Category Archive YESU KRISTO

DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?

Je Damu ya yesu inanenaje mema kuliko ya habili?..Nini madhara ya kuidharau sauti ya Damu ya thamani ya Yesu Kristo?

Shalom! karibu tujifunze Neno la Mungu kwa pamoja, Leo tutajifunza juu ya damu ya YESU kwa ufupi. Naamini utaongeza kitu juu ya vile ulivyojaliwa kuvijua na Bwana..

Tukisoma katika kile kitabu cha Mwanzo, tunamsoma Kaini aliyemwua ndugu yake Habili, kwasababu sadaka yake haikukubaliwa na Mungu, na ya ndugu yake kukubaliwa..Habari hiyo tunaisoma katika kitabu cha…

Mwanzo 4: 8 “Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.

9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

10 Akasema, Umefanya nini? SAUTI YA DAMU YA NDUGU YAKO INANILILIA KUTOKA KATIKA ARDHI.

11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;

12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao”.

Tunaona hapo Bwana alimwambia Kaini “sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.”..kumbuka haikusema “sauti ya roho ya ndugu yako”, hapana bali ilisema “sauti ya damu”..ikiwa na maana kuwa damu ina sauti na inanena.

Pia haikusema “sauti ya damu inanililia kutoka mbinguni”..bali ilisema “sauti inanililia kutoka katika ardhi”..kwahiyo kuna uhusiano pia wa damu na ardhi..tutakuja kuiona huko mbeleni..

Lakini pia tukisoma kitabu cha Waebrani Mlango 12: 24 inasema “Na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, INENAYO MEMA kuliko ile ya Habili”.

Hapa tunaona kuna damu mbili ya Kwanza ni ya Habili na ya pili ni ya Bwana Yesu…Lakini tunasoma damu ya YESU KRISTO inanena mema kuliko ile ya Habili.

SASA DAMU YA YESU INANENAJE MEMA KULIKO YA HABILI?
Habili tunamsoma alikuwa ni mtu wa Haki, na alienda katika ukamilifu, hata akapata ufunuo bora wa kumtolea Mungu sadaka, na zaidi ya yote alimtolea katika sehemu zilizonona na katika wazaliwa wa kwanza wa wanyama wake…Ikionyesha kabisa kuwa alikuwa ni mtu wa Haki aliyemjali Mungu, na kumfanya Mungu kuwa wa kwanza katika maisha yake..Na pia alikuwa anakwenda katika maagizo yake na sheria zake…Na hivyo mpaka kufikia wakati anauawa na ndugu yake, hakuwa na hatia yoyote na hivyo damu yake ikawa ni kama damu ya mtu asiyekuwa na hatia..Na ilipofika ardhini ikaanza kutoa sauti ikimlilia Mungu..

Na kadhalika Bwana Yesu Kristo, aliuawa pasipo hatia yoyote, yeye hakuwa na kosa lolote hata kuuawa pale Kalvari,

Matendo 4: 25 “Nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha babaetu Daudi, mtumishi wako, Mbona mataifa wamefanya ghasia, Na makabila wametafakari ubatili?
26 Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
27 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu YESU, ULIYEMTIA MAFUTA,”

damu ya Yesu

 Lakini Tunaona matokeo ya damu ya Habili kumlilia Mungu kutoka katika ardhi ni ndugu yake Kaini kulaaniwa juu ya ardhi na kuwa mtu mtoro asiyekuwa na kikao….Kwahiyo kwa ufupi damu ya Habili ilinena hukumu juu ya Kaini juu ya nchi.

Lakini tukirudi kwa upande wa Yesu Kristo, tunaona matokeo ya Damu ya Yesu Kristo hayakuwa hukumu kwa wale waliomwua..Bali yalikuwa ni rehema na msamaha, na kuhesabiwa haki bure kwa Neema..Na ndio maana Bwana kabla hajakata roho alimaliza na Kusema “Baba wasamehe” kwakuwa hawajui watendalo…lakini Habili hakusema hivyo, na zaidi ya yote Bwana Yesu alisema “Imekwisha” lakini Habili hakusema hivyo…Kwahiyo damu ya Yesu ni Bora kuliko ya Habili, Damu ya Yesu imetuletea msamaha wa dhambi badala ya hukumu, Damu ya Yesu imetuletea Baraka badala ya Laana..Kwahiyo Inanena mema sana..

Kwa ufupi wale wote waliomsulibisha Bwana Yesu Kristo pale msalabani, pamoja na sisi sote tunaomsulibisha sasa Yesu Kristo kwa matendo yetu, tulistahili kulaaniwa juu ya ardhi kama alivyolaaniwa Kaini na hata zaidi ya pale, kwasababu tulimwua Mwana wa Mungu asiyekuwa na hatia…Lakini kwasababu Damu yake inanena mema kuliko ya Habili..tumepata rehema badala ya Hukumu, ardhi imebarikiwa kwa ajili yetu badala ya kulaaniwa..zaidi sana tumepewa tumaini la uzima wa milele Haleluya!.

Huo ni msamaha wa kipekee sana, Hakuna mwanadamu yoyote duniani leo ambaye mwanawe mpendwa auawe kikatili tena pasipo hatia, halafu badala ya kuwalipizia kisasi wale wauaji,na kuwalaani anawabariki kupitia mauti ya mwanae..Huo ni upendo usio kuwa na kipimo.

Damu ya Yesu ilimwagwa juu ya ardhi hapa duniani, miaka 2,000 iliyopita na si mbinguni..ili inene mema kwa wanadamu wa vizazi vyote vya duniani. Kwa kupitia damu ya Bwana isiyoharibika, mambo yote yanafanyika kuwa mapya, na kwa kupitia damu ya Bwana tunakikaribia kiti cha Neema kwa ujasiri.

Tukiyajua hayo, ni wakati wa kujichunguza na kuogopa, na kutetemeka kwasababu kama tulistahili kulaaniwa kama Kaini lakini Bwana hajatulaani, sio wakati tena wa kuidharau hii DAMU YA THAMANI YA YESU KRISTO, sio wakati wa kujisifu kuwa tunajua..Jambo ambalo watu wengi hawalifahamu ni kwamba Neema yote tunayoiona leo hii duniani ni kwasababu damu ya YESU bado inafanya kazi juu ya NCHI. Mvua tunazozipata kwa wakati ni kwasababu ya Damu ya thamani ya Yesu bado inafanya kazi, majanga tunayoepushwa nayo duniani ni kwasababu Damu ya Yesu bado inafanya kazi licha ya kwamba maasi ya sasa yamezidi yale ya Sodoma na Gomora lakini bado tunafaidika na neema hii kwa kitambo.,

tunavipindi vizuri vya usiku na mchana, na hewa safi ni kwasababu damu ya thamani ya Yesu ipo inayonena Mema.Unafuu wowote tunaouona duniani ni kwasababu ya Damu ya Yesu. Utafika wakati Hii damu itafikia mwisho wa kufanya kazi yake ya kunena na mambo mengine yatafunguliwa, kwasababu kumbuka sio wakati wote Mungu atakuwa anafanya kazi ya kuokoa, upo wakati wa mambo mengine kufunguliwa..hapo ndipo ile dhiki kuu itakapoanza…wakati huo hakuna mtu atakayeweza kununua wala kuuza pasipokuwa na chapa ya mnyama…wakati huo maji ya dunia nzima, na chemichemi zote zitakapogeuzwa kuwa damu, wakati huo ambao Jua litatiwa giza na nyota za mbinguni zitakapoanguka, wakati huo ambao gonjwa zito ya ajabu yataikumba dunia nzima,

Kipindi hicho sio cha kutamani kufika, ni kheri ujisalimishe Kwa Yesu Kristo leo kama hujafanya hivyo, kabla ya nyakati hizo, ukatubu na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na Kwa jina la Yesu Kristo, upate ondoleo la dhambi zako, usiidharau hii Neema iliyopo leo na kufanya dhambi kwa makusudi, na kama ulikuwa hujasimama imara katika wokovu wako huu ni wakati wa kuweka mambo yako sawa..Biblia inasema katika..

Waebrania 10: 26 “Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAIBAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI;

27 bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.

28 Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.

29 MWAONAJE? HAIKUMPASA ADHABU ILIYO KUBWA ZAIDI MTU YULE ALIYEMKANYAGA MWANA WA MUNGU, NA KUIHESABU DAMU YA AGANO ALIYOTAKASWA KWAYO KUWA NI KITU OVYO, NA KUMFANYIA JEURI ROHO WA NEEMA?

30 Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.
31 NI JAMBO LA KUTISHA KUANGUKA KATIKA MIKONO YA MUNGU ALIYE HAI.”

Ndugu yangu/kaka yangu unayesoma haya ambaye ni mlevi, ni mwasherati, unafanya anasa, unakula rushwa, unatazama pornography, n.k mambo hayo yote ni njia panda ya kuelekea kuzimu,Dada unayesoma haya..unayevaa vimini na suruali, unayepaka lipstick na wanja, unayevaa hereni na wigi na unayesokota dread, unayesikiliza na kushabikia miziki na fashion za kidunia..mambo yote hayo kama hautaamua kuyaacha yatakupeleka kuzimu.

Mkabidhi Bwana leo maisha yako kikamilifu, pasipo kuwa vuguvugu..ili damu ile izidi kunena Mema juu yako.

Print this post

MJUE SANA YESU KRISTO.

Moja ya jukumu la muhimu sana la kufanya baada ya kuzaliwa mara ya pili, ni kuzidi kumjua Yesu Kristo kwa undani, kwasababu Agano jipya lote linamuhusu Yesu Kristo, kiini chote cha biblia kinamuhusu Yesu Kristo, Agano la kale lilimuelezea Yesu Kristo kimafumbo lakini agano jipya limemwelezea kwa uwazi wote, Ukristo utakuwa haujakamalika kwa namna yoyote kama tutashindwa kumwelewa vizuri Yesu Kristo.

Tukishindwa kumwelewa Bwana Yesu , ni nani, kwanini alikuja duniani, anatendaje kazi, anataka nini kwetu, na sisi tunahitaji nini kutoka kwake, yuko wapi sasa hivi, anafanya nini n.k basi hatutaweza kumwelewa pia yule anayempinga yeye (Mpinga-Kristo) ni nani na anatoka wapi? Kadhalika Hatutaweza kujua mpinga-Kristo anatendaje kazi.

Kwasababu ni wazi kuwa huwezi kumjua adui ya mtu kabla hujamjua huyo mtu mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kufahamu maadui wa mtu asiyemjua, sharti kwanza amjue huyo mtu anapotokea na maisha yake ndani nje yalivyo ndipo aweze kuwatambua na maadui zake. Vivyo hivyo hatutaweza kumjua Mpinga-Kristo kama hatutamjua Yesu Kristo vizuri kwa undani.

Miaka mingi, sana kabla ya mwanadamu wala wanyama kuumbwa, Bwana Mungu alikuwa peke yake, alikuwa hana cheo chochote kwasababu katika hali ya kawaida, ili mtu awe na cheo sharti awepo mtu aliye chini yake.

Sasa Mungu kabla ya kuumba wanadamu wala malaika, kulikuwa hakuna mtu chochote chini yake wala juu yake, hivyo alikuwa hana cheo chochote, alikuwa ni yeye kama yeye tu! na alikuwa pia hana jina, kwasababu jina kazi yake ni utambulisho kwa wasio kujua, hivyo yeye wakati huo alikuwa hana bado wasio mjua wala wanaomjua, hivyo alikuwa ni yeye kama yeye,Na ndio maana alimwambia Musa jina lake ni “MIMI NIKO AMBAYE NIKO”..sasa hilo sio jina kama ukilitafakari kwa makini, bali ni sentensi inayojaribu kuelezea uwepo wa Mungu. Hapo ni Bwana alikuwa akijaribu kumweleza Musa nafasi yake aliyokuwepo nayo kabla ya uumbaji wa kitu chochote kile.

Sasa ulipofika wakati wa uumbaji alipoanza kuumba malaika, ndipo hapo akaanza kuitwa Mungu, kwasababu maana ya Neno Mungu ni “mtengenezaji/au muumbaji” ndipo vikawepo viumbe chini yake vilivyoumbwa na yeye, viumbe hivyo vikaanza kumwita yeye Mungu, lakini kabla ya hapo alikuwa haitwi Mungu. Kwasababu hata katika maisha ya kawaida, Mtu hawezi akaitwa Baba kabla hajapata watoto, siku atakapopata watoto ndipo hapo atakapoitwa Baba au Mama, na ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu hakuitwa Mungu, mpaka siku alipoumba.

Na ulipofika wakati wa mwanadamu kuumbwa, ambao aliwaita watoto wake, Cheo chake kilizidi kubadilika na Kuwa Baba, hivyo akawa na vyeo viwili yaani Baba pamoja na Mungu mwenyezi, kwasababu sisi wanadamu tuliomwamini yeye, Mbele za Mungu wetu ni kama watoto wake, Malaika sio watoto wa Mungu, bali sisi wanadamu ndio tunaoitwa watoto wa Mungu..

Waebrania 1:5 “Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?” .

Hivyo ulipofika wakati wa Yeye kujidhihirisha kama Baba ni pale alipowatoa wana wa Israeli kutoka Misri akafunua jina lake kama YEHOVA,(Kutoka 6:1-6) Kwahiyo jina la Baba likawa ni YEHOVA, lakini ndio yule yule Mungu mwenyezi na ndio yule yule Baba Yetu. Aliwaokoa wana wa Israeli kama watoto wake kutoka katika mikono ya Farao kwa jina lake Yehova.

Kutoka 4:22 “Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; nami nimekuambia, MPE MWANANGU RUHUSA AENDE, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako”.

Hosea 11: 1 “Israeli alipokuwa mtoto, nalikuwa nikimpenda, NIKAMWITA MWANANGU ATOKE MISRI”.

Unaona Sasa kwasababu Israeli ni Mzaliwa wa Kwanza, ni lazima awepo mzaliwa wa pili, na huyo sio mwingine zaidi ya watu wa mataifa, Hivyo watu wa Mataifa nao pia waliingizwa katika neema hii ya kuitwa wana wa Mungu..

Warumi 9:23 “tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu;

24 ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ILA NA WATU WA MATAIFA PIA?

25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea, Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu, Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.

26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa, NINYI SI WATU WANGU, HAPO WATAITWA WANA WA MUNGU ALIYE HAI”.

Lakini kama tunavyojua agano la kwanza halikuweza kumkamilisha mwana wa kwanza (wana wa Israeli) kuwa mkamilifu, kadhalika lisingeweza pia kumkamilisha mwana wa pili (yaani watu wa mataifa) kuwa wakamilifu, hivyo Bwana Mungu mwenyezi akatengeneza njia nyingine ya kuwakamilisha wana wake wote wawili (yaani wayahudi na watu wa mataifa), ambayo katika hiyo watakuwa wakamilifu kweli kweli…. Na ndio hapo akauvaa mwili yeye mwenyewe YEHOVA na kuwa mwanadamu, ili kuwa kipatanishi kati ya wanadamu na nafsi yake mwenyewe.


Akauvaa mwili akazaliwa kama mwanadamu, akatembea kama mwanadamu akaishi kama mwanadamu, akajinyenyekeza kama mwanadamu, hakufanya vile kwa wazi bali alifanya kama siri mpaka utakapofika wakati wa kufunuliwa kwa siri hiyo, kwamba Yesu Kristo alikuwa ni Yehova mwenyewe katika mwili wa kibinadamu, na ndio maana Malaika Gabrieli alimwambia Bikira Mariamu amwite jina lake YESU, sasa tafsiri ya jina Yesu kwa kiebrania ni YEHOVA-MWOKOZI, kwahiyo ni yule yule YEHOVA KATIKA MWILI WA KIBINADAMU, Isipokuwa Jina lake limeongezeka na kuwa YEHOVA-MWOKOZI hivyo amekuja kwa kuokoa. Siri hiyo hawakufunuliwa watu wote isipokuwa wale ambao Bwana alipenda kuwafunulia. Na ndio maana Mtume Paulo aliileza siri hiyo kwa ujasiri katika..

1 Timotheo 3: 16 “Na bila shaka SIRI YA UTAUWA NI KUU. Mungu alidhihirishwa KATIKA MWILI, Akajulika kuwa na HAKI KATIKA ROHO, Akaonekana na malaika, AKAHUBIRIWA KATIKA MATAIFA, AKAAMINIWA KATIKA ULIMWENGU, AKACHUKULIWA JUU katika utukufu”.

Unaona hapo Mtume Paulo anamzungumzia Yesu Kristo, Mungu katika mwili, lakini anasema ni SIRI?

Sasa unaweza ukajiuliza kama Yesu alikuwa ni Mungu katika mwili kwanini aliruhusu watu wamwite yeye mwana wa Mungu? au aruhusu kujulikana kama mwana wa Adamu? Au mwana wa Daudi?.

Bwana Mungu, alipouvaa mwili wa kibinadamu, alijishusha kuwa mdogo sana, sasa mtu hawezi kujishusha na kuwa mdogo na bado atafute kuitwa mkubwa, bila shaka atakuwa ni mnafki. Ndio maana aliwaambia wanafunzi wake, mimi mnaniita Bwana na ndivyo nilivyo lakini sikuja kutumikiwa bali kutumika, na akawaambia mtu akitaka kuwa mkubwa kuliko wote basi awe mtumishi wa wote, hivyo yeye alikuwa kielelezo namba moja cha maneno hayo,

Ili kuelewa vizuri hebu jaribu kutafakari mfano huu, kulikuwa na tajiri mmoja mwenye mali nyingi sana, na mwenye makampuni mengi na wafanya kazi wengi sana, na wengi wa wafanyakazi wake walikuwa hata hawamjui kwa sura kutokana na ukuu wake, wengi walikuwa wanamsikia tu, lakini yule tajiri akaona kuna kasoro Fulani katika moja ya makampuni yake yaliyopo katika moja ya majimbo yake, akasikia kwamba kwenye moja ya hilo kampuni lake, wafanya kazi wananyanyaswa hawalipwi mishahara yao kwa wakati, na kuna ubadhilifu wa fedha mahali Fulani, sasa yule tajiri akaona njia pekee ya kwenda kutafuta suluhisho la hilo tatizo na kujua ukweli wa Mambo sio tu kutuma mawakili wake, bali akaona njia pekee ni kujibadilisha na kutoka kwenye ukurugenzi wake, na kusafiri mpaka kwenye hiyo nchi ambapo kampuni lake lipo na kwenda kujifanya kama nayeye anatafuta ajira ndani ya hilo kampuni, na akishapata naye awe kama mmoja wa watumwa wadogo wa lile kampuni walioajiriwa,..

Sasa kwasababu yeye yupo pale sio kwa kutafuta ukubwa bali kwa kutafuta chanzo cha tatizo, hivyo hawezi kuanza kujitangaza kwamba yeye ndiye Mmiliki wa lile kampuni, hapana bali atafanya mambo yake kwa siri siri, atajifanya mtumwa, na zaidi ya yote, atazitii zile sheria ambazo yeye ndiye aliyezipitisha katika enzi zake, kama vile sio yeye aliyezipitisha, atakipa heshima kile cheo cha mkuu wa makampuni kama vile sio chake, mpaka utakapofika wakati wa yeye kuondoka labda ndio atawaambia moja wa wafanyakazi wake kwamba YEYE NDIYE MKUU WA MAKAMPUNI YALE. Hapo ni baada ya kile alichokuwa anakitafuta kukipata.

Na ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Yesu Kristo, yeye alikuwa ni Mungu katika mwili, isipokuwa katika SIRI asingeweza kujiita Mungu kwa namna yeyote ile, alikubali kuitwa mnazareti, alikubali kuitwa mwana wa Mungu, alikubali kuitwa mwana wa Yusufu, alikubali kuitwa mwana wa Daudi , n.k ingawa yeye hakuwa mwana wa Yusufu wala mwana wa Daudi.. kwasababu yeye mwenyewe mahali Fulani aliwauliza mafarisayo…

Mathayo 22:41 “Na Mafarisayo walipokusanyika, Yesu aliwauliza, akisema, Mwaonaje katika habari za Kristo?

42 Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.

43 Akawauliza, Imekuwaje basi Daudi katika Roho kumwita Bwana, akisema,

44 Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako?

45 Basi, DAUDI AKIMWITA BWANA, AMEKUWAJE NI MWANAWE?

46 Wala hakuweza mtu kumjibu neno; wala hakuthubutu mtu ye yote tangu siku ile kumwuliza neno tena.”

Unaona hapo Bwana anawauliza mafarisayo kama yeye ni mwana wa Daudi, inakuwaje tena Daudi anamwita Kristo Bwana? Kwahiyo unaweza ukaona Bwana Yesu Kristo, kujidhihirisha kama mwanadamu, au kama mwana wa Mungu, au kama mwana wa Yusufu haimaanishi kwamba yeye ni mwanadamu au yeye ni mtoto kweli wa Daudi au yeye ni mtoto kweli wa Yusufu, au yeye ni wa ulimwengu huu.

Hivyo Baada ya Mungu kumaliza kazi ya upatanisho kwa njia ya msalaba pale Kalvari, alirudi katika enzi yake kama Mungu Mkuu, lakini akaituma Roho yake kama Roho Mtakatifu, ambaye ndio yeye mwenyewe lakini katika mfumo wa Roho, kwa namna ya kawaida huwezi kumtenganisha Mtu na Roho yake, mahali mtu alipo ndipo na Roho yake ilipo, huwezi ukasema mtu na Roho ni vitu viwili tofauti hapana ni kitu kimoja, na ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu, ni yeye yule aliyekuwa kama Baba mbinguni, kisha akajidhihirisha kama mwana duniani, na sasa yupo pamoja nasi kama Roho Mtakatifu.

Na jina lake ni lake ni YESU KRISTO (YAANI YEHOVA-MWOKOZI). Ana nafsi moja tu, Na hatujapewa jina lingine litupasalo sisi kuokolewa kwalo isipokuwa jina lake YESU KRISTO, kwa jina hilo tunapata msamaha wa dhambi, na kufunguliwa vifungo vyetu, kwa jina hilo tunabatiziwa, kwa jina hilo tunatolea pepo, kwa jina hilo la Yesu tunatenda mambo yote ya mwilini na rohoni. Na wala hapana wokovu kwa mwingine yoyote isipokuwa kwa Mungu wetu (YESU KRISTO, MUNGU MKUU BWANA WA UTUKUFU).

Kwahiyo Mtu akimkataa Yesu Kristo, amemkataa Mungu mwenyewe, mtu akimpinga Yesu Kristo amempinga Mungu mwenyewe.

Kaka/Dada leo hii umefahamu kuwa Yesu ndiye Mungu, mtazamo wako juu yake upoje? Yeye ndiye atakayeketi katika kiti chake cha enzi na kuhukumu mataifa yote. Jifunze sana kumjua huyu kwasababu yeye ndio Njia pekee ya kuufikia uzima wa milele sio kuwa na dini wala dhehebu au kujiunga na mojawapo ya hayo, njia pekee ya kuupata uzima wa milele ni kumwamini yeye na kutubu kwa kumaanisha kuacha dhambi na maisha ya kale, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina lake hilo “Yesu Kristo” kulingana na ( Matendo 2:38. Mdo 8:16, mdo 19:5 na Mdo 10:45) Na Bwana mwenyewe atakupa kipawa cha Roho Mtakatifu. Ni maombi yangu kwamba Bwana atakukirimia neema yake kuyapata hayo na kuzidi kumfahamu sana yeye..

Waefeso 4: 13 “hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.

15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo”.

Ubarikiwe!

Tafadhali “share ” ujumbe huu kwa wengine.

Jiunge na magroup yetu ya whatsapp kwa kubofya hapa > Group-whatsapp

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

TUZIJARIBU HIZI ROHO.

MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.

ITAMBUE KARAMA YA MUNGU.

UMEPATA UHAKIKA WA KUTOKUINGIA HUKUMUNI KATIKA SIKU ILE?

JE! ADAMU ALIWASALIANA NA MUNGU KWA LUGHA IPI PALE BUSTANINI?

JE! KUCHORA TATTOO NI DHAMBI?


Rudi Nyumbani

Print this post

MAISHA YETU NI MILKI YA YESU KRISTO.

Kanisa linafananishwa na mwanamke, Bwana ndio kapenda kulifananisha kanisa lake na mwanamke, akifunua kwamba kama vile mwanaume ampendavyo mkewe ndivyo Kristo anavyolipenda kanisa lake. Na kama ijulikanavyo huwa kuna hatua zinafuatwa kabla ya mwanamume kumtwaa mwanamke awe mkewe, na moja ya hatua muhimu sana inakuwa ni MAHARI. Mahari kazi yake ni kumwongezea ujasiri mwanamume kwamba hakumpata mke wake kirahisi, amemgharimia. Na baada ya kulipa mahari ,ni ndoa kufungwa,hapo Yule mwanamke anahama kwao na kuhamia kwa mume wake, na zaidi ya yote jina lake la ukoo linabadilika, Jina la ukoo linabadilika kuonyesha kwamba kuanzia huo wakati na kuendelea yeye sio milki ya ukoo wa wazazi wake tena, bali anakuwa milki ya ukoo mwingine wa mume wake.

Sasa Bwana aliruhusu huo utamaduni uendelee kuwepo mpaka leo katikati ya wanadamu, ili kuufanya wokovu ueleweke kirahisi kwetu, kwa kulinganisha namna mwanamke anavyotwaliwa kutoka kwa wazazi wake, mpaka anapotolewa mahari, mpaka anapokuwa mke halali wa mwanaume tutapata picha namna kanisa la Kristo navyo lilivyotawaliwa kutoka katika dunia.

Hatua ya kwanza Kristo anawahubiria watu wake watoke katika ulimwengu kwa ishara na miujiza mingi, kama vile mwanamume amshawishivyo mwanamke katika hatua za awali, kisha baada ya hapo Bwana Yesu ni kulipia mahari, na Mahari anayolipa ni damu yake aliyoimwaga pale Golgotha ambapo alitoa nafsi yake kama fidia kwa mkewe (YAANI KANISA), Gharama hii aliyoingia ilimfanya yeye awe na uhalali wa kulimiliki kanisa asilimia 100%.

Na hatua ya mwisho ni mtu kubadilishwa jina na kupewa jina jipya la mumewe, kama vile jina la mwanamke la ukoo linavyobadilika na kuhamia moja kwa moja kwa mumewe. Sasa mwanamke au mwanamume asipopitia hatua zote hizo ndoa yake inakuwa sio halali.

Sasa mimi na wewe, ili kwamba tuweze kuwa wake halali wa Bwana wetu Yesu Kristo, sharti ni lazima tukubali kumwamini na kumgeukia yeye na kuacha wazazi wetu waliotuzaa, yaani kuuacha ulimwengu na mambo yake yote, sharti lazima tumtii kwa kutubu na kumaanisha kabisa kuacha dhambi na maisha ya nyuma ya anasa na kufanyika viumbe vipya.

Kisha hatua inayofuata baada ya kumkubali Yesu moyoni mwetu, Ni Bwana Yesu mwenyewe kutusafisha kwa maji na kwa damu kwa gharama aliyoingia pale Golgotha, Na ndio maana pale Golgotha wale askari wa kirumi walipomchoma mkuki ubavuni, kulitoka maji na damu, ambayo ile ni kama ishara ya mahari kwetu, kwamba tunasafishwa kwa maji na damu.

1 Yohana 5: 6 Huyu ndiye aliyekuja KWA MAJI NA DAMU, Yesu Kristo; si katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli”.

Hatua hii inamfanya mtu kuwa mke halali aliyetwaliwa kwa gharama, Bwana anakusafisha dhambi zako zote, na kukuweka kuwa huru na dhambi. Na Neno lake ndio maji yanayotusafisha na Neno lake linasema…

Matendo 2: 37 “Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? Petro akawaambia, TUBUNI MKABATIZWE KILA MMOJA KWA JINA LAKE YESU KRISTO, MPATE ONDOLEO LA DHAMBI ZENU, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu”.

Unaona hapo? namna mke halali wa Yesu Kristo anavyoandaliwa?…sio kwa kujiunga na dhehebu au kanisa bali ni kwa KUTUBU, Na KUBATIZWA KATIKA JINA LA YESU KRISTO, na kupokea kipawa cha Roho. Na kuanzia huo wakati jina lako linabadilika, na kuitwa Mkristo au wa-Yesu Kristo. Kwasababu umebatizwa kwa hilo jina, na Huwezi kuwa mkristo kama hujapitia hizo hatua.

Huwezi kuitwa wa Yesu Kristo kama haujabatizwa kwa hilo jina, sehemu zote kwenye maandiko watakatifu walibatizwa kwa hilo jina, yaani jina la Yesu, ukisoma mistari ifuatayo utaona jambo hilo {Matendo 2:38. Matendo 8:12, Matendo 8:16, Matendo 10:48 na Matendo 19:5}

Kwahiyo kama tu mwanamke aliyeolewa,anakuwa hawezi kujiamulia tu mambo, kwamba anaweza akalala popote atakapo, au akafanya chochote atakacho juu ya mwili wake, bali anakuwa ameingia kama kwenye kifungo Fulani, ambacho hakimpi uhuru wa kuwa na mahusiano ya karibu na kila mtu. Vivyo hivyo na kwa mkristo aliyempa Bwana maisha yake kwa kutubu na, na kubatizwa kwa jina lake Yesu Kristo, anakuwa ni milki halali ya Yesu Kristo, hana ruhusa ya kujiamulia mambo tu, au kufanya chochote anachojisikia akiwa katikati ya mahusiano yake yeye na Bwana.. Na ndio maana Biblia inasema katika

1 Wakoritho 6: 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? WALA NINYI SI MALI YENU WENYEWE;

20 maana MLINUNULIWA KWA THAMANI. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.

Unaona hapo, biblia inasema “SISI SI MALI YETU WENYEWE” ikiwa na maana kwamba ni “sisi tuliozaliwa mara ya pili ni milki ya mtu mwingine” na huyo si mwingine zaidi ya YESU KRISTO, hivyo hatuwezi kujiamulia chochote katika miili yetu, au katika aina ya maisha tunayotaka tuishi, Kwasababu yeye (Yesu Kristo) alitununua kwa thamani, nyingi maandiko yanasema hivyo.

Kwahiyo Bwana anao uhalali wa kutufanya chochote endapo tukijihusisha na mambo yoyote katika maisha yetu au katika miili yetu yatakayomtia wivu, au kumuudhi au kumhuzunisha. Kama biblia inavyosema katika..

1 Wakoritho 3: 16 “Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?

17 KAMA MTU AKILIHARIBU HEKALU LA MUNGU, MUNGU ATAMHARIBU MTU HUYO. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.

Sasa tukiliharibu hekalu la Mungu yaani miili yetu, Bwana naye atatuharibu, kwahiyo tunapokuwa wakristo sio suala la kujichagulia maisha hapana ni suala la kuchaguliwa maisha na yeye aliyetutolea mahari sisi, Wivu wa Bwana unakuwa kwa wale aliwatolea mahari yaani wale aliowasafisha dhambi zao kwa damu yake, Maovu makubwa yanayomchukiza sio ya watu waliomkataa, hapana bali ni yale ya watu walio wake na bado wanafanya dhambi,(wanakuwa vuguvugu) katika maisha ya kawaida hakuna mwanamume yeyote aonaye wivu akiona mwanamke mwingine asiye wake anafanya uasherati, lakini ataona wivu zaidi endapo akimwona mke wake aliyemtolea mahari na kumwoa anamsaliti na kufanya uasherati. Na ndio maana Bwana baada ya kuwatoa wana wa Israeli Misri aliwapatia amri 10 wao tu! Hakuwapa zile amri kumi watu wote wa ulimwengu mzima, au watu wa Misri. Kwanini? Ni kwasababu Misri hakuwa mke wake halali bali Israeli.

Dada/kaka unayesoma ujumbe huu, kama kweli umeamua kumfuata Bwana na umepita hizo hatua tatu, yaani KUTUBU, na KUBATIZWA KATIKA JINA LA YESU na kupokea ROHO MTAKATIFU. Na bado unajiamulia maisha, nakushauri usifanye hivyo tena, badilisha mtazamo wako, usiwe kama mwanamke mpumbavu aliyeingia kwenye ndoa na asijue mikataba na makubaliano ya hiyo ndoa, kama umeamua kuwa mkristo mwili wako ni hekalu ya Roho Mtakatifu, usilichore tattoo, usifanye uasherati, usiunyweshe pombe, wala usiuvutishe sigara, usiuvalishe nusu uchi, wala usiuvalishe mavazi yasilolipasa ya jinsia nyingine, wala usiufanye mwili usiwe katika hali yake ya asili. Kwasababu mwili huo sio milki yako mwenyewe ni Milki ya mtu mwingine ambaye anaweza kukufanya lolote endapo ukiuharibu na hautapata mtetezi.

Zipo faida leo ukidumu katika uaminifu wako kama bibi-arusi wa Kristo, asiye na hila wala mawaa, kwasababu biblia kama inavyosema katika mbingu mpya na nchi mpya Uje mji mtakatifu wa Mungu yaani YERUSALEMU mpya ushukao kutoka mbinguni ndio bibi-arusi wa Kristo(Ufunuo 21), Mungu atakaa ndani yake, Na katika huo (ambao ndio sisi) Mungu ndio atafanya maskani kumbuka hatafanya maskani kwa kila mtu tu atakayekuwepo huko hapana, bali kwa bibi-arusi tu.. Hivyo tukaze mwendo kama bibi-arusi wa kweli wa Kristo.

Ubarikiwe.

Tafadhali “share” ujumbe huu kwa wengine, na Bwana akubariki.

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP


Mada Nyinginezo:

ALIPO NA ATAKAPOKUWEPO BIBI-ARUSI WA YESU KRISTO.

JE! NYWELE ZAKO ZINAOTA AU ZIMESIMAMA?

UNAFANYA NINI HAPO?

BWANA ALIMAANISHA NINI KWENYE MSTARI HUU MARKO 2:21″ HAKUNA MTU ASHONAYE KIRAKA CHA NGUO MPYA KATIKA VAZI KUKUU;?

ULE MFANO WA WANAWALI 10 (MATHAYO 25), WALE WATANO HAWAKUWA NA MAFUTA YA ZIADA KATIKA CHUPA ZAO JE YALE MAFUTA YA ZIADA YANAWAKILISHA NINI?


Rudi Nyumbani

Print this post

KWANINI YESU KRISTO ALIKUJA DUNIANI?

Tukisoma kitabu cha mwanzo 1, Biblia inasema Hapo mwanzo, Mungu aliziumba mbingu na nchi. Lakini tunaona hakueleza aliumbaje umbaje hii mbingu na nchi yaani, miti, jua, mwezi, milima, wanyama, mwanadamu n.k.

Lakini tukija kusoma kwenye kitabu cha waebrania 11:3 tunaona

” Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri. “

 Kwahiyo siri inaonekana hapo ni kwamba mbingu na nchi ziliumbwa kwa NENO la Mungu.

Sasa swali linakuja hili NENO ni nini?

Tukisoma Yohana 1:1-3″

1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. “

Kwahiyo kulingana na mstari huu biblia inaeleza kuwa Neno lilikuwapo kwa Mungu, na lilikuwa ni Mungu, maana halisi ya “Neno” kulingana na tafsiri ya Kigiriki iliyotumika ni WAZO au NIA. Kwahiyo wazo lilikuwapo ndani ya Mungu, Na hivyo vitu vyote vilivyoumbwa vimetoka katika hilo wazo la Mungu mfano dunia, malaika, wanadamu, sayari, miti n.k. 

Mfano mzuri ni kama wewe kitu chochote ulichokitengeneza kama nyumba, kiti, meza, nguo, vilitoka kwanza katika wazo lako au nia yako. Hii ikiwa na maana kwamba kama usingekuwa na hilo wazo usingeviumba vitu hivyo vyote, Vivyo hivyo na kwa Mungu pia kama WAZO  lake (ambalo ni Neno lake) asingekuwa nalo hapo mwanzo asingeweza kuumba chochote.

Kwahiyo kabla ya mwanadamu kuasi hili NENO lilikuwa pamoja na mwanadamu, Mtu alikuwa na ushirika na Mungu kwa asilimia zote, kwasababu NENO lilikuwa ndani yake kama lilivyokuwa ndani ya Mungu kitu kilichomfanya mpaka mwanadamu kuonekana kuwa kama mfano wa Mungu, Adamu alikuwa na mamlaka yote duniani, kama vile YESU leo alivyo na mamlaka yote duniani na mbinguni biblia inasema hivyo. Na ndio maana utajua sababu ya Mungu kutuita sisi ni miungu duniani, Na yeye ni MUNGU WA miungu.

Lakini baada ya anguko Adamu aliyapoteza yote aliyokuwa nayo kwasababu alijitenga na NENO la Mungu kwa kutokutii. Hivyo yeye na NENO (nia ya Mungu) vikawa ni vitu viwili tofauti. Kuanzia wakati huo baada ya anguko, lile NENO likaanza kumtafuta tena mwanadamu limrudishe tena katika ile hali ya kuwa na mahusiano na Mungu na mamlaka yote aliyokuwa nayo kabla hajayapoteza. Na ndio maana kuna mahali Yesu alisema sio ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua nyinyi.

Sasa tangu huo wakati lile NENO likaanza kutafuta njia nyingi za kumrejesha mwanadamu, likaanza kuzungumza na wanadamu kwa kupitia MBINGU, nyota,sayari na kwa  vitu vya asili, kwa dhumuni la kumrejesha tu, lakini mwanadamu bado hakutaka kutega sikio lake kusikia.

Baadaye lile NENO likaanza kuzungumza kupitia watu, mfano manabii wa Mungu, tunaona manabii kama Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Eliya, Danieli, Yeremia, Isaya n.k..lilisema nao kwa nguvu na kwa udhihirisho mwingi liliwapigia kelele wanadamu wamrudie Mungu, warudi  katika ule ushirika waliokuwa nao kwanza na Mungu. Lakini wanadamu bado hawakutega sikio lao kulisikia, zaidi ya yote waliwaua manabii waliotumwa kwalo.

Lakini japokuwa NENO hili limezungumza mara zote hizi kwa vizazi na vizazi kupitia vitu vya asili na manabii, bado ule uhusiano uliokusudiwa mwanadamu awe nao na Mungu wake haukufanikiwa kurejeshwa kwasababu ya ugumu wa mioyo ya wanadamu. 

Ndipo wakati ulipofika lile Neno likaona liuvae mwili, lije lenyewe katika mwili,liishi na wanadamu, lihubiri mambo yote lililohubiri ndani ya manabii na vitu vya asili kwa kusudi lile lile la  kumrejesha mwanadamu  kwa muumba wake. Hili jambo linazungumziwa kwenye..

Waebrania 1:1-2″ Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. ” 

Sasa umeona mwisho wa yote Neno limekuja kuzungumza na sisi kupitia nini? sio kanisa wa chochote bali mwana.

Hili NENO likajichagulia mwili unaoitwa YESU KRISTO, Haleluya! ni furaha kiasi gani Mungu alivyojirahisisha kwetu sisi ili tukae na hilo NENO kwa jinsi ya kimwili, likiongea, likifundisha, likijibu maswali, likitembea na sisi wazi kabisa, linafurahi na sisi, kitu ambacho hapo mwanzo ilikuwa ni ngumu kulielewa lizungumzapo lakini hapa lipo pamoja nasi (IMANUELI)..Embu tutazame mstari ufuatao;

1 Yohana 1:1-3″

1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, TULILOLISIKIA, TULILOLIONA kwa macho yetu, TULILOLITAZAMA, na mikono yetu IKALIPAPASA, kwa habari ya NENO la uzima;

2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);

3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.”

Habari hiyo inaelezea lile NENO ambalo zamani lilikuwepo lakini sasa limefanyika mwili na lipo katikati yetu kama mwanadamu.

Hivyo basi BWANA YESU KRISTO alipokuja akaanza kutufundisha na kuturejesha katika utimilifu wote na Mungu tuliokuwa nao pale Edeni hata na zaidi ya pale.,Jambo la kwanza alilolifanya ni kutupatanisha sisi na Mungu kwa kumwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi zetu maana biblia inasema pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo (waebrania 9:22)

Na jambo la pili ni kutufanya sisi kuwa wana wa Mungu (miungu)
Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; “

Tukisoma 

2 Wakoritho 5:18-19 “Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu NENO la upatanisho. “

Kama tulivyosema lile NENO ni wazo/nia ya MUNGU nalo ni Mungu, ikiwa na maana usiipotii nia ya Mungu haujamtii Mungu. Na nia ya Mungu ni nini? Ni kuturujesha sisi tuwe na mahusiano naye kama ilivyokuwa hapo mwanzo ili tumwabudu MUNGU katika Roho na Kweli. Na ndio maana WAZO/NIA yake iliuvaa mwili kwa dhumuni la kutuhubiria sisi tumgeukie Baba.

Kwasababu hiyo basi Yesu Kristo ndiye NJIA, NA KWELI, NA UZIMA, MTU HAFIKI KWA BABA ISIPOKUWA KWA NJIA YAKE YEYE.(Yohana 14:6), alisema aliyeniona mimi amemwona BABA, usipomtii YESU KRISTO na kumwamini umeukataa mpango wa Mungu kwa wanadamu na viumbe vyake vyote kama shetani alivyofanya. 

Natumaini utakuwa umeshaiona sababu ya YESU KRISTO Kutokea ni nini?, ni hiyo hapo juu, Neno la Mungu liliuvaa mwili, kutuhubiria sisi na kuturejesha kwa Mungu wetu ili tumwabudu yeye katika roho na kweli. 

Wakolosai 2:9 “Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. “


Kwahiyo Mungu hana nafsi tatu, Nafsi ya Mungu ni moja tu. Mungu kuonekana katika mwili hakumfanyi yeye kuwa na nafsi tatu. Alifanya hivyo tu ili kutupatanisha sisi na yeye. Kama tusingeanguka katika dhambi kulikuwa hakuna haja ya yeye kuuvaa mwili na kuja duniani, Yeye ni Roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

NEEMA YA BWANA YESU KRISTO IWE PAMOJA NAWE!

Pia unaweza ukapata mafundisho haya Kwa njia ya Whatsapp yako, jiunge na channel yetu Kwa kubofya hapa >> WHATSAPP

Kwa mawasiliano/Ushauri/kuokoka/Whatsapp. Namba zetu ni hizi 

+255693036618/+255789001312


Mada Nyinginezo:

BADO KITAMBO KIDOGO HAMNIONI

VIUNO VYENU VIWE VIMEFUNGWA NA TAA ZENU ZIWE ZINAWAKA

VIUMBE VINATAZAMIAJE KUFUNULIWA KWA WANA WA MUNGU?

NINI MAANA YA MSIMWITE MTU BABA DUNIANI?

KAINI ALIPATIA WAPI MKE?


Rudi Nyumbani

Print this post