Category Archive YESU KRISTO

Je ile nyota ya asubuhi inamwakilisha shetani au Bwana Yesu?

Swali: Katika Ufunuo 22:16, tunasoma ile nyota inamwakilisha Bwana Yesu, lakini tukirudi katika Isaya 14:12, tunasoma ile nyota inamwakilisha shetani, hapa imekaaje?

Jibu: Tusome..

Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi”.

Tusome tena..

Isaya 14:12 “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa”

Kwa haraka ni rahisi kufikiri au kutafsiri kuwa hiyo ni nyota ile ile moja inayozungumziwa hapo, lakini ki uhalisia sio nyota moja bali ni nyota mbili tofauti, isipokuwa zote ni nyota za asubuhi.

Sasa tofauti ya nyota hizi mbili ni ipi?.

1.MAJIRA

Nyota inayotajwa katika Ufunuo 22:16 ambayo inamwakilisha Bwana Yesu inatajwa kama Nyota ya asubuhi, lakini ile ya Isaya 14:22 ambayo inamwakilisha shetani inatajwa kama ni nyota ya alfajiri. SASA ALFAJIRI na ASUBUHI, ni majira mawili tofauti.

Alfajiri ni mapema zaidi kuliko asubuhi, alfajiri inaanza saa 10 usiku mpaka saa 12 na asubuhi inaanza saa 12 mpaka saa Tano na dakika 59.

Sasa hapo biblia inaposema shetani ni nyota ya alfajiri maana yake ni kuwa nyota hiyo inaonekana alfajiri tu wakati wa giza na kukisha pambazuka inapotea lakini hiyo nyingine ambayo inamwakilisha Bwana Yesu ni Nyota ya asubuhi maana yake ni kuwa wakati kunapopambazuka na ile nyota ya alfajiri inapopotea kutokana na mwanga wa jua, hii nyota ya asubuhi bado itakuwa inaendelea kuangaza..

Sasa kama wewe ni mtu wa kupenda kuchunguza anga, utakuwa umegundua kuwa kunakuwepo na nyota moja asubuhi ambayo wakati nyota nyingine zimeshapotea yenyewe bado inaangaza.. Sasa nyota hiyo ndiyo inayomwakilisha Bwana Yesu, na ndio nyota ya asubuhi.

Na sifa nyingine ya hii nyota ya asubuhi, huwa pia ndio ile ile ya jioni, wakati ambapo nyota nyingine bado hazijatokeza kutokana na mwanga wa jua, hii ya asubuhi ndio inakuwa ya kwanza kutokeza..hiyo ikifunua tabia nyingine ya Bwana Yesu kuwa yeye ndiye MWANZO na MWISHO. (Alfa na Omega, Ufunuo 22:13).

Sasa kwa mapana na marefu kuhusu hii nyota ya asubuhi, na tabia zake kwa undani unaweza kufungua hapa >>> NYOTA YA ASUBUHI

Sababu hii ya majira itatupeleka moja kwa moja kuelewa tofauti nyingine inayofuata ya nyota hizi mbili.

2. MNG’AO

Nyota inayotajwa katika Ufunuo 22:16, ambayo inamwakilisha Bwana Yesu Kristo inatajwa kama ni nyota yenye KUNG’AA  Lakini inayozungumziwa katika Isaya 14:12 haitajwi kama inang’aa, ni kama nyota nyingine  tu ambazo zinaangaza usiku…lakini ya asubuhi haing’ai..maana yake kukisha pambazuka basi yenyewe inaisha nguvu, lakini nyota ya Bwana Yesu inang’aa katika giza na vile vile katika Nuru. Na hata mchana kwasababu ya ukamilifu wa Mkuu wa uzima Yesu.

Mithali 4:18 “Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, Ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu.

Je umemtumainia Yesu aliye Nuru ya kweli, ambayo  wakati wa mchana atakuwa nawe na wakati wa usiku utamwona?.

Shetani ni nyota inayoangaza kwa nuru ya uongo ndio maana haitajwi kama ni nyota ing’aayo (Soma 2Wakorintho 11:14), na inayopotosha, na inayoangusha wengi kama maandiko yanavyosema hapo katika Isaya 14:12.

Hivyo Kama bado hujampokea Yesu mpokee leo, na unampokea kwa kuamini kuwa yeye ni Bwana na alikuja kufa kwaajili ya dhambi zako na kukiri kwa kinywa chako, na kuungama dhambi zako zote kwa kumaanisha kutorudia tena kuzifanya.

Na baada ya hapo kutafuta ubatizo sahihi ambao ni kwa jina la Bwana Yesu Kristo na kwa maji mengi (Matendo 2:38),

Na baada ya hapo Roho Mtakatifu atakuongoza na kukutia katika kweli yote ya maandiko.

Maran atha!.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

NYOTA YA ASUBUHI.

NAYAJUA MATENDO YAKO.

MIAMBA YENYE HATARI.

Miungu wasio na kikao pamoja na wenye mwili.

MAFUNDISHO KWA WANAWAKE

Rudi nyumbani

Print this post

Je! Ni Kristo au Kristu? Lipi ni neno sahihi?

JIBU: Neno Kristo limetoka katika lugha ya kigiriki (Khristos) ambalo likitafsiriwa katika Kiswahili linatamkika kama KRISTO.

Lakini Neno hili hili, kwa lugha ya kilatini  (Christus), likitafsiriwa katika Kiswahili linatamkika kama  KRISTU.

Swali ni Je! Ipi ni tafsiri sahihi?

Tufahamu kuwa biblia yetu  (husasani sehemu kubwa ya agano jipya) haikuandikwa katika lugha ya kilatini, au kiingereza, au kichina, au kifaransa.. Hapana bali iliandikwa katika lugha ya Kigiriki ya kale. Hivyo tafsiri ya biblia yetu ya Kiswahili tunaitolea moja kwa moja kutoka katika lugha hiyo ya kigiriki, na sio kiingereza au kilatino.

 Hivyo ni vizuri tukitumia lahaja ya lugha ya asili, iliyotumika kwenye biblia(Kigiriki) kuliko nyingine.

Japo wapo wanaotumia lahaja ya kilatino (Kristu), pia hawafanyi makosa, maadamu ni Kristo Yule Yule analengwa na sio mwingine. Ni sawa na anayesema ‘Sulemani’ au ‘Solomoni’. Ni Yule Yule mlengwa isipokuwa katika lahaja mbili tofauti.

Maana ya Kristo ni “Mtiwa-Mafuta” Ambapo kwa lugha ya kiyahudi anaitwa “MASIHI”. Hivyo tunaposema Yesu Kristo, tunamaanisha Yesu mtiwa mafuta.  Yaani Yesu aliyeteuliwa na Mungu mahususi kwa kazi ya kuwakomboa wanadamu. Ni yeye tu ndiye mwokozi wa ulimwengu wala hapana mwingine.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

Mada Nyinginezo:

JINA LA MUNGU NI LIPI?

Akida ni nani kibiblia, na kazi yake ni ipi? (Mathayo 8:5)

Nini maana ya ELOHIMU?

SEMA KWA LUGHA NYINGINE.

Babewatoto ni nani katika biblia?(Isaya 34:14).

Ni nani aliye kipofu, ila mtumishi wangu?

Mharabu ni nani katika biblia?

Rudi nyumbani

Print this post

Kwanini Yesu Kristo ni mwana wa Adamu?

JIBU: Vipo vyeo vitatu maalumu ambavyo vilimtambulisha Bwana Yesu Kristo…1) Mwana wa Mungu 2) Mwana wa Adamu 3) Mwana wa Daudi. Vyeo hivi kila kimoja kina maana yake..

Sasa kabla ya kuendelea mbele zaidi…ni muhimu kufahamu kuwa cheo cha “Mwana” ni cheo cha “urithi”…Maana yake ni kwamba mfano ukiwa na mtoto wako mmoja wa pekee huyo atarithi kila ulicho nacho…ikiwemo enzi yako yote, mali zako pamoja na hata jina lako…

Sasa katika biblia..mahali popote ambapo Neno Mwana linaanza kwa herufi kubwa…hilo linamzungumzia mtu mmoja tu maalumu ambaye ni Yesu Kristo…lakini ukiona neno “mwana” limeanza kwa herufi ndogo kama hivyo, basi fahamu ni mtu mwingine tofauti na Yesu anayezungumziwa hapo.. Kwa mantiki hiyo basi “wana wa Mungu” wapo wengi lakini “Mwana wa Mungu ni mmoja tu”…mimi na wewe tuliompokea Yesu ni wana wa Mungu….kadhalika wana wa Daudi wapo wengi..lakini “Mwana wa Daudi” ni mmoja tu ambaye ni Yesu…Sulemani alikuwa pia ni ‘mwana wa Daudi’, Hezekia, Yosia, Manase wote hao walikuwa ni wana wa Daudi….Hali kadhalika pia “wana wa Adamu wapo wengi”…mimi ni mwana wa Adamu(au kwa kifupi Mwanadamu)..wewe ni mwana wa Adamu lakini “Mwana wa Adamu” yupo mmoja tu ambaye ni Yesu…ni kama vile miungu wapo wengi lakini Mungu ni mmoja tu!.

Sasa tukirudi kwenye shabaha yetu ya msingi, ambapo tumeona kuwa Neno ‘mwana’ linazungumzia ‘urithi’

Hivyo basi vyeo hivyo vitatu tunaweza kuviweka katika mnyumbuliko ufuatao…1)Mrithi wa Mungu 2) Mrithi wa Adamu na 3) Mrithi wa Daudi.

Sasa unaweza kujiuliza Kristo alirithi nini kutoka kwa hawa watatu?

  1. Mrithi wa Mungu.

Kama mtu ataitwa Mwana wa Mungu maana yake ni kwamba ni Mrithi wa enzi yote ya Mungu na Ukuu …na huyo si mwingine zaidi ya Yesu Kristo, ambaye alirithishwa vyote.

Waebrania 1:1 “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika MWANA, ALIYEMWEKA KUWA MRITHI WA YOTE, TENA KWA YEYE ALIUFANYA ULIMWENGU.

3 Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu”

Kwahiyo hiyo ndio sababu ya Kristo kujulikana kama MWANA WA MUNGU..Ni kwasababu amerithi milki zote za Mungu..

Mathayo 28:18 “Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani”.

  1. Mrithi wa Daudi.

Cheo cha pili ni cheo cha MWANA WA DAUDI/Mrithi wa Daudi..Sasa ili kujua ni kwanini Kristo aliitwa mwana wa Daudi ni vizuri kumjua kwanza Daudi alikuwa ni nani…(kwa maelezo marefu unaweza kututumia ujumbe inbox tutakutumia somo lake)…lakini kwa ufupi ni kwamba Daudi alikuwa ni mfalme pekee aliyepata Hekima ya kufikiria kumjengea Mungu nyumba ya kifalme katika wa Yerusalemu…na hivyo kumfanya Mungu kuuchagua ule mji kuwa makao makuu yake ya kifalme Duniani (yaani Yerusalemu).

Kama sio Daudi basi mpaka leo pengine Mungu asingekuwa na mji wake maalumu duniani kati ya miji ya Israeli…(Tusingelisikia hili neno Yerusalemu au Sayuni likirudiwa rudiwa katika maandiko, kwani ungekuwa mji kama miji mingine tu, wala ile Yerusalemu mpya kwenye ufunuo pengine ingeitwa kwa jina lingine)…

Lakini Daudi ndiye aliyefanya Yerusalemu ikawa mji wa kifalme wa mwokozi..na Mungu alimwahidi hatakosa mtu wa kukaa katika kiti cha kifalme kutoka katika uzao wake…na katika uzao wake huo yupo mmoja ambaye ni mkuu sana alitabiriwa kutokea huko na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO mwenyewe(kasome Mathayo 1:1-17) ambaye atakuwa mfalme juu ya Dunia nzima! Na ndiye atakayeijenga Yerusalemu mpya ile itakayoshuka kutoka mbinguni…na kukaa na watu wake. Na ndio maana Kristo ilimpasa aitwe mwana wa Daudi kufuatana na yale Daudi aliyoyafanya na kukabidhiwa.

  1. Urithi wa Adamu.

Na cheo cha Mwisho cha Yesu Kristo ni cheo cha MWANA WA ADAMU au Mwana wa mtu,…sasa kama tunavyomjua Adamu alikuwa ni mtu wa kwanza kuumbwa na kupewa Urithi wote na mamlaka yote duniani, kwamba atawale kila kitu, na kwamba viumbe vyote vitamwogopa!….lakini kama tunavyojua aliuuza na kuupoteza ule urithi wake aliopewa na Mungu kwa adui shetani…Hivyo ili urithi huo umrudie tena mwanadamu..basi hakuna budi aje kutokea Adamu mwingine wa pili, ambaye atakaribiana sana kufanana na Yule Adamu wa kwanza,…ambaye ataurithi ule urithi na enzi yote aliyopewa Adamu ya kwanza…

1Wakorintho 15:45 “Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha”.

Adamu wa pili atakuwa ni mwanamume kama Yule wa kwanza, naye atapewa mamlaka kama Yule wa Kwanza wa pale Edeni, na yeye ni lazima awe wa kwanza kuumbwa …na huyo si mwingine zaidi ya Yesu Kristo..ambaye ndiye limbuko letu rohoni na ndiye aliyekabidhiwa mamlaka yote ya duniani. Hiyo ndiyo sababu Yesu anaitwa Mwana wa Adamu…ni kwasababu amerithi mamlaka yote na enzi yote Yule Adamu wa kwanza aliyokuwa nayo (aliyopewa na Mungu)..

Mathayo 11:27 “Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia”.

Hivyo Yesu Kristo ndiye Mwanzo na Mwisho, Alfa na Omega…Ndiye mwanadamu kamili, ndiye aliye na mamlaka yote sasa, ndiye mwenye enzi ya kifalme, ndiye Mungu mwenyewe katika mwili. Na ndiye njia ya kufika mbinguni…Kama hujamwamini wala kumpokea…ni vyema ukafanya hivyo kwasababu hakuna njia nyingine yoyote unaweza kumfikia Mungu kama isipokuwa kwa kupitia yeye..

Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 MIMI NI ALFA NA OMEGA, MWANZO NA MWISHO, WA KWANZA NA WA MWISHO.

14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake”.

Bwana atubariki. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

USIPOKUWA MWAMINIFU, NAFASI YAKO ITACHUKULIWA.

TAZAMA, MWISRAELI KWELI KWELI, HAMNA HILA NDANI YAKE!

Kuna ufufuo wa aina ngapi?

MAPIGO YA VITASA SABA, NA SIKU YA BWANA.

MAJESHI YA PEPO WABAYA.

Rudi Nyumbani:

Print this post

Kwanini Kristo hakuitwa Imanueli badala yake akaitwa Yesu?

SWALI: Unabii uliotolewa na Isaya kumuhusu Kristo unasema angekuja kuitwa Imanueli (Isaya 7:14), lakini badala yake tunaona alikuja kuitwa Yesu? Ni kwanini?


JIBU: Tukisoma pale katika Mathayo 1:19-23 Inasema..

Mathayo 1:19 “Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.

20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.

22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema,

23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; NAO WATAMWITA JINA LAKE IMANUELI; YAANI, MUNGU PAMOJA NASI”.

Jiulize ni kwanini biblia haijaishia tu pale kwenye jina Imanueli, badala yake ikamalizia kuandika mpaka tafsiri yake, yaani “Mungu Pamoja nasi”?..Ni Kwasababu msisitizo upo hapo kwenye hiyo tafsiri na sio jina tu..

Ukiangalia tena utaona Malaika anasema “Nao watamwita” Ikimaanisha “sisi” ndio tutakaomwita yeye kuwa ni Mungu ambaye yupo Pamoja nasi..Lakini yeye jina lake hasaa sio hilo bali ni YESU ..ambayo tafsiri yake ni (YEHOVA-MWOKOZI).

Jambo hilo limekuja kutumia kama lilivyo kwasababu sisi ndio tunaojua Yesu kwetu sisi si mwokozi tu, bali ni Zaidi ya mwokozi,..Ni Mungu kwetu, aliyeutwaa mwili akaishi Pamoja nasi..Kama maandiko yanavyosema..

Yohana 1:1 “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu”…..

14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli”.

1Timotheo 3:16 “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.”

“Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili”(Wakolosai 2:9) .

“tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;(Tito 2:13)

Hivyo tunao ujasiri wote wa kusema kuwa YESU ni MUNGU WETU..

Yaani IMANUELI.

Haleluya. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Mada Nyinginezo:

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

nini maana ya haya maneno aliyosema Bwana ; Tuliwapiga filimbi wala hamkucheza; Tuliomboleza wala hamkulia?

 

WINGU KUBWA LA MASHAHIDI.

BWANA HUWAJUA HAO WAMKIMBILIAO.

NA YEYE ALIYEKETI JUU YA WINGU AKAUTUPA MUNDU WAKE JUU YA NCHI, NCHI IKAVUNWA.

Je! kuna ubaya wowote kuwaombea ndugu zetu waliokufa katika dhambi, Mungu awakumbuke katika ufalme wa mbinguni?.

NG’OMBE MWEKUNDU ALIYEZALIWA ISRAELI, ANAFUNUA NINI?

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWANINI YESU KRISTO NI WA MUHIMU KWETU SASA?

Kwanini yesu kristo ni wa muhimu kwetu?

Moja ya majukumu tuliyonayo ni “Kumfahamu sana Yesu Kristo”..Hili ni moja ya jukumu kubwa sana tulilonalo kwasababu ndio msingi wa ukombozi wetu..Tusipomfahamu Yesu kwa mapana na marefu basi ni ngumu kujua nafasi zetu pamoja na Neema tuliyopewa…Na matokeo ya kutomwelewa Yesu ni kuishia kuidharau neema na kupotea.

Sasa jukumu la kumjua Yesu, sio kujua sura yake alikuwa ni mzuri  kiasi gani, au alikuwa na rangi gani, au alikuwa na nywele za namna gani, au alikuwa anapenda kula nini?..Hapana hilo sio jukumu tulilopewa la kumfahamu kwa namna hiyo..Jukumu tulilopewa ni KUIFAHAMU VIZURI ILE NAFASI ALIYONAYO. Tukishaifahamu ile nafasi basi tutamjua Mungu sana. Na mpaka sasa hakuna aliyefikia kikomo cha kuijua hiyo nafasi yote..bali kwa siku zinavyozidi kwenda tunazidi kuilewa na ndivyo tunavyozidi kumpenda Mungu na kumheshimu.

Waefeso 4:13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo”

Leo tujikumbushe ni kwa namna gani kifo cha Yesu kilivyokuwa na umuhimu kwetu sisi tuliokuwa tumepotea kwenye dhambi.

Katika Biblia tunasoma muda mfupi kabla ya Bwana Yesu kupandishwa msalabani..Pilato aliwafungulia mfungwa mmoja ambaye alikuwa ni mkatili katika mji ule..Na huyo si mwingine Zaidi ya BARABA.

Huyu Baraba alikuwa na Kesi ya mauaji ya watu kadhaa hapo mjini, na alikuwa ni mkatili..Biblia inamwita “mfungwa mashuhuri” (Mathayo 27:16). Watu wote walimshuhudia kuwa alikuwa ni mkatili, hivyo walikuwa hawamhitaji hata kidogo, hivyo alikamatwa na warumi na kutiwa gerezani akisubiria hukumu yake ipite..Na bila shaka angeuawa kifo cha kikatili kuliko mtu mwingine yoyote yule, kwasababu kila mtu alikuwa amemkinai. Na alivyokuwa kule gerezani kila mtu pamoja na yeye mwenyewe alikuwa anajua ndiye anayestahili adhabu kubwa kuliko wote. Kulikuwa hakuna uwezekano wa kupona hata kidogo…Lakini kama wasemavyo watu “hata mnyororo ulio imara sana, lazima utakuwa na sehemu yake dhaifu”..Hata kama sehemu inaonekana hakuna njia basi Mungu anaweza kufanya njia.

Baraba akiwa mule gerezani labda moyo wake ukaanza kumchoma na kujihisi alifanya makosa, aliua wale watu pasipo hatia, akitazama pembeni anajua kuna mtu aliua tu mtu mmoja na alihukumiwa kukatwa kichwa yeye akijiangalia kashaangusha watu kadhaa huko nyuma hukumu yake itakuwaje?…

Siku moja tu asubuhi alishangaa anaitwa nje, atoke gerezani..na alipotoka akijua anakwenda kuuawa na pengine wafungwa wote wakajua anakwenda kumalizwa kwa hasira nyingi..ghafla anatoka nje anaona watu wengi wanamshangilia nje, wanafurahi kufunguliwa kwake..anaona wanampigia mpaka vigelegele, Baraba afunguliwe! Baraba afunguliwe!… kwa pembeni anamwona Pilato anamwambia kuanzia leo upo huru kama watu wengine, rudi nyumbani kwako kafurahi na mke wako na Watoto wako, upo huru..Wakati anashangaa jambo hilo linawezekanaje labda walikosea wanamaanisha Baraba mwingine…. kwa pembeni kidogo anaona mtu amewekwa taji la miiba kichwani kakaa kimya sana, mpole kama mwanakondoo anayekaribia kuchinjwa….Pilato anamwambia Yule kabeba hukumu yako…Yule atakufa kwa niaba yako…Ni wazi bila shaka alishangaa kidogo..

Naamini Maisha yake yalianza kubadilika kuanzia pale na kuendelea…Kwasababu alijua chanzo cha uzima wake na uhuru wake ni nini?..kwamba kama si Yesu kuwa vile alivyokuwa, kufanyiwa yale aliyofanyiwa, kama sio Yesu kukataliwa yeye angekufa…kwasababu kama Yesu angekubaliwa basi yeye asingepona…Hivyo kwa kupingwa na kupigwa kbbwake Yesu yeye amepona!.

Je mtu wa namna hiyo atarudia tena kuua?, atamkebehi YESU?, Ataudharau msalaba? Atajisifu?…Na je mfano akiudharau msalaba na kutoka pale na kuendelea na mauaji yake unahisi ni nini kitampata mbele za Mungu na watu?

Hiyo ndiyo nafasi ya Yesu kwetu ilivyo… Baraba ni mfano wa mimi na wewe…Sasa ni kwa namna gani Bwana Yesu anachukua dhambi zetu?..Sio kwa kubeba kifurushi na kukiweka mabegani kwake…Hapana ilimgharimu Maisha yake…ilimgharimu kukataliwa, kupingwa, kutemewa mate, kutukanwa, kudhihakiwa..Kwajinsi alivyodhihakiwa sana na kutukanwa sana ndipo thamani ya Baraba kule gerezani ilivyokuwa inazidi kupanda. Hadhi ya Bwana Yesu ilishuka ili yetu ipande.

Wakati Baraba yupo kule gerezani alikuwa hajui kama Kristo anatukanwa huko nje kwaajili yake.

Ndugu yangu…Msalaba sio jambo la kupuuzia au kuchezea hata kidogo…Mambo yote mema unayoyapata leo hii ni kwasababu ya Yesu Kristo, kama sio yeye dunia ingeshaisha siku nyingi…Mungu angeshaimaliza dunia kwa laana kitambo sana…Maisha yangeshaisha miaka mingi sana iliyopita huko nyuma.

Watu wengi hawajui kuwa wanapiganiwa na Mungu pasipo hata wao kumwomba Mungu, wengi hawajui hata katika uasherati wao ni Mungu ndiye anayewapa riziki pasipo hata wao kumwomba, na hawajui ni hiyo neema, ni kwasababu ya YESU KRISTO. Kama sio Yesu kuteseka miaka 2020 iliyopita hakuna mwasherati ambaye mpaka leo angekuwa anaishi..Wote tulistahili kufa.

Lakini Neema hii unaichezea..unadhani ni haki yako kuishi na usherati wako, uwizi wako, ufisadi wako, ulevi wako, uuaji wako, utukanaji wako, usagaji wako, ulawiti wako, uchafu wako n.k Hii Neema ipo siku itaisha na siku hiyo ndipo utakapojua kuwa Hii neema ilikuwa ni ya thamani kiasi gani.

Hii Neema itakapoondolewa, itaondoka na kanisa..watakatifu wataondolewa ulimwenguni, dhiki kuu itaanza, mpingakristo atanyanyuka, ataua wengi na baadaye maji ya bahari na visima na mito yote itageuzwa kuwa damu, utatokea ugonjwa wa majipu ulio hatari kuliko huu uliozuka sasa unaoitwa CORONA. Utasambaa duniani kote hakuna mtu atakayesalimika kwa wale watakaoachwa kwenye unyakuo, wakati huo hakutakuwa na mtu wa kukwambia utubu dhambi zako.

Siku hizo hakutakuwa na masinema tena watu wanayokwenda kuangalia michezo , hakutakuwa na mipira watu wanayokwenda kuangalia, barabara zitakuwa wazi, kila mtu atakuwa peke yake peke yake akiugulia mapigo hayo..Unaona leo ugonjwa huu wa Corona leo ulivyosababisha mabarabara kufungwa, mashule kufungwa, hakuna mtu kwenda kazini kwenye mataifa yaliyoathirika, kila mtu kajifungia ndani..siku hizo itakuwa mara 100 ya hiyo, hata mnyama wako wa kufugwa hutamsogelea, kutakuwa hakuna kutembea mabarabarani..kila mtu anashiriki mapigo hayo kivyakevyake.

Katikati ya gonjwa hilo la ajabu litakalolipuka la majipu…mvua zitaacha kunyesha, jua litashushwa chini, kutakuwa hakuna kitu chochote kilicho kijani kitakachoonekana, mvua ya mawe itashuka, sio ya mawe ya barafu..mawe kama mawe, makubwa kama talanta, kutatokea matetemeko na milipuko ya volcano duniani kote, na baada ya siku za maunguzo ya jua kupita….jua litakuja kuondolewa kutakuwa na giza la ajabu kuliko lile lililotokea kipindi cha Farao, nyota hazitakuwepo, mwezi utaonekana kuwa mwekundu kama damu kwa kipindi kirefu, mambo hayo yote yanakuja ndani ya wakati mmoja..na mambo mengine mengi ya ajabu yatakuwepo, mambo haya sio hadithi za kutunga kasome Ufunuo 16 yote, utaona, na kama unyakuo utakupita basi utayashuhudia hayo yote.

Waebrania 10:25 “wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.

26  Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;

27  bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

28  Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29  MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?

30  Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.

31  Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.”

Kama hujageuka na kutubu mlango wa Neema leo upo wazi…Ni heri usitumie muda ku-comment na ku-like badala yake ukatubu kama hujatubu. Usisome tu kama hadithi ya kukufurahisha, bali ujumbe huu ukawe sababu ya mageuzi kwako..

Na maana ya kutubu ni “kugeuka”..maana yake unadhamiria kuyaacha yale uliyokuwa unayafanya yasiyompendeza Mungu, na unakwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi na kupokea Roho Mtakatifu. Mambo hayo unayafanya kwa moyo wako wote.

Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako

jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa > WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

Tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu ni ipi?

 Habari ya UZIMA? Naomba unisaidie tofauti ya kazi ya Damu ya Yesu na Jina la Yesu Kwa Sisi Tumwaminio/wafuasi wake. Je! Damu ya Yesu inakazi ya Kutulinda sisi au Mali zetu pale tunapoomba kupitia Damu? Ni sahihi kuomba hivyo? Je! Damu ya Yesu inatumikaje Kwa sisi wakristo?

JIBU: Ili kuelewa tofuati ya utendaji kazi wa damu ya YESU na Jina Jina la Yesu, Ni vizuri kwanza tukajifunza katika maisha ya kawaida…Katika maisha ya kawaida mtu anayo DAMU na vilevile analo JINA…Jina la mtu linaelezea utambulisho wa mtu yule, cheo alicho nacho, heshima aliyo nayo, nguvu aliyo nayo na mamlaka aliyonayo.. Kwamfano katika nchi yoyote mtu mwenye jina kubwa na lenye nguvu kuliko wote ni Raisi wa nchi hiyo…

Vilevile katika upande wa pili DAMU ya mtu inaelezea Uzima wa huyo mtu, asili ya mtu huyo, Undugu alionao na wanafamilia wenzake, na inaelezea pia Urithi alionao..yaani watu atakaowarithisha mali zake.

Na kila Raisi wa nchi au Mfalme, anayo DAMU na vilevile analo JINA.

Sasa tukirudi katika mamlaka ya kimbinguni ambayo hiyo ni kuu kuliko ya kiduniani…Tunaye Mfalme mmoja, naye ni Yesu Kristo (Huyo ni Zaidi ya Raisi yeyote wa nchi)…Na huyu analo JINA vilevile na anayo DAMU.

Kama tulivyosema damu inaelezea undugu wa mtu, yaani uana-familia.….na Bwana Yesu pia anao ndugu zake wa damu,..ambao ni wale wote waliozaliwa mara ya pili…Hao wanayo mamlaka ya kumsogelea katika meza yake na kula naye, na kumwomba lolote kwa jina lake na kupewa…Mtoto wa mfalme akiomba apewe jimbo fulani kutoka kwa Baba yake…haitachukua mlolongo mrefu kupewa haja ya moyo wake..mara moja tu baba yake atamwandikia hati ya nakala kwa jina lake na kuipeleka mahali husika kupata anachokihitaji…Na huyo mtoto kwa jina la Baba yake anaweza kupata lolota katika nchi…..Lakini hebu mtu wa kawaida tu amsogelee mfalme wa nchi na kumwomba apewe hicho kipande cha ardhi uone mlolongo wake!…anaweza kufukuzwa au hata asipofukuzwa basi ombi lake linaweza kuchukua muda mrefu sana kujibiwa…

Sasa yote hayo ni kutokana na nini?

Ni kutokana na kwamba mtoto wa Mfalme anatumia DAMU kupata lolote kwa JINA la Baba yake…wakati wengine wanatumia bahati tu!..kwamba ombi lao likikubaliwa ni kama wamepata bahati tu!..wangeweza kukataliwa…lakini mtoto wa Mfalme anauhakika kwasababu anatumia damu.

Kwahiyo tukirudi kwenye swali: Tofauti kati ya damu ya Yesu na jina la Yesu ni ipi? Tumeshaiona hapo juu na …na je ni sahihi kuomba kutumia damu ya Yesu kutulinda sisi na mali zetu? (damu ya Yesu inatumikaje)

Jibu: Mtu aliyeokoka tayari damu ya Yesu inanena mema juu yake..kama kwa hiyo mifano tuliyoiona hapo juu…Haihitaji kumweleza sana Baba wa mbinguni kwamba unahitaji ulinzi..kitendo tu cha kuwa mwanawe wa damu tayari ni jukumu lake kukulinda wewe na mali zako..na kwa jina lake kupewa chochote katika huu ulimwengu..Tofauti na mtu ambaye hajaokoka…huyo si mwana wa Mungu,..huyo hana uhusiano wowote na damu ya Mungu…Kwahiyo hata akiomba lolote kwa jina la Yesu kwake ni bahati nasibu kupata anachokiomba…

Je umeokoka?…

Umefanyika kuwa mwana wa Mungu?..umekuwa damu moja na Mungu?..Kama hujaokoka basi fahamu kuwa ni ngumu wewe kupokea upendeleo wowote kutoka kwa Mungu..Kwasababu Mungu anawaangalia kwanza wanawe kuwapatia mema (Soma Warumi 8:28-29)..na hao ndio atakaowarithisha uzima wa milele…hawezi kuwarithisha watu wasio wanawe…hata wewe mwenyewe ni ngumu kumrithisha mtoto asiye wako mali zako na kuwaacha wanao bila urithi…

Sasa kwanini uwe kama Yatima siku ile?..wakati wenzako wanairithi mbingu…wewe unarithi ziwa la moto kutoka kwa baba yako ibilisi?..mwache shetani aende kuzimu mwenyewe wewe mgeukie Kristo, mwenye urithi udumuo.

Hivyo unachopaswa kufanya ni kutubu kama hujatubu, kama ulikuwa ni mwasherati unatubu kwa kuacha kufanya hivyo, kama ulikuwa unaweka make-up unaacha, kwasababu mabinti wa Mungu waliozaliwa kwa damu ya Mungu hawafanyi hivyo, ..kama ulikuwa unasuguliwa kucha na wanaume saloon, utubu na kuacha,.., kama ulikuwa unavaa vimini, unapamba uso, unavaa surali, unatubu na kuacha kama ulikuwa ni mlevi, mvutaji wa sigara na mfanyaji masturbation na mtazamaji wa picha chafu katika mitandao unatubu na kuacha, kama ulikuwa ni mwizi vivyo hivyo…

Na baada ya kutubu kwa kudhamiria kabisa na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. …utakuwa umezaliwa mara ya pili na kuhesabika mwana-familia wa familia ya kimbinguni. Na hivyo kuwa mrithi, na ile damu ya thamani isiyoisha muda wa matumizi, damu ya Yesu Kristo itaanza kunena mema juu yako.

Na hivyo hata ukiitamka jambo lolote kwa jina lake utapata.

Bwana akubariki.

Tafadhali share na wengine. jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

Rudi Nyumbani:

Print this post

KWANINI YESU KRISTO NI MWANA WA DAUDI?

Shalom, Mtu wa Mungu, karibu tujifunze biblia, Jukumu kubwa tulilopewa miongoni mwa mengi ni jukumu la kumfahamu sana YESU KRISTO, Na lengo kuu la kumfahamu sio kwasababu yeye anauhitaji sana wa Utukufu, au uhitaji sana wa kutafuta ajulikane, hapana! Hilo sio lengo…kwasababu pale tu alipo tayari anajulikana…Lakini bado anatuasa tunapaswa tumfahamu sana yeye…Hivyo hiyo ikimaanisha kuwa kwa jinsi tunavyomfahamu yeye ni tofauti na yeye anavyotaka sisi tumfahamu…

Kwasasa Mtu maarufu kuliko wote duniani kwa wakati wote ni YESU KRISTO, hakuna mwanadamu yeyote aliyewahi kufikia kiwango cha umaarufu alionao Bwana Yesu Kristo, ukienda kwa wachina, wahindu, wabudha wote wanamjua Yesu Kristo…Hata watu ambao sio wakristo kwa namna moja au nyingine walishawahi kumsikia Yesu Kristo katika Maisha yao..kwahiyo yeye ni maarufu tayari.

Biblia inasema katika…Waefeso 4: 13 “ …hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu”

Na kwanini anataka sisi tumfahamu sana yeye? Mstari wa 14, hapo juu umetupa majibu… Ni ili tusiendelee kuwa Watoto wachanga, tukitupwa huku na huko, tukidanganywa na kila upepo wa elimu, na kuishia kuzifuata njia za udanganyifu.

Kwahiyo hakuna Elimu nyingine itakayoweza kutufanya tusiweze kudanganyika na elimu ya mashetani, isipokuwa Elimu ya kumfahamu Yesu Kristo, hakuna namna yoyote utakayoweza kuifahamu na kuidhibiti noti bandia pasipo kwanza kuijua noti halali ilivyo, ukishaifahamu noti halali ilivyo na tabia zake ndivyo utakavyoweza kuijua noti bandia..Kadhalika tunajukumu kubwa sana la kumfahamu Yesu Kristo kwa undani ili tuweze kuyadhibiti mafundisho ya mashetani na wapinga Kristo.

Leo tutajifunza kwanini Yesu Kristo, anajulikana kama Mwana wa Daudi na kwanini ni MFALME.

Sasa ni Dhahiri kabisa tunajua kuwa Yesu hakuwa na Baba wa kimwili, lakini kuna mahali kwenye maandiko kajitambulisha kuwa Mwana wa Daudi.. Sasa kwanini alijiita hivyo?

Sababu pekee ya Bwana Yesu kujulikana kama mwana wa Daudi, ni kutokana na Baraka Daudi alizozibeba, lakini si kutokana na undugu wa kidamu..Wewe unaitwa mwana wa Baba yako kutokana na uhusiano wa kidamu..lakini unaweza ukaitwa mwana wa Raisi wako, ila si kwa uhusiano wa kidamu bali wa pengine wa kiitikadi fulani….

Kwamfano pia sisi wakristo tunaitwa Wana wa Mungu, si kwasababu tumezaliwa familia moja na Muumba wetu,hapana au kwamba tuna damu moja na Mungu, hapana ni kutokana na Baraka za kimbinguni zinavyohusiana na sisi ndio maana tunaitwa wana wa Mungu.

Vivyo hivyo tunajulikana kwamba ni wana wa Ibrahimu , sio kwasababu sisi tuna damu moja na Ibrahimu, hapana bali ni kwasababu ni warithi wa Ahadi zile zile alizopewa Ibarahimu na Mungu, ndio maana na sisi tunajulikana kama wana wa Ibrahimu, Na Bwana Yesu ndio hivyo hivyo, Baraka alizopewa Daudi na mnyororo wa ukoo wake wote zilimhusu pia Bwana wetu Yesu Kristo…Daudi alikusudia kumjengea Mungu, Nyumba na hivyo Mungu akambarikia yeye na uzao wake kuwa uzao wa kifalme milele.(soma 2 Samweli 7:1-12)

kwasababu alizaliwa katika nyumba ya Yusufu ambaye alikuwa ni wa ukoo wa Daudi uliobarikiwa (ukoo wa kifalme),..Moja ya Baraka za ukoo wa Daudi ni kwamba utakuwa ni ukoo wa kifalme, kwamba wazao wote wa Kwanza wa Daudi walipakwa Mafuta na Mungu wawe wafalme soma (2 Wafalme 8:19,). Na ndio maana Bwana Yesu alipozaliwa katika nyumba ya Yusufu kama mzaliwa wa kwanza, roho ya kifalme ilikuwa juu yake. Kwahiyo kwa namna yoyote ile ni lazima angekuja tu kuwa Mfalme..

Je! Unajua kuwa Yusufu baba yake Yesu angepaswa awe mfalme wa Israeli kwa kipindi kile, kulingana na ahadi Mungu aliyomahidia Daudi?…Lakini kutokana na dhambi zao, Taifa la Israeli lilikatwa na uzao wa Daudi wa kifalme ukasimamishwa katika kutawala na ulisimamishwa kipindi gani?..

Kama ukisoma kitabu cha Wafalme, baada ya Daudi kufa, akafuata mwanawe Sulemani akawa mfalme kweli kulingana na ile Ahadi lakini naye pia akafa, na ikaendelea hivyo hivyo, kwa wajukuu na vitukuu vya Daudi, mpaka mfalme wa mwisho aliyetawala Yuda aliyeitwa Sedekia, ambaye alikuwa ni kitukuu cha 20 cha Daudi, huyu ndiye mfalme wa Mwisho kutawala Yuda, baada yake yeye, ndio Watu wakapelekwa Utumwani Babeli, hiyo ndiyo siku waliokatwa na waliporudi kukawa hakuna mfalme tena katika Israeli…vitukuu vya Daudi vilivyozaliwa baada ya Sedekia Mfalme wa Mwisho kufa, wakawa ni watu tu wa kawaida, kama watu wengine…

Ndio maana Yusufu baba yake Yesu alikuwa ni mtu wa kawaida tu maskini, ingawa alikuwa ni mwana wa kifalme…(Kwa urefu fuatilia ukoo huu wa Yesu kwenye kitabu cha Mathayo 1:1-17), laiti Israeli asingeasi na kupelekwa utumwani, Yusufu baba yake Yesu angekuwa mfalme wa Yuda, na Kristo angezaliwa huko…

Hivyo Israeli iliendelea kuwa kama mti uliokatwa baada ya kutoka Babeli…Wayahudi wakakaa mamia ya miaka bila mfalme….kukawa hakuna dalili yoyote ya Mfalme kunyanyuka katika uzao wa Daudi,..kwani Utawala wa Rumi ulikuwa umekamata dunia nzima, na Warumi waliwaweka watu wao kwenye makoloni yao yote, mpaka Israeli ilikuwa ni koloni la Warumi..Hivyo mtawala aliyetawala koloni la Israeli alikuwa ni Mrumi…jambo hilo liliendelea kwa miaka mingi…lakini Biblia ilitabiri katika Isaya Mlango wa 11 kuwa litatoka chipukizi katika shina la Yese….Kumbuka Yese alikuwa ni Baba yake Daudi, kwahiyo ni sawa na kusema litatoka chipukizi katika shina la Daudi au katika uzao wa Daudi. Tunasoma hayo katika…

Isaya11:1 “ Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.

2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana”.

Kama ni msomaji mzuri wa maandiko utagundua kuwa…hilo shina linalozungumziwa hapo si lingine Zaidi ya BWANA YESU KRISTO mwenyewe…Biblia inasema litatoka shina, ikiwa na maana kuwa ni kutoka katika mti uliokatwa, nalo litazaa sana matunda… Kama ulishawahi kuona mti mkubwa uliokatiwa chini kabisa..linakuwa linabaki tu kama gogo…halafu baada ya kipindi fulani unaona kitawi kidogo cha kijani kinajitokeza ubavuni mwa lile gogo, na kama hakitakatwa na chenyewe, baada ya kipindi fulani kitakuwa kikubwa na hatimaye kuwa tena mti mkubwa kama ulivyokuwa mwanzo…

Ndicho kilichotokea baada ya uzao wa Daudi kukatwa na kupelekwa Babeli…ni sawa na mti uliokatwa…lakini chipukizi likatoka, katika uzao huo huo wa Daudi..

Bwana Yesu, Mwana wa Daudi, mzao wa kifalme, mwenye ahadi ya kifalme juu yake, alizaliwa huko Bethlehemu, alikuwa ni mfalme aliyetoka katika shina lililokatwa ndio maana utaona alizaliwa katika zizi la ng’ombe, familia ya kimaskini, laiti Yusufu baba yeke angekuwa mfalme basi naye pia angezaliwa katika familia ya kifalme..Lakini kinyume chake alizaliwa katika ufalme uliokatwa…

Lakini maandiko yanatabiri, huyo atakuja kuwa mti mkubwa na utazaa sana matunda, na ufalme wake utaenea duniani kote…kipindi alichokuja miaka 2000 iliyopita, roho ya Bwana ilikuwa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana” Kwa hekima, na maarifa aliyoyabeba alituletea sisi Wokovu…ambao mpaka sasa tunanufaika nao…., Lakini katika utawala wa miaka 1000 ijayo, ndio tutamwona vizuri kama Mfalme, aliyeketi katika kiti cha Kifalme…katika wakati huo, yeye pamoja na sisi ambao sasa tumemwamini, tutatawala naye, sisi tutakuwa wafalme nay eye atakuwa kama Mfalme wa wafalme.

Wakati huo Mamlaka yote ya kifalme atakuwa nayo yeye, utakuwa sio wakati wa wokovu tena bali wakati wa utawala, sasa hivi ndio tupo wakati wa wokovu, nyakati hizo zitakuwa ni nyakati za utawala mkuu wa Yesu Kristo. Dunia yote itajawa na kumcha Bwana, kutakuwa hakuna vurugu, kutakuwa na Amani isiyo ya kawaida..simba na kondoo watakaa pamoja na hawatadhuriana, mtoto atacheza na nyoka, na hakutakuwa na madhara yoyote.

Tusome tena Isaya hii 11 Mpaka mwisho..

“1 Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.

2 Na roho ya Bwana atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha Bwana;

3 na furaha yake itakuwa katika kumcha Bwana; wala hatahukumu kwa kuyafuata ayaonayo kwa macho yake, wala hataonya kwa kuyafuata ayasikiayo kwa masikio yake;

4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.

5 Na haki itakuwa mshipi wa viuno vyake, na uaminifu mshipi wa kujifungia.

6 Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.

7 Ng’ombe na dubu watalisha pamoja; watoto wao watalala pamoja; na simba atakula majani kama ng’ombe.

8 Na mtoto anyonyaye atacheza penye tundu la nyoka, na mtoto aliyeachishwa atatia mkono wake katika pango la fira.

9 Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua Bwana, kama vile maji yanavyoifunika bahari.

10 Na itakuwa katika siku hiyo, shina la Yese lisimamalo kuwa ishara kwa kabila za watu, yeye ndiye ambaye mataifa watamtafuta; na mahali pake pa kupumzikia patakuwa na utukufu”.

Ufunuo 3:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 YEYE ASHINDAYE, NITAMPA KUKETI PAMOJA NAMI KATIKA KITI CHANGU CHA ENZI, KAMA MIMI NILIVYOSHINDA NIKAKETI PAMOJA NA BABA YANGU KATIKA KITI CHAKE CHA ENZI.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”

Na pia alisema..

Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.

15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.

16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.

17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”

Kama hujampa Yesu Kristo Maisha yako, jua umechelewa sana, lakini mlango bado hujafungwa ingia kabla mlango hujafungwa..mwisho wa mambo yote umekaribia, na Kristo yupo Mlangoni kurudi, atakaporudi nyakati hii ya mwisho atakuja kama mfalme na mtawala mkuu hatakuja tena kama mwokozi.

Bwana akubariki.

Tafadhali share kwa wengine


Mada Nyinginezo:

MWANA WA MUNGU.

ANGUKO LA UFALME WA SHETANI:

JIWE LA KUSAGIA

HUDUMA YA MALAIKA WATAKATIFU.

JE! MTU KUSIKIA SAUTI ZA WATU WALIO MBALI, KUNAWEZA TOKANA NA MUNGU?

BWANA ALIMAANISHA NINI KUSEMA “HERI WALIOTASA, NA MATUMBO YASIYOZAA, NA MAZIWA YASIYONYONYESHA”?


Rudi Nyumbani:

Print this post

MWILI NA DAMU YA YESU KRISTO.

Shalom, karibu katika kujifunza Neno la Mungu, ambapo leo tutajifunza juu ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu…kama maandiko yanavyotuambia.. “tumfahamu sana mwana wa Mungu hata kufikia cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo Waefeso 4:13”. Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba “tunapaswa tumfahamu na kumwelewa Yesu Kristo mpaka kufikia kile kiwango ambacho yeye anataka sisi tumfahamu”…Ndio jukumu pekee tulilopewa hapa duniani, Ili kwamba tusipelekwe na kuchukuliwa na kila aina ya upepo wa elimu zilizozagaa za kidini.

Kwahiyo kuna umuhimu sana wa kumwelewa Yesu Kristo, ni dhahiri kuwa usipomwelewa mtu fulani, huwezi kutembea naye, wala huwezi kuishi naye…hata mazungumzo yenu mnaweza msielewane au mkapishana. Kila mmoja asielewe nia ya mwenzake ni ipi hiyo ni kwasababu hamfahamiani. Na kwa Yesu Kristo ndio hivyo hivyo tusipomwelewa vizuri tutapishana naye tu kwa kila kitu.

Kuna maneno mengi ambayo Bwana Yesu aliyaongea ambayo pasipo Roho kumjalia mtu kuyaelewa, kamwe hatayaelewa na mwisho wa siku ataishia kutafsiri kwa akili tu.

Kwamfano kuna mahali Bwana Yesu alimwita Herode Mbweha.

Luka 13: 32 “Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika”.

Kwa sentensi hiyo ni rahisi kusema Bwana kamtusi Herode, Nimewahi kukutana na watu wanasema Bwana alimtusi Herode, na hivyo Mungu gani anatukana.

Kadhalika kuna mahali Bwana alisema..

Luka 14.25 “Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia,

26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu”.

Kwa maneno hayo, pasipo msaada wa Roho, unaweza ukasema Bwana anahalalisha chuki kwa wazazi na ndugu.

Sentensi nyingine tena ya Bwana yenye utata mkubwa ni pale aliposema maneno haya…

Yohana 6:52 “Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi MWILI wake ili tuule?

53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.

54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.

56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.”

Kwa maneno hayo, hata wewe unaweza ukasema Bwana anahalalisha unywaji wa damu..na ulaji wa nyama ya mtu.

Na yapo maneno mengine mengi sana, katika maandiko ambayo pasipo msaada wa Roho-Mtakatifu ni rahisi kutafsiri kivingine..

Lakini hebu tuzichambue baadhi ya hizi sentensi kwa ufupi kisha tujifunze kitu..

Pale Bwana alipomwita Herode Mbweha..hakumaanisha kumtusi kwamba Herode ni Mbweha..kama sisi wanadamu tunavyotukanana na kuvunjiana heshima…Hapana Bwana alimwita Herode Mbweha kufunua tabia yake ya ndani..tabia yake ya ndani ya kurarua na kuwinda vitu vidogo vidogo aliifananisha na Mbweha, kwasababu Mbweha ndio anatabia hizo…Kwahiyo alikuwa anaangalia tabia ya rohoni ya Herode na kuifananisha na aina Fulani ya mnyama…Ndio maana yeye Bwana mwenyewe pia alijifananisha na Mwana-kondoo na sio tu yeye alijifananisha na mwana-kondoo bali hata Yohana Mbatizaji alimwita Bwana Yesu “mwana-kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu”…Yohana alimwita Bwana kondoo kwa kuiona tabia ya Bwana ya Upole kama kondoo na ya unyenyekevu….sasa kama Bwana alimtukana Herode na yeye mwenyewe atakuwa anajifanyaje?..maana kama ni matusi basi ni heri uitwe Mbweha kuliko kondoo..wafugaji wanawaelewa kondoo walivyo..Nimewahi kukutana na mfugaji mmoja akaniambia mtu anitukane matusi yote duniani, lakini asiniite mimi kondoo…kwao ni kama tusi kubwa sana.

Tukirudi kwenye mfano wa pili Bwana alisema… “mtu akija kwangu naye hamchukii Baba yake na Mama yake hawezi kuwa mwanafunzi wangu”..Na sentensi hii pia ni sentensi yenye utata sana..lakini Hebu tafakari…Inawezekanaje Bwana Yesu aseme sehemu moja, “wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi”…halafu na hapa ajisahihishe tena aseme “mtu akija kwangu ahakikishe amemchukia Baba yake na Mama yake”..unaona hiyo inawezekana kweli??..Ni dhahiri kuwa haiwezekani kwasababu Bwana Yesu hawezi kusema hapa hivi na baadaye ageuke aseme vile…kwasababu yeye sio kigeugeu..Kwahiyo hapo Bwana alikuwa haizungumzii chuki ya kuwachukua wazazi au ndugu, hapana bali chuki inayozungumziwa hapo ni chuki ya mapenzi ya wazazi..mfano mzazi mapenzi yake ni wewe usimfuate Bwana, hayo mapenzi unapaswa uyachukie…mzazi mapenzi yake ni wewe kuwa mlevi na mtu wa kidunia vuguvugu, mapenzi yake ni wewe uwe mganga, au mvaaji kama wanawake wa kidunia, hayo mapenzi ndio ya kuyakataa, na kuyafuata mapenzi ya Mungu, na kwa kuyakataa ndio kuyachukia kwenyewe huko.

Lakini sio kwenda kumtukana mzazi, au kumchukia kabisa na kukataa kuongea naye na kumwekea uadui…hapana hiyo sio maana yake..Tunapaswa tuwapende wazazi na kuwaombea…lakini kuna mipaka ya uhusiano wetu na Mungu, wasiyopaswa wao kuyaiingilia.

Na tukimalizia na huo mfano wa Mwisho Bwana aliousema Mtu asipoula mwili wangu na damu yangu hana uzima ndani yake hapa ndipo kiini cha somo letu kilipo…Hapo Bwana hakuhalalisha tukamshike na kumchinja na kuila nyama yake na kuinywa damu yake kama wachawi wanavyofanya..

Hapana bali alimaanisha kuula mwili wake katika roho na kuinywa damu yake katika roho kama yeye alivyosema…

Kwasababu katika roho tunakula na kunywa kama tunavyokula na kunywa katika mwili.. Na hivyo kumla Bwana Yesu Kristo ni KUYASIKIA MANEO YAKE NA KUYAAMINI NA TAFAKARI MANENO YAKE, NA KUYAISHI..na maana ya kuinywa damu yake ni KUTAFAKARI UWEZO ULIOPO KATIKA DAMU YAKE NA KUUTUMIA.. Hiyo ndiyo maana ya kuula mwili wa Yesu na kuinywa damu yake…Na kwa nje tunashiriki kama ishara tu! Ambayo ndio ule MKATE na DIVAI. Ambao ni ishara tu ya nje kuelezea mlo unaoendelea rohoni.

Sasa hata leo wapo watu wanaokula nyama ya Bwana Yesu na kuinywa damu yake, hao ndio wale watu wanaojifunza Neno lake na kulitafakari usiku na mchana na kuishi katika hilo na kuna watu wanakula nyama za watu wengine na kuna wengine wanakula nyama za miili yao wenyewe..Kama tulivyotangulia kusema…nyama ya mwili wa Bwana Yesu ni MANENO YAKE, kadhalika nyama za watu wengine ni Maneno ya hao watu…Na nyama za mtu binafsi ni maneno yake mwenyewe.

Kuna kipindi mwanzoni mwanzoni tu wakati nimempa Bwana maisha yangu..kuna vitu nilikuwa navitafakari halafu navipatia majibu mwenyewe pasipo kutumia mrejesho wa Biblia..Ilikuwa hivyo tu, na nilikuwa nayaamini majibu yangu zaidi kuliko kitu kingine..Na kwasababu nilikuwa bado ni mchanga kiroho, nilikuwa sielewi hata namna ya kuisikia sauti ya Mungu, wala kuithibitisha..Kwahiyo ilikuwa nikisoma mstari mmoja kwenye maandiko nilikuwa nauchukua huo na kuutafakari kwa jinsi niuelewavyo na kisha kuupatia tafsiri..

Siku moja usiku nilisoma mstari mmoja katika kitabu cha Mwanzo, na kuupatia tafsiri mwenyewe na kuiamini hiyo tafsiri nikaenda kulala…Usiku nikaota ndoto nimekaa kwenye kiti halafu miguu yangu ipo kwenye sufuria inayotokota maji….sasa wakati ile miguu yangu inachemka kule majini nilikuwa sisikii maumivu hata kidogo, na maji yale yalikuwa yamechemka mpaka miguu imekuwa meupe, na kuna mtu nilikuwa kama naongea naye mbele yangu ninayemfahamu…wakati tunaongea nikajikuta kama kuna sahani imeletwa mbele yangu yenye nyama..nikawa nakula zile nyama…na nikataka kama kumkaribisha Yule mtu niliyekuwa naongea naye..kabla hajaanza tu na yeye kuila ile nyama.. nikaangalia chini..nikaja kugundua kuwa zile nyama nilizokuwa ninazila zilikuwa zinatoka kwenye miguu yangu mwenyewe hiyo iliyokuwa inachemka hapo chini..na nilikuwa nimeshaanza kuila nakaribia kuimaliza..nikaacha!. Na ghafla nikashtuka usingizini…Nikawa natafakari maana ya ndoto hiyo nikiwa pale pale kitandani, Niliogopa sana.

Wakati naitafakari hiyo ndoto Nikasikia kama maelezo Fulani yamekuja kichwani yanayosema “nisizifuate akili zangu bali niliangalie Neno la Mungu”…Saa hiyo hiyo nikapata tafsiri ya ile ndoto nikikumbuka na mistari niliyokuwa nasoma jana usiku ambayo nilijitengenezea tafsiri yake mwenyewe…Kuwa ile nyama niliyokuwa naila ni nyama ya mwili wangu mwenyewe..Na kama unavyojua mtu ukijikata mguu na kuula, na ukajikata mkono nakuula maana yake, ni unajimaliza mwenyewe na mwishowe utakufa…Kwahiyo siku hiyo ndio nikaelewa madhara ya kuyafuata na kuyaamini maneno yangu mwenyewe ambayo hayana mrejesho wa kutosha kwenye maandiko…mwishoni yataniletea mauti ya kiroho. Nikamshukuru Mungu kwa kunionyesha hilo, Kwahiyo nikabadilika kuanzia siku hiyo na kuanza kuisoma biblia kwa undani sana…kitabu kwa kitabu, sura kwa sura, Kabla ya ufunuo wowote kuuamini ni lazima niuhakiki kwenye maandiko kwa nguvu zote, na niwe na mistari ya kutosha kuisimamia Roho Mtakatifu akiwa ni msaidizi wangu wa pembeni..Na nikaja kuelewa kuwa nilikuwa najipoteza mwenyewe, kwa kujiaminisha mwenyewe na mitazamo yangu..Nikaja kugundua nilivyokuwa nawaza ni tofauti kabisa na Maneno ya Mungu..ingawa katika kile kipindi nilikuwa najiona nipo sawa..

Kwahiyo ndugu Maneno ya Yesu Kristo ndio maneno ya Uzima, yanayotupa afya mwilini mwetu. Tunapoula mwili wake (Maneno yake) na Damu yake ipasavyo ndivyo tunavyojiongezea afya katika roho zetu, na tusipoula mwili wake na damu yake ndivyo tunavyojidhoofisha wenyewe kwasababu yeye mwenyewe anasema… “AMIN, AMIN, NAWAAMBIENI, MSIPOULA MWILI WAKE MWANA WA ADAMU NA KUINYWA DAMU YAKE, HAMNA UZIMA NDANI YENU”…Na zaidi ya yote unapotegemea maneno yako mwenyewe ndivyo unavyojimaliza mwenyewe na mwishowe utakufa…

Ifuatayo ni mifano michache tu ya mtu anayekula nyama ya mwili wake mwenyewe.(mawazo yake).

1) Imani ya kuamini kuwa Mungu hawezi kuiteketeza dunia na watu wote hawa..ndugu hiyo ni unajilisha nyama ya mwili wako mwenyewe.

2) Imani ya kuwa utakwenda mbinguni kwa kutenda mema tu pasipo kumwamini Bwana Yesu Kristo.

3) Imani ya kuwa ubatizo ni ubatizo tu, uwe wa maji mengi au machache haujalishi.

4) Imani ya kuwa siku moja Mungu atamsamehe shetani.

5) Imani ya kuwa hakuna Mungu wala shetani.

6) Imani ya kuwa Mungu haangalii mavazi yangu wala mwonekano wangu bali anaangalia roho yangu peke yake.

7) Imani ya kuwa Yesu Kristo harudi leo wala kesho, 

8) Imani ya kuwa hakunaga Jehanum ya moto mtu akifa amekufa tu.

9) Imani ya kuwa Biblia ni kitabu kilichotungwa na wanadamu. N.K

10) Imani ya kujiona wewe huna dhambi nyingi sana kustahili kuzimu kama yule.

Na unapotegemea maneno ya watu wengine ambao Hawamhubiri Kristo katika utimilifu wa Neno lake, ndivyo unavyokula nyama zao zilizotengenezwa kuzimu…Na mwisho wa siku unazizoelea hata unapoletewa chakula cha kweli cha uzima (yaani maneno ya Yesu Kristo) hutaki tena kusikia..Kwasababu umenenepeshwa kwa nyama hizo.

Na ifuatayo ni baadhi tu ya mifano ya Nyama zinazotengenezwa kuzimu watu wanazolishwa pasipo wao kujijua.

1) Ibada za Sanamu, hizo ni nyama kutoka kwa Yule adui…haihitaji mtu awe mchawi ndio ale nyama hiyo..Ibada hizo tu tayari ni uchawi.

2) Mafundisho ya kwenda toharani ni nyama za Yule adui. Watu wanalishwa mchana na usiku.

3) Ubatizo wa vichanga ni nyama za Yule adui.

4) Mafundisho ya ndoa za Mitara (mwanamume mmoja wake wengi).

5) Mafundisho yasiyolenga utakatifu wala Toba, badala yake yanalenga tu mafanikio na elimu za kichawi…Ni nyama za Yule adui. N.k.

Kwahiyo ndugu yangu kama umeshalishwa NYAMA zozote za aina hiyo, zieupuke sasa, na kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, Nakushauri ufanye hivyo leo, kabla wakati wa hatari haujafika..Na yeye anakupenda na hataki upotee ndio maana anakuhitaji leo utubu, akupe uzima wa Milele. Akupa chakula chake cha uzima bure. Akupe mwili wake na damu yake halisi…Na sio nyama za mashetani.

Hivyo unachopaswa kufanya ni KUTUBU KWANZA KWA KUDHAMIRIA KUACHA DHAMBI Zako zote. Unadhamiria kuacha uasherati, uwongo, ulevi, rushwa, pornography, wizi, uvaaji mbaya, utukanaji, utoaji mimba, anasa na mambo yote uliyokuwa unayafanya yasiyompendeza Mungu, Na baada ya kufanya hivyo nenda ukabatizwe katika ubatizo sahihi wa kimaandiko wa kuzamishwa mwili wako wote kwenye maji na kwa jina la YESU KRISTO kulingana na (Matendo 2:38, 8:16, 10:48, na 19:5,) ili upate ondoleo la dhambi zako..Na kisha Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho wake mtakatifu atakayekusaidia kushinda dhambi na kukuongoza katika kuijua kweli yote ya kimaandiko..

Usikubali kulishwa nyama za watu wengine watakaokuambia utaokoka siku ile tu pasipo Yesu Kristo, au wanaokuambia kwamba ubatizo sio wa muhimu..Wala usikubali kula nyama za mwili wako mwenyewe zinazosema hakuna Mungu, wala hakuna jehanum,wala Yesu Kristo harudi..

Badala yake uule mwili wa Yesu Kristo unaosema… “Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa Luka 16:16” na unaosema

“ Ufunuo 22:12 “Tazama, naja upesi, na ujira wangu upamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho”…..

Ufunuo 22:16 “Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile nyota yenye kung’aa ya asubuhi.

17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure”.

Bwana akubariki sana. Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

MEZA YA BWANA, NA KUTAWADHANA MIGUU

MANA ILIYOSHUSHWA KUTOKA MBINGUNI.

CHAKULA CHA ROHONI.

HADITHI ZA KIZEE.


Rudi Nyumbani

Print this post

MWINUE YESU KRISTO KATIKA MAISHA YAKO.

Shalom! Mtu wa Mungu, karibu tujifunze Neno la Mungu, kwa Neema zake, leo tutajifunza kuhusu umuhimu wa kumwinua Yesu Kristo katika maisha yetu, Tunaweza tukajifunza katika safari ya wana wa Israeli wakati wametoka Misri, ambapo tunaona wakati Bwana amewatoa katika utawala mgumu wa Farao, wakiwa njiani kuelekea nchi yao ya ahadi, walikutana na jeshi la shetani kuwapinga safarini. Na hawa hawakuwa wengine zaidi ya WAAMALEKI. Waamaleki walikuwa ni watu kutoka katika uzao wa Esau ndugu yake Yakobo..

Kama unakumbuka Isaka wakati anawabariki wanawe Esau na Yakobo, Yakobo alimnyang’anya ndugu yake mbaraka wake, kwasababu ya yeye kutokuujali ukubwa Mungu aliompa. Hivyo ikatengeneza aina fulani ya chuki kati ya hao ndugu wawili, yaani Esau na Yakobo, na Baba yao tunasoma baada ya kumbariki Yakobo alimwambia Esau maneno haya…

Mwanzo 27: 38 “Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.

39 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako,Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.

40 Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo; NA ITAKUWA UTAKAPOPONYOKA, UTALIVUNJA KONGWA LAKE KATIKA SHINGO YAKO.

41 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo”.

Kwahiyo unaweza kuona hapo hizo Baraka, hazikuwa kwa Esau na Yakobo tu peke yao, bali ni kwa vizazi vyote vya Esau na vizazi vyote vya Yakobo,.Kwamba Israeli atakuwa akimshinda Esau lakini endapo Israeli atalemaa katika roho basi Esau atampiga na kulivunja kongwa lake katika shingo yake.

Sasa hapa baada ya miaka mingi sana zaidi ya miaka 400 Kupita..tunaona uzao wa Yakobo ambao ndio wana wa Israeli unakutana tena katika mapambano na uzao wa Esau ambao ndio hao Waamaleki. Hivyo Israeli walijua kabisa endapo tusipokuwa makini, na hawa wakiwa na bidii basi unabii unaosema hatutamshinda Esau utatimia juu yetu..Hivyo ile vita haikuwa ya kawaida palikuwa na changamoto kubwa sana katika, Israeli hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kumgeukia Mungu na kumtegemea yeye…

Ndipo tunasoma Musa baada ya kupata hizo habari kuwa waamaleki wamewazunguka alikwenda kumwomba Mungu wa Israeli na Bwana akampa maagizo ya kufanya kama tunavyosoma katika…

Kutoka 17: 8 “Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.

9 Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu.

10 Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima.

11 Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.

12 Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa.

13 Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga”.

Hapa tunaona mkono wa Musa ndio uliowapa ushindi waisraeli, alipounyanyua juu, ndivyo waisraeli walivyokuwa wanapata nguvu vitani, na alipoushusha waamaleki waliwapiga waisraeli..Lakini kama tunavyosoma mwisho wa siku Israeli walishinda kutokana na Mikono ya Musa kusimama juu muda wote.

Ni nini tunachoweza kujifunza katika habari hii ??

Wakristo sisi ni uzao wa Mungu, ambapo tumefanyika kuwa uzao wa Mungu kweli kweli, kupitia Yesu Kristo Bwana Wetu, Mkuu wa Uzima, sisi tunafananishwa na Uzao wa YAKOBO ambao umebarikiwa…Lakini pia upo uzao wa yule Adui, huo unafanana na uzao wa ESAU, na huo kazi yake ni kupambana na sisi kila siku kutupinga katika safari yetu ya kwenda mbinguni,..Na Bwana alitoa unabii kama alivyotoa kwa Yakobo na Ndugu yake kwamba Yakobo atampiga Esau lakini pia Esau akiponyoka atamvunja kongwa Yakobo katika shingo yake {Kwa tafsiri iliyo nyepesi ni hii: Esau akijitahidi na kupata nguvu, basi ataweza kuondoa utawala wa ndugu yake juu yake}..Na pia Bwana alizungumza juu yetu, na kusema.

“nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Mwanzo 3:15”

Wengi tunaishia hapo kwamba, uzao wako utamponda kichwa, lakini tunasahau kuwa pia uzao wa nyoka umepewa mamlaka ya kutuponda sisi kisigino, tusipokuwa makini”

Kwahiyo katika ulimwengu wa Roho ni vita vikali vinaendelea, hivyo inahitajika umakini mkubwa sana, na msaada ya Mungu.

Sasa Biblia inasema… “kama vile Musa alivyomwinua nyoka wa shaba jangwani” ili kila amtazamaye yule nyoka wa shaba apone, ndivyo hivyo hivyo Mwana wa Adamu alipaswa ainuliwe msalabani ili kila mtu amtazamaye aokolewe..

Kadhalika kama Musa alivyounyanyua mkono wake juu ili kila Mwisraeli aliyeko vitani apate kupona na kuteka na kupata ushindi dhidi ya Maadui zake..NA WAKRISTO VIVYO HIVYO HATUNA BUDI KUMWINUA YESU KRISTO KATIKA MAISHA YETU ili tuweze kupata ushindi dhidi ya maadui zetu (yaani roho ya uadui inayotenda kazi ndani ya watu na majeshi ya mapepo wabaya).

 Na kumbuka kumwinua Kristo katika maisha yetu sio kumwimbia mapambio na nyimbo za kuabudu, hiyo ni sehemu mojawapo, Lakini sehemu kubwa ya kumwinua Mungu katika maisha yetu ni kumaanisha kumwamini kwa kuzitubia dhambi na kuzicha, na kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kuishi maisha ya utakatifu yanayoonekana mbele za watu kuanzia huo wakati na kuendelea, huko ndiko kumwinua Kristo kunakozungumziwa.

Kumbuka pia hakuna ushindi pasipo Yesu Kristo kuinuliwa juu ya maisha yetu. Musa alipoishiwa nguvu watu walikuja kumsaidia kuitegemeza mikono yake ili isishuke…Na sisi katika maisha yetu ya kikristo ya vita, tunapoishiwa nguvu…tunapaswa tufanye juu chini tusiiangushe imani yetu kwa Kristo tuishikilie kwelikweli kwa bidii zote maana hiyo tumekabidhiwa mara moja tu!…Biblia inasema “Mpende Bwana Mungu wako kwa nguvu zako zote, kwa akili zako zote, na kwa moyo wako wote”.

Vinginevyo tukisema tuiache Imani, shetani yupo na amepewa amri ya kutuponda visigino. Amri hiyo kapokea kutoka kwa Mungu.

Ndugu unayesoma ujumbe huu, Yesu Kristo ni muhimu sana katika maisha haya…kama ulimsikia kwa juu juu tu!! kanisani, au mahali popote pale, kama umehubiriwa ni wa-mafanikio-ya-kibiashara Yesu ni zaidi ya hapo!…. jaribu tena kutenga muda umtafakari, hakuna tumaini, wokovu, hakuna maisha, hakuna mafanikio yoyote nje ya Yesu Kristo!…Waliomwamini ndio wanaoitwa wabarikiwa. Huwezi kumpendeza Mungu wala kumwelewa Mungu, wala kumshinda shetani nje ya Yesu Kristo!…Kama ule mkono haujanyanyuliwa juu (Yesu Kristo) hata kama unajiona unatenda wema kiasi gani kama hujamnyanyua juu ni kazi bure! Ni sawa na mtu anayefanya kazi katika shirika ambalo hajaajiriwa, wala hawamjua akitumai kupata mshahara mwisho wa mwezi kutoka huko.. mipango yako ni mizuri lakini nje! Ya Yesu Kristo ni bure!..

Suluhisho ni kumtamani aje aingie katika maisha na kuanza maisha mapya katika yeye..

Bwana akubariki sana.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Zinazoendana:

ACHENI MJUE YA KUWA MIMI NI MUNGU.

USIMWABUDU SHETANI!

NEHUSHTANI (NYOKA WA SHABA)

JAWABU LA MAISHA YA MTU.


Rudi Nyumbani

Print this post

NI KWASABABU YA YESU KRISTO.

Wakati tunakaribia kumaliza Mwaka ni kipindi maalumu sana cha kukaa na kutafakari na kuchukua hatua ya kumshukuru Mungu kwa Mengi aliyotutendea…Jambo kubwa la kuweza kumshukuru Mungu, ni juu ya pumzi aliyotupatia mwaka mzima, Katika safari ya mwaka mzima, kuna vipindi vingi tumepita lakini bado tunaishi..jua linachomoza na kuzama kila siku, hatujapitia matetemeko ya ardhi mwaka mzima, hatujapigana vita mwaka mzima, Mungu katuepusha na majanga mengi, katuepusha na magonjwa mengi, na hata tulipopata ugonjwa Bwana alituponya n.k Unafikiri ni kwasababu ya nani? Mpaka Mungu atuepushe na hayo yote?

si kwasababu tuna unafuu mbele zake, au kwasababu tunazingatia mlo kamili, wala si kwasababu tunajitunza sana na kujipenda, wala si kwasababu tunaustaarabu mzuri wa maisha, wala si kwaajili ya haki yetu sisi, wala si kwasababu sisi ni watakatifu, wala sio kwasababu tunabidii ya kumtafuta yeye, wala si kwasababu tunatenda mema sana, wala si kwasababu tunafunga sana, wala si kwasababu tunaomba sana, wala si kwasababu ni washirika wazuri wa kanisani au watoaji sadaka wazuri au wenye upendo sana.. Hakuna hata jambo moja kati ya haya ambayo Baba yetu wa mbinguni anayaangalia ili kutunyeshea sisi mvua yake, au kutupa pumzi, au kutupatia mema, au kutupatia uzima au kutuangazia jua lake, Hakuna hata moja!!

Sasa swali linakuja kama sio kwa ajili ya hayo yote, tunaumaliza mwaka salama..basi ni kwasababu gani? Kama si kwaajili ya utakatifu wetu, au bidii zetu, au juhudi zetu, au matendo yetu, au utakatifu wetu ni kwasababu gani basi tunapokea neema hii?.

Jibu ni rahisi, ni kwasababu ya haki ya mtu mmoja, ni kwasababu ya utakatifu wa mtu mmoja, ni kwasababu ya bidii ya mtu mmoja, ni kwasababu ya juhudi ya mtu mmoja, ni kwasababu ya matendo ya mtu mmoja, ni kwasababu ya maombi ya mtu mmoja, na huyo mtu ni BWANA YESU KRISTO, kwa huyo Baba wa mbinguni ndiye aliyependezwa naye.

Baba wa mbinguni hakupendezwa na maelfu waliopo duniani, hakuona mwenye haki hata mmoja duniani, wote tulikuwa tumetenda dhambi, tunakasoro nyingi, zisizokuwa na hesabu.

Zaburi 14: 2 “Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja”.

Unaona! Sasa kama hakuna hata mmoja aliyemwona duniani mwenye haki??..unadhani vipi kama kuna ambaye angestahili kupokea baraka yoyote kutoka kwake?..hakuna hata mmoja..angestahili kupata pumzi kwa haki yake,wote tumestahili hukumu ya milele, Ndio maana inapasa atoke mtu mwingine kutoka mbinguni mwenye haki ambaye angestahili kupokea baraka kutoka kwa Mungu, kwasababu duniani hakuna hata mmoja mwenye akili, wote tumepungukiwa na utukufu wa Mungu..Hakuna hata mmoja mwenye unafuu.

Kwasababu hiyo basi kwa kuwa Yesu Kristo pekee ndiye aliyekuwa mkamilifu, ambaye hakutenda dhambi tangu kuzaliwa kwake mpaka ameondoka, yeye peke yake ndiye aliyehesabiwa haki kwa matendo yake binafsi, yeye peke yake ndiye Baba wa mbinguni aliyemwona mwenye AKILI anayemtafuta Mungu, alimchungulia toka juu akamwona akamtangaza “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” …hakusema hawa ndio wanangu wapendwa wangu..hapana bali “huyu ndiye”..maana yake yupo mmoja tu!! kwa haki yake amestahili kubarikiwa kwa kila namna. Ndugu mtu asikudanganye kwamba kuna wabarikiwa wengi..Mbarikiwa ni mmoja tu! Yesu Kristo.. Maandiko yanasema hivyo..

Mathayo 21:5 “Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda,

Na mwana-punda, mtoto wa punda.

6 Wale wanafunzi wakaenda zao, wakafanya kama Yesu alivyowaamuru,

7 wakamleta yule punda na mwana-punda, wakaweka nguo zao juu yao, naye akaketi juu yake.

8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya

miti, wakayatandaza njiani.

9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, HOSANA , MWANA WA DAUDI; NDIYE MBARIKIWA , yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni”.

Sasa basi kwasababu ni mmoja tu! Ndiye aliyestahili baraka, Yesu Kristo pekee asiyestahili kufa wala kuangamizwa milele…Yeye Yesu Kristo Bwana wetu alitununua sisi tusiokuwa wakamilifu kwa Baba wa mbinguni, akatushirikisha baraka zake alizobarikiwa na Baba wa mbinguni, akatuhusisha katika fadhili zake alizofadhiliwa na Baba, japokuwa sisi hatukustahili kubarikiwa, wala kupewa uzima, wala kuangaziwa jua..lakini sasa tunayapata hayo yote kupitia Yesu Kristo.

Kwasababu hiyo basi hata kipindi hichi tunachomaliza mwaka, kama bado tunaishi…tusijisifu ni kwa matendo yetu, sio kwa matendo yetu hata kidogo, bali kwa ajili ya matendo ya Yesu Kristo aliyoyaishi hapa duniani yaliyompendeza Baba..si kwa ajili tuna bidii za kujitunza hapana…wapo waliokuwa na bidii ya kujitunza sana lakini wameondoka..ni kwaajili ya Huruma ya Yesu Kristo juu yetu.

Sio kwasababu ya juhudi zetu, ndio tumebarikiwa na kupata mema ya nchi hapana ni kwasababu ya Mbaraka Bwana Yesu aliobarikiwa na Baba yake kwa haki yake..na sisi ndio tunaoushiriki . Yesu Kristo pekee yake ndiye Mbarikiwa, sisi ni kama waalikwa tu! Tumealikwa kwenda kula baraka za Yesu Kristo..Ndio maana na sisi tunajumuishwa kama miongoni mwa waliobarikiwa, lakini Mbarikiwa ni mmoja tu!

Kwahiyo ndugu, tukimfahamu Yesu Kristo kwa namna hiyo, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa ajili yake, hatuna budi kunyenyekea sana na kumwambia Bwana Ahsante…Ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa jambo moja moja alilotutendea kuanzia mwanzo wa mwaka huu hata mwisho. Hata kama bado ni mgonjwa mshukuru sana! Hata kama bado hukupata mwaka huu ulichokitamani, mshukuru tu Maadamu bado unaishi…Kwa wakati wake ukifika, atakutimizia matakwa yako.

Mshukuru kwasababu bado upo kwenye Imani, hujaanguka, shetani alikutafuta mwaka mzima kama simba angurumaye..Mshukuru kwasababu amekuepusha na yule mwovu..mshukuru kwasababu kama sio yeye kukubaliwa na Baba wa mbinguni usingekuwa hapo ulipo..kama sio yeye kuishi maisha makamilifu tangu anazaliwa mpaka anakufa usingepata hata hiyo pumzi, kama sio yeye kuwa mwenye akili ya kumtafuta Mungu, kwa kufunga na kuomba, na dua na sala nyingi…leo hii dunia pengine isingekuwepo, wote tungekuwa ni wana wa Jehanum ya moto.

Mshukuru kwa kila nyanja ya maisha yako, na pia mwombe Neema zaidi kwa Mwaka unaokuja, ukazidi kumtafuta yeye na kumsogelea zaidi, na kumjua yeye zaidi na uwezo wake, Akakupe Neema zaidi ya kuushinda ulimwengu na mambo yake, maana mambo ya ulimwengu huu yanapita, na yeye yupo mlangoni kurudi, na maandiko yanasema atakuja kama mwivi usiku wa manane!..Siku moja inapopita ndivyo tunavyokaribia mwisho, mwaka mmoja unapopita ndivyo siku ile tunavyozidi kuikaribia. Tumwombe Bwana neema na yeye atatusaidia..

Bwana akubariki sana!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

MTETEZI WAKO NI NANI?

TAFUTA KUJUA MAMBO YAJAYO:

KWANINI USIICHAGUE TUZO ISIYOHARIBIKA?

EDENI YA SHETANI:


Rudi Nyumbani

Print this post