“Bonde la vilio” ni nini katika biblia?(Zaburi 84:6)

“Bonde la vilio” ni nini katika biblia?(Zaburi 84:6)

“Bonde la vilio” ni nini katika biblia?(Zaburi 84:6)


Neno hili linaonekana mara moja tu katika biblia, tunalitosoma katika mistari hii;

ZABURI 84:4 “Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima.

5 Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.

6 WAKIPITA KATI YA BONDE LA VILIO, Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka 7 Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu”.

Ukianzia kusoma juu Zaburi yote hiyo ya 84 utaona inazungumzia uheri wa watu wale, wanaopenda kwenda nyumbani kwa Bwana kumtafakari yeye daima,kumuhimidi yeye, kumwabudu yeye, kusikiliza maneno yake, unazungumzia juu ya watu wale wanaopenda wakati kuwa uweponi mwa Mungu, nyumbani mwake kumtafakari yeye,..

Biblia inasema, watu wa namna hiyo hata ikifika wakati wakapita katika bonde la vilio, Mungu ataligeuza bonde hilo kuwa chemchemi ya maji, na  kulinyeshea mvua ya vuli.

Kibiblia yapo mabonde mengi, kama vile lilivyo bonde la uvuli wa mauti, ambalo tafsiri yake ni sehemu ambayo mtu atapita haoni tumaini la kuishi tena, inaweza ikawa ni maadui wanamwinda, au magonjwa yanamsumbua kama vile Kansa,Ukimwi n.k., au kesi za mauaji zinamkabili, au sehemu za hatari sana anazipitia sasa n.k..Hilo ndio bonde la Mauti ambalo Daudi alisema nijapopita hapo, sitaogopa mabaya kwa maana Bwana atakuwa pamoja nami (Zab 23:4).

Vivyo hivyo Bonde la vilio nalo lipo, bonde hili ni bonde la ukame, kiu na njaa, bonde la kutokuwa na kitu, na kupungukiwa kabisa, lakini kwa mtu Yule ambaye amekuwa akipenda kuwepo nyumbani mwa Bwana daima kumuhimidi, kumshukuru, kumsujudu, kumwabudu..Mungu anasema bonde hilo kwake litageuzwa na kuwa chemchemi ya vijito vya maji, na mvua ya vuli italinyeshea.

Wana wa Israeli walipita katika bonde hili walipokuwa jangwani , wakalia sana kwa kukosa maji, lakini Mungu aliwapasulia miamba maji yakatoka kama mto wakanywa wakafurahi.(Kutoka 17:1-7, Hesabu 20:1-8) Vivyo hivyo na mtu Yule ambaye Nyumbani kwa Mungu (Kanisani) na sehemu yeyote ile Mungu ambayo Mungu anakaa ndio mahali pake pa kustarehe. Mungu anasema hata ajapopitia wakati mgumu Mungu atakuwa mvua yake ya vuli.

Na ndio maana mtunzi wa Zaburi akamalizia na kusema..

Zaburi 84:10 “Hakika siku moja katika nyua zako Ni bora kuliko siku elfu. Ningependa kuwa bawabu nyumbani mwa Mungu wangu, Kuliko kukaa katika hema za uovu”.

Bwana atujalie na sisi tuone umuhimu wa kuwepo nyumbani mwake wakati mwingi.

Shalom.

Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema, na pia kama utapenda tuwe tunakutumia mafundisho ya Neno la Mungu ya mara kwa mara kwa njia ya email yako au Whatsapp basi tutumie ujumbe kwenye namba hii +255 789001312

Mada Nyinginezo:

Nini maana ya “Siku moja nyuani mwa Bwana ni bora kuliko miaka elfu”?

FAIDA ZA KUFUNGA NA KUOMBA.

SIKU YA UNYAKUO ITAKUKUTAJE?

ROHO HUTUOMBEA KWA KUUGUA KUSIKOWEZA KUTAMKWA!

JINSI ROHO MTAKATIFU ANAVYOWAFUNULIA WATU MAANDIKO.

BONDE LA KUKATA MANENO.

Rudi Nyumbani:

Print this post

About the author

Admin administrator

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments