SWALI: Biblia inaposema “Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake”, ina maana gani?
Isaya 53:5 “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.
JIBU: Ili kuelewa neno hilo, wazia mfano huu; Mtu mmoja ameshitakiwa na mahakama kwa kosa la uchafuzi wa mazingira, hivyo, akapewa adhabu ya kulipa faini ya sh. Milioni 5 ndani ya wiki 3, au jela miaka 3. Sasa ikatokea mtu huyu akawa hana cha kulipa,.. Unadhani atakuwa katika hali gani? Ni wazi kuwa atapoteza amani yote, hawezi kuwa katika furaha, hawezi kuwa katika raha wakati wote huo kwasababu anajua hukumu ya kifungo ipo mbele.. Ili amani yake irudi, hana budi apate kiwango hicho alipe. Lakini akatokea mtu, akasema mimi nitakuchukua adhabu hiyo nitamlipia deni lake. Bila shaka furaha na amani ya yule mdaiwa itarejea tena.
Hivyo tunaweza kusema, ili kuirejesha ile amani yake ya mwanzo, alikuwa hana budi kutumikia adhabu kwanza..
Sasa tukirudi katika huo mstari ..biblia inaposema;
Huyo ni Bwana Yesu anayezungumziwa hapo, sasa anaposema, Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”. Ni kwamba ili sisi kuipokea Amani yetu, tuliyoipoteza tangu kule edeni, ilitupasa kwanza tutumikie adhabu ya makosa.. Lakini ashukuruwe Kristo kwasababu alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, akapigwa na kuteswa ili sisi tupone. Adhabu ya amani yetu aliichukua yeye.
Na ndio maana Warumi 8:1 inasema; “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu”.
Ukiwa ndani yake, amani yako inarejeshwa bila kulipa gharama yoyote. Lakini inastaajabisha kuona bado wapo watu hawataki kulipiwa deni zao. Wakidhani kuwa wataweza kustahimili hukumu ya Mungu siku ile. Ndugu ikiwa upo nje ya Kristo huna tumaini lolote. Ukifa ni moja kwa moja jehanamu kwenye ziwa la moto. Adhabu yako ni Mauti katika lile ziwa la moto milele.
Hiyo ndio sababu kwanini unamuhitaji Yesu Kristo leo, kwasababu ukishakufa leo hakuna tumaini, wala huna matendo yoyote ya kumshawishi Mungu, afute dhambi zako. Wasubiri nini, usimgeukie Bwana Yesu akusafishe Maisha yako angali ukiwa hai? Tubu sasa mpokee yeye. Muda ni mchache.
Maran Atha.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;
Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Mada Nyinginezo:
KAMA SI YESU, HABARI YETU INGEKUWA IMEISHA ZAMANI SANA.
BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?
Je Mungu ana njia ngapi za kuzungumza?
Sadaka ya Amani ilikuwaje?
Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?
Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa watoto wake wote.
Rudi nyumbani
Print this post
SWALI: Naomba kufahamu maudhui ya mstari huu,
1Timotheo 1:20 “Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu”.
JIBU: Awali ya yote, kabla ya kufahamu ni kwanini Mtume Paulo anatoa hukumu kali kama hiyo tuangalie mistari ya juu yake ambayo inaeleza sifa, za hao watu.
Ukisoma mstari wa 19, Paulo anamuasa Timotheo, awe ni mtu mwenye Imani, lakini sio Imani tu, bali pia “dhamiri njema”.. Ni vitu vinavyokwenda sambamba.
1Timotheo 1:19 “uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.20 Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.”
1Timotheo 1:19 “uwe mwenye imani na dhamiri njema, ambayo wengine wameisukumia mbali, wakaangamia kwa habari ya Imani.
20 Katika hao wamo Himenayo na Iskanda, ambao nimempa Shetani watu hao, ili wafundishwe wasimtukane Mungu.”
Dhamiri ni kile kitu cha ndani kinachomshuhudia mtu kwamba anachokifanya ni sahihi au sio sahihi. Hivyo pale mtu anapokuwa na dhamiri njema, maana yake ni kuwa, anaitii nafsi yake, inapofanya kosa, pale inaposuta, anakuwa tayari kugeuka. Hivyo mtu kama huyu huwa anaishi kwa kujichunga, na kuwahurumia na kwa kuogopa hukumu pale anapojaribu kuwapotosha watu.. Kwasababu dhamiri yake njema inamshitaki.
Lakini mtu ambaye hana dhamiri njema, ni kwamba, hata anapoona jambo Fulani alifanyalo ni baya, anastahili hukumu, yeye hajali, bali anafanya atakalo, kwa maslahi yake. Atakuwa tayari kuwafundisha watu mafundisho potofu kwa makusudi kabisa akijua kabisa alifanyalo ni upotevu, lakini yeye ataendelea kufanya, kwa furaha kabisa..
Sasa ndio hapo mtume Paulo, anawatolea mfano watu hao, waliokosa dhamiri njema. Ambao ni Himenayo, na Iskanda. Watu hawa walikuwa ni wabaya, kwasababu walikuwa wanapindua Imani za watu kwa makusudi, wala sio kwa bahati mbaya wakiwafundisha kinyume na mafundisho ya mitume,.
Kwamfano huyu Himenayo, tunasoma tena, Paulo akieleza mafundisho yake potofu, ya kuwaambia watu Ufufuo wa wafu tayari umeshatokea.. Hivyo watu wengi wakaiacha Imani na kumgeukia yeye.
2Timotheo 2:16 “Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,17 na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha”.
2Timotheo 2:16 “Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea zaidi katika maovu,
17 na neno lao litaenea kama donda-ndugu. Miongoni mwa hao wamo Himenayo na Fileto,
18 walioikosa ile kweli, wakisema ya kwamba kiyama imekwisha kuwapo, hata kuipindua imani ya watu kadha wa kadha”.
Na mwezake Iskanda, ambaye wengi wanaamini ndio huyu aliyezungumziwa katika vifungu hivi; Ambaye alimpinga sana Paulo katika kazi zake za kihuduma.
2Timotheo 4:14 “Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake.15 Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu”.
2Timotheo 4:14 “Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake.
15 Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu”.
Hivyo, makundi haya, Mtume Paulo hakushughulika nayo kabisa, bali kwa mamlaka aliyopewa, aliwaacha mikoni mwa shetani, ili wafundishwe wasimtukane Mungu. Maana yake ni kuwa, ulinzi wa Mungu uliondolewa juu yao, ili shetani apate nafasi ya kuwashughulikia, ili yamkini watubu.
Aidha walikumbwa na magonjwa, au mapigo, au hata vifo hatujui.. Lakini kuwekwa mikoni mwa shetani, adhabu kali kama hizo utakumbana nazo.(Tunaona kwa ayubu pale alivyoondolewa wigo wa ulinzi na Mungu, jinsi majangwa makali yalivyompata)..Ndivyo ilivyokuwa kwa hawa wakina Himenayo na mwenzake.
Yapo mamlaka ambayo Watakatifu wamepewa, kwa watu ambao wanauchezea ukristo, Ikiwa unafanya dhambi kwa makusudi, angali unaujua ukweli, na upo ndani ya mwili wa Kristo, kuwa makini sana, kwasababu hukumu yoyote itakayotolewa juu yako na wao lazima ikupate.. Na kama utakuwa unafanya kwa siri, kanisa halitajua, lakini Mungu atajua.. Na yeye mwenyewe atakuweka mikononi mwa ibilisi, upigwe. Ukishafikia hatua hii, waweza hata poteza Maisha yako.
Soma;
1Wakorintho 5:1 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu”.
1Wakorintho 5:1 “Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.
2 Nanyi mwajivuna, wala hamkusikitika, ili kwamba aondolewe miongoni mwenu huyo aliyetenda jambo hilo.
3 Kwa maana kweli, nisipokuwapo kwa mwili, lakini nikiwapo kwa roho, mimi mwenyewe nimekwisha kumhukumu yeye aliyetenda jambo hilo, kana kwamba nikiwapo.
4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;
5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu”.
Bwana atupe Imani ya kweli na dhamiri safi.
Shalom.
DHAMBI YA MAUTI
Dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ni ipi?
MFANO WA MAMBO HAYO NI UBATIZO.
MAZUNGUMZO MABAYA HUHARIBU TABIA NJEMA.
NINI TOFAUTI KATI YA MATENDO YA SHERIA NA MATENDO YA IMANI?
KAMA UNAPENDA MAISHA, NA KUTAKA SIKU YAKO IWE NJEMA.
Gumegume ni nini? (Isaya 50:7)
SWALI: Nini maana ya huu mstari;
Mithali 28:8 “Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida, Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.
JIBU: Huyo anayezungumziwa azidishiye mali zake kwa riba na faida ni mtu ajipatiaye mali kwa njia zisizo za haki, kuwadhulumu wanyonge.
Kwamfano katika biblia Mungu aliwaangiza wana wa Israeli, wasiwatoze riba maskini, pindi wawakopeshapo, na pia wasichukue faida kutoka kwa ndugu zao, isipokuwa kwa wageni tu.
Kutoka 22:25
“Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida”.
Soma pia, Walawi 25: 35-37, kumb 23
Hivyo kulikuwa na kundi kubwa la matajiri walioihasi hii sheria ya Mungu, wakawa wanawatoza riba na kujipatia faida isivyo haki, Matokeo yake Wakafanikiwa kujikusanyia mali nyingi kama mavumbi ya ardhini.
(Ayubu 27: 13-16 )
Lakini bado maandiko, yanatoa matokeo au hatma ya watu kama hawa. Mwisho wa siku Mungu anawapokonya na kuligawia kundi lingine la watu lenye kuwahurumia maskini.
Utajiuliza inawezekanikaje..biblia inasema mali ina mbawa, inaweza kupaa ghafla, au ikatumiwa kwa matumizi yasiyo ya muhimu ikapukutika yote, au wewe ukafa ukamwachia mwingine. Lakini kule inapoelekea, sio popote tu ilimradi, hapana, bali ni kwa mtu yule ambaye anawahurumia maskini.
Ndio Mungu anaweza kufanya hivyo..usipoitumia talanta yako vema. Anasema mnyanganyeni yule mwenye moja mkampe yule mwenye 10 (Mathayo 25:28),.Bwana anaweza kukunyang’anya ulichonacho.
Tukiwa watu wa kutenda haki na kuwahurumia maskini, kwa kuwapa vitu, basi tujue kuwa tayari kuna watu wameshaandaliwa kwa ajili ya kutuletea hazina hizo, na watu wenyewe ndio hao waovu, wanaojilimbikizia mabilioni ya pesa katika akaunti zao za benki kwa dhuluma, na hila, na biashara haramu, na sio kwa njia halali.
Hii ni kuonyesha kuwa watu wanaopenda kuwapa wengine vitu, wanayo hazina kubwa sana hapa dunia.
Bwana atusaidie kuzifahamu hekima hizi tupende kuwasaidia watu wanyonge.
Tafadhali shea na wengine ujumbe huu Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp: Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312
Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Kiburi cha Uzima ni nini? (1Yohana 2:16)
Biblia ina maana gani inaposema akonyezaye kwa jicho huleta masikitiko?
UBATILI.
Je Malaika Mikaeli ndiye Yesu mwenyewe?
SHINA LA UCHUNGU, LISICHIPUKE NDANI YETU.
DORKASI AITWAYE PAA.
Bwana Yesu asifiwe, karibu tena tujifunze maneno ya uzima. Leo nataka tuone jambo ambalo, wengi wetu tuliookoka hatulifahamu kuhusiana na tabia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Ili tuelewe vema kiini cha somo, naomba tusome hivi vifungu vitatu, kwa umakini sana;
Marko 2:1Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.
Mathayo 13:1 “Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari. 2 Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani”.
Mathayo 13:1 “Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari.
2 Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda chomboni, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani”.
Mathayo 14:13 “Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao. 14 Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao”.
Mathayo 14:13 “Naye Yesu aliposikia; hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa miguu kutoka mijini mwao.
14 Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao”.
Kama tunavyosoma hapo, kuna wakati Bwana Yesu alikaa nyumbani kwake, mahali ambapo panajulikana, kwamfano kama mtu angemuulizia angeambiwa anakaa pale kwenye kaya ile namba Fulani..Utamkuta ameketi kwenye kochi lake, sebuleni kwake, au yupo jikoni kwake anajipikia chai, atakukaribisha na mtazungumza mengi tu.
Soma,
Yohana 1:37 “Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi”.
Yohana 1:37 “Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.
38 Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
39 Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi”.
Lakini upo wakati aliondoka hapo, akaenda katika mazingira ambayo yana watu, lakini hayana nyumba ndio hapo unamwona anatoka nyumbani kwake anakwenda kuketi kando ya bahari.. Sasa kumpata hapa, si kurahisi kama ilivyokuwa nyumbani, Leo hii ni rahisi mtu kukwambia tuonane hoteli Fulani, au nyumba Fulani, kuliko kukwambia tuonane fukweni, wavuvi walipo. Ni ngumu kwasababu hakuna ofisi au makazi pale.
Lakini kama hiyo haitoshi, aliondoka tena huko fukweni ambapo alikuwa anakwenda mara kwa mara kuwafundisha watu, akakaa sehemu isiyokuwa na watu kabisa, maana yake nyikani/ jangwani. Huku ndiko kubaya kabisa, kwasababu hakuna upatikanaji wa mahitaji yoyote ya kijamii. Hakuna maji wala chakula, wala kivuli, ni jua tu, na vumbi..
Lakini katika sehemu zote hizi, watu waliokuwa na shida kwelikweli walimfuata, isipokuwa ni kwa ugumu sana, kwasababu iliwabidi watembee kwa miguu umbali mrefu, kama tunavyosoma hapo juu, waende mahali ambapo hawajui kama watarudi salama, au mizoga.
Na ndio maana kule nyikani, ilifikia hatua wanawafunzi wake wakamwambia Bwana awaage makutano, waende kujitafutia chakula kwasababu wamekaa naye siku tatu, usiku na mchana, bila chochote, watazimia,…Lakini Yesu alijua ni nini anakitengeneza ndani yao.
Mathayo 14:15 “Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula”.
Ndugu yangu, pindi unapookoka, ni sawa na ile hatua ya kwanza ya Yesu kukaa nyumbani kwake. Wakati huu Kristo anakuwa karibu sana na wewe, mda wowote utampata, itakuwa ni rahisi yeye kuchukuliana na wewe kwa hali zako zote.. Lakini jambo hilo halitaendelea sana..
Ataondoka nyumbani kwake na kwenda ufukweni.. Hapo ndipo itabidi umfuate. Ukikaa katika mazingira yale yale, miezi inaenda miezi inarudi, huonyeshi bidii yoyote kwa Kristo, wewe mwenyewe utashuhudia tu ukame utakaouona moyoni mwako. Utadhani kwamba Kristo amekuacha, kwasababu ile raha uliyokuwa mwanzo, au vile vitu alivyokuwa anakuonyesha mwanzo vimekata. Ukishaona hivyo, hapo ndipo unapaswa ujiongeze, zidisha bidii yako, kufanya ibada, kuomba, kusoma Neno na kujitenga na uovu. Ukizingatia hayo, utaanza kumwona tena akikufundisha..
Lakini hapo napo hatadumu kwa muda mrefu sana kama unavyodhani.. Atapiga hatua nyingine na kwenda nyikani, pasipokuwa na kitu/watu. Na huko nako huna budi kumfuata.. Hapo ndipo inapokugharimu, kuuaga ulimwengu, inapokugharimu, kupoteza nafsi yako kwa ajili yake,. Unamfuata Yesu hujui kesho yako utakula nini, hujui hatma ya maisha yako itakuwaje, unakubali kupukutika naye pale nyikani, huku ukimsikiliza tu,
Wakati huu usijijali sana, ikiwa unahaja kweli na Yesu.. Kwasababu hatua hii ya kujikana nafsi, inafikiwa na wachache, lakini huku ndipo Kristo anajifunua kwa mtu kwa viwango vingine kabisa. Utaona wale makutano walioweza kustahimili naye, siku tatu kule nyikani, bila kitu chochote, walipata faida mbili, ya kwanza ni kupokea uzima wa milele, na ya pili, ni kugawanyiwa mikate, ambayo waliila na kusaza. Sasa mikate pale inafunua, [rizki zao], maana yake ni kuwa Kristo aliwabariki, rizki zao, kule waliporudi, walipata vingi, kupita kiasi mpaka wakasaza, Kama kulikuwa na muuza genge alipata wateja mara mbili zaidi n.k..yaani kwa ufupi uchumi wao ulirekebishwa na Bwana.(Mathayo 14:19-21)
Lakini hiyo yote ilitokana na nini?
Ni kuwa radhi, kujitwika msalaba wako na kumfata Yesu. Hili haliepukiki kwa mtu yeyote anayemaanisha kumfuata Bwana Yesu. Ikiwa hauwi tayari binti kutupa vimini na suruali, na maurembo ya kidunia, kuukana ulimwengu kweli kweli, huwezi kumwona Bwana katika viwango vingine, ikiwa kijana, upo nusu nusu, vuguvugu, mizaha, na matusi, miziki ya kidunia, kubeti, mipira, punyeto, pamoja na udunia vimekutawala, hapo usiseme nimemwona Bwana.
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. 35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. 36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? 37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?”
Marko 8:34 “Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?”
Tukizijua tabia hizi za Bwana Yesu, basi tutajifunza kuwa watu wa kupiga hatua kila siku, kumfikia yeye. Kwasababu Bwana hayupo sehemu moja. Tukatae ukristo mgando.
Bwana atusaidie.
KUNA WAKATI YESU ATAPITA NA WATU HAWATAJUA.
RABI, UNAKAA WAPI?
JE UPANGA UMEINGIA MOYONI MWAKO?.
LEO WOKOVU UMEFIKA NYUMBANI HUMU
NINI MAANA YA KUWA MKRISTO?
Je! ni sahihi kuning’iniza picha nyumbani mwako kama ya Yesu?
“Bonde la vilio” ni nini katika biblia?(Zaburi 84:6)
Biblia inaposema “Wote tumetenda dhambi” si inamaanisha hakuna mtakatifu duniani?
Karibu tujifunze hekima, zilizo katika Neno la Mungu, Tukisoma Mithali 24:30-34 inasema..
30 “Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili. 31 KUMBE! LOTE PIA LIMEMEA MIIBA; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka. 32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho. 33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
30 “Nalipita karibu na shamba la mvivu, Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.
31 KUMBE! LOTE PIA LIMEMEA MIIBA; Uso wake ulifunikwa kwa viwawi; Na ukuta wake wa mawe umebomoka.
32 Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana; Naliona, nikapata mafundisho.
33 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi!
34 Hivyo, umaskini wako huja kama mnyang’anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha”.
Sulemani anaeleza, tukio alilokutana nalo katika shamba la huyu mtu ambaye alimtambua kama mvivu, Na tukio lenyewe lilimtafakarisha sana.. Yeye alidhani, kwa kulala kwake, na kuchelewa kwake kulilima shamba lake, basi ndio litabakia vilevile, bila chochote kuwepo juu yake. Lakini kilichomstaajabisha ni kuona mazao mengi sana, tena makubwa yaliyostawi, lakini hayakuwa yale aliyoyapanda bali ni miiba.
Kuonyesha kuwa shamba halimsubirii wala halimtambui mkulima, kazi yake ni kuchepusha chochote kile kinachokuja kupandwa juu yake.. Kama ni mchicha, kama ni gugu, kama ni mwiba, kama ni mbigili, kama ni bangi, kama ni tumbaku, haijali kipandacho, hiyo ndio tabia ya shamba lolote Maandiko yanasema hivyo katika (Marko 4:26-29)
Hivyo mtu asipowajibika mwenyewe, kusafisha shamba lake, na kuhakikisha, anayatoa yale yasiyostahili, au analipalilia mara kwa mara, ajue kuwa ataangukia hasara, na mwisho wa siku kazi yake inakuwa bure. Sikuzote kazi nzito ya ukulima ipo katika kupalilia na kulitunza shamba, dhiki ya wavamizi, na magugu, na sio katika kupanda. Kwasababu kupanda kunaweza kuchukua siku moja au mbili basi. Lakini kulitunza shamba ni jambo lingine, linalomgharimu mkulima, kila siku awe anaamka asubuhi na mapema, na mara kwa mara kulitembelea shamba lake, kulitazama na kulipalilia.
Mioyo yetu ni mashamba..Chochote kinachopandwa iwe na Mungu, au ibilisi, au mwanadamu, ni lazima kimee tu, tupende tusipende.. Hapo ndipo umakini unapohitajika sana, Hii ndio sababu kwanini maandiko yanasema, tuilinde mioyo yetu kuliko yote tuyalindayo (Mithali 4:23). Kwasababu chochote kile kinamea.
Hivyo, ikiwa huna tabia ya kuutazama tazama moyo wako, basi rohoni unatafsirika kama mvivu wa hali ya juu, unalala, pale unaposema, aaa, kesho nitasoma Neno, wiki ijayo, nitakwenda Ibadani, hujui kuwa shamba lako (moyo wako), unamea miiba usiyoijua wewe na viwavi kila siku…
Ndugu kusema nimeokoka tu, hakutoshi, ni lazima kila siku uhakikishe umeongeza jambo jipya katika maisha yako ya kiroho, jiulize, je! Lile Neno ulilohubiriwa au ulilolisoma, umeliishi vipi katika siku yako, au wiki yako yote. Ni lazima ufanye hivyo kila siku. Usijisahau, ukawa unaikumbuka roho yako, jumapili kwa jumapili, hiyo ni hatari kubwa sana,..Hata hiyo ibada haiwezi kukusaidia chochote, kwasababu magugu ni mengi kuliko ngano, hivyo utalemewa tu, ukristo wako utakuwa ni mzito sana..
Kama hujui kila inapoitwa leo shetani anaturushia mbegu zake mioyoni mwetu, unapopita barabarani na kusikia miziki ya kidunia, unapokuwa ofisini na kusikia lugha za mizaha kwa wafanyakazi wenzako, hizo ni mbegu, unapokuwa shuleni na kusikia matusi kwa wenzako, unapofungua tv, internet, whatsapp, youtube, na kuona mambo yasiyokuwa na maadili, zote hizo ni mbegu, ambazo kama usipozishughulikia mapema ndani ya siku, zitamea tu, haijalishi wewe ni nani…
Hivyo tunazishughulikia , kwa kusali kila siku, kutafakari maneno ya uzima, kujitenga na uovu, kukaa katika utulivu, kuomba rehema, na kujizuia sana. Tukizingatia haya kila siku. Basi mbegu halisi za Mungu tu, ndio zitakazokuwa zinamea mioyoni mwetu. Na matokeo yake tutakuja kula matunda yake baadaye.
Hivyo tusiwe watu, wa kukumbushwa kumbushwa habari za maisha yetu ya kiroho, tuamke usingizini, tuondoe uvivu, tukayatazame mashamba yetu kila siku. Anza sasa kuwajibika kwa kila kitu kinachoukaribia moyo wako, ikiwa hakimpendezi Mungu, hakikisha unashughulika nacho, hadi kiondoke.
Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza. 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.
Waefeso 5:14 “Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana”.
NI NANI ATAKAYEUCHUKUA MSALABA WA YESU?
MWENGE WAKO WA UHURU UPO WAPI?
AINA TATU ZA WAKRISTO.
Kwanini Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wasichukue chochote isipokuwa fimbo tu?
UTENDAJI KAZI MWINGINE WA ROHO MTAKATIFU USIOUFAHAMU.
Wakati wakina Shadraka wanatupwa katika tanuru la moto, Danieli alikuwa wapi?
SWALI: Naomba kufahamu biblia inaposema wenye kuhadaa roho zisizo imara ina maana gani? (2Petro 14)
JIBU: Tusome;
2Petro 2:14 “wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, WENYE KUHADAA ROHO ZISIZO IMARA, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.17 Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa”.
2Petro 2:14 “wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, WENYE KUHADAA ROHO ZISIZO IMARA, wenye mioyo iliyozoezwa kutamani, wana wa laana;
15 wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;
16 lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda, asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu, aliuzuia wazimu wa nabii yule.
17 Hawa ni visima visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa”.
Katika siku za mwisho biblia inatabiri kuwa litatokea kundi Fulani la watu mahususi, lenye kazi ya “kuhadaa roho za watu watu”.
Kuhadaa ni kudanganya, Lakini biblia bado haisemi kundi hili litahadaa kila mtu tu, hapana bali inasema, litahadaa watu “wenye roho zisizo imara”.
Kwa kawaida kitu kisicho imara ni kitu kisichoweza kudumu kwa muda mrefu, kisichoweza kustahimili mazingira ya mtikisiko, au mazingira magumu kwa muda mrefu kwasababu kimeundwa chini ya ubora. Kwamfano, ukinunua kiatu cha ngozi, na mwingine akanunua kile cha plastiki, mkavitembelea wote kwa pamoja, utaona baada ya muda mfupi kile cha plastiki, kinachakaa na kuisha kabisa, lakini kile cha ngozi kinaendelea kudumu, Kwasababu gani? Ni kwasababu kiatu kile cha plastiki sio imara.
Vivyo hivyo katika roho siku hizi za mwisho, Kuna wakristo walio imara, na wengine ambao sio imara, kuna wenye nguvu ya kudumu katika wokovu haijalishi ni mitikisiko mingapi inawakumba kwasababu hapo mwanzo walimaanisha kweli kweli kumfuata Kristo.. Hawa wana heri sana, ibilisi hawezi kuwahadaa.
Lakini kundi lililo hatarini ni hili ambalo leo linaokoka kwa Bwana, kesho linarudi nyuma, leo ni moto kesho ni vuguvugu, leo linahudhuria mikesha, kesho linasahau, leo linaeleweka, kesho halieleweki, leo lipo ibadani wiki ijayo halifiki kabisa, likiwa na wapendwa linazungumza habari za Mungu, lakini likikaa na watu wa kidunia, linabadilika rangi, linafanana na wao. Lipo hapo katikati, Kudondoka kiwepesi katika dhambi ni jambo la kawaida kwao, ukiliuliza mbona umefanya hivi litakuambia nimepitiwa tu na shetani.
Sasa watu kama hawa ni lazima shetani atawahadaa tu,kwa hila zake, Na watakapodanganywa hawawezi kufahamu kwasababu wao ni roho zisizo imara. Kama Balaamu alipowahadaa wana wa Israeli, kwa kuwashawishi wazini, na mwisho wa siku Mungu akawapiga kule jangwani, Pale Edeni Hawa alipodanganywa na nyoka hakujua chochote, kwasababu moyo wake haukuwa imara kwa Mungu.
Ndugu kama na wewe ni mmojawapo tubu dhambi mgeukie Bwana, kisha maanisha kabisa kumfuata Yesu kwa gharama zozote, Kumbuka hizi ni nyakati za mwisho. Watu waliovuguvugu Bwana ameahidi kuwatapika, na wewe angalia usitapikwe. Au kudanganywa na ibilisi. Simama imara kwa Bwana. Kataa ukristo feki, au wa juu juu usioingia gharama.
1Wakorintho 16:13 “Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari”.
1Wathesalonike 3:12 “Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote”.
1Wathesalonike 3:12 “Bwana na awaongeze na kuwazidisha katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile sisi nasi tulivyo kwenu;
13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote”.
KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 1
Nini maana ya mstari huu: (Mtu ambarikiye mwenzake kwa sauti kuu asubuhi na mapema; Itahesabiwa kuwa ni laana kwake.Mithali 27:14 )?
kwanini yule kijana aliitupa ile nguo ya kitani chini na kukimbia uchi?
Ni mlima gani Yule Mwanamke Msamaria aliokuwa anaumaanisha? (Yohana 4:19)
Ni wayahudi wa aina gani wanaotajwa kuwa sinagogi la shetani? (Ufunuo 2:9, Ufunuo 3:9)
Nini maana ya siku moja kwa Bwana ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja? (2Petro 3:8)
SWALI: Nini maana ya huu mstari? Hapo anaposema yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
Mhubiri 10:8
[8]Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
JIBU: Mistari hiyo inawazumgumzia watu ambao wanasababisha matatizo kwa wenzao. Au watu wanaowakosesha wengine waliokuwa tayari katika njia sahihi.
Na ndio maana hapo anaanza kwa kusema mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake..Akiwa na maana kuwa dhara lile unalolipanga kwa mwingine limpate ndilo hilo hilo litakupata wewe.
Mfano wa watu kama hawa katika biblia ni Hamani, ambaye alikua adui wa Mordekai na wayahudi wote, mpaka akafikia hatua ya kumtengenezea msalaba Mordekai, lakini kinyume chake msalaba ule ndio ukamtundika yeye mwenyewe.
Lakini kwenye hicho kipengele cha pili anasema Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.. Maana yake ni kuwa maboma sikuzote hujengwa kwa lengo la kudhibiti maadui, tukiachilia mbali wanadamu, lakini pia wanyama wakali kama fisi, mbweha na nyoka wasivamie mifugo.
Hivyo anaposema abomoaye boma..anamaanisha aondoaye ulinzi wa mwenzake ili maadui kama nyoka wapite, wawadhuru, kinyume chake atadhurika yeye.
Hii ikifunua nini?
Wapo watu leo hii, wanaoondoa maboma ya watu wengine kwa hila zao. Na maboma yanayomaanishwa hapo si mengine zaidi ya YESU KRISTO. Yeye ndio boma letu, Biblia inasema hivyo..
Zaburi 18:2
[2]BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Hivyo watu watu wanawakosesha kwa kuwalaghai ili ibilisi awameze, wanawazuia wasimwabudu Mungu sawasawa na mapenzi yake, wanawazuia wasimwombe Mungu wao, ili wapoe..lakini kinyume chake wao ndio watamezwa. Na Bwana atawaponya watu wake.
Mfano wa watu kama hawa,ni wale maliwali wa Umedi waliompangia visa Danieli, ili asimwombe Mungu wake, kutwa mara tatu. Wakidhani kuwa ndio atapotelea mbali kwenye tundu la simba. Lakini kinyume chake wao ndio walimezwa na ibilisi.
Hivyo kamwe usijaribu kumkosesha mtu wa Mungu, wala usijaribu kumwondolea boma lake (Yesu Kristo), ukadhani ndio tayari atarudi nyuma. Wewe ndio utarudishwa nyuma na shetani.
Tusiwe watu wa kusababisha mabaya/madhara kwa wengine. Ndio kiini cha mistari hiyo.
Wale Nyoka wa Moto jangwani, walikuwa ni wa namna gani?
JIHADHARI NA UONGO WA SHETANI UNAOKARIBIANA NA UKWELI.
NJIA YA KUPATA WOKOVU.
Mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili
MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.
SWALI: Kuota nasubiriwa mahali Fulani, nihutubie halafu mimi nachelewa, au natingwa na mambo mengine ina maana gani?
JIBU: Ndoto ya namna hii, mara nyingi huwa inaotwa na makundi ya watu ambao wanawajibika katika kuwahudumia wengine, aidha ni viongozi, au wahubiri.
Na huwa zinakuja katika sura tofauti tofauti, wengine wanaota wanasubiriwa kwenye mikutano wahutubie, lakini wanajikuta, wakicheleweshwa na mambo madogo madogo, pengine foleni, au watu, au vishughuli visivyokuwa na msingi. Wengine wanaota wanapaswa wapande madhabahuni wawahubirie wengine, lakini mara wanajiona wapo uchi, wanatafuta suti zao wavae, hawazioni, muda unazidi kwenda, mpaka mwishoni watu wanaondoka, wote na yeye bado hajatokea madhabahuni. N.k.
Hivyo ukiota ndoto ya namna hii tafsiri yake ni kuwa, wewe kama kiongozi kiwango chako cha utayari katika nafasi hiyo Mungu aliyokuweka bado kipo chini. Na ndio maana unashindwa kufika pale, yapo mambo ambayo yanatia vikwazo kwako. Bwana anasema..
2Timotheo 4:2 “lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho”
Hivyo unachopaswa kufanya ni kuondoa visababu, au hivyo vizuizi vidogo vidogo, mbele yako, ambavyo pengine vinakusababishia uone huo sio wakati ufaao, kwa kumtumikia Mungu, kisha kuwa tayari, kusimama na Bwana kwa ukamilifu wote, kama askari ambaye amevitwa utayari miguuni kwa ajili ya vita.
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu UTAYARI tupatao kwa Injili ya amani”
Waefeso 6:13 “Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 na kufungiwa miguu UTAYARI tupatao kwa Injili ya amani”
Kwa kuzingatia hayo, utakuwa umelitatua hilo tatizo, katika wito wako.
Bwana akubariki.
Kuota unapigana na mtu.
KUOTA UPO KANISANI.
KUOTA UNALIA/UKIOTA UNALIA KWA UCHUNGU.
KUOTA UMECHOMWA KISU/KUOTA UMEPIGWA RISASI.
MTAWATUPIA MBWA NYAMA HIYO.
NDIPO HUENDA AKACHUKUA PEPO WENGINE SABA.
Kama Malkia Esta alijipamba je! Kuna ubaya gani wanawake wa wakikristo wa leo kujipamba?.
Shalom, jina la Bwana libarikiwe.
Ni vema tukajifunza tabia kadha wa kadha za Mungu, ili na sisi tuziige hizo tuwe wakamilifu kama yeye. Leo tutajifunza tabia mojawapo ya Mungu, ambayo pengine unaweza ukastaajabu Mungu anawezaje kuonyesha angali yeye ni Mungu. Hivyo kwa kupitia hiyo tutajifunza na sisi mienendo yetu.
Kwamfano ukisoma kitabu cha Mwanzo, baada ya Mungu kumaliza uumbaji wake wote, baadaye utaona tena anasema “si vema”(Mwanzo 2:18). Sasa utajiuliza iweje aone tena si vema, kwani kazi yake hapo mwanzo ilikuwa haijakamilika? Inahitaji marekebisho.. Mpaka aanze tena uumbaji mwingine wa kumpa Adamu msaidizi?..
Jibu ni kwamba Sio kwamba hakulijua hilo? Hapana alishalijua na tayari alikuwa ameshamuumba Hawa katika akili yake tangu zamani (Soma Mwanzo 1:27). Lakini alijifanya kana kwamba amesahau, ili kutufundisha sisi pia, tuwe watu wa kupenda marekebisho. Marekebisho sio dhambi, ni karama ya Mungu..Kwani kwa kupitia hiyo tutafikia ukamilifu, ukiwa mtu wa kuridhika na maisha yaleyale, mienendo ile ile, huna maboresho yoyote, ujue tabia hii ya Ki-Mungu haipo ndani yako.
Vivyo hivyo kuna tabia nyingine, ya kushangaza aliionyesha Mungu, na leo tutajifunza. Utakumbuka wakati ule, anakwenda kuiteketeza Sodoma na Gomora, alikutana kwanza na Ibrahimu, na alipomaliza kuzungumza naye akabidi pia amweleze Ibrahimu mpango wake, akamwambia maneno haya;
Mwanzo 18:20 “Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, 21 BASI, NITASHUKA SASA NIONE KAMA WANAYOTENDA NI KIASI CHA KILIO KILICHONIJIA; NA KAMA SIVYO, NITAJUA. 22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana”
Mwanzo 18:20 “Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana,
21 BASI, NITASHUKA SASA NIONE KAMA WANAYOTENDA NI KIASI CHA KILIO KILICHONIJIA; NA KAMA SIVYO, NITAJUA.
22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana”
Tafakari kwa ukaribu hayo maneno..“nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua”.. Ni nini unajifunza hapo, kwamba huyu ni mtu asiyechukua maamuzi ya haraka kwanza bila kwenda kuthibitisha kwa undani ukweli wa tukio lenyewe.
Sio kwamba Mungu alikuwa hana uhakika wa kilichokuwa kinaendelea..Lakini alijifanya kana kwamba hajui, akaacha shughuli zake mbinguni, akateremka chini, aingie sodoma, atembee kwenye miji yake, ili apate uhakika wa taarifa zilizomfikia. Alijipa nafasi kati ya kile anachokisikia na maamuzi anayoyatoa.
Na kweli alikuta vilevile kama vilio vyao vilivyomfikia, lakini faida yake ni kuwa ndani yake alimwona mwenye haki mmoja, naye ni Lutu na familia yake, ndipo akamwokoa na ghadhabu ile. Lakini kama Bwana angetoa hukumu yake moja kwa moja kutoka kule mbinguni, pindi tu alipopokea taarifa na kusema ‘haya nyie malaika kapigeni kiberiti miji ile’.. Lutu angeonekania wapi?.
Tumeyabomoa maisha yetu sana, tumewaharibu wakina Lutu wetu, kwa kuchukua maamuzi ya haraka kwa kila tukio/Taarifa tunayoisikia, masikioni mwetu, au kwa kila jambo linalotokea ghafla mbele yetu.
Kwamfano Umesikia ndugu yako amekusengenya, usiwe na haraka wa kurudisha majibu ya chuki. Jifanye kama hilo ulilolisikia ni la uongo hata kama umelithibitisha.. Hiyo itakupa nafasi ya wewe, kutafakari kujua chanzo cha tatizo ni nini, na hatimaye utajikuta huwenda wewe ndio ulikuwa sababu ya yeye kuwa vile, na hapo utamsamehe, au kumwombea, au kujiombea wewe rehema. Lakini ukarudisha majibu ya kumchukia, au kumsema na wewe. Utajibomoa zaidi kuliko kujijenga.
Waweza sikia taarifa mbaya, au hujapendezwa na jambo Fulani au tukio fulani kwenye kanisa, kabla hujazira na kuondoka, pata nafasi ya kuomba, na kumshirikisha Mungu, kupitia viongozi wako wa kiroho, kama vile Mungu alivyomshirikisha rafiki yake Ibrahimu. Hiyo itakusaidia kuchukua maamuzi yaliyo ya busara zaidi.
Hata katika mambo ya maisha, kwenye familia, ukoo, pengine hata kazini kwako, ofisini, n.k, zipo taarifa nyingi zinaweza kukufikia za wafanyakazi wenzako, hupaswi kuzimeza moja kwa moja na kuzitolea maamuzi hata kama umezithibitisha kuwa ni za kweli.. Tuliza moyo wako, tafakari, omba, ndipo baadaye Mungu akuongoze cha kutenda. Utafanya vizuri zaidi.
Ni muhimu sana, kuweka “NAFASI” Katika mioyo yetu. Kile kinachoingia, kisirudishe majibu hapo hapo. Ni heri viingie mia, kikatoka kimoja chenye majibu ya busara, kuliko kuingia 100, vikatoka vyote 100, vyenye kisasi, na maumivu, na mapigo. Ilimgharimu Bwana asiziamini taarifa zake, iweje wewe uamini za kwako, au za wanadamu wengine?
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
NGUVU ILIYOPO KATIKA MAAMUZI.
DHAMBI ILIYOMKOSESHA SHETANI:
UUMBAJI BORA WA MUNGU, UPO NDANI YA MWANADAMU.
JINSI YA KUMSIKIA MUNGU, NA KUPOKEA MAFUNUO AU JUMBE KUTOKA KWAKE.
Je ni kweli ilikuwa desturi ya Bwana kuishika sabato?(Luka 4:16)
Ni miaka mingapi ya njaa Daudi aliyoambiwa achague? Ni miaka 7 au miaka 3?
MAFUNDISHO MAALUMU KWA WANAWAKE.
Kuwa mwombolezaji:
Yeremia 9:20 “Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia”.
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo Bwana wetu, mkuu wa uzima, karibu katika kujifunza maneno ya uzima. Huu ni mwendelezo wa mafundisho maalumu yawahusuyo wanawake.
Leo nataka tuone jambo ya kitofauti lililokuwa linawatokea wanawake wengi wa-Kimungu katika biblia. Na kwa kupitia hilo naamini lipo la kujifunza wewe kama mwanamke, uliyeokoka.
Na jambo yenyewe ni “kufungwa Tumbo la uzazi”. Ukisoma kuanzia mwanzo, wanawake wengi hodari walioitwa wacha Mungu, walifungwa matumbo yao wasiweze kuzaa, tukianzia kwa Sara, mpaka Rebeka, tukiendelea hadi kwa Raheli, na Ana-Mama yake Samweli, na Mke wa Manoa aliyemzaa Samsoni, na Elizabeti mama yake Yohana. Wote hawa walikuwa ni matasa. Unajua ni kwanini?
Wengi wanachukulia katika jicho la laana na mikosi, lakini ukitafakari vizuri, hakukuwa na laana yoyote juu ya watu hawa, kwasababu maandiko yanatuambia ni Mungu mwenyewe ndio aliyewafunga matumbo yao, Tengeneza picha Sara ambaye wafalme waliojaribu kumuiba wamfanye mke wao, Bwana aliwaadhibu vikali, mtu kama huyo iweje awe amebeba laana?
Hivyo lipo funzo kubwa sana nyuma yake, linalowahusu wanawake wote. Na funzo lenyewe ni kwamba Mungu anataka mwanamke yeyote, awe mwombolezaji, ili kusudi lake litimie, aulekeze moyo wake kwake kwa machozi mengi na dua, maombi, kwasababu kwa kupitia yeye, Mungu atalifanikisha kusudi lake kubwa duniani. Na ndio maana ilimgharimu Mungu awafunge matumbo wale wanawake wote, ambao alijua kabisa kwa kupitia wazao wao, Mungu atatukuzwa.
Ndio hapo utamwona mwanamke kama Ana, mke wa Elkana analia kama mlevi kule hekaluni, juu ya uzazi wake, yeye akidhani kwamba Mungu anasikiliza dua za tumbo lake, kumbe Mungu alikuwa anasikiliza maombi ya kuletwa mwamuzi Samweli duniani… Kwasababu ili shujaa aje ilihitaji maombolezo mengi sana.
Lakini kama moyo wake ungelitambua hilo tangu mwanzo, kuomba kwa bidii juu ya mwamuzi Israeli, kulikuwa hakuna sababu ya yeye kufungwa tumbo. Yanini?
Ndivyo ilivyokuwa kwa Raheli na Elizabeti, na wanawake wengine.
Binti, dada, Mama, bibi.. Tambua kuwa wewe umewekwa, kama mzalisha Nuru ulimwenguni. Maombi yako, machozi yako, sala zako, maombolezo yako, ni changizo kubwa sana la Mungu kuleta mapinduzi katika kanisa, familia, na hata taifa kwa ujumla.
Usisubiri Mungu akufunge tumbo lako, ndipo uanze kulia, na kuomboleza,. Bali jitambue sasa, Kumbuka Tumbo, linaweza kuwa pia kazi yako, au afya yako n.k ukiona hicho ndicho kinachokukosesha raha sasa, na umekiombea kwa muda mrefu bila mafanikio, basi tambua umefungwa hivyo na Mungu makusudi, ili uuelekeze moyo wako kwake.
Sasa hapo usiombe Mungu akupe mtoto au akupe kazi au akuponye huo ugonjwa, au akukombe kiuchumi, hapana omba Mungu, alete geuko kwa kanisa, kwa familia yako, kwa taifa, kwa kupitia wewe, ombea sana rehema na toba. Na hayo yaliyosalia Mungu alishakujibu siku nyingi yeye mwenyewe alishayatimiza. Kutokukujibu kwake haraka sio kwamba akutese hapana, machozi yako kwake hayajatosha, na umeyaelekeza pasipostahili.
Mwanamke usipokuwa mwombolezaji, fahamu kuwa unalididimiza kanisa, usipokuwa mwombaji, unalidhoofisha kanisa la Kristo kwelikweli. Tambua huduma hii, ili Kanisa liweze kusimama vema, wachungaji waweze kuhubiri, vipawa na karama vinyanyuke kwenye kanisa hadi kwenye familia, wewe ndio unayeweza kufungua milango hiyo.
Bwana atusaidie kujua hilo;
Yeremia 9:17 “Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; 18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji. 19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu. 20 Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia. 21 Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu”.
Yeremia 9:17 “Bwana wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje; 18 na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
19 Maana sauti ya maombolezo imesikiwa toka Sayuni, Jinsi tulivyotekwa! tulivyofadhaika sana! Kwa sababu tumeiacha nchi, kwa kuwa wameangusha makao yetu.
20 Lakini lisikieni neno la Bwana, enyi wanawake, Na masikio yenu yapokee neno la kinywa chake; Mkawafundishe binti zenu kuomboleza, Na kila mmoja jirani yake kulia.
21 Kwa maana mauti imepandia madirishani mwetu, imeingia majumbani mwetu; Ipate kuwakatilia mbali watoto walio nje, na vijana katika njia kuu”.
mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10
MAFUNDISHO KWA WANAWAKE.
NAO WAKAMSHINDA KWA DAMU YA MWANA-KONDOO.
Katika (Mathayo 25:8 na Marko 16:8) Wale wanawake walitangaza kufufuka kwa Bwana au walikaa kimya?
HIZO NDIZO ROHO ZA MASHETANI.
MWANAMKE, BINTI, MAMA. (Sehemu ya 3)
Nini maana ya kupiga Kite! Katika biblia.
Shetri ni nini kama tunavyosoma katika Marko 3:38?