Category Archive Uncategorized @sw-tz

Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe;

SWALI: Je ni kweli, mpagani akioa au akiolewa na yule aliyeamini, na yeye pia anahesabiwa kuwa mkamilifu kulingana na mstari huu?

1Wakorintho 7:13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.

14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu

JIBU: Ifahamike kuwa hakuna mtu anayehesabiwa mkamilifu kwa ukamilifu wa mtu mwingine. Maandiko yapo wazi katika hilo; yanasema kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe, na kila mtu atatoa Habari zake mwenyewe siku ile, mbele za Mungu (Wagalatia 6:5, Warumi 14:12).

Lakini je! Mstari huo unamaanisha kwamba ikiwa umeolewa au kuoa mtu aliyeamini, hata kama wewe ni mtenda dhambi utahesabiwa mtakatifu kwa yeye?na ukifa utaenda mbinguni? Jibu ni hapana, ukisoma vifungu vya chini yake kidogo utaelewa vizuri..Tusome..

1Wakorintho 7:12 “Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.

13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe.

14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu.

15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani.

16 KWA MAANA WAJUAJE, WEWE MWANAMKE, KAMA UTAMWOKOA MUMEO? AU WAJUAJE, WEWE MWANAMUME, KAMA UTAMWOKOA MKEO”?

Paulo anamaanisha kwamba, ikiwa wewe umeamini, na mwezi wako hajaamini, hupaswi kumuacha na kwenda kuoa/kuolewa na mwingine. Bali unapaswa kuendelea kuishi naye ikiwa tu bado yupo radhi kuwa nawe. Kwasababu kwa kufanya hivyo ni rahisi yeye kuvutwa kwenye Imani yako, ikiwa ataona mwenendo wako mzuri,.. Na kwa matokeo hayo Paulo anasema ni nani ajuaje na yeye atashawishwa kuokoka kama wewe?

Na ni kweli ukisikiliza shuhuda za ndoa nyingi zilivyomrudia Mungu, utasikia moja inakuambia Baba aliokoka baada ya mkewe kuwa mcha Mungu, au mama alimrudia Mungu baada ya mumewe kuokoka. Umeona? Lakini hilo  haimaanishi kuwa moja kwa moja ndio tayari na yeye kaokoka,kisa tu mwenzake kaokoka hata kama ataendelea kutenda dhambi, hapana.

Wanaweza wakakaa hivyo, na bado mmoja akaendelea kutokuamini hadi kifo na kuzimu akaenda. Lakini hiyo nayo hutokea mara chache, ikiwa kweli huyo mwenzi mwingine, anaishi Maisha ya haki, na ya kumpendeza Mungu, na ya kumwombea kwa bidii mwenzake.

Lakini pia ni lazima tufahamu kuwa biblia hairuhusu, mkristo kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini. Mazingira yanayozungumziwa hapo, ni yale ambayo wokovu umemkuta tayari yupo kwenye ndoa ya namna hiyo. Leo hii kumekuwa na migogoro mingi ya kindoa, kwasababu ya maamuzi mabaya, yanayofanywa na wakristo, ambao hawazingatii maagizo ya Mungu yaliyosema tusifungwe nira Pamoja na wasioamini (2Wakorintho 6:14).

Ulinzi wa kwanza unapaswa uwe katika Imani yako, sio katika familia. Hivyo ikiwa bado hujaoa/ au hujaolewa, Imani ndio iwe ni kipimo cha kwanza cha kumtambua mwenzi sahihi. Lakini wewe ambaye tayari upo kwenye ndoa ya namna hiyo. Unalojukumu la kumvuta huyo mwenzi wako, kimatendo, kimaombi, na kimafundisho. Kwasababu huwezi jua kama atavutwa au la!.

Bwana akubariki

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

NDOA NA TALAKA:

KWANINI NDOA NYINGI ZINAVUNJIKA? (Sehemu ya 2: Upande wa wanawake)

NDOA NI NINI?

Je! Ni halali kuoa/kuolewa na mtu ambaye tayari anao watoto?

Nini Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ?

JE NI DHAMBI KUWA NA MAHUSIANO KABLA YA NDOA?

NJIA SAHIHI YA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KIBIBLIA.

Rudi nyumbani

Print this post

Tofauti kati ya maandiko na Neno ni ipi?

Wapo wanatofautisha maneno haya mawili, na wapo wanayoyaona kama ni kitu kimoja..

Ni kweli Bwana Yesu alituonyesha  kuwa  “maandiko na Neno” la Mungu ni kitu kilekile  kimoja, na ndivyo ilivyo..

Soma Yohana 10:35

Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka);

Isipokuwa  tofauti yao ndogo ni kwamba maandiko yanajifunga tu katika maandishi.. lakini Neno la Mungu, ni aidha katika maandishi au kuzungumzwa.

Bwana anaweza kutoa ujumbe wake kwa sauti kinabii, vilevile anaweza kuzungumza kwa biblia (maandiko). Na zote zikawa sauti zake zenye majibu.

Lakini tulichopewa, na tunapaswa tukitegemee sana ni Neno la Mungu katika maandiko, alisema,  “maandiko hayawezi kutanguka”, yaani kilichoandikwa kimeandikwa. Lakini Neno lake katika sauti anaweza kulitangua mwenyewe, au akaghahiri, au likawa la muda tu, tofauti na Neno katika maandishi.

Hivyo ukiishi kwa hilo, utakuwa salama. Lakini tukiwa wavivu wa kujifunza biblia. Tuwe na uhakika kuwa tunapoteza maisha yetu.

Marko 12:24

[24]Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?

Tupende Biblia zaidi ya chakula, tuone kuwa hatuwezi kuishi bila hilo; Daudi alisema.

Zaburi 119:140

[140]Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.

Tuyapende maandiko, kwani ndio uhai wetu.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

Gombo ni nini?

Chuo cha vita vya Bwana ni kipi?(Hesabu 21:14)

Kitabu cha YASHARI kinachozungumziwa katika 2Samweli 1:17-18, ni kitabu gani?

Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

Nini maana ya “Torati na manabii”?

Yeshuruni ni nani katika biblia?

URIMU NA THUMIMU NI NINI KATIKA BIBLIA?

Rudi nyumbani

Print this post

UNYAKUO WA KANISA UMEPITA LEO!!

“Unyakuo wa kanisa umepita leo!. Hakuna tena toba”

Je taarifa hizi zimekushtua??.

Hebu jiulize Siku taarifa hizi zitakapokuwa kweli utakuwa katika hali gani?
Mpaka sasa, unyakuo bado, haujatokea lakini siku utakapotokea utakuwa katika hali gani, utakapopewa taarifa kuwa watakatifu wamenyakuliwa na wewe umewachwa???..

Je utashtuka kama ulivyoshtushwa leo au utaona kawaida?.

Kama umeshtuka leo, hiyo ni kuonyesha kuwa wewe hupaswi kuwa wa ulimwengu, nyumbani kwako sio huku..ndio maana umeshtuka na kuogopa kusikia umeachwa!.
Rudi leo utubu kwasababu Siku hiyo pengine utaamka asubuhi na kukutana na hizo taarifa “Unyakuo umepita”..ukikumbuka kuwa masaa kadhaa tu nyuma yaliyopita, ulisikia mahubiri na ulipuuzia.

Tubu leo hii na umpokee Yesu, kwasababu ni kweli upo karibuni kutokea.

Kama leo hii utatamani kumpa Yesu maisha yako, basi piga namba hizi, tuweze kuomba pamoja na kukuongoza sala ya Toba.
0789001312.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Print this post

Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?

SWALI: Yohana alimaanisha nini aliposema..10]Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana?

Je hiyo siku ya Bwana ni ipi? Na kwanini  itajwe pale?

Ufunuo wa Yohana 1:10

[10]Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,


JIBU: Mtume Yohana alikuwa katika kisiwa cha Patmo, kwa ajili ushuhuda wa Kristo, Na kwa mara ya kwanza alipotokewa na Bwana Yesu  na kuonyeshwa mambo yanayohusiana na siri za siku za mwisho na kanisa, anasema siku hiyo aliyotokewa iliangukia  siku ya Bwana.

Swali je siku hiyo ni siku ipi?

Ikumbukwe kuwa tangu awali wakristo wa kwanza, waliifanya siku ya kwanza ya juma( Yaani jumapili) kuwa ni siku ya Bwana, kufuatana na tukio la kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Na ni siku ambayo Bwana alikuwa akiwatokea wanafunzi wake (Soma Marko 16:9, Yohana 20:19 ).

Vilevile Siku hii hii ndio siku ambayo kanisa lilipokea ahadi ya Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza..Kwahiyo watakatifu wote, tangu enzi za mitume, hadi wakati wetu huu wa sasa waliifanya siku hii kuwa ni siku ya Bwana.

Soma vifungu hivi;

Matendo ya Mitume 20:7

[7]Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.

1 Wakorintho 16:2

[2]Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;

Na ndio hapa sasa  tunaona mtume Yohana anaeleza Kwamba alipokuwa katika Roho, siku ya Bwana (yaani jumapili) ndio alitokewa na maono hayo..

Zingatia:  Mtazamo ambao siku hiyo ilikuwa ni jumamosi, si sahihi. Jumamosi, haikuwahi kuadhimishwa na wakristo wa kwanza kwa shughuli rasmi za kibada, kwa mujibu wa maandiko.

Lakini kulikuwa na umuhimu gani habari ya siku hiyo kuandikwa?

Sio kwamba Bwana anaithamini jumapili, zaidi ya siku nyingine zote, hapana au siku hiyo ni takatifu zaidi ya nyingine zote, Hapana bali anachotaka kutuonyesha ni umuhimu wa siku tunazoziweka wakfu kwa ajili yake kwamba anaziheshimu na kwamba kwa kupitia hizo, ni rahisi yeye kujifunua kwetu.

Ikiwa siku yetu kwa Bwana ni jumamosi, basi tuithamini kwa kuwa katika Roho kama vile Yohana alivyokuwa mpaka Kristo akamtembelea siku hiyo..

Kama ni jumapili, tuifanye vivyo hivyo, kama ni jumatano tuipe heshima yake. Hizi siku tusizichukulie juu juu tu,

Lakini leo hii tunapuuzia ibada kuu za kila wiki (Jumapili), tunakosa mafundisho ya biblia kanisani, au hata tukienda siku hiyo hatuwi katika roho, tunaenda ili kutimiza tu wajibu . Halafu tunataka Bwana ajidhihirishe kwetu tunapokuwa nyumbani tunaangalia tv.

Kamwe Usiruhusu, siku yako ya ibada  iliwe na uvivu au mambo ya ulimwengu huu, kama vile anasa, na mihangaiko ya dunia, hata kama upo katika mazingira ambayo hayana watakatifu..Nenda milimani huko, au maporini ukasome biblia na kuomba kama Yohana..kuliko kumwachia shetani akupangie ratiba zake kwenye siku takatifu ya Bwana..

Ithamini siku ya ibada. Na kwa hakika atajidhihirisha kwako.

Ubarikiwe.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

Sabato halisi ni lini, Je! ni Jumapili au Jumamosi?, Ni siku gani itupasayo kuabudu?

Dini ni nini, na Imani ya kweli ni ipi?

UFUNUO: Mlango wa 1

Nini maana ya kumwabudu Mungu katika Roho na kweli?

JE KANISA LITAPITIA DHIKI KUU?

JIWE LILILO HAI.

Rudi nyumbani

Print this post

NIFANYE NINI ILI NIPENDWE NA MUNGU?

Ni jambo la kawaida katika familia yoyote, si Watoto wote watakuwa na mahusiano sawa na wazazi wao. Wapo ambao wataonekana kuaminiwa Zaidi ya wengine, wapo ambao watapendwa Zaidi ya wengine, pia wapo ambao watategemewa na wazazi wao kuliko wengine,  n.k. Lakini hilo haliwafanyi wale wengine wasiwe Watoto wa wazazi wao.

Inatokea hivyo, kutokana na aidha tabia zao, ujuzi  au nafasi walizonazo. Vivyo hivyo na kwa Mungu katika familia yake ya watakatifu (Waliookoka), Si watakatifu wote watakuwa vipenzi wa Mungu, si wote wataaminiwa na Mungu, na si wote watategemewa na Bwana. Lakini hayo hayawafanyi hao wengine wasiwe Watoto wa Mungu.

Leo tutatazama mambo ambayo tukiwa nayo, basi tujue tutakuwa Watoto ambao tutapendwa sana na Mungu. Hivyo Ili tufahamu hayo tutaangalia katika biblia, mifano ya watu watatu (3) ambao, walipendwa na Mungu, ili na sisi tuige tabia kama zao tupendwa na Mungu.

Tabia ya kwanza ni Upendo.

Upendo ndio tabia ya kwanza itakayokuzogeza karibu na Mungu, na upendwe sana. Kati ya mitume 12 wa Bwana Yesu, Mtume Yohana peke yake ndiye aliyependwa na Yesu sana. Mpaka akawa muda wote anaegemea kifuani pake.

Yohana 21:20 “Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?)

21 Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?

Lakini lililomfanya apendwe na Yesu, ni upendo ambao aliuiga kutoka kwake. Na ndio maana utaona injili zake zote anahimiza upendo, kwasababu Mungu mwenyewe ni Upendo. Hivyo ili na sisi tupendwe na Bwana, hatuna budi kuonyesha bidii katika kupendana,

Na tabia za upendo tunazisoma katika 1Wakorintho 13:4-8….ambazo ni hizi;

13.4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

13.5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

13.6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

13.7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

13.8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

Tabia ya pili ni Kuwa na moyo thabiti kwa Mungu.

Maana yake, ni kuwa tayari kukataa mambo yote yanayoweza kukukosesha na Mungu bila kujali gharama/hasara gani utakayoingia kwa kutokufanya hivyo. Huo ndio uthabiti wa moyo Mungu anaoutaka. Ambao alikuwa nao Danieli, ndio uliomfanya Mungu ampende sana.

Danieli 10:11 “Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.

Soma pia Danieli 10:19,

Unaona Danieli, alikuwa ni mtu aliyependwa sana. Hiyo yote ni kutokana na moyo wake wa msimamo, tangu alipoingia kule Babeli wakati wayahudi wote, wapo vuguvugu, akiwa bado ni kijana mdogo alipoitwa akae katika milki za mfalme hakusita kutaa vyakula najisi vya kifalme..Na hata bado akiwa mzee, walipotaka kumzuia asimwabudu Mungu wake, bado aliendelea kumwabudu kutwa mara tatu, bila kuogopwa kutupwa katika tundu la simba.

Moyo kama huo unaonyesha upendo mkamilifu kwa Mungu wake, hivyo Mungu naye angeonyesha upendo wake tu. Na ndio maana Danieli kila alipotembelewa na Malaika alianza kwa kuambiwa mtu upendwaye sana.

Vivyo hivyo na sisi, katika mambo yetu, Ikiwa boss wako/ kazi yako vinakuzuia usiwe karibu na Mungu wako kwa ule muda unaokupasa umwabudu. Ukionyesha uthabiti, kwamba ni lazima ukamtumikie Bwana wako, ukamfanyie ibada, Bwana atakupenda..Ikiwa kazini kwako wanakulazimisha uvae suruali na vimini wewe kama binti uliyeokoka, ukakataa na kusema Imani yangu hainiruhusu bila kuogopa kufukuzwa kazi, basi ujue, upo katika njia ya kupendwa na Mungu kama Danieli.

Mwisho, Tafuta kuwa na Hekima, ya kuwasaidia watu wa Mungu.

Sulemani, ni mtu mwingine ambaye biblia inatuambia alipendwa na Mungu. Tunalithibitisha hilo katika,

Nehemia 13:26 Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. TENA ALIPENDWA NA MUNGU WAKE, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; walakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.

Ni kwasababu gani? Ni  kwasababu yeye hakuwa kama wafalme wengine, kama Sauli, ambao akili zao zilielekea katika kutawala tu, na vita  dhidi ya maadui. Bali yeye alitamani kupata njia ya namna ya kuyatengeneza mambo kwa hekima, watu wa Mungu wafurahi katika Bwana na kumtimikia katika utulivu. Ndipo Mungu akasikia ombi lake, akampatia. (1Wafalme 3:1-15)

Ndio hapo utaona hata vile ambavyo hakuomba, kama vile Mali Mungu alimpatia, kwasababu alipendwa sana na Mungu kwa kile alichokitamani. Na kama isingekuwa yeye mwenyewe kuja kukengeuka mwishoni, basi angekuwa ni mfano mkubwa sana wa kuigwa katika biblia nzima.

Vivyo hivyo na wewe, ukiitafuta hekima, ujue unatafuta kupendwa na Mungu, na hekima ya Mungu ipo katika Neno lake. Ukiwa ni mtu wa kujifunza biblia, na sio msomaji tu, kama gazeti, Hekima hiyo itaingia yenyewe moyoni mwako (Mithali 2:10). Na Mungu atakusaidia kuwapa wengine neema hiyo. Na mwisho wa siku utapendwa na Mungu.

Hekima zote za kimaisha, za kiutumishi, za kifamilia, za kijamii, zipo katika Neno la Mungu. Hivyo hakuna namna utaweza kuishi bila kusoma biblia.

Hivyo mambo hayo matatu tukiyachanganya. Yaani UPENDO, UTHABITI WA MOYO, NA HEKIMA.

Basi tujue kupendwa na Mungu, ni lazima kutatokea tu kwetu, . Na faida yake ni kuwa, tutaonyeshwa na mambo makubwa Zaidi ya tunayoyajua. Danieli na Yohana ndio waliopewa siri za nyakati za mbeleni. Na mpaka sasa tunagemea sana nabii zao ili kutambua nyakati na majira ya siku za Mwisho. Vilevile hata na vyote tunavyovisumbukia vya mwilini, ikiwa tutapendwa na Mungu basi yeye mwenyewe atavisogeza karibu na sisi. Kama alivyofanya kwa mtumwa wake Sulemani, na Danieli.

Bwana akubariki, na nikutakie kupendwa kwema na Bwana.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

UPENDO NI NINI NA JE! KUNA AINA NGAPI ZA UPENDO?

Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

NITAUPATAJE UPENDO WA KI-MUNGU NDANI YANGU?

Donda-Ndugu ni nini?

MAISHA ULIYOPITIA NYUMA NI USHUHUDA TOSHA WA WEWE KUMTUMIKIA MUNGU

Kile kinara cha Taa ndani ya Hekalu la Sulemani kilikuwa kinawakilisha nini?

Moabu ni nchi gani kwasasa?

Kigao ni nini? Na Je kinafunua nini kwa agano jipya?

Rudi nyumbani

Print this post

Tofauti kati ya kukana na kusaliti ni ipi?

Kukana ni kitendo cha kumkataa mtu aliyekaribu nawe, kwa hofu/shinikizo Fulani pengine aidha kwa hofu ya kuaibishwa, au kudharauliwa, au kuuliwa au kutengwa, au kuchekwa n.k. Lakini kimsingi sio kwamba humpendi au huyo mtu hana thamani yoyote kwako.

Lakini kusaliti, ni jambo  baya Zaidi, kwasababu linahusisha, kumkataa mtu Fulani aliye karibu nawe kwa hiari yako mwenyewe, pasipo shinikizo lolote, kwa maslahi yako binafsi, ni kitendo cha moyo-baridi kabisa.

Kwamfano Petro alimkana Bwana, kutokana na shinikizo la hofu ya yeye kukamatwa na kwenda kupigwa kama Bwana..Lakini hapo nyuma utaona, alidhubutu kumuhakikisha kabisa Bwana kwamba hata wenzake wote wajapomkana, yeye hatofanya hivyo (Mathayo 26:33-35)

Utaona tena hata baadaya ya kutubu kwake baadaye, alipokutana na Bwana kule baharini bado alimuhakikisha mara tatu kuwa anampenda yeye..(Yohana 21:15-17). Kuonyesha kuwa ni shinikizo ndio lililompeleka kufanya vile, lakini moyo wake bado upo kwa Yesu.

Lakini Yuda tangu mwanzo alikuwa hampendi Bwana, japokuwa yeye alipendwa sana, mahali pengine mpaka Yesu akawa anampa siri zake za ndani japokuwa alikuwa mwizi, biblia inasema hivyo katika Zaburi 41:9

9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.

Lakini kinyume chake akarudisha mabaya badala ya mema. Utaona yeye mwenyewe kwa hiari yake akawafuata wakuu wa makuhani bila shinikizo lolote, akawaambia mtanipa nini, nikiwapa Kristo!. Wakamuahidia Pesa. (Mathayo 26.14-16)

Usaliti unafanana na mtu ambaye yupo tayari kumuua au kumletea madhara mzazi wake, kwa faida zake mwenyewe, pengine mali, au cheo, au heshima. Bila kujali kuwa yeye ndiye aliyemnyonyesha, aliyemtunza tangu akiwa tumboni, ndiye aliyemsomesha na kumvisha n.k.

Lakini kibiblia, vyote viwili yaani “kukana na kusaliti” hatupaswi kuwa navyo kwa Bwana wetu.

Leo hii wapo watu wanaomsaliti Bwana..Ndio hawa manabii na makristo wa uongo. Ambao wanajua kabisa waliokolewa kwa thamani, walitolewa chini matopeni, lakini wanapokuzwa kidogo, wanaanza kumgeuza Kristo kuwa biashara yao. Wanaacha utumishi walioitiwa, wanatumia fursa ya Kristo, kuyashibisha matumbo yao tu… Hawa ndio wakina Yuda.

Wafilipi 3:18 “Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo;

19 mwisho wao ni uharibifu, mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.

Lakini Wakanaji, ni wakristo wote, ambao mioyo yao haipo kikamilifu kwa Bwana..wapo nusu nusu, ndio wale wakipitia dhiki kidogo, wapo tayari kumwacha Kristo, kisa ndugu, au wazazi, au shughuli, au ujana au anasa..hali na mazingira yanawafanya wamkane Bwana wao moja kwa moja, kwa matendo yao.

Na hii ni mbaya sana Bwana Yesu mwenyewe alisema..

Mathayo10:32 “Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

33 Bali mtu ye yote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.

34 Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.

35 Kwa maana nalikuja kumfitini mtu na babaye, na binti na mamaye, na mkwe na mkwe mtu;

36 na adui za mtu ni wale wa nyumbani mwake.

37 Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

38 Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili.

39 Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona”.

Umeona?..Lipi bora, uchukiwe na ulimwengu leo, lakini siku ile utukuzwe na Yesu, au leo hii umkane halafu siku ile ukwane naye? Majibu yanajulikana.

Hatupaswi kuogopa kuonekana washamba kisa tumeokoka, hatupaswi kuogopa kupigwa, au kuchekwa, au kuonekana tumerukwa na akili sababu ya Yesu, mwokozi wetu. Bali tumkiri yeye kwa matendo yetu, kwasababu hata yeye mwenyewe alidharauliwa lakini akayapuuzia maradhau yao (Isaya 53:3).

Hivyo sote tujifunze kujitwika misalaba yetu tumfuate Kristo. Ufalme wa mbinguni unapatikana kwa nguvu,.

Bwana atubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kubofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx10

Mada Nyinginezo:

Je! Yuda atahukumiwa na Mungu kwa dhambi yake ya usaliti?

Chapa zake Yesu ni zipi hizo?

Na ulimi laini huvunja mfupa.(Mithali 25:15)

WAPENZI, MSIIAMINI KILA ROHO.

Neno ‘Kima’ linamaanisha nini Katika biblia? (Mathayo 27:9 )

Je! Ni kanisa lipi sahihi kumuabudia Mungu?

Matulizo ya mapenzi ni nini? (Wafilipi 2:1).

Rudi nyumbani

Print this post

Ijumaa kuu ni nini? Na kwanini iitwe kuu?

Ijumaa kuu ni ijumaa ya mwisho kabisa ya Bwana wetu Yesu Kristo kuwepo hapa duniani, ni siku ile ambayo alipitia mateso mengi, na kusulibiwa, na kufa na kisha kuzikwa. Siku hii huadhimishwa na wakristo wengi ulimwengu, kama kukumbuka la mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo kila mwaka.

Kwanini iitwe ijumaa kuu?

Lakini swali ni kwanini iitwe ijumaa kuu na sio ijumaa ya mateso au ya huzuni? Kwanini iwe kuu? Wakati siku hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana ya mamlaka ya giza, ya huzuni na masumbufu ya Yesu mwokozi wetu?

Ni kweli kwa jicho la nje! Ni siku isiyo nzuri, lakini kwa jicho la Roho ni siku ya furaha sana tena sana kwetu sisi wanadamu, Kwani ni siku ambayo kwa mara ya kwanza tulifutiwa mashtaka yetu ya hukumu, tangu tulipopoteza uzima pale Edeni. Kwani asingekufa Yesu, tusingepata msamaha wa dhambi.. Hivyo kifo chake, kilileta ukombozi mkuu sana kwetu, na matokeo yake hatupaswi kulia, kinyume chake tufurahie, kwani siku kama ya leo, karibia miaka 2000 iliyopita, tuliwekwa huru…Hivyo ni sahihi kuitwa ijumaa kuu na sio ijumaa ya mateso.

Ni sawa na mfano wa Samaki anayevuliwa, yeye kwa upande wakw kweli atapitia mateso ya kufa, lakini yule anayemvua atafurahia kupata kitoweo. Hivyo tunaweza kusema ni uchungu kwa Samaki lakini furaha kwa mvuvi..

Kifo cha Bwana wetu Yesu kilikuwa ni faida kubwa kwetu, kwasababu kama damu yake isingemwagika, tusingepata ondoleo la dhambi zetu (Waebrania 9:22).

Na je! kuna agizo lolote la kutokula nyama siku hii ya ijumaa kuu?

Jibu ni La, desturi ya kutokula nyama (ya wanyama-damu moto), ni pokeo tu la kanisa katoliki, ambao kwa mujibu wao, wanafanya hivyo kwa heshima ya Kristo, kuutoa mwili wake, kama sadaka kwetu, kwasababu nyama ni chakula cha starehe, hawafanyi hivyo ili kuyatafakari mateso ya Bwana, na sio tu katika siku ya ijumaa kuu, bali  pia siku ya jumatano ya majivu, pamoja na ijumaa nyingine zote, zinazofuata katika mfungo  hawali nyama .

Lakini agizo hilo halipo mahali popote katika maandiko. Kama ukila haufanyi makosa, au usipokula vilevile haufanya makosa.

Lakini swali lingine ni je! Kuadhimisha sikukuu hii ni dhambi?

Jibu ni la!, Biblia haijatupa agizo wala katazo la mtu kuiadhimishi siku Fulani kwa Mungu wake.

 Ni kwa jinsi yeye anavyoamini tu!.

Warumi 14:5 “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.

6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu”.

Hivyo ikiwa wewe hauoni kama siku ya ijumaa kuu inafaida yoyote kwako, basi usimuhukumu yule ambaye anaiadhimisha kwa Mungu wake, lakini pia wewe ambaye unaidhimisha usimuhukumu yule ambaye haiadhimishi. . Ikiwa unaona mfungo huo kwa kipindi hicho cha pasaka hauna maana kwako, hufanyi kosa, lakini pia usimuhukumu yule ambaye anafunga kwa ajili ya Bwana wake aliyemfia msalaba.Ndivyo ilivyo

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Easter ni nini?. Na je tunaruhusiwa kuisheherekea?

PASAKA NI NINI? NA JE TUNARUHUSIWA KUSHEHEREKEA PASAKA?

Je! kuna sikukuu za pasaka mbili? (Hesabu 9:11)

SIKUKUU 7 ZA KIYAHUDI ZINAFUNUA NINI KWETU?

Mwandamo wa mwezi/Mwezi mpya Ni nini kibiblia?

BIBLIA INAITAJA NJIA KUU YA MFALME, NJIA HII NI IPI?

KRISIMASI (CHRISTMAS) NI NINI? JE IPO KATIKA BIBLIA?

Panda/ Sauti ya panda ni nini kibiblia?(Danieli 3:5)

KITABU CHA YUDA: SEHEMU YA 3

Rudi nyumbani

Print this post

Tofauti kati ya mtu na mwanadamu ni ipi?

Mtu ni kiumbe cha kwanza kilichoumbwa na Mungu duniani, chenye mfano wake na sura yake, kilichoumbiwa utashi na ujuzi ndani yake, kilichotofautishwa  na wanyama wote na viumbe vyote vilivyoumbwa na  Mungu duniani Ndicho kinachoitwa mtu.

Tunasoma hilo katika,

Mwanzo 1:26

[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

Lakini jina Binadamu/mwanadamu, ni neno lililozuka kufuatana na jina la mtu wa kwanza aliyeitwa Adamu.

Jina hilo alipewa na Mungu..Hivyo watu wote waliozaliwa na yeye waliita “wana wa Adamu”kwa kifupi “wanadamu” ambapo jina hilo kwa kiharabu linatamkwa “bin-Adam” ambapo sisi tunatamka “Binadamu”

Lakini ni mtu yule yule..isipokuwa asingeweza kuitwa binadamu siku ile ya kwanza alipoumbwa kwasababu alikuwa bado hajapewa jina, na pia halikuwa hana baba wa mwilini.

Ni sawa na Neno mwebrania na mwisraeli… kabla ya Yakobo kubadilishwa jina lake wana wote wa Ibrahimu hata Ibrahimu mwenyewe aliitwa Mwebrania..(Mwanzo 14:13)

Lakini Yakobo alipobadilishwa jina na kuitwa Israeli, utaona uzao wake wote baada ya pale ulizoeleka na kuitwa waisraeli mpaka leo. Lakini bado mahali pengine waliendelea pia kuitwa waebrania kwa asili yao.

Ndivyo ilivyo kwa mtu na mwanadamu. Ni yule yule kulingana na majira.

Shalom.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Tofauti kati ya uchafu wa mwilini na rohoni ni  ipi?

Pango la Makpela ni lipi, je lina umuhimu wowote kwetu?

Uru wa Ukaldayo ni nini?

MAOMBOLEZO YA HADADRIMONI.

Utasi ni ugonjwa gani? (Marko 7:32).

Mjoli ni nini/ ni nani katika biblia?

Tofauti kati ya mbinguni, peponi, Kuzimu, Jehanamu, na Paradiso ni ipi?

Rudi nyumbani

Print this post

Neno ‘Kima’ linamaanisha nini Katika biblia? (Mathayo 27:9 )

Tofauti na “Kima” mnyama ambaye anajulikana (jamii ya nyani), ukirudi katika biblia Neno hili lina maana nyingine pia.

Kima maana yake ni “thamani ya kitu katika pesa”.

Kwa mfano tukisema kima cha nazi ni Tsh. 1000. Maana yake ni kuwa thamani ya nazi ni sh. 1000.

Kwamfano Neno hilo utalipata katika vifungu hivi;

Mithali 31:10 “Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani”.

Yaani thamani mke mwema, inazidi thamani ya madini ghali ya Marijani (Ruby).

Mathayo 27:9 “Ndipo likatimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema, Wakavitwaa vipande thelathini vya fedha, kima chake aliyetiwa kima, ambaye baadhi ya Waisraeli walimtia kima;”

Walawi 27: 11 “Na kama ni mnyama ye yote asiye safi, wa namna ambayo hawamsongezi kwa Bwana, basi atamweka huyo mnyama mbele ya kuhani;

12 na kuhani atamtia kima, akiwa mwema akiwa mbaya; kama wewe kuhani utakavyomtia kima, ndivyo itakavyokuwa.

13 Lakini kwamba ataka kumkomboa kweli, ndipo atakapoongeza sehemu ya tano juu ya hesabu yako.

14 Na mtu atakapoiweka nyumba yake iwe wakfu kwa Bwana ndipo kuhani ataihesabu kima chake hiyo nyumba, ikiwa njema ikiwa mbaya; kama kuhani atakavyoihesabu kima chake ndivyo itakavyokuwa”.

Soma pia Walawi 27:23, Ayub 18:28, Matendo 7:16

Je, kipo kima kinachozidi thamani ya Bwana Yesu?

Yuda alijaribu, kumsaliti Bwana kwa kima cha fedha, lakini Pamoja na kupokea mapesa yote, bado mwisho wa siku aliona, thamani yake hailinganishwi na utajiri wowote wa ulimwengu, ijapokuwa alikuwa ni mwizi lakini utaona alirudisha fedha zao zote, na kwenda kujinyonga.

Sasa Ikiwa watu waovu wanauona uthamani wa Bwana, hadi kwenda kujiua, iweje wewe uone kazi ni bora kuliko Bwana Yesu, anasa ni bora kuliko ibada?.

Je! thamani ya Bwana wako inazidi thamani ya huu ulimwengu? Bwana Yesu alisema Itakufaidia nini uupate ulimwengu mzima halafu upate hasara ya nafsi yako? Itakufaidia nini?

Tubu mgeukie Bwana..

Ikiwa hujampa Bwana Yesu Maisha yako, na upo tayari kufanya hivyo leo, kwa kumaanisha kabisa, basi fungua hapa kwa ajili ya mwongozo wa Sala ya Toba. >>> KUONGOZWA SALA YA TOBA

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Konde la Soani ni nini? (Zaburi 78:12,43)

Deraya ni nini? Kama tunavyosoma katika Isaya 59:17

Bushuti ni nini?

Nondo ni nini kama tunavyosoma katika biblia?

Tunguja ni nini katika biblia? (Mwanzo 30:14).

Hisopu/ Hisopo ni nini katika biblia?(Zaburi 51:7)

Kuhusuru ni nini kibiblia? (Luka 19:43)

Kujuzu ni nini kama tunavyosoma katika 2Wakorintho 12:4?

Rudi nyumbani

Print this post

Pango la Makpela ni lipi, je lina umuhimu wowote kwetu?

Ni eneo la pango ambalo lilikuwa karibu na mji wa Israeli unaoitwa Hebroni, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa mtu mmoja aliyeitwa Efroni, kwa ajili ya maziko ya mke wake Sara.

Mwanzo 23:13 “Akamwambia Efroni, na watu wa nchi wanasikiliza, akisema, Tafadhali unisikilize; nitatoa kima cha shamba, nawe ukipokee kwangu, nami nitamzika humo maiti wangu.

14 Efroni akamjibu Ibrahimu, akamwambia,

15 Bwana wangu, unisikilize. Sehemu ya nchi, ambayo thamani yake ni shekeli za fedha mia nne, n’nini hii baina yako na yangu? Basi uzike maiti wako.

16 Ibrahimu akakubali maneno ya Efroni. Ibrahimu akampimia Efroni ile fedha aliyotaja masikioni mwa wazawa wa Hethi, shekeli za fedha mia nne za namna inayotumika na wenye biashara”.

Eneo hilo baadaye lilikuja kugeuka kuwa kaburi la kifamilia, kwani hapo hapo ndipo Ibrahimu alipokuja kuzikwa na watoto wake, halikadhalika, ndipo Yakobo na Esau walipomzikia baba yako Isaka,

Na wakati wakiwa kule Misri, Yakobo aliwaagiza Watoto wake,pia  wakamzike katika kaburi hilo la familia, la Makpela.

Mwanzo 49:29 “Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;

30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.

31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;

32 shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi”.

Eneo hilo kwasasa, pale Israeli limejengwa msikiti, ujulikanao kama “msikiti wa Ibrahimi”, japo wote wayahudi na waislamu, hakuna hata mmoja anaweza kusema anao umiliki wa moja kwa moja wa hapo.

Lakini Je pango la makpela lina umuhimu kwetu hadi sasa au kwa Wayahudi?

Pango hili, au lolote lile ambalo lilizikiwa watakatifu, halina umuhimu wowote katika Imani yetu, Zaidi ya mambo ya kihistoria tu. Myahudi au mkristo yoyote ukizikwa karibu na eneo hilo, hakutakufanya uende mbinguni, Wapo wengine wanafikiri, wakienda Yerusalemu na kuomba kwenye ule ukuta wa Nehemia wa maombolezo, ndio maombi yao yatasikiwa. Au wakienda kubatizwa katika mto Yordani kama Bwana Yesu ndio ubatizo wao utapokelewa, jambo ambalo sio kweli.

Halikadhalika na Pango hilo la makpela halina umuhimu wowote, kwa mtu yeyote, kuzikiwa pale.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

Watoto wa Ibrahimu/Wana wa Ibrahimu walikuwa ni wangapi?

Je! ni halali kwa mtu wa Mungu kutumia njia za uzazi wa mpango,ikiwamo mipira?

Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri.

MWENGE WAKO WA UHURU UPO WAPI?

Uru wa Ukaldayo ni nini?

Rudi nyumbani

Print this post