Title December 2022

JIHADHARI NA MKUTANO WA WATU WALIOCHANGANYIKANA.

Jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe, karibu tujifunze biblia Neno la Mungu wetu, lililo Taa ya miguu yetu na Mwanga wa njia yetu.

Kuna jambo la muhimu la kujifunza juu ya safari ya Wana wa Israeli kutoka Misri kuelekea Kaanani. Maandiko yanaonesha kuwa wana wa Israeli hawakutoka wenyewe Misri, bali walitoka na Kundi lingine lililochanganyikana.

Hebu tusome..

Kutoka 12:35 “Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila kuhesabu watoto. 

38 NA KUNDI KUBWA LA WATU WALIOCHANGAMANA MNO WAKAKWEA PAMOJA NAO; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana”

Umeona hapo?.. Kulikuwa na watu wengine tofauti na Waisraeli walioondoka Misri pamoja na wana wa Israeli.

Sasa swali ni je! kundi hilo lilikuwa ni kundi gani?.

Kundi hilo lilijumuisha baadhi ya Wamisri ambao huenda walikuwa hawataki kuendelea kuishi Misri, labda kutokana na aina ya Maisha ya Misri, pamoja na Wamisri ambao walioana na Waisraeli, maana yake huenda (mwanamke wa kimisri aliolewa na Mwisraeli) hivyo ni lazima aondoke na mumewe, au mwanamke wa kiisraeli aliolewa na Mmisri, na hivyo huyo Mmisri, hataki kumwacha mke wake huyo na akawa radhi kuondoka naye, na kwenda na wana wa Israeli.  Hivyo lilikuwa ni kundi kubwa sana!!..

Sehemu nyingine iliyotaja kundi hili lililochanganyikana ni mchanganyiko katika kile kitabu cha Mambo ya Walawi 24:10-16. (Kisa cha Yule mwana wa kiMisri, aliyechanganyikana).

Walawi 24:10 “Ikawa mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, ambaye babaye alikuwa Mmisri, akatokea kati ya wana wa Israeli; na huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli, na Mwisraeli mmoja, wakapigana pamoja ndani ya marago; 

11 kisha huyo mwana wa mwanamke wa Kiisraeli akalikufuru hilo Jina, na kuapiza; nao wakamleta kwa Musa. Na jina la mamaye alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila ya Dani. 

12 Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa Bwana.

13 Na Bwana akasema na Musa, na kumwambia,

14 Mtoe huyo aliyeapiza nje ya marago; na wale wote waliomsikia na waweke mikono yao kichwani mwake, kisha mkutano wote na wamwue kwa kumpiga kwa mawe.

15 Nawe nena na wana wa Israeli na kuwaambia, Mtu awaye yote atakayemlaani Mungu wake atachukua dhambi yake. 

16 Na yeye atakayelikufuru jina la Bwana hakika atauawa; mkutano wote watamwua kwa kumpiga kwa mawe; kama ni mgeni, kama ni mzalia, hapo atakapolikufuru jina la Bwana atauawa”.

Sasa tukirudi katika habari ya Huu Mkutano uliochanganyika, huenda mkutano huu ukaonekana kama ulikuwa ni mwema, lakini kinyume chake ulikuja kuwa mwiba mkubwa kwa wana wa Israeli, kwani uliwakosesha sana mbele za Mungu wao.

Katika biblia tunasoma kwamba sio wana wa Israeli walioanza kumlalamikia Mungu kuhusu kutaka Nyama jangwani, bali tunasoma ni hili kundi lililochanganyikana ndilo lililoanza kunung’unika na hatimaye kushawishi mkutano mzima hadi wa wana wa Israeli kunung’unika, na kusababisha kuwa dhambi kubwa sana kwa wana wa Israeli.. Hebu tusome habari hiyo…

Hesabu 11:4 “Kisha MKUTANO WA WAFUASI WALIOKUWA KATI YAO, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule?

 5 Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu”

Umeona tena hapo?.. maandiko yanasema “MKUTANO WA WAFUATI WALIOKUWA KATI YAO” ndio walioanza kushikwa na tamaa..wakata nyama..na ndipo Israeli wote nao wakaingiwa na tamaa.

Maandiko yanasema, agano la kale ni kivuli cha agano jipya..Safari ya wana wa Israeli kutoka Misri kuelekea Kaanani , inafananishwa na safari yetu ya kutoka katika utumwa wa dhambi, hapa duniani na kuelekea mbinguni.. Hivyo basi tunapokuwa katika safari hii, hatuna budi kujihadhari na watu waliochanganyikana, (yaani watu waliovuguvugu katika imani), kwasababu kwa nje wanaweza kuonekana hawana madhara yoyote, lakini tukijifunga Nira nao, na kutembea nao huko mbeleni watatukosesha na Mungu wetu na kuturudisha nyuma pakubwa sana, kama hawa walivyowakosesha wana wa Israeli.. Ndivyo maandiko yanavyosema..

2 Wakorintho 6:14  “Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

15  Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?

16  Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

17  Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.

18  Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike”

Unapoanza safari ya Wokovu, ni Mungu kakuita wewe, na si wewe pamoja na rafiki yako au mfanyakazi mwenzako.. kama bado yeye hajaokoka hupaswi kujifunganisha naye Nira, maana yake ni kwamba kama mlikuwa mmezoea kwenda bar pamoja unaacha!, (wewe unapaswa umhubirie wokovu kuanzia huo wakati na kuendelea na si kujishikamanisha naye tena), kama mlikuwa mnaketi kuwasengenya watu, unaacha!, unajitenga naye katika hilo eneo.. Na mambo mengine yote mabaya hupaswi kuambatana naye, mpaka na yeye atakapobadilika na kuwa kama wewe.

Lakini usipoamua kujiachanisha naye katika utu wenu wa kale..basi tambua kuwa atakuja kuwa kikwazo kwako kumaliza safari yako salama ya Imani, (atakuwa ni lango la shetani kumtumia kukurudisha wewe nyuma) kama alivyolitumia lile kundi liliochanganyikana kuwarudisha Israeli nyuma kiimani.

Bwana atusaidie katika safari yetu ya Imani.

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > WHATSAPP-Group

Mada Nyinginezo:

KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.

Hema ya kukutania ni nini, na ilikuwaje?

JINSI MUNGU ANAVYOIPIGA NA KUIPONYA AFRIKA.

KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.

Kiti cha Rehema kilikuwaje? (Kutoka 40:20)

Rudi nyumbani

Print this post

BASI NIKAOGOPA, NIKAENDA NIKAIFICHA TALANTA YAKO.

Shalom…Bwana wetu Yesu Kristo atukuzwe milele. Karibu tujifunze maneno yake ya uzima.

Lipo la kutafakarisha sana, katika ile habari ya yule mtu aliyesafiri, na kuwaita watumwa wake watatu na kumpa kila mmoja talanta ya Fedha wakafanyie biashara.

Kama tunavyoijua habari yule wa kwanza aliyepewa talanta tano, akaleta faida ya talanta nyingine tano, Vilevile yule aliyepewa talanta mbili akachuma nyingine mbili…lakini yule aliyepewa moja..maandiko yanatuambia hakuchuma chochote…

Na sababu iliyomfanya ashindwe kufanya vile si nyingine zaidi ya  “WOGA”…Tusome..

Mathayo 25:24-30

[24]Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;

[25]basi NIKAOGOPA, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.

[26]Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;

[27]basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

[28]Basi, mnyang’anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.

[29]Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.

[30]Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Aliogopa nini?

Aliogopa atakapojaribu kuifanyia biashara ataipoteza…aliogopa kupata hasara..hivyo akaona ni heri aihifadhi tu..mahali fulani mpaka Bwana wake atakaporudi amrudishie kilicho chake wamalizane..

Aliogopa kuchekwa, na kudharauliwa, na kudhihakiwa, alijiona hawezi kuzalisha kile alichopewa, hana uzoefu na biashara..hakutaka kujitosa kama wale wenzake…ambao wao pia waliijua hatari ya biashara kwamba kuna kupata na kupoteza, lakini hawakutaka kuzipa kipaumbele… lakini yeye akasema sitaki kupata magonjwa ya moyo..wacha niihifadhi tu..kwani nini! , maadamu sijamtapeli..akirudi nitamrudishia kilicho chake.

Ndugu hii hali ipo kwa wakristo wengi hadi sasa..hawataki kupiga hatua moja mbele kuuzalia matunda wokovu wao kisa tu HOFU, ya kupata hasara..

Hasara ya nini?

Hasara ya ndugu kuwatenga, kama ndugu zao wakisikia kaokoka, wakiwatenga itakuwaje?

Hasara ya kuonekana wamerukwa na akili,..

Hasara ya marafiki kuwacheka, kuwaona ni washamba, wamepitwa na wakati..kwasababu wameacha mtindo fulani wa maisha.

Hasara ya kufukuzwa kazi, au kushushwa cheo kazini, kisa tu hawali rushwa tena.

Hasara ya kuachwa na mke/mume kisa tu wamejitwika msalaba wao na kuwafuata..

Hivyo hofu kama hizi na nyingine nyingi zimekuwa kigezo  cha wakristo wengi kufukia talanta zao chini..wanasubiria tu siku ya kufa, Kristo aje na kuwauliza mmezalisha Nini kwenye Wokovu niliowapa siku ya kwanza…wenyewe waseme hakuna zaidi tu ya kuokoka..

Hii ni hatari kubwa sana…na jambo la kuhuzunisha..Ni lazima tujue “hakuna hatua moja mbele kama hakuna kujikana” Yesu aliye Bwana wetu alikubali kuchukiwa, kutengwa, kuonekana karukwa na akili, hadi kuuliwa, ili tu amzalie Mungu matunda yaliyo bora..(Yohana 7:5)

Marko 3:21

[21]Jamaa zake walipopata habari wakatoka kwenda kumkamata; maana walisema, Amerukwa na akili.

Na yeye mwenyewe akatuambia tusipojitosa kama yeye hatuwezi kuwa wanafunzi wake…

Luka 14:26-27

[26]Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

[27]Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Akasema pia..ili mbegu ya ngano iweze kuzaa na kuleta matunda mengi haina budi kuoza kwanza chini ya ardhi, ndipo baadaye ichipuke na kukukua na kuzaa..(Yohana 12:24)

Ni lazima tuonekane tumekufa kwanza ndipo tuzalishe talanta zetu..tuonekane tumepotea kwa ajili ya Kristo ndipo tupate karama zake, tukilikimbia hili, tujue hatutazalisha chochote, ukristo wetu utakuwa ni ule ule wa miaka nenda, miaka rudi.

Ndugu/dada umedhamiria kumfuata Yesu, embu acha udunia kwa moyo wako wote..acha vimini, acha marafiki wasiofaa, acha miziki, na tamaa za ujanani, mtafute Mungu kwa moyo wote, elekeza nguvu zako zote huko..Epuka kuwa mkristo-jina…yule wa kusema nimeokoka-nampenda Yesu, halafu maisha yako hayana ushuhuda hata chembe..

Maanisha sasa..kwasababu siku zinavyozidi kwenda, siku moja utakufa na utatolea hesabu wokovu uliopewa, ukauchezea kwa hofu za wanadamu na ulimwengu.

Bwana atusaidie..

Maran atha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 1)

Azidishaye mali yake kwa riba, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

Talanta ni nini katika biblia (Mathayo 25:14-30)

Nini maana ya huu mstari? “Yeye mwenyewe ataokolewa lakini ni kama kwa moto”

ANGALIA JINSI USIKIAVYO:

Yesu alifundisha kwa mifano. Je hiyo mifano maana yake nini?

HUJAPEWA MBAWA ZA KUKIMBIA MATATIZO.

Rudi nyumbani

Print this post

Mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?

SWALI: Naomba nifahamishwe mbona ni maskini tu huwa ndio wanaolipuka mapepo, na sio matajiri?


JIBU: Si kweli, Nguvu za giza huwa hazichagua, hali ya mtu ya kimaisha, zinawavaa matajiri vilevile vinawavaa maskini, zinawavaa wanaume, zinawavaa wanawake, zinawatesa watoto (Marko 9:21), vilevile zinawaathiri mpaka wanyama (Soma Mathayo 8:31 )..Kwasababu kazi ya shetani sikuzote ni kuuharibu mpango mzima wa Mungu kwa viumbe vyake vyote.

Hivyo usidanganyike kuwa matajiri hawawezi kuwa na mapepo, huwenda ni kwasababu wewe hujakutana na visa hivyo, lakini vipo vingi. Pia katika maandiko walikuwepo matajiri ambao walisumbuliwa na mapepo.

Soma..

Luka 8:1  “Ikawa baada ya hayo alikuwa akizunguka-zunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza habari njema ya ufalme wa Mungu; na wale Thenashara walikuwa pamoja naye,

2  na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,

3  na Yoana mkewe Kuza, wakili wake Herode, na Susana, na wengine wengi, waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao”

Umeona hapo, Hao wanawake wanaotajwa wote walikuwa ni matajiri, hakuna maskini, tukianzia na huyo Mariamu Magdalena, ambaye alitoa marhamu yake yenye thamani ya mamilioni ya pesa akammwagia Kristo miguuni pake, mpaka kwa Yoana mkewe Kuza, wakili wa Herode.

Mawakili kwa zamani ni sawa tu na mawaziri wakuu na wakuu wa majeshi  sasahivi, hivyo huyu mke wa waziri mkuu alikuwa akimfuata Yesu, huwezi kusema ni maskini, alikuwa tajiri na wanawake wengine hapo wakitajwa walikuwa wakimuhudumia kwa mali zao.

Hivyo, hakuna mtu aliye na ofa kwa Mungu au kwa shetani, kwasababu ya hali yake ya kimaisha. Sote tunahitaji wokovu, tunahitaji msaada kwa Kristo sawasawa, tunahitaji kufunguliwa na yeye.

Tahadhari:

Epuka  mahubiri yanayopigia kampeni utajiri, ambayo ndio yanayoendelea sikuhizi za mwisho kana kwamba ndio uhai wa mtu ulipo, yatakupoteza. Mkimbilie Kristo akupe uzima wa milele.

Efatha.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kwanini kuna watu wanafanyiwa deliverance (Maombi ya kufunguliwa), lakini baada ya muda wanarudiwa tena na hali ile ile sababu ni nini?

MWANAMKE, USIFUNGUE MLANGO WA MAPEPO KUKUINGIA!.

SI MAPEPO YOTE NI YA KULIPUKA.

JINSI MUNGU ATAKAVYOTOA THAWABU ZAKE, NA VIGEZO ATAKAVYOTUMIA. (Sehemu ya 4)

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

MAPEPO YANATAFUTA HIFADHI NDANI YAKO KWA BIDII SANA.

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

Rudi nyumbani

Print this post

Masihi ni nani?

Je! neno Masihi linamaanisha nini?

“Masihi” ni Neno la Kiebrania, linalomaanisha “Mpakwa mafuta” (Yaani mtu aliyeteulewa na Mungu kwa kusudi Fulani). Katika biblia watu walioteuliwa na Mungu rasmi kuwa Wafalme, hao waliitwa masihi wa Bwana, vile vile waliochaguliwa na Mungu kuwa manabii, nao pia waliitwa masihi wa Bwana.

Tafsiri nyingine ya neno Masihi ni “Kristo”. Kwahiyo katika biblia mamasihi (yaani makristo au watiwa mafuta) walikuwa wengi lakini aliyekuwa MASIHI KIKWEKWELI alikuwa ni Mmoja tu! Ambaye ni YESU KRISTO.

Mamasihi wengine ni kweli walipakwa mafuta na Mungu lakini hawakuwa wakamilifu asilimia zote..Daudi alikuwa ni masihi wa Bwana (Soma 1Samweli 16:6-13) lakini hakuwa mkamilifu asilimia zote, kwani aliua na pia alimtwaa mke wa Uria na kumfanya wake.

Vile vile Mfalme Sauli maandiko yanasema alikuwa ni masihi wa Bwana lakini tunasoma alikuja kukengeuka na kumdharau Mungu na maagizo yake..

1Samweli 24:9 “Daudi akamwambia Sauli, Kwa nini unasikiliza maneno ya watu wasemao, Tazama, Daudi anataka kukudhuru?

10 Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi Bwana alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA”.

Soma pia 1Nyakati 16:22

Hawa wote walikuwa ni watiwa mafuta lakni walikuwa na kasoro nyingi,  Lakini Yesu Kristo alikuwa ni mkamilifu kuliko hao wote..Kwahiyo yeye ndiye aliyetiwa Mafuta Makuu kuliko wote, ndio maana tunasema aliye Masihi peke yake ni YESU.

Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio”.

Kwahiyo Wayahudi wote, na wasamaria wote, walikuwa wanautazamia ujio wa huyu Masihi mmoja ambaye atakuwa mkamilifu, asiyekuwa na dhambi hata moja, ambaye atawafundisha sheria za Mungu na kuwaokoa na dhambi zao.

Yohana 4:25 “Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.

26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye”

Yohana 1:40 “Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.

41 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). .

Huyu Masihi Yesu Kristo, alishakuja miaka zaidi ya elfu 2 iliyopita, akapaa mbinguni, na sasa yupo hai, na pia amekaribia sana kurudi. Atakapokuja hatakuja tena kwa kusudi la wokovu, bali kwa HUKUMU.

Yohana 5:22 “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote”

Je umemwamini Masihi Yesu?.. Umetii agizo lake la ubatizo?, na je umempokea Roho wake Mtakatifu.. Fahamu kuwa kama umekosa vitu hivyo vitatu, bado hujaokolewa kulingana na Neno lake. Hivyo ni vyema ukafanya uamuzi wa kumwamini na kutubu leo na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu Kristo, na mambo mengine yaliyosalia Roho Mtakatifu utakayempokea atakuongoza katika kweli yote.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

ISHARA ITAKAYONENEWA

JUMA LA SABINI (70) LA DANIELI

Je tunaruhusiwa kujipaka mafuta au kujipulizia marashi?

 Je! Ni sahihi kutumia maji ya upako,katika kufanya maombezi?

IFAHAMU HUZUNI NA FURAHA YA MALAIKA.

Rudi nyumbani

Print this post

USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU UKAE NANYI NYOTE.

Je! Unataka Roho Mtakatifu afanye kazi vizuri ndani yako?

Fuatilia somo hili.

Maandiko yanasema..

2Wakorintho 13:14  “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote”

Unaweza kujiuliza ni kwanini, ofisi hizo kuu tatu za Mungu, zitajwe na sifa zao? Na si zenyewe tu kama zilivyo, (yaana Mungu, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu).. Bali kila mmoja inaelezewa na sifa yake pembeni, yaani ‘Pendo’ la Mungu, na ‘Neema’ya Yesu Kristo, na ‘Ushirika’ wa Roho Mtakatifu? Kwanini iwe hivyo?

Ni kwasababu Mungu anataka tujue kwa ukaribu tabia kuu iliyotenda kazi katika kila ofisi,

Kwamfano Anaposema Pendo la Mungu…Maana yake ni kuwa Palipo na upendo, Mungu yupo, hivyo kazi zote za Mungu(Baba), zinadhihirika kwa upesi sana pale ambapo pana upendo kwasababu maandiko yanasema kuwa yeye ni upendo..

Ukitaka umuone Mungu kama baba yako, basi hauna budi kuwapenda watu kwa moyo.

1Yohana 4:16  “Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake”.

Usipopenda maana yake ni kuwa Mungu(kama Baba), kamwe hatakaa ajidhihirishe kwako.

1Yohana 4:20  “Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona”

Halidhalika, maandiko yanasema.. “Neema ya Bwana Yesu Kristo, ikae nanyi nyote”. Ikiwa na maana kuwa Kristo yupo katika neema. Neema ni ile hali ya kutoa kitu ambacho mtu hajastahili kukipata. Kwamfano mtu anayefaulishwa, kwa kuhurumiwa na wakati hakusoma..Hiyo inatafsirika kama neema, ndicho Yesu alichokifanya sana akiwa duniani..

Kwanza aliacha enzi na mamlaka na uweza kule mbinguni, akaja duniani, ili kutupa sisi wokovu bure, bila kuusumbukia, akamwaga damu yake ili sisi tupate ondoleo la dhambi. Tukahesabiwa kuwa tumestahili uzima wa milele bure bila matendo. Kwaufupi Maisha yake yote yalikuwa yamejaa neema! neema! tu

Hivyo Kristo naye ili atembee na sisi, ni lazima nasi tuwe watu waliojaa neema kwa wengine.. Ndio maana akasema, ndugu yako akikukosa hata 7 mara 70, huna budi kumsamehe. Vilevile tujifunze kuachilia, na kutokuhukumu. Hivyo tukitaka tutembee kama Kristo duniani, basi tabia hii ni lazima tuwe nayo kwa wingi.

Lakini Pia maandiko yanasema..

‘Ushirika’ wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote” ..

Maana yake ni kuwa utendaji kazi mkuu wa  Roho Mtakatifu, upo katika ushirika.. Neno ushirika, limetokana na neno ushirikiano.  Anachotaka kwanza ni ushirikiano wetu sisi na Mungu, lakini zaidi sana ushirikiano wetu sisi kwa sisi (tuliokoka).

Kanisa la sasa tunakosa kuona nguvu za Roho Mtakatifu kwasasababu hatuna ushirikiano. Kila mmoja anatembea kivyake, kila mmoja ana nia yake, na matazamio yake binafsi. Hivyo basi Roho Mtakatifu anashindwa kufanya kazi kama anavyotaka. Tunamwita Roho Mtakatifu lakini haji kwasababu hatujui kuwa yeye yupo katika ushirikiano.

Siku ile ya Pentekoste, maandiko yanasema, kabla Roho Mtakatifu hajashuka, walikuwa kwanza mahali pamoja wote, wakidumu katika kusali.

Matendo 2:1  “Hata ilipotimia siku ya Pentekoste WALIKUWAKO WOTE MAHALI PAMOJA. 2  Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

3  Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

4  Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka”.

Hata baada ya pale, bado waliendelea kuwa wamoja, na kudumu katika nia moja.(Matendo 5:12)

Hivyo Roho Mtakatifu akatenda kazi sana miongoni mwa watu.

Hata sasa, ukitaka Roho Mtakatifu ajae kwa haraka sana ndani yako usiepuke, kuwepo katika ibada na wenzako, katika mikesha, katika maombi, katika ushirikia wowote mwema, hapo Roho Mtakatifu yupo sana, kwasababu yeye kiini chake ni ushirika. Ukitaka aitumie vizuri karama yako, hakikisha unakuwepo miongoni mwa kanisa, ili idhihirike, kwasababu haiwezi kudhihirika mahali ambapo upo peke yako.

Kwasababu vipawa hivyo yeye mwenyewe anasema anavitoa kwa lengo la  kuwakamilisha watakatifu, na kuujenga mwili wa Kristo (Waefeso 4:12), na si vinginevyo, Hivyo utaujengaje mwili wa Kristo endapo unajitenga na wenzako?

Kumbuka ofisi kuu, tuliyonayo sasa ni ya Roho Mtakatifu. Hivyo, tunamuhitaji sana ajae ndani yetu ili atuongoze katika kweli yote. Tukimzimisha, au tukimuhuzunisha, tutashindwa kumshinda shetani katika zama hizi za siku za mwisho.

Hivyo penda ushirika, penda umoja na watakatifu. Na Roho Mtakatifu atachukua nafasi yake juu yako.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JE! UMEPOKEA KWELI ROHO MTAKATIFU?

NITAUVUTAJE UWEPO WA ROHO MTAKATIFU KARIBU NAMI?

ZIFAHAMU KAZI TATU ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA ULIMWENGU.

Roho Mtakatifu ni nani?.

MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

Je! Unaweza kubatizwa na usipokee Roho Mtakatifu?. Na Je! Unaweza kupokea Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono?

USINIONDOLEE ROHO WAKO MTAKATIFU.

Rudi nyumbani

Print this post

Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali ni chukizo kwa BWANA.

SWALI: Nini maana ya huu mstari?

Mithali 20:10

[10]Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA.

JIBU: Ni mstari unaolenga ubadhilifu katika biashara au maisha…kwamfano labda mtu ni muuzaji wa mchele..na kwenye duka  lake anakuwa na mawe mawili ya mizani…moja la haki na lingine lenye uzito wa chini kidogo..hivyo akija mtu kumuuzia anampimia kwa lile jiwe la uzani wa chini, ili yeye abakiwe na kingi..

Au mwingine ni muuzaji wa mkaa, lile kopo la kipimo analibonda bonda ili lisichukue mkaa mwingi…sasa haya yote ni machukizo kwa Bwana..ndio hapo maandiko yanasema.. “Vipimo mbalimbali, na pishi mbalimbali, Vyote viwili ni chukizo kwa BWANA”.

Udanganyifu katika biashara ni tatizo sugu, na lipo katika nyanja mbalimbali pia kwamfano …utakuta mtu anauza maziwa ya ng’ombe, sasa ili apate faida kubwa zaidi anatia maji ili yawe mengi, kisha anauza…hayo ni machukizo..

Mwingine ni mama ntilie, ananunua sahani ndogo, au vikombe vidogo ili auze chai kidogo kwa bei ileile ya sikuzote apate faida kubwa.

Vilevile kuonyesha upendeleo kwa wengine ni machukizo kwa Mungu, kwasababu hivyo navyo ni vipimo mbalimbali. Labda ni muhuguzi, ambaye anawaongoza watu katika foleni ya kumwona daktari, anapokuja mtu wake wa karibu au mwenye pesa, anampitisha mlango wa nyuma, hamweki kwenye foleni.

Hivyo Bwana anatutaka tuwe watu wa usawa na wa haki. Kwasababu na yeye pia ni Mungu wa haki

shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Majina mbalimbali ya Mungu na maana zake.

VIPIMO MBALIMBALI VYA KIBIBLIA.

Maana Ya Maneno Katika Biblia.

Tofauti kati ya kuhukumu na kulaumu ni ipi?

Kuhimidi ni nini?(Zaburi 31:21)

JINSI EDENI ILIVYOKUWA.

Rudi nyumbani

Print this post

SALA YA BWANA. (Namna ya kuiomba)

Sala ya Bwana ni sala ambayo Bwana wetu Yesu Kristo aliwafundisha wanafunzi wake, kabla ya kuondoka kwake. Na kwa kupita sala ile, hakuwafundisha tu wanafunzi wake bali alitufundisha na sisi pia, maana yake ni kwamba, nasi pia tunapaswa tuombe kama vile Bwana alivyowaelekeza wanafunzi wake.

Lakini ni muhimu kuielewa sala hii kwa mapana, ili kusudi tuisikose shabaha tunapoomba.. Kwa maana tusipoielewa vizuri basi tutajikuta tunaifanya kama Mashairi (kwa kuirudia rudia kama watu wa mataifa, wanavyofanya wanapoiomba miungu yao).. Sisi biblia imetuambia tusifanane na hao.(Mathayo 6:7).

Sasa sala ya Bwana Imegawanyika katika vipengele vikuu nane (8).. Na vipengele hivyo sio sala yenyewe bali ni kama “maelekezo ya sala”. Sala yenyewe hatuwezi kuandikiwa, bali tunaomba kila mtu kulingana na anavyoongozwa au kujaliwa na Roho Mtakatifu.

Ni sawa mtu akupe vipengele saba vya kuombea, akakuambia ombea Familia, ombea Taifa, ombea Kanisa, ombea Marafiki.. Sasa kwa kukwambia hivyo huwezi kwenda kupiga magoti na kusema naombea Taifa, kanisa, ndugu na marafiki halafu basi uwe umemaliza!, Huwezi kufanya hivyo.. bali utakachofanya ni kuzama ndani kwa kila kipengele kukiombea..

Kwamfano Katika kipengele cha kuombea Taifa utaombea Viongozi wote na Hali, na hali ya Taifa, na  ya Imani kwa ujumla katika Taifa zima, jambo ambalo linaweza kuchukua dakika kadhaa au masaa kadhaa, vile vile katika Familia, na katika kanisa utafanya hivyo hivyo..zitahitajika dakika nyingi kwasababu  kuna watu wengi katika familia, na kuna matatizo mengi ambayo ukianza kuyataja mbele za Mungu, huenda yakachukua dakika nyingi au masaa mengi.. Hivyo kwa vipengele tu hivyo vichache unaweza kujikuta unasali hata masaa 6.

Vile vile katika sala ya Bwana, ni hivyo hivyo,  vile alivyoviorodhesha Bwana ni vipengele tu, na sio sala yenyewe, maana yake Mitume hawakuchukua hiyo sala na kuikariri kama shairi na kisha kuirudia rudia kila wakati kabla na baada ya kulala, kama inavyozoeleka leo kufanyika hivyo.

Sasa hebu tuisome sala yenyewe na kisha tutazame kipengele kimoja baada ya kingine.

Mathayo 6:7 “Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

8 Basi msifanane na hao; maana BABA YENU ANAJUA MNAYOHITAJI KABLA NINYI HAMJAMWOMBA.

9 BASI NINYI SALINI HIVI; BABA YETU ULIYE MBINGUNI, JINA LAKO LITUKUZWE, UFALME WAKO UJE,

10 MAPENZI YAKO YATIMIZWE, HAPA DUNIANI KAMA HUKO MBINGUNI.

11 UTUPE LEO RIZIKI YETU.

12 UTUSAMEHE DENI ZETU, KAMA SISI NASI TUWASAMEHEVYO WADENI WETU.

13 NA USITUTIE MAJARIBUNI, LAKINI UTUOKOE NA YULE MWOVU. [KWA KUWA UFALME NI WAKO, NA NGUVU, NA UTUKUFU, HATA MILELE. AMINA.]”

1.BABA YETU ULIYE MBINGUNI

Hiki ni kipengele cha kwanza, ambacho Bwana anatuelekeza tuanze nacho katika sala zetu. Kwamba maombi yetu tuyaelekeze kwa Baba aliye mbinguni, kwamba tumwite Baba asikie maombi yetu na haja zetu, na yeye ni mwaminifu atatupa kama tutakavyomwomba, ikiwa tutaomba sawasawa na mapenzi yake.

Na jambo la kuzingatia hapo ni kwamba Bwana Yesu anatufundisha kuomba kwa “Baba” na sio  kwa “Mungu”. Sasa Baba ndio huyo huyo Mungu, lakini cheo cha ubaba kinahubiri mahusiano mazuri zaidi kwetu na aliyetuumba kuliko cheo cha UMUNGU.  Viumbe vyote vinamwona muumba kama Mungu, lakini kwetu sisi wanadamu tumepewa heshima ya kipekee kwamba tumwite Mungu, Baba yetu (1Yohana 3:1).

Kwahiyo tunapoingia kwenye sala/ maombi ni vizuri sana kuomba kwa kumwita muumba wako Baba kuliko Mungu, kwasababu wewe ni zaidi ya kiumbe chake bali ni mtoto wake.

Luka 11:11 “Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?

12 Au akimwomba yai, atampa nge?

13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?”

2. JINA LAKO LITAKASWE/ LITUKUZWE

Baada ya kumwita Baba aliye mbinguni kwamba atege sikio lake na kusikia maombi yetu sisi watoto wake, Hoja ya kwanza tunayopaswa tumpelekee ni kwamba JINA LAKE LITAKASWE au LITUKUZWE. Wengi hawajui kuwa jina la Mungu linachafuliwa kila siku kutokana na maovu watu wa Mungu wanayoyafanya..

Warumi 2:22 “Wewe usemaye kwamba mtu asizini, wazini mwenyewe? Wewe uchukiaye sanamu, wateka mahekalu?

23 Wewe ujisifuye katika torati, wamvunjia Mungu heshima kwa kuiasi torati?

24 KWA MAANA JINA LA MUNGU LATUKANWA KATIKA MATAIFA KWA AJILI YENU, kama ilivyoandikwa”.

Madhara ya jina la Mungu kutukanwa katika mataifa, ni watu wengi kupotea na kuifanya thamani ya msalaba isionekane.. Hivyo basi mwenye uwezo wa kulitakasa jina lake ni Mungu tu, (yeye mwenye jina), hivyo tunapochukua nafasi hiyo ya kuomba kwamba Bwana alitakase jina lake, maana yake tunaomba Mungu alete utukufu katika Injili yake.. Kwamba Bwana ajalie watu kuliogopa jina lake, kwa kuonyesha matendo makuu na ya ajabu, na hivyo wengi kutubu na kumrudishia yeye utukufu.

Kwahiyo hii inapaswa iwe sehemu ya sala kwa kila mkristo kila mahali..

3. UFALME WAKO UJE.

Siku ambayo Ufalme wa Mungu utakuja duniani ni siku ambayo Mateso yatakuwa yameisha, tabu zitakuwa zimeisha, huzuni zitakuwa zimeisha, na maumivu yatakuwa yameisha.. (hakika huo ni wakati mzuri sana). Dunia ya sasa imejaa tabu na mahangaiko na majaribu mengi.. hivyo kila siku hatuna budi kuomba kwa Baba kwamba aharakishe kuileta ile siku ambayo tutapata pumziko la hakika, dhidi ya haya majaribu mengi ya ulimwengu.

Kwa mtu ambaye anatamani kuondokana na haya maisha na kutamani kukaa na Mungu milele, basi atatumia muda wa kutosha kumwomba Bwana aulete ufalme wake. Na kwa kuomba hivi maana yake, tunaomba pia watu wengi waokolewe, kwasababu ile siku haitakuja mpaka kondoo wa mwisho aliyekusudiwa uzima wa milele, aingie ndani ya zizi.. Hivyo basi kwa kuomba ufalme wake uje basi moja kwa moja pia tutakuwa tumeomba Bwana aharakishe kuwavuta watu wake ndani ya Neema.

4. MAPENZI YAKO YATIMIZWE.

Baada ya kuomba kwamba ufalme wake uje, basi hatua inayofuata ni kuomba kwamba Mapenzi yake yatimizwe.. Tunayo mapenzi yetu (yaani matakwa yetu), lakini pia yapo mapenzi ya Mungu ambayo huwenda sisi hatuyafahamu.. Bwana Yesu kabla ya kuteswa alimwomba Baba na kusema, “kikombe hiki kiniepuka lakini si kama nitakavyo mimi bali utakavyo wewe  soma Mathayo 6:39.

Na sisi hatuna budi kuomba kuwa mapenzi ya Mungu yatimizwe hapa duniani, katika shughuli zetu, katika utendaji kazi wetu, na katika mambo yote yanayoendelea, mapenzi yake yakatimizwe kama yanavyotimizwa huko mbinguni, mahali malaika walipo..

5. UTUPE LEO RIZIKI ZETU.

Baada ya kuomba mapenzi yake yatimizwe, sasa ni wakati wa sisi kupeleka haja zetu, kama chakula, mavazi, makazi, fedha, na mambo yote tunayoyahitaji katika mwili na katika roho, Baba akatupatie.. Na Mungu anayesikia maombi atatupa kama ni fedha, au chakula au makazi au malazi, vile vile katika kipengele hiki ndicho kipengele pia cha kuwaombea wengine Bwana awape pia riziki, hivyo kinaweza kuchukua muda mrefu, kulingana na haja mtu alizonazo.

6. UTUSAMEHE DENI ZETU.

Ipo tofauti ya Deni na dhambi,  Mtu anaweza kusamehewa dhambi lakini Deni la adhabu lipo palepale, Daudi alisamehewa dhambi yake ya kumtwaa mke wa Uria, lakini deni la kuadhibiwa yeye na mtoto wake halikuondoka, na hapa sala ya Bwana inatuelekeza kwamba tumwombe Bwana atusamehe Deni zetu, huenda tumemkosa Mungu na tukamwomba msamaha na yeye akatusamehe lakini adhabu bado hajaiondoa.. hivyo hatuna budi kumwomba Mungu kwa kuugua sana kwamba atuondolee dhambi zetu pamoja na madeni yetu,

Hapa mtu anaweza kutumia muda mrefu, kujiombea mwenyewe na kuwaombea wengine. Lakini tunapoomba tusamehewe madeni ni sharti kwamba na sisi tuwasamehe wadeni wetu, tusipowasamehe wadeni wetu na Baba yetu aliye mbinguni hatatusamehe sisi.

7. USITUTIE MAJARIBUNI, BALI UTUOKOE NA YULE MWOVU.

Shetani anatutafuta usiku na mchana ili atuingize katika kukosa, sasa hila zote za shetani ili kutuangusha sisi ndio “majaribu yanayozungumziwa hapo”

Bwana anatufundisha kumwomba Baba, atuepushe na mitego hiyo ya mwovu, ambayo kaiweka kila mahali ili kutuangusha, na mitego hiyo shetani kaiweka makanisani, mashuleni, makazini na kila mahali.. hivyo lazima kuomba kwa muda mrefu kwaajili ya mahali ulipo, au unapokwenda ili kusudi usianguke katika mitego ya ibilisi. Na pia unapaswa uwaombee na wengine. (Wagalatia 6:2).

8. KWA KUWA UFALME NI WAKO, na Nguvu na Utukufu

Hii ni hatua ya mwisho ya kumtukuza Mungu na kumwadhimisha, na kumshukuru..hapa mtu anaweza kupaza Sauti yake kama Daudi kwa nyimbo au kwa kinywa na kusema  Bwana ni mwenye Nguvu, asikiaye maombi , ajibuye maombi..Bwana ni mwenye haki, Bwana ni mwenye enzi na mamlaka..utukufu una yeye milele na milele.

Tukisali kwa namna hiyo, au kwa ufunuo huo basi tutakuwa tumeomba sawa sawa na mapenzi yake.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Kuna tofauti gani kati ya SALA na DUA?

SALA YA UPONYAJI/MAOMBI YA UPONYAJI.

NITAJUAJE KAMA MAOMBI YANGU YAMEFIKA (YAMEJITOSHELEZA)?.

KUNA AINA NGAPI  ZA MAOMBI?

JINSI SHETANI ANAVYOZUIA MAJIBU YA MAOMBI YETU.

Rudi nyumbani

Print this post

WANAWAKE WAOMBOLEZAJI

(Masomo maalumu kwa wanawake)

Wanawake waombolezaji maana yake nini?, Na je hadi leo wapo?, au wanapaswa kuwepo?.

Kabla ya kuingia ndani kuhusiana na wanawake waombolezaji, hebu tujue kwanza maana ya neno kuomboleza.

Kuomboleza maana yake “ni kuingia katika sikitiko kuu, kutokana na tukio ambalo limetokea au litakalotokea!”.. Sikitiko hili linaambatana na Toba, na Majuto.

Kwamfano mtu anayeomboleza kutokana na msiba alioupata anakuwa katika hali ya huzuni kuu, akitafakari kwa undani tukio lililotokea huku akiomba rehema na msamaha kwa Mungu, na huku akiomba Mungu amponye majeraha yake na pia akiomba jambo kama hilo lisijirudie tena, (huyo ndio mtu anayeomboleza kibiblia kutokana na tukio lililotokea).Na mtu anayeomboleza kwajili ya tukio lijalo pia anakuwa katika hali hiyohiyo.

Hebu tuangalie mifano ya watu walioomboleza kabla ya tukio Fulani/msiba Fulani kutokea na watu walioomboleza baada ya Tukio kutokea.

1.KABLA YA TUKIO.

Mfano wa watu waolioomboleza kabla ya Msiba kutokea ni wana wa Israeli kipindi cha Malkia Esta, wakati ambapo waraka wa kuuawa wayahudi uliposomwa katika majimbo yote ya Mfalme Ahasuero, ambapo uliasisiwa na Hamani, aliyekuwa adui wa wayahudi.

Lakini tunasoma mara baada tu ya waraka ule kutolewa, Wayahudi wote wakiongozwa na Mordekai walifunga, kwa kulia na kuomboleza.

Esta 4:1 “Basi Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.

 2 Pia akafika hata mbele ya mlango wa mfalme; maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa magunia. 

3 Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake imewasili, PALIKUWAKO MSIBA MKUU KWA WAYAHUDI, NA KUFUNGA, NA KULIA, NA KUOMBOLEZA; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu”

Na matokeo ya maombolezo haya ni USHINDI KWA WAYAHUDI, na Mauti kwa maadui zao.

2. BAADA YA TUKIO.

Mfano wa maombolezo ambayo yalifanyika baada ya tukio Fulani/msiba Fulani kutokea ni yale ya NABII YEREMIA.

Baada ya wana wa Israeli, kuuawa kikatili na Mfalme Nebukadreza na baadhi yao kuchukuliwa mateka mpaka Babeli, tukio hilo lilikuwa ni tukio baya ambalo halikuwahi kutokea kama hilo katika Israeli, kwani wanawake wajawazito walipasuliwa matumbo yao, na vijana na wazee walichichwa kikatili pale Yerusalemu, na zaidi sana kundi dogo lililosalia lilipelekwa utumwani kwa aibu, kwani walikuwa uchi kabisa na wengine nusu uchi. Na wachache sana ambao walikuwa ni maskini na walemavu ndio waliobakishwa Israeli ili wayatunze mashamba.

Sasa miongoni mwa waliobaki alikuwa ni Yeremia, yeye hakuwa maskini wala mlemavu, lakini Mungu alimlinda na maangamizi hayo kwasababu alikuwa anamcha yeye,  Kwasababu hiyo basi YEREMIA, baada ya kulishuhudia tukio hilo, alilia kwa machozi mengi na kuomboleza siku nyingi.. (na ndio akaandika maombolezo yake katika kitabu, ambacho ndio sisi leo tunakisoma kama kitabu cha Maombolezo).

Maombolezo 3:47  “Hofu imetujilia na shimo, Ukiwa na uharibifu. 

48 Jicho langu lachuruzika mito ya maji Kwa ajili ya uvunjifu wa binti ya watu wangu. 

49 Jicho langu latoka machozi lisikome, Wala haliachi; 

50 Hata Bwana atakapoangalia Na kutazama toka mbinguni. 

51 Jicho langu lanitia huzuni nafsini mwangu, Kwa sababu ya binti zote za mji wangu.

 52 Walio adui zangu bila sababu Wameniwinda sana kama ndege”

Sasa ni Maombolezo gani kati ya hayo mawili, Mungu anayotaka sisi tuyafanye??

Jibu ni “Maombolezo ya kabla ya tukio”. Mungu hataki tuomboleze baada ya tukio, bali anataka tuomboleze kabla ya tukio..

Leo hii dunia tayari imeshatamkiwa hukumu na Mungu, huenda Taifa lako limeshatamkiwa hukumu, huenda familia yako imeshatamkiwa hukumu na Mungu, huenda Nyumba yako imeshaandikiwa hukumu na Mungu, kutokana na mambo yanayoendelea humo yasiyompendeza yeye.

Huenda Kanisa lako limeshaandikiwa hukumu, washirika wenzako wameshaandikiwa hukumu, mchungaji wako kashaandikiwa na kashakusudiwa kuadhibiwa na Mungu hapa hapa duniani kabla hata hajaondoka..Hivyo kabla hukumu hizo hazitimia, Bwana Mungu anataka tuwe na jicho la kuona na KULIA NA KUOMBOLEZA KWA TOBA NA MSAMAHA, NA KWA KUTAKA REHEMA kwa Mungu ili Mabaya haya yasitokee, Kama Akina Esta, Mordekai na Wayahudi wote walivyofanya kipindi cha Hamani.

Sasa pamoja na hayo, lipo kundi moja la Watu, ambalo  ni rahisi kuzama katika Maombolezo na hata kuvuta rehema za Mungu, na fadhili za Mungu upesi.

Na kundi hilo si lingine zaidi ya kundi la Wanawake.. Mwanamke anapoomba kwa hisia (iliyo ya kiMungu), basi ni rahisi maombi yake kufika kwa Baba mbinguni zaidi ya wanaume.. Hivyo biblia imewataja wanawake kama viungo vifaavyo kusimama katika hii nafasi ya kuomboleza.

Hebu tulithibitishe hili kimaandiko…

Yeremia 9:17 “Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; 

18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji. 

19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu”. 

Umeona Nafasi yako wewe mwanamke?..Wewe umewekwa na Mungu katika hilo kanisa ili ulie na kuomboleza kwaajili ya Uovu, ili Bwana akumbuke rehema, wewe umewekwa katika hilo Taifa ili ulie na kuomboleza Bwana aachilie neema na rehema.. Hiyo ndio nafasi yako ambapo usipoitumia siku ile utakwenda kuulizwa!!.

Biblia haijashindwa kuwaweka hapo wanaume, na kusema wao ndio waomboleze!!.. lakini imewaweka pembeni na kuwapa vipaumbele wanawake!..Sasa sio kwamba ina upendeleo haina upendeleo..bali ni kutokana na jinsi wanawake walivyoumbwa!.. Kadhalika mwanamke usikimbilie kuwa mchungaji, hiyo ni nafasi ya wanaume..(kasome 1Wakorintho 14:34). Kwahiyo biblia imetoa majukumu kwa kila jinsia..

Je umewahi kulia na kuomboleza kwaajili ya Nyumba yako, au kanisa lako au Taifa lako? Kama bado halafu wewe ni mwanamke unayesema umeokoka, basi badilika leo.. Litii Neno na lifuate hilo, usijiamulie utumishi au usijitwike wito ambao hujawekewa juu yako.. kaa katika nafasi yako hiyo na Mungu atakutumia.

Na baada ya kujua nafasi yako hii basi wafundishe na wanawake wengine kuwa kama wewe (mwombolezaji)..ndivyo biblia inavyoelekeza..

Yeremia 9:20 “Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.

  21 Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu”.

Bwana akubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

TUKIO LA MUSA NA ELIYA KUMTOKEA BWANA, LIMEBEBA UJUMBE GANI?

NAFASI YAKO NI IPI KATIKA MWILI WA KRISTO?

MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.

Kwanini wanawake wengi huwa wanalipuka mapepo?

Sadaka ya Moyo ipoje? (Walawi 22:21).

Rudi nyumbani

Print this post

BWANA UNIJULISHE MWISHO WANGU.

Karibu tujifunze biblia..

Daudi anasema..

Zaburi 39:4 “Bwana, unijulishe mwisho wangu, Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani……..”

Hapa si kwamba Daudi anataka aijue siku ya kufa kwake!, Hapana!, Mungu hajawahi kumwahidia mwanadamu hayo maarifa..(Hakuna maombi ya mtu kufunuliwa siku yake ya kufa).  Bali hapo Daudi anaomba Mungu ampe KUZIJUA SIKU ZAKE DUNIANI KWAMBA SI NYINGI, Kwamba siku za mwanadamu ni kama maua! Si wa kudumu (Zaburi 103:15).

Hivyo Daudi alijua Mungu akimpa moyo wa kuelewa kuwa “Yeye ni kama mpitaji tu hapa duniani, na siku zake si nyingi”.. basi atakuwa mnyenyekevu zaidi, na ataishi maisha ya kumtafuta Mungu, kumcha Mungu na kuishi kwa hekima duniani..

Zaburi 90:12 “Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima”.

Na sio tu yeye aliyepaswa kuomba maombi kama haya, bali hata sisi pia watu wa siku za Mwisho, ni lazima tumwombe Mungu atujulishe siku zetu! (Yaani atupe mioyo ya hekima kujua kuwa sisi ni wapitaji tu, na siku zetu za kuishi si nyingi).

Faida ya kuomba Moyo huu kutoka kwa Mungu, ni kwamba tutakuwa watu wa kutazama maisha yajayo zaidi kuliko maisha haya ya hapa duniani ya kitambo!.. Kwasababu ndani ya akili zetu tutajua kuwa siku zetu si nyingi!..kwamba siku yoyote safari ya maisha yetu itafikia mwisho.

Watu wengi wenye huu moyo, utaona ndio watu wenye mioyo ya kumtafuta Mungu kwa kujikana nafsi kwelikweli…ndio watu wenye mioyo ya kusaidia wengine, ndio watu wenye mioyo ya kuwahubiria wengine mwisho wa maisha haya.

Na watu kama hawa, hata kama wakiambiwa kuwa watapewa miaka elfu moja ya kuishi duniani, bado tu!, watajiona kuwa siku zao ni chache, kwasababu tayari ndani yao wamepewa mioyo ya “kuzihesabu siku zao na kujijua kuwa wao si kitu, ni kama maua tu, yaliyopo leo na kesho kutupwa kwenye tanuru” hivyo maisha yao yatakuwa ni yale yale siku zote ya kutafuta kutengeneza maisha yajayo ya umilele.

Shetani hapendi watu wawe na moyo huu, anataka watu wawe na moyo wa kufikiri kwamba wataishi milele katika hii dunia, hataki watu wajue kwamba siku yoyote safari ya maisha yao itafikia ukingoni, kwasababu anajua watu wakilijua hilo, basi watatengeneza maisha yao hapa kwaajili ya huko waendako, na hivyo atawapoteza wengi. Na yeye (shetani) hataki kumpoteza mtu hata mmoja, anataka wote waende katika ziwa la moto kama yeye!!.

Kwahiyo kila siku ni muhimu sana kuomba Bwana atupe huu moyo.. “Atujulishe miisho yetu, na siku zetu za kuishi” ili tufahamu kuwa “sisi ni wapitaji tu”.

Moyo huu utaupata kwa kufanya mambo yafuatayo matatu (3)

1.Kwa kuomba

Majibu ya mambo yote tunayapata katika maombi, kama vile Sulemani alivyoomba kwa Mungu apewe moyo wa hekima na Mungu akamsikia, vile vile pia Moyo wa kujua kuwa wewe ni mpitaji tu, unatoka kwa Bwana, ndio maana hata hapo Daudi anaonekana kama anaomba.. “Bwana nijulishe”..Na wewe siku zote sema “Bwana nijulishe”

2. Kwa kutafakari matukio ya vifo yanayotokea.

Unapotenga muda wa kutafakari matukio ya Ajali yanayotokea, au unapotazama wagonjwa mahututi, au unapokwenda kwenye nyumba za misiba..sehemu hizo ni sehemu ambazo Mungu anaitengeneza mioyo ya wengi.. Hivyo na wewe huna budi kuhudhuria misiba, au kufuatilia matukio (Wengi hawapendi kufuatilia haya), kwasababu hawataki kuumia moyo, lakini ndani ya mioyo yao wana viburi vya maisha, wanajiona kama wao wataishi milele.. Biblia inatufundisha pia tuhudhurie sehemu za Misiba, sio kwenye karamu tu, ili tukajifunze huko..

Mhubiri 7:2 “Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake. 

3 Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo”.

3. Kwa kusoma Neno.

Unaposoma Biblia, huko ndiko utakapopata Maarifa kamili ya Neno la Mungu, na maneno ya kuunyenyekeza moyo wako, biblia ndio kioo kamili cha kujijua wewe ni nani?.. ukitaka kujijua wewe ni mtu wa namna gani, basi soma Biblia.

Bwana atubariki.

Maran atha!

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

KWA MIOYO YAO WAKAREJEA MISRI.

Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?

REKEBISHA YAFUATAYO ILI UCHUMI WAKO UKAE SAWA.

Je mwanamke anaruhusiwa kupanda madhabahuni akiwa katika siku zake?

Rudi nyumbani

Print this post

Nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho,

SWALI: Mtume Paulo alikuwa na maana gani kusema..

Wakolosai 2:5  “Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo”

Je! Kwasasa kauli hii inasimama katika mazingira gani?

JIBU: Katika mazingira ya kibinadamu kuna wakati inatokea, hutakuwa karibu na watakatifu wenzako kimwili, pengine kwasababu kadha wa kadha, lakini biblia bado inatoa tumaini kuwa hali hiyo ni kweli inaweza kuathiri mwili , lakini roho bado ikawa pale pale inashiriki neema na Baraka kana kwamba hukuondoka, lakini hiyo yote mpaka ifikiwe zipo taratibu zake..

Inahuzunisha kuona Neno hili linachukuliwa juu juu.. Utaona watu wanatoa udhuru zao, halafu mwishoni wanamalizia na hili Neno “Kimwili sipo nanyi, lakini nitakuwa nanyi kiroho” Wakidhani kuwa ni rahisi kiivyo.

Embu tuangalie Paulo aliyesema haya maneno kwa Wakolosai alichochewa na nini mpaka akapata ujasiri wa kusema vile..

1) Ni kwasababu ya vifungo vyake ndio maana alishindwa kuwa karibu na kanisa la wakolosai:

Alilisisitiza hilo mwishoni kabisa mwa waraka wake akasema..

Wakolosai 4:18  Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi

Maana yake ni kuwa kama isingekuwa ni vifungo vile, kulikuwa hakuna udhuru wowote wa yeye kutokuwepo katika mwili na watakatifu. Lakini leo, watakatifu hawapo magerezani, wapo bize na kazi wanasema nimetingwa siwezi kuja kanisani, Hawapo nje ya mikoa au nchi, wapo mtaa wa pili lakini wanasema, kanisani ni mbali, nitakuwa nanyi kiroho. Hapo usijidanganye ndugu, hakuna muunganiko wowote ulio nao wa watakatifu wenzako..Upo nje ya kundi.

2) Alikuwa anawaombea sana kwa dua na sala:

Anasema..

Wakolosai 1:9  Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni.

Japokuwa alikuwa vifungoni, lakini hakupotelea moja kwa moja huko, lakini alifanya bidii kila siku usiku na mchana, kuwaombea ndugu zake aliombali nao. Akiwaombea waimarike, wajazwe maarifa na hekima. Lakini ni mara ngapi, mpendwa mmoja akihama mkoa, au akisafiri nje ya kanisa, ndio anasahau kabisa kuliombea kanisa lake, Hapo Paulo aliliombea kwa Dua..Dua ni maombi ya kuzama ambayo yanaambatana na kufunga na kuomboleza kwa kipindi kirefu. Je na sisi tunafanya hivyo tuwapo mbali?

Na kwa kawaida mtu wa namna hii, atampenda Mungu hata na kwa matoleo yake, na dhabihu, kwa ajili ya kanisa lake. Kwasababu maandiko yanasema, hazina yako ilipo ndipo utakapokuwepo na moyo wako (Mathayo 6:21).

3) Alikuwa akiwaulizia mienendo yao, na kuwapelekea ndugu wa kuwaimarisha

Wakolosai 4:7  Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mjoli wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote; 8  ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu; 9  pamoja na Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu. Hao watawaarifu mambo yote ya hapa petu.

Zaidi sana alikuwa anawaandikia nyaraka kama hizi, pamoja na kuwatumia za makanisa mengine wazisome, ili waimarike,(Wakolosai 4:16). Je! Na sisi tunaweza kuwa wafuatiliaji wa wapendwa wetu tuliowaacha nyuma? Au tutaliachia kanisa la kule lihusike lenyewe. Kwani wewe si haupo, ya nini tena, kuwaandikia waraka? Lakini Paulo hakuwa hivyo, alijitahidi kutumia karama yake hata kwa kuandika waraka, akiwa huko huko mbali lengo lake likiwa ni karama yake iifaidie kanisa.

.

4) Alikuwa tayari kutoa ripoti na changamoto zake na maendeleo yake katika huduma:

Wakolosai 4:10-13,14 

“Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni. 11  Na Yesu aitwaye Yusto; hao ni watu wa tohara. Tena hao peke yao ni watendaji wa kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao walikuwa faraja kwangu. 12  Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu……

14  Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.”

Hakujificha, wala hakufanya mambo yake kwa siri, kanisa la Kolosai lilikuwa linafahamu kwa kina maendeleo ya kiroho ya Paulo, kwasababu Paulo mwenyewe alikuwa tayari kueleza wazi. Hakusubiri kufuatiliwa, lakini sasa kigezo cha watu kuwa mbali, ndio sababu ya kutokueleza maendeleo yao, wanapotea kabisa. Hapo hakuna muunganiko wowote.

Hivyo baadaya ya yeye kuyatimiza hayo ndipo sasa Roho Mtakatifu akamshuhudia aandike waraka ule kwamba japokuwa yupo nao mbali kimwili lakini kiroho yupo nao.

Hata sasa, mtu yeyote aliyembali na kanisa anayekidhi vigezo hivyo vyote, rohoni anakuwa hana tofauti na kama tu yupo pale. Hivyo wakibarikiwa wenzake na yeye atabarikiwa, wakipata neema na yeye atapata, Lakini kama atapoteza sifa hizo, haijalishi atatamka kwa maneno mazuri namna gani, hayupo kiroho na wenzake. Na hivyo hawezi shiriki chochote kitokacho kwa Mungu.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

AMEFANYIKA BORA KUPITA MALAIKA!

Nini maana ya kuabudu malaika? (Wakolosai 2:18)

Maongeo ni nini?(Wakolosai 2:19)

Uasherati wa Kiroho ni nini?

EPUKA MAKUNDI ILI UTAKATIFU WAKO UDUMU!.

KUMJUA YESU SI KUPATA UZIMA WA MILELE.

KUTII NI BORA KULIKO DHABIHU.

Rudi nyumbani

Print this post