtu aliyeenda na Mungu; Maana yake Njia zake zilimpendeza Mungu mpaka kufikia hatua ya Mungu kumtwaa, na kabla ya Mungu kumtwaa biblia inasema alionyeshwa ujio wa Bwana, siku ile atakayokuja na watakatifu wake kwaajili ya vita vya Harmagedon na utawala wa miaka 1000 duniani.

Yuda 1:14  “Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,

15  ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake”

Bwana atusaidie na sisi tuwe watu wa kwenda  na Bwana katika njia zake kama alivyokuwa Henoko.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Je! tunapaswa kukiamini Kitabu cha Henoko?

JE! Kaini alimpatia mke wake wapi?

Mtu wa kwanza kufa alikuwa nani?

Wanefili walikuwa ni watu gani?

EPUKA MAKUNDI ILI UTAKATIFU WAKO UDUMU!.

Rudi nyumbani

Print this post

Wakolosai 3:5 inamaana gani?

SWALI: Wakolosai 3:5 inamaana gani?. Tofauti kati ya tamaa mbaya na kutamani ni ipi?


JIBU: Wakolosai 3:5 Inasema..

  “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;”

Hapo anaanza kwa kusema vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi. Ikiwa na maana kuwa kuna viungo vya duniani ambavyo kazi yake kimsingi ni kutimiza mapenzi ya duniani (ya shetani). Tofuati na vile vya ki mbinguni ambavyo vinatimiza mapenzi ya Mungu. Viungo hivi sio mikono, miguu, macho, masikio au pua hapana, bali viungo vya rohoni.

Viungo vya kimbinguni vimeelezwa kwenye mstari wa 12-17. Lakini vya duniani ndio hivi vinavyozungumziwa hapa katika mstari wa 5, ambavyo tunapaswa tuviue. Navyo ni;

1) Uasherati.

Uasherati unajumuisha kitendo chochote cha zinaa nje ya ndoa pamoja na mambo yafanywayo kinyume na asili. Ikiwemo Uzinzi, ufiraji, na ulawiti. Vitu hivi havipaswi vipewe nafasi kwa mtakatifu yoyote.

2) Uchafu

Uchafu ni kinyume na usafi. Mtu mchafu kimsingi anakuwa amebeba takataka katika mwili wake. Vivyo hivyo, mtu ambaye anaruhusu takataka za hii dunia zimtawale ni mchafu kiroho. Mfano wa takatakata hizi ni miziki ya kidunia, anasa, matusi, ulevi, kubeti, mazungumzo yasiyofaa, kutazama vitu visivyojenga mitandaoni, ushabiki n.k. Epuka kujitia unajisi na vitu vya ki-ulimwengu.

3) Tamaa mbaya.

Kuzipa tamaa za mwili nafasi ya kukutawala. Na matokeo ya tamaa hizi mbaya kukutawala ndani yako, utaishia, ni kutazama picha chafu, muda wote kuwa na mazungumzo ya kizinzi, kuchat na jinsia tofauti na wewe kusikokuwa na sababu, kuvaa mavazi ya namna hiyo au kujiwekwa kimwili uvutie uzinzi kwa mwengine. Tabia hizi ndani yako unapaswa uziue.

4) Mawazo mabaya.

Mawazo mabaya ni kinyume cha mawazo mazuri. Mtu mwenye mawazo mazuri huwaza yaliyo mazuri, ya kujenga. Lakini mwenye mawazo mabaya sikuzote ni kubomoa. Mawazo hayo ni pamoja na wivu, rushwa, uongo, wizi, uuaji, unafki, visasi,. Hivi havipaswi kuonekana ndani ya mkristo.

5) Kutamani.

Kutamani kunakozungumziwa hapa sio kule kwa tamaa za mwili, hapana, bali tamaa ya mambo ya kidunia, mfano tamaa ya kuwa na mali, tamaa ya kufanana na watu wa kidunia, wanamiziki, wanamitindo n.k., na hizo ndizo zinazompelekea mtu, kugeuza vitu hivyo kuwa kama mungu wao, kuvitafuta na kuvisumbukia sikuzote .Na ndio maana mwandishi anamalizia kwa kusema “Ndiyo ibada ya sanamu” maana yake rohoni vinaonekana ni miungu kwao. Jiepushe na kutamani.

Hivyo  tukifanikiwa kuviua viungo hivi, basi mwili hauwezi kuwa na matunda yoyote, kwasababu hakuna kiungo chake hata kimoja kina uhai. Lakini pia anasema,

Wakolosai 3:12  Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu,

13  mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

14  Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.

15  Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

16  Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

17  Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.

Hivyo ndivyo viungo vya kimbinguni, Tujitahidi vituvae.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Uasherati wa Kiroho maana yake nini?

WALA MSIUANGALIE MWILI, HATA KUWASHA TAMAA ZAKE.

Nini maana ya huu mstari “sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”

WAPENDENI ADUI ZENU, WAOMBEENI WANAOWAUDHI.

Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?

Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?

Rudi nyumbani

Print this post

Birika walilooga Makahaba lilikuwaje?

Swali: Katika kifo cha Ahabu, biblia inasema alikufa na gari lake likaenda kuoshwa katika birika ambalo wanaoga Makahaba, (1Wafalme 22:38)..hili birika walilokuwa wanaoga makahaba lilikuwaje?

Jibu: Turejee.

1Wafalme 22:37 “Hivyo akafa mfalme, akachukuliwa Samaria, wakamzika mfalme huko Samaria. 

38 Wakaliosha gari penye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake; (basi ndipo walipooga makahaba); sawasawa na neno la Bwana alilolinena. 

39 Na mambo yote ya Ahabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na nyumba ya pembe aliyoijenga, na miji yote aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?”

Ikumbukwe Ahabu alimwua Nabothi Myezreeli na kumdhulumu kiwanja chake, (1Wafalme 21:1-16), na baada ya kumwua ndipo unabii ukaja kupitia Eliya, kumwambia kuwa atakufa na damu yake italambwa na mbwa kama alivyomwua Nabothi (soma 1Wafalme 21:17-27).

Baada ya miaka mitatu, ndipo unabii huo unakuja kutimia, Mfalme Ahabu alikufa alipokuwa vitani na damu yake ikalambwa na mbwa mahali pale pale mbwa walipolamba damu ya Nabothi.

Lakini tunasoma tena jambo lingine lililoambatana na kifo cha Ahabu, kwamba mahali pale gari lake lilipooshwa ni mahali pia Makahaba wanapooga.

Sasa biblia haijaeleza kwa kina hili birika ambalo walikuwa wanaoga makahaba lilikuwaje. Lakini ni wazi kuwa hili halikuwa birika la kiyahudi, Kwani mabirika/ mabwawa ya kiyahudi yalikuwa yanatumika na makuhani na watu wa kawaida katika kuoga(kutawadhia) ili kujitoa unajisi.

Walawi 15: 16 “Na mtu ye yote akitokwa na shahawa yake, ndipo ataoga mwili wake wote majini, naye atakuwa najisi hata jioni”.

Soma pia Walawi 15:13, Kumbukumbu 23:10-11.

Lakini hili Birika/bwana hili ambalo makahaba walikuwa wanaoga, lilikuwa katika mji wa Samaria mtaa wa Yezreeli, ambao ndio ulikuwa kitovu cha ibada zote za mungu baali. Hivyo hili halikuwa bwawa la dini ya kiyahudi, bali lilikuwa ni bwawa la mungu baali. Huenda makahaba walikuwa wanaoga hapo kulingana na desturi zao za kibaali, kwani desturi nyingi za dini ya kibaali zilikuwa zinakaribia kufanana na za dini ya kiyahudi.. (mfano wa hizo utaona ni ile sadaka Ahabu aliyoitoa katika 1Wafalme 18:20-30).

Hivyo huenda nao pia walikuwa na desturi kama hiyo ya wayahudi ya kujiosha katika mabwawa/mabirikia.

Lakini lililo kubwa la kujifunza hapo ni kuwa Neno la Mungu kamwe halipiti.. Alisema Ahabu atakufa na damu yake italambwa na mbwa, na kweli alikufa sawasawa na neno hilo miaka mitatu baadaye, katika kifo cha aibu zaidi hata ya  kile alichomuua Nabothi.

Na vile vile alisema, kuwa atarudi tena pamoja na ujira wake kulimlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo, Neno hilo halitapita, ni lazima litimie na sasa tupo katika siku za kurudi kwake, muda wowote unyakuo unatokea!

Ufunuo 22:12  “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13  Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14  Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”

Je umeokoka kikweli kweli au bado una uvuguvugu?…Ufunuo 3:16 “Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu”.

Mathayo 24:35 “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

Je Mungu anaweza kumdanganya mtu?

BIRIKA LA SILOAMU.

USIMPE NGUVU SHETANI.

Baali alikuwa nani?

Birika ni nini?, na yale Matao matano katika birika la Bethzatha ni nini?.

Rudi nyumbani

Print this post

Chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ndio kipi? (Matendo 21:25).

Jibu: Turejee,

Matendo 21:25 “Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati”


Vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu ni vyakula vyote vinavyotolewa kwa maagizo ya kishetani.
Mfano wa vyakula hivyo ni vile vya kimila au vya waganga wa kienyeji.

Mfano wa vya kimilia ni vile ambavyo mtu anakula au analishwa kwa lengo la kumkinga na madhara fulani ya kiroho kama uchawi au kumpatanisha na roho fulani..


Ndio hapo utakuta mtu anaambiwa alete mbuzi, au kondoo na kisha yule kondoo achinjwe kama sadaka/kafara kwa mizimu na kisha ale sehemu ya nyama ya huyo mnyama aliyetolewa sadaka… Sasa endapo mtu huyo akila hiyo nyama au sehemu ya hiyo nyama tayari anakuwa amekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.


Au utakuta mtu anaenda kwa mganga wa kienyeji na yule mganga anamwambia ili tatizo lake litatulike basi alete mnyama fulani aidha mbuzi, au ng’ombe au kuku na achinjwe kama kafara na nyama yake au damu yake inywewe na mhusika.. Mtu anayekula hiyo nyama anakuwa tayari amekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.


Au anaweza asiambiwe alete mnyama, bali akaambiwa alete hata nafaka fulani na kisha ile nafaka ikatolewa kwa miungu na mtu akaambiwa ashiriki sehemu ya ile nafaka..sasa mtu huyo endapo akila kile chakula au sehemu ndogo ya kile chake basi anakuwa amekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.


Na mtu anayekula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu, anakuwa anajiungamanisha na ile madhabahu ya kishetani..ndivyo biblia inavyosema.


1 Wakorintho 10:19-22 “Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?
20 Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.
22 Au twamtia Bwana wivu? Je! Tuna nguvu zaidi ya yeye?


Hiyo ni tahadhari kwetu kuwa tujiepushe na vyakula vya namna hiyo kwani ni hatari kiroho.
Lakini kama umealikwa mahali na umetengewa chakula ambacho kimetolewa sadaka kwa sanamu na ukala bila kujua kuwa kilikuwa kimetolewa sadaka kwa miungu, hapo hupaswi kuogopa kwasababu lile andiko ya kwamba “tutakula vitu vya kufisha navyo havitatudhuru (Marko16:18)” litatimia juu yako.


Lakini kama umeshajua kuwa chakula hicho ni cha miungu basi hupaswi kula kabisa..


Je umewahi kula au kulishwa chakula cha namna hiyo katika familia yenu au ukoo wenu au kwa waganga wa kienyeji?..Kama ndio basi fahamu kuwa siku ulipokula tayari ulijiungamanisha na hiyo miungu, na hivyo roho za hiyo miungu zitayaongoza maisha yako siku zote.


Hivyo suluhisho ili uweze kufunguka ni wewe kwanza kutubu mbele za Bwana kwa kumaanisha na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Bwana Yesu Kristo (Matendo 2:38) na mwisho kupokea Roho Mtakatifu..Kwa hatua hizo utakuwa umefunguliwa moja kwa moja.


Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na kundi letu la mafundisho ya Biblia whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Mada Nyinginezo:

JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.

“Kinga kilichotolewa motoni “Kinafunua nini kibiblia?

Sadaka ya Amani ilikuwaje?

Biblia inapotumia neno “Bila kazi ya mikono”, ina maana gani?

HERI WAPATANISHI, MAANA HAO WATAITWA WANA WA MUNGU

Rudi nyumbani

Print this post